Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1545 | 1546 | (Page 1547) | 1548 | 1549 | .... | 1903 | newer

  0 0


   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiteta jambo na Maher Al Barwani kutoka nchi ya Oman mwenye asili ya Tanzania ambaye amesafiri kwa muda wa miezi saba kupitia mataifa mbalimbali hadi kufika Tanzania kwa pikipiki kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania nchini humo, alipotembelea ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma. 
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiteta jambo na Maher Al Barwani kutoka Oman mwenye asili ya Tanzania ambaye amesafiri kwa muda wa miezi saba kupitia mataifa mbalimbali hadi kufika Tanzania kwa pikipiki kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania nchini humo alipotembelea ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma jana. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala, Tutubi Mangazeni. 
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akiteta jambo na Maher Al Barwani kutoka Oman mwenye asili ya Tanzania ambaye amesafiri kwa muda wa miezi saba kupitia mataifa mbalimbali hadi kufika Tanzania kwa pikipiki kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania nchini humo alipotembelea ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma jana. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
   Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Maher Al Barwani, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala, Tutubi Mangazeni.
   Maher al Barwani akimuelezea Ndugu David ambeye ni Afisa Usafirishaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii jinsi alivyoweza kutumia usafiri huo wa pikipiki kutoka nchini Oman hadi Tanzania.
   Maher al Barwani anapatikana kupitia Mawasiliano hayo.
   Kwa muda wa miezi saba Maher al Barwani ameweza kusafiri umbali wa kilomita 18,035.6 kutoka Oman hadi ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma.
   Pikipiki anayotumia aina ya BMW ina uwezo wa kukimbia kwa spidi 240.
  Maher al Barwani akiondoka baada ya kusalimiana na viongozi wa viwaza mjini Dodoma. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU-DODOMA)

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akitoa salamu za pole za Manispaa ya Ilala kwa wafiwa wakati wa msiba wa Mama yake Naibu Meya Omary Kumbilamoto.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwa katika majonzi wakati wa kumzika mama yake Mzazi Mwanaisha Omary katika makaburi yaliyopo kijijini kweao Kauzeni Wilaya ya Kisarawe mkoani pwani.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro akitoa salamu za pole za ofsi ya Mkuu wa Wilaya kwenye msiba wa mama yake Naibu Meya wa Manispaa hiyo , Omary Kumbilamoto.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum,akitoa mawaidha wakati wa msiba wa Mama yake Naibu Meya
  Waombolezaji wakiswalia mwili wa Marehemu Mama yake Naibu Meya wa Mwanaisha Omary Kumbilamoto katika ibada iliyofanyika nyumbani kwa Naibu Meya Vingunguti Dar es Salaam.
  waombolezaji wengine ambao ni Dada zake Naibu Meya Wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika majonzi mazito.
  Mkuu wa Kikosi Cha Anga 622, Canala Haule akitoa salamu za pole kwa familia hiyo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambapo mmoja wa mtoto wa marehemu anafanyakazi jeshini.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akitoa pole kwa wafiwa katika msiba wa Mama yake Niabu Meya wa Manispa aya Ilala, Mwanaisha Omary.
  Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa waliofika kumfariji Naibu wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto
  waombolezaji wakiwa wanahuhifadhi mwili wa Marehemu Mwanaisha Omary Kumbilamoto Kaburini.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitia saini  ya mkataba wa Makubaliano ya kulifanya Bara la Afrika Kuwa eneo huru kwa niaba ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli leo March 21, 2018, makubaliano hayo yamefanyika  Jijini Kigali Rwanda PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  0 0

  Waziri wa ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman  akimpa zawadi mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akishuhudia. Tangu mwaka 2015 JKCI kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo  kwa watoto.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto na wazazi wao ambao walifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel.  Mhe. Liberman  alitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo .  
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi ya kitenge  Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman  alitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo. 
   Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman  akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto, kusomesha madaktari na wauguzi kati  ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu .
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman  wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walisoma nchini Israel kwa udhamini wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo.  Picha na JKCI


  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mauricio Ramos Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Millicom International Service LLC (wanne kutoka kushoto)ambayo inamiliki Kampuni ya simu ya Tigo aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Watendaji Wakuu wa Kampuni ya FERROSTAAL kutoka nchini Ujerumani na Denmark Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Denmark Einar Hebogard Jensen aliyeongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

   PICHA NA IKULU

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimkabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  akimkabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwashuhudia Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi na IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kuwaapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Rwanda katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan,  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi balozi John Kijazi Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Ramadhani Mwinyi pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama katika picha ya pamoja na Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi na IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu baada ya  kuwaapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Rwanda katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 21, 2018. Picha na IKULU


  0 0

  Mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Faraja Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii jinsi alivyopigwa na kuumizwa na wafugaji wa nchini Uganda kwa kosa la kukamata mifugo ya waganda iliyokula mazao ya wananchi wa Tanzania katika kijiji hicho mwaka 2016 (Picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi).

  Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Nape Nnauye ameishauli Serikali kuboresha mipaka ya nchi kwa wakati ili kuondokana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara kufuatia uvamizi wa wahamiaji kutoka nchi jirani.

  Ameyasema hayo katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembea mipaka kati ya Tanzania na Uganda Wilaya ya Missenyi upande wa Tanzania Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Isingiro upande wa Uganda.

  Nape amesema suala la kulinda mipaka ni muhimu hivyo ni vyema serikali kupitia Wizara ya Ardhi ikatenga fedha za kutengeneza barabara zilizoko mipakani ili kurahisisha ulinzi na usalama wa mipaka yetu na kuwezesha wakazi wa nchi hizi mbili kutambua mipaka ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua mpaka wa Tanzania na Uganda katika eneo la mto kagera.

  “Tumebaini kuwa kuingia kwa wananchi wa Uganda hasa kuleta mifugo yao katika lanchi ya Missenyi kunachangiwa na kutokuwepo njia maalumu na alama maalumu zinazotenganisha kati ya nchi na nchi hivyo watu wanaingia kupitia katika vichochoro visivyo rasmi na kuhatarisha amani kwa wakazi wa mipakani alisema Nnauye”

  Kamati hiyo pia ilifanikiwa kufika katika vijiji vya Rwengiri, Bwenkoma na Bubale vilivyopo kata ya Kakunyu na kubaini kuwa baadhi ya alama zilizowekwa mpakani zimepotea hivyo wafugaji kutoka maeneo mbalimbali wanaendelea na shughuli za ufugaji bila kujali sheria.

  Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikikagua mipaka na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kama barabara itatengenezwa katika mipaka yote ya Missenyi kazi ya kuwabaini waarifu itakuwa rahisi.
  Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James Mtamakaya akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii mipaka iliyopo kati ya Tanzania na Uganda.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa mpaka sasa Wizara imepokea shilingi bilioni 4 za kuimarisha mipaka ambapo fedha zitakazotumika kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda ni shilingi Bilioni 1.9 na shilingi Bilioni 2.1 kwa mpaka wa Tanzania na Kenya.

  0 0


  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

  Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam.

  “Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo basi wananchi wanaaswa kuwa, wakipata homa wahakikishe kuwa wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue, au sababu nyingine, ili hatua stahiki zichukuliwe.

  Waziri Ummy amesema kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa  kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wizara itaendelea Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa nchi nzima kwa kutumia mfumo uliopo wa ukusanyaji wa taarifa (IDSR), ambapo tunaendelea kupata taarifa za kila siku juu ya mwenendo wa ugonjwa huu na Kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

   Mbali na hayo Waziri Ummy amesisitiza kuwa  hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri wanaoingia na wanaotoka nchini na  Wizara itaendelea kushirikiana na wadau na sekta mbalimbali katika kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huo.

  Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi wenye madoa madoa meupe yenye kung’aa.

  0 0

   Gavana wa mji wa imo nchini Nigeria, Rochas Okorocha, akimpongeza mwanafunzi wa darasa la Sita, Anati Mujib wa Shule ya Msingi Makumbusho, anayefanya vizuri katika masomo yake darasani, wakati Gavana huyo alipoitembelea shule hiyo akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, (kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na kuchagua baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu ili kuwasomesha katika shule na Chuo chake kilichopo nchini Nigeri. Gavana huyo akiwa shuleni hapo alitoa zawadi ya Dola 100 kwa kila mwanafunzi aliyeongoza kimasomo katika darasa la tano, Sita na Saba kwa kila mmoja, na Dola 200 kwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Makumbusho, Raymond Kalistus, anayefanya vizuri kimasomo darasani, ambapo pia alitangaza kumdhamini mwanafunzi huyo wa Darasa lasaba, Abdul Ausi kwa kumsomesha Sekondari hadi Chuo Kikuu kuanzia sasa kutokana na kufiwa na wazazi wotewawili. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Gavana akimkabidhi zawadi ya Dola 100 mwanafunzi, Anati Mujibu
   Gavana akikumbatiana kwa furaha na mwanafunzi, Abdul Ausi wa daeasa la saba aliyetangaza kumsomesha kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, kwa kuchagua nchi yeyote aipendayo kwenda kupata elimu.
   Gavana akisalimiana na baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaosoma katika shule hiyo
   Gavana akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiaga kuondoka shuleni hapo
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitafsiri hotuba ya mgeni wake Gavana wa mji wa Imo nchini Nigeria, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya msingi Makumbusho.
   Gavana huyo akiendelea kuzungumza huku Naibu Spika akiendelea kutafsiri. Kulia ni msaidizi wa Gavana huyo, Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa Nigeria.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitoa hotuba yake na kushukuru ugeni huo.
   Wakielekezana jambo. Kulia ni Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Gavana huyo....
   Wakisalimiana na viongozi baada ya kuwasili Shule ya Msingi Makumbusho
   Gavana akipozi kwa picha na mwanafunzi Abdul aliyemtangaza kuwa ni mwanawe kuanzia jana
   Picha ya pamoja
  Picha ya pamoja....

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati akifungua na kuzindua mkutano wa Baraza hilo leo Mkoani Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga (Kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo Dkt.Leonard Chamuriho mkataba wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua na kuzindua mkutano wa Baraza hilo leo Mkoani Dodoma.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo Dkt.Leonard Chamuriho na Viongozi wengine wa Baraza hilo wakiimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa Ufunguzi na Uzinduzi wa Baraza hilo leo Mjini Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Mkoani Dodoma. Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) wakisIkiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga (hayupo pichani) wakati akizindua na kufungua mkutano wa Baraza hilo Mkoani Dodoma.

  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi ) mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo na watumishi wote kutimiza wajibu wao kwa kutumia muda wa kazi ipasavyo kwa kufanya kazi kwa bidii.

  Ameyasema hayo leo wakati akizindua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi leo Mkoani Dodoma.

  Aidha mhandisi Nyamhanga amesema kuwa Wizara (Sekta ya Uchukuzi) inatambua mchango mkubwa wa wafanyakazi wa ngazi zote katika kufikiwa kwa maamuzi mbalimbali ya kisera na kitaalam na hivyo kufanikisha shughuli za sekta hiyo hali inayochochea Sekta ya Uchukuzi na utabiri wa hali ya hewa kutoa Huduma zenya ubora wa hali ya juu ndani na nje ya nchi.

  Akifafanua mhandisi Nyamhanga amesema kuwa sekta ya Uchukuzi na Tabiri za Hali ya hewa zinatakiwa kutoa huduma zenye ubora wa kiwango cha juu ndani na nje ya nchi.

  “Dhana hii ya ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu sana kwa jumuiya yeyote na katika ngazi yeyote,hivyo niwashukuru sana kwa kuzingatia dhana hii muhimu na ninashauri muiendeleze” Alisisitiza Nyamhanga.

  Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuzingatia maelekezo ya kisheria wakati wa kuchangia taarifa muhimu za sekta na kushirikiana katika utekelezaji wake ili kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kusisitiza kuwa Serikali haitosita kumwajibisha mtumishi yeyote ambaye ataonekana kuwa chanzo cha kutotimiza malengo ya bajeti na mpango kazi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi la Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) Dkt.Leonard Chamuriho amesema Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi kama walivyo watumishi wengine katika utumishi wa umma wamejipanga kuhakikisha wanafanya zao kwa weledi, uadilifu, juhudi na maarifa katika kutimiza wajibu wao ili kuchangia katika kutekeleza malengo ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Tunafahamu wazi kwamba kutokusimamiwa na kuendelezwa kwa miundombinu ya uchukuzi na huduma zake hakutowezesha sekta nyingine za kiuchumi na kijamii kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa,hivyo tutaendelea kuboresha miundombinu ya uchukuzi na huduma zake”,Aliongeza Dkt.Chamuriho.

  Uzinduzi wa Baraza hilo ulienda sawia na Uchaguzi wa katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo ,Baraza linafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 21 hadi 22 machi 2018.

  0 0

  RAIS wa chama cha Mpira wa Kikapu nchini Phares Magesa ametoa salamu za rambirambi kwa Mchezaji wa kikapu wa timu ya JKT Yvonne Christopher Wambura aliyefariki ghafla leo.

  Phares ametoa  salamu za pole kwa  uongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kuondokewa na mchezaji wa timu kwa Wazazi, Ndugu na jamaa wa marehemu Yvonne, Uongozi  JKTwa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa DSM (BD) , wanakikapu na wadau wote wa michezo kwa msiba huu wa ghafla. Mungu amleze Yvonne mahala pema peponi, Amina.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati akifungua na kuzindua mkutano wa Baraza hilo leo Mkoani Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga (Kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo Dkt.Leonard Chamuriho mkataba wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua na kuzindua mkutano wa Baraza hilo leo Mkoani Dodoma. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo Dkt.Leonard Chamuriho na Viongozi wengine wa Baraza hilo wakiimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa Ufunguzi na Uzinduzi wa Baraza hilo leo Mjini Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Mkoani Dodoma. Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) wakisIkiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.Joseph Nyamhanga (hayupo pichani) wakati akizindua na kufungua mkutano wa Baraza hilo Mkoani Dodoma. 

  Na Daudi Manongi,MAELEZO. 

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi ) mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo na watumishi wote kutimiza wajibu wao kwa kutumia muda wa kazi ipasavyo kwa kufanya kazi kwa bidii. 

  Ameyasema hayo leo wakati akizindua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi leo Mkoani Dodoma. 

  Aidha mhandisi Nyamhanga amesema kuwa Wizara (Sekta ya Uchukuzi) inatambua mchango mkubwa wa wafanyakazi wa ngazi zote katika kufikiwa kwa maamuzi mbalimbali ya kisera na kitaalam na hivyo kufanikisha shughuli za sekta hiyo hali inayochochea Sekta ya Uchukuzi na utabiri wa hali ya hewa kutoa Huduma zenya ubora wa hali ya juu ndani na nje ya nchi. 

  Akifafanua mhandisi Nyamhanga amesema kuwa sekta ya Uchukuzi na Tabiri za Hali ya hewa zinatakiwa kutoa huduma zenye ubora wa kiwango cha juu ndani na nje ya nchi. 

  “Dhana hii ya ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu sana kwa jumuiya yeyote na katika ngazi yeyote,hivyo niwashukuru sana kwa kuzingatia dhana hii muhimu na ninashauri muiendeleze” Alisisitiza Nyamhanga. 

  Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuzingatia maelekezo ya kisheria wakati wa kuchangia taarifa muhimu za sekta na kushirikiana katika utekelezaji wake ili kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kusisitiza kuwa Serikali haitosita kumwajibisha mtumishi yeyote ambaye ataonekana kuwa chanzo cha kutotimiza malengo ya bajeti na mpango kazi. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi la Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Uchukuzi) Dkt.Leonard Chamuriho amesema Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi kama walivyo watumishi wengine katika utumishi wa umma wamejipanga kuhakikisha wanafanya zao kwa weledi, uadilifu, juhudi na maarifa katika kutimiza wajibu wao ili kuchangia katika kutekeleza malengo ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo. 

  “Tunafahamu wazi kwamba kutokusimamiwa na kuendelezwa kwa miundombinu ya uchukuzi na huduma zake hakutowezesha sekta nyingine za kiuchumi na kijamii kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa,hivyo tutaendelea kuboresha miundombinu ya uchukuzi na huduma zake”,Aliongeza Dkt.Chamuriho. 

  Uzinduzi wa Baraza hilo ulienda sawia na Uchaguzi wa katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo ,Baraza linafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 21 hadi 22 machi 2018.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi wa kisima cha maji katika kata ya Kisukulu ikiwa shemu ya maadhimisho ya wiki ya maji katika Wilaya hiyo ambapo Kisima hicho kitaweza kusaidia wakazi wote wa kata hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,akikata utepe na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wa Kata ya Kisukulu wakati wa kuweka jiwe la smingi wa kisima kirefu cha maji cha kata ya Kisukuru.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa Kisima cha maji cha kata ya Kisukuru leo.
  Diwani wa kata ya Kisukuru, Joseph Kasaenda akitoa neno la Shukrani kwa mkuu wa Wilaya mara baada ya uzinduzi wa jiwe la msingi katika kata hiyo.
  Makada wawili wa Chama Cha Mapinduzi na CHADEMA, wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa jiwe la msingi la Kisima Cha Maji.
  baadahi ya wakazi wa Kisukulu waliofika katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa uzinduzi wa kisima cha maji.

  0 0

  Aliyesimama ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, akiongea na watumishi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, pamoja na watafiti hawapo pichani, alipotembelea kituo hicho, kulia ni Dkt Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, na kushoto ni Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo katika chuo cha mafunzo ya uvuvi FETA Kigoma, Bw. Simtie Ambakisye, Naibu Waziri Ulega alifanya ziara katika kituo cha TAFIRI Kigoma pamoja na kutembelea mialo ya Muyobozi na Kibiri.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifigo ya kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa kama Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza mazao hayo ya mifugo na uvuvi kutoka nje ya nchi.

  Naibu waziri Ulega aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa Samaki wa Muyobozi Uliyopo Wilayani Uvinza,Mwalo wa Kibirizi na kituo cha Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.

  “Sioni kwanini tuagize nyama na maziwa toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama, maziwa na hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za ndani katika mifugo na samaki na kuongeza pato la taifa? “Aliuliza Ulega.

  Ulega aliongeza kwa kusema kuwa Wizara yake haitawavumilia waafanyabiashara wanaoagiza nyama, maziwa na mazao ya samaki toka nje ya nchi kwani sekya ya mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.

  Tarkibani “tani elfu 20 za samaki zinaingizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka, samaki ambao wanafugwa katika maeneo mengine duniani, lakini sisi hapa nchini tunao katika mazingira ya asili.” Alisema

  Na hapa Mhe. Ulega aliitaka TAFIRI kuhakikisha wanawafikia wafugaji wa samaki kwa kufanya tafiti zao ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kujua namna ya kuzitatua, akitolea mfano wa chakula sahihi kinachotakiwa kupewa masamki wanaofugwa na kuangalia miundombinu ya kufugia. 

  Akizungumzia suala la zana za uvuvi katika ziwa Tanganyika alipokuwa akiongea na watafiti na watumishi wa TAFIRI, Ulega alisema “TAFIRI mfanye tafiti ya aina ya nyavu zinazotumiwa kwa kiasi kikubwa na wavuvi ili kuona kama zinafaa kuendelea kutumika, maana kumekuwa na malalamiko toka kwa wavuvi yanayopelekea kushuka kwa kiwango cha upatikanaji wa samaki na dagaa katika ziwa hili kutokana na matumizi ya nyavu hizo.” Alisema

  Sambamba na hilo Ulega alisema Wizara yake ina mpango wa kuimarisha eneo la tafiti kwa kuongeza rasilimali fedha kwa kukarabati miundombinu na kuongeza rasilimali watu.

  “Kila Mwaka TAFIRI itakuwa inafanya tafiti kuhusu mambo ambayo Wizara itakuwa imeyaelekeza ili kuondokana na suala la watafiti hawa kufanya kazi za watu wengine.” Alisema

  Akizungumzia swala la mafanikio ya soko la nyama la nje ya nchi, Ulega alisema, “Hatuwezi kusafirisha nyama nje ya nchi kama mkakati wetu wa chanjo ya mifugo hauko sawa, lazima tuwe na mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo, soko la kimataifa linaangalia sana swala hili, Sisi kama Wizara tunaenda kusema kuwa kwa yoyote anayetaka kufuga swala la chanjo ni lazima.” Alisisiza Ulega.

  Ulega aliendelea kusema kuwa ni lazima wizara kutengeneza mikakati ambayo itamfanya mfugaji asitaabike wazo wambalo amesema kama litaridhiwa litafanyiwa kazi.

  “kuna watu wanaona mifugo ni balaa, mifugo siyo balaa mifugo na neema.” Alisisitiza.

  Aidha Ulega alisisitiza suala la uwekezaji kwa ufugaji wa samaki kama njia ya kusaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uvuvi haramu wa samaki katika maeneo mbalimbali nchini, huku akipongeza jitihada za taasisi ya utafiti wa samaki TAFIRI kushirikiana na wananchi na kuonesha mfano wa namna ya ufugaji bora wa samaki unaowaonesha wafugaji wa samaki kuitumia ili kufikia malengo waliyokusudia.

  Naibu Waziri Ulega pia alisema Serikali imepanga kuongeza makusanyo katika sekta ya mifugo kutoka bilioni k na sita hadi bilioni hamsini baada ya kuifanya mifugo ya ndani kuwa bora na kuwa ya kiushindani katika soko la kimataifa, hivyo suala la chanjo litakuwa la lazima
  Kulia Dkt. Emmanuel Sweke Kaimu Mkurugenzi wa kituo wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega aliyekaa katikati wakiwa katika boat wakielekea kuangalia kizimba cha kufugia samaki katika maji ya ziwa Tanganyika, kushoto ni Afisa Mifugo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Noel Byamungu.
  Kushoto Dkt. Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma akimuonyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega katikati, kizimba cha kufugia samaki kilichopo katika maji ya ziwa Tanganyika hakipo pichani, alipotembelea kituo hicho mjini kigoma jana. Kulia ni Afisa Mifugo wa Mkoa Bw. Noel Byamungu.

  0 0


   Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu leo. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga.
   Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akikabidhi  cheti cha kuzaliwamara baada ya  kuzindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu leo. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. 

  Wafanyakazi wa Tigo wakiendelea kufanya usajil kwa wakazi wa Musoma baada ya  uzindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu . Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill.
  Kikundi cha burudani kiktumbuiza wakati wa uzinduzi wa   zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu . Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill.  

   Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na RITA na mara baada ya  uzinduzi wa  zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu . Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill.
  0 0


  Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Idara ya TTCL Pesa, Moses Alphonce mara baada ya makubaliano ya matumizi ya huduma za miamala ya makampuni hayo itakayowezesha mtumiaji kuingiza pesa moja kwa moja kwenye akaunti ya mtumiaji kwa gharama nafuu, hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo.

  Shirika kubwa zaidi la kitanzania la mawasiano ya simu, na watoa huduma ya simu zisizohamishika, broadband, bidhaa na huduma za internet wanaoongoza Tanzania pamoja kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania, Tigo. Leo wameingia katika ubia mkubwa, ambapo wateja kutoka katika taasisi hizi mbili wataweza kutuma na kupokea fedha kati ya mitandao hiyo miwili moja kwa moja katika akaunti zao.

  Akiongea wakati wa kutangaza ubia huo katika ukumbi wa Golden Jubilee Towers Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Huduma za Fedha kwa njia ya simu za mkononi wa TTCL, Moses Alphonce amesema kwamba, “Tunafuraha sana kutia sahihi makubaliano ya ushirikiano huu ambao unaenda kuwanufaisha wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla. Ujio wa TTCL PESA katika sekta hii ya mawasiliano ina lengo la kutengeneza ushirikishwaji wa masuluhisho ya kifedha kwa watanzania wote. Lengo letu ni kubadilisha mahitaji ya kila siku ya kifedha ya watu wetu yawe yasiyo ya fedha tasilimu na kuwa wawezeshaji wa miamala yote ya kidigitali inayofanyika Tanzania”.

  Aliongezea kuwa, tuna mifumo bora sana ambayo inaweza kutoa uwezo kwa makampuni na taasisi za kiserikali uwezo wa kutoa malipo ya kidigitali kwa mamilioni ya watanzania.

  TTCL PESA inatoa huduma ya kifedha ya kidigitali ambayo ni bei nafuu, ya haraka na salama ambayo inazidi huduma za benki kupitia simu za mkononi, huduma za malipo, kuongeza muda wa maongezi na uhamishaji wa fedha.

  Kwa upande wake, Afisa mkuu wa Huduma za kifedha za simu za mkononi wa Tigo, Hussein Sayed amesema kwamba makubaliano haya kuwa ni mwanzo wa ushirikiano mkubwa lakini pia jukumu la uanzilishi la Tigo katika huduma za fedha kupitia simu za mkononi, ushirikiano tayari umeshasainiwa. Jambo hili limeziakikishia kampuni hizi mbili zenye shauku ya kuwapatia wateja wao huduma ya kiwango cha juu katika zama hizi za huduma za kifedha za kidigitali. 
   
  “Kwa makubaliano haya kwa mara nyingine tena tunaisaidia Tanzania kuimarisha jukumu lake lisiliokwepeka katika waanzailishi wa ushirikishwaji wa kifedha kwa njia za kidigitali duniani. Ushirikiano mara zote huwa ni chachu ya ukuaji katika sekta ya fedha kwa njia za simu za mkononi.” Alisema Sayed.

  “Tumetambulisha sokoni idadi kadhaa ya bidhaa zenye ubunifu na tuna nia ya kupanua watumiaji wetu kwa kushirikiana na watoa huduma wenzetu walioko sokoni” Aliongeza Hussein.

  Katika mwezi June 2014, Tigo iliibuka kuwa ya kwanza baada ya kufanikiwa kuzindua makubaliano ya ushirikiano ya kwanza ya aina yake ambayo yanawawezesha mamilioni ya wateja wa Tigo Pesa kutuma fedha na kupokea fedha kwa watoa huduma wengine waliosajiliwa.

  0 0

   Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda jana machi 21/2018 ametembelea eneo la Chuo cha Kilimo MATI mkoani Mtwara ili kujionea uvamizi uliofanywa na baadhi ya wananchi kwenye eneo la chuo ambapo wavamizi wamefyeka na kupanda mazao ya kudumu kuashiria kujitwalia isivyo halali maeneo hayo.

  Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mtwara wakati walipokagua eneo la chuo cha Mati Mtwara lililovamiwa na wananchi.
  Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akimsikiliza Mmoja wa wazee majirani walioshuhudia wakati serikali ikitwaa eneo hilo la hekta 560 na kuwalipa fidia wenyeji mwaka 1974 wakati akiongea na kamati
  Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akizungumza baadhi ya wajumbe wakati wa ukaguzi wa eneo hilo la hekta 560 ambalolimevamiwa na wananchi.

  Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mtwara Bw. Evod Mmanda akizungumza baada ya kukagua eneo hilo la hekta 560 ambalo serikali ililitwaa na kuwalipa fidia wenyeji mwaka 1974.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini mkataba wa Makubaliano ya kulifanya Bara la Afrika kuwa eneo huru la Biashara, kwaniaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 21, 2018, jijini Kigali, Rwanda. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.
  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.

  Majaliwa aliyasema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini Kigali ambapo alisema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali , Waziri Mkuu alisema Tanzania itahakikisha mkataba huo unatelekezwa bila kuathiri huduma zinazozalishwa ndani.Alisema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu ambayo imesainiwa inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.

  Mikataba iliyosaioniwa na mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara la Afrika kuwa eneo huru la biashara, Itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanyakazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.

  Azimio la tatu ni Azimio la Kigali ambalo limejumuisha mawazo ya uanzishwaji wa mchakato huo.“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa kutilia maanani suala hili hadi kufikia hatua hii ya kusaini mkataba.

  “Tanzania kama wadau wakuu wa mkataba huu tunakwenda kujipanga kuhakikisha mkataba huu unatekelezwa bila kusababisha vikwazo vyovyote.
  “Hata hivyo tunakwenda kupeleka baadhi ya masuala haya katika vikao vya Baraza la mawaziri ili kuangalia sheria zetu zisije kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkataba huu.

  “Kwa mfano Tanzania tunayo sera ya viwanda, lazima tuangalie ili tusije kuruhusu bidhaa kuingia nchini mwetu na kuathiri biashara na bidhaa zetu za ndani.Vile vile katika uhuru wa biashara ya anga ambapo Tanzania bado tuna ndege chache ili tusije kuruhusu kiholela, l;azima tuwe waangalifu katika hilo.“Aidha Tanzania tumeruhusu maeneo ya kuzalisha bidhaa, kwa hiyo lazima tuwe makini ili tusije kuruhusu na kuharibu mwenendo wa kiuchumi.

  Awali akihutubia katika ufunguzi wa sherehe hizo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyataja maeneo makuu ambayo mkataba huo umeangazia kuwa ni pamoja na eneo huru la biashara ya anga, miundombinu ya reli na barabara ambayo itaziunganisha nchi za Afrika kuwasiliana kwa urahisi.

  Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), alisema mkataba huo unatoa nafasi maalum ya Ukanda wa Afrika kujali utu, kumnufaisha mkulima, mfanyabiashara na wabia wengine wa maendeleo kuja kutafuta fursa Afrika.

  “Azimio hili linatoa nafasi kununu na kuuza bidhaa sambamba na kupata wabia duniani kote, biashara huru itatuweka pamoja na muafaka wa Afrika tutakayo” alisema Rais Kagame.Mkataba huo ulisainiwa jana baada ya vikao vya maadalizi vilivyohusisha timu za wataalam na mawaziri wa biashara na mambo ya nje ya nchi zinazounda Umoja huo.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 wanachama wa AU ambao walisaini mkataba huo.

  0 0

  Aipongeza Taasisi ya Uongozi kuwaandaa watumishi wa Serikali kuwa uongozi wazuri

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amewataka Jeshi la Polisi kuwa mstari wa mbele katika kukomesha vitendo vya rushwa huku akisisitiza kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya utawala bora.

  Mkuchika ametoa kauli hiyo jana jioni jijini Dar es Salaam kwa maofisa wa Jeshi la Polisi 32 kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).

  Mafahali hayo ni ya kwanza kutolewa na taasisi hiyo ambayo wameshirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland na hivyo kufanya mafunzo hayo kutambulika na kukubalika kimataifa kuhusu masuala ya uongozi.

  Hivyo akizungumza na maofisa hao pamoja na wageni wengine waalikwa ,Mkuchika amewapongeza wahitimu hao lakini awakata kuwa mstari wa mbele wao pamoja na jeshi la polisi kwa ujumla wake kupambana na komesha rushwa.

  Amesema katika mataifa mbalimbali maeneo ambayo rushwa inaangaliwa sana ni katika Mahakama na Polisi .Hivyo ni vema polisi nchini wakawa mstari wa mbele kukomesha rushwa.

  "Mataifa mengi yanapimwa katika mambo ya kupambana na rushwa pamoja na kuangalia maeneo mengine pia wanaangalia na Jeshi la Polisi.Na kwa bahati mbaya kwenye nchi nyingi baadhi ya polisi wamekuwa wakituhimiwa kujihusisha na rushwa, hivyo ni vema waliopata mafunzo hayo ya uongozi wakawa mabalozi wa kukemea rushwa nchini,"amesema Mkuchika.

  Amefafnua wizara anayaoingoza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), ipo chini yake na ndio maana amezungumzia suala la kupambana na rushwa na kueleza hata akipata mualiko kwenye sherehe za harusi bado atazungumzia umuhimu wa kukomeshwa rushwa nchini kwani ni adui wa haki.

  Amewataka Polisi nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuheshimu misingi ya utawala wa bora na kusisitiza kuwa taaswira ya nchi wakati mwingine inapimwa kwa kulitazama jeshi hilo.Hivyo waliopata mafunzo hayo ya uongozi watakuwa washauri wazuri kwa maofisa wengine wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yao na mafunzo hayo yawe chache katika maeneo ya kazi.

  Mkuchika amesema anatambua gharama ya mafunzo hayo, hivyo wahitimu wajue wanalo deni kubwa la kuwatumikia Watanzania na kuthibitisha kwa vitendo wameiva kwenye mafunzo ya uongozi ambayo yamewajenga katika kutoa maamuzi ya kimakakati.Kuhusu Taasisi ya Uongozi, Mkuchicha amesema anatambua kazi kubwai inayofanywa na taasisi hiyo chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu wake Profesa Joseph Semboja ya kupika na kuandaa watumishi wa umma katika masuala ya uongozi nchini.

  "Kutokana na umuhimu wenu ndani ya nchi yetu, nilikuwa Dodoma na nilichofanya ni kuwaombea bajeti kwa ajili ya kuendesha shughuli zenu.Niwaambie bajeti ile imepitishwa.Serikali tunatambua mchango wenu katika kuandaa watumishi kuwa viongozi wazuri."Nikiri wapo ambao wamezaliwa na kipaji cha uongozi lakini ukweli uko palepale tafiti zinaonesha uongozi unasomewa na kujifunza kutoka kwa wengine kupitia vitabu, majarida na kukaa darasani,"amesema Mkuchika.

  Amewapongeza wahitimu hao pamoja na wale ambao wamejiunga katika taasisi hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo yanatarajia kuanza hivi karibuni na miongoni mwa waliomba mafunzo hayo yupo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

  Kwa upande Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema mahafali hayo ni kwanza kwa Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi ambayo taasisi hiyo wameianzisha.Stashahada ya Uzamili ya Uongozi ni programu ya mafunzo ya utawala yanaendeshwa na taasisi hiyo pamoja na Chuo Kikuu cha Kifini cha Aalto cha Mafunzo ya utawala.

  Programu hiyo inalenga hasa kutoa mbinu na nyenzo za uongozi kwa viongozi wa Serikali wa ngazi za juu,nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla ili kufikia maendeleo endelevu.Stashahada hiyo ina moduli 10 na ni ya kipindi cha mwaka mmoja.Kundi la kwanza la washiriki wa Stashahada hiyo wamehitimu jana na walianza mafunzo Aprili mwaka 2017.

  Ambapo Profesa Semboja amefafanua mafunzo hayo yanajenga uwezo wa kiongozi katika kusimamia masuala mbalimbali na hasa kufikiri kimkakati na kutenda na kuamua kwa njia iliyosahihi."Mafunzo ya Stashahada ya Uzamili inatoa nafasi ya kumuandaa mhitimu na kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza na kuandaa viongozu wenye uwezo wa kufikiria vema.

  " Pia mhitimu wa mafunzo haya anaweza kujiendelea kielimu katika Chuo cha Aalto ambacho ni moja chuo kikubwa nchini Finland,"amesema Profesa Semboja.Amesema changamoto kubwa ya Staahahada ya Uzamili ya uongozi ni gharana kubwa na kufafanua wahitimu wapatao 32 wamehitimu na anaamini watatoa mchango mkubwa katika maeneo yao ya kazi.

  Profesa Semboja amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwa uamuzi wake wa kuomba kujiunga na taasisi hiyo ili naye apate mafunzo hayo ya Uongozi.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na ujumbe kutoka nchini Israel uliokuwa ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman wa kwanza (kushoto kwake) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wa nne kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florence Turuka wa kwanza kushoto aliyesimama mstari wa nyuma pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wa sita kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florence Turuka wa pili kutoka kushoto pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi mara baada ya kumalizika kwa kikao chao na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 1545 | 1546 | (Page 1547) | 1548 | 1549 | .... | 1903 | newer