Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1547 | 1548 | (Page 1549) | 1550 | 1551 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana, Femina Hip limetoa tuzo kwa washindi kumi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi, lililoshirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa kumi na tano nchini.

  Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji tuzo kwa washindi, Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles amesema shindano hilo lililenga kuleta uelewa pamoja na kubaini changamoto kuhusu masuala ya hedhi wanazokabiliana nazo watoto wa kike katika jamii.

  Amesema wanafunzi karibu 88 walishiriki shindano hilo, ambapo wavulana walikuwa 27 na wasichana 61. Na kwamba walioibuka washindi ni wasichana 5 na wavulana 5, huku shule ya Sekondari Chang’ombe ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya washindi na washiriki.“Shindano hili lililenga kupaza sauti za changamoto za wasichana wanazokutana nazo wakiwa katika siku zao.Huu mradi ulilenga kumsaidia mtoto wa kike kuwa shuleni siku zote ambazo ana hedhi, kuhakikisha uwepo wa maji shuleni na vyoo visafi,” amesema.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Femina Hip, Sauda Simba amesema shindano hilo limebainisha changamoto wanazopata watoto wa kike wakiwa kwenye siku zao, ikiwemo ukosefu wa taulo za kujihifadhi-Pad, na kuitaka serikali pamoja na jamii kuhakikisha watoto wa kike wanapata hedhi salama.

  Kwa upande wake, Balozi wa masuala ya hedhi salama, Badru Juma ameitaka serikali na jamii kutatua changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike hasa wa kijijini. Washindi hao ni pamoja na Veronica Felician kutoka Kondoa Girls High School kutok Dodoma, Jemima Carlos, Yasin Said,, Humphrey Otedo wote kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe, na Latifa Salumu kutoka Shule ya Sekondari Zinga.   Wanafunzi kutpka shule za sekondari walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo.
  Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akionyesha jarida la Fema
  Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Yassin Haji kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.
  Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi.
  Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akiwa na baadhi ya washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi na wachama wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip.
  Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Humphrey Otedo kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.
   

  0 0

  Maofisa wa Benki ya Azania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya kuanza kwa mkutano uliondaliwa na TCCIA kwa ajili ya wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo katika uwekezaji.  Mkutano huo ulidhaminiwa na benki hiyo.
   Washiriki wa mkutano wakijadiliana jambo.
   Wadu wa sekta ya biashara wakiwa katika mkutano huo.
   Wadau.
   Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group Ltd, Imani Kajula (kushoto), akimkaribisha Ali Mfuluki katika mkutano huo.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Itembe (kushoto), akibadilishana mawazo na  Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group Ltd, Imani Kajula, kabla ya kunza kwa mkutano wa wafanyabiashara.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki (kushoto), akibadilishana mawazo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Itembe (kulia).
   Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Itembe na Makamu wa Rais wa TCCIA, Octavian Mshiu.
   Washiriki wa mkutano huo.
  Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano.
   Makamu wa Rais wa TCCIA, Octavian Mshiu, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Azania, Charles Itembe ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua mkutano huo. 
   Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay (kulia), akijiandaa kutoa mada wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Wakulima, Wafanyabiashara na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), kwa ajili ya kuhamasisha wafanyabiashara kuchangamkia fursa za uwekezaji na kutumia taasisi za kibenki kupata mitaji, mkutano huo ulidhaminiwa na benki hiyo.
   Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, akitoa mada katika mkutano huo.
   Wadau.
   Kaimu Meneja Huduma na Uwezeshaji Brella, Bosco Gadi, akitoa mada katika mkutano huo.
  Mwakilishi kutoka UWURA, Mr. Keneth akitoa mada.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki akizungumza katika mkutano huo.

   Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja akizungumza katika mkutano huo. 
   Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja, akizungumza katika mkutano huo. 

  0 0

   Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala (Kulia) pamoja na Meneja wa mahusiano  wa Halotel Stella Pius kwa pamoja  wakiongea na wananchi katika soko la makumbusho, Dar es Salaam, jana ,kuhusu  kampeni yao mpya ya kununua bando kwa Halopesa  ambapo mamilioni ya wateja kunufaika kwa kupata huduma za mawasiliano kwa bei nafuu Zaidi, ikiwa ni muendelezo wa kampeni yao ya kufikia mteja mmoja mmoja . 
   Katika kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano nchini, Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel imeendelea kubuni mbinu mpya kuhakikisha kwamba wateja wake wa kada zote wanapata suluhisho la changamoto ya gharama za mawasiliano na kupata huduma hii kwa urahisi zaidi.

  Ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuboresha huduma, Halotel, Imepunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wake kwa kuzindua huduma mpya ya Nunua Vifurushi maalum kwa Halopesa ili kuwawezesha wateja wa mtandao huo kuepuka gharama kubwa za mawasiliano.

  Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo, Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Nguyen Van Son, amesema kuwa huduma hiyo itawawezesha wateja wote nchi nzima kuweza kununua vifurushi maalum kupitia Halopesa ambapo wamezingatia uhitaji wa mahitaji yao

  “Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya chini wanaofanya mawasiliano yanayolingana na wenye vipato vya kati lakini wanapata huduma hii kwa gharama nafuu kwa kujiunga kupitia Halopesa tofauti na wateja wengine, aliongeza Son”.

  Mfano; kwa mteja anayetumia shilingi mia tano (500) kwa siku, kwa sasa anaweza kujiunga na kifurushi hiki maalum kupitia Halopesa akapata hadi dakika 32 za kupiga simu mitandao yote, Mb 250 za intaneti na ujumbe mfupi (SMS) 550, vilevile kwa shilingi mia tano (500)hiyohiyo mteja anaweza kujiunga na kifushi cha wiki akapata Mb 300 za intaneti za kutumia kwa wiki nzima. 
   
  Hatuishi hapo, kwa mteja anayetumia shilingi elfu moja ( 1000) anaweza kujiunga na kupata hadi dakika 52 za kupiga mitandao yote, Mb 350 za intaneti na ujumbe mfupi (SMS) 1000 za kutumia kwa wiki nzima kujiunga kupitia Halopesa kupiga code namba *150*88# na kuchagua namba 2. ” Alisema Son.

  Halopesa ni huduma ambayo inaendelea kukua zaidi, ambapo mbali na mteja kuweza kupata huduma za miamala ya kifedha, kulipia bili mbalimbali kupitia simu ya mkononi, lakini pia mteja anaweza kujiunga na vifurushi mbalimbali kwa punguzo ya asilimia 30 ya gharama kwa kiasi cha pesa atakachotumia na punguzo la kiasi hicho cha pesa atawekewa kwenye akaunti yake ya muda wa maongezi ambapo anaweza kutumia apendavyo. 

  Halopesa ni huduma iliyozinduliwa rasmi tarehe 15 Octoba 2015, ikiendelea kukua kwa kasi na imeenea sehemu kubwa nchini kwa asilimia 95% ya watanzania mijini na vijijini na ni ya haraka ambapo inapatikana kwa code namba ya *158*88#.

  “Kwa kutumia Halopesa mteja anaweza kufanya malipo mbalimbali kama vile kutuma na kupokea fedha, kupokea au kutuma fedha kupitia benki na kulipia huduma nyingine kama Luku, Dawasco, na ving’amuzi vya televisheni mfano. DSTV, ZUKU, mifuko ya jamii wa GEPF, TCU na Polisi, kulipia michezo mbalimbali ya kubashiri kama Sportpesa na Mojabet, kununua muda wa maongezi na vifurushi mbalimbali kwa mtandao wa Halotel”, Aliongeza Son.
   
  “Tangu tumeanza kutoa huduma kwa Watanzania tumekuwa tukizingatia sana utoaji wa huduma kulingana na mahitaji halisi na hali ya kiuchumi kwa  Watanzania jinsi ilivyo, Tutaendelea kuhakikisha wateja wetu wanapata vifurushi vinavyoendana na uhalisia wa maisha yao.
   
  Tunatarajia kifurushi hiki kitaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wetu na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wakulima na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia intaneti kwa uhakika.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipeana amani na Masista wa Kanisa Katoliki walipojumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti takatifu wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018. Picha na IKULU

  0 0

   Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga.

  MARA, tarehe 20 Machi, 2018 – Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000 walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo.

  Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa wa Katiba na Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri. Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili.


  Mfumo huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.

  Zoezi hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao. Inatatua suala la msingi la upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa katika usajili wa vizazi nchini Tanzania.

  Kwa kuanza kwa mfumo huo katika mikoa miwili, wazazi wanaweza kufikia kwa urahisi zaidi ya vituo 790 vya usajili kulinganisha na vituo 11 vya usajili vilivyokuwepo awali. Zaidi ya Maafisa Usajili 1,700 wameshapewa mafunzo kwaajili ya kusaidia mchakato wa usajili.

  Pamoja na mfumo mpya serikali pia imefuta ada ya usajili na nakala ya kwanza ya cheti cha usajili kinatolewa bure, jambo linalofanya ‘hatua fupi za mchakato wa usajili kwawazazi kupata cheti cha kuzaliwa. Kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi taarifa husafirishwa mara moja kwa njia ya ujumbe mfupi SMS, karahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya usajili hapo kwa hapo .

  Mfumo huu wa kujitegemea unarahisisha kwa kiasi kikubwa usajili wa vizazi kwa eneo la Tanzania bara, baada ya kudorora kwa miaka mingi. “Tunabadilisha mfumo kurahisisha watoto na familia kuweza kupata haki yao ya kuwa na cheti cha kuzaliwa," alisema Emmy Hudson Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA), anayewajibika katika usajili wa matukio muhimu ikiwemo kuzaliwa. 
  Aliongeza kwamba; “Sasa wazazi wanaweza kupokea vyeti vya kuzaliwa kutoka katika kituo husika cha kutolea huduma za afya au kupitia ofisi za mtendaji wa kata kwa wakati. Mfumo huu umewasaidia maelfu ya watoto katika mikoa hiyo ambako mfumo huu unafanyakazi na tunapanga kusambaza mfumo huu katika mikoa yote ya Tanzania bara ndani ya muda mfupi kadri iwezekanavyo.” Aliendelea kuongeza zaidi kwamba, “Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Serikali yaCanada, UNICEF na TIGO kwa mchango wao katika suala hili”.
  Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ms Maniza Zaman alisema kwamba "Kila mtoto ana haki ya kupata utambulisho. Mfumo huu mpya unarekebisha kiwango kidogo cha usajili wa uzazi na matokeo yake mamilioni ya watoto wa chini ya miaka mitano ambao walikuwa hawaonekani katika takwimu za taifa sasa watakuwa wanaonekana. Hii itasaidia watoto wengi wa kitanzania kudai haki yao na kulindwa, na serikali itakuwa na takwimu bora zaidi kwaajli ya sera na mipango."

  Serikali inatekeleza mfumo mpya tangu 2012 kwa kushirikiana na UNICEF, TIGO na Serikali ya Canada, ambayo inatoa fedha. Kuanza kwa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, utaongeza mikoa 2 ambayo itakuwa ikiongezeka kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Geita, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa and Njombe ambayo tayari imeshaanza na kufikia watoto milioni 2 walioko chini ya umri wa miaka mitano.

  Serikali ya Canada wanaamini katika haki za watoto, wakiwa wanashikilia kwamba kila mtoto anahitaji ushahidi wa kudumu wa kuzaliwa kwake kwani inatengeneza utambulisho wa mtoto kitaifa na haki zao.

  "Usajili wa kuzaliwa unasaidia kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma za kiafya na za kijamii walizonazo kwa kisheria", alisema Ian Myles, Kamishina Mkuu wa Canada nchini Tanzania. “Canada wanajivunia kuunga mkono juhuduza tanzania katika kukuza usajili wa uzazi, kuwasaidia watoto na familia zao kujipatia haki zao za msingi kama wananchi wa Tanzania . Tunafuraha kuona uzinduzi wa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, ikiwa ni mwenyelezo wa mafanikio ya uzinduzi wa mfumo huu katika mikoa ya Iringa, Njombe, Geita na Shinyanga, Lindi, na Mtwara.” Mpaka sasa mfumo huu umezifikia Halmashauri za wilaya 58 katika mikoa 9 ya Tanzania bara.

  Msaada wa kifedha kutoka serikali ya Canada umewezesha uanzishwaji wa mfumo endelevu wa usajili wa vizazi yenye lengo la kufikia mamilioni ya wasichana na wavulana walioko chini ya umri wa miaka mitano. Mfumo huu utachangia katika Usajili wa Raia wenye ufanisi na Mfumo wa Takwimu Muhimu katika nchi, ambao unaanzishwa. TiGO inaunga mkono juhudu hizo kupitia teknolojia ya simu, ambayo inahakikisha kwamba taarifa za usajili ya vizazi unaingizwa na kutumwa kwenye database kuu iliyoko RITA wakati huo huo. TIGO pia inatumia vyombo vya habari kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa usajili wa uzazi nchini Tanzania.

  Akiongea katika sherehe za uzinduzi, Mkurugenza wa TIGOKanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa amesema “kwa pamoja tuna dhamana ya kuhakikisha ustawi wa nchi na wananchi wake. Maamuzi yaTIGO kuunga mkono juhudu hizi inasisitizia jitihada zetu za kujenga mfumo imara wa kijamii ambao uleta ahadi ya teknolojia katika jamii tunakofanyia kazi.    Kwa uvumbuzi huu, TIGO inatoa mchango mzuri na mkubwa kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu na kulinda haki za watoto. Kwa kuongezea, ushirikiano huu unadhihirisha nafasi ya kampuni za simu katika kutatua mahitaji ya kijamii kupitia matumizi ya teknolojia yako na ujuzi wao.’

  0 0

   Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Zakia Meghji akitoa maneno ya hamasa kwa vijana wa Girl Guides katika semina iliyofanyika Makao Makuu ya TGGA, Mtaa wa Kibasila, Upanga Dar es Salaam.

  Meghji ambaye aliwaelezea historia ya maisha yake tokea utotoni, shuleni, chuoni na ya kisiasa, aliwataka Girl Guides kuwa jasiri, waadilifu, wazalendo na wachapakazi pamoja na kuwa na vision..

  Aliwafundisha jinsi ya kupambana na wanaume walaghai wanaowataka kimapenzi na kuwaharibia ndoto yao ya kielimu na maisha kwa ujumla.

  Pia aliwataka kuheshimu mila nzuri, desturi na utamaduni mzuri pamoja na kuwaheshimu wazazi na jamii bila kusahau kushirikiana nao katika masuala mbalimbali.

  Aliwaambia kuwa baadhi ya mambo muhimu ni kuwa na tabia ya kushirikiana na watu mbalimbali kwa lengo la kubadilisha uzoefu, mawasiliano na kwamba unatakiwa kuanza uongozi ukiwa kijana siyo ukiwa mzee.

  Anawaeleza kuwa ushupavu wake ulimfanya kwa mara ya kwanza awe mbunge mwaka 1985, amekuwa Mkuu wa wilaya na waziri kwa muda mrefu mpaka alipoamua kustaafu.


   Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
   Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akisalimiana na Girl Guides kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na mikoani.
   Mkufunzi wa TGGA Makao Makuu ya TGGA,  akielezea historia ya chama hicho
   Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Grace Makenya akitoa maneno ya hamasa kwamba daima hastaafu na kwamba yeye hivi sasa ana miaka 70 lakini bado ni Girl Guides

   Girl Guides wakiimba wimbo wa hamasa
   Yess Girl, Nadine Ratovoson kutoka Madagascar akijitambulisha. Yupo nchini kwa ziara ya mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana mafunzo.
   Yss Girl kutoka Zambia ambaye yupo nchini kwa ziara yamiezi sita ya  kubadilisha mafunzo
   Miryam Mjema na Grace Makenya
   Kamishna wa TGGA, Temeke, Komba akijitambulisha
   Sophia Simon (kulia) Mkufunzi wa TGGA Temeke, akijitambulisha
   Kamishna wa TGGA Ilala, Stellah Kasisika akijitambulisha
   Girl Guide wakiwa na furaha
   Meghji akisisitiza jambo
   Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi (kulia) akiwa na Mdau wa TGGA, Asiah Abdul Azizi na Candida Bahame.
  Mwanafunzi kutoka Shule ya Zanaki, Winhope Mgalega, akimmuliza Zakhia Meghji ni nini siri ya mafanikio yake.

  0 0

  Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Rehema Myeya, akimkaribisha Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, kufunga semina elekezi kwa waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania bara, mkoani Morogoro.
  Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, akifunga semina elekezi kwa waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote ya Tanzania bara (hawapo pichani), iliyokuwa na lengo la kuwajengea ujuzi, uwezo na njia mbadala za kuongeza idadi ya wanawake katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, mkoani Morogoro.

  Baadhi ya waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote ya Tanzania bara wakifurahi jambo wakati wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, wakati akifunga semina elekezi iliyoandaliwa na Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), na kufanyika katika ukumbi wa chuo hicho mkoani humo.

  Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali (kulia aliyekaa kwenye kiti) akiwa na waratibu wa shughuli za ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka mikoa yote Tanzania bara, mjini Morogoro. Pembeni yake ni Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Rehema Myeya.


  ………………..


  Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema itahakikisha wanawake walio katika Sekta ya Uhandisi na Ukandarasi wanapata fursa za kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na matengenezo ya barabara.Hatua hii inalenga kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika sekta hiyo ili kufikia lengo la kuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume ifikapo mwaka 2025.

  Akizungumza mkoani Morogoro, wakati wa ufungaji wa semina elekezi kwa waratibu wa mikoa wa ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka ofisi za Wakala wa Barabara (TANROADS), mikoa yote Tanzania bara, Mkuu wa Chuo cha Ujenzi, Morogoro Bw. Melkzedeck Mlyapatali, amewashauri kuwa mabalozi wazuri wa kuwahamasisha na kuelimisha wanawake katika maeneo yao ya kazi kuchangamkia fursa hizo.

  Aidha amewaasa waratibu hao kuhakikisha wale wanawake ambao tayari wamefanikiwa kupata kazi hizo zifanywe kwa kuzingatia ubora, gharama nafuu na kuzingatia muda uliopangwa kwenye mkataba.Bw. Mliyapatali ametumia fursa hiyo kutoa wito na kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao hususan wa kike katika Vyuo vya Ufundi ili kupata ujuzi wa masuala ya Ujenzi utakaosaidia kuondoa dhana kuwa masomo ya ufundi ni kwa ajili ya watoto wa kiume tu.

  “Mimi pia ni mwalimu hapa chuoni, kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa ukimfundisha mtoto wa kike anakuwa mahiri na weledi wa hali ya juu, tofauti na mtoto wa kiume”, amesema Bw. Mlyapatali.Kwa upande wake Mratibu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Rehema Myeya, amewahimiza waratibu walioshiriki semina hiyo kutoka Mikoa mbalimbali kuwa chachu ya maendeleo katika vituo vyao vya kazi na kuhakikisha kuwa wanawake watakaopata kazi za ujenzi au matengenezo ya barabara zinakuwa katika viwango vinavyokubalika.

  Naye Mratibu kutoka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Prisilla Mushi, ameahidi kusimamia, kuelimisha, kuhamasisha na kutoa msukumo kwa jamii katika ushiriki wa wanawake kwa kutumia teknolojia katika kazi za barabara.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma


  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James (MCC) Kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Kufungua Semina Elekezi kwa Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Wa Chama cha Mapinduzi leo Mjini Dodoma.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kutoa maelezo na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo Maalum kwa Wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa.
  Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini
  Dodoma.

  Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini
  Dodoma.

  Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini
  Dodoma.

  Washiriki wakifuatilia semina elekezi ,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini
  Dodoma.

  Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni Ndg.Steven Kazidi akiwasilisha Mada katika Semina Elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana CCM Taifa,leo katika Ukumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini
  Dodoma.

  Meza kuu ikifuatilia Semina

  (Picha zote na Fahadi Siraji wa UVCCM)

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

  Na Hamza Temba, Dodoma
  ..........................................................

  Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


  Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.


  Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.


  "Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.


  Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3.5 zilitumika.


  "Awamu ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017 na utarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimetumika katika awamu hii ya mradi" alisema.


  Alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti wa mazao mbalimbali ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati mipya ya kukuza Utalii hapa nchini.


  Warsha hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

  Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


  Naibu Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


   Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa warsha hiyo.
   Wajumbe wa Meza Kuu.

  Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
   Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
  Warsha ikiwa inaendelea.
  Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0


  0 0


  Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti 205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
  Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson , akikabidhi meza na viti 205,Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal, kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja
  Mkurungezi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Bi. Safia Rijal akikabidhi moja ya meza na viti kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi za Kijiji cha Kijini Maatemwe na Wawakilishi wa International Volunteers Oman Hemed Mohammad, Danny Kim na Nahya Khamis wa Mradi wa Best Of Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A, Unguja.
  Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson akiwa na Mwakilishi wa Internalional Volunteers Oman Danny Kim, wamekali meza na viti walivyokabidhi kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja, kulia Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalazi Bi, Safi Rijal na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Kijini.
  Mwakilishi wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Mohammed Issa akitowa maelezo kabla ya hafla ya makabidhiano wa vifaa kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.
  Mwakilishi wa International Volunteers Oman Danny Kim akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205, kwa Skuli za Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja Skuli hizo zinapata ufadhili kupitia Mradi wa Bset of Zanzibar, uliooko chini ya Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, inayojenga kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.
  Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibar B. Safia Rijal akizungumza wakati wa hafla hiyoya kukabidhiwa Viti na Meza 205 kutoka kwa Mradi wa Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Internalional Volunteers Oman, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja.na kuhudhuriwa na Wananchi wa kijiji hicho.
  Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekongari na Msini Kijini Matemwe Mwalimu Ulimwengu Mkadam akitowa neno la shukrani kwa msaada huo na kusema umefika wakati muwafaka.
  Wazee wa Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Meza na Viti vyake 205 kwa ajili ya matumizi ya Skuli ya Sekondari na Msini Kijini Matemwe, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Kijini.  Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Limited Brian Thomson, akiwasalimia Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kijini baada ya hafla ya kukabidhi Meza na Viti vyake 205 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Zanzibat Bi. Safia Rijal kwa ajili ya Skuli ya Sekondari na Msingi ya Kijini Matemwe, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar kwa kushirikiana na International Volunteers Oman, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja  Pennyroyal Limited kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii Best of Zanzibar wakishirikiana na International Volunteers kutoka Oman wametoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Tsh 18,000,000/- ( Shilingi millioni kumi na nane).


  Akiongea katika sherehe za kukabidhiana, Mkurungezi Mkuu Bw. Brian Thomson alikua na haya ya kusema:“Best of Zanzibar imejitolea kuboresha elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Tumejiwekeza katika progamu tofauti za kielimu katika shule hizi mbili zikiwemu Masomo ya ziada (After Hours Tutoring program) kwa wanafunzi 500, na kuwasomesha walimu 30 masomo ya lunga ya Kingereza na mbinu za kufundishia ili kuongeza uwezo na ujuzi wa walimu hao.

  Tunawashukuru sana International Volunteers kwa moyo wao wa kujitolea na kushirikiana nasi katika kutoa huduma kwa mashule.”Mkurungenzi huyo alisisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii na ukuwaji wa uchumi wa nchi, ndio maana Best of Zanzibar imejikita katika uboreshaji wa elimu Zanzibar.

  “Nia yetu kuu ni kuleta manufaa na kuedeleza msingi mzuri wa kiuchumi Zanzibar. Kwa muda mrefu sana watoto wa shule ya msingi Kijini na Mbuyu Tende wamekaa chini bila madawati kuwaletea ugumu katika kuelewa masomo na kupunguza ufanisi wao wa masomo.

  Best of Zanzibar inashirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Elimu katika kuboresha viwango vya elimu katika shule za Kijini na Mbuyu Tende. Na tunaishukuru sana Wizara ya Elimu kwa kutuunga mkono katika program zetu.” Aliongezea Bw. Brian Thomson.

  Shule ya Kijini ina wanafunzi 903 na Mbuyu Tende inawanafunzi 603, katika wanafunzi hao 353 wanakaa chini bila madawati.Mkurungezi wa Masomo ya Pre-Msingi na Msingi Wizara ya Elimu, Bi Safia Rajil alikua katika hafla hiyo na alipongeza wawekezaji hao kwa msaada wao.

  “Kwa niaba ya Wizara ya Elimu napenda kutanguliza shukurani zetu za dhati kwa Best of Zanzibar na International Volunteers kwa kutoa madawati haya kwa shule hizi mbili. Msaasa huu utaleta madadiliko nakuongeza ufanisi wa watoto.”

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kijini Bw. Ulimwengu Mkada Makame alishukuru sana kampuni ya Pennyroyal Ltd kwa msaada wao.“ Shule yetu ilikua haina madawati kwa muda mrefu sana, tunashukuru Best of Zanzibar kwa kutukumbuka shule yetu.”

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

  Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori.
  Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi 10 ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Inasemekana majeruhi waliopelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wengine wao wamekatika viongo mbalimbali vya mwili.Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
  Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya.Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ,aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini .
  Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe.

  "Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.  0 0

    Gavana wa Rotary District 9211, Ken Mugisha alizinduwa Mradi wa 'Rotary Mission Green'  wa miaka 5 tokea 2017-2021 wenye lengo la kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuboresha viwango vya mapato kwa jamii. Kuhamasisha na kuongeza ufahamu na umuhimu wa upandaji miti kubadili maisha ya watu na kuongeza ukuaji na maendeleo.Ndege Beach Development Association kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni wamepanda miti 4000 eneo la Mbweni kwenye kampeni ya Mkakati wa Kijani' Mission Green' wenye lengo la kupanda miti milioni 5. 
    
   
   
  Mhandisi Florence Msambila (kulia) pamoja na wakazi wengine wa Ndege Beach Development Association wakianza zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018. (IMEANDALIWA NA ROBERT OKANDA BLOGS)
  Sehemu ya wakazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018. 
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malindi Estate/ Ndege Beach akishiriki zoezi la upandaji miti kwa ushirikiano baina ya Ndege Beach Development Association na Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018. 
  Mhandisi Florence Msambila (kulia) pamoja na Mratibu wa Mkakati wa kijani, Rotarini Jane Pesha wakishiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa ushirikiano kati ya Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni na Ndege Beach Development Association wa kampeni ijulikanayo kama'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Mratibu wa Mkakati wa kijani, Rotariani Jane Pesha (katikati)  pamoja na wakazi wengine wa Ndege Beach Development Association wakianza zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Sehemu ya wakazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Mjumbe wa Ndege Beach Development Association Godwin Makyao akishiriki katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani 'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Sehemu ya wakazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Binti Hairati Hidary akishiriki kampeni ya upandaji miti, kufuata nyayo za mama yake Heriat Magalla, Rotariani wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika Ndege Beach Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Baadhi  ya wakazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani' MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Mkazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club ya Dar es Salaam mikocheni wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani' MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Ule usemi wa wahenga, samaki mkunje angali mbichi unadhihirishwa hapa, Binti Mkunde Sembotya akipanda mti pamoja na mkazi wa Ndege Beach Development Association wakipanda mti katika zoezi la upandaji miti huku baba yake akishudia (kulia) zoezi lililoendeshwa na Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni na Association hiyo, wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani'MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Mwezeshaji wa Mawasiliano wa Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni Rotarian Leina Lemomo akielezea machache kuhusu faida na manufaa ya wana Rotariani kwa sehemu ya wakazi wa Ndege Beach Development Association baada ya kushiriki katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Rotary Club hiyo, wakati wa kampeni ya Mkakati wa kijani' MISSION GREEN' eneo la Ndege Beach jijini Dar es Salaam Machi 24 2018.
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malindi Estate/ Ndege Beach (katikati) pamoja na wakazi wengine wa Ndege Beach wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mawasiliano wa Rotary Club ya Dar es Salaam Mikocheni Rotarian Leina Lemomo alipotoa muhtasari wa kazi za Rotary Clubs duniani. 
  Gavana Msaidizi wa District, Alfred Woiso akizungumza machache kuhusu uwanachama wa Rotari Clubs duniani wakati wa kampeni hiyo.
  Wakazi wa Ndege Beach wakijumuika pamoja baada ya kushiriki kampeni ya upandaji miti ya Mkakati wa Kijani.
  Mhandisi Florence Msambila Mjumbe wa Ndege Beach Development Association akishukuru washiriki wa kampeni hiyo.
  Picha ya Pamoja kuhitimisha zoezi la upandaji miti. 


     

  0 0

  Kongamano la biashara lililoandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) limefanyika jijini Dar es salaam na kuzungumzia mambo kadha wa kadha hususani fursa katika bomba la mafuta la Tanga hadi Hoima, Huduma za fedha kurahisisha biashara za kimataifa na pia makubaliano ya biashara kati ya TCCIA na Chemba ya biashara kutoka China.
  Akizungumza wakati wa kufungua rasmi kongamano hilo Charles Itembe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania alisema “ ikiwa wafanyabiashara watatumia huduma za fedha za kimataifa kama Letter of Credit basi itapunguza utapeli na hivyo kukuza biashara. Pia alielezea jinsi benki ya Azania ilivyo tayari kushirikiana na wafanya biashara katika kukuza biashara na uchumi wa viwanda”Nae Mwenyekiti wa Infotech group Ali Mfuruki aliwaasa wafanya biashara kujenga viwanda vyenye kusaidia lengo la Serikali la kuhakikisha viwanda vinajengwa.
  Makamu wa Rais wa TCCIA Octa Mshiu alishukuru wanachama wa TCCIA na waalikwa  kwa kufika na kibadilishana uzoefu na changamo.Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo kwa kushirikiana na TCCIA,Imani  Kajula “ alisema mkutano huu ni mwendelezo wa lengo la TCCIA kuwawezesha wanachama wake kuwa na jukwaa la mashauriano.
  Wadhamini wa kongamano hilo ni Azania, ATCL na Zurich Insurance.

  0 0

  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi yao 
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya. 


  WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.

  Hayo ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinachow asaidiawaat hirika wa madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.Waziri Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.

  Alisema nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.“Jambo linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.

  Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo lakutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.

  “Jamani hawa watu wasiishi kw a kuombaomba lazima wapatiwe eneo lao na waanzishe miradi yao itakayowasaidia kujikimu na mahitaji ya kila sikuna tukifanya hivi tutaokoa kundi kubwa la vijana linaloangamia sikihadi siku”Alisema Waziri Ummy.Mbali na hilo alisema akiwa kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha dawa za Methadol zinafika Moani hapa kama ilivyo katika mikoa mingine ili kuweza kuwasaidia vijana hao kupunguza makali ya madawa.

  “Kwanza nashangaa kama tanga haipati dawa hizi za methadol ikiwa ni mkoa wa pili baada ya dare s salaam kwa wingi wa watumiaji wa mada ninayo dhaama na dawa hazi zitafika sasa kwa ajili ya vijanawetu”Alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Said Bandawe alisema kwasasa wanaishi katika nyumba ya kupanga na wamepewa eneo na wamepewa eneo la mtu kwa kuazimwa kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga nashughuli za ufugaji.

  Alisema maisha ya vijana bado magumu hasa swala la chakula,malazi,dawa za Methadol, na namna ya kupata mahitaji ya kila siku kwa ujumla huku akijaribu kutafuta mahitaji kwa kuomba misaada kuwasaidia vijana haowanaokadiriwa kufikia 68 (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Ndunguru (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza wadau mbalimbali kufungua bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mkinga mkoani Tanga. 
  Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi. 
  Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania, Isack Abdiel, akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari. 
  Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo. 
  Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya. 
  Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.

  Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water Missions International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi mkubwa utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utaowawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi yao na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi. 

  Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji salama, kutokana na kutokuwepo na vyanzo vya uhakika vya maji katika eneo hilo.Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni, Mwakihonda and Karoyo vimekuwa vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka tanki la zamani la kusambaza maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere, ambalo limekuwa halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji hivyo. 

  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu wilayani hapa kutawezesha wananchi kupata maji safi ya uhakika wakati wote,kwa niaba ya serikali nalishukuru shirika la Water Missions International Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini”. 

  Mhandisi Ndunguru, alisema mradi huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi wakazi wa Mkinga na kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia .

  Alitoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa shirika hilo sambamba na kutunza miundo mbinu itakayowekwa katika maeneo yao ili kuwezesha mradi kuwa endelevu. “Mradi huu muhimu hapa Mkinga pia utaimarisha afya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa mbalimbali yanayosababisha na ukosefu wa maji na matumizi ya maji yasiyo salama kwa kuwa hivi sasa tuna uhakika wa kupata maji salama,”alisisitiza. 

  Kwa upande wake,Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania ,Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kuzindua mradi wa maji katika wilaya ya Mkinga ,ukiwa ni mwendelezo wetu wa kuunga mkono serikali ya Tanzania kuboresha upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwenye jamii zenye upungufu wa maji nchini,tunayo imani wananchi mmeupokea vizuri na mtaulinda ili uwe mradi endelevu ili unufaishe mpaka vizazi vijavyo”.

   Aliwashukuru watendaji wa serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali inayoshirikiana nayo na wadau wote ambao wamefanikisha jitihada za kuanzisha mradi huu wilayani Mkinga. Shirika la Water Missions International Tanzania,lilianza kufanya kazi nchini mnamo mwaka 2013, likiwa limejikita katika kuendesha miradi ya kuondoa kero ya maji kwenye jamii ,sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi ya maji.Hadi kufikia sasa shirika limefanikisha miradi ya maji katika mikoa zaidi ya 6 nchini,ikiwemo mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Kagera na Tanga.

   Ofisi za makao makuu ya Water Missions International Tanzania nchini yapo jijini Dar es alaam na ndipo inaporatibiwa miradi yote ya maji inayoendeshwa na shirika nchini .Tanzania ni nchi ya 10 kuwa na miradi ya shirika hili.Baadhi ya nchi nyingine linapoendesha miradi ya maji ni Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, na Belize.

  0 0

  Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ibuka mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.
  VICE PRESIDENT Joha 352 Joyce 248. SECRETARY Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. ASST SECRETARY Saria 360 DMK 23. ASST. TREASURY Magret 263 Mikidadi 329.... BOARD Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

  0 0

   ​muonekano wa soko kwa nje​
   ​Mstahiki Meya mwenye suti ya kaki akiwa ameongozana na baadhi ya wananchi wakielekea kuzindua soko​
   ​Mstahiki Meya wa Manispaa ya kigamboni Mh. Maabadi Hoja akifungua kitambaa cha jiwe la msingi kuonesha uzinduzi rasmi wa soko​
   ​Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akisoma kibao cha uzinduzi mara baada ya kuzindua
   ​Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa soko​
   ​Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi kabla ya uzinduzi.​

   ​wananchi na Meya wakisoma maandishi ya uzinduzi wa soko mara baada ya kuzinduliwa.​
   ​Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabadi Hoja akikata utepe kuonesha ishara ya uzinduzi rasmi wa soko ​
   ​Mstahiki Meya akiwa ameongozana na wananchi wakikagua soko mara baada ya uzinduzi. 
   Mstahiki meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akizungumza na wananchi mara baada ya uzinduzi wa soko
  Mwananchi na mfanyabiashara Bi. Rehema kambi akishukuru kufunguliwa kwa mradi huo na kuomba kuletewa miradi mingine ili wananchi wanufaike.

  Wananchi wa mtaa wa Tungwi-Songani Kata ya Pembamnazi Manispaa ya Kigamboni wametakiwa kutunza miundombinu ya soko ili soko liweze kudumu kwa muda mrefu na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla. 

  Rai hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja alipokuwa akizindua mradi wa soko hilo ijumaa lililojengwa Mtaa wa Tundwi-Songani , alisema kuwa mradi huu umenza ujenzi muda mrefu tangu mwaka 2002, hivyo tunatarajia ukamilikaji wake utaleta maendeleo kwa wananchi wote wa Tundwi Songani na jamii nzima ya Kata ya PembaMnazi hivyo ni muhimu kuhakikisha unatunzwa. 

  Alisema kuwa ulinzi uimarishwe wa miundombinu na kuhakikisha lengo lililokusudiwa la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na wananchi wa Tundwi na kata ya Pemba Mnazi kwa ujumla linafikiwa. 

  Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Manispaa ya kigamboni Bi.Janet Kacholi alisema kuwa, mradi wa soko ni miongoni mwa miradi iliyoibuliwa na wananchi kupitia program ya TASAF, ambapo umelenga kutoa ajira kwa vijana kwa kupata fursa ya kuuza mazao mbalimbali na kuiwezesha Serikali kupitia Halmashauri kukusanya mapato kutokana na ushuru mbalimbali utakaotozwa kwa wafanyabiashara. 

  Aliongeza kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo jumla ya Tsh.91,858,842.24 zimetumika ambapo wananchi wamechanga kiasi cha Tsh.34.040.427.27 mchango wa TASAF ni Tsh.26,416,827.27 na Halmashauri ya Manispa ya kigamboni imetoa Tsh.31,401,587.7 ambazo zimekamilisha ujenzi wa meza za ndani baada ya Halmshauri ya Temeke kushindwa kutoa fedha za ukamilishaji kama ilivyoahidi wakati wa uibuaji wa mradi kabla ya kugawanywa. 

  Soko lipo tayari kwa matumizi ambapo vizimba /meza 60 sawa na wafanyabiashara 60 wataweza kufanya biashara ndani ya soko hilo na eneo la nje kuzunguka soko linakadiriwa kuchukua wafanyabisahara 80 ikiwa watapangwa na kusimamiwa vizuri. 

  Aidha Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Tundwi Bw. Mikdadi Simba alisema kuwa wananchi wamelipokea soko kwa mikono miwili na litawaletea maendelo kwa sababu wataweza kufanya biashara kisasa zaidi kwa kuzingatia mji unapanuka. 

  Mfanyabiashara Rehema Kambi amesema tunashukuru kwa mradi huu wa soko kwani tunauhakika wa usalama wa bidhaa zetu hazitaweza kuharibiwa kwa mvua kama kipindi cha nyuma hivyo tunaomba Manispaa ituletee miradi mingine mizuri zaidi ya huu. 

  Mwenyekiti wa mtaa wa Tundwi Bw.Rajabu Kihimbo aliongeza kuwa anaiomba manispaa ione namna ya kuwasaidia kwenye suala la umeme ili waweze kuimarisha ulinzi na wafanyabiashara waweze kufanya biashara hata nyakati za usiku. 

  Uzinduzi wa soko umekuja mara baada ya kukamilika kwa ujenzi uliohusisha awamu mbili awamu ya kwanza ikiwa ni ujenzi wa jengo la soko , vyoo na nyumba ya kuhifadhia vifaa mbalimbali na awamu ya pili ujenzi wa vizimba. 

  Imenadaliwa na 

  Kitengo cha Teknolojia Habarai na Mawasiliano 
  Manispaa ya Kigamboni.

  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
   Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
   Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa na waandishi wa habari wa mkaoni Iringa wakitembelea maeneo ya kiwanda cha Ivori Iringa
  Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari katika jengo jimpya ambalo litafunguliwa kiwanda kipya hivi karibuni
  Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa pamoja na mdau wa chama cha mapinduzi (CCM) Hamza Ginga.

   Na Fredy Mgunda,Iringa.

   KAMPUNI ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa imempongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna alivyolipatia ufumbuzi suala la sukari ya viwandani ikisema litanusuru viwanda vilivyotaka kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

  Katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 19, pamoja na mambo mengine yanayohusu sukari, Rais Magufuli alisema hakuna sababu kwa taifa kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza sukari toka nje ya nchi wakati uwezo wa wafanyabishara kuzalisha sukari hiyo nchini upo.

  Dk Magufuli alisema mahitaji ya sukari nchini ni tani 590,000 kwa mwaka, ambapo tani 455,000 ni kwa ajili ya matumizi ya majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya viwandani.

  Alisema kwasasa kuna upungufu wa tani 125,000 za sukari ya kutumia majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.

  Akizungumza na wanahabari wakati akielezea mafanikio na changamoto uzalishaji katika viwanda hivyo, mkurugenzi wa kampuni hizo, Suhail Esmail Thakore alisema wamepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa serikali wa kushughulikia upungufu huo.

  “Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua ya haraka sana kushughulikia tatizo la sukari. Taarifa tuliyopata mara baada ya kikao kile ni kwamba taratibu za kupata vibali vya kuagiza sukari ya viwandani kwa kuzingatia mahitaji ya viwanda vyetu zinaendelea. Hiiimetupa uhakika wa kuendelea na uzalishaji,”alisema.

  Alisema viwanda vyake viliingiwa na hofu ya kusimamisha uzalishaji baada ya serikali kuzuia uagizaji wa sukari hiyo toka Novemba mwaka jana.

  “Viwanda vyetu vivyoatumia malighafi zinazozalishwa na wakulima wa ndani ya nchi, zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazojulikana kwa jina la Ivori zikiwemo tomato na chill sauce, pipi, chocolate na unga wa cocoa,” alisema.

  Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Thakore alisema kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya bidhaa hizo ndani ya nchi, na zinahitajika sana katika nchi jirani za Kenya, Kongo, Rwanda na Burundi hali inayowasukuma kuongeza uwekezaji ili kuunga mkono azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.

  Thakore alisema kwasasa viwanda vyao vinazalisha asilimia 30 tu ya mahitaji yao yote ya soko na katika kukabiliana na changamoto hiyo wameanza na ujenzi wa kiwanda kipya cha pipi kitakachowawezesha kufikia hadi asilimia 50 ya soko.

  “Tunatarajia kufungua kiwanda hicho kipya kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu. Na mwaka 2019/2020 tutaanza ujenzi wa kiwanda kingine kikubwa cha kuzalisha bidhaa hizo hatua itakayotuwezesha kukaribia mahitaji ya soko letu,” alisema.

  Akitoa mfano wa mahitaji ya soko la nje ya nchi, mfanyabishara huyo alisema walitakiwa na wafanyabiashara wa Burundi kusambaza tani 30 za bidhaa hizo kila mwezi lakini wanashidwa kufikia kiwango hicho kwasababu uzalishaji wa sasa hauwawezeshi kufanya hivyo.

  Akizungumzia mahitaji ya sukari kwa ajili ya viwanda vyao alisema, wanahitaji zaidi ya tani 1,600 kwa ajili ya kiwanda cha Ivori Ltd na tani zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kiwanda cha Iringa Food and Bevarage.

  “Hata hivyo mahitaji hayo yataongezeka mara mbili zaidi kutokana na upanuzi wa kiwanda tunaofanya. Kwahiyo tutaiomba serikali itusaidie kupata sukari hiyo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyote na upanuzi wake,” alisema.

  Thakore alitoa wito kwa watanzania kujiwekea kipaumbele cha kutumia bidhaa za ndani ili kuinua maendeleo ya viwanda, na kuongeza ajira na mapato ya wadau na Taifa.

  0 0

   Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose tweve akiwa na Naibu Katibu Mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) Taifa, Eva Kihwele pamoja na katibu wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer wakiangalia shughuli zinazofanywa na vikundi vya wanawake wa UWT tarafa ya mazombe

older | 1 | .... | 1547 | 1548 | (Page 1549) | 1550 | 1551 | .... | 1897 | newer