Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1530 | 1531 | (Page 1532) | 1533 | 1534 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii

  KWA mara ya kwanza wamepatia!Ndivyo ambavyo kwa siku ya leo
  baadhi ya wananchi hasa wa Jiji la Dar es Salaam wanavyodai baada
  ya mvua kunyesha kama ambavyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
  (TMA )ilivyotabiri.

  Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakidhani TMA wamekuwa wakibahatisha kwenye tabiri zao hasa pale inapotokea walitabiri mvua kunyesha katika eneo fulani halafu mvua hainyeshi na kusababisha maswali.

  Siku za hivi karibuni, TMA ilitoa taarifa kwa umma kuwa mwanzo mwa Machi mwaka huu mvua zitaanza kunyesha na kuomba wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka athari za mvua.
  Hivyo kitendo cha mvua kunyesha leo jijini Dar es Salaam ambayo ni mwanzoni mwa Machi , wananchi ambao wamezungumza na Michuzi Blog wamedai ni kwa mara ya kwanza Mamalaka ya Hali Tanzania imetabiri kwa usahihi na kuwataka kuendelea kutoa tabiri ambazo zinaendena na ukweli ili kuendelea kuaminika.

  Mshana John ambaye ni mkazi wa Kigamboni ametoa pongezi kwa TMA huku akidai alikuwa anasubiri ka hamu Machi ifike ili aone kama utabiri kuhusu mvua ulikuwa wenye ukweli lakini sasa ameamini na kusisitiza kwake ni mara ya kwanza kuona kilichotabiriwa kinakwenda na wakati.

  "Niwe kweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa taarifa kuhusu hali ya hewa, ila kuna wakati wanatabiri kuwa mvua itanyesha lakini matokeo yake hakuna mvua na jua linabaki kuwa kali.Ila kwa mara ya kwanza wamepatia lazima tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya.

  "Huenda sasa watakuwa wamejiimarisha kwa kuwa na vifaa ambavyo vinakwenda na taarifa sahihi na ndio maana wametabiri uhalisia .Walisema mvua itanyesha mwanzoni mwa Machi na leo ndio mwanzo wenyewe na kweli imenyesha,"amesema John.


  0 0  Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akikabidhi zawadi ya shilingi milioni 10 kwa Bw. Reuben Bulugu Kinamhala mshindi wa Bahati nasibu ya “Daka Mkwanja” iliyoendeshwa na Benki hiyo kwa muda wa miezi minne kwa wateja wake kuweka fedha kwenye akaunti zao na kutunza kiwango kisichopungua shilingi milioni moja , Bw. Reuben Bulugu ambaye ni mtumishi katika kanisa ni mteja wa benki hiyo katika tawi la Mtoni Temeke jijini Dar es salaam.

  Katika picha kulia ni Mke wake Jane Bulugu akishiriki kupokea kiasi hicho cha fedha na kutoka kulia wanaoshiriki kukabidhi fedha hizo kwa mshindi ni Linda Mario Mkuu wa uratibu wa Mauzo na Nimael Mdeme Meneja wa Matawi ya Benki ya Boa Kanda ya Dar es salaam na Zanzibar.

  Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake pamoja na washindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi  Tigo, Sylvia Balwire akisaini ubao wa uzinduzi wa mfumo usajili wa laini za simu unaotumia alama za vidole kuhakiki taarifa za wateja wa makampuni ya simu Tanzania(BIOMETRIC), anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano ,Dkt. Maria Sasabo leo kwenye viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.
  Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano ,Dkt. Maria Sasabo (mwenye kilemba) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano TCRA, Mhandisi. James Kilaba na Wakuu mbalimbali wa makampuni ya simu Tanzania leo.
  Mtaalam wa Kitengo cha Upatikanaji wa Wateja Wapya Tigo, Keneth Ndulute akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa mfumo usajili wa laini za simu unaotumia alama za vidole kuhakiki taarifa za wateja wa makampuni ya simu Tanzania(BIOMETRIC).
  Mtaalam wa Kitengo cha Upatikanaji wa Wateja Wapya Tigo, Keneth Ndulute akielezea jambo kwa Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi. James Kilaba.
  Meneja Mradi wa Biometric wa Tigo, Mohamed Sufian akiwa kwenye banda la Tigo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa laini za simu.

  0 0


  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kikai kazi kilichofungwa jana cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Paulina Mkwama akitoa utambulisho wa wageni waalikwa wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara mjini Dodoma.


  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara ambapo amewaasa washiriki hao kutumia fedha za Serikali kwa kufuata sheria.

  Mheshimiwa Ndalichako alisema Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais,TAMISEMI kwa kuwaadhibu wale wote wanaoenda kinyume na matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Elimu bila ya kuzingatia sheriaa na miongozo ya utekelezaji wake.

  “Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya RAis TAMISEMI itawachukulia hatua Wale wote wataokula fedha za miradi na hawatopelekewa pesa za miradi mingine hadi wakamilishe miradi ambayo haijakamilika na kutoa mchanganua wa matumizi yake,”Amesema

  Ndalichako alihamasisha uzingatiaji wa taratibu za fedha kwani Viongozi wa ngazi ya juu hususani Mawaziri wamekua wakijibu tuhuma za ubadhilifu wa fedha kwa wakaguzi wakati hawakuchukua fedha hizo.

  “Wengine mpaka leo miradi ya 2016 haijakamilika kutokana na ubadhilifu wa fedha. hivyo serikali haita wavumilia hata kidogo,” Alisema Ndalichako.

  Katika hatua nyingine, Ndalichako amewataka Wataalam wa Elimu kutoa taarifa kwa wakati na kama kuna mambo hayaendi sawa katika Halmashauri zao, Viongozi wajuu waweze kutoa maamuzi sahihi na kwa wakati ikiwa ni pamoja na takwimu sahihi.toeni taarifa kwa wakati, andikeni ripoti kwa wakati, na hakikisheni matumizi yenu yanazingatia miongozo na taratibu za fedha. Muwe waungwana, kwani muungwana ni kutenda”

  Alizungumzia pia suala la maudhurio shuleni na watoto kuacha shule kabla ya kumaliza mzunguko kwani kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016 unaonesha bado kunatatizo la mdondoko wa wanafunzi na hapa amewataka Wasimamizi wa Sekta ya Elimu kuwa makini kufuatilia na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kusaidia watoto.

  Aliagiza maafisa Elimu Mkoa kuchagua wanafunzi kulingana na idadi ya madarasa kwani watoto wamekua wakilundikana kwenye darasa moja wanafunzi zaidi ya 200 wakati shule husika ina uwezo wa kupokea wanafunzi wa mkondo mmoja (wanafunzi 40).

  Aliagiza Shule zote za kidato cha tano ambazo hazijasajiliwa zikaguliwe ambazo zimekidhi viwango basi zisajiliwe na zipokee wanafunzi wa kidato cha tano kwani Maafisa Elimu wamekua wakipangia wanafunzi shule ambazo hazijasajiliwe na hapa amewapa miezi mitatu watatue tatizo hili la kidato cha tano na zile shule zilizolundika wananfunzi kwamba baada ya hapo hatua nyingine zitachukuliwa dhidi yao.

  Awali akimkaribisha mgeni rasmi kabla ya kufunga kikao kazi hicho, Naibu Katibu Mkuu (ELIMU)Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda alisema mambo mbalimbali ambayo yalijadiliwa kwenye kikao hicho ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, kilimo, ufundi na biashara, uhaba wa vitendea kazi kwa maofisa elimu hasa usafiri pamoja na utoaji motisha kwa walimu ili kuongeza ufanisi mashuleni.

  Pia alisema katika kikao kazi, kila mmoja amepewa jukumu la kutekeleza ikiwa ni pamoja na usalama wa watoto.“Kila mmoja katika kikao hiki amepewa jukumu la kufuatilia miradi kwa ukaribu, kusimamia taaluma na usalama wa watoto wawapo mashulen” Alisema

  kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu, na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara kimedumu kwa siku mbili na matarajio ni kwamba kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini hususani masuala ya kitaaluma.

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu kushoto akimkabidhi sehemu ya vitanda 40 magodoro 40 na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel ikiwa mpango wao kupitia kampeni ya benki ya exim ya miaka 20 ya kujali jamii wa pili kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Mohamed Abdallah kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim mkoa wa Tanga,Emanuel Mwamkinga.

  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel akiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki ya Exim Stanley Kafu wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vitanda na magodoro 40 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
  Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel kushoto ni Meneja wa Exim Benki Mkoa wa Tanga Emanuel Mwamkinga
  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mohamed Abdallah kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko ya Benki ya Exim Stanley Kafu
  Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo Beatrice Rimoy akizungumza kuishukuru benki ya Exim kwa kuwapatia msaada huo wa vitanda na magodoro 40
  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mohamed Abdallah akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya vitanda na magodoro 40 iliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo
  Sehemu ya vitanda na magodoro vilivyotolewa

  Sehemu ya watumishi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia matukio hayo

  BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitanda 500 na magodoro kwa hospitali za rufaa kwenye mikoa 13 hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusheherekea miaka 20 ya kuitumikia jamii.

  Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo, Stanley Kafu wakati akikabidhi vitanda na magodoro 40 kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inayolengo la kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini.

  Alisema ili kukabiliana na hali hiyo ndio maana waliamua kutoa msaada ili kuweza kusaidia tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa katika kukabiliana na uhaba unaosumbua Taifa.

  “Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma mwezi wa Agosti mwaka jana,kwa kuzindua kampeni ya mwaka mzima uuitwao ‘Miaka 20 ya kujali jamii”ambao benki hiyo itawekeza katika sekta ya Afya Tanzania…Sisi kama Benki ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka wa 1997 hivyo benki hiyo inafafanua mafanikio yake jinsi inavyoleta mabadiliko kwa wateja na jamii kwa ujumla “Alisema.

  “Hospitali ya rufaa mkoa wa Tanga ni hospitali ya saba kupokea mchango huu, baada ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya mwezi uliopita, Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha mwezi Desemba, Hospitali ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, Hospitali ya rufaa Ligula mkoani Mtwara mwezi Octoba,Hospitali ya Mnazi mmoja Unguja Visiwani Zanzibar mwezi Septemba na hospitali ya rufaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka huu”Alisema

  Katika halfa hiyo tukio hilo la makabidhiano ya msaada huo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano na mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Matibabu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Clemence Marcel pamoja na Kaimu Mganga mkuu wa hospitali Dkt Mohamed Abdallah.

  “Katika kipindi cha miaka 20 benki imetambua umuhimu wa jamii zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa kwa benki ya Exim…..Tunaamini kwamba tuna nafasi kubwa katika kuchangia mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali kwa jamii zetu “Alisema

  “Lakini pia benki iliamua kusheherekea miaka hiyo kwa kusaidia jamii kwa njia ya kampeni inayoitwa “Miaka 20 ya kujali Jamii” kuonyesha jinsi tunavyowashukuru kwani benki hiyo imekwisha kutoa vitanda na magodoro ya hospitali kwa hospitali nchini kote kila mwezi kwa mwaka mzima”Alisema

  Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel aliipongeza Exim benki kwa juhudi zake za kusaidia kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye hospitali ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.

  Alisema upungufu wa vitanda katika hospitali umekuwa ni changamoto kubwa hivyo kukabidhiwa vitanda 40 na magodoro utasaidia sana kupunguza vikwazo vya namna hiyo kwa jamii.

  Benki ya Exim inatambuliwa kama Mwajiri bora wa kitanzania mwaka 2017 na taasisi ya The Banker ya Afrika mashariki na sasa inasheherekea miaka 20 ya mafanikio,ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika.

  “Exim Benki iliyoanzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro(2007),Djibouti(2010) na Uganda (2016) lakini pia benki hiyo inajuivunia kuwa benki ya kwanza kubwa ya kitanzania nay a kwanza kuingia katika masoko ya nje ya nchi.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

   Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya katika pozi
   Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya katika pozi akionyesha mtindo wake mara baada ya kupambwa katika saloon ya Nazmeen Mekeup iliyopo makutano ya Barabara ya Uhuru na Mwanza Dar es Salaam  
    Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya katika pozi mara baada ya kuvishwa pete ya uchumba na Mume wake mtarajiwa, hafla iliyofanyika nyumbani kwao biharusi, Yombo Relini Dar es Salaam
   Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya katika pozi
   Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya akipambwa katika saloon ya Nazmeen Mekeup iliyopo makutano ya Barabara ya Uhuru na Mwanza 
   Bi harusi mtarajiwa Grace katika pozi

  Bibi wa bi harusi mtarajiwa, Rose Makwaya akifatilia jambo wakati washughuli za taratibu wa utoaji mahari ukiendelea nyumbani kwao na bi harusi Yombo Relini Dar es Salaam
  Dada mkubwa wa bwana harusi, Nuru Benedicti akisaidiana na baba mdogo wa bi harusi, Joseph Binamungu kuikunjua shuka 
  Dada mkubwa wa bwana harusi, Nuru Benedicti akizungumza jambo na mshenga, Elizeus Munyigo mara walipofika nyumbani kwao bi harusi katik kukamilisha taratibu za mahari
  Dada mkubwa wa bwana harusi, Nuru Benedicti akizungumza jambo na mshenga, Elizeus Munyigo na kulia ni shemeji wa Bwana harusi
   Dada mkubwa wa bwana harusi, Nuru Benedicti akimkabidhi pesa baba mdogo wa bi harusi, Joseph Binamungu kati ya moja ya makubaliano katika kukamilisha utaratibu wa  utoaji mahari
   Bwana harusi mtarajiwa, Adam Benedict akimvisha pete mkewe mtarajiwa, Grace Makwaya
   Bwana harusi mtarajiwa akiibusu pete ya mchumba wake, Grace Makwaya  mara baada ya kumvisha
   Bwana harusi mtarajiwa, Adam Benedict  akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kumvisha pete mkewe mtarakiwa, Grace Makwaya

   Maharusi watarajiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa wa pande zote mbili

  Bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya katika picha ya pamoja na baba mlezi Dokt, David Makwaya (wa pili kushoto) akiwa na mkewake na kulia ni Mume Mtarajiwa wa bi harusi, Adam Benedict  


   Bwana harusi mtarajiwa Adam Benedict akiwa katika pozi na mkewe mtarajiwa,  Grace Makwaya
   Bwana harusi mtarajiwa Adam Benedict (kushoto) akiwa na familia yake mara baada ya kuwasili nyumbani kwao na bi harusi mtarajiwa Grace Makwaya  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga (CCM) amefanya ziara ya kukutana na akina mama wafanyabiashara ndogo ndogo zaidi ya 250 wanaofanya shughuli zao katika Soko Kuu, Mtaa wa Sukari na Nguzo Nane mjini Shinyanga kwa lengo la kusikiliza shida zao na kujadili namna ya kuboresha biashara zao.

  Mhe. Mayenga amefanya ziara hiyo leo Alhamis Machi 1,2018 akiwa ameambatana na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone, Afisa Biashara wa Manispaa hiyo,Sunday Deogratius, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shumbuu Katambi na madiwani wa viti maalum Zuhura Waziri na Mariam Nyangaka.

  Alisema lengo la kukutana na akina mama hao ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji na mazingira yasiyo rafiki ni kutoa elimu na kubadilishana mawazo kuhusu ya namna ya kuondoka katika hali waliyonayo ili wapige hatua kimaendeleo.

  “Nimeanzisha utaratibu huu wa kukutana na akina mama bila kujali itikadi za vyama vya siasa,dini wala rangi kwani maendeleo hayaangalii mambo haya, wanawake wana nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii hivyo lazima tushirikiane na tujumuike pamoja kumaliza changamoto zinazowakabili ili tujikwamue kiuchumi”,alieleza.

  Mhe. Mayenga aliwahamasisha akina mama kuunda vikundi ambavyo watavitumia kuomba mikopo katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwani serikali haiwezi kutoa pesa kwa mtu mmoja mmoja.

  Aidha aliwaomba akina mama hao kuunda umoja na kila mmoja kuwa anachangia shilingi 1000 kila siku,fedha ambazo zitasaidia katika kupata mitaji mikubwa na kuinua vikundi vyao ili waweze kuinuka kiuchumi.

  Katika kuunga mkono wazo hilo,Mhe. Mayenga alitoa mchango wa shilingi milioni 2.5 kwa ajili akina mama hao,kati ya fedha hizo shilingi milioni moja ni kwa akina mama katika Soko kuu,shilingi moja,Soko la Nguzo Nane na shilingi laki tano kwa ajili ya akina mama wanaofanya biashara ya mboga mboga katika mtaa wa Sukari mjini Shinyanga.

  Katika hatua nyingine alizitaka halmashauri za wilaya kufuatilia vikundi vinavyopewa mikopo ili iwe na tija kwa wakopaji na kuwakumbusha akina mama wajibu wa kufanya kazi kwani serikali awamu ya tano inayoongoza na rais John Magufuli inataka kila mtu afanye kazi.

  Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone alisema halmashauri hiyo inasajili bure vikundi huku akiwataka kuaminiana na kushirikiana pamoja na kuwa na nidhamu ya fedha.

  “Kwenye biashara hakuna urafiki,pesa haina urafiki hivyo ili ufanikiwe katika biashara yako lazima uwe na nidhamu ya fedha na pia muwe makini na taasisi zinazotoa mikopo kwani siyo rafiki sana kwa wafanyabiashara”,alieleza Kiwone.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga (CCM) akizungumza na akina mama wanaofanya biashara zao katika Soko Kuu Mjini Shinyanga waliokutana naye katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Machi 1,2018 kwa ajili ya kutoa elimu na kubadilishana nao mawazo namna ya kuboresha biashara wanazofanya - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akizungumza na akina mama zaidi ya 100 wanaofanya biashara zao katika Soko Kuu mjini Shinyanga.
  Mfanyabiashara katika Soko Kuu Mjini Shinyanga,Winfrida Rwehumbiza akimshukuru Mbunge Lucy Mayenga kwa kuwafikia akina mama wafanyabiashara wenye mitaji midogo.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akizungumza na wafanyabiashara katika Mtaa wa Sukari mjini Shinyanga.
  Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone akitoa elimu ya vikundi kwa wafanyabiashara wa mbogamboga katika mtaa wa Sukari mjini Shinyanga
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akinunua tende katika mtaa wa Sukari mjini Shinyanga wakati wa ziara yake ya kukutana na wafanyabiashara wadogo wadogo.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga akichukua fungu la bamia katika mtaa wa Sukari
  Lucy Mayenga akizungumza na akina mama wanaofanya biashara zao katika Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya utapeli kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

  Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imethibitika kuwa Shilole alipatiwa kiasi cha fedha Tsh. Milioni tatu kutoka kwa muandaaji wa tamasha hilo Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mton-Kijichi jijini Dar es Salaam.

  Mbele ya mahakama imethibitisha kuwa Shilole alipokea fedha hizo lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

  Kutokana na kitendo hicho, mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo hivyo kumsababishia mwandaaji hasara ya Milioni 14 ambazo mahaakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.

  Baada ya tukio hilo, Mary alifungua kesi mahakamani hapo akiomba kulipwa kiasi hicho cha fedha kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na Shilole kushindwa kufika lakini msanii huyo anadaiwa kupuuza wito wa mahakama.

  Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya hivyo hadi mahakama ilipomuandikia wito mwingine kwenye Gazeti la Uhuru lakini hakufika pia.

  Shilole aliambatana mahakamani hapo na mumewe, Uchebe, na wakili wake ambapo mahakama imemuamuru azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.

  0 0
 • 03/01/18--21:51: TANGAZO
 • CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA, KILICHOPO USA-RIVER, ARUSHA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2018/2019 KAMA IFUATAVYO:


  ASTASHAHADA (CERTIFICATE)

  1.      Astashahada (Certificate) ya ICT (mwaka 1)

  2.      Astashahada (Certificate) ya Usimamizi wa Biashara/ Business Administration (mwaka 1)

  3.      Astashahada (Certificate) ya Uhasibu (Accounting) (mwaka 1)

  4.      Astashahada (Certificate) ya Sheria/Certificate in Law (mwaka 1)  Sifa zinazohitajika:

  ·        Mwombaji awe na ufaulu wa kuanzia alama “D” katika masomo manne.

  AU

  ·        Ufaulu wa kiwango cha ‘subsidiary’ kwa Kidato cha 6

  KOZI ZA STASHAHADA (ORDINARY DIPLOMA)

  5.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika ICT (miaka 2)

  6.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5& 6) Usimamizi wa Biashara/Business Administration (miaka 2)

  7.      Stashahada/Diploma (NTA Level 5 & 6) katika Uhasibu/Accounting (miaka 2)

  8.      Stashahada ya Sheria /Diploma in Laws (mika 2)

  Sifa zinazohitajika:

  ·        Mwombaji awe na Cheti cha NTA Level 4 kutoka chuo kinachotambulika na NACTE

  AU

  ·        Ufaulu kwa kiwango cha “Principle” moja (1) na “Subsidiary” moja (1) kidato cha Sita (A-Level)  NB: Nakala za vyeti vya nje viambatane na Fomu ya uthibitisho wa tathmini toka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

   

  Maombi yafanyike kupitia mtandao wa chuo“ONLINE APPLICATION”katika tovuti ya chuo, yaani: www.makumira.ac.tz  AU

  Chuoni, Tumaini University Makumira, Ofisi ya Msajili.  Mwisho wa maombi kupokelewa ni tarehe 30/03/2018.  Msajili,

  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira,

  S. L. P. 55, Usa River, Arusha

  Simu:  027 254 1034

  Simu za Mkononi: 0753 293986 au 0753 008084


  0 0


  .........................................................................................
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufiga ndani kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani Kagera.

  Ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake wilayani Karagwe mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kupokea taarifa na malalamiko ya kukamatwa kwa mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha Mubali huku kukiwepo mazao yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda katika kisiwa kingine cha Izinga.

  “Ndani ya siku saba hicho kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya msaidie mtengeneze kikosi kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule, inakua ngumu kuadministrate (kutawala) wengine wa kwetu tunawatoa alafu wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza kwa mshangao Dk. Kigwangalla.

  Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji  jambo ambalo alisema  ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kenyata alisema atatekeleza agizo hilo la Waziri Kigwangalla kwa haraka ndani ya muda uliotolewa ili kumaliza mgogoro huo.


  Katika hatua nyingine Waziri Kigwangalla alikataa ombi la Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa la kuiomba Serikali iwamegee wananchi wa vijiji jirani sehemu ya eneo katika Pori la Akiba Kimisi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.


  “Ardhi mimi sitatoa, sjui mlima sjui nini, siwezi kwenda kupeleka hilo ombi kwa Mhe. Rais, kabisa, hicho ni kitu ambacho hatuwezi kufanya kwa sasa’,” Alisisitiza Dk. Kigwangalla.


  Mbunge huyo pia aliiomba Serikali kuweka uzio wa waya kwa ajili ya kutenganisha mpaka wa hifadhi hiyo na vijiji kwa madai ya kuepuka ukamataji wa mifugo ya wananchi unaofanywa na askari wa wanyamapori kwenye ardhi za vijiji na kuingizwa hifadhini na kutozwa faini, hoja iliyopigwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka.


  Hata hivyo, Dk. Kigwangalla alikataa ombi hilo na kusema kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ni mikubwa kuwezesha utekelezaji wa ombi hilo. Alisema Serikali itatengeneza mtandao wa barabara zinazounganisha hifadhi hiyo na vijiji kwa ajili ya kuimarisha doria na shughuli za utalii pamoja na kujenga ofisi ndogo za pori hilo katika kila wilaya inayohusika na pori hilo.


  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka aliwataka wananchi wanaofanya vitendo vya kuingiza mifugo kwenye pori hilo wakati wa usiku kuacha mara moja kwa kuwa wakimatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.


  Alisema malalamiko ya wananchi hao kuwa askari wa wanyamapori wanakamata mifugo yao kwenye maeneo ya vijiji na kuiingiza hifadhini kwa lengo la kuwatoza faini kuwa sio ya kweli na kwamba malalamiko yanakuja kwakuwa hukamatwa asubuhi wakiwa wameshatoka kulisha mifugo hifadhini.


  Kisiwa hicho cha Izinga ambacho kipo katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kina ukubwa wa Kilomita za Mraba 12 na kinapakana na nchi Rwanda.
  Pori la Akiba Kimisi liliqnzishwa mwaka 2003 kwa Tangazo la Serikali na 116 na lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,030. Pori hilo lina wanyamapori mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Simba na Chui. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mwisheni alipofika kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka wakati akikagua Pori la Akiba Kimisi akiwa kwenye ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha mpaka wa Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. Kulia ni Mkuu wa Karagwe, Godfrey Mheluka na Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (kulia kwake).
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia baadhi ya mifugo iliyokamatwa ndani ya Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya Ngara mkoani Kagera jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).

  0 0

  Mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi ,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa pichani .(picha na Mwamvua Mwinyi)
  Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS ) ,Leonard Maboko akizungumza jambo ,mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .(picha na Mwamvua Mwinyi)


  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  TUME ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS), inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kujua afya zao kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.
  Aidha imeeleza ,kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.

  Pamoja na hayo ,kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS ,Leonard Maboko aliyaeleza hayo mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .

  Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .

  Alielezea ,wanaandaa kampeni hizo kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya ukimwi ya mwaka 2016/2017 inayoonyesha idadi ya watu wanaopima na wanaogundulika kuambukizwa wanaoanza kutumia dawa ni wanawake kuliko wanaume.

  “Asilimia 45 ya wanaume ndio wanaoaminika kuwa wamepima na kujua hali zao ,hali ambayo inaonyesha ni kiwango cha chini “.“Simaanishi wenye ukimwi wote wameshapima kujitambua ,lakini inahitajika hamasa ili tufikie malengo”alisema Maboko.

  Hata hivyo Maboko alisema ,maambukizi mapya ya ukimwi yanaongezeka zaidi kwa kundi la vijana hususan wa kike .“Hii inaonyesha huko kipindi cha nyuma hakukuwa na hali hiyo hivyo haina budi kundi hilo likatiliwa mkazo ,ili kupunguza ongezeko hilo ” 

  “Hali ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.1 ,hali inapungua lakini inatakiwa tuendelee kupambana na maambukizi mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana” alisema Maboko.Aliwaambia wajumbe wa mkutano huo ,kuwa asasi mwamvuli zinarahisisha kazi ya uratibu kwa TACAIDS lakini changamoto waliyonayo ni kutopata ripoti za asasi hizo .

  Nae mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi ,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa alisema wanawajengea uwezo wa kielimu viongozi wa dini wanaoishi na virusi hivyo ili kupambana na ukimwi na kuwa vielelezo kwa wengine.

  Sandewa alisema, ugonjwa huo hauchagui ,muumini,viongozi wa dini wala mwalimu hivyo aliiomba jamii kuachana na unyanyapaa.Meneja ufuatiliaji na takwimu ,kutoka baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (NACOPHA) ,Rachel Jacob alifafanua wanaratibu shughuli za masuala ya ukimwi kwa kulenga mtu mmoja mmoja,kundi na mtandao .

  Kwa mujibu wake ,katika kufanikisha shughuli hizo wameshafikia halmashauri 154 nchini kwa kushirikiana na viongozi walioteuliwa ambao wana maambukizi kwa ajili ya kusaidia kuwafikia watu na vikundi hivyo .

  Rachel alibainisha ,kwasasa wana wajumbe 616,984 miongoni mwao asilimia 44 ni wanaume waliojitokeza kuweka wazi afya zao .Alifafanua zoezi hilo nao wanaendelea nalo ,kuhakikisha kufikia halmashauri zote hasa kundi la wanaume ambalo bado halina mwamko huo.

  Katika mkutano huo ,asasi mwamvuli zilizoshiriki ni pamoja na NACOPHA,TAIFO,BAKWATA,FAJISAM-PENTECOSTE,TANERELA,TEC,BAHAI,National Steering Committe, na TIENAI.

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipomtembelea ofisini kwake kupata taarifa ya Viwanda na uwekezaji katika mkoa huo, leo tarehe 1 Machi, 2018.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri walipofika ofisi za SIDO Mkoa wa Njombe kuona utendaji wake.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua eneo litakalojengwa majengo makubwa kwa ajili ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akimsikiliza meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Njombe kuhusu utaratibu wanaotumia katika kupima mizigo ya wakulima na wafanyabiashara mkoani Njombe.
  Muonekano wa Kiwanda cha kuchakata Chai cha Unilever kilichopo mkoani Njombe ambacho kipo katika hatua za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua uenzi wa kiwanda cha Chai cha Unilever, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018.
  Wadau na wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe waliokusanyika kumsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Hayupo pichani) na baadae kuuliza maswali kutokana na changamoto wanazokutana nazo na kupatiwa majibu.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano na wafanyabiashara kujadili changamoto zianazowakabili wafanyabiashara katika mkoa wa Njombe Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza mapema jana mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar kuhusiana na  maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018  litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
   
  Msama ameanza kuwatangaza baadhi ya waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo ambalo limekuwa likiwavutia waimbaji wengi kila linapoanza kuandaliwa na hatimaye kukamilika,Msama amemtaja mwimbaji mahiri jukwaani Boniface Mwaiteje,Christina Shusho,Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake mpya siku hiyo, na wengineo ambao wanaendelea kujiunga kuhakikisha tamasha hilo linafana. Pichani kulia ni mwimbaji Paul Clement pamoja na Beatrice Mwaipaja,ambao walitambulishwa rasmi hapo jana.
  Beatrice Mwaipaja akifafanua zaidi namna ambayo ananendelea kujiandaa na maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa kushoto ni Mwimbaji mwenzake Paul Clement.
   Mwimbaji Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa, kulia ni Mwimbaji mwenzake Beatrice Mwaipaja .

  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Anayemsikiliza ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bwana Tito Kasambala
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bwana Richard Mayongela (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Wakala wa Ndege za Serikali
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali inayosafirisha viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali wakati wa ziara yake kwa Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
  Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Mhandisi Bernard Mayila akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akifanya ukaguzi ndani ya ndege mojawapo inayosafirisha viongozi wa ngazi za juu wa Serikali wakati wa ziara yake alipotembelea Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka baada ya kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali wakati wa ziara yake kwenye Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam

  ……………….

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ndege za Serikali ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali ambapo alizungumza na Menejimenti na wafanyakazi na kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga kuboresha Wakala hiyo

  Mhandisi Nditiye alisema kuwa azma ya Serikali ya Awamo ya Tano inayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinafanya kazi zake kwa weledi na uadilifu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi. “Serikali inatambua umuhimu wa Wakala hii na ina imani kubwa nanyi katika kuhakikisha kuwa mnafanya kazi zenu za kusafirisha viongozi kwa usalama na kwa uhakika ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na tayari ina nia ya kuboresha taasisi hii”, amesema Mhandisi Nditiye.

  Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA Bwana Tito Kasambala amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa taasisi yake ina ndege nne ambazo zinatumika kusafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali katika kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia watanzania na tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 11.4 kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya shughuli mbali mbali za Wakala ikiwemo matengenezo ya ndege, mafunzo kwa wanahewa na ukarabati wa karakana.

  Mhandisi Nditiye amewaeleza wajumbe wa Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala hiyo kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wao na umuhimu wa wahandisi wa ndege na marubani wa kupata nafasi ya kuendesha ndege na kozi za mafunzo mbali mbali kuendana na taaluma zao ambapo tayari makubaliano yamefanyika baina ya Wizara na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ya kuwapatia nafasi marubani wa ndege za Wakala wa Ndege za Serikali nafasi ya kurusha ndege mara kwa mara ili kuendana na matakwa ya taaluma zao.

  Ameongeza kuwa Serikali inashughulikia suala la miundo ya watumishi wa umma ambapo Wakala wa Ndege za Serikali ni mojawapo ya taasisi ambayo muundo wake unafanyiwa kazi ili kuweza kuzingatia taaluma, kada za watumishi na maslahi yao. “Natumaini wote mnatambua na kuelewa kuwa kipindi cha hapo nyuma kidogo utumishi wa umma uliingiwa na baadhi ya watu wachache ambao walikuwa wanafanya ujanja ujanja na kuharibu utumishi wa umma ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wetu, imelifanyia kazi jambo hili na ameunda bodi maalumu ambayo inafanyia kazi suala la muundo, kada na maslahi ya watumishi wa umma,” amesema Mhandisi Nditiye.

  Aidha, wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali wamemuomba Mhandisi Nditiye kuwasilisha ombi lao kwa Serikali la kuwaongezea mishahara yao kuendana na hali ya soko la ajira ya marubani ilivyo nchini kwa sasa.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandis Seth Luswema akitoa ripoti ya kuhusu sekta ya umwagiliaji kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso katika kikao na watumishi wa tume hiyo.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao kilichofanyika katika ofisi za tume hiyo.
  Sehemu ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliohudhuria katika kikao na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso.  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema wizara yake itaifanyia mabadiliko makubwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutokana na udhaifu mkubwa aliougundua kiutendaji, hali inayosababisha kutotimiza majukumu yake kwa ufanisi.

  Naibu Waziri Aweso amesema kuwa tume hiyo kwa muda mrefu imekuwa haifanyi kazi yake vizuri na imembidi afike katika tume hiyo ili kufahamu undani wa tatizo hilo, kwa kuwa Serikali imeazimia kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuunga juhudi za kuinua uchumi wa viwanda nchini.

  ‘‘Tuna zaidi ya hekta milioni 29.4 za ardhi kwa ajili ya kilimo, lakini hekta 468,000 sawa na asilimia 24 pekee ndio zimeendelezwa, hii manake bado tuko nyuma sana katika uzalishaji wa chakula pamoja na kuwa na eneo kubwa. Hili ni tatizo ambalo wizara italichukulia hatua za haraka’’, alisema Naibu Waziri.

  Aliendelea kusema kuwa kuna haja ya kuipa nguvu sekta ya umwagiliaji kwa kuwa dhana ya uchumi wa viwanda inategemea sana kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea msimu wa mvua, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakikidhi mahitaji ya taifa.

  ‘‘Sijaridhishwa kabisa na utendaji wa Tume ya Umwagiliaji na kuna tatizo katika menejimenti yenu na kusababisha utendaji mbovu, mabadiliko makubwa yanahitajika ili kuleta ufanisi wa tume hii ili tuanze kuona tija katika sekta ya umwagiliaji,’’ alisema Aweso.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji, Mhandisi Seth Luswema amesema kuwa amefarijika na ujio wa Naibu Waziri kwa kuwa hawajawahi kuwa na kikao ambacho wameweza kueleza changamoto zao, na kukiri kuwa kuna kasoro nyingi za kurekebisha kiutendaji ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.

  0 0

  Mhe Stanislaus Mabula Leo amemkabidhi tenki kubwa la maji Diwani mteule Kata ya Isamilo Mhe Charlse Nyamasiriri linaloweza kuhifadhi lita 10000 za maji kwa ajili ya shule ya Secondari ya Ole Njoolay iliyopo Kata ya Isamilo. Hii ni sehemu ya ya utekelezaji wa mkakati wa kuondoka kero za tatizo la maji katika shule za msingi na sekondari Jiji la Mwanza.

  Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini za mbunge Jimbo la Nyamagana.

  Mwanza kwanza, Tukutane kazini

  Tulianza na Mungu, tutaendelea na Mungu

  Imetolewa na,
  Ofisi ya Mbunge
  Jimbo la Nyamagana🇹🇿 @ Mwanza.

  0 0

   Zaidi ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

  Madiwani hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).

  Madiwani hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi unaotekelezwa katika eneo hilo.

  Pamoja na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.

  Wakiwa kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.Eneo hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.

  Aidha katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kujifunza, faida za mabunge ya jamii, na kujifunza miradi ya maendeleo ya kuwezesha wananchi kiuchumi ambayo inatekelezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wananchi wa Kipunguni.

  Katika mabadilishano ya uelewa mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya, Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao.

  Alisema awali alikuwa akidhani kwamba asasi hiyo ina mlengo wa kisiasa kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwao lakini baada ya elimu hii amebadili uelekeo na kuitaka taasisi hiyo kupeleka elimu Tanzania nzima.

  Alisema, "Anaona kwamba TGNP ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika nyanja zote."Diwani huyo wa Ijombe ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii alisema pamoja na kubadili mwelekeo aliwataka wabunge kuona kwamba wanapoandaa miradi hawaandai mbunge mpya bali kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.

  Katika mkutano huo walitoa maazimio kadhaa ya kufanyiwa kazi katika halmashauri.Miongoni mwa maazimio hayo ni namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake kuhusu ile asilimia 5 na kutekeleza dhana ya viwanda.

  Kwa mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.

  Pia imeelezwa haja ya TGNP Mtandao kuendelea kutoa elimu kwa kusaidiwa na mabaraza ya halmashauri kuhusu rasilimali fedha na kufuatilia uwekezaji katika ujenzi wa hosteli kupunguza umbali wa watoto wa kike kutembea kufuata shule.Mambo mengine ni kuona kwamba uandaazi wa bajeti unaanzia ngazi ya kijiji au mtaa badala ya kata na kukosekana kwa sauti za wananchi katika bajeti.

  TGNP Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha miaka 25 sasa, kwa kipindi chote hicho kimeshirikiana na taasisi za serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

   Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.  Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.Diwani wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Ukenyenge ya wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Anderson Mandia akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washiriki wakiendelea kujadiliana wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 03/02/18--00:03: tangazo


 • 0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017 unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa. 
  Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin. 
  Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
  Mkutano ukiendelea. 
  Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha.

  0 0


   Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiwaonyesha mmoja ya sehemu zinazotunzwa tablets ambazo zinatumiwa kufundishia wanafunzi akiwa na wafadhili wa mradi huo

  Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akiwaongoza wafadhili wa mradi huo kutembelea maeneo mbalimbali unapotekelezwa wilayani Pangani
    Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akiwa na wafadhili wa mradi huo wakiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kutumia teknolojia ya Tablets
  Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiteta jambo na wafadhili wa mradi huo
  Wadau wa mradi  wa  miaka mitano wenye lengo la kutumia  teknolojia ya kisasa kuwawezesha watoto waliona fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) wameeleza kuridhishwa kwao na maendeleo ya majaribio hayo.

  Wadau ambao walikuwa na ziara ya siku moja kutembelea vijiji mbalimbali vya nradi huo katika wilaya za Muheza na Pangani wadau aho ambao walikuwa pamoja na Mwakilishi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Tanzania, Michael Dunford, Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Kanda ya Afrika Mashariki, Anne Ndong-Jatta wakiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said.
  Wakitoa maoni wakati wakipewa maelezo walisema ni wazi mradi umeanza kuonyesha uwezo wa teknolojia kuamsha ari ya kujifunza na kusoma.
  Taarufa za awali za mradi na ushuhuda tuliouona inaonyesha kuwa mpango huu wa kiteknolojia una uwezo wa kuwasha mwamko wa elimu miongoni mwa watoto na wazazi na unapaswa kutiliwa maanani, alieleza  Mhandisi Said wakat wa ziara hiyo.
  Pia Mhandisi Said alisema kuwa ni wazi pia kuwa kuwatambulisha wananchi katika teknolojia ya kisasa wakiwa na umtri mdogo kunawahakikishia  watoto hao kuwa hawawezi kunyanyaswa hapo baadaye wakiwa wakubwa.
  Naye Ndong-Jatta alisema kuwa mradi unaonyesha haja ya kuangalia uwezekano wa kupunguza tatizo la kutojua kusoma na kuandika kwa wazazi kama njia mojawapo ya kuamsha mwamko wa elimu miongoni mwao na kuwawezesha kuwasukuma watoto kwenda shule.
  Zaidi ya watoto 2,500 kutoka katika vituo 142 vilvyopo katika wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza na Pangani walipewa tablet mpya aina ya Google Pixel C, zilizotolewa kwa hisani ya Google. Tableti hizo zimewekewa mifumo ya elimu kutoka kwa washindi watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE. Washindi hawa walichaguliwa kutoka katika timu 198 napaneli ya majaji 11 wa kujitegemea na walio wataalamu na kutangazwa mwezi September, 2017 wakati wa wiki ya BarazaKuu la Umoja wa Mataifa
  Mradi huo wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Mareka ni milioni 15. Mradihuu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wa bunifu kubuni na kuandaa zana za kusaidia kuondoa ujinga duniani na kuwasaidia watoto ambao hawajapata fursa ya kwenda shule kujifunza wakiwa nyumbani (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

older | 1 | .... | 1530 | 1531 | (Page 1532) | 1533 | 1534 | .... | 1898 | newer