Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

BODI YA MFUKO WA FIDIA YA ARDHI YAZINDULIWA

$
0
0
Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi imezinduliwa rasmi mjini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi.

Akizindua Mfuko huo kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi; Naibu Katibu Mkuu; Dkt. Moses Kusiluka alisema, Mfuko wa Fidia ya Ardhi umeanzishwa kwa mujibu wa Kanuni zilizoundwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 kwa lengo la kuondoa kero za ulipaji wa fidia katika utwaaji wa Ardhi. 

Kuundwa kwa Mfuko huu ni hatua mojawapo muhimu sana katika kuiwezesha Serikali kutekeleza kwa ufanisi zaidi matakwa ya Sera ya Ardhi na sheria zake, hususan katika ulipaji wa fidia pindi ardhi inapotwaaliwa kwa manufaa ya umma.

Dkt. Kusiluka alisema; Bodi hii inatarajiwa kufanya kazi kwa karibu sana na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Mthamini Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Alisema; “Mkitekeleza majukumu yenu kwa ufanisi mtaisadia sana Serikali kukidhi matarajio ya wananchi katika kuwaletea maendeleo na kuwaondolea kero. Hivyo, ni imani yangu kwamba mtatumia weledi wenu katika kutekeleza majukumu yenu”.

Aidha, Dkt. Kusiluka alitoa wito kwa taasisi zote kuhakikisha kuwa mipango yote ya utwaaji wa ardhi inazingatia matakwa ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo. Aliendelea kusema kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi zake zote zitafanya kazi kwa karibu na Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.

Naye, mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko; Bwn. Martin Madekwe alisema kuwa anashukuru kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti katika Bodi hiyo na kuwa anatambua kuwa Bodi anayoiongoza inategemewa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu Mkuu. Alisema; “ Bodi tumejipanga kufanya kazi kwa ufanisi, uwazi, ueledi na uadilifu na tutajitahidi kuzingatia kuwa wale wote wapaswao kufidiwa, wanafidiwa ipaswavyo”.

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi, inaoongozwa na Mwenyekiti Madekwe, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Katibu wake ni; Grace Gulinja, ambaye ni Afisa Ardhi Mkuu katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akisoma Hotuba ya Waziri wa Ardhi; Mhe. William Lukuvi akiwa amemwakilisha katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi ( Mijini), Paul Luge na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo; Bwn. Martin Madekwe.
Wajumbe wa Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Kanali Mstaafu; Joseph Simbakalia, aliyewahikuwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, mmoja wa wajumbe katika Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi akionekana kwa karibu akifuatilia kwa Makini Hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi katika Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.


TRA YAWAPA SOMO WANAHABARI JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi, 2018.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Bibi Diana Masalla (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi, 2018. 
Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa baadhi ya Watendaji wa Mamlaka hiyo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), 3 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-SPRO-TRA HQ)

WAZIRI UMMY AIKABIDHI TIMU YA COASTAL UNION KIWANJA,AWAHIDI NEEMA

$
0
0

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga katika akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Coastal Union wakati akipokwenda kuwakabidhi kiwanja eneo la Maweni Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed


  Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni Jijini Tanga

 Diwani wa Kata ya Maweni(CCM) Colvas Joseph akizungumza katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu ya Coastal Union akizungumza katika halfa hiyo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga (TRFA) Saidi Soud kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
 Mwenyekiti wa baraza la wazee timu ya Coastal Union Salimu Bawaziri akizungumza 
  Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa TRFA Saidi Soud na Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto


 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa umakini Diwani wa Kata ya Maweni (CCM) Colvas Joseph
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akishiriki kucheza wakati wa halfa hiy
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameipongeza Kampuni ya City Plan kwa kuunga mkono juhudi zao za kutaka kuimarisha klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kwa kuisaidia kupata kiwanja chao eneo la Maweni Jijini Tanga.

Hatua hiyo inatokana na viongozi kufanya kazi kubwa wakishirikiana na wadau kuhakikisha wanapambana ili kuiwezesha timu hiyo kurudi kucheza michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kucheza madaraja ya chini kwa kipindi.

Kiwanja hicho ambacho kina ukubwa wa square mita 7632 kipo Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambacho kina gharimu kiasi cha sh.milioni 38 kimepatikana baada ya kuwepo kwa juhudi kubwa za Waziri Ummy kuiomba kampuni hiyo kuisaidia timu hiyo eneo lake la kiwanja.

Kukabidhiwa kwa kiwanja hicho  inafungua ukurasa mwengine wa mafanikio kwa timu hiyo kongwe hapa nchini.Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja hicho, Waziri Ummy alisema kitendo cha kampuni hiyo kutoa eneo hilo kimesaidia mipango iliyokuwa nayo timu hiyo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua nyengine.

Alisema suala hilo linatokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi waliopo wakiwemo wapenzi, mashabiki na wanachama huku wakiwataka kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya ligi kuu.

“Kwanza niwapongeze timu ya Coastal Union kwa kuonyesha mshikamano na kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu na kama mtu anafanya vizuri watu wengi wanakuwa tayari kuweza kuwaunga mkono “Alisema.

Alisisitiza kuwa kufanya vizuri kwa timu hiyo kumefanya kuvuta wadau ambao wameweza kuwasaidia kiwanja nawashukuru kwani wakati tunapongezana nilihaidi kuwatafutia wadau pia niwaambie bado tunaendelea kutafuta wadau  na nihaidi hata ile block yenye square mita 9600 yenye thamani milioni 48 atatafuta wadau ili waweze kupata eneo hilo.
Alisema atasaidia kutafuta wadau ili kupata eneo hilo ambalo litakuwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa Hosteli,Gym na Ukumbi wa sherehe wa Coastal Union kwa sababu watu wa Tanga wana fanya sherehe na kitchen party kila siku .

Hata hivyo alisema pia katika kiwanja ambacho wamekabidhiwa timu hiyo leo atagharamia gharama za hati za usajili mpaka kupata hati yenye jina la klabu ya Coastal Union na baadae atakwenda kuwakabidhi
Waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Tanga wanaotaka kuwekeza waende eneo la Pongwe ambalo lina viwanja 937 hivyo watu waende kuwekeza kwa sababu Coastal Union wakiwa hapo itavutia lakini pia ameitaka kampuni hiyo kuwepo kwa eneo kwa ajili ya zahanati kama walivyofanya kutoa kwa shule ya Msingi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mayeji alimpongeza Waziri Ummy kwa kazi kubwa kwa kuongea na wadau kuona Coastal Union inapata sehemu ya kufanyia mazoezi na mafunzo ya soka kwani jambo hilo linaonyesha namna alivyokuwa na dhamira kubwa ya kusaidia kuinua michezo mkoani Tanga akiwa namba moja Sports Lady namba moja.

Kwa hilo Mh Waziri umefanya kazi kubwa sana kwani hatua hiyo inaisongeza timu ya Coastal Union kwenye mafanikio kutokana na kupata eneo ambalo wataweza kulitumia kufanya mazoezi na masuala mengine ya kimichezo “Alisema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto alisema furaha kubwa aliyonayo huku akiimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia timu hiyo kwa hatua yake ya kuisaidia timu hiyo kuweza kurudisha heshima yaa soka mkoa wa Tanga

“Mh Waziri hapa nilipo nimeishiwa maneno ila nisema mama Ummy umetusaidia sana ulikuwa wapi siku zote kauli ya Mungu anasema nitakuwa muda na saa usizotarajia kila tunapofanyaa tukio kubwaa tunaona nyota inatuandama tulipata basi wakati tunapanda daraja kipindi kile safari hii tumepanda nyota nyengine imekuja kiwanja tuendelee kuomba na kushikamana”alisema.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud alisema tumehemewa na furaha kwenye jambo hilo ambalo ni la kihistoria kutokana na Waziri Ummy kuwa mama wa kweli kwa kuwashika mkono.

“Landa nisema Waziri Ummy ni mama wa kweli nakumbuka wakati unasema utatushika mkono huko mbele tulikuwa tunasuasua lakini ujio wako umesaidia kuvunja hata makundi yaliyokuwa yakirudisha nyuma maendeleo “Alisema

Akizungumza katika Halfa hiyop, Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema walipata ombi kutoka kwa Waziri Ummy Mwalimu kuona namna ya kupata eneo la Michezo kwa timu ya Coastal Union

Alisema baada ya hilo waliweza kulijadili na kuliwasilisha kwa wadau ambao ni wananchi wa eneo la hapa na kuweza kupatikana kwa eneo hilo ambapo pia walitoa viwanja cha mpira ni hamsini kwa mia moja lakini panazaidi ya eneo la pitch ya mpira.

Tulikubaliana kuhifadhi viwanja 16 upande block za chini kuna masuala wanaendelea na majadiliano vitalipiwa kwa ajili ya kuweka maeneo mbalimbali ya michezo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku alisema mambo hayo yote yanatokea kwa sababu watu wapo pamoja hiyo kuwataka kuendelea kushikamana kwa kumuomba mwenyezi mungu siku zijazo ili waweze kupata mafanikio zaidi.

Hata hivyo alisema uongozi ni uongozi huku akiwataka viongozi wasiogope kurushiwa maneno badala yake washirikiana kuhakikisha klabu hiyo inafanana na hadhi yake iliyokuwa nayo ya miaka ya nyuma.

Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema jambo ambalo limefanywa na Waziri Ummy ni nzuri na la kupongeza kwani msaada wake ndani ya timu hiyo ni mkubwa sana.

Alisema atajitahidi kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ili kuwasaidia kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa zaidi
“Lakini nimpongeza Mh Waziri kwa kutusaidia kufanikisha na kurudisha umoja na ushindi kwenye timu hiii, tuache na tusahau yaliyopita tugange yajayo “Alisema

(Habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya Tanga Raha)

TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

$
0
0
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo Pichani), kuhusu mapato na matumizi ya bandari hiyo, wakati Waziri huyo alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa gati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiangalia eneo ambalo linajengwa maegesho ya kawaida ya mizigo katika bandari ya Mtwara, alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari hiyo.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya mradi wa Gati katika bandari ya Mtwara. Gati hiyo yenye urefu wa mita 300 inatarajiwa kukamilika mwaka 2019 na upanuzi wake utagharimu kiasi cha shiliingi zaidi ya bilioni 100.
Mhandisi wa Bandari ya Mtwara, Eng. Twaha Msita ambaye ni (katikati), akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la mradi wa kuegesha mizigo ya kawaida, alipokagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari ya Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Karim Mattaka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Karim Mattaka (kushoto), alipokagua maendeleo ujenzi wa gati, Mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd (kushoto), anaejenga Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake mkoani Mtwara. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoani Mtwara, Eng Dotto Chacha. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Bw. Evod Mmanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na wakazi wa Nanguruwe Mkoani Mtwara alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha Lami.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazokwamisha mradi wa ujenzi wa gati mpya.

Prof. Marawa ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati mpya inayojengwa Mkoani Mtwara kwa ubia wa kampuni mbili za Kichina za China Railways Major Bridges Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) na China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na kubaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo.

“Hatuwezi kuendelea kuchelewesha mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mtwara, wakati fedha zipo na mikataba imeshasainiwa, naiagiza TPA kuhakikisha kuwa inatatua changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi mitatu ili mradi ukamilike kwa wakati,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na Wakandarasi wazawa chini ya usimamizi wa TPA isimamiwe kwa kuzingatia viwango na muda uliopangwa na kuahidi kurejea baada ya miezi mitatu kukagua maendeleo ya miradi hiyo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka amemuhakikishia Prof. Mbarawa kuwa TPA itasimamia kwa karibu mradi huo na kuhakikisha mapungufu yote yanafanyiwa kazi kwa wakati.

“Nipende kukuhakikishia Waziri kuwa TPA tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo na kuanzia wiki ijayo tutaongeza kasi ya kutatua mapungufu yaliyopo ili mradi huu ukamilike kwa wakati,” amesema Mhandisi Mattaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali amesema kuwa kwa sasa mradi wa ujenzi wa gati namba mbili (2) umefikia asimilia 15 na utakapokamilika utawezesha Meli kubwa na za kisasa aina ya Panamax kuhudumiwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwaka 2019.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua ujenzi wa Barabara ya Mtwara hadi Mnivata KM 50 na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kulipa madai ya Mkandarasi Kampuni ya M/s Dott Services ltd mapema iwezekanavyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

‘Nimhakikishie Mkandarasi kuwa madai yake aliyowasilisha tunajipanga kuyalipa ili kasi iwe kubwa na mradi huu ukamilike kwa wakati kwa kuwa umesubiriwa na wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa muda mrefu’ Amesisitiza Prof. Mbarawa.

Aidha, Mkandarsi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd amemhakikishia mhe. Waziri kuwa watahakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango kama ilivyoahidiwa.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) , Mkoani Mtwara, Eng. Dotto John ametanabahisha kuwa wakala umejipanga kuhakikisha unasimamia barabara hiyo kwa kuhakikisha viwango na ubora vinazingatiwa na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Prof. Mbarawa yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya miradi ya Miundombinu ya Barabara na Bandari.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

$
0
0
IMMAMATUKIO BLOG

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri kupeleka wakaguzi kwenye Shule ya Sekondari Joel Bendera iliyopo Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi.

Ni kutaka kubaini ukweli kuhusu matumizi ya fedha baada ya sh. milioni 150 zilizopelekwa shuleni hapo kumalizika, kabla ya ujenzi wa mabweni mawili kumalizika, huku tena zikihitajika sh. milioni 17 kumalizia ujenzi huo.

Chatanda alibaini hilo baada ya Machi 3, 2018 kufanya ziara kata ya Kwamsisi, na kusomewa taarifa na Mkuu wa Shule hiyo Nasson Msemwa kudai sh. milioni 150 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kujenga mabweni hayo ikiwa ni pamoja na kuweka samani, fedha zake zimekwisha.

“Mheshimiwa Mbunge, Serikali ilituletea sh. milioni 230, ambapo sh. milioni 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana na wavulana na sh. milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya manne. Fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tupo kwenye hatua za mwisho zimekwisha. Na ili tukamilishe mabweni hayo kunahitajika sh. milioni 17.

“Kwa upande wa ujenzi wa madarasa manne, bado tunakwenda vizuri, kwani pamoja na ujenzi kuwa kwenye hatua za mwisho, bado tuna sh. milioni 28” alisema Msemwa.

Chatanda alisema kwa uzoefu wake, tangu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, na sasa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhandisi Robert Gabriel, wamekuwa wakijenga namna hiyo kazi inakamilka na fedha inabaki, iweje kwao imekwisha kabla ya kazi kumalizika.

“Sisi tuna uzoefu, kwa pesa hizi mlizoletewa na Serikali, mnapowashirikisha wananchi kuchimba msingi, kuleta mchanga na kokote, huku mkitumia mafundi wa kawaida, fedha hizi zingetosha na kubaki. Hili sikubaliani nalo, na ninamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuleta wakaguzi ili kubaini ukweli wa matumizi wa hizi fedha.

“Mnataka tuonekane kazi hii ya kufanya vizuri kujenga madarasa na mabweni na kudhibiti matumizi ilikuwa inafanywa na mtu mmoja Robert Gabriel (sasa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Nina hakika Bodi ya Shule haikuwashirikisha wananchi ndiyo maana mabweni hayakuisha, lakini kama hamkushirikisha wananchi na viongozi wa vijiji na kata, ambao ndiyo wenye shule yao, maana yake kuna chembechembe za ubadhirifu” alidai Chatanda.

Diwani wa Kata ya Kwamsisi Nassor Mohamed alisema Bodi ya Shule awali wakati wanaanza ujenzi wa shule hiyo kwa njia ya msalagambo chini ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhandisi Gabriel, walishirikisha watu wote, lakini baada ya Serikali kuingiza sh. milioni 230 kwenye akaunti ya shule, mambo yalibadilika.

“Mwanzo walitushirikisha, lakini fedha zilipoingia Bodi ya Shule ilikuwa inafanya kazi peke yake bila kushirikisha viongozi wa vijiji wala kata, muulize Mkuu wa Shule huyu hapa, alikuwa mbogo pindi ninapomuulizia mambo yanayohusu fedha ama maendeleo ya ujenzi” alisema Mohamed.

Akijibu tuhuma hizo, Msemwa alisema hakuna fedha imeliwa, bali mabweni hayo ni makubwa tofauti na Shule ya Sekondari Mnyuzi, kwani kila moja linachukua wanafunzi 40, lakini yupo tayari kukaguliwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mji Korogwe Dkt. Elizabeth Nyema, ambaye alikuwa ameambatana na Chatanda kwenye ziara hiyo, alisema amepokea maagizo hayo na watayafanyia kazi.
Mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda (wa tatu kulia) akisikiliza taarifa inayosomwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Joel Bendera Nasson Msemwa (wa pili kushoto). Hapo ndipo Chatanda aliliamsha ‘dude’ kutaka kujua kwa nini sh. milioni 150 zimeshindwa kukamilisha mabweni mawili.Yussuph Mussa, Korogwe
Madarasa mapya manne ya Shule ya Sekondari Joel Bendera, Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Madarasa hayo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho kukamilika, Serikali ilitenga sh. milioni 80 kujenga madarasa hayo. (Picha na Yusuph Mussa).
Moja ya mabweni yaliyopo Shule ya Sekondari Joel Bendera Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Mabweni mawili yaliyojengwa shule hiyo, kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.PICHA ZOTE NA YUSSUPH MUSSA

SERIKALI YATOA BIL. 1.4 KUBORESHA VITUO VYA AFYA RUANGWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akichanganya udongo wa tofali, wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akifyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018,Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vitatu vya afya katika wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Machi 04, 2018) wakati alipotembelea kata ya Mandawa kwa ajili ya kukagua mradi wa uboreshaji wa kituo cha afya cha kata hiyo.“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”

Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. milioni 400 kwa ajili ya kituo cha Mandawa, sh. milioni 500 kituo cha Mbekenyera na sh. milioni 500 Nkowe.Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi huo chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.Pia Waziri Mkuu amekabidhi gari la kutolea huduma za afya vijijini. Gari hilo linauwezo wa kutoa huduma za afya kama Zahanati.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameshiriki katika zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Matambarare.Amesema kata hiyo yenye vijiji vinne ilikuwa haina shule ya sekondari, hivyo kusababisha wanafunzi kutembea umbali wa kilomita tano kwenda kusoma kwenye shule za kata nyingine.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI KITAIFA MKOANI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga (kushoto) wakiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanyamapori Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma juzi. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Wanyamapori jamii ya Paka wamo hatarini kutoweka- TUWALINDE”. (Picha na Hamza Temba-WMU).

MAKATIBU WAKUU 15 KUTAFUTA SULUHU ZA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ZIWA MANYARA NA TISHIO LA KUKAUKA KWAKE.

$
0
0
Lango Kuu la Kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara ambapo Makatibu Wakuu zaidi ya 10 kutoka Wizara mbalimbali wametembelea kujionea hali ya tishio lililopo la Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali katika kikao cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mwenyeji wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara kwa Makatibu Wakuu hao.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu hao .
Miongoni mwa Majengo yaliyokuwa yakitumika kama Vyoo katika Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara likionekana kuharibika baada ya maji ya Mvua yaliyoambatana na Mawe zilizonyesha miaka michache iliyopita. 
Muonekana wa majengo mengine yaliyokuwa yakitumika kama vyo kwa wageni waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara baada ya kuharibika kutokana na Maji hayo ya Mvua.
Sehemu ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu .
Mkuruenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (Mwenye kofia) akiwaonesha Makatibu Wakuu waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara maeneo ya Ziwa Manyara ambayo yameanza kukauka.
Eneo moja wapo la Vivutio vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara likionekana kuanza kukauka kutokana na Athari za kimazingira zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ,Kilimo Uchimbaji wa Madini katika maene ya jirani na Ziwa hilo. 
Viabda vinavyotumiwa na Wachimbaji wa Madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Moja ya Mtambo unaotumika katika shughuli za Uchimbaji wa madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ukiwa umehifadhiwa katika eneo mojawapo la Uchimbaji.
Maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji wa Madini umekuwa ukifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Kijana akifanya shughuli ya uchekechaji wa Mchanga katika moja ya mito inayo peleka maji Ziwa Manyara ,shughuli hi imekuwa ikifanyika kwa lengo la kujipatia Madini ana ya Dhahabu ,Hata hivyo zoezi hili linatajwa kuwa moja ya Uharibifu wa Mazingira unaochangia kukauka kwa Ziwa Manyara.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akiwanesha baadhi ya Makatibu Wakuu namna ambavyo athari za kimazingira zimeanza kuonekana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakitizama kwa mbali Ziwa Manyara.
Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wa serikali katika mikoa ya Arusha na Manyara mara baada ya kihitimisha ziara hiyo.Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI MBILI KWA JESHI LA POLISI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akikabidhi pikipiki mbili kwa Kamanda Mkoa wa Lindi, ACP. Pudensiana Protas, zilizotolewa na kampuni ya WU ZHOU Investment Company kwa Jeshi la Polisi, wakati alipo tembelea kituo hicho jana, Machi 4, 2018 , Wilayani Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA

$
0
0
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akipita katika kichaka kuelekea katika kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa nchi hizo mbili eneo la Horohoro.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akitafuta kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kwa kuchimba eneo ambalo kigingi hicho kilikuwepo katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga. Nyuma zinazoonekana nyumba zimejengwa katikati ya mpaka huo wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia baadhi ya nyumba zilizojengwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya katika kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkinga mbele ya nyumba iliyojengwa upande ukiwa Tanzania na mwingine Kenya, kuanzia diwani Hassan Bakari Ally (wa nne kulia aliyevaa kofia) kuelekea kulia wako upande wa Kenya.wengine ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki (wa pili kulia) na wa tatu kushoto ni mbunge wa jimbo la Mkinga Dustan Kitandula.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akioneshwa kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kilichowekwa wakati wa utawala wa muingereza na Mwenyekiti wa kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga Nassoro Mbarouk Nassoro wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akieleza jambo mara baada ya kupata maelezo juu ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha Saruji,nishati ya umeme joto, mabegi, vifaa vya ujenzi pamoja na bandari ndogo katika eneo la Mtimbwani wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki wakati alipofanya ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akipata maelezo kuhusiana na mpaka wa Tanzania na Kenya kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mahandakini Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga Nassoro Mbarouk Nassoro wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki na wa nne kulia ni Mbunge wa jimbo la Mkinga Danstan Kitandula.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi)

………………………………………………………………………..

Na Munir Shemweta, Mkinga Tanga

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.

Katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha umbali wa mita mia kama eneo huru.

Eneo lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake wamejenga nyumba zao zikiwa karibu kabisa na mpaka huku baadhi yake sehemu ikiwa upande wa Tanzania na nyingine upande wa Kenya.

Hata hivyo, Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshuhudia upande wa Tanzania katika eneo la Horohoro ukiwa umezingatia umbali unaotakiwa kati ya mpaka ukilinganisha na wakenya wanaoishi kijiji cha Jua kali Lungalunga ambao wamejenga karibu kabisa na mpaka wa Tanzania.

Kufuatia hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wakazi wanaoishi katika maeneo hayo ya mpakani kukumbwa na zoezi la kubomolewa nyumba zao ingawa kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea baina ya Tanzania na Kenya kuhusu umbali gani pande hizo zinaweza kukubaliana ili kunusuru baadhi ya wananchi wa pande zote mbili.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema, kwa sasa umbali unaotambulika kama eneo huru baina ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja ingawa kuna mazungumzo yanayoendelea katika ngazi ya wataalamu juu suala la umbali wa eneo huru.

Kwa mujibu wa Mabula, pamoja na sheria kuweka bayana kuwa umbali unaotakiwa katika eneo huru kati ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja lakini pande hizo zinaweza kukubaliana kama ilivyofanyika kwa nchi ya Uganda na Burundi ambapo kwa Uganda eneo huru litakuwa mita thelathini huku Burundi likiwa mita kumi na mbili na nusu.

Amesema, ukaguzi wa mipaka anaoufanya una lengo la kuhakikisha mipaka ya Tanzania na nchi jirani inakuwa katika hali nzuri hasa ikizingatiwa alama za mipaka zilizopo ni za muda mrefu huku baadhi yake zikiwa zimeharibika.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesisitiza kuwa, kwa sasa Tanzania haina mgogoro na Kenya juu ya mipaka na kinachofanyika ni kuimarisha usalama wa nchi zote mbili hasa ikizingatiwa njia za panya ziko nyingi.

Mabula amesema, awamu ya kwanza ya kuweka alama za mipakani itafanyika katika mipaka baina ya Tanzania na Kenya pamoja na mpaka kati ya Tanzania na Uganda na fedha yote kwa ajili ya kazi hiyo imeshatolewa kinachosiriwa ni kuanza tu kwa zoezi..

Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula kuwa Wilaya yake imekuwa lango la raia wanaokimblia afrika kusini, dawa za kulevya kama mirungi na mpango wa wilaya ni kutaka kufyeka miti na vichaka vilivyopo katika mpaka kati ya Tanzania na Kenya.

Aidha, amesema wilaya ya Mkinga ina tatizo la wahamiaji waloweza na zoezi la kuwatambua limeanza ili kuwabaini sambamba na kuthibiti vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amehitimisha ziara yake ya siku kumi na mbili mkoa wa Tanga, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na uhamasishaji ulipaji kodi hiyo ambapo ziara ilianzia mkoa Mara, Arusha na Kilimanjaro.

ASSEMBLY COMMENCES ITS SITTING IN ARUSHA

$
0
0

ASSEMBLY COMMENCES ITS SITTING IN ARUSHA


East African Legislative Assembly, Arusha, March 5, 2018: The East African Legislative Assembly (EALA) resumes its Sitting in Arusha, Tanzania, this week. The Assembly convenes for the Third Meeting of the First Session of the 4th Assembly, which commences today March 5th , 2018 and runs until March 23rd, 2018.

Key items at the Sitting include the debate on the East African Community Oaths Bill, 2017. The Bill anticipates the provision for the taking and administering of Oaths in relation to the specific persons appointed to serve in the Organs or Institutions of the Community or required to take oath before giving evidence at the East African Court of Justice. 

The Bill moved by the Chair of the Council of Ministers, Rt Hon Dr Ali Kirunda Kivejinja, avers that whereas there are specific persons who are required by the Treaty like in the case of the Judges and Registrars of the East African Court of Justice if in justice matters, or an Act of the Community like in the case of EALA Members, in all other cases, oaths of allegiance are administered and taken in accordance with staff rules and regulations or by practice. 

 The Bill which sailed through the First Reading at the recent Sitting in Kampala (2nd Meeting of the First Session) therefore hopes to cure the lacuna by providing for the administration of an oath as a statute.

In addition, the Report of the EALA on the on-spot assessment (tour) of the Northern and Central Corridors shall also be tabled and debated. The report follows the recent 13-day (February 12th-23rd, 2018) assessment of the institutions, facilities and installations of the EAC programmes in the Partner States undertaken by the Assembly.

At the tour, one team inspected the Northern corridor, commencing in Mombasa port and covering a total of 1,444 Kilometres to Kigali – through Nairobi, and Kampala. Another delegation of Members traversed concurrently, through the Central Corridor, from Dar es Salaam through to Bujumbura and eventually Kigali. Both teams then convened in Kigali, to crystallize the findings and for a wrap-up of the two-week tour.

The tour was initialised to enable Members to appreciate the operations of EAC Institutions and Authorities/Agencies that provide services, and the corresponding gains and challenges of integration. The tour also provided several fora to receive requisite feedback and recommendations from the citizens on their perception of the integration efforts so far.

Upon debate and if adopted, the Assembly shall provide the way forward in recommendations to be forwarded to the EAC Council of Ministers.

The Assembly also anticipates resumption of debate on the Address of the Chairperson of the EAC Summit of Heads of State delivered on January 23rd, 2018 at the Sitting in Kampala, Uganda. Delivering the speech, President Yoweri Kaguta Museveni reiterated need for the bloc to go full throttle and to unite the markets for prosperity of the people. 

The President remarked the region stood to gain much more as a unified front. He cited the strategic security as key in integration and called on the region to effect better use of the existing common natural resources for its own prosperity citing Lake Victoria as a case in point.

The Sitting is also to be interspersed in Week 1 by rigourous Committee work as well as further induction for Members largely on audited accounts and the EAC Budget processes and framework.

Mbio za Tigo Kili Half Marathon zafana mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro

$
0
0
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon upande wa wanaume, Gefrey Kipchumba kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:03 kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi jana. 
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni upande wa wanawake, Grace Kimanzi kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:13kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi jana 
Washiriki wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni wakiwa katika mashindano hayo mapema jana Mjini Moshi 
Babu Joram Mollel katikati akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo, pamoja na Mkurugenzi wao Simon Karikari kwa pamoja na kauli mbiu yao TUMETISHA KAMA BABU.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akiwa na mzee Joram Mollel maarufu kama BABU, mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 zijulikanazo kama Tigo Kili Half Marathon mapema jana. 
Mshindi wa upande wa wanawake mashindano ya kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon toka Kenya Grace Kimanzi (katikati) akiwa na washindi wa pili toka Tanzania Fainuna Abdi na mshindi wa tatu, Pouline Nkehenya toka Kenya, wakinyanyua mfano wa Hundi juu mara baada ya kutangazwa kushinda mbio hizo. Kushoto ni waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari mapema jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo TaKarikari Simon Karikari wakimkabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanaume, Gefrey Kipchumba toka Kenya leo kwenye viwanja vya Chuo cha Ushirika mjini Moshi.

UVCCM KIGOMA WAHAMASISHWA KUBUNI MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapindizi(UVCCM), Mkoa wa Kigoma wametakiwa kubuni miradi ya kimaendeleo kwa lengo la kupunguza kuomba misaada na kubwa zaidi kujiimarisha kwenye uchumi ili kuunga mkono kauli mbiu ya Uchumi wa viwanda.

Mwito huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa MNEC, Kilumbe Ngenda aliyekuwa mgeni rasmi, Katika Baraza la Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kigoma katika uchaguzi wa wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa na kumthibitisha Katibu wa uhamasishaji na chipukizi.

Ambapo aliwataka vijana hao kubuni miradi na kuendeleza miradi waliyonayo kama jumuiya nyingine zinavyo fanya na kuwataka kuwa na miradi yao binafsi ili kupunguza tabia ya kutembea na mabakuli kuomba.
Pia ameahdi kutoa mifuko 50 ya saruji ili wabuni mradi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda na kuiboresha nyumba ya wageni ambayo ipo chini ya vijana hao iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.Aidha Mbunge kupitia Vijana mkoa huo, Zainabu Katimba, amesema yeye kama kiongozi wa vijana ameamua kutoa Sh.milioni saba kwaajili ya kuwasaidia vijana Wilaya zote kuanzisha miradi ikiwamo miradi itakayohusisha viwanda.

Pia ametoa cherehani tatu kwa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Mwandiga na kuwataka waendelee na jitihada za kuhakikisha vijana wote wanakuwa na shughuli za kufanya na kila Wilaya wabuni miradi."Sisi viongozi tutahakikisha tunawasaidia kuwawezesha ili kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wengi,"amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Wa Kigoma, Silvia Sigura amesema wao wamejipanga kufanya siasa za uchumi na si siasa za maneno na kwa kudhihirisha hilo wmeanza harambee kwa vijana katika baraza lililofanyika na kufanikiwa kuchangisha mifuko ya saruji 130 ili kuanza kujenga vibanda 12 katika kiwanja chao.

Amesema kwa michango walioipata watahakikisha wanaanzisha miradi kwa kila wilaya na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili wajiajiri katika masuala ya ujasiriamali.

MNEC SALIM ASAS ATOA MILIONI 24 KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT WILAYA YA MUFINDI

$
0
0
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi. Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akikabidhiwa shati na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi baada ya kukabidhiwa kofia ambayo ameifaa hapo 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akifurahia jambo na viongozi wa chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.

Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati,Rose Tweve na mama Mwamwindi.

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya mufindi kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kujenga kipanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni sita ili mfikie malengo yenu.

“Sijaona changamoto ila nimeona matarajio ambayo ni kuanzisha mradi wa kuuza sare za chama,kumalizia ujenzi wa vibanda vya umoja wenu,kutafuta eneo la ekar 5 kwa ajili ya kilimo cha viazi na kupanda miche ya miparachichi na kutafuta kiwanja kikubwa kwa ajili ya uwekezaji na ndio sababu iliyonifanya niwachangie kiasi hicho cha pesa” alisema Asas

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba kwa kutoa kiasi cha silingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.

“Ametoa shilingi mioni sita kwa UWT na ametoa milioni kumi na nane kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kaleghela

ARUSHA WAENDELEA KUFANYA BIASHARA YA FILAMU ZISIZOFUATA TARATIBU NA SHERIA ZA NCHI


ALIYOYASEMA MSEMAJI WA SERIKALI MAPEMA LEO MJINI DODOMA

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA 2018 YAZIDI KUNOGA,WAIMBAJI WAENDELEA KUTAMBULISHWA

$
0
0
Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.

Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 yameendelea kunoga huku waimbaji mbali mbali wakiendelea kutambulishwa.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, RainFred Masako wakati akimtambulisha mwimbaji wa nyimbo za injili Martha Baraka.

Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.

Kwa upande wake mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Baraka amesema kuwa yupo tayari kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwa vile amejiandaa vyema."Tunaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa mjitokeze kwa wingi kuhudhuria Tamasha hilo ambalo nitaungana na waimbaji wenzangu kutoa burudani ya kukata na shoka," amesema Martha Baraka.

Tamasha hili linatarajiwa kufanyika Aprili 1-2, 2018 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Uwanja wa Halmashauri mkoani Simiyu,ambapo Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhando atazindua albamu yake mpya.

Waimbaji ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki ni Christopher Mwahangila, Jessica BM Honore. Wengini ni Solomoni Mukubwwa, Danny M- Kenya na Ephraim Sekeleti.

 Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka akieleza namna alivyojiandaa katika tamasha la pasaka 2018,mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani).Kushoto ni Meneja wa Msama Promotions Ltd,Jimmy Charles
Mmoja wa waratibu wa tamasha la Pasaka 2018, RainFred Masako akimkaribisha na kumtambulisha mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar

Airtel yazindua bando za uhuru zaidi kwa wateja ‘Yatosha Mitandao Yote

$
0
0


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mitandao yote nchini. 

Taarifa iliyotolewa na Airtel leo imesema bando za uhuru zinakuja baada ya serikali hivi karibuni kuweka punguzo kubwa la gharama za kuunganisha simu zinazokwenda mitandao mingine (interconnection rate) na hivyo Airtel kuona vyema kuwapa wateja wake fursa ya kufurahia punguzo hilo kupitia huduma yake itakayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Wateja wote watapiga na kutuma sms mtandao wowote nchini baada ya kujinunulia bando nafuu ya shilingi 1000 au bando mpya ya shilingi 600 tu.

 ‘Yatosha Mitandao Yote’ ni bando bora kuliko zote nchini zinazowawezesha wateja wa Airtel kujipatia vifurushi vyenye muda wa maongezi mara mbili zaidi ya  ilivyokuwa awali. Mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24, hapo awali kifurushi hiki cha shilingi 1000 mteja alipata dakika 25 tu. 

Vilevile kwa kifurushi kipya kimeongezwa faida ili kumpa mteja dakika 16, 2MB na 50 sms  kwenda mitando yote kwa shilingi 600 tu. Zaidi ya hapo wataendelea kujipatia vifurushi nafuu kwa SIKU, WIKI, MWEZI kwa kujiunga baada ya kununua vocha kwa kupiga *149*99# kisha chagua YATOSHA MITANDAO YOTE au kujiunga kupitia huduma ya Airtel Money na kufurahia Uhuru wa kuongea.

Akiongea jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindua wa Yatosha Mitandao Yote, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa “wateja wanabaki kuwa ndio nguzo kuu yetu kwenye biashara, ni furaha kubwa kwetu kuzindua huduma ya Yatosha Mitandao Yote ambayo itawapa wateja wa Airtel unafuu zaidi na uhuru  wa kutumia huduma za mawasiliano. Tunaendelea kufanya utafiti kufahamu mahitaji ya wateja pamoja na kuongeza ubunifu ili kuleta huduma nafuu zaidi ”

“Tunaipongeza serikali yetu kwa kupunguza gharama za kuunganisha simu mitandao mingine kutoka Shilingi 26.96 kwa dakika hadi shilingi 15.6 kwa dakika kuanzia januari, Airtel tunaona fahari sana kuwapa wateja wetu unafuu huo kupitia huduma yetu ya Yatosha Mitandao Yote. Mteja anatakiwa kuwa tu na laini iliyosajiliwa ya Airtel ili kufurahia huduma zetu bora na nafuu” aliezeza Colaso 

Yatosha Mitandao Yote inawafanya wateja kufurahi na kufanya mipango ambayo inayoendana na hali ya maisha na kutoa Uhuru wa kuunganisha familia, marafiki na wanafanya biashara kupitia mtandao wa Airtel kwenye mitandao mingine nchini kote na kwa muda wowote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa “Airtel tumeboresha upya huduma ya Yatosha bando ili kuongeza muda wa mangezi na kupanua uhuru  kwa  kutoa fursa kwa wateja kutumia huduma ya Yatosha Mitando Yote kwa kutuma sms, kupinga simu kwenda mitandao yote kwa kuanzia shilingi 600 tu. Ukiwa na Airtel Yatosha mahitaji yako ya mawasiliano yametimia!

“Kwa kujiunga na Yatosha Mitando Yote, wateja watatakiwa kupinga *149*99# halafu changua 3 ili kununua bando ya ‘Yatosha Mitandao Yote’ kulingana na mahitaji yako. Tuna uhakika kuwa huduma ya Yatosha Mitandao Yote itarahisisha maisha” alisisitiza Bi Singano

Yatosha Mitandao Yote ni moja ya bidhaa za Airtel Yatosha, Airtel hivi karibuni pia ilizindua bando za intaneti za Yatosha SMATIKA Intaneti ambayo inatoa 2GB kwa Tzs 2000 ambazo zinadumu kwa siku 3. Wateja wa Airtel wanaojiunga na Smatika bando wanajishindia simu mpya za smartphone, modem na 1GB kwa wateja 1000 kila siku.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania, Sunil Colaso(katikati), Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano(kulia) na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Sunil Colaso.

UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu, UNAMID.

Umoja wa mataifa UN umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.

Hayo yalibainishwa na mwakilishi Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Watoto (Special Representative of Secretary general of Child Abuse and AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha Amani.

“Sina budi kuipongeza Serikali chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani” Alisema Profesa Virginia.

Aliongeza kuwa kutokana na kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.

“ Najivunia Tanzania naweza kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.

Pia aliwataka Wananchi wa Sudan kuiga Mfano wa Tanzania waliowasha mwenge katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kuwa ishara ya Amani Afrika na kumulika dhidi ya maovu mbali mbali ikiwemo dhidi ya watoto kwa kuwasha moto wa amani utakaoangazia watoto wote wa Sudan.

Aliongeza kuwa ni wajibu wa Sudan kuuiga Tanzania kwa kuwasha moto wa Amani kwani wana kila sababu ya kufanya hivyo bila kutegemea msaada wowote kwani ni nchi yenye rasilimali nyingi za kiuchumi lakini kinachokwamisha ni Amani ili kujiletea maendeleo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa mataifa mbali na kutembelea vijiji mbalimbali alitembelea kambi ya Shangilitobaya inayokaliwa na Kikosi cha Tanzania chini ya kikosi cha 11 kinachoongozwa na Kanali William Sandy na kuwapongeza Askari wake kwa kazi nzuri ya Ulinzi wa Amani Duniani kote.

Tanzania kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linashiriki katika mpango wa Ulinzi wa Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa mataifa na Umoja wa Afika UNAMID nchini SUDAN ambayo sasa inaingia hatua ya Pili ambayo majeshi ya Tanzania yameunganihswa katika kikosi maalum ambacho kinaanza kazi katika safu za Milima ya jebel Marra Mashariki maeneo ambayo hayakunufaika kwa kufikiwa na UNAMID kwa kipindi chote.

Wanajeshi wa Tanzania hivi karibuni walipongezwa kuyafikia maeneo ya safu za Milima ya Jaber Mara na kufanya Doria ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa UNAMID na mashirika ya Umoja wa Mataifa kutokana na maeneo hayo kukaliwa na Waaasi na ubovu wa Miundombinu.
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima Mawe Khor Abeche Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Msafara Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya kijiji cha Shardai Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Shilingi Trilioni 1 Zatengwa Kulipa Madeni Mbalimbali Mwaka wa Fedha 2017/2018

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1 mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali ya watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameeleza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.
"Kati ya shilingi Trilioni 1 zilizotengwa kulipia madeni kwa mwaka huu wa fedha, shilingi Bilioni 896.3 zimeshalipwa kwa watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Serikali," alisema Dkt. Abbasi.

Amesema hesabu hiyo inajumuisha shilingi Bilioni 43 ambazo zimelipwa Februari, 2018 ikiwa ni malimbikizo ya wafanyakazi  wa sekta ya Umma. 
"Madeni mengine uhakiki unaendelea na yataendelea kulipwa siku zijazo na tutawajulisha," alifafanua Dkt. Abbasi.

Vile vile amesema, Serikali katika kuwaondolea adha ya usafiri kwa wananchi wa maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria. Kwa upande wa Ziwa Victoria,  mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwezi huu kwa ajili utengenezaji wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400.

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu. Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani hilo.

Aidha Dkt. Abbasi amesema Julai mwaka huu nchi itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi kote nchini.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images