Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1553 | 1554 | (Page 1555) | 1556 | 1557 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Bw. Pang Xin Xing kabla ya mazungumzo yao, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Pang Xin Xing (watatu kushoto) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa aWaziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Star Media Tanzania Limited,Wang Xiao Bo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Makampuni ya Star Times Group,Zhang Ye na kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Star Media Tanzania Limited, Juma Suluhu Sharobaro.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  SERIKALI imetenga kiasi cha sh.bilioni 39 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa umeme mkubwa unaotarajiwa kupitishwa kwenye maeneo yao.

  Pamoja na hilo ,baadhi ya miradi ya awali ambayo fidia imechelewa kwa walengwa ,uhakiki tayari umekamilika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi watoe shaka kwani serikali inataka ikabiliane na ubabaishaji.

  Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu alipokuwa akizungumzia suala la fidia kwa baadhi ya wananchi watakaokuwa na haki ya kupatiwa.Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na utagharimu fedha nyingi.

  Subira alielezea mradi unaanzia Rufiji, Kinyerezi,Kibaha na Chalinze na baadaye Dodoma ambapo wananchi watalipwa wakati utakapoanza.“Suala la fidia ni kubwa na kwa ile miradi ya awali ambayo haijalipwa ni kweli kwani baadhi bado hawajalipwa lakini wananchi wasiwe na wasi wasi kwani watalipwa fidia zao mara uhakiki utakapokamilika,” alisema Subira.

  Alielezea ,kwa bajeti ambayo inaendelea kwa sasa zimetengwa kiasi cha sh.bilioni 21 kwa ajili ya fidia kwa laini inayoanzia Kinyerezi, Kibaha, Chalinze na Arusha ya umeme wa KV 400.Kwa mujibu wa Subira,mradi huo ulifanyiwa tathmini 2014/2015 na fidia imechelewa hivyo serikali inaomba radhi kwa hilo.

  "Serikali ina majukumu na vipaombele mengi, haikusudii kuchelewesha bali mwaka unaoendelea wa bajeti zitalipwa tu,” alisema Subira.

  Aidha alisema ,wakati Rais Dk. John Magufuli anaingia madarakani kulibainika kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na wizi mkubwa kwenye suala la fidia kwani walikuwa wakilipwa watu wasiostahili ambapo fedha inayopangwa na serikali inabadilishwa na kuwekwa viwango vingine hasa inapofika ngazi ya wilaya.

  “Walikuwa wanabadili watu wanaopaswa kulipwa wanabadilisha majina na kila kitu hadi picha hata akilipwa anayestahili analipwa kiwango kisichotakiwa hali iliyosababisha hazina kufanya uhakiki,” alifafanua.

  Subira alisema, uhakiki tayari umefanyika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya kucheleweshewa fidia zao bali serikali inataka iondokane na ubabaishaji

  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunz wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
  Baadhi ya walimu mahiri 40 waliochaguliwa kufundisha na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha sita (kutoka shule 11 mkoani Simiyu) na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani humo.
  Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu, wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu.

  Akifungua kambi hiyo Aprili 03 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.

  “Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafundisha na kuwaelekeza na akawataka kujiamini wakati wa mtihani wao wa mwisho.

  Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema Mkoa huo una mpango wa kuondoa daraja la nne na sifuri katika matokeo ya Mitihani ya Taifa, hivyo wanayo matumaini makubwa kuwa, kupitia makambi hayo ya kitaaluma Mkoa utaweza kufikia lengo hilo kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

  “ Tumeamua kuwaleta pamoja wanafunzi ili waweze kunyanyuka kama kundi moja la mama mmoja (Simiyu) na kuweza kupandisha ufaulu, tumewaleta hapa ili kuweza kunyanyua morali wa kazi kuwaleta pamoja anayeweza na asiyeweza ili tuweze kunyanyuka pamoja kama kundi” alisema Mwl.Nestory.

  Amesema katika siku 10 za kambi wanafunzi wa kidato cha sita watapitishwa katika miiko ya watahiniwa wakati wa mitihani kwa kuwa mkoa wa Simiyu unapinga suala la udanganyifu kwenye mitihani, watapitishwa katika maswali na mada ambazo baada ya tathmini ilionekana hawakufanya vizuri katika mtihani wa kanda na mtihani wa Mkoa.

  Akizungumza kwa niaba ya walimu mahiri 40 ambao watakuwa wakiwafundisha na kuwasaidia wanafunzi hao, Mwl.Majaliwa Chibona wa Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu amesema, wamejipanga kuwasaidia wanafunzi katika kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kujiandaa na mitihani wao wa mwisho ili waweze kufaulu.

  Nao baadhi ya wanafunzi wamesema kambi hiyo itawasaidia sana katika kuwajengea hali ya kujiamini kwa kuwa watasaidiwa na walimu katika maeneo yote yanayoonekana magumu kwao, watasaidiana wa kwa wao kupitia makundi na watapewa mbinu zitakazowasaidia kujiandaa vema na hatimaye kufanya vizuri.

  0 0

  TIMU ya soka ya Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), imeichapa bila huruma timu ya soka ya ZSSF 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka.

  Mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa kuzikutanisha timu mbili za mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na ZSSF ambapo lengo la michizo hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya mashirika hayo mawili.

  Mchezo huo uliianza kwa kasi kubwa iliwachukua dakika 4 NSSF kujipatia bao la kwanza baada ya mwamuzi wa mchezo huo Fikiri Yusuph kutoa Penalti baada ya beki wa ZSSF kuunawa mpira katika harakati za kuokoa, mshambuliaji wa NSSF Said Mwinyi aliipiga penalti hiyo na kuipatia timu yake bao la kwanza.


  Kuingia kwa bao hilo la mapema kuliwafanya ZSSF kucharuka na katika dakika ya 10 nusura wajipatie bao la kusawazisha baada ya shuti kali lililopigwa na Juma Mbwana kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa timu ya NSSF.

  ZSSF waliendelea kulisakama lango la NSSF lakini walinzi wa timu ya NSSF wamkiongozwa na beki wa wa timu hiyo Hemed Kagobe waliweza kuondoa hatari hizo na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa timu ya ZSSF.

  Katika dakika ya 27 ya mchezo nusura ZSSF wapate bao la kusawazisha lakini golikipa wa NSSF, Sadick aliweza kuokoa kiki iliyopigwa na Rashid Suleimani na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

  Time hizo zilirndelea kushambuliana kea zamu hadi mapumziko NSSF ilitoka ikiwa inaongoza 1-0.

  Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo ZSSF waliwatoa, Hassani Omar, Abasi Yahaya Abasi, Maulid Suleiman na Hamis Thani na nafsa zao kuchukuliwa na Yusuf Said, Abdulkarim Rajabu, Khamis Haji na Mohamed haji Khamis. 

  NSSF waliwatoa Nassoro Nassor, Ally Chuo, mfungaji wa bao la kwanza Said Mwinyi, Sadick Jongo na nafasi zao kuchukuliwa na Bakari Becco, Mwinyi Mzee, Prosper Lyoba na Shaban Enzi.

  Mabadiliko hayo yalibadilisha sura ya mchezo katika dakika ya 82 mshambuliaji wa timu ya NSSF, Katunguja aliifungia timu ya bao la pili banda ya kupokea pasi kutoka kwa  Mwinyi Mzee aliyeingia kipindi cha pili, kuingia kwa bao hilo kuliongeza kasi ya mchezo ambapo ZFF walikuja juu wakitaka kupata bao angalau la kufutia machozia lakini kikwazo kikubwa alikuwa mlinda mlango wa timu ya NSSF, Sadick ambaye alikuwa nyota ya mchezo kwa kuokoa mashuti yaliyokuwa yakielekezwa langoni mwake.

  Wakati huohuo katika mchezo wa netiboli timu ya NSSF ilingára vilivyo baada ya kuichapa ZSSF kwa jumla ya magoli 23-19 na kunyakua kombe la michuano hiyo kwa mwaka 2018.

  Akizungumza wakati akitoa zawadi kwa washindi wa michezo hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete, alisema kuwa michezo hii imelenga kujenga ushirikiano baina ya mifuko, kuimarisha uhusiano na pamoja na kuboresha afya kwa wadu wa michezo kupitia mifuko hiyo.

  “Lengo la mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa kukutanisha  wanamichezo mbalimbali kutoka katika mashirika  ya ZSSF na NSSF ambapo  kushiriki kwa pamoja michezo mbalimbali pamoja na kutoa zawadi kwa wanamichezo vote walioshiriki katika tamasha hilo."

  ambapo mwakani itafanyika mjini Zanzibar na kuandaliwa na ZSSF watakuwa wenyeji wa michezo hiyo Zanzib imelenga kujenga ushirikiano baina ya mifuko, kuimarisha ushirikiano baina ya ZSSF na NSSF pia imelenga kujenga ushirikiano, uhusiano baina ya wafanyakazi kutoka ZSSF pamoja na NSSF  katika kuimarisha ushirikiano.
  Wanamichezo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.
  Wanamichezo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.

   Mapokezi.
  Ofisa wa NSSF, Pili Mogella (kulia), akimkaribisha Ofisa wa ZSSF.  
   ZSSF wakiwasili bandarini.
   Wachezaji wa ZSSF wakiwa ndani ya basi.

  Kocha wa timu ya netiboli ya NSSF, Joseph Ngánza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. 
   Kocha wa timu ya ZSSF, Hadia Ahmada, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
  Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, akikagua timu ya netiboli ya ZSSF.
  Meneja Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro akikagua timu ya netiboli ya NSSF.
   Kikosi cha timu ya ZSSF.
  Kikosi cha NSSF.
  Mshambuliaji wa timu ya netiboli ya ZSSF, Mwasiti Vita, akiwa katika harakati za kufunga huku Amina Jumanne (kushoto), wa NSSF akijaribu kumzuia katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
   Mchezaji wa NSSF, Maliti, akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa ZSSF, Yasinta (GD).
   Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akichuana na mchezaji wa ZSSF, Fatuma Sule (kushoto).
    Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akimiliki mpira.
   Timu ya netiboli ya NSSF wakiwa katika mazoezi.
  Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro (kulia), akizungumza na wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa netiboli ya ZSSF.
   Timu ya NSSF ikiwa mapumziko.
  Mashabiki wa timu ya netiboli ya NSSF. 
   Wachezaji wa ZSSF wakiwa katika mazoezi
   Kocha wa timu ya soka ya NSFF, Sanifu Lazaro.
  Zawadi za washindi.
  Mshambuliaji wa NSSF, Katunguja, akimtoka Rashid Suleiman wa ZSSF (kulia).
  Shaban Enzi (kulia), akichuana na Ismail Hubi wa ZSSF.
  Ally Chuo wa NSSF (chini), akichuana na Rajabu Said wa ZSSF.
  Wachezaji wa NSSF wakishangilia bao la pili la timu hiyo.
  Mchezaji wa ZSSF, Seif Hafidh (kulia), akichuana na Said Mwinyi wa NSSF.
   Nahodha wa timu ya netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Pili Mogella, akipokea kombe la Ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete (kushoto), baada ya kuifunga ZSSF magoli 23-19  katika mchezo ulifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya soka ya NSSF, Mzee Mfaume, baada ya kuwafunga ZSSF mabao 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
   Wachezaji wa timu ya soka ya NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa ZSSF, Abdallah Mbwana.
  Maofisa wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.
  Maofisa wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.

  0 0

  Kwaya ya Vijana KKKT-Kimanga wakiimba mbele ya wakazi wa mji wa Bariadi katika uwanja wa Halmashauri,siku ya jumatatu ya pasaka.
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Joshua Mlelwa akiimba mbele ya mashabiki wake ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Baridi,ndani ya jumatatu ya Pasaka mkoani Simiyu.
  Washabiki wa muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo
  Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu Sifaeli Mwabuka akiwaimbisha washabiki wake mapema mwishoni mwa wiki jumatatu ya pasaka ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Bariasi mkoani Simiyu.Tamasha hilo lilianzia mkoani Mwanza na baadaye kufanyika simiyu na jumapili hii ndani ya mkoa wa Dodoma katika uwanaja wa Jamuhuri.
  Wapenzi wa muziki wa Injili wakifurahia waimbaji katika tamasha hilo la Jumatatu ya pasaka mjin Bariadi mkoani Simiyu.
  Mwimbaji machachari wa nyimbo za Injili Martha Baraka akiimba pamoja na mashabiki wake
  Baadhi ya Wapenzi wa nyimbo za Injili wakishangilia vilivyo mara baada ya muimbaji Martha Baraka kushuka jukwaani na kuwafuata mashabiki wake uwanjani
  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akisalimia mashabiki akiwa na waimbaji pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu katika tamasha la Pasaka lililofanyika leo kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu

  Ilikuwa ni buradani na furaha kwa wakazi wa Bariadi na vitongoji vyake wakati waimbaji wa nyimbo za injili walipokuwa wakitumbuiza uwanjani hapo
  Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasa hilo
  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akizungumza na Wakazi wa Bariadi waliojitokeza kwenye tamasha la Pasaka lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
  Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakiburudika wakati waimbaji wa nyimobo hizo walipokuwa wakitumbuisha katika tamasha hilo
  Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiendelea kuwateka mashabiki wake katika tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
  Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kibao chake kipya cha “Lazima Wakae” huku akicheza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka katika tamasha la Pasaka lililofanyika jumatatu ya Pasaka kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

  0 0


  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge alipozungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda ya Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (katikati) akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) alipofanya ziara fupi kukagua maeneo yanayoweza kuwekewa miundombinu muhimu na kutumika kama kituo cha daladala cha Mjini, jana Aprili 3, 2018. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Ludigija Ndwata. 


  Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi

  MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameelekeza matumizi ya kilichokuwa kituo Kikuu cha Mabasi madogo maarufu kama Daladala cha Jamatini Mjini Dodoma kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo yaendelee kama kawaida wakati Manispaa ikiandaa eneo mbadala.

  Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza ‘ruti’ za Daladala zifupishwe kama ilivyokuwa awali, na kwamba upangaji wa ‘ruti’ ndefu ujadiliwe upya na wadau wote wanaohusika na endapo utakubaliwa na wengi ndipo utekelezaji wake uanze.

  Dokta Mahenge ametoa maelekezo hayo leo Aprili 3, 2018, alipokuwa akizungumza na wadau wa usafirishaji katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani cha muda kilichopo Nanenane Manispaa ya Dodoma baada ya kituo hicho kufungwa wiki iliyopita kwa ajili ya kupisha mradi wa Reli ya Kisasa.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano na wadau wote ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMTRA), Manispaa, Jeshi la Polisi, na Shirika la Reli ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, na kwamba matumizi ya stendi hiyo yataendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia sasa, kipindi ambacho Manispaa itatakiwa kuwa imeshapata na kuandaa stendi mbadala.

  Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema Manispaa imepokea maagizo yote na itahakikisha inaandaa eneo kwa ajili ya Stendi ya Mabasi madogo Mjini katika kipindi cha miezi miwili kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa.

  Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza mabasi yote yanayosafirisha abiria Mikoa mbalimbali Nchini kupakia na kuanzia safari zao katika kituo Kikuu cha mabasi ya muda kilichopo Nanenane na Kampuni itakayokiuka itachukuliwa hatua kali za Kisheria.

  “Namuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa kuwa, kuanzia kesho mabasi yote yauze tiketi na kuanza safari zao hapa katika kituo hiki Kikuu cha mabasi cha muda cha Nanenane…hakuna Mkubwa wala mdogo katika kutoa huduma kwa Wananchi” alisisitiza Dkt. Mahenge.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akikagua ujenzi wa Vivuko katika barabara ya Namelock-Loltepes-Sunya yenye urefu wa Km 88 iliyopo katika Wilaya ya Kiteto.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Vivuko katika barabara Namelock-Sunya wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.
  Huu ni muonekano wa baadhi ya Kivuko kinachojengwa katika barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya ambavyo Waziri Jafo amesimamisha ujenzi wake kutokana na dosari zilizojitokeza.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya yenye urefu wa Km 88 wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.  Nteghenjwa Hosseah, Kiteto

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesimamisha ujenzi wa vivuko vyote katika ujenzi wa barabara ya Namelock-Loltepes Sunya yenye urefu wa Km 88.1 inayojengwa katika Wilaya ya Kiteto na Mkandarasi Deniko Constraction Ltd.

  Waziri Jafo ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa ziara yake Wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kubaini mapungufu makubwa katika ujenzi wa vivuko zaidi ya kumi alivyovipitia ndipo alipoagiza kusitisha ujenzi huo mara moja hadi hapo Wataalamu wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) watakapofika kukagua barabara ma kuwasilisha ripoti.

  Aidha kutokana na hali hiyo ya aligiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo Deniko Construction sambamba na Mhandisi Mshauri Luptain Consult Ltd, Mhandisi Consulting Engineers pamoja na ACE Consultant kufika Ofisini kwake mara moja kutoa maelezo ya kina ya mapungufu hayo yaliyojitokeza katika ujennzi wa barabara hiyo.

  “Ni mara ya tatu sasa nakuja kukagua Barabara hii na kila mara nabaini changamoto tofauti sjui kuna tatizo gani nahitaji kusikia zaidi kutoka kwa wataalamu wa pande zote ili tutafute suluhisho kwa pamoja”Alisema Jafo.

  Aliongeza kuwa hapo awali Barabara hii iligawanywa kwa wakandarasi wajenzi wawili ambaye ni huyu Deniko alikuwa anajenga upande mmoja wenye Km 44 na Km 44 zilizobakia alipewa Maginga Construction ambaye alishindwa kabisa kazi hii ndipo nilipoagiza taratibu zifuatwe ili kuvunja mkataba wa awali na kazi ile apewe Mkandarasi mwingine.

  “Kazi hiyo aliongezewa Deniko Construction ambaye kwa sasa ndiye anayejengwa barabara hii yote yenye Km 88. Hapo awali kazi yake ilionekana nzuri sana na ya kuridhisha lakini baada ya mvua za msimu huu mapungufu makubwa yamebainika hasa katika vivuko vyote vilivyojengwa haviendani na mahitaji ya barabara hii” Alisema Jafo.

  Naye Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kiteto Elias Paul alisema kuwa tatizo lililobainika katika ujenzi wa vivuko hivyo ni Vivuko hivyo haviendani na wingi wa maji ya maji yanayopita na vipenyo vya vivuko ni vidogo hivyo havina uwezo wa kuhimili maji na takataka zingine zinazotakiwa kupita hapo na ni rahis sana kuziba na hata kivuko chote kubebwa na maji ndani ya kipindi kifupi.

  Mradi wa ujenzi wa barabara ya Nmelock – Loltepes – Sunya unatekelezwa na Serikali kupitia Fedha za wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) chini ya mpango wa (FEED FOR FUTURE) unaotekelezwa katika Wilaya Nne Nchini ambazo ni Kilombero, Mvomero, Kongwa na Kiteto.

  Wilaya ya Kiteto kupitia kwa Wakala wa Babarabara za Mijini na Vijiji (TARURA) inahudumia mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa Km 1,088.35 kati ya barabara hizo km 2.8 ni za Lami, Changarawe Km 132 na Udongo Km 955.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Mtalaam wa Bidhaa wa Tigo,  Jacqueline Nnunduma (kulia) wakiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi wa promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Gladness Mori (alieyeketi)
  zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Diana Pumpuni  zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Charles Shabani  zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 

  Nyaka Nyaka Bonus - Promosheni ya Tigo Inayoongeza Matumizi ya Intaneti Nchini

  • Zaidi ya simu 400 na bonasi za intaneti bado zinashindaniwa!
  Dar es Salaam, Aprili 5, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania inazidi kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti nchini baada ya kuwazawadia wateja wake 676 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
  Katika promosheni hii murwa ambapo Tigo inatoa jumla ya simu janja 12 kila siku, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter.

  ‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.

  Akizungumza katika hafla kama hiyo iliyofanyika mjini Morogoro leo, Mtalaam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G.

  ‘Tunataka kila mtu awe sehemu ya mabadiliko makubwa yanayotokana na kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kufurahia huduma bora zenye uwezo wa kubadili maisha zinazotopatikana katika mtandao wetu wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.

  Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.

  ‘Tunawaasa wateja wetu kuchangamkia fursa hii kubwa ya kuwa sehemu ya mageuzi ya ulimwengu wa kisasa wa kidigitali kwa kununua bando intaneti kupitia *147*00# ili wajipatie bonasi za intaneti pamoja na nafasi ya kujishinidia simu janja aina ya Tecno R6 kutoka Tigo.’ Woinde alibainisha.


  0 0


  Food safety is one of the most important angle of human survival, Scientific research over the last decades has shown that a diet rich in fruits and vegetables is protective against many cancers and lowers the occurrence of coronary heart disease. This has contributed to substantial increase in consumption of fresh fruits and vegetables.
  The importance of fresh fruits and vegetables for human health, together with their marked increase in the year-round availability from a global market, has contributed to the substantial increase of their consumption.
  However, the recent increase in reports of food borne illness and outbreaks linked to fresh fruits and vegetables as a result of microbial infection has raised concerns from public health agencies and consumers about the safety of these products, more the less due to a higher rate of fruits and vegetables consumption a threat towards the consumers raised eyebrows of COLEACP and SOLIDARIDAD to gather key number of stakeholders to mention few among them being Tanzania Bureau of Standards (TBS), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) and farmers discuss about fruits and vegetables threats and safety as whole in Dar es salaam and together agreed on the following points as a measure
  a) importance of good health and hygiene for personal health and food safety;
  b) importance of hand washing for food safety and the importance of proper hand washing techniques;
  c) importance of using sanitary facilities to reduce the potential for contaminating fields, produce, other workers, and water supplies; and
  d) techniques for hygienic handling and storage of fresh fruits and vegetables by transporters, distributers, storage handlers and consumer
  e) importance of tidy and developed environment

  But also vowed each stakeholder at a respected area of technicality to make sure they be ambassadors and key participants to make sure the goal having safe food including fruits and vegetables is achieved.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue, ameitaka Menejimeti ya Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano wa kusimamia ujengaji wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira. 

  Chezue amesema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wakati akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo.

   “Kuna wakuu wa idara na vitengo wanaingia moja kwa moja kutokana na idara zao msisubiri kuambiwa fanya kitu Fulani jitume na washirikishe waliochini yako ili kufanikisha lengo hili kwani uwanja huo ni wa Halmashauri na si Mkurugenzi pekee yake ”Amesema Chezue. 

  Aidha Mkurugenzi amesema uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutokana na kukodisha Hostel, kukodisha vibanda vya biashara na viingilio vya milangoni. Pia kuinua kipato cha wajasiriamali ambao watapata fursa ya kufanya biashara wakati wa michezo, na jamii itapata fursa ya kuziona timu mbalimbali. 

  Vilevile amesema lengo la kujenga uwanja huu ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana wa Ruangwa kwenye michezo mbalimbali ili kuweza kupata ajira kwani michezo kwa sasa ni ajira. “Uwanja huo utatumika kwa michezo ya kitaifa na kimataifa kwasababu vipimo vyake ni vya kimataifa”Amesema Chezue. Naye Afisa Michezo wa Wilaya Simon Mwambe amesema kwasasa kazi zinaendelea wameishapeleka mchanga kwa ajili ya kufyatua tofali za kujengea ukuta katika uwanja huo. 

  “Tumeisha chimba msingi wa kujenga ukuta, tuna cement za kutosha na maji yapo tumefunga pampu kwenye kisima kilichochimbwa uwanjani hapo na kesho zoezi la kufyatua tofali litaanza” amesema Mwambe. Hata hivyo Afisa Michezo amesema suala la kuazima vitendea kazi kwa watu binafsi linasababisha kazi zisimame kwa sababu wakati vifaa vinaenda kukodiwa na muhusika anakuwa amekodisha au anatumia kwa shughuli zake.

  0 0

  Na Verdiana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge

  WASOMI na wananchi wapenda maendeleo waishio nje na ndani ya Kijiji cha Butata wameungana pamoja ili kufanikisha ujenzi wa zahanati katika kijiji chao ili kuondoa adha kubwa ya ukosefu wa huduma za kiafaya kijijini hapo.

  Awali akizungumza na Msaidizi wa Mbunge ambae ni mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Butata Ndugu Cleophace M. Kasala ameeleza kuwa Wananchi wa Kijiji cha Butata wamekuwa na muamko katika suala la ujenzi wa zahanati hata kufikia hatua ya kuhamasishana kwa kuchangia nguvu kazi ili kuwaunga mkono ndugu zao waliojitolea kuwachangia mifuko ya saruji na fedha za kujengea zahanati hiyo.

  "Wananchi baada ya kupata Wafadhili ambao ni Wazawa wa Kijiji cha Butata wao wamehamasika na kujitolea kuchimba msingi, kusomba mawe, mchanga n.k"

  Kwa upande wake Amina Kasaka ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Butata ameeleza kuwa, wao kama akina mama kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu sana katika upatikanaji wa huduma za afya. Ameongezea kuwa hali hiyo imekuwa ikihatarisha maisha ya mama na mtoto na hata wazee.

  Naye Diwani wa Kata ya Bukima Mh. January Simula ameeleza mpango kazi wa Kata yake katika ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji. Katika kutekeleza Ilani ya CCM, wamefanikisha kwa vijiji viwili ambapo hadi sasa wana zahanati moja ya Bukima na ya pili wameanza ujenzi wake Kijijini Butata. Pia Serikali ya Kata hiyo imeanza hatua za upanuzi wa Zahanati ya Bukima kuwa Kituo cha Afya cha Kata.

  Katika kulifanikisha hilo, Diwani amesema yuko bega kwa bega na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. S. Muhongo kwa hamasa na michango yake kwenye sekta za Afya, Elimu na Kilimo ikiwa ni vipaumbele vya Jimbo la Musoma Vijijini.

  Ofisi ya Mbunge imesema inashirikiana na wananchi wapenda maendeleo wa Kijiji cha Butata kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo.

  Picha ya hapo chini inaonyesha ujenzi wa Zahanati ya Butata ikiwa kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.

  Ofisi ya Mbunge
  www.musomavijijini.or.tz

  0 0

  Kikosi cha Usalama barabarani kimesema sheria zilizopitwa na wakati zimetajwa kuwa chanzo cha ajari za barabarani nchini hivyo zinatakiwa zifanyiwe marekebisho.

  Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Marison Mwakyoma alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) ili kujadili mapendekezo ya mabadiliko na maboresho ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. Amesema sheria ya usalama barabarani ilitungwa mwaka 1973na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambayo ni ya muda mrefu ukilinganisha na mabadiliko yaliyopo ikiwemo magari kuongezeka pamoja na watu.

  Mwakyoma alisema sheria ya mwaka 1973 ikibadilishwa itaweza kupunguza ajali za barabarani alitolea mfano ukisoma sheria ya kufunga mkanda hakuna sheria haijamzungumzia abiria kama afunge mkanda na haimlazimishi imuadhibu kwa sheria gani.
   
   Pia kwa upande wa magari madogo sheria inasema anayetakiwa kufunga mkanda ni dereva na abiria aliyepanda mbele lakini aliyepanda nyuma haionyeshi kwenye sheria anatakiwa afunge mkanda Mwakyoma alisema abiria wanaopanda basi ambalo limejaa bado wanaengia kusimama hakuna sheria inaonyesha yule aliyesimama adhibiwe.

  Hivyo sheria hiyo ikirekebishwa na kuwekwa adhabu inayoendana na kosa husika watu wataogopa kuvunja sheria za usalama barabarani na itasaidia kupunguza ajari zinazoendelea kutokea. Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Isabella Nchimbi alisema utafiti waliofanya walibaini kuwa mapungufu katika sheria ya usalama barabarani vinavyosababisha ajali nyingi ikiwemo dereva kutumia simu ya mkononi wakati anaendesha gari akiwa barabarani. Mapungufu mengine uvaaji wa kofia ngumu kwa dereva na abiria wa pikipiki,uvaaji wa mikanda wakati ukiwa kwenye gari,kuendesha mwendo kasi na matumizi ya uvukaji kwenye vivuko . 
  Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Marison Mwakyoma akiongea na washiriki katika semeina ya kujadili sheria za usalama barabarani
  Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Bi Isabella Nchimbi akiwasilisha hutuba ya ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za usalama barabarani.
  Picha ya pamoja

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  UJIO wa ndege za serikali kutaongeza huduma ya usafiri wa anga,mapato ya serikali pamoja na wananchi kuona huduma ya usafiri wa anga sio anasa kama ilivyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.

  Hayo ameyesema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA),Richard Mayongela wakati akizungumza na Michuzi Media, amesema kuwa katika kwenda na uchumi wa viwanda ni lazima kuwepo kwa viwanja bora vya ndege katika kurahisisha usafiri mali ghafi pamoja na abiria.

  Amesema kuwa viwanja vyote vya ndege vinaboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wa anga katika mikoa mbalimbali ambapo ndege zinazonunuliwa zitatumika katika safari za mikoa hiyo.Mayongela amesema kuwa fedha zinazotumika kujenga viwanja hivyo ni za watanzania kutokana na nguvu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika ukarabati wa viwanja ili kuweza kutoa huduma bora katika usafiri.

  “Mapinduzi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli anayoyafanya katika sekta ya usafiri wa anga kwa kununua ndege baadhi ya watu hawawezi kujua faida lakini watajua baada ya muda mfupi kutokana na ajira katika viwanja vya ndege pamoja na usafirishaji wa haraka wa bidhaa ambazo zinaharibika kwa muda mfupi kwenda kuuza nje ya nchi”amesema Mayongela.

  Amesema katika viwanja vya ndege watajenga sehemu za kuhifadhi bidhaa ambazo zinaharibika katika kipindi kifupi ikiwa ni kuwafanya wafanyabiashara kuwa na uhakika bidhaa hizo katika kusafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili soko.Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika kipindi hiki hakuna kulala ikiwa nia ya kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati wenye maisha bora ya watanzania.

  “Kazi yetu mamlaka ni kusimamia huduma ya usafiri kwa kujenga viwanja vya kisasa ili ndege zinazotumia viwanja hivi viweze kusukuma maendeleo ya nchi yetu na kama watanzania tunayofanya kazi hizi kuacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo” amesema Mayongela.Amesema ujenzi wa Rada ni moja ya kuhakikisha hali ya usalama wa usafiri wa anga ina kuwa kwa viwango vya kimataifa ambavyo vimeanishwa katika utoaji wa huduma za ndege.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini,(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini, leo jijini Dar es Salaam.
  Muonekano wa sehemu ya uwanja wa Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ndege zikiwa katika uwanja huo .

  0 0

  Serikali imesema kuwa haitasitisha mkataba na Mwekezaji wa Kampuni ya Chai Maruku, iliyoko mkoani Kagera, kwa sababu mgogoro wa malipo uliopo baina ya  kampuni hiyo na wakulima pamoja na wafanyakazi wake unaelekea kutatuliwa.

  Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba Vijijini Mhe. Jason Rweikiza (CCM), aliyetaka kujua sababu za Serikali kutovunja mkataba na mwekezaji huyo na kurejesha umiliki kwa Serikali au kwa mwekezaji mwingine atakayejali maslahi ya wakulima na wafanyakazi.

  Katika swali lake la msingi, Mhe.   Rweikiza alisema kuwa tangu Kampuni hiyo ibinafsishwe kwa mwekezaji, kumekuwa na malalamiko ya wakulima kutolipwa  fedha za mauzo ya chai kwa wakati na wafanyakazi kutolipwa  mishahara na stahiki zao ipasavyo.

  Dkt. Kijaji alisema kuwa, katika kutatua mgogoro huo Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa utendaji na uendeshaji wa Kampuni hiyo kwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera, Bodi ya Chai na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima wadogo wa Chai (TASHTIDA).

  Alisema kuwa katika vikao hivyo haki ya kila upande ilizingatiwa ikiwemo suala la haki za wafanyakazi pamoja na madai ya wakulima, ambapo mpaka sasa mwekezaji amekubali kulipa madai ya wakulima kiasi cha Sh. milioni 12 huku wakiendelea kujadili namna ya kutatua suala la madai ya wafanyakazi.

  Dkt. Kijaji aliahidi kuwa Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kuhakikisha haki za wakulima na wafanyakazi hazipotei.

  Imetolewa na:
  Benny Mwaipaja
  Mkuu wa  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  4/4/2018

  0 0

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.

   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.

   Baadhi ya Wauguzi na Wakunga wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha uuguzi na Ukunga Dodoma wakiwakilisha salamu zao kwa kutumia wimbo kwa  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA DODOMA.

   
   NA WAMJW-DODOMA.
   
  Serikali imewataka Wauguzi na Wakunga nchini kufuata na kusimamia misingi ya maadili ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.

  Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini.

  Najua kuwa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga inalishughulikia suala la maadili kwa wauguzi na wakunga hivyo nitoe msisitizo tena huduma za Uuguzi na Ukunga zinapimwa zaidi na uadilifu wa mtoa huduma hivyo muendelee kusimamia kwa ukaribu misingi ya maadili ya taaluma zenu amesema Dkt Ndugulile.

  Aidha, Dkt Ndugulile amewataka Wauguzi na Wakunga kupitia vyama vyao vya kitaaluma kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea kuwakumbusha mara kwa mara wauguzi kuhusu maadili ya taaluma yenu.

  Mteja anapokuja kwenye vituo vya kutolea huduma anategemea kupata huduma ya upendo na huruma, anategemea kupewa maneno ya faraja na matumaini hivyo basi, wale wote wanaoichafua taaluma yenu kwa kutotekeleza wajibu wao kwa wakati, kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wateja wenu wabainishwe na wahimizwe kujirekebishaamefafanua Dkt Ndugulile.

  Ninawapongeza sana kwa kuweka msisitizo kwa mambo yanayohusiana na kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga hiyo ni moja ya agenda muhimu ya Serikali ya  Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuliameongeza Dkt. Ndugulile.

  Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa serikali inazifanyia kazi changamoto zinazowakumba Wauguzi na Wakunga kwa namna mbalimbali ambapo hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha bajeti kwa ajili ya kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, na vitendanishi katika Bohari ya Dawa.

  kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo amesema kuwa kongamano hilo limeandaliwa ili kuwakumbusha wauguzi na wakunga maadili ya taaluma yao pindi wanapokuwa sehemu zao za kazi.

  Aidha Bw. Moyo amesema kuwa Akizungumzia Kongamano hilo limebeba kauli mbiu isemayo isemayo Kuelekea Huduma za Uuguzi na Ukunga Zinazozingatia Ubora, Utu, Huruma na Usalama wa Wagonjwa; Katika Kupunguza Vifo vya Akinamama na Watoto.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa miundo mbinu katika mradi wa maji utakao nufaisha wakazi wa elfu saba mia tano (7500) katika Shehia 4 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi Kikawajuni kwa Mselem katika jimbo la Kikwajuni, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud .Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namba umeme wa majumbani na viwandani unavyofanya kazi kutoka kwa mkufunzi wa umeme wa Chuo cha Mwenge Community College Mwalimu Mohamed Mbarawa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais chuoni hapo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Zanzibar.
   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa kozi ya uuguzi wanaosoma kwenye chuo cha Mwenge Community College kilichopo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya uuguzi wanaosoma kwenye chuo cha Mwenge Community College kilichopo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi.
   

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa, itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China,[Picha na Ikulu.] 04/04/2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Salama Aboud Twalib wakati alipotembelea Eneo la Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Ufukwe wa Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China,
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (Mwenye kipaza sauti) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) wakati wa ziara maalum Rais alipotembelea Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo kutembelea Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China


  Eneo la ufukwe wa Mpigaduri,Maruhubi linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Ujumbe wa Baraza la Mapinduzi walifika kuangalia Alama Maalum za mipaka ya ujenzi wakati alipotembelea Eneo la Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Ufukwe wa Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji wakati alipotembelea Eneo la Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Ufukwe wa Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Siara Ubwa Mamboya (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (Kushoto) alipofika Eneo la fukwe ya Bwawani wakati wa ziara maalum ya kutembelea eneo hilo sambamba na kutembelea Mpigaduri na Maruhubi Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China,


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (katikati) alipofika Eneo la fukwe ya Bwawani wakati wa ziara maalum alipotembelea Eneo hilo linalotarajiwa kujengwa Mji Mpya wa kisasa
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelekezo wa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi wakati walipofika Eneo la fukwe ya Bwawani wakati wa ziara maalum kutembelea eneo hilo sambamba na kutembelea Mpigaduri na Maruhubi Eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China

  Picha na Ikulu

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha vyama vya msingi vya ushirika vya mazao ya kilimo na masoko vinavyozalisha mazao ya kimkakati ya biashara ya pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku. 
  Amesema katika mwaka 2018/2019, Serikali inalenga kuimarisha masoko ya mazao hayo kwa kuhamasisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo mazao hayo yatazalishwa na kuuzwa kupitia vyama vya ushirika kwa njia ya minada. 

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

  Waziri Mkuu amesema pamoja na hatua hizo, Soko la Bidhaa ambalo limeshaanzishwa, litasaidia sana kuimarisha masoko ya mazao kwani yatakuwa yanauzwa kwa njia ya ushindani mkubwa huku wakulima wanaozalisha kwa ubora wakinufaika na bei ya juu zaidi.

  “Serikali imeamua kuweka mkazo maalum wa kuyaendeleza kwa kasi mazao matano ya biashara ambayo ni chai, kahawa, korosho, pamba na tumbaku. Lengo ni kuongeza mapato ya wakulima, kuwa chanzo cha kuaminika cha malighafi katika uchumi wa viwanda, na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira na fedha za kigeni. 

  Amesema uamuzi wa kuongeza usimamizi katika uzalishaji wa mazao hayo makuu ya biashara unatokana na ukweli kwamba, kwa kipindi kirefu uzalishaji ulishuka kutokana na changamoto kadhaa. 

  “Miongoni mwa changamoto hizo ni kupungua tija katika uzalishaji, baadhi ya wakulima kuacha kulima mazao hayo kutokana na kukata tamaa kwa sababu mbalimbali zikiwemo vyama vya ushirika kutotekeleza vema wajibu wao, wizi, dhuluma na pia ushiriki mdogo wa maafisa kilimo katika kusimamia kilimo cha kitaalamu,” alisema. 

  Alizitaja sababu nyingine za kushuka uzalishaji wa mazao hayo kuwa ni huduma zisizoridhisha za ugani na utafiti, ukosefu wa pembejeo bora, utitiri wa tozo na wingi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika. 

  Akitolea mfano, Waziri Mkuu alisema uzalishaji wa pamba ulipungua kutoka tani 456,814 mwaka 2013/2014, hadi tani 282,809 mwaka 2015/2016. Kwa upande wa tumbaku, Waziri Mkuu alisema uzalishaji katika kipindi cha miaka minne ulishuka kutoka tani 126,624 mwaka 2010/2011 hadi kufikia tani 60,929 mwaka 2015/2016.

  “Serikali imechukua hatua za kuimarisha utawala bora kwenye vyama vya ushirika kwa kusimamia chaguzi za vyama 2,537, chaguzi za viongozi wa bodi za vyama vya ushirika 532 na kufanya kaguzi katika vyama vya ushirika 2,896 vikiwemo vyama vikuu. Kazi za kusimamia vyama vya ushirika zinaendelea,” alisema. 

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema Serikali inasimamia uendelezaji wa mazao hayo moja kwa moja kupitia maafisa kilimo na Bodi za Mazao na kwamba imechukua hatua za kufuta baadhi ya tozo zilizokuwa kero katika mazao makuu ya biashara pamoja na kuhakikisha kwamba mauzo yanafanyika kwa njia ya wazi na inayoleta ushindani. 

  “Kutokana na hatua zinazochukuliwa na Serikali kusimamia mazao makuu ya biashara, tayari tumeanza kuona matokeo chanya kwa kuongezeka uzalishaji wake. Kwa mfano, hadi mwezi Machi 2018, uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara ulifikia tani 804,025. Uzalishaji huu unaashiria ongezeko la mavuno ikilinganishwa na mwaka 2016/2017. Ongezeko hilo la uzalishaji wa mazao ya biashara linakwenda sambamba na kuimarika kwa mwenendo wa bei za mazao hayo hususan korosho na kahawa,” alisema.

  Waziri Mkuu aliliomba Bunge likubali kupitisha sh. 143,618,762,698 zikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2018/2019 ambapo sh. 74,527,321,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 69,091,441,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. 

  Vilevile, Waziri Mkuu aliliomba Bunge liidhinishe sh. 125,521,100,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo sh. 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,315,613,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.

  JUMATANO, APRILI 4, 2018

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

  Prof.Kabudi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 : kwanini ushindani ni muhimu.

  Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani ,ukiongozwa na viwanda , pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  akizungumza  baada ya ufunguzi wa washa hiyo Profesa Kabudi ametaja hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini na kufafanua kinachoendelea ni kuangalia jinsi gani kufanya bidhaa za Tanzania kuwa na ushindani kwenye soko la Dunia.

  "Kuna mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini .Nikumbushe tu wakati tunapata uhuru tulikuwa na viwanda viwili , hivyo jukumu la wakati ule ikawa ni kuanza kujenga viwanda na vilijengwa na kutoa ajira kwa wananchi.

  "Hata hivyo ilipofika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tukarudi nyuma kidogo na baadae tukaingia kwenye vita dhidi ya Uganda ambapo tulitumia dola za Marekani milioni 5 kwenye vita.Hivyo tukawa hatuna fedha za kuendeleza viwanda.

  "Pamoja na magumu ambayo tumeyapitia bado leo hii tunavyo viwanda vingi ingawa jukumu la Serikali ni kujenga viwanda zaidi ili kuboresha maisha ya wananchi wake katika kuleta maendeleo,"amesema Profesa Kabudi.

  Amefafanua kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina hatua ambazo zinatakiwa kuchukuliwa katika kufikia malengo la kujenga viwanda na kuboresha maisha ya wananchi na kutumia nafasi hiyo kueleza tayari Serikali  imeanza kuchukua hatua kadhaa na baadhi ni elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari ambayo inatoa fursa ya kuandaa wasomi kwa maendeleo ya nchi.

  Pia amesema jitiahada nyingine zinaendelea katika ujenzi wa miundombinu ya barabara reli na bandari na kwamba miundombinu hiyo ni muhimu katika kujenga msingi imara wa kukuza na kuimarisha uchimi wa Tanzania.

  Prof.Kabudi amezungumzia namna ambavyo Serikali imejikita katika kuboresha sekta ya afya ili kuwa na wananchi wenye afya imara watakaoshiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.Pia amegusia hatua zinazochukuliwa katika kuongeza nishati ya upatikanaji wa umeme kwa kuanzisha miradi mikubwa ya umeme na jana Rais John Magufuli amezindua mradi wa umeme wa Kinyerezi II.

  Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa ujenzi wa viwanda na kueleza huko nyuma wakati kukiwa na viwanda vya kutosha wanawake na wasichana wengi walipata ajira na kuondoa wale ambao wanaonekana wanazurula mtaani.Hivyo viwanda vikijengwa vitatoa ajira ikiwamo kwa wanawake.

  Kuhusu malalamiko ya kodi kubwa , Profesa Kabudi amesema tayari Rais Magufuli ameshatoa maelekezo ya kuhakikisha kodi inakuwa yenye unafuu na juzi juzi amekutana na wafanyabishara kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya biashara na uwekezaji nchini ,hivyo kwenye eneo hilo mambo yanakwenda vizuri.

  Kwa upande wa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Amina Salim Ali amesema warsha hiyo imekuja wakati muhimu kwani yapo mambo ya kiseria ambayo yanajadiliwa na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kuinua uchumi wa wananchi na kwa Zanzibar kuna hatua mbalimbali ambazo wamezichukua katika kuboresha maisha ya wananchi.

  Amesema kwenye eneo la ujenzi wa viwanda, bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa Zanzibar imejikita pia katika kufufua viwanda vya zamani  na ujenzi wa viwanda vipya kulingana na bajeti ya fedha ambayo wameitenga.

  Pia wameamua kuimarisha kilimo cha bahari na katika hilo kuna baadhi ya vijana wapo nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo ya uvuvi hasa kwa kuzingati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenunua meli ya uvuvi kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi.

  Amesema wameimarisha kilimo cha mbogamboga kwani wanatambua kuna nchi za Uarabuni ambazo zinanunua mbogamboga kutoka Zanzibar huku akielezea hatua kadhaa ambazo zinachukuliwa na Serikali katika kuinua uchumi wa wananchi.

  Kuhusu sera ya viwanda, amesema Zanzibar wameweka mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizopo katika sekta ya viwanda na kuelezea namna ambavyo wameondoa urasimu kwa wanaotaka kufanya bishara na kuwekeza huku akizungumzia hatua ambazo wamechukua katika kuimarisha sekta ya utalii visiwani huo kwa kuhakikisha watalii wakienda wanakaa muda mrefu.

  Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk.Donald Mmari amesema pamoja na kushuhudia ukuaji mzuri wa uchumi wa Tanzania kwa miaka 15 iliyopita, tafiti zinaonesha viwango vya tija katika sekta nyingi bado ziko chini na ushindani wake kulinganisha na nchi nyingine duniani bado haujaridhisha.

  "Hata hivyo Tanzania ina uwezo wa kujiweka katika nafasi kubwa zaidi katika uchumi wa dunia  kwa kujenga uwezo wa ushindani ukiinuliwa na uwepo wa faida za kipekee ikiwemo eneo la kijiografia , wingi wa rasilimali za asili na utulivu wa kisiasa na kijamii.

  "Lengo la warsha hii ni kujadili na kupata maoni yatokanayo ma tafiti na uzoefu wa nchi nyingine ili yatuongoze katika kushiriki na kuchangia zaidi kwenye juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi wa viwanda ikizingatiwa kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitato(2021/22-2025/26) utajikita katika kuimarisha uwezo wa Tanzania kushindana na kuongeza ukuaji wa uchumi kupitia mauzo ya nje ya nchi,"amesema Dk.Mmari.

   Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti ya REPOA leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
   Mtoa mada Mkuu wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika katika mausuala ya forodha(SACU), Paulina Mbala Elago akitoa mada yake juu kwanini Ushindani na jinsi ya kuufikia katika maendeleo ya viwanda katika nchi hizo.
   Mkurugenzi Mkuuu wa Tasisi  ya utafiti nchini Repoa Dk Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha msemaji mkuu katika warsha hiyo ya kwanini ushindani juu ya viwanda kufikia 2025
  Mkurugenzi Mtendaji wa Infotech Investment Group LTD , Ali Mufuruki akiongoza majadiliano ya hali ya biashara kwa sasa katika Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Repoa nchini.
   Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
    Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
  Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi  watatu kushoto akiwa katika picha ya  pamoja na wafanyakazi wa Tasisi ya utafiti nchini Repoa pamoja na wadau wa utafiti

  0 0

  Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Songea Namtumbo ( SONAMCU) kilichopo Songea Mjini mkoani Ruvuma kinatarajia kuanza kufanyakazi ya ya kusindika tumbaku katika msimu wa 2018- 2019 mara tu baada kukamilika kwa matengenezo.

older | 1 | .... | 1553 | 1554 | (Page 1555) | 1556 | 1557 | .... | 1898 | newer