Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Smartphone zaidi zatolewa Kwa Washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

$
0
0
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka,Agness Maganga(katikati)mkaazi wa Temeke akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam,  Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama .
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Farashuu Hasaan (katikati) mkaazi wa Zakhem akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam,  Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama .
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Issa Salum (katikati) mkaazi wa  Mbagala akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam,  Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama .
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Samwel Kivuge (katikati) mkaazi wa Mbagala maji matitu akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam,  Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama 


Dar es Salaam, Marchi 2, 2018 –‘Wateja 84 wa Tigo wiki hii wamejishindia simu za Smartphone aina ya TECNO R6. Hii ni Droo ya nne ya Promosheni inayoendelea ya Tigo NYAKA NYAKA inayowawezesha wateja wa Tigo kujishindia simu mpya za kisasa zenye uwezo wa 4G  na jumla ya simu 12 utolewa kwa kila siku.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama alisema “Hii ni sehemu ya kuwawezesha wateja wetu waweze kutumia simu za kisasa zenye  uwezo wa 4G ili wafuruhie kuperuzi intaneti na kuweza kuangalia  mambo mbalimbali kwenye simu zao”.
Aliongeza “Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu janja 800 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murua inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “.

Kwa upande wa washindi mzee  Issa Salum mkaazi wa Mbagala alisema “Sikuwa naamini mara baada ya kupigiwa simu nilijua matapeli wa mjini wenye kurubuni watu, baadae nikaamini nilipopewa maelezo yaliyojitosheleza” Naomba niseme hivi Tigo sio wababaishaji ni ukweli mtupu na nawashukuru kwa zawadi hii ya simu ya kisasa itakayoniwezesha kupiga picha na matumizi mengine mengi. Alimalizia kusema.

Nae, Farashuu Hassan mkaazi wa Mbagala alisema “Nilikuwa natumia simu yangu ndogo isiyokuwa na uwezo wa intaneti lakini sasa nimepata simu yenye uwezo mkubwa wa 4G ya TECNO R6, itakayoniwezesha kuingia kwenye Instagram, What’s App na kadhalika ili niwe wa kisasa kwenye ulimwengu wa mtandao”.

‘Washindi wetu wote 240 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi ya 800 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Bushagama alisema.

Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhi tiketi za ndege za watu wanne kwa ajili ya safari ya matibabu ya kijana Ahmed Albaity ambaye ambaye anakwenda kutibiwa nchini China kwenye Hospitali ya Beijing.

Albaity amekuwa akiteseka kwa zaidi ya miaka 10 akiwa kitandani kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu lakini leo hii Makonda amefanikisha ndoto yake ya kumkabidhi tiketi kwa ajili kwenda nchi humo akatibiwe.
Makonda mbali ya kukabidhi tiketi, pia amejitolea kugharamia fedha za matibabu na malazi na alitoa ahadi ya kumsaidia Albaity wakati wa mchakato wa upimaji afya bure kwenye meli ya Jeshi la China mwishoni mwa mwaka jana baada ya kugundulika kijana huyo anahitaji matibabu maalumu ambayo yanapatikana katika nchi ya China tu.

Hali hiyo ilimfanya Makonda kutokwa na machozi na kuahidi kumpeleka China akatibiwe kwa gharama yoyote ili maumivu na mateso anayoyapata yafike mwisho.Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu dola za Marekani 26,000 sawa na Sh.milioni 52.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi tiketi hizo,Makonda amesema Albaity atasafiri nchini China siku ya Jumapili akiongozana na watu wengine watatu wa kumsaidia ambapo gharama zake ni zaidi ya Sh.milioni 100.Makonda amesema shauku yake ni kugusa maisha ya kila mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema ahsante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu na kuongeza "Ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu.
"Na katika hilo watu wote watakuwa sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao na tunachokifanya ni sehemu ya utumishi wetu.Niwashukuru wote waliochangia kwa ajili ya kusaidia kufanikisha matibabu haya,"amesema Makonda.

Ametoa mwito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Albaity ili apone na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.Kwa upande wa Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu. 

"Wakati naomba watu wanichangie wapo watu waliokuwa wananivunja moyo kwa kuniambia siwezi kupona lakini Makonda ameonesha moyo wa kipekee,"amesema.

UHABA MADARASA WASABABISHA WANAFUNZI 346 KIDATO CHA KWANZA KUSHINDWA KURIPOTI SHULE WILAYANI KAKONKO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

JUMLA ya wanafunzi 346 wa kidato cha kwanza wilayani Kakonko mkoani Kigoma,wameshindwa kuripoti shuleni kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Hali iliyo walazimu viongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na wananchi kujenga vyumba viwili kwa kila shule.

Akitoa takwimu hizo jana katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko ya kutembelea ujenzi wa vyumba hivyo, Ofisa elimu sekondari wilayani humo Clouds Nzabayanga amesema miongoni mwa wanafunzi 1714 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza walishindwa kuripoti ni 346.

Amefafanua wanafunzi hao waliopangiwa katika shule ya Kanyonza, Muhange na Gwanumpu.Amesema katika shule ya Kanyonza kuna wanafunzi 78, Muhange 97 na Gwanumpu 171 ambao bado hawajapewa barua zao za kujiunga shuleni hapo hadi hapo shule hizo zitakapo kamilisha ujenzi wa madarasa hayo.

Ameongeza kila shule inatakiwa kujenga madarasa mawili kwa nguvu za wananchi na Serikali kuchangia mabati pamoja na ukarabati wa vyumba hivyo.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,amewapongeza Watendaji wa kijiji pamoja na Wenyeviti wa kijiji kwa juhudi kubwa walizozionesha za kuwashawishi wananchi kujitoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Amesema wameonesha namna ambavyo wanataka iliwanafunzi waanze kupata elimu kama wengine, na kumuagiza mkurugenzi kutoa fedha za mabati na ukarabati ili wanafunzi wapewe barua zao na waanze kuripoti shuleni.

Mkuu huyo alisema Serikali inatamani kuona kila mtoto anapata elimu lakini lazima wazazi wajitoe kutatua changamoto zinazo jitokeza kwakuwa Serikali haiwezi kufanya kila kitu na kutatua changamoto zingine na kuwaagiza Wenyeviti kupita kuchangisha fedha na michango mingine kwa wananchi ili watoto wao wapate elimu.

Ameahidi kuchangia bati 30 katika shule ya Kanyonza na bati 20 kwa shule ya Gwanumpu ambazo zimekwisha kamilisha ujenzi wa vyumba hivyo kwa kiasi na kuwataka walimu na wenyeviti kushirikiana kukamilisha madarasa mawili katika shule ya Muhange.

" Niwaombe wananchi mnapoambiwa elimu bure si kwamba hata kujitolea kwenye ujenzi mshindwe.Watoto ni wa kwenu lazima mnapoona Serikali haijakamilisha jambo fulani mfanye nyie."Suala hili ni letu sote lazima wanafunzi wote wapate elimu ni haki yao hakuna urithi mwingine tutakao waachia watoto wetu zaidi ya elimu.

"Lazima mtambue kunagharama lazima muingie kuhakikisha changamoto hizi zinakwisha", amesema Kanali Ndagala.Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa vyumba hivyo Ofisa Mtendaji Kata ya Kanyonza Johni Chondi amesema changamoto wanayoipata ni wazazi wengine kugomea michango wakidai yakuwa elimu ni bure.

Hivyo wanashindwa kuchangia hali inayosababisha kupata ugumu katika kazi hiyo.Amessema wazazi wanaulizia ni lini watoto wao na wao watapangiwa shule na kumuomba Mkuu huyo kumuhimiza Mkurugenzi mtendaji kupeleka bati na mbao alizo ahidi wakati wa Ziara ya mkuu wa Mkoa kwamba halmashauri itachangia bati na mbao na kukarabati wananchi wainue ukuta Serikali itamalizia.

FINCA yasherehekea kutimiza miaka 20 Jijini Dar es salaam kipekee.

$
0
0
 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Finca MicrofinaceTanzania , Issa Ngwegwe akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni ni Mwenyekiti wa bodi ya Finca, Mike Gama-Lobo  na Rais na Afisa mtendaji mkuu wa  Makampuni  ya Finca Duniani, Andree Simon.
 Rais na Afisa mtendaji mkuu wa  Makampuni  ya Finca Duniani, Andree Simon akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo.
Mwenyekiti wa bodi ya Finca, Mike Gama-Lobo  akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam leo.

Tarehe 2 Machi 2018, Dar es salaam: Benki ya FINCA Microfinance, moja kati ya benki maarufu zinazotoa mikopo midogo midogo nchini Tanzania, imefikisha miaka 20 tangu ianzishwe Tanzania.

Sherehe zinatarajiwa kuanza kwa hafla ya kupendeza na chakula cha jioni itakayokuwa imepambwa kwa rangi nzuri  katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
FINCA imesisitizia nia yake ya kuendelea kuwa taasisi inayoongoza katika ushirikishaji wa kifedha nchini. 

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 300 ambao ni pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa FINCA, Uongozi wa FINCA, wafanyakazi na viongozi wa juu kutoka katika mtandao wa FINCA Duniani. 

Raisi  na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon aliipongeza FINCA Tanzania kwa safari yake yenye mafanikio waliopata ambayo imewafikisha katika miaka 20 ya maendeleo na mabadiliko, yaliyosaidia taasisi hiyo kuendelea kuwa taasisi ya kutoa mikopo midogo na kufikia kuwa Benki ya kutoa mikopo midogo ilivyo sasa. 

Makamu wa Raisi wa Tanzania Mheshimiwa Samia Sululu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya chakula cha jioni kwa kusherehekea miaka 20 ya Benki hiyo.Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA ambaye pia ni Makamu  wa Raisi na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike Gama-Lobo aliwashukuru wajumbe wenzake wa Bodi na viongozi wa juu wa Benki kwa kuonyesha juhudi za kuigwa ambazo zimepelekea katika kukua kwa FINCA, kufikia maendeleo makubwa katika mazingira ya biashara yenye changamoto nyingi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe amesema:  "Mafanikio haya ya miaka 20 ni ushuhuda wa hamasa ya FINCA katika kutoa huduma za kifedha zilizokuwa salama na kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania
Akielezea kuhusu  hali ya ukopeshaji ya FINCA, Ngwegwe alisema: "Tangu FINCA ilipoanzishwa mwaka 1998, tumeweza kutoa zaidi ya TZS 900 Billioni katika mikopo kwa wajeja zaidi ya milioni 1.1  wakiwemo wajasiriamali wadogo, kukuza biashara zao,  kutengeneza ajira na kuboresha kiwango cha maisha. Katika miaka ijayo, tutaendelea kutekeleza wajibu wetu katika kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo (SMEs) ambao ndio msingi wa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.  

Aliongeza kusema zaidi kwamba FINCA ilikuwa imejidhatiti katika mpango wake wa kuondoa umaskini kupitia suluhisho la kudumu ambalo linasaidia watu kujenga rasilimali zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango chao cha maisha.
 


MAGARI 13 KUSHIRIKI MBIO ZA MAGARI MKOANI TANGA MAARUFU KAMA MKWABI TANGA RALLY 2018

$
0
0



Mratibu wa Mashindano ya Magari Tanzania,Faheem Ao akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na Mashindano hayo wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Mkoani Tanga Akida Machai
Mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Mkoani Tanga Akida Machai kulia akizungumza kuhusiana na mashindano hayo
Meneja wa Mkwabi Super Market ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo,Lawi Sozigwa


ZAIDI ya magari 12 yanatarajiwa kushiriki kwenye michuano ya Mbio za Magari ya Mkwabi Tanga Rally 2018 yatakayoanza leo Jumamosi na Jumapili kwenye eneo la Super Market ya Mkwabi Jijini Tanga kuzunguka maeneo mbalimbali mkoani hapa na kurejea yalipoanzia
Hayo yalibainishwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Mkoani Tanga (TMSC) Akida Machai wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kuelekea mashindano hayo. 

Alisema maandalizi ya mashindano hayo hivi sasa yanaendelea vizuri ikiwemo kufanya mazungumzo na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani,Jeshi la Zimamoto na Madaktari kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo . 

“Kwa kweli haya ndio mashindano ya kwanza tokea mwaka huu ulipoanza hivyo tutahakikisha yanafanyika kwa mafanikio makubwa kwa lengo la kutoa burudani kwa wakazi wa maeneo yatakapokuwa yakipita kama ilivyokuwa miaka ya nyuma “Alisema. 

Kwa upande wake,Mratibu wa Mashindano ya Magari Tanzania,Faheem Alo alisema msimu huu mashindano hayo yatakuwa ya aina yake kutokana na kufanya maandalizi mapema jambo ambalo limeongeza hamasa. 

Alisema mashindano hayo yataanza saa mbili asubuhi eneo la Mkwabi Super Market kuelekea eneo la Pongwe km 15 toka Tanga mjini na baadae kuelekea kwenye maeneo waliopangiwa kwa ajili ya kupita hivyo kuwataka wakazi wa Jiji hilo kuona namna ya kujitokeza kwa wingi kuweza kushuhudia namna madereva wanavyochuana. 

Aidha alisema kwa siku ya Jumapili mashindano hayo yataanzia Hotel ya Tanga Beach kuelekea Mkinga na baadae kwenda Duga Sigaya ambapo kwenye maeneo ambayo yatapita wananchi wametakiwa kuwa makini na watoto wao. 

“Tumejipanga vizuri kwenye masuala ya ulinzi na usalama kwa kuzungumza na askari wa usalama barabarani wakiwemo wa Jeshi laZimamoto kw lengo la kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa
mashindano hayo “Alisema. 

Hata hivyo aliwataka watu kuhakikisha wanazuia familia zao
zisijitokeze barabarani wakati mashindano hayo yanaendelea kwa lengo la kuepukana na madhara wanayoweza kukumbana nayo. 

Naye kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo,Lawi Sozigwa alisema kampuni hiyo imelenga kuhakikisha mchezo huo unapata mafanikio makubwa na ndio maana wakaona watoe mchango wao huo. 

Alisema pia watatumia mashindano hayo kuweza kujitangaza kwa jamii ya wakazi wa mkoa wa Tanga na nje ya mkoa kwa lengo la kuweza kutambulika zaidi. 

“Sisi kama Mkwabi Super Market tumekuwa wafadhili wa mashindano hayo na sasa ni mwaka wa pili huu hivyo nisema tu tunatumia nafasi hii pia kuweza kujitangaza “Alisema Sozigwa(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

JUKWAA LA WANAWAKE SOMANGILA, KIGAMBONI LAZINDULIWA LEO

$
0
0
Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Wanawake wajasriliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo  Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani katika soko.

Alivishauri vikundi vya wanawake wajasiriamali kwenda kuomba mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye mikopo ya riba nafuu.

Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.
 Wanawake wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kaya ya Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa uhuru FM Angel Akilimali (kulia) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Jukwaa hilo wakati wakipokea maandamano ya Wanawake wajasiriliamali kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo, leo
 Viongozi wa Vikundi mbalimbali vya Wanawake Wajasili na Jukwaa la Wanawake wakiwa tayari kupokea maandamano ya wanawake Wajasiriamali. Kushoto ni Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM angel Akilimali akipunga mikono
 Viongozi wakimwayamwaya kupokea maandamano hayo ,
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.
 Diwani wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Francis Chihi (kulia) akionyesha umahiri wa kusakata muziki pamoja na Kinamama wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo, leo
 Mwanamke Mjasiriamali wa kutengeneza vifaa vya ujenzi Amina Zakumera (kushoto) akimpatia maelezo ya utaalam wake Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali (Wapili kulia) alipokuwa akikagua bidhaa za Wanawake wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wanawake wa Kata ya somangila, Kigamboni, leo 
 Angel Akilimali akipata maelezo kuhusu bidhaa za mwanamke Mjarismali  Winifrida Jafari (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somanga, Kigamboni leo. Wapili kushoto ni Mjasiriamali Joha Amour wa Joha Fashion.

 Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto).
 Angel Akilimali (kushoto) akimuuliza Mwanamke Mjasiriamali jinsi anavyotengeneza bidhaa zake.
 Angel Akilimali na Diwani Chichi wakinywa togwa kwenye banda la maonyesho la Mwanamke Mjasiriamali, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni. 
 Wanawake wajasriamali wa Kata ya Somangila wakijimwayamwaya kucheza muziki kufurahia uzinduzi wa Jukwaa lao, leo
 Mtendaji wa Kata ya Somangila Munna Msafiri akitambulisha viongozi wa vikundi mbalimbali na Jukwaa la wanawake kutoka maeneo mbalimbali
 Viongozi wa Majukwaa ya Wanawake kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Kigamboni wakitambulishwa
 Diwani wa Kata ya Somangila Ndugu Chichi akifanya harambee ya uchangiaji wa fedha kutunisha mfuko wa Jukwaa la wanawake katika kata yake.
 Mkuu wa Polisi Kata ya Somangila Mwakila Chile akizungumza baada ya kutambulishwa na Diwani Chichi.
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akiungana na Wanawake wajasiriamali kusakata muziki wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akicheza ngoma na msanii wa kikundi cha Vijana wa Somangila wakati wa Sherehe hizo za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila 
 Mgeni rasmi katika Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya somangila Kigamboni Angel Akilimali akifurahia vijana walivyokuwa wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
 Kijana akiwa kihwa chini miguu juu, tena hewani wakati akicheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
 Wasani wa kikundi cha sanaa cha Vijana wa Smangila wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo.
 Mgeni rasmi katika sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, Angel Akilimali akinadi kiatu alipoendesha mnada wa vitu mbalimbali vya wanawake wajasriamali wakati wa sherehe hizo
 Mwekezaji wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akikitazama kwa makini kiatu hicho baada ya kukubali kukinunua kwa sh 50,000
 Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo.
  Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo
 Angel Akilimali akipongezwa na MC katika sherehe hizo
 Angel Akilimali akiwa na mtunza Fedha wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kigamboni Pili Doto mwishoni wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake kata ya Somangila
 Angel Akilimali (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa New Life Queen Bahati mwishoni mwa sherehe hizo
 Angel Akilimali akiwa na baadhi ya Wanawake wajasiriamali
Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la wanawake Kata ya Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Angel Akilimali akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jukwaa hilo katika kata mbalimbali za Kigamboni na Viongozi wa vikundi vya Wanawake wajasiriamali wa kata hiyo baada ya uzinduz leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA YATOA ONYO KALI KWA MATAPELI WA BIMA.

$
0
0
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima(TIRA) Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.   Vero Ignatus, Dodoma.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imetoa onyo kali kwa watu wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia bima za kugushi na hivyo kuwasababishia hasara na kuikosesha Serikali mapato,Matapeli hao ambao wengi wao hawana leseni za kufanya biashara ya Bima wametakiwa kuacha mara moja wizi huo kwani mkono wa sheria unawasaka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa bima katika Vyombo vya moto lililofanyika Mjini Dodoma ,Bibi Stella Guli Rutaguza amesema jumla ya magari 586 yalifanyiwa ukaguzi, ambapo  wamebaini  magari 25, pikipiki za miguu mitatu 5(bajaj) pikipiki za miguu miwili 2 yakiwa na Bima za kugushi huku magari mengine 19 yakiwa hayana bima.

 Rutaguza amesema kuwa wamefaminikiwa kuwakamata watu Wawili ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kuuza bima za kugushi kwa wananchi na tayari wako mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Bibi Stella Rutaguza amesema zoezi la kuwasaka watu wanaouza bima feki kwa na kuwaibia wananchi na Serikali ni endelevu hapa Dodoma na Nchi nzima kwa ujumla.

"Tunataka kukomesha tabia hii chafu kwenye Soko la Bima", hivyo tunawataka vishoka wa Bima popote walipo watafute kazi halali ya kufanya maana Mamlaka ya Usimamizi wa Bima haitawafumbia macho na mkono wa sheria hawataukwepa", alisema Rutaguza.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kutokuibiwa na matapeli hawa wa Bima kwa kununua Bima kwenye ofisi zilizosajiliwa na kupewa Leseni na Serikali kwa ajili ya kufanya biashara ya Bima na kuacha kununua Bima kiholela mitaani kwa watu wasiofahamika.

"Kuna wananchi wananunua bima faki kwa kutokujua na kuibiwa na watu hawa wasio waaminifu lakini pia tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wananchi wananunua bima feki kwa hiari yao wenyewe kwa sababu bima  hizo zinauzwa bei ya chini sana kuliko bima halali, Tukibaini kuwa ulinunua bima feki kwa hiari yako basi wote wawili mnunuzi na muuzaji mtaakuwa na hatia ya kupanga njama  za wizi na utapeli wa kuiibia Serikali mapato Yake Sheria itawashughulikia wote." alisisitiza.

Amesema kuwa Mteja wa Bima au mtu yeyote anaweza kuhakiki bima aliyonunua kama  ni halali au ni feki kwa kutumia njia ya mfumo wa TIRAMIS. Mfumo huu umetengenezwa na Mamlaka kwa ajili ya kudhibiti wezi wa mapato ya Bima za vyombo vya moto kwa Serikali,
Makampuni ya Bima na pia kumrahisishia Mwananchi kuepuka kuibiwa fedha zake.

Meneja huyo wa kanda ya kati Stella Rutaguza pia ametoa rai kwa wafanyabiashara wa bima kufuata sheria na miongozo ya ufanyaji biashara hiyo kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009 na hivyo kuepusha usumbufu kwa Wananchi wakati wanapotakiwa kupata fidia ya bima.

Amesema kuwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za utendaji na kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa wananchi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na Mamlaka kumfutia leseni yake.

Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA)  kanda ya kati ,Adamu Maneno (katikati)akihakiki stika ya bima kama ni halali au feki stendi ya  Hiace jamatini Dodoma,kulia kwake ni PC Majenga,kushoto kwake ni Liberath wakala wa bima mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kati Rojas Msagati (katikati)akiwa anahakiki moja ya gari katika stendi ya jamatini Dodoma ,kulia.kwake ni WP 4079CPL Karitas.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Haule Reward, Meneja Dodoma Jubilee Insurance .
Muonekano wa Stendi ya hiace Jamatini Dodoma.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani G.8922PC.Bashiru wa kwanza kushoto,pamoja na H.5987PC Majenga walishirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kati katika zoezi la ukaguzi wa bima kanda ya kati.
Baadhi ya vyombo vya moto vilivyokamatwa vikiwa katika kituo cha Polisi Dodoma.Picha na Vero Ignatus Blog

NAMNA YA KUHAKIKI BIMA YAKO YA GARI:

 *************************1. Kwa kutumia ujumbe wa simu: Nenda kwenye uwanja wa kutuma ujumbe mfupi, andika neno Stika, acha nafasi, andika namba ya Stika ya Bima, Tuma kwenda namba 15200.

2. Kwa kutumia mfumo wa TIRAMIS.

Pakua (download)  TIRAMIS kwenye simu yako, Bonyeza (click) neno Tiramis, utakuja Uwanja wa TIRAMIS kwenye simu yako ambapo utaona Maneno yanayokueleza hakiki hati  ya bima ( validate insurance covernote) na Maneno mengine yanasema hakiki Stika ya Bima  (validate insurance sticker) Kuhakiki hati ya Bima unahakiki kwa kutumia namba ya gari lako.

Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza hapo kwenye validate insurance cover,  utaandika namba yako ya gari halafu utabonyeza neno hakiki  (validate) baada ya hapo utapata Maelezo ya Bima ya gari unayohakiki.

Unaweza pia Kuhakiki kwa kutumia stika ya Bima yako. Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza neno validate insurance sticker(hakiki Stika ya bima),andika namba yako ya Stika  halafu bonyeza neno validate(hakiki). Baada ya hapo utapata majibu yanayokueleza kuhusu hiyo Stika ya Bima. Majibu utakayopata kwenye Kuhakiki bima kupitia namba ya gari na Kuhakiki kupitia namba ya Stika ya Bima yote yanafanana kama. Majibu yanakuwa na Maelezo yafuatayo:-

1. Utaambiwa uhai wa bima hiyo.
2.Bima imekatwa kwa Kampuni gani.
3. Namba ya gari. iliyokatiwa bima hiyo.
4.Aina ya Bima kwa mfano ni Comprehensive au thirdparty.
5.Namba ya Stika.
6. Aina ya Stika kwa mfano, ni private,public service, n.k.
7. Bima ni halali mpaka tarehe ngapi.

MUHIMU: Ukiona majibu unayoyapata unapohakiki bima yako ni tofauti na Maelezo ya Bima unayohakiki kwa mfano tofauti ya namba ya gari,Kampuni ya Bima iliyokatiwa bima hiyo, namba ya stika, muda wa kuisha bima hiyo n.k. wasiliana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka ili kukuepusha   kupata hasara.



TUTAENDELEZA UTALII WA PICHA KATIKA PORI LA AKIBA BURIGI - DK. KIGWANGALLA

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Twiga katika fukwe za ziwa Burigi ndani ya Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera.
Baadhi ya Twiga wanaopatikana katika Pori la Akiba Burigi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Malmlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata kuhusu mipango mbalimbali ya mamlaka hiyo kuendeleza utalii katika Pori la Akiba Burigi alipotembelea pori hilo jana mkoani Kagera.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari fukwe ya ziwa Burigi kwa kutumia darubuni alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka ngazi kwa ajili ya kukagua fukwe za ziwa Burigi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki kusukuma boti iingie kwenye maji kwa ajili ya kunza ziara ya kukagua fukwe za ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga kasia tayari  kwa kwa kuanza Safari ya boti kwa ajili ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana. 
Ndege aina mbalimbali pia ni kivutio katika pori hilo.
Viboko nao wanapatikana katika pori hilo ndani ya ziwa Burigi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti baada ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Utalii wa fukwe ni moja ya kivutio muhimu cha utalii katika pori hilo ambapo watalii hupata fursa ya kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo viboko, simba, tembo, pundamilia na ndege aina mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti baada ya kukagua fukwe ya ziwa Burigi alipotembelea Pori la Akiba Burigi mkoani Kagera jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi.
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na watumishi wa Pori la Akiba Burigi.
Picha ya pamoja. (Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Malisili na Utalii)

MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL KILICHOKO MKOANI TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, TANGA.

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amekitoza faini ya shilinhgi milioni 35 (milioni thelathini na tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange Mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

Naibu Waziri Mavunde, alikuta wafanyakazi wa kiwanda hicho ambacho kina mashine nyingi na kutokana na mfumo wa utendaji kazi wake, kinatoa kelelenyingi hawakuvaa vifaa vya kujikinga na madhara kazini, (protective gears).

Mhe. Mavunde aliwakuta baadhi yao wakiwa wamevaa kandambiloi, wengine hawana vifaa vya kuziba masikio kujihami na kelele, pamoja na vifaa vingine. Hatua hiyo ilimkasirisha Mhe. Navu Waziri na kumuagiza Afisa wa OSHA, kuchukua hatua mara moja ambapo kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 35 kwa kukiuka Sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo pamoja na mambo mengine inasisitioza usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi kuvaa vifaa vya kujihami.

Aidha Mhe. Mavunde ambaye kabla ya kufika Mkoani Tanga, alitembelea mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kilimanjaro, ameuagiza uongozi wa kiwanda hivho kuondoa kasoro hizo mara moja.Sambamba na hilo, Mhe. Mavunde amesema, serikali haitabadili msimamo wake wa kuwafikisha mahakamani waajiri wote ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kwani kwa kutofanya hivyo wanakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo kupelekwa mahakamani ambapo mwajiri atakayepatikana na hatia atalazimika kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi Milioni 50,000, (Milioni Hamsini), au kifungo kisichopungua miaka mitano (5) au vyote kwa pamoja.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao bado hawajajisajili na WCF na ambao hawafuati sheria ya ajira na mahusiano kazini, mkoani Tanga Ijumaa Machi 2, 2018, Mhe. Mavunde alisema.

“Si jambo zuri kwa waajiri kutekeleza matakwa hayo ya kisheria hadi wanapoona kiongozi wa serikali amewafikia, hii siyo sawa, na kuonya kuwa ni muhimu waajiri wakatambua kuwa zama zimebadilika, hakuna kichaka cha kujificha, vichaka vyote vinawaka moto hivi sasa.” Alisema.

Mhe. Mavunde pia aliwatahadharisha waajiri ambao wamejisajili kwa kupeleka taarifa za uongo kuhusu shughuli zao ikiwa ni pamoja na idadi ya wafanyakazi wao na viwango vya malipo ya mishahara ya wafanyakazi hao, kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai.

Naibu Waziri ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Aira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alilotoa mwishoni mwa mwaka jana, la kuwataka waajiri kutoka sekta rasmi (umma na binafsi) Tanzania Bara, kutekeleza takwa la kisheria linalowataka kujisajili na kutoa michango Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

“Kama nilivyowaeleza wenzenu kwenye mikoa niliyotembelea ya Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro na leo hapa Tanga ninarudia tena, nia ya serikali ni kuwaondolea mzigo wa gharama waajiri, ya kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakati wakitekeelza majukumu yao ya kikazi, na badala yake wajibu huo uchukuliwe na serikali kupitia Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi”.

Tunataka ninyi waajiri mjikite zaidi kwenye shughuli zenu za msingi za kufanya biashara na uwekezaji, na jukumu la kuwahudumia wafanyakazi wanapodhurika kazini tuachieni sisi serikali, alisisitiza Mhe. Antony Mavunde.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, Mkoa wa Tanga una jumla ya waajiri 769 na kati ya hao, ni waajiri 413 tu ndio wamejisajili, huku wengine 356, bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye Mfuko.
Naibu Waziri akitembelea kiwanda hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018.
Nabu Waziri Mavunde, akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, wakati walipotembelea kiwanda bhicho cha PPTL.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (katikati), akizungumza na Mkuu wa Kituo cha Afya, Tumaini Health Centre kilichoko Chumbageni Mkoani Tanga, Sister Flora Mushi, (kulia), ambapo alibaini bado mwajiri huyo hajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuagiza afikishwe mahakamani kwa kosa hilo la jinai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter.
Naibu Waziri na ujumbe wake, wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe.Martin Shigela, (katikati), mwanzoni mwa ziara yake aliyoifanya mkoani humo Machi 2, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa, (kushoto), akizungumza na Naibu Waziri Mabunde, (watatu kulia), Bw. Anselim Peter, (wapili kulia) na Kamishna wa Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde, akiwa na Bw. Anselim Peter, wakati wa ukaguzi huo.

Mhe. Mavunde akisalimiana na Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde akisalimiana na Bw. Anselim Peter (kulia).
Mhe. Mavunde akizungumza kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu, shule ya Sir John iliyoko Ras Kazoni Mkoani Tanga. Katikati ni Bw. Anselim Peter na Bi. Rehema Moyo.

DKT MWIGULU AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba  ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi wilaya ya Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto uliyotokea mwaka jana umefikiaje mpaka sasa na kuridhika na hatua iliyofikia.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
Nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa zikiwa tayari ,nyumba hizo zimejengwa kufuatia hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huo uanze mara moja

Dkt mwigulu amesema ameridhika na hatua iliyofikia ya ujenzi wa nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa na kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huu uanze mara moja, pia mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewashukuru Wafanyabiashara wa Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo kamilika, kwani walichukua hatua mapema tu pale moto ulipotokea.

"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, hili ni jambo jema ,kama Waziri namshukuru sana Rais Dkt Magufuli,na kwa hakika jambo hili litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya" ,alisema Dkt Mwigulu.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru waziri Mwigulu kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo na kufikia hapo kwani kama Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya ndani amekuwa karibu nao sana na kukagua kila hatua inayofikiwa.
RC Gambo ameongeza kusema kuwa kwasasa wamemuomba waziri Mwigulu awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio ya kiharifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo na askari wanategemea gari linalotoka kituo kikuu cha polisi Arusha.

MABINGWA TIMU YA IRINGA UNITED KUUWAKISHA MKOA WA IRINGA KWENYE LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi kombe kampteni wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja

mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi mchezaji bora wa mashindano Razack Kibuga ambaye ametoka katika timu ya Iringa United
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi golikipa bora wa mashindano Nelly Mkakilwa ambaye ametoka katika timu ya Iringa United
Baadhi ya wadau na mpira wa mikuu mkoani Iringa wakiwa wapo sambamba na kiongozi wa Iringa United walipokuwa wakifuatilia kwa ukaribu mechi katika ya Iringa United na Mtwivila City kutoka kushoto anaitwa Frank Lyimo kutoka kituo cha TV cha IMTV ,Ally Msigwa ambanye ni mkurugezi mtendaji wa Iringa Football Academy na anayefuata ni Steve Lihawa mtangazaji wa kipindi cha michezo cha radio Ebony fm iliyopo mkoani Iringa
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

TIMU ya Soka ya Iringa United imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi penati 3 - 1 dhidi ya Mtwivila Fc.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Samora timu ya Mtwivila Fc walikuwa wa kwanza kupata bao dk 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari David Mwanga baada uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kuponyokwa na mpira na kumpita tobo.

Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila walikuwa wakiongoza bao 1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha kufika fainali ya ligi ya Mkoa kwa Mtwivila wakitaka kuongeza huku Iringa wakitaka kurudisha.Mchezaji bora wa mechi ya nusu fainali Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya kusawazisha goli katika dk 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana.

Mara ya dakika 90 kumalizika ndipo hatua za kupigiana matuta ilipowadia ambapo timu ya Mtwivila fc ilikosa penati 3 na Iringa United kupata penati 3 dhidi ya 1. Kutokana na ushindi huo timu ya Iringa United imejinyakulia jezi seti moja, mipira miwili huku timu ya Mtwivila wakiondoka na jezi na mpira mmoja.Mchezaji bora wa mashindano hayo aliibuka Razack Kibuga wa Iringa United aliyeondoka na zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa United aliyepata sh.50000

Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa soka Mkoani hapa Feisal Abri Asas ambaye alikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa Iringa united, Ahmed Kivike.Akizungumza kabla ya kukabidhi kombe hilo Feisal alisema kuwa anatarajia kudhamini ligi ya Mkoa mwakani kwa kuwa mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa.

Wakati huo huo ya soka ya Mkimbizi fc imefanikiwa kushika nafasi ya tatu ya ligi ya mkoa baada ya kuwafunga timu ya soka ya Mshindo fc mabao 5 - 4.Katika mchezo huo mkali uliopigwa majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Samora timu ya Mshindo 'wabishi wa mjini' itabidi wajilaumu kwa kuwa hadi kipindi cha kwanza walikuwa wanaongoza goli 3 - 2 kwa magoli yaliyofungwa na Michael Chader dk za 8,17 na 23.

Magoli ya Mkimbizi fc yalifungwa na Said Kaliumi aliyefunga magoli matatu katika dk za 10 na 29 na 53.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Mshindo Fc kufunga goli la nne kupitia Michael Chader katika dk 50 lililodumu hadi dk ya 53 ambapo Mkimbizi Fc walijipatia goli kupitia kwa Said Kaliumi.Mkimbizi Fc wakiwa nyuma kwa goli mbili walikuja kwa kasi na kuanza kufunga katika dk za 64 na 70 na kufanya matokeo kuwa 5 - 4

Kwa ushindi timu ya mkimbizi imefanikiwa kuwa Mshindi wa tatu katika ligi ya Mkoa na kuondoka na zawadi ya jezi seti moja.

FINCA MICROFINANCE BANK YASHEREHEKEA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban akitoa hotuba yake katika hafla ya FINCA Microfinance Bank kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania ambapo ameipongeza benki hiyo kwa jinsi ambavyo imekuwa ikisaidia wajasiriamali wadogowadogo vijijini na mijini, Benki hiyo imeweza kusaidia wajasiriamali wapatao Milioni moja tangu ilipoanza kutoa huduma  za kifedha.02
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe akizungumzia mafanikio ya sherehe zake FINCA Microfinance kutimiza miaka 20 ya utendaji wake wa shughuli za kifedha nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake.
2
Dk. Bernald Yohana Kibese akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban ili kutoa hotuba yake katika hafla hiyo.
3
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akiipongeza FINCA Microfinance kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
4
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA ambaye pia ni Makam wa Rais na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike Gama-Lobo akizungumza katika mkutano huo.
5
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa FINCA Microfinance Bank kutoka Mataifa mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo ya miaka 20 ya benki hiyo.
67891011
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya FINCA Microfinance wakiwa katika hafla hiyo.
12
Jimmy Ngoye meneja wa FINCA mkoani Arusha akionyesha tuzo yake aliyokabidhiwa kwa kuwa mfanyakazi bora katika taasisi hiyo kwa upande wa mameneja.
13
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akimpongeza  Jimmy Ngoye meneja wa FINCA Microfinance mkoani Arusha baada ya kushinda tuzo ya ufanyakazi bora kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
14
15
Kikundi cha burudani kikiongozwa na Msanii maarufu Bob Rich kikitumbuiza katika hafla hiyo.16
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa FINCA Duniani pamoja na wa Tanzania.

TAHLISO YATOA TAMKO KUHUSU WANAFUNZI WANAOTAKA MWIGULU AJIUZULU KWA KIFO CHA AKWILINA.

$
0
0

Mwenyekiti wa Tahlisi George Albert  Mnali  wa pili kutoka kulia akizungumza na baraza Kuu la Senate leo  kushoto ni Katibu Mkuu wa Tahliso John Mboya kulia ni Katibu wa Baraza hilo Faidhaa Msangi na kulia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Rais wa Chuo cha Zanzibar University
JUMUIYA YA TAASISI ZA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA
(TAHLISO)OFISI YA MWENYEKITI TAHLISO
TAARIFA KWA UMMA.
Nduguwaandishiwahabaritunawashukurusanakwakukubaliwitowetuwakujakujumuikapamojanasisi. Leo tarehe 3/3/2018 tumekuta na viongozi wa vyuo vikuu nchi nzima kwa ajili yakujadili changamoto zinazotukabili. Kikao hiki ni cha TAHLISO BarazaKuu (SENATE) kinacho husisha Maraisi wa serikali za wanafunzi wa VyuoVikuunchini.
Tunatambuakwambakunakifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilini,mwanafunziwachuo cha NIT kilichotokea mwezi wa pili. Tunawashukuruwanafunziwenzetukwautulivumkubwanamshikamanowaliouoneshatangumsibaulipotokea, wakatiwakipindi cha majonzihadikufikiasasa.
TunamshukuruMhe.Raisi wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuingilia kati suala hili na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika na kifo cha AkwilinaAkwilini. 
VileviletunaishukuruWizarayaElimu, Sayansi na Teknolojia kwa ukaribu waliouonesha katika kipindi chote cha msiba.Tunaomba wanafunzi waendelee kuwa watulivu wakati maagizo yaMh. Raisi yakitekelezwa.
Aidha tunapenda jamiii tambue kuwa TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi wote nchi nzima Tanzania na sio kikundi kingine chochote kile. 
Vipovikundivingivimejitokezanakutoamatamkombalimbalibaadayakifohikikutokea, vikundivinginevikaendambali Zaidi kwakuwataka baadhiya watendajiwa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo yaNdani kujiuzulu jambo ambalo linaashiria vikundi hivyo kuongozwa ama kutumika namakundiyakisiasa, haiwezekani kutaka watendajiwa Serikali wajiuzulu wakati uchunguzi bado unafanyika na matokeoya uchunguzi huo bado hayajatoka.
 Sehemu ya Marais wa Vyuo Vikuu nchini wakiwa kwenye mkutano huo
Jambo la kusikitisha Zaidi kuna baadhi ya vikundi vimejitangaza kwamba vinaungwa mkono na Maraisi waVyuoVikuu jambo ambalo sio la kweli, Marais wote waVyuo Vikuu tuko hapa Dodoma tunaendelea na vikao vyetu vya kujadili changamoto zinazowakabili wanafunziwa VyuoVikuu.
Tunatoa wito kwa vikundi vyote vinavyojihusisha nakutumia mwamvuliwa Marais waVyuoVikuu kama kinga yao ili kuu hadaaUmma kwamba wanaungwa Mkono, vikundi hivyo viache tabia hiyo vinginevyo tutawachukulia hatua za kinidhamu.
TAHLISO tunasubirimatokeoya Uchunguzi unaofanyika juu ya kifo cha Akwilina na tunaimani wahusika wote watachukuliwa hatua kali zakisheria. 
Tunawaombawanafunzi wote tuendelee kuwa watulivu wakati tukisubiri matokeo hayo na kujiepusha na maandamano na vitendo vyovyot e vitakavyo sababisha uvunjifu wa Amani nakuleta mgawanyo miongoni mwawanafunzi. 
Hata hivyo namna bora yakufikisha hoja nikutumia njia ya majadiliano kama wasomi badala ya kutumia nguvu ama maandamano kwakutofuata taratibu na madhara yake ni kusababisha vuruguzi sizotakiwa na hatimaye kuhatarisha usalama na hivyo kuathiri jamii kwaujumla wake.
Vurugu zozote zitokanazo kwakutozingatia taratibu zinaweza kudhorotesha shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Uchumiwa Taifa letu. Vile vile zinapoteza mvuto kwawawekezaji wanje na wandani, ikiwemo shughuli za utalii nchini ambazo zinachangia pato la Taifa letu. 
Athariza Vurugu na kukosekana kwa amani zipo wazi natunaziona kwa nchi nyingine zikiwemo baadhi ya nchi jirani zetu ambao wamekua wakimbizi nchini kwetu kila siku.
Tunaona kuwa kama wanataaluma tunajukumu kubwa la kuelimisha jamii na kuwamfano bora wakutumia njia za majadiliano katika kujenga hoja zetu ilizitatuliwe kuliko kutumia njia ya maandamano au vurugu zisizo na ulazimawowote.

Taasisi hii ndio yenye dhamana ya kutetea nakusimamia maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo na vyuovikuu Tanzania na si vinginevyo.
………………………………….
GEORGE ALBERT MNALI
MWENYEKITI TAHLISO

MSIUZE UFUTA WENU MASHAMBANI PELEKENI MINADANI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na mzee Omar Issa, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee Omar Issa kulia na mzee Mussa Lambamba katikati, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa ufuta katika mikoa inayolima zao hilo nchini kuuza kwa kutumia njia ya minada na si mashambani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Machi 03, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Nachihungo, Narungombe na Chikwale.Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi amesema ili wakulima waweze kupata tija ni vema wakauza ufuta wao kwa kupitia minada kama inavyofanyika katika zao la korosho

“Usikubali kumuuzia mtu yeyote ufuta wako ukiwa shambani kwa sababu bei atakayonunulia ni ndogo kulinganisha na soko, naamini ufuta wote ukiuzwa katika minada mtaona faida.”Kufuatia agizo hilo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue aandae utaratibu wa maeneo ya kukusanyia ufuta na kufanyia minada.

Amesema ufuta unaolimwa nchini ni bora na unapendwa sana duniani hivyo wasiwe na wasiwasi. Baadhi ya Mikoa inayolima ufuta kwa wingi ni Lindi, Pwani, Dodoma, Manyara, Kigoma na Singida.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema vijiji vote visivyokuwa na umeme nchini vikiwemo vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa katika REA awamu ya tatu.

Amesema wananchi waendelee kuwa na subira kwa sababu tayari mkandarasi ameshaanza kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji vingine vya wilaya hiyo na atafika kwenye maeneo yao.Alibainisha kuwa mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wote nchini waunganishiwa nishati ya umeme kwenye majumba yao, hivyo waendelee kuwa na subira na kushirikiana na Serikali yao.
 
Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama alisema, “Huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji”.

Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kote nchini kutunza vyanzo vya maji ili kuliepusha taifa kugeuka jangwa pia miradi inayoletwa na Serikali iwe endelevu

MBUNGE LUCY MAYENGA AMWAGA MABATI UJENZI WA ZAHANATI KATA YA CHADEMA KITANGIRI

$
0
0
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) ametoa msaada wa mabati 128 kwa ajili ya kuezeka zahanati ya Kitangiri iliyopo katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga ambayo ipo kwenye hatua ya upauaji. 

Akizungungumza wakati wa kukabidhi mabati hayo, Mhe. Mayenga juzi alisema uamuzi wa kusaidia hatua hiyo unatokana na ari aliyonayo ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kusafiri umbali mrefu.

"Mheshimiwa diwani wa kata ya Kitangiri wewe ni Chadema lakini nimefarijika umehudhuria zoezi hili la makabidhiano, hii inaonesha dhamira ya kutekeleza ilani yetu ya CCM na unamuunga kwa dhati mheshimiwa rais wetu katika jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa" alisema Mhe. Mayenga.

Aidha Mayenga alibainisha kuwa maendeleo hayana itikadi za vyama vya siasa,dini wala rangi hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itamnufaisha kila mtu.

"Tunataka zahanati hii ikamilike ili wananchi wapate huduma bora za afya,niwakumbushe tu kuwa ugonjwa huwa hauangalii kwamba wewe ni CCM,Chadema au ACT Wazalendo ama chama chochote kile, naomba tuweke pembeni itikadi za vyama kwenye masuala ya maendeleo",aliongeza.

Mbunge huyo pia aliahidi kusaidia kununua magodoro yote katika zahanati hiyo pindi itakapokamilika.Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema) alisema amefarijika kwa kata yake kupata msaada huo kwani zahanati hiyo ikikamilika itasaidia kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) alisema alilazimika kumuomba mbunge Lucy Mayenga msaada wa mabati kutokana na changamoto ya umbali wa kupata huduma wanayoipata wananchi wake.

Alisema kata hiyo yenye zaidi ya wakazi 13,000 wananchi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hivyo wengine kulazimika kwenda zahanati binafsi kupata huduma."Mheshimiwa Mayenga leo umetukomboa kwa msaada huu naomba mkurugenzi wa halmashauri amalize haraka hatua zilizobaki ili zahanati ifanye kazi",aliongeza.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 128 kwa ajili ya ujenzi wa zanahati ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa mtaa wa Kitangiri Mohammed Mulabo (CCM) wakati wa kukabidhi mabati katika zanahati ya Kitangiri. Aliyevaa nguo nyeupe kulia ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Omar Ngunila (Chadema).
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akiendelea kukabidhi mabati hayo.
Zoezi la makabidhiano likiendelea

CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0
Diwani wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’ Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Afisa Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana na Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Afisa Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa vipeperushi kwa wanafunzi wa Shule ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana na Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisoma vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakionesha vipeperushi mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali(wanne kulia) akiwa katika picha na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Rose Minja(wa tatu kulia) pamoja na waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Haneti mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani Chamwino.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .

Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.

“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa  elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.

“Wanafunzi, Walimu, Wazazi na walezi tuweke mikakati thabiti ya kupambana na tatizo hili la mimba za utotoni” alisisitiza Bi. Rose.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala ameeleza kuwa Wilaya ya Chamwino imejipanga katika kuzuia mimba za utotoni kwa kuhakikisha wanawafikia wahusika katika ngazi za shule na familia na kutoa elimu kwa watoto wote wa kike wanaowazunguka ili kuondokanana tatizo la mimba za utotoni katika wilaya yao.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na kampeni ya kuzuia mimba za utotoni chini katika shule za Msingi na Sekondari ijulikanayo kama Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima sambamaba utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na watoto katika ngazi mbalimbali nchini ili kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022.

BITEKO: TUFANYE SIASA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa Kijimbo uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo, Jana 3 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Pamoja na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018.



Na Mathias Canal, Geita

Wanasiasa hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi zinazoonekana za kuleta maendeleo. 

Rai hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa katika ziara ya kijimbo ya siku nne.

Mhe Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa namna yoyote.

Alisema kuwa Maendeleo ni majumuisho ya mwendelezo wa shughuli za kujiongezea kipato, amani ya nafsi na uhuru ambapo Maendeleo yeyote ambayo hayana mwendelezo wa amani ya nafsi, kipato na uhuru, hayo si maendeleo bali ni mabadiliko yenye ukomo ambayo kwayo hayaleti amani ya nafsi na uhuru wa kudumu bali kipato cha muda mfupi na furaha ya muda mfupi na mwisho wake ni mshangao wenye haiba ya huzuni ambatano na maswali yasiyo na majibu.

"Maendeleo ni mchakato mi sidhani kama kuna watu hapa ambao wamekamilisha kila jambo katika familia zao, ila kila siku mnapanga na mnatekeleza jambo moja baada ya jingine, sasa watakuja watu hapa watasema watawaletea kila kitu kijijini kwenu, sasa kwa mtazamo wenu jambo hilo linawezekana kweli? wananchi wakaitikia HAPANA"

Mhe Biteko alisisitiza kuwa katika kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja wananchi wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kushadihisha maendeleo hayo kwa kufanya kazi kwa weledi.

Aidha, Mhe Biteko aliwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kufanya mambo mawili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wasaidizi wake wote, Mosi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za utendaji lakini pili ni kumuombea ili atomize matakwa ya wananchi na kusudio la ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

SEED trust yapokea vitabu1000 vya Malengo ya Dunia kwa wasioona

$
0
0

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju (wa pili kushoto) sehemu ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa SEED Trust Tanzania, Mh. Margaret Mkanga (kushoto) na Meneja Programu wa SEED Trust Tanzania, Peter Mwita (kulia).

Umoja wa Mataifa umetoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia vilivyochapishwa kwa herufi nundu (braille)(hizi ni herufi zilizovimbishwa na ambazo watu wasioona au wenye uoni hafifu husoma kwa kugusa na kidole) kwa taasisi ya Seed Trust Tanzania katika jitihada za kuwafikia wasioona. Kuna takribani watu milioni 39 wasioona na wenye uoni hafifu kote duniani leo; miongoni mwao takribani milioni 5.8 wako Afrika. Nchini Tanzania, kuna taarifa kwamba takribani asilimia 1.2 ya watu wenye ulemavu huu walitoa taarifa kwamba wana matatizo ya kuona.

Msaada huu kwa shirika la Seed Trust, ambalo ni asasi inayojishughulisha na uwezeshaji wa kijamii na kiuchumi wa watu wenye ulemavu nchini Tanzania, ni juhudi za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa za kutomwacha mtu yeyote nyuma katika utekelezaji wa Malengo ya Dunia kama wito unavyotolewa kupitia Agenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030.

Vitabu hivyo vya taarifa vilikabidhiwa leo na Mratibu Mkazi wa UN, Bw. Alvaro Rodriguez, kwa shirika la Uwezeshaji wa Kijamii na Kiuchumi Tanzania (SEED Trust Tanzania). Msaada huu unaendelea kujenga uelewa kuhusu Malengo ya Dunia ulianzia na semina iliyoandaliwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu mwaka janana Bw. Rodriguez na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, kwa kushirikiana na Seed Trust Tanzania. Ushirika huu kati ya UN na Seed Trust unalenga kuwajengea uwezo wenye ulemavu kujumuishwa katika jitihada za kufikia Malengo ya Dunia nchini Tanzania.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumzia kuhusu Umoja wa Mataifa kuwafikia watu wenye ulemavu katika kuhakikisha taarifa za Malengo ya Dunia zinawafikia watu wote wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Akibabidhi vitabu hivyo vya taarifa, Bw. Rodriguez alizungumzia umuhimu wa msaada huo: “Bila kujali kama ni mitandao ya kijamii au ni matini yaliyochapwa, kujenga uelewa tulioufanya kuhusu Malengo ya Dunia kunahusisha kusoma,” alisema. “Kutoa msaada wa vitabu hivi vya taarifa vilivyochapwa kwa herufi nundu ni hatua ya kwanza kuhakikisha kwamba watu wenye matatizo ya uoni wanaweza kuchangia katika kufikiwa kwa Malengo ya Dunia kwa sababu vitawasaidia kuyaelewa malengo hayo.”

Akisisitiza umuhimu wa kuwajumuisha wenye ulemavu katika shughuli za maendeleo, Bi. Margaret Mkanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Seed Trust Tanzania na Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu akiwakilisha wenye ulemavu alisema: “Malengo ya Maendeleo Endelevu ni ajenda ya dunia itakayodumu hadi mwaka 2030.
 
Malengo haya ni zaidi ya ajenda ya kawaida, shabaha zake na viashiria vinatoa fursa ya kufanya marejeo katika ngazi tofauti katika ratiba ya utekelezaji wake. Ushiriki wa watu wenye ulemavu ni muhimu katika kufanikiwa kwa ajenda hii. Vitabu hivi vya taarifa tunavyovipokea leo ni hatua nyingine kuelekea katika ushirikishwaji wa watu wenye matatizo ya kuona katika ajenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.”
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju, akitoa salamu za serikali na kupongeza juhudi za Umoja wa Mataifa kuwafikia wenye ulemavu kwa kutoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za UN ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo ya Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju.Akizungumzia juhudi za UN kuwafikia wenye ulemavu, Mh. Amonalisema: “Lengo la 4 la Malengo ya Dunia linahusu elimu bora iliyo jumuishi na usawa wenye haki na kuhamasisha upatikanaji wa fursa za kujifunza za kudumu kwa wote. Lengo la 10 linahusu kuhakikisha kupungua kwa tofauti ndani na kati ya nchi nanchi.

Lengo la 17linahusu kuimarisha njia za utekelezaji na kuhuisha ushirika duniani ili kufikia Maendeleo Endelevu. Shabaha hizi kwa namna ya pekee zinataja ulemavu kama kitu kitakachosaidia kuhakikisha ushirikishwaji na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji, usimamizi na tathmini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ujumuishwaji kwa hakika utahakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma. Kujumuishwa kwa watu wenye ulemavu kunatoa fursa kwao kushiriki na kutoa dukuduku zao pia.
Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu pia aliongeza, “Serikali ya Tanzania imejizatiti kuunga mkono utekelezaji wa Malengo ya Dunia katika ngazi zote. Vitabu hivi vya taarifa vitasaidia sana watu wenye matatizo ya uoni nchini Tanzania katika kupata taarifa zinazohusu malengo ya dunia na vitawasaidia nao kutoa mchango wao katika utekelezaji wake.”

Wakazi wa DSM kuanza kutumia gesi asilia kwa matumizi ya Nyumbani Na Zuena Msuya Dodoma,

$
0
0

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amelitaka na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) kuharakisha uunganishaji wa huduma ya gesi asilia katika baadhi ya nyumba za wananchi kwenye maeneo ya jiji la Dar Es Salaam kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Dkt.Kalemani aliyasema hayo ofisini kwake mkoani Dodoma alipokutana na watendaji wa TPDC kwa lengo la kujadili suala la usambazaji wa Gesi asilia katika nyumba za Wananchi pamoja na bei watakayouziwa wananchi hao.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kalemani aliwataka TPDC kuunganisha nyumba kuanzia Hamsini( 50) na kuendelea, na huduma ya gesi asilia katika maeneo la Mwenge na Mikocheni, kwa kuwa tayari miundombinu ya bomba la gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani imepita maeneo hayo.

Wakizungumzia suala la bei ya kuwauzia wateja, Dkt. Kalemani alisema kuwa pamoja na mambo mengine Gesi hiyo itauzwa kwa Wananchi kwa pungufu ya 40% ya bei ya mitungi ya gesi itayokuwa sokoni kwa wakati huo.

" Hii ni gesi yetu na bomba ni la kwetu vyote vinapatikana hapahapa nchini, ni vyema iuzwe kwa bei ya chini zaidi ya ile iliyopo sokoni kwa sasa, ili kila mwananchi aweze kumudu gharama zake pia ni rafiki wa mazingira, itasaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kulinda misitu yetu", alisema Dkt. Kalemani.

Hata Hivyo Dkt. Kalemani aliwaagiza TPDC kuendelea na taratibu za kuwaunganisha wananchi wa Mtwara na huduma ya gesi asilia katika nyumba zao kwa matumizi ya nyumbani kama itavyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Aidha amelishauri shirika hilo, kutumia wataalamu wake wa ndani kupitia shirika lake la kulinda miundombinu ya gesi( GASCO) ili kusambaza gesi asilia kwenye nyumba za wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani badala ya kutegemea wakandarasi ambao mchakato wa kuwapata unachukuwa muda mrefu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba, alifafanua kuwa gharama za uunganishwaji wa huduma ya gesi asilia katika nyumba za wananchi itategemea na ramani ya nyumba husika pamoja na umbali wa nyumba hiyo kutoka ilipopita miundombinu ya bomba la gesi asilia linalotumika kusambaza gesi katika maeneo ya makazi.

Vilevile, Mhandisi Musomba aliweka wazi kuwa mfumo wa kusambaza gesi asilia katika nyumba za wananchi utakuwa kama ule unaotumika kusambaza huduma ya maji, lakini ulipaji wa gharama za matumizi ya gesi hiyo utakuwa kama ule unaotumiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Lipa Umeme Kadri Unavyotumia( LUKU) kwa maana kwamba kila mtumiaji wa gesi asilia nyumbani kwake atalipia huduma hiyo kwa kadri atakavyokuwa akitumia.

Gesi itakayokuwa ikisambazwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ni ile inayozalishwa katika Visima vya gesi vilivyopo katika Mkoa wa Lindi na Mtwara. 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na watendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) ,na watendaji wa Wizara ya Nishati, kuhusua suala la usambazaji wa gesi asilia katika nyumba za wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ofisini kwake mkoani Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( kushoto)na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba( kulia) wakizungumza kuhus suala la usambazaji wa gesi asilia katika nyumba za wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

CHUMVI, CHOKAA ZINAWEZA KUITAJIRISHA KIGOMA - NYONGO

$
0
0

Na Veronica Simba – Kigoma 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, amesema kwamba ikiwa wananchi wa Kigoma watatumia vyema fursa za upatikanaji wa Madini ya Chumvi na Chokaa, zilizopo katika Mkoa huo, wanaweza kutajirika. 

Akihitimisha ziara yake katika Mkoa huo, jana Machi 3, baada ya kutembelea Migodi mbalimbali ya Madini ya Chokaa na Chumvi, Nyongo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa upatikanaji wa Chumvi na Chokaa ni neema kwa wananchi hao kutokana na uhitaji wake mkubwa katika maisha ya kila siku. 

“Ni fursa kubwa sana kwa wananchi wa Kigoma. Wasidhani kwamba fursa iliyopo hapa ni ya uvuvi na mawese peke yake; wanaweza kuwa matajiri wakubwa kupitia Madini ya Chokaa na Chumvi.” 

Akifafanua zaidi, Nyongo alisema kuwa, katika siku mbili za ziara yake mkoani Kigoma, ameshuhudia maeneo mengi yenye Chokaa ya kutosha na kwamba uzalishaji wake ni rahisi sana kwani kinachohitajika ni kuyachoma mawe husika na kusaga; basi. 

Akizungumzia upande wa Chumvi, alisema kuwa, Mgodi wa kuzalisha Chumvi wa Nyanza, uliopo Uvinza unafanya kazi nzuri katika uzalishaji lakini kwa bahati mbaya asilimia 70 ya bidhaa wanayozalisha, huiuza nje ya nchi hususan katika nchi jirani za Kongo na Burundi. 

Alisema kuwa, pamoja na kwamba wawekezaji hao wanalazimika kuuza asilimia kubwa ya chumvi yao nje ya nchi kutokana na sababu za kijiografia na miundombinu ya usafirishaji; Serikali inaona suala hilo siyo sawa, hivyo inaweka mikakati kuhakikisha wazalishaji hao na wengine wote wanatosheleza Soko la Ndani ya nchi kwanza; ambalo ni kubwa, kabla ya kuuza nje. 

“Mahitaji ya Chumvi kwa Tanzania ni takribani tani 250,000 kwa Mwaka na takwimu zilizopo zinaonesha tunaagiza kiasi kikubwa cha Chumvi kutoka nje ya nchi, hususan Kenya, wakati hii ya kwetu tunayozalisha nchini, tunaiuza nje. Hii siyo sawa. Ni lazima sasa tuweke mikakati itakayowezesha wawekezaji wetu kutosheleza Soko la Ndani kwanza,” alisisitiza. 

Kuhusu mikakati ambayo Serikali inaifanya katika kuboresha sekta hiyo ndogo ya chumvi; Naibu Waziri alisema kuwa, ni pamoja na kuwawezesha wachimbaji wadogowadogo, waweze kuzalisha chumvi nyingi itakayotosheleza Soko la Ndani na la Nje. 

“Mathalani, tumedhamiria kufungua Vituo vya Mfano (Centre of Excellence) sehemu mbalimbali nchini. Tumekwishaanza na Lindi, tutafanya hivyo kwa Mikoa mingine ikiwemo huu wa Kigoma ili wachimbaji wajifunze namna ya uzalishaji bora wa chumvi ikiwemo kuiongezea madini joto, ambao ni mkakati wa kidunia pamoja na kuifungasha katika hali ya ubora iweze kukidhi viwango vya Soko la Ndani na hata vya ushindani katika Soko la Nje.” 

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa, ili kuwawezesha zaidi wawekezaji katika sekta husika; Serikali kupitia Wizara ya Madini pamoja na Idara nyingine zinazohusika, watakaa pamoja wajadili namna wanavyoweza kupunguza wingi wa kodi zinazotajwa kufikia 14 na kulalamikiwa na wawekezaji, ili waweze kufanya biashara hiyo kwa tija zaidi. 

Alisema kuwa, ni suala linaloleta ‘ukakasi’ kuona wingi wa kodi inayotozwa kwa wazalishaji wa chumvi wa ndani ya nchi na wakati huohuo nchi inaagiza chumvi kutoka nje pasipo kodi yoyote, hivyo akasisitiza kuwa Serikali imeona kuna umuhimu mkubwa kwa wadau kukutana, kujadili na kuweka mikakati itakayoleta suluhisho lenye tija. 

Awali, akiwasilisha Taarifa ya Mgodi wa Uvunaji Chumvi wa Nyanza kwa Naibu Waziri, Meneja wa Mgodi Bonny Mwaipopo, alisema kuwa jumla ya kodi iliyolipwa kwa Serikali kwa kipindi cha Mwaka 1999 hadi 2016 ni shilingi bilioni 8.8 za kitanzania. 

Wizara ya Madini imekuwa ikieleza dhamira yake ya kuhakikisha uchangiaji wa sekta hiyo katika Pato la Taifa unakua zaidi ya ilivyo sasa, kupitia usimamizi mzuri utakaowezesha ongezeko la wawekezaji wenye kulipa kodi na tozo zote stahiki za Serikali.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu. 
Mmoja wa wafanyakazi katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza, ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), akifunga Mifuko ya Chumvi tayari kupelekwa Sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), Mgodini hapo, Machi 3 Mwaka huu.
Shughuli za uchakataji chumvi zikiendelea katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mine), siku Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), alipotembelea Mgodi huo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu. 
Mmoja wa wafanyakazi katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza, ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), akifunga Mifuko ya Chumvi tayari kupelekwa Sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), Mgodini hapo, Machi 3 Mwaka huu.
Shughuli za uchakataji chumvi zikiendelea katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mine), siku Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), alipotembelea Mgodi huo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 3 Mwaka huu.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images