Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1523 | 1524 | (Page 1525) | 1526 | 1527 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Na Zuena Msuya, Geita.

  Serikali  inadhamiria kujenga vituo maalum vya uchenjuaji na kuvizungushia ukuta katika kila eneo lenye wachimbaji wadogo ili kudhibiti wizi na uuzwaji holela wa madini ya dhahabu katika maeneo hayo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila alisema hayo Februari 20, 2017 mkoani Geita ,wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Mfano na Mafunzo kwa wachimbaji wadogo kinachojengwa katika eneo la Rwamgasa mkoani humo.

  Prof. Msanjila alisema kuwa vituo hivyo vitakapojengwa vitarahisisha ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia wachimbaji kuuza dhahabu yao kwa bei halisi na kudhibiti walanguzi katika maeneo ya wachimbaji.
  Vilevile alifafanua kuwa utaratibu unaotumiwa na wachimbaji wadogo hivi sasa kuchenjua dhahabu, umekuwa ukipoteza dhahabu nyingi ikilinganishwa na utumiaji wa njia za kisasa: Pia hakuna kumbukumbu sahihi na taarifa zilizo wazi zinazoonyesha soko halisi la uuzaji wa dhahabu inayochimbwa na wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali nchini.

  "Tunawachimbaji wadogo wa dhahabu wengi sana nchini hii, na wanapochimba wanapata dhahabu lakini ukiwauliza wanauza wapi dhahabu yao hakuna majibu sahihi, pia ukiuliza bei kila mmoja anamajibu yake, na kwa mtindo huu wanaikosesha serikali mapato, hali hii haikubaliki lazima idhibitiwe" alisisitiza Msanjila.

  Profesa Msanjila alisema kuwa lengo la serikali ni kuwaewezesha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo ili wanufaike na rasilimali hiyo ya madini hivyo ni wajibu wao pia kuilinda sekta hiyo kwa kuzingatia kanuni na sheria za madini ili kuleta maendeleo yenye tija.

  Akizungumzia Kituo cha Mfano na Mafunzo kwa wachimbaji wadogo kilichopo Rwamgasa, Msanjila alisema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho hadi ulipofikia sasa na kuwaeleza wasimamizi wa ujenzi wa kituo hicho kuwa wahakikishe kinajengwa katika ubora unaotakiwa ili kukidhi mahitaji husika.

  Pia alimuagiza mkandarasi anayejenga kituo hicho kuwashirikisha wachimbaji wadogo kuanzia hatua za awali ili waweze kupata elimu ya kutosha na pia watoe mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosomea elimu hiyo kwa kuchukua wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.

  Aidha Msanjila, aliwataka viongozi wa serikali ya kijiji pamoja na wale wa wachimbaji wadogo wa mkoa wa geita( GEREMA) kuwasisitiza wachimbaji wao kufuata kanuni na sheria za uchimbaji madini ili kundoa adha ya kubughudhiwa na serikali.  

  Eneo la ukubwa wa hekta 19 litatumika kutekeleza mradi wa  Kituo cha Mfano na mafunzo katika eneo la Rwamgasa Mkoani Geita ambapo kwa sasa ni hekta tano tu ambazo zimetumika katika ujenzi wa kituo hicho, pia vituo vingene saba kama hivyo vitajengwa katika Mikoa tofauti hapa nchini.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila, akishuka chini ya mgodi uliojengwa katika Kituo cha Mfano na Mafunzo ili kujiridhisha na ujenzi huo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila( katikati) akiwa chini ya mgodi uliojengwa katika kituo cha Mfano na Mafunzo kilichopo Rwamgasa, mkoani Geita.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila, akipata maelezo namna ya mtambo wa uchenjuaji utakavyofanya kazi katika Kituo cha Mfano na Mafunzo, kutoka kwa Mkandarasi anayejenga Kituo cha Mfano na Mafunzo, Mhandisi Rogers.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila,( tatu kulia) na maafisa kutoka wizara ya madini na serikali ya kijiji waakiwa juu ya sehemu ya mtambo wa uchenjuaji katika Kituo cha Mfano na Mafunzo ,wakifanya ukaguzi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (tatu kushoto) na alipotembelea mgodi wa Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo mkoani Geita (GEREMA) Christopher Kadeo( tatu kulia).

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Mkutano huo Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa nne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukipigwa katika ukumbi wa mkutano uliopo katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akifungua Mkutano huo maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki Kampala nchini Uganda.
  Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya a Afrika Mashariki wakifatilia hotuba mbalimbali katika Mkutano huo maalum.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Sekta ya Miundombinu na Afya.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir mara baada ya Mkutano Maalum wa 19 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Kampala nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kampala Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda.

  PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0
  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za Kiroho (Injili) Rose Muhando anatarajia kuizindua albamu yake ndani ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .


  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo, amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na wanatarajia kuanzia katika jiji La Mwanza ndani ya Uwanja wa CCM-Kiruma Aprili 1, 2018 na kuelekea uwanja wa Halmashauri mjini Simiyu. "Kwa kipindi kirefu Mwimbaji Rose Muhando amekuwa kimya kwa muda mrefu ila kwasasa namtangaza Kinara Rose Muhando ndiyo atakayeongoza jahazi la Tamasha la Pasaka kwa Mwaka 2018 hivyo wananchi mjitokeze kwa Wingi," amesema Msama. 

  Aliongeza kuwa mbali na uzinduzi huo, tukio lingine kubwa litakalofanyika ni kuombea nchi amani,hukua kauli mbiu itakuwa "Upendo na Amani "Nipende kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha la Pasaka ambalo litakuwa la namna yake na waje wajionee vipaji lukuki kutoka ndani ya Tanzania na nje. 

  Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya  Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .
   Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya  Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .

  0 0

  Tanzania, Rwanda Zang’ara EAC Vita ya Rushwa .

  MISIMAMO thabiti ya Rais John Pombe Magufuli katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa imezidi kuleta mafanikio ambapo ripoti mpya katika mapambano dhidi ya rushwa imeonesha Rwanda na Tanzania kuongoza katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2017. 

  Kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Rushwa (Corruption Perception Index) iliyotolewa jana Februari 21, 2018 na Taasisi ya Transparency International, juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano Tanzania chini ya Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa zimezidi kuzaa matunda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 

  Taarifa hiyo iliyokusanya takwimu za mwaka mzima wa 2017 zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizopanda kwa kiasi kikubwa katika kupambana na rushwa huku nyingi nyingi zikishuka au kubaki pale pale. 

  Wakati mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ya 116 duniani, katika ripoti hiyo mpya Tanzania imepanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 103 huku ikizizidi kwa mbali nchi kadhaa kubwa duniani katika utafiti huo uliohusisha mataifa 180. 

  Aidha, kwa eneo la Afrika Mashariki, Tanzania imekuwa nchini ya pili baada ya Rwanda iliyoongoza kwa kupunguza rushwa ambapo katika alama za mtazamo wa rushwa Tanzania imepata 36, alama ambazo ni nyingi kuwahi kufikiwa na nchi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. 

  Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania, kufikia nafasi hiyo ya juu, imeonesha kufanikiwa katika kufanyiakazi mianya mingi ya rushwa, kwa mujibu wa vigezo vya rushwa kupungua katika taasisi mbalimbali za Serikali na kwa mujibu pia wa mtazamo wa wafanyabiashara na wawekezaji. 

  Ripoti hii inakuja ikiwa ni hivi karibuni tu Tanzania chini ya juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano ilitajwa na ripoti ya jarida la The Economist kuongoza katika EAC kwa utawala bora na demokrasia (Democracy Index). 

  Akizungumzia ripoti hii jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema ripoti hiyo ni sehemu tu ya kuonesha kuwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini inafanikiwa. 

  “Unaweza kuyapima mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna nyingi katika kupambana na rushwa, ripoti hii kuonesha tumepanda kwa kuzipita nchi 13 katika mwaka mmoja ni moja tu ya ishara kuwa vita yetu hii ya haki ni ya haki kweli na inapaswa kuendelea,” alisema. 

  Dkt. Abbasi aliongeza: “Kama nchi tutaendelea kutekeleza. Tutaendelea kuhakikisha kile kidogo wanachokichangia wananchi kinatumika kwa maendeleo ya Taifa kama mnavyoona namna tunavyotekeleza miradi mikubwa na ya kihistoria karibu katika kila sekta.” 

  Hivi karibuni Ripoti nyingine ya Taasisi ya Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliitaja Tanzania kuwa ya pili Afrika na ya kwanza katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika nyanja za uchumi jumuishi. 

  Mafanikio yote haya yanakuja wakati ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais aliyeahidi na anayetekeleza mageuzi, Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa inaendelea kwa kasi kusimamia maendeleo ya Taifa.   0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa FNB Tanzania, Warren Adams akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kwenye mkutano wa kujadili uchumi unaofanyika kila mwaka nchini. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.  Mwendeshaji wa mkutano na Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi Barani Afrika kutoka Rand Merchant Bank ya Afrika Kusini, Neville Mandimika akizungumza na wadau kutoka sekta mbalimbali katika mkutano ulioendeshwa na First National Bank na kujadili uchumi unaofanyika kila mwaka nchini.
  Wadau kutoka sekta mbali mbali wakihudhuria katika mkutano wa kujadili uchumi unaofanyika kila mwaka nchini ulioendeshwa na First National Bank Tanzania jijini Dar es salaam leo.

  0 0
 • 02/22/18--08:00: TAARIFA KUTOKA BENKI KUU


 • 0 0  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Badwel na viongozi wengine wa wilaya ya Bahi.
    Daraja la Chipanga linaloendelea kujengwa
  Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Chipanga.


  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Medes Company Limited na Millenium Master Builders (T) Limited anayejenga daraja la Chipanga wilayani Bahi, kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo mwezi Julai, mwaka huu bila visingizio vyovyote.

  Akikagua ujenzi wa daraja hilo, Jafo amesema awali kazi ya ujenzi wa Daraja hilo ilitarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu lakini kutokana na Mvua zilizokuwa zikinyesha amewaelekeza kukamilisha ifikapo Julai mwaka huu.

  Jafo amewaagiza wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kukaa na mkandarasi kukubaliana tarehe ya mwisho ya kukamilika kazi hiyo lakini kinachotakiwa ifikapo Julai mwaka huu daraja hilo liwe limekamilika.

  Amebainisha kuwa daraja hilo ni kiunganishi cha kata ya Chipanga na Makao makuu ya wilaya ya Bahi na ujenzi wake unagharimu kiasi cha Sh. bilioni 2.11.

  Akizungumza katika mkutano wa hadharana wananchi wa Chipanga, Waziri Jafo amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kupitisha ng'ombe na majembe ya ng’ombe kwenye barabarani zinazojengwa kwa kuwa wanasababisha uharibifu wa barabara.

  Amesema serikali haiwezi kuvumilia uharibifu wowote wa miundombinu ambayo inagharimu gharama kubwa.

  0 0

  Mhe. Mchembe akishiriki ugawaji chakula kwa wanafunzi Shule ya Msingi Kibedya mara baada ya kutembelea baadhi ya shule Kata ya Kibedya na Chakwale.  Wanafunzi wakipata chakula cha mchana. 

   
  Mkuu wa Wilaya ya Gairo akishiriki uchimbaji wa mtaro wa kutandaza mabomba. Waliopo nyuma yake ni Mhe. Maneno Diwani wa Chakwale na Mtendaji Kata ya Chakwale 
  Mhe. Mchembe akiongea na wananchi kuhamasisha umaliziaji wa madarasa 5 shule shikizi ya Iringa. 
  Diwani wa Kata ya Mangapi Mhe. Maneno akiongea na wananchi. Waalimu wa mazoezi wote wa shule shikizi wanaishi nyumbani kwa Diwani kama familia.

  0 0

  Kufuatia kuwashwa kwa kituo hicho, Wananchi wa Mbagala ,Kigamboni ,Tandika na Mkuranga na Wenye Viwanda watapata Umeme wenye Nguvu na wenye uhakika ambao hautokatika.

  Naibu waziri wa Nishati, amewapongeza wananchi wakazi wa maeneo hayo Kwa kuwa na subira huku akiwapa pole kwa kero ya umeme ya muda Mrefu.
  Aidha, alisema amewashukuru Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Kigamboni Dk Ndungulile na Mhe Mangungu na Wakuu wa Wilaya Kwa kufuatilia Jitahada za kuondosha Kero hiyo ya Upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika Maeneo hayo.

  Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa kutekeleza mradi huo ili wananchi waondokane na kero hiyo.

  Alisema kufuatia ushirikiano alionao yeye pamoja na Waziri wa nishati Dk Medard Kalemani wameweza kufanikisha Miradi mbalimbali ya Nishati ya umeme hapa nchini hali inayopelekea wananchi kujenga imani na serikali yao ya awamu ya tano katika utekelezaji wa miradi.

  Aliongeza kwa kusema kuwa, kufuatia ushirikiano na Waziri wa nishati, imepelekea kuwa karibu na Wataalam wote wa TANESCO pamoja na Wakandarasi na hatimae kufanikisha mradi huo na miradi mingine iliyo chini ya wizara hiyo.
  @

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, (hawapo pichani) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. 
  Kiongozi wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bi. Beth Arthy akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani wakati wa kikao leo jijini Dar es Salaam.
  Kiongozi wa ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bw. Nicholas Leader akiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.  DfID MDAU WA MAENDELO WA SERIKALI YA TANZANIA

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameishukuru Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kwa kuwa moja kati ya wadau wa maendeleo nchini.

  Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Ninapenda kuishukuru DfID pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

  Mhe. Mkuchika amesema DfID kama moja ya washirika wa maendeleo wamechangia kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali za kupambana na rushwa, na moja ya matokeo yake ni kuongeza uwajibikaji katika utoaji huduma kwa wananchi na kuondosha rushwa kupungua.

  Mhe. Mkuchika ameuhakikishia ujumbe wa DfID kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari muda wowote kushirikiana na DfID katika kuleta maendeleo.Kiongozi wa DfID nchini, Bi. Beth Arthy ameahidi kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo nchini.

  0 0

  Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Pix 1
  Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiangalia bidhaa mbalimbali za uchongaji na ushonaji toka kwa wajasiriamali wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
  Pix 2
  Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (katikati) akiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika Ahmad Ahmad na kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Wallace Karia.
  Pix 3
  Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akivalishwa urembo wa mkononi wenye rangi za bendera ya Taifa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Pix 4
  Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Leodger Tenga mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Pix 5
  Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza (kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino, zawadi mbalimbali toka bodi hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirikisho hilo mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
  Picha na Idara ya Habari – MAELEZO

  0 0


  MENEJA Mahusiano na Maendeleo ya Biashara .wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (wa pili kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mlezi wa ‘New Hope for Girls Organization’ Consoler Wilbort kwenye makazi ya watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa na familia hiyo Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Anayeshuhudia (nyuma kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij. (Picha na Robert Okanda Blogs).
  MENEJA Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto, Loveness Julius (kulia) na Rechol Lazaro wanaolelewa kwenye makazi ya ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa na familia hiyo. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij.
  Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni Kampuni ya BAM International, Wim Mulderij akigawa dawa za mswaki kwa sehemu ya watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Noreen Mazalla.
  MLEZI wa ‘New Hope for Girls Organization’ Consoler Wilbort (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla wakati wa hafla hiyo, Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. 
  MENEJA Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Pamoja nao (nyuma kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino,jijini Dae es Salaam.
  SERIKALI ya Tanzania inalipongeza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na shirikisho hilo katika mapambano dhidi ya rushwa.

  Kauli hiyo imetolewa leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kikao chake na Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino kilichofanyika jijini Dae es Salaam.

  “Serikali tunaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo pamoja na matumizi mabaya ya fedha na ya madaraka yanayofanywa na FIFA”.Waziri Mkuu amesema wanaunga mkono mapambano hayo ili Taifa liweze kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye maono ya mbali katika kuendeleza mchezo huo.

  Amesema FIFA ambayo ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo , hivyo Tanzania inaiunga mkono kwa kuhakikisha sekta ya michezo inatumia vizuri fedha zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo.Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inasimamia matumizi sahihi ya madaraka katika sekta ya michezo nchini ili kuleta maendeleo kwenye mpira wa miguu.

  Serikali inaipongeza FIFA kwa jitihada za dhati za kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kuwa mipango mbalimbali ya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana wadogo wa kike na wa kiume nchini.“Tunatambua msukumo wa FIFA wa kuendelea mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na kuboresha viwanja vya michezo pamoja na maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta hiyo.

  Pia ameishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani jijini Dar es Salaam na kwamba Serikali itayasimamia vizuri na inajiandaa kwa kushinda.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa FIFA Bw. Infantino kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendesha mkutano mkubwa wa viongozi wa mpira wa miguu duniani Tanzania. Mkutano huo ulihusisha Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 21.

  Pia alimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Bw. Ahmad Ahmad kwa jitihada zake za anazozifanya katika kuendeleza mpira barani Afrika na kwamba Serikali ya Tanzania inamuunga mkono.

  Rais wa FIFA Bw. Infantino ambaye ameahidi kuisaidia Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo aliwasili nchini leo alfajiri akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Bw. Ahmad Ahmad kwa ajili ya mkutano wa FIFA uliofanyika nchini Tanzania February 22, 2018.

  Bw. Infantino amewasili kwa mara ya kwanza Tanzania toka awe Rais wa FIFA na alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dtk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leodger Tenga na Rais wa TFF Bw. Wallace Karia.

  0 0

  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bungoni Ilala, Barua Mwakilanga akikabidhi bati 150 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, leo jijini Dar es Salaam. Ametoa bati hizo kuitikia mwito ulitoalewa hizi karibuni na Waziri Mkuu majaliwa Kassim Majaliwa kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchangisha fedha kwa wadau ili kupatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati Ilala.
  "Asante sana" Sophia Mjema akimshukuru Barua wakati akipokea bati hizo
  Sophia Mjema akizungumza baada ya kupokea bati hizo
  "Bati hizi pelekeni kuzihifahdhi kuleee", Sophia Mjema akiwaelekeza vijana baada ya kupokea bati hizo
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Sophia Mjema akizungumza na Waandishi baada ya kupokea mabati hayo. Katikati ni Ndugu Barua. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu
  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi hilo John Bukuku kulia ni Katibu akifuatiwa na katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi hilo Edgar Mdime
  Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akisoma risala fupi katika ziara ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali iliyokuwa na lengo la kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu
  Katibu Mkuu wa Tawi hilo akizungumza machache
  Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
  Mmoja wa wanachama wa Simba kutoka Tawi la Simba Cream Chongowe akiuliza swali
  Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akiteta jambo na mwanachama wa tawi hilo
  Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
  Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa Simba Jijini Tanga
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali akiwa kwenye picha na Katibu Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina wa Tawi hilo  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ili iweze kuwa hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.

  Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ambao wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka vingi.

  Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huukatika tawi la Simba Cream la Tanga mjini ambalo lilianzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais wa Simba Evans Aveva.

  Alisema uanzishwaji wa timu hiyo utakuwa na faida kubwa kwa kusaidia timu hiyo kuwa na hazina ya wachezaji ambao wanaweza kuwatumia kwa miaka ijayo ili kuendelea kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini.

  “Kwani timu hiyo inapoanzishwa na kuweza kuwa imara itatuwezesha tunapotaka wachezaji tunakuja kuchukua mkoani Tanga kwa sababu tutakuwa tumewekeza mtaji mkubwa wa vijana”Alisema.

  Hata hivyo alisema tawi la Simba la Kinondoni kwa miaka ya nyuma ndio ambalo liliwasaidia kuwapelekea mchezaji Uhuru Selemani na baadae yeye kumpeleka kwenye klabu ya Coastal Unon . (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga wakati wa mkutano Mkuu wa Mwaka wa sita wa taasisi ya kutoa huduma za viwango vya barcodes na mifumo ya ufatiliki Tanzania(GS1) wa watumiaji wa Barcodes na Mkutano wa saba wa wadau . Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam katika jengo la LAPF . NIC ilikuwa moja ya taasisi zilizodhamini mkutano huo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza wakati wa mkutano Mkuu sita wa Mwaka wa taasisi ya kutoa huduma za viwango za Barcodes na mifumo ya ufatiliki Tanzania(GS1) wa watumiaji wa Barcodes na Mkutano wa wa saba wa wadau . Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam katika jengo la LAPF, NIC walidhamini mkutano huo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza wakati wa mkutano Mkuu huo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akifatilia kwa makini mkutano huo.

  0 0

  1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda.
  3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda.
  4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao Kampala nchini Uganda.
  5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Mawaziri pande zote mbili za Kenya na Tanzania mara baada ya kikao chao Kampala nchini Uganda.
  8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kikao chake na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Kampala jijini Uganda.
  9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi ajambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Kampala jijini Uganda.
  10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Kampala jijini Uganda.
  11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kabla ya mazungumzo yao jijini Kampala.
  14
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Kampala Uganda-
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Bondia wa Kimataifa Francis Cheka anatarajia kupigana na Bondia Arney Tinampay Kutoka Nchini Ufilipino katika Pambano la raundi 10 litakalofanyika katika Uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara mwanzoni mwa mwezi wa Nne.

  Kwa mara ya Kwanza Bondia Franciss Cheka anapigana Mchezo wa Kimataifa wa Kutetea Ubingwa wa Mkanda wa UBO wa kilogram76 katika Mkoa wa Mtwara,ambapo tayari ameanza Kufanya maandalizi ya Mazoezi tayari kwa Pambano hilo.AKiongea na waandishi wa habari Promota Jay Msangi anasema Bondia Kutoa Ufilipino anatoka katika Historia ya mabondia wakubwa.

  “Bondia huyu anahistoria anatokea katika kambi ya Man Pacquiao na anayemfundisha  aliwah pia kumfundisha Pacquiao na ni Bondia mwenye kushika daraja la pili katika Nchi ya Ufilipino kenye uzito wa Kilogram 76 na hivyo unaweza kuona kwa Francis Cheka anakutana na Bondia Mwenye uwezo mkubwa”alisema Promota Jay Msangi.

  Naye Fransis Cheka anasema anajiamini licha ya kuwa hamfahamu Bondia huyo Kutoka Ufilipino lakini uwezo wake ni mkubwa kupigana na bondia yeyote wa kiwango chake.

  “Sifahamu Uwezo wa Mfilipino lakini najifahamu uwezo wangu kwa sababu nimeshakuwa Bingwa wa Dunia na hivyo nawahakikishia Watanzania hususani wakazi wa mkoa wa Mtwara nitafanya vizuri,Simfahamu huyo Bondia lakini nitakapokutana naye Ulingoni tutafahamiana Hapo Hapo”Alisema ChekaCheka.

  Wakati huo huo Bondia Francis Cheka amekabidhiwa Ubalozi wa Kuitangaza Eneo la Mikindani ambalo lina majengo ya Kihistoria. 
   Mzee Mohammed Kidume Akimsimika Ubalozi wa Mikindani Bondia Francis Cheka katikati kwa lengo la Kutangaza historia ya Majengo ya Kale ambayo yalitumiwa na Wakoloni.
  Bondia Francis Cheka akiwa na wazee wa Mikindani Mara baada ya kukabidhiwa Ubalozi wa kutangaza Hotel ya Old Boma Iliyopo Mkoani Mtwara.

  0 0

   Uongozi wa Halmashauri ya Wilayaya Handeni umekabidhiwa rasmi mradi wa choo cha matundu sita kilichojengwa na shirika lisilo la Kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) lenye thamani ya Milioni 19 za Kitanzania  kwa lengo la kuboresha huduma ya vyoo kwa wanafunzi wa shule za Msingi. 
   Akipokea mradi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Aweso Bakari ( Afisa Tarafa Mkumburu) alisema kuwa anashukuru sana CDMT kwa kuona uhitaji wa Shule ya Masatu na kuamua kusaidia ujenzi wa choo chenye  matundu 6 yatakayosaidia kupunguza changamoto ya vyoo shuleni hapo.

  Kaimu Mkurugenzi alisema kuwa, Shule ya Masatu kwa mujibu wa ripoti ya Mwalimu Mkuu ilikuwa na upungufu wa matundu 29 ya vyoo, Hivyo kwa mradi wa matundu 6 yaliyojengwa na Shirika la CDMT umepunguza na kufikia matundu 23, hivyo  anashukuru Shirika hilo  kwa jitihada za kuunga Mkono Serikali katika ujenzi wa miundombinu.
   Aidha aliwataka viongozi wa shule na Kijiji kuhakikisha wanatunza mradi huo kwa kuzingatia usafi wa mazingira ili hata waliofadhili mradi huo wakija kuutazama wafarijike na waweze kuisaidia Serikali kutatua changamoto nyingine ambazo bado zinaikabili shule hiyo.

  “Naishukuru sana CDMT, Viongozi wa shule na Kijiji msimamie mradi huu vizuri kuhakikisha hauharibiwi kwa michoro ya ajabu na usafi uzingatiwe ili hata wafadhili wakija kutembelea waone thamani yake” alisema Aweso
   Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Segera Mh. Yassin Mtamike alisema kuwa, anaishukuru CDMT na yeye kama Diwani atahakikisha mradi huo unatunzwa na kulindwa ili kuwapa nafasi wafadhili waweze kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu.
   Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) na Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Emile Philipo alisema kuwa baada ya kufika Handeni aligundua changamoto ya vyoo bora kwa Shule za Msingi na kuamua kuandika andiko la kuomba msaada kwa Serikali ya Marekani yenye fungu la fedha la Rais wa Marekani linalosaidia Afrika kwa lengo la kupunguza changamoto ya vyoo.
   Aliongeza kuwa kwa tafiti zake  za awali aliamua kusaidia shule tatu za msingi ambapo shule  mbili za Msomera na Masatu zipo Hamashauri ya Wilaya ya Handeni na shule moja  1 ya Seuta Halmashauri ya Mji Handeni.

  Miradi yote imekamilika kwa jumla ya Milioni 58 za Kitanzania ambapo kila shule imejengewa matundu 6 ikiwa matundu 3 kwa  wanafunzi wa kike na 3 kwa wanafunzi wa kiume.


older | 1 | .... | 1523 | 1524 | (Page 1525) | 1526 | 1527 | .... | 1896 | newer