Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1540 | 1541 | (Page 1542) | 1543 | 1544 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituo hivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo ikiwa vitumike katika maeneo ya mkoa huo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
   Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
   Askari wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi kutoka Mkoa wa Polisi Kinondoni, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
  Moja ya Vituo Mwendo vya Polisi vilivyozinduliwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ambavyo vitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ametoa miezi miwili kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha linakamilisha uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kuwezesha jengo hilo kuhudumia abiria wengi zaidi kwa wakati mmoja.

  Ametoa agizo hilo, mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa jengo baina na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) na NHC na kusema kuwa kukamilika kwake kutawezesha abiria zaidi ya 100 kuhudumiwa kwa wakati mmoja ambapo kwa sasa jengo linahudumia abiria 35.

  “Mkataba tunaoshuhudia ukisainiwa leo unaitaka NHC kukamilisha mradi huu ndani ya miezi mitatu lakini niagize mradi huu ukamilike ndani ya miezi miwili kwa sababu fedha zipo na cheti mlichonacho cha daraja la kwanza kinaonyesha namna mnavyoweza kufanya kazi hii kwa haraka’ alisema Mhandisi Nditiye.

  Aidha Naibu Waziri Mhandisi Nditiye ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), pamoja na maboresho hayo kuhakikisha inafanya maboresho kwa kujenga maduka ya kubadilishia fedha na bidhaa ili abiria watakaotumia kiwanja hicho hiyo waweze kupata huduma mbalimbali wakati wanaposubiria kupanda ndege.

  Ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu ya Serikali hivyo miradi yote inayotekelezwa chini ya Wizara lazima izingatie viwango na thamani ya fedha ili kuendana na hadhi ya mji.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Antony Mavunde ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo na kumuomba Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, kuwafikiria wananchi waliopisha upanuzi wa kiwanja hicho kwa kuwalipa fidia mapema.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema Serikali inaendelea na mipango ya kuboresha viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga.

  Ameongeza kuwa Serikali imepanga kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa katika eneo Msalato ambapo kwa sasa wataaalam wanapitia usanifu wa kiwanja hicho na wakati wowote zabuni itatangazwa ambapo kiwanja hicho kitaweza kuhudumia ndege kubwa za kisasa kwani kinatarajiwa kuwa barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa Kilomita 4.5 mpaka 5.

  Awali akitoa taarifa yake kabla ya utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, amesema kuwa Fedha zinazotumika kukarabati jengo hilo ni fedha za ndani za mamlaka hivyo jengo hilo litakamilika kwa wakati na viwango.

  Uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma utagharimu takribani kiasi cha shilingi milioni 600 na utahusisha mifumo ya kisasa ya Tehama, mifumo na maji taka , mifumo ya matangazi ya ratiba za ndege pamoja na mgahawa.

  Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia), akioneshwa na Meneja Mradi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Focus Kadege, jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ambalo litafanyiwa uboreshwaji ili kuweza kuchukua abiria 100 kwa mara moja, Mkoani humo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa kuboresha jengo la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde, akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini wa uboreshaji wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege Dodoma, Mkoani humo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi (kulia waliokaa), wakisaini mkataba wa uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (kulia), Felix Maagi wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma mara baada ya kusaini, Mkoani humo. 

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
  Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
  Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.
  Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua kiwanda hicho. PICHA NA IKULU.


  0 0

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda 
  amepokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Vyama vya ushirika 27 vya Mkoa huo vilivyoguswa na kempeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.

  Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwa ajili ya Walimu. 

  Akizungumza baada ya kupokea mifuko hiyo Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri  na amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Tumaini Wilfred amesema wameguswa na jitiada zinazofanywa na Makonda katika  kuboresha mazingira ya walimu.

  Amesema ndio maana wameona umuhimu wa wao kama ushirika wasibaki nyuma  katika kufanikisha jambo hilo ambalo ni jema na na la ukombozi wa fikra na kuongeza ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na Makonda.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  wakwanza kulia akizungumza  machache leo jijini mara baada ya upoea kupokea  tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul  Makonda akiwa ameambatana na  viongozi mbalimbali wakiwasiri 
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul  Makonda  akipokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji  kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Tumaini Wilfred leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  akamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (MNH), Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (katikati) akitambulisha viongozi na wajumbe wa Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

  Viongozi wa kamati ya Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu wakijitambulisha.
  Viongozi wakifuatilia uzinduzi huo.
  Kiongozi kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakitoa mafunzo elekezi na wawezeshaji kwa kamati zilizochaguliwa.

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro (wa tatu toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa kamati mbili zilizochaguliwa.
  Picha/Habari: Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


  BODI ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Menejimenti yake imejiwekea mikakati mbalimbali katika mpango mkakati wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2022 unaolenga kuimarisha utawala bora ambao ni muhimu katika utekelezaji wa mikakakati mingine inayolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

  Amesema pamoja na ueledi wa kazi, uadilifu katika utumishi wa umma ni pamoja na kutokuomba rushwa au kutoa rushwa wakati watumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao. "Hospitali ya Taifa Muhimbili inaunga mkono mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa awamu ya tatu (2017-2022).

  "Nina imani kwamba kamati hizi zitatekeleza majukumu yake ipasavyo kuhakikisha kwamba mkakati huu unatekelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali," amesema Dk. Mkondya-Senkoro.

  Ameongeza utawala bora ni pamoja na kuwepo kwa uadilifu wa hali ya juu katika taasisi ambao kawaida unasimamiwa na Bodi ya wadhamini na pia kuzingatiwa kwa ukaribu na viongozi watendaji na watumishi katika taasisi husika.

  "Kwa mantiki hiyo, bodi ya wadhamini na Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na menejimenti yetu tumejiwekea mikakakati yetu ya miaka mitano na lengo kuu ni kuhakikisha tunaboresha huduma kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa," amesema.

  Amefafanua kamati ambazo wamezizindua leo ni kwamba ya kamati ya kwanza itakuwa ya uratibu ambayo itakuwa kamati ya uongozi itakayosimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti uadilifu katika hospitali hiyo.

  Amesema kamati ya pili ni kamati ya kudhibiti uadilifu ambayo ndio itahusika na utekelezaji na mikakati ya kudhibiti uadilifu na kuziwasilisha taarifa zake katika kamati ya uongozi kwa hatua zaidi.

  "Niwaambie kwamba wajumbe kamati hizi mbili wamepewa mafunzo elekezi na wawezeshaji kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  "Nina imani kubwa baada ya ya mafunzo kamati zitaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo kama yalivyoanishwa kwenye mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu," amesema.

  0 0

  Kamati ya Maadili ilikutana tarehe 14/3/2018 kupitia shauri linalomhusu Ndugu Michael Richard Wambura, Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ambaye anashtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa matatu ya kimaadili.

  TUHUMA ZILIZOWASILISHWA
  Sekretarieti ya TFF iliwasilisha mbele ya Kamati mashtaka matatu (3) ambayo ni;

  1.    Kupokea/kuchukua fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo  hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

  2.    Kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

  3.    Kufanya vitendo vinavyoshusha Hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015)

  MAELEZO YA KOSA

  Ndugu Michael Richard Wambura alichukua fedha isivyo halali kwa kughushi barua ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED ya kujipa mamlaka ya kulipwa kwa kula njama na waliokuwa Viongozi Wakuu wa TFF; Rais na Katibu Mkuu waliopita. Kitendo hiki ni kuvunja maadili na kushusha hadhi ya Taasisi ya TFF.

  SHAURI LILIVYOENDESHWA

  Ndugu Wambura alipelekewa wito wa kufika mbele ya Kamati siku ya tarehe 14/3/2018 ili awasilishe utetezi kuhusu tuhuma zinazomkabili. Ndugu Wambura alipewa hiari ya kutoa utetezi huo kwa mdomo, kutuma kwa maandishi, kuleta mashahidi au kutuma mwakilishi kama kifungu cha 58 cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013 kinavyoelekeza. Ndugu Wambura alimtuma mwakilishi wake, Wakili Emanuel Muga, aliyefika na kuthibitisha kuwa ametumwa na mteja wake (Ndugu Michael Richard Wambura) kuwasilisha utetezi wake mbele ya Kamati.

  Baada ya kuelezwa mashtaka yanayomkabili mteja wake, Wakili Muga aliiomba Kamati kuwa mteja wake anaomba kupewa muda wa kupitia shauri hilo ili aandae utetezi, vielelezo, na mashahidi. Mara baada ya kutoa ombi hilo Kamati ilimruhusu asubiri ili ipitie kabla ya kufanya uamuzi. Baada ya majadiliano wajumbe walikubaliana kuwa suala hili si geni kwa Ndugu Wambura; hivyo siyo kweli kuwa hana ufahamu nalo. 
  Pia moja ya vielelezo vilivyowasilishwa mbele ya Kamati ni utetezi wa maandishi wa Ndugu Wambura kuhusiana na suala hilo ulioandikwa 4/12/2017. Hivyo Kamati ilijiridhisha kuwa Ndugu Wambura anao ufahamu wa kutosha wa suala hilo na alikuwa na uwezo wa kufika mbele ya Kamati ili kutoa maelezo ya ziada.

  Kamati ilimjulisha Wakili Muga kuhusiana na uamuzi huo na kumtaka aanze kujikita katika kujibu mashtaka yaliyowasilishwa mbele yake. Hata hivyo Wakili Muga hakutaka kufanya hivyo na badala yake aliomba apewe muda zaidi wa kuandaa utetezi, vielelezo, na mashahidi. Kamati ilimkumbusha Wakili Muga kuwa wito wake ulijieleza vizuri hivyo ilikuwa ni wajibu wake kumshauri mteja wake ipasavyo na kumsaidia katika kujibu mashtaka yaliyofikishwa mbele yake. Baada ya maelezo hayo Kamati ilimuuliza Wakili Muga kama yuko tayari kuendelea na shauri au vinginevyo na yeye akaridhia kuwa shauri liendelee.


  Baada ya makubaliano hayo, Wakili Muga alipewa nafasi ya kujibu mashtaka matatu yanayomkabili mteja wake.


  Shitaka la kwanza:

  “Kupokea/kuchukua fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo  hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.”

  Sekretarieti iliwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa Ndugu Michael Richard Wambura alipokea malipo kutoka Chama cha Miguu Tanzania (FAT) na baadaye TFF ikiwa ni marejesho ya mkopo ambao FAT ilikopeswa dola la kimarekani $30,000 kutoka katika kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa michuano ya Kombe la Chalenji mwaka 2002. Mkataba wa deni hilo ulisainiwa na Ndugu Wambura akiwa Katibu Mkuu wa FAT. 
  Hata hivyo Kamati haikupata nyaraka wala kumbukumbu zozote zile zinazoonyesha kuwa Ndugu Wambura alipata idhini ya kukopa kiasi hicho cha fedha kutoka katika Kamati Tendaji ya FAT. Vilevile Kamati haikuona uthibitisho wa kiasi hicho kupokelewa kwenye akaunti za FAT zaidi ya Mkataba ambao ulisainiwa na Ndugu Wambura peke yake bila kuwa na shahidi mwingine kutoka FAT kinyume na taratibu za kawaida za mikataba. Vile vile Kamati imeshangaa ni taratibu gani zilitumika kwa taasisi kama FAT kuchukua mkopo mkubwa kama huo kwenye kwenye kampuni hiyo badala ya taasisi za fedha kama vile benki ambazo ndizo zinazojishughulisha na masuala hayo.

  Sekretarieti iliwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa Ndugu Wambura, kwa nyakati tofauti, alipokea jumla ya sh.84,000,000.00 kutoka FAT na baadaye TFF kama marejesho ya mkopo kwa niaba ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED. Hata hivyo Kamati haikupata uthibitisho wa kisheria kutoka kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED unaomuidhinisha Bw. Wambura kupokea malipo ya mkopo huo kwa niaba yake zaidi ya barua Kumb. Na. JKC/CONT/TFF/2014 ya tarehe 13/1/2014 kutoka kwa kampuni hiyo. Hata hivyo barua hiyo, licha ya kuandikwa miaka 10 baada ya Bw. Wambura kuchukua nusu ya mkopo huo, haikuwahi kupokelewa TFF na wala haikidhi matakwa ya kisheria ambayo ni kuwa na Power of Attorney iliyosajiliwa kwa Msajili wa Hati na Nyaraka.

  Kulingana na ushahidi uliowasilishwa na Sekretarieti malipo ya mkopo huo yalifanyika kwa awamu ambapo mara ya kwanza Ndugu Wambura alilipwa $15,000 alizopokea tarehe 29/4/2004. Hata hivyo Kamati ilibaini mapungufu katika fomu hiyo kwani maombi ya kulipwa fedha hiyo yalitolewa na Ndugu Wambura na kuidhinishwa na yeye mwenyewe, kinyume na taratibu za fedha.

  Malipo hayo ya mkopo hayakufanyika kwa kipindi cha miaka 10, chini ya Uongozi wa Ndugu Leodgar C. Tenga, mpaka alipoondoka madarakani na kuingia uongozi mpya chini ya Ndugu Jamal Malinzi ndipo yalipoanza kufanyika tena. Kamati inapata mashaka juu ya uhalali wa deni na malipo hayo kwani hakukuwa na madai wala malalamiko yoyote yaliyowasilishwa kudai au kukumbushia deni hilo kwa kipindi chote hicho. Katika hali ya kawaida siyo rahisi kulipa deni hilo bila kujiridhisha uhalali wake.


  Shitaka la pili

  “Kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.”

  Sekretarieti iliwasilisha nakala ya barua ya tarehe 21/6/2016 kutoka kwa Bibi Irene W. Maganga ambaye ni  mke wa mmiliki wa kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED, Marehemu Enock Maganga na mmoja wa wasimamizi wa mirathi ya marehemu walioteuliwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam. Barua hiyo inakanusha kuwa kampuni hiyo haikuwahi kupokea malipo yoyote ya deni hilo.
   Hii inaonyesha kuwa Ndugu Wambura hakuwahi kupewa mamlaka ya kupokea fedha hizo na pia hakuwahi kuziwasilisha kwa wamiliki wa kampuni hiyo fedha alizopokea kutoka FAT na TFF. Kwa msingi huo hata uhalali wa barua Kumb. Na. JKC/CONT/TFF/2014 ya tarehe 13/1/2014 kutoka kwa kampuni hiyo aliyoiwasilisha kuonyesha kuwa ameidhinishwa kupokea malipo hayo unatia shaka. Ndugu Wambura hajawahi kukanusha maelezo yaliyomo kwenye barua hiyo licha ya kupewa nafasi akiwa Makamu wa Rais wa TFF.


  Shitaka la tatu:

  “Kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015)”

  Kamati imejiridhisha bila shaka kuwa vitendo vya Ndugu Wambura vinashusha hadhi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF). Kitendo cha Ndugu Wambura kuiingiza FAT na baadaye TFF katika mkopo wa $30,000 bila kufuata taratibu zozote ni ukiukwaji mkubwa wa maadili. Vile vile kitendo hicho kimelipaka matope shirikisho hilo mbele ya umma kwani mambo aliyoyafanya hayaakisi ukubwa na umuhimu wa taasisi hiyo. Kwa nafasi yake ya Makamu wa Rais, Ndugu Wambura ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, hivyo vitendo hivyo haviendani na hadhi na majukumu ya nafasi yake hiyo.


  HUKUMU

  Kosa la kwanza:

  Kulingana na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013, Ndugu Michael Richard Wambura, amefanya kosa la kifisadi ambalo adhabu zake ni;

  (i) faini isiyopungua shilingi 10,000,000.

  (ii) kifungo cha cha kutojihusisha na mpira wa miguu kwa miaka isiyopungua 5

  Kama suala ni zito na limekuwa likijirudia rudia, kifungo cha kutojihusisha na mpira wa miguu maisha.

   Kosa la pili:

  Kwa kosa la kughushi kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013, kinatoa adhabu ya kifungo cha cha kutojihusisha na mpira wa miguu kwa miaka isiyopungua 5.


  Kosa la tatu:

  Kwa kosa la kushusha hadhi ya Shirikisho ni kwenda kinyume na Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015). Hili ni kosa la kimaadili ambalo adhabu zake zinaenda sambamba na adhabu nyingine zinazotolewa na Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

  Baada ya kupitia shauri hili na kuridhika pasipo na shaka kuwa Ndugu Michael Richard Wambura ametenda makosa hayo yote, Kamati imemfungia Ndugu Michael Richard Wambura kifungo cha kutojihusisha na mpira wa miguu maisha. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia uzito wa kosa lake kwa mujibu wa Kifungu cha 73(1)(c) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

  Kwa kuwa suala hili linahusisha masuala ya rushwa, Kamati inaielekeza Sekretarieti, kwa kupitia kifungu cha 6(3) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013, ilifikishe suala hili la Ndugu Michael Richard Wambura katika vyombo vya dola ili vifanye uchunguzi. Aidha Kamati inakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Ukaguzi kuwa waliokuwa viongozi wakuu wa TFF wakati malipo hayo yanafanyika, Ndugu Jamal Malinzi (Rais) na Ndugu Celestine Mwesigwa (Katibu Mkuu) nao waunganishwe katika uchunguzi huo.

  HITIMISHO
  Kamati haikupendezwa na taarifa zilizowasilishwa na Sekretarieti kuhusu juhudi zilizofanywa na vyombo mbalimbali kuizuia isifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015) na Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013. Kamati inaviasa vyombo hivyo kutoingilia mambo ya mpira wa miguu, hasa vyombo vya kimaamuzi, kwani athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa ustawi wa mpira wa miguu nchini.

   IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

  0 0

  Na Ripota Wetu, Blogu ya jamii

  KAMISHNA wa Uhamajia nchini, Dk.Anna Makakala na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemva wamemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuwapa fedha Sh.bilioni 10 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa ofisi za Idara ya Uhamiaji mkoani Dodoma.

  Kwa upande wake Dk.Makakala ametoa shukrani hizo kutokana na uamuzi wa Rais kutoa fedha hizo Sh.bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo ameagiza zijengwe ofisi za idara hiyo ambazo zitakuwa za kisasa.Dk.Makakala amefafanua tayari wameshapata eneo kubwa kwa ajili ya kujenga ofisi zao.
  "Sisi Idara ya Uhamiaji tunajukumu la kufuata taratibu zote kwa haraka iwezekanavyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liwe limekamilika kwsababu tayari fedha zipo,"amesema Dk.Makakala.

  Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Mwigulu Nchemba aambaye naye ametembelea eneo hilo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma Mjini, ambako ndiko patajengwa ofisi hizo ambapo naye amemshukuru Rais kwa kutoa fedha hizo.

  Dk. Mwigulu amemshukuru Rais, kwa kuwapa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji na tayari kwa sasa eneo kubwa lenye mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa Idara hiyo.
  "Tunashumkuru Rais Magufuli kwa kutoa fedha ambazo zitatumika kwenye ujenzi wa ofisi za Idara ya Uhamiaji ambazo zitakuwa za kisasa.Eneo ambalo tumepata ni kubwa na litatosha kujengwa ofisi hizo,"amesema Dk.Mwigulu.

  Amefafanua ni eneo ambalo lipo karibu na ofisi nyingine muhimu ikiwamo ya Ofisi ya vitambulisho vya Taifa, Zimamoto na ofisi nyingine za Serikali ambapo zitasaidia mtu anapofika eneo hilo kupata huduma kadri anavyohitaji.

  Dk.Migulu ametoa rai kwa idara ya Uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma.
  "Iwapo fedha ambazo Rais amezitoa wangefuata utaratibu wa bajeti basi ingechukua muda mrefu kuzipata lakini uchapakazi wao umemfanya Rais kutoa fedha hizo,"amesema Dk.Mwigulu.

  0 0

  Wananchi wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamempongeza Rais John
  Magufuli kwa wema wake katika kuwajali wananchi.

  Pongezi hizo zimetolewa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya cha Usa river kinachoboresha kwa kukijengea jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya daktari na maboresho
  mengine ya majengo ya kituo hicho.

  Katika ziara hiyo, wananchi walionyesha furaha yao kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha kuwajali sana kwa kuwafanyia maendeleo makubwa sana katika kituo cha cha afya. Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amewataka wananchi wa Arumeru kuendelea kushirikiana na serikali kwa hali na mali kwa ajili ya maendeleo yao na Tanzania kwa ujumla.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo akitoa maelekezo alipokuwa akikahua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
  Wataalam wa Afya wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha wakiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo huku wakionesha furaha yao baada ya kujengewa majengo mapya.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa wataalam wa ujenzi wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
  Moja ya majengo mapya yanayojengwa kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo akikagua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha unaoendelea.

  0 0


  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. WANG KE alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika
  Mratibu wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kushoto) pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Habari wakifuatilia majadiliano ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) na Balozi wa China nchini walipokutana kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia kitabu alichopewa na balozi wa China nchini Mhe. WANG KE (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo yanayohusu masuala ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer wakiangalia moja ya historia iliyoifadhiwa ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika baada ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam .
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimuonyesha Bolozi wa Umoja wa Ulaya (wapili kushoto) Mhe. Roeland Van de Greer pikipiki zilizotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika. Kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Harambee hiyo, Hassan Msumari na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamis Mgoda.

  Na Mwandishi Wetu

  MAKAMU  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.


  Akizungumza katika mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kuwa hafla hiyo itakayoanza Kesho Ijumaa saa 12 jioni  kwenye Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki, Dar es Salaam itaambatana na chakula cha usiku kwa wageni waalikwa.

  Hivi sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.

  Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

  Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

  Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.

  "Kesho tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.

  "Mgeni rasmi kwenye tukio hilo la harembee ya kuchangisha fedha atakuwa Makamu wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa wachangiaji ambao tumewapa kadi ya kuja kwenye harembee hiyo kila mchangiaji atachangia kuanzia Sh.milioni moja kwa walio na kadi.Na wote ambao tumewaalika kesho wana kadi za mualiko,"amsema.

  Amefafanua kwa wale ambao wanahitaji kadi ni vema wakawasiliana naye kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi ya 0713 341937 ili wapatiwe kadi huku akifafanua pia mbali ya wale ambao watafika kesho kwenye harambee hiyo pia wameandaaa utaratibu mwingine wa kuchangia ujenzi huo.

  Mhandisi Tumbo amesema ili kufanikisha ujenzi huo wanapokea mchango wa kiasi chochote cha fedha na hao wachangie kupitia Tigopesa au M-pesa kwa kutumia namba 395533 ambayo kumbukumbu namba ya kampuni ni 123.

  "Tunatambua jitihada za Serikali katika kutatua changamoto kwenye sekta ya afya, na hasa Muheza lakini kwa upande wetu tumeamua kuanza kwa kuchangishana, wapo wanaotoa fedha, wapo wanaochangia kokote, mchanga , saruji na vifaa vingine vya ujenzi.Tumeanza vizuri kwani tayari msingi wa wadi ya akina mama na watoto umejengwa na lengo letu hadi Oktoba mwaka huu tuwe tumekamilisha ili wananchi wapate huduma za afya.

  "Tukifanikiwa kuwa na Hospitali ya Wilaya Muheza mwananchi anayehitaji huduma za matibabu ya afya atakuwa na nafasi ya kuchagua aende kwenye Hospitali ya Anglikana au ya Wilaya.Niishukuru Hospitali ya Anglikana kutokana na kutoa huduma za tiba kwa wananchi wa Muheza,"amesema Mhandisi Tumbo.

  Pia amesema wakati wanaendelea kutafuta fedha kujenga Hospitali ya Wilaya ya Muheza, wanaendelea na jitihada za kujenga zahanati na ujenzi huo unaendelea kwa kasi kutokana na wananchi kuhamasika kuchangia ili kuondoa changamoto ya uhaba wa zahanati za vituo vya afya.
   Baadhi ya waandishi wa habari walihudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya 
  Golden Tulip katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Katikati ni Adam Ngamange Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), ambaye kwa asilimia kubwa alisaidia kuaandaa mkutano huo.
   Sehemu ya wanahabari hao
   Mkuu wa Wilaya, Tumbo akifafanua jambo ambapo aliwaomba wananhi kujitokeza kutoa michango kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Desderia Haule.
   Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo
   Mkuu wa Wilaya ya Muheza akijibu maswali ya wanahabari
   Wajumbe wa Kamati ya Harambe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano na wanahabari kwenye Hoteli ya Golden Tulip, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Juma Mgazija,  Mwenyekiti wa Kamati, Hamis Mgoda, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mwanasha Tumbo, Katibu Tawala wa Wilaya, Desderia Haule na Katibu wa Kamati, Hassan Msumari.


  0 0


   Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kinondoni Mjini,Mussa Embe akizungumza na waandishi wa habari nakufafanua kwamba mtaa wake unanyumba unanamba za nyumba nyumba 490 tu.
  Ally Abdi akinonesha nyaraka mbalimbali za nyumba hiyo aliyo
   
  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kitengo cha ardhi , imemtaka Msajiri wa Hati wa Wizara ya Ardhu,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuta mara moja hati namba 105525 wa Kiwanja namba 1003 kilichopo Mtaa wa Sekenke Kinondoni, chenye mgogoro uliodumu kwa miaka 10.

  Kiwanja hicho kilikuwa kinagombewa na wananchi wawili ambao ni Ally Abdi na Seleman Marashed kutokana na familia kukiuza mara mbili huku pia kikiwa na namba mbili ambazo ni 212 na 1003.Ofisi hiyo imebaini kunaupindishaji mkubwa wa taratibu za uuzwaji na upimaji wa kiwanja hicho ambacho kilikuwa ni mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

  Kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya mkuu wa mkoa kwenda Wizara ya Ardhi, iliyosainiwa na Ofisa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Edgar Msolla, ya Februari 15 mwaka huu, baada ya uchunguzi mzito kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni ilibaini kuwepo ukiukwaji wa sheria.Uchunguzi huo umekuja baada ya Abdi kuwasilisha malalamiko katika ofisi hiyo kuhusu kiwanja hicho namba 212 ambacho kipo kwenye mchoro wenye Survey Plan D1.503/23 wa mwaka 1994.

  Kiwanja hicho kina ofa iliyotolewa Aprili 18 mwaka 1964 kwa NHC ambao walikiuza kwa Moshi Majungu akiwa msimamizi wa mirathi ya baba yake Kondo Majenga.Abdi anadaiwa kununua kiwanja hicho mwaka 2004 kutoka kwa Moshi Kondo Majenga kwa niaba ya familia ya Kondo Majengo.Hata hivyo baada ya taratribu za mauziano hayo taratibu za kuhamisha miliki hazikukamilika.Imedaiwa kwa mara ya pili kiwanja hicho kiluzwa kwa tena na Moshi Mussa Majenga aliyeuwa msimamizi wa mirathi ya Kondo Majenga kwa Marshed mwaka 2008.

  Baada ya mauziano hayo taratibu za kuhamisha miliki zilikamilishwa.
  Katika hali ya kushangaza kiwanja hicho kilianza kutambulika kama kiwanja namba 1003 ambacho hakipo kabisa katika ramani ya eneo hilo lenye nyumba 490 tu.Inaelezwa Marshed alifanya upimaji pandikizi kwenye Survey D1.503/61 wa mwaka 2008 na kupata kiwanja kingine chenye namba 1003 juu ya kiwanja namba 212 hivyo kusababisha mgogoro mzito.

  Kiwanja hicho wakati kinamilikiwa na NHC kilikuwa kinasomeka NHC/KIN/SEK/212.

  Uchunguzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa umebaini kuwepo mkataba batili baina ya Marshed na msimamizi wa mirathi kwa kutumia mkataba uleule aliotumia kumuuzia eneo Abdi mwaka 2004. Imebainika kiwanja namba 1003 kipo juu ya kiwanja namba 212 na kwamba usajili wa kiwanja namba 1003 chenye hati namba 105525 katika ofisi ya msajili hakina hati halali.

  Kwa upande wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, ilimuandikia barua Kamishna wa Ardhi ya Agosti 21, mwaka 2017, ikisainiwa na Rehema Mwinuka kwa niaba ya mkurugenzi yenye kumbukumbu namba KCM/LD/51043/65/ARR, kwenda Ofisi ya Kamishna wa Ardhi ili kiwanja hicho kufutwa.

  Taarifa hiyo ya manispaa ilisema baada ya kupokea malalamiko ya Abdi, ikiwemo hukumu ya sheria namba 62/2009 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi, ofisi ilimtaka Abdi kuwasilisha malalamiko yake katika vyombo vya dola kama vile polisi na makama ili hatua stahili za kisheria zichukuliwe kwani jambo hilo linadalili za upatikanaji wa nyaraka na fedha kwa njia ya udanganyifu zisikokubalika.

  Ilisema ofisi ya manispaa iliendelea kufanya uchunguzi na kubaini kiwanja namba 212 kiliuzwa mara mbili na kuita pande zote mbili kwa mazungumzo.“Baadhi ya wanafamilia waliofika katika ya manispaa walithibitisha kuuza nyumba yao iliyopo katika kiwanja namba 212 kwa Abdi na kukataa kutoa ridhaa ya kwa msimamizi wa mirathi kuuza nyumba hiyo na kwamba msimamizi huyo alighushi saini zao,”ilisema taarifa hiyo.

  Pia ilieleza pamoja na kwamba Mahakama katika kesi namba 62/2009 ilimpa ushindi Marsged ofisi ya manispaa ilishauri hati iliyotolewa kwa Marshed ifutwe au iondolewe kwenye daftari la msajili wa hati na Abdi apewe haki yake.

  0 0

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imefanya ziara ya kutembelea mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kukagua miradi ya maji na umwagiliaji inayotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa lengo la kujionea maendeleo na changamoto ya kazi zinazofanywa na wizara hiyo kuelekea Bunge la Bajeti Mwaka 2018/19.

  Kamati hiyo imetembelea Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na kujionea mradi mkubwa wa majisafi na majitaka na eneo linalotarajiwa kujengwa skimu ya umwagiliaji.Ziara hiyo imehusisha wajumbe wa kamati 18 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mahmoud Mgimwa, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
   Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya GKW Consul, Michael Mwamkinga akitoa taarifa mbele ya wajumbe wa kamati, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Mahmoud Mgimwa, Mkuu wa Wilaya ya KIgoma, Samson Anga na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika chanzo cha maji cha Amani Beach, Kigoma.
  Mwenyekiti wa Kamati, Mahmoud Mgimwa (katikati) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso wakiwa pamoja na wajumbe wa kamati na wataalamu kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji katika eneo la kuendeshea mitambo.

  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiangalia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Kigoma Mjini.

  Moja ya bwawa la majitaka katika eneo la Luiche ambapo kumejengwa mradi wa majitaka wilayani Kigoma.
   

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

  MVUA za masika zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam jana ziliacha watu njia panda baada ya daraja linalounganisha maeneo ya Goba, Tegeta na Madale kukatika na kusababisha adha kwa wakazi hao.

  Mvua hizo zilianza kunyesha saa moja jioni hadi saa nne usiku ikiwa imeambatana na upepo mkali.Wakizungumza na Michuzi blog, leo jijini Dar es Salaam baadhi ya mashuhuda hao wamesema iliwalazimu kukesha katika maeneo hayo ili kulinda magari yao na wengine kutumia njia ya Tegeta A kufika majumbani kwao.

  Aidha wakazi wengi walibaki maeneo hayo hadi saa saba usiku ambapo kivuko cha dharura kwa watembea kwa miguu kiliwekwa.Hadi asubuhi ya leo hali imeendelea kuwa tete kwani kivuko kilichopo kinawafaa watembea kwa miguu na pikipiki hali iliyoleta adha kwa wanafunzi wa Atlas Madale ambao imewalazimu kuchukua muda mrefu kufika shuleni.

  Wakati hali ikiwa hivyo kwenye maeneo hayo,katika eneo la Jangwani Dar es Salaam zimebabisha daraja la eneo hilo maji kupita juu.Hali hiyo imesababisha usafiri kuwa mgumu kwa asubuhi ya leo kiasi cha mabasi ya mwendo kasi kusitisha kutoa huduma ya kusafirisha abiria.

  Hivyo imesababisha kuwa na changamoto kwa wakazi ambao wanatumia usafiri huo.Hata hivyo taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa huduma ya usafiri licha kusitishwa hatimaye imeanza na sasa mabasi hayo yanaendelea kutoa huduma.Athari za mvua zimesababisha kwa mara ya kwanza mabasi ya daladala za kutoka Mbagala-Kariakoo kuhamishiwa njia ya mbezi ili kusaidia kusafirisha abiria.

  Na kubwa zaidi daladala hizo ziliruhusiwa kupita barabara ya mabasi ya mwendo kasi.Hata hivyo hali ya foleni katika barabara ya Morogoro haikuwa kubwa kutokana na njia nyingi ambazo magari yanaingia kwenye hiyo kutoka katika makazi ya watu nazo hazikuwa zinapitika.Hivyo kupunguza idadi ya gari ambazo zingeingia barabara hiyo.
   
  WAKATI HUO HUO.
   
   Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inapenda kuuujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo zimerejea kuanzia saa 3:00 asubuhi tarehe 16/03/2018 baada ya kusitishwa kwa muda tangu saa 11:00 alfajiri kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Deus Bugaywa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART.

  0 0


  0 0


  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliifanyika leo katika viwanja jirani na ofisi za MUWSA.
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa juu ya utoaji wa Huduma ya Maji kwa mgeni rasmi ,Kippi Warioba katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro.
   Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Emanuel Kishosha akitoa maelezo kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba wakati wa maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa malipo ya Ankara za Maji kwa njia ya NMB Mobile.
   Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha Mti katika eneo la chanzo cha Maji cha Kaloleni.Jumla ya ya miti 500/imeoteshwa katika eneo hilo ikiwa ni msaada uliotolewa na taasisi ya Kilimanjaro Project.
   Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akiotesha mti katika eneo la chanzo cha Maji cha Kaloleni Mara baada ya kuzindua wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro ikibeba kauli mbiu ya "hifadhi maji na mfumo Wa kiikologia kwa maendeleo ya jamii"
   Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba(Wa Pili kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Malipo ya Ankara za Maji kwa njia ya NMB Mobile leo,uzinduzi ulioenda sambamba na uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mkoa wa Kilimanjaro.Wengine toka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Michael Mwandezi,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru,akifuatiwa na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha.
   Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akikagua baadhi ya mabanda ya maonesho yaliyopo katika viwanja vilivyopo jirani na ofisi za MUWSA.

  0 0

  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Vijijini Ndugu Castor Tindwa amemkabidhi bajaji mpya Ndugu Godfrey Saire mshindi wa promosheni inayojulikana kama Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa Tanzania wakishirikiana na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime vijijini alisema “Binafsi nimefarijika sana kwa maana huu mchezo upo na upo kihalali na kisheria, watu wengi wamenufaika sana kupitia mchezo huu mfano mzuri ni Ndugu Godfrey Saire ambaye amekabidhiwa bajaji yake”

  Hili ni jambo zuri na kuhamasisha kwa kampuni kama SportPesa kutushirikisha sisi viongozi wa serikali katika makabidhiano haya, kwani inaona na kutambua mchango wetu katika jamii, napenda kumpongeza sana Godfrey na naamini kupitia hii bajaji itakwenda kubadilisha maisha yake na familia yake kiujumla.Kwa upande wa mshindi Ndugu Godfrey Saire alisema “Nimeshawahi kushinda pesa taslim shilingi laki tano, laki tatu hadi laki moja kwahiyo niseme kupitia SportPesa imeweza kuniendeshea kipato changu kwa kiasi flani’

  “Nashukuru sana kwa hii zawadi itaenda itasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye ulipaji wa ada ya watoto wangu na kufanikisha shughuli zingine za kimaisha, baada ya kuchezesha droo nilipigiwa simu na hamisi tambwe ambaye alinipa taarifa juu ya ushindi wangu. Akaunti yangu ya Mpesa huwa natumia kuwalipa mafundi wangu kutokana na shughuli mbali mbali, natuma salio pamoja na kulipia bili mbali mbali.”Ikiwa zimebaki bajaji kumi mpaka kumalizika kwa promosheni hii,

  watumiaji wa mtandao wa Vodacom wanahamasishwa kushiriki ili kujishindia bajaji mpya aina ya Tvs King Deluxe. Ili kushiriki kwenye promosheni mteja wa Vodacom anatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa, kuweka ubashiri wake na moja kwa moja ataingia kwenye droo itakayompelekea yeye kushinda bajaji hiyo.

  Mshindi wa promosheni ya Jiongeze na Mpesa, Shinda na SportPesa, Godfrey Saire(aliyekalia Bajaj) baada ya kukabidhiwa bajaji na Mkurugenzi wa Wilaya ya Tarime Vijijini Castor Tindwa. Pembeni ni wawakilishi kutoka Kampuni za Vodacom na SportPesa.

  0 0

  BENDI kongwe ya muziki wa dansi hapa nchini, The African Stars Twanga Pepeta, inatarajiwa kuonyeshana ubabe na msanii wa muziki wa singeli anayetamba nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu' katika shoo ya uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup, utakaofanyika Machi 24, katika Uwanja wa Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga kuanzia asubuhi hadi jioni itakapomalizika mechi ya ufunguzi ya mpira wa miguu.

  Ligi hiyo inayoratibiwa na Kambi Mbwana kwa kushirikiana na Chama Cha Soka wilayani Handeni (HDFA), inasubiriwa kwa hamu na wadau wa michezo na burudani katika viwanja mbalimbali vya Kata wilayani Handeni, ambapo mbali na Twanga Pepeta na Msaga Sumu, wasanii wengine watakaotumbuiza ni Nyota wa Bongo Fleva, Top C, Bendi ya Handeni Super Makoba, wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa Handeni na vikundi vya burudani vya asili.

  Akizungumzia tukio hilo, Mbwana ambaye pia ni mdau wa maendeleo wilayani Handeni, alisema uzinduzi huo utaweka historia kutokana na mikakati kabambe ya kuhakikisha kwamba mashabiki wanapata kitu kizuri kutoka kwa wasanii na wacheza soka kwa ujumla.

  "Bendi ya Twanga Pepeta itakuwa na ziara Tanga Mjini kuanzia Machi 23 katika Ukumbi wa Tanga Hotel na Machi 24 usiku katika ukumbi wa Rombo Hotel, hivyo tumewaomba wakitoka Tanga, wapitie uwanjani Mkata ili wawape burudani ya dansi kwenye uzinduzi huo ambapo wameridhia.


  " Ukiacha Twanga ambao pia watafanya burudani wilayani Korogwe katika ukumbi wa Mamba Club Machi 25 siku ya Jumapili, pia Msaga Sumu atakuwepo uwanjani Mkata ili kuonyesha namna gani mwanaume atakuwa machine kama mashairi yake yanavyosema, tukiamini kuwa wasanii wote waliothibitishwa kuwapo Mkata kwenye uzinduzi huo watafanya vitu vya hali ya juu, hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kujipatia burudani," Alisema Mbwana.

  Kwa mujibu wa Mbwana, viingilio vya uzinduzi wa ligi hiyo Machi 24 Mkata vitakuwa Sh 3,000 kwa watu wazima na Sh 1,000 kwa watoto, huku onyesho la Handeni Mjini la Twanga Pepeta na Msaga Sumu Ukumbi wa Rombo likiwa ni sh 7,000, wakati lile la Tanga Hotel Machi 23 nalo ni Sh 7,000 kama litakavyokuwa onyesho la Korogwe Mjini Jumapili ya Machi 25 ambapo mashabiki wa bendi ya Twanga Pepeta watalazimika kulipa sh 7,000.

  Twanga Pepeta wameamua kuja mkoani Tanga kujibu kiu za mashabiki wao baada ya kutokuja muda mrefu, hivyo mashabiki wao wa wilayani Handeni, Korogwe na Tanga Mjini watapata sehemu nzuri za kuangalia makali ya bendi hiyo ambapo katika Ukumbi wa Mamba Club (Korogwe) na Tanga Hotel (Tanga), watakuwa peke yao jukwaani, tofauti na Msaga Sumu na wengineo watakaopanda jukwaani Mkata na Handeni mjini Machi 24.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott pamoja na Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto).

  Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott (wa pili kulia) 


  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). Waliombatana naye ni Mkurugenzi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohammed (wa kwanza kulia),  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto).


  Mkurugenzi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohammed (wa kwanza kulia)  
  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). Ameambatana na 


  Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott (wa pili kulia)


  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto).


  Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto) 
  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz).    Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto),    Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott (wa pili kulia)   Mkurugenzi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohammed (wa kwanza kulia)  
  Tigo Tanzania na Jumia wanaungana kutoa punguzo la hadi asilimia 60% kwa simu za kisasa

  Ofa za moja kwa moja hadi GB 18 za intaneti kutoka Tigo kwa kila simu itakayonunuliwa kupitia Mobile Week

  Dar es Salaam, 15 Machi, 2018.  

  Wateja watafurahia punguzo kubwa la bei hadi 60% kwa simu za kisasa (smartphone) kupitia Jumia Mobile Week (wiki ya simu) itakayofanyika kwenye mtandao wa manunuzi ya bidhaa wa Jumia (www.jumia.co.tz). Pamoja na punguzo hili kubwa la bei, simu zote za kisasa zitakazouzwa katika promosheni hii zitakuwa na ofa ya hadi GB 18 ya intaneti bure kutoka kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania.

  Katika uzinduzi wa gulio hilo la simu kwa njia ya mtandao, Jumia pia walizindua Ripoti ya Sekta ya Simu za Mkononi Tanzania inayoonesha kuwa asilimia 83% ya Watanzania walitembelea mtandao wa Jumia kupitia simu zao za mkononi, ikilinganishwa na asilimia 17% tu waliotumia kompyuta. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa Watanzania wengi wamevuka kigezo cha matumizi ya kompyuta na badala yake wanatumia teknologia ya  simu za mkononi kutekeleza shughuli zao za kila siku.

  Akitangaza ushirikiano huo kabambe jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Mobile Week itakayoanza 24 – 30 Machi ndio muda muafaka zaidi wa kununua simu ya kisasa kwa sababu simu zote zitapatikana kwa bei nafuu zaidi ambazo hazijawahi kutokea nchini, huku kila simu ikiwa na ofa ya hadi GB 18 za intaneti kutoka Tigo.

  ‘Tigo inaongoza katika mageuzi ya maisha ya kidigitali. Lengo letu ni kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wote wanapata huduma bora, za uhakika za mtandao. Huduma bora za kidigitali zinaanza na vifaa  bora, ndio maana ushirikiano wetu na Jumia utahakikisha kuwa kila mmoja anapata simu mpya ya kisasa pamoja na ofa za intaneti zitakazomwezesha mtumiaji kuwa sehemu ya maisha ya kidigitali,’ alisema.

  Akifafanua jinsi ya kupata ofa hizi za simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott aliwashauri wateja kutembelea tovuti ya www.jumia.co.tz ambapo watapata aina mbali mbali za simu kutoka kwa wauzaji mbali mbali. Baada ya hapo wanaweza kuchagua aina ya simu wanayoipenda na kutoa maelekezo ya sehemu ambapo wangependa kuletewa simu yenyewe na watoa huduma wa Jumia. Wasiokuwa na huduma za mtandao wanaweza kupiga simu namba 0800 710024 bila gharama yoyote ili kutoa maombi ya simu wanayoitaka. 
  ‘Nawahamasisha nyote mchangamkie ofa kabambe za simu zitakazopatikana katika mtandao wa Jumia katika kipindi hiki cha Mobile Week. Tunafurahia kuleta pamoja baadhi ya kampuni kubwa zaidi za simu duniani kama vile Tigo,  Samsung, Tecno na Infinix kushiriki katika gulio hili la kila mwaka. Kwa pamoja tumefanikiwa kuwaletea ofa ambazo hazijawahi kutokea kwa simu za kisasa, ikiwemo simu zenye uwezo wa 3G zitakazopatikana kuanzia TZS 50,000/- pekee na zile za 4G zitakazopatikana kwa chini ya TZS 150,000/- tu,’ Zadok alisema.


  ‘Wateja wana uhuru wa kuja kuchukua simu zao kutoka katika ofisi za Jumia ama wanaweza kuletewa simu zao mahali popote walipo. Malipo kwa ajili ya simu yatafanyika kwa njia ya Tigo Pesa au kwa pesa taslim mara tu baada ya mteja kupokea simu aliyoagiza na sio vinginevyo. Hii inaondoa hofu ya  kutapeliwa,’ Zadok alimaliza.

  Ukuaji wa simu za kisasa (smartphone) unatoa fursa kubwa kwa matumizi ya mtandao kutoa huduma mbali mbali kwa Watanzania kupitia mifumo kama Jumia. Hivi karibuni idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini ilifikia watu milioni 40, huku idadi ya wanaotumia mtandao ifikia watu 23 milioni.

  “Idadi ya watu wanaotumia simu za kisasa inakua kwa kasi siku hadi siku. Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya simu za mkononi, ila upatikanaji wa vifaa vya kisasa bado ni changamoto kubwa. Jumia imejikita kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata simu za kisasa, hasa katika kipindi hiki cha Mobile Week,” Zadok alibainisha
older | 1 | .... | 1540 | 1541 | (Page 1542) | 1543 | 1544 | .... | 1898 | newer