Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1544 | 1545 | (Page 1546) | 1547 | 1548 | .... | 1903 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa yasiyo ambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.

  Aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Machi 19, 2018) wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)

  Alisema magonjwa yasiyo ambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakatoa mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.Waziri Mkuu alisema magonjwa hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.

  “Magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”

  Waziri Mkuu alisema magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo kwa katika baadhi ya nchi.

  Pia, Waziri Mkuu aliongeza kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya nchi zote zikiwemo zilizoendelea na zinazoendelea, hivyo changamoto zote zinazoikabili zinapaswa zipewe kipaumbele katika utatuzi.Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya Afya na kuyapatia ufumbuzi.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ambazo ni Tanzania, Malawi, Lethoto, Uganda, Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Muwakilishi kutoka nchini Mauritious.Pia Katibu wa jumuiya hiyo Profesa Yoswa Dambisya, Muwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Paolo Belli pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi hizo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 20, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya wa Uganda .Sarah Opendi ,wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) kushoto ni Wazri wa Afya wa Malawi Atupele Muluzi,Waziri Mkuu amefungua mkutano huo jana March 19, 2018 Jijini Dar es salaam.
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba. Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

  Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi. Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.

  Kwa Upende wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi kufanya kazi kwa taratibu na sheria lakini pia alitoa wasihi kwa wanasiasa wanaochochea vurugu kwani wao watachukuliwa kama wahalifu na si wanasiasa. Ziara ya Makamu wa Rais imekamilika leo ambapo pia alitembelea Hospitali ya Abdala Mzee ambapo alijionea vifaa vya kisasa vilivyowekwa na huduma bora zinazotolewa.

  Makamu wa Rais pia aliweka mawe ya Msingi katika ujenzi wa madarasa katika skuli ya sekondari ya Ali Khamis Camp pamoja na ujenzi wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Ole. 

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Hafidh Jabir Ali mwenye umri wa miaka 3 aliyelazwa kutokana na kuungua na chai katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Rayna Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja aliyelazwa kutokana na kuungua moto katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Wuxiao Shu juu ya matibabu ya mguu wa mtoto AzarAli mwenye umri wa miaka aliyelazwa  katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi nje ya majengo ya hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya hospitali hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.

  Pia limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani Kasulu.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo kuwa Machi 19 mwaka huu, tano usiku kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.
  Amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata.
  "Baada ya kuhojiwa na polisi waliwataka wenzao na kufanikiwa kuwakamata wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio mauaji, na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

  "Hata hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu,"amesema.Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.

  Amesema hali hiyo ilisababisha askari kulala chini na watuhumiwa hao ambapo watu hao watuhumiwa hao wa ujambazi walifariki dunia. Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo watanza msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.

  Wakati huohuo Solomoni Ntihazo kwa kosa la kukutwa na pembe za ndovu vipande tisa ambapo vipande viwili ni vikubwa na vipande saba ni vidogo.


  0 0  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  Watu wawili wamEfariki wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufutia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

  Kamanda wa Jeshi la polisi Martini Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

  Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

  Kamanda Otieno aliongeza kuwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

  Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

   Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika ku
   Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

  .

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
  kuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akihutubia mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipokea mifuko ya saruji zaidi ya elfu sita kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Tanga Cement Bw.  Lawrence  Masha jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.

  Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es salaam. Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert " alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure. Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.

  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa takriban watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016. Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

  Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.


  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome Bi. Upendo Jeremiah.
  Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimueleza jambo Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akisisitiza jambo kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati
  Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah akizungumza katika ziara hiyo kulia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi 
  Sehemu ya jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo ujenzi wake unaendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akitoka kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akisalimiana na mmoja wa wakina mama wanaofanya kazi kwenye ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akitembelea maeneo mbalimbali mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Halmashauri hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Seif Ally katikati ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)akisalimiana na wakazi wa Mji huo kabla ya kuvuka kivuko kuelekea upande wa pili wilayani Pangani akiwa kwenye ziara yake
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiingia kwenye kivuko cha kuvuka mto Pangani kuelelea ng'ambo ya pili ya mji wa Pangani wakati wa ziara yake
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)wa pili kushoto akifurahia jambo na mmoja wa wananchi wakati akiwa kwenye kivuko cha Mto Pangani kuelelea ng'ambo ya pili ya mji wa Pangani kwa ajili ya kufanya ziara kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akishuka kwenye kivuko kuelekea ng'ambo ya pili ya mto Pangani kuendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatakuwa tayari kuona fedha za miradi ya maendeleo zinatumika vibaya huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sabasi Chambasi kuwa makini nayo.

  Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali kujengwa chini ya kiwango jambo ambalo linasababishwa na kutokuwa makini kwa viongozi wanaoisimamia. 

  Aweso aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo limegharimu kiasi cha milioni 600 linalosimamiwa mkandarasi Kisyeri Chambiri kutoka kampuni ya Wesers Limited.

  Alisema mradi huo una umuhimu mkubwa sana kwa wilaya hiyo hivyo lazima watumishi wakiwemo wale ambao wanasimamia suala hilo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza suala hilo.

  “Mkandarasi huu mradi ni muhimu sana kwa Halmashauri yetu hivyo sitopenda kuona unajengwa chini ya kiwango lakini pia hakikisheni unakamilika kwa wakati kwa lengo la kufanya kazi “Alisema.

  Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alimuagiza mkurugenzi huyo kuweka umakini mkubwa kwenye ujenzi huo ili kuepukana na utekekelezaji wake kuwa chini ya kiwango kutokana na kutumia fedha nyingi.

  Hata hivyo alimwambia Mkurugenzi huyo wa Pangani kuhakikisha anamsimamia vizuri mhandisi mshauri wa mradi huo ambae ni mwajiriwa wa Halmashauri hiyo ili ukamilike kwa wakati na kuondoa adha kwa watumishi ya kutokua na Halmashauri yenye ubora.

  “Si kitu cha busara kuona mhandisi mshauri ambae ni mtu muhimu katika mradi huo kutokuonekana, Mkurugenzi ninamashaka na mradi huu kama kweli utakamilika kwa muda uliopamnga ambapo ni mwezi Juni mwaka huu”Alisema.

  Hata hivyo aliwatahadharisha viongozi wa Halmashauru kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali ambazo zinatolewa na Serikali au wadau mbalimbali wa maendeleo kwani bila kufanya hivyo wanaweza kuzorotesha maendeleo (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MWENYEKITI wa Chama cha APPT-Maendeleo Peter Kuga Mziray amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rabincia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

  Mwanasiasa huyo mkongwe amefariki jana saa nne asubuhi wakati akiendelewa kupatiwa matibabu ambako alilazwa hapo kwa muda wa wiki mbili kabla ya umauti kumfika.

  Akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kifo cha Mziray,Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda amesema baraza hilo limeshutushwa na kifo cha mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kupogania maslahi ya watanzania na Taifa.

  Shibuda amesema kwa mujibu wa taarifa za kaka wa marehemu Mziray ni kwamba msiba upo maeneo ya Faya nyuma ya kituo cha Mafuta ambako kuna nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)zilizopo eneo hilo.

  Amesema ameelezwa taratibu za kuupumzisha mwili wa marehemu Mziray zitafahamika baada ya mkewe ambaye yupo nchini Japan kuwasili nchini."Taarifa ambazo ninazo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa kutoka kwa ndugu wa marehemu Mziray zinasema mkewe anaweza kuingia nchini kati ya siku mbili hizi.

  " Akifika ndio watajua wanazika lini na huenda mwili ukaaga Jumamosi.Hata hivyo tutajua zaidi baada mkewe kuwasili nchini."Tumejulishwa mazishi ya marehemu Mziray yatafanyika katika kijiji cha Kihurio wilayani Same mkoani Kilimanjaro," amesema.

  Akimzungumzia Mziray wakati wa uhai wake,Shibuda amesema baraza hilo na siasa za Tanzania kwa ujumla zimempoteza kiongozi muhimu ambaye mchango ulikuwa bado unahitajika."Ni pigo kubwa kuondokewa na mwanasiasa ambaye alikuwa anaipenda nchi na siku zote alisisimamia masuala yenye tija kwa nchi yetu.

  " Alikuwa na masikio sikivu katika kusikiliza ushauri na kubwa zaidi siasa zilijikita katika kuunganisha Taifa.Ni mwanasiasa ambaye hakuwa anaamua mambo kishabiki bali aliamua kwa kuangalia maslahi ya nchi kwanza,"amesema Shibuda.

  Amefafanua nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini ambayo anaitumikia hivi sasa aliichukua kutoka kwa Mziray baada ya kumalizima muda wake wa kuliongoza baraza hilo.

  Hivyo amesema akiwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kuna mambo mengi mazuri aliyayofanya kwa maslahi ya vyama vya siasa,"amesema.

  Shibuda amesema kwa niaba ya Baraza la vyama vya siasa anatoa pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki,wanasiasa wote na watanzania kwa ujumla na Mungu ailaze mahali pema popeni roho ya marehemu Mziray.

  0 0  0 0
  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Milama, iliyopo mkoani Morogoro baada ya kukabidhi mbegu bora ya mahindi ya Wema 2109 kwa ajili ya shamba darasa. Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani humo leo.
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli (katikati) mbegu ya Wema 2109 kwa ajili ya kuwakabidhi wakulima wa wilaya yake ili waanzishe mashamba darasa. Wengine kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mvomero, Hilali Focus Riddy, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mvomero, Daina Muywanga na kulia ni Mtifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Mvomero wakiandaa shamba kwa ajili ya kupanda mbegu ya Wema katika shamba darasa.
  Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
  Uzinduzi ukiendelea.
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
  Wanafunzi wa shule hiyo wakikabidhiwa mbegu hiyo ya Wema.
  Mkulima Yacob Patrick, akikabidhiwa mbegu hiyo.
  Mkulima Mohamed Maungo, akikabidhiwa mbegu.
  Mkulima Tatu Mbonde, akikabidhiwa mbegu.
  Walimu wa Shule ya Msingi Mvomero wakikabidhiwa mbegu.
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero.
  Mtifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu ambao ndio waliofanya utafiti wa mbegu hiyo, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
  Uzinduzi wa shamba darasa katika shule ya msingi Mvomero.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero wakiwa katika upandaji wa mbegu hizo.
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli akizindua shamba darasa kwa kupanda mbegu hiyo ya Wema 2109
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utalli, akizungumza na wakulima wanaounda kikundi cha Tupendane kilichopo Kijiji cha Didamba.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Kijiji cha Didamba, Mwanahamisi Omari (kushoto), akikabidhiwa mbegu.
  Mkulima Maulid Adamu kutoka Kikundi cha Kazibanza kilichopo Kijiji cha Milama akikabidhiwa mbegu.


  Na Dotto Mwaibale, Mvomero-Morogoro.

  WANAFUNZI wa Shule ya Msingi ya Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi ili waweze kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti.

  Mwito huo umetolewa wilayani humo leo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi ya Wema E2109 inayostahimili ukame iliyotolewa na COSTECH kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

  "Ninyi wanafunzi nawaomba someni sana masomo ya sayansi ili hapo baadae muweze kuwa watafiti wa masuala mbalimbali jambo litakalosaidia taifa" alisema Hussein.Alisema tafiti zozote zinafanywa na wataalamu waliobobea katika masomo sayansi hivyo aliwataka wanafunzi hao kujifunza kwa bidii masomo hayo ya sayansi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mohamed Utalli aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kupeleka mradi huo katika wilaya yake ambapo amewataka wananchi kuzichangamkia mbegu hizo.

  "Tuna bahati sana katika mkoa wetu kwani katika mikoa tisa ambayo mradi huo utafanyika na sisi tupo hivyo ni fursa kwetu tusiiache ikapotea bure" alisema Utalli.Utalli aliwataka wakulima wilayani humo ulimopita mradira huo kuhakikisha wanayatunza mashamba hayo ili kuleta tija katika zao la mahindi.

  Alisema mradi huo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kufanya kazi kwa bidii wakati taifa likiingia katika uchumi wa kati wa viwanda.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

  Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

  Mtifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

  Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.

  0 0

  Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wa pili kulia) akiongea na jumla ya Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa kwanza kushoto ni Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kulia ni Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha.
  Baadhi ya Mahakimu wapya wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi
  Wakiendelea kumsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi
  Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (Katikati), Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania (aliyeketi kushoto) na Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni.(Picha na Mary Gwera, Mahakama


  Na Mary Gwera, Mahakama

  MAHAKIMU wapya wanaotarajia kuanza kazi rasmi ndani ya Mhimili wa Mahakama wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Mhimili huo.

  Akizungumza na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni katika Ukumbi wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam mapema Machi 20, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali amewaasa Waajiriwa hao kufanya kazi kwa maadili na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

  “Katika ufanyaji kazi wenu wa Uhakimu, mnatakiwa kuzingatia mambo makuu manne ya msingi ni; Ujuzi wa taratibu na mazoea ya Kimahakama, Uelewa kuhusu Sheria za Msingi ‘Substantive law’ na Sheria za Mwenendo ‘Procedural Law’ kuangalia mazingira ya utoaji haki na kadhalika,” alieleza Mhe. Wambali.

  Aidha Jaji Kiongozi pia aliwataka Mahakimu hao pia kufanya kazi kwa kuwaheshimu Wadau wote wanaojumuika nao katika mchakato mzima wa utoaji wa haki, ikiwa ni pamoja na Makarani, Wazee na Baraza na wengineo.

  “Heshimuni kila mtu mnayeingia naye Mahakamani, kila mtu ana mchango katika upatikanaji wa haki, na moja ya sifa ya Hakimu ni upole lakini upole sio udhaifu,” alisisitiza Mhe. Jaji Wambali.Mbali na kuwaasa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, Mhe. Jaji Kiongozi aliwaasa pia Mahakimu hao kutojihusisha na masuala ya siasa katika kazi zao.

  “Ibara ya 113A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema, Hakuna Jaji au Hakimu anayeruhusiwa kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha Siasa” alisisitiza Mhe. Jaji Kiongozi.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo amesema kuwa jumla ya Mahakimu wapya 78 kati ya 100 wameripoti kazini.

  “Jumla ya Mahakama wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo wameripoti, hata hivyo baadhi wametoa taarifa ya kushindwa kuripoti kutokana na dharura mbalimbali,” alisema Mkurugenzi huyo.Bw. Nkembo ameeleza kuwa baadhi ya Mahakimu na Watumishi wa Kada watakaoshindwa kuripoti ndani ya siku 14 tangu Machi 20, nafasi zao zitatafutiwa watu wengine watakaoomba na kukidhi vigezo.

  Mahakimu hao na Watumishi wengine wa Kada mbalimbali walioajiriwa na Mahakama hivi karibuni watasambazwa katika Mahakama mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuongeza nguvu kazi katika kuendelea kuboresha huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  SERIKALI ya kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mpango wa taifa wa kuboresha huduma upasuaji ambayo kila mtu anaweza kumudu kufikia 2025. 

  Akizungumza wakati wa uzinduaji wa mpango huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa mpango huo umekuja wakati mwafaka kutokana na sera ya afya miaka mitano kuisha hivyo mpango huo kuingia katika sera ya miaka mitano. 

  Dk.Mpoki amesema kuwa mpango huo uko katika muda mwafaka kutokana na hatua mbalimbali za uboreshaji afya kwa wananchi katika upatikaji wa huduma za upasuaji hali ambayo itaokoa maisha pamoja na kuongeza uzalishaji. 

  “Upasuaji salama ni ishara ya kila mtanzania anaweza kupata huduma za afya na kuongeza uzalishaji ,kuboresha huduma za upasuaji bora pamoja na dawa za usingizi ni muendelezo wa kuboresha afya ya uzazi kwa nchi nzima” amesema Dk.Mpoki. 

  Amesema Tanzania ni nchi ya tatu duniani ambayo imejizatiti katika utoaji wa huduma za upasuaji endelevu na kuingiza katika mpango wa taifa wa upasuaji pamoja watalaam wa dawa za usingizi. Amesema kuwa serikali itasomesha madakitari pamoja na wataalam wa dawa usingizi ili kuweza katoa huduma bora za upasuaji kwa kiwango kikubwa kulingana na wahitaji wa upasuaji. 

  Aidha amesema mpango utakuwa na tija kutokana na wizara ilivyojipanga katika kushughulikia changmoto za afya kwa wananchi katika kuweza kutoa huduma bora za afya katika pande zote. Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi amesema kwa moja ya jarida linaonyesha Tanzania kiwango cha upasuaji kidogo katika mpango uliozinduliwa kiwango hicho kitapanda. 

  Dk.Maongezi amesema kuwa watu wanapata matatizo katika upasuaji hivyo mpango wa taifa utakuwa suluhisho kutokana kusomesha wataalam wa upasuaji pamoja na wataalam wa dawa za usingizi. Amesema kila mtu akifanya katika nafasi yake tutaokoa wanawake kupata uzazi salama katika upasuaji kwa hospitali zote zilizopo nchini. 

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese amesema Tanzania imejipanga katika utaoaji wa huduma ya upasuaji kwa kuingiza katika mpango wa taifa. Amesema kuwa viongozi wa Tanzania wako imara katika kuboresha huduma za afya ikilinganishwa na nchi nyingine.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa taifa wa huduma ya upasuaji, jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese akizungumza kuhusiana na Tanzania kupokea mpango wa upasuaji na kuingiza katika mpango wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi akizungumza hali ya upasuaji nchini, jijini Dar es Salaam.
  Sehemu wataalam wa afya wa nchi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa afya unaofanyika nchini.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kushoto) akizindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akionesha nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri huo na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimkabidhi mkazi wa Manispaa ya Musoma cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri wa chini ya miaka mitano, mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA), Bi. Emmy Hudson akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa salama za Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Wasanii wa Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Wagoyangi kutoka Maswa mkoani Simiyu wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mikoa ya Simiyu na Mara mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wasajili wa vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwenye mikoa ya Simiyu na Mara, kufanya kazi hiyo kwa umakini na uzalendo mkubwa katika kuhakikisha wanawasajili watoto wenye sifa.

  Waziri Kabudi ametoa rai hiyo Machi 20 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, katika mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

  “Mikoa ya Mara na Simiyu ina muingiliano mkubwa sana na wananchi wa nchi jirani hivyo wasajili wawe makini na watangulize uzalendo wakati wa kutekeleza mpango huu, tusisajili mtoto ambaye hahusiki na pale ambapo tuna mashaka kuwa mtoto huyo anaweza kuwa wa nchi za jirani, tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili hatua za kiusalama zichukuliwe” alisema Profesa Kabudi.

  Amesema kuwa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano unafanyika bila malipo hivyo wasajili wasitumie kwa namna yoyote mpango huo kama fursa ya kujipatia fedha kwa udanganyifu.Aidha, Waziri Kabudi ameahidi kutoa tuzo maalum kwa mkoa (kati ya Simiyu na Mara) utakaofikia asilimia 80 ya lengo la usajili kwa kipindi cha miezi miwili tangu usajili ulipoanza na wakati huo huo akawataka Viongozi wa Taasisi zote Umma kuvitambua vyeti vitakavyotolewa chini ya mpango huo kwa kuwa ni vyeti halali

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA) Profe. Hamis Dihenga amesema kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, RITA inakusudia kusajili jumla ya watoto 735, 545 katika mikoa ya Simiyu na Mara kwenye vituo 463 (Mara) na Vituo 324 (Simiyu).

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Adam Malima amesema hadi sasa Mkoa huo umesajili jumla ya watoto 78, 625 na watahakikisha watoto wote wanaopaswa kusajiliwa wanasajiliwa ndani ya miezi miwili na baadaye kuendelea na usajili kwa watoto watakaozaliwa.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga, akitoa salamu za Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesisitiza wananchi kutambua umuhimu wa kuwasajili watoto wao ili waweze kutambulika, kupewa vyeti vya kuzaliwa na Serikali iweze kupata takwimu sahihi.

  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Watoto (UNICEF) hapa nchini ambao ni miongoni mwa wafadhili wa mpango huu, Bi. Maud Droogleever , amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

  Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Simiyu na Mara walioshirikia katika Uzinduzi wa Mpango huo wameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huo kwa kuwa umewarahisishia huduma ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa kuwasogezea huduma hiyo katika Ofisi za kata tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya

  0 0

  MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.

  Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  Thadeus alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.

  “Maafisa Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.

  Aidha, alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.

  Akifafanua zaidi alisema Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika maeneo yao ya kazi, hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao wa kazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja mbalimbali zinazoulizwa na kujitolea majibu kwa wakati.

  Aliongeza kuwa matumizi ya tovuti ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo wa utoaji wa habari na taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili kuhakikisha kunakuwepo na daraja la mawasiliano baina ya Serikali na wananchi katika kupata suluhu ya masuala mbalimbali ikiwemo migogoro inayotokea mara kwa mara.

  Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima alisema uboreshaji wa tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dhana halisi ya utawala bora hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zinazozingatia muda na mahitaji yaliyopo.

  Aliongeza ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa na Serikali yao katika kuwapatia huduma mbalimbali.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
  Mwezeshaji na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah akiwasilisha mada kuhusu mtindo wa uandishi wa habari katika tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
  Afisa Tehama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred Chali akichangia hoja wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  0 0

   Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani katika shule za Msingi Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa uboreshaji wa usalama barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili wa Mfuko wakampuni ya Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti,  walimu na maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani.
   Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi msaada wa jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha miaka miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani na shule hiyo.
   Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akishirikiana na wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba nyimbo zenye mafunzo ya usalama barabarani.

  Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti akizungumza kwenye hafla hiyo.

   Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti,  walimu  na wanafunzi  wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
   Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti,  na maofisa wa shirika la Amend,  Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani, walimu  wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
  Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akigagua miundombinu ya usalama barabarani iliyojengwa kupitia mpango huo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Bw Philippe Corsaletti

  0 0  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  WATU saba wamefariki dunia kwenye ajali ya gari aina ya Scania katika kijiji cha Mkongoro barabara ya kutokea Manyovu wilayani Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma .

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Maltini Otieno, amesema Machi 21 mwaka huu, saa tatu asubuhi huko katika Mlima wa Kasagamba gari hiyo yenye T741AAB ilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la SIRI Hamis (43 na utingo wake) Ramadhani Saidi (23).

  Mbali ya hao pia walikuwa wamebeba watu wanne na mizigo.Watu hao majina yao hajafahamika.Amesema ajali hiyo pia ilisababisha kifo cha mwanafunzi Eliakimu Muha (15 )aliyekuwa akitembea kwa miguu.

  Aidha Kamanda Otieno amewaambia madereva kuzingatia sheria za barabarani na kuhakikisha gari za mizigo hazibebi abiria.

  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Mosi (MoCU) Prof ,Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi wa Chuo hicho pamoja na Wategemezi wao, zoezi ambalo linafanyika katika kituo cha Afya kilichopo chuoni hapo . 
  Baadhi ya Wauguzi wanaohudumu katika kituo hicho fcha Afya pamoja na Watumishi wa Chuo hicho wakifuatilia hotupa ya Uzinduzi wa zoezi la Upimaji wa Homa ya Ini iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Eustace Ng'weshemi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa Homa ya Ini katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi .
  Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi ,wakiwa katika uzinduzi huo.
  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) Dkt , Eustace Ngw'eshemi akimuonesha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi ,Prof Faustine Bee namba ya siri itakayotumika wakati wa kupokea majibu baada ya zoezi la upimaji kukamilika.
  Mkuu wa kitengo cha Maabara katika Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika (MOCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Prof Faustine Bee alipoongoza zoezi la upimaji wa Homa ya Ini kwa watumishi wa chuo hicho.
  Mkuu wa Kitengo cha Maabara katika kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Mmmoja wa watusmihi katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Julieti Bee wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa Homa ya Ini chuoni hapo.
  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) Dkt , Eustace Ngw'eshemi akizungumza na mmoja wa watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kabla ya kumfanyia vipimo.


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

  CHUO kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) kimezundua zoezi la upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi ,Wategemezi wao pamoja na majirani wa cuo hicho ikiwa ni njia ya tahadhari licha ya kutokuwepo ushahidi wa mlipuko wa ugonjwa huo nchini. 

  Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa watumishi wake kwani afya bora ni rasilimali muhimu kwa maendeleo na maenedeleo ya Taifa yataletwa na wananchi pamoja na watumishi wenye Afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali na kutoa huduma stahiki kwa umma wa Tanzania. 

  Katika kuzingatia sera na miongozo ya Afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka 2007 ,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) kama mdau imeanza kutoa huduma ya upimaji wa Ini kupitia Kituo chake cha Afya kilichopo chuoni hapo. 

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Prof Faustine Bee akatumia zinduzi huo kutoa wito kwa watu wengine waishio nje ya mazingira ya Chuo hicho kutumia kituo hicho pindi wanapohitaji huduma za matibabu. 

  Zaidi ya watumishi 456 wanashiriki katika zoezi la Upimaji wa Ini chuoni hapo huku Menejimenti ikiwa katika mazungumzo na Hospitali ya Rufaa ya KCMC ukiona uwezekano wa Wagonjwa wanaohitaji rufaa kwenda moja kwa moja KCMC badala ya kupitia Hosptali ya Mkoa ya Mawenzi kama ilivyo sasa.

older | 1 | .... | 1544 | 1545 | (Page 1546) | 1547 | 1548 | .... | 1903 | newer