Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1557 | 1558 | (Page 1559) | 1560 | 1561 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa kuleuliwa, Salma Kikwete, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo, akizungumza na Waziri wa Madini, Angela Kairuki, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mbunge wa kuteuliwa, Salma Kikwete, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 9, 2018, katikati ni Mbunge wa jimbo la Tarime Bw. John Heche.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Tarime Bw. John Heche, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Na Benny Mwaipaja

  Serikali imeeleza kuwa kiasi chote cha dola za Marekani milioni 65 zilizokopwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutoka Benki ya CRDB kwa udhamini wa Serikali mwaka 2004 kimewekezwa nchini na hakijapelekwa kuwekeza katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda hicho kukopa kiasi hicho cha fedha ambacho kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji uliofanywa katika Kiwanda cha Kagera ni wa takribani dola za Marekani milioni 250 hivyo haiwezekani mwekezaji kukopa dola milioni 65 na kuzipeleka Congo ili hali kiwango cha uwekezaji nchini ni kikubwa.

  “Mwekezaji wa Kiwanda hicho ni wa ndani na amejitahidi kuajiri watanzania wengi hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kukiwezesha kiwe cha mfano ili kiendelee kuleta matokeo chanya kwa watanzania”, alisema Dkt. Kijaji.

  Katika swali la msingi la Mbunge huyo, alitaka kujua kiwango cha hisa ambacho Serikali inamiliki katika kiwanda cha Sukari cha Kagera na kiasi cha fedha kilichokopwa na kulipwa na mwekezaji huyo kupitia udhamini huo wa Serikali.

  Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa sasa haimiliki hisa zozote katika kiwanda hicho na kuongeza kuwa hisa zake katika kiwanda hicho ziliuzwa mwaka 2001 baada ya kukibinafsisha kiwanda hicho kwa Kampuni ya Kagera Saw Mills Limit.Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mwekezaji wa Kiwanda hicho alikopa kiasi cha dola za Maerekani milioni 65 kwa kutumia udhamini wa Serikali mwaka 2004, ikiwa ni udhamini (guarantee) wa kipindi cha miaka 12.

  Alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho mimerejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 56.88, sawa na asilimia 87.5 ya mkopo wote, na kwamba marejesho ya mkopo uliobaki wa Dola milioni 8.12 yatafikia ukomo wake mwezi Julai, 2019.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Bungeni Mjini Dodoma, aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kagera, kukopa kiasi cha dola milioni 65 za Marekani ambacho amedai kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

  0 0  Na Hamza Temba - WMU
  ........................................................
  JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa nchini.

  Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla muda mfupi baada ya kukagua jengo hilo ambalo linasemekana kuwa refu kuliko majengo yote jijini Arusha likiwa na jumla ya ghorofa 18.

  Alisema jengo hilo ambalo linatizamana na Round About ya AICC katikati ya jiji hilo, limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja (One Stop Centre) cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla.

  Alisema jengo hilo litatoa fursa kwa wadau mbalimbali wanaotoa huduma za utalii kuweka ofisi zao ikiwemo mabenki, watoa huduma za usafiri, mashirika ya ndege, mawakala wa safari za utalii na huduma, maduka ya bidhaa za utalii na mahoteli.

  "Tutapamba pia jengo hili na" live screen" (Mabango ya Video Mubashara) za vivutio, hivyo wanyama wakiwa wanapita huko porini watakuwa wanaonekana "LIVE" (Mubashara) kwenye jengo hili kupitia LED Screen ambazo zitakuwa zimezunguka jengo hili" alisema Dk. Kigwangalla.Alisema huduma nyingine zitakazotolewa katika Jengo hilo ni pamoja na zile za kuangalia jiji la Arusha kupitia darubini, huduma za burudani ikiwemo kumbi za starehe na migahawa.

  Kwa upande wake Mkandarasi wa jengo hilo, Mhandisi Bismas Meela wa Kampuni ya Inter-Consult limited alisema ujenzi wa jengo hilo ambalo ulianza mwezi Novemba, 2013 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.Alisema jengo hilo ambalo lina uwezo wa kupaki magari 67 kwa wakati mmoja katika ghorofa za chini linagharimu shilingi za Kitanzania bilioni 45.

  Katika ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa jengo hilo, Dk. Kigwangalla aliongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi na Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu kuhusu jengo la kitega uchumi la mamlaka hiyo lililopo katikati ya Jiji la Arusha ambalo limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Jiji la Arusha akiwa juu ya Jengo la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kutoka kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu na  Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi. 
  Dk. Kigwangalla akiendelea kupata maelezo kuhusu jengo hilo kutoka kwa Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa mamlaka hiyo, Asangye Bangu. 

   Dk. Kigwangalla na msafara wake wakiangalia umbo la uso wa simba uliotengengenezwa katika moja lango la kuingilia kwenye lift ndani ya jengo hilo. Milango yote ya kuingilia kwenye lift ndani ya jengo hilo itapambwa kwa taswira mbalimbali za wanyamapori.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ngazi maalum zinazotumia nishati ya umeme ndani ya Jengo hilo. Kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu na nyuma yake ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi. \
  Waziri Kigwangalla akikagua kabati la kuhifadhia vitu katika moja ya Hotel Aprtment ndani ya jengo hilo. Kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu.
  Muonekano wa jengo hilo kutokea barabara ya Makongoro Jijini Arusha.

  0 0  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa huku ikijivunia mafanikio ya kuongezeka kwa biashara kuanzia mwaka 2011.

  Pia mapato yamekuwa yakiendelea kupanda na kuanzia Julai mwaka 2017 hadi mwaka 2018 shehena iliyokuwa ikiingia ilianza kupanda na meli zinazoingia kufikia takriban 3000 kwa mwezi.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati akielezea Wiki ya Mamlaka hiyo iliyoanza jana na kilele chake kufikiwa Jumapili.Ambapo watatumia maadhimiaho hayo kueleza walikotoka tangu April 2005, walipo na wanakotarajia kwenda kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma kwa biashara. 

  Amesema TPA imekuwa ikiendelea kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza masoko huku wakikusanya Sh.bilioni 420 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita."Mamlaka hiyo, inalenga kuboresha zaidi huduma zake, kwa kuandaa mazingira ya serikali kupata mapato yake kwa kuwa kati ya asilimia 45 hadi kufikia 55 ya kodi inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato, hupatikana TPA," amesema.

  Kakoko amesema wanatarajia kutekeleza mradi ya ujenzi wa bandari kavu katika baadhi ya mikoa ikiwemo Kigoma, Arusha, Mbeya na hata Mwanza wanalenga kuwapa unafuu wateja wao kutoka nje ya nchi wanaokuwa wakifuatilia bidhaa katika Mamlaka hiyo.

  Kuhusu maadhimisho hayo ya miaka 13,amesema watatoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara namna ya utendaji wa Mamlaka hiyo.Pia, kuchangia damu kwa wagonjwa, kutoa viti vya walemavu vya magurudumu mawili na vifaa vya kisasa vya kupima joto mwilini.

  “Nia ya bandari ni kuongoza katika biashara kwa utoaji huduma ya uhakika katika mtandao wa uchukuzi katika Kanda zinazozunguka."Ikiwa pamoja na kuongeza mapato kwa kusimamia bandari katika kutoa huduma bora na nafuu kwa kutumia mbinu na teknolojia kisasa Ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika ,”amesema Kakoko

  Ameongeza Mamlaka hiyo inatekeleza miradi katika kuboresha utoaji wa huduma na katika eneo la miundombinu, wana mpango wa kuchimba lango kuu ya kuingilia bandari katika eneo la Feri, jijini Dar es Salaam.Amesema jambo hilo litasaidia kuingia kwa wingi meli kubwa pamoja na makasha mengi zaidi.

  Pia amesema Mamlaka inatekeleza miradi ya maendeleo mbalimbali katika bandari ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na katika bandari zilizopo maziwa makuu ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa kwa kujenga magati na kuboresha yaliyopo.Ameongeza pia ununuzi wa vifaa mbalimbali ili kuweza kuwa na bandari za kisasa zitakazokuwa na uwezo wa kuhudumia shehena kubwa zaidi.

  “Uboreshwaji wa miundombinu ya bandari si tu kwa Bandari ya Dar es Salaam lakini na Mtwara na Tanga na hata katika maziwa yote makuu,” amesema.Akizungumzia usalama Kakoko amesema wameendelea kuboreshwa ulinzi na wana mpango wa kuweka mashine za kukagulia mizigo (scanning machine) katika mipaka yote na ofisi zote

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya TPA, Profesa Ignatus Rubalatuka amesema ili Mamlaka iyafikie malengo yake inatekeleza vipaumbele vitano ambavyo ni maendeleo ya rasilimali watu, uboreshwaji wa miundombinu,matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kudumisha ulinzi na usalama pamoj ana kuongeza juhudi za kimasoko.

  Amesema suala la ulinzi na usalama wa mali za wateja alisema ni jambo linalopewa kipaumbele kwa kuhakikisha ipo miundombinu ya vifaa vya ulinzi vya kisasa.

  Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka usimamizi wa bandari yaliyoanza leo , jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deosdidit Kakoko akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya kuanzishwa kwa mamlaka ya usimamizi wa bandari, leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Fransisca Muindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma watazozitoa katika maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  *Majina ya wanaume waliotelekeza watoto kuanikwa hadharani

  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

  MKUU wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda leo April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.

  Ambapo ameeleza  maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda amesema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.

  Ameeleza hawapo kwa  ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.Amesema Makonda  ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto  na kuwe na usawa.

  Amewataka akina  Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.Makonda ameeleza  Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.

  Akizungumza na Michuzi blog Lucy Peter wa Tegeta ameeleza kuwa alitelekezwa mara baada ya kupata ujauzito hadi sasa mtoto wake wa kiume ana miaka 5, na amefika kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa ili baba wa mtoto huyo aweze kutoa huduma mtoto huyo kwani hadi sasa mama huyo anaishi kwa wazazi wake.Aidha Nasra Mohammed ameeleza amefurahi kwa hatua ya Mkuu wa Mkoa ya kuwasaidia wamama waliotelekezwa, hivyo anaamini kuwa mtoto wake atapata huduma stahiki kutoka kwa baba yake aliyemwachia mtoto akiwa na mwezi mmoja.

  Hata hivyo wamama hao wamefurahi na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa kuamua kuwasaidia wao na watoto wao hivyo Mungu ambariki sana.Aidha mkuu wa mkoa ameeleza kuwa watahudumia watu 500 kwa siku na maeneo yote nchini hata kama si mkazi wa Dar es salaam kwani ni haki yao na hakuna kuogopau vitisho vya aina yoyote bali waangalie kupata zao za msingi.
  Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.
    01.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda  akizungumza na  waliotelekezwa na waume zao juu   kulinda haki za Mama na Mtoto ambapo kama Baba wa watoto   hatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.(Pacha na Emmanuel Massaka,Globu ya jaii)
   .Mkuu wa Mkoa akizungumza na maofisa mbalimbali wanaotoa huduma na kusisitiza wawasikilize  wakina mama wote hata wale wasio wakazi wa Dar es salaam. .(Pch na Emmanuel Massaka,Globu ya jaii)
  04.Seheu ya akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam.
   Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.


  0 0

  Imeelezwa kuwa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa fursa kubwa za maendeleo ya kiuchumi na biashara kuliko nchi nyingine zote za Afrika Mashariki, na kutolea tuu mfano wa sekta moja ya usafiri na usafirishaji, Tanzania imeelezwa kuwa ni nchi yenye bahati sana, kuzungukwa na nchi 8 ambazo hazina bahari, hivyo fursa tuu za usafirishaji kwa kutumia bandari, reli, maziwa na anga, zikitumiwa vizuri, zinaweza kuipaisha Tanzania kiuchumi na kujiendesha, bila kutegemea sekta nyingine zozote.

  Bahati hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.

  John Ulanga, amesema Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazina bahari kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki, hivyo Tanzania ikichangamkia kutumia fursa hii kibiashara, itakuza uchumia sio tuu wa Tanzania pekee, bali hata wan chi za jirani zetu, na kule kote njia hizi zinakupita, maeneo hayo yana fursa za kustawi kiuchumi.

  Ulanga amesema, Tanzania imekana na nchi nane ambazo hazina bahari, nchi hizo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji, na kusema kama tutazizatiti na kusafirisha mizigo yote ya nchi hizi, pato la usafirishaji pekee litakuwa kubwa kuweza kuendesha nchi, hata bila kutegemea sekta nyingine.

  Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane, ameishukuru TradeMark kwa ufadhili huo na kueleza fedha hizo zitasaidia sana katika kutimiza majukumu ya CCTTFA ikiwemo uhamasishaji wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuelezea faida za Bandari ya Dar es Salaam ukilinganisha na bandari nyingine.

  Naibu Mkurugenzi  wa Trademark East Africa, Bi. Monica Hangi amesema, kwa vile lengo la Trademark ni kusaidia kurahisisha biashara, hivyo ufadhili huo utasaidia sana kurahisisha biashara ya usafirishaji watu na mizigo kwa nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

  Mkurugenzi wa Miundombini wa TradeMark East Africa, tawi la Tanzania, Smark Kaombwe, amesema biashara ni ushindani, hivyo ili bandari ya Dar es Salaam iweze kuvutia zaidi nchi majirani waitumie, lazima iboreshe utendaji wake mizigo ichukue muda mfupi kutoka, na pia iwe na gharama nafuu kuliko bandari majirani zetu.

  Meneja Mradi wa Uangalizi wa Usafirishaji wa Central Corridor, Eng. Melchior Balentandikye, amesema kabla ya msaada huo, Central Corridor imekuwa ikijihusisha na usafiri wa barabara pekee, lakini sasa msaada huo, utawasaidia kushughulikia usafiri wa barabara, reli na usafiri wa majini na usafiri wa anga.

  Meneja wa Fedha na Utawala wa Central Corridor, Costaph Natay, amesema msaada huo utasaidia sana kuboresha ufanisi, hivyo Central Corridor itaboresha ufanisi wa shughuli zake, hivyo kuongeza ufanisi katika usafirisha abiria na mizigo katika ukanda wa kati.

  Meneja Mawasiliano wa Central Corridor, Flory Okadju, amesema msaada huo utaisaidia Central Corridor kuboresha mawasiliano na utoaji wa elimu kwa umma katika nchi zote tano za Ukanda wa kati, hivyo kutoa uelewa mkubwa zaidi kuhusu ubora na unafuu wa bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuvutia zaidi wafanyabiashara wan chi hizi, kupitishia mizigo yao bandari ya Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, akionyesha njia za Ukanda wa Kati, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
  Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakitia saini mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
  Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakibadilishana mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.

  0 0

  TradeMark East Africa (TMEA) Tanzania Country Director, John Ulanga (L) hands over a Memorandum of Association (MoU) to the Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (R) during the ceremony of signing a financing agreement to provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021) held in Dar es Salaam last week. (Photos by Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG).
   TradeMark East Africa (TMEA)  Tanzania Country Director, John Ulanga explain to journalist how the TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency whey are working. TradeMark East Africa (TMEA) is an aid-for-trade organization that was established with the aim of growing prosperity in East Africa through increased trade. TMEA operates on a not-for-profit basis and is funded by the development agencies of the following countries: Belgium, Canada, Denmark, Finland, the Netherlands, Norway, UK, and USA. TMEA works closely with East African Community (EAC) institutions, national governments, the private sector and civil society organizations.
  Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (C) explaining a few things to the journalist about their publications that help traders in offering them various education.
  TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) have signed a financing agreement geared towards strengthening and enhancing the Central Corridor Transport Observatory (CCTO). The financing will specifically improve monitoring of the Central Corridor performance in-order to support evidence-based advocacy and decision making to remove trade barriers. To that effect, TMEA will provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021). 

   “TradeMark East Africa is delighted to provide this support to CCTTFA because the organization is producing reliable and timely data on the performance of the Central Corridor Transport Network. This support therefore will further strengthen that work and enable the countries served by the corri dor to design interventions to further improve performance of the corridor” said John Ulanga, the Tanzania Country Director.

   “CCTTFA highly appreciates this funding support from TMEA for our Central Corridor Observatory work, the funding will go a long way to support our ongoing efforts and enable us to work with various stakeholders in central corridor partner states to further improve efficiency of the corridor and hence increase the volume of trade going through the corridor for the benefit of the countries”. said Captain Dieudonne Dukundane, Executive Secretary of CCTTFA.

   To accomplish the above, the CCTTFA will enhance the CCTO into a one stop center platform for availing and accessing relevant information and data related to movement of goods along the Corridor. Specifically, this support will enable CCTTFA maintain and improve the current online information portals, develop mobile data collection tools, roll out the central corridor dashboard to other member states, develop trade costs and transport predictive models and develop tools to monitor processes and effectiveness of initiatives along the Central Corridor.

  0 0

  Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameitaka Serikali kuhakikisha inasambaza mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

  Chumi amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima hawakupata mbolea'

  'Sio hivyo tu, hata hiyo 64% hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa, mkulima wa Itimbo, Kitelewasi, Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia mwezi February wakati uandalizi wa mashamba unaanza mapema Oktoba.'

  Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni kuwaonea wakulima Akizungumzia wakulima kuuza mazao yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani 2.6milioni ya chakula, lakini Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani 26,000(elfu ishirini na sita tu), afu mkulima anazuiwa kuuza mahindi yake, jambo ambalo sio sawa.

  Tunawafanya wakulima wa nchi hii kama raia daraja la pili (second citizens),mbolea tuwacheleweshee, ziada ya mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa' alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza kuwa ni vizuri serikali ikaangalia changamoto ilizokutana nazo katika usambazaji wa mbolea mwaka huu na kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima kupata mbolea kwa bei nafuu, kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.

  Awataka Wawekezaji Mafinga kuwajali wafanyakazi

  Akizungumzia haki za wafanyakazi, Chumi alisema kuwa anapongeza jitihada za Rais John Magufuli kuvutia wawekezaji, lakini akaitaka Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira kutupia jicho haki za wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga.

  Uchumi wa Viwanda lazima uendane na welfare ya wafanyakazi, itakuwa haina mana kuwa na viwanda lakini hali za wafanyakazi zinakuwa duni, lazima walipwe vizuri, waangaliwe huduma za afya na kulipiwa nssf , alisisitiza Mbunge huyo.

  Akifafanua, alisema sio haki mfanyakazi anatoka Changarawe, anatembea mpaka kilometa nne kwenda kazini, sio haki.ni hatari sana, unakuta mama anaamka saa kumi alfajiri kuwai kazini ambako nako halipwi vizuri, nikuombe mama Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu) na kaka yangu Mavunde (Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Vijana) nadhani ni mdogo wangu kufika Mafinga na kutoa maelekezo.

  Apongeza Mhe Rais kukutana na Wafanyabiashara, ashauri akutane nao Kisekta

  Tumeona ambavyo Jumuiya ya wafanyabiashara walieleza kero zao na Mhe. Rais na Rais akaagiza Mawaziri wazifanyie kazi, lakini nimuombe Mhe Rais akutane na Wafanyabiashara kisekta mana siku ile wote tuliona muda ulikuwa mdogo kwa mfano anaweza kukutana na sekta ya usafirishaji.

  Akizungumza baadae na Mwandishi wetu, Chumi alisema kuwa mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga hayaridhishi na wanapolalamika kwa baadhi ya viongozi taarifa hurejeshwa kwa wenye viwanda kwa siri na matokeo yake mlalamikaji hutafutiwa visa na kufukuzwa kazi.

  0 0

  Leo Aprili 10 ni siku ya kuzaliwa kwa Journalist/Photojournalist na Blogger Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog (www.kajunason.com) na Mwandishi/Mpigapicha wa MMG. 
   
  "Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifikisha siku ya leo ya kuzaliwa kwangu, hakika yeye ni mwema maana amenivusha katika milima na mabonde na amekuwa akinifanyia mambo makubwa katika maisha yangu.
   
   Pili nipende kutoa shukrani kwa familia yangu, ndugu jamaa na marafiki wote ambao mmekuwa bega kwa bega pale ambapo nimekuwa nikikwama mmekuwa mkinishika mkono na kunivusha hakika sina cha kuwalipa bali mwenyezi Mungu awaongezee busara, upendo na amani. 
   
  Tatu, kabisa nipende kutoa shukrani za pekee kwa Mke wangu, Mama yangu Mzazi, baadhi ya ndugu na marafiki ambao bila wao labda nisigekuwa hapa leo, nianze na Familia ya Kajuna Jr (Kennedy), Familia ya Michuzi Media Group ikiongozwa na Ankali Michuzi, Michuzi Jr na Othman hakika najivunia ukarimu na upendo wetu kwangu najivunia kuwa mmoja ya mwanafamilia, 
   
  Familia ya Jackson Mmbando, rafiki zangu Seki David, Edwin David, Portnes, Mwesiga Kyaruzi, Shebby Mpondela, Franklin Alexander, Ally Jamal, Imani Ntila, James Jonathan na Dr. Heri Tungaraza. Wengine ni Raymond Maganga, Myoma Kapya - Chilala, Mike Mukunza, Muhidin Sufian, Bakari Kimwanga, John Bukuku, Abraham Mossi, Sylvia Mwehozi, Leah Mushi, Mary Masinda, Tiba Josephat Lukaza, Ruben (Baba Countinho) na wale wote ambao nimekuwa nikishirikiana nao kwa namna moja au nyingine katika kusaka ugali wetu wa kila siku. 
   
  Mwisho, Shukrani za pekee ziwaendee wanachana wote Tanzania Bloggers Network (TBN) popote mlipo nawaomba tuendelee kushirikiana kwa pamoja, Umoja ni Nguvu.

  Ni mimi Cathbert A. Kajuna.

  10.04.2018

  0 0


  VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali wakiongozwa na Rais mstaafu Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete wameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa (76) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Mzee Mtopa amefariki dunia jana asubuhi ya  Aprili 9 mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

  Kwa mujibu wa ratiba ya maziko ya mzee Mtopa anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani  Kijijini kwake Nanjilinji wilayani Kilwa mkoani Lindi ambako leo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walijitokeza kumuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Mwili wa mzee huyo ulianza kuagwa saa mbili asubuhi na kuendelea hadi mchana hospitalini hapo.  Kabla ya kuaga mwili huo viongozi kadhaa akiwamo Mzee Mwinyi, mzee Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana walishiriki kwenye ibada iliyofanyika katika msikiti uliopo katika Hospitali hiyo ya Muhimbili.
  Mbali ya viongozi hao walikuwepo viongozi wengine kadhaa ambapo kila mmoja aliyepata nafasi ya kumzungumzia Mtopa wamesema kifo chake ni pengo kwa CCM kwani alikuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele.
  Baada ya kuagwa kwa mwili huo safari ya kuusafirisha mwili huo ilieneza kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Lindi.  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii  Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete,  Rais Mstaafu, Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa leo katika Mskiti wa Mhimbili , jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.
  Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Dk.Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa mtoto wa marehemu wa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa mara baada ya kuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika viunga vya hospitali ta Taifa Muhimbili baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa.

  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  RAIS Dk. John Magufuli kesho anatarajia kuzindua rasmi  Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika Ukumbi wa Mikutno wa Jakaya Kikwete ulioko Ikulu, Dar Es Salaam. 

  Rais mstaafu Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya JMKF na uzinduzi huo rasmi utahusisha maofisa waandamizi wa Serikali, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania na hasa mabalozi wa Afrika ambako Taasisi hiyo inalenga kufanya kazi mbali ya Tanzania, wakuu wa taasisi mbali mbali za kimataifa, wadau wa Taasisi ya JMKF, wakuu wa asasi zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) na wakuu wa taasisi za kijamii wakiwemo viongozi wa dini.

  Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Pioneer Communications Limited kwa niaba ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)imesema uzinduzi huo  utafuatiwa na chakula cha jioni ambacho Rais Magufuli atawaandalia wageni watakaohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi, akiwemo Rais Kikwete mwenyewe na mkewa Mama Salma Kikwete.

  "Taasisi ya JMKF iliyosajiliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka Februari, 2017, ilianza kazi Machi, mwaka jana wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Wadhamini ya Kimataifa ya Taasisi hiyo ilipofanya kikao chake kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt mjini Dar Es Salaam,"imesema taarifa hiyo.

  Imeongeza taasisi hiyo inayolenga kufanya kazi na kuelekeza nguvu zake katika maeneo matano, itaanzia na maeneo matatu ambayo ni Afya ya Mama na Mtoto, Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji wa Wakulima Wadogo katika maeneo ya vijijini na mashambani katika jitihada zao za kujinasua katika umasikini ama kupunguza athari na madhara ya hali ya umasikini.

  "Mheshimiwa Kikwete anasaidiwa katika uendeshaji wa Taasisi hiyo na Bodi ya Wadhamini yenye sura ya Kimataifa ambayo wajumbe wake wanatoka nchi za Tanzania, Marekani, Afrika Kusini, Ureno na Malaysia.Wadhamini hao ni Balozi Ombeni Sefue aliyepata kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi wa Tanzania katika  Canada na Marekani.

  "Pia Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa miaka mingi, Profesa William Mahalu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustine mjini Mwanza na Balozi Mwanaidi Sinare Majar ambaye amepata kuwa Balozi wa Tanzania katika Uingereza na Marekani,"imefafanua.

  Wengine ni Mfanyabiashara maarufu Abubakar Saidi Bakhressa, Balozi Charles R. Stith aliyepata kuwa Balozi wa Marekani katika Tanzania, Msomi na Mtumishi wa Umoja wa Mataifa Bwana Carlos Lopez, Waziri mwandamizi katika Serikali ya Malaysia, Dato Sri Idris Jala na  Mtaalamu wa Masuala ya Fedha kimataifa Genevive Sangudi, Mtanzania mwenye makazi yake Afrika Kusini na Marekani.

  Kutokana na kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Udhamini Machi mwaka jana, wataalamu mbali mbali pamoja na washauri wa kila aina, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa JMKF,  Omari Issa wamekuwa katika matayarisho makubwa ya kuandaa nyaraka mbali mbali za msingi za kuongoza dira na dhima ya Taasisi hiyo kwa ajili ya uzinduzi rasmi na kwamba shughuli hiyo ya Ikulu itatangazwa moja kwa moja kwenye Televisheni ya Taifa ya TBC na vyombo vingine.

  0 0


  Waandisi na mafundi sanifu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo ya tathmini ya mazingira katika miradi ya barabara,yanayoendelea mjini Morogoro.
  Mhandisi Melania Sangeu akiwasisitiza jambo washiriki wa mafunzo ya tathmini ya mazingira katika miradi ya barabara,yanayoendelea mjini Morogoro,ambao ni waandisi wa mafundi sanifu.
  Mhandisi Chacha Harun,akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya tathmini ya mazingira katika miradi ya barabara,kwa mafundi sanifu yanayoendelea mjini Morogoro.
  Washirikiwa mafunzo ya tathmini ya mazingira katika miradi ya barabara,yanayoendelea mjini Morogoro wakimsikiliza mmoja wa watoa mada Mhandisi Albina John(Hayupo Pichani) wakati wa mafunzo hayo.

  ……………….

  Imeelezwa kuwa mafanikio endelevu katika sekta ya barabara na uchukuzi hapa nchini yatafikiwa endapo mkakati wa muda mrefu unaohitaji juhudi za pamoja za wadau wote utatekelezwa kikamilifu.

  Mkakati huo ni kuwawezesha wadau wote katika jamii kuelewa umuhimu wa barabara na kuhakikisha mazingira yanayozunguka barabara hizo yanalindwa na kutuzwa na kila mmoja katika nyanja yake.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi msaidizi wa idara ya Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Melania Sangue wakati akifungua mafunzo ya tathimini na usimamizi wa mazingira kwa mafundi sanifu wa barabara, mafunzo yanayoendelea mjini Morogoro.

  Mhandisi Sangeu amewataka mafundi hao kutoa elimu wanayoipata kwa wadau wote wa barabara ili kuwezesha ujenzi na usimamizi wa barabara kuzingatia kanuni za mazingira na maendeleo endelevu.

  “Hakikisheni miradi yote ya barabara inafanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira Enviromental Impact Assesment EIA,ili iwe endelevu na isiyo changia madhara kwa jamii,”alisisitiza mhandisi huyo.

  Aidha pamoja na maagizo hayo amewataka wataalamu hao wa ujenzi kusimamia ujenzi wa barabara na hifadhi za barabara kwa kudhibiti uchimbaji wa mawe na mchanga kandokando ya barabara hali inayochangia uharibifu wa barabara kwa muda mfupi pindi ujenzi unapokamilika.

  Kwa upande wake mdau wa mazingira Mhandisi Mary Assey amewataka mafundi hao sanifu kuhakikisha kuwa mafuriko,mmomonyoko wa udongo katika miradi ya ujenzi vinadhibitiwa wakati wote wa ujenzi na mara baada ya ujenzi huo kukamilika.

  Mhandisi huyo amesema miradi mingi ya barabara inapokamilika wakandarasi wamekuwa wakiacha jamii zikiathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira na kwamba kama wajenzi wa barabara hawatachukua hatua madhubuti za kudhibiti maeneo walikofanya uchimbaji mchanga athari zitakuwa endelevu.

  Naye mtaalamu wa ujenzi Mhadisi Chacha Harun kutoka wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano amesema kwa sasa wamejipanga kuhakikisha uharibifu wa mazingira unaosababishwa na miradi ya ujenzi wa barabara unadhibitiwa na miradi hiyo kuwa endelevu kwa jamii husika.

  Mafunzo hayo yametolewa kwa wahandisi 425 na mafundi sanifu 466 kutoka miko yote ya Tanzania bara ikiwa ni mkakakati wa kuhakikisha ujenzi wa barabara unakwenda sambamba na usimamizi wa usalama wa mazingira katika miradi yote nchini.

  0 0


  *Mapato yapanda kutoka sh. milioni 147 hadi sh. milioni 714

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Mererani kutasaidia kuongeza mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite.

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

  Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo uliozinduliwa Aprili 6, mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutasaidia pia kudhibiti ulanguzi na biashara ya magendo pamoja na kuimarisha usalama kwenye mgodi, kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Tanzanite.

  “Kukamilika kwa ujenzi huo pia kutasaidia kuongeza mapato ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, Serikali imekusanya takriban shilingi milioni 714 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi milioni 147.1 kwa mwaka mzima wa 2017,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema kabla ya ujenzi huo, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya madini ya Tanzanite yaliyokuwa yanazalishwa kila mwaka, yalitoroshwa kwa njia za panya na Serikali yetu haikuambulia chochote. “Hii ni kutokana na kukosekana udhibiti wa kutosha wa madini ya tanzanite kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwa wauzaji,” alisema.

  Alisema mbali na kuwepo kwa eneo la wachimbaji ndani ya ukuta wa Mererani, pia kutajengwa maduka ya Tanzanite na viwanda vya kuongeza thamani, hususan vya ukataji, uchongaji na ung’arishaji. Vilevile, kutakuwa na maeneo ya burudani ambayo yatastawisha zaidi biashara ya Tanzanite na kuwavuta watalii wengi kwenda kutembelea eneo hilo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) itakayokuwa na urefu wa km. 1,219 utarahisisha usafiri wa mizigo na abiria na kuongeza itaongeza biashara hapa nchini pamoja na nchi za jirani.

  Waziri Mkuu alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kusafirisha tani milioni 17 kwa mwaka, ikilinganishwa na tani milioni tano za sasa na kwamba utaongeza mapato kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kutunza barabara ambazo zimekuwa zikiharibika mapema kutokana na kusafirisha mizigo mizito.

  “Reli hii ya kisasa itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa takriban tani 10,000 kwa mara moja, ambayo ni sawa na malori (semi trailers) 500 yenye uwezo wa kubeba tani 20 kila moja. Hii, itasaidia sio tu kutunza barabara zetu bali pia kupunguza gharama za kukarabati barabara hizo mara kwa mara,” alisisitiza.

  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Yusra Ali Ramadhani (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 83 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.


  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Hamisi Mohammed Yusuph (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00#  tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
  Baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wakitazama simu zao aina ya Tecno R6 walizoshinda baada ya kukabidhiwa zawadi hizo jana katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo.  
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakabidhi washindi 84 wa wikii hii katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus  iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam.


  • Zaidi ya simu 300 na bonasi za intaneti bado zinashindaniwa!
  Dar es Salaam, Aprili 10, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imewazawadia wateja wake 84 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
  ‘Katika promosheni hii murwa, Tigo inatoa bure jumla ya simu janja 12 kila siku.  Pamoja na haya, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter,’

  ‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo, ambapo kufikia sasa tumewazawadia wateja 756 simu hizi janja zenye uwezo wa 4G’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.

  Kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.

  Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.

  0 0

  Awataka waulinde, aonya sukari isiwe sababu


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waulinde Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na akawaonya wasitumie Bunge hilo kuupotosha.

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

  Waziri Mkuu amesema mjadala ulioibuka jana kuhusu suala la Muungano haukuwa na afya na kwamba hatarajii kuona hali hiyo ikijirudia tena Bungeni kuhusiana na suala la Muungano.

  “Mjadala wa jana sijaupenda kabisa na wala haukuwa na afya, ulikuwa ni malumbano baina waheshimiwa wabunge wawili. Hatuzuii Mhe. Mbunge kuuliza jambo ili apate ufafanuzi lakini pia haturuhusu mtu na mtu watumie Bunge kupotosha ukweli wa mambo,” alisisitiza.

  Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba kuna maboresho ambayo yanafanywa hivi sasa na Serikali za pande zote mbili lakini akatumia fursa hiyo kulihakikishia Bunge kwamba majadiliano bado yanaendelea kwenye vikao halali vya SMT na SMZ ambavyo vinaongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha malumbano hayo, Waziri Mkuu alisema kiini cha malumbano hayo ni suala la uagizaji sukari kutoka nje ya nchi ili kufidia upungufu wa sukari uliopo nchini (gap sugar). Alisema katika kutimiza azma hiyo, Serikali haiangalii kama muagizaji ametoka Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar.

  Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika mwaka 2016, upungufu uliojitokeza ulikuwa tani 140,000 lakini waagizaji waliopewa vibali walikuwa wawili kutoka Zanzibar, watatu kutoka Bara na kiwanda cha sukari cha Mahonda kilipewa kibali cha kuagiza tani 390.

  “Katika mwaka 2017, gap sugar ilikuwa tani 140,000 na waliopewa vibali walikuwa ni wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara, lakini kwa mwaka huu (2018) gap sugar ni tani 135,000. Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii tumewapa vibali wenye viwanda ndiyo waagize sukari kutoka nje. Kwa hiyo, jambo hili la sukari lisivuruge Muungano wetu,” alisisitiza.

  Waziri Mkuu alisema nia ya Serikali ni kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini ili nchi ijitegemee na kawataka Mawaziri wa Biashara wa Zanzibar na Tanzania wawe makini ili sukari inayoagizwa nje isije kufurika soko la ndani kwa sababu gharama za uzalishaji sukari ya ndani ni kubwa.

  0 0
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akijibu hoja za Wabunge walizochangiana kuhusu Ofisi yake wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni Dodoma Aprili 10, 2018.
  B2
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akijibu hoja za wabunge zinazohusu Ofisi hiyo Aprili 10, 2018 Bungeni Dodoma.
  B3
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akijibu hoja zinazohusu masuala ya watu wenye ulemavu Bungeni Dodoma.
  B4
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Naibu wake Mhe.Antony Mavunde anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana Bungeni Dodoma.
  B5
  Manaibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu wakiteta jambo wakati wa Mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma, aliyekaa ni Mhe.Stella Ikupa anayeshughulikia watu wenye Ulemavu na Mhe.Antony Mavunde (Kazi, Ajira na Vijana)
  ????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Mhe.George Simbachawene (Mb) nje ya Ukumbi wa Bunge Aprili 10, 2018
  ????????????????????????????????????
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akizungumza na Mhe.George Simbachawene wa kwanza kushoto Katibu Mkuu masuala ya Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip Mpango nje ya Viwanja vya Bunge Dodoma.

  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  0 0


  MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
  PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza wakati akiwakaribisha wageni kwenye sherehe hizo zilizofanyika kwenye viwanja v ya Bandari Jijini Tanga
  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio mbalimbali kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald NgaireAfisa Tehama wa Bandari ya Tanga Ally Isaka akimueleza kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival SalamaMeneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Bandari leo akiwa ameambatana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdallah na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha SalimMkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akisalimiana na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga
  Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias MwilapwaSehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa Zoezi la utoaji wa damu likiendelea kwenye sherehe hizo

  SERIKALI mkoani Tanga imesema kuwa haitakuwa na simile na wananchi watakaokamatwa kujihusisha na kuingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu kwani wanachangia kuikosesha mapato serikali. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo.

  Alisema kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia bandari bubu kupitishia bidhaa za magendo ambazo sio salama kwa matumizi ya binadamu. Katika hili hatutakiwa na msamaha wala kumuonea mtu haya tukikukamata chombo tutakitaifisha pamoja na mali zake huku muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheri nilazima wananchi wajifunzi kuona umuhimu wa kutumia bandari rasmi”alisema DC Mwilapwa.

  Aidha aliitaka Mamlaka ya usimamizi wa bandari Mkoani Tanga kuhakikisha utendaji kazAwali Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kuwa maboresho ya vifaa na vitendea kazi katika bandari hiyo yameweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka siku kumi hadi nne.

  Alisema kuwa kuhudumia shehena za mizigo katika kipindi kifupi kumesaidia kupunguza gharama kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo . “Licha ya kuhudumia mizigo kwa awamu mbili lakini uwepo wa vifaa umesaidia kuboresha uwezo wa bandari yetu ya kuhudumia mizigo kwa ufanisi zaidi”alibainisha Mkuu huyo.

  Sherehe hizo zinakwenda sambamba na kauli mbiu Bandari za TPA ni chachu ya uchumi Viwanda na Ustawi nchini Tanzania (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kitabu kutoka kwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza kamati za Bunge hilo leo, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka tarehe 26 Aprili, 2018 Mjini Dodoma.
  V25A8531
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  V25A8704
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na bendera ya Bunge hilo walioongozwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (watatu kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya kamati za Bunge hilo linaloanza leo tarehe 10 Machi, 2018, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka Tarehe 26 Aprili, 2018 vitakavyofanyika Mjini Dodoma.
  V25A8558
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  V25A8617
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya kamati za Bunge hilo linaloanza leo, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka Tarehe 26 Aprili, 2018 vitakavyofanyika Mjini Dodoma.
  PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0  ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND NCHINI 11-13 APRILI 2018


  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland, Mhe. Prof. Jacek Craputowicz atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 hadi 13 Aprili 2018.  Katika ziara hiyo, Prof. Craputowicz pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) Jijini Dar Es Salaam tarehe 12 Aprili 2018.  Viongozi hao watajadili namna ya kuboresha mahusiano na mashirikiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Poland, hususan katika eneo la uwekezaji na biashara.   


  Poland ni moja ya nchi zinazounga mkono Sera ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020. Katika kuunga mkono Sera hiyo, Serikali ya Poland imetoa mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 110 kwa Serikali ya Tanzania.


  Kati ya fedha hizo, Dola za Marekani milioni 55 zimetumika kujenga kiwanda cha kuunganisha matrekta Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani ambacho kimeshaanza kazi na Dola za Marekani milioni 55 ni kwa ajili ya kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya kilimo katika mikoa minane ya Rukwa, Katavi, Manyara, Ruvuma, Dodoma, Shinyanga, Njombe na Songwe.


  Prof. Craputowicz na mwenyeji wake watashiriki hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa ofisi ya Ubalozi wa nchi hiyo zilizopo nyumba namba 15, mtaa wa Mtwara, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Aprili 2018. Poland ilifungua upya Ubalozi wake nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya.


  Baada ya ufunguzi viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi hizo saa tano asubuhi. 


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

  Dar es Salaam

   10 Aprili, 2018  0 0


   Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN  (Katikati)akizungumza na wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Tecno ambayo ni Tecno CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3.
  Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN (Wapili kutoka kushoto) wakionesha simu aina ya Tecno  CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3 mara baada ya kuzindua simu hiyo.
  KAMPUNI ya simu za mkononi inayofanya vizuri barani Afrika inaendelea kutanua soko lake baada ya kuzindua simu mpya TECNO CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3, ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘TECNO CAMON’ iliyozinduliwa nchini NIGERIA (LAGOSI), Tarehe 5/4/2018.

  Katika uzinduzi huo TECNO imejihakikishia uzalishaji na usambazaji wa simu zenye technolojia na ubora zaidi katika masoko zaidi ya 40 hasa katika nchi za Afrika. Kampuni ya simu ya TECNO hivi karibuni imeweza kuingia mkataba na moja kati ya kampuni bora katika upande wa mitandao (GOOGLE) iliyozindua mfumo mpya ya uendeshaji wa simu za mkononi Android 8.0Oreo (Go edition), utakaotumika katika matoleo yote ya TECNO kwa ndani ya mwaka 2018.

  Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING Sambayo ni kampuni mama ya TECNO, Bwana Andy VAN amesema, “TECNO haizalishi simu kwa kuzingatia maoni ya wafanyakazi wetu tu, ila kampuni inazingatia zaidi ushauri na maoni ya watumiaji ili kuwapatia kilichobora zaidi ukilinganisha na zilizopita”.older | 1 | .... | 1557 | 1558 | (Page 1559) | 1560 | 1561 | .... | 1898 | newer