Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1546 | 1547 | (Page 1548) | 1549 | 1550 | .... | 1897 | newer

  0 0


   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

  Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.

  Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.
  “Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.
  Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.
  Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
  Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
  “Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
  “Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
  Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
  Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
  “Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.

   
   Mshiriki akisoma machapisho yenye taarifa za WCF
   Dkt. Abdulsalaam (katikati), akifafanua baadhi ya hoja. Wengine, ni Bi. Naanjela Msangi, (Kushoto), na Bw. Faustine George
   Bi. Naanjela Msangi.
   Bw. George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
  George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
    Bi. Naanjela Msangi(kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge
   Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo
   Baadhi ya washiriki wakipitia vipeperushi vyenye maelezo kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
   Baadhi ya washiriki wa semina.
   Washiriki wakijiandikisha
   Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa WCF.
   Robert Duguza, Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.
  Bi. Tumaini J.Kyando, Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa Kazi kutoka Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio walioandaa semina hiyo, akinakili baadhi ya hoja zilizojitokeza.
  Baadhi ya washiriki

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael ( katikati) akizungumza na waadishi wa habari katika hafla ya ushirikiano kati ya Tigo Tanzania na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo. Wengine kulia Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa Tigo, Davidi Umoh. Hafla ilifanyika Jijini Dar es salaam
  Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, Davidi Umoh ( katikati), Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael wakizindua simu mpya za kisasa aina ya Sumsang S9 na Samsung S9+ ambazo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kwa mara ya kwanza.

  Wapenzi wa smatphone wanayo sababu nyingine ya kutabasamu baada ya kampuni inayoongoza ya mtindo wa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania kuungana na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.

  'Tigo ni kampuni pekee ya simu za mkononi na ya kwanza kuwa na simu mpya za kisasa za Samsung S9/S9+ nchini. Hakuna mwendeshaji mwingine yeyote wa mtandao wa simu au duka ambalo tayari limeshapokea simu hizi za kisasa za smartphone,' Mkuu wa idara ya Bidhaa na Hudumawa Tigo (Head of Products and Services), Davidi Umoh aliabainisha.

  Umoh aliongeza kuwa 'Tigo imeshika usukani wa mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidigitali . Tuna lenga katika kuendelea kuongeza upatikanaji wa simu za smartphone nchini wakati huo huo tukiwa tunahakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi wa 4G ambao ndio uliosambaa zaidi hapa nchini.

  Akielezea kuhusu Ushirikiano uliopo, Meneja wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Suleiman Mohammed amesema"Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Tigo kwaajili ya kuleta fursa za kusisimua na ofa kwa wateja wa Tanzania. Hii ni hatua ya msingi sana katika ukuzaji wa sekta ya simu za mkononi ambayo inaruhusu wateja kupata simu za kisasa katika wakati huo huo ambapo simu hizo zinazinduliwa duniani kote".

  Kuna njia tatu za kununua simu ya smartphone ya Samsung S9/S9+ Kwanza mteja anaweza kutembelea duka lolote la Tigo nchi nzima nakulipia na kujipatia simu mpya ya kisasa aina ya Samsung S9 na S9+. Njia ya pili ya kununua simu hizo nikutembelea Tigo Store katika ukurasa wa mtandao wa manunuzi wa jumia www.jumia.co.tz/tigo-shop. Mwisho wateja wanaweza kupiga menyu mpya ya Tigo *147*00# na kisha kuchagua duka la simu ambako utaweza kuchagua namna ya kulipia ambayo inaruhusu kulipia kidogo kidogo na kuchukua simu yake baadae.

  Simu za smartphone za kisasa za Samsung S9/S9+ zinapatikana katika rangi nyeusi, kijivu na zambarau na zitauzwa reja reja kwa bei ya TZS 2,049,000 kwa Samsung S9 na TZS 2,315,000 kwa Samsung S9+.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori amehitimisha maadhimisho ya Wiki ya maji jijini yenye kauli mbiu ya Hifadhi Maji na Mifumo ya Ekolojia kwa Maendeleo ya Jamii.

  Ametumia hitimisho la maadhimisho hayo kufungua mradi mdogo wa utakatishaji maji taka katika eneo ya Mburahati jijini.Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Makori amesema maji yanayopatikana jijini kwa sasa ni asilimia 75 pekee na hadi kufikia mwaka 2020 maji yatapatikana kwa asilimia 95 na kufikia mwaka 2025 wakazi wote wa jiji watapata maji kwa asilimia 100.

  Akizungumzia kuhusu mafanikio ya miradi maji Makori amesema miradi inayotekelezwa na DAWASA na DAWASCO katika mradi wa Ruvu chini ni lita milioni 270 kutoka lita milioni 182 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa Bagamoyo, Kawe na maeneo ya jirani na mradi wa Ruvu juu lita 196 kutoka lita milioni 82 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kibaha, Mbezi, Ubungo na maeneo ya jirani. 

  Amesema zaidi ya visima 20 vimechimbwa na kunufaisha wakazi wa Kimbiji Mpera na maeneo yake.Amepongezwa wananchi kwa kukubali kuunganishwa na huduma ya maji kutoka laki 123,000 hadi kufikia 228,000.Pia amewataka wananchi kushiriki shughuli za usafi licha ya kuwa na asilimia 10 tu ya wakazi wanaopata huduma hiyo na amehaidi hadi kufikia 2020 asilimia 30 ya wakazi watafikiwa na huduma hiyo.

  Makori amesema mwaka 2017 hadi mwaka 2020 miradi 50 ya uondoaji maji taka itajengwa Jangwani na kusaidia maeneo yenye wakazi wengi, mlipuko wa magonjwa na watu wenye kipato kidogo.
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori akizungumza katika  maadhimisho ya wiki ya maji jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori (alievaa kofia ya kijani) akipanda mti katika mradi wa kuchaata maji taka.
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori akiweka jiwe la msingi la ujenzi katika mradi wa kuchaata maji taka.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisare Makori  aiwa ameambana na viongonzi mbalimbali wakigangua eneo la mradi huo.

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (kushoto) akiongozwa Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya anayestaafu Bibi Mayasa Hashimu (Kulia) kuingia kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango kwa ajili ya kufunga mkutano wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.

  Afisa Elimu wa mkoa wa Pwani bwana Abdul Maulid (kulia) aliyekaa mstari wa mbele akiwa pamoja na Maafisa wenzake wa Elimu wa Mikoa na Wilaya wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Joseph Kakunda (hayupo) pichani wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Paulina Nkwama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI kufunga Mkutano wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Joseph Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya nchini.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Joseph Kakunda akimpongeza Bibi Dyness mosha ambaye ni mmoja wa Maafisa Elimu wanaostaafu mwaka huu.


  Na Mathew Kwembe, TAMISEMI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema uamuzi wa Serikali kuwahamisha baadhi ya Walimu wa shule za Sekondari wanaofundisha masomo ya sanaa kwenda kufundisha shule za Msingi ulilenga kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu uliopo katika shule za Msingi nchini na kamwe siyo adhabu.

  Katika hotuba yake Waziri Jafo iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Joseph Kakunda katika mkutano mkuu wa tano wa mwaka wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya Tanzania Bara jana mjini Dodoma,ametaka maafisa elimu hao kuwapanga walimu kwa vigezo vilivyoweka na serikali na sio kama adhabu.Amema kamwe maafisa elimu wasiwapangie walimu hao wa sekondari kwenda shule ya msingi kwa kigezo cha kutoa adhabu kwa walimu bali wazingatie vigezo hivyo.Waziri huyo amesema ameshaagiza kuwa kigezo cha mikondo ndio kiwe kigezo sahihi cha kupanga walimu.

  “Nitalisimamia kwa karibu sana suala hili, pia kigezo cha kupanga walimu shule za msingi kwa kutumia idadi ya wanafunzi kinazinyima shule zenye wanafunzi wachache kuwa na walimu wa kuweza kufundisha darasa la Awali hadi darasa la saba kwa ufanisi. “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa upo upungufu wa walimu kwa shule za msingi na walimu wa sayansi kwa shule za sekondari,” amesema.

  Kwa mujibu wa Waziri Jafo, amesema kuna upungufu wa walimu wa shule za msingi 85,000 nchini wakati ziada ya walimu wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari ni 21,000.Waziri Jafo amesema kulingana na takwimu hizo serikali imeona ni vema walimu hawa wa masomo ya sanaa wapelekwe kufundisha shule za msingi kwani uamuzi huo wa serikali umezingatia suala la matumizi mazuri ya rasilimali watu.

  Amesema kutokana na wingi wa walimu wa sanaa katika shule za sekondari mwalimu mmoja wa sanaa alikuwa akifundisha chini ya vipindi 10 kulinganisha na mwalimu wa sekondari ambaye alikuwa akifundisha vipindi 20. Aidha Waziri Jafo pamoja na kutambua kuwepo kwa upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo kwa upande wa msingi na sekondari, ameziagiza halmashauri zote 185 kuweka nguvu katika kukamilisha miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari pamoja na maabara.

  Pia Waziri Jafo amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza agizo la kununua magari na kutenga fedha za ununuzi wa magari kupitia bajeti za Mikoa na Halmashauri. Kuhusu wahitimu wa Darasa la saba wa mwaka 2018 kupata vyeti vyao, Waziri Jafo amesema kuwa serikali imelichukua ombi hilo kwa uzito unaostahili.

  Katika risala yake, Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya Bibi Mayasa Hashimu ameiomba serikali iwasisitize wakurugenzi wa halmashauri kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya.

  Pia ameiomba serikali kuweka msisitizo wa pamoja katika usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa Matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, maabara na hosteli shuleni.

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.

  Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.

  Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.

  "Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.

  Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."

  0 0

  Muonekanao wa E-Passport zilizotolewa mapema mwaka huu.
  Passport ya Uingereza ambayo kampuni ya De La Rue ilikuwa inazitenegeneza kabla ya kufutiwa mkataba wao. *Ni ile iliyonyimwa zabuni ya kutengeneza hati mpya za kusafiria Tanzania *Uingereza nayo yaamua kuvunja nayo mkataba kutokana na gharama kubwa *Uongozi wa kampuni wachanganyiwa, hisa zao zashuka kwa kasi soko la hisa 

  Na Mwandishi wetu 

  KAMPUNI ya De La Rue ambayo ilishindwa kwenye zabuni ya E-Imigration ambapo ingetengeneza e-passport, e-Visa, e-Imigration nchini Tanzania imepata pigo jingine baada ya mkataba wake kusitishwa na Serikali ya Uingereza ya kuendelea kutengeza hati za nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Aliance News imesema kuwa kampuni ya De La Rue ilikuwa na mkataba na Uigereza wa miaka 10 lakini nchini hiyo imeamua kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo.

   Imefahamika lengo la Serikali ya Uingereza kuvunja mkataba huo wa kutengenezwa hati za kusafiria ni kutokana na gharama kuwa kubwa za utengenezaji wa hati hizo na hivyo kuamua kuipa zabuni kampuni ya French firm Gemalto. "Hati mpya za kusafiria za Uingereza hazitatengenezwa tena na kampuni ya De La Rue ambayo ndio iliyotengeneza hati zitumikazo kwa sasa. 

  "Hivyo hati hizo mpya za rangi ya blue ambazo zitatumika baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya zitatengenezwa na kampuni ya French firm Gemalto. Kubadilika kwa rangi ya hati hiyo kunatafsiriwa kuwa ni alama ya kurudi kwa nguvu ya Uingereza, umesema mtandao ulitoa taarifa hizi. Pia taarifa zinaeleza kuwa Kampuni ya De La Rue inafikiria kukata rufaa baada ya kukosa na kushindwa katika zabuni ya kutengeneza hati hizo mpya. 

  Kampuni hiyo imeripotiwa ikidai haikuridhishwa kwa kupoteza zabuni hivyo hivyo inaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza Hata hivyo Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya De La Rue Jitesh Sodha amesema kitendo hicho kimesababisha hisa za kampuni yao kutoka asilimia 14 ya Jumanne ya wiki hii hadi kufikia asilimia 0.4 leo Machi 22 ya mwaka huu. 

   "Tumechukizwa na kitendo cha Serikali ya Uingereza kusitisha mkataba wetu wa kutengeneza hati za kusafiria za nchi hiyo wa miaka 10 kwani ulikuwa mkataba unamalizika Julai mwakani. Hivi karibuni katika uzinduzi wa E-Passport, Rais Dk. John Magufuli amesema kuwa kuna wajanja awali walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507. 

  Rais Magufuli alisema baada ya kugundua ujanja huo Rais alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380. 

  Moja ya kampuni ambayo ilikosa zabuni ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria nchini Tanzania ni hiyo ya De La Rue na moja ya sababu ilikuwa ni kiasi kikubwa cha fedha ambazo walikihitaji lakini Serikali iliwashutukia na kuamua kutoa zabuni kwa kampuni nyingine iliyotengeza kwa gharama nafuu. Hata hivyo vyanzo vya kuaminika kutoka Serikali ya Tanzania vilibanini mambo mazito yaliyoibuka baada ya kubainika kampuni hiyo kuhonga mamilioni ya fedha ili kuichafua mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.

  0 0

  Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza agizo la kuzifutia leseni za makampuni manne ya Ushauri na Udalali wa bima (Insurance Brokers) kwa kukiuka malengo ya leseni zao. Picha na Cathbert Kajuna. 

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)imeamua kuzifutia leseni za kampuni nne za ushauri na udalali wa bima (Insurance Brokers). Akizungumza leo Dar es Salaam, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware amesema kampuni hizo za udalali na ushauri wa Bima yaliyofungiwa yalikuwa yamesajiliwa na kupewa leseni ya kufanya biashara ya bima kwa mujibu wa sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009. 

  Ametaja kampuni ambazo zimefutiwa leseni ya udalali wa bima ni kampuni ya udalali wa Bima ya HANS, ENDEAVOUR, LEGEND OF EAST AFRICA, pamoja na SWIFT. Kamishna Dk.Saqware ameongeza kapuni hizo zimefungiwa kwa kosa la kutowasilisha ada za bima kwa kampuni ya bima ambapo mawakili wa kampuni wamefunga ofisi bila kulipa ada stahiki na kufuta taratibu zilizowekwa za kufunga ofisi. 

  Aidha amesema mamlaka imetathimini mwenendo wa kampuni hizo na kuona ni vema ikachukua hatua za haraka zilizo ndani ya uwezo wake kwa mujibu wa sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 kifungu cha 74, ambayo ni kuyafutia leseni ya biashara kampuni hizo. 

  Dk.Baghayo amesema kinachotakuwa ni kuhakikisha wateja wa Bima kupata haki na heshima ya soko hilo inalindwa hata baada ya kampuni hizo kufutiwa leseni. Amewataka wananchi kutambua uwepo wa mamlaka ya usimamizi wa shghuli za Bima hapa Nchini." Wananchi wasilalamike na kunung’unika pale wanapopata matatizo ya kibima na kwa kutokuja wapi pa kwenda. 

  "Mamlaka kupitia ofisi zetu za makao makuu na katika kanda za Nyanda za juu kusini (Mbeya jengo ka NHC-mtaa wa Lupa), kanda ya kati (Dodoma)katika jengo la LAPF-mataa wa Makole, kanda ya ziwa (Mwanza :jengo la PPF Bara bara ya Kenyatta) na kanada ya Kaskazini (Arusha :jengo la NSSF-Mataa wa Kaloleni).

   "Pia kuna Kanda ya Pwani (Dar es Salaam) na ofisi ya Mamlaka ya Visiwani Zanzibar katika jengo la TIRA Mtaa wa Kilimani)tuko tayari kusikiliza kila mwananchi.Mamlaka iko imara katika kuhakikisha Sekta za bima nchini inakuwa sehemu za chachu ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla,"amesema. 

  Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa sheria mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Magreth Mngumi ametoa mwito kwa watanzania kuwa na imani na mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini na wateja waendelee kufurahia huduma zao ili kongezeka pato la taifa.

  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael ( katikati) akizungumza na waadishi wa habari katika hafla ya ushirikiano kati ya Tigo Tanzania na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo. Wengine kulia Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa Tigo, Davidi Umoh. Hafla ilifanyika Jijini Dar es salaam jana.
  Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, Davidi Umoh katikati), Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael wakizindua simu mpya za kisasa aina ya Samsung S9 na Samsung S9+ ambazo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kwa mara ya kwanza.


  Wapenzi wa smatphone wanayo sababu nyingine ya kutabasamu baada ya kampuni inayoongoza ya mtindo wa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania kuungana na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.

  'Tigo ni kampuni pekee ya simu za mkononi na ya kwanza kuwa na simu mpya za kisasa za Samsung S9/S9+ nchini. Hakuna mwendeshaji mwingine yeyote wa mtandao wa simu au duka ambalo tayari limeshapokea simu hizi za kisasa za smartphone,' Mkuu wa idara ya Bidhaa na Hudumawa Tigo (Head of Products and Services), Davidi Umoh aliabainisha.

  Umoh aliongeza kuwa 'Tigo imeshika usukani wa mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidigitali . Tuna lenga katika kuendelea kuongeza upatikanaji wa simu za smartphone nchini wakati huo huo tukiwa tunahakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi wa 4G ambao ndio uliosambaa zaidi hapa nchini.


  Akielezea kuhusu Ushirikiano uliopo, Meneja wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Suleiman Mohammed amesema"Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Tigo kwaajili ya kuleta fursa za kusisimua na ofa kwa wateja wa Tanzania. Hii ni hatua ya msingi sana katika ukuzaji wa sekta ya simu za mkononi ambayo inaruhusu wateja kupata simu za kisasa katika wakati huo huo ambapo simu hizo zinazinduliwa duniani kote".

  Kuna njia tatu za kununua simu ya smartphone ya Samsung S9/S9+ Kwanza mteja anaweza kutembelea duka lolote la Tigo nchi nzima nakulipia na kujipatia simu mpya ya kisasa aina ya Samsung S9 na S9+. Njia ya pili ya kununua simu hizo nikutembelea Tigo Store katika ukurasa wa mtandao wa manunuzi wa jumia www.jumia.co.tz/tigo-shop. Mwisho wateja wanaweza kupiga menyu mpya ya Tigo *147*00# na kisha kuchagua duka la simu ambako utaweza kuchagua namna ya kulipia ambayo inaruhusu kulipia kidogo kidogo na kuchukua simu yake baadae.

  Simu za smartphone za kisasa za Samsung S9/S9+ zinapatikana katika rangi nyeusi, kijivu na zambarau na zitauzwa reja reja kwa bei ya TZS 2,049,000 kwa Samsung S9 na TZS 2,315,000 kwa Samsung S9+.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  KWA Ujinga wangu naomba niseme mapema tu, mimi si mfanyabiashara ila 
  nimekuwa karibu kwasababu nanunua bidhaa za wafanyabishara.

  Nanunua bidhaa za wafanyabishara kulingana na mahitaji yangu ya kila 
  siku.Ndio ukweli maana maisha yangu ni kwamba nikijipata vijesenti naenda dukani nanunua nachojitaji.Kwa kuwa nimekuwa karibu na wafanyabishara , nikiri nimekiwa nikifuatilia 

  mambo yao mbalimbali.Hata wanapotoa malalamiko yao kuhusu kukwamishwa kwa mambo yao nimekuwa nikisia.Malalamiko ya tozo kubwa za kodi kwenye masuala ya biashara nayo nimekuwa nikiwasikia wafanyabishara wakilalamika.

  Nawasikia kwasababu mbali ya kuwa ni sehemu ya mteja wao , bado nami ni Mtanzania ambaye nashukuru Mungu ni muumini wa kufuatilia kila jambo nchini kwetu.Hata Rais wangu Dk.John Magufuli wakati unatoa maagizo kwa Waziri wa Fedha na Mpango kukaa na Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA)kuangalia namna ya tozo za kodi.

  Ukasema kuwa kodi zimekuwa kubwa kiasi cha kufanya kuwa kero.Ukaeleza 
  namna ambavyo unataka kodi iwe jambo la heshima kwa Taifa na si kuwa kero kwa mlipaji.Kwa Ujinga Wangu baada ya kusikia utakutana na wafanyabishara kutoka maeneo mbalimbali nchini.Nikasema kwenye mazungumzo hayo lazima kitaeleweka.

  Rais Magufuli ukaamua kutoa nafasi ya kila mfanyabishara kutoa dukuduku lake.Nakumbuka kwenye mkutano huo ambao wewe uliongoza ulieleza namna ambavyo unataka kumsikia kila mmoja wao.Wafanyabishara nao kwa kuwa kuna mambo ambayo yalishikuwa kero kwao waliamua kusema kila kitu.Hakuna ambacho wamekificha maana waliona ndio sehemu pekee ya wao kusikilizwa.

  Wakaeleza changamoto ambazo wanakutana nazo kutoka kwa TRA.Wakaeleza namna ambavyo wanaojihusisha na biashara ya mazao kuharibikia njiani.Wakaeleza namna ambavyo wanatamani Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara.Wafanyabishara hao wakaelezea mambo mengi.Wakaeleza namna ambavyo wanaamini kikao hicho kati yao na Rais kitakuwa na mafanikio makubwa.Kama nilivyotangulia kueleza awali mimi si mfanyabiashara lakini nimevutiwa na mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

  Kw Ujinga wangu nikawa nawaza kwanini kikao hichi kimechelewa kufanyika?Hata hivyo nikajijibu mwenyewe kuwa ratiba yako imebana kutokana na majukumu mbalimbali ya kuwatumikia Watanzania.Kwa mtazamo wangu kikao hicho kitakuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu.Tunatambua mchango wa wafanyabishara katika kujenga uchumi wa nchi yetu.

  Natambua TRA kutokana na makadirio ya kodi kuwa juu , kuna wafanyabishara wengi wamefunga maduka yao.Wameyafunga si kwasababu wanapenda bali mazingira ya kodi yamekuwa kikwazo kwao.Nieleze ni kweli kuna malimbikizo ya madeni ya kodi ambayo wafanyabishara wanadaiwa lakini nilidhani TAR wangekuwa na jukumu la kukaa na wafanyabishara na kisha kuangalia njia nzuri ya kuhakikisha madeni yanalipwa na wafanyabishara wanaendelea kufanyabishara.

  Naamini kikao kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara kitafungua ukurasa mpya katika sekta ya biashara nchini.Rais wakati anazungumza kwenye kikao hicho alitumia nafasi hiyo kushughulikia baadhi ya malalamiko.Akatumia nafasi hiyo kutoa maagizo na maelekezo kulingana na hoja za wafanyabiashara.

  Hata hivyo kukosekana kwa baadhi ya mawaziri au makatibu wakuu kwenye kikao hicho kilisababisha Rais Magufuli kuhoji kwanini hawakufika.Sababu ya kuwaliza ilitokana na kuamini kuna baadhi ya mambo yanaweza kushughulikiwa na wizara moja kwa moja.

  Pamoja na kukosekana kwa baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu ambao nao walialikwa kwenye kikao hicho bado lengo la mkutano ulifanikiwa.Hakika mkutano huo umefungua ukurasa mpya kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara.Sote tunafahamu kuna wakati ilijengeka dhana kuwa hakuna uhusiano mzuri kati ya wafanyabiashara na Serikali.Hata hivyo unapomsikiliza Rais Magufuli na wafanyabishara hao unabaini hakuna tatizo bali yapo mambo yaliyokuwa yanasababisha manung'uniko.

  Kabla ya kuhitishwa kwa kikao hicho, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipata nafasi ya kutoa maelezo yake na akatumia nafasi hiyo kuonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya maofisa wa TRA kuwa kero katika eneo la ukusanyaji kodi.Akasema wamesababisha kufungwa kwa maduka bila sababu za msingi na akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo amechukua kukomesha tabia hiyo.

  Wakati Rais Magufuli wakati anahitimiza kikao hicho, amesema yapo baadhi ya mambo ufumbuzi wake utakuwa wa haraka na mengine watakwenda kujipanga ili kutafuta ufumbuzi wake.

  Akawaambia wafanyabishara hao kuwa katika utawala wake watatajirika sana na anachokifanya ni kuondoa kona kona ambazo zimekuwa zikikwamisha wengine.Akaleza namna ambavyo baadhi ya wafanyabishara wanatozwa kodi kubwa na wengine hawatozwi kodi.

  Akawahakikishia kuwa Serikali yake inawapenda wafanyabiashara na itakuwa nao bega kwa bega.Rais akasema katika eneo la uchumi kuna vita kubwa na hivyo ni Watanzania kwa umoja wao kusimama imara.Ni maoni yangu kuwa Rais Magufuli baada ya kikao hicho kuna mengi ambayo ameyapata kutoka kwa wafanyabishara hao na yakifanyiwa kazi tutasonga mbele.

  Kwa Ujinga Wangu naomba nieleze wazi kikao hicho kimenifanya hata mimi nisiye mfanyabishara nianze kufikia kufanya biashara kwani mazingira ya biashara chini ya Rais yanayonekana kuanza kuwa bora zaidi.Ahsante kwa kunisoma
   Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam hivi karibuni

  0 0


  Mganga Mkuu wa Serikali, Prof Muhammad Bakari Kambi akizungumza wakati akifungua mdaharo uliowahusisha wataalamu mbali mbali kujadili ni kitu gani kinasababisha vifo katika hospitali, kufuatia utafiti uliofanywa na  Taasisi ya Taifa Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMRI). Kupitia matokeo ili kutoa ushauri wa kisera ili serikali iweze kutilia mkazo ambapo Prof. Kambi amesema changamoto inazikumba hospitali nyingi ni magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa ni changamoto kubwa inayopelekea kuzigharimu sana. Kaimu Mkurugenzi wa NIMRI akimkaribisha mgeni rasmi. 
   Washiriki kutoka taasisi mbali mbali za serikali na hospitali za mikoa wakifuatilia kwa makini.
   Mgeni rasmi akiwa na Washiriki kutoka taasisi mbali mbali za serikali na hospitali za mikoa.

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

   HOSPITALI za Mkoa wa Dar es Salaam zimebainika zilikuwa na wagonjwa wengi ambao walikufa kutokana na malaria, Ukimwi , ajali, maambukizi ya bakteria kwenye damu, upungufu wa damu, saratani na kifua kikuu(TB) ukifuatiwa na mkoa wa Morogoro. Imefahamika malaria na upungufu wa damu ulichangia vifo vingi kwenye kundi la watoto chini ya miaka mitano na vifo kutokana na Ukimwi na Kifua Kikuu viliathiri zaidi kundi la watu wazima, vifo vinavyotokana na ajali viliathiri zaidi kundi kubwa la vijana wakati saratani ziliathiri makundi ya umri wote. 

   Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) wakati ikielezea matokeo ya utafiti wa vifoo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania. Imeelezwa na NIMR taarifa za vifo ni moja ya vyanzo muhimu vya takwimu katika kupanga mipango na kuandaa sera ya afya ambapo uchambuzi wa takwimu katika makundi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na kundi la ajali na majeraha ulionesha tofati kubwa kati ya mikoa na mikoa. 

   Utafiti huo umebaini mikoa ya Pwani, Geita na Katavi imeonekana kuathirika zaidi na magonjwa ya kuambukiza na utapia mlo. Wakati vifo kutokana na ajali na majeraha viliathiri zaidi mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Kigoma. Kundi la magonjwa yasiyoambukiza limeathiri zaidi mikoa ya Ruvuma, Manyara, Dar es Salaam na Mwanza.

   "Kati ya mwaka 2006 na mwaka 2015, mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida, Manyara) mikoa ya kaskazini (Arusha na Kilimanjaro) ndiyo iliyobeba mzigo mkubwa wa vifo vilivyosababishwa na maradhi ya mifumo ya kupumua, upungufu wa damu uliathiri zaidi mikoa ya Dodoma, Simiyu na Mtwara,"imesema. Imeeleza utafiti umeanisha changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali zilizopo nchini na kumekuwa na matumizi hafifu ya majina rasmi ya magonjwa kwa kutumia mwongozo wa kimataifa. 

   "Vyanzo vikuu vya vifo hospitalini nchini Tanzania ni pamoja na malaria, maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua, Ukimwi, upungufu wa damu na magonjwa ya moyo. "Kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya watoto wachanga na magonjwa ya mfumo wa kupumua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. 

   Mapendekezo ya utafiti huo Serikali kuandaa mwongozo thabiti wa ukusanyaji, matumizi, utunzaji na uhifadhi bora ya takwimu za afya,"amesema NIMR. Pia pendekezo lingine ni kujenga uwezo wa watumishi wa afya katika uchanganuzi na matumizi ya takwimu, kuimarisha mfumo wa takwimu wa kielektroniki na kuimarisha mafunzo ya madaktari katika utumiaji wa mwongozo wa kimataifa wa kuainisha vyazo rasmi vya maradhi na vya vifo. Imefafanua zaidi kuhusu utafiti huo amesema kuanisha vyanzo vya vifo katika hospitali zetu ni muhimu kufuatilia matukio ya vifo, kutathimini ubora wa huduma zinazotolewa na kuanisha vipaumbele katika huduma za afya.

   "Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuanisha matukio ya vifo katika hospitali za Tanzania ili kutambua maradhi yanayoathiri jamii yetu. Utafiti pia ulichunguza uwepo,upatikanaji, utunzaji na ubora wa takwimu za vifo hospitalini,"imeongeza. Kuhusu mbinu za utafiti huo, inaeleza ulifanyika kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2016 na ulihusisha hospitali 39. Hospitali hizo ni pamoja na hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospital Maalum na hospitali za Wilaya.

   "Taarifa za vifo vilivyotokea kuanzia mwaka 2006 had mwaka 2015 zilikusanywa.Takwimu hizo zilipatikana kutoka kwenye rejesta za hospitali na vibali vya mazishi kutoka kwa Wakala wa Vizazi na Vifo katika ofisi za Wilaya. "Taarifa zilizokusanywa zilihusu jinsia ya mgonjwa, tarehe ya kulazwa hospitali, tarehe ya kufariki na sababu za kifo. Vyanzo vya vifo viliwekwa katika makundi 45 kulingana na utaratibu wa makundi ya magonjwa wa Shirika la Afya Duniani,"imesema. 

   Kuhusu matokeo, amesema jumla ya hospitali 39 zilishiriki katika utafiti huu. Kwa ujumla kulikuwa na ugumu katika upatikanaji wa takwimu na utunzaji wa takwimu katika hospitali nyingi ulikuwa una mapungufu makubwa. "Baadhi ya takwimu hazikupatikana katika baadhi ya hospitali au katika baadhi ya miaka.Utunzaji wa takwimu ulikuwa mzuri kiasi katika hospitali za rufaa za kanda kuliko za mikoa na wilaya.

   "Matumizi ya majina ya magonjwa kwa kufuata mwongozo wa kimataifa yalikuwa hafifu. Baadhi ya dalili za ugonjwa ziliandikwa kama ndiyo sababu za kifo. Jumla ya vifo 247,976 vilitolewa taarifa katika kipindi cha miaka 10 (2006-2015). Kulikuwa na tofauti kubwa katika idadi ya vifo kati ya jinsia ya kiume na ya kike,"imesema NIMR wakati inaelezea utafiti huo.

  0 0

  RC Paul Makonda


  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  amewataka wanawake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto wafike ofisini  Jumatatu ya  Aprili 9 kwa lengo la  kupatiwa msaada wa kisheria.

  Taarifa ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

  "Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali yako itasimama na wewe hadi upate haki yako," amesema Makonda.

  0 0

  Mkazi wa Moshi Ndugu Erasto Dismas Floridi (22) akabidhiwa bajaji yake mara baada ya kuibuku kuwa mmoja kati ya washindi wa promosheni ijulikanayo kama Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa inayoendesha na kampuni ya michezo ya mubashiri SportPesa wakishirikiana na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom PLC.

  Najishughulisha na biashara ya duka kama unavyoona na watu wa kwanza juwapa taarifa juu ya ushindi wangu ni marafiki zangu, kusema ukweli hakuna aliyeamini juu ya ushindi wangu mimi mwenyewe sikuamini ila nikasema ngoja nione mwisho wa hichi kitu utakuwaje”

  Sikuwahi kufikiria kama siku ntapata bajaji katika maisha yangu, hii ni zawadi kubwa kwangu na naimani itabadili maisha yangu kwa kiasi kikubwa kwa sababu ntaifanyia biashara na pesa ntakayoipata ntawekeza ili kuchukua mkopo na kufungua duka langu mwenyewe huku biashara yangu ikiwa inaendelea”
  Mimi ni kaka wa familia na nina mdogo wangu ambaye namsomesha kwa sababu mama yetu ni mjane kupitia bajaji hii itakuwa imetusaidia sana kwenye kulipia vitu mbali mbali vya familia ikiwemo kumalizia nyumba yetu”.

  Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Bi. Sabrina Msuya alisema “Mpaka sasa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kupata washindi watatu huku mikoa mingine kama Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Nj’ombe, Mara, Musoma Songea na Sumbawanga ikiwa na mshindi mmoja mmoja”

  “Pointi zetu za kuweka ubashiri wako ni nzuri kulinganisha na kampuni nyingine, endapo mteja wetu atashinda kwenye ubashiri wake pesa itaingizwa muda huo huo mara baada ya mechi kuisha, kitengo chetu cha huduma kwa wateja kinafanya kazi saa ishirini na siku saba za wiki ili kuhakikisha mteja wetu anapata huduma inayostahili sambamba na kuhakikisha inasikiliza na kutatua matatizo ya wateja wetu.”

  0 0


  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.
   Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji  cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.  
   Wasanii akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi,  jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.
   Balozi wa Tanzania hapa nchini Wang Ke akisaini kitabu ca wageni alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba moani Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
   Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe (mwenye gauni la bluu) na Regina Chonjo wakiselebuka muziki na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho mkoani Morogoro. 
   Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
   Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. 
   Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
   Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
   Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho cha Mtego wa Simba.
   Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akipongezwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo baada ya hotuba yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya gairo Siriel Mchembe  
   Benjamin Amos akizungumza wati wa uzinduzi wa kwanza wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China. uzinduzi huo ulienda pamoja na uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
   Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo hicho
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo na Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (kulia) wakijiandaa kufungua mabango yenye maelezo, wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
   Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
   Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakifurahi baada ya kufanya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakionyeshana bango lenye maelezo baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
  Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Cha China na Viongozi wa mkoani Morogoro baada ya uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  By Dr. Herman Louise Verhofstadt.
   “A BIT like President Donald Trump, Tanzania’s president, John Magufuli, likes to fire employees on television. In November Mr. Magufuli used a live broadcast from a small town in the north of the country summarily to dismiss two officials,” this is an extract from a recent online article I came across from the newspaper that I admired when I was growing up in Europe back in 1990’s; the Economist. 

   Before I venture into other serious issues, the excerpts above contains gross factual errors; my own fact-check indicates that in the named public rally during the opening of Kagera Airport, there was no summary dismissal of the two officials instantly on television, as alleged. Instead, the two, one District Executive Directors for Bukoba Urban and another for Rural were relieved their duties later through a press release from President’s Office. 

   This is my prima impressio reading the Economist this week, a publication known for its top notch ethical and analytical standards, that has now vanished into a hell of sensational journalism, half baked facts, lack of objectivity and a clear sense of bias. 
   Contrary to the fact deprived article, it is my candid observation that to objectively critique Magufuli’s presidency in the circumstances of the transformation he is doing for his people in Tanzania, requires the level of conscious that is unfortunately lacking in the current editorial team at the Economist. 
   Living in Tanzania for close to half a decade now, it makes me a better eye-witness than the Westminster based editorial team. To say the least, this man Magufuli rose into power in a country that was downed by massive corruption scandals, political demonstrations that caused deaths and worse enough he found media fraternity that was being corrupted to work for interest groups. In my stay here before and after his presidency, I have witnessed real transformation, his work is exemplary and fascinating one. 
   Everybody here—may be just like what Theresa May is doing in London and what Trump is focusing in Washington, is aware that Tanzania is on the move towards pro-people development; something the Economist is unhappy for and would frame it with usual western biases; suppression of democracy, violation of press rights etc etc! 
   Under Magufuli’s “rogueness” I have seen leaders going into prison or dismissed for lack of action in protecting public funds, I’m seeing public service regaining its lost fame and massive social projects being implemented across the country-sadly the Economist would reduce all these far-fetching achievements to nothing but “rogueness.”

  0 0

  Etihad Airways Boeing 787-inflight
  Abu Dhabi, UNITED ARAB EMIRATES – Etihad Airways and Swiss International Air Lines (SWISS) have launched a new codeshare partnership with bookings effective immediately.

  Under the agreement, Etihad Airways will have its EY flight code on SWISS services between Geneva and Zurich, two key gateway cities served in Switzerland from Abu Dhabi.

  SWISS will market its LX code on Etihad Airways’ services between Zurich and Abu Dhabi, offering its passengers codeshare flights to and from the UAE’s capital city. The codeshare services are bookable now, for travel from 26 March.

  Peter Baumgartner, Etihad Airways Chief Executive Officer, said: “This codeshare deepens Etihad Airways’ commitment to the Swiss travel market and Switzerland, a key destination for travellers from our UAE home, neighbouring Gulf countries, and across our Asia Pacific network. The partnership further strengthens the historic cultural, business and tourism ties that the UAE and Switzerland have enjoyed over many decades.

  “For travellers from Switzerland, our new relationship with SWISS will provide access to Etihad’s award-winning service and the hospitality for which our Abu Dhabi home is known.”

  The new agreement is part of the codeshare cooperation which began in 2016 between the Lufthansa Group, of which Swiss is part, and Etihad Aviation Group.

  Etihad Airways operates the technologically advanced Boeing 787-9 Dreamliner on its daily flights from Abu Dhabi to Zurich. Both airlines’ customers will experience acclaimed inflight service and award-winning cabin interiors, including 28 Business Studios, and 271 Economy Smart Seats.

  0 0

  Muonekanao wa E-Passport zilizotolewa mapema mwaka huu.
  Passport ya Uingereza ambayo kampuni ya De La Rue ilikuwa inazitenegeneza kabla ya kufutiwa mkataba wao. *Yavuja mkataba na kampuni iliyonyimwa tenda ya kutengeneza passport ya kielekroniki za Tanzania *Lengo ni kukataa kutengeneza passport kwa gharama kubwa *ni baada ya kugundua Tanzania imeokoa fedha nyingi kwa kuinyima tenda kampuni hiyo iliyokuwa na mkataba wa miaka kumi na serikali ya uingereza KAMPUNI ya De La Rue ambayo ilishindwa kwenye zabuni ya E-Imigration ambapo ingetengeneza e-passport, e-Visa, e-Imigration nchini Tanzania imepata pigo jingine baada ya mkataba wake kusitishwa na Serikali ya Uingereza ya kuendelea kutengeza hati za nchi hiyo. 

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Aliance News imesema kuwa kampuni ya De La Rue ilikuwa na mkataba na Uigereza wa miaka 10 lakini nchini hiyo imeamua kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo. Imefahamika lengo la Serikali ya Uingereza kuvunja mkataba huo wa kutengenezwa hati za kusafiria ni kutokana na gharama kuwa kubwa za utengenezaji wa hati hizo na hivyo kuamua kuipa zabuni kampuni ya French firm Gemalto.

   "Hati mpya za kusafiria za Uingereza hazitatengenezwa tena na kampuni ya De La Rue ambayo ndio iliyotengeneza hati zitumikazo kwa sasa. "Hivyo hati hizo mpya za rangi ya blue ambazo zitatumika baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya zitatengenezwa na kampuni ya French firm Gemalto. Kubadilika kwa rangi ya hati hiyo kunatafsiriwa kuwa ni alama ya kurudi kwa nguvu ya Uingereza, umesema mtandao ulitoa taarifa hizi. 

   Pia taarifa zinaeleza kuwa Kampuni ya De La Rue inafikiria kukata rufaa baada ya kukosa na kushindwa katika zabuni ya kutengeneza hati hizo mpya. Kampuni hiyo imeripotiwa ikidai haikuridhishwa kwa kupoteza zabuni hivyo hivyo inaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza Hata hivyo Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya De La Rue Jitesh Sodha amesema kitendo hicho kimesababisha hisa za kampuni yao kutoka asilimia 14 ya Jumanne ya wiki hii hadi kufikia asilimia 0.4 leo Machi 22 ya mwaka huu. 

   "Tumechukizwa na kitendo cha Serikali ya Uingereza kusitisha mkataba wetu wa kutengeneza hati za kusafiria za nchi hiyo wa miaka 10 kwani ulikuwa mkataba unamalizika Julai mwakani. Hivi karibuni katika uzinduzi wa E-Passport, Rais Dk. John Magufuli amesema kuwa kuna wajanja awali walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507. 

  Rais Magufuli alisema baada ya kugundua ujanja huo Rais alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380. 

  Moja ya kampuni ambayo ilikosa zabuni ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria nchini Tanzania ni hiyo ya De La Rue na moja ya sababu ilikuwa ni kiasi kikubwa cha fedha ambazo walikihitaji lakini Serikali iliwashutukia na kuamua kutoa zabuni kwa kampuni nyingine iliyotengeza kwa gharama nafuu. Hata hivyo vyanzo vya kuaminika kutoka Serikali ya Tanzania vilibanini mambo mazito yaliyoibuka baada ya kubainika kampuni hiyo kuhonga mamilioni ya fedha ili kuichafua mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.

  0 0  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
  Tanga,Dkt Asha Mahita

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
  Tanga,Dkt Asha Mahita


  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

  SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).

  Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

  "Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.

  Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.

  Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

  Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).


  0 0

  Na Maura Mwingira, Dodoma 

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Palamagamba Kabudi ( Mb) amesema, Wizara yake pamoja na Taasisi ambazo zipo chini yake, imeendelea kutekeleza ahadi zote za Ilani ya Chama cha Mapinduzi zinazoambatana na na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria. 

  Waziri Kabudi ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma. 

  "Wizara yangu imekuwa ikiwajibika vilivyo katika kuhakikisha kuwa inatekeleza ahadi zote za Ilani zinazoambatana na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria" ameeleza Mhe. Waziri 

  Akazitaja ahadi hizo kati ya nyingi, kuwa ni, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubathirifu wa mali ya umma, kukuza, kulinda haki za binadamu na utawala wa sheria katika ngazi zote za uongozi, kuimarisha mfumo wa utoaji wa haki na kukamilisha mchakato wa Katiba mpya. Akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Wizara na Taasisi zake nane, Waziri aliiomba Kamati hiyo kupitisha zaidi ya Sh. 183.223.058,000bn/- zikiwa ni fedha za mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kwa Wizara na Taasisi zake. 

  Pamoja na kuwasilisha Mpango na Makadirio ya bajeti kwa mwaka 20018/2019, Waziri Kabudi alianisha baadhi ya mafanikio ya Wizara hiyo na taasisi zake katika bajeti ya 2017/2018. Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na wananchi kupata haki zao kwa wakati kutokana na kupungua kwa mlundikano wa mashauri katika mahakama ya Tanzania kufika chini ya asilimia kumi. 

  "Mhe. Mwenyekiti mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa vipaumbele hadi kufikia tobo ya tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018 na kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi na matumizi ya utajiri na rasilimali za nchi kutokana na kuwekewa miongozo ya kisheria" akabainisha Waziri Kabudi. 

  Akayataja mafanikio mengine kuwa ni huduma za mahakama kutolewa karibu zaidi na wananchi kwa kujengwa kwa mahakama mpya, kuimarika na kukua kwa mifumo ya ufikiaji wa haki za kisheria na haki za binadamu, kuendelea kuimarika kwa viwango vya usajili kitaifa hususani kwa watoto wa umri chini ya miaka miaka mitano. 

  Mafanikio mengine ambayo Mhe Waziri ameyaelezea wakati wa uwasilishaji wa Mpango na Makadirio ya Bajeti kuwa ni pamoja na, kuogezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu haki zao, namna ya kudai haki zao na uwezo wa serikali katika kuwapatia huduma ya msaada wa kisheria. Kama hiyo haitoshi, Mhe Waziri Kabudi ameileza Kamati kwamba, katika utekelezaji wa   mpango na bajeti ya mwaka 2017/2018, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika uendeshaji wa mashauri ya daawa ( madai) hadi kufika mwezi february 2018,ili pata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na thamani ya shilingi 1,064,581,955,743bn/-. 

  Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na Sheria ushindi huo umewezesha pamoja na mambo mengine, maamuzi ya serikali pamoja na sheria za nchi kutobadilishwa kwa msingi ya kuikuka Katiba. Mafanikio mengine ambayo yametajwa na Waziri Kabudi ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama sehemu ya utelelezaji wa Ilani ya CCM,kuendelea na utoaji wa ushauri wa kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali yanayofanywa na Wizara Idara na Taasisi za Serikali . 

  Katika eneo hilo , hadi kufikia mwezi February, 2018 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki na kutoa ushauri wa mikataba 691 yenye thamani ya Shilingi 1,720,026,713,823bn/- na Dola za Kimarekani 1,0884,472,366, mikataba hii ilihusu ununuzi , ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii na ujenzi wa barabara. 

  Katika uendeshaji wa kesi za jinai, Waziri wa Katiba na Sheria aliieleza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwamba, katika kipindi kinachoishia February 2018. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendelea na uratibu wa shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai mahakamani 

  Mashauri ya jinai yaliyoshughulikiwa ni pamoja na yaliyohusu wanyamapori, dawa za kulevya, uhujumu uchumi, rushwa na mauaji. Ambapo washtakiwa waliotiwa hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa ambapo jumla ya shilingi za kitanzania 2,169 ,983,500 zilitozwa kama faini kutoka kwa washtakiwa. 

  Aidha kwa upande wa mali zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya Shilingi 2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya shilingi 908,019,979. Mali nyingine zilizotaifishwa ni pamoja na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika banari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba. 

  Mali nyingine zilizotaifishwa katika kipindi hicho ni pikipiki, mifugo, mafuta na basi la abiria lililokuwa likitumika kusaifirishia meno ya tembo yanazokadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya shilingi 3,242,787, 915. 

  Kwa upande wa uandishi wa Sheria, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliandaa jumla ya miswaada 15 ya sheria ambayo iliwasilishwa Bungeni na kupitishwa na kuwa sheria. Hali kadharika, iliadaa sheria ndogo na matamko mbalimbali ya serikali yapatayo 164 ambayo yalichapishwa kwenye gazeti la serikali. 

  Mafanikio mengine ni pamoja na kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. 

  Katika kikao cha Ijumaa mafungu yaliyopitishwa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria na Katiba ni yale ya Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka . 

  Kikao hicho cha uwasilishaji wa mpango na bajeti ya Wizara kilihudhuriwa pia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Ngwembe, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria. 

  Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto. 

  Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi amesema Wizara yake   pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika sekta ya sheria, ambapo pamoja na mambo mengine, wananchi wanauelewa mkubwa wa namna ya kutafuta na kupata haki yao kisheria. Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.Pamoja naye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi.


  0 0

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Neema Tawale (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi, Salome Kasanga.

  The Ambassador of Kuwait in Tanzania His Excellency Hon. Jaseem Al Najem (L) Handing Over Equipments to support Premature babies at Benjamin Mkapa Hospital to the Executive Director of the Hospital, Dr. Alphonce Chandika, A support from the Embassy of Kuwait in Collaboration with Doris Mollel Foundation end of this week in Dodoma. second from left is Ms. Doris Mollel Founder of Doris Mollel Foundation and Ambassador to Preterm babies in Tanzania , Neema Tawale(second from right) together with Acting Director of Nursing at Benjamin Mkapa Hospital Sr Salome Kasanga.
   Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa hivyo vilivyogharimu dola za Marekani elfu ishirini (20,000 USD) huku Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (kulia) wakimsikiliza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem,  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Januarius Hingi wakati akitoa maelezo ya namna vifaa hivyo vitakavyosaidia wakina mama wanaojifungua watoto wanaozaliwa kawaida na wale wanaozaliwa kabla ya wakati. 
  Sehemu ya vifaa hivyo.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  “Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie

  SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.

  Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania. 
   
  Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni

  “Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi huyo.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, 

older | 1 | .... | 1546 | 1547 | (Page 1548) | 1549 | 1550 | .... | 1897 | newer