Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SIMBA CEMENT YATOA MIFUKO 3000 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi leo katika anayeshughudia ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Mashariki leo katika anayeshughudia ni kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akimkabidhi Msaidizi wake,Abdallah Salimu mifuko hiyo mara baada ya kukabidhiwa anayeshughudia katikati nyuma ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart

Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea sehemu ya mifuko ya Saruji 3000 kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi katika kulia anaye shughudia ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akieleza mikakati ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye hayupo pichani ambaye alikwenda kiwanda hapo kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya Elimu Jimboni kwake Iramba Magharibi
aziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na vyombo vya habari mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya saruji ambapo alikishukuru kiwanda cha Simba Cement kwa kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake kuli ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swat
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya Saruji kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya Elimu Jimboni Kwake

Sehemu ya Saruji mifuko 3000 aliyokabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Simba Cement Reinhardt Swat wakitembelea kiwanda hicho kabla ya kukabidhiwa mifuko 3000 ya Saruji Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat kulia akimuonyesha eneo ambalo wanalotumia kwa shughuli za kiwanda Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema katika ambaye alitembelea kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho,Beny Lema Meneja wa Kiwanda cha Simba Cement Beny Lema akimuogoza Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kushuka ngazi mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kulia akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa ajili ya kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu kwenye Jimbo lake la Iramba Magharibi
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Jijini Tanga wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema kushoto akiwa na wafanyakazi wengine wa kiwanda hicho wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba katika akiwa na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia kushoto ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim wakiongia ukumbini kwa ajili ya kupata taarifa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga ambao nao waliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani katika makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdalla(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

MASAUNI AONGOZA KIKAO BARAZA LA TAIFA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda, akichangia hoja wakati wa wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto).
Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakishiriki kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Article 0

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amezindua Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.
Uzinduzi huo umefanyika Februari 20,2018 katika hospitali ya Sekou Toure na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), ICAP na wafadhili ambao ni wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and Prevention (CDC).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia alizindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses) ambao unalenga kuwawezesha wamiliki wa nyumba hizo kuziendesha vizuri na kuwasaidia ipasavyo.
Waziri Mkuu aliwatahadharisha watanzania wasijishughulishe kuzalisha,kusambaza,kuuza na kutotumia dawa za kulevya kwani Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.
“Leo hii mmeona na tumeshuhudia ushuhuda wa vijana walioathirika na dawa za kulevya walikuwa wanaleta athari katika jamii,walikuwa wanaleta vurugu,wanakaba lakini baada ya kufika katika kliniki hali zao zimekuwa nzuri,nataka wanaouza dawa hizo waache na watumiaji wafike hospitali”,alisema Waziri Mkuu.
“Serikali tuna wadau wanaotuunga mkono kuna AGPAHI, ICAP, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wanatufanya tufike hapa tulipo,niwasihi watanzania popote mtakapoona vijana wetu wameathirika na dawa waleteni kliniki wasajiliwe,wapewe dawa na niiombe jamii iwaamini hawa waliobadilika kwani wamejua athari za dawa za kulevya”,aliongeza Waziri Mkuu.
Aidha alisema hivi sasa serikali inaendelea kutafuta maeneo kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali ili watu watakaotaka kujifunza ujasiriamali watumie maeneo hayo kwa ajili ya kuokoa vijana.
Naye Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani, Dk. Maestro Evans ambao wamesaidia kuanzishwa kwa kliniki hiyo kupitia shirika la AGPAHI na ICAP kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia CDC alisema kliniki hiyo itasaidia kupunguza athari zinazotokana na dawa za kulevya kama vile maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Dk. Evans aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutambua mchango wa serikali ya Marekani katika kuwahudumia wananchi katika masuala ya afya ikiwemo VVU na Ukimwi, Malaria na huduma za mama na mtoto.
Aidha alisema serikali ya Marekani itaendelea kusaidia kazi zinazofanyika katika eneo la kushughulikia dawa za kulevya na kupunguza athari zinazotokana na dawa za kulevya na kusaidia waathirika.
Akizungumza wakati uzinduzi huo Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Leonard Subi alisema kituo hicho kimetokana na mchango mkubwa wa wadau wakiwemo AGPAHI, ICAP kwa msaada wa watu wa Marekani.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kuwasaidia watu walioathirika na dawa za kulevya ili kukabiliana na madhara yatokanayo na dawa hizo ikiwemo homa ya ini na maambukizi ya VVU.
“Wadau wetu ICAP na AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani wamesaidia fedha kwa ajili ya dawa na samani za ndani ya kliniki hii",alisema.
Nao waathirika wa dawa za kulevya,Abdallah Abdul na Nyamizi Sospeter waliishukuru serikali kwa kuwaondoa katika wimbi hilo la dawa za kulevya na kuahidi kuwa watu wazuri kwa kutofanya vitendo vya uhalifu mtaani.
Aidha waliiomba serikali kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kufanya kazi na kupata kipato kitakachowasaidia kujiinua kiuchumi kwani hawakuwa na kazi za kufanya zaidi ya kukaba watu mtaani.
Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Rogers Siyanga alisema kliniki hiyo iliyozinduliwa italeta nafuu kubwa kwa waathirika wa dawa za kulevya lakini pia kupunguza madhara ya arosto na madhara yatokanayo na dawa hizo mfano Ukimwi,homa ya ini,magonjwa ya ngozi na magonjwa ya meno.
Alisema serikali itawapatia vitambulisho waathirika wa dawa za kulevya walioanza kupata matibabu ili kuwaepusha na usumbufu unaoweza kujitokeza mtaani kwa baadhi ya watu kutoamini kama waathirika wa dawa hizo wamebadilika tabia baada ya kuanza kuhudhuria kliniki.
“Vyombo vya dola vitakapokutana na watu hawa,naomba tusiishi kwa historia,wakikuonesha kitambulisho kwamba anahudhuria hospitali kupata dawa naomba umpeleke hospitali usiendelee kumwadhibu”,alisema Siyanga.
Siyanga alitoa wito kwa watu walioathirika na dawa hizo wajitokeze kupata matibabu ili wawape nafuu na familia za watu waliothirika na dawa za kulevya wawapeleke ndugu zao wakapate dawa katika Kliniki ya Methadone iliyopo katika hopitali ya Sekou Toure.
Muonekano wa jengo la Methadone Kliniki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa wakati wa uzinduzi wa Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la  ICAP nchini Tanzania, Dk. Fernando Morales.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Leonard Subi akisoma taarifa kuhusu Methadone Kliniki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la uzinduzi wa Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la uzinduzi wa Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi katika Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ndani ya jengo la Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika moja ya chumba katika kliniki hiyo. Aliyevaa nguo nyeupe kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Rogers Siyanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiondoka katika jengo la Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waathirika wa dawa za kulevya wanaopata huduma ya tiba katika Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasisitiza waathirika wa dawa za kulevya kuendelea na tiba.
Wadau mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye jengo la Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Kijana Abdul Abdallah akitoa ushuhuda mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jinsi alivyoathirika na matumizi ya dawa za kulevya na jinsi alivyobadilika baada ya kuanza kuhudhuria kliniki. Alisema yeye na mke wake walikuwa wanatumia dawa za kulevya aina ya heroine yeye ametumia dawa hizo kwa takribani miaka 20 na muda wote huo alikuwa anakaba watu ili apate fedha za kununulia dawa za kulevya.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiondoka katika Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki”.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza Dk. Leonard Subi akisoma taarifa kuhusu dawa za kulevya mkoa wa Mwanza ambapo alisema mkoa huo una zaidi ya watu 10,000 wanaotumia dawa za kulevya.
Baadhi ya vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya na sasa wamebadilika tabia baada ya kuanza kupata tiba katika Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akiwasalimia wadau waliohudhuria uzinduzi wa Methadone Kliniki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa Kliniki Saidizi kwa waathirika wa dawa za kulevya “Methadone Kliniki” katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Wadau wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumza ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na tume ya kudhibiti dawa za kulevya,ICAP,AGPAHI na wadau wengine. Alisema Mwanza ni kati ya waathirika wakubwa wa dawa za kulevya na kwamba changamoto iliyopo katika mkoa huo ni wimbi kubwa la wauzaji wa dawa za kulevya na kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaendelea kupambana nao. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Siyanga akizungumza ambapo aliishukuru serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua huku akitoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Muathirika wa dawa za kulevya Nyamizi Sospeter akitoa ushuhuda kuhusu madhara ya dawa za kulevya. Alisema alitumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka saba na muda wote huo alikuwa akiisumbua familia yake kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu aliyokuwa akiyafanya ili apate fedha za kununulia dawa za kulevya.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani, Dk. Maestro Evans akizungumza ambapo alimhakikishia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa serikali ya Marekani kuwa itaendelea kusaidia katika sekta ya afya nchini Tanzania. 
Dk. Maestro Evans akiendelea kuzungumza.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses) . Alisema dawa za kulevya zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo Ukimwi na kikuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameshikilia kitabu cha Mwongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses). 
Burudani ya ngoma ya Kisukuma ikiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MISS KK KUZINDUA VIDEO YA WANANUNA JUMAMOSI

$
0
0
Na Karama ,Kenyunko,Globu ya jamii

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Latifa Mussa a.k.a Miss KK Jumamosi ya Februari 25, mwaka huu anatarajia kuzindua video yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Wananuna.

Uzinduzi wa video hiyo yenye Mandhari ya tofauti tofauti utafanyika katika kiota cha Pallet Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo wa kutoka Wanene entertainment ambao ni moja kati ya wafadhili wa msanii KK.

Katika Video ya Wananuna ambayo inamandhali ya kuvutia hasa ikiwa imeshutiwa jijini Arusha na Dar es Salaam na kufanyiwa editing nchini Afrika Kusini, wananchi watapa fursa ya kuona hata utalii wa ndani.

Msanii KK  aliyekuwa akifanya shughuli zake za mziki nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu amesema, lengo lake kubwa na kufanya muziki nchini ni kuwafanya wanamuziki kutoka Tanzania wana perfoam Afrika Kusini na vilevile kwa Afrika Kusini.

Aidha katika usiku huo kutakuwa na usiku wa black Carpet. " Napenda kuwaambia wasanii wapya wanaochipukia kwenye muziki, watuliee, waache papara kuwa na malengo na wasikubali kuyumbishwa."

 Sherehe za uzinduzi huo zinatatajiwa kuanza SAA Moja usiku na watu wakwanza kufika kuanzia muda huo mpaka saa tatu watapata kuponi za vinywaji za bure na kati yao watapata vocha kutoka kwa mdhamini wake Coast airline kwenda mbuga za wanyama za Ruaha kwa Siku  mbili.
Msanii wa Muziki, Latifa Mussa, mwenye shati nyekundu, akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uzindizi wa video yake inayokwenda kwa jina la wanune inayotarajiwa kuzinduliwa February 24, katika kiota cha Pallet Mbezi beach, pembeni ni Meneja wake, Erikson Kinywele aka DJ Kinywele

NAIBU WAZIRI WA MAJI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
Naibu Waziri wa Magi na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipokea maelezo ya mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa maji wa Makongo Juu kutoka kwa Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos, P.G Rajan na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wa kwanza kushoto.
Naibu Waziri wa Magi na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisikiliza changamoto kutoka kwa Michael John mmoja ya wafanyakazi wanaotekeleza mradi wa maji wa Salasala, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Magi na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na mazugumzo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASA), Modesta Mushi (kulia), Meneja Mradi wa Kampuni ya Wapcos, P.G Rajan (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.

………………

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni katika ziara yake kikazi katika manispaa hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Aweso amejionea utekelezaji wa miradi mikubwa ya majisafi na majitaka unaoendelea katika maeneo ya Mwenge Mlalakuwa, Makongo na Salasala inayotekelezwa na Serikali chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASA), pamoja na kuzungumza na Kamati ya Jumuiya ya Watumiaji Maji ya Mabwepande.

Aidha, pia amedhishwa na kiwango cha upatikanaji wa maji kwa manispaa hiyo ambacho kimefikia asilimia 76 kwa sasa, pamoja na hatua za kutatua kero ya maji kwa wananchi na usimamizi mzuri wa miradi ya maji.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amesema kuwa manispaa yake itasimamia miradi yote ya maji kwa umakini, iweze kukamilika kwa wakati na kuwa yenye faida kwa wananchi wote wa manispaa hiyo na hakuna mkandarasi asiyekuwa na uwezo atakayepata kazi.

NAIBU WAZIRI MADINI AKERWA USIRI WA MAPATO YA MUWEKEZAJI MGODI WA SUNSHINE

$
0
0

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amekerwa na usiri wa mapato na matumizi ya muwekezaji wa mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Mhe Biteko ameonyesha masikitiko makubwa wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo mara baada ya uongozi wa mgodi huo kushindwa kumpatia taarifa ya mapato na matumizi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua shughuli za uchimbaji Madini.

Kumbukumbu hizo zimekosekana kufuatia viongozi wa ngazi ya juu ya mgodi kutokuwepo kwenye kikao hicho pamoja na kukiri kupokea taarifa ya ujio wake kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.Alisema kuwa viongozi hao kukosekana pamoja na kuwa na taarifa ya muda mrefu juu ya ziara hiyo ni utovu mkubwa na nidhamu kwa serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa pamoja na kutokuwepo kwao lakini taarifa zilitakiwa kuwepo ofisini kwani ni kosa kisheria kukosekana kwa taarifa za mgodi ilihali sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaeleza vyema kuwa mmiliki wa leseni ya Madini anatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi kwa miaka mitano.

"Endapo atashindwa kufanya hivyo serikali itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo cha mwaka mmoja jela ama faini ya shilingi Milioni 50 mpaka milioni 150" Alisema Naibu Waziri huyo.Mhe Biteko akizungumza huku akionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika eneo la ofisi ya mgodi huo huku wakishindwa kuhudhuria katika kikao hicho cha kazi alisisitiza kuwa muwekezaji wa mgodi huo anapaswa kuzingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Sambamba na hayo pia Mhe Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kutoa taarifa sahihi za uwepo wa mashapu katika mgodi waliyokuwa wakichimba au kama mashapu katika mgodi huo yameisha wafuate taratibu za kisheria za ufungaji wa mgodi ikiwemo kuyarudisha mazingira katika halo take ya kawaida.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na mmoja wa kiongozi wa Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.

RC KILIMANJARO AKAGUA UTENDAJI KAZI WA TANESCO MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka, pembeni ni Mhandisi mkuu wa mkoa Bagabuje Joseph, Mkuu wa wilaya ya Moshi Mh. Kippi Warioba na Meneja wa Tanesco Himo, Bw, Mohamed Kayanda.
Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yared Ngalaba akifafanua kwa Mkuu wa mkoa Mh Anna Mghwira mifumo ya usafirishaji umeme mkoani Kilimanjaro.
Kutoka kushoto Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yaredi Ngalaba, Mhandisi mkuu Bagabuje Joseph, Afisa uhusiano Tanesco Kilimanjaro Bw. Samuel Mandari na Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira.
Msimamizi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiyungi Joseph Mwisongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa Mh Anna Mghwira.


- KATIKA ZIARA HIYO AMETEMBELEA VITUO VYA KUPOOZA UMEME (SUBSTATIONS) ZA KIYUNGI, TRADE SCHOOL, BOMA MBUZI NA KIA.

Mkuu wa Mkoa Amewataka watumishi wa TANESCO kuendelea Kutekeleza majukumu yao  kwa bidii ili kuhakikisha huduma ya umeme inakuwepo muda wote na ameahidi kuwaunga mkono katika ulinzi wa miundombinu ya umeme mkoani hapa.

Nae meneja wa TANESCO Kilimanjaro mhandisi MAHAWA MKAKA amemuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwepo kwa umeme wa kutosha kwa wawekezaji wa viwanda Mkoani Kilimanjaro.

Katika Ziara hiyo Mkuu wa mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na wakuu wa wilaya za Moshi na Hai pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa na Wilaya.

KATA YA TOMONDO YAPATA NEEMA

$
0
0
Kiongozi waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwa katika darasa la Shule ya Msingi Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini alipotembelea shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani wa Chama hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kutoa bati za madarasa mawili.
Kiongozi waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia), akiwa na diwani wa chama hicho, Hamisi Msangule (kulia) pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho wakitoka kwenye darasa la Shule ya Msingi Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini alipotembelea shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani wa Chama hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kuchangia bati za madarasa mawili.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati), akiwa na viongozi wa chama hicho wa Mkoa wa Morogoro na Jimbo la Morooro Kusini Mashariki kwenye eneo la mto Lugwazi ambako mradi wa barabara utapita kwa kumwagwa zege kwenye eneo hilo, ambako Chama hicho kimechangia mifuko 20 ya saruji kati ya 60 inayohitajika.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa kwenye usafiri wa bodaboda wakati akienda kukagua miradi ya maendeleo ya Kata ya Tomondo Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki jana.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Viongozi wa chama hicho mkoa wa Morogoro Wilaya na Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wakimsaidia mkazi wa Kijiji cha Vuleni kuandaa mahindi wakati wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi yamaendeleo kwenye kata ya Tomondo inayoongozwa na chama hicho.
Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe kuangalia chanzo cha maji kinachotumika na wakazi wa Kijiji cha Vuleni Kata ya Tomondo ambako chama hicho kimeahidi kuchimba visima virefu kila Kijiji haraka iwezekanavyo.
…………………

WAKAZI wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wiki hii imekuwa ni ya neema kwao kutokana na kupata ufumbuzi wa baadhi ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo.

Kata hiyo inayoongozwa na diwani wa chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule jana ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto za maendeleo.

Changamotokubwa ambayo imepewa kipaombele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji inayowakabili wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho imeahidi kuwapeleka wataalamu wa kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi huu.

Akizungumza kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo jana Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza kero hiyo haitakuwa na aana tena chama hicho kupewa dhamana tena kuongoza.

“Chama chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao, alisema.

Mbali ya ahadi ya kumaliza kero ya maji kiongozi huyo pia amechangia mifuko ishirini ya saruji kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara inayokatiza kwenye mto Lugwa kwenye Kijji cha Vuleni.

Neema iliendelea kuwaangukia Kijiji cha vuleni baada ya Kiongozi huyo kuahidi kuchangia bati zote zitakazo hitajika kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili kati ya saba yanayohitajika shuleni hapo, yatakapoanza kujengwa.

Awali akitoa maelezo kwa Kiongozi huyo, diwani wakata hiyo, Hamisi Msangue alisema, Kata hiyo kwakuwa ni mpya ina changamoto nyingi hivyo kunahitajika nguvu nyingi ili kuweza kufanikisha maendelo na kutekeleza ahadi walizoahidi wananchi.

Diwani huyo aliwaeleza viongozi wa chama hicho kuwa zahanati yao ina manesi wawili tu na haina mganga jambo linalowaletea usumbufu wa kupata huduma za afya kwa wananchi.

Aidha changamoto nyingine nyingi zilielezwa kuwa zinahitaji ufuatiliaji kwa mamlaka zinazohusika kwaajili ya kupata majibu na kuahidi kupeleka mrejesho haraka iwezekanavyo.

Kata hiyo kama zilivyo kata nyingi za mkoa wa Morogoro nayo haikuachwa nyuma kwenye migogoro ya aridhi, kutokana na wanachi wengi kumlalamikia mwekezaji wa kizungu anaemiliki hekta 600 za Kijiji hicho bila ya kufata taratibu.

Ziara za Chama hicho kukagua maendeleo kwenye kata zinazoongozwa na madiwai wa chama hicho zinaendelea.

MAKAMU WA RAIS APOKEA MISAADA KUTOKA UBALOZI WA CHINA KWA AJILI YA MAENDELEO MKOANI SIMIYU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 178,488,00/- kutoka kwa Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nkoma iliyopo Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Vyerehani 50 kwa ajili halmashauri ya mji wa Bariadi ili kuanzisha Kiwanda cha Ushonaji.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

WAKANDARASI WASIO WAZALENDO WASIPEWE KAZI NDANI YA JIJI LA DAR - NAIBU WAZIRI AWESO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miundo mbinu ya maji safi na maji taka iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemshukuru Naibu Waziri Aweso kwa msikamano ambao amekuwa akiufanya na wilaya yake ya kuwapa kipaumbele cha kuwatembelea mara kwa mara hali inayoamsha maendeleo zaidi.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASCO, Injinia Aron Joseph amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwa vile kwasasa wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati alipofanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya  maji kwa jiji la Dar es Salaam ambapo amejionea maendeleo mbali mbali ya ujenzi. Pichani akiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya alipoanzia ziara hiyo.
Akikagua mradi wa Maji Taka (DEWAT) - Mlalakuwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji eneo la Makongo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipewa maelezo machache na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati Waziri Awezo alipofanya ziara ya mradi wa maji eneo la Makongo juu ambapo ujenzi bado unaendelea.
Viongozi wa DAWASA, DAWASA pamoja na uomgozi wa serikali ya kijiji wakimsikiliza Naibu Waziri Aweso.
Wakitoka kukagua mradi wa ujenzi wa makongo juu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi akisalimiana na Meneja wa DAWASCO-Kimara, Peter Fumbuka. Ambapo aliweza kumshukuru na kumpongeza kwa utendaji kazi wake na kumuomba achape kazi kwa bidii.
Muonekani wa ujenzi tanki la maji Makongo juu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na mmoja ya wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAMIMBIKI IPANDISHWE HADHI KUWA PORI LA AKIBA

$
0
0

Na Hamza Temba - WMU-Bagamoyo, Pwani
....................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.


Ametoa agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani yake pia kuna mapito ya wanyamapori.


Dk. Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi hiyo kwa asilimia 100.


"Sisi kama jamii tumeshindwa, tunaomba msaada wa Serikali, itusaidie kuondoa hawa wavamizi na ikiwezekana ichukue jukumu la kulinda hifadhi hii kwa asilimia 100," alisema Tofiki.


Alisema jumuiya hiyo ambayo ni muunganiko wa vijiji 24 inakabiliwa na changomoto kubwa ya ujangili uliokithiri ambao umepelekea kuuwawa kwa wanyamapori zaidi ya asilimia 90 ya waliokuwepo tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 1997.


Alisema changamoto nyingine ni kukosekana kwa muwekezaji na mapato ya kujiendesha, uvamizi wa mifugo ndani ya hifadhi hiyo na majungu yanayosababishwa na baadhi ya wananchi na viongozi wanaonufaika na vitendo vya ujangili na uharibifu wa hifadhi hiyo.


Dk. Kigwangalla alisema jumuiya hiyo imefeli katika kila eneo jambo ambalo linalazimu kuanzishwa kwa mchakato wa kuirudisha Serikalini ili iweze kuhifadhiwa vizuri. Alitoa wito kwa viongozi wa Wilaya na vijiji kuanza kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupandishwa hadhi jumuiya hiyo kwa faida ya pande zote.


"Nimepokea maombi mengi ya kuongeza idadi ya wanyamapori katika hifadhi ya Saadan, tatizo kubwa hapa ni kwamba wanyamapori wanapotoka nje ya hifadhi hiyo na kupita kwenye eneo la Wamimbiki wanavunwa na majangili ambao wengi wao wanasuply (wanasambaza) nyamapori Jijini Dar es Salaam," alisema Dk. Kigwangalla akielezea umuhimu wa kupandishwa hadhi hifadhi hiyo.


Kwa upande wake Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Abraham Julu amesema Serikali imekuwa ikisaidia katika ulinzi wa eneo la jumuiya hiyo kwa kushiriki kwenye doria mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kuondoa makazi ndani ya hifadhi hiyo.


Alisema eneo hilo ni muhimu sana kwa uhifadhi wa wanyamapori kwa kuwa ni moja ya eneo la mazalia ya wanyamapori na shoroba nne (mapito ya wanyamapori) zinazounganisha hifadhi ya Taifa ya Saadan, Mikumi na Pori la Akiba la Selous.


Katika hatua nyingine baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan, Dk. Kigwangalla ameuagiza uongozi wa TANAPA kupitia hifadhi hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Bagamoyo na vijiji kuweka utaratibu maalum utakaowawezesha wananchi kupita katika barabara zilizopo ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo kuwatengenezea vitambulisho maalum.


Ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete kuwa wananchi wake wanazuiliwa kutumia barabara hizo kwa madai ya kushiriki kwenye vitendo vya uharibifu wa hifadhi hiyo.




Amewataka pia viongozi wa hifadhi hiyo ya pekee barani Afrika ambayo ipo katika fukwe za bahari ya Hindi kuwa wabunifu zaidi kwa kuanzisha bidhaa mpya za utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo. Alisema hifadhi hiyo ambayo ipo karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanga ni fursa nzuri kwa watalii kutumia ukaribu huo kuweza kuwaona wanyamapori mbalimbali wakiwemo Simba, Twiga na Tembo pamoja na utalii wa fukwe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Stephano Msumi wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
Picha ya pamoja

"Dunia inawaangusha watoto wachanga"- UNICEF

$
0
0
Duniani kote, vifo vya watoto wachanga bado viko juu sana kiasi cha kuwa tishio, hasa miongoni mwa nchi maskini zaidi ulimwenguni, UNICEF imesema katika ripoti yake mpya kuhusu vifo vya watoto iliyozinduliwa leo mjini New York. Ripoti hiyo imebainisha kuwa watoto wanaozaliwa katika nchi za Japani, Iceland na Singapore wana nafasi kubwa zaidi ya kuishi, wakati wale wanaozaliwa katika nchi za Pakistani, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Afghanistani wanakabiliana na hatma mbaya kabisa ya maisha yao.

 “Wakati ambapo tumepunguza kwa zaidi ya nusu idadi ya vifo miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano katika robo karne iliyopita, bado hatujafaulu kwa kiwango kama hicho katika kukomesha vifo miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya mwezi mmoja,” alisema Henrietta H. Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF. 

“Kwa kuwa vifo hivi vingi vinazuilika, ni wazi kwamba, tumewaangusha watoto walio maskini zaidi duniani,” alisisitiza mkurugenzi huyo wa UNICEF. Ulimwenguni, katika nchi za kipato cha chini, wastani wa vifo vya watoto wachanga ni vifo 27 katika kila vizazi hai 1,000, ripoti inasema. Katika nchi za kipato cha juu, kiwango ni vifo 3 kwa kila vizazi hai 1,000. Nchini Tanzania, viwango vya vifo vya watoto wachanga ni 25 katika kila vizazi hai 1,000, kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya wa Tanzania (TDHS 2015-16). 

Ikiwa kila nchi itapunguza viwango vya vifo vya watoto wake wachanga hadi katika viwango vya nchi za kipato cha juu ifikapo mwaka 2030, maisha ya watoto milioni 16 yataokolewa, ripoti hiyo imebainisha. Ripoti hiyo inaeleza pia kwamba miongoni mwa maeneo 8 kati ya 10 yaliyo hatari zaidi kwa mtu kuzaliwa, basi Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, ni mojawapo, ambapo wanawake wajawazito wana uwezekano mdogo wa kupata msaada wakati wa kujifungua kwa sababu ya umaskini, migogoro na taasisi zisizo na ufanisi. Watoto wanaozaliwa katika nchi zenye hatari zaidi wana uwezekano wa hadi mara 50 wa kufa kulinganisha na wale wanaozaliwa katika nchi zilizo salama. 

Nchini Tanzania, kuna hatua kubwa imepigwa katika kupunguza vifo miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, hata hivyo hatua hiyo bado haijafikiwa katika kukomesha vifo vya watoto wachanga na akina mama. Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu sana vya vifo vya watoto wachanga duniani: takribani watoto 39,000 hufariki kila mwaka, miongoni mwao, 17,000 hufa katika siku yao ya kwanza duniani. Wengine zaidi 47,550 wanazaliwa wakiwa wameshakufa na akina mama wapatao 8,000 hufa kila mwaka wakati wa kujifungua. Kuna hatua kubwa imepigwa nchini inayowapa watoto wa Kitanzania nafasi kubwa zaidi ya kuishi hata baada ya kutimiza miaka mitano tangu kuzaliwa kwao. 

Hata hivyo, bado kuna changamoto. Kila siku, watoto 270 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufa, wengi kutokana na magonjwa yanayozuilika kama vile malaria, homa ya mapafu na kuhara. “Karibu vifo 6 katika 10 hutokea katika siku yao ya kwanza ya maisha, wakati vifo 4 katika 10 hutokea katika mwezi wa kwanza wa maisha. Tunaweza kuokoa vifo hivi kwa huduma rahisi na nafuu, zilizo bora ambazo zinapaswa kumfikia na kufikiwa na kila mama na mtoto wake mchanga kote nchini. 

UNICEF imedhamiria kuunga mkono juhudi za serikali katika kupunguza viwango vya vifo vya watoto wachanga. Sote tunapaswa kudhamiria kumpa kila mtoto nafasi stahiki ya kuanza maisha. Ni haki na jambo la maana la kufanya,” alisema Maniza Zaman, Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, zaidi ya asilimia 80 ya vifo vya watoto wachanga vinatokana na kuzaliwa njiti, matatizo wakati wa kujifungua au maambukizi kama vile homa ya mapafu na bakteria katika tishu. 

Vifo hivi vinaweza kuzuiwa kama huduma ya zuazi itatolewa na wakunga wenye mafunzo, huku kukiwa na uhakika wa maji salama, dawa za kuzuia vijidudu, unyonyeshaji katika saa ya kwanza, kumkumbatia mtoto na lishe bora. Hata hivyo, upungufu wa watumishi wa afya wenye mafunzo bora na wakunga kunamaanisha kwamba maelfu hawapati msaada huu muhimu wa kuokoa maisha yao katika kipindi hiki muhimu. 

Kwa mfano, wakati ambapo huko Norway kuna madaktari, manesi na wakunga 218 wa kuwahudumia watu 10,000 uwiano ni 1 kwa kila wahitaji huduma 10,000 kule Somalia. Mwezi huu, UNICEF inazindua kampeni kote duniani ya Every Child ALIVE (Kila Mtoto Abaki HAI), ambayo inataka na kutoa suluhisho kwa ajili ya watoto wachanga wa ulimwengu. Kupitia kampeni hiyo, UNICEF inatoa wito wa haraka kwa serikali, watoa huduma za afya, wafadhili, sekta binafsi, familia na biashara kuhakikisha kila mtoto anabaki hai. “Kila mwaka, watoto wachanga milioni 2.6 kote duniani huwa hawaishi zaidi ya mwezi wao wa kwanza. Watoto milioni moja hufa siku ileile wanapozaliwa,” alisema Fore.

 "Tunajua kwamba tunaweza kuokoa uhai wa watoto walio wengi miongoni mwa hawa kwa suluhu rahisi na matunzo bora ya afya kwa ajili ya kila mama na kila mtoto mchanga. Hatua chache ndogondogo kutoka kwa kila mmoja wetu zinaweza kusaidia kuhakikisha kunakuwa na upigaji hatua kwa kila uhai mpya wa watoto hawa wachanga.” Nchini Tanzania, kampeni ya mwaka mzima imepangwa ili kusaidia upazaji sauti kuhusu masuala yanayohusua akina mama na watoto wachanga nchini. Lengo litakuwa ni kuunda vuguvugu la kitaifa kuhusiana na suala hili, kwa kulenga vijana walio kwenye balehe na walio hatarini zaidi, wanawake wajawazito na wanawake wanaonyonyesha.

DED MNASI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI ZA WILAYA YA ILEJE

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu 
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akibadilisha mawazo na baadhi ya viongozi walikuwa kwenye eneo la ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu


Na Fredy Mgunda,Ileje 

HALMASHAURI ya wilaya ya Ileje mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR ambazo hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi alisema kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa inayotolewa na serikali inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu kwa faida ya sekta ya elimu.

“Serikali inatoa pesa nyingi sana hivyo tusipo simamia vizuri pesa hizi zitapotea kitu ambacho Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli hataki kabisa kusikia kuna pesa ambayo haitumiki kama ilivyokusudiwa ndio maana nimeamua kuanza kukagua miradi yote ambayo inatekelezwa katika halmashauri yetu” alisema Mnasi 

Mnasi aliwaomba wananchi kuchangia nguvu zao kuhakikisha shughuli za ujenzi wa madarasa na vituo vya afya wanajitolea vilivyo ili kuendelea kufanya kazi sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano.“Mimi binafsi nawaomba wananchi wajitolee kufyatua tofali ,kuchota maji,kubeba mchanga na kusomba tofali ambazo zinakuwa zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya ujenzi ambao utakuwa na faida kwao na vizazi vijavyo” alisema Mnasi

Aidha Mnasi aliwapongeza wananchi wa halmashuri ya Ileje kwa kuendelea kujitolea kufanya kazi kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya wamu ya tano ambayo imelenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake

“Mpaka sasa kuna asilimia kubwa ambayo wananchi wamekuwa wakijitolea kufanya kazi za kimaendeleo ambazo zinawahusu japo sio kwa asilimia kubwa kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaoishi katika wialya hii hivyo nitoe wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwenye maendeleo ili kuijenga ileje yetu mpya” alisema Mnasi

Mnasi alisema kuwa kipaumbele cha halmashauri kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wanaboresha sekta ya elimu na sekta ya afya ili kukuza maendeleo ya wilaya kwa kasi kubwa.“Ujenzi unaendelea ni wa madarasa ya shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao” alisema Mnasi

Naomba nimalizie kwa kupongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli kwa kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kuboresha sekta za elimu,miundombinu afya na n.k

PROFESA JOHN SHAO AZUNGUMZIA UZOEFU WAKE KATIKA MASUALA YA TIBA: NI KWENYE SEMINA YA WCF KWA MADAKTARI

$
0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Moshi
DAKTARI bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, ameelezea uzoefu wake  juu ya mahangaiko waliyokumbana nayo wafanyaakzi walioumia wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi inapofikia muda wa kulipwa fidia.
Akitoa uzoefu huo mbele ya madaktari wanaoshiriki mafunzo ya siku tano (5) ya tathmini yaMfanyakazi aliyepataulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 21, 2018, Profesa Shao ambaye kwa sasa amestafu kazi, alisema uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), utawezesha wafanyakazi walioumia kazini kwa mazingira mbalimbali waweze kupata haki zao stahiki.
Ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tathmini wakati huo, kulipelekea shida nyingi kwa wafanyakazi waliopata madhara kazini.
Aidha Profesa Shao ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi za tiba akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC Moshi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, na pia aliwahi kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Karatu, aliushauri Mfuko katika kutekeleza majukumu yake ni lazima sasa ujikite katika mambo ambayo aliyaona wakati huo yakiwa na mapungufu.
“Kuwe na utaratibu katika ngazi ya vituo vya afya vya binafsi na vya serikali ambavyo vitawapokea wagonjwa kama hawa na kuwapima kutokana na jinsi walivyoumia na kuwapatia rufaa ya kwenda katika hospitali za wilaya, mkoa au hizi za madaktari bingwa ili waweze kupata huduma hiyo na vile vile kutathminiwa kwa usahihi.” Alisema.
Alishauri kuwa kazi hii ya kufanya tathmini isiachiwe kwa Daktari mmoja au muuguzi mmoja au afisa mmoja tu bali pawepo na kikundi (team work) ambacho kimepata mafunzo mazuri kinachoweza kupima na kutoa muelekeo mzima na katika kufanikisha hili lazima pawepo na mfumo mzuri endelevu wa mafunzo kama haya.
“Uwepo mfumo wa wataalamu (madaktari) wanaopata mafunzo haya watoke kila kada ili wapatiwe mafunzo stahiki ya kuwahudumia wagonjwa wanaopata madhara yatokanayo na kazi, ili wawe na uwezo wa kutoa tathmini iliyo sahihi.
Pia alishauri kuwepo na mfumo wa kuimarisha uanzishwaji viwanda walau kuwe na Minimum Standard ya viwanda vinavyoanzishwa vikidhi mazingira salama ya kazi na hatua hiyo iende sambamba na mafunzo kwa wafanyakazi walioajiriwa wawe na muda wa kupewa elimu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye mazingira yao ya kazi na jinsi gani wanaweza kujiepusha nayo.
Aidha gwiji huyo wa uchunguzi wa vijidudu na madawa, aliwaasa madaktari hao kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kuongeza uwajibikaji, moyo wa kujitolea na kutojiona kama vile mgonjwa aliyeumia anatumiwa kama mojawapo ya kuongeza kipato kwa watendaji.
Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuhudumia wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na usalama mahala pa kazi wakati wa mafunzo ya madaktari wanaojifunza namna ya kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 21, 2018
 Mshiriki akifuatilia kwa makini nasaha za Profesa Shao.
 Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Assessment Manager), wakifuatilia nasaha za Profesa Shao. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.
Profesa Shao, (kushoto), akiteta jambo na mmoja wa washiriki.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
 
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), akisalimiana na Profesa John Shao.
 Profesa John Shao, akisalimiana na  Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), Dkt. Ali Mtulia.
 Sehemu ya washiriki.
 Profesa John Shao.
MABINGWA WANAPOKUTANA:
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina,(kulia) na Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, wakisalimiana. 
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina, akifafanua jambo.

WAFUASI 28 CHADEMA WAFIKISHWA KORTINI KWA KUTUHUMIWA KUFANYA MKUSANYIKO ISIVYOHALALI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WATU 28, wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA), wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukusanyika isivyo halali.

Mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, watuhumiwa hao wote wanadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa halali.
 
Mwendesha Mashtaka wakili wa Serikali, Faraji Nguka leo akisoma mashtaka amedai, lengo la mkusanyiko huo wakiwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kuhusika kwenye tukio hilo na baadhi yao wameweza kutimiza mashati ya dhamana ambayo yamewataka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atayesaini bondi ya shilingi milioni moja na nusu.

 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machine 8, mwaka huu.

Baadhi ya majina ya watuhumiwa hao ni, Tabitha Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mnombo, Abdallah Hamisi, Hussein Kidela, Paulo Kimaro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edina Kimaro.

Wengine ni Fatuma Ramadhani, Asha Kileta, Salha Ngondo, Ally Rajabu, Raphael Mwaipopo, na Athumani Mkawa.
WATU 28, wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia Chadema (CHADEMA), wakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukusanyika isivyo halali.

NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AFANYA ZIARA WILAYA YA SHINYANGA KUKAGUA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi kwani serikali haitaki kuingia kwenye matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu zake za kutolewa huduma ya afya. 

Dk. Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Shinyanga, Februari 21,2018 akikagua shughuli za huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.

Dk. Ndugulile alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2017-18) serikali kwenye bajeti ya wizara hiyo ya afya imetenga jumla ya shilingi bilioni 270, tofauti na mwaka wa fedha (2015-16) ambapo zilikuwa milioni 30 hivyo hawatarajii kusikia sehemu za kutolewa huduma zake za kiafya kuwa zina upungufu wa dawa.

Akiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha Afya cha Kambarage manispaa ya Shinyanga na kukagua bohari za dawa, Dk. Ndugulile alitoa tahadhari kwa wauguzi kuwa ni marufuku dawa hizo za serikali kukutwa zinauzwa kwenye maduka ya watu binafsi na ikibainika watachukuliwa hatua kali.“Serikali ya awamu hii ya tano imedhamiria kuboresha huduma za afya hapa nchini, na ndio maana hata bajeti yake imetolewa ni ya fedha nyingi hivyo sisi kama wizara husika hatutarajii kuwepo kwa upungufu wa dawa kwenye sehemu za huduma za afya”,alieleza.

Pia aliwataka wananchi kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu hasa pale watakapougua na kukutwa hawana pesa ambapo wataweza kutibiwa kwa shilingi hiyo 10,000/= ili kuokoa maisha yao.

Naye kiongozi wa Mradi wa Maendeleo ya Tuimarishe Afya (HPSS) kutoka makao makuu Dodoma Profesa Manoris Meshack, alisema mradi huo wa Bima ya afya ya jamii CHF ulianza mwaka 2011 mkoani Dodoma, na baada ya kufanya vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga na Morogoro.

Alitaja takwimu za kaya katika mikoa hiyo mitatu zilizojiunga na CHF iliyoboreshwa hadi sasa kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya kaya 1,220,413, na hadi kufikia Disemba 2017 kupitia uandikishaji wa wanachma wamekusanya shilingi bilioni 7,027,605,547. ambapo shilingi bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.

Nao baadhi ya wazee kati ya kumi wasiojiweza ambao walikatiwa Bima hiyo ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa na Naibu Waziri huyo wakati wa ziara hiyo,Mohamed Mkumbola na Regina Kulwa waliipongeza serikali kwa kujali makundi hayo maalumu, na kuomba wazee wote wakatiwe Bima hiyo pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wajiunge.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya kata ya Kambarage mjini Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu na Steve Kanyefu
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ameshika kopo la dawa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga na kusisitiza kuwa dawa zenye nembo ya dawa za serikali MSD hazitakiwi kutoka nje ya hospitali za serikali.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia mgonjwa katika kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga huku akiangalia dawa alizopewa mgonjwa na kupiga marufuku wagonjwa kuambiwa dawa hakuna na kwenda kununua kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulileakikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga, na kuagiza jengo hilo lifanyiwe marekebisho ili kuendana na hadhi ya chumba cha upasuaji, sababu haliridhishi kuendana na huduma ambayo itakuwa ikitolewa.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoka kwenye jengo la chumba cha upasuaji katika kituo cha afya kata ya Kambarage mjini Shinyanga na kuacha maagizo lifanywe marekebisho.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akihamasisha wananchi wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu pale watakapo patwa na ugonjwa gafla harafu hawana pesa ambapo bima hiyo itasaidia kupata tiba na kuokoa maisha yao.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hamasa kwa wananchi kwa vitendo juu ya ukataji wa Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kukata Bima hiyo papo hapo, na hapo akipigwa picha na Ofisa uandikishaji CHF Kata hiyo ya Kambarage Marry Budigila.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akijaza taarifa zake wakati akiendelea na zoezi la ukataji Bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kutoa hamasa kwa wanachi kujiunga nayo huku akikatia watu 10 bima hiyo ambao hawajiwezi wakiwamo wazee.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa hamasa ya wananchi kujiunga na bima hiyo ya Afya CHF iliyoboreshwa, pamoja na kusaidia kuwaunga watu watano wasiojiweza kwenye Bima hiyo.Matiro alimuunga mkono Naibu waziri kwa kutoa elimu kwa vitendo huku akiwataka wadau kujitokeza kusaidia kukatia Bima hiyo watu waliokatika makundi maalumu.
Ofisa uandikishaji wa Bima ya afya CHF iliyoboreshwa Jackson Njau, akiendelea na zoezi la kuingiza taarifa kwa wananchi ambao wamejitokeza kujiunga na Bima hiyo ya afya ya jamii.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi Kadi ya CHF Mzee Mohamed Mkumbola ambaye ni miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi kadi ya CHF bi Regina Kulwa ambaye ni miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Mzee Mohamed Mkumbola akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakatia kadi ya bima ya afya wazee wasiojiweza, huku akimuomba kumsaidia kupata madai yake katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga anayodai mara baada ya kuacha kufanya kazi, ombi ambalo liliahidiwa kushughulikiwa na kukabidhiwa majukumu hayo katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga, wakisikiliza nasaha kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile juu ya kujiunga na Bima hiyo ya afya CHF, ambayo itakuwa msaada mkubwa katika kuokoa maisha yao pale watakapopatwa na magonjwa na kukutwa hawana pesa.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kujiunga na Bima ya CHF iliyoboreshwa, ambapo mtu akikata shilingi 10,000 yeye na familia yake watu watano watatibiwa bure kwa mwaka mzima.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga kuangalia namna huduma za afya zinavyotolewa dhidi ya wananchi, huku upande wa mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, na mkono wa kulia ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Geogre Masigati.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia huduma ya mfumo wa malipo ya kielekroniki kwenye hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kukuta mfumo huo haufanyi kazi ambapo hapo awali aliambiwa unafanya kazi na kusababisha kuwepo na upotevu wa fedha.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia majalada ya wagonjwa na namna wanavyopatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia mzazi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kumuliza maswali juu ya huduma anazopewa ikiwemo kama aliagizwa kwenda kununua dawa yoyote ama vifaa kwa ajili ya kujifunguli na kupewa majibu kuwa kahudumiwa vizuri na vitu vyote kapewa hapo hospitalini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipitia taarifa ya hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kubaini kuna upotevu mkubwa wa pesa kutokana na kutofanya kazi mfumo wa ukusanyaji pesa kwa njia ya kielektroniki na kuagiza ufanye kazi haraka sana.
Baadhi ya wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakisikiliza ujumbe kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na kusisitizwa watoe tiba vizuri kwa wananchi pamoja na kutoa kauli nzuri kwa wagonjwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kusikiliza taarifa za huduma ya afya kutoka kwa wakurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na Shinyanga vijijini
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisoma taarifa ya huduma ya afya ya manispaa hiyo. Alisema katika manispaa hiyo kuna vituo Viwili vya afya, zahanati 28 na hakuna tatizo la uhaba wa dawa,na kutaja takwimu za Kaya zilizojiunga na bima ya afya ya jimii CHF kuwa ni Kaya 7,136 sawa na asilimia 21.2 ya kaya zote, na kaya zilizo hai hadi sasa ni 3,781na zinaendelea kupata huduma ya matibabu sawa na asilimia 11.2, ambapo lengo la kitaifa ni kufikia asilimia 30 na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na bima hiyo ya CHF.
Mkurugenzi wa halmashuari ya Shinyanga vijijini Bakari Kasinyo, akisoma taarifa ya huduma za afya kwenye halmshauri hiyo ambapo alisema kuna vituo vya afya vitano na zahanati 35 na hakuna tatizo la dawa na kutaja idadi ya kaya zilizojiunga na bima ya CHF iliyoboreshwa,kuwa ni 10,615 kati ya kaya 59,321 sawa na asilimia 11.3 ,na kubainisha mkakati ulipo ni kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na Bima hiyo ya CHF.
Kiongozi wa mradi wa maendeleo ya tuimarishe afya (HPSS) kutoka makao mkuu Dodoma Prof Manoris Meshack, akisoma taarifa ya mradi huo wa Bima ya afya ya jamii CHF kuwa ulianza mwaka 2011 mkoani Dodoma, na baada ya kufanya vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga na Morogoro.

Alitaja takwimu za kaya katika mikoa hiyo mitatu zilizojiunga na CHF iliyoboreshwa hadi sasa kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya Kaya 1,220,413 na hadi kufikia Dicemba 2017 kupitia uandikishaji wa wanachma wamekusanya shilingi bilioni 7,027,605,547. ambapo shilingi bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakikagua Jengo la Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambayo inajengwa katika kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nje wa jengo jipya la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Marco Maduhu na Steve Kanyefu

BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU

$
0
0
Uwekezaji katika sekta ya elimu Nchini kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu (EQUIP-Tanzania) ambao umelenga kuboresha mchakato wa kufundisha na matokeo ya kujifunza kwa watoto nchini umeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa Mkoani Simiyu.

Uwekezaji huo ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) umeleta ufanisi wa elimu na kufanya viwango cha ufaulu kuwa juu kutoka asilimia 36 mwaka 2013 mpaka asilimia 68 2017.

Na katika kutimiza hayo Jumla ya kiasi cha shilingi Bil 1.7 kutoka DFID kupitia mradi wa kuinua ubora wa Elimu Nchini (Equip) zimetolewa kwa Serikali ya Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu Mkoani humo .

Akizungumzia nia ya serikali ya Uingereza wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan , Mkuu wa DFID-Tanzania Elizabeth Arthy alisema wametoa kiasi hicho cha fedha kwa serikali ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya miundombinu iliyopo.

Arthy alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho kinatarajiwa kutumika katika kuboresha miundombinu hiyo na kujenga vyumba vya madarasa, ofisi za walimu pamoja matundu ya vyoo kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufanisi wa utoaji elimu kwa walimu na wanafunzi.

Mkuu huyo alieleza kuwa tangu shirika lake lianze kusaidia katika Elimu ,Mkoa wa Simiyu umeweza kupata mafanikio makubwa na ya haraka ambayo yamesaidia kuuweka Mkoa katika nafasi nzuri Kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka aliuelezea mpango wa kuinua ubora wa elimu Tanzania kwa Mkoa wake kuwa ni mpango ambao umeweza kuleta mabadiliko makubwa ya kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi.

Mtaka anaeleza wanalishukuru shirika la maendeleo ya uingereza (DFID) kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu kwa kuona kuwa Tanzania na Mkoa wake unahitaji msaada huo wa kuinua kiwango cha ufaulu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya elimu.

Amesema kupitia msaada huo wa fedha kiasi cha shilingi Bil 1.7 zilizotolewa kwao na shirika la DFID kwa mwaka huu za kuboresha mazingira ya elimu ,zitawasaidia kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambavyo vyote hivyo ni changamoto kubwa Mkoani kwake.

Anaongeza kuwa kupitia fedha hizo anaanimi tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo utapungua kwa kiasi kikubwa na kwamba atasimamia vema fedha hizo ili ziweze kutumika ipasavyo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Raisi utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akizungumza mbele ya makamu wa Rais juu ya mchango wa serikali ya Uingereza katika kuboresha elimu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya msingi Gamondo A iliyoo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Bibi Elizabeth Arthy alipotembelea shule ya msingi Gamondo A mkoani Simyu, kuona utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania.

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MAHAFALI YA 34 YA CHUO KIKUU HURIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki matembezi ya mahafali ya 34 ya Chuko Kikuu Huria pamoja na Mkuu wa chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (kulia) kuelekea kwenye uwanja wa Halmashauri ya  Bariadi kwenye sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mahafali ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya Wanafunzi waliohitimu katika Chuo Kikuu Huria wakiwa kwenye sherehe za mahafali ya 34 ya chuo hicho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KASESELA, ASIA JUMA WATINGA KARIAKOO DAR ES SALAAM, LEO, KUPATA UZOEFU WA NAMNA BORA YA KUSIMAMIA VEMA MACHINGA

$
0
0
Na Victor   Masangu, Chole  Kisarawe   
WAKINAMAMA  wajawazito katika kijiji  cha Kihare kata ya Maluwi Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani  waliokuwa wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya kutokana na  ukosefu wa kutokuwa na  wodi maalumu  ya kujifungulia kwa  kwa kipindi cha  muda mrefu na kuwalazimu kutembea umbari wa kilometa 15 kufuata huduma hatimaye kilio chao kimepata mkombozi baada kukamilika kwa jengo la wazazi.

Aisha Ramadhani na Fatma Iddy ni baadhi ya wakinamama ambao walisema kwa miaka mingi wamekuwa wanateseka pindi inapofika wakati wa kujifungua kutokana na zahanati ya Kihare ambayo  walikuwa wanaitumia katika kupata huduma ya matibabu ilikuwa haina jengo la wodi ya wazazi hivyo ilikuwa inawalazimu kufunga safari ya umbari wa kilometa 15 kwa kutumia usafiri wa baiskeli,pikipiki au wakati mwingine kutembea kwa  miguu.

Walisema  kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua kutokana  na kutokuwepo kwa wodi ya kujifungulia hivyo walikuwa wanachanganywa na wagonjwa wengine wa kawaida kitu hali ambayo ji hatari kwa afya zao na mtoto, hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na juhudi za Mbunge wa jimbo lao  kwa kuamua kujenga jengo hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa katika utoaji wa huduma.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu  amekiri kuwepo kwa changamoto ya wakinamama wa kijiji cha Kihare  kutembea umbari mrefu wa kilometa 15 kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya kujifungua katika kituo cha afya chole,ambapo kwa sasa wameanza harakati za ujenzi wa  wodi kwa kutumia  za halmashauri pamoja na michango ya wananchi.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi  Selemani Jafo amebaini kuwepo kwa hali hiyo wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati ya Kihare ambapo  amesema kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya.

Jafo alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaborsha sekta ya afya hivyo ujenzi wa vituo hivyo vya afya vitaweza   kupunguza adha ya wagonjwa hususan kwa  wakinamama wajawazito kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.

“Kwa kweli katika hili la wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata shida kubwa sana, kwani wakti mwingine wanasumbuka ya kufuata huduma ya afya kwa kutembea umbali mrefu, hivyo tumetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500, kwa kila ujenzi wa  kituo cha afya kimoja nah ii kwa kweli itapunguza sana adha ya wakinamama waliyokuwa wakiipata pamoja na wananchi wote kwa ujumla,”alisema Jafo.

Waziri Jafo akiwa  katika ziara yake ya kikazi  Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ambapo ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu, afya maji, pamoja na kuweza kukutana na viongozi, watendaji , pamoja na kungumza na wananchi wa vijiji,vitongoiji, kata kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo kwa lengo la kuweza kuzitatua.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akizungumza na baadi ya viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, barabara, pamoja na elimu pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais  Tamisemi,  Seleman Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wauguzi na madaktari wa  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbai ya maendeleo pamoja na kuzungumz na wananchi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

KASESELA, ASIA JUMA WATINGA KARIAKOO DAR ES SALAAM, LEO, KUPATA UZOEFU WA NAMNA BORA YA KUSIMAMIA VEMA MACHINGA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (watatu kushoto) alipowapeleka Kasesera na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah katika eneo la biashara za Machinga katika Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna Wilaya ya Ilala ilivyofanikiwa katika kuboresha mazingira na kuwaweka pamoja machinga hao katika shughuli zao. Wapili kushoto ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah kwa Machinga wakati wa ziara hiyo
 Baadhi ya kinamama wakimweleza kero Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa na ugeni huo
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akiwa katika Mtaa wa Kongo kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendesha na Machinga wa Kariakoo
 Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera ukipita katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendesha na Machinga
 Kasesera akiwa na Mwenyekiti wa Machinga wa kariakoo katika ziara hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesera akitazama bidhaa za machinga ambazo alisema hadhi ya bidhaa hizo inaonekana ni zaidi na za machinga
 Kasesera akitazama sampuli ya baadhi ya vifaa vya jikoni vinavyofanya kazi ambavyo anauza Machinga
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ricard Kasesera akihoji mfumo kwenye kompyuta alipoingia katika Ofisi ya Umoja wa Machinga kujua wanavyofanya kazi.
 Machinga ambaye ni mtaalamu wa programu za kompyuta namoyo Yusuf, akimpa maelezo Kasesera ya namna ambavyo Umoja wa Machinga unavyohifadhi kumbukumbu zote za machinga katika komyupta. Kulia ni Mbunge wa Kilolo Asia Juma akifuatilia kwa karibu
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma akimweleza jambo Ofisa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya walipokuwa kwenye ofisi hiyo ya Machinga Kariakoo
 Kasesera na ujumbe wake wakitoka katika Ofisi ya Machinga
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera na Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Juma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Machinga wakati wa ziara hiyo
 Kasesera akimfurahia Ustadhi ambaye ni mmoja wa machinga Kariakoo
 Kasesera akifurahia jezi la Timu ya Machinga baada ya kuzawadiwa katika ziara hiyo 
 Kasesera na Amina wakichagua nguo kwenye vitalu vya biashara za Machinga wakati wa ziara hiyo
 Kasesera akilipa fedha baada ya kuchagua nguo alizopenda
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akiagana na Mwenyekiti wa Machinga Stephen Lusinde mwishoni mwa ziara hiyo 
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akifanya majumuisho na ujumbe wake bada ya kurudi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifanya utambulisho na kutoa maelezo machache kabla ya kuanza ziara hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza ofisini kwake na ujumbe huo kabla ya ziara hiyo kuanza
 Kasesera akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kabla ya ziara kuanza
Kasesera na ujumbe wake wakijiandaa kuondoka ofisi kwa Mkuu wa wilaya kuanza ziara hiyo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images