Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU ALIPOZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO JUMATATU MACHI 19,2018 KWENYE HOTEL YA SEASCAPE.

$
0
0
UTEKELEZAJI WA TFF KATIKA MAENEO MBALIMBALI

Ndugu Waandishi wa Habari,Sekretarieti ya TFF, Watanzania wote wanaotuangalia na kutusikiliza,mabibi na mabwana habari za asubuhi.
 Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa siku ya leo tukiwa wazima wa Afya,Lakini pia nichukuwe nafasi hii kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.Joseph Pombe Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ninaoupata katika uendeshaji wa mpira wa miguu, nimekuwa karibu sana na Serikali kuhakikisha juhudi zetu za kuendeleza mpira zinafanikiwa kwa kasi kubwa sana na mafanikio ya ujio wa Rais wa FIFA ni kielelezo cha karibuni kuonyesha ushirikiano mkubwa tunaoupata toka kwa Serikali hasa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh.Dr,Harrison Mwakyembe na timu yake.
Lakini niwashukuru kwa nafasi ya kipekee ndugu zangu Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhabarisha umma kuhusu habari za mpira wa miguu,Pia pongezi zenu kwa kazi nzuri mliyoifanya wakati wa ujio wa FIFA, mlifanya kazi kubwa sana kutangaza ziara ya Rais wa FIFA, mmetupa heshima kubwa sana.
Ndugu zangu, leo nitaongelea mambo makubwa mawili ili waTanzania wapate kufahamu kinachoendelea katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.
Moja nitaongelea kuhusu mambo ambayo tumeyafanya kwa kipindi cha miezi saba nilichokuwepo madarakani lakini la pili ni mambo yanayoendelea sasa hivi kwenye Shirikisho.
MAMBO AMBAYO TUMEYAFANYA KWA MIEZI SABA TOKA TUINGIE MADARAKANI

HALI NA SHUGHULI ZA TAASISI
Kwa Mazingatio ya Utekelezaji Makini na wa Maendeleo wa Shughuli za Taasisi Tulitambulisha Muelekeo na Dira ya TFF ambapo Kazi iliyo Mbele yetu ni Kuzitoa na Kuimarisha Utambuzi na Utekelezaji wake. Sasa ni wakati Tunajiandaa Kutoa baadhi ya Mipango yetu na kutoa Dira za Utekelezaji wake. Pamoja na Mipango hiyo Bado TFF tumekuwa Tukitekeleza Shughuli za Mpira katika Mgawanyiko wake na labda kwa kifupi kugusia Miongoni mwake.
Mashindano.
Tumeendesha mashindano mbalimbali kwa ufanisi mkubwa yakiwemo mashindano ya Azam Sports Federation Cup, Ligi ndogo ya Wanawake kwa ajili ya kupata timu za kupanda daraja,Ligi Kuu ya Wanawake hatua ya makundi na hatua ya nane bora inayoendelea,Mashindano ya soka la ufukweni kwa timu za vyuo vikuu,Mashindano ya  kimataifa ya soka la ufukweni yajulikanayo COPA DAR ES SALAAM.
Azam Sports Federation cup;
Mashindano hayo kwa msimu huu 2017/18 tumeyaendesha kwa ufanisi na umakini mkubwa tofauti na huko nyuma kwa kuhakikisha upangaji wa ratiba umekuwa wa wazi usio na upendeleo wowote ule hivyo kupunguza malalamiko,jambo lingine tulihakikisha timu zote zinapata stahiki zao kwa wakati na kiwango kilichopangwa,kadiri tunavyoelekea hatua za mwisho wa mashindano tutahakikisha changamoto zote zilizojitokeza huko nyuma tunakabiliana nazo na kuzitatua ili kuhakikisha mashindano hayo yanaisha vizuri.
Ligi kuu ya Wanawake;
Mwaka huu tulianza kucheza Ligi ndogo ya Wanawake kutafuta timu za kupanda Ligi Kuu ya Wanawake katika vituo vya Dar es salaam na Dodoma,ikafuatiwa na Ligi ya Wanawake katika kituo cha Arusha na Dar es Salaam ili kupata Timu 8 za kucheza hatua ya Nane bora ya Ligi hiyo.
Katika hatua ya makundi, TFF ilizigharamia timu zote kwa asilimia 100 kuanzia malazi, usafiri, chakula, gharama za maadalizi ya timu na nauli ya kwenda na kurudi,ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu wa Wanawake kwa TFF kugharamia kwa kiwango hiki.
Katika hatua ya Nane bora ya  Serengeti Lite Women Premier League vilabu vyote vilishapewa fedha zao kwa ajili ya hatua ya kwanza ambayo imesimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) ambayo inajiandaa na mashindano ya kufuzu michuano ya Afrika kwa Wanawake ambapo tayari timu ya Taifa ipo kambini ikijiandaa na mchezo huo dhidi ya Zambia.
Taasisi iliendesha kwa mafanikio makubwa mashindano ya soka la ufukweni (Copa Dar es Salaam) kwa kuzialika timu za Uganda, Malawi, Zanzibar na wenyeji Tanzania bara ambazo tulizigharamia malazi, chakula na usafiri wa ndani.
PROGRAMU ZA TIMU ZA TAIFA
Toka tumeingia madarakani, tumekuwa tunafanyia kazi program mbalimbali za maendeleo ya Timu za Taifa.



Taifa Stars
Tumekuwa tukiendelea na program mbalimbali za Timu ya Taifa za kuhakikisha inafuzu Fainali za kombe la mataifa Afrika 2019.
Kuhakikisha hili Taifa Stars ilicheza na Benin, Malawi, Botswana na wiki hii tunacheza na Algeria pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika kalenda ya mechi za kimataifa ya FIFA.
Ili kuongeza hamasa ya wachezaji tumeongeza posho ya ndani kwa asilimia 100 na asilimia 50 kwa posho za nje.
Kilimanjaro Stars
Timu yetu ya Tanzania bara ilishiriki mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Kenya mwezi Desemba 2017, mbali na kushiriki ili ichukuwe kombe sababu nyingine ilikuwa ni kuendelea kupata mechi nyingi za kimataifa.
Timu ilicheza dhidi ya Rwanda, Kenya, Zanzibar na Libya, Tunaamini kwa wachezaji vijana waliokuwa sehemu ya kikosi hicho imewajengea uwezo katika soka la kimataifa.
Timu za Taifa za Vijana
Katika eneo hili  tumekuwa na mpango wa muda mrefu kuhakikisha vijana wa timu zetu za Taifa za miaka chini ya 23, 20, 17 na 13 zinakuwa na maandalizi bora na kwa kuanzia toka tuingie madarakani tumekuwa na kambi za timu za vijana kila mwezi kwa kuwakutanisha siku 14 za mazoezi na kuwatafutia mechi za kirafiki za kimataifa.
Timu ya U23
Timu ya Taifa chini ya miaka 23 ambayo ni kikosi cha pili cha timu ya Taifa kimeshaitwa kambini mara kadhaa na tumethibitisha kushiriki mashindano ya Olimpiki ambayo fainali zake zitafanyika nchini  Japan, lengo ikiwa ni kuhakikisha tunawapatia vijana hawa mechi nyingi za kimataifa ili wawe tayari.
Timu ya Vijana U20
Timu ya Vijana U20 ambapo jana ilicheza na Morocco na Jumatano itacheza na Msumbiji, ikiwa ni maandalizi ya mechi dhidi ya timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo(DRC) ikiwa ni mchezo wa kufuzu fainali za Vijana Afrika chini ya miaka 20.
Timu ya Vijana U16
Timu hii nayo imekuwa ikiingia kambini kila mwezi na hata sasa hivi ninavyozungumza na nyinyi, timu hii ipo kambini ikijiandaa kwa mashindano ya CECAFA na tunafanya jitihada za kuhakikisha inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla haijaenda Burundi.
Timu hii ndiyo ambayo itashiriki fainali za Afrika chini ya miaka 17 zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019.
Baada ya kutoka Burundi itakuwa na program maalum kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano mengine ya kufuzu AFCON U17, 2019 ambayo yatafanyika nchini mwezi Agosti ambayo lengo ni kupata mwakilishi wa CECAFA na vijana wetu watashiriki kama wenyeji. TFF imeamua kushirikisha Timu yenye Umri mdogo zaidi kwa u17 bila ya kujali Matokeo zaidi ya Ujenzi wa timu kwa kuandaa timu moja katika matukio yote haya ili kuiweka tayari kwa Mashindano ya u17 ya 2019 mwakani ambapo vijana hawa ndio watakuwa rasmi u17
Timu ya Vijana ya U13
Timu ya Vijana ya U13 katika kutafuta namna ya Kuwaimarisha vijana  hawa baada ya Utambuzi na Uteuzi wa timu imepata nafasi ya kushiriki mashindano ya kirafiki ya vijana chini ya miaka 13 yatakayofanyika nchini Ubelgiji mwezi Agosti 2018,Tayari orodha ya kwanza ya wachezaji 69  waliopatikana katika mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMITA) ipo TFF na idara ya ufundi inaandaa utaratibu wa kuwaita pamoja na kupata michezo ya kirafiki dhidi ya Zanzibar kwa ajili ya kupata kikosi cha pamoja cha Tanzania.
Timu ya Taifa ya Wanawake U20
Tumeanza kuandaa kikosi cha Vijana cha timu ya taifa ya Wanawake U20 ili kuwa na kikosi bora cha Twiga Stars kilichoandaliwa kwa muda mrefu na tayari ilishacheza michuano ya kufuzu fainali za vijana za Afrika chini ya miaka 20 na kutolewa na Nigeria.
Baadhi ya wachezaji wa timu hii wamepandishwa kikosi cha wakubwa na sehemu kubwa wanacheza Ligi Kuu ya Wanawake kupitia vilabu mbalimbali.
Tutaendelea na utaratibu wa kuwaita kambini kila wakati kutakapokuwa na nafasi ili kuzidi kuimarisha kikosi.
Twiga Stars
Kikosi cha Twiga Stars kimeingia kambini kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars inakabiliwa na mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia utakaochezwa Aprili 4,2018 Uwanja wa Taifa na marudiano kuwa Aprili 8,2018 nchini Zambia.



MAPATO NA MATUMIZI

MAPATO

Katika kipindi cha miezi Saba(7),Shirikisho limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tzs 3,670,397,199.00 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ambavyo ni pamoja na mapato kutoka kwa wadhamini Tzs 2,295,472,151 sawa na 62.5% ya mapato yote, makusanyo ya viingilio uwanjani Tzs 378,139,866 sawa na 10.3%. 27.2% ilitokana na Fedha kutoka CAF na FIFA.
MATUMIZI
Katika kipindi hiki Shirikisho lilitumia kiasi cha Tzs 3,752,001,171.00. Sehemu kubwa ya matumizi yalielekezwa kwenye usimamizi wa ligi mbalimbali pamoja na kuandaa timu za taifa ambapo jumla ya Tzs 2,409,150,732 sawa na 64% ya matumizi yote zilitumika.
Asilimia 36 ya Fedha zilizobaki ilitumika kulipia madeni ya Taasisi, Kulipa mishahara ya wafanyakazi, kusaidia mikoa katika maeneo ya miundo mbinu, kuwajengea uwezo wafanyakazi pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali.
Kama Rais wa TFF sijapokea HOJA wala USHAURI wala MAPENDEKEZO yoyote kutoka kwa Wajumbe wangu katika Ngazi zote kuhusiana na Matumizi ya Taasisi, Nasikitika kama kuna anayedai amehoji sijui wapi kwa kuwa kama Rais sijapokea hoja yoyote wala kuwasilishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji iliyopita ambayo Taarifa ya Kamati ya Fedha iliwasilishwa nakupokelewa na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
MADENI
Katika kipindi hiki,Shirikisho lilianza zoezi la kutathmini madeni iliyoyarithi kutoka kwenye Uongozi uliopita, ambapo deni hilo linafikia Tzs 2,172,000,000 linalodaiwa na watoa huduma mbalimbali, wafanyakazi,wachezaji na makocha.
Asilimia kubwa ya deni hili lilitokana na malimbikizo ya deni la TRA, Workers Compensation Fund na NSSF ambalo lililimbikizwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Shirikisho lilifanikiwa kulipa deni lote la michango ya wafanyakazi NSSF jumla ya Tzs 88,000,000 zilizokuwa hazijalipwa kipindi cha miaka miwili, na lilifanya majadiliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu ulipaji deni la kodi linalofikia Tzs 1,077,000,000, ambapo jumla yaTzs 315,000,000 zimelipwa na kiasi kilichobaki tumekubaliana kitalipwa kwa awamu kadhaa mpaka deni lote litakapomalizika.
Pia shirikisho limefanikiwa kupunguza mishahara kwa wafanyakazi kutoka Tzs   85,063,092.00 mpaka kufikia 50,000,000.00 baada ya kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21.
Baada ya kuingia madarakani tulifanya majadiliano na makocha wa timu za Taifa kuhusu uhalisia wa malipo yao na kufanikiwa kuokoa zaidi ya dola laki mbili(USD 200,000) kwenye mikataba yao na fedha zilizookolewa zitasaidia shughuli nyingine za mpira wa miguu.

UFUNDI
1. Kliniki iliyoendeshwa na Kocha PiaSundhage kutoka Sweden
2. Kozi ya ngazi ya awali ya makocha wa mpira wa miguu
ilifanyika katika mikoa ya Kigoma,Songwe, Lindi, Morogoro na Pwani
3. Kozi ya ngazi ya kati ya makocha wa mpira wa miguu
  Ilifanyika katika mikoa ya Kigoma mara mbili, Manyara na Morogoro.
4.Grassroot & Live your goal project
Kozi hii ilifanyika katika mikoa ya Lindi ambapo washiriki walitoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Pia kozi nyingine ilifanyika katika mkoa wa Mbeya ambapo washiriki walikuwa ni kutoka katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Katavi, Songwe na Rukwa
Aidha hii kozi ilifanyika Kigoma na kushirikisha washiriki wa mikoa ya Kigoma na Tabora.
5.Mafunzo ya awali ya Utawala mikoani
 Kuna kozi ya utawala na masoko iliyofanyika Dar es Salaam ili kuwaongezea watu wa masoko uwezo wa kuwavutia wadhamini.
6.Mafunzo ya waamuzi
  Mafunzo ya waamuzi wa FIFA na Waamuzi wa ngazi ya juu yalifanyika mara tatu jijini Dar es Salaam.
7. Kozi ya kupandisha daraja kwa Waamuzi
Kozi hii ilifanyika mara mbili katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.
8. Ziara za Mafunzo na kubadilishana uzoefu
 Zilifanyika ziara mbalimbali za Waamuzi wetu za kubadilishana uzoefu katika nchi mbalimbali.

9. Mpango wa ugawaji wa vifaa vya vijana na mafunzo
Tulipoingia madarakani tulikuta uongozi uliopita wameshanunua mipira na imekaa stoo, katika kutekeleza azma ya maendeleo ya vijana ili tuwe na timu za Taifa imara Shirikisho limegawa mipira (100 kwa kila Mkoa) saizi 4 na 3 kwa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Mikoa imepewa vifaa vya kufundishia (cones and markers) ili vijana wapate fursa ya kuonesha na kuendeleza vipaji vyao kwa maslahi ya Mpira hapa nchini.

Uzinduzi wa zoezi hili ambalo linategemewa kuwa endelevu lilifanyika Uwanja wa Taifa Agosti 3, 2017.

Rais wa TFF aliwakabidhi wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa niaba ya Mikoa yao kwenye Kanda husika, Kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa ZFA alikabidhiwa mipira hiyo kwa ajili ya Mikoa ya Zanzibar.

MASOKO NA HABARI
Tumeendelea kuongeza wadhamini katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha Taasisi inanufaika na bidhaa zake.Lakini pia tumeendelea kuimarisha idara ya habari kwa kuwanunulia nyezo za kufanyia kazi.

UTAWALA BORA
Katika kipindi hiki cha Miezi saba nimesimamia eneo hili kwa uadilifu mkubwa, Kamati zimekuwa zinakutana kabla ya vikao vya Kamati ya Utendaji ili kuhakikisha kila mmoja anashirikishwa.
Mfano, Wakati nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,kwa miaka 4 nilikaa kikao kimoja cha Kamati ya Fedha,Katika Utawala wangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ndani ya miezi saba ameitisha vikao visivyopungua vitano.
Nilimuagiza Kaimu Katibu Mkuu kuhakikisha kila Kamati ya Fedha inapohitaji kukutana ahakikishe inakutana na Mtendaji Mkuu amekuwa anatekeleza.
Na kwa sababu nafasi ya Makamu wa Raisi Kikatiba ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, basi hata mazungumzo ya Mkataba wa Udhamini wa Ligi Kuu msimu 2018/2019 yeye ndiye aliyekuwa anasimamia.
Nimekuwa nafanya hivi ili Taasisi iendeshwe kwa uwazi na kushirikisha kila mmoja,Na nimeendelea kusisitiza kuwa mapato ya matumizi ya Taasisi yatatolewa kwenye vyombo vya Habari ili yawe wazi kwa umma.
SEKRETARIETI YA TFF
Toka tuanze kuunda sekretarieti tumeajiri Wakurugenzi Watatu na Meneja mmoja na wote hawa waliajiriwa na Kamati ya Utendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu haijawahi kuajiri mfanyakazi hata mmoja kufikia sasa.
Nafasi ambayo haijajazwa ni nafasi ya Katibu Mkuu ambako Ndugu Kidao Wilfred bado anakaimu.
Kwanza nikiri kazi nzuri inayofanywa na mtendaji mkuu aliyekuwepo katika kuhakikisha Taasisi inapiga hatua kwa kasi kila ninapokutana na watendaji wakuu wa FIFA, CAF na CECAFA wamekuwa hawasiti kunimwagia sifa kwa kuwa na sekretarieti mahiri iliyobadilika katika kufanyia kazi changamoto za Taasisi.
Raisi wa FIFA alisema anaona mabadiliko makubwa ya hatua tunazochukuwa, Lakini Katibu Mkuu wa FIFA alisema nina Sekretarieti ya Vijana wenye hali, nguvu na maono ya kuipeleka Taasisi mbele huo ndio ujumbe wao.
Nimeyasema haya kuwahakikishia nikiwa msimamizi wa sekretarieti, mambo yote ambayo Kaimu Katibu Mkuu amekuwa akiyafanya ni maelekezo yangu au utekelezaji wa maamuzi halali ya kamati ya Utendaji, Kwahiyo nichukuwe fursa hii kupongeza kasi ya sekretarieti katika kusimamia mambo mbalimbali.
 AJIRA
Katika kipindi changu cha uongozi (Kamati ya Utendaji) kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Mkuu tumeweza kupunguza wafanyakazi kutoka Wafanyakazi 44 tuliowakuta wakati naingia madarakani hadi kufikia 21,Ni hatua kubwa na tunafanya upembuzi makini kabla hatujaanza kuajiri watu tuwe na mahitaji stahiki.
KATIBU MKUU
Kumekuwa na maneno mengi juu ya nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho, Ndugu zangu wakati naanza kazi niliona ni muhimu nafasi hii ikaimishwe kwa mtu anayelijua shirikisho vizuri na ambaye sina shaka na uwezo wake,Sifa zote hizi alikuwanazo KIDAO WILFRED na wajumbe wa Kamati ya utendaji chombo ambacho kinahusika nakupitisha kilibariki awe Kaimu Katibui MKuu.
Kutoka nje ya Ofisi na kukaimu hii siyo mara ya kwanza,wakati Ndugu Tenga anashinda Uraisi alimuomba Bi.Lina Kessy ambaye alikuwa mtumishi wa Serikali kuwa Mratibu wa Ofisi, nafasi iliyokuwa kama Mkuu wa sekretarieti wakati huo.
Hata wenzetu wa CAF, Rais ndiye anayepeleka jina bila kujali Mchakato utakavyokuwa kwa maana wanaweza wakatangaza au wasitangaze,na hata Katiba ya TFF inahitaji Rais wa TFF atoe mapendekezo ya Katibu Mkuu ili Kamati ya Utendaji ijadili, haya yanafanyika kwa sababu Rais kama msimamizi wa Sekretarieti anafanya kazi kwa karibu sana na Katibu Mkuu hivyo FIFA wanahitaji watu hawa  wawe wanaoweza kufanya kazi kwa karibu sana,ndipo Rais wa TFF anapopewa kipaumbele cha mtu wa kufanya naye kazi kwakuwa ndio nguzo ya Taasisi kwakuwa Rais ndio mkuu wa Taasisi na Katibu Mkuu ndio mkuu wa Sekretarieti.
Lakini pamoja na yote hayo bado nilikuwa napeleka ajenda ya Ajira kwenye Kamati ya Utendaji ili kushauriana njia bora ya kupata Katibu Mkuu kwa maslahi mapana ya Mpira wa Miguu na siyo mtu.
Niwahakikishie kikao kijacho cha kamati ya Utendaji kitaamua njia sahihi ya kupata Katibu Mkuu na tutahakikisha tunakuwa na Katibu Mkuu ndani ya muda mfupi ujao.   

Mipango Mbalimbali
Tumekuwa katika Ujenzi wa Mipango Mbalimbali kama nilivyoainisha kwenye Ilani yangu ambapo Katibu Mkuu amekuwa Kiungo muhimu katika kunisaidia kwenye Ujenzi wa Mipango yangu hiyo lakini kwa bahati Mbaya Kaimu Katibu Mkuu Kidao amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuandamwa na Maneno na Vitendo vinavyolenga na kufanikisha kumkwamisha na kumkosesha mazingira bora na rahisi ya kufanyia kazi zake na hivyo imekuwa ni atahri kwa TFF kwa Baadhi ya Mipango yake kuwa inakwama kutoka Mpaka sasa na hiyo ni athari kwa Mpira wetu kwa Ujumla.


Ndugu zangu jambo la pili ambalo nimeona niligusie ni jinsi vyombo vya maamuzi vya TFF vinavyofanya kazi,
Ndugu waandishi, TFF inafanya kazi kwa mujibu wa Katiba yake ya mwaka 2013 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2015. Katiba hii inataja Kamati ya Utendaji itaundwa na Wajumbe wafuatao;
1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Wajumbe 13 kutoka kanda zilizotajwa ibara 32 ya katiba ambazo ni Kanda namba 1-Kagera na Geita
Kanda namba 2- Mara na Mwanza
Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu
Kanda namba 4- Arusha na Manyara
Kanda namba 5- Kigoma na Tabora
Kanda namba 6- Katavi na Rukwa
Kanda namba 7- Mbeya, Iringa na Songwe
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma
Kanda namba 9- Lindi na Mtwara
Kmada namba 10- Dodoma na Singida
Kanda namba 11- Pwani na Morogoro
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Tanga
Kanda namba 13- Dar es Salaam
4. Wajumbe wawili wanowakilisha vilabu vya Ligi Kuu
5.Mwenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake.
6. Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba
7. Wajumbe wawili wa kuteuliwa na Rais wa TFF.

Rais wa TFF amepewa nafasi za kuteua wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji ili kumsaidia kufanya kazi na watu ambao wanajua muelekeo wake lakini ambao anaamini watamsaidia kwenye maeneo mbalimbali katika Taasisi.
Kamati ya Utendaji inafanya kazi na vyombo mbalimbali ambavyo ni Kamati ndogondogo, Bodi ya Ligi na Kamati za Kisheria pamoja na Kamati za Uchaguzi.
Kamati Ndogondogo;
  1. Fedha na Mipango
  2. Mashindano(Kamati ya Tuzo na Soka la Ufukweni)
  3. Ufundi na Maendeleo
  4. Vijana
  5. Wanawake
  6. Waamuzi
  7. Katiba, Sheria, na Hadhi za wachezaji.
  8. Tiba
  9. Ukaguzi (ambayo yenyewe ni kama Kamati huru)


    Kamati za Kisheria;
  1. Nidhamu
  2. Rufani ya Nidhamu
  3. Maadili
  4. Rufani ya Maadili
Kamati za Uchaguzi;
  1. Uchaguzi
  2. Rufani ya Uchaguzi
Ufanyaji wa kazi wa Kamati hizi umeelezewa katika Katiba ya TFF kwa maana Kamti za Kisheria zinajitegemea huwa haziingiliwi kwenye maamuzi yake.Ingawa vikao vyake vyote huwa vinaratibiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.
Kwahiyo maamuzi ya Kamati hizi huwa ni ya kujitegemea hivyo watu wote ambao wamekuwa wanahukumiwa na Kamati hizi ni vyema wakawa wanajua utaratibu wa Kamati zinavyofanya kazi.Na mimi binafsi nimeendelea kuheshimu Kamati zifanye kazi bila kuingiliwa na mtu yoyote vile.
Ndiyo maana wakati nachaguliwa niliahidi kusimamia Taasisi kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea aibu mtu yeyote, wala kumuogopa mtu na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kupambana na uchafu  wa aina zote katika serikali,Nami nimeamua kusafisha Taasisi kama nilivyoahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi ulioniweka madarakani,niseme wazi hakuna mtu asiye muadilifu atabaki katika mpira,Na nimpongeze  Kaimu Katibu Mkuu wangu kwa kusimamia kwa ujasiri mkubwa usimamiaji wa maagizo yote halali ya Kamati mbalimbali,Amekuwa anasimamia bila uoga bila kujali anavyosakamwa kwangu linanipa faraja sana.
Tumekuwa tunachukuwa hatua katika kila eneo tumeshaanza kuchukuwa hatua kwa wizi wa Mapato ya milangoni, kuna viongozi wamefungiwa,hatukuishia hapo tayari viongozi walioghushi leseni za usajili wamefungiwa,Hiyo yote ikiwa ni kuonesha sina masihara hata kidogo kwenye kuhakikisha mpira unakuwa sehemu ya watu waadilifu.
FIFA walituma Timu ya Uchunguzi(Investigation Team) kuangalia yale yote yaliyofanyika toka mwaka 2013 mpaka mwaka 2017,Timu ilikaa nchini kwa takribani wiki mbili ikifanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Katibu Mkuu,Yaliyogundulika yameacha doa kubwa na walitoa Ripoti na Maelekezo ya mambo ya kuyafanyia kazi na ya kuchukulia hatua.
Masharti yote haya yaliambatana na kuzuiwa kwa fedha zetu za miradi nia na wenzetu wachache, Lakini tumekosa pesa zinazoitwa Operation Cost ikiwa ni shinikizo la Dola Milioni Tatu ambazo tulipaswa kulipwa toka mwaka 2015-2018.
Karibia nchi zote Duniani zimenufaika kwa kupata pesa hizi, isipokuwa Tanza kuhakikisha tunatekeleza masharti ya FIFA, Hivyo tulipopata ripoti tumeamua kutekeleza kwa asilimia mia moja maagizo yote ya FIFA. Haya yanayotokea ni Miongoni mwa Matokeo ya Utekelezaji wa Taarifa za Wakaguzi wa TFF na Wakaguzi na Timu ya Uchunguzi kutoka FIFA. Jambo hili limepitia Hatua stahiki kwa Mujibu wa Taratibu zinazohusiana na Taarifa za kiUkaguzi na wahusika wameshirikishwa ipasavyo na Utetezi wao walipeleka kwenye Kamati husika ya Ukaguzi miezi iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu.
Niseme tu unaposafisha Taasisi kuna gharama zake TFF inahitaji Kuungwa Mkono zaidi kwa Hatua Madhubuti inazochukua za Kujisafisha na Kusonga Mbele.
Katika VITA hii ya Kupambana na Udhalimu kwenye Mpira wetu Hatutarudi Nyuma, Tutapambana bila hofu wala woga almuradi Hakuna dhulma wala Uonevu wala Upendeleo kwa yeyote. Na Nitoe wito kama kuna Kiongozi au Mdau yoyote anayejua ana Pesa za TFF kinyume cha Utaratibu Natoa WITO Ajisalimishe Mwenyewe.
Ahsanteni kwa kunisikiliza naamini mtaniunga mkono ili kuusogeza mbele Mpira wa Tanzania.
Mwisho niwakumbushe TFF inaendelea na maandaalizi ya Matayarisho wa AFCON U 17,2019 .Timu ya ukaguzi ya CAF itakuja mwezi wa Tano, tumekuwa tunalifanyia kazi kwa ukaribu  na serikali kuhakikisha changamoto za viwanja vitavyochezea mashindano pamoja na viwanja vya mazoezi vinakuwa tayari kwa wakati.Tutaendelea kulitolea ufafanuzi kila wakati.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Sehemu ya Mawaziri, Wabunge na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Mhandisi Raymond Mbilinyi  akisoma risala yake katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  akisoma muhtasari wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Maonda akitambulishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Makatibu wakuu wakitambulishwa lishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakitambulishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 
  Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiipongezwa baada ya kuongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  

 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  

 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  

  Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Pic ha na IKULU.
 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) .Geoffrey Mwambe,  alipowasili kushiriki katika  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Kulia kwake ni   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.

MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI5

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwonekano wa ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba

TIGO TANZANIA NA UBER WAUNGANA KULETA OFA MPYA KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari(wa pili kushoto) akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado(wa pili kulia) mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo. 


“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza katika hafla ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure, iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo, Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado pamoja na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed.

Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. 

Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha. 
Kampuni hizi mbili zitashirikiana katika bidhaa na promosheni zitakazoboresha huduma kwa wateja wa sasa na wa siku zijazo. Tigo na Uber nchini Tanzania wanatarajia kutangaza ofa zaidi kabambe zitakazowawezesha wateja kufurahia huduma za Uber jijini Dar es Salaam ambapo huduma za Uber zinapatikana kwa sasa.

JWTZ – KUJENGA VIWANDA KATIKA KAMBI ZA JKT

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akimuelekeza kitu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme ambaye ameshika punje za mahindi kiganjani kwake, alipotembelea kiwanda cha kisasa cha kuchakata mahindi cha kikosi cha JKT Mlale Songea Mkoani Ruvuma. “ Tunakikosi cha JKT Mbalali kilichopo Mbeya kinalima zao la kahawa na niwazalishaji wazuri wa zao hilo napotutajenga kiwanda cha kuchakata kahawa ili tuwe na Kahawa Product ya JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA ,Tunasambaza viwanda hivi kwa faida ya wananchi wa Tanzania, kwa maendeleo yao ,kwa maendeleo yetu wote, tunaimani tumeanza kuthubutu,tunaimani tutaweza ”

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YATEMBELEA CHANZO CHA MAJI, IFUNDA

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge Biashara na Mazingira mwishoni mwa wiki imetembea chanzo cha Maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoani Iringa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa jitihada zao za kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kunyweshea mifugo ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji na kuwataka kuondoa miti iliyopo pembezoni mwa chanzo hicho ambayo inanyonya maji kwa wingi.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola amezitaka Halmashauri na Wilaya zote nchini kupanda miti kwa wingi ambayo ni rafiki kwa mazingira. “Endapo tutapanda miti kwa wingi, tutaendelea kuwa na mvua za kutosha na kila Halmshauri zinatakiwa kuwa na Sheria ndogo ndogo za Mazingira”.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amewataka waheshiwa wabunge kuwa mstari wa mbele kuhimiza kilimo cha umwagiliaji kwa kutimia ‘matone’ ili kupunguza matumizi ya maji katika maeneo yao.
Diwani wa Kata ya Ifunda Bw. Elicus Chumila Ngwetta akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea eneo la Ifunda na kujionea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichohifadhiwa vizuri. Uhifadhi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Kamati ya Bunge mwishoni mwa wiki ilipata fursa ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kinachopeleka maji yake Mto Lyandembela ambao nao unamwaga maji Ruaha Mkuu mwaka mzima, Mto ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa viumbe hai. Kushoto ni Mhe. Hawa Mwaifunga na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akiwaonyesha waheshimiwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mifugo kunywa maji katika eneo la Ifunda ikiwa ni jitahada za Mkoa huo kuhifadhi vyanzo vya maji.

Rais Magufuli akutana na Rais wa AB-INBEV, TBL kujenga kiwanda Dodoma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Ricardo Tadeu Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev katika ukanda wa Afrika ambao ni Wanahisa wakuu wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango kabla ya kuanza kikao chake na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu katika ukanda wa Afrika ambao ni Wanahisa wakuu wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd ambayo inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha Bia mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu ambao ni wanahisa wakuu wa Kampuni hio ya TBL.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mmoja wa Wakurugenzi wa TBL katika ukanda wa Afrika Mashariki Roberto Jarrin mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo.
Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu ambao ni wanahisa wakuu wa Kampuni ya TBL akizungumza na wanahabari kuhusu TBL ambayo itajenga kiwanda kikubwa cha Bia mkoani Dodoma.PICHA NA IKULU

MSAJILI AZITAKA NGOs KUWASILISHA TAARIFA

$
0
0
MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yaaswa kuwasilisha taarifa za Mwaka kwa mujibu wa Kifungu Na. 29 cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004) kabla ya tarehe 15 Aprili, 2018.

Hayo yameainishwa katika taarifa ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Marcel Katemba kwa vyombo vya habari  jijini Dar es Salaam leo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa “Mashirika yasiyo ya kiserikali kuwasilisha Taarifa za Mwaka kwa mujibu wa Kifungu Na. 29 cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004), kama ilivyorekebishwa na Kanuni Na. 6 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2014 (GN 8, 2015)”.

 “Taarifa hiyo ijumuishe Taarifa za utendaji kazi, Taarifa za fedha zilizokaguliwa, NGO Fomu Na.10 na Stakabadhi ya malipo ya ada ya mwaka” 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mashirika yatakayoshindwa kutekeleza agizo hili ndani ya kipindi tajwa, yatachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.

WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KADIRI kengele inavyogonga kuashiria sikukuu ya Pasaka ipo jirani, ndivyo dhahiri kuwa siku za kuelekea Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Tumezoea mara nyingi kushuhudia Tamasha la Pasaka likifanyika jijini Dar es Salaam lakini waandaaji wa tamasha hilo wameamua mwaka huu iwe zamu ya Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, watu wa Kanda ya Ziwa watahemewa kwa burudani ya nyimbo zenye kumsifu na kumtukuza Mungu na litanenwa neno la Mungu.
Hivyo Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi kwenye Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu. Hakuna ubishi tena katika sikukuu ya Pasaka mwaka huu wakazi wa Kanda ya Ziwa, eneo ambalo litakuwa sahihi kwao kuisheherekea siku hiyo ni kwenye Tamasha la Pasaka.
Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na  kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
 Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake.Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, kati ya wengi watakaofanya kweli, atakuwepo mwanamuziki maarufu nchini Rose Mhando na wengine zaidi ya 15 kutoka ndani na nje ya nchi.Inafahamika kuwa Rose Muhando huwa hahitaji utambulisho. Ni mwanamuziki mwanamuziki mkubwa ambaye Muumba wa Mbingu na Ardhi amemjaalia kipaji cha kuimba kilichoambatana na sauti maridadi. Muziki wa Rose Mhando unapopigwa wapo ambao wanasimamisha shughuli zao kwa muda.
Natamani kutaja baadhi ya nyimbo zake atakazoimba siku hiyo lakini acha nikae kimya. Sitaki kukumalizia uhondo. Vema ufike CCM Kirumba kisha Uwanja wa Halmashauri, Simiyu ili macho na masikio yako yapate kumuona na kumsikiliza Rose Mhando. Uwezo wake wa kuimba umemfanya awe nyota ya muziki wa Injili.Kwa Rose Mhando mwenyewe anajua ukubwa wa Tamasha la Pasaka. Wakati anazungumzia tamasha hilo ameeleza wazi amejiandaa vya kutosha. Hivyo atakuwa Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuonesha kile ambacho amewaandalia. Na siku hiyo ataitumia kuzindua albamu yake mpya inayoitwa Jipe Moyo.
Imekuwa kawaida kwa matamasha ya Pasaka kuleta wanamuziki kutoka nje ya nchi. Kwa taarifa tu ni kwamba atakuwepo Ephrem Sekeleti kutoka zambia. Mashabiki wa muziki wa Injili wanamfahamu vema Sekeleti na ubora wa kazi zake.Mkazi wa Mwanza na Simiyu ni zamu yako mwaka huu kupitia Tamasha la Pasaka kuweka historia ya kumshuhudia mwanamuziki Sekeleti akitoa burudani tena ndani ya ardhi ya Tanzania. Karibu Sekeleti wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa wanakusubiri kwa hamu kubwa.
Kwa kuwa nimeamua kukutajia baadhi ya wanamuziki, naomba niendelee kwa kumtaja pia mwanamuziki Solomon Mkubwa ambaye anatoka nchini Kenya. Sitaki kumzungumzia zaidi mwanamuziki huyo kwa sababu kazi zake zimesababisha awe mwenye kufahamika na walio wengi nchini kwetu.Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama kwa kutaka wakazi wa Mwanza wapate burudani inayostahili hasa kwa kuzingatia ndiyo mara ya kwanza Tamasha la Pasaka kufanyika Kanda ya Ziwa, alisema aliona itampendeza Mungu pia mkali Christine Shusho akiwepo.
Hakuishia hapo alisema lazima awepo Martha Baraka, Clement Paul, Beatrice Mwaipaja, Upendo Nkone, John Lisu, Christopher Mahangila, John Mlelwa, Jescar Honore, BM na wengine wengi.John Lisu alipokuwa analizungumzia tamasha hilo, aliwahakikishia wakazi wa Mwanza na Simiyu kuwa wamejipanga vema kutoa burudani inayoambana na neno la Mungu kwa ajili yao.
Akawaomba wasikose kwani wanamuziki wote ambao watakuwepo siku hiyo watasafiri kutoka majumbani kwao na kuwafuata wakazi wa Kanda ya Ziwa ili kuwapa burudani yenye tani nyingi.Kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Msama ameeleza vema kuwa kila kitu kipo sawa. Usalama wa wananchi na mali zao kwa watakaofika siku hiyo upo wa kutosha.Msama amewaomba wakazi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo kimsingi mbali ya wanamuziki wa Injili kutoa burudani pia linasambaza ujumbe unaohusu umoja, upendo na mshikamano.
Msama alisema, jambo kubwa la kuenezwa katika tamasha hilo ni kila mmoja kutambua wajibu binafsi wa kuhakikisha amani iliyopo nchini inaendelea kutunzwa.Alisema, mapato ya Tamasha la Pasaka kwa sehemu kubwa yanakwenda kusaidia makundi ya watu wenye uhitaji maalum. Alifafanua: “Miongoni mwa makundi hayo ni watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na yatima. Hivyo ushiriki wako kwa namna moja au nyingine utakufanya uwe miongoni mwa waliosaidia jamii yenye uhitaji maalum.”

WAZIRI MWIGULU KUMUWAKILISA MAKAMU WA RAIS TAMASHA LA PASAKA KANDA YA ZIWA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akitoa ufafanuzi juu ya ujio wa mgeni rsmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu ambaye atawakilishwa na  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Jimmy Charles (kushoto).
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwandaaji wa tamasha la Pasaka kanda ya Ziwa,Alex Msama alipokuwa akielezea kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo sambamba na mambo mbengine mbalimbali

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Aprili Mosi mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Nchemba amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo.

Msama ameongeza kuwa awali mgeni rasmi alikuwa awe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu lakini imeshindikana kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kikazi na hivyo Waziri Mwigulu atamwakilisha katika uzinduzi wa tamasha hilo.

Mbali na Mwigulu, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Angelina Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi.

Aidha, Msama amesema kwamba katika tamasha hilo kunatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya waimbaji wa kitaifa na kimataifa na akawataja baadhi ya waimbaji ambao tayari wamethibitisha kuhudhuria kuwa ni, Rose Mhando, ambaye atazindua albamu yake mpya ya ‘Usivunjike Moyo’, Angel Benard, Bonny Mwaitege, Jesca Honore, Christina Shusho, Christopher Muhangila, Upendo Nkone na wengine kibao.

“Niwaambie ndugu waandishi wa habari, maandalizi yanaenda vizuri kwani tumejipanga vyema kuhakikisha wananchi watakaofika siku hiyo wanapata burudani ya kutosha na kulishwa neno la Mungu kupitia ujumbe wa nyimbo za waimbaji na ulinzi wa kutosha utakuwepo kwani tayari jeshi la polisi litakuwepo kuhakikisha amani na utulivu upo na hivyo nawaomba wakazi wa maeneo hayo wajitokeze kwa wingi,” amesema.

Amebainisha kuwa viingilio siku hiyo kwa wakazi wa Mwanza na maeneo mengine yanayozunguka eneo hilo kwamba vitakuwa ni Shilingi 5,000 kwa wakubwa na shilingi 2,000, kwa watoto huku kwa Mkoa wa Simiyu Aprili 2 mwaka huu, wakubwa wataingia kwa shilingi 3,000 na watoto 2,000.

WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI WA AFYA NA WADAU WA AFYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
aziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (wakatikati) akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa mwisho kulia), wakiwa katika kikao cha kimataifa cha masuala ya Afya ambacho kimejumuisha nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini, kikao hicho kimefanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia mbele ya Wadau wa masuala ya Afya wakiongozwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini katika mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya uliofunguliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya, uliohudhuliwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Wadau wa masuala ya Afya kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini wakati wa kikao cha kimataifa cha kujadili masuala ya Afya kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia moja kati ya Wadau wa afya baada ya kumaliza kikao cha kimataifa cha kujadili masuala ya Afya kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimtembeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika banda la Bohari ya Dawa (MSD) mda mchache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

MBEGU BORA YA MAHINDI YA WEMA 2109 KUWAONGEZEA TIJA WAKULIMA CHALINZE

$
0
0

Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein Rajab (kulia), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata ya Msoga mkoani Pwani. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani Kapilima George. Mbegu hiyo imetolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).


Mkulima wa kutoka Kikundi cha Gezaulole kilichopo Msoga, Shabani Mbogo akielezea changamoto za kilimo katika eneo hilo.







Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la Kikundi cha Gezaulole katika Kata ya Msoga.








Mkulima Ally Mhenga akichangia jambo kuhusu changamoto za kilimo zinazowakabili.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein akiangalia mbegu ya Wema.


Mkulima akisubiri majibu ya maswali yake kuhusu mbegu ya Wema.
Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu (wa nne kushoto), akielekeza namna ya kupanda mbegu hiyo kwa wanakikundi cha Gezaulole.
Hapa akielekeza vipimo vya upandaji wa mbegu hiyo.
Zoezi la upandaji wa mbegu hiyo likiendelea.
Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibindu, Juma Athumani (kushoto), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata hiyo Mbwewe mkoani Pwani. Wengine kutoka kulia ni ni Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George.
Wanawake wa Kata ya Kibinda wakiwa kwenye uzinduzi wa mbegu hiyo.
Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, akitoa maelezo ya upandaji wa mbegu hiyo kwa wakulima wa Kata ya Kibindu.
Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya , akichangia jambo.
Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.


Na Dotto Mwaibale, Chalinze

WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani wa Pwani wamefurahia kupokea mbegu bora ya mahindi aina ya Wema 2109 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa katika halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hiyo kwenye uzinduzi wa mashamba darasa katika vijiji vya Diozile na Kibindu vilivyopo Kata ya Msoga mkoani humo Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George alisema mbegu hiyo itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi katika halmshauri hiyo hivyo amewataka wakulima kuichangamkia.

"Tuwashukuru COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hii ambayo kwetu itakuwa ni mkombozi mkubwa katika mkoa wetu hasa kwa wakulima wa Kata ya Kibindu ambao ni vinara kwa kilimo cha mahindi katika mkoa wetu" alisema George.

Alisema mkoa wa Pwani kwa mwaka jana ulizalisha tani 110 za mahindi huku tani 65 zikizalishwa na Kata ya Kibindu jambo la kuwapongeza wakulima wa kata hiyo.Alisema mbegu hiyo itaongeza msukumo wa kilimo ilimo cha mahindi kwenye halmashauri hiyo hivyo kujikwamua kupata baa la njaa na ziada kuuza.

Aliwaomba wakulima hasa kwa wanavikundi waliopata mbegu hizo kuhakikisha wanayatunza mashamba darasa hayo kwa manufaa ya wakulima wote wa wilaya hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein alisema .kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.

Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kwa mkoa huo wametoa mbegu kilo 58 kwa ajili ya mashamba darasa katika wilaya ya Bagamoyo na Chalinze ambapo kwa wakulima mmoja mmoja wametoa kilo 42 pamoja na mbolea ya kupandia.

WAZAZI WAHIMIZWA KUFUATA MAADILI YA MTANZANIA KATIKA MALEZI YA MTOTO

$
0
0

Na Woinde Shizza-Arusha.

WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto kwa kufuata maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.

Imefafanuliwa kuna baadhi ya tamaduni za kigeni wanazoziiga zinachangia kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii zetu .Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Tanzania Gara Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano la kujadili maadili mema na uzalendo kwa ajili ya ustawi wa Arusha yao na Taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Arusha na lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na  viongozi mbalimbali wa Serikali na sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A jijini hapa.

Mheluka amesema wazazi wengi wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata tamaduni za wenzetu wa nchi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa watoto na ya kisasa kitu ambacho si kizuri kwani baadhi ya tamaduni za  wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi zinaporomosho maadili kwa watoto wetu.

“Ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha mtoto nae akathamini tamaduni hizo hizo ujue umempoteza mtoto na umemuaribu kabisa.Unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja.

"Huo si ujanja ni ujinga na ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio vyema.Nikiwauliza wazazi hivi nyie mngelelewa hivyo au mngelelewa vibaya je leo mngekuwepo hapo mlipo?Ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuandaa viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “amesema Mheluka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Arusha Dk.John Palanjo amesema mzazi anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa mtoto wake na mtoto akitakiwa kutimiza wajibu wake kwa mzazi. Ameongeza pia niwajibu wa kila mzazi kumfatilia mtoto wake na kujua maendeleo yake mwenyewe na si kumuachia mwalimu au dada wa kazi amfatilie huku akibainisha mzazi yeyote asitafute mchawi wa mtoto wake kwani mtoto anapokosa naadili.

Amesema asilimia kubwa ya wazazi wao wenyewe ndio wachawi wawatoto wao na kuwashauri wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto wao na kuzungumza nao kipi kibaya na kipi kizuri. " Hii itasaidia kuwawezesha watoto wetu kukuwa kwa kuendana na yale yanayopendeza kwa jamii inayowazunguka

"Mimi na imaini iwapo mzazi akijua wajibu wake hatakubali hata kidogo mtoto wake aharibike ,hivyo ni vizuri mzazi utambue wajibu wako, umrudie Mungu maana ukiwa na hofu ya Mungu lazima utamlea mtoto
kwa kufuata kanuni za kimungu,”amesema. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Arusha Ally Meku  amewataka baadhi ya wazazi kupunguza migogoro ndani ya familia ili watoto nao wasiige tabia mbaya kwani wanapoaanza migogoro katika familia wanashindwa kuwale watoto wao.

Amefafanua na badala yake watoto hao wanaanza kutangatanga hovyo na kuanza kuiga tabia mbaya.
Naibu Katibu Mkuu Wazazi CCM Tanzania bara Godfrey Mheluka akiwahutubia wananchi waliohudhuria kongamano la kujadili 'aadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha.
kamanda wa vijana UVCCM mkoa wa Arusha Philemon Molel maarufu kama Monabani akiongea na wananchi waliohudhuria kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha .
Baadhi ya viongozi  mbalimbali meza kuu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano hilo. 
RTO mkoa wa Arusha Joseph Bukombe nae alikuwepo katika kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wazazi na vijana waliouthuria katika kongamano hilo kufuata maadili ,huku akiwasihi wazazi kuwakumbusha vijana wao kuvaa kofia ngumu wakati wanapoendesha pikipiki zao pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kutokea mara kwa mara
mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo 
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Edmond Rice nao waliuthuria katika kongamano hilo
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Arusha Dkt John Palanjo akizungumza na wananchi waliohudhuria katika kongamano hilo

DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NA VIJANA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana manispaa ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia vizuri fedha za mikopo walizopewa na manispaa hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanawake na vijana 60 kutoka vikundi 20 vya wajasiriamali ambao wamepata mikopo ya shilingi milioni 125.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo Jumatatu Machi 19,2018 Matiro aliwataka vijana na wanawake hao kutumia fedha walizopewa kwa malengo waliyokusudia na kuhakikisha wanaanzisha viwanda vidogo vitakavyoinua uchumi wao.

“Tumieni mikopo hii kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli anayetaka Tanzania iwe nchi ya viwanda,pale mnapokwama tafadhali wasilianeni na viongozi wa serikali,tutawasaidia na pia tutatembelea miradi yenu ili tujue mnachofanya”,alisema Matiro.

Aidha aliwataka vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ,mikopo ambayo haina masharti magumu wala riba kubwa ukilinganisha na taasisi za kifedha (benki).“Msikubali kukata tama kwamba maisha ni magumu,hata siku moja serikali haiwezi kugawa pesa kwa mtu mmoja mmoja,anzisheni vikundi vya ujasiriamali,kisha ombeni mikopo kwenye halmashauri,pesa zipo”,aliongeza Matiro.

Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone alisema vikundi hivyo vimepata mkopo wa shilingi milioni 125 kutoka mfuko wa wanawake na vijana ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya manispaa hiyo.“Katika mwaka wa fedha 2017/18 manispaa imelenga kutoa shilingi milioni 208 kwa ajili ya vijana na wanawake,katika awamu hii ya kwanza tumetoa shilingi milioni 125 kwa vikundi 11 vya wanawake na 9 vya vijana”,alieleza Kiwone.

“Baada ya kutoa mikopo hiyo,tumeona ni vyema tuwape elimu ya kuhusu namna ya kunufaika na mikopo,mafunzo yamedumu kwa muda wa siku tatu,na kipaumbele cha manispaa ya wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo”,aliongeza Kiwone.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya vijana Manispaa ya Shinyanga,Charles Luchagula alisema manispaa hiyo inaendelea kupokea maombi ya mikopo kwa vijana na wanawake ili kujiinua kiuchumi na kujikimu kimaisha.

Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema kupitia mafunzo hayo ya siku tatu wamepata elimu kuhusu namna ya kuanzisha biashara na kutafuta masoko,kutengeneza mnyororo wa thamani kutunza kumbukumbu na vifungashio na umuhimu wa uwekaji lebo.

Walisema pia wamejifunza taratibu za utoaji wa mikopo na urejeshaji wa mikopo,wajibu wa kiongozi wa kikundi,ukweli kuhusu Ukimwi,ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na elimu kuhusu mfuko wa bima ya afya (CHF iliyoboreshwa.
Washiriki wa mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana  wa manispaa ya Shinyanga wakiwa wamesimama baada ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuingia ukumbini kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanawake na vijana kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa pesa za mikopo walizopata
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiimba wimbo kuhusu wanawake ...."Wanawake wote hongeraa...."
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanja akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akielezea lengo la mafunzo hayo ya siku tatu. Alisema lengo  ni kuwajengea uwezo  wanufaika wa mkopo huo kutumia vizuri fedha walizopata.
Afisa Maendeleo ya vijana Manispaa ya Shinyanga,Charles Luchagula akiwasisitiza wanawake na vijana kutumia fedha walizopata kuanzisha viwanda vidogo.
Washiriki katika mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakijaza mkataba wa mkopo waliopata katika kikundi chao.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Diwani mwingine wa Chadema Arusha Ajiuzulu na kujiunga na CCM

$
0
0
 
Diwani wa kata ya Kaloleni Halmashauri ya jiji la Arusha, Ndg.Emmanuel Kessy wa CHADEMA (pichani kati) amejiuzulu uanachama na udiwani mapema jana na kutangaza kujiunga na chama cha CCM, kwa kile alichoeleza kuwa amefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Mh.Rais Magufuli.Diwani huyo amepokelewa na Katibu mwenezi wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.Abrahamu Mollel pamoja Katibu Hamasa wa Vijana Mkoa wa Arusha Ndg. Omary Lumato

HOTUBA YA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA 19 MARCH 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA NENO KWA MAWAZIRI WA AFYA WA AFRIKA MASHARIKI,KATI NA KUSINI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

SERIKALI ya Tanzania imewahakikishia mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini kuwa itaendelea kuisaidia sekretarieti ya ECSA yenye makao makuu yake jijini Arusha.

Imesema kuwa inatambua majukumu ya Sekretarieti hiyo katika sekta ya afya huku ikiwaomba mawaziri hao na wadau wengine kuboresha mifumo ya afya ili kusaidia kuondoa changamoto zinazojitokeza wakati wa utoaji wa huduma bora za afya.

Akizungumza Dar es Salaam jana jioni wakati anafungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka Afrika Mashariki,Kati na Kusini,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni jukumu la Serikali ya Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji na kusaidia sekretarieti ya ECSA.Waziri Mkuu amesema pia mawaziri hao katika mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam wajadili mambo yote muhimu yanayohusu sekta ya afya na kufafanua wasiache hata jambo moja nyuma na zaidi ni nini kifanyike kuboresha sekta ya afya.

"Niwaombe mawaziri wa afya ambao mmekutana katika mkutano huu ,wekeni mikakati yenye lengo la kuboresha sekta ya afya na kuangalia namna ya kuondoa changamoto ambazo zinakuwa vikwazo katika utoaji wa huduma bora za afya."Boresheni mifumo ya afya na kubwa zaidi ifikapo mwaka 2030 tuwe tumefikia malengo ya Maendeleo Endelevu(SDG's) katika eneo la afya.

"Jukumu la Serikali ya Tanzania ni kuendelea kusaidia na kuwa mwenyeji wa sekretarieti ya ECSA-HC," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.Ametumia mkutano huo kuwataka mawaziri hao na wadau wengine wa afya ambao wamedhuria mkutano kuweka mkakati wa namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama TB na magonjwa ya kuambukiza.

Mbali ya kuzungumzia mambo yanayohusu uboreshaji wa huduma za afya,Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba washiriki kabla ya kuondoka watembelee vivutio vya utalii vilivyopo nchini.Kwa upande wa baadhi ya washiriki wa mkutano wameelezea hatua wanazochukua kuboresha sekta ya afya huku wakiisifu Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ambavyo upo imara katika usimamizi mzuri wa mambo mbalimbali.Kauli mbiu ya mkutano huo wa 65 kwa mawaziri hao wa afya unasema Ushiriki wa sekta ya afya katika kupata mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu(SDG's).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya, uliohudhuliwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini.

TAZAMA SHEREHE ZA MKOMAULA KABILA LA WAYAO MKOANI RUVUMA

$
0
0
Kulia ni Sultani Mataka ambaye ni sultani wa tano wa kabila la wayao Tanzania akisalimiana na Mwandishi wa Ruvuma TV Nancy Mbogoro .
………………….
Kupitia kipindi cha Utalii cha Talii na Ruvuma TV tumekuandalia kipindi maalum kinachohusu Sherehe za asili za kabila la Wayao katika mkoa wa Ruvuma, Sherehe hizi zinakwenda kwa jina la Mkomaula, Sherehe hizi hufanyika kila mwaka na kuongozwa na Sultan Mataka ambaye ni Sultan wa tano wa kabila la Wayao Tanzania. Hii hapa chini Video yake.

MAWAKALA WA TIGO PESA NCHI NZIMA WAENDELEA KUJISHINDIA ZAWADI

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo ,Kanda ya Kaskazin,Henry Kinabo akimkabidhi wakala wa Tigo Moshi mjini ,Hassan ,mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Mbili kwa kuibuka mshindi wa pili wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini. Promosheni hii inawahusu Mawakala zaidi ya 73000 wa Tigo Pesa nchi nzima huku zawadi za Shilingi za kitanzania Milioni 144 zikishindaniwa. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo ,Kanda ya Kaskazin,Henry Kinabo akimkabidhi wakala wa Tigo wilaya ya Same Real Stationary ,mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni tatu  kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini. Promosheni hii inawahusu Mawakala zaidi ya 73000 wa Tigo Pesa nchi nzima huku zawadi za Shilingi za kitanzania Milioni 144 
zikishindaniwa. 


Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni ,mbili kwa Juliana Shilatu aliyeibuka kama wakala wa pili bora wa kanda ya Ziwa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa. Zawadi zenye thamani ya TZS 88 milioni zimetolewa na Tigo pesa kwa mawakala wake 73,000 nchini kote walioshiriki katika promosheni hiyo.

Meneja wa Tigo Mkoa Iringa Davis Kisamo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi millioni 3/- kwa wakala wa Tigo Pesa, Gibson Chaula wa Songea mwishoni mwa wiki mkoani Iringa.

Meneja wa Tigo Mkoa Iringa Davis Kisamo (kushoto) na Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa Iringa, Samuel Chanay (kulia) wakimkabidhi mfano wa hundi wakala wa Tigo pesa Asha Ramadhani aliyeshindia zawadi ya shilingi millioni 2/-  kwenye hafla iliyofanyika mkoani Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.


Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro

$
0
0
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12  pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini  hapo.

Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.  Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya  upasuaji wa ubingwa wa juu.

“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu  walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”.  amesema Dkt. Magandi.

Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu  ya nusu ya vitanda hivyo.  “Hivyo  msaada huo umekuja wakati muafaka  kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
 Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
 Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
 Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images