Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1529 | 1530 | (Page 1531) | 1532 | 1533 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Uganda, Mhe. Edward Sekandi (kushoto) kwenye Mkutano wa kuboresha mazingira ya Biashara kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mhe. Sekandi ndiye alikuwa Mgeni Rasmi na ndiye aliyefungua Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo, Nchini Uganda kuanzia tarehe 28 Februari hadi 01 Machi, 2018.

  0 0

  Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.

  Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

  Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu  alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko  hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.  

  Naye mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.

  Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika masuala ya maabara.

  Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Shirika la Maabra  SANDIA na DTRA  wameandaa mkutano wataalam hao.
   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akieleza  jambo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
   Mtaalamu Masuala ya Mpango Mkakati  wa Maabara  kutoka Shirika la Maabara –SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
   Baadhi ya Wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,  wakijadiliana namna ya kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi  na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
   Wataalamu wa Afya moja wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya   mkutano wa kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.

  0 0


   Mwenyekiti wa Kavazi la kwanza la Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2018 Dkt. Ng’wanza Kamata ambaye ni mahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), akichokoza mada kuhusu matumizi ya mbegu za GMO na teknolojia ya uhandisi jeni katika kilimo. Kulia ni Dk.Richard Mbunda  kutoka UDSM. 
   Wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dar es Salaam jana.
   Mkutano ukiendelea.
   Dk.Richard Mbunda  kutoka UDSM, akielezea changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi ya mbegu za GMO katika kilimo.

  Usikivu katika mkutano huo. 
   Dkt. Aloyce Kulaya akichangia jambo kwenye mkutano huo.
   Dkt. Adolphine Kateka akichangia.
   Dkt. Goodluck Ole Medeye, akielezea umuhimu wa mbegu hizo katika kilimo.
   Alfred Mmbaga kutoka Tanzania Meat Board akichangia mada.
    Elisa  Greebe kutoka Chuo Kikuu cha Leeds akichangia.
   Mkulima mdogo Ernest Likoko akichangia mada.
   Dk Emmarold Mneney akichangia mada kwenye mkutano huo.
   Emma Nyerere kutoka Taasisi ya Pawo Pan African Women Organisation Tanzania akichangia jambo.
   Dkt. Nicholous Nyange, akizungumza kwenye mkutano huo.
  Mada zikichangiwa.
  Dkt.Roshan Abdallah kutoka Agricultural Innovation Research Foundation Tanzania, akichangia jambo.

  Na Mwandishi Wetu

  WASHIRIKI wa Kavazi la kwanza la Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2018 wameomba elimu zaidi itolewe kwa jamii ili kusaidia kuwa na uelewa wa pamoja kama nchi katika kuelekea kutumia teknolojia ya uhandisi jeni kukablina na changamoto zinazomkabili mkulima nchini kwa sasa na kuinua tija.

  Wakichangia mjadala huo uliolenga kuangalia nafasi ya mbegu za GMO na teknolojia ya uhandisi jeni katika kilimo wadau hao kutoka sekta na taasisi mbalimbali nchini wamesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na watafiti kwa kushirikiana na serikali na makampuni mengine ya nje jamii inahitaji kuelimishwa ili kuondokana na mashaka ambayo yamekuwa yakizunguzwa na baadhi ya wadau kuhusu mbegu hizo.

  Wamesema wakulima wengi uzalishaji wao ni mdogo kutokana na  kutumia zana duni,kutozingatia kanuni bora za kilimo,Mbegu zisiszo bora  na teknolojia zingine ambazo zimewafanya wakulima kuendelea kubaki palepale na kuona kilimo sio kazi yenye tija na thamani kama kazi zingine na hivyo wadau hao kuomba mjadala mpana ufanyike wa kitaifa kuhusu teknolojia ya GMO na kuona kama ina mchango katika kusaidia kumkomboa mkulima kutoka katika hali yake ya sasa.

  Akizungumzia umuhimu wa mbegu hizo za GMO kwa taifa na wakulima nchini aliyekuwa (Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika serikali ya awamu ya nne) ????? Dkt. Goodluck Ole Medeye alisema kuwa mchakato wa kuanza au kutokuanza kutumia mbegu za GMO ulianza zamani lakini serikali kupitia waalamu wake walikaa chini na kutathimini uhitaji wa teknolojia hiyo na kuona kuwa ni mkubwa na hivyo kuamua kuwapa nafasi watafiti kufanya kwanza utafiti ili kujiridhisha juu ya faida na hasara zake.

  Alisema kuwa yeye binafsi alikuwa mtu wa kwanza kupinga matumizi ya mbegu zinazotokana na teknolojia hiyo lakini baada ya kuwapa nafasi watafiti kueleza na kuwaelimisha mawaziri na viongozi wengine wa serikali aliona kuwa hakuwa sahihi na kwa pamoja wakafikia uamuzi wa kuwaruhusu watafiti wafanye utafiti nchini ili kujiridhisha kuwa na uwezo wa kutambua mbegu na bidhaa zitokanazo na teknolojia hiyo.

  Dkt. Medeye aliongeza kuwa hakuna namna ambayo Tanzania itakwepa kutumia mbegu hizo au bidhaa za GMO kwakuwa Tanzania sio kisiwa kama nchi zinazoizunguka Tanzania zinafanya tafiti kwa kasi na kutumia mbegu hizo basi Tanzania itajikuta wananchi wake wanatumia mbegu hizo kwani kwa sasa nguo nyingi tunazovaa zinatoka nchi zinazozalisha pamba ya GMO na baadhi ya vyakula  tunavyokula kutoka nje vinatokana na mbegu za GMO.

  Waziri huyo wa zamani amebainisha kuwa wakulima wengi wa Tanzania kwa miaka nenda rudi bado wanazalisha chakula kidogo sana ambacho hakikidhi mahitaji ya kaya zao na kupata ziada kwaajili ya kuuza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo zana dunia,kutotumia mbinu bora za kilimo na hasa mbegu bora hivyo ni wakati sasa nchi ikaona umuhimu wa kumuinua mkulima kwa kumpatia mbegu zenye kumletea matumani na tija.

  Kwa upande wake mtafiti mstaaafu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dkt. Nicholous Nyange ambaye alikuwa mtafiti kwenye masuala ya tafiti za bioteknolojia za kilimo nchini aliyewasiliasha mada juu umuhimu wa teknolojia na mbegu za GMO amesema kuwa inakadiriwa kuwa Tanzania kwa sasa inawatu wapatao milioni 58 na idadi hii inaongezeka kila siku na kama sayansi haitatumika kusaidia kuzalisha chakula cha kutosha basi huenda taifa likasumbuliwa na njaa kila mwaka kwenye maeneo mengi.

  Alisema wakulima pamoja na jitihada kubwa zinaofanywa na wakulima kulima na kupanua mashamba kila siku lakini bado hawajaweza kuzalisha chakula cha kutosha kutokana nasababu mbalimbali ikiwemo wadudu,magonjwa na changamoto zingine zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Ukame kwenye maeneo mengi ya nchi kwa sasa.

  Dkt,Nyange  amesema kawimu zinaonyesha kuwa Tanzania kwenye uzalishaji wa mahindi unakadiriwa kufikia ati ya tani 1.5 hadi tani mbili pale ambapo hali ya hewa na mtawanyiko wa mvua utakuwa mzuri lakini kwa nchi zilizoendelea kama vile marekani wanazalisha tani 8 hadi 9 kwa ekari kutokana na kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji .

  Alisema kuwa pamoja na uchumi wa taifa kukua kwa silimia 7 lakini kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa mtanzania ambao zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanakitegemea chenyewe kinakua kwa asilimia 3 tu na hivyo kusema kuwa kama teknolojia ikitumika na wakulima wakawezeshwa kilimo kitaweza kuchangia vyema kwenye pato la taifa na kuwanufaisha wakulima ambao tunaona TASAF inawapa fedha kupitia mpango wa serikali wa kusaidia  kaya masikini.

  Aliongeza kuwa eneo linalofaa kwa kilimo na makazi likigawanywa kwa idadi ya watu waliopo nchini katika kipindi kifupi kichacho halitatosha kupata maeneo ya kutosha kwaajili ya kilimo makazi na shughuli zingine za kibinadamu hivyo njia pekee ni kuwawezesha wanananchi na wakulima kutumia mbinu za kisasa kuzalisha kwa wingi kwenye maeneo madogo ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu na eneo la nchi lililopo ambalo haliongezeki.

  Kwa upande wake Dkt. Aloyce Kulaya mtafiti wa zao la mahindi mstaafu na mshauri wa mradi wa Water efficient Maize for Africa (WEMA) alisema kuwa suala la GMO linaangalia tuu kwenye vyakula lakini teknolojia hiyo inatumika zaidi kwenye kutengeneza madawa kama yale ya kisukari na kubainisha kuwa hata kama dawa ya ukimwi ikipatikana basi inaweza kuwa kwa kutumia njia hii pekee na sio nyingine.

  Alisema teknolojia ya uhandisi jeni sio ndio njia pekee ya kupata ufumbuzi wa matatizo ya wakulima lakini pale mbinu za kawaida zinaposhindwa ndio teknolojia hiyo pekee hutumika katika kupata ufumbuzi wa haraka na sahihi wa changamoto za magonjwa,ukame na wadudu ambazo zinawasumbua wakulima nchi nzima ambayo binu za kawaida zimeshindwa.

  Dkt. Kulaya aliongeza kuwa kwa wasiwasi wa watu kuwa mbegu za asili zitapotea hauna maana kwakuwa mbinu hizo za kuupatia mmea kinga na uwezo wa kuwa na sifa fulani kunaweza kufanyika pia kwenye mbegu zetu za asili na hivyo kuziwezesha mbegu hizo kuhimili magonjwa,wadudu na changamoto zingine na kumuwezesha mkulima kupata mazao ya kutosha.

  Kwa upande wake Profesa, Rwaitama ameitaka serikali kuwezesha vituo vyetu vya utaifa nchini kuwa na uwezo wa kufanya tafiti hizi ambazo zinaweza kusaidia kuwainua wakulima kupambana na changamoto zinazowakabili badala ya kutegemea wafadhili pekee ambao wanapoleta fedha kwenye utafiti Fulani wanakuwa na vigezo vyao na sio lazima view kipaumbele cha nchi.

  Alisema vituo vingi vya utafiti vya zamani vilikuwa vinafanya kazi nzuri katika kazi za utafiti lakini kwa sasa vimeshuka utendaji wake na kuonekana kuwa na mchango mdogo sana kwa maendeleo ya nchi ili kuweza kuwa na udhibiti wa kile kinachozalishwa kuwa mali ya taifa kwakuwa kitakuwa kimezalishwa kwa kutumia fedha za wananchi.

  Prof. Rwaitama akitolea mfano wa utafiti wa Panya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) alisema ni moja ya matunda makubwa ambayo yanaipatia Tanzania na watafiti wake heshima kubwa katika kutumia panya kufanya kazi mbalimbali kubwa duniani kama vile kutambua mabomu,makohozi ya TB kwa haraka.

  Naye Mwenyekiti wa mkutano huo Dkt. Ng’wanza Kamata ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) alisema kuwa Kavazi la Mwalimu Nyerere litaendelea kufanya mijadala juu ya jambo hili kila mara ili kusaidia kuwepo kwa mjadala mpana katika kujadili faida na hasara za teknolojia ya Uhandisi jeni kabla teknolojia hiyo haijamfikia mkulima.

  Alisema wananchi wote wakielewa vizuri jambo hili litasaidia kuondoa mashaka juu ya usalama wa teknolojia ambao umekuwa ukitolewa na watu mbalimbali na mashaka hayo yakiondoka ndipo sasa kila mtu anaweza kuwa huru kuchagua kuitumia teknolojia hiyo au la kwa manufaa yake na manufaa ya taifa kwa ujumla.

  Profesa, Kamata aliongeza kuwa mashaka ni lazima kwa jambo lolote au teknolojia yoyote mpya inapoingia sokoni na huu ndio wakati muafaka wa watafiti kusikia mashaka na watu na kisha kuyatafutia majibu ya kisayansi kwani hakuna mtu anayeweza kufurahia jambo bila kuwa na wasiswasi hususani kwa teknolojia mpya yoyote.

  Awali akiwasilisha mada yake ambayo ilitakiwa kujibiwa na Dkt. Nyange dhidi ya GMO mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaamu, Richard Mbunda alisema bado kuna taarifa ambazo zinapishana katika kiwango ambacho mbegu za GMO zinazostahimili ukame ambazo zinefanyiwa majaribio kwenye kituo cha utafiti wa kilimo makutupora katika uwezo wake wa kupunguza hasara kwa mkulima.

  Mbunda amesema mashaka makubwa wanayoyaona baadhi ya watu ni kuhusu usalama wa vyakula vinavyotokana na mbegu za GMO kama chakula kwa maana ya afya na mazingira mambo ambayo ni lazima watafiti wayaangalie na kujiridhisha kabla ya kuzipeleka mbegu hizo kwenye mamlaka za serikali zinazopitisha mbegu zote nchini.

  Mtoa mada huyo alieleza wasiswasi wake na kutaka kujua juu ya namna mkulima mdogo atakavyoweza kunufaika na teknolojia hiyo ili isijemfanya mkulima kuwa mtegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi na kutaka kujua namna wakulima watakavyoweza kupata mbegu hizo kwa urahisi na bei nafuu pale ambapo zitapitishwa na kuwa mbegu ili kutumika hapa nchini.  0 0  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.


  Na Bashir Nkoromo, Pugu

  Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.

  Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo, Waziri wa Mifugo na Uvivi Luhaga Mpina ametoa agizo hilo kunusuru hali ya fukuto la mapigano katika ya wafanyabiashara kwenye mnada huo kudai Wanakijiji hicho cha Bangulo kuvamia eneo la malisho.

  "Baadhi yenu mmeonyesha hapa hati za kumiliki makazi, lakini pia tunafahamu kuwa eneo la Mnada lilikuwa na ukubwa wa ekari 190, hivi sasa limebaki eneo kama asilimia 20 tu ya malisho. Hali hii inaufanya Mnada huu kukosa sifa, hivyo wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu naagiza shughuli zote za ujenzi na kilimo zisimame kwanza kuanzia leo," alisema Mpina.

  Waziri Mpina amewataka wananchi kuishi bila hofu akisema suala lao litapatiwa ufumbuzi ambao utakuwa wa kudumu.

  Sehemu ya eneo la Mnada wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkaribisha kufanya ziara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alipowasili kwenye Mnada wa Pugu wilayani hummo, Dar es Salaam, leo
  Waziri Mpina akimsalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipowasili kwenye Mnada wa Pugu leo
  Waziri Mpina akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kabla ya kuanza ziara
  Sohia Mjema akimuongoza Waziri Mpina kwenye eneo la kufanya mazungumzo na uongozi wa Mnada huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo
  Mkuu wa Mnada wa Pugu Kevamba Samwel akizungumzia hali ya maendeleo na changamoto za Mnada huo
  Matibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na mkuu wa Mnada huo
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akieleza anavyozijua na alivoanza kuzishughulia baadhi ya changamoto za Mnada huo hasa mgogoro wa arhi baina ya Mnada na Wananchi
  "Naona mda unakwenda mbio, hebu tuanze utembeleaji mipaka..." akasema waziri Mpina huku akitazama saa yake
  Waziri Mpina akijadiliana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kipi waanze kati ya kuzungumza kwanza na wananchi au kukagua mipaka
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akiwa ameweka bakora begani wakati safari ya kukagua mipaka ikianza. Kushoto ni Katubu wa Mwenezi tawi la CCM Bangulo Kata ya Pugu Stesheni Loyce Hamisi
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kushoto) akiongoza kupanda moja ya vilima vilivyo katika Kijiji cha Bangulo wakati akikagua mipaka ya kijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema naye akijiandaa kupanda kilima hicho
  "Kwa hiyo hadi kulee ni eneo la malisho ya Mnada?" Waziri Mpina akiuliza maofisa aliofuatana nao. Wapili kushoto ni DC Mjema
  Afisa wa Mnada akimpatia maelezo waziri Mpina kuhusu lilivyo eneo la malisho ya Mnada wa Pugu
  Kamanda wa Polisi wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi Salim Hamduni akiongoza msafara wakati wa kushuka baada ya Waziri Mpina kukagua badhi ya maeneo ya mipaka kati ya kijiji cha Bangulo na Mnada wa Pugu
  Kisha waziri Mpina naye akashuka kilima hicho
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
  Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Bangilo kinachodaiwa kuvamia eneo la malisho ya Mnada wa Pugu. Kushoto ni Waziri Mpina
  "Wenyewe mpo?" Waziri Mpina akiuliza huku akichungulia kwenye geti la nyumba moja inayoonyesha kujengwa hivi karibuni ambayo inadaiwa kuwa miongoni mwa nyumba za wananchi wa kijiji cha Bangulo waliovamia eneo la malisho la Mnada wa Pugu.
  Aloyce Malya mkazi wa Kijiji cha Bangulo akizungumza wakati waziri Mpina alipozungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya wanankijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
  Kisha Aloyce akatia hati yake ya umiliki wa ardhi na kumkabidhi waziri Mpina
  Waziri Mpina akiipitia kwa makini hati hiyo baada ya kuipokea
  Hati yenyewe kwa karibu
  Waziri Mpina akizungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mipaka kati ya wananchi na Mnada wa Pugu
  Wananchi wakimsikiliza waziri Mpina
  Waziri Mpina akiwaaga baada ya mazungumzo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  SERIKALI imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

  Hayo yalibainika jana (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara yake.

  Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi alisema fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.Alisema jumla ya sh. bilioni 1.2 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kwenye Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji kutobadilisha matumizi.

  Waziri Mkuu alisema ujenzi huo utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha kuhifhadhia maiti.“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”

  Aidha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.

  Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema Serikali itawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili kuwazuia wasipate mimba.Bw. Byakanwa alisema wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wamebainika kuwa wanatumia dawa za kuzuia mimba wakiwa shuleni, hivyo kuwaruhusu kushiriki katika matendo yasiyokuwa ya kimasomo.

  Alisema Serikali itafanya msako wa kuwatafuta wote wanaotumia dawa hizo pamoja na wanaowapa na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa sababu jambo ni hatari kwa maendeleo ya wanafunzi hao.Naye, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Josephat Kakunda alisema alisema Serikali imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ili kuboresha huduma za afya.

  Asema kati yake sh. milioni 700 zilipelekwa katika kituo cha afya cha Nanyamba ambapo sh. milioni 300 zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa na sh milioni 400 ukarabati wa kituo, huku sh. bilioni 1.2 ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Njengwa.Haya hivyo, Waziri huyo alisema kuwa Serikali inampango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto kwa kuondoa kipengele cha dhamana kwa watu watakaotuhumiwa kuwapa mimba watoto wa shule.

  Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya watuhumiwa hao wanapopewa dhamana kwenda kuzungumza na wazazi au walezi wa binti jambo linalochangia katika kuharibu ushahidi.” Ni bora wakakaa rumande hadi hukumu itakapotolewa na kama hawatokutwa na hatia watarudi uraiani”.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 01, 2018.

  0 0


   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika shughuli ya kupokea vifaa vya shule kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akipokea baadhi ya vifaa vya kuwasaidia watoto wenye ulemavu kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la ADD Bi.Rose.

     Viongozi mbalimbali wakishiriki katika upokeaji wa vifaa vya aina mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto wenye ulemavu vilivyotolewa na ADD.

  Viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji wa ADD walioshiriki zoezi la ugawaji vifaa vya watoto wenye ulemavu.

  ............................................................
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameagiza mikoa yote kukamilisha uundwaji wa kamati za walemavu kwa ngazi za mkoa, wilaya, na kata kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2017/2018.


  Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa akipokea vifaa vya kufundishia watoto wenye ulemavu mbalimbali kutoka kwa Shirika la kimataifa linaloshughulikia walemavu la ADD.


  Amesema amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na na kusuasua kwa uundwaji wa kamati hizo ambazo zimeelekezwa kwa mujibu wa sheria.


  Naye,Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania, Ummy pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la ADD Rose, wameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Magufuli kwa kuwajali sana walemavu hapa nchini.


  Hata hivyo wameomba kuendelea kushughulikia  changamoto ambazo bado zinawakabili watoto zikiwemo uchakavu na upungufu wa miundombinu hususan vyumba vya madarasa, vifaa vya kutosha vya kujifunzia, pamoja na mazingira wezeshi kwa walemavu hususan baadhi ya  miundombinu inayojengwa kutokuzingatia mahitaji ya walemavu.  Katika zoezi hilo, Shirika la ADD limesaidia vifaa mbalimbali vya kuwawezesha watoto wenye  ulemavu  kusoma vizuri vyenye thamani ya sh. milioni 174.

  Click here to Reply or Forward 5.1 GB (34%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 26 minutes ago Details

  0 0


  Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii

  MEYA  wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita ametemtembelea nyumbani kwakwe na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwasisi na mkongwe wa Chadema Victa Kimesela ambaye anaumwa kwa muda mrefu sasa.

  Kimesela ni miongoni mwa waasisi walioshiriki kuandaa Katiba ya chama hicho mwaka 1992, anaugua kwa muda ambapo familia yake ilimueleza Meya Mwita kuwa alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hivyo kuruhusiwa Jumatano iliyopita.

  Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Christina Mwagala amesema muda fupi baada ya  Meya Mwita kufika nyumbani  kwa mwasisi huyo, afya yake ilibadilika.

  Hivyo kwa kushirikiana na familia hiyo  walitoa taarifa Muhimbili ili kupatiwa gari ya kubebea wa gonjwa.Aidha  gari hiyo ilifika na kisha Mwita na familia hiyo waliambatana pamoja kumuwahisha kwa mara nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu awali.

   Mwagala amesema kuwa Kimesela amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chadema, ikiwepo kuwa Katibu mtendaji wa chama hicho wakati wa utawala wa mzee Edwin Mtei.

  Pia amewahi kuwa Katibu mkuu wa muda wakati wa utawala wa Bob Makani(marehemu)na hivyo kumuachia nafasi hiyo Dk.Wilblod Slaa ambaye kwa sasa amestaafu siasa tangu  mwaka 2015.
   
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita akiwa pamoja na familia ya Kimesela ,wakitoa msaada wa kumpakiza kwenye gari ya kubebea wagonjwa ya hospital ya Taifa Muhimbili jana alipomtembelea nyumbani kwakwe.Kimesela anaumwa na kwa sasa amelazwa katika hospital ya Taifa Muhimbili.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na mke wa  Kimesela , Suzani Kimesela alipomtembekea nyumbani kwake jana .

  0 0

   

  NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na sehemu ya wakulima wa chai alipowasili kwenye kijiji cha Lwangu Wilaya ya njombe mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
  Sehemu ya wakulima wa chai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipozungumza nao. 
  Sehemu ya wakulima wa chai wakikusanya zao hilo baada ya kutoka kuvuna wakati Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara na kuzungumza nao. 
  NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea na wakulima wa chai alipotembelea kijiji cha Lwangu Mkoa wa Njombe hivi karibuni. 
  Sehemu ya wakulima wa chai wakimpongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya nao mazungumzo wakati wa ziara yake kwa wakulima hao. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akimwagiza Meneja Mkuu wa Njombe Outgrowers Services Company (NOSC), Fibert Kavia (kushoto) kuhakikisha risiti zao zinaonyesha kiasi cha fedha mkulima wa chai anachotakiwa kulipwa baada ya kupima bidhaa hiyo wakati kuuza zao hilo kwa kampuni hiyo. Wanaosikiliza (wa pili kushoto) ni Mkulima wa chai iliyopimwa, Juliana Casian na Karani wa NOSC, Flora Sanga. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto) akiangali kitalu cha mbegu za kupandikizwa za maparachichi alipofanya ziara na kuzungumza na wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Nundu, Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe. Kushoto ni Afisa Kilimo wa Wakulima wa zao hilo, Damasi Kasalala, Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo na ujumbe wa viongozi wa serikali. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya mche uliopandikizwa wa parachichi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (kulia) na Afisa Kilimo, Damasi Kasalala alipofanya ziara na kuzungumza nao wakulima wa zao hilo. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo. 
  Wataalamu wa kuandaa mbegu za parachichi, Henry Mwepel (kulia), na Lugano Mwalusi wakifanya upandikizaji wa miche ya parachichi kutoka ule wa asili kuwa wa kisasa katika kitalu maalumu cha uzalishali wa zao. 
  NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, alipowatembelea na kuzungumza nao kujua changamoto zao na kutoa ushauri wake kukabiliana nazo. Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. 
  Wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, wakimpokea kwa furaha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akiwasabahi wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe alifanya ziara mkoani humo. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kulia) Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga wakifuatilia jambo Mhe. Mwanjelwa alipozungumza na wakulima hao. 
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kukusanya, kuchambua, kufungasha na kuuzia viazi mviringo kijiji cha Lusitu, namna bora ya uzalishaji wa viazi wakati Mhe. Mwanjelwa alipofanya ziara na kufanya nao mazungumzo. 

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI  ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo ambayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess
  Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

  Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii

  KAMPUNI  ya Jumia Tanzania  inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo.

  Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

  “Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’  "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania.

  " Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema.

  Ameongeza ni  mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott.

  Akifafanua namna Jumia ilivyodhamiria kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara nchini ameelezea wafanyabiashara wanakumbwa na changamoto lukuki katika uendeshaji wa biashara zao.

  Ametaja baadhi yake ni  gharama kubwa za pango hususani kwenye maeneo yenye wateja wengi. "Hali hii husababisha wafanyabiashara wengi kuwa na idadi ya wateja walewale kulingana na eneo walilopo,” amesema na kuongezea,

  “Ili kuwafikia wateja kuwajulisha kuhusu biashara zao, inamlamzimu mfanyabiashara kufanya matangazo na kutafuta masoko, jambo ambalo ni gharama kubwa na sio wote wanakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.”

  Amefafanua Jumia ndio suluhu pekee kwa wateja na wafanyabiashara kwani imekusanya bidhaa za aina tofauti sehemu moja, ikitoa bei zenye ushindani, pamoja na kumfikishia mteja popote alipo kwa urahisi.

  Amesema mteja anaweza kufanya manunuzi mwenyewe kwa kuingia kwenye mtandao wao, akachagua bidhaa azipendazo na kisha akapelekewe mpaka alipo baada ya kuagiza.

  " Katika kujenga uaminifu kwa wateja wetu, malipo hufanyika baada ya kumfikia mteja. Kwa kuongezea, mteja huwa hadaiwi malipo pindi asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa au akitaka ifanyiwe mabadiliko.

  "Hivyo, tunawaahidi wateja wetu bidhaa nyingi zaidi kukidhi mahitaji yao, bei zenye ushindani zaidi na kuwafikishia bidhaa popote walipo kwa haraka, urahisi na gharama nafuu,” ameongezea.

  Amesema zaidi ya kampuni 50,000 za kiafrika zinauza bidhaa zake kupitia Jumia kila siku na kwamba wanafanya jitihada za kuhamisha shughuli za kiuchumi kwenda mtandaoni

  Na kuziwezesha kampuni za Kiafrika ndogo, za kati na kubwa kupata wateja wapya na kuwahudumia kwa mbinu mpya.

  " Takribani wajasiriamali na wafanyabiashara 50,000 wanauza bidhaa zao kupitia Jumia, zaidi ya bidhaa 10,000 zinajitangaza kupitia Jumia.

  "Pia kampuni kadhaa za usafirishaji husafirishaji mamilioni ya bidhaa kila mwaka kwa sababu ya Jumia. Kila siku, tunasaidia na kuhamasisha migahawa, hoteli, wafanyabiashara wadogo, bidhaa, mawakala wa makazi na usafiri,

  "Makampuni makubwa, kampuni za usafirishaji kuwa bora na kubwa, kwa kutumia msaada wa ripoti za tafiti mbalimbali kuzisaidia kuwa bora na kutoa huduma nzuri kwa wateja," amesema .

  Ameongeza wanaamini  kupitia hivyo wataleta mabadiliko chanya barani Afrika.

  Prescott amesema mojawapo ya fursa ambayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania bado hawajaigundua ni namna ya kuwafikia wateja wanaopatikana mtandaoni.

  Ambapo amesema ni kwa kujiunga na Jumia, watawapatia fursa ya kukuunganisha na mamilioni ya wateja waliopo mtandaoni.

  " Tunaweza kumuwezesha mfanyabiashara mdogo anayefanya shughuli zake kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam kuuza bidhaa zake kwa wateja walioko Tanzania nzima.

  "Tunazitangaza bidhaa tofauti kwa kuziwezesha kuonekana kwa mtu yeyote aliyeunganishwa na mtandao wa intaneti,” amesema.

   Mkurugenzi Mkuu huyo mpya wa Jumia nchini Tanzania,amesema  “wafanyabiashara wanaojiunga nasi hawana haja ya kugharamia shughuli za kutafuta masoko au kukodisha maduka kwa gharama kubwa.

  "Hii ni huduma ambayo Jumia huitoa kwa kamisheni nafuu kupitia mauzo yatakayofanyika mtandaoni. Kitu pekee tunachokihitaji kutoka kwao ni kuuza bidhaa zenye ubora na bei nafuu kwa wateja wetu.”

  Katika jitihada za kujenga hamasa ya biashara mtandaoni, Jumia huandaa shughuli za mara kwa mara za kimasoko ndani ya mwaka kama vile kuzindua bidhaa mpya, ofa kabambe na mapunguzo lukuki kwa ajili ya wateja.

  Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James alipata fursa ya kugusia juu ya Jumia kuzindua kwa mara ya kwanza ‘Wiki ya Simu,’ kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Tigo.

   Ameelezea kampeni hiyo inafanana na kampeni yao ya kila mwaka ya ‘Black Friday,’ lakini hiyo itajikita kwenye bidhaa za simu za mkononi pekee.

  "Kampeni hii itahusisha uzinduzi wa bidhaa mpya, ofa kabambe, zawadi na punguzo kwa wateja. Tukio hili tayari limekwishafanyika kwenye nchi za Kenya na Nigeria ambapo ni kubwa na maarufu, na kwa mara ya kwanza watanzania watanufaika na mapunguzo ya kuvutia na promosheni zitakazoletwa kwa ajili yao na Jumia.

  "Itakuwa ni wiki ya aina yake kwa ajili ya kununua bidhaa za simu.Wiki ya Simu’ itaanza Machi 19 mpaka Machi 25 mwaka huu ambapo itazinduliwa kwa muda wa siku mbili, Machi 17 & 18 katika viwanja vya Leaders Club," amesema.

  Ameongeza uzinduzi huo utazileta pamoja kampuni mbalimbali maarufu za simu nchini katika tukio ambalo litakuwa ni la kipekee, la kifamilia, ambapo wahudhuriaji watakuwa na mazingira mazuri ya kununua bidhaa za simu na kufurahia chakula na muziki mzuri kwa ajili yao.

  "Tukio hili litawapatia wateja fursa ya kununua na kujionea matoleo mapya ya bidhaa za simu ambazo zinatawala soko kwa sasa kwa gharama nafuu pamoja na kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu Jumia,” ameelezea James.

  Akijaribu kufafanua kwa kifupi kuhusu bidhaa na ofa zitakazokuwepo kwenye ‘Wiki ya Simu,’ Mkuu huyo wa Masoko amesema Jumia kwa kushirikiana na Tigo, zimekuwa ndiyo kampuni za kwanza kuwapatia wateja fursa ya kuagiza simu ya Samsung S9 na S9+ kabla haijaingia sokoni.

  " Mchakato wa kuagiza Samsung S9 lilianza mara moja kupitia Jumia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa simu hiyo kufanyika kwa njia ya mtandao duniani kote kutoka kwenye Mkutano wa Dunia wa Simu za mkononi uliofanyika jijini Barcelona, Hispania Februari 25  mwaka huu.

  “Wateja watakaoagiza kupitia mtandao wa Jumia wataweza kujipatia simu zao wiki moja kabla ya Wiki ya kampeni, na watapokea kifaa cha kuchaji kwa haraka kinachotumia waya na miezi 6 ya bure ya kuunganishwa na intaneti kutoka Tigo,"amesema.

  Amefafanua vilevile watakuwa na zawadi za kushtukiza siku ya tukio, katika wiki hiyo wateja wao watapatiwa ‘chemsha bongo’ ya kuitafuta simu ya Samsung S9 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2, Amesena ambayo itakuwa imefichwa kwenye mtandao wao kwa kununua bidhaa zenye gharama isiyopungua Sh. 100,000

  " Mteja wa kwanza kuivumbua ataweza kujipatia simu hiyo kwa gharama nafuu zaidi nchini. Tutakuwa na ofa za kuvutia, vocha na mapunguzo ambavyo vitawekwa wazi kadri tutakavyokaribia uzinduzi wa wiki hiyo,” amesema James. 

  Kabla ya kujiunga na Jumia Tanzania, Zadok Prescott alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Millicom (kampuni mama ya Tigo na Zantel) katika kitengo cha Kutafuta na Kuunganishaji biashara mpya kuanzia mwaka 2014 mpaka 2018.

   Prescott anao uzoefu mkubwa katika masuala ya ushauri wa mikakati, utafutaji na uunganishaji wa biashara mpya, kuboresha biashara, ambapo uzoefu wake unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kupelekea Jumia kuwa mojawapo ya kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa za huduma za biashara mtandaoni nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

  0 0
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI

  SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..

  Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.

  Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.

  Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.

  “Serikali ilikwishatoa matamko mbalimbali yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria, na leo hii hakuna njia nyingine, Waajiri hawa tuliowabaini hapa Mkoani Kilimanjaro naagiza WCF iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.” Alisema.

  Baadhi ya waajiri ambao Naibu Waziri na timu yake walifanya ukiaguzi huo ni pamoja na kampuni ya Machare Investments, Scholastica Schools iliyoko Himo nje kidogo ya mji wa Moshi.Alisema sio lengo la serikali kuwatisha au kuwadhalilisha waajiri hao bali nia ni kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa lakini pia kuwaondolea jukumu waajiri la kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakiwa kazini.

  “Tunataka ninyi wawekezaji, (waajiri), mjielekeze kwenye shughuli zenu za msingi kwa maana ya kufanya uwekezaji na biashara zenu na hili la kumuhudumia mfanyakazi aliyepatwa na madhara kazini lishughulikiwe na serikali.” Alisisitiza.

  Tayari Mhe. Mavunde amefanya ziara kama hiyo mkoani Mwanza na Shinyanga na kubainisha kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini waajiri wasiotekeleza takwa hilo la kisheria litafanyika nchi nzima, na kuwataka waajiri kufanya hivyo haraka ili wasijikute kwenye matatizo.

  “Tumewasambaza maafisa wetu wa WCF mikoani na wanaednelea na utaratibu wa kuwafuikisha mahakamani waajiri wote ambao wameshindwa kufuata sheria.
  Naibu Waziri ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria 
  Mhaisbu wa Shule ya Scolastica mjini Moshi, Kilimanjaro Bw. Moshi W. Moshi, na Mkuu wa shule hiyo Bw.Michael Shiloli, wakisikilzia maagizo ya Naibu Waziri Mvunde. 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
  Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia)
  Bw. Anselim Peter akizungujza na waandishi wa habari
  Mhe. Mavunde akisisitiza jambo kwa viongozi wa shule ya Scolastica.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kamishna wa kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, (katikati), na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika

  0 0


  Mzee Joram Mollel maarufu BABU mwenye umri zaidi ya miaka 90 akijisajili kushiriki mbio za kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Mtoa huduma wa Tigo, Mohammed Ally akiwasajili Aghata Philii na Poling Nikesa raia wa Zambia kushiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwenye viwanja vya Kibo Palace Arusha juzi. Mbio zinatarajiwa kutimua vumbi jumapili ya wiki hii Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akimkabidhi Babu Molell  NAMBA ya ushiriki wa mbio za  kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.  Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akifurahi mara baada ya kumkabidhi  Babu Molell  NAMBA ya ushiriki wa mbio za  kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashanti Kijaji amesema kuwa mamlaka ya Masoko na Mitaji ni injini katika maendeleo ya uchumi hivyo ni lazima mamlaka hiyo iwafikie wateja.

  Kijaji aliyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mamlaka hiyo waliopata kwa kushirikiana na chuo cha Uingereza CISI katika fani ya masoko na mitaji, amesema kuwa watu hawana uelewa juu ya masoko na mitaji hivyo wanatakiwa kufikia wateja katika kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano yenye Kauli mbiu ya nchi ya viwanda.

  Amesema Mamlaka kwa kutumia watalaam hao lazima wafanye kazi katika kujenga nchi  na kutoa elimu  kuhusiana na masoko na mitaji.Amesema kuwa kampuni zipo nyingi lakini hazijaweza kuingia katika soko la hisa ni kutokana na kampuni hizo kushindwa kufikiwa ikiwa ni pamoja na kupata elimu.

  Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kufanya kazi mamlaka hiyo lazima iweke mpango mkakati katika kuhamasisha kampuni ziingie katika soko la hisa.Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dk.John Mduma amesema kuwa wanaendelea katika kutoa huduma ikiwa ni pamoja kufanyia kazi maagizo ya Naibu Waziri katika kuwafikia wateja na kuleta matokeo chaya ya maendeleo ya uchumi.

  Dk. Mduma amesema kuwa katika kuwa sasa watafungua dirisha la  uhamasishaji katika  kufikia kampuni ziweze kuingia katika soko la hisa.
  Afisa Mtendaji Mkuu , Nicodemus Mkama amesema mkataba wa huduma kwa wateja waliouzindua watawafikia wateja wote kuingia dhamana ya masoko na mitaji katika kuendrleza miradi mbalimbali nchini.

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizungumza mara baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko ya mitaji na uzinduzi wa Mkataba wa huduma kwa Wateja.
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi w akitabu cha huduma kwa wateja.

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizindua kitabu cha Msaada wa huduma kwa wateja
   Mwenyekiti wa TSEBA,George Fumbuka akitoa neno la Shukrani kwa waziri mara baada ya kumaliza kuzinduliwa kwa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa wateja.

    Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko
   Baadhi ya Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu cha huduma kwa wateja

  0 0

  Vee Money App katika kilele cha maendeleo ya mziki Afrika na dunia nzima
  Vanessa Mdee anaungana na mastaa maarufu duniani ambao wanamiliki ‘majukwaa ya mtandaoni’ ya kuwasiliana na mashabiki wao

  Je unafahamu kitu gani kinachowafananisha Taylor Swift, Ciara, na Vanessa Mdee? Naam, pamoja na kwamba wote ni wasanii wenye sauti nzuri na vipaji vikubwa, wote watatu wanamiliki majukwaa ‘app’ za kuwasiliana na mashabiki wao mtandaoni.

  Hii ni njia mpya inayotumiwa na wasanii wakubwa ambao wana mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, ukweli ni kwamba pamoja na mitandao hiyo mikubwa ya kijamii kutengeneza mabilioni ya dola kila mwaka wasanii hawapati mapato ya moja kwa moja kutokana na biashara hiyo.

  Sababu nyingine kubwa ambayo inawafanya wasanii kama Kim Kardashian kuwa na majukwaa yao mtandaoni ‘app’ ni kwa sababu hawamiliki mashabiki wao wa mtandaoni ila mitandao ya kijamii ndiyo ina haki juu ya watu wanaoitumia, hii inamaanisha msanii mkubwa akifungiwa akaunti yake ya Facebook au Instagram anaweza kukosa njia ya kuwasiliana na mashabiki wake (Rob Kardashian ni mfano halisi).

  Pamoja na ukweli kwamba majukwaa‘app’ pia zinaruhusu wasanii maarufu kuuza bidhaa mbalimbali na tiketi kwenye simu za mkononi lakini cha muhimu zaidi, inasaidia wasanii kufaidika kutokana na makampuni makubwa kutangaza kupitia majukwaa yao.

  Kama ilivyonukuliwa kwenye mtandao maarufu wa FORBES, tangu Juni 2014 Kim Kardashian ameingiza mapato ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 200. Hiyo si pesa ndogo na ni hivyo ni rahisi kuwaelewa wasanii kama Taylor Swift, Ciara, na mwanadada anayeitikisa Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ambao wote wamezindua majukwaa yao ili kukamata fursa hiyo katika mazingira ya sasa yaliyojaa maendeleo makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

  Vanessa Mdee amechukua fursa hii kwa kuzindua Vee Money App mwezi Januari mwaka huu. Vee Money App, ambayo ilitengenezwa na kampuni ya teknolojia ya Marekani ya Converge Media, imepokelewa na inaendelea kufanya vizuri kwenye soko.

  Pamoja na kutoa maudhui ya kipekee kwa mashabiki wake, Vee Money App pia ni jukwaa kwa watangazaji ambao wanataka kuwafikia mashabiki halisi wa Vanessa. Hapo awali, makampuni walipotaka kutangaza bidhaa zao kwa mashabiki wa Vanessa waliingia mikataba moja kwa moja na Facebook au Instagram (ambao ndio wana taarifa za mashabiki) bila kumhusisha Vanessa mwenyewe. Uwepo wa Vee Money App unamfanya sasa Vanessa kuwa mstari wa mbele katika masuala yote yanayohusiana na matangazo kwa mashabiki wake hivyo watangazaji sasa wanaweza kuwasiliana na kuingia mikataba moja kwa moja na yeye binafsi.

  Mdee bado hajaacha mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter, hata hivyo, maamuzi yake ya kuzindua jukwaa lake la kuwasiliana na mashabiki kwa njia ya mtandao ni jambo la ujasiri linalompa mwelekeo mzuri katika sekta ya mziki kama inavyoonekana kwa Taylor Swift na Ciara. Kwa Mdee ‘Vee Money App’ ni maendeleo ya asili katika ukuaji wake kwa ujumla katika sekta ya mziki.

  ‘Kwa kadri ninavyoendelea kuwa katika mziki nimetambua kwamba umiliki wa kazi zako ni muhimu sana; kuanzia kumiliki mziki wako, mashabiki wako, na majukwaa yako ya mtandaoni na kama hutafanya hivyo mtu mwingine atakusaidia’ alisema Mdee.

  Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Converge Media, Nick Brunelle, umiliki wa wasanii ndio sababu ya uwepo wa kampuni hiyo. "Tulitaka kujenga mazingira ambapo wasanii kama Vanessa wanaweza kuwa na umiliki si tu katika mapato ya matangazo lakini pia umiliki katika taarifa na habari zinazohusiana na majukwaa yao" alisema Brunelle.

  Maana yake ni kwamba tofauti na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii, Vanessa anamiliki habari zote zinazozalishwa na Vee Money App na ana udhibiti wa taarifa hizo na namna zinavyotumiwa. "Vanessa hakika ameyapokea mabadiliko mapema hasa kwa Afrika," aliongeza. "Ameona wazi mziki unapoelekea kimataifa na yeye amefuata mkondo huo na kuwa kinara barani Afrika"

  Kwa sasa jukwaa la Vanessa Mdee, Vee Money App, inapatikana bure kupitia ‘Apple App store’ na ‘Google play store’ (Kama vile kwa Taylor Swift na Ciara apps) . Wakati utaamua namna wasanii wanaomiliki majukwaa yao watavyokuwa wamepiga hatua huko mbeleni lakini kwa hakika kuna ongezeko kubwa la mashabiki wanaotamani kuwa karibu zaidi na wasanii wanaopenda kuliko ilivyo sasa katika mitandao ya kijamii. Na Mdee ameamua kuwa kinara katika kutimiza kiu ya mashabiki wake. 
   

  0 0

  Na Rhoda Ezekieli, Kigoma

  BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameikataa miradi minne ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni mbili iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2012.

  Miradi hiyo inafadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na ikiwa chini ya uangalizi wa Wilaya ya Kibondo ambayo mpaka sasa bado haijakamilika.

  Madiwani hao wameitaja miradi hiyo ni wa maji Nyagwijima, Kiduduye, Katanga na Muhange ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu licha ya fedha zote zilishatolewa lakini haikamiliki na sasa wamechoka kupewa majibu ya kuahidiwa kila kukicha.
  Wakizungumza jana katika kikao cha baraza hilo, madiwani hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipewa majibu ambayo hayaeleweki huku wakiahidiwa miradi hiyo itakamilika ndani ya mwezi mmoja baada ya kikao cha baraza la madiwani na mpaka sasa kimekuwa kitendawili kisicho na majibu.

  Diwani wa Kata ya Gwarama Elia Kanjero amesema imekuwa kama desturi kupewa majibu mepesi katika suala hilo na hawataendelea kuona miradi hiyo ikionekana kuwepo katika maeneo yao bila faida yoyote kwa wananchi.

  Alisema ni aibu miradi hiyo hata wafadhili wakija kuiangalia wanaweza kuacha kutoa fedha zao katika miradi mingine."Miradi hii inaonesha kutokuwa na tija kwa wananchi na haifai kabisa kutokana na fedha zilizotumika na ukizingatia fedha zote zimekwishalipwa lakini miradi ni mibovu," amesema.
  Aidha Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ambaye kwenye baraza hilo alikaimu nafasi Mwenyekiti, Toy Butono amesema baraza linapendekeza Mhandisi wa Maji wilaya hiyo avuliwe madaraka yake.Pia achunguzwe kutokana na kushindwa kufuatilia miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa adhabu nyingine ili kukomesha uzembe kwa watumishi unaoweza kuigharimu halmashauri.

  "Baraza tunaikataa miradi hii na tunaomba Mhandisi wa Maji anyang'anywe madaraka kwa kipindi hiki apewe mtu mwingine, yeye kazi hii imemshinda kila siku tunapokea malalamiko kutoka kwa wananchi." Kuhusu miradi hiyo kwa sasa hatuihitaji hadi itakapo kamilika na Mhandisi atuambie labda alishiriki kufanya miradi hiyo isikamilike kwanini ashindwe kufuatilia", amesema Butono.

  Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema suala hilo atalifikisha Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) ili hatua zichukuliwe kwa wanaokwamisha miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa wananchi.

  "Wapo baadhi ya wananchi waliochangia nguvu zao bila kupewa haki zao mpaka sasa na kuwapongeza madiwani kwa uamuzi mgumu waliouchukua," amesema.Kwa upande wake Ofisa Utumishi wa halmashauri hiyo , Lusajo Ngabo ametoa ushauri kuhusu uamuzi uliochukuliwa na kuomba nhusika apewe siku 18 ili ajitetee kuhusu tuhuma zinazomkabili na baada ya hapo sasa ndio hatua nyingine zifuatwe.

  0 0


  Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akikabidhi zawadi ya shilingi milioni 10 kwa Bw. Reuben Bulugu Kinamhala mshindi wa Bahati nasibu ya “Daka Mkwanja” iliyoendeshwa na Benki hiyo kwa muda wa miezi minne kwa wateja wake kuweka fedha kwenye akaunti zao na kutunza kiwango kisichopungua shilingi milioni moja , Bw. Reuben Bulugu ambaye ni mtumishi katika kanisa ni mteja wa benki hiyo katika tawi la Mtoni Temeke jijini Dar es salaam.

  Katika picha kulia ni Mke wake Jane Bulugu akishiriki kupokea kiasi hicho cha fedha na kutoka kulia wanaoshiriki kukabidhi fedha hizo kwa mshindi ni Linda Mario Mkuu wa uratibu wa Mauzo na Nimael Mdeme Meneja wa Matawi ya Benki ya Boa Kanda ya Dar es salaam na Zanzibar.


  Bw. Muganyizi Bisheko Meneja wa Masoko Utafiti na Maendeleo Benki ya BOA akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake pamoja na washindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo.

  0 0  Na Emmanuel Masaka ,Globu ya Jamii

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

  Zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wanachi kwa kushirikiana na Mbunge huyo itagharimu zaidi ya Sh. million 98,ambapo mpaka sasa zaidi ya Sh. million 43 zimeshatumika katika ujenzi huo.

  Huku zaidi ya Sh.million 50 zikihitahika kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.Aidha katika kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika kwa wakati Ulega aliendesha harambee kijiji hapo ambapo zilipatikana Sh. 430800,mifuko ya saruji 35, mabati 19 na ahadi 150000.

  Hata hivyo, Ulega alimpongeza Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Kibamba kwa kusimamia fedha za ujenzi wa jengo hilo kwa uaminifu."Huyu bwana ni muadilifu na mwaminifu wake ndio umefanikisha ujenzi wa jengo hili,hivyo natoa mwito kwa wanachi kuwa waaminifu pindi mnaposimamia miradi msitumie fedha kwa matumizi yenu," amesema.

  Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji wamesema kukamilika kwa jengo hilo kutawapunguzia changamoto kwa kiasi kikubwa.Wamesema kwa sababu sasa wanafuata huduma ya afya mbali hali inayopelekea kinamama kujifingulia njiani.

  Ujenzi wa Zahanati hiyo umekuja baada ya Mbunge wa jimbo hilo kuona changamoto kubwa za huduma ya afya zinazowakabili wananchi hao,na kuamua kuitisha harambee ya ujenzi wa Zahanati hiyo mnamo mwaka jana.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali akiweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga ,Abdalah Ulega aliendesha harambee kijiji hapo ambapo zilipatikana Sh. 430800,mifuko ya saruji 35, mabati 19 na ahadi 150000
  Muonekano wa jego la Zahanati ya Kibamba iliyopo Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga ,Abdalah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibamba Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa Mkuranga ,Abdalah Ulega akikagua ujenzi wa shule ya msingi Chatembo iliyopo kata ya Mwandege.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amekutana na ugeni kutoka nchini Uturuki ukiongozwa na Balozi wao Dkt. Ali Daoutoglu mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

  Ugeni huo umejadili namna ya kuboresha Sekta ya Afya nchini hususani katika kuboresha huduma za dharura, uzalishaji wa dawa na ubadilishanaji uzoefu wa Wataalamu wa Afya kati ya nchi hizo mbili.

  Balozi Ali Daoutoglu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tazania na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuimarisha Sekta ya Afya nchini.
   

  0 0

  Umoja wa Wanafunzi waliomaliza Shule ya Msingi Bunge mwaka 1997 iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam wametoa msaada wa viti 20 kwa shule hivyo ambayo vitatumiwa na walimu ambao wanafundisha katika shule hiyo. Akizungumza kuhusu msaada huo, Mwenyekiti wa umoja huo, Bernard Chezue alisema msaada huo ni sehemu ya shukani yao kwa shule hiyo kwa kuwapatia eleimu ambayo imewasaidia kimaisha mpaka sasa wakiwa na mafanikio. Alisema wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuisaidia shule hiyo ili iwe na mwonekano mzuri jambo ambalo litachochea wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii. 
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997, Bernard Chezue akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi viti 20 kwa uongozi wa shule ya Bunge.
   "Tumekabidhi vitu hivi sabau tunaona tuna umuhimu wa kusaidia kwa sababu tumsoma hapa na sisi tumekuwa na mafanikio kwa kupitia shule hii, tumekuja kutoa shukrani kwa waliu wetu na shule kw ujumla, "Huu ni mwanzo tu tutaumika nafasi yetu kutoa misaada zaidi na zaidi kwa namna Mungu anavyotujalia maana kuja kupata rangi, kubadilisha madarasa na hata baadae kuja kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri," alisema Chezue. Pia Chezue aliwataka watu wengine ambao walisoma katika shule hiyo kuungana kwa pamoja na kusaidia mahitaji mbalimbali ambayo yanahitajika shuleni hapo. 
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997 kwa kutoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo.

  Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi aliwashukuru wanafunzi hao kwa kutambua kuwa bila shule hiyo yanawezekana wasingekuwa na mafnikio hayo lakini pia kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo wa kuisaidia kwa mahitaji mbalimbali. 

  "Nimefarijika sana na wanafunzi waliomaliza mwaka 1997 kutuletea msaada, kwamba wametambua mwalimu ni hazina na mafinikio waliyoyapata yametokana na mwalimu na wameona ni vyema wawasaidie wadogo zao ili na wao wafanikiwe kama wao walivyofanikiwa, "Tunaamini watakuja tena kufanya vitu vikubwa sana sababu msingi waliopata katika maisha yao walipata katika Shule ya Msingi Bunge hivyo tunaamini wameamini mafanikio yao yametokana na shule hii," alisema Mfalingundi. 
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997, Bernard Chezue akimkabidhi kiti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi. Umoja huo umetoa msaada wa viti 20 katika shule hiyo.
  Wanachama wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997 wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya bunge.

  0 0

   Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi funguo ya gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.
   Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi kadi ya gari ya gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.
   Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi kibao cha namba za gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa.
   Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC, Saidi Chiwina (katikati) akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kukabidhiwa gari lake mjini Tanga leo. 
   Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC, Saidi Chiwina akijaribu kuwasha gari lake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NBC Tawi la Tanga, Asia Chambega mjini Tanga leo. 
  Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC, Saidi Chiwina (wan ne kushoto) akipozi kwa picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari lake mjini Tanga leo baada ya kuibuka kidedea katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na Viongozi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wataalam wa Takwimu katika utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi unaoendelea hapa nchini ili kuwezesha upatikanaji wa  takwimu halisi na sahihi Mkoani humo.

  Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wake na   waandishi wa habari, wataalam wa Takwimu na Viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika Februari 28 Mjini Bariadi.

  Amesema Utafiti huo utatoa makadirio ya uchumi jumla(macroeconomic), hususani matumizi ya kaya kwa ajili ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product-GDP), kupata mwenendo wa matumizi ya moja kwa moja ya kaya  ili kuwezesha uchambuzi wa hali ya soko na kupata taarifa za umilikaji wa vifaa vya kudumu pamoja na nyenzo za uzalishaji wa kipato.

  Amesema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2015 kila mwananchi anawajibika kushiriki katika utafiti kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu rasmi ambazo zitatumika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.

  “ Lengo mama la utafiti huu ni kujua hali ya kipato kwa kaya zetu asije mtu akapotosha kuwa watafiti wana agenda nyingine, ndiyo maana nimeona viongozi wa Dini nao walifahamu hili ili wasaidie kuwaeleza kwa ufasaha waumini wao; Serikali inahitaji takwimu sahihi ili ipange bajeti  na kuweka mipango ya maendeleo, niwaombe wananchi na viongozi tutoe  ushirikiano” alisema Mtaka.

  Aidha, amemuagiza Meneja wa Takwimu mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ushiriki wao katika utafiti huu hususani kaya zilizochaguliwa na akamtaka yeye na wataalam wa Takwimu wa Mkoa huo kufanya mikutano katika minada na magulio pamoja na maeneo ya yenye idadi kubwa ya watu yakiwemo ya Makao Makuu ya Wilaya na miji midogo(centers) ili kujenga uelewa kwa wananchi.

  Meneja wa Takwimu Mkoa wa Simiyu, Nestory Mazinza amesema tangu utafiti huu uanzae Desemba Mosi 2017 jumla ya kaya 102 zimeshafanyiwa utafiti kati ya 408 zinazotarajiwa kufikiwa mpaka kumalizika kwa zoezi hilo mwezi Novemba  2018.

  Naye Bi.Joyce Luhende Mdadisi kutoka Wilaya ya Meatu amesema wanapofanya utafiti huu wanakutana na changamoto mbalimbali na kubwa ikiwa ni baadhi ya wanakaya kuogopa kutoa taarifa zinazohitajika wakati wakihojiwa hali inayopelekea kukosekana kwa taarifa sahihi.

  Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikiristo Tanzania(CCT) Mkoa wa Simiyu, Mchungaji Martine Samson Nketo amesema kupitia ibada  watasaidia kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utafiti huu na kuwaeleza umuhimu wake katika mipango ya maendeleo inayopangwa na Serikali.

    Kaya zilizochaguliwa k kufanyiwa utafiti huu zinatoka katika maeneo 34 (Vijiji/Mitaa) kwenye Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu yaliyopo katika kata za Nkindwabiye, Nyangokolwa, Sakwe, Nyakabindi, Dutwa, Matongo,Gilya, Sima,Mwamtani, Mwaswale, Mwamapalala, Nhobora, Zagayu, Kinang’eli, Mwanhuzi, Mwandoya, Sakasaka, Mwabuma, Lubiga, Ng’oboko, Busilili, Seng’wa, Masela, Mwamashimba, Buchambi, Badi, Nyalikungu, Kiloleli,Kalemela, Mkula na Ngasamo.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Bariadi.
   Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah akifafanua jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
   Meneja wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
   Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kati yake na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
   Mmoja wa Wadadisi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
   Baadhi ya Wadadisi na Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kati yake na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza(wa pili kulia) na baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini mara baada ya kumalizika kwa kikao  kati yake na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.

older | 1 | .... | 1529 | 1530 | (Page 1531) | 1532 | 1533 | .... | 1897 | newer