Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zinatarajia kufanyika April Mosi mwaka huu, huku msanii maarufu kutoka nchini India wa tamthilia ya Beintehaa Pritika Rao 'Aliyah' akitarajiwa kuwa mgeni mwalikwa kuja kushuhudia utowaji wa tuzo hizo.

Hayo yamesemwa wakati wa utangazaji wa vipengele vinavyoshindanishwa katika upatikanaji wa washindi wa tuzo hizo vikiwa katika makundi 19 ikiwemo tuzo ya chaguo la watazamaji (viewers Choice Awards).

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi mtendaji wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa SZIFF ni tuzo za kwanza kubwa kabisa kufanyika nchini ikiwa ni katika malengo mojawapo ya kuibua na kuendeleza tasnia ya Sanaa ya maigizo na filamu ambapo filamu shiriki kutoka Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda na DRC Kongo zimeingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

"Timu nzima ya tuzo za SZIFF waliweza kupita mikoa yote nchini na waliweza kupata filamu nyingi sana mikoani na hata nje ya nchi ikiwemo Kenya,Burundi,Rwanda na DRC na zikiwa zimeingia katika kinyang'anyiro cha ushiriki wa tuzo hizo kubwa nchini ikiwa ni mara ya kwanza,"amesema Mhando.

Mhando amesema kuwa SZIFF imejikita zaidi katika filamu zenye maudhui ya kiswahili ambapo takribani filamu 143 zilifanikiwa kupambanishwa na kuruka kila siku kupitia chaneli ya Sinema Zetu na watazamaji waliweza kupata fursa ya kupiga kura.

Kwa upande wa Msimamizi wa tuzo za SZIFF Zamaradi Nzowa amesema kuwa tuzo hizi ni kubwa na mbali na washindi kupata tuzo pia wataweza kuondoka na kitita cha pesa taslimu na utambulisho maalumu na kipekee kwenye soko la tasnia ya filamu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.

"Tuzo za SZIFF zitaweza kuitangaza nchi yetu sehemu mbalimbali sambamba na lugha ya kiswahili na pia washindi watajinyakulia pesa taslimu kwani filamu zaidi ya 500 ziliweza kuchujwa kwa vigezo vilivyokuwa vimeweka na majaji wetu ambao hawakuweza kutangazwa hadharani," amesema Zamaradi.

Katika kuweza kuwapata washiriki na washindi mbalimbali,Azam Tv waliweza kushirikiana na COSOTA, BASATA pamoja na bodi ya filamu nchini katika safari ya mchakato mzima wa kuwania tuzo za SZIFF ulioanza rasmi Januar Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 12 ambapo filamu zaidi ya 500 zilipokelewa na kuchujwa kwa kutumia vigezo vya kisheria na ubora wa maudhui.

Baadhi ya tuzo zinazowaniwa ni pamoja na Best film, best director, best actor, best actress, best commedian na Best screen play. Zingine ni best editing, best original music, best cinematography hizo zikiwa katika filamu ndefu,filamu fupi pamoja na makala.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akizungumza na wanahabari wakati kutangaza vipengele vya tuzo za Sinema Zetu Film Festival (SZIFF)  inayotarajiwa kufanyika April Mosi Mwaka huu na muigizaji wa tamthilia ya Beintehaa Pritika Rao 'Aliyah' akitarajiwa kuwa mgeni mwalikwa. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa Azam Media Jacob Joseph.

 Jaji Mkuu wa Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) Martin Mhando akitaja vipengele vyinavyowaniwa katika tuzo hizo zitakazofanyika April Mosi. Kulia ni Msimamizi wa Tuzo hizo Zamaradi Nzowa
 Baadhi ya Wana habari wakifuatilia mkutano huo
  Msimamizi wa tuzo za Sinema Zetu Film Festival (SZIFF) Zamaradi Nzowa akielezea jambo kwa wanahabari wakati wa utajaji wa vipengele 19 vinavyowaniwa kwenye tuzo hizo

TUMEJIANDAA VILIVYO TAMASHA LA PASAKA CCM KIRUMBA APRILI 1-JOHN LISSU

$
0
0
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. lex Msama kushoto  akifafanua kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu, mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar,kulia ni mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za Kiroho (injili) John Lissu akifurahi jambo kwenye mkutano huokuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. lex Msama kushoto  na Mwanamuziki wa Injili John Lissu wakiimba wimbo  wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu.

 

*Awaambia wakazi wa Kanda ya Ziwa wafika kuona burudani, Msama awahakikishia usalama, maandalizi yamekamilika

Na Said Nwishehe,Globu ya jamii

MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za Injili John Lissu amewaomba mashabiki wa muziki huo na Watanzani kwa ujumla hasa wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 1 mwaka huu.

Lissu ametoa kauli hiyo leo jiiini Dar es Salaam wakati akizungumzia Tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu litafanyika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza siku ya Aprili 1 na Aprili 2 litafanyika mkoani Simiyu katika uwanja vya Halmashauri mjini Bariadi.

Mwanamuziki huyo ameeleza kuwa wanamuziki mbalimbali maarufu wa muziki wa Injili ndani na nje ya Tanzania wataonesha vipaji vyao vya kuimba,hivyo kikubwa ni wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Tamasha hilo ambalo huwa linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotioni kupitia Mkurugenzi Mkuu Alex Msama ,wamehakikisha kuwa kutakuwa na  idadi kubwa ya wanamuziki wa Injili ili watu  wataofika kwenye tamasha hilo wapate burudani inayoambatana na ujumbe wenye kumpendeza Mungu

"Tunawaomba wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla tukutane uwanja vya CCM Kirumba siku ya Aprili 1 mwaka huu,wanamuziki wa Injili tumejiandaa vizuri,mashabiki karibuni muone kile ambacho tumekiandaa kwa ajili yenu.

" Siku hiyo mashabiki wa muziki wa Injili watarajie  mambo makubwa zaidi hasa kwa kuzingatia ukubwa wa Tamasha hilo nwa kwamba linafanyika wakati wa Pasaka na mwaka huu tupo Kanda ya Ziwa kwa mara ya kwanza,"amesema John Lissu.

Amefafanua kuwa kingine ambacho mashabiki watashuhudia siku hiyo ni uzinduzi wa Albam mpya ya mwanamuziki Rose Mhando inayofahamika kwa jina la Jipe moyo.John Lissu amefafanua kuwa Rose Mhando kwa muda mrefu amekuww kimya kwa kutotoa albam kwa zaidi ya miaka mitano na hatimaye mwaka huu atazindua albam hiyo.

"Watu wamemisi kumuona mwanamuziki Rose Mhando ambaye hajazindua albamu lakini kwa kutumia tamasha hilo atazindua albamu mpya ya Usife Moyo na kufanya mambo makubwa kwa kuimba nyimbo zake ambazo zimekuwa zikitamba kipindi chote," amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Msama Promotion,Alex Msama amesema  maandalizi ya tamasha hilo yanakwenda vizuri na usalama upo wa kutosha ,hivyo watu wasiwe na hofu huku akiwahakikishia usalama wao na mali zao upo wa kutosha.

Pia amesema wanaangalia pia namna ya kufanya tamasha hilo katika mikoa ya Iringa na Dodoma  mara baada ya kumalizika kwa tamasha hili na kueleza lengo ni kutoa nafasi kwa mikoa mingine nayo kushuhudia namna tamasha hilo linavyovuta hisia za watanzania wengi na hasa wanaopenda muziki wa Injil.

Pia amesema ni tamasha ambalo pamoja na kuimbwa zaidi nyimbo za Injili pia linazungumzia kudumisha umoja,upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

TIDO MHANDO AELEZEA UBALOZI WA LULU TUZO ZA SZIFF.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa baada ya balozi wa Tuzo za Sinema Zetu internationa Film Festival Elizabeth Michael 'Lulu' kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela hawajatafuta mbadala wake.

Mhando amejibu swali aliloulizwa wakati wa utangazaji wa vipengele vya tuzo za SZIFF zinazotarajiwa kufanyika April Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Akitolea ufafanuzi suala hilo,Mhando amesema kuwa mchakato wa kumpata balozi wa SZIFF kwa hiyo baada ya matatizo ya Lulu hawakuona umuhimu wa kupata mtu mwingine ,kwani muda haukuwa rafiki kwao.

"baada ya kutokea kwa matatizo kwa balozi wetu wa SZIFF Lulu, ambapo ili kumpata mwakilishi mwingine kunachukua muda mrefu hatukuona umuhimu wa kufanya hivyo na kuacha tuendelee na mchakato wa tuzo zetu ambazo tayari ulikua umeshaanza,"amesema Mhando.

Tuzo za SZIFF zilizinduliwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe ikiwa ni katika mchakato wa awali kabisa wa timu ya SZIFF kwenda mikoani kwa ajili ya kutafuta filamu mbalimbali huku balozi wa tuzo hizo Lulu akitambulishwa kwa mara ya kwanza kabisa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na aliyekuwa Balozi wa Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu (SZIFF) Bi. Elizabeth Michael alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa tuzo hizo Oktoba mwaka jana jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zinaratibiwa na Azam Media zinatarajiwa kutolewa  April Mosi ambapo zinazoshirikisha filamu za Kiswahili.

AZAM WAANZA MAANGAMIZI YA KUMUUA MTIBWA KOMBE LA FA

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Kikosi cha Azam FC, kimeanzamaandalizi ya kuivaa Mtibwa Sugar huku Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Idd Cheche akiahidi mchezo mzuri na kuondoka na ushindi kwenye mtangane wa robo fainali ya kombe la Azam Sports HD dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) unatarajia kufanyika Uwanja wa Azam Complex Machi 30 mwaka huu saa 1.00 usiku, ambapo tayari kikosi cha Azam FC kimeshaanza maandalizi tokeo jana jioni.

“Mashabiki waendelee kutusapoti kwa sababu mchezo wa mpira unahitaji sapoti, mchezo wa mpira una wachezaji, una viongozi, una mashabiki na mashabiki ndio wanaoongeza chachu ambayo inakuja kufanya mchezo uwe pendwa duniani.

“Kwa hiyo mashabiki waje kwa wingi watusapoti na sisi tutahakikisha tunawapa furaha ile ambayo wanaitarajia, watarajie mchezo mzuri na wenye ushindi,” alisema Cheche.

Cheche aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya vijana ya Azam FC (Azam U-20) kabla ya desemba mwaka juzi kupewa nafasi hiyo timu kubwa, alisema mchezo huo utakuwa ni tofauti sana na ule waliocheza kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu na kutoka sare ya bao 1-1.

“Mchezo wa ligi ni tofauti na FA, huu ni mchezo wa mtoano (knockout) lazima mmoja afungwe kama mnatoka sare mnafika kwenye hatua ya penalti lakini sisi tunataka kuhakikisha mchezo tunaumaliza ndani ya dakika 90 lakini kikubwa mno kwanza ni kuanza kuwajenga wachezaji wetu mazoezini kwa sababu mazoezi ndiyo yatatupelekea kufanya vizuri huu mchezo kwa hiyo tuko makini kuhakikisha watu wanafanya mazoezi vizuri ili mechi iweze kuwa nyepesi kwetu,” alisema.

Akizungumzia maandalizi waliyoanza, Cheche alisema kuwa kwa sasa watafanyia kazi mazoezini makosa waliyofanya kwenye mechi zilizopita ikiwemo kuwadukua wapinzani wao Mtibwa Sugar.

“Tunafanyia kazi matatizo tuliyokuwa nayo kidogo kwenye mechi zetu za ligi tulizocheza huko nyuma, kurekebisha makosa, kuangalia kitu gani cha kufanya, kuiangalia Mtibwa uzuri wake na udhaifu wake ili tuandae vijana wetu wahakikishe tunakwenda kuwaangamiza Mtibwa,” alisema.

Msimu uliopita timu hizo zilikutana kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, mchezo ukifanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex saa 10.00 jioni na Azam FC ikafanikiwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0, liliwekwa kimiani na Ramadhan Singano ‘Messi’, akiunganisha pasi safi ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Mshindi wa mchezo huo, atacheza ugenini kwenye nusu fainali na mshindi wa robo fainali nyingine kati ya Stand United na Njombe Mji, mchezo huo ukipigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Machi 30 mwaka huu.

UNUNUZI WA VICHWA VYA TRENI 11 VILIVYOPO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
UNUNUZI WA VICHWA 11 VYA TRENI.
Shirika la Reli Nchini TRC limetiliana saini ya makubaliano ya kuvinunua Vichwa 11 vya Treni kutoka Kampuni ya Progress Rail Locomotives ya Marekani ambayo inavimiliki Vichwa hivyo Vyenye namba 9014 hadi 9024.
Mnamo Tarehe 27 September 2017 , Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili ya kubaini kama Vichwa hivyo ni vipya au lah.
Mkurugenzi Mkuu wa Shiridka la Reli Nchini Ndugu Masanja Kadogosa amekutana na Vyombo vya habari, na kutoa taarifa hiyo.
Masanja amesema kuwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa ya kuvinunua Vichwa hivyo kwa Bei ya Dola za Kimarekani Milioni mbili  na laki nne, badala ya Dola Milioni tatu na laki mbili ambazo zilitumika kununua vichwa 13 mwaka 2015, Serikali imeokoa Dola Milioni nane na laki nane.
Kwa upande  wake Meneja wa Kanda  ya Kusini Mwa Jagwa la Sahara wa Kampuni hiyo ya Progress Rail  Barend Hanekom amesema amefurahishwa  kwa  mara nyingine tena kufanya baishara na Serikali ya Tanzania.
Katika Mkataba huo, imelezwa kuwa itapaswa kufanyika kwa majaribio ya Vichwa hivyo kwa awamu tatu, kwanza ni ukaguzi wa kuvitizama , yaani Visual Inspection , pili ni kuviwasha na kuvipa mzigo lakini vikiwa havitembei yaani Load Box, na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo  wenye tani 700 kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro na kasha Tani 1200 kutoka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Ununuzi wa Vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa Shirika la Reli kwani sasa hivi Shirika lina Vichwa 29 madhubuti kati ya 47 vinavyohitajika ili kutoa huduma nzuri na uhakika.

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YAVUTIWA NA MIRADI YA TASAF MKOANI SIMIYU.

$
0
0
NA ESTOM SANGA- BARIADI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wamefanya ziara mkoani Simiyu na kuvutiwa na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF-mkoani humo.

Wajumbe hao walianza ziara yao kwa kusomewa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo Katibu Tawala wa Mkoa huo , Jumanne Sagini aliwajulisha Wajumbe hao kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,umekuwa chachu muhimu katika kuleta maendeleo ya wananchi katika mkoa huo mpya.

Amesema kupitia Mpango huo Walengwa wameboresha maisha kwa kuendelea kujenga mkazi bora, kuchimba visima vya maji, uanzishwaji wa mashamba ya pamba ili kujiongezea kipato huku pia sekta za Afya na Elimu zikiendelea kunufaika na utekelezwaji wa Miradi ya TASAF.

Wakiwa katika Wilaya ya Maswa ,mkoani humo, Wajumbe hao walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Stephen Rweikiza, walipata fursa ya kutembelea baadhi ya kaya za Walengwa ambako walishuhudia mafanikio ya ujenzi wa Nyumba ya mmoja wa Walengwa wa TASAF ,Monica Kwilasa katika kijiji cha Shanwa ambaye ametumia sehemu ya ruzuku aliyopata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuboresha Makazi yake.

Kama Wahenga wasemavyo “ Kuona ni kuamini” Wajumbe wa kamati hiyo walionyesha kushangazwa na mafanikio ya Mlengwa huyo ambaye aliwajulisha namna alivyotumia fedha alizozipata kutoka TASAF kuanzisha biashara ndogo ndogo iliyomwongezea kipato na kumwezesha kujenga nyumba kwa matofali ya saruji na kuezeka kwa mabati.

Akizungumza na Walengwa na Wananchi katika eneo la shule ya Sekondari ya Nyalikulungu ambako pia TASAF imejenga majengo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Rweikiza,amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana katika utekelezaji wa Mpango huo ni kielelezo cha namna Serikali inavyopiga vita umaskini kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo amesema zinapaswa kuungwa mkono na wananchi. Zifuatazo ni picha za ziara hiyo ya kamati ya huduma za jamii ya bunge.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma ya Jamiii wakiwa mbele ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa Walengwa kwa ruzuku ya TASAF Bi. Monica Mwalu, (aliyekamata karatasi) katika kijiji cha Shanwa wilayani Maswa . Aliyevaa kofia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii,Mhe. Venance Mwamoto (aliyevaa koti) akitoka ndani ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa kwa ruzuku ya TASAF.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Wakikagua moja ya Majengo yaliyojengwa na TASAF katika shule ya Sekondari ya Nyalikulungu katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Waziri Mkuchika (aliyevaa kofia ) na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya huduma za Jamii wakikagua zoezi la ilipaji wa ruzuku kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Shanwa Wilayani Maswa ruzuku ambayo imeanza kuboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyalikulungu wilayani Maswa wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma za jamii Mhe.Steven Rweikiza (hayupo pichani).
Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Shanwa wilaya ya Maswa wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya huduma za jamii Mhe. Steven Rweikiza( hayupo pichani) wakati kamati hiyo ilipokagua miradi ya TASAF mkoani Simiyu.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma za Jamii, wakimsikiliza mmoja wa Walengwa wa TASAF Bi.Monica Mwalu mkazi wa kijiji cha Shanwa wilayani Maswa namna alivyotumia sehemu ya ruzuku kujiongezea kipato na kujenga nyumba (iliyoko nyuma yao) kuboresha makazi yake.

TCRA:EPUKENI KUWEKA TAARIFA NYINGI ZINAZOWAHUSU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0
Na.Vero Ignatus. Arusha

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Katika kuadhimisha siku ya walaji duniani inayo adhimishwa kila mwaka machi 15,imetoa mafunzo kwa waalimu wanafunzi zaidi ya 300 katika chuo cha ualimu Monduli mkoani Arusha.

Akizungumzia Madhumuni ya kutoa elimu hiyo Kaimu meneja wa Mamlaka ya mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu amesema ni katika jitihadha zilezile za serikali za kuhakikisha kwamba inamlinda mlaji kwa kumpa elimu juu ya haki na wajibu wawatumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kuleta maendeleo.

Katika kuadhimisha siku ya walaji wameitumia kutoa elimu juu ya haki, na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano kama sehemu ya walaji,tahadhari za kuchukua katika mawasiliano hususani mitandao.

Msungu amesema kwamba walaji,ni kundi kubwa la kiuchumi ambalo huwa linaadhirika na kuathiri maamuzi ya kiuchumi yanayofanywa na mataifa na makampuni ya kibiashara."Sisi kundi hili la walaji ni kundi lile ambalo maoni yetu huwa suala la kusikilizwa kwa makini katika maamuzi ambayo yanafanywa ya kiuchumi" alisema.

Kwa upande wake Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaaya ametoa tahadhari kwa jamii kutokuweka taatifa nyingi zinazowahusu kwenye mitandao kwani siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la uhalifu ambalo wanatumia mitandao kufuatilia taarifa za watu.Jan amesema ni muhimu kuhakikisha unapoweka taarifa ako katika mitandao hii ya kijamii,usiweke taarifa zako nyingi zinazomiwezesha mtu kuzitumia hizohizo katika kukudhuru wewe mwenyewe.

Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex amezungumzia suala la uninuzi wa simu na kisema kuna sheria ya Mawasiliano ya kieletroniki na posta ya mwaka 2010/ambayo inamtaka mnunuzi wa simu kuhakikisha baadhi ya vitu kabla hajakabidhiwa simu.

Ahakikishe amepewa risiti,garantii ya mwaka mzima,auziwe simu ikiwa kwenye box lake,pia aangalie simu yake ni bandia ama la kwa kutumia *#06

Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu
Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaay akizungumza na waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kaimu mkuu wa chuo cha Ualimu Monduli Jesca Moiro akizungumza katika mafunzo hayo kama mwenyeji wa wanafunzi waalimu.Picha na Vero Ignatus Blog.Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini (wa kwanza kulia) Julius Filex akizungumza na waalimu wanafunzi katika chuo cha ualimu Monduli ,(kushoto )Afisa kutoka (TCRA) Osward Octavian akionyesha vitabu ambavyo ni muongozo kwa watumiaji wa mawasiliano.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Baadhi ya washiriki ya mafunzo hayo yaliyoandaiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA) nakufanyika katika chuo cha Ualimu Monduli mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALI MBALI WILAYANI RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Lindi katika kikao kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakati alipowasili kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali na ukarabati wa mabweni ya wafungwa leo tarehe 17 Machi, 2018 Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Cosato Chumi akizungumza wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Lindi katika kikao kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ndg. Rajab Bakari (kushoto) akifafanua jambo pale kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama ilipokuwa inakagua miradi mbali mbali na ukarabati wa mabweni ya wafungwa leo tarehe 17 Machi, 2018 Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Mussa Zungu
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Lindi katika kikao kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE

TAGCO WAIKUMBUKA SHULE YA FAMILIA YA MZEE LAIBON ILIYOPO MTO WA MBU MKOANI MANYARA.

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Laiboni iliyopo Mto wa Mbu mkoani Manyara ,Rashid Mohamed msaada wa Madaftari 2500 kwa ajili ya wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas wakigawa Daftari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon.
Mwenyekiti TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya kukabidhi Msaada huo.Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Laibon ,Rashid Mohamed wakati akikabidhi msaaada wa Matenki mawili ya kuhifadhia maji shuleni hapo .kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo.
Mwenekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza jambo na Wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon.
Moja ya majengo ya Shule ya Msingi Loibon iliyojengwa na Mfugaji wa Jamii ya Kimaasai,Loibon Ole Mapii baada ya Mungu kumjalia watoto Zaidi ya 200 na wajukuu Zaidi ya 400 na kulazimika kujenga shule kwa ajili ya familia yake.
Wenyeji wa eneo ilipo shule hiyo Jamii ya Wafugaji wa Kimasaai waliandaa Nyama kwa ajili ya ugeni uliotembelea shule hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari,Mawasilianona Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete na maafiwa Habar wenzake wakingojea kipande cha nyama .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Arusha.

MAKAMU WA RAIS AFANIKISHA UCHANGIAJI UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwezesha kupatikana kwa shilingi bilioni moja na milioni mia saba kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais aliwapongeza uongozi wa Wilaya ya Muheza na mkoa wa Tanga pamoja na wananchi kwa kuamua kujenga hospitali yao ya wilaya ili kuboresha hali ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Makamu wa Rais alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuimarisha ubora wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutoka kiwango cha vifo 66 kati ya vizazi hai 1,000 hadi kufikia kiwango cha angalau vifo 40 kati ya vizazi hai 1,000. Aidha, Serikali imedhamiria kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kutoka 556 kwa mwaka 2017 katika vizazi hai 100,000 hadi kufikia 292 ifikapo mwaka 2020.

Sambamba na hilo Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo tuna mkakati wa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya Vituo vya afya 208 ili kuimarisha utolewaji wa huduma mbalimbali za afya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza  wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
  aziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizungumza wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akizungumza wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela(kushoto) akimkabidhi Makamu wa Rais zawadi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchangiaji jana kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam​

BENKI YA CRDB YAJITOSA KUKISAIDIA CHAMA CHA MAAFISA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI (TAGCO)

$
0
0

Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akizungumza mara baada ya kuwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB ,Godwin Semunyu wakati wa mkutano huo. kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAGCO,Pascal Shelutete,Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamadunina Michezo,Susan Mlawa.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo.
Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada juu ya mfumo maalumu wa kadi za kielektroniki maarufu kama Credit Card ,huduma ambayo inatolewaa na Benki ya CRDB.



Baadhi ya Washiriki wa Mkutano mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu .






Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .

BENKI ya CRDB imeahidi kuendelea kukisaidia Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikali na kwamba kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji wa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati sahihi.

Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu wakati akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC) jijini Arusha ,sambamba na mkutano mkuu wa chama hicho (TAGCO) 

"Benki ya CRDB tunaamini "with right information" ambao hawa ni haki yao kuifikisha kwa wananchi ambao watakuwa aware nini kinaendelea,sio tu katika kutangaza nafasi za kazi kama baadhi ya watu wanavyofikiria ,pia wanahusika katika kutangaza Zabuni zilizopo,nafasi za Maendeleo,Nafasi za uwekezaji na sSehemu gani hasa unaweza kuwekeza kwa ajili ya maendeleo."alisema Semunyu.

Amesema Maafisa Habari wa taasisi za Serikali ndio daraja la kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi na kwamba kupitia kwao kila kinachofanyika ndani ya Serikali kitwafikia wananchi kwa njia na wakati sahihi.

"Kama alivyosema Msemaji Mkuu wa Serikali kwamba kuna tofaui kubwa ya kufikisha habari na kufikisha habari sahihi,kwa hiyo daraja hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa halipati heshima stahiki sasa litapa heshima."alisema Semunyu.

JAFO AGIZA MAAFISA HABARI SERIKALINI KUINGIA KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI imeziagiza Halmashauri kuhakikisha Maafisa Habari wanaingia katika vikao vya maamuzi ili waweze kupata na kutoa habari sahihi huku akiwatuhumu baadhi ya maafisa wa Halmashauri kuwa huendi ndio wanazuia maafisa habari kuingia katika vikao kwa lengo la kuficha baadhi ya taarifa.

 Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Serikaliza Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo wakati wa kufunga kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku tano.

 afo pia ameziagiza Halmashauri kutenga fungu katika Bajeti zao kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Maafisa Habari ili kusaidia katika kutekeleza majukumu yao kwa urahisi ya kuhabarisha umma shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali.

 Mapema katika hotuba yake Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi amesema kikao kazi hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwa Maafisa HABAI hao na kwamba kwa sasa watakuwa na uwezo mkubwa wa kuisemea serikali.

 Kikao hicho kimemalizika kwa Mgeni rasmi Waziri ofisi ya Rais ,Serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kutunuku vyeti kwa Wadhamini wakuu waliofanikisha mkutano huo pamoja na viongozi wa zamani wa Chama cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza wakati wa kufunga Kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanika kwa siku tano katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Sanaa ,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi akizungumza wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikali kilichofanyika jijini Arusha.
Waziri Jafo akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari ,Maelezo ,Dkt Hassan Abbas pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawa (hayupo pichani) .
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa kuhitimisha siku tano za Kikao kazi cha maafisa hao kilichofanyika jijini Arusha.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti kwa Mwenyekiti Mstaafu wa TAGCO ,Innocent Mungi ikiwa ni ishara ya utambuzi wa mchango wake katika chama hicho. 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti kwa Mmoja wa viongozi wa zamani wa TAGCO,Silvia Lupembe ambaye pia ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ,Morogoroikiwa ni ishara ya utambuzi wa mchango wake katika chama hicho. 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) Leila Muhaji kutambua mchango wa Shirika hilo katika kufanikisha kikao kazi cha maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano  Serikalini kilichofanyika jijini Arusha. 
Mgeni rasmi katika ufugaji wa Kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ,Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa kikao hicho.

MRISHO MPOTO AKOSHWA PROGRAMU YA UMILIKISHAJI ARDHI NCHINI,AKUTANA NA WANANCHI WALIOKABIDHIWA HATI ZAO

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali, kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Programu hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Programu hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga. Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.

Mpoto ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Mshairi huyo amesema baada ya kuzungumza na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao (viwanja na mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.

“Kwa miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme (LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho Mpoto.
“Binafsi kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii programu. 

Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii programu inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.

Alisema bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada atawasiliana wahusika kwaajili ya kutatua kero za wananchi.

Kazi nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi, Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.

Viongozi wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu iko katika Wilaya zao.

Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu hiyo na kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula nae alifanya ziara katika eneo la programu.

RAIS DKT MAGUFULI AMRUDISHIA PROFESA MAHALU HADHI YA UBALOZI

JAFO AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOA TATIZO LA OMBAOMBA MIJINI.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wakuu wa mikoa kubuni mikakati ya kuondoa tatizo la ombaomba mijini.

Waziri Jafo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam ambao umelenga kuvutia watalii mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya jiji hilo.Katika uzinduzi huo, Jafo amesema ombaomba hao wamekuwa wakikaa barabarani hali ambayo haileti sura nzuri kwa nchi na kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii nchini.

Waziri Jafo amesema changamoto ya watoto wa mitaani na tatizo kubwa la ombaomba ni vyema wakuu hao wakabuni mbinu mbalimbali zikiwemo za kuwawekea maeneo maalum ya kujihusisha na shughuli za ufugaji na kilimo cha bustani ili kuwaondoa mitaani.

“Tukifanya hivi tutakuwa tumefanikiwa kuondokana na kitendo cha wao kukaa barabarani kwa kuwa hakileti sura nzuri kwa nchi yetu kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii hapa nchini,”amesema Jafo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika uzinduzi wa Utalii wa jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika Uzinduzi wa Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam.
Kikundi cha sanaa kikitumbuiza kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mpango wa Utalii katika jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda pamoja na viongozi mbalimbali na wasanii katika uzinduzi wa Utalii wa jiji la Dar es salaam.
 

Twanga Pepeta waipania Tanga hatari

$
0
0
WAKALI wa muziki wa dansi nchini Tanzania, The African Stars Band, Twanga Pepeta 'Wazee wa Kisigino', wameipania vilivyo ziara yao ya Mkoa wa Tanga, wakisema wanakwenda kuonyesha makali yao halisi kwa mashabiki wao wa muziki, kwa kuanzia na onyesho la Ijumaa Machi 23, katika Ukumbi wa Tanga Hotel, jijini Tanga kwa kiingilio kidogo tu cha Sh 7,000.

Twanga wanapanda jukwaani ikiwa ni miezi kadhaa tangu walivyoenda katika Mkoa wa Tanga, maarufu kwa Wagosi wa Kaya, jambo linaloongeza mguso kwenye shoo zao zote za Mkoa huo kutokana na kiu kubwa ya wadau wao waliokuwa na shauku ya kuiona bendi yao hiyo ikiwa jukwaani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Twanga Pepeta, Martin Sospeter, alisema wanamuziki wao wamejipanga imara ili kudhihirisha makali yao katika tasnia nzima ya muziki wa dansi kwa kuongozwa na Luiza Mbutu, Kalala Junior, Haji Ramadhan, Msafir Diouf na wengineo wanaotamba kwenye bendi yao.

"Hakuna ubishi kuwa bendi ya Twanga Pepeta ndio alama ya muziki wa dansi nchini, hivyo ili kuonyesha umwamba huo wa kuimba vizuri, kupiga mdundo pamoja na kushambulia jukwaa, niwaombe mashabiki waje kwa wingi Ijumaa katika Ukumbi wa Tanga Hotel, kwakuwa ndio sehemu yetu ya kutangaza makali yetu.

"Mbali na onyesho la Tanga Hotel tutakaloanza mapema kabisa mishale ya saa 1 jioni, tutaendeleza dozi zetu katika Ukumbi wa Rombo Hotel Handeni Mjini siku ya Jumamosi ya Machi 24 na Jumapili ya Machi 25 tutawapa burudani mashabiki wetu wa Korogwe Mjini katika Ukumbi wa Mamba Club, huku kote viingilio vikiwa ni sh 7,000 tu," Alisema Sospeter na kuwataka mashabiki wao waende kwa wingi ukumbini kujionea umahiri wa bendi yao kongwe nchini.

Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi zinazotamba hapa nchini ikiongozwa na mwanamama Asha Baraka, huku ikiweza kujikita kileleni kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake, huku ikiwa na nyimbo kali kama Mwana Dar es Salaam, Mtu Pesa, Nazi Haivunji Jiwe, Marry na nyinginezo zinazotesa katika ulingo wa muziki wa dansi nchini.

WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMANA ILI WATENGENEZA FURSA ZA KIUCHUMI

$
0
0

 Mkurugenzi wa Taasisi ya I-learn East Afrika, Noelah Bomani (Kulia) akimkabidhi tuzo Mwanamke aliyefanya vizuri na kuwa kivutio katika mafanikio yake katika kipindi cha mwaka 2017/2018, Joyce Ibengwe Nangai ambaye ni Meneja Mawasiliano na Masoko  wa Chama cha Waajiri  Tanzania (ATE). (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada.
Mawenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko akizungumza kuwaelezea  uzoefu aliopitia na kuwasisitizia umuhimu wa kuchangaman ili waweze kutengeza fursa za kiuchumi hata kijamii wakati wa usiku wa Wanawake na tunzo kwa Mwanamke aliyefanikiwa kwa mwaka 2018 iliyoandaliwa na Tasisi ya Shangwe ambapo wanawake kutoka sehemu mbalimbali walikutana na kuzungumza mambo ya ujasilimali na namna ya kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Meneja Bima ya magari kutoka shirika la Bima ya Taifa (NIC) Emakulata Mwaitege, akizungumza umuhimu wa Wanawake kujiwekea bima katika biashara zao na maisha yao hili waweze kusimama tena pindi majanga yanapowakuta.
Muigizaji na  Msanii waTabasam PR Consultant, Regina Beraldo Kihwele akitumbuiza  katika kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mshereheshaji wa Kongamano hilo, Angela Kileo akiwajibika katika hafla hiyo. 
 Meneja mafao kutoka mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Rosemary Mchagula akileza umuhimu wa wanawake kujiunga na mfuko huo kutokana na mafao yanayotolewa katika kuwasaidi kwa kulitaja fao la uzazi. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shangwe Event, Deus Ntukamanzina.
Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo  akichangia katika mada zilizokuwa zkitolewa kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia matukio katika kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo  akichangia katika mada zilizokuwa zkitolewa kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. Kulia ni wazazi wa Afisa Mtendaji wa Shangwe Events, Deogratiasi Ntukamzina na Mke wake (wa pili kulia) 
Afisa Masoko wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Latifa Kigoda akileza ni namna gani wanawake wanaweza wakaungana na kuwa wawekezaji wakubw akatika mapinduzi haya ya uchumi wa Viwanda nchini.
 Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo kutoka TIB, Lisa Zavalla akichangia juu ya umuhimu wa wanawake kujikwamua kiuchumi katika mapinduzi ya uchumi wa Viwanda.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano hilo.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano hilo. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Uchui na Uwekezaji Nchini (EPZA) Grace Lemunge . 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya I-learn East Afrika, Noela Bomani akieleza umuhimu wa wanawake kuchangamana na watu mbalimbali hili waweze kujikwamua kiuchumi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri fursa ziwafate.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mwanasaikolojia na Mshauri wa masuala ya familia, Sadaka Said, akieleza umuhimu wa mwanamke kuambatana na mabinti zao katika maisha hili kuwajenga kwa ajili ya kesho yao kuliko kuwaacha nyumbani.
Afisa Mtendaji mkuu wa Shangwe  Event, Deus Ntukamanzina akizungumza na  Wanawake waliofika katika hafla hiyo na kuwashukuru kwani kukutana kwao ndio mwanzo wa wao kupiga hatua kubwa zaidi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Secrets Lingerie, Fatna Tambwe (kushoto) na Afisa Masoko wa Kimtandao wa Mult-Choice Tanzania Grace Mgaya wakifuatilia mada katika konganano hilo. 

SERIKALI INA MTAZAMO WA KUIFANYA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI KUWA SEKTA YA UZALISHAJI -ULEGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Hamis Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ameiambia kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji kuwa, Serikali ina mpango wa kuifanya sekta ya Mifugo na Uvuvi kuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa. 

Naibu Waziri HamisUlega ameyasema hayo leo Mkoani Kigoma mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, ilipokuwa katika ziara ya kutembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya kigoma jana. 

Mhe. Ulega amesema Wizara yake ina Mkakati wa kulinda rasilimali za Mifugo na Uvuvi, kwa kuimarisha uvuvi wa bahari kuu na kuitoa sekta hiyo kwenye kuchangia kiasi na shilingi Bilioni 19 kwa mwaka katika pato la taifa hadi kufikia kuchangia zaidi ya shilingi Bilioni 50 kwa mwaka. 

“Tunaweza kufikia malengo haya kwanza kwa kuimarisha uvuvi wa Bahari kuu kwa kuhakikisha kwanza tasisi yetu ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu inakuwa na nguvu kwa kuweka vizuri sheria na kanuni zetu za uvuvi ikiwa ni pamoja na kufufua shirika letu la TAFICO, Alisema Ulega.” 

Sambamba na hilo, Ulega alisema Serikali ina mkakati wa kuwa na Meli ambayo itakuwa na uwezo wa kwenda kuvua na kuchakata mazao ya samaki, jambo ambalo litakwenda sambamba na ufunguaji wa viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi. 

Naibu Waziri Ulega pia alisema serikali ina lengo la kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya Uvuvi kupitia mafunzo, utafitu na elimu ya ugani kupitia vyuo vya Feta , ili kuweza kuwa na wataalam wa kutosha pamoja na kuipa nguvu wakala hiyo ili kuweza kutoa wataalam kwani mpaka sasa sekta ya uvuvi ina uhaba wa wataalam na kuongeza kwa kusema kuwa kwa upande wa utafiti serikalii ina mkakati mkubwa wa kuweza kuiwezesha TAFIRI kwa kuipa kazi maalum za tafiti akitolea mfano wa uelewa mdogo wa baadhi ya wavuvi kuhusiana na zana halali za uvuvi. 

Akizungumzia suala la kuingiza samaki aina ya vibua na sato kutoka nje ya nchi, Ulega alisema, “Ukiangalia kwa makini sioni sababu ya kwanini tutoe mathalani kiasi cha shilingi Bilioni 50 kwa mwaka tuwapelekee wavuvi wengine na tuingize tani elfu 20 na zaidi kuleta hapa ndani za samaki ambao sisi wenyewe tunao.” Alisisitiza Ulega. 

“ Ipo Mikakati kwa serikali ya kuwatengenezea wafanya biashara ya samaki mazingira mazuri ili pesa hiyo iwekezwe hapa nchini.” Alisema. 

Awali akitolea mfano wa ulinzi wa rasilimali za uvuvi Ulega alisema “Tumefanya ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria kwa muda mfupi tu ikiwa ni pamoja na ulinzi wa utoroshwaji wa Mazao ya Uvuvi nje ya nchi na tumeingiza kiasi kikubwa cha fedha.” Alisema. 

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Sekta ya Uvuvi Dkt. Yohana Budeba alisema kuwa njia ya ufugaji wa samaki wa kisasa kupitia chuo cha FETA kitatengeneza wataalam na kuongeza ajira na kupatikana samaki wengi na kupelekea mchango mkubwa wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa taifa hili. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) kulia akiongea na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji ilipotembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana, wabunge wa kamati hiyo wameambata na maafisa mbali mbali kutoka serikalini.
Kushoto Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) akizunguma katika kikao na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana, kati kati ni mwenyekiti wa kamati Hiyo Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa (Mb.) Kalenga na kulia ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Christine Gabriel Ishengoma (Mb).
Pichani Mbele ni baadhi wa wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji wakifuatilia mazungumzo katika kikao wakati wa ziara yao katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana,wengine ni watumishi wa serikali.

Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

$
0
0
NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu', amesema anashukuru kwa kupata shoo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akisema kuwa anakwenda kwa watu wake wa nguvu kutokana na kufahamu kuwa wanaupenda muziki wake.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Msaga Sumu anayetamba katika muziki huo alisema kuwa wilaya la Handeni ni kati ya maeneo yaliyoupaisha muziki wake, simu chache baada ya kuibuka kwenye tasnia hiyo kutokana na watu wengi wakiwamo waendesha bodaboda waliokuwa wameziweka nyimbo zake kwenye vyombo vyao vya usafiri na kuzicheza muda wote.

Alisema hivyo shoo mbili alizopata kwa kuanzia Jumamosi ya Machi 24 asubuhi hadi jioni kwenye uwanja wa Mabatini, Mkata, wilayani Handeni pamoja na ile itakayofanyika usiku katika siku hiyo hiyo kwenye Ukumbi wa Rombo Hotel kwa kushirikiana na bendi ya Twanga Pepeta, ni sehemu ya kwenda kutuliza kiu ya mashabiki wake wa muziki wilayani humo, mkoani Tanga.

"Handeni nitaanza Mkata kwenye uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Machi 24 na baadae nitakuwapo Rombo Hotel, Handeni Mjini, nikiamini ni sehemu nzuri kwangu kutokana na nguvu ya mashabiki wangu kwa namna moja ama nyingine.

" Ni watu wa nguvu kwasababu wanaupenda sana muziki wangu, ukizingatia kuwa mimi msanii hivyo napaswa kufahamu mahala gani nakubalika ili kuhakikisha kuwa nalinda tbamani yao kwangu kama njia ya kuendelea kuniletea mafanikio katika kona ya muziki wa singeli ambao bila kuficha mimi ndio mfalme wao kutokana na uwezo wangu kimuziki,"Alisema Msaga Sumu.

Msaga Sumu anayetamba pia na nyimbo ya Mwanaume Mashine, Shemeji na nyinginezo, alitumia muda huo kuwataka mashabiki wake kuingia kwa wingi kwenye maonyesho mawili ya uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Mkata na lile la Rombo Hotel, ili wajionee mambo mapya kutoka kwake.

Ligi ya Handeni Kwetu Cup inaanzishwa na mdau wa michezo Kambi Mbwana, huku ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 24 na kufikia ukingoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku ikishirikisha timu mbalimbali za wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Mwisho

Viongozi Mkoa wa Iringa hamasisheni wananchi kutunza historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika – Mwakyembe

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (katikati) akizungumza na waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) alipofanya ziara katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bibi. Wamoja Ayubu
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bibi. Wamoja Ayubu
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na askari magereza wa gereza la Mgagao lililopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa alipotembelea gereza hilo jana kama moja ya kambi iliyotumiwa na wapigania uhuru kutoka Afrika ya Kusini wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza nyimbo za kihehe wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 
 Vijana walio na mchanganyiko wa kitanzania na Kizulu wakiimba wimbo wa taifa wa Afrika ya Kusini wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilolo wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa Lugalo alipotembelea mnara wa Lugalo walipozikwa Askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala
 Baadhi wa wananchi wa Kilolo wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyeshika mkuki) katika picha ya pamoja na wananchi wa Lugalo alipotembelea Mnara wa Lugalo walipozikwa Askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images