Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1550 | 1551 | (Page 1552) | 1553 | 1554 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili waliojumuika pamoja wilayani Tarime mkoani Mara kupanga namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa pamoja. Wa tatu kutoka kulia (walioketi) ni Mkuu wa Msafara wa wataalam kutoka Tanzania Bw. Huruma Lugala na kulia kwake ni Mkuu wa Msafara kutoka Kenya Bw. Julius Rotich.
  Mkuu wa zoezi la Uhamasihaji katika kazi ya kuhakiki na kuimarisha mipaka ya Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya Bw. Raymond Bagenda kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha wataalam wa masuala ya upimaji ardhi kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili. Kikao hiko kilichofanyika wilayani Tarime mkoani Mara kinapanga namna ya kutekeleza kazi hiyo kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais nchini Kenya inayohusika na Usimamizi wa Mipaka ya Kimataifa (KIBO) Bw. Joseph Rotich.

  Baadhi ya Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na katika ofisi zingine za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo kuhusu namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania.

  …………………………………………………………………….

  Na Rehema Isango, Tarime, Mara

  Timu za watalaamu wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania na taasisi za usimamizi wa Ardhi nchini Kenya zimekutana wilayani Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kazi ya kuhakiki na kuimarisha mpaka wa Kimataifa baina ya nchi hizi mbili.

  Mapema mwezi Machi, Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alitangaza azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kuimarisha mipaka yake kwa nchi jirani za Kenya na Uganda baada ya ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

  Hatua ya uhakiki na uimarishaji wa alama za mipaka ya mikataifa inatokana na mpaka huu kuwa wa siku nyingi na haukuwa wazi katika maeneo mengi pia baadhi ya alama hizo kuharibiwa, kung’olewa au kuchakaa na hivyo kusababisha Serikali pande zote kushindwa kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama.

  Katika uimarishaji wa alama hizo za mipaka hivi sasa, kutaongezwa alama mpya ndogo zinazoonana kwa umbali wa mita 100 pamoja na kubainisha eneo la ardhi huru kwa kila upande wa nchi (buffer zone).

  Mpaka kati ya Tanzania na Kenya una jumla ya urefu wa Kilommita 760 kuelekea bahari ya Hindi ambapo awamu ya kwanza ya kazi ya uimarishaji mpaka inayofanyika hivi sasa itahusisha urefu wa Kilomita 238 kutoka kando ya Ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natron mkoani Arusha.

  Baadaye, kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka itaendelea katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga na kisha itafanyika katika maeneo yote yanayohusika na mipaka ya kimataifa nchini.

  Uimarishaji wa mipaka ya kimataifa nchini umefanyika mara ya mwisho mwaka 1975 kwa kurudishia alama ambazo ziliondolewa na kuongeza nyingine mpya kwa kuzingatia alama zilizopo.

  Mbali na Kenya nchi nyingine zinazopakana na Tanzania ni; Msumbiji, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi, Rwanda, Uganda pamoja na visiwa vya Komoro na Shelisheli.

  0 0
 • 03/28/18--03:00: TANZIA


 • 0 0

   Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakibonyeza kiwashio ikiwa ni sehemu ya kuuwasha umeme umeme mtaa wa Mbwawa Mkoleni,wilayani Kibaha.
  Picha na Mwamvua Mwinyi

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  SERIKALI imetoa tahadhari kwa watumishi ,wakandarasi na wadau wa sekta ya Nishati wanao husika na miradi wasitikise kiberiti kwa kuhamasisha maandamano kupitia shida za wananchi.

  Aidha wizara ya Nishati imesema itatumia kiasi cha shilingi trilioni sita kwa ajili ya kuyafikia maeneo 7,873 nchi nzima ili yaunganishwe na huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

  Hayo yalisemwa kwenye mtaa wa Sagale Magengeni kata ya Viziwaziwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoko kwenye miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

  Alisema kuwa ole wake anayetumia tumia shida za wananchi kuhamasisha maandamano kwani akibainika chamoto atakiona.

  Mgalu alieleza hayo baada ya kauli ya mwananchi mmoja ambaye alikuwa akitaka umeme na kuambiwa kama anataka umeme aandamane maandamano ya Mange Kimambi.

  “Serikali imeshtushwa tena inatokea maeneo haya kwa watu waliopewa dhamana mkandarasi ni dhamana huwezi kuleta jeuri kama unazo fedha usingeomba kazi hizi ni fedha za Rais Dk. Magufuli usilete jeuri,” alisema Mgalu.

  Alisema kuwa, hawezi kuamini kama ni watumishi wa serikali wanaweza kufanya hivyo lakini kutokana na kauli hiyo ya mwananchi kujibiwa hivyo watavituma vyombo vinavyohusika vifanye kazi kumbana aliyetoa kauli hiyo kwani watawatafuta kwa udi na uvumba hadi wapatikane.

  “Kama hatapatikana itabidi tuitishe gwaride la utambulisho kuweza kumbaini mtumishi aliyetoa kauli hiyo mbaya ambayo inawakatisha tamaa wananchi wakati kupata huduma ni haki yao ndo maana sisi tuko huku ingukuwa hivyo tusingekuja tungekaa lakini tunawatumikia wananchi hivyo hao wakamatwe wajieleze,” alisema Mgalu.

  Alisema kuwa tanesco mkoa wa Pwani itabidi wahakikishe mtu au watu waliohusika na kutoa kauli hiyo wanabainika ambao walikuwa wakifuatilia masuala ya mita huko eneo la Viziwaziwa.

  Alibainisha kuwa maandamano hayo hayapo na hakuna mtu atakayethubutu kufanya hivyo wananchi hawapaswi kushughulika na suala hilo watu waendelee na kazi zao waachane na watu wasiyoitakia nchi mema.

  Akizungumza mbele ya naibu Waziri mwananchi huyo jina tunalo alisema kuwa waliambiwa waweke mfumo wa umeme kwenye nyumba zao ili waunganishiwe umeme.

  Alisema kuwa walijibana lakini chaajabu nguzo za umeme zikapelekwa watu ambao wanaviwanja tu hakuna hata nyumba wao waliojenga na kuweka mfumo wa umeme hawakuwekewa nguzo.

  “Tuliambiwa kuwa huu ni umeme wa msaada umefikia kilometa moja tu tukafuatilia hadi tanesco kwani tunajua umuhimu wa umeme lakini wakati wale wasomaji wa mita walivyokuja tulipouliza majibu yalikuwa kama tunataka tuandamane na maandamano ya Mange Kimambi,” alisema kwa masikitiko mwananchi huyo.

  Aidha mwananchi huyo alisema kuwa kama umeme huo wa REA hautakuwepo basi wapewe wa Tanesco ambapo naibu Waziri alisema kuwa atafuatilia suala hilo ili waliohusika wachukuliwe hatua kama ni wa Tanesco au ni upande wa mkandarasi.

  Wakati huo huo Mgalu akiwa Mbwawa alieleza kwenye awamu ya kwanza kupitia REA awamu ya kwanza waliyafikia maeneo 3,559 awamu ya pili wameyafikia 4,314 na kwa sasa bado maeneo 7,873 nchi nzima ili kufikisha huduma hiyo kwa wananchi wengi ambapo kwa mkoa wa Pwani kwa miradi hiyo imetumia kiasi cha shilingi bilioni sita.

  “Tunatarajia kuhakikisha watu wanahiotaji umeme kwa wale wa vijijini ambapo zinatakiwa trilioni sita kuhakikisha tunawafikia wananchi pia tunataka kutekeleza agizo la Rais ifikapo Juni 2021 nchi nzima watu wawe wamepata huduma ya umeme,” alisema Mgalu.

  Suala la ujazilizi tumeomba awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza na tayari tumeomba fedha kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 kutotimia kwenye maeneo

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alisema serikali iko pamoja na wananchi katika kuhakikisha wanapata huduma hiyo muhimu ya nishati ya umeme kwani ni sehemu ya maendeleo ya nchi.

  Alisema serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kama ilivyoahidi ambapo inaendelea kutekeleza ahadi zake na kumshukuru Rais kwa jitihada zake za utekelezaji miradi ya umeme.

  Koka alibainisha kutokana na umuhimu wa suala la nishati rais aliamua kuifanya wizara hiyo kujitegemea na imeonyesha matumaini kwani sasa mawaziri wanashuka hadi kwa wananchi.

  0 0

  Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaongoza hapa nchini unawapa fursa Watanzania kushinda kitita cha Shilingi milioni 260 katika droo itakayofanyika jumapili ya pasaka na kuonyeshwa moja kwa moja saa 3:30 usiku

   Taifa linapojiandaa na sherehe za Pasaka, Tatumzuka imeungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka. Kitita hicho kinono cha milioni 260 ambacho hakijawahi kutolewa kwa mtu katika historia ya nchi hii sasa kitatolewa kwa mshindi mmoja atakayebahatika kwenye ‘PasakaMzukaJackpot’ siku ya tarehe 31/3/2018.

  Bwana Sebastian Maganga, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatumzuka, ameuelezea umma namna ilivyo rahisi kuingia katika droo. “Wiki hii ukiwa na shilingi 500 tu, kwa kutumia; Mpesa, Tigo pesa au Airtel Money, ingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111, kisha weka namba zako tatu za bahati na hapo utakuwa umeingia rasmi kwenye droo ya milioni 260 za PasakaMzukaJackpot” alielezea Maganga

  Hicho sio kitu pekee ambacho Tatumzuka inatoa msimu huu wa sikukuu, pia una nafasi ya kushinda milioni 10 kila siku na milioni 6 kila saa.“Ukinunua tiketi moja ya shilingi 500, Tatumzuka inakupa nafasi ya kuingia katika droo 3 tofauti na hivyo kukuongezea nafasi za kushinda tofauti na michezo mingine ya namba” Maganga alisisitiza

  Tatu Mzuka pia imetumia fursa hiyo kuwatambulisha washindi wa wiki iliyopita ambao walitokana na droo ya 34 ya Tatumzuka jackpot.Bi Hanifa kutoka Magomeni, Dar es Salaam alijishindia milioni 5. Bwana Juma Mkombozi kutoka Magomeni, Kagera alijishindia milioni 7. Bwana Prosper Munuo kutoka Bunju A alijinyakulia milioni 5 na Magreth Nkwabi wa Kahama, Shinyanga alipata milioni 3.

  Washindi wote wakiwa wenye furaha baada ya ushindi walisisitiza kwamba wataendelea kucheza kujaribu bahati zao kwenye dau la kihistoria la milioni 260 jumapili hii.‘Droo hii ya kihistoria itaonyeshwa moja kwa moja kupitia ITV, Clouds TV na TV1 jumapili hii saa 3:30 usiku’ Bwana Maganga aliufafanulia umma. 
   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano  Sebastian Maganga akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar akielezea kuhusu Tatumzuka kuungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka.
   Mmoja ya washindi akikabidhiwa mfano wa Hundi yake yenye thamani ya shilingi milioni tano na la  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sebastian Maganga.
   Washindi wa Tatu Mzuka Jackpot wa wiki iliyopita kwa pamoja wakifurahi

  0 0
  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya Tamasha hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
  Mwimbaji Jesca Honore akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Chrstopher Mwahangila mwimbaji mwingine ambaye atashiriki katika tamasha hilo mkoani Mwanza na Simiyu na katikati ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa tamasha hilo.
  Mwimbaji Upendo Nkone akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye pia atakuwepo katika tamasha hilo katikati ni Ufo Saro mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo.
  Mwimbaji Martha Baraka akitibitisha kushiriki katika tamasha hilo kutoka kushoto ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo na katikati ni Mzee Rainfred Masako mmoja wa Viongozi wa Dira TV.
  Mwimbaji Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake na kuthibitisha kwamba yuko tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha a Pasaka Kanda ya Ziwa kushoto ni Mwimbaji mwenzake Beatrice Mwaipaja .
  Mwimbaji Christopher Mwahangila akifanya vitu vyake katika moja ya video zake alizowahi kurekodi.

  .................................................................................................

  Ni siku nne zimebaki kengele ya Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja  wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

  Mara nyingi Tamasha la Pasaka limekuwa likifanyika jijini Dar es Salaam safari hii Msama Promotion imeamua kulifanya tamasha hilo Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, wapenda muziki wa injili wa Kanda ya Ziwa na viunga vyake watapata burudani ya nyimbo za kumsifu na kumtukuza Mungu huku wakipata mahubiri kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo.

  Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu ambako nako watasheherekea kwa nyimbo za injili.

  Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

  Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake na kubwa zaidi ni kwamba kuna baadhi ya waimbaji wataimba wakipiga vyombo vya muziki Live ili kuleta ladha na burudani zaidi katika tamasha hilo..

  Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, mwimbaji Rose Muhando atazindua albam yake mpya “Usivunjike Moyo” kati ya waimbaji wengi kutoka hapa nchini Tanzania na nje watakaofanya mambo makubwa katika tamasha hilo.

  Inafahamika kuwa Rose Muhando huwa hahitaji utambulisho. Ni mwanamuziki mkubwa kati ya waimbaji wa muziki wa injili ambaye Muumba wa Mbingu na Ardhi amenyanyua kipaji cha kuimba kilichoambatana na sauti maridadi. Muziki wa Rose Mhando unapopigwa wapo ambao wanasimamisha shughuli zao kwa muda ili kumsikiliza kwanza.

  Kwa Rose Mhando mwenyewe anajua ukubwa wa Tamasha la Pasaka. Wakati anazungumzia tamasha hilo ameeleza wazi amejiandaa vya kutosha. Hivyo atakuwa Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuonesha kile ambacho amewaandalia. ambapo pia atazindua albamu yake mpya inayoitwa

  Imekuwa kawaida kwa matamasha ya Pasaka kuleta wanamuziki kutoka nje ya nchi. Kwa taarifa tu ni kwamba atakuwepo Ephrem Sekereti kutoka Zambia. Mashabiki wa muziki wa Injili wanamfahamu vema Sekeleti na ubora wa kazi zake.

  Wakazi wa Mwanza na Simiyu ni zamu yenu mwaka huu kupitia Tamasha la Pasaka kuweka historia ya kumshuhudia mwanamuziki Sekereti akitoa burudani tena ndani ya ardhi ya Tanzania. Karibu Sekereti wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa wanakusubir.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda  Mhe.Ernest Mangu na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi  wa  Urusi leo wamekutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma.

  Mabalozi hao walifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani Dodoma  kwa lengo la kumuaga ,walimuahidi Makamu wa Rais kufanya kazi kwa ajili ya Tanzania.

  Wamemuambia Makamu wa Rais wanajua dhamana kubwa waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na dhamira yake ya Tanzania ya Viwanda .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi(kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu(kulia) ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

   Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa, Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto kwake) alieambatana na baadhi ya Mawaziri.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassim Majaliwa (kushoto) akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho pia kilihudhuriwa na Baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Suleiman Kakoso (watatu kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao cha uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Adelardus kilangi (katikati) na Mjumbe wa Kamati, Mhe. David Silinde (kushoto) kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri.
   Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.

  Na Hamza Temba - WMU-Dodoma
  ...........................................................................
  Kufuatia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutafuta wawekezaji wa Kimataifa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta utalii hapa nchini, Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China imejitokeza kwa lengo la kuwekeza katika utoaji wa huduma za kitalii zenye ladha na mandhari ya Kichina.

  Mwenyekiti wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Tony, amesema kampuni hiyo imepanga kujenga hoteli za kitalii za kichina katika mji wa Karatu jijini Arusha na Serengeti mkoani Mara.

  Akizungumza na Waziri wa Maliasil na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ofisini kwake mjini hapa jana kwa ajili ya kutambulisha mradi huo, Tony alisema mradi huo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii wa China wanaotembelea Tanzania.

  Alisema kupitia mradi huo jumla ya magari 500 ya safari  za utalii yatanunuliwa (Safari Cars) kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii hao wakati wa kutembelea maeneo ya vivutio hapa nchini.

  Pamoja na magari hayo alisema kampuni hiyo pia imepanga kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege kutoka China hadi Tanzania ili kupunguza muda wa usafiri na gharama.

  "Kupitia mradi huu, tunategemea kuhudumia watalii 200,000 kwa mwaka kutoka nchini China na kutengeneza ajira zaidi ya 200 kwa Watanzania" alisema Tony.

  Alisema kwa sasa ni watalii 35,000 tu kutoka China wanaotembelea Tanzania kwa mwaka, na kwamba kupitia mradi huo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

  Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema mradi huo umekuja wakati muafaka  wakati huu Serikali kupitia Wizara yake imeshaweka mikakati mahususi ya kupanua wigo wa soko la utalii nchini China.

  Alisema miongoni mwa mikakati hiyo inayolenga kuvutia watalii zaidi ya 200,000 kwa mwaka katika kipindi cha muda mfupi wa miaka mitatu, ni kuwakaribisha wachina wenyewe kuja kuwekeza kwenye mahoteli na huduma zenye ladha na mandhari ya kikwao. Mataifa mengine ni Israel, Urusi na Oman.

  Alisema kwa sasa ni idadi ndogo tu ya watalii wa China wanaotembelea Tanzania ukilinganisha na ukubwa wa soko la nchi hiyo.

  Aliahidi kuwapa ushirikiano wawekezaji hao ikiwa ni pamoja na kuwapa maeneo kwa ajili ujenzi wa hoteli hizo za kitalii ndani ya maeneo ya hifadhi ili kuwezesha ongezeko la watalii kutoka nchini humo.

  "Kwa yale maeneo mtakayohitaji ambayo yapo nje na maeneo yetu ya hifadhi tunayoyasimamia, tutawasiliana na mamlaka husika ili muweze kuapatiwa maeneo ya kuanzisha uwekezaji huo muhimu kwa taifa" alisema Dk. Kigwangalla.

  Aliwataka pia wawekezaji hao kupitia taratibu zote za kuwekeza hapa nchini ikiwa ni pamoja na kujisajili katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kusajili kampuni ya utalii hapa nchini na kuwasilisha andiko la mradi na namna ya utekelezaji wake.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
   Wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Kigwangalla ofisini kwake mjini Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi flash yenye picha za wanyamapori wa Tanzania Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing, aliyefahamika kwa jina moja la Tony kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza hapa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
   Waziri Kigwangalla akiendelea na mazungumzo na wakezaji hao.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
     Mazungumzo yakiwa yanaendelea.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana baada ya kampuni hiyo kuwasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.

  0 0  Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam,
  Serikali imeanza maadalizi ya kutengeneza Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

  Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

  “Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi”, alisema Kichere.

  Kichere alieleza kuwa, uwepo wa wakuu hao na wadau wa sekta binafsi katika mkutano huo ni kiashiria cha kuunga mkono adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

  Kamishna huyo Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliongeza kuwa, Serikali imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.

  Naye Mratibu wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena kutoka TRA Felix Tinka amezitaja faida za mfumo huo  kuwa ni pamoja na kurahisisha na kuwezesha biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali kwa waingizaji na waondoshaji wa mizigo.

  “Mfumo huu una faida nyingi, mbali na hizo nilizozitaja awali, pia kuna kuimarisha usalama, kuimarisha uadilifu na uwazi katika utendaji kazi, kupunguza biashara haramu, kupunguza gharama, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo katika vituo vya forodha pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati”, Alisema Tinka.

  Utekelezaji wa Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani umegawanyika katika maeneo makuu matano ambayo ni eneo la usimamizi wa mapato, uwezeshaji wa usafiri na uchukuzi, utekelezaji wa sera na biashara, pamoja na usimamizi wa afya na usalama wa umma, usalama wa uchumi pamoja na ugawaji.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mussa Shilla. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga  (TCAA), Hamza Johari akitoa mchango wake wakati wa mkutano huo. 
  Mwakilishi wa Mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo akichangia hoja leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.
  Katibu Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Abel Urono akitoa mchango wake katika mkutno huo. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere (kulia) akibadilishana mawazo na Nibu Kamishna wa TRA, Zanzibar Mcha Hassan baada ya kuhudhuria mkutano huo. 
  Mshauri wa Tehama, Abdulrahman Mbamba akitoa mada kwa washiriki wa Mkutano huo. 
  Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwenye mkutano huo. 

  0 0


  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

  Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima .

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo .

  Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vya afya, na kuwepo kwa vipimo cha kuchunguzia ugonjwa huo na matumizi ya vyandarua vilivyopigwa dawa.

  Amesema vyandarua ndio kinga tahabiti ya kujikinga na Malaria ambapo kwa Zanzibar Asilimia 77 ya Wananchi wanatumia vyandarua kiwango ambacho bado hakijaridhisha kufikia vigenzo vya wizara ya afya zanizbar ya Asilimia 100 na shirika la afya ulimwenguni WHO Asilimia 85.

  Hata hivyo Meneja Abdallah amesema kwa sasa licha ya Zanzibar kupunguza maambuzi ya wagonjwa wa Malaria lakini amekiri ugonjwa huo bado upo chini ya Asilimia moja na ambapo vigezo vinavyotumika kuhakikisha Wananchi wanaobainika kuwa na vimelea anafuatiliwa katika familia yake ili kuhakikisha anakuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.

  Aidha amesema bado kuna maeneo ambayo yanatoka wagonjwa wengi wanaobainika kuwa na vimelea vya Malaria ikiwemo Wilaya ya Maghariba A na B , Wilaya ya kati na Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba na kwa wale Wananchi ambao wanatoka Tanzania bara katika mikoa ya Mwanza na Geita.

  Kwa upande wake Waziri Nyoni Meneja Miradi wa VectorWorks amesema watakuwa na kazi ya kuhamasisha Jamii kuhakikisha vyandarua wanavyopatiwa wanavitumia ipasavyo ili kujikinga na ugonjwa na Malaria.

  Kampeini ya kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP .  Meneja wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ally akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
  Meneja Miradi kutoka VectorWorks akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti


  0 0

  Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza. 

  Msaada huo umetolewa Jumanne Machi 27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kupanga mipango na mikakati ya kupambana na VVU na Ukimwi. 

  Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mashine hizo ni kwa ajili ya vituo vya afya vya Katunguru na Kabila vilivyopo wilaya ya Sengerema, hospitali ya Ngudu iliyopo wilayani Kwimba na zahanati ya Kirumba na kituo cha afya cha Buzuruga vilivyopo wilayani Ilemela. 

  Dk. Sekela alisema mashine hizo tano zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 zitatumika kutolea tiba mgando kwa akina mama wanaokutwa na dalili za mwanzo za kansa ya uzazi. “Mbali na shirika letu kuendelea kuboresha huduma za kinga na matunzo pia tunatoa huduma ya uchunguzi wa dalili saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama”,alieleza. 

  Alisema huduma hiyo hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza. Dk. Sekela alisema shirika hilo mpaka sasa limetoa msaada wa ‘cryotherapy machines’ 17 katika mikoa sita ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Tanga,Geita,Simiyu na Mara zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 115.6. 

  Dk. Sekela pia alikabidhi kompyuta 18 zitakazotumika kuhifadhi takwimu za wateja wa CTC katika vituo vya afya husika na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi Zaidi mkoani Mwanza. “Tangu tuanze mradi wa Boresha, tutakuwa tumetoa jumla ya kompyuta 82 kwa mkoa wa Mwanza ambazo zinatumika kutunza taarifa za watu wenye VVU na Ukimwi”,alisema. 

  Akizungumza kwa niaba ya wilaya zilizopokea mashine hizo,Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alilishukuru shirika la AGPAHI kwa kutoa msaada huo na kwamba watatumia vifaa vilivyotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa. Awali akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella aliwataka wadau wote kuungana na kushirikiana ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya VVU mkoa huo ambayo sasa ni asilimia 7.2 yanapungua. 

  AGPAHI ni shirika la Kitanzania linalofanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kutoa huduma za afya hususani watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi kwa fadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC). 
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kabla ya makabidhiano ya kompyuta na mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’.- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea namna shirika hilo linavyotoa huduma ya kuwapima saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake. 
  Dk. Sekela akizungumza na wadau wa afya mkoani Mwanza. 
  Maboksi yenye kompyuta na mashine za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ zilizotolewa na shirika la AGPAHI kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Mwanza. 
  Kulia ni Dk. Mwakyusa akiwa ameshikilia moja ya mashine inayotumika kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’. 
  Dk. Sekela akizungumza ukumbini. 
  Katikati ni Dk. Sekela Mwakyusa akikabidhi mashine kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella (wa pili kushoto) na viongozi wa wilaya ya Sengerema. 
  Zoezi la makabidhiano likiendelea. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa CDC nchini, Dk. Eva Matiko. 
  Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha akipokea cryotherapy machine. 
  Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole akitoa neno la shukrani baada ya makabidhiano ya mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kompyuta 18 zilizotolewa na shirika la AGPAHI. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0


   Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
   Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
   Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)

   Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na 
  umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

   Na Fredy Mgunda,Iringa.

  MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

  Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

  “Mradi wowote ule ukiwa na ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema  Masenza

  Masenza alisema kuwa mradi huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.

  Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.

  “Jamani wananchi ambao mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza

  Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya maji.

  “Sisi kama RDO ambao ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali

  Filipatali  alisema kuwa mradi huo wa maji  utazaliza ujazo wa lita 776  kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.

  “Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali

  Filipatali alisema kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali  kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo


  “Hizi changamoto zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali

  0 0  Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Taifa (NIC) Sam Kamanga akiwa na watendaji wake jana katika banda la NIC Mlimani City wakati wa maonyesho ya wadau wa sekta ya bima kandokando ya mkutano wao maarufu kama African Insurance Summit 
  Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza wakati wa mkutano huo. 
  Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba akizungumza wakati alipotembelea banda Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwenye maonyesho ya makampuni ya Bima nchini yaliyofanyika jana Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT), kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga na kulia ni Afisa Bima Mwandamizi wa NIC Konjeta Mwaipopo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Masoko waShirika la Bima la Taifa Elisante Maleko, akimkabidhi zawadi ya kikombe Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba alipotembelea banda la NIC katika maonyesho ya wadau wa bima Jijini Jana 
  Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba kando kando ya mkutano huo wa wadau wa bima African Insurance Summit

  0 0

   Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akizungumza wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga.
   Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akizungumza wakati wa kukabidhi Vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupitia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel Tanzania.Kulia ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
   Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga,akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Mohammed Ali Mohammed.Katikati ni ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
  Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Elias Joseph. Katikati ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya

  MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) leo imekabidhi vyeti kwa wanafunzi26 waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao kupitia aplikesheni ya VSOMO ambapo kati yao wanafunzi 18 ni kutoka VETA kipawa na 8 VETA Mwanza
  VSOMO ni mfumo unaotoa mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao unaotolewa chini ya ushirikiano kati ya kampuni ya simu ya Airtel pamoja na Mamlaka ya mafunzo stadi VETA ambao unalenga kuleta tija katika mapinduzi ya elimu nchini.
  Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti, Mkuu wa VETA Kipawa, Bwn Sospeter Dickson Mkasanga aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana nao katika  kuanzisha aplikesheni ya VSOMO inayowawezesha wanafunzi kupata masomo ya ufundi wakati wowote mahali popote nchini kupitia simu zao za mkononi. Pia aliwapongeza wanafunzi waliamua kutumia technologia ya simu katika mambo ya msingi na kupata vyeti”.
  Mkasanga aliongeza kwa kusema lengo kubwa la kutumia mfumo huu wa njia ya mtandao ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa mafunzo ya ufundi katika maeneo mbalimbali nchini, jitihada zinazoenda sambamba na adhima ya Serikali ya kutoa elimu kwa wote hususani watanzania waishio katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.
   tumeanza kuona jinsi mfumo huu umeanza kuleta tija ambapo mpaka sasa wanafunzi 105 wameshahitimu mafunzo yao na kati ya 36 wanafanya mafunzo ya vitendo katika vituo mbalimbali vya VETA nchini. Hii kwetu ni hatua kubwa kuelekea kuwawezesha watanzania wote kufikiwa na masomo ya ufundi ili kuwa na nguvu kazi yenye ueledi. Napenda kuwapongeza vijana wanahitimu masomo yao leo na kuwahamasisha jamii kuendelea kujiandikisha katika masomo haya”.
   Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrce Singano Mallya “ tunajivunia kushuhudia mabadiliko katika matumizi ya technologia ya simu  kwa kuwezesha maelfu ya watanzania kusoma kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuwatengenezea program mbalimbali zitakazowasaidia kukuza ujuzi na kuleta ufanisi katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Tunaamini VSOMO utawavutia vijana wengi kujiunga na masomo ya ufundi kwani inaenda sambamba na ukuaji wa technologia, ni ya gharama nafuu na rahisi kupatikana kupitia simu zao za mkononi lakini pia  masomo yake yamedhibitishwa na mamlaka ya ufundi stadi VETA”.
  “tunapenda kuendelea kuwahakikishia kuwa  Airtel itaendelea kushirikiana na VETA pamoja na mashirika mengine katika kuhakikisha inatumia techonologia ya simu kutatua changamoto na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi kwa ujumla” aliongeza Mallya
  Kozi 13 za ufundi zinapatikana katika aplikesheni ya VSOMO ni pamoja na  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki  Mushi  wa pili kutoka k ulia ni akimkabidhi vyakula na vifaa Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza MwanzangeJijini Tanga Otilia Chilumba kutoka kwa wanafunzi wa chuo cha utumishiwa Umma tawi la Tanga ikiwa ni mkakati wa kusaidia jamii isiyojiweza kulia ni Dastan Kingalu ambaye ni Mratibu wa shughuli hiyo
   Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki  Mushi  wa pili kutoka kulia ni akimkabidhi mbuzi mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kwa niaba ya wenzake
  CHUO cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga kimetoa msaada kwenye kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ikiwa ni mpango wao wa kuona namna ya kusaidia jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali.
  Msaada uliokabidhiwa ni mchele kg 500, unga kg 300, sukari mifuko 2 kg100,sabuni ya unga mifuko 3,sabuni ya maji box 10,sabuni ya kuogeakatoni 2,maharagwe kg 100,chumvi katoni 10,mbuzi wawili.

  Vitu vyengine ambazo vilikabidhiwa ni majani ua chai katoni 2,dagaa kg10,ngano kg 50,miswaki katoni 5,dawa za meno katoni nne,mafuta yakula ndoo tatu na mafuta ya kupikia katoni 10 vyote vina thamani yash.milioni 2.2
  .
  Akizung umza wakati wakikabidhi msaada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma JijiniTanga Elibariki Mushi aliwataka wanafunzi wajifunze taaluma hiyokatika mtazamo mpana ambao utawasaidia kuwajenga katika nyanja yakutatua changamoto zinazozikabili jamiihusika.

  Mushi alisema mbali na wanafunzi hao ku jifunza mambo mbalimbali yauga vi na utawala pia wanaowajibu wa kuona umuhimu wa kujali jamii hasazile zinazoishi katika mazingira magumu. “Tunaimani wanafunzi wetu wanajifunza masuala  ya  kuutumikia um ma lakini lazima wajikite kuangalia uhalisia halisi katika jamii zetuzinazotuzunguka na tukifanya hivyo tunaweza kuzifikia malengo yakuzisaidia jamii zilizo katika maisha duni”Alisema.

  Aidha alisema swala la maadili lipo katika mitaala ya masomo yao hivyolazima wanafunzi hao wajifunze kivitendo kusaidia jamii h itajikaambapo walijitolea kupitia michango yao kwa kujitolea vyakula.Awali kziungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzange Jijini Tanga Otilia Chilumba aliwashukuru huku akiwataka kuwa makini kwa kuzingatia masomo ili waweze kupata manufaa kwenye maisha yao 
  “Ndugu zangu niwaambieni kuwa ujana ni maji ya moto tuutumie vizuri lakini pia acheni kukataa mimba mnazowapa wasichana mtoto utakayemzaandie anaweza kuja kukuokoa baadae “Alisema.

  “Wapo baadhi ya wazee walishawahi kunililia walikwisha kuwate lekeza  watotowao ndio sababu za kuwepo kwenye kambi za kulea wazee hivyo niwasihiacheni kuwakataa kwani mnaweza kukumbana na changamoto mbeleni

   
  Alieleza pia sababu za baadhi ya wazee wengi kuishi maisha ya t a bu na kulazimika kulelewakwenye vituo maalumu imeelezwa kuchangiwa na baadhi yao kuwakanawatoto wao jambo ambalo linawapelekea kujikuta wakiingia kwenyechangamoto za namna hiyo.

  Hatua hiyo inat ajwa kuwapa majukumu mazito wasichana ambao wamekuwaw akikumbana na kadhia hiyo ambao kwa asilimia kubwa wanakuwa wakiishikwa manunguniko (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
  Click here to Reply, Reply to all, or Forward 3.93 GB (26%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 40 minutes ago Details

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua mjadala wa wadau wa maendeleo ulioshirikisha wawakilishi kutoka taasisi za umma na Serikali na asasi za kiraia kujadili uchambuzi uliofanywa na taasisi hiyo kuangalia sera, mikakati na mipango ya Serikali kumuwezesha mwanamke kuelekea uchumi wa viwanda.
  Profesa Flora Kessy, Mtafiti wa TGNP akiwasilisha uchambuzi alioufanya kwa washiriki.
  Washiriki wa mjadala wa wadau wa maendeleo ulioshirikisha wawakilishi kutoka taasisi za umma na Serikali na asasi za kiraia kujadili uchambuzi wa sera, mikakati na mipango ya Serikali kumuwezesha mwanamke kuelekea uchumi wa viwanda wakiwa katika majadiliano.
                           Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji mada katika kikao hicho

  Mtandao imekutanisha wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya wadau wa maendeleo wakiwemo wawakilishi kutoka taasisi za umma na Serikali na asasi za kiraia kujadili uchambuzi uliofanywa na taasisi hiyo kuangalia sera, mikakati na mipango ya Serikali kumuwezesha mwanamke kuelekea uchumi wa viwanda.

  Akizungumza wakati akifungua majadiliano, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi leo jijini Dar es Salaam amesema taasisi hiyo imefanya uchambuzi wa sera, mikakati na mipango ya Serikali kuangalia ushiriki wa wanawake na makundi mengine ya pembezoni katika Tanzania ya viwanda.

  Alisema katika uchambuzi huo uliofanywa na Profesa Flora Kessy, Mtafiti wa TGNP umeangalia maeneo mbalimbali ikiwemo changamoto za kundi la wanawake linavyoweza kushirikishwa kwa mafanikio ya Tanzania ya viwanda.

  Akifafanua zaidi, Bi. Liundi aliwataka wajumbe hao kujadiliana kwa kuzingatia kuwa takwimu za 'UN Women' zinaonesha mwanamke ni uti wa mgongo wa maendeleo kutokana na kuchangia takriban kwa asilimia 43 katika nguvu kazi duniani na kwa nchi nyingine asilimia hiyo inafikia hadi 70.

  Alisema kwa upande wa Tanzania kilimo kinaajiri zaidi ya asilimia 65.5 ya Watanzania huku idadi kubwa ya kundi hilo wakiwa ni akinamama, jambo ambalo linaonesha upo umuhimu mkubwa wa kundi hilo kuangaliwa kipekee katika uwezeshwaji kufikia malengo kuelekea uchumi wa viwanda.

  Hata hivyo alisema bado kuna changamoto nyingi katika kundi la wanawake kuelekea uchumi wa viwanda, ukizingatia kundi kubwa la wanawake liko katika sekta isiyo rasmi (asilimia 51.1), idadi ndogo ya wanawake wanaomiliki ardhi (asilimia 8) ukilinganisha na wanaume, idadi kubwa ya wanawake kuwa katika kundi la umasikini (asilimia 60) ukilinganisha na wanaume.

  "...Jinsia ni suala la Maendeleo hatuna budi kwa pamoja kutoa kipaumbele ili kuongeza ushiriki wa wanawake wenye tija katika maendeleo ya uchumi wa nchi. Ni wazi kuwa mkutano huu utatumika kujadili kwa kina na kupanga mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wanawake pamoja na sera hizo bado kuna changamoto ya utekelezaji ili kuwezesha ushiriki wenye tija kwa wanawake na makundi ya pembezoni," alisema Bi. Liundi.

  "Katika kusisitiza ushiriki wa Wanawake katika Tanzania ya Viwanda tuzingatie kanuni (principle) ya malengo endelevu ya dunia ya kutomwacha mtu nyuma kwa kufanya uchambuzi wa kina kwa jicho la jinsia ili kuleta ushiriki jumuishi na wenye tija. Ikumbukwe kwamba tukiacha kundi la wanawake nyuma tunapoteza fursa na mapato kwa kiasi kikubwa hivyo kutuchelewesha kufikia uchumi wa kati na dira yetu ya 2025," alisema.

  Kwa upande wake Mtafiti Prof. Kessy akiwasilisha uchambuzi kwa washiriki hao alibainisha kuwa shughuli wanazozifanya akinamama kwa sasa zinaweza kuboreshwa zaidi kulingana na mahitaji hivyo kujikuta kundi hilo linajengewa uwezo.

  Alisema shughuli kama uzalishaji mdogo mdogo unaofanywa na kundi hilo unaweza kuongezewa teknolojia, masoko pamoja na nguvu za uzalishaji na kukuta inamuinua mwanamke na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda.

  Kundi hilo kwa pamoja litajadili na kuchakata changamoto hizo na kutoka na mapendekezo ambayo watajaribu kuishirikisha Serikali kupitia wizara husika ili kuona uwezekano wa kuzingatiwa kwa mapendekezo ya wadau hao.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
   Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
   Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
  Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na
  umegharimu kiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

  Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

  “Mradi wowote ule ukiwa na ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema Masenza

  Masenza alisema kuwa mradi huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.

  Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni Igonongo, Ludilo, Kidete, Ikanga, Nandala, Ibwanzi, Isipii, Mkonge, Lulanzi, Luhindo, Barabara mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.

  “Jamani wananchi ambao mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza

  Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya maji.

  “Sisi kama RDO ambao ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali

  Filipatali alisema kuwa mradi huo wa maji utazaliza ujazo wa lita 776 kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.

  “Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali

  Filipatali alisema kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo

  “Hizi changamoto zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akitoa maelezo kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu kwa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria ili kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifafanua jambo wakati kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
  Baadhi ya Wajumbe wa kikao wakifuatilia mada zinazowasilishwa wakati wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha kamati yake wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 27,62,65 na 15 ya Ofisi hiyo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hoja wakati wa Kikao cha Kamati hiyo.
  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
  Baadhi ya Wajumbe wa kikao wakifuatilia mada zinazowasilishwa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

                              (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)

                                                                                                 Na.MWANDISHI WETU

  Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kujikwamua katika nyanja zote na kuchangia katika maendeleo nchini.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019 kwa mafungu ya Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi hiyo Mjini Dodoma.

  Waziri Ikupa alieleza kuwa tayari Serikali imeanza mikakati ya kuboresha mazingira ya watu wenye Ulemavu kwa kuvifufua vyuo na vituo vyao ili kuwapa nafasi nzuri ya kujifunza katika mazingira yanayowapa uhuru na tija kulingana na aina za ulemavu walionao.

  “Tayari tumeanza kuboresha mazingira ya vyuo vya ufundi ikiwemo kile cha Yombo kilichopo Mjini Dar es Salaam na Sabasaba ili kusaidia kuwapa fursa za kujifunza katika mazingira rafiki hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna kuwa na vifaa vya kutosha”.Aliongezea

  Sambamba na hilo Serikali inaendelea na hatua za kuboresha mazingira ya Watu wenye ulemavu kwa kuwajengea uwezo, kuongeza wataalam wa kuwafundisha, kuwapa mafunzo maalumu yenye kuleta tija pamoja na kuwashirikisha katika fursa za maendeleo.

  Aliongezea kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo mbalimbali ili kupata taarifa sahihi za mahitaji halisi ya watu wenye ulemavu yatakayosaidia kuwa na kanzidata ya kudumu yenye taarifa hizo.

  “Jitihada zilizopo ni pamoja na kushirikisha Wizara ya Elimu ili kuweza kupata taarifa muhimu za watu wenye ulemavu zitazosaidia kuwa na kanzi data ya uhakika inayowatambulisha kwa idadi, aina ya ulemavu na ujuzi alionao ili kuwapa nafasi wenye sifa za kushiriki katika programu za kukuza ajira”.Alisisitiza Mhe.Ikupa

  Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Mhe.Amina Mollel alishauri kuwe na mikakati madhubuti yenye tija kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kutoa semina kwa watumishi wa serikali juu ya namna bora ya kuwahudumia watu wenye ulemavu kwa kuzingatia mahitaji yao.

  “Ifike mahali kuwe na mikakati madhubuti ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum hususani kwa kuwajengea uwezo watumishi kujua namna nzuri ya kuwahudumia watu wenye ulemavu pamoja na kusaidia kuzikabili changamoto wanazokabiliana nazo”.Alisema Mhe.Mollel.

  0 0


  Mwanzilishi Mwenza wa  Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland. 
  Meza Kuu pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo.
  Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao 
  Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.
  Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
  Muonekano wa chumba cha mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale

  MAONYESHO ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi mbili mwezi huo.

  "Wanafunzi wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.

  Kamugisha alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.

  Alisema onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)

  "Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Alisema udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Kamugusha aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

  Alisema wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.


  0 0

  Na Leandra Gabriel, globu ya jamii

  WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe leo Machi 29 ametoa tamko kuhusu wasanii waliofungiwa kazi zao za sanaa.

  Akizungumza jijini Dar es salaam Dk.Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali haina ugomvi na msanii yeyote ila ugomvi wao upo katika suala la mmomonyoko wa maadili na suala hilo halitofumbiwa macho, pia ameeleza kuwa kuna mipaka katika kulinda maadili na wasanii ndio mabalozi, kuhusu suala la Abdul Naseeb maarufu kama Diamond la kutoa kauli nzito mtandaoni Mwakyembe amesema kuwa wanampenda sana Diamond na wanataka afike mbali zaidi na amefurahi sana kwani vijana hao wameelewa.

  Akieleza maamuzi hayo naibu Waziri wa wizara husika Juliana Shonza amesema hawana ugomvi wala chuki na msanii wa Tanzania na kuhusu suala msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty kind amesema amefurahishwa na hatua alizochukua kama kujisajili katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaamini amebadilika hivyo wanamsamehe adhabu yake iliyotakiwa kuisha Julai Mosi mwaka huu.

  Pretty kind ameshukuru Wizara pamoja na Baraza la sanaa la taifa (BASATA) kwani kupitia wao amejifunza mengi na atakuwa balozi mzuri wa maadili nchini na amewashauri wasichana hasa wasanii kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na BASATA na wabadilike kupitia yeye.Kuhusu suala la Roma Mkatoliki, Shonza ameeleza kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilimpa maelekezo ya mabadiliko ya wimbo wa kibamia na kuhudhuria kikao kilichopangwa na Baraza hilo vitu ambavyo Roma hakuvitekeleza.

  Aidha Shonza ameeleza kuwa Roma aliandika barua ya kupunguziwa adhabu ombi ambalo wamelipokea ila lazima akajisajili BASATA pamoja kufanya marekebisho ya wimbo huo.Baada ya msanii Roma kuamua kwa ridhaa yake mwenyewe mbele ya vyombo vya habari kwamba wimbo huo uondolewe kabisa kwenye vyombo vya habari hasa kwa mfumo wa sauti na video Waziri Mwakyembe amesema kuwa pindi atakapokamilisha usajili wake na kuwa na hati kutoka BASATA adhabu yake itakuwa imeishia hapo.

  Mwisho waziri Mwakyembe amewaomba wasanii kuwa mabalozi wa maadili ya watanzania kwa kumnukuu baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kusema Taifa lisilo na maadili yake ni taifa mfu.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza (katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao baada ya kuongea na wanahabari.

older | 1 | .... | 1550 | 1551 | (Page 1552) | 1553 | 1554 | .... | 1897 | newer