Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1520 | 1521 | (Page 1522) | 1523 | 1524 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni  wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu  Akwiline jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar,Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuiya maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba jukumu la Mazishi yake.

  Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli  amesema amesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi huyo,Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT)."Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu  Akwiline pamoja na ndugu jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar,Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuiya maandamano ya chama cha CHADEMA.
   Mama wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jioni hii na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.

  Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.

  Katika ziara hiyo itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .

  Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.

  Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.

  Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)

  Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji la Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.

  Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .

  0 0

  Picha na Josephat Lukaza
  Na Josephat Lukaza - Dog Tips Tanzania
  Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine na pindi unapofikiria kufuga mbwa basi kwanza Jiulize Maswali yafuatayo. Moja Upo tayari kumuhudumia mbwa wako kwenye Chakula, Maradhi, Matibabu, Mafunzo na Kutoa Muda wako wa angalau kuanzia nusu saa  mpaka masaa mawili kwaajili ya kukaa nae, kucheza nae na uangalizi? Kama jibu ni HAPANA basi fahamu kuwa hujafikia hatua ya kufuga Mbwa ni heri uache maana vinginevyo yatakuwa mateso kwako na kwa mbwa mwenyewe. 

  Mbwa anahitaji upendo kama ambavyo Binadamu tunavyowapenda binadamu wenzetu na hata kuwahudumia pale wanapokuwa wagonjwa basi na Mbwa ni hivyo hivyo unapoamua kufuga mbwa fahamu ya kuwa naye  ni mnyama kama mnyama mwingine ambapo akiumwa anahitaji matibabu. Leo tutaangalia Makundi mbalimbali ya Mangonjwa yanayoweza kumshambulia mbwa, mnyama anayekaribia uhusiano na mbwa, na hata binadamu pia.
  Leo tutaangazia Makundi Mawili tu huku Makundi mengine yataangaziwa Katika post zetu zijazo kikubwa ni endelea kufuatilia post zetu kupitia Hapa DOG TIPS TANZANIA ili upate ufahamu na kuweza kutunza vizuri mbwa wako. Kuna aina nyingi ya magonjwa ya mbwa na magonjwa hayo tutayafahamu kupitia katika makundi haya mbalimbali. Makundi hayo Mawilin ni kama yafuatavyo
  1: VIRAL INFECTIONS
  Viral infections ni magonjwa yanayosababishwa na virusi kutoka kwa mnyama mmoja kwenda kwa mnyama mwingine ambapo magonjwa haya yapo mahususi kwaajili ya mbwa na hata binadamu. Katika Kundi hili la Viral kwa mbwa kuna magonjwa kama vile Rabies (Kichaa cha Mbwa), Canine parvovirus ,Canine coronavirus, Canine distemper ,Canine influenza, Infectious canine hepatitis , Canine herpesvirus , Pseudorabies na Canine minute virus Haya ni baadhi tu ya magonjwa ambayo ni kwaajili ya mbwa lakini pia yapo ambayo yanaweza kumdhuru binadamu pia kama hatochukua tahadhari mapema. >>>  SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA

  0 0

  Wadhamini wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa wito kwa watanzania na washiriki wengine kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili kushiriki katika mbio za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na kuwavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
  Rai hii inakuja takriban wiki mbili kabla kufanyikakwa mbio hizo maarufu ndani na nje ya nchi ambazo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000 kutoka nchi zaidi ya 45 mjini Moshi ambapo mbhio hizi hufanyika.

  Akizungumza jinini Dar es Salaam,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu, alisema tayari usajili umeshafunguliwa na kuwataka washiriki hususan wale wa mbio za kilometa 42 zinazodhaminiwa na bia hiyo, kujisajili kwa wingi ili Milioni 20 walizotenga za zawadi zibaki Tanzania.

  “Bila shaka tunatarajia kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi ndio maana tunasisitiza kuhusu usajili mapema ili kuepuka usumbufu dakika za mwisho,” alisema huku akiwapongeza waandaaji kwa maandalizi mazuri huku wakazi wa Dar es Salaam wakipewa nafasi ya kujisajilipia Februari 24 na 25 katika viwanja vya Mlimani City.

  Alisema wao kama wadhamini wakuu pia watatoa milioni moja kwa mTanzania wa kwanza wa katika mbio za kilometa 42 na milioni moja pia kwa mwanamke. “Hii ni mojawapo ya njia za kuongeza hamasa katika mbio hizi ambazo miaka ya nyuma zimetawaliwa na Wakenya."
  Meneja Masoko wa Grand Malt Warda Kimaro akizungumza kuhusu Kili Marathon.
  Naye kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alitoa wito kwa washiriki wote wa kilometa 21 kuanza maandalizimapema ikiwemokujisajili tayari kwa mbio hizo zitakazofanyika Moshi Machi 4 katika Cuo Kikuu cha UshirikaMoshi (MoCU).

  “Mbio zetu za kilometa 21 zimekuwa maarufu zaidi na tunasisitiza kuhusu kujisajili mapema ili tuwe na washiriki wengi zaidi mwaka huu na kuendelea kutuunga mkono Tigo katika kufanyambioza kilometa 21 kuwa maarufu zaidi,” alisema na kuongeza kuwa wametenga milioni11 kwa ajili ya zawadi.

  Meneja Masoko wa Grand Malt, Warda Kimaro ambaye kinywaji chake kinadhamini mbio za kilometa 5maarufu kama fun run, alisema mbiohizi zimekuwa maarufu sana kwani zinahusisha watu wa rika zote huku akiwataka wajisajili mapema kabla ya kufika Moshi ili waepuke usumbufu.
  Wadhamini wengine katika mbio hizi ni First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum na AAR as ambao ni wabia katika masuala ya tibabu. 

  Usajili Arusha utafanyika Februari 27 na 28 katika hoteli ya Kibo Palacekuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja na Moshi ni Machi 1 kuanzia saa sita mchana hadi saa moja usiku, Machi 2 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni na Machi 3 kuanzia saa tatu hadi saa sita mchana. 

  Kilimanjaro Marathon, ambayo mwaka huu itafanyika Machi 4 katika viwanja vya MoCU, huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions.

  0 0


  0 0

  Katika kusambaza upendo kwa jamii ya Tanzania ,Shirika lisilo la kiserikali la Rise Charry leo limeadhimisha kilele cha msimu wa wapendanao kwa kutoa msaada katika kituo cha sixten Anderson Orphanage Center kilichopo mkoani pwani, wilaya ya kibaha ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa na shirika hilo

  Maadhimisho hayo ambayo yamehusisha marafiki na wananchi mbalimbali ambao ni watu wa karibu Rise charity pamoja na watoto wa sixten Anderson Orphanage Center yamefanyika katika uwancha wa kituo hicho kwa kusheherekea kwapamoja
  Watoto waishio katika kituo cha sixten Anderson Orphanage Center wakipata chakula

  Viongozi mbalimbali wa Rise Charity, Wadau pamoja na watoto wa sixten Anderson Orphanage Center wakiwa katika picha ya pamoja
  Viongozi wa Rise Charity Kulia Mkurugenzi Mtendaji Mr Innocent Horomo, kushoto katibu wa Rise Charity Mr Atley Kayuni na watoto wa sixten Anderson Orphanage Center

  0 0


  Na Faustine Ruta, Bukoba

  Ligi ya mpira wa Miguu "Kamala Cup 2018" imefunguliwa leo Mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudia Timu ya Bakoba ikichapwa bao 2-0 na Timu ya Kahororo. Bao la kwanza la Timu ya Kahororo Fc lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 80 na Juma Baezwa baada ya kuwachomoka walinzi wa Timu ya Bakoba. Bao la pili lilifungwa dakika ya 83 na Jordan John na mtanange kumalizika kwa 2-0 dhidi ya wenyeji Baokoba Fc. 


  Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo ameipongeza timu hiyo kwa kuanza Ligi hiyo kwa ushindi pia amewataka Wananchi kuendelea kujitolea kuja kuzishabikia Timu za Kata zao na pia akiwashukuru kwa kujitokeza kwa Wingi kama walivyoingia leo kwenye Uzinduzi. 


  Ligi hii ilikuwa ianze siku ya Alhamisi lakini ilisogezwa mbele kutokana na michezo ya Ligi kuu Vodacom inayeondelea hivi sasa. Mdhamini ametaja zawadi za Washindi katika Ligi hiyo kuwa wa kwanza atazawadiwa kitita cha Tsh. Milioni mbili(2) na Mshindi wa Tatu atapatiwa kitita cha Milioni 1 na nusu huku mshindi wa tatu akijinyakulia kiasi cha milioni moja. Ligi itaendelea tena kesho tarehe 19/02/2018 na kuzikutanisha Timu ya Vetran Bkb vs Ijuganyondo na Bilele vs Rwamishenye.
   Katika Uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mnec wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Mutabuzi(kulia). Hapa akiambatana na mdhamini wa Ligi hiyo Diwani Mh. Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo kwenda kusalimia Timu zote mbili muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.
  Bw. Cletus akiteta Jambo na Mgeni rasmi Mh. Mutabuzi leo kwenye Ufunguzi wa Kamala Cup 2018.
  Wadau wa Soka mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Ufunguzi huo ulioanza kwa kishindo hii leo kwenye Uwanja wa Kaitaba.
  Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wamejitokeza kwa wingi katika Ufunguzi huo na kumpa sapoti ya Nguvu Diwani mwezao katika Ufunguzi huo wa Ligi ya mpira wa Miguu. Pia Mgeni rasmi amesema yeye atatoa kiasi cha shilingi Milioni moja kama sapoti yake katika Ligi hiyo.Mgeni Rasmi Mh. Mutabuzi akitoa neno wakati wa Uzinduzi huo.
  Msimamizi na mratibu wa Ligi hiyo ya Kamala Ndg Malik Tibabimale a.k.a (Kadunguda) akitoa maelekezo machache katika Uzinduzi huo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
  Mgeni rasmi akisalimiana na Waamuzi wa Mtanange huo ambao ufunguzi wake umefanyika leo hii na kuhudhuliwa na Mamia ya Mashabiki kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Kikosi cha Timu ya Bakoba Fc kilichoanza dhidi ya Timu ya Kahororo Fc leo hii kwenye Ufunguzi wa Ligi ya Kamala.Kikosi cha timu ya Kahororo Fc kilichoanza kupambana na Timu ya Bakoba Fc leo hii.Mchezaji wa Timu ya Kahororo Fc Erick Edson(Zenden) akimiliki mpira.Mchezaji wa Kahororo Fc jezi naba 10 Jordan John akimtoka mchezaji wa Bakoba. Kipindi cha kwanza Timu zote mbili hakuna laiyeliona lango la mwenzake zilienda mapumziko zikiwa 0-0.
  Wakati wa Mapumziko Ngoma ilipamba Moto.

  Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo akiwatuza Wacheza Ngoma.Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo nae alipata muda akashiriki Ngoma hiyo pendwa ya Kihaya wakati wa Uzinduzi wa Ligi yake na huku mpira ukiwa mapumziko.Dakika chache wakati wa Mapumziko Ngoma iliendelea kuchukua nafasi...Mashabiki wakafurahia Ngoma hiyo!Ngoma ikiwa imeshika kasi!!!


  Kipindi cha pili kiliendelea....Kipa wa Bakoba Fc akikimbilia mpira...

  Mchezaji wa Kahororo Fc Juma Baezwa akimiliki mpira

  Wadau wakitazama mpira


  Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo akiwa Meza kuu na Mgeni rasmi wakiutazama mpira wakati wa kipindi cha pili. Timu ya Kahororo Fc imeibuka Bingwa kwa bao 2-0 dhidi ya Timu ya Bakoba Fc.
  Mashabiki waliingia kwa Wingi katika Uwanja huo wa Kaitaba wakati wa Ufunguzi wa Kamala Cup 2018
  Dakika ya 80 Juma Baezwa akipongezwa na wenzake mara baada ya kufunga bao.Kipa wa Kahororo ( kulia) nae alisogea kumpongeza mfungaji.
  Matangazaji wa Radio  Kasibante 88.5 Fm  Slay akiteta jambo na Shabiki wa Timu ya Kashai wakati wa Uzinduzi wa Ligi hiyo iliyoana leo.

  Bao la pili lilifungwa na Jordan John dakika ya 83 na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Timu ya Bakoba Fc.

  Raha ya bao...

  2-0

  Kulia kiongozi wa Timu ya Kahororo nae alisogea kuwapongeza Wachezaji wake kwa kuanza kwenye Ligi hiyo huku dakika zikiwa zimeyoyoma.
   Mpaka dakika 90 zinakamilika Bakoba Fc 0 Kahororo 2.

  0 0

   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam wakati apokwenda kusuluhisha mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.
   Wakazi wa Mbondole kata ya Msongola wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi. 
   Wakazi wa Mbondole wakimpokea Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi wakiwa na mabango

   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi akikagua maeneo yaliyovamiwa katika eneo la Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam. 
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi mhe. William Lukuvi akikagua maeneo yaliyovamiwa katika eneo la Mbondole kata ya Msongola Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu, wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ya barabara mkoani humo. Wa Kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe.

  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98, mkoani Simiyu. Ujenzi huo umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46.  Gari maalum likimwaga lami ya mwisho katika barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3, wilayani Maswa, Mkoani Simiyu. Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 61.46.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe kuhusu umuhimu wa kutunza barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Simiyu,
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3, wilayani humo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Kushoto ni Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu.

  ……………………………………………………………………………………………..

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wakazi wa wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, kuilinda miundombinu ya barabara iliyokamilika kujengwa ili kupunguza gharama za matengenezo ambayo yanaepukika.

  Ametoa rai hiyo Wilayani humo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusema kuwa barabara hiyo itawaunganisha wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kukuza uchumi kupitia mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye mikoa hiyo.

  “Barabara hii sasa imekamilika ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kuilinda na kuhakikisha inadumu kwa kipindi kilichokadiriwa”, amesema Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa barabara hiyo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi watakaotumia usafiri wa reli ya kisasa pindi utakapokamilika kwani watatoka kwenye mikoa ya jirani kupandia kwenye stesheni ya Malyampaka ambayo iko kwenye barabara hiyo.

  Aidha, amewapongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha sehemu ya barabara hiyo na kumuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa miundombinu hiyo italindwa ili idumu muda mrefu.

  “Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuikamilisha barabara hii kwa kiwango cha lami kwani kwa sasa muda na gharama za usafirishaji wa mazao zitapungua”, amesema Dkt. Shekalaghe.

  Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema mradi mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 98 na kazi zilizobaki ni kuweka alama za barabarani na ujenzi umezingatia viwango vinavyohitajika.

  Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 imejengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46 na zote zikiwa zimefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akionyesha kopo lenye dawa aina ya Ampicilin isiyosajiliwa na mamlaka ya TFDA leo jijini Dar es Salaam.

  ………………………………………………………………………………..
  MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) iliendesha ukaguzi maalum wa dawa , vifaa tiba na vitendanishi katika Halmashauri na Manispa zilizo Kanda ya Kati na kubaini kuwepo kwa vifaa tiba na vitendanishi bandia duni ambavyo hajasajiliwa pamoja na dawa za serikali katika maduka ya dawa binafsi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Agnes Kijo amesema kuwa mamlaka haitawaacha watu wafanye vitu kiholela pamoja na kuwafikisha watu hao mahakamani.

  Amesema ukaguzi huo umefanyika kati ta Februari 5 hadi 7 mwaka huu katika Manispaa ya Dodoma , Morogoro na Mkoa wa Singida umefanyika katika wilaya ya Manyoni ,Iramba , Wilaya ya Gairo ,Mvomero , Kongwa na Chamwino.

  Kijo amesema jumla ya maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi 172ambapo 48 ni Famasi za dawa za binadamu , tano ni Famasi za dawa za mifugo ,tatu ni Hospitali na tatu zingine vituo vya afya , 76 ni maduka ya dawa muhimu za binadamu , 30 ni maduka ya dawa muhimu za mifugo, 1 ni zahanati pamoja na sita vituo vya huduma za tiba za mifugo .

  Amesema kuwa katika ukaguzi wamepata makopo 12 ya dawa bandia aina ya Ampicillin 250mg ambapo ni tofauti na dawa halisi ya Ampicillin iliyosajiliwa na TFDA.

  Amewataka ambao wenye bidhaa ambazo wanaziuza na kuweka katika mitandao wajisalimishe bila kufanya hivyo hatua kali za kisheria  zitachukuliwa.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.

  Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.

  Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.

  “Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanaitaji kurudi makwao,naagiza muwaandikie barua leo hii kuwa hao wakimbizi ambao wapo katika kambi za Nduta,Nyarugusu na mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanaitaji kurudi kwao wakajilete maendeleo” alisema Dr Mwigulu

  Waziri Nchemba aliongeza kuwa hatakaa kikao cha pande tatu kujadili kuhusu kuondoka kwa wakimbizi hao kwani wamesha kaa mwaka jana wakakubaliana jinsi ya kuondoka kwa wakimbizi hao nchini kwani mda huu ndii mda wa kilimo na kuwapeleka mwezi wa nne huko nikiwafanya wakaishi maishi magumu zaidi.

  Naye mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma Tonny Laizer amesema kutokana na hali ya usalama nchini burundi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutopokea waomba hifadhi, kituo cha Lumasi kinafungwa na serikali ya wilaya itakabidhiwa na UNHCR kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

  0 0

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wakandarasi wa ujenzi wa daraja la Kimalamisale wilayani Kisarawe.
  Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.

  …………………………………………………………….

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi anayejenga daraja wa Kimalamisale wilayani Kisarawe kufanyakazi usiku na mchana ili daraja hilo liweze kukamilika kabla ya Mvua za masika hazijaanza.

  Waziri Jafo ametoa agizo hilo alipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa daraja hilo ambao unagharimu kiasi cha Sh.Milioni 390.

  Hatua hiyo ya Jafo imetokana na mradi huo kuchelewa hapo awali kutokana na Mvua kubwa za vuli zilizokuwa zinanyesha.

  Amesema mradi huo unatarajiwa kuwa kiungo muafaka kwa barabara ya Kimalamisale ambapo kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi.

  Amebainisha kuwa kwasasa mvua zinaponyesha magari yanashindwa kupita kutokana kujaa maji mengi katika mto Muyombo unaotenganisha wilaya ya Kibaha na Kisarawe mkoani Pwani.

  Katika ukaguzi huo, Mkandarasi wa mradi huo amemwambia Waziri Jafo kuwa ameshanunua jenerata kubwa ambalo watalitumia wakati wa usiku ili aweze kukamilisha ujenzi huo.

  Ameahidi kwamba watajitahidi kufanyakazi kwa kasi kubwa ili kuwahi Mvua za masika na wasipate hasara ya kuchelewesha mradi.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati akijibu maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu na watumishi wa Halmashauri hiyo, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziori Mkuu
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kitazama madawati ya madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa wilayani Ukerewe Februari 18, 2018. Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mabweni mawili ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa wilayani Ukerewe Februari 18, 2018. Wasita kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa wilayani Ukerewe kuzindua mabweni mawili ya Kidato cha Tano na Sita, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtwika ndoo ya maji, Stella Masumbuko wakati alipozindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijaza maji katika ndoo ya Janet Magayi (kushoto) wakati alipozindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe, akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimtwika ndoo ya maji, Janet Magayi wakati alipozindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

  Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.

  Amesema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.” Namtaka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.”

  Waziri Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo.

  Pia Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84 zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa ni sh. milioni 60 tu.

  “Kama mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa sababu Serikali haiwezi kuvumia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”

  Waziri Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si vinginevyo.

  Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie utendaji wa viongozi na watumishi katika wilaya zote za mkoa huo na kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi.

  Amewataka viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.

  0 0

  KIJANA JONES MBWAMBO ANASUMBULIWA NA TATIZO LA UVIMBE KATIKA UTI WA MGONGO AMBALO LIMESABABISHA KUPOOZA KWA MWILI WOTE. ANATAKIWA KUPELEKWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU. 

  GHARAMA ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 30,  TUNAOMBA MSAADA WAKO ILI KUWEZA KUFANIKISHA MATIBABU HAYO NA KUOKOA UHAI WAKE. UNAWEZA KUTUMA FEDHA ZA MATIBABU KWA MPESA: 0754295650 AU TIGO PESA: 0716913937 JINA LA MPOKEAJI NI JAINA MSUYA MAMA WA JONES. AKAUNTI YA BENKI NI 0112020233500. 

  TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA DHATI NA MUNGU AWABARIKI NA KUWAZIDISHIA PALE MTAKAPOTOA.

  0 0


  0 0


  Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Gharama za Taxify Bajaji kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo ya kuanzia TZS; Sh 750, TZS 350 kwa kila kilometa moja. TZS 75 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 2000

  Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
  Fenelisti Simon Metumba, Dereva wa Usafiri wa Bajaji jijini Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji'. App maalum iliyozinduliwa na kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri jijini Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam.
   
   
   Februari 2018, Dar es Salaam. Taxify, ambayo imejitanua katika utoaji wa huduma zake barani Ulaya na Afrika, leo imetambulisha huduma yake mpya ya ‘Taxify Bajaj’ ambayo ni App maalum kwa ajili ya Usafiri wa Bajaj huku wakiichagua Dar es salaam kuwa jiji la kwanza katika uzinduzi wa huduma hii.

  Kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify sasa imepiga hatua zaidi katika jitihada zake za kupunguza msongamamo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya usafiri wa teksi miezi miwili iliyopita.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji alisema, ‘Taxify Bajaj’ ni App mpya ya Taxify jijini Dar es Salaam ambayo inaunganisha watumiaji wa usafiri wa Bajaji na madereva ndani ya dakika chache.

  "Tunafurahi sana kuanzisha huduma hii kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam pia ni tumaini letu kuwa huduma hii itapokelewa vyema. Tunaamini kwamba huduma hii inaendana na utamaduni wa wakazi wa jiji hili na kwamba itatoa urahisi wa watu kuchagua usafiri anaoutaka kwa gharama nafuu pindi mtu anapotaka kufanya safari zake za mjini”

  Bei ya Taxify Bajaj ni kama ifuatavyo: -Nauli halisi ni TZS 750, TZS 350 kwa Km, TZS 75 kwa dakika, wakati bei ya chini kabisa itakuwa ni TZS 2,000.

  Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS na ina sifa za kipekee kama kutumia ETA yako na rafiki au mpendwa wakati wa safari, ambapo itakuwezesha kufanya makadirio ya kukodisha kabla ya safari na pia kupata msaada wa huduma kwa wateja kutoka ndani ya programu.

  Kwa upande wake, Meneja Mwendeshaji wa Teknolojia hiyo nchini Tanzania, Remmy Eseka alisema, programu yao ya teksi ambayo ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam imepokelewa vizuri sana mpaka kufikia sasa, zaidi ya kampuni ilivyotarajia hivyo inawahakikishia watumiaji wa wake kuwa Taxify itaendelea kuwepo hapa nchini.

  "Kama kampuni ya teknolojia, Taxify daima inaangalia njia ambazo inaweza kufanya ili kutoa ufumbuzi bora katika usafiri. Sisi daima tunaendelea kujibu haraka na kwa ufanisi mahitaji ya masoko mbalimbali ambako tunafanya kazi. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa mbele kwenye soko la ushindani na kuwa namba moja kuongoza katika masoko yetu yote, "alisema Eseka.

  Usafiri wa Bajaj unekuwa maarufu sana katika miji mikubwa likiwemo jiji la Dar kwa sababu usafiri huu ni suluhisho kwenye njia zenye foleni zaidi kuliko magari.Kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huu, unazifanya kampuni mbalimbali za Kiteknolojia kama Taxify kuja na suluhisho na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanapenda aina hii ya usafiri.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Coastal Union baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao katika halfa iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum 
  Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
  Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa 
  Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda katika akiwa na Kocha wa Makipa Salim Waziri kushoto na kocha Msaidizi Joseph Lazaro kulia 
  Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akisalimiana na mchezaji wa timu hiyo,Athumani Iddi Chuji
  Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Mchezaji Athumani Iddi Chuji ambazo zimeandaliwa na mfadhili wa timu hiyo ,Nassoro Binslum kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kuipandishi timu hiyo kucheza Ligi kuu
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Mlinda Mlango wa timu ya Coastal Union Sharifu Kasilasi kwa mchango wao wa kusaidia timu hiyo kupanda daraja
  Kocha Msaidizi wa timu ya Coastal Union Joseph lazaro akipokea naye tuzo kutrokana na mchango wao waliuonyesha kwenye michuano ya Ligi Daraja la kwanza na kusaidia timu hiyo kupanda daraja(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha) 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda baada ya kufanikisha timu ya Coastal Union kupanda daraja
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Kocha wa Makipa wa timu ya Coastal Union,Salim Waziri 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo beki wa timu ya Coastal Union Hamad Juma 
  Sehemu ya wachezaji wa timu ya Coastal Union wakiwa na wake zao wakipata chakula kwenye halfa hiyo 
  Mwenyekiti wa Kamat ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora kushoto akiteta jambo na Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando 
  Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort Joseph Ngoyo akiteta jambo na mdau wa michezo wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora katika akiwa na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Salim Bawaziri


  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu ya Coastal Union,Hafidhi Kidoh kulia akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Majira Tanga Mashaka Mhando kwenye halfa hiyo ya kupongeza wachezaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga 


  UONGOZI wa timu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” umetakiwa kushikamana na kutoruhusu migogoro na makundi yasiyokuwa na tija kwani yanaweza kukwamisha ndoto zao za kupata mafanikio katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara. 
  Lakini pia waaache vurugu na chokochoko iwapo wanataka kupata mafanikio huku wakitakiwa kuangalie wale wachache watakaopelekea hali hiyo wasiwaunge mkono kwa kuonyesheni mfano wamewachoka. 
  Hayo yalibainishwa na Mfadhili wa timu hiyo,Nassoro Binslum wakati akizungumza kwenye ghafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo sambamba na utolewaji wa zawadi baada ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort 
  Alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likirudisha nyuma mafanikio ya timu hiyo ni majungu,fitina na makundi ndani na nje ya timi hiyo hivyo ni bora viongozi,wapenzi ,wanachama wakabadilika na kuongeza mshikamano . 
  Binslum alisema umoja ulioonyeshwa na viongozi,wanachama na washabiki wakati timu ilipokuwa inatafuta nafasi ya kupanda ligi kuu unatakiwa uendelezwe ili uwe na tija kwa timu hiyo ili iweze kurudisha heshima yake ya miaka ya nyuma kuchukua ubingwa. 
  Aidha alisema wakati timu zinapokuwa kwenye madaraja ya chini kunakuwa hakuna majungu wala makundi maana kipindi hicho hakuna udhamini wale fedha lakini inapopanda timu kila mtu anaweza kujitokeza kwa kueleza anaweza kuongoza. 
  “Ndugu zangu niwaambie tuwaache viongozi,benchi la ufundi na wadhamini na sisi wengine tubaki tu kama wachezaji wa kumi na mbili kuisapoti timu na tukifanya hivyo tutafanikiwa sana kwani tutakuwa tumeweka msingi mzuri na imara “Alisema Binslum. 
  Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya usajili Hemed Aurora alisema mbali na mafanikio hayo jambo kubwa litakalozingatiwa kuhakikisha makundi hayatakuwa na nafasi ili kuepusha yaliyoikuta timu hiyo na kupelekea kushuka daraja. 
  Aurora alisema uwendeshaji wa timu unagharama kubwa itakayokuwepo si kutafuta ubingwa wa ligi kuu bali kuhakikisha kunajengwa umoja utakaoleta mafanikio na kupambana na wale wasiokuwa na nia njema na timu hasa baada ya timu hiyo kupanda. 
  “Tunatambua sasa kazi ndio inaanza ni zaidi ya miaka 30 kihistoria tangu timu hiyo iliptwaa ubingwa lakini ubingwa si kazi kama tutashikamana na kuwapinga kwa pamoja wale maadui zetu wanaosubiri timu ipande waseme timu yao tutawashughulikia safari hii”Alisema. 
  Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa alisema timu kurudi kucheza ligi kuu kunafaida kubwa sana kwa wanamichezo tu ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwani itasaidia kuinua ukuaji wa uchumi ndani ya Halmashauri ya Jiji. 
  Aidha alisema serikali iliahidi vitu vingi juu ya timu hiyo siku ya
  mapokezi yake ilipokuwa ikitokea Morogoro na jukumu lililopo ni utekelezaji wake ambao unaweza kuleta tija zaidi na timu nyingine kupanda na kufikia idadi kama ya zamani. 
  Hata hivyo alisema serikali imejitoa zaidi kuhakikisha inaisaidia timu hiyo iweze kuwa tishio na kwenye michuano ya Ligi kuu msimu ujao huku akizitaka zilizobakia nazo kuhakikisha zinaweka mipango imara ya kupanda ili kukuza vipaji vya vijana wetu na uchumu wa pato mkoa kwa kupitia michezo. 
  Kwa upande wake,Mwenyekiti wa timu hiyo,Steven Mguto alisema wataendelea kushikamana ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao. 
  Aliongeza kuwa mshikamano waliouonyesha wakati wa michuano hiyo ya Ligi Daraja la kwanza wataendelea nao ili kuhakikisha wanarudisha enzi za miaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

  0 0

  Na: Veronica Kazimoto-Arusha

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa mara nyingine ndani ya wiki mbili imekamata na kutaifisha tani moja ya sukari, mafuta ya kupikia katoni 10 na gari lililotumika kusafirisha bidhaa hizo kutoka nchini Kenya kupitia njia za magendo mpakani Namanga mkoa wa Arusha.

  Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapo Edwin Iwato alisema bidhaa hizo zimekamatwa usiku wa kuamkia leo na ni mali ya mfanyabiashara Paul Swai, ambaye alitumia gari namba T 496 AFE Nissan Carravan mali ya Christian Nko ambalo limetaifishwa pamoja na bidhaa husika.

  "Tumemkamata mfanyabiashara mwingine aitwae Paul Swai akiwa anaingiza nchini bidhaa kutoka Kenya kuelekea mkoani Arusha kupitia njia za magendo bila kibali wala kulipa ushuru wa Serikali", alisema Iwato.

  Iwato amefafanua kuwa tani moja iliyokamatwa ambayo ni mifuko 20 ya sukari ina thamani ya shilingi 2,200,000 na mafuta ya kupikia ambayo ni kilogramu 12 yana thamani ya shilingi 520,000.

  Mfanyabiashara huyo pamoja na dereva wa gari lililotaifishwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Forodha na bidhaa hizo baada ya kukaguliwa na kugundulika kuwa zinafaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA.

  Hii ni mara pili katika mwezi huu ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania imekamata na kutaifisha bidhaa mbalimbali zikitokea nchini Kenya kupitia njia za magendo mpakani Namanga mkoa wa Arusha.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya wananchi  wa Ukerewe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia  mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio  Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio kuhutubia mkutano wa hadhara, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa chanjo ya Polio kwa mtoto mchanga aliyepakatwa na mama yake mzazi, Dianna Malele (kushoto)  wakati alipozindua  zahanati ya Nakatunguru wilayani Ukerewe, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa chanjo ya Polio kwa mtoto mchanga aliyepakatwa na mama yake mzazi, Rizika Shaka (kushoto)  wakati alipozindua zahanati ya Nakatunguru wilayani Ukerewe, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1520 | 1521 | (Page 1522) | 1523 | 1524 | .... | 1897 | newer