Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1552 | 1553 | (Page 1554) | 1555 | 1556 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akipokelwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudensi Milanzi mjini Dodoma jana ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 25 wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo.

  Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143 mwaka 2017 hali iliyopelekea kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

  Akizungumza wakati wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika mjini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Wizara yake itaendelea kuvutia watalii wengi zaidi ili kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa. 

  “Mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 2.1 mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani Bilioni 2.2 mwaka 2017” alisema Dk. Kigwangalla.Akifafanua Dkt. Kigwangala amesema lengo la Serikali ni kuona mafanikio haya yanazidi kuimarika, hivyo kila mtumishi katika Wizara hiyo lazima atimize wajibu wake ipasavyo katika kutimiza lengo la Wizara hiyo ambalo ni kuhifadhi na kusimamia maliasili, malikale na kuendeleza utalii.

  Aliongeza kuwa ili kufanikisha majukumu ya Wizara hiyo ipasavyo ni muhimu kuwa na bajeti ambayo itawezesha kushughulikia changamoto za migogoro ya mipaka katika maeneo ya hifadhi, kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali, upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea kazi, kutoa elimu ya maadili na kusimamia watumishi. 

  Alisema Wizara yake itaendelea na mapambano dhidi ya ujangili, biashara haramu ya nyara, magogo na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wote watakaogundulika kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kushiriki katika vitendo hivyo.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudensi Milanzi amesema kuwa Wizara hiyo itazingatia ushauri utakaotolewa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo ili kuongeza tija katika kutatua changamoto zinazojitokeza.

  “Wizara itaendelea kupambana dhidi ya ujangili, biashara haramu ya nyara na magogo na kuwachukulia hatua kali watumishi wote watakaogundulika kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kushiriki katika vitendo hivyo “ Alisisitiza Meja Jenerali Milanzi.Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 iliendelea na utaratibu wa kuendeleza watumishi katika mafunzo ya aina mbalimbali kama ifuatavyo:-Jumla ya watumishi wanne (4) wanahudhuria mafunzo ya muda mrefu nje na ndani. Aidha, mtumishi mmoja(1) yupo nje ya nchi.

  Watumishi wengine kumi na moja (11) walihudhuria mafunzo ya muda mfupi. Mafunzo haya yalihusu watumishi wa kada mbalimbali.Jumla ya watumishi saba (7) wamehudhuria mafunzo ya ujasiliamali unaohusiana na maandalizi ya kustaafu. Aidha, Wizara bado inaendelea na utaratibu wa kuwaandaa watumishi wote wanaokaribia kustaafu kuhakikisha wanapata mafunzo hayo. 

  Akifunga mkutano huo wa siku moja Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kufikia lengo lililokusudiwa la uhifadhi wa maliasili, malikale na kuendeleza Utalii.
  Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Dodoma jana.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudensi Milanzi akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa mkutano huo.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wa baraza wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. HamisI KigwangalLa (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudensi Milanzi pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Wafanyakazi.
  Baadhi ya ya Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Wakiimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi wakati wa mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akisalimiana na Katibu Mteule wa Tughe Tawi la Wizara ya Maliasili na Utalii, William Mwita muda alipowasili kufunga mkutano huo wa baraza. Katikati anayemtambulisha kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
  Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara wizara hiyo, Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi muda mfupi kabla ya kufunga mkutano huo wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
  Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na watumishi wa wizara hiyo wakatika akifunga mkutano huo wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
  Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara hiyo walioshiriki baraza hilo.
  Baadhi ya watumishi wa Wizara na wajumbe wa baraza hilo.

  0 0

  Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho kulia akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
  Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,
  Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, KawkabHussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu
  Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo  MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika Jumamosi wiki hii mjini hapa.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya washiriki wakithibitisha kushiriki.

  Alisema katika mashindano hayo msimu huu watazamia washiriki zaidi ya600 ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo medali ambazo zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.

  Aidha alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo hilo.

  “Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha umahiri wao.

  Alisema njia zitakazopitia mashindano hayo zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa wakimbiaji ili kuweza kuepukana na adhari zinazoweza kujitokeza wakati yakiendelea.Naye kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi.

  Alizitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa kwanza km 21 atapata700,000 wa pili 500,000, huku mshindi wa tatu akipata 300,000 huku wengine kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha 50,000.

  Hata hivyo alisema katika kilomita 10 mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa pili 150,000 na wa tatu 100,000 huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne mpaka 10 watapewa 30,000 pia kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa huduma ya maji kwa wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0  MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo jijini humo kuhusu upokeo na maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi,ndani ya  uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.
  MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo kwenye moja ya hoteli jijini humo,akieleza kukamilika  rasmi kwa maandalizi ya tamasha la pasaka,linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

  Msama amewashukuru Maaskofu hao na Wachungaji kwa kujitoa na kuunga mkono Tamasha la Pasaka 2018,ambalo kwa mara ya kwanza linaanzia kufanyika jijini Mwanza na baadae kuhamia mkoa wa Simiyu ndani ya mji wa Bariadi April 2 ndani ya uwanja wa Halmashauri,aidha tamasha hilo litakuwa na waimbaji lukuki ambao tayari wameishatangazwa kushiriki,kuhakikisha tamasha hilo linafana.
   
  Kwa upande wa Maaskofu wameipongeza Kampuni ya Msama Promotions,chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama kwa kuupa mkoa wa Mwanza kipaumbele kwa kuleta tamasha hilo mkoani humo,Wameongeza kuwa tamasha hilo litawavuta waumini wengi na wapenzi wa muziki wa injili na kuwaleta pamoja ili kupata neno la mungu na uponyaji kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo za injili .
  katika picha kutoka kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza na Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa.

  Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa kampuni ya Msama Promotion Kanda ya Ziwa,akitoa ufafanuzi wa namna tamasha hilo la Pasaka 2018 lilipofikia na maandalizi yake kwa ujumla,mbele ya kikao cha Maaskofu na Wachungaji kilichofanyika mapema leo jijini humo,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza.

  Mmoja wa maaskofu akitoa mchango wake katika kikao hicho kilichofanyika jijini Mwanza leo.
  Askofu Joyce Mangu wa kanisa la Calvary Assemblies Of God Mjini Kati jijini Mwanza akizungumza wakati akitoa mchango wake katika kuboresha tamasha hilo siku za usoni na kwamba amefurahishwa sana na ujio wa tamasha hilo kwa jiji la Mwanza.
  Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakifuatilia kikao hicho. 

  0 0

  Leo asubuhi nimefika alipokua akiishi msanii Man Dojo.Taarifa ya awali inaonesha kuwa eneo alilojenga kuna viwanja vitatu ambavyo vina hati na kuna watu walipewa mwaka 2003.Mwaka 2013 viwanja hivyo vikiwa havijaendelezwa,Man Dojo aliuziwa na mtu aliyedai ni mmiliki wa eneo hilo kwa Tsh milioni 3 wakimuaminisha kuwa ni mali yao.

  Wenye hati wameeleza kuwa walifungua kesi na kushinda katika Baraza la ardhi la wilaya, hivyo kupata amri ya kubomoa.Baada ya yake kubomolewa, kwa sasa Man Dojo na familia yake wanalala nje.

  Baada ya kuona na kusikiliza mechukua hatua zifuatazo kwa awali:-

  1. Nimeelekeza Man Dojo atafute nyumba ya kujistiri yeye na mkewe eneo la Mbweni kwa kipindi cha mpito ambayo nitamlipia kwa miezi sita.

  2. Nimeagiza wote waalioshiriki kumtapeli Man Dojo kwa kumuuzia kiwanja huku wakijua si mali yao wakamatwe na jeshi la Polisi haraka iwezekanavyo.Kitendo walichofanya ni jinai na lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

  3. Nimemuita Man Dojo ofisini kwangu siku ya jumanne saa 4 asubuhi na wenzie ambako tutafanya kikao na mashauriano na wataalam wa ardhi wa manispaa na uongozi wa kata ya Mbweni ili kujiridhisha kiini cha jambo hili, kupitia nyaraka zote na kuona namna tutakavyomsaidia kwa kutumia HEKIMA, BUSARA NA UBINADAMU.

  4. Nimeagiza, Mkurugenzi kupitia idara ya ardhi na Mipangomiji Kinondoni kuniletea taarifa ya watu wote waliopewa viwanja kwa kuanzia na Mbweni ambao hawajaendeleza viwanja vyao hadi sasa (kama masharti ya hati yanavyowataka).

  Kutoendeleza viwanja kunatoa mwanya kwa matapeli kuwatapeli wananchi wenye shida ya dhati ya ardhi ya kujenga makazi kama ilivyokua kwa ndugu yetu.Wako watu walipewa viwanja mwaka 2003 lakini hadi leo wameshindwa kusafisha na kuendeleza viwanja vyao.Badala yake viwanja hivyo vimekua vichaka na maficho ya wahalifu.

  5. Siku ya jumatano wiki ijayo nitazungumza na umma juu ya nini kimejiri katika kikao changu cha jumanne na namna gani tutamsaidia na kumshauri Man Dojo.Nafahamu jinsi ilivyo taabu kujenga, nafahamu jinsi kazi ya sanaa ilivyo ngumu hadi kudunduliza na kujenga.

  Lakini nawaasa wananchi wote wa Kinondoni kuchukua tahadhari na kujiridhisha kabla ya kufanya manunuzi yoyote ya kiwanja.Ni vyema kupata ushauri kwa wataalam wetu wa ardhi kabla ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi.
  Msanii Man Dojo akielezea jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi sambamba na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbweni.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi akimsikiliza Msani  Man Dojo akielezea namba tukio la nyumba yake lilivyokuwa,mapema leo jijini Dar


  0 0

    Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
   Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry akiongea kabla ya kumwalika Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  kufungua  mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
     Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
     Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
    Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na wajumbe baada ya kufungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akilakiwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry alipowasili kufungua  mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani. 

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 31, 2018) kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo. 

  “Dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa katika amani ya nchi yetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu” 

  Waziri Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa sana kwa binadamu na ndio maana wote wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au kikundi chochote kujaribu kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini. 

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea kuwaunganisha waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao au madhehebu yao.  

  Waziri Mkuu amesema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote amekuwa akisisitiza jambo hilo na kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo chao. 

  “Ni muhimu sana kwa ninyi wasaidizi wa Mufti mlio kusanyika hapa muhakikishe mnalisimamia hili katika maeneo yenu. Katika hili napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yenu iko pamoja Mheshimiwa Mufti kutekeleza nia hiyo njema.” 

  Amesema ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ni kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kusikiliza maoni, ushauri na  mapendekezo yeyote kutoka kwa viongozi wa dini . ‘Milango iko wazi saa zote ‘ 
  Ameongeza kuwa yeye si mtaalamu sana kama walivyo Masheikh hao lakini anakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani sura Al Imran aya ya 103 yanayosema “ Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane” 

  Mkutano huo umehudhuriwa na  Sheikh Mkuu wa Mufti wa Tanzania Sheikh Zubeir, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wajumbe wa Baraza la Ulamaa, Masheikh na viongozi wa BAKWATA wa mikoa na wilaya zote Tanzania.  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa kwa furaha na Paroko Msaidizi Venance Tegete walipojumuika na waumini wengine katika Maadhimisho ya Misa ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na waumini wengine wakisikiliza kwa makini mahubiri ya Paroko Msaidizi Venance Tegete  katika Maadhimisho ya Misa ya Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka katika Maadhimisho ya Misa ya Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimia waumini wenzie  baada ya Maadhimisho ya Misa Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo  Jumapili Aprili 1, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na waumini wengine wakifurahia jambo wakati wa  mahubiri ya Paroko Msaidizi Venance Tegete  katika Maadhimisho ya Misa ya Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na waumini wengine baada ya Maadhimisho ya Misa Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo  Jumapili Aprili 1, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimia waumini wenzie  baada ya Maadhimisho ya Misa Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu  Joseph jijini Dar es salaam leo  Jumapili Aprili 1, 2018

  0 0


  Waziri Wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasihi viongozi mbalimbali wa dini nchini wakiwemo Maaskofu na Mashekh kutumia muda wao mwingi kwa kutembelea mikoa mbalimbali nchini kunapotokea zaidi matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ili kuhubiri injili wananchi wawe na hofu na Mungu jambo litakalopelekea kupunguza ukatili na watu kumjua Mungu. 

  Dkt Nchemba ameyasema hayo Wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mamia ya waumini kwenye Tamasha La muziki Wa Injili lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ambayo huratibu matamasha hayo kila mwaka. 

  Dkt Mwigulu aliwasihi wananchi kwa mshikamano na wingi wao Kuendelea kumuombea Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani anafanya kazi kubwa katika kuwatumikia watanzania ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri Wa Rasilimali za Taifa ambazo amekusudia kuwanufaisha watanzania wote kupitia uchumi fungamanishi. 

  Alisema nia na Dira ya Rais Magufuli ni msisitizo mkubwa Wa umuhimu Wa maslahi kwa watanzania huku akiwasihi maaskofu Wa makanisa yote nchini kuendelea kueneza neno la Mungu kwani matukio yanayotokea ya mauaji yanasababishwa na wananchi kutomjua Mungu kwa kufanya imani za kishirikiana na ukatili kwa watoto, ubakaji wa wanawake, ulawiti, unyanyasaji wa wazee na wananchi wengi kwa ujumla wake. 

  Katika tamasha hilo Dkt Mwigulu pia Amezindua albamu ya Msanii nguli Wa nyimbo za injili nchini Tanzania Bi Rose Muhando ijulikanayo kama USIVUNJIKE MOYO na kununua albamu hiyo kwa Shilingi 500,000 huku tamasha hilo likichagizwa na waimbaji 17 Wa ndani na nje ya nchi. 

  Akijibu risala ya Kampuni ya Msama Promotion kuhusu wizi Wa kazi za wasanii, Mhe Mwigulu alisema kuwa serikali inatambua kadhia hiyo inayowakumba wasanii Wa dini nchini hivyo atawasiliana na Wizara ya Habari, sanaa, utamaduni na Michezo ili kuweka msisitizo katika kuratibu shughuli ya kuepusha wizi Wa wasanii. 

  Awali akisoma risala ya kampuni ya Msama Promotion Askofu Zenobiasi Sisaya Wa kanisa la Filadephia, alisema kuwa Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kudumisha amani na mshikamano ambapo pia amesisitiza serikali kupigia chepuo kwa kuzitambua kazi za wasanii na kuwatia nguvuni wale wote wanaochakachua kazi za wasanii. 

  Alisema kuwa hali hiyo inawafanya wasanii wanaotumia kazi kubwa kiakili na kimwili kutengeneza kazi hizo lakini pasina kuwa na faida kwao kwani wezi hao wanazalisha kazi nyingi ambazo zipo chini ya kiwango na hatimaye kulikosesha faida Taifa kwa kutolipa kodi. 

  Aliiomba serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya nchi na Wizara ya Habari, sanaa, utamaduni na Michezo kuwachukulia hatua za haraka wezi Wa kazi hizo za wasanii kupitia wakuu Wa wilaya na mikoa kufanya msako endelevu kwa wote wanaofanya jukumu hilo. 

  Dhifa hiyo ya Tamasha la Pasaka imehudhuriwa pia na Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Mhe John Mongela, Naibu waziri Wa Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Ilemela, Maaskofu Wa makanisa mbalimbali nchini sambamba na Mbunge Wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu.
   Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba na Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion wakizindua albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jana jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo waimbaji mbalimbali wa injili wameshiriki katika tamasha hilo.

  Mwimbaji Rose Muhando amefanya mambo makubwa wakati alipotumbuiza moja ya kibao chake kipya cha "Lazima Wakae" kilichomo katika albam yake hiyo ambapo mashabiki walishindwa kukaa jukwaani na kucheza wakati wote alipokuwa akitumbuiza.

  Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika tamasha hilo leo kwenye tamasha hilo ni, Upendo Nkone, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Martha Baraka,  Joshua Mlelwa, ,Paul Clement, Sifaeli Mwabuka Dan M kutoka Kenya, Christopher Mwahangila,Bonny Mwaiteje, na wengine wengi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionesha albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando,  kulia ni  Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana jioni
   Dk Mwigulu akimpongeza Rose Muhando mara baada ya kuizindua albamu yake iliyosheni nyimbo kazi nzuri alioifanya ya utunzi wa nyimbo zenye kuielimisha jamii katika nyanja.
  Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhanda akiimba moja ya wimbo wake mpya uliomo kwenye albamu yake mpya  ya 'Usife Moyo' uitwao 'lazima wakae 'mbele ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Mwigulu Nchemba.
   Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akipokelewa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mh.John Mongela mara baada ya kuwasili uwanja wa CCM Kirumba,tayari kwa kuzindua tamasha la pasaka kwa mara ya kwanza chini ya Kampuni ya Msama Promotions Ltd sambamba na uzinduzi wa albamu ya Muimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhanda iitwaya 'Usife Moyo' yenye jumla ya nyimbo saba. 
   Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika tamasha la pasaka mapema jana jioni ndani ya uwanja wa CCM 
  Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akimtunza muimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila mapema jana jioni ndani ya tamasha la pasaka.

   

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 2, 2018
   Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku ikipewa heshma ya  kumwagiwa maji(water salute) mara baada ya kutua.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


   Marubani walioileta ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 kutoka Canada (wawili waliosimama kulia) na marubani na wahudumu wa ATCL mara baada ya kuwasili kwa ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa viongozi wa dini na wa ATCL wakiwa ndani ya ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome na marubani walioileta ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakala wa Safari (TASOTA) Bw. Mustapha Khatawa kwa kuwasili kwa ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

  0 0

  Na Munir Shemweta, Pwani

  Mkoa wa Pwani umeanza uhamasishaji wa uwekezaji katika zao la muhogo ili kuwawezesha wakulima kujiongezea kipato sambamba na kuendanana soko la China ambapo Tanzania imepata fursa kuuza muhogo nchini humo. Hali hiyo imebainika mwishoni mwa wiki wakati maofisa kutoka Wizara ya Kilimo walipotembelea mkoa huo ikiwa ni mkakati wa wizara kuhamasisha ulimaji zao la muhogo na kuangalia changamoto zake kwal engo la kuongeza tija na uzalishaji waza ohilo.

  Akielezea harakati za wilaya ya Kibiti katika kuhamasisha zao la muhogo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Bwenda Ismail alisema, uhamasishaji huo unaenda sambamba na utoaji mafunzo, utoaji mbegu bora kwa wakulima pamoja na kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari moja ya muhogo jambo litakaloongeza uzalishaji. Kwa mujibu wa Ismail sasa hivi zao la muhogo katika wilaya ya kibiti limekuwa la kibiashara na hali hiyo inatokana na usafirishwaji wa muhogo mbichi kwa wingi kila siku kutoka wilaya hiyo kuenda dar es salaam.
  Afisa Kilimo Wilayaya Kibiti Bwenda Ismail (kulia) akiwa na AfisaUgani wa wilaya hiyo Organess Semwenda wakiangalia muhogo unaolimwa katika shamba la Kibiti Farm Estate lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti.

  Alisema kuwa, hatua nyingine inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Kibiti ni kusaidia wakulima katika uuzaji muhogo hasa baada ya kubainika wakulima katika wilaya hiyo wamekuwa wakipunjwa wakati wakuuza muhogo kwa wafanyabiashara na sasa wilaya imejenga soko la pamoja lililogharimu milioni 65 na mategemeo ya wilaya ni kuwa muhogo utauzwa kwa vipimo stahiki tofauti na sasa ambapo wakulima wanapunjwa kwa mihogo kutenganishwa ile mikubwa na midogo.

  Afisa kilimo huyo wa wilaya ya Kibiti alisema, uhamasishaji umewekwa pia katika ujenzi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha muhogo unaonunuliwa kutoka kwa wakulima unasindikwa sambambana kuhakikisha wilaya kibiti m inatenga maeneo kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi, wawekezaji wakubwa, wakati na wadogo pamoja na maeneo kwa ajili ya vijana na msisitizo ukiwa kila kata itenge eneo.
  Meneja wakiwanda cha kusindika muhogo cha Ukaya kilichopo Mkuranga Joseph Mtanga (kulia) akimueleza Afisa Mazao wa Wilaya hiyo Derick Samuel namna kiwanda chake kilivyokwama kuendelea nauzalishaji kutokana na kukosekana kwa umeme.

  Kwa sasa Wilaya ya Kibiti umekamilisha sheria ndogo ambapo kila kaya itatakiwa kulima zao la muhogo jambo litakalosaidia kusukuma watu kuingia shambani ikiwemo vijana ambapo sasa watalazimika kuingia katika kilimo ili kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda na soko la china la muhogo kwa kuzalisha muhogo wa kutosha.

  Kwa upande wa wilaya ya Mkuranga, serikali wilayani humo katika bajeti yake imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kununua na kusambaza mbegu za muhogo kwa wakulima mbalimbali. Afisa Kilimo wilayani humo Bi. Julita Bulali amebainisha kuwa kutokana na jitihada za kusambaza mbegu kwa wakulima kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu kuwekeza katika zao la muhogo.
  Shamba la muhogo lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani.

  Hata hivyo, changamoto kubwa katika wilaya hiyo ni kusitishwa kwa huduma katika kiwanda cha Ukaya farm ambacho imekuwa mkombozi mkubwa wa kununua muhogo kutoka kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa umeme katika kiwanda hicho.

  Kwa mujibu wa meneja wa kiwanda hicho bw. Joseph Mtanga, awali kiwanda hicho kilikuwa kikitumia jenereta lakini mara baada ya kuharibika najitihada za kupataumeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kushindikana shughuli za kiwanda zimesimama na hivyo kuwakosesha wakulima kuuza muhogo katika kiwanda hicho. Meneja huyo wa kiwanda cha Ukaya Farm alisema kiwanda chake hununua wastani wa tani nne mpaka mpaka kumi na mbili kwa siku kutoka kwa wakulima na kusitishwa kwa usindikaji kumesababisha pia ajira za watu thelathini mpaka arobaini kusimama. Baadhi ya wakulima mkoani humo walisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la uhakika jambo linalosababishwa mzunguko wa biashara kutoenda vizuri.
  Baadhi ya wakulima wa zao la muhogo wilaya ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja.

  Walisema biashara ya muhogo wakati mwingine inakwama kutokana na masuala ya kisera ambapo bidhaa zao zinahitaji kuhalalishwana shirika la viwanga Tanzania (TBS) jambo linalofanya kushindwa kuingia katika ushindani kutokana na kutokidhi vigezo. Pia ukosekanaji wa vipimo stahiki katika uuzaji muhogo katika magari unawanyonya wakulima kwa kuwa bei wanayakubaliana mazao yakiwa shambani tofauti nabei wanayouza.

  0 0

    Mheshimiwa Godwin Aloyce Mollel akiapa kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 
    Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Maulid Mtulia kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 
   Mheshimiwa Maulid Mtulia akiapa kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Godwin Aloyce Mollel kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia, (kushoto kwake) na ujumbe wa wapenzi na mashabiki wa CCM kutoka Kinondoni waliomsindikiza mbunge huyo kutoka Dar es salam hadi bungeni Dodoma Aprili 3, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, Godwin Aloyce Mollel, (kushoto kwake) na ujumbe wa wapenzi na mashabiki wa CCM kutoka Kinondoni waliomsindikiza mbunge huyo kutoka mkoani Kilimanjaro hadi bungeni Dodoma Aprili 3, 2018.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akizungumza na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 3, 2018.
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Tanzania, Leo Mjini Dodoma.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akijibu hoja za wabunge wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Tanzania, Leo Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwasilisha Bungeni azimio la Bunge la Kuridhia makubaliano ya Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa mabadiliko ya Tabia nchi, Leo Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Adelardus Kilangi, wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Tanzania, Leo Mjini Dodoma.

  Picha na MAELEZO

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (wa pili kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na aliofuatana nao leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
   
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na baadhi Viongozi wa Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo chini ya kiongozi wake Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (katikati),[Picha na Ikulu.
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya shamba la mpunga katika bonde la Kizimbani toka kwa Katibu wa Jumuiya ya Wakulima Kizimbani Bw. Shafii Kibwana Said ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuweka kaa kwenye maji kama ishara ya kuhamasisha utunzaji mazingira na uzalishaji wa kaa katika eneo la Fuoni Kibondeni. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kibondeni mara baada ya kuweka jiwe la ujenzi wa Tawi hilo mkoa wa Mjini Magharibi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  Makamu wa Rais ameahidi kuwapatia trekta moja wakulima wa mkoa wa Mjini Magharibi ili liweze kusaidia wakulima kulima kwa wakati.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Mradi wa Wakulima wa Mpunga katika bonde la Kizimbani lililobo wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

  Makamu wa Rais aliwaambia wakulima hao kuwa Mjenga Nchi ni Mwanachi na aliwahimiza viongozi wote kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za kuleta maendeleo na kushirikiana bega kwa bega na wananchi.

  Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku nne ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya CCM Zanzibar, amewataka viongozi na wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kushirikiana na kudumisha amani ya nchi.

  Pamoja na kutembelea shamba la mpunga ambapo alisimamia zoezi la upandaji mpunga Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea eneo la Fuoni Kibaoni ambao alishuhudia upandwaji wa miti ya mikoko kwa kiasi kikubwa ikiwa shemu ya utunzaji wa mazingira lakini pia utunzaji na uzalishaji wa Kaa.

  Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliambata na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

  0 0


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibofya kitufe kuashiria kuzindua  rasmi mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 .
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Waziri wa Nishati Dkt. Menard kalemani  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa    Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dkt.Tito Mwinuka  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018  
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018
   Bila kujali mvua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi II eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA

  0 0

  Rais Magufuli amemteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko (pichani) kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali

  0 0


  0 0
  Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Ujenzi wa Makazi ya Muriya, Ghizlane El Gouchi (wa pili kushoto) akiwaonyesha wageni waliohudhuria hafla ya kuitambulisha kampuni hiyo kuelekea maonyesho ya biashara yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam hadi Aprili 5 na Zanzibar Aprili 6. Kushoto ni Mshauri wa Mradi Mona Abel Malak, mshauri mwandamizi, Faisal Alzakwani,Mshauri Hamad Al Balushi na mshauri mwingine Omar Saleh.


  Watanzania wameaswa kuchangamkia nyumba zinazouzwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake Muscat nchini Oman, ili kujiweka katika kundi sahihi la kibiashara sanjari na kujipatia maendeleo makubwa kutoka kwa nchi ya Tanzania na Oman.

  Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko na Kampuni ya Muriya Ghizlane El Gouchi, wakati anazungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nyumba zinazouzwa na kampuni yao huku maonyesho hayo yakifanyika jana katika Hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wenye ndoto za uwekezaji wa majengo.
  Maonyesho hayo yaoiendelea leo jijini Dar es Salaam leo latina Hoteli ya Hyatt.


  Alisema kwamba Tanzania na Oman ni nchi mbili zenye uhusiano mkubwa wa kindugu na kibiasharaa, hivyo ni wakati wa Watanzania wenye ndoto za kuwa wafanyabiashara wakubwa, kujitokeza kwa wingi katika uwekezaji wa majengo yanayotolewa na kampuni yao pembeni mwa viwanja vya Golf na pembezoni mwa bahari.

  Muriya ni kampuni kubwa iliyojikita katika utoaji wa huduma za makazi na utalii nchini Oman, ambao tumeingia katika soko la Tanzania baada ya kufanikiwa pia kwenye soko la ndani, tukiamini kuwa ni wakati mzuri wa kutoa fursa za makazi kwa Watanzania wote.

  “Taratibu za malipo ni rahisi kwa sababu mtu atakayekuwa tayari kununua, anakuwa na fursa ya malipo kwa awamu nane ndani ya miaka miwili ambapo mteja atalipia asilimia 10 mara baada ya kujisajili na asilimia 10 ya mwisho ni atakapokabidhiwa, huku gharama zetu zikianzia Dola 98,000 tu,” Alisema El Gouchi.

  Kwa mujibu wa El Gouchi, mradi wao wa Jebel Sifa ni mwendo wa dakika 40 tu kutoka Muscat, karibu na ufukweni ambayo yana ukubwa hadi wa square meter 365,000, ukiwa ni mradi mkubwa unaowahusu Watanzania wote na ni fursa nzuri za uwekezaji.

  Maonyesho hayo ya kibiashara ya makazi yanayouzwa na Kampuni ya Muriya mbali na kufanyika jijini Dar es Salaam, Hyatt Regency Hoteli kuanzia tarehe Aprili 3 hadi 5, pia yanatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar Aprili 6 Park Hyatt Hoteli kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni kwa ajili ya kuendeleza kutoa elimu juu ya fursa hizo za makazi inayotolewa na Muriya, kampuni iliyoanzishwa nchini Oman.

  0 0


  Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba.


  Na Fredy Mgunda,Dodoma.

  Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amelibana jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo

  Mbunge Rose Tweve mapema hii leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo.Akijibu swali la mbunge Rose Twelve Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba alisema kuwa jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani limeweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 43 kwa mwaka 2017

  Mwigulu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856 ambazo zilisababisha vifo 3256 na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017 kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo 2533 na majeruhi 5355.Waziri Mwigulu ameongeza kuwa kwa kipindi cha januari hadi februari 2018 kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo 334 na majeruhi 698.

  Akiuliza swali la nyongeza mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda wahanga wa ajali hizo,sasa mheshimu waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha wanamapungufu mengi na watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo na kwanini tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.

  Akijibia swali la Nyongeza la Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia, Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa ajali 1583 wakilipwa fidia takribani Bilioni 7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.

  Katika hatua nyingine Mwigulu Nchemba amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500 yanayosababishwa na uzembe wa madereva huku serikali ikipanga kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.

  “Ni kweli serikali itahakikisha inawachukulia hatua madereva wazembe ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili kupunguza idadi ya madereva ambao wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuepkukika” alisema Mwigulu nchemba.

older | 1 | .... | 1552 | 1553 | (Page 1554) | 1555 | 1556 | .... | 1898 | newer