Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

uzinduzi wa Filamu ya foolish age ndani ya mlimani city jijini dar jana

$
0
0
 Elizabeth Michael Aka Lulu akitoa Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Proin Promotions Limited Geofrey Lukaza (Kushoto) akiwa na Waifu wake Groly Lukaza (katikakati) pamoja na Pedeshee Mamaa Ng'onzi wakijiachia Mbele ya Kamera ya Lukaza Blog usiku wa kuamkia Leo katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited
 Lady Jay Dee aka Anaconda akitoa Burudani katika Uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Lady Jay Dee akiwa pamoja na Machozi Band walitoa Bururdani Safi Sana katika Uzinduzi huo Uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
Msanii Barnaba akitoa burudani katika uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu uliofanya na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
 Katikati ni Mama Mzazi wa Elizabeth Michael akiongea kwa furaha huku akitoa machozi na Msanii wa Filamu Tanzania Wema Abraham Sepetu(kushoto) na Rafiki yao katika Uzinduzi wa Filamu ya Lulu ulioandaliwa na kufanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Wema Sepetu (aliyepiga magoti) akikumbatiana na Mama yake mzazi Lulu wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Mwanae Elizabeth Michael katika Ukumbi wa Mlimani City, uzinduzi uliokwenda sambamba na burudani kutoka Kwa Wasanii mbalimbali wa Muziki wa Bongo Fleva katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo.
Wadau wakisakata Mduara katika uzinduzi huo wa filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa kuamkia leo, Uzinduzi huo wa Kufa mtu uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ulifana kupita Kiasi
 Baadhi ya Wadau Mbalimbali waliojitokeza katika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Pron Promotions Limited.
Meza ya Viongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Kuanzia Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Bw Geofrey Lukaza, akifuatiwa na Pedeshee Mamaa Ng'onzi, Bwa Johnson Lukaza Mwenyekiti waa Makampuni ya Proin Tanzania, Gadna G Habash na Lady Jay Dee aka Anaconda wakiwa makini Kufuatilia Uzinduzi Mzima wa Filamu Mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Paul SekaBoy Mkurugenzi Wa Sekaboyi Production akiwa na rafiki yake katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City Usikuwa kuamkia leo
Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat Lukaza akiwa katika Picha ya Pamoja na Mmoja wa Watembeleaji wakubwa kabisa wa Lukaza Blog Maa Fetty katika Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Lady jay Dee akituzwa Mahela katika Uzinduzi wa Filamu Mpya ya LULU iitwayo Foolish Age ndani ya ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo

SERIKALI KUJENGA CHUO KIKUBWA CHA MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwasisitizia wahitimu na wageni (hawako pichani) waliofika katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora kuwa serikali lazima ijenge Chuo KIkubwa Cha Ufugaji Nyuki Tabora.


========  =======  ========
Na Tulizo Kilaga, Tabora


SERIKALI imeahidi kujenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufugaji nyuki katika eneo la Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika katika uzalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki.

Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda aliyekuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora alipokuwa akiwahutubia wahitimu kabla ya kuwatunuku vyeti na zawadi.

Mhe. Pinda alisema pamoja na mapungufu ya chuo hicho yaliyotokana na tabia ya kuhamisha mafunzo yake mara kwa mara kwenda kwenye vyuo mbalimbali vya Wizara ya Maliasili na utalii nchini, chuo kina umuhimu mkubwa kutokana na kuwa ni chuo pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Siku za nyuma chuo kiliweza kupata watu kutoka nchi za nje kuja kujifunza, hivyo serikali haiwezi kukiacha solemba! Kama tumeweza kujenga Chuo kikubwa cha Serikali za Mitaa, Hombolo kinachotufanya tushindwe kujenga chuo  kikubwa hivi ni nini? Kwamba hatuoni thamani yake? Si kweli, miaka kumi ijayo thamani yake itaonekana tu,” alisema Mhe. Waziri Mkuu.

Aliongeza kuwa, tatizo la kutoendelezwa kwa chuo hicho wakati mwingine kunatokana na viongozi kutojua kinachoendelea, hivyo aliomba uongozi kuwakilisha mpango mkakati wake ili serikali iweze kuipembua na kuona wapi pakuanzia.

Aidha, Mhe. Pinda aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uamuzi wake wa kukirudisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora na kutoa onyo kwa yoyote atakayetaka kujaribu kukihamisha tena kutofanya hivyo ili serikali iweze kujipanga na kusonga mbele.

Aliongeza kuwa, Tanzania ina hifadhi za misitu na maji ya kutosha inayotoa fursa ya kuzalisha asali nyingi, hivyo amewaasa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kuiwezesha nchi kushika namba moja kwa nchi za Bara la Afrika zinazozalisha asali.

“Tanzania hivi sasa inapitwa na Ethopia kwa uzalishaji asali, nchi ambayo haina misitu yakutosha, hili haliwezekani tuangalie mpango mikakati yetu. Ufugaji asali hauhitaji mtaji mkubwa, na soko lake ni la uhakika, tumshinde Ethiopia na hili linawezekana kama tutapanua mawazo yetu juu ya sekta hii,” alisema Mhe. Pinda.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa moyo wake wakusimamia kidete sekta ya ufugaji nyuki nchini na kutoa fursa za ajira kwa wananchi wengi.

Aidha, Mhe. Pinda alisisitiza kiu yake ya kuona Tanzania inazalisa asali nyingi kwa kuwaahidi wahitimu kuwapa zawadi ya mizinga 100 endapo wataunga na kuunda kikundi cha ufugaji nyuki na kutumia elimu waliopata kuweza kujipatia kipato.

Katika kusisitiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bi. Fatma Mwasa naye aliwahidi wahitimu ambao ni wakazi wa mkoa wake, kuunda vikundi vya  watu waiopungua kumi kwa kikundi ili aweze kuwapatia mtaji wa mizinga.

Bondia Francis Cheka awafurahisha waTanzania,Amfumua mmarekani na kunyakua Ubingwa wa Dunia

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
 Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang'anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
 Chukua hiyoooooo...
 Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
 Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.
Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo.

VIDEO YA MCHEZO INAKUJA.

wakazi wa mtwara waipokea kwa shangwe semina ya fursa kwa vijana leo.

$
0
0
Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semina ya FURSA kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.


 Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpo ambaye pia ni mwanachama wa NSSF,akizungumza fursa mbalimbali alizozipata ndani ya shirika hilo la NSSF,mbele ya wakati lukuki wa mji wa Mtwara waliojitokeza kushiriki semina hiyo,iliyokuwa na mafanikio makubwa. 
 Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semini hiyo


 
 Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.Katika semini hiyo vijana wemejitokeza kwa wingi.
 Msanii wa Kughani mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na Wana wa Mtwara kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huu,kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika leo mkoani humu. 
 Baadhi ya Waendesha Bodaboda walipata wasaa wa kuacha kazi zao na kushiriki semina ya Fursa kwa Vijana.
 Baadhi ya vijana wakiwa nje wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea ukumbini

DAUDI MWANGOSI ATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUUWAWA KWAKE MKOANI IRINGA.

$
0
0
Ndugu zangu,

HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu.

Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa,Daud Mwangosi kuawa.

Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile  itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja  kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi.


Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu,  nilisitisha mazoezi yale ya watoto. Nikawapa taarifa zile.  Nilipowaambia kuwa nimepata taarifa sasa hivi kuwa mwandishi wa habari ameuawa Mafinga, mtoto mmoja akaniangalia na kuniuliza; “ Kwanini?”

Ndiyo, swali la mtoto yule ndilo umma wa Watanzania unapaswa uendelee kujiuliza hata leo; KWA NINI?



Mwandishi wa habari ni mjumbe katika jamii. Anapokuwa akifanya kazi yake hapaswi kuwa na hofu ya kudhuriwa kwa kukusudia na waliopata mafunzo ya  kutumia silaha.  Ndivyo ilivyo kwa watumishi wa Msalaba Mwekundu, wanapokuwa kazini kwenye maeneo hata ya vita.


Askari asiyejua kutofautisha kati ya mwanahabari aliyeshika kamera, mtu wa Msalaba Mwekundu aliyeshika mkoba wa Huduma ya  Kwanza na raia anayefanya vurugu au adui aliyeshika silaha vitani, huyo hawezi kuwa ni askari makini.

Na hakika, kama  Taifa,  tunafanya makosa kuamini,  kuwa  nchi yetu ni ya amani kwa vile wananchi wetu hawagombani. Kama watu hawagombani kuwa na maana nchi ni ya amani  yaweza kuwa tafsiri potofu ya maana nzima ya amani.  Maana, kama watu hawagombani mahali pasipo na haki, usawa na uadilifu wa viongozi; mahali palipojaa dhuluma,unyanyasaji na maovu mengine  wanayotendewa au wanaotendeana wanajamii,  basi, amani hiyo itakuwa ni ya muda tu.
Maana, kwa watu wenye kuishi kwenye mazingira hayo bila kugombana wala kutokea uvunjifu wa amani, hiyo  itakuwa na maana ifuatayo; ama watu hao hawaelewi kuwa wanaishi katika mazingira hayo ya dhuluma na maovu mengine wanayotendewa au kutendeana, au wamejawa na  hofu.



Hivyo basi, kwa hilo la mwisho, itakuwa ni amani iliyojengeka katika misingi ya hofu. Na hofu hiyo haiwezi kuwa ya kudumu. Kuna siku mwanadamu hufikia ukomo wa kuhofia. Ukimwandama sana mjusi, mwisho hugeuka nyoka! Ndipo hapo tunapoona nchi zinalipuka na watu kuchinjana.

Hii ni nchi yetu. Katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania kwa kutanguliza maslahi ya Tanzania. Kuna umma uliopo na unaokuja. Umma  unaotegemea sana busara katika uongozi wetu. Tuanze sasa kujenga utamaduni wa kuitumikia nchi yetu kwa kufanya na kuamua yale yenye maslahi kwa Tanzania. Hivi vyama vya siasa vipo leo na kesho havipo. Vinakuja na kuondoka, lakini Tanzania kama nchi itakuwapo daima.

Tusifike mahali  tukabaki tunawaangalia wanasiasa wetu, kwa maslahi yao binafsi, ya makundi yao na vyama vyao,  wakashinikiza au kuelekeza yale  yenye kuchochea machafuko makubwa ya kijamii. Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.
Na tunafanyaje pale tunapowaona viongozi  wa kisiasa na watendaji wakifanya maamuzi yasiyo na busara na kusababisha Watanzania wenzetu kupoteza uhai na hata kuchochea machafuko?
Jibu; Kama Watanzania wazawa na wazalendo wa nchi hii, tuna wajibu wa kuyalaani matendo yao maovu.

Na katika nchi zetu hizi, ni kazi rahisi sana kuanzisha vurugu  na kujenga mazingira ya chuki na  uhasama, lakini, ni kazi kubwa sana kumaliza vurugu na kuondosha mazingira hayo ya chuki na uhasama. Na nchi yetu kamwe haiwezi kupiga hatua za maana za maendeleo katikati ya mazingira ya vurugu, chuki na uhasama, uwe wa vyama vya siasa au wanajamii.

Kihistoria, Watanzania tumeishi kwa amani na upendo bila kuwa na chuki na uhasama miongoni mwetu unaotokana na tofauti zetu za kidini na kikabila. Tunaziona sasa, dalili za baadhi ya wanasiasa, kwa malengo ya kisiasa,  kutaka kupandikiza miongoni mwetu uhasama na chuki kwa kutumia tofauti zetu za kidini na kikabila, tofauti zetu za kiitikadi.  Wanafanya hivyo mara ile wanaposhindwa kujenga hoja za kisiasa kwenye majukwaa ya kisiasa. Hawa ni watu hatari sana kwa maslahi ya taifa letu.

Katika nchi zetu hizi, ni wanasiasa wa aina hii ambao, katika kufanikisha malengo yao,  huwa tayari hata kuwalipa vijana wasio na ajira na kuwavutisha bangi ili washiriki vurugu za kisiasa, kidini na kikabila.  Tumeyaona hayo Liberia, Ivory Coast na hata katika nchi jirani na kwetu.
Tusipokuwa makini, yako karibu kupisha hodi kwenye nchi yetu, kama si tayari kuwa yameshaingia ndani ya nchi yetu.

Hii ni nchi yetu. Tutafanya makosa makubwa kuwaachia viongozi wa kisiasa pekee, jukumu la kulinda maslahi ya nchi yetu.  Tunapita sasa katika kipindi kigumu tangu tupate Uhuru. Dunia imebadilika, na nchi yetu inapitia kwenye kipindi cha mabadiliko. Hakuna  mtu au chama cha siasa kinachoweza kuyazuia mabadiliko  haya. Kufanya hivyo ni kutuletea machafuko na kuvunja amani yetu. Tuna jukumu la kufanya tunayoweza, na kwa kutanguliza busara, kuipitisha salama nchi yetu katika kipindi hiki cha mabadiliko.

Maana, tukiingia kwenye machafuko, basi, hakutakuwa na mshindi, maana, sote tutashindwa. Na kifo cha Daudi Mwangosi kinatutaka tuyatafakari haya.
Maggid,
Iringa.

Baada ya wakazi wa mtwara sasa serengeti fiesta 2013 inatia timu mkoani mbeya na iringa mwishoni mwa wiki hii.

$
0
0
 Tonya Time,Tonya Boy,Matonya yote waweza kumuita katika anga ya muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva,akiwatumbuiza wakazi wa Mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kushiriki pamoja tamoja la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo mwishoni mwa wiki.
 Tajiri wa mahaba mwenye nyimbo lukuki za kubembeleza,Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Mtwara na Vitongoji ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
 Wanaume Halisi wakiongozwa na mkongwe katika anga ya muziki wa bongofleva,Juma Nature wakilishambulia jukwaa kwa pamoja,huku mayowe ya washabiki wao yakisikika kila kona ya uwanja. 
 Mmoja wa wasanii mahiri wa miondoko ya hip hop (bongofleva),Godzilla a.k.a Mzee wa salasala akishusha mistari yake live kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki.
 Pichani kati ni  Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume akiwa sambamba na wadau wengine,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2013,lililofanyika ndani ya uwanja wa Nangwaanda Sijaona,Mkoani Mtwar mwishoni mwa wiki.
Iliku ni noma saana ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona.Tamasha la serengeti fiesta limekwishafanyika ndani ya mikoa minne mpaka sasa,ikiwemo Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara na sasa linaelekea mkoani Mbeya ambapo linatarajiwa kufanyika Septemba 6 na baadae septemba nane ndani ya Mkoa wa Iringa.

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE REDDS MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2013

$
0
0

Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa p[icxha mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kutinga nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013. 
********   ********
Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013. 

Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi kwa picha na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka mshindi wa taji la Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda.(
Warembo wengine Walioshiriki shindano hilo wakifuatilia utangazwaji wa matokeo hayo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View katika kambi yao. 
=======  =======  =======
Mrembo wa Mkoa wa Dodoma,  na mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa  mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013. 


Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.

Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.

Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.

Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa kwashangwe.

Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa aliyeibuka mshindi.

Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.

Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa. 

Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.

bondia francis cheka apokewa kwa shangwe mkoani morogoro.

$
0
0
Bondia Francis Cheka akiwa sambamba na Mkanda wake aliokabidhiwa Agost 30 baada ya kumtwanga Mmarekani Phil William  mwishoni mwa wiki ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,pichani bondia huyo akiwa na mashabiki wake wakati alipokuwa akiwasili mkoani Morogoro anakoishi mapema jana jioni.
                 Msafara kuelekea katikatika ya mji ukiendelea

Cheka akizungumza na umati mkubwa wa watu uliofurika kwenye ukumbi wa Old Vai jana majira ya saa 12 jioni kwenye mapokezi hayo ya Cheka kulikuwa na vituko kibao kikiwemo cha Mlemavu wa miguu aliyenusurika kugongwa na gari alipotaka kumshika mkono Cheka baada ya kuona tukuio hilo Cheka alisimamisha msafara huo na kumshika mkono Mlemavu huyo kwa habari na picha za tukio hilo la kuhudhunisha zitawajia hivi punde

PICHA ZOTE NA KWA HISANI YA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO-

Mlemavu wa macho awastaajabisha wakazi wa Mtwara ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013 mwishoni mwa wiki

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI BREWERIES YAZINDUA KINYWAJI CHAKE KIPYA CHA TUSKER LITE KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Wakizundua rasmi bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini
Mwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa Dilip Chudasama na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto). 
 Burudani murua kabisa ilitolewa na bendi.
 Baadhi ya viongozi wa idara ya masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiwaonesha wageni waalikwa(hawapo kwenye picha) chupa ya bia ya Tusker Lite  katika hafla ya uziduzi wa bia hiyo kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia ya
Serengeti Bi Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker, Bi Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto).
 Timu nzima ya mauzo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kanda ya ziwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa  bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.
 Muda wa maakuli baada ya uzinduzi.
Meneja wa vinywaji vya Tusker,Sialuoise Shayo akitoa ufafanuzi kwa wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.

Diamond Platnumz - Number One [DJMwanga comHD]

Free Mind Events waianza Septemba kwa chakula na watoto yatima Kigamboni

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya Free Mind Events yenye makazi yake jijini Dar es Salaam, AbdulMalik Fundikira akiwa na Mzee Maiko, mmoja kati ya walezi wa kituo cha New Hope, kilichopo Mjimwema, Kata ya Ungindoni, eneo la Kigamboni jijijni Dar es salaam ambapo jana kampuni yake ilifungua mwezi Septemba kwa kula chakula cha mchana na watoto hao
 Chakula kilipikwa na kampuni hiyo inayotoa pia huduma ya Catering, hapa Malik akionesha chakula na kukionja kuhakikisha kwamba ni salama kwa kuliwa
 msafara ukielekea eneo la maakuli, alyevaa kofia ni mlezi wa kituo hicho Anita Diagle
 Hapa ni maandalizi yakiendelea, Abdul Malik, na Anna Mwakatundu ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Free Mind Events wakiwa washughulikaji wakuu
 Msosi fresh, pamoja na watoto
 Baadhi ya watoto wa kituo cha New Hope wakiendelea na msosi
Na baada ya chakula, kesho shule itakuwaje? Ilibidi Abdulmalik ajipinde, watoto wakichukua nauli zao hapa kwa ajili ya siku inayofuata

MISS TANZANIA 2012 BRIGITTE ALFRED AONDOKA LEO KWENDA KAMBI YA MISS WORLD INDONESIA

$
0
0
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini leo kwenda nchini Indosia katika kambi ya Miss World 2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii tayari kwa safari hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya kuondoka.
 Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.
 Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
  Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia hii leo.  SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG

Weruweru Public Lecture by Mama Kamm

$
0
0
Among other things scheduled to commemorate the Golden Anniversary of Weruweru Girls School,the Weruweru Alumni Foundation brings you a public lecture by the amazing Dr. Maria Kamm. The public lecture is geared at communicating the Power of Educating the Girl Child, followed by a Panel discussion on the same topic,by distinguished guests.
The lecture is OPEN to all interested members of the public....

Venue: Julius Nyerere Convention Center
When: 12th September,10a.m
Invitees: You!

See you all,there.

xoxo
Missie Popular
...................... Sent from my iPad >

Amsha Maisha Yako

$
0
0
 Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka gestures as he addresses the media at the launch of Amsha Maisha Yako na Coca-Cola campaign in Dar es Salaam over the weekend. A total of 200 Honda motorcycles (Boda Bodas) and Tsh400m will be won during the two-month campaign. 
 Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka gestures as he addresses the media at the launch of Amsha Maisha Yako na Coca-Cola campaign in Dar es Salaam over the weekend. A total of 200 Honda motorcycles (Boda Bodas) and Tsh400m will be won during the two-month campaign. 

 Coca-Cola Kwanza Sales and Marketing Manager Nalata Hettiarachchi rides on one of the 200 motorcycles (Boda Bodas) to be won during a two-month Amsha Maisha Yako na Coca-Cola campaign launched in Dar es Salaam over the weekend. Others from right are Coca-Cola Tanzania Assistant Brand Manager Warda Kimaro, Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka and Nyanza Bottling Marketing Manager Marco Masaka.
==========  =========  =========
Coca-Cola Tanzania has today launched a consumer promotion that will enable Coca-Cola consumers to win brand new Boda Bodas and cash prizes of up to Tshs1m. Other cash prizes are Tshs500,000, Tshs100,000, Tshs50,000, Tshs20,000, 10,000, 5,000 and free drinks.


The two-month promotion dubbed Amsha Maisha Yako na Coca-Cola creates yet another unique platform for the beverage company to interact closely with its customers and consumers throughout the country.


“The promotion we are launching here today will certainly transform the lives of some lucky Tanzanians who will get the opportunity to win the stated prizes, especially the Boda Bodas which have in recent years become a source of employment to thousands of Tanzanians using them in rendering transport service to the community”, said Coca-Cola Tanzania Brand Manager, Maurice Njowoka.


Over the years Coca-Cola has always believed in empowering the community in which it operates through such kind of rewarding promotions and “Amsha Maisha Yako na Coca-Cola is aimed to achieve the same purpose”. Last year, hundreds of Tanzanians benefitted from a similar Coca-Cola promotion named “Vuta Mkwanja na Coca-Cola” in which lucky consumers became instant millionaires through this Coca-Cola initiative.   


In this year’s campaign, winners will be obtained through drinking 300ml and 350ml return glass bottles of Coca-Cola, Fanta and Sprite. “The mechanics is simple: drink Coke, Fanta or Sprite and look under the crown to reveal your prize instantly, to win a Bodaboda one will need to collect three crowns i.e. making his own Bodaboda by collecting a front wheel, back wheel and the engine”, says Njowoka.


While winners of free sodas will be able to claim their drinks at the same sales points, winners of Boda Bodas and the cash prizes will be allowed to collect their prizes after presenting their crowns at designated redemption centers along with their identity cards. Employees of the Coca-Cola, its agents and other companies involved are not allowed to enter into this contest.


Njowoka has asked Coca-Cola consumers and the general public to participate in this life transforming promotion and stand a chance to raise sustainable daily income if one wins Bodaboda or cash, courtesy of the beverage company.

 

He underlined The Coca-Cola Company’s commitment to continue producing and supplying only the best quality beverages. 

DKT SHEIN;ZANZIBAR IMECHANGIA SANA KUKUZA NA KUENEZA USTAARABU MAENEO YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO ZANZIBAR   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dkt. Ali Muhammed Shein amesema Historia inaonyesha kuwa Zanzibar imechangia sana katika kukuza na kueneza ustaarabu wa kiislamu katika maeneo ya Afrika Mashariki.
Amesema Masheikh na Maulamaa wa Zanzibar  walikwenda kueneza Uislamu katika maeneo  ya Ukanda huo na wengine walifika visiwa vya Comoro  na nchi nyengine za Afrika ya Kaskazini na baadhi ya nchi za Asia.
Dkt. Shein ameeleza hayo alipokuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika nch za  Afrika Mashariki linalofanyika katika Hoteli ya Lagema, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema anaamini kuwa kutokana na Historia  na vigenzo  vyengine vingi ndio viliopelekea  Mamlaka ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Falme  ya Oman kuichagua Zanzibar kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la Kimataifa la kiislamu kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Kwa hakika Zanzibar ndiyo kitovu cha Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika nchi za Afrika Mashariki, hivyo kuichagua Zanzibar kuwa mwenyeji wa kongamano hili ni pahala pake,”alisisitiza Dkt. Ali Muhammed Shein.
Amongeza kuwa yapo maelezo ya kihistoria yanayoeleza kwamba msafara wa viongozi wa dini ya kiislamu ukiongozwa na Sayyid Jaffar bin Abu Talib waliingia Zanzibar na kufikia kijiji cha Ndagoni Pemba kabla ya viongozi wengine wa dini kuingia Madina.
Amesema  lugha ya Kiswahili imekuwa chombo muhimu cha   kueneza na kuendeleza ustaarabu na mafundisho mengine ya dini ya kiislamu kupitia mawaidha, darsana pia tafsiri za vitabu vya dini ya  kiislamu katika ukanda wa Afrika Mashariki.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema kuwa ithibati ya kuingia dini ya kiislamu Afrika Mashariki katika karne ya tisa  ni  mabaki ya baadhi ya misikiti iliyojengwa katika karne ya kumi na kugunduliwa kwenye baadhi ya maeneo ya miji ya kale ya Zanzibar ikiwemo Unguja Ukuu Kae Pwani kwa Unguja na Mtambwe mkuu kwa upande wa Pemba.
“Kadhalika  msikiti mkongwe wa Kizimkazi Dimbani ni kumbukumbu isiyo na shaka, inayobainisha wazi kuwa Zanzibar  ilikuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislamu katika kipindi cha mwishoni mwa karne ya 11 AD na kuingia karne ya  12 AD,”alisema Rais Shein.
Amebainisha Uislamu unafaida kubwa katika kuimarisha na kuendeleza Utamaduni na maisha ya kila siku na umekuwa ukijitokeza katika masuala mbali mbali yakiwemo mavazi, malezi, vyakula, elimu, sheria na utawla, shughuli za mazishi ndoa na hata sanaa katika ujenzi wa nyumba za kale.
Dkt. Ali Muhammed Shein ameeleza  kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango muhimu unaotolewa na Taasisi za kidini na ndiyo sababu ya kuanzisha Ofisi ya Mufti kusimamia masuala ya kidini ikiwa ni pamoja na kuziendeleza madrasa na kuyaendeleza malezi ya watoto.
Amesisitiza haja ya kuimarisha Umoja na kuepuka mifarakano katika jamii na pia amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuishi vizuri na waumini wa dini nyengine duniani kote.
“Uislamu ni dini ya amani  na kwa hakika mifarakano na vitendo vinavyohatarisha amani na Ustawi wa Jamii si sehemu ya Ustaarabu wa Kiislamu.” alisisitiza Rais wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar amelitaka kongamano hilo liwe chemchem ya tafiti zaidi za Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu Afrika Mashariki na kuzingatia uwezekano wa kuanzisha kituo cha Historia na Utamaduni wa Kiislamu Zanzibar.
Akizungumza katika Kongamano hilo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) Dkt. Emeleddin Ihsan amesema uislamu ni dini inayosisitiza amani na maelewano duniani.
Hata hivyo a mesema hivi sasa imezuka dhana  ya kupigwa vita na kuonekana kama ni dini hatari  inayozalisha magaidi  jambo ambalo sio la kweli.
“Dini ya kiislamu inapinga ugaidi na ni dini ya usalama inayosisitiza amani na maelewano ili kuishi kwa usalama duniani kote  hivyo  tusikubali baadhi ya watu wanaoipiga vita dini hii, ”Dkt. Ihsan alisema.
Kongamano hilo la siku tatu linatarajiwa  kumalizika Jumatano ijayo ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Muhammed Gharib Bilal atakuwa mgeni rasmi siku  ya ufungaji.     
               
                                                  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


DK ALBERIC KACOU AFUNGUA WARSHA KWA WARATIBU WAKAZI MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA JIJINI DAR LEO

$
0
0
IMG_5252
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akifungua warsha siku tano kwa Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika inayosisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli na majukumu ya Umoja wa Mataifa katika za Kusini mwa Afrika yenye ujumbe wa Delivering As One (DAO) kutoa matokeo ya pamoja katika kuratibisha na kuboresha majukumu ya Umoja wa Mataifa katika nchini hizo.

Akifungua warsha hiyo Dk. Kacou amesisitiza umuhimu wa mkutano kuwapa jukwaa wafanyakazi wote wa Ofisi za waratibu wakazi jinsi ya kujielimisha na kupata habari ya mabadiliko ya Dunia na majukumu ya Kikanda yanayoendana na maboresho ya kuratibu shughuli za Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuleta matokeo ya pamoja.

Alisema warsha hiyo itawajengea uwezo kwa washiriki umuhimu wa kujenga mazoea ya kujielimisha kimkakati na stadi za kazi zenye kuleta ufanisi katika kusaidia kuleta mabadiliko ya kazi za Umoja wa Mataifa katika nchi za Kusini mwa Afrika.

Dk. Kacou ameongeza katika kuleta matokeo ya pamoja Waratibu wakazi wanajukumu la kuhakikisha Haki za Binadamu na Mashirika yanayotetea Haki za Binadamu yanapewa wigo mpana katika kushiriki kwenye mchakato wa Demokrasia na Haki za Binadamu.

Amefafanua kuwa Mkutano huu unafanyika Tanzania kwa sababu ni nchi iliyoonyesha mafanikio katika nyanja hizi za Kiuchumi, Kisiasa, Demokrasia na Haki za Binadamu.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Kikanda cha Maendeleo Umoja wa Mataifa (UNDG) Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya kuchukua na kupeleka mbele mabadiliko ya kimkakati yanayoleta matokeo ya pamoja.
IMG_5294
Kamishina Msaidizi wa Bajeti Wizara ya Fedha Bw. Jerome Buretta akizungumza kwenye majadiliano ya warsha hiyo kwamba Serikali ya Tanzania iliamua kuingia katika mpango huu wa matokeo ya pamoja(DAO) na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ili kuleta ufanisi katika nyanja mbalimbali ambazo zinafadhiliwa na Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Bw. Buretta amesema katika mpango huo inaiwezesha Serikali kukaa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kupanga Bajeti na matumizi ya fedha zitolewazo na nchi wahisani ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwenye jamii.
IMG_5266
Baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku tano iliyoanza leo jijini Dar.
IMG_5304
Kwa upande wake Kansela wa Mambo ya Siasa Ubalozi wa Norway nchini Bi Elisabeth Schwabe Hansen amesema kwamba nchi yake ya Norway ni mdau wa muda mrefu wa maendeleo nchini Tanzania katika kuhakikisha maboresho na mipango ya Umoja wa Mataifa yanapitia katika mkondo sahihi kuhakikisha miradi ya maendeleo na ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania unaleta matokeo ya pamoja.
Bi. Hansen ameongeza kuwa katika mipango hiyo ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ni kuhakikisha inajenga uwezo wa rasilimali watu na kuratibu programu za Umoja wa Mataifa ambazo zinaendana na dira ya maendeleo ya Taifa.
IMG_5333
Mmoja wa Afisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akibadilishana uzoefu juu ya Programu hii ya matokeo ya pamoja kwa baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.


IMG_5338
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
IMG_5216IMG_5213IMG_5313
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria ufunguzi wa warsha ya Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa Mashariki na Kusini mwa Afrika inayoendelea jijini Dar katika Hoteli ya Kunduchi Beach Resort.
IMG_5380
Mwezeshaji wa warsha hiyo Bi. Jacqueline Olweya kutoka UNDG (kushoto) akimsindikiza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou (katikati) kwenda kupata picha ya pamoja na washiriki. Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo.
IMG_5389
Washiriki wa warsha ya siku tano ya Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka nchi 21 kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo leo.

tazama Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililopelekea baadhi yao kutoka nje.!

Wadau wa Utoaji Haki wa Chama cha Majaji Wanawake nchini wakutana kujadili Utokomezaji wa matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na Rushwa ya Ngono

$
0
0
Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo ya siku 1.
 ke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) , mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono..Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

GUMZO LA JIJI "THE AJ UBAO SHOW-SWEET PETER JEETER"

$
0
0
COMING UP SOON ON SWAHILI RADIO

 "THE AJ UBAO SHOW-SWEET PETER JEETER"

MAISHA YA NDOA,MUZIKI, NA MAHUSIANO: KIPINDI CHA 



REDIO KITAHUSU KUTOA 

USHAURI,KUIMARISHA,KUJENGA,KULINDA,KUJADILI,

KU-SHARE 

CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO. ITAKUWA LIVE SHOW

 SIMU ZA RADIO MOJA KWA MOJA HEWANI, WATU DUNIANI

 KOTE WATACHANGIA. MWENDESHA SHOW MTAALAMU

 WAKO SWEET PETER JEETER WA SWAHILI RADIO

HAPA HAPA SWAHILI RADIO



Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images