Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA WANAFUNZI LA 'MTAKUJA' KUFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 14/09/2013

$
0
0
Baada ya muda mrefu kupita bila kuwa na tamasha lolote la wanafunzi hasa wa shule za Sekondari, uongozi wa Mtakuja Secondary School ua Kunduchi kwa kushirikiana na mtangazaji maarufu Allan Lucky 'Rais wa Wanafunzi' wa kipindi maarufu cha Skonga ambacho hurushwa kupitia televisheni ya vijana ya EATV umeandaa tamasha la wanafunzi linalotarajiwa kuhudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 3000 kutoka katika shule zaidi ya 20 za jijini Dar-es-salaam.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbali mbali za Dar-es-salaam kwa pamoja na kupata changamoto kimawazo na kiburudani, pia kuwakutanisha wadau mbali mbali wa elimu katika kufanikisha uboreshwaji wa elimu na kusaidia katika kutekeleza mpango wa 'Matokeo Makubwa Sasa', linatarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo tarehe 14/09/2013 katika viwanja vya shule hiyo.

Miongoni mwa shule ambazo zitashiriki ni: Mtakuja, Kondo, Jordan, St. Gasper, Mbezi Beach, Boko, Goba, Twiga, Maendeleo, Mwambao, Kisauke, Kinzudi, londa, Makongo, Kawe Ukwamani, Tegeta, Mbweni, Teta, Hananasif na Mtongani, zote ni za sekondari.

Tamasha hilo linatarajiwa kuhusisha wadau mbali mbali wa elimu watakaokutana katika kubadilishana mawazo na kupata burudani kwa kushuhudia vipaji lukuki walivyo navyo wanafunzi kutoka shule mbali mbali.

Miongoni mwa shughuli zitakazoendeshwa ni pamoja na maswali na majibu, fashion show, uimbaji, ufokaji, na wanafunzi wenye vipaji mbali mbali maalum watapewa nafasi.

Msemaji wa tamasha hilo ambaye pia ni mwalimu wa michezo wa Mtakuja Beach Sekondari Bw Misonji Charles amewataka wadau mbali mbali wa elimu kuhudhuria na kushuhudia vipaji vya wanafunzi mbali mbali na pia amewataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi katika kuchukua habari na matukio mbali mbali yatakayojitokeza. Pia amewaomba wadau mbali mbali wenye uwezo wa kuchangia katika kufanikisha tamasha hili wajitokeze, kwa kuwa linaandaliwa kwa nguvu za shule na kamati maalum ya maandalizi pekee.

Kwa maelezo na kama unataka kushiriki, tafadhali wasiliana na Msemaji wa Tamsha Bw Misonji Charles kupitia 0714642442.

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AZINDUA MADARASA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI,ZANZIBAR.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

TAARIFA KWA UMMA

$
0
0

imeanzishwa kisheria kama Eneo la matumizi mseto ya ardhi ikiwa na shughuli tatu kuu.  Shughuli hizo ni:


1.           Uhifadhi wa maliasili katika Eneo la Hifadhi;

2.           Kuendeleza wenyeji na shughuli zao za ufugaji;

3.           Kuendeleza utalii.


Katika shughuli za kuendeleza utalii, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hutoa maeneo ya uwekezaji wa mahoteli, kambi za kudumu na kambi za msimu za kulala wageni.


Kumekuwepo na taarifa potofu kwenye vyombo vya habari kuhusu ugawaji wa vitalu kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.  Taarifa hizi ni potofu kwa kuwa Mamlaka haihusiki na ugawaji wa vitalu. Jukumu hilo ni la Idara ya Wanyamapori.


Aidha, katika taarifa zilizolipotiwa, Kampuni ya Leopard Tours imetajwa kupewa kitalu, jambo ambalo siyo kweli.  Leopard Tours imepewa “Special Campsite” ambayo amekuwa akiitumia siku zote - Ndutu Extra kutoka mwaka 2005 hadi sasa.  Alikuwa akiitumia kama “Season Campsite” kwa zaidi ya miezi 5 – 8 kwa mwaka.


Kilichofanyika ni kuipatia nafasi zaidi Leopard Tours itumie kambi husika kama “special campsite”.  Uamuzi huu ulizingatia kuwa Kampuni hii ni mdau mkubwa wa shughuli za uhifadhi kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani pato la Mamlaka huchangiwa kwa asilimia kumi (10%) na Kampuni hiyo ikifuatiwa na Kampuni ya Ranger Safari ambayo huchangia asilimia sita (6%).  Kwa maana nyingine Leopard Tours ndiyo kampuni inayoleta wageni wengi Hifadhi ya Ngorongoro kulinganisha na Kampuni nyingine zinazochangia.  Kampuni nyingine zinachangia asilimia tatu (3%) hadi 0.13% kwa mwaka.


Aidha ieleweke kuwa, kwa mujibu wa taratibu za uwekezaji za Mamlaka, eneo lenye ukubwa wa ekari kumi ambalo alipaswa kupewa mwekezaji Fazal wa Leopard Tours lilipaswa kulipiwa kiasi cha dola elfu sitini (60,000), hata hivyo Fazal alipewa eneo linalokaribiana na nusu ya eneo alilostahili kupewa.


Kutokana na hilo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliamua mwekezaji huyo alipe nusu ya pesa aliyopaswa kulipa ambayo ni dola za Marekani elfu thelathini (30,000).


Hivyo basi Mamlaka inasisitiza kuwa taarifa zilizolipotiwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mwekezaji huyu zilipotoshwa.



KAULI MBIU YETU

“UTALII UANZE NA MTANZANIA KWANZA”

Imetolewa na KaimuMhifadhi

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

Head Office :P.O.Box 1 Ngorongoro Crater.

Tel .+255 27 2537006/19 Fax +255 27 2537007

Direct Line +255 27 2537046

Email:ncaa_faru@cybernet.co.tz

Telegram: NGOROASILIA

Liason Office: P.O.Box 776 Arusha

Tel.+255 27 2503339 Fax +255 27 2548752

Information Office: Tel. +255 27 254625

Fax +255 27 2502603


MIE MJUMBE TU,IMETOKA KWA MDAU !

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watanzania dhidi ya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambae pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bwana Reginald Mengi. 

Malalamiko hayo ambayo yameendelea kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari na kupelekea hata baadhi ya wahusika kutoka wizarani, Idara na Mashirika yake kutakiwa kujibu na kutolea ufafanuzi malalamiko na tuhuma hizo nzito dhidi yao. 

Moja ya vyombo hivyo ni gazeti la NIPASHE linalomilikiwa na IPP media la tarehe 6 septemba, 2013 katika ukurasa wake wa tatu kuna habari inasema “SERIKALI YAZIDI KUPUUZA USHAURI WA TPSF” Inaeleza habari hiyo kuwa“ 

..Wakati taasisi ya sekta binafsi (TPSF) ikiishauri kuharakisha sera ya gesi badala ya ugawaji vitalu, serikali imeendelea kupuuza ushauri huo na sasa kupitia Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) imetangaza rasmi kuharakisha suala hilo kwa madai ya kuwahi ushindani wa masoko ulimwenguni..”

Lakini TPDF nao katika gazeti la UHURU la jana Ijumaa katika ukurasa wake wa tatu imeandikwa habari yenye anuani “MWENYEKITI TPDC: UBINAFSI UNAWAPONZA WATANZANIA. ->wengi wanalalamika uwezo hawana,

-> Zabuni za vitalu mwezi ujao.” katika habari hiyo Mwandishi ameandika kuwa “Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) , Michael Mwanda, amesema ubinafsi miongoni mwa watanzania ndio unaowafanya washindwe kunufaika na fursa za kiuchumi zilizopo nchini, zikiwemo mafuta na gesi. 

Mwanda alisema hayo jana jijini Dar es salaam, alipokuwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari juu ya malalamiko ya baadhi ya watanzania kuwa hawapewi nafasi kushiriki katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.”


Malumbano hayo kupitia vyombo vya habari baina ya pande mbili yaani Mengi na IPP yake na Muhongo na Mashirika yake ambayo yamedumu kwa muda, sasa yanachukua sura mpya baada ya kuwepo kwa taarifa za chini chini kuwa Mwenyekiti huyo wa TPSF na IPP ameandaa mpango wa kuwatumia vijana wa Chama Cha Siasa cha Upinzani (CHADEMA) kufanya kongamano lenye maudhui “rasilimali za nchi na manufaa kwa wazalendo” ambapo kongamano hilo limepangwa kupewa airtime katika kituo maarufu cha television hapa nchini cha ITV ambacho kinamilikiwa na IPP media lakini pia posho, chakula na incentives mbalimbali zimepangwa kutolewa katika Kongamano hilo.

Kama ilivyo katika mkakati huo, lengo lililopo nyuma ya pazia la kongamano hilo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa Waziri na Wizara kwa ujumla haijali maslahi ya wazawa na kwamba viongozi wakuu wa Wizara husika hawana Utaifa wala Uzalendo (kwa maana ya upendo kwa Taifa) hivyo wanataka kuzitumia nafasi zao ndani ya wizara katika kujitajirisha binafsi na kufanya upendeleo kwa wawekezaji wageni ambao hawana manufaa ya moja kwa moja katika maendeleo ya wananchi.

Madhumuni ya andiko langu hili na kuvuta utafakari makini na wa wengi katika suala hili ambalo kama hatua muhimu na za haraka hazitachukuliwa katika kulikabili linaweza kuleta tafsiri hasi kwa jamii na hivyo kuwagawa na kuwavuruga watanzania na hasa kuwafanya wapoteze imani na matumaini yao kwa Serikali, Waziri, Wizara, Idara na Mashirika yaliyopewa dhamana ya usimamizi wa rasilimali za nchi hii.



Naomba ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa seke seke la aina hii kuzuka ama kuzushwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mzee Mengi. Na mara zote amekuwa akitumia nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari anavyovimiliki katika kutafuta kuungwa mkono na hata kuonyesha ubaya wa wabaya wake. Ubaya, malumbano na mizengwe mingi ambayo huzalishwa na kusimamiwa na Mzee wangu huyu asili yake ni Ubinafsi na kuguswa kwa maslahi ya kiuchumi aliyonayo katika Sekta mbalimbali hapa nchini.

Hivi karibuni kulizuka sekeseke mfano wa hili la sasa ambalo lilihusu VING'AMUZI na kabla ya hapo TBC, UBINAFSISHAJI WA KILIMANJARO HOTEL, SUALA LA YUSUPH MANJI, SHEIKH AL BASALEHE na katika migogoro yote hiyo Mzee Mengi amekuwa akitumia vyombo vya habari katika kuwakandamiza, kuwazushia, kuwatuhumu na hata kuwadhalilisha wapinzani wake. Nitaomba wanajamvi wakumbuke kuwa Mwaka 2008 kulipokuwepo mgogoro baina ya Mzee Mengi na Al Basalehe, Katika mgogoro huo Mzee mengi alimrubuni Ustadhi Mmoja wa madrasa (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) na kuwatumia wanafunzi wa madrasa hiyo kutunga nyimbo za kaswida za kumdhalilisha Sheikh Al Basalahe na kisha nyimbo hiyo kupewa airtime katika kituo cha ITV, na kwa mfano kama huo akaitumia ITV kuwataja washindani wake kiuchumi kuwa ni MAFISADI PAPA.
Sina kumbukumbu kuwa alitumia vigezo gani kuwataja wapinzani wake hao kibiashara kama mafisadi papa, ila kumbukumbu yangu inaniambia aliwataja hadharani na kupelekea baadhi kumpeleka mahakamani na kumfungilia kesi ambazo hata hivyo hazikupata airtime za kutosha kwenye vyombo vya habari na hata mwisho wake haukuwa umefahamika kwa wengi.

Tukirudi katika hoja yetu ya vitalu vya gesi ambavyo Mwenyekiti huyo wa IPP na TPSF amekuwa akividai kwa hamu kubwa na kuwatuhumu Viongozi wa Wizara, Wakuu wa Idara na Mashirika yanayohusu Rasilimali gesi na mafuta kuwa hawana hata chembe ya Uzalendo na wabinafsi, nahofu nitaeleweka vibaya kwa baadhi ya watu nikisema kuwa kauli hii haina uhalisia na si ya kweli, na kwamba inalenga kuchochea hisia za chuki na imetolewa kwa misingi ya Chuki, it's simply a hate speech that hate are produced.

Kwa mujibu wa TPDC, kuchimba kisima kimoja kwa ajili ya kutafuta gesi na mafuta katika nchi kavu ni dola za Marekani milioni 40 (Tshs. Bilioni 64) na kwa kina kirefu cha bahari ni dola 120 (Tshs Bilioni 190) na pia ili kupata mafuta au gesi baada ya kupata uhakika, mwekezaji anapaswa kuchimba visima vinne hadi vitano, hivyo inahitaji mwekezaji kuwa na mtaji usiopungua dola za kimarekani milioni 600 ~ 800 kiasi ambacho watanzania wengi hawana (MENGI akiwemo) na kwa Kauli ya Mwanda, Mwenyekiti wa TPDC alisema kuwa Watanzania ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo, hawana budi kuungana na wabia wenye uwezo wa kimtaji na teknolojia (Suala ambalo Mengi analipinga)

Tatizo la kimsingi hapa ni Ubinafsi wa baadhi ya watu ambao wanataka upendeleo kwa maslahi binafsi ya kibiashara kwa nembo ya uzalendo na uzawa. Kumekuwepo na rekodi zenye kusikitisha ambazo zinaonyesha tatizo la msingi linalowakabili hawa tycoon wetu katika mikopo waliyochukua katika mabenki makubwa mbalimbali hapa nchini na hata nje ambapo bado hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kutokopesheka tena kwa miradi mikubwa kama hii ya vitalu vya gesi lakini pia zipo rekodi nyingine zinazoonyesha wametumia mikopo kwa shughuli ambazo hawakuombea mikopo hiyo ikiwemo mikopo kutoka benki ya kilimo (Takwimu zipo)

Kama hayo ya mikopo hayatoshi, tayari Kampuni za Mzee Mengi zinashikilia vitalu takribani 59 vya madini vyenye Ukubwa wa mita za mraba 3,752. 37 (sq km) na baadhi ya vitalu hivyo alivyovishikilia ameshindwa kuviendeleza na matokeo yake Serikali inakosa mapato kutokana na kutoendelezwa kwa vitalu hivyo lakini pia watanzania wanakosa ajira na manufaa mengine, najiuliza kama hii ndio tafsiri ya UZAWA ambayo Mzee Mengi anaizungumza, ama ni AINA nyingine ya UFISADI ambayo watanzania walio wengi bado hawajaung'amua kwa kuwa vyombo vya habari haviandiki wala kusema kuhusu habari hizi. Katika attachment ni orodha ya vitalu mbalimbali vinavyomilikiwa na Kampuni za Mzee Mengi hapa nchini.

Tunaweza kutofautiana katika mengine lakini katika yale yanayohusu mustakabali wa nchi naomba watanzania tuungane na tuseme hapana. Matumizi ya Vyama vya Siasa, wanasiasa na hata pressure group katika kutetea maslahi ya baadhi ya tycoon wa hapa nchini ni hata nje ni katika makosa makubwa ambayo yanaweza kutuletea madhara makubwa sana hasa kutokana na rasilimali zilizopo hivi sasa hapa nchini. Nitoe ombi kwa Vijana hawa wa Chadema, watambue nafasi yao kama vijana na Safari waliyonayo ya kuijenga kesho yao na kusahau posho za siku moja na vyakula. Ni wakati wa kusimamia haki na kuitetea kweli, hata ikiwa kweli hiyo inakinzana na maslahi binafsi.

RAIS KIKWETE;SIO KAZI YA SERIKALI KUVIOKOA VYAMA VYA USHIRIKA KUTOKA KWENYE MADENI!

$
0
0
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafurahia wasanii chipukizi Gosbert Bwere(4) anayepiga ngoma na mwenzake Nyambari Mganga(5) walipokuwa wanamtumbuiza muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nansio,Ukerewe, kwa ziara ya kikazi. 
=======   ======= 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siyo kazi ya Serikali kuviokoa vyama vya ushirika kutoka kwenye madeni kwa sababu shughuli za ushirika ni za sekta binafsi na maliya wanachama wenyewe.


Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa makosa ya ushirika na wezi wa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika hatimaye yanabebeshwa vyama vya siasa.


Kama namna ya kuwasaidia wananchi, Rais Kikwete amewataka viongozi mbali mbali wa mikoa kuwasaidia wananchi ili kupata viongozi waadilifu na waaminifu na wala siyo wezi kama ilivyo sasa kwa vyama vingi vya ushirika.


Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 7, 2013, wakati alipopokea Ripoti ya Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanza kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.


Rais Kikwete aliwaambia viongozi hao wa Mkoa wa Mwanza: “Tumewahi huko nyuma kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika. Nia ilikuwa kuvisaidia vyama hivyo na wanachama wake kujipanga upya na kupata uhalali wa kuweza kukopa fedha za kjuendesha shughuli zao. Lakini sasa, vyama hivyo, vimerudi kule kule kwenye madeni.”


Alitoa mfano wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani kama moja ya vyama vya ushirika ambavyo madeni yake yalilipwa na Serikali lakini sasa kina deni kubwa zaidi kuliko hata lile lililolipwa na Serikali.


“Wale watu wa Pwani walikwenda kukopa na benki moja ikakubali kuwapa fedha. Wameshindwa kulipa na ule ushirika nadhani utakufa. Njia bora kwa vyama vya namna hiyo ni kuviachia vife tu kwa sababu havina faida yoyote kwa mkulima.”


Aliongeza: “Vyama vya ushirika siyo maliya Serikali. Ni mali ya wanaushirika na hivyo ushirika ni sekta binafsi. Lakini hakuna shaka kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanatesa wananchi. Wanakopa fedha kwenye mabenki lakini wanashindwa kuzirudisha fedha hizo na hilo linapotokea Serikali inalaumiwa kwa hali hiyo.”


Rais alikuwa anatoa maelekezo yake baada ya kuambiwa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza cha Mkoa wa Mwanza kilikuwa kinakamilisha mpango wa kukopa kiasi cha sh bilioni saba kutoka Benki ya Raslimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununulia pamba.


Lakini aliwaambia viongozi hao: “Uamuzi wa kukopa ama kutokukopa ni wa kwenu. Nyanza ni mali yenu, wezi waliopata kukibebesha madeni chama hicho mliwachagua nyie wenyewe. Fedha ni zenu lakini hatimaye athari za makosa yenu yanaiathiri Serikali na hata vyama vya siasa.”


“Kuna wakati viongozi wa Chama cha Nyanza walipata kuuza godown ya thamani y ash milioni 600 kwa sh milioni 50 tu. Hawa ni wezi wa mchana wanaoiba kweupe. Wanaiba lakini wanataka Serikali iwasaidie. Kwa nini? Nadhani kazi yetu kama viongozi ni kuwasaidia wananchi kupata viongozi adilifu na aminifu siyo wezi,” alisema Mheshimiwa Rais Kikwete na kuongeza:



“Tatizo ni kwamba hata sisi viongozi tunakataa kuwashughulikia wezi kwa sababu hawa ni watu maarufu na wakati mwingine baadhi ya viongozi wanakula nao na jambo hilo limekuwa tatizo kubwa sana. Tunavifikisha vyama vya ushirika mahali ambako sina uhakika kama bado ni mali ya wakulima. Wakulima wanakutana na ushirika wakati wa kuchagua viongozi tu na baada ya hapo wakulima hawaonekani tena.”

SIKILIZA KIPINDI CHA INJILI KUTOKA SWAHILI RADIO NA MTANGAZAJI WAKO MARY MGAWE

$
0
0
LEO JUMAPILI SEPTEMBA 08, 2013 KATIKA KIPINDI  CHA INJILI  SWAHILI RADIO 
Muasisi na aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola enzi wa Uhai wake
Mtangazi wako Mary Mgawe anazungumzia  wasifu na mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT (EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA) Dkt. Moses Kulola nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi uliopita Tanzania ilikumbwa na msiba wa kitaifa baada ya kumpoteza Askofu Dkt. Moses Kulola, aliyetambulika na wengi kama Baba,Babu, na hata mlezi wa mafunzo ya kiroho katika maisha ya watu wengi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho na kuweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Muasisi na askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza Septemba 4,2013.
Sikiliza Swahili Radio Online Kipidi cha Injili na Mary Mgawe sasa hivi  Baada ya hapo miziki mchanganyiko ya Injili na kipindi kinarudiwa tena.
LINK 
http://tunein.com/radio/Swahili-Radio-s206110/

 Sikiliza kupitia simu yako ya mkononi
 Download app ya tunein kwa simu yako kisha search swahili radio.
Ukiona logo yetu ya swahili radio bofya na sikiliza.

Tuko hewani masaa 24 tukiwatangazia kutokea Jijini Washington D.C.  Marekani.



RAIS KIKWETE AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI WA MAGU

$
0
0
  Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la  Ilungu karibu na mji wa Magu.  Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika. 
 Rais  Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu
Rais  Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Kwa picha zaidi  na John Lukuwi BOFYA HAPA

NARIETHA BONIFACE ATWAA TAJI LA REDD’S MISS TANZANIA TOP MODEL

$
0
0
 Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface akipozi kwa picha mara baada ya kushinda taji hilo jana na kuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.
Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Elizabeth Pert (wapili kushoto), mshindi wa tatu Svetlana Nyameyo (wapili kulia), mshindi wan ne Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2013 na Mshindo wa tano Latifa Mohamed, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Narietha amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.
 Warembo walipo jinadi kwa pozi kali na miondoko ya kufa mtu katika kuwania taji hilo la Redd's Miss Tanzania Top Model  2013 ndani ya Snow View Hotel Arusha.
Wadau kutoka TAN MEDIA ambao ni waendeshaji wa Radio Gwala (Radio 5) ya jijini Arusha wakifuatilia kwa ukaribu shindano hilo wakiongozwa na Fransic.
 Emma Mroso kutoka JAZZ Collection ya jijini Arusha akipozi na warembo waliovaa mavazi kutoka kampuni hiyo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.

JAHAZI YAFUNIKA DAR LIVE

$
0
0
Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki walifurika Dar Live.
Mashabiki wakiwa wamembeba juujuu mlemavu ambaye alipagawa na burudani za Jahazi.
Khadija Yusuf akijinafasi stejini.
Jukwaa likiwa juu wakati Leila Rashid akiwapa raha mashabiki.
Mzee Yusuf (kushoto) akiwa na Dude 'Yahaya' wakiimba kwa pamoja.
Mzee Yusuf akiendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live.
Mcharaza gitaa wa Jahazi, Musa Musa akiwa kazini. Pembeni ni mabango ya wadhamini.
Wanamuziki wa Jahazi wakiimba kwa pamoja.
Leila Rashid akiwapagawisha mashabiki.
Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa jukwaani kusalimia mashabiki.
Baadhi ya mashabiki waliofurika wakiserebuka.
Mzee Yusuf akiserebuka na mpiga gitaa wa bendi hiyo, Mauji.
Hata sehemu ya kutema mate haikuwepo kwa jinsi mashabiki walivyofurika.
BENDI ya Jahazi Modern Taarab usiku wa kuamkia leo imefunika vilivyo katika onyesho lao la nguvu lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
Shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf na kundi lake ilizikonga nyoyo za mashabiki na kuwaacha roho safi.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

Serikali yahimizwa kurahisisha kilimo cha mkataba

$
0
0
Sekta ya pamba nchini ina uwezo wa kuwakwamua wakulima wa pamba katika dimbwi la umaskini endapo serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wataweza kusaidia uwepo kilimo cha mkataba nchini.
Akiongea na vyombo vya habari hivi karibu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Gabriel Mwalo, alisema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamiaji mzuri pamoja na ukosefu wa uungwaji mkono wa kutosha kutoka Serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika katika mfumo.
Sasa wakati umefika kwa Serikali kuyaangalia matatizo yanayokwamisha kilimo cha mkataba na mkazo uwekwe kwenye uzalishaji wa pamba pasiwepo ucheleweshaji wa utekelezaji wa sera ya Serikali,” Bw. Mwalo alisema.
"Mfumo wa kilimo cha mkataba (ambao umesimamishwa) lazima uboreshwe ili kuwawezesha wakulima kuongeza tija.
“Sekta ya pamba, kupitia msaada wa Serikali, wasindikaji na wawekezaji, ina fursa ya kufanya maendeleo kwa wakulima kwa ujumla na inaendana vizuri na ahadi ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Kama Serikali, inapaswa kuingilia kati na kuweka mazingira yatakayohakikisha kunakuwepo na maendeleo na mkulima kuwa endelevu pamoja na kilimo cha mkataba kwa ujumla.
"Wawekezaji wakubwa wanahitaji wakulima wanaoweza kuwasambazia pamba zitakazotumika kwenye vinu vyao, huku wakulima nao wanahitaji wawekezaji kuwapa mitaji kuendesha mashamba yao na kuongeza mavuno.
"Kama Serikali inaingilia kati na kusimamia vizuri kilimo cha mkataba, itakuwa ni hali ya ushindi,” Bw. Mwalo alisisitiza.
Aliongeza kusema kwamba hivi leo ekari moja huzalisha kuanzia kilo 250 mpaka 300 za pamba na kama kilimo cha mkataba kitaungwa mkono ipasavyo na Serikali na matatizo machache ya msingi kushugulikiwa, panaweza pakawepo na mavuni kuanzia kilo 1200 mpaka 1500k kwa ekari moja.


Afisa huyo aliyataja baadhi ya matatizo kama vile mbegu za pamba zisizothitishwa, wakulima kutumia mbolea kidogo au kutotumia mbolea kabisa pamoja na kuwepo dawa kidogo za kuulia wadudu na ukosenekaji wa zana za kilimo kama sababu kubwa zinazofanya mavuno ya pamba kuwa machache nchini.
Kuna mahitaji makubwa ya zao la pamba duniani, kama takwimu za hivi karibuni kutoka Benki Kuu Tanzania ni za kuzingatiwa, thamani ya mauzo ya bidhaa za asili nje ya nchi yaliongezeka kwa sababu ya ongezeko la uuzaji wa pamba nje ya nchi ikiambatana na hali nzuri ya hewa sehemu za upandaji pamoja na bei nzuri iliyokuwa ikitolewa miaka iliyopita.
Ripoti ya marejeo ya uchumi ya BoT inaonesha kwamba mwishoni mwa Juni mwaka huu thamani ya mauzo ya nje ya pamba yalikuwa Shilingi bilioni 254.4 (dola milioni 159.3).
Pamoja na Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa pamba inayoshika nafasi ya nne Afrika baada ya Mali, Burkina Faso na Egypt, kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo, juhudi zaidi kwa Serikali zinahitajika kutekelezwa ili kufikia lengo laTCB la kupata kilo 1500 kwa ekari moja.
"Pamba bado inaweza ikawa zao la biashara linaloweza kuiingizia Tanzania fedha nyingi Tanzania ingawa kiwango cha mavuno kimedumaa kwa kiasi kikubwa kwa miaka mingi na kuna haja kubwa ya kuboreshwa,” alisema.
Uzalishaji wa pamba Tanzania uliongezeka kwa asilimia 57 mwaka jana kutoka tani 225,000 zilizozalishwa 2011, na hiyo imetokana na kusaidiwa na kilimo cha mkataba nchini kufutatia miaka mitatu ya mpango wa majaribio kaskazini magharibi ya Mkoa wa Mara.
Chini ya mfumo huo, wakulima walikubaliana na wanunuzi kusambaza viwango maalumu na kuzingatia ubora wa zao hilo, na wakulipa walipata fursa ya kupata mikopo ya pembejeo kama vile dawa za kuulia wadudu, Mwalo alisema.
Hali hiyo inataka kuwepo na haja ya mawakala na wakopeshaji wa ndani kurahisisha mahusiano katika ya wazalishaji na wanunuzi, alisema he said.
Kama Serikali itachukua hatua za haraka kuunga mkono kilimo cha mkataba, mauzo ya pamba nje ya nchi huenda yakaongezeka na kuwaingizia wakulipa mapato mazuri.
Msimu uliopita ulishuhudia wakulima wakiingiza shilingi 700 kwa kila kilo ya pamba.
Septemba mwaka jana, serikali ilisisiza kwamba wakulima waingie katika kilimo cha mkataba, kwani ni mfumo ulio bora zaidi katika kuongeza uzalishaji wa pamba.
Sekta ndogo ya pamba Tanzania, ambayo inaajiri watu milioni 14, kiasi cha asilimia 40 ya idadi ya watu nchini, huenda ikafa kabisa, au Serikali ikitaka ichukue hatua za hataka kuokoa hali.
Jana, mkaguzi wa pamba, Igore Maanonga, aliiambia 'Citizen' wakulima wengi walishawishika au kudanganywa na wafanyabiashara wasio waaminifu katika dhana kwamba kilimo cha mkataba kinapunguza mapato ya wakulima.
"Wengi wa wafanyabiashara hawa wanaona kwamba watapoteza biashara kama wakulima wataingia katika kilimo cha mkataba na wanaamua kusambaza propaganda mbaya kwa wakulima,” alisema.
Jana, mkulima mmoja wa pamba na mkazi wa kijiji cha Kinyambwita, kata ya Ubutu mkoani Mwanza, Magore Masungura, aliliambia gazeti la 'Citizen' kwamba kilimo cha mkataba kimebadili maisha yake.
"Baada ya kuingia kilimo cha mkataba mavuno yangu ya pamba yaliongezeka kutoka kilo 500 mwaka 2011 hadi kilo 2980 mwaka 2012 katika shamba langu la ekari mbili," anasema.
Kutokana na mafanikio yake - Magore anasema ameweza kununua nyumba mbili kubwa na pikipiki.
Hivi leo uzalishaji wa pamba umeongezeka zaidi hadi kufikia tani 2.981 kwa ekari moja,ambapo aliweza kuuza kilo moja ya pamba kwa shilingi 700.
“Kilimo cha mkataba ndo ufumbuzi wa kilimo cha pamba nchini. Kwa ukweli kilimo cha mkataba ni chachu ya maendeleo ya wakulima wa pamba nchini Tanzania,” Bw. Magore anasema.
Ameishauri Serikali ya Tanzania kuwapa wakulima pembejeo zaidi ili waweze kufaidika zaidi kupitia mfumo mpya wa kilimo cha mkataba ambao tayari umekwisha badilisha maisha ya wakulima wengi.
Magore anasema zaidi kwamba tatizo la wakulima kuondolewa kwenye mfumo mpya wa kilimo ni propaganda ambayo inaendeshwa na wanasiasa, wafanyabiashara kwa ndiyo hao wanaomiliki maduka ya pembejeo za kilimo.

Zaidi ya makampuni 40 ya usindikaji na zaidi ya watu milioni 14 walioajiriwa katika sekta ndogo ya pamba, wakati umefika sasa kwa serikali kuunga mkono kwa ukamilifu kilimo cha mkataba,” alihitimisha kusema Bw. Gabriel.

Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika Ndani ya Tamasha la Jinsia wafana

$
0
0
Burudani ya ngoma ikiendelea katika Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika Ndani ya Tamasha la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya (wa pili kulia) akiwa na wageni wake pamoja na wanachama wa TGNPBaadhi ya wageni waalikwa ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MWILI WA MWANAMKE ALIEUWAWA KIUKATILI KAWE JIJINI WASAFIRISHWA KWA MAZISHI MKOANI DODOMA

$
0
0

 Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukiwa tayari kwa kuagwa Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,na kuanza kwa safari ya mazishi yatakayofanyika kijiji cha Nzasa  Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma. 

 Mtoto wa Marehemu Baraka Simon(12)akimuaga mama yake mzazi kabla ya safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi kuanza aliemshikilia ni mama yake mkubwa Lucy Ngorido.

 Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Yusta Mkali likiwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yatakayofanyika hapo kesho.
Wakinamama wakilia kwa uchungu
Mtuhumiwa Musa Senkando ambaye bado anatafutwa na Polisi kwa mahojiano akiwa mtuhumiwa wa mauaji hayo. Wananchi tunaomba msaada wenu kwani huyu mtu ni hatari sana katika jamii yetu.

ASAS AHIDI KUTOA MILIONI TANO KUSAIDIA VIKUNDI KAMATA FURSA TWENZETU MKOANI IRINGA LEO.

$
0
0
 sehemu ya meza kuu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu,ASAS amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia vikundi vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na kuendelea kuwa wajasiliamali katika fursa mbalimbali. 
  Mfanyabiashara mkubwa wa mjini Iringa,Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akionesha baadhi ya fursa zilizopo mkoani Iringa kwa kuonesha kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zinazopatikana mkoani humo,ASAS ameeleza kuwa vitunguu hivyo vinauzwa kwa kilo kwenye SuperMarket nyingi,anasema kuwa vitunguu hivyo vinadaiwa kutoka nje ya nchi,lakini vitunguu hivi inawezekana kuvipanda hapa mkoani Iringa na vijana wakanufaika kupitia mradi wa vitunguu hivyo.

 Mdau mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya rasilimali zilizopo mkoani hapo.

Msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto, akizungumza na wakazi wa Iringa waliojitokeza kusikiliza mafunzo ya namna ya kujikwamua kimaisha kwa kutumia fursa kwa rasilimali zilizopo mjini Iringa.
 Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu Dominic  mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
 Mwakilishi kutoka NSSF Makao Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.

 Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Kamata fursa twenzetu mepema leo mchana ndani ya mkoa wa Iringa.

 Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwey´nye Semina ya kamata fursa kwa vijana twenzetu. 
 Wanafuatilia. 



 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nick wa pili akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Iringa ,namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani hamu kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
 Bwana Shamba Yona Daniel akizungumza na wakazi wa Iringa tayari kwa kuwaonyesha namna ya kutumia Fursa kupitia kilimo.

 Wakifuatilia mada mbalilmbali ndani ya semina hiyo. 
 Meneja wa Mkoa wa Iringa kutoka taasisi ya PSI-Tanzania,Rogers Ari akizungumza fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo na suala zima la kujilinda kiafya  kwa namna yoyote ile,ili kuwa fiti katika suala zima la kuzitumia fursa wanazokumbana.

ASAS AWAAMSHA VIJANA KAMATA FURSA TWENZETU MKOANI IRINGA LEO,AHIDI KUTOA MILIONI TANO KWA VIKUNDI VYA FURSA!

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 NOMA SAANA NDANI YA IRINGA USIKU HUU..!

$
0
0


Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
  Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.

 Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta  linafanyika usiku huu.

Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
 Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba jukwaani usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora. 
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
  Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Ni noma saana
Anaitwa Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma kila kona ya uwanja.
 Anajiita Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wa Nani kaiba yangu usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mmoja wa madansa machachari sana kutoka THT,aitwaye Msami akiwa amebebwa juu na mashabiki baada ya kuonesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jukwaani.
Wasanii wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja.

Rais Kikwete azindua mradi wa kufua umeme na ahutubia maelfu ya wananchi jijini Mwanza leo

$
0
0
 Maelfu ya wakazi wa Mwanza na miji ya jirani wakimsikiliza Rais Kikwete katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na miji ya jirani katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.Rais Kikwete yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Picha na Freddy Maro
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa na kubonyeza kitufe kuashiria kuzindua mradi wa kufua umeme wa megawati 60 huko Nyakato,Mwanza leo asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo.Uzinduzi wa mitambo hiyo ni sehemu ya ufumbuzi wa tatizo la umeme uliokuwa unaikabili kanda ya ziwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kufua umeme wa megawati 60 muda mfupi baada ya kuzindua mitambo hiyo huko Nyakato Mwanza leo. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia akiwa na mavazi maalumu) akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani mwanza leo  mchana.


========  ========
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Septemba 8, 2013, amezindua mtambo wa kufua umeme kiasi cha megawati 60 katika eneo la Nyakato mjini Mwanza, umeme ambao utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza shida ya umeme katika Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.



Aidha, Rais Kikwete ameiangiza Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanza mara moja maandalizi ya kupeleka umeme kwenye machimbo ya madini ya nikeli yaliyoko Kabanga, Ngara, Mkoa wa Kagera.



Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaharakisha mipango ya kujenga reli hadi kwenye eneo hilo kama maandalizi ya kuanza kuchimbwa kwa madini hayo ambayo ni mazito na kuyasafirisha kwa barabara kwenda bandarini Dar Es Salaam kutaharibu kwa haraka barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa nchini.



Akizungumza kabla ya kuzindua mtambo huo, Rais Kikwete  ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuharakisha mipango ya kuunganisha eneo la Kabanga, Ngara, Mkoani Kagera kwenye Gridi ya Taifa ili uzalishaji wa madini ya nikeli usije kukwamishwa na ukosefu wa umeme. Amesema kuwa mgodi huo utahitaji umeme mwingi kiasi cha megawati 40.



Rais amesema kuwa Serikali yake itahakikisha inafikisha reli kwenye eneo la Kabanga mapema ili kuhakikisha kuwa nikeli inayozalishwa inasafirishwa kwa reli badala ya barabara. Amesema kuwa madini hayo ni mazito mno na kuyasafirishwa kwa barabara kutaharibu kabisa na katika muda mfupi barabara ambazo zinajengwa nchini kwa gharama kubwa.'



Mtambo wa Umeme wa Nyakato wenye uwezo wa kuzalisha megawati 60 ulianza kujengwa mwaka jana, 2012, baada ya Serikali ya Tanzania kutiliana mkataba wa ujenzi na Kampuni ya Semco and Rolls Royce ya Norway mwaka 2011 wakati maandalizi ya ujenzi huo yalipoanza.



Gharama za ujenzi wa mtambo huo ambazo ni sh bilioni 130 (Euro milioni 48.7 na dola za Marekani 15.9) zimelipwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania. Akizungumza na wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi huo, Rais Kikwete amesema kuwa umeme siyo anasa bali ni moja ya vigezo vya msingi na muhimu kabisa vya maendeleo.

“Vipo vigezo vingi vya maendeleo ya nchi na binadamu, lakini moja ya vigezo hiyo ni umeme. Na ukiangalia matumizi ya umeme kwa kila nchi yanaonyesha kiwango cha maendeleo cha nchi hiyo. Katika Marekani, kwa mfano, kila mwananchi anatumia kiasi cha kilowati 12,000 kwa wastani. Sisi katika Tanzania ni kilowati 89 tu na wastani wa Bara la Afrika ni kilowati 150,”  amesema Rais Kikwete na kuongeza:



“Nc hi yetu ya Tanzania ina umeme kiasi cha megwati 1,450 tu wakati katika Afrika Kusini ni megawati 45,000 na unaweza kuona tofauti ya maendeleo. Hivyo, ni muhimu sana kwetu kuongeza kiwango cha kuzalisha umeme katika nchi yetu.”



Katika siku ya tatu ya ziara yake kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza, Rais Kiwete pia amefungua Kituo cha Polisi cha Nyakato ambacho kimegharimu sh milioni 450, Serikali ikiwa imechangia kiasi cha asilimia 20 cha gharama hizo.



Kituo hicho cha kisasa kilianza kujengwa mwaka 2003 lakini ujenzi wake ukawa unakwamakwama kutokana na ukosefu wa bajeti hadi uongozi wa polisi wa Mkoa wa Mwanza ulipoamua  kukijenga kituo hicho kwa njia ya kuishirikisha jamii na ikaundwa Kamati ya Ujenzi chini ya uenyekiti wa Bwana Alfred Wambiura.




Akizungumza kwenye sherehe ya ufunguzi wa kituo hicho, Rais Kikwete ameahidi kuwa atajenga nyuma moja kwa ajili ya mkazi ya polisi. Kituo hicho kina jumla ya askari polisi 65.


YALIYOJIRI KWENYE TAMASHA LA "TUKO WANGAPI? TULIZANA" NA KUNOGESHWA NA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA

$
0
0
Wafanyakazi wa Tulizana wakiwaamasisha wananchi waliofika kwenye viwanja vya Leaders Clubs kupima Virus vya Ukimwi na pia kutoa elimu ya maambukizi ya Virus hivyo
Mmoja wa wafanyakazi akimweleza jambo kwa umakini kijana aliyekuja  kupima ili aweze kutoka kwenye mtandao wa ngono kwenye viwanja vya Leaders Club
Mmoja wa wananchi waliochangia damu kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" kwenye viwanja vya Leades Clubs jana mchana
Mfanyakazi wa Tulizana akitoa elimu kuhusu matumiza ya Kondom aina ya Dume  kwa vijana waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wamepumzika baada ya kazi ngumu ya kuelimisha jamii juu ya kuachana na mtandao wa mapenzi  ambao unaweza kusababisha maambukizi ya vurus vya UKUMWI wakati wa Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Mfanyakazi wa Tulizana akitoa elimu kuhusu matumiza ya Kondom aina ya Salama  kwa vijana waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Upimaji wa Afya ukiendelea

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO ZIMA KWA KUBOFYA HAPA CHINI



Mfanyakazi wa Tulizana akitoa jinsi gani wataondoa mtandao wa kuwa na wapenzi wengi elimu  kwa vijana waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Vijana wakisikiliza kwa umakini elimu wanayoipata juu ya maambukizo ya Ukimwi na hasa katika utumiaji wa mipira wakati wa mapenzi waliofika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Vijana wakisikiliza kwa umakini elimu wanayoipata juu ya maambukizo ya Ukimwi na hasa katika kuondoa mtandao wa kuwa na wapenzi wengi kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Rais wa Bendi ya Fm Akademia akimpa zawadi mshindi wa shindano la Kuzungusha Peni
Wakiwa kwenye picha ya pamoja
Madansa wa Fm Akademia wakiwa kazini kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Fm Akademia wakiendelea kutoa burudani kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Rais wa Fm Akademia akiongoza timu yake wakiuzunguka Uwanja huku wakicheza ilikuwa furaha
Rais wa Fm Akademia na timu yake wakiendelea kutoa burudani
Wadau wakiendelea kuburudika kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Vijana wakitengeneza mfano wa Mtandao wa mapenzi ambao unaweza kusababisha maambukizi ya virus vya ukimwi
Baada ya kumaliza kutengeneza mtandao huo wakapiga picha ya pamoja kwenye "Tuko wangapi? Tulizana"
Suma Mnazaleti akiwa kwa stage wakati wa Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Clubs
Suma Mnazaleti akiendelea kutoa burudani
Baadhi ya wafanyakazi wa Tulizana wakiwa kwenye picha ya pamoja katika tamasha la
"Tuko wangapi? Tulizana"
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye Viwanja hivyo vya Leaders wakifuatilia tukio zima
Snura akiwapagawisha mashabiki wake kwenye Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club
Snura akiendelea kutoa burudani
Timu nzima ya Snura ikiendelea kutoa burudani
Sasa ikafika muda wa kukata viuno ilikuwa ni hatari kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Kweli yalikuwa majanga
Mc katika tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" akizungumza neno
Mc wa kike akizungumza neno
H Baba akitoa burudani wakati wa tamasha la Mc katika tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" na pia kulikuwepo upimaji wa virus vya ukimwi uliofanyika kwenye viwanja vya Leader Club
H Baba  akiendelea kutoa burudani
Densa wa H Baba akionesha umachachali wake kwenye stage
Shetta akiwa kwa Stage kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Madansa wa msanii Shetta wakitoa burudani
Sasa ilifika kazi ya Shetta  kufanya ya wake kamo unavyoona anakata mauno
Wadau wakiwa  wametokelezea kwenye Camera ya yetu kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" nao hawa walikwenda kupima na wewe je utaenda lini?
Diamond akiwa Back Stage ya Tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"
Diamond akiwa kwenye Stage ya "Tuko wangapi? Tulizana" ambapo tamasha ilo lilifanyika kwenye viwanja vya Leader Club
Diamond akiendelea kutoa burudani
Kazi ndo kwanza kama imeanza
Diamond akiimba na shabiki wake wimbo wa Muziki gani aliyekuwa anaimba kama Ney wa Mitego
Wananchi walikuwa wengi waliofika kwenye  tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana" lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders
Watu walikuwa wakutosha kwenye tamasha la "Tuko wangapi? Tulizana"

PICHA ZOTE NA PAMOJAPURE /PAMOJA BLOG

ASKOFU DUNSTAN MABOYA KUFANYA HUDUMA USA

Wanokwenda Nigeria Airtel Rising Stars watajwa

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza kikosi cha wachezaji 32 wanaosafiri kwenda Lagos, Nigeria wiki ijayo kushiriki mashindano ya kimataifa kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars.

Afisa maendeleo wa TFF Salum Madadi amewataja wachezaji wanaounda timu ya wasichana kuwa ni walinda mlango Najihati Abbasi kutoka mkoa wa kisoka wa Kinondoni na Niwale Halfan (Temeke). Wengine ni Stumai Abdallah, Anastazia Anthony, Tatu Iddi (Kinondoni), Vumilia Maharifa, Donisia Daniel, Maimuna Hamisii na Amina Ally (Ilala).

Aliwataja wachezaji wengine kuwa ni Shelda Boniphace, Rehema Yahya na  Anna Hebron (Kinondoni), Khadija Hiza (Tanga), Neema Paul, Amina Ramadhani na Latifa Ahmed (Temeke). Wanaounda kikosi cha wavulana ni Arafat Mussa (Ilala) Aziz Hashim (Ilala), Rothan Mkanwa na Petro Mgaya (Morogoro), Bruno Shayo (Mwanza), Thomas Chideka (Temeke), George Chota (Morogoro), Luseke Kiggi (Mwanza) na Ramadhani Kondo (Morogoro).

Wengine ni Martin Luseke (Mwanza), Omary Hussein (Ilala), Joseph Mushi (Ilala), Miraj Kwangaya na Salum Issa (Temeke), Optanus Lupekenya (Morogoro) na Athanas Mdam (Mwanza). Mashindano haya ya vijana ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya pili mwaka baada ya yale ya uzinduzi kufanyika jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana pekee ambayo hata hivyo ilitolewa katika hatua za awali huku timu ya Niger ikitawazwa kuwa mabingwa.

Airtel imeanzisha mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza kujiendeleza zaidi kisoka. 

Hivi sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika hatua ya usajili ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.

Ilikuwa hivi ndani ya uwanja wa Samora,mkoani Iringa Serengeti Fiesta 2013,noma saana.!

$
0
0
Hivi ndivyo Serengeti Fiesta 2013 noma saana ilivyokuwa ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa usiku wa kuamkia leo. Mkali mwingine wa mitindo huru a.k.a freestyle,Godzilla akikamua vilivyo jukwaani.Na video chini ni msanii Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images