Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU MPYA ITUMIKE KUDHIBITI WANAOCHIMBA MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI YA MTO ZIGI JIJINI TANGA

$
0
0

Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
..........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria


"Nimeagiza watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.


"Kwasababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama"  alisema Dk. Kigwangalla.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo alisema pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda wote.


"Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wananchi hawaingii ili tusiwe tunawashtukiza kuwakamata na kwachukulia hatua, lazima tuwe watu wa kuzuia uhalifu usitokee, nia yetu ni kuwa na kituo mara moja kama alivyoelekeza Mhe. Waziri na hili jambo tumelichukua kama maelekezo na tutalitekeleza kwa nguvu kabisa," alisema Prof. Dos Santos Silayo.


Awali Dk. Kigwangalla alitembelea kikundi cha wafugaji wa vipepeo katika Tarafa ya Amani ambao waliiomba Serikali ifungulie vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo nje ya nchi, aliahidi kuyafanyia kazi maombi yao huku akiwataka kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani.


Akiwa mkoani Tanga alitembelea pia Kituo cha Mambo ya Kale cha Mapango ya Amboni na kusema Wizara yake itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini viweze kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.


Katika ziara hiyo ya siku moja mkoani Tanga alitembelea pia shamba la miti ya Mitiki Longuza, Makumbusho ya Shaban Robert na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vipepeo katika moja shamba la wafugaji katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana. Mbali na biashara ya kuuza vipepeo hao nje ya nchi aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaidia baadhi ya watu kupanda mlima baada ya kukagua chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho kipo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani wilayani Muheza mkoa wa Tanga. Ameiagiza TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hilo linalovamiwa na wananchi kwa madai ya kuchimba madini ya dhahabu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kuhusu kivutio cha utalii cha umbo la asili la ramani ya Afrika alipotembelea mapango hayo jana Jijini Tanga. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuhusu asali inayozalishwa na Wakala huyo kupitia shamba la Miti Sao Hill muda mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Asha Shaban ambaye ni dada yake na aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya Shaban Robert alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Asha Shaban ambaye ni dada yake na Shaban Robert aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya zawadi ya asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kupitia shamba la Miti Sao Hill alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kukagua Kituo cha Mapango ya Amboni wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Tanga jana ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya namna ya kupanda miti ya Mitiki kutoka Meneja wa shamba la Miti Longuza alipotembelea shamba hilo jana wilayani Muheza Mkoani Tanga. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Tanga. 

KAMANDA MUSLIMU AZUNGUMZIA BODABODA KUPIGWA BARABARANI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii. 

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu amesema hakuna sheria inayoruhusu askari polisi kupiga wanaotumia vyombo vya usafiri barabarani wakiwamo waendesha bodaboda huku akielezea kuwa atafuatilia ili kubaini iwapo kuna askari wenye tabia ya kupiga waendesha bodaboda. 

Muslimu ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana kwenye kupunguza ajali za barabarani ambapo Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limetoa tathmini ya mpango mkakati wa awamu ya kwanza na awamu ya pili unaonesha ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi kikubwa nchini. 

Hivyo ameelezea pia umuhimu wa watumiaji wa barabara wakiwamo waendesha pikipiki maarufu bodaboda kuzingatia sheria za usalama na kuelezea kuwa wanapaswa kufuata sheria bila shuruti. Hata hivyo waandishi wa habari waliokuwa kwenye mkutano huo walitaka kufahamu ni kwanini baadhi ya askari polisi hasa maeneo ya makutano ya Tazara, Ubungo, Mwenye na Daraja la Salenda wamekuwa wakiwapiga waendesha bodaboda na kusababisha hali ya sintofahamu. 

“Sheria hairuhusu mtu yoyote kumpiga mwingine na kama kuna makosa yamefanyika hatua za kisheria zinastahili kuchukuliwa lakini si kupiga mtu.Hii ya kwamba askari wanawapiga bodaboda tutafuatilia lakini nachofahamu hakuna askari anayeweza kumpiga mtu wa bodaboda.

 “Pia ifahamike tunazo sheria za usalama barabarani ambazo tunazisimamia na wakati huohuo zipo sheria ndogondogo za Jiji ambazo nazo kuna watu wanaozisimamia na kuzitekeleza.Suala la bodaboda kukamatwa hilo lipo chini ya Jiji na Tambaza ndio wanaohusika na waendesha bodaboda,”amesema Kamanda Muslimu. 

Amefafanua licha ya kwamba hakuna askari anayeweza kupiga waendesha bodaboda barabarani ameahidi kufuatilia kwa kwenda maeneo yanayolalamikiwa kupata ukweli wake na ikibainika atachukua hatua. Ameongeza wao wanalojukumu la kusimamia sheria za usalama barabarani na pia wanalo jukumu la kukabiliana na wahalifu.

DC Mtanda Kuanzisha Wangabo Cup kupongeza juhudi za Wana Kirando.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda kuandaa tamasha la michezo ili kuwapongeza wananchi wa Kata ya Kirando kwa kujitokeza kwa wingi katika songambele ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kirando pamoja na ujenzi wa madarasa manne katika Shule ya Sekondari Kirando.

Ameyasema hayo baada ya kuona umati wa wananchi wa kata hiyo ulipojitokeza wake kwa waume kushambulia ujenzi wa msingi wa kituo cha afya cha kirando, ujenzi ambao unatarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu ukihusisha majengo manne ya maabara, mochwari, jengo la wazazi pamoja na wodi ya kinamama.

“Wanakirando Mmekuwa na mshikamano bila ya kujali Vyama vyenu na itikadi zenu…ninyi mnaongoza kwa kujitokeza katika songambele kuliko mahali kwengine popote, Mh. DC nakutaka unazishe tamasha la michezo ili kupongeza kwa hiki kilichotendeka hapa.” Rc Wanagbo alisema.

Pamoja na hayo Mh. Wangabo aliahidi kutoa mipira ya miguu Minne, ya Netball miwili pamoja na Vikombe viwili vya mashindano hayo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda baada ya kupokea maelekezo hayo alianzisha harambee kwaajili ya kuanzisha mashindano hayo na hatiame madiwani, na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Nkasi walichanga fedha na vifaa mbalimbali ili kufanikisha tamasha hilo ambalo Mkuu wa Wilaya alilipa jina la Wangabo Cup.  
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (jezi ya Njano) akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki Songambele ya Upanuzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kirando iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza Kushoto).

POLAND KUFUNGUA OFISI ZA UBALOZI WAKE NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mhe. Krzysztof Szczerski  wakati alipoleta salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe mara baada ya kukabidhi  salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski wakati alipoleta salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski  mara baada ya kupokea salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Poland nchini Tanzania Mh. Krzysztof Buzalski mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati walipoleta salamu na mwaliko wa Rais wa Poland kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, Waziri Mwakyembe aliokea salamu hizo kwa niaba ya Rais Magufuli. Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO

Na Ismail Ngayonga
SERIKALI ya Jamhuri ya Poland mapema mwezi April mwaka huu inatarajia kufungua upya Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini ambazo zilifungwa kwa muda, hatua inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 23, 2018) Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa Salamu za Rais wa Poland kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mwakyembe alisema hatua zote muhimu za ufunguzi wa Ubalozi huo, taratibu zote muhimu kwa ajili ya ufunguzi Ofisi za Ubalozi huo tayari zimekamilika na kuongeza kuwa kufunguliwa kwa ubalozi kutazidi kudumisha ushirikiano na urafiki wa muda mrefu baina ya Tanzania na Poland pamoja na kuimarisha diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo.

 “Serikali ya Jamhuri ya Poland imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania, ambapo matunda ya ushirikiano ni kwa Serikali yetu kupata wa mkopo wa masharti nafuu uliofanikisha uanzishaji wa kiwanda kikubwa cha matrekta kibaha Mkoani Pwani” alisema Dkt. Mwakyekmbe.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Krzysztof Szczerski  alisema ziara yake ya kuja nchini ni kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Poland ambapo pamoja na mambo mengine Serikali ya nchi hiyo imekusudia kuimarisha mahusiano yake ya kiuchumi na Tanzania.

Aliongeza kuwaa katika kuendeleza jitihada zake za kuimarisha uhusiano wake na Tanzania, Serikali ya Poland tayari inaendesha miradi mbalimbali ya uwekezaji nchini ambapo Rais wa Poland ameahidi kuimarisha ushirikiano huo baina yake na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

“Niwewasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Poland ambapo pamoja na mambo mengine, amemualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda nchini Poland kwa ajili ya ziara maalum ya kiserikali” alisema Szczerski.

KAULI YA RAIS MAGUFULI,KENYATA KUHUSU KUONDOLEWA TOFAUTI ZA KIABISHARA

Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele ya uzinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

$
0
0
Zaidi ya wananchi 1200 wa kata ya Kirando inayojumuisha vijiji vinne vya Mtakuja, Mpata, Kichangani na Kamwanda, Wilayani nkasi Mkoani Rukwa, wajitokeza katika kuhakikisha uchimbaji na uwekaji wa msingi wa kituo cha afya cha kirando unakamilika ili kuweza kuanza upanuzi na ujenzi wa kituo hicho kitakachohudumia kata zaidi ya nne katika tarafa ya Kirando.  

Wananchi hao wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha huduma hizo za kiafya zinasogezwa karibu na wananchi yao ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito, watoto na wahitaji wengine wa huduma hizo ambao wanaishi karibu na kituo hicho na kuongeza kuwa umbali wa kutoka Kirando hadi hospitali ya Wilaya iliyopo Namanyere ni Kilometa 61.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyeongoza harambee hiyo amesema kuwa wameamua kuungana na wananchi pamoja na kuwashirikisha ili kuwajulisha wananchi juhudi zinazofanya na wananchi na kuonyesha mshikamano kuwa maendeleo hayaji bila ya mshikamano.

“Kila mtu anaguswa na afya, mtoto, mzee na kijana wote, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli imeamua kuboresha na kupanua vituo vya afya ili huduma zisogee karibu kuliko kutegemea hospitali za wilaya, kwa hali hiyo ndio maana serikali inapanua vituo vya afya ili tuupunguze msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali zetu pamoja na kwenye vijiji na tarafa huduma ziwe bora zaidi.” Alifafanua.

Miongoni mwa kinamama waliohudhuria katika Songamebele hiyo Hamisa Heri amesema “Tunamshukuru Mh. Magufuli kwa muda mrefu kumekuwa na shida ya huduma ya uzazi mapaka uende Namanyere ni mbali, mtu unakuwa na shida lakini hapa baadhi ya vifaa hakuna na kama alivyosema mkuu hapa kama vifaa hivyo vitapatikana maana yake vitatusaidia na hata wengine waliopo vijiji vinavyozunguka hapa, kituo hichi kitawasaidia.”

 Nae binti aliyeshiriki katika songamebele hiyo Deliza Mngumenya ametoa shukurani zake kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za upanuzi wa kituo hicho na kusogeza huduma bora karibu na wananchi ambapo ana uhakika kituo hicho kitakapokamilika wataweza kupata vipimo vyenye ufanisi.

Upanuzi wa kituo hicho utahusisha majengo manne ikiwemo jengo la Wazazi au mama na mtoto, Chumba cha Upasuaji, Maabara pamoja na Mochwari pamoja na vifaa vyake vitakayogharimu jumla ya shilingi milioni 700, kati ya hizo shilingi milioni 300 zitatumika kununulia vifaa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na kinamama walioshiriki kwenye Songambele ya Ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Kirando muda mfupi kabla ya kinamama hao kuruhusiwa na kuwaachia wanaume kuendelea na kazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili kutoka kushoto) akipokezana na wananchi mawe ya msingi yanayojengewa msingi wa kituo cha afya cha kirando siku ya uzinduzi wa songambele ya upanuzi wa ujenzi wa kituo hicho.
 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando. 

 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando.

SIMBA YAANZA KUJIFUA UWANJA WA VETERANI

$
0
0

Na Agness Francis Globu ya jamii. 

 VINARA wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba SC mara baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano na Gendarmarie sasa wanaanza mazoezi rasmi leo ili kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC. Mazoezi hayo yataanza leo jioni saa 10 jioni katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam. 

 Ikiwa ni mzunguko wa 2 round ya 19 katika michuano ya kuania Ubingwa wa Tanzania Bara ambapo mchezo uliopita Simba alitoka sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. 

 Hata hivyo Kikosi hicho kilipewa muda wa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gendarmerie ambapo kikosi cha Simba kiliibuka na Ushindi wa goli 1-0 na kujiandikishia tiketi ya kwenda hatua ya mbele zaidi katika Michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

UWEPO WA VIWANDA UTACHANGIA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA KILIMO-MHANDISI STELLA MANYANYA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la uhakika.

Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Amesema ili kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara."Tasisi za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema.

Mhandisi Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha wawekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani.

“Kuna changamoto kadhaa katika taasisi za fedha ambazo ni lazima zifanyiwe kazi kwa sababu wafanyabiashara wengi wanapokopa fedha kwa mfano kununua mashine wanatumia muda mrefu kutafuta ushauri. Niwaombe kuwasaidia kuwapa ushauri pale mnapowakopesha,"amesema Mhandisi Manyanya

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Geofrey Simbeye, ameishauri Serikali kuanzisha benki maalumu zitakazosadia kutoa mikopo ya kuanzisha na kuendeleza viwanda kama imekusudia kufikia uchumi wa kati unaotegemea sekta hiyo.

Pia Simbeye amesema licha ya ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuonesha Sh. trilioni 16.3 zilitolewa kwa sekta binafsi ni alisimia 9.8 tu ya fedha hizo iliyoelekezwa sekta ya uzalishaji huku kiasi kikubwa kikielekezwa kwenye biashara.

“Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Charles Kimei, amezungumza mambo mengi, lakini ninachosisitiza ni lazima tuwe na mfumo mpya, kwa sababu kama fedha zilizokopeshwa kwa private sekta ni Sh.trilioni 16.3, kwa mujubu wa taarifa ya BoT.

“Na ripoti ya Benki Kuu hiyo hiyo, inaonesha katika hizo ni asilimia 9.8 tu ndizo zimekwenda kwenye viwanda. Sasa tunajiuliza kwa ‘rate’ hiyo tutafika kwenye viwanda? Amehojia Simbeye.Amesema benki za kibiashara zimekuwa zikiangalia zaidi wapi zinapata faida ambapo mikopo inaweza kurudi haraka, ambapo mikopo mingi imekuwa ikielekezwa kwenye biashara ambako watu wengi hukopa ili kuagiza bidhaa za biashara na kujenga nyumba tofauti na uwekezaji wa viwanda ambao ni wa muda mrefu.

“Sasa tunajiuliza swali je, tutaendelea kutegemea benki hizi za kibiashara katika kuendeleza viwanda hapa Tanzania? Tunatakiwa kufikiria nje ya boksi nini tufanye.

“Kujenga uchumi wa viwanda nchini Tanzania ni sawa sawa na projecti ya kitaifa yaani ni project ya kujenga Taifa ndiyo itakayotulepeka kwenye uchumi wa viwanda na kama tunaichukua kama project ya kitaifa lazima tuje na mfumo tofauti wa kuiwezesha,” amesema Simbeye.

Amesema mchakato wa ujenzi wa viwanda unapaswa kuchukuliwa kama unavyochukuliwa mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge) ambapo Rais amesema anazo zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.5 za kujenga mradi huo kuanzia Dar es Salaam hadi makao makuu ya nchi Dodoma.

Amesema hivyo ni vema kuwa na chombo maalumu kitakachokuwa kikitoa mikopo ya maendeleo hasa sekta ya viwanda ili kuwezesha kufikia lengo la uchumi wa kati unaotegemea viwanda.“Hakuna kiwanda kinaanzishwa kikae miaka mitano, kiwanda ni project za milele na milele, wewe mwanzishaji utakufa lakini kile kiwanda kipo, kwa hivyo vinahitaji uwekezaji wa muda mrefu.

“Tatizo hapa wanaangalia faida zaidi lakini tukiwa na ‘industrial development bank’ kama TIB ni kama una-empower watu kuanzisha viwanda,” amefafanua Simbeye.Ameongeza sensa ya maendeleo ya viwanda ya mwaka 2013 iliyozinduliwa mwaka 2016 inaonesha Tanzania ina jumla ya viwanda 49,242 lakini viwanda vikubwa ni 1,322 tu. "Hivyo ni vema kujiuliza kwanini viwanda vidogo ndiyo vingi na kwanini visianzishwe viwanda vikubwa".

Amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa mitaji, hivyo ni vema kusaidia kuanzishwa viwanda vingi vikubwa vitakavyosaidia pia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vitakavyokuwa vinazalisha malighafi kwa za viwanda vikubwa na kutoa ajira nyingi kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki ya Tanzania, Dk. Charles Kimei, amesema licha ya taasisi za fedha kuwa na jukumu la kusaidia upatikanaji wa fedha kwa watu bado kuna changamoto nyingi nchini ikiwamo wafanyabiashara wengi wazawa kutoaminika katika taasisi za fedha hususani za kigeni.

Dk. kimei amesema kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wajasiriamali wadogo na wa kati taasisi za fedha nchini zinapaswa kuongeza ushirikiano na wajasiriamali hao badala ya kufikiria viwanda vikubwa tu.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) kuhusu wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei akichokoza mada wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Sekta Binafsi Nchini(TPSF),Geoffrey Simbeye, akichokoza mada wakati wa kongamano la kujadili umuhimu wa mabenki na sekta binafsi katika maenedeleo ya Viwanda.
Naibu Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dr.Thomas Ndaluka akitoa neno kwenye Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania. 
Mhadhiri wa Chuo Cha MNMA, Binto akitoa mada ya Ujasiliamali ktika Uwekezaji wa Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Mkurugenzi wa Uchumi ,Utafiti na Sera , Benki kuu ya Tanzania Johson Nyela akichangia jambo wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akiwa ameketi pamoja na Washiriki wengine wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof Shadrack Mwakalila wa kwanza kulia akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya (Katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei 
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.

KAIMU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MBUNGE KUTOKA UTURUKI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mhe. Zehra Taskesenlioglu, Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Bunge la Uturuki wanaounda Kundi la Wabunge Marafiki na Wabunge wa Bunge la Tanzania alipofika Wizarani tarehe 23 Februari, 2018. Katika mazungumzo yao walizungumzia umuhimu wa kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Uturuki katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu. 
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kulia) akiwa pamoja na Bw. Aytak Dincer, Mwekezaji na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Tanzania na Uturuki wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Mhe. Zehra (hawapo pichani) 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) akiwa na Bw. Hassan Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo 
Kikao kikiendelea

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI ULIOMALIZIKA LEO JIJINI KAMPALA NCHINI UGANDA

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo katika siku ya mwisho ya Kikao chao kilichofanyika Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatoka katika ukumbi wa mkutano pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC vilivyofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa EAC katika siku ya mwisho jijini Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

ZARI ALIPOHOJIWA NA BBC SWAHILI JIJINI LONDON

Article 2

$
0
0

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOSHI

MADAKTARI na watoa huduma kutoka Kanda ya Kaskazini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano (5), ya kufanya tathmini yamfanyaakzi aliyepataulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi amesema wamepata nyezo muhimu itakayowasaidia kutekeleza majukumu hayo kwa usahihi na haraka.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika mjini Moshi, Februari 23, 2018, Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre alisema, wengi wao walikuwa hawafahamu nini cha kufanya wanapomuhudumia mfanyakazi aliyepata madhara yatokanayo na kazi, ili kumfanyia tathmini kwa ajili ya kulipwa Fidia stahiki bali walitumia uwezo wao wa kawaida wa kidaktari.

“Mafunzo yametuwezesha ni jinsi gani daktari utafanya tathmini na ukadiriaji wa matatizo mbalimbali yatokanayo na kazi mbalimbali aliyopata mfanyakazi, kuelewa mgonjwa wa aina fulani anapofika kupatiwa huduma utamuhudumia kwa kutumia vigezo vilivyopo kisheria, lakini pia usahihi wa kujaza takwimu zake katika kumbukumbu za kitabibu.” Alisema.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Moshi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja

Aliupongeza Mfuko kwa kuandaa mafunzo hayo kani yatawezesha kuwepo na madaktari ambao wamepatiwa mafunzo maalum ya kufanya tathmini ili kutoa fidia inayostahili.

“Tulikotoka jamani hatukuwa na utaratibu maalum unaoeleweka kwamba ukiumia kazini unaenda kumuona nani na huyo mtu unaeenda kumuona hujui ni lini atakufidia kulingana na ulemavu ulioupata.” Alisema Bw. Masanja.

Lakini pia, aliwaasa madaktari na watoa huduma hao, kutumia elimu waliyopata ili kutoa tathmini sahihi na hatimaye mgonjwa aliyeumia aweze kupata haki stahiki na kwa haraka.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar alisema, jumla ya washiriki 66 kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga walishiriki mafunzo hayo, chini ya wataalamu wa WCF na wawezeshaji waliobobea kwenye maswala ya usalama mahala pa kazi kutoka taasisi ya Mifupa MOI.

Alisema mafunzo haya ni mundelezo wa mafunzo kama haya ambayo yamekuwa yakifanyika kwa awamu kwenye kanda mbalimbali nchini, ili kujenga mtandao wa wataalamu wa kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi kwa mujibu wa mkataba.

“ Idadi ya madaktari ambao wamepatiwa mafunzo haya nchi nzima hadi sasa ni 655 na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi ili wafanyakazi waweze kupata huduma kwa ukaribu lakini kwa haraka na usahihi.” Alifafanua Dkt. Abdulsalaam.

Baadhi ya Madaktari na watoa huduma za afya wakionyesha stika, watakazobandika kwenye milango ya ofisi zao ili kumrahisishia mfanyakazi anayehitaji kufanyiwa huduma ya tathmini. Stika hizo zimetolewa na WCF kwa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini yamfanyaakzi aliyepataulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yaliyomalizika Februari 23, 2018 mjini Moshi.
Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza.
Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi wa WCF, (mbele), akiwa na washiriki
 
Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre, akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akionyesha stika hizo za utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akimkabidhi stika ya utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini, DktJosephine Rogate, kutoka Hospitali ya Mawenzi.
 Mmoja wa washiriki Dkt. Theresia Temu
 Mgeni rasmi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bw. Sebastian Masanja, akimkabidhi cheti Dkt. Theresia Temu, cha ushiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini yamfanyaakzi aliyepataulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi,  yaliyowaleta pamoja madaktari 66 kutoka mikoa ya Kaskazini, 


 Baadhi ya washiriki

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)


Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
 

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)

 Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar.
  Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa kuwapa uzoefu wake wa kazi katika sekta ya afya na tiba washiriki hao.
 Profesa Shao, (kulia), akiagana na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
 Profesa Shao, (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi.Laura Kunenge, katikati), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi 
 Wawezeshaji (watoa mada), kutoka kushoto, Dkt. Hussein, Dkt. Mshashu na Dkt. Mhina.
Afusa mwandamizi kutoka WCF, Dkt. Pascal Magesa,  akigawa fomu za tathmini ya mafunzo
 Picha ya kwanza ya pamoja 
Picha ya pili ya pamoja


MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YAWANUFAISHE WATANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini  alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Rukwa


Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.


Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K


Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.


Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa) ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.


"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa


Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.


Aidha, aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao katika migodi mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao jambo litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.


Sambamba na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi mbalimbali ambao wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi kuwa muda wa starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.


Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.

RC TELACK AHAMASISHA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack amewataka wananchi mkoani Shinyanga kutoa taarifa sahihi kwa watafiti wanaofanya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi mkoani humo. 

Telack ametoa rai hiyo leo Ijumaa Februari 23,2018 katika mkutano na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga akizungumzia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018. Utafiti huo unaosimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaoendelea nchini katika kata 796 utazifikia kaya 9,552 nchini ambapo kaya 408 zitafikiwa katika kata 34 za mkoa wa Shinyanga.

Telack alisema njia pekee ya kufuatilia utekelezaji wa program za maendeleo ni kufanya tafiti mbalimbali kama huu unaoendelea ambao unalenga kutoa takwimu za hali ya umaskini na takwimu nyingine ili kuisaidia serikali na wadau kutathmini hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo ya kitaifa. “Suala la ukusanyaji wa takwimu rasmi za serikali ni shirikishi na ni wajibu wa kila mwananchi kutoa taarifa sahihi,natoa wito kwa viongozi kuanzia ngazi ya mitaa,vitongoji,vijiji,kata,wilaya na mkoa kutoa ushirikiano wa karibu kwa watafiti watakaozifikia kaya 408 zilichaguliwa katika mkoa wetu”,alisema Telack.

“Utafiti huu wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa mwaka 2017/2018 unahitaji sana ushirikiano kutoka kwa wananchi wote hasa katika kaya zilizochaguliwa kitaalamu kuwakilisha sampuli za kaya zilizopo mkoani Shinyanga”,aliongeza. Alibainisha kuwa kila kaya iliyobahatika kuchaguliwa itahojiwa kwa siku 14 mfululizo na mdadisi atakutana na mkuu wa kaya ambaye hatatakiwa kubadilishwa ili kupata takwimu sahihi kwa ajili kupanga maendeleo ya nchi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema utafiti huo utasaidia kuweka msingi katika kutambua viashiria vya msingi vya kiuchumi,ajira na ustawi wa jamii ambavyo vitatakiwa kufuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya jumla ya mwenendo wa matumizi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei. Telack alizitaja kata 34 za mkoa wa Shinyanga zitakazofanyiwa utafiti kuwa ni Ngokolo,Mwawaza,Ndala,Ndembezi,Songwa,Mwadui Lohumbo,Kishapu,Mwakipoya,Lagana,Talaga,Didia,Mwakitolyo,Iselamagazi,Mwamala,Nyida na Lyabusalu. Kata zingine zitakazofikiwa ni Lyamidati,Lunguya,Chela,Bulige,Jana,Isaka,Chambo,Igunda,Sabasabini,Bulungwa,Ushetu,Ubagwe,Mondo,Nyahanga,Zongomera,Nyihogo,Majengo na Kilago.

Kwa upande wake Meneja wa Takwimu (NBS) wa mkoa wa Shinyanga, Evarist Tairo alisema huo ni utafiti wa saba tangu nchi ipate Uhuru na utasaidia kwa kiasi kikubwa kupata takwimu halisi za mapato na matumizi ya kaya binafsi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akizungumzia kuhusu Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018 wakati wa mkutano wa waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 23,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi yake - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akielezea umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi unaoendelea mkoani Shinyanga. Kushoto niMeneja wa Takwimu (NBS) wa mkoa wa Shinyanga, Evarist Tairo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Dk. Rashid Mfaume ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Waandishi wa habari wakichukua matukio: Telack alisemaUtafiti huo unatarajia kukusanya taarifa kutoka katika kaya binafsi zinazohusu kaya na wanakaya,uzazi na unyonyeshaji,elimu,afya,uraia,uhamiaji,ulemavu,bima,hali ya ajira,biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini: Taarifa zingine zitazokusanywa katika utafiri huo ni matumizi ya nishati,huduma za maji safi na maji taka,utalii wa ndani,uwekezaji wa kaya,matumizi ya kaya ya huduma za kifedha,upatikanaji wa usalama wa chakula,matumizi,kilimo na mifugo pamoja na taarifa za umiliki wa mali kijinsia.
Meneja wa Takwimu (NBS) wa mkoa wa Shinyanga, Evarist Tairo akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwasisitiza wananchi mkoani Shinyanga kuwapa ushirikiano wadadisi/watafiti watakazifikia kaya 408 zilizochaguliwa.
Meneja wa Takwimu (NBS) wa mkoa wa Shinyanga, Evarist Tairo akielezea umuhimu wa kufanya tafiti katika nchi.

Waandishi wa habari Sam Bahari (Mtanzania/Rai) na Eunice Kanumba (Kahama Fm) wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mwandishi wa habari wa habari kutoka Radio Faraja ya Mjini Shinyanga,Moshi Ndugulile akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mwandishi wa habari wa Channel Ten,John Mponeja akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Afisa Masoko wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Andrew Punjila ambaye pia ni Mhamasishaji wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa mwaka 2017/2018 akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emmanuel Ghulla akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Dk. Rashid Mfaume ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa mkutano huo.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, waandishi wa habari ,maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, waandishi wa habari ,maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu. icha zote na Kadama Malunde/Frank Mshana

DK MWANJELWA AZIASA TAASISI KUIGA MFANO WA IOP, WAANZISHA SHAMBA DARASA KWA 'SINGLE MOTHERS' MKOANI IRINGA

$
0
0
 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea machache na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Pamoja naye (kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga viongozi wa wasaidizi wake mkoani humo. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogs)

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na mmoja wa wageni alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia) alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga.

 NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiagana na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Amina Masenza baada ya kufanya naye mazungumzo ofisini wakati wa kuanza kwa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Katikati ni mwenyeji wao, Mhe Amina Masenza Mkuu wa Mkoa.


NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na Osmund Ueland Mshauri wa Shamba sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kushoto) Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP), Berit Skaare.



NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya ujenzi wa makazi maalumu ya kujifunzia kutoka kwa Osmund Ueland Mshauri wa Shamba (kulia) kwenye eneo la shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga na Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP) Berit Skaare. 

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kulia) ni Mshauri wa Shamba hilo, Osmund Ueland, Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (nyuma kulia), Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP), Berit Skaare na viongozi wengine wa serikali wa mkoa huo.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiwahusia vijana yatima Ajolin Mgeveke (wa pili kulia) na Atilio Mbungu ambao ni wanufaika wa Ilula Orphan Program (IOP) alipofanya ukaguzi wa shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani iriga jana. Kulia ni Mwasisi wa IOP, Berit Skaare.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Shamba hilo, Osmund Ueland wakati alipofanya zaira kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiwabadilishana mawazo na wakina mama wanajitegemea 'Single mothers' baada ya kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiondoka baada ya kuzungumza na wakina mama wanaojitegemea amabao watakaonufaika na shamba darasa kuendesha maisha yao. Pamoja naye (toka kulia) ni Mkurungenzi Mtendaji wa IOP, Edson Msigwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga, Mshauri wa Shamba hilo, Osmund Ueland, Mwasisi wa IOP, Berit Skaare na Mmoja wa watakaonufaika wa IOP,  Atilio Mbungu. 

SIMON GROUP YACHANGIA MILIONI 25 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akipokea hundi ya shilingi milioni 25 iliyotolewa na Kampuni ya SIMON GROUP kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kutoka kwa Ndg.Leonald Kitwala ambaye aliyekabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampun hiyo Ndg.Robert Kisena.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo akitoa shukrani kwa Kampuni ya SIMON GROUP kupitia kwa Ndg.Leonald Kitwala aliyekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo picha) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg.Robert Kisena, kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu.


Na Stella Kalinga, Simiyu

Kampuni ya Simon Group imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika mkoa wa Simiyu

Akikabidhi hundi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Simon Group, Ndg. Leonard Kitwala amesema Kampuni hiyo imetoa fedha hizo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu na kwa kuwa Simiyu ni mahali alipozaliwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Simon Kisena ameona ni vema asaidie maendeleo ya elimu nyumbani kwao.

Aidha, Kitwala amesema kama kampuni wameamua kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ya Elimu Simiyu kwa kuwa wamependezwa na juhudi za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.

Akipokea hundi ya shilingi milioni 25 kwa niaba ya Viongozi na wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amesema anaishukuru Kampuni ya Saimon Group ambayo inaendesha mradi wa Usafrishaji wa Mabasi Dar es Salaam(UDA) kwa kuamua kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani humo.

“Nawashukuru sana SAIMON GROUP kwa kuamua kusaidia ujenzi wa miundombinu ya elimu Simiyu, shilingi milioni 25 ni fedha nyingi sana kwenye kufanikisha ujenzi wa mundombinu ya elimu hasa kwa mkoa kama wa kwetu ambao shughuli nyingi za ujenzi tunatumia “Force Account” , tunatumia nguvu za wananchi na Serikali ina nafasi yake katika ujenzi wa miradi hiyo” alisema

“ Zaidi sana namshukuru Mkurugenzi wa SIMON GROUP ndugu Robert Kisena ambaye ni mzaliwa wa Mkoa huu kwa kuona arudishe sehemu ya faida ya biashara zake nyumbani, kwa niaba ya viongozi wenzangu ninamkikishia kwamba mchango huu utaenda kwenye matokeo yanayoonekana, hata wakati wa uzinduzi wa madarasa yatakayojengwa tutaipa nafasi Kampuni ya SIMON GROUP kuja kuona alama waliyoweka katika mkoa wetu” alisisitiza Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo amesema mchango huo wa SIMON GROUP umekuja katika muda muafaka ambao mkoa huo una uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Kisena na kuahidi pia kuwa fedha hizo zitafanya kazi iliyokusudiwa.

UBUNIFU WA KIJANA OMARY WAMVUTIA DK.KAMALA, AAHIDI KUSAIDIA VIJANA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NKENGE

$
0
0
Na Ripota Wetu, Misenyi

MBUNGE wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dk. Kamala amempongeza kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.

Kijana Omary wakati Rais Dk.John Magufuli akiwa kwenye ziara katika mkoa huo Novemba mwaka jana alitoa kilio chake kwa Rais kuwa kuna moja ya maofisa mifugo alifika kwenye shamba lake na kufyeka mazao yake.

Hata hivyo kijana huyo bado anaendelea na kilimo hicho baada ya Rais kutaka asisumbuliwe bali aachwe.

Hivyo Dk.Kamala ameamua kwenda kwenye shamba la kijana Omary kuona shughuli anazofanya, ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa jitihada zake kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda.

Dk.Kamala ameona haja ya kutembelea shamba hilo na alipofika akavutiwa na ubunifu wa kijana huyo na hivyo ameshauri ni vema vijana wakaanzisha kikundi ambacho kitajikita kwenye aina hiyo ya kilimo.Amesema yeye ameahidi kutoa vitendea kazi ikiwamo mashine za umwagiliaji.
 Sehemu ya shamba la Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akikagua shamba la kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akiungumza jambo na kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.

RAIS MAGUFULI AONDOKA UGANDA MARA BAADA YA KUHUDHURIA VIKAO VYA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa ndege wa Entebe mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao ulimalizika hapo jana jijini Kampala nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU

MPINA AZIPIGA FAINI MELI 19 ZILIZOTOROKA BILA KUKAGULIWA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlakaya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi Tanzania Bara Dkt. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA) wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina  (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. 
Kiongozi wa Kampuni ya Linghang kutoka china inayoshughulika na uendelezaji wa Utalii wa Zanzibar nchini china Tom Zhang (katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)


Na John Mapepele

Serikali imezipiga faini ya bilioni kumi na tisa meli 19 ikiwa ni shilingi bilioni moja kwa kila meli na kuamuliwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili kwa kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara ama Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Shillingi Billioni moja (Tshs. 1,000,000,000) kila moja zinatakiwa kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).

Aidha Mpina amesema meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.

Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba kuiamru Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizi kuwajulisha kuhusiana na maamuzi haya pia kuwajulisha Kamisheni ya Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia sheria kwa mujibu wa Sheria husika. 

Aidha imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/ andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States (Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua. Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.

Wakati huo huo Waziri Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha 18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe 25/01/2018-27/01/2018. 

Pia meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine ambao idadi yao ilikuwa mabaharia 10.Aidha meli hii pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.

Kutokana na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Shillingi Billion moja (Tshs. 1,000,000,000) ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG 1.

Mbali na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI XIANG 2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI XIANG 9 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.

Meli nyingine ni TAI XIANG 10 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI XIANG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/463, TAI HONG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN SHIJI 81 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN SHIJI 72 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/473.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba amewataka wawekezaji kwenye bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia masharti na taratibu za kisheria ili nchi na wawekezaji waweze kunufaika.“Taratibu zipo wazi ni muhimu kuzinangatia sheria namna nyingine tutaendelea kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye” Alisisitiza Dkt. Budeba

Amesema hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzipiga faini meli hizo ni somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa yoyote atakayebainika kutenda makosa ya uvuvi haramu katika bahari na maziwani.

Aidha amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara na mtu yoyote ambaye atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi mbalimbali duniani.Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.

Aliwashukuru wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa na wadau mbalimbali nchini.

WAZIRI KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA, ATUMA SALAMU KWA MUWEKEZAJI ANAECHOCHEA MGOGORO KATIKA HIFADHI HIYO

$
0
0


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa TANAPA alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ausha jana na kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia). 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya eneo lenye mgogoro ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha alipotembelea hifadhi hiyo jana na kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia). 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Martin Loibooki  alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana na kukagua shughuli mbalimbali  za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
Picha ya pamoja Waziri Kigwangalla na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA.
Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki kuhusu Kreta ya Hifadhi ya Ziwa Manyara muda mfupi kabla ya kuhitimisha ziara yake katika hifadhi hiyo jana jioni. (Picha na Hamza Temba-WMU)
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images