Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 151 | 152 | (Page 153) | 154 | 155 | .... | 1897 | newer

  0 0

  1Adoh Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akipokea vifaa maalum vya kuhifadhia fedha na nyaraka mbalimbali kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa uzinduzi wa Huduma za Bimaya Afya (CHF)katika halmashauri hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Mkapa Garden Mjini Kilwa, wa pili kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi wa (NHIF) Khamis Mdee na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF mkoani Lindi.wananchi mbalimbali wakiwemo wazee walijitokeza katika zoezi la upimaji wa afya yakiwemo magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu ikiwani pamoja na kupima Uzito Urefu. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA.
  2  6Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda akipima urefu na Dr. Hilda Mwakipesile kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo 7Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda akikabidhi kadi ya bima ya afya CHF iliyolipiwa miaka miwili kwa Aziza Said Abas Mshindi wa shindano la kukuna nazi8Mshindi wa shindano la kukuna nazi Aziza Abas akipongezwa na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF Mkoani Lindi pamoja na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano la kukuna nazi jana.9Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw. Khamis Mdee akimpongeza Aziza Abas mara baada ya kushinda katika shindano la kukuna nazi 10Akina mama wakichuano vikali kukuna nazi ilikuwa si mchezo11Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda akizungumza katika uzinduzi huo wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo wa tatu kutoka kushoto, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Khamis Mdee na mwisho ni Mama Fatma Said Ali.13Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Khamis Mdee14Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Khamis Mdee akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda na kushoto ni mama Fatma Said Ali15Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akiwatambulisha madaktari waliokuwa wakichukua vipimo katika zoezi hilo16Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akizungumza na wananchi17Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF Mkoani lindi akizungumza na Paul Marenga Ofisa Mwandamizi wa NHIF mkoani Lindi.19Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo akikabidhi ubani wa shilingi 100.000 kwa mzee Yusf Abdalla ambaye alifiwa na mwanafamilia jirani kabisa na viwanja vya Mkapa Garden mjini Kilwa ambapo ndipo palipofanyika uzinduzi wa huduma za Bima ya Afya wilayani huo20Afisa Mawasiliano wa NHIF Bw. Ruhende Singu akiwatambulisha wachekeshaji Abdallah Salum Kulia Shoti na Rashid Omary. 21Wachekeshaji Abdallah Salum Kulia Shoti na Rashid Omary wakifanya vitu vyao 22Kikundi cha ngoma cha mjini Kilwa kikitumbuiza katika uzinduzi huo

  0 0


  0 0

  Na Veronica Kazimoto – MAELEZO,Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Penina Mlama (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari - MAELEZO leo, Uteuzi huo wa Profesa Mlama unaanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016.

  Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Aidha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka huu.

  Walioteuliwa ni pamoja na wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni Dkt. Vincensia Shule, John Kitime, Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick Shigongo na Alex Msama.

  Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce Fisoo. Wanaoingia kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa BASATA.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

  Kabla ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa.

  Wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye, Prof. Emanuel Mbogo, Dkt. Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na Katibu Mtendaji wa BASATA.

  Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

  Wajumbe hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa, Dkt. Issa Zidi, Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.

  Wengine ni Mmanga Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth Konga, Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.

  Wajumbe wengine ni Ally Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin Mgendera. Taarifa hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la BAKITA atachaguliwa na wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha kwanza.

  0 0

  MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM. 

   Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,

  Napenda nitumie fursa hii kuwafahamisha wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Mwenge wa Uhuru utawasili Mkoani kwetu  kesho tarehe 04/09/2013 ukitokea Mkoa wa Pwani na makabidhiano rasmi yatafanyika pale Airport Terminal 1 saa 3:00 asubuhi. Baada ya makabidhiano Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya zote tatu kama ifuatavyo;-  


  1.Tarehe 04/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni.

  2.Tarehe 05/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala.

  3.Tarehe 06/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Temeke.


  Ndugu Wananchi,

  Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam utazindua, kufungua au kuweka mawe ya Msingi katika miradi 26 yenye jumla ya thamamni ya T.shs. BILIONI 23.2. Mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakuwa katika sehemu tofauti tofauti kulingana na Wilaya husika. Katika Wilaya ya Kinondoni Mwenge  wa Uhuru utakesha katika SHULE YA MSINGI BUNJU “A”. Katika Wilaya ya Ilala Mwenge wa Uhuru utakesha katika SHULE YA MSINGI MAJANI YA CHAI. Katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utakesha katika VIWANJA VYA ZAKHEM-MBAGALA KUU.

   Ndugu Wananchi.


  Ujumbe wa Mwenge mwaka huu unasema WATANZANIA NI WAMOJA TUSIGAWANYWE KWA MISINGI YA TOFAUTI ZETU ZA DINI, ITIKADI, RANGI NA RASILIMALI. Ujumbe huu umeandaliwa kwa mwaka huu ili kutoa msisitizo juu ya umuhimu wa kuimarisha Umoja na Amani katika jamii yetu.

  Sambamba na ujumbe huu suala la Mapinduzi  Matukufu ya Zanzibar litafafanuliwa kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuenzi historia na maendeleo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia mapambano dhidi ya UKIMWI, Rushwa na Matumizi ya Dawa za kulevya yataendelea kusisitizwa. Ujumbe huu utatolewa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya zote tatu hususani katika mkesha wa Mwenge.

   Ndugu Wananchi,


  Kila eneo ambalo Mwenge umepangiwa kuzindua miradi au kuweka mawe ya msingi patatolewa ujumbe mahsusi wa Mwenge na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Juma Ali Simai kama ilivyo desturi nawaomba mjitokeze kwa wingi kuulaki Mwenge wetu wa Uhuru katika maeneo yote.

    Ndugu Wananchi,


  Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake hapa Mkoani tarehe 07/09/2013 na utakabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ndege wa Kilwa Masoko saa 3:00 asubuhi.

   Ndugu Wananchi,


  Napenda nitoe wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wetu wa Uhuru kama ilivyo desturi yetu kwa Utulivu, Amani, Umoja na Mshikamano na kushiriki kikamilifu katika maeneo yote tuliyopanga kuzindua miradi na kuweka mawe ya msingi.


  IMETOLEWA NA 

  Saidi Meck Sadiki

  Mkuu wa Mkoa

  DAR ES SALAAM

  03/09/2013  0 0

   Meneja Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Road License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Wanaoshuhudia katika ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo.
   Mmoja wa waandishi wa habari  kutoka kituo cha Channel Ten Bw.Fred Mwanjala(katikati)akiuliza swali katika uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.
   . Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa (katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)wakifuatilia jambo kwa umakiini wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.
  ======   ======  =======
  M-PESA SASA RASMI KUKUSANYA ADA YA LESENI YA MAGARI.


  Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini - TRA leo imezindua rasmi mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia utatartibu wa M-pesa huku tayari mfumo huo ukionekana kukubalika zaidi na walipa kodi hiyo nchini.  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa kampuni ya Vodacom Kelvin Twissa amesema kuzinduliwa kwa utaratibu huo ni mwendelezo wa namna ambavyo maisha ya watanzania yanavyozidi kuwezeshwa kuwa rahisi wakati ambapo M-pesa inazidi kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya Mtanzania.  Twissa amesema ukuaji wa kasi wa matumizi ya M-pesa unathibitisha umuhimu wake hapa nchini na kuongeza kuwa kutumika kwenye ukusanyaji wa kodi ni hatua nyingine muhimu kwa faida ya walipa kodi ambapo sasa M-Pesa ni sehemu ya maisha ya watanzania na hakuna tena sababu ya kupanga foleni ndefu na kutumia muda mwingi.  "Ni Wakati mwingine M-pesa inavyowapa wananchi na walipa kodi wengine wote hapa nchini utataribu mwepesi, rahisi, salama na wa uhakika zaidi wa kulipa ada  za leseni ya magari kwa urahisi zaidi wakati wowote mahali popote."Alisema Twissa.  "Tunapotambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya nchi hatuna budi kufurahia hatua hii ambayo tayari katika kipindi cha muda mfupi kisichozidi wiki mbili M-pesa imeshaonesha mafanikio makubwa katika makusanyo, hili linatupa furaha kama kampuni na ni wazi kila mmoja analifurahia."Aliongeza Twissa
  Twissa amesema Vodacom itaendelea kuuwezesha mfumo wa M-pesa kuwa wenye kutoa suluhisho la masuala mengi zaidi ili kukidhi shabaha ya kampuni hiyo ya kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya huduma za simu za mkononi.  "Tumekuwa imara wakati wote tangu M-pesa ilipozinduliwa nchini mwaka 2007, hata hivyo bado tunashauku ya kufanya mapinduzi makubwa zaidi kupitia M-pesa tukitambua kwamba hiyo ni kiu ya kila mmoja kuzingatia kile ambacho tayari M-pesa inayaywezesha kupitia viganja vya mikono yao."Alisema Twissa Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo amesema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa Mamlaka katika ukusanyaji wa ada za leseni ya magari .  "Ni jambo jema kwa mamlaka kuona inawapatia wateja wake(walipa kodi)utaratibu rahisi zaidi kwao katika kuwawezesha kutimiza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi pasi na kuwepo usumbufu wa aina yoyote huku pia utaratibu huo ukileta ufanisi kwa mamlaka."Alisema Kayombo Amesema TRA ina imani kuwa ushirikiano wake na Vodacom utakuwa wenye tija zaidi katika siku zijazo kwa kuhakikisha mfumo wa M-pesa unatoa uwezo zaidi kwa walipa kodi kuutumia katika kuleta urahisi kwao kulipa kodi mbalimbali. Inakidiwa kuwa katika kipindi cha wiki mbili TRA imekusanya kaisi cha Bilioni 2 cha malipo ya ada za magari kupitia M-pesa pekee.

  0 0

   Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki Adam Kimbisa akieleza kwa waandishi wa Habari sababu iliyopelekea wao kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati wa vikao vya bunge hilo, wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy.
   Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.

   Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi wa waandishi wa habari wakiwasikiliza wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
  =======   =======  =====
  DONDOO MUHIMU ZA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI 03/09/2013 – MAELEZO


  Bunge la tatu la Afrika Mashariki lilikuta vikao vya Bunge vikifanyika kwa njia ya mzunguko kwa nchi 4 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi) pamoja na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya.


  Katika kikao cha Kamati ya Uongozi, Wabunge wa Tanzania walitoa pendekezo kwamba vikao vya Bunge kwa mwaka huu wa fedha August 2013 –June 2014 vifanyike Arusha, kwa vile tayari kuna makazi ya kudumu yaani jengo jipya lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kiwanja kilitolewa na Serikali ya Tanzania.


  Hata hivyo Wabunge wenzetu walipendelea vikao vya Bunge viendelee kwa mzunguko na Wabunge Watanzania tuliendelea na msimamo wa vikao kufanyika Arusha.


  Motion ililetwa Bungeni na mwenzetu kutoka Kenya kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko….Spika alimwambia mleta Motion kufuata kanuni ambapo ilitakiwa mjadala wake uendelee katika kipindi cha masaa 24 baada ya kuwasilisha.


  Wabunge wenzetu hawakukubaliana na uamuzi wa Spika na kuamua kutoka nje na kusababisha kikao cha Bunge kuahirishwa mpaka siku inayofuata.


  Kwa utaratibu wa kanuni za Bunge, iwapo nchi moja isipokuwa na Wabunge wasiozidi zaidi ya watu basi kikao cha Bunge kinavunjwa kwa dakika 15 na Bunge kuanza tena na baada ya hapo ikiwa bado akidi ikiwa haitosh, kikao cha Bunge huvunjwa mpaka siku inayofuata.


  Wabunge wa Tanzania tuliamua kwa pamoja kuwa na msimamo wa kutoka ndani ya Bunge kwa kuonyesha kusikitishwa na kitendo cha wenzetu kumdhalilisha Spika wa Bunge pamoja na kuonyesha msimamo kwamba Wabunge Watanzania vile vile tuna msimamo na hatukubali kuyumbishwa.


  Baada ya hapo, ndio tuliweza kukaa meza moja na kufikia makubaliano kwamba Arusha ipate vikao viwili na Tanzania vile vile ipate kikao kimoja. Makubaliano hayo yalipelekea Motion ya kutaka vikao vifanyike kwa mzunguko kufanyanyiwa marekebisho ili kuongeza Arusha kupata Vikao viwili na Tanzania kimoja sambamba na nchi zingine za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata vikao kwa njia ya mzunguko.


  Vikao vya Arusha vina umuhimu sana kwani ni Kikao cha Bajeti kitasaidia kupunguza gharama kubwa kwani wafanyakazi wa Secretariet, Maafisa pamoja na vitabu vya bajeti na vitendea kazi havitasafirishwa nchi yeyote isipokuwa vitabaki Arusha. Hali kadhalika kikao cha Ukaguzi vile vile kitapunguza gharama kwa kiasi kikubwa.


  Mhe. Adam Kimbisa

  Mwenyekiti
  0 0

  Kisiwa cha Saanane kimetangazwa rasmi kuwa Hifadhi ya Taifa kufuatia Tangazo la Serikali Namba 227 lililotolewa hivi karibuni.


  Kutangazwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kunafuatia kupitishwa kwa Azimio la Bunge mwezi Oktoba mwaka jana lililoridhia kupandishwa hadhi kwa kisiwa hicho kutoka Pori la Akiba na kuwa Hifadhi ya Taifa.


  Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane itakuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 2.18 na itajumuisha maeneo ya lililokuwa Pori la Akiba , Visiwa vya Chankende kubwa na ndogo pamoja na eneo la maji ya Ziwa Victoria linalozunguka visiwa hivyo.


  Kuanzishwa kwa Hifadhi mpya ya Taifa ya Saanane kutawezesha haja ya kuongeza spishi mbalimbali za wanyamapori na hivyo kuongeza utalii wa mjini, utalii wa ndani, utafiti na kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi na wananchi watakaotembelea hifadhi hii mpya. Aidha, uamuzi huu utasaidia kutunza hali ya bioanuwai, uhifadhi wa mazalia na makuzio ya samaki na uendelezaji wa utalii wa mjini kuendelea kuimarika.


  Kabla ya kupandishwa hadhi, Kisiwa cha Saanane kilikuwa Bustani ya wanyama mwaka 1964 kabla ya kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba mwaka 1991. Ilipofika mwaka 2006, Serikali ilikikabidhi kisiwa hicho kwa Shirika la Hifadhi za Taifa kwa ajili ya kukiendesha na kusimamia mchakato wa kukipandisha hadhi kuwa Hifadhi ya Taifa.


  Kufuatia uamuzi huu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) sasa litakuwa na jumla ya Hifadhi 16 nchi nzima ambazo nyingine ni pamoja na Serengeti; Ziwa Manyara; Tarangire na Arusha. Nyingine ni pamoja na Kilimanjaro; Mkomazi; Saadani; Mikumi; Milima ya Udzungwa; Ruaha; Kitulo; Katavi; Gombe; Milima ya Mahale na Kisiwa cha Rubondo.


  Wakati huohuo, eneo la Hifadhi ya Taifa Gombe limeongezwa ukubwa kutoka Kilometa za mraba 33.74 hadi kufikia kilometa za mraba 56. Uamuzi huu unatokana na Tangazo la Serikali Namba 228 lililotolewa hivi karibuni ambalo linafuatia Azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotolewa mwaka jana linalohusu kuridhiwa kwa uamuzi wa kurekebisha mipaka ya Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kuondoa eneo la makaburi na kuliacha kwa wananchi pamoja na kujumuisha eneo la ufukwe wa maji ya Ziwa Victoria na eneo la ukanda wa maji.


  Kuongezeka kwa eneo la ufukwe wa ziwa na ukanda wa maji kwenye eneo la hifadhi kutaongeza wigo wa shughuli za utalii katika Hifadhi kama vile kuogelea, utalii wa boti, mitumbwi na uvuvi wa kitalii.

  Imetolewa na Idara ya Uhusiano
  Hifadhi za Taifa Tanzania
  S. L. P 3134
  ARUSHA

  03.09.2013  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa Asasi ya Kisiasa ya Konrad Adenauer Foundation ya Ujerumani, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Rais Mstaafu wa Bunge la Umoja wa Ulaya Dkt. Han-Gert Pottering (kushoto) kwa Makamu, aliyeongoza na Ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Sept 3, 2013 kwa mazungumzo. Picha na OMR. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Asasi ya Kisiasa ya Konrad Adenauer Foundation ya Ujerumani, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Rais Mstaafu wa Bunge la Umoja wa Ulaya Dkt. Han-Gert Pottering, aliyeongoza na ujumbe wake baada ya mazumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Sept 3, 2013. Picha na OMR 

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mke wa Rais Mama salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete, akiwafariji wafiwa wakati alipofika kuaga mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa wakati alipofika kuaga mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mke wa Rais Mama salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, wakijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo. 

  0 0

  Na Georgina Misama-MAELEZO.

  Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki watoa msimamo wao kuhusu vikao vya bunge hilo kufanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama wa jumuia hiyo.


  Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo Tanzania Adam Kimbisa alisema kuwa  Wabunge wa Tanzania walitoa pendekezo kwamba vikao vya Bunge kwa mwaka huu wa fedha 2013/ 2014 vifanyike Arusha, kwa vile tayari kuna makazi ya kudumu.


  “Tulipendekeza vikao vyote vya bunge vifanyikie  hapa nchini kwasababu Arusha ni Makao Makuu ya Bunge la Afrika mashariki, pia vikao  vya Bajeti vikifanyika Arusha itasaidia kupunguza gharama kubwa za usafiri kwa wafanyakazi wa Secretariet, Maafisa pamoja na vitabu vya bajeti”. Alisema Kimbisa.


  Aidha aliongeza kuwa Arusha kuna vitendea kazi vyote vya Bunge na Wabunge wote wana Ofisi katika jengo hilo, hivyo kurahisisha uratibu wa vikao vya Bunge. Akitolea ufafanuzi suala la Makongoro Nyerere kubaki ndani ya ukumbi wa bunge wakati wabunge wote wa Tanzania walipotoka ukumbini humo, Kimbisa aliwaomba Watanzania wasimlaumu Mbunge huyo kwani alibaki kwa ridhaa yao ikiwa ni njia ya kufikisha ujumbe kwamba idadi haijatimia na hatua hiyo ilifanikisha lengo lililokusudiwa.

  Kikao cha makubaliano kilifanyika na makubaliano yalifikiwa kwamba Arusha ipate vikao viwili na Tanzania vile vile ipate kikao kimoja. Makubaliano hayo yalipelekea hoja ya kutaka vikao vifanyike kwa mzunguko kufanyiwa marekebisho ili kuongeza Arusha kupata Vikao viwili na Tanzania kimoja sambamba na nchi zingine za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata vikao kwa njia ya mzunguko.


  Katika mkutano huo na waandishi wa habari Kimbisa aliongozana na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki akiwemo ShyRose Bhanji ambae ni katibu kwenye kamati ya Bunge, Nderakindo Kessy na Makongoro Nyerere.


  Akihitimisha mkutano huo, Kimbisa aliwaomba waandishi kuwa wazalendo na kuitetea nchi yao hasa inapotokea mgongano baina ya Tanzania na nchi nyingine.   

  0 0

  Na Amina Abeid (ZJMMC)  .

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Davis Adolf Mwamunyange leo amewatunuku Nishani Maafisa na Askari 39 wa JWTZ katika hafla iliyofanyika Kambi ya Jeshi ya Bavuai nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

  Mwamunyange amefanya zoezi hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kufanya Idadi ya Wanajeshi waliotunikiwa Nishani msimu huu kutimia 939 Tanzania kwa ujumla.

  Zoezi hilo limefanyika kwa Maafisa na Askari Jeshi wenye sifa za kulitumikia Jeshi kwa muda mrefu na kwa tabia ya kuweza kusifika katika Jeshi hilo.

  Katika Zoezi hilo Maafisa wawili walitunikiwa Nishani ya Utumishi uliotukuka, Maafisa sita Wametunukiwa Nishani ya muda mrefu ambapo  Askari 31 wametunukiwa nishani ya tabia njema.

  Akifafanua kuhusu Nishani hizo Mwamunyange amesema Nishani ya Utumishi uliotukuka hutolewa kwa Maafisa wenye cheo cha Meja kwenda juu ambao wametumikia Jeshi kwa miaka isiopungua 20 mfululizo.

  Amesema Nishani ya Utumishi mrefu hutolewa kwa Maafisa na Askari wa JWTZ ambao wametimiza utumishi usiopungua miaka 15 mfululizo na nishani ya Utumishi mrefu na tabia njema huvishwa Askari wa JWTZ waliotumikia Jeshi mfululizo kwa muda usiopungua miaka 15.

  Mkuu huyo wa Jeshi amesema Utaratibu huo wa kutunuku nishani umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu kwa lengo la kupata Viongozi na Makamanda bora wa Jeshi ambao wametumikia Taifa lao kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu.

  Kwa upande wake mmoja wa Watunukiwa wa Nishani ya Utumishi wa Muda mrefu na tabia njema Saida Said amesema, amefarajika kupata nishani hiyo kwani itamtambulisha Jeshini kuwa ana tabia njema.

  Zoezi la kutunuku nishani kwa Maafisa na Askari wa JWTZ limefanyika katika kituo cha KJ 12,Zanzibar na linatarajiwa kuendelea kwa vituo vingine nchi Nzima.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Bondia Kalama Nyilawila akijifua kujiimarisha kusubiri mpambano wake yeye  na Thomasi Mashari baada ya kumdhihaki yeye pamoja na Bondia mada Maugo aliyepigwa hivi karibuni kwa kuwaita midori yake.
  Bondia Kalama Nyilawila akijifua kujimarisha kusubiri mpambano wake yeye na Thomasi Mashari baada ya kumdhiaki yeye pamoja na Bondia mada Maugo aliyepigwa hivi karibuni kwa kuwaita midori yake.
  Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shadrack Ignas wakati wa mazoezi yanayoendelea katika klabu yao iliyopo sinza makaburini Dar es salaam Kalama anafanya mazoezi kwa ajili ya kumtafuta bondia Thomasi Mashali baada ya kumdhihaki kwa kumuita yeye na mwenzie Mada Maugo kuwa ni Midori yake, ambapo maugo amepigwa na bondia huyo hivi karibuni Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0


   Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda (wapili kushoto) akiwasalimia baadhi ya watumishi wa makao makuu ya Jumuia hiyo, jijini Dar es Salaam, alipowasili kuripoti rasmi ofisini kwake, kwenye jengo la makao makuu hayo ya UVCCM, lililopo kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Lumumba. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Mfaume Ally Kizigo ambaye Baraza Kuu la UVCCM lililofanyika Zanzibar juzi, lilimuithinisha kuendelea na nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia zaidi ya miaka minne sasa.
   "HAPA NDIYO OFISINI KWAKO MKUU" Kizigo akisema, wakati wakiwa ofisini kwa Sixtus, makamo makuu ya UVCCM, Dar es Salaam.
  Sixtus na Kizigo wakipeana mikakati ya kazi, baada ya mapokezi ya viongozi hao makao makuu ya UVCCM Dar es Salaam, leo. Imetayarishwa na: theNkoromo Blog

  0 0

   Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja wakioneshana upendo na mapenzi teeele,usiku wa leo kwenye sherehe yao.
   Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa katika picha ya kumbukumbu kabla ya tukio adhimu la kukata keki
   Dkt.Elmi akimlisha keki ya upendo na kwa madaha kabisa,Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura  jioni ya leo.
  Lisha nikulishe ndiyo ishara ya upendo
   Dkt.Elmi akikata keki tayari kwa kumlisha Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura na wegeni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tafrija hiyo,kulia kwake ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiwa na MKewe Mariam Shamo.
   Anti Ashura akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Mumewe Dkt.Elmi aliyekuwa akitimiza miaka 80 tangu kuzaliwa kwake ikiwemo na sambamba na kusherehekea miaka 20 ya ndoa yao.
   Keki ikiwa imeandaliwa saafi kabisa.
   Baadhi ya Wageni waalikwa wakijadiliana jambo kwenye hafla hiyo iliyofanyika ndani ya kiota kipya kabisa cha maraha,Escape One kilichopo nyuma ya Carnival,njia panda Makao makuu ya Red Cross,jijini Dar.
   Dkt.Elmi akiwa na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura akiwa amepozi na Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiwa na MKewe Mariam Shamo.
    Baadhi ya Wageni waalikwa wakijadiliana jambo kwenye hafla hiyo iliyofanyika ndani ya kiota kipya kabisa cha maraha,Escape One kilichopo nyuma ya Carnival,njia panda Makao makuu ya Red Cross,jijini Dar
   Dkt.Elmi akiwa na Mkewe almaarufa kwa jina la Anti Ashura akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa na Mkewe,CEO wa kampuni bingwa ya Burudani ya hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd,Bi.Johayna Kusaga
   Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa picha ya pamoja ya ndugu jamaa na marafiki kwenye hafla hiyo iliofanyika usiku wa leo  ndani ya kiota kipya kabisa cha maraha,Escape One kilichopo nyuma ya Carnival,njia panda Makao makuu ya Red Cross,jijini Dar.
  Anti Ashura na Wanae katika picha ya pamoja.

  0 0


  Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishiana misuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika September 29 katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

  ========  ========  =======
  MABONDIA Fransic Miyeyusho na Sadiki Momba wametambulisha mpambano wao wa kirafiki wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam

  Akizungumza mmoja wa waratibu wa mpambano huo Ramadhanu Uhadi 'Rama Jah' amesema mpambano huo uliokuwa ukisubiliwa na mamia ya mashabiki wengi baada ya mabondia howo kutambiana kwa mda mrefu bila ya kuwepo na mpambano wao.

  Ameongeza kwa kusema siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi likiwemo ya vijana chpkizi na wakongwe vile vile watakuwepo baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo katika utangulizi ni

  Mussa Sunga atakaemenyana na Fadhili Awadhi  raundi 6 uku bondia Iddy Mnyeke kotoka kambi ya Ilala akimenyana na Keis Amari  mpambano wa raundi 4 na Ambukile Chusa atapambana na Fadhili Kambi 

  0 0

  Kweli Tembea uone mengi !

  Kinshansa au KIN kama wanavyopaita wenyeji wa mji huo,
  ni mji uliojaa vioja vya kila aina kama kawaida ya miji mingi
  barani Afrika, lakini kinacho shangaza panapotokea msiba
  wakazi wa mji huo wa Kinshansa wao wanaombeleza ki aina
  yao yaani Sebene kama kazi kitu ambacho kinapingwa na
  wakazi wa miji mingine nchini DRC lakini jionee mwenyewe
  matanga ya Kinshasa aka KIN.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Ussu Mallya akizungumza kuwakaribisha wageni mbalimbali katika tamasha hilo na kutoa machache juu ya miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi za TGNP.
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Bi. Mary Rusimbi akizungumza kwenye mkutano wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013. Mwanachama wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi akitoa mada kwenye Tamasha hilo.
  [caption id="attachment_37254" align="aligncenter" width="500"]Washiriki wa mkutano wa tamasha la jinsia tanzania 2013 wakiandamana kuingia katika viwanja vya TGNP kabla ya kuanza kwa maadhimisho. Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kusherehekea miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi za mtandao huo.
  [caption id="attachment_37245" align="aligncenter" width="500"] Baadhi ya wageni kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifa wakifuatilia matukio anuai katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2013.[/caption][caption id="attachment_37260" align="aligncenter" width="500"] Baadhi ya wageni waalikwa na washiriki wa tamasha hilo wakifuatilia mada na matukio anuai.[/caption][caption id="attachment_37268" align="aligncenter" width="500"] Watu wenye ulemavu wa kusikia wakielezewa kwa kutumia ishara masuala anuai yanayiowasilisha katika tamasha.[/caption][caption id="attachment_37248" align="aligncenter" width="500"] Wakati mwingine burudani zilipozidi washiriki walishindwa kuvumilia na kujikuta wakiingia kati na kusakata rumba. Vikundi mbalimbali vya muziki na sanaa vilikuwa vikiburudisha.[/caption][caption id="attachment_37258" align="aligncenter" width="500"] MC wa sherehe ya Maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Tanzania 2013 akitoa maelekezo kwa wanatamasha.
  [/caption][caption id="attachment_37266" align="aligncenter" width="500"] Utambulisho kwa washiriki kutoka mikoa anuai[/caption][caption id="attachment_37244" align="aligncenter" width="500"] Utambulisho kwa washiriki kutoka mikoa anuai[/caption][caption id="attachment_37243" align="aligncenter" width="500"] Washiriki kutoka mikoa anuai wakijisajili kabla ya kuanza ushiriki wa Maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Tanzania Jijini Dar es Salaam [/caption][caption id="attachment_37247" align="aligncenter" width="500"] Kundi la wasanii wa Parapanda wakifanya manjonjo yao katika tamasha hilo.[/caption][caption id="attachment_37282" align="aligncenter" width="500"] Kundi la wasanii wa Parapanda wakifanya igizo kuonesha jamii ya wanawake inavyonyanyasika katika maeneo ya ajira.[/caption][caption id="attachment_37279" align="aligncenter" width="500"] Mmoja wa wasanii akighani ngonjera katika maadhimidho hayo.[/caption]: 
  Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Hon. Deputy Secretary General Political Federation
  Your Excellency  Charles Kinyanjui Njoroge


  Charge d’ Affaire German Embassy Dar es Salaam

  Dr. Hans Koeppel


  Hon  Head of EAC Political Affairs

  Ms Isabelle Waffubwa


  My fellow outgoing EAC Youth Ambassadors from Kenya, Uganda, Burundi and Rwanda


  Mr. Tayebwa James EAC Youth Amb. to Republic of Uganda

  Ms. Milly Mbedi     EAC Youth Amb. to Republic of Kenya

  Mr. Desire Bigirimana EAC Youth Amb to Republic of Burundi

  Mr. Gashegu Muramira EAC Youth Amb to Republic of Rwanda


  Distinguished Selected Youth for the 2nd EAC University Debate  Invited Guests ,    Ladies and Gentlemen.

  First and foremost allow me once again to welcome you all in Tanzania and indeed to her beautiful emerging business city, so known as the Haven of Peace, Dar es Salaam.


  On behalf of my fellow East Africa Community Youth Ambassadors, I would like to take this opportunity and great honor to stand before you this morning and share with you a successful story on our journey towards a complete East Africa integration and youth total participation as movers and shakers of the development wave.


  Article 120 (c) of the EAC Treaty provides for adoption of common approach for involvement of the youth in the integration process through education, training and mainstreaming youth issues into the EAC policies, projects and programs for strategic interventions.


  Youth are important stakeholders and given an opportunity, we influence the dissemination of information on EAC integration, sensitization and education of youth and participation in policy development in view of our creativity and energy.


  Since the EAC Secretariat opened the youth platform to be included in championing the integration process by forming the East Africa Community Youth Ambassadorial program together with the Best Youth Debaters, it has juxtaposed the post independence generation of the federation to enjoy unparalleled participation in decision making and policy formulation.


  The East Africa Community Youth Platform championed by the Youth Ambassadors has indeed proven to be the epitome of youth inclusion for our common interest in exercising our talents and opening the doors of opportunity to every citizen of East Africa to become part and parcel of the development wave.


  For the period of one year, we have been able to reach out a larger audience and a leading East Africa population, to sensitize on the importance and benefits of integration by conducting seminars in our major cities of the partner states including Bujumbura, Kigali, Nairobi, Kampala, Arusha and in my own city Dar es Salaam. The call for youth involvement and participation in the regional level is quite resounding and many have joined the platform including our very best selected colleagues of today to learn and disseminate the information to our peers of all races and categories within the region and those in Diaspora.


  Through the youth platform, East Africa Community has indeed opened the doors to learn and embrace good governance by participating fully in any given democratization process which is among the core pillars towards attaining sustainable leadership; leadership that will lift our families, leadership that will sustain our community and indeed leadership that will transform our generation.  In echoing such responsible leadership, for the first time in the history of our Community, the Youth Ambassadors played a significant role on democracy by being among the EAC Election Mission Observers to the Kenyan General election that was conducted early this year on March 3rd 2013.  As EAC Youth Ambassadors, our task and mandate was to observe and make a report on how the election in Kenya was conducted and supervised at all levels before, during and after election results.  Here, I would just like to congratulate once more the Kenyan people for conducting a peaceful election and heartfelt congratulations to the Kenyan youth for being the champions for peace before during and after the election results.  

  I also salute them for being able to turn out in a larger number that the East Africa region has never experienced before as they made their choice by casting the ballot.  This indeed has proven to the region, the continent and the world at large that young people can make a difference.


  Through our tenure as the focal point on youth affairs in the region, we  faced the great challenges of our time with renewed vigor, zeal and zest and of course with new speed towards adopting lasting solutions.  Achieving quality education and employment has been a major cry towards achieving sustainable development in the region.  Our task and mandate forward is to influence our policies and the policy makers within the region to re-structure and re-frame the current policies that will fit in with the current paradigm shift. We have challenged and influenced both the East Africa Business Council and the East Africa Inter-University Council by putting the youth ideas forward ( the targeted people) on reforming and reshaping our policies that will open the doors of opportunity to every young person who belongs to the region.'


  Speaking from the same breath, the harmonization of the education policy within the East Africa region is underway and private sectors and industry opening opportunities for youth to exercise their talents in their organizations through internship programs speaks the same.


  We have indeed spearheaded the formation of the East Africa Model Union where students and young people within the Community will simulate the EAC National Assembly, debating and coming out with concrete solutions that will help the EAC Secretariat to build a stronger and committed Community.


  Our Message:

  Through our work as EAC Youth Ambassadors, we have learned that East Africa region and Africa at large has nascent intelligentsia that we can empower ourselves to become the quality intelligentsia that our Community and the Continent deserves. The knowledge that we have emerged wiser and stronger from setbacks means that we are, ever after, secure in our ability to make  our East Africa Community survive and reach its ultimate goal to federation.


  As we demand for more voice and participation within our respective countries, we have learned that the way we vote, the way we live, the way we protest, the pressure we  bring to bear on our governments, has an impact way beyond your borders; and therefore we are the custodians to our East Africa Community.  Vote of Thanks

  We acknowledge and appreciate the committed effort of our EAC Secretary General H.E Ambassador Dr. R. Sezibera  and EAC Secretariat for giving a youth a platform to participate and be part of the decision making at the regional level.  The formation of the EAC Youth Policy speaks beyond commitment of the Community to achieve her mission and vision.

  We acknowledge GIZ Organization and indeed the Germany Embassy as a partner to our East Africa Community integration for sponsoring most of our work on youth affairs whenever necessary.  We also extend our sincere hand of appreciation to  all other partners of East Africa Community including the East Africa Business Council and East Africa Inter University Council for giving youth a space and place to put their ideas and influence the policies that will work for the betterment of the entire community.

  We salute the best people at hand who are always ready to air our voices. The East Africa Media and the international media for disseminating the information to our peers within the region and those in diaspora on the successful story about young people within the East Africa Community.


  In conclusion, as we look forward to inherit the future and lead the East Africa Community’s  vision and mission to her fulfilment in our generation, we the young people are called upon today to remind ourselves once more that; we are never too young to lead and we should never doubt our capacity to triumph where others have not.  The education that we have received and that which we continue to receive should prepare us to lead the way without fear and timid but with courage and team work. Out of many we are one.  East Africa One People One Destiny.


  And finally,on a closing note, I cannot overemphasize our gratitude to the EAC community for giving us the youth of the federation this great opportunity to tell our story.  I have heard that unless lions have historians, the hunt will always glorify the hunter...this is not the case for us, we are lions with historians, long live the EAC, long live the EAC youth.

  Thank you very much

  Long Live East Africa Community

  God bless Africa

   

  Raymond C Maro

  EAC Youth Ambassador to United Republic of Tanzania

  East Africa Community


  Dar es Salaam Tanzania- 03-09-2013 


  0 0


  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  UHAMIAJI haramu ni ile hali ya mtu wa Taifa lingine kuingia kwenye nchi nyingine bila kufuata sheria. Kwa mfano, raia wa Rwanda kuingia Tanzania kienyeji.

  Hafuati utaratibu uliowekwa na nchi huru yenye mamlaka zake. Huyo anavunja sheria, hivyo kwa ujio wake huo, anaweza kufanya vyovyote anavyotaka.  Hali hii ya uhamiaji haramu si ngeni duniani. Kumekuwa na mwingiliano na sababu nyingi zinazowafanya watu watamani kuingia katika nchi nyingine bila kupiga hodi.

  Kila siku wanasikika waliokamatwa baada ya jaribio lao la kuzamia kushindwa. Wapo wanaorudishwa makwao bila kupenda na wale pia wanaowekwa kizuizini.  Wakati tunaangalia jambo hilo, lazima tukubali kuwa sheria zetu, utendaji kazi wetu umewapa urahisi watu wengi kuingia Tanzania soni.

  Wahamiaji haramu wanaingia na kuweka makazi bila hata kuonwa na kuendelea na maisha yao. Na wale wanaonekana, wakati mwingine hawafikishwi popote, hasa kama watafanikiwa kutoa chochote kitu kwa watu wa uhamiaji au hata polisi.  Akiwa mkoani Kagera katika ziara yake ya kikazi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, aliwatangazia vita wahamiaji haramu.

  Aliwataka wote walioingia Tanzania bila kufuata sheria wabebe kilichokuwa chao na kurudi kwenye nchi zao. Akaonyesha ukali zaidi kwa kuwapa siku 14 kabla ya kuingia kwenye oparesheni ya kuwarudisha makwao.  “Nilitoa maagizo kwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama yaani JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Uhamiaji watengeneze mpango kabambe wa kuyashughulikia matatizo hayo. 

  Watayarishe na kutekeleza operesheni maalum itakayo au zitakazokomesha ujambazi, kuondoa wahamiaji wasiokuwa halali na kuondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume na utaratibu na ile iliyoko kwenye maeneo yasiyo stahili,” Rais Kikwete aliyasema haya pia katika Hotuba yake ya kila mwezi.  Pamoja na kusema hayo, lazima watu tufahamu kuwa kasi inayapoonekana mikoani ya wahamiaji haramu, ni zaidi katika majiji makubwa, hasa Dar es Salaam.

  Dar es Salaam ndio jiji pekee linaloweza kuwaficha wahalifu, wahamiaji haramu bila kuonekana. Ni rahisi kuona mtu anaendelea na biashara zake maeneo mbalimbali bila kuwa na kibali cha kuishi na ambaye pia hajafuata taratibu za kuingia.  Ni tofauti na Mataifa mengine. Nchini Botswana, wameweka sheriaa kali mno ya wahamiaji haramu. Hata wale waliofanikiwa kuwa na kibali cha kuishi huko wanapata shughuli pevu.

  Kwa mfano Mtanzania anayeishi nchini humo, anaposhindwa kufahamu mwisho wa kibali cha kuishi humo, ni sababu yake ya kurudi kwao hata kama hataki.  Hata atakapojisalimisha katika ofisi za uhamiaji, hatapata ushirikiano wowote zaidi ya kurudi anapotoka. Ndio hapo anapotoka kwanza nje ya mipaka ya nchi hiyo na kurudi tena kama mgeni, ambapo hapo atapewa siku kadhaa za kuishi.

  Haya ni tofauti na Tanzania. Nchi ya ukarimu na kitu kidogo. Ndio maana maeneo mengi hasa Dar es Salaam yanakumbwa na ongezeko la wahamiaji haramu.  Maeneo ya Kinondoni Shamba na mengine yote yana idadi kubwa ya watu wasiokuwa raia wa Tanzania na ambao hawajafuata sheria. Huko utakutana na watu wa Malawi wakiishi bila wasiwasi wowote.
  Na inapotokea mjumbe au mwenyekiti anajua mtaa wake una wahamiaji wasiokuwa na kibali cha kuishi, basi amepata uhakika wa kupata hela ya sukari siku anapoamka mweupe.  Anachofanya ni kujichukulia visenti kutoka kwa watu hao na kushindwa walau kuwashauri wafuate taratibu za kuishi nchini. Hili ni jambo la kushangaza mno.
  Rais Kikwete ameyasema hayo bila kujua kuwa maagizo yake mengi yanaishia njiani. Ni zima moto. Hakuna mipango kabambe, hivyo matamko yake kuishia kudharauliwa.  Siku 14 alizotoa kamwe haziwezi kuwa na faida. Zaidi zimeripotiwa kuchochea uhasama kwa wale wanaoshi sehemu mbalimbali za Tanzania, hasa vijijini, ambapo imeripotiwa baadhi ya watu hao kuingiza mifugo kwenye mashamba ya Watanzania, kama ishara ya kukerwa na kauli ya Kikwete.
  Muleba suala hili ni kama mkuki kwao. Kwa kupitia Mbunge wao wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, alizungumza kwa machungu pale aliposikia malalamiko ya wapiga kura wake kutokana na wafugaji kutoka nchini Rwanda kuingiza mifugo yao kwenye mashamba yao Watanzania.
  Tamko la Mheshimiwa Kikwete lilielemea sana kwa Mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita, huku majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Tanga yakiachwa.  Mkoa wa Tanga nao una idadi kubwa ya wahamiaji haramu wanaotoka kwenye nchi zao na kuweka makazi ya kudumu au wanaofanya njia ya kuelekea kwingine wanapohitaji.
  Mapema mwaka huu, maafisa wa uhamiaji wa Tanzania mkoani Tanga waliwakamata wahamiaji haramu 227 katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2012.  Idadi kubwa ya wahamiaji hao walikuwa ni Waethiopia, lakini baadhi walitokea nchi nyengine kama vile Pakistan, Bangladesh, Denmark, Zambia, China, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea, Switzerland, Sri Lanka, Uturuki, Msumbiji na Italia
  Hivyo kauli japo kauli ya Rais Kikwete ni njema, iliyosababishwa na raia wa Tanzania kukosa uhuru na usalama wa kutembea anavyotaka, ila juhudi sielekezwe nchi nzima.
  Ingawa si dhambi raia wa Kenya, Uganda, Msumbiji, Malawi, Zambia, Congo na wengineo kuja kuishi Tanzania, ila muhimu ni kufuata sheria zilizowekwa.
  Na inapotokea mtu ameweza kuja kuishi Tanzania, isiwe sababu ya kujifanya wapo juu ya sheria na kuanza kuwaletea kasumba zisizokuwa na maana kwa wenye nchi yao.
  Mwaka 1982, Rais wa awamu ya kwanza, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliweza kuwaruhusu wakimbizi wanaopenda kuwa raia wa Tanzania.
  Historia inaonyesha kuwa jumla ya wakimbizi 30,000 waliweza kutumia fursa hiyo, wakati mwaka mwaka 2010 wakimbizi 160,000 wa kutoka nchini Burundi nao walikuwa raia wa Tanzania.
  Serikali iwabane zaidi watendaji wake na pia juhudi za kukomesha uhamiaji haramu usibaki mikoa ya Kagera kama alivyotangaza rais Kikwete, maana janga hilo lipo pia jijini Dar es Salaam.
  Tusipokuwa makini, tunaweza kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu mikoa inayopakana na nchi jirani, lakini idadi kama hiyo kutokomea kwenye majiji yenye mwingiliano mkubwa.
  Kama mtu anaweza kuishi Dar es Salaam bila kufanywa chochote, tamko la kudhibiti suala hilo lina mhusu nini? Kama leo hii mtu mwenye asili ya China anaweza kuja na kuishi kama wanavyoishi wengine, kwanini aishi kwa presha?
  Sitaki kuamini kama watu wote wanaoishi jiji la Dar es Salaam ni raia au wanaishi kwa kufuata sheria. Wakati wao wakiishi bila presha, lakini kwao wao Mtanzania hawezi kuishi kwa raha kama atakuwa ameingia kienyeji kama nzi wa chooni.
  Leo hii Mtanzania hawezi kuishi China ovyo ovyo bila kuwa na shughuli ya uhakika, ila wao wameweka makazi. Tena wengine wanafanya kazi inayostahili kufanywa na Mtanzania.
  Ndio hapo utakapowakuta wamesheheni katika miradi mingi ya kimaendeleo, hasa ujengwaji wa barabara, ambapo nao wanashika chepe au kuwasimamia Watanzania.
  Na kama huo uhalifu utakwisha sehemu ya mikoani na kuhamia jijini Dar es Salaam, hatauoni kama tunapoteza muda bure? Naheshimu utendaji kazi wa Rais Kikwete ila mara nyingi anaangushwa na washauri wake. Wale wanaovunja sheria kwa sababu ya kuneemesha matumbo yao.
  Wale wanaojua fika kuwa operesheni za kudhibiti wahamiaji haramu zina maanufaa kwao kwasababu waya Kagera, tumie Aidha, niliwataka Maafisa wa Uhamiaji watimize ipasavyo wajibu wao. 
  Ukweli ni kwamba, mambo haya kuendelea kwa muda mrefu kiasi hiki ni kwa sababu ya udhaifu wa mamlaka husika.


older | 1 | .... | 151 | 152 | (Page 153) | 154 | 155 | .... | 1897 | newer