Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1549 | 1550 | (Page 1551) | 1552 | 1553 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wabunifu na Wavumbuzi, Edward Magoti(Wapili kulia) akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho hayo, leo jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho ya wabunifu na wavumbuzi  yatayofanyika Aprili 27 hadi 29, leo  jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  KAMATI ya Maonesho ya Wavumbuzi na Wabunifu Tanzania(TICE) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  wameandaa maonesho ya yayanayotarajia kufanyika kuanzia Aprili 27 hadi 29 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza leo Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Magoti amesema maonesho hayo yatahusisha Wavumbuzi na wabunifu na yatakuwa ya aina yake katika ujenzi wa sekta ya viwanda nchini.

  Magoti amesema maonesho hayo ni fursa ya wabunifu na wavumbuzi katika nyanja ya kutengeneza mtandao , kujitangaza katika mtandao wa kufanya ubunifu na uvumbuzi pamoja kuendeleza kazi na uzoefu na watu wengine katika sekta hiyo.

  Amesema wakati wa maonesho hayo wavumbuzi na wabunifu wa nchini Tanzania watapa fursa ya kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali ,wafanyabiashara wakubwa na kati taasisi za Serikali , Taasisi za fedha na viongozi.

  Aidha amesema washiriki watatu kwenye maonesho hayo watapata zawadi ya milioni  Sh.35 kwa mshindi wa kwanza na mshindi mshidni wa tatu Sh.milioni 5.
  Kwa upande wa Ofisa wa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola amesema maonesho hayo yatakutanisha watoa huduma wote ambapo ni fursa kwa wabunifu na wavumbuzi kukutana na watoa huduma hao.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo  ya mikopo mbali mbali kwa wateja wao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce  Malai katikati wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.

  Na  Agness Francis, Blogu ya Jamii
  BENKI ya BancABC  imesema imetekeleza Sera ya fedha  ya Benki  Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja  wake wapya kuwezesha  kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha amesema benki hiyo ni  sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa  katika soko la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji.

  Hivyo Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na  ya nyumba na kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi.

  "Hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa kupunguza masharti kama vile kiwango cha  chini cha fedha kwa mabenki,"amesema Botha.

  Ameongezea viwango vya punguzo,hati fungani za hazina na kukopesha 
  mabenki kwa viwango vya chini na hiyo imewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na kampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha uchumi. "Na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi kuhusu punguzo hili."

  Aidha Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo amesema kuwa benki hiyo inahudumia wateja zaidi ya 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti za kibenki

  Mwasomengo amesema fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja kupata mikopo ya Nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa Daraja la kati na chini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Mlai amemalizia kwa kusema katika kujenga nyumba wanaungana na Serikali kuwapa fursa ya kuwapatia mikopo ya Nyumba  wafanyakazi wa aina zote sekta binafsi,serikalini pmoja na wafanya biashara.

  0 0

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia wawaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.

  Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.

  “Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda”

  Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi wa Michezo kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na kuwataka Viongozi wa Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya kushiriki michezo ya SHIMMUTA.Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.

  Aidha Mwenyekiti wa SHIMMUTA Ndugu Hamis Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya katika kukuza michezo nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Wajumbe wakifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)    0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani.

  JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata wahamiaji haramu kumi raia wa nchi ya  Ethiopia ,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

  Jeshi hilo pia, limemtia nguvuni mwanamke -Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye silaha aina ya shortgun, huko kijiji cha Manda Mazingara kata ya Miono,tarafa ya Mkange wilaya ya Bagamoyo.

  Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP), Jonathan Shanna alisema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa machi 26, wakiwa porini ,Pingo Shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze na askari waliokuwa doria kufuatia kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

  Akielezea matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Tagen Alam (19), Abraham Wolde (19) na Musama Kamal (16).Wengine ni Abush Tamaskel (16), Ayela Erapo (18) na Ngusie Kechine (18), Zarabel Faisa (16), Tsedhj Yshgee (19), Teyey Ally (18) na Tuktigo Clemag (17).

  Watuhumiwa wote hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.Kamanda Shanna alielezea ,jeshi hilo linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu waliowasaidia kuingia nchini bila kufuata utaratibu wa sheria.Katika tukio jingine , mwanamke aliyejulikana kwa jina la Felister Mtinga (30-36) amekutwa kitandani akiwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Moreto,iliyopo Chalinze.

  Kamanda Shanna alisema kuwa, mwili wa mwanamke huyo ulibainika machi 26 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi baada ya wahudumu kutomuona akitoka tangu alipoingia ndani machi 25 katika nyumba hiyo.

  Alifafanua , mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi wa awali na kubaini kutokuwa na majeraha ya aina yoyote hali inayosababisha kuondoa mashaka kuhusu kifo chake na umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.Katika tukio la kukutwa na silaha, kamanda Shanna alibainisha wamekamata silaha mbalimbali katika misako inayoendelea kufanyika mkoani hapo, ikiwemo SMG .R.6134, mapanga manne, sime moja na risasi 23.

  Alieleza, saa sita usiku machi 27,walimkamata mwamke aliyetambulika kwa jina la Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye short gun na Ramadhani Mdoe akiwa na silaha aina ya SMG.R.6134 .“Tunaendelea na misako kabambe inayoongozwa na kikosi chao cha siri, tunafanya misako uvungu kwa uvungu,giza kwa giza,pori kwa pori,tunashukuru inazidi kufanikiwa na ni endelevu “alisisitiza kamanda huyo.

  Kamanda Shanna aliwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za wale wachache ambao wanawadhania ni wahalifu kwenye maeneo yao.
   Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akizungumza kuhusiana na misako na doria zinazoendelea Mkoani humo.
   Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akiakionesha baadhi ya siraha alizokamata.

  Wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia ambao wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani ,huko porini Pingo shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze.

  0 0


  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.

  Watuhumiwa waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.
  Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

  Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

  Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

  Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali.Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za awali April 10 mwaka huu.

  0 0

  Mkuu Wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Ally Salum Hapi Anawaalika Wajasiliamali Wote Wilaya Ya Kinondoni Kesho Siku Ya Jumatano

   MAHALI: Ukumbi Wa King Solomoni- Namanga

  MDA: Saa 3 Asubuhi
  LENGO: Kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili

  WOTE MNAKARIBISHWA


  0 0


  0 0


  0 0

  Na.Vero Ignatus Arusha.
  WAFANYAKAZI watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.

  Watuhumiwa waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.

  Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

  Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

  Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.

  Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

  Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali

  Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za  awali April 10 mwaka huu.

  0 0


  0 0

  Waziri Jafo akigawa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za sekondari zitakazoshiriki. Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
  Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo, akiongea wakati wa uzinduzi huo.
  Waziri Jafo katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa UMISSETA baada ya uzinduzi.

  MASHINDANO ya shule za sekondari ya UMISSETA ngazi ya mkoa yamezinduliwa mkoani Dodoma, na mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri wa TAMISEMI,Selemani Jafo.Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari,walimu, viongozi mbalimbali wa mkoa na michezo.

  Mbali na uzinduzi,Waziri alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo.Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.

  Waziri Jafo, alisema kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka ,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo.

  “Nafahamu kuwa udhamini wa Coca-Cola wa mashindano haya unamalizika mwishoni mwa mwaka huu,lakini natoa ombi maalum iangalie uwezekano wa kuendelea kuongeza kipindi cha kutoa udhamini .Mashindano haya ya UMISSETA ni tanuru ya kuibua vipaji na rekondi ipo ya wachezaji wazuri wa soka waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika michezo mbalimbali,vipaji vyao viliibuliwa katika mashindano haya wengi pia wamechezea baadhi ya klabu kubwa za soka za Yanga na Simba”alisema.

  Waziri Jafo,alitoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya michezo kuanzia ngazi za chini,na kusisitiza kuwa sekta ya michezo inazidi kukua ambapo hivi sasa lengo lake sio burudani bali ni biashara kubwa na ushahidi wa suala hili upo wazi.


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na vingozi wenzake watano, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka nane yakiwemo ya uchochezi na uasi.

  Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni  Peter Msigwa, Salum Salum, John Mnyika, Ester Matiko na Dk Mashinji.

  Katika mashtaka hayo nane, shtaka la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote sita, huku Mbowe peke yake anakabiliwa na mashtaka matano, yaani shtaka la tatu hadi la saba na Msigwa akikabiliwa na shtaka moja la peke yake la nane.

  Akisoma hati ya mashitaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa Februari 16, mwaka huu washtakiwa kwa pamoja, wakiwa katika barabara ya Kawawa wilayani Kinondoni, walifanya mkusanyiko na maandamano isivyo halali kinyume na sheria,

  Imedaiwa walikusanyika kutekeleza lengo la pamoja kufanya mkusanyiko usio wa halali wenye vurugu na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.

  Aidha Nchimbi ameongeza kudai kuwa, Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni, washtakiwa wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano hayo,licha ya kutolewa tamko la kuwataka kutawanyika...waligoma kutii amri hiyo na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwkilina kusababisha askari wawili kujeruhiwa kutokana na mkusanyiko huo.

  Katika shtaka la tatu imedaiwa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, jijini mshtakiwa Mbowe peke yake wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi ya kuhamasisha chuki maneno ambayo yalipelekea chuki mioyoni mwa wana jamii wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Pia Mbowe anadaiwa kufanya uchochezi na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ya watanzania kinyume na sheria.Aidha Nchimbi amedai
  Katika mashitaka ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe, inadaiwa katika maeneo hayo akiwa katika mkutano wa hadhara, akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau kwa watanzania dhidi ya uongozi wa kiserikali uliopo madarakani kisheria, alitamka maneno yenye kupandikiza chuki na kuleta ushawishi wa uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kisheria

  Nchimbi aliendelea kudai, katika tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya mamlaka halali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

  Katika shitaka la saba, Mbowe anakabiliwa na tuhuma za kutenda kosa la kushawishi kutendeka kwa kosa la jinai, ambapo amedaiwa siku hiyo, akiwa pia amejumuika na wengine ambao hawako mahakamani, aliwashawishi wakazi hao wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio wa halali.

  Mshtakia Msigwa anadaiwa kushawishi raia kutenda kosa la jinai shtaka analodaiwa kutenda February 16, mwaka huu katika maeneo hayo hayo ya Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam,Imedaiwa siku hiyo Msigwa aliwashawishi wananchi wa Kinondoni kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

  Washitakiwa wamekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba ipangwe kesho au keshokutwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. 

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
  JOPO la wataalam kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, maofisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi wa dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama ambao wametelekezwa na hawapati fedha za matunzo ya watoto kutoka waume zao.

  Ofisi ya Mkuu wa Dar es Salaam ilitangaza kutoa msaada wa kisheria kwa kuwasikiliza wanawake hao na kwamba watatoa msaada huo kwa siku tano kuanzia Aprili  kuanza April 9 mwaka huu.

  Akizungumza na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na baba zao.

  Makonda amesema lengo la mchakato huo si  ugomvi bali ni kumwezesha mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya Serikali ya awamu ya tano. 

  Pia amesema amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.

  Pamoja na hayo Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewaomba kinamama kufika Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya na watalaamu ili waingie kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.

  "Ifike hatua mwanaume ukimpa mwanamke ujauzito bila mpangilio aogope kama ilivyo kwenye ubakaji,"amesema Makonda.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum. Wa kwanza kutoka Kulia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambio ya Kale Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo.
  Balozi Seif alisalimiana na baadhi ya Viongozi na Waasisi wa Vyama vya Siasa Nchini alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume Zanzibar.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Viongozi wa Serikali na vyama vya Kisiasa Ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP) mara baada ya Kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume.
  Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Bwana Ali Davutoglu kati kati akimtambulisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mkurugenzi Mkuu wa Maarifa Foundation School iliyopo Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

   Mwenyiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa katika gari ya Polisi tayari kwa kupelekwa Segerea baada ya kukosa Dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kutokana na Mashtaka yanayo wakabili.
    Mwenyiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho (Zanzibar) Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara) na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu baada ya kesi yao kuarishwa na kuamuriwa kurudi rumande bila dhamana.

  *Mahakama yaamua kuwanyima dhamana kwa usalama wao
  *Hatma yao kujulikana Ijumaa iwapo watatoka mahabusu au la

  Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
  MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho ambao wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamepelekwa mahabusu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilishwa maombi ya kuwanyima dhamana.

  Mbali ya Mbowe wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.
  Hivyo ni baada ya kusikilizwa mabishano marefu ya upande wa Jamhuri na ule wa utetezi juu ya dhamana ya washtakiwa kama wapate au la, mahakama imesema itatoa uamuzi Machi 29 mwak huu, mshtakiwa Mbowe na wenzake wamepelekwa rumande.

  Mapema upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kunyimwa dhamana kwa washtakiwa kwa njia ya mdomo.
  Akiwasilisha sababu za kupinga dhamana mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mkuu Dk. Zainabu Mango amedai  ni kwa sababu za usalama wa jamii na nchi kiujumla kama ilivyoelezwa kwenye hati ya mashtaka.

  Amedai wanatambua dhamana ni haki ya mshtakiwa lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwani Mashtaka yao wanaashiria kutokutii amri yao kikatiba, utekelezaji wa haki binafsi unapaswa kuzingatia haki za watu wengine.

  Alidai alidai kwamba makosa yanayowakabili yanahatarisha usalama nchi na kuwapa dhamana ni kuendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kufanya makosa hayo.

  "Jukumu la dhamana liko chini ya mahakama hii. Hata  hivyo kabla ya mahakama kutumia mamlaka yake kutoa ama kuzuia dhamana inapaswa kuangalia mazingira ya kosa husika", amedai Dk.mango. Ameiomba Mahakama kuzingatia maslahi ya umma kwa ujumla wake kwa hatari ya makosa wanayoshtakiwa nayo na usalama wa taifa.

  Wakili Faraja alidai kuwa kama washtakiwa wataruhusiwa kurudi uraiani baada ya matamko hayo ni wazi kwamba haki ya upande wa pili itapotea, matamshi yaliyotolewa na washtakiwa yana madhara endelevu kwa watanzania kwani tuna taarifa za upelelezi kwamba baadhi ya mambo yaliyoongelewa, ushawishi uliotolewa unaonekana kuna utekelezaji wa kihalifu.
  Akijibu hoja hizo Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai hakuna chochote cha kisheria kilichozungumzwa kutoka kwenye dawati, kilichoko mbele ya mahakama sio maombi ni pingamizi la dhamana na hakuna ushahidi wowote kwa yaliyosemwa.
  Pia Kibatala amedai Wakili anashindwa kutofautisha askari mpelelezi na mawakili wasomi na Mahakama haiwezi kumnyima mtu dhamana kwa taarifa ambazo haziko mahakamani. Aliendelea kudai  hati ya mashtaka haina jina wala sahihi ya aliyeandaa jambo ambalo limekatazwa na Mahakama Kuu.
   Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakiwa wamekaa katika benchi la mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusubiri kusomewa mashtaka yao
   Mwenyiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa na washtakiwa wenzake  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji, Peter Msigwa, Kaimu katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba , John Mnyika , Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini , Ester Matiku wakipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

  Baadhi ya viongozi wa Vyma vya Siasa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama kusuburi kushuhudia msafara wa viongozi wakuu wa Chadema wakipelekwa Rumande

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).

  Imesema mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya Tanesco makao makuu imesema shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali,hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake.

  Pia Kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki. 

  "Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa Tanesco itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike Tanesco ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.

  " Baadhi ya taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji. Tunapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka,"imesema taarifa hiyo.

  Ufafanuzi huo wa Tanesco unakuja baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadai mkataba kati ya Tanesco na Maxcom(MaxMalipo)wa kuuza token za umeme utakwisha mwisho mwa nwezi hui na hakuna dalili wataongezewa mkataba.

  Taarifa hiyo ikadai kutokana na hali hiyo ni vema wateja wakachukua tahadhari kwani baada ya Machi 31anayetaka kununua umeme itabidi aende ofisi za Tanesco.

  Hivyo Tanesco wameamua kufafanua kuhusu mfumo mpya ambao utatumika wateja kununua umeme na kuwahakikishia wataendelea kununu kama zamani na hakutakuwa na tatizo lolote.

  0 0
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,(WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri jijini Mwanza ili kupata elimu juu ya umuhimu wa kuzingatia kanuni za Usalama na afya mahala pa kazi ili kumlinda mfanyakazi na madhara yatokanayo na mazingira duni ya kufanyia kazi. Semina hiyo imefanyika jijini humo leo Machi 27, 2018 na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza. Katikati ni Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, ambaye idara yake ndiyo imeandaa semina hiyo.
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID-MWANZA
  TATHMINI ya majanga (risk assessment), mahala pa kazi inapaswa kufanywa kila mwaka kwa mujibu wa sheria, Meneja Tathmini za Usala na Afya mahala pa kazi wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Naanjela Msangi amesema.
  Bi. Msangi ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya majanga (Risk Assessment) kwenye viwanda na maofisini wakati wa semina ya mafunzo kwa Mameneja na Maafisa Waajiri waandamizi kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Mwanza, Machi 27, 2018.
  “Sheria inatamka kiwanda au ofisi yoyote ile inapaswa kufanya tathmini kabla ya kuanza uzalishaji, majanga haya yanaweza kutokea wakati tayari uko kwenye operations,(uendeshaji) sasa ni vema uanze kufanya risk assessment kabla ya kuanza uzalishaji.” Alifafanua.
  Akizungumzia sababu za kufanya tathmini kila mwaka, Meneja huyo alisema, yawezekana kiwanda au ofisi kubadilisha njia ya uzalishaji kutoka ilivyokuwa awali hivyo itasaidia kujua vile viwango vya hatari ya kutokea majanga vimeongezeka au la ili uchukue hatua za kujikinga na kutokea kwa majanga mahala pa kazi.
  Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, aliwaasa waajiri kuzingatia sheria na mahusiano mahala pa kazi ambayo pamoja na mambo mengine inamtaka mwajiri kuhakikisha wafanyakazi wake wanafanya kazi katika mazingira salama, kwa kuwapatia vifaa vya kujikinga na majanga (Personal Protective equipments).
  “Pamoja na wajibu wetu wa msingi wa kusajili waajiri na kuhakikisha wanawasilisha michango ya kila mwezi kwa ajili ya wafanyakazi wao, ili panapotokea ajali, kuumia au kifo mahala pa kazi na hatimaye Mfuko kuchukua jukumu la kulipa Fidia kwa muathirika au wategemezi wake,  lakini pia tunalojukumu la kuzuia majanga yasitokee mahala pa kazi kwa kutoa elimu na ndiyo lengo mahsusi la semina hii ya leo.” Alisema Dkt. Omar.
  Alisema, dhumuni lingine la semina hiyo ni kuzungumzia masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu wa WCF na masuala hayo n I pamoja na kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda na kudumisha usalama na afya mahala pa kazi na masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.
  “Vile vile ni kuelimisha haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika kuwezesha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kushughulikia kwa ufanisi madai ya Fidia kwa Wafanyakazi.” Alifafanua.
  Kwa ufupi niseme tu kwamba Mfuko una faida kubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa kwa ujumla kwani hivi sasa wafanyakazi wanauhakika wa kinga ya kipato kutokana na majanga yasababishwayo na ajali, magonjwa au vifo kutokana na kazi, alisema Dkt. Omar.
  Mmmoja wa washiriki wa semina hiyo Bi.Asmini Gombo, ambaye ni Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya Mincom Rockdrills Tanzania Limited, alisema wao kama kampuni swala la kufanya tathmini ya majanga mahala pa kazi lina umuhimu mkubwa kwani sio tu linakusaidia kutambua ni vitu gani ambavyo kampuni inaweza kuboresha ili kuepuka majanga lakini pia inasaidia kudumisha usalama na afya za wafanyakazi, “Sisi huwa tunafanya tathmini kila baada ya miezi mitatu na hii imekuwa ikitusaidia sana kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu unazingatiwa na nitoe rai tu kwa wenzangu wajenge ratiba ya kufanya zoezi hili si lazima iwe kila baada ya miezi mitatu kama tunavyofanya sisi lakini hata kila baada ya miezi sita kwani utapunguza majanga na hivyo kuokoa rasilimali watu na mali za kampuni pia." Alisema.

  Pia alisipongeza WCF kwa kutoa elimu kwani awali walijua kazi kubwa ya Mfuko ni kusajili na kukusanya michango kutoka kwa waajiri kumbe pia inao wajibu wa kuelimisha waajiri kuepukana na majanga yanayoweza kutokea sehemu za kazi.
  Asmini Gombo, Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya Mincom Rockdrills Tanzania Limited, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu elimu aliyopata kutokana na semina hiyo.
  Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Dkt. Omar.

  Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina.
  Mshiriki akisoma kijarida chenye maelezo yahusuyo shughuli za Mfuko.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto), Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia), na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, wakiwa tayari kuanza kwa se mina hiyo.
  Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, akitoa mada juu ya wajibu wa mwajiri kutekeleza sharia iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi. ambapo alizungumzia wajibu wa mwajiri kujnisajili na Mfuko, kupeleka michango kila mwezi, na kutoa taarifa za wafanyakazi wake kwa usahihi.
  Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Dkt. Omar.

  Washiriki kwa umakini wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa WCF.
  Bi. Naanjela Msangi

  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa WCF jijini Mwanza Machi 27, 2018.
  Dkt. Abdulsalaam(kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki mwishoni mwa semina.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, (katikati), na Robert Duguza, (kushoto), Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, wakimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye alihitaji ufafanuzi Zaidi kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko huo mwishoni mwa semina.
  Meneja Tathmini za Usala na Afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi(kushoto), akimsikiliza mmoja wa washiriki aliyehitaji ufafanuazi Zaidi wa masuala yaliyozungumzwa kwenye semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar (mwenye tai) na Meneja Tathmini za Usala na Afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (wapili kulia), wakisikiliza hoja mbalimbali za washiriki wa semina mara baada ya kumalizika kwake.
  Afisa Matekelezo (Compliance Officer), wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. George Faustine(mwenye tai), akifafanua masuala mbalimbali kwa washiriki mwishoni mwa semina hiyo.
  Sehemu ya picha ya pamoja ya washiriki

  0 0


  0 0  BancABC Tanzania Limited Managing Director Dana Botha addresses the media in Dar es Salaam yesterday after the bank announced the reduction of lending rates for term loans, over draft and mortgages. He is flanked by the banks Head of Retail and Commercial banking Joyce Malai.
  BancABC Tanzania Limited Managing Director Dana Botha – right, Head of Retail and Commercial banking Joyce Malai center and the banks Head of Treasury Barton Mwasamengo hold placards after the bank’s announcement of reduction of lending rates for term loans, over draft and mortgages.


  · Amongst the First to act on the BOT’s monetary policy

  BancABC, which is part of Atlas Mara a London listed entity, has made yet another step ahead of the market and is announcing a reduction in lending rates aimed at easing the repayment burden and increasing borrowing to existing and new customers with effect from April 1, 2018.

  Speaking in Dar es Salaam, the BancABC Managing Director, Mr. Dana Botha said they will be reducing their lending rates for term loans, over draft and mortgages for customers of a good standing.

  “Last year, most banks experienced liquidity challenges which ultimately affected their lending capabilities. For a couple of months now the Government through BOT has stepped up and has been advocating the reduction of lending rates from Commercial Banks through reducing regulatory requirements such as Statutory Minimum Reverse, Discount rates, Treasury Bills and lending to Banks at a lower rates. This has enabled lending to be more affordable for Individuals, SME’s and Corporates borrow consequently enhance / boost their businesses with the aim of improving the business economy and we are glad to be amongst the first Banks to announce this move,” he said.

  He said their customers will now enjoy a new or renewed loans at much more affordable payback rate. “We believe more customers will now come knocking at BancABC because of this new move,” He said and added that lower rates will attract the majority of Tanzanians individuals and businesses alike – in urban and rural areas to have an opportunity in prove the quality of life or increase business. This will ultimately stimulate economic growth.

  “High lending rate has been a challenge to majority of Tanzanians especially the middle class but we now believe even those who could not borrow can use this opportunity to boost their businesses and improve lives in general,” He said.

  According to Dana the new measures by the government will stimulate growth by encouraging banks to lend rather than invest in Treasury and Government bonds and this will attract our customers in borrowing and increase quality of life and business growth.

  The banks’ Head of Retail and Commercial Banking, Joyce Malai said that BancABC serves over 60,000 retail customers with different products, with this new move it gives us an opportunity to cross sell and attract even more products per customer with is a key focus on more affordable mortgage rates which has been a cry for many middle class Tanzanians. We also take this advantage to support our SME and Corporate customers with affordable loans and Overdrafts from one of the best financial institution in the country.

  “Today’s announcement of low lending rates is a key milestone to BancABC as we align our vision to the premier financial service institution in Sub- Saharan Africa and obtain top 5 market position in countries that we operate, said Malai.

  BancABC is leading this challenge put to the industry by the BOT to reduce rates.  0 0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zilizochukuliwa na wizara kwa kufungia baadhi ya nyimbo zinazokiuka maadili, kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza na kulia Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’. 
  Naibu Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zilizochukuliwa na wizara kwa kufungia baadhi ya nyimbo zinazokiuka maadili, katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe na kulia ni Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’. 
  Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maridhiano yaliyofikiwa kati yake na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana jijini Dar es Salaam, Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. Picha na Idara ya Habari - MAELEZO

older | 1 | .... | 1549 | 1550 | (Page 1551) | 1552 | 1553 | .... | 1898 | newer