Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1519 | 1520 | (Page 1521) | 1522 | 1523 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Buchosa wakati alipoingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyehunge wilayani Sengerema kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 15, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo cha Dotto Posho Mill, Bw. Alexander Dotto (kushoto) kuhusu unga na Mchele unaozalishwa na kiwanda hicho kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Miongella.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Sengerema baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kusaga nafaka na kukoboa mpunga cha Dotto Posho Mill kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji na wakuu wa idara mbalimbali kuhakikisha wanatenga muda na kwenda vijijini kuwahudumia wananchi.Amesema wananchi hususani waishio maeneo ya vijijini wanachangamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi na watendaji hao.

  Aliyasema hayo jana (Alhamisi, Februari 15, 2018) alipozungumza kwa nyakati tofauti na watumishi na wananchi katika kata ya Nyehunge na Ibisabageni wilayani Sengerema akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.

  Alisema Serikali imedhamiria kwa dhati kuwatumikia kwa lengo la kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo hakuna sababu ya watendaji kukaa maofisini.“Watumishi wanawajibu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao hasa vijijini kwa sababu si kila mwananchi anauwezo wa kufuata huduma katika ofisi zenu na atakayeshindwa kufanya hivyo hatutomvumilia.”

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali inawawezesha watumishi wake kwa kuwapatia vitendea kazi kama usafiri ili waweze kuwahudumia wananchi ipasavyo.Alisema kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wananchi wanaofanya kazi katika kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya nafaka cha Doto Alex Posho Meel kuwa waaminifu.Waziri Mkuu alisema wafanyakazi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wafanye kazi kwa bidii ili kukiwezesha kiwanda hicho kuendelea na uzalishaji.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, FEBRUARI 16, 201

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema (kulia) moja ya kompyuta mpakato kuashiria makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa kwa ajili ya kuimarisha majukumu ya Bodi ya Filamu alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Jasons Televisheni (JTV) Bw. Sanstus Mtsimbe (kulia) alipotembelea studio za televisheni hiyo kuangalia namna kazi za filamu zinavyoandaliwa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akiangalia moja studio za Starline Films zilizopo Mikocheni alipotembelea studio hiyo kuangalia namna kazi za filamu zinavyoandaliwa jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema na kushoto ni meneja wa studio za Starline Films Bw. Silver Oddo
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akifafanua jambo alipokua akizungumza na wafanyakazi wa Studio za Starline Films (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kutembelea Studio zinazojishughulisha na uandaaji wa kazi za filamu na muziki jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Studio za Wanene Bw. Darsh Pandit (wapili kushoto) baada ya kuangalia baadhi ya kazi zilizoandaliwa na studio hizo wakati wa ziara yake kutembelea studio mbalimbali zinazojishughulisha na uandaaji wa kazi za filamu na muziki jana Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kiandika maoni yake katika kitabu cha wageni baada ya kutemblea studio za Wanene zilizopo Mwenge wakati wa ziara yake kutembelea studio mbalimbali zinazojishughulisha na uandaaji wa kazi za filamu na muziki jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na kushoto ni Mkurugenzi wa Studio za Wanene Bw. Darsh Pandit
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akitoa taarifa fupi ya majukumu ya bodi ya filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Filamu (hawapo pichani) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe hao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
  Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Filamu na wajumbe wa kamati ya maudhui ya filamu wakifuatilia maagizo ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiashuhudia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kula kiapo kuwa mabalozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba akiongea machache baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Wilbrod Slaa baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Mohamed aliyeungana na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kushuhudia kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi na wakuu wa vyombio vya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi na maofisa kutokla Wizara ya Mambo ya Nje wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bw. Rogers Sianga pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kushuhudia kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 .
  PICHA NA IKULU

  0 0


   Maofisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) wakishuhudia wakati mabasi ya Kampuni  ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (UDART) yalipokuwa yakishushwa kutoka katika meli jijini Dar es Salaam leo hii asubuhi. Jumla ya mabasi 70 yalipokelewa.
   Sehemu ya kupita mabasi hayo ikiandaliwa wakati wa ushushaji wake kutoka katika meli ya Kichina.
   Moja ya mabasi hayo likitoka katika meli.
   Moja kati ya mabasi hayo likiwa limetoka katika meli.
  Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea mabasi hayo.

  Na Dotto Mwaibale

  KAMPUNI ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (UDART), imeingiza nchini mabasi mapya 70 kutoka China kwa ajili ya kuongeza nguvu ya usafirishaji abiria.

  Akizungumza wakati wa upokeaji wa mabasi hayo Bandarini jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe alisema hiyo ni hatua nzuri kwa kampuni hiyo yenye lengo la uhakika wa kutoa huduma bora ya usafiri kwa abiria jijini.

  Alisema mabasi hayo yataongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria hivyo kuwapunguzia adha ya usafiri wakati wa jiji la Dar es Salaam.

  Alisema mabasi hayo yataongeza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wananchi na kupunguza gharama ya usafiri ambapo kwa wale wenye magari wataacha kuyatumia magari yao kwenda kazini ambapo wataokoa sh.8000 katika kila sh.10000 waliyokuwa wakiitumia kwa siku kununulia mafuta.

  "Wenye magari sasa hivi watakuwa wanaokoa sh.8000 kila siku ambapo watakuwa wakitumia mabasi yetu kwa sh.2000 tu kuja kazini na kurudi majumbani kwao" alisema Newe.

  Alisema kiasi hicho cha fedha kitakachookolewa kitaweza kwenda kufanya shughuli zingine za maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja.

  Akizungumzia mabasi hayo alisema yanauwezo wa kubeba watu kuanzia 150 hadi 160 na kuwa bei ya basi moja ni limenunuliwa kwa dola za Marekani 260,000 na kuwa mabasi hayo yanafikisha idadi ya mabasi 210 huku mahitaji ya mabasi hayo ikiwa ni 305 kwa awamu ya kwanza.

  Alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni uchache wa mabasi yaliyokuwepo ambapo watu walilazimika kupanda kwa wingi lakini kwa ongezeko la mabasi hayo itasaidia kupunguza changamoto hiyo.

  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi mabati 280 kwa wastaafu 14.

  Amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania(CWT)Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.

  Akikabidhi mabati hayo juzi kwa wastaafu katika ofisi za CWT wilayani Kakonko Kanali Ndagala aliwapongeza wastaafu hao na kuwasisitiza kutumia zawadi waliyopewa kukamilisha nyumba zao au kuanzisha biashara itakayowasaidia kuendeleza maisha yao.

  Amesema kila mhsataafu amepewa mabati 20 kama zawadi za pongezi kutokana uadilifu.Pia pamoja na kujituma wakati wakiitumikia Serikali katika sekta ya elimu ambapo chama hicho kimetambua utendaji wao uliotukuka.

  “Niwapongeze kwa kumaliza salama muda wenu, mnapoenda kuanza maisha mapya na mazuri, huu ni mwanzo mzuri kama hujamalizia kibanda kamalizie."Kama tayari ni vizuri kujenga kibanda cha biashara au kufuga ilikuweza kujikimu kwa kipindi hiki maana kuna maisha baada ya kustaafu,”, amesema Kanali Ndagala.

  Aidha ametoa mwito wa kujitoa na kuwaomba watumishi wanapokuwa kazini wajiandae kustaafu kwani kustaafu si mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mengine uraiani na fursa ni nyingi endapo watazitumia vizuri.Amewataka kutokata tamaa kutokana na changamoto zinazojitokeza kazini kwani Serikali inatatua changamoto moja hadi nyingine na kuomba ushirikiano udumishwe ndani ya chama cha walimu.

  Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kakonko Tumaini Daniel amewaomba walimu wastaafu kuwakumbusha walimu waliopo kazini kujituma wakati wa kazi na kuiomba halmashauri itenge bajeti ya kuwarudisha makwao wastaafu baada ya kustaafu na Halmashauri iwaingize waalimu kwenye bajeti ya 2018/19 ili wapande madaraja kwani kuna waalimu zaidi ya 400 wanaotakiwa kupanda madaraja.

  Mmoja wa wastaafu Masuhuko Magwaya aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Bukiriro alieleza kufurahishwa na zawadi hizo walizopewa.Amewaomba walimu waliopo kazini wafanye kazi kwa uadilifu na kujitoa kwa moyo katika kuhakikisha wanatoa elimu bora kwani wanafunzi hao ndio tegemeo la kesho.

  Mninga Lameck mstaafu kutoka Shule ya Msingi Kabingo amewasisitiza walimu kufanya kazi kwa kujitoa pia watambue kazi ya ualimu ni wito na kuwataka kutotanguliza taama za kutopenda malipo kabla ya kazi ili kujengea heshima na kuweza kustaafu vizuri.
   MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi mabati 280 kwa mmoja wa wastaafu kati ya 14.Ndagaka amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.
  Baadhi ya Wastaafu hao hao wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali (hayupo pichani),Hosea Ndagala mara baada ya kuwakabidhi mabati 280

  0 0
 • 02/16/18--02:20: NEC YAJIBU HOJA 6 ZA CHADEMA
 • Jana 16/02/2018 baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, walifika ofisi za Tume ya Taifa kuwasilisha malalamiko yao kadhaa ambayo walikuwa wanahitaji ufafanuzi kutoka NEC kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kupitia hoja za Chadema, inapenda kutoa ufafanuzi wa hoja hizo: 

  Hoja ya kwanza, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni amekaa kuwaapisha mawakala wa ziada wa upigaji kura kutoka CHADEMA ambao ni asilimi kumi na tano (%15) ya Mwakala wote wanaohitajika kwenye vituo 613, na kuwa utaratibu huu umekuwa unatumiwa katika Chaguzi zilizopita. 

  Ufafanuzi, kwa mujibu wa kifungu cha 57(1)(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, kila Chama cha Siasa kilichopata ridhaa ya kuweka wagombea, kinaweza kuteua wakala mmoja wa upigaji kura kwa kila kituo ndani ya jimbo. 

  Aidha, Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 inakitaka kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi siyo zaidi ya siku saba (7) kabla ya siku ya Kupiga Kura kiwe kimewasilisha kwa maandishi kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina ya Mawakala, anwani zao na vituo walivyowapangia. 

  Vilevile, kifungu cha 57(3) cha Sheria tajwa, kimeweka utaratibu na mazingira ambayo wa Chama kilichosimamisha Mgombea kuweka wakala mbadala wa upigaji kura. 

  Tunashauri CHADEMA kuzingatia matakwa ya kifungu cha 57(3) cha Sheria husika pale patakapohitajika uwepo wa mawakala mbadala. 

  Hoja ya pili, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi amekataa kuwaruhusu na Viongozi wa CHADEMA kuwa Mawakala wa upigaji kura, kwa maana hiyo atakichagulia chama mawakala wa upigaji kura, na kwamba, orodha ya viongozi hao watambuliwe na kuapishwa kuwa Mawakala wa upigaji kura. 

  Ufafanuzi, kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 vimeweka utaratibu wa muda wa kuwasilisha orodha ya mawakala na muda wa kuwaapisha kuelekea siku ya Uchaguzi. 

  Kwa maana hiyo, siku ya kuwasilisha na kuapishwa mawakala ilikuwa tarehe 10 Februari, 2018. Hivyo, kupokea na kuwaapisha mawakala wengine itakuwa ni kinyume cha masharti yaliyowekwa chini ya kifungu na kanuni niliyoitaja. 

  Hoja ya tatu, kwamba, Mawakala wa upigaji kura wa CHADEMA hawajapewa nakala za hati zao za kiapo cha kutunza siri. 

  Ufafanuzi, kwa mujibu wa Kanuni ya 48(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 kila Wakala wa Upigaji kura anapaswa kuapa kiapo cha kutunza siri katika Fomu Na. 6 kabla ya kutekeleza wajibu wake katika kituo cha kupigia kura. 

  Kwa takwimu zilizopo jumla ya vituo vya kupigia kura ni 613 na jumla ya Vyama vya Siasa 12 vinashiriki katika uchaguzi huo. Kwa kuwa kila Wakala mmoja alijaza nakala mbili ya Kiapo cha kutunza siri, hapo unazungumzia uwepo na viapo 14,712. 

  Kanuni ya 48(3) ya Kanuni tajwa, Wakala wa Upigaji Kura atapaswa kupewa barua na Msimamizi wa Uchaguzi ya kumtambulisha kwa Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura. Hapa unazungumzia nakala 22,068 kwa sababu, nakala moja atapewa wakala, nakala itabaki kwenye jalada kwa kumbukumbu na nakala itapelekwa kwa Msimamizi wa Kituo kwa urahisi wa rejea. 

  Hata hivyo, taarifa tulizonazo ni kuwa, Msimamizi wa Uchaguzi ameanza kutoa nakala hizo za Viapo kwa Wawakilishi wa Vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi mdogo ili wawapatie Mawakala wa Vyama husika. Utaratibu huu nidyo uliokubaliwa kwenye vikao vya Msimamizi wa Uchaguzi na Wawakilishi wa Vyama. 

  Hoja ya Nne, kwamba, Msimamzi wa Uchaguzi ametoa maelekezo kuwa Mawakala wawe na utambulisho wa kumtambulisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi mbali ya barua kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Utambulisho huo ni Vitambulisho vya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva, Hati ya Kusafiria na Kitambulisho cha Kitaifa. 

  Ufafanuzi, kwa kuzingatia matakwa ya vifungu vya 13(2) na 61(3)(a) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imeruhusu wapiga kura walioandikishwa kwenye Daftari ya Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 na ambao wamepoteza kadi za kupigia kura au zimechakaa au zimeharibika, watumie Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiri na Leseni ya Udereva kupiga kura. 

  Kwa kuwa Wakala wa upigaji kura aliyeandikishwa ndani ya Jimbo la Kinondoni anayohaki ya kupiga kura, na kwa kuwa inawezekana wakawa wamepoteza kadi za kupigia kura au zimeharibika au kuchakaa. Hivyo, mahitaji ya vitambulisho hivyo ni kuwezesha utekelezaji wa matakwa ya vifungu vilivyonukuliwa. 

  Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa, siku ya upigaji kura, baadhi ya mawakala wanao kwenda vituoni siyo Mawakala waliokura kiapo cha kutunza Siri katika Fomu Na. 6 na siyo waliotambulishwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa Msimamizi wa Kituo. 

  Hivyo, tunapenda ieleweke kuwa, endapo itatokea wakala wa upigaji kura aliyepo katika kituo cha kupigia kura siyo aliyeapa kiapo cha kutunza siri na siye aliyetambulishwa na Msimamizi wa Uchaguzi, utakuwa ni ukiukwaji wa Sheria, na atachukuliwa hatua za kisheria mara moja. 

  Hoja ya Tano, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi hajatoa na kuweka wazi kuhusu kituo kikuu cha majumuisho. 

  Ufafanuzi, Tume imejiridhisha kuwa Msimamzi wa Uchaguzi kupitia barua yenye Kumb. Na.KMC/U.21/06/119 ya tarehe 14 Februari, 2018 alivijulisha Vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Kinondoni eneo na muda wa kuanza kujumlisha hesabu za kura. Kwa mujibu wa barua hiyi ambayo CHADEMA walipatiwa, Kituo cha majumuisho ya hesabu za kura ni Biafra na zoezi la majumuisho ya hesabu za kura litaanza majira ya saa kumi na mbili jioni (12:00) siku ya Uchaguzi. 

  Aidha, kupitia barua hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi alivitaka Vyama vya Siasa vyenye wagombea kuwasilisha majina ya Mawakala wa Kujumlisha Kura. 

  Hoja ya Sita, kwamba, Uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo ambao ni Makada wa Chama cha Mapinduzi kutoka Temeke, Ilala na Kinondoni na majina yao kutowekwa hadharani. 

  Ufafanuzi, Kifungu cha 7(4)(5) 2015 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343, ikisomwa pamoja na Kanuni ya 14 na 15 ya Kanuni cha Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 na kipengele cha 10.1.(ii) cha Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea ya mwaka 2015 kwa pamoja umewekwa utaratibu wa namna ya kuwapata Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo na namna Vyama vinavyoshiriki uchaguzi vinavyoweza kuhusishwa katika utaratibu wa kuwapata Watendaji hao. 

  Kwa mujibu wa taarifa ambazo Tume inazo, taratibu zote za kuwapata watendaji hao zilizingatiwa ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi za kazi, waliohitaji kuomba, kuchujwa waliokuwa na sifa zinazohitajika, kufanyika usaili na majina ya walioteuliwa kuwa Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi wa Vituo Wasaidizi kubandikwa kwenye mbao za matangazo katika Ofisi za Kata zote kumi katika Jimbo la Kinondoni. 

  Hata hivyo, kwa mujibu wa barua yenye Kumb. Na. KMC/U21/06/12 ya tarehe 11 Februari, 2018 Msimamzi wa Uchaguzi aliwasilisha orodha ya Watendaji hao kwenye Vyama vinavyoshiriki katika Uchaguzi. 

  Kuhusu, kuwepo kwa wapiga kura 3065 watakaopiga kura na ambao hawakuadikishwa katika Jimbo la Kinondoni. Tunapenda kuwakumbusha kuwa, kifungu cha 63(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kimeweka utaratibu wa nani anayeruhisiwa kupiga kura. Hivyo, hakuna atakayeruhusiwa kupiga kura iwapo hajaandikishwa na jina lake halipo katika orodha ya wapiga kura waliopo katika daftari. 

  Nashukuru kwa ushirikiano wako. 

  Kailima, R.K 

  MKURUGENZI WA UCHAGUZI 

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi, (kulia), akipeana mikono na Meneja Mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari makao makuu ya TPB jijini Dar es Salaam Februari 16, 2018.BENKI ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF), kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. Mradi huo unaoitwa “Digitalizing Informal Savings Mechanisms”
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  BENKI ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF), kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. Mradi huo unaoitwa “Digitalizing Informal Savings Mechanisms” utaendeshwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ambapo TPB inatarajia kuwaunganisha kwenye mfumo rasmi wa kifedha wateja wapya laki Mbili na nusu hadi kufikia mwaka 2020, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 16, 2018.

  Kitangaza mradi huo mbele ya waandisahi wa habari, Bw. Moshingi alisema, mradi huo utaanzia Mkoa wa Ruvuma, na baadae kupelekwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Njombe, Iringa na Morogoro.

  “Watanzania wengi waishio kwenye mikoa ya pembezoni, hususani wenye vipato vidogo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma za kifedha. Kupitia ushirikiano huu na SatF, TPB itawawezesha wananchi kupitia makundi au mtu mmoja mmoja, kujiwekea akiba kupitia teknolojia rahisi na salama isiyowalazimu kwenda kwenye tawi la benki ili kupata huduma hizo za kifedha. Njia hii itawawezesha wananchi kutatua changamoto zao mbalimbali za kifedha na pia kuwaingiza kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi.

  Akifafanua zaidi Bw. Moshingi alisema, Benki ya TPB ni benki ya kwanza hapa nchini kuanzisha utoaji wa huduma za kibenki kwa makundi kupitia simu za mkononi, maarufu TPB POPOTE. Hivi sasa, wateja kupitia vikundi vyao wanaweza kuweka akiba na hata kukopa kupitia simu zao za mkononi.

  Kwa upande wake, Meneja wa mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey, amesema benki ya TPB ndio benki ya kwanza kufanya kazi na taasisi yake hapa nchini, na walivutiwa na namna ambavyo TPB imeonyesha dhamira ya dhati ya kuwasaidia wananchi hao kupata huduma za kifedha.

  Pia, amesema taasisi yake inayo furaha kubwa kupata nafasi ya kufanya kazi na benki ya TPB , taasisi ya fedha yenye sifa na historia ndefu  katika jitihada za kupeleka huduma za kifedha kwa wananchi wake popote walipo. Hii ni fursa nzuri kwa SatF na TPB kujenga umoja imara utakaowawezesha kuwafikia wananchi maskini.

  “SatF ni programu maalum yenye malengo ya kuhakikisha huduma za kifedha za uhakika zinawafikia wananchi wengi walio nje ya mifumo rasmi ya kibenki, programu hii inaratibiwa na shirika la Oxford Policy Management kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya MasterCard Foundation, dhumuni kuu ikiwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi na jamii zenye vipato vya chini kwenye nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara.” Alifafanua Bw. Peachey

  Aidha Bw.Peachey aliendelea kwa kusema kuwa lengo kuu la SatF ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma endelevu za kifedha, na kwa sababu hiyo, wapo tayari kushirikiana na benki ya TPB kwa kutoa msaada wa kifedha na kiufundi.

  “Tunaamini kuwa jitihada tunazofanya zitakuza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi ambao hapo awali walitengwa na huduma hizi, na hivyo kukuza uwezo wao kiuchumi”, alisema.

  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya Finscope mwaka 2017, asilimia 59 ya Watanzania wanavipato vya msimu, na miongoni mwa changamoto zinazowakabili kubwa ni pamoja na uwezo wa kumudu gharama za matibabu, na malipo ya ada za shule kwa ajili ya watoto wao. Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 40 ya Watanzania hukopa fedha kutoka kwa jamaa ama rafiki kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za kifedha zinapojitokeza. Kiasi cha Watanzania Milioni 7.8 wametengwa na huduma za kifedha, na hili limeleta uhitaji mkubwa wa mazingira bora ya kuwawezesha wananchi hao kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha.

   Meneja wa mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey(kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Bw. Sabasaba Moshingi.
  Meneja Mkuu, anayeshuhughulikia masuala ya Kampuni ya TPB Bank, Bi. Noves Moses, akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo.
   Bw. Moshingi, na Bw.Peachey, wakiwa na maafisa wa TPB Bank, na SatF.
   Maafisa wa TPB wakisikiliza

   Bw. Moshingi akifafanua jambo huku Bw. Peachey, (wakwanza kushoto), na Bw.Ignas Jacob kutpoka SatF, wakisikiliza.
  Maafisa wa TPB, wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0


  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga (mwenye kofia) akinyanyua samaki aina ya Jodari mara baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37 ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS Salaam kwa ajili ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki aina ya Jodari na inavua kwa kutumia mishipi. (Picha na John Mapepele).
  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga (mwenye kofia) akipima samaki aina ya Jodari mara baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37 ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS Salaam kwa ajili ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki aina ya Jodari na inavua kwa kutumia mishipi.
  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga (mwenye Kofia) na Katibu Mkuu wa Uvuvi Dkt. Yohana Budeba wakikagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37 ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS Salaam kwa ajili ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki aina ya Jodari na inavua kwa kutumia mishipi (Picha na John Mapepele)


  Na John Mapepele

  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuharakisha mchakato wa kuomba kibali cha Mahakama ili kutaifisha meli ya Kampuni ya Buah Naga One ya nchini Malaysia baada ya mmiliki wa meli hiyo kukaidi amri halali ya Serikali iliyomtaka kulipa faini ya Dola za Kimarekani 350,000 sawa na sh milioni 770 ndani ya siku saba baada ya kubainika kukiuka Kanuni ya 66 ya Kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

  Mpina amesema, Januari 25 mwaka huu meli hiyo ilikutwa na makosa mawili ambayo ni kukutwa na mapezi na mikia ya samaki aina ya papa 30 bila kuwepo miili yake na Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan raia wa Malaysia kukutwa na bastola aina ya Bereta na risasi kumi ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha sheria.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37 ya nchini China kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi ambapo aliipongeza kwa kufuata taratibu za kimataifa za ukaguzi, Waziri Mpina aliagiza vyombo vya dola kuisaka na kuichukulia hatua kali za kisheria meli ya Kampuni ya Tai Hong No. 1 ambayo pia ilikaguliwa na kukutwa na mikia ya papa 44 bila kuwa na miili yake kinyume cha sheria za uvuvi.

  Waziri Mpina alisema meli hiyo ilitoweka katika mazingira ya kutatanisha na kuagiza vyombo vya dola kufuatilia ili ikamatwe na hatimaye ifikishwe katika vyombo vya sheria.“Tutahakikisha meli hii tunaikamata ili sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa bahari ya Tanzania siyo shamba la bibi” alisisitiza Mpina

  Katika hatua nyingine Waziri Mpina amevitaka vyombo vya dola kuzisaka hadi kuzipata meli nyingine 16 zilizopewa leseni ya kuvua katika bahari ya Tanzania ambazo zilitoroshwa na wenye meli kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu mara baada ya kuanza kwa operesheni Jodari aliyoiunda hivi karibuni iliyojumuisha vyombo mbalimbali vya Serikali kudhibiti uvuvi haramu.

  Waziri Mpina alisema doria hiyo pia inalenga kudhibiti utoroshaji wa samaki na mazao yake, kudhibiti biashara haramu ya madawa ya kulevya, biashara ya binadamu, usafirishaji wa silaha na magendo, utupaji wa taka hatarishi kutoka katika meli na uhalifu wowote unaoweza kujitokeza katika maji ya nchi yetu.

  Aidha Mpina alisema jumla ya meli 24 zilipewa leseni ya uvuvi wa bahari kuu ambapo hadi sasa ni meli 8 tu ndizo zilizokaguliwa huku 16 zikitoroshwa.Waziri Mpina aliyataja baadhi ya maeneo manne ambayo Serikali imeyafanyia maboresho katika marekebisho ya Kanuni za uvuvi za mwaka 2009 na kuweka vifungu vipya ambavyo vitasaidia Serikali kudhibiti uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi kuwa ni pamoja na;

  Kufanya ukaguzi wa meli zote zinazokuja kuvua nchini kabla ya kuanza kuvua na baada ya kumaliza kuvua ili kubaini idadi halisi ya kiasi cha raslimali za uvuvi inayovunwa na kutozwa kodi halisi ili kuinua pato la taifa.

  Kupakia asilimia 10 ya mabaharia wazawa katika kila meli inayokuja kuvua katika maji ya Tanzania ili kuwajengea uwezo na na kuwapatia ajira. Kushusha samaki waliovuliwa bila kutarajiwa na kukabidhi katika kwa Serikali kwa vile ni mali ya serikali ili wauziwe wananchi kwa taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa mnada.

  Pia kutoza mrabaha wa dola za kimarekani 0.4 kwa kila kilo ya samaki walengwa(targeted species) kuongeza pato la nchi.Wakala wa meli ya XISHIJI 37 nchini Abdulkarim Karia Maina kutoka kampuni ya Scaforth Gereral Agencies ya jijini Dar es Salaam amesifu juhudi zinazofanywa na Waziri Mpina katika kudhibiti meli zilizokuwa zinalihujumu taifa kwa kutofuata taratibu na kusema kuwa zinapashwa kuigwa na watumishi wote katika Wizara yake.

  “Mageuzi yanaofanywa na Mheshimiwa Mpina katika kudhibiti uvuvi haramu nchini yataleta mapinduzi makubwa katika sekta katika siku za hivi karibuni na kuliingizia taifa mapato makubwa” alisisitiza Maina

  Naye Katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba alisifu miongozo inayotolewa na Waziri Mpina kuendeleza Sekta ya Uvuvi na kuahidi kusimamia kikamilifu maelekezo yote ili sekta iweze kuchangia inavyositahili kwenye uchumi wa nchi yetu.

  Kwa upande wake, Bw. Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Dawati linalohusiana na Makosa ya Mazingira, amesisitiza kuwa Tanzania imejizatiti kuhakikisha kwamba Sheria zinachukua mkondo wake ili kudhibiti uhalifu wowote unaotokea katika bahari ya Tanzania.

  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kulia) akimkabidi Mariam Akida (kati) mkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea. Kushoto ni Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.

  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakabidhi baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaonunua bando za intaneti kupitia menu *147*00* wanapata bonasi za bure hadi GB 1 za intaneti pamoja na fursa ya kushinda simu janja.


  Wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure

  Zaidi ya simu 1,000 bado zinashandaniwa!

  Dar es Salaam, Februari 16, 2018 – Wateja wa kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, wanazidi kufaidi zawadi za simu aina ya Tecno R6 pamoja na bonasi za data bure katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

  Akitangaza washindi 36 waliopatikana katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu, Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna simu zaidi ya 1,000 zinazoshindaniwa na wateja wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#.

  ‘Kufikia sasa tumepata jumla ya washindi 72 kutoka sehumu mbali mbali za nchi ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Lindi, Mtwara, Zanzibar, Arusha,, Pwani, Dodoma, Mwanza, Singida, Iringa, Mbeya na Tabora. Kwa hiyo nawahamasisha wateja wetu wote nchi nzima wazidi kununua bando za intaneti kuanzia shilingi 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wapate nafasi ya kushinda mojawapo ya simu hizi bora zenye uwezo wa 4G,’ alisema.

  Alibainisha kuwa ofa kabambe ya Nyaka Nyaka ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini.

  Mmoja wa washindi, Ibrahim Mohammed Mtuliya, mkaazi wa Kigamboni Dar es Salaam alisema kuwa simu hiyo itamwezesha kupanua wigo wa biashara yake ya useremala kwa kupiga picha ya bidhaa zake nakuwatumia wateja kupitia mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp na Instagram.

  Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zaidi ya elfu moja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo kila saa.

  Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

  0 0

  Dar es Salaam – Etihad Airways sponsored the Chinese Chamber of Commerce of Kaiakoo’s Chinese New Year event to mark the Year of the Dog. 

  The prestigious event was held at Zhonghua Huiguan Chinese restaurant and attracted nearly 300 guests.

  Attendees who joined Etihad Guest, the frequent flyer programme of Etihad Airways, went into a draw to win return tickets from Dar es Salaam to Abu Dhabi.

  Grand prize winner Jiang Yong Tao was congratulated by Allen Okoromu, Etihad Airways Country Manager Tanzania.

  Etihad Airways offers direct flights between Dar Es Salaam and the UAE capital, where passengers can easily connect to Chinese cities Beijing, Shanghai and Chengdu, as well as Hong Kong.

  Guests travelling on Etihad Airways will experience the airline’s award-winning service by multinational cabin crew and onboard nannies, extensive inflight entertainment selections, and a choice of complimentary international meals and beverages. Those travelling from Africa are entitled to generous baggage allowances of xxkg in Economy class and xxkg

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Makontena 20 Kati ya 36 yenye samani (furniture) zenye thamani ya Shillingi Billion 2 zilizotolewa na Diaspora waishio Nchini Marekani waliounga mkono kampeni ya RC Makonda ya ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam.

  Ndani ya Kontena hizo zipo Meza za umeme zenye hadhi ya kimataifa 2500, Meza za kawaida 2500,Viti zaidi ya 5,000,Makabati makubwa ya vitabu 1300, Ubao za kisasa (writing board) zisizotumia chaki 700 ambazo kwa kiasi kikubwa utaenda kupunguza mateso ya walimu kuumwa vifua kutokana na vumbi la chaki.
  IMG-20180216-WA0072
  Vifaa hivyo vya kisasa vimetolewa na Jumuiya ya watanzania waishio Marekani ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington iliyomuunga mkono RC Makonda kutokana na kuguswa na kazi kubwa anayoifanya kwenye kuboresha mazingira ya walimu.
  IMG-20180216-WA0073
  Akizungumza wakati wa kupokea makontena hayo RC Makonda amesema jumla ya kontena zilizotolewa na jumuiya hiyo ni 36 na Kati ya hiyo 20 yamefika na mengine 16 yapo njiani ambapo ameshukuru jumuiya kwa kutambua thamani ya mwalimu.

  RC Makonda amesema lengo lake ni kuboresha mazingira ya walimu na kurejesha heshima yao ili  wapate morali ya kufundisha wanafunzi na mwisho wa siku kusaidia taifa kuwa na wataalamu wa kutosha. 
  IMG-20180216-WA0071
  Aidha ameshukuru Bank ya Walimu kwa kusaidia kulipia usafirishaji wa makontena matatu na kuwaomba wadau kusaidia kulipia gharama za usafiri wa makontena mengine Kama mchango wa kutambua thamani ya mwalimu.
  Walimu walioshuhudia makontena hayo wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyoboresha mazingira yao ya kufanya kazi na kueleza kuwa vifaa walivyovishuhudia leo wanaamini sasa watafanya kazi kwa bidii zaidi na kuongeza ufaulu kwa walimu.

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthoy Mtaka(kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na Wilaya ya Meatu wakiondoka eneo la mradi wa maji wa Itinje mara baada ya kukagua mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akitoa maelezo juu ya mradi wa Lubiga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akihoji jambo juu ya ujenzi wa tanki katika mradi wa Maji wa Itinje wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.
  Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akifafanua jambo wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani humo
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo akifafanua jambo wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimsikiliza Katibu wa Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Bukundi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu  Mchungaji Daniel Philimoni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Nselema Associtates Co. Ltd anayetekeleza mradi wa Lubiga akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu  Mwanasheria wa Mkoa wa Simiyu, Bi.Mwanahamisi Kawega akifafanua jambo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka baada ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.  Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Seksheni ya Maji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, akifafanua jambo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka baada ya kukagua miradi ya maji wilayani Meatu.  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa akifafanua jambo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka baada ya kukagua miradi ya maji wilayani humo.  Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, John Lugembe akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani humo.

  ………….

  Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesitisha malipo ya shilingi bilioni 1.9 kwa wakandarasi watatu, ambao ni Simiyu Investiment Co. Ltd, Nselema Associtates Co. Ltd na Great Lakes Construction Co.LTD, wanaotekeleza miradi saba ya maji wilayani MEATU ambayo imeshindwa kukamilika tangu mwaka 2014.

  Agizo hilo amelitoa wilayani Meatu, mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Lubiga, Itinje na Bukundi na kutoridhishwa na kazi iliyofanyika.

  “Tunasitisha malipo yote ya wakandarasi watatu wanatekeleza miradi saba ya maji ndani ya Wilaya ya Meatu, malipo yafanyike baada ya Wataalam wetu wanasheria, wahandisi wa maji wa Halmashauri ya Meatu, Mhandisi wa Maji Mkoa, Mwanasheria ya Mkoa na timu ya Mkoa kujiridhisha; ikiwa wanastahili kulipwa watalipwa ikibainika hawana sifa tunavunja mkataba” alisisitiza Mtaka.

  Pamoja na kusitisha malipo hayo Mtaka amesema makampuni hayo hayataruhusiwa kufanya kazi za ukandarasi katika miradi yoyote wilayani humo.

  Katika hatua nyingine Mtaka amewataka Viongozi wa Kisiasa wilayani Meatu wanaomiliki Makampuni ya Ukandarasi kuacha mara moja kuomba kazi za ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo, badala yake waombe katika Halmashauri jirani Mkoani humo ili kuepuka mgongano wa kimaslahi.

  Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi hao wa kisiasa ya kuwapigia simu watumishi wa Halmashauri kwa lengo la kuomba kazi au kudai malipo ya kazi zao na akawahadharisha kuwa endapo hawataacha tabia hii majina yao yatawekwa wazi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Ndg.Fabian Manoza amesema kuwa wakandarasi hao waliochaguliwa na bodi ya zabuni na kupitishwa katika vikao vya baraza la madiwani kutekeleza miradi hiyo hawana uwezo.

  “Wakandarasi wanaotekeleza miradi hii hawana uwezo wanasubiri walipwe ndiyo kazi ifanyike, pia nikiri kuwa ni kweli kabisa miradi hii inatekelezwa na wanasiasa ndiyo maana hii Halmashauri ya Meatu kuiongoza tunapata shida sana, pale unaposimamia sheria unaitwa kwenye vikao na kuazimiwa, lakini kama viongozi hasa tulioteuliwa tutasimamia sheria na taratibu” alisema Manoza.

  Naye Afisa Ugavi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Manunuzi Ndg. Emmanuel Marwa amesema kuwa taratibu za manunuzi hazikufuatwa katika upatikanaji wa wakandarasi hao ikiwa ni pamoja na Kampuni moja kupewa kusaini mkataba wa kazi zaidi ya moja.

  Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani, ameunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kusitisha malipo na kuangalia namna ya kuvunja mikataba itakapobidi na akabainisha kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto katika utekelezaji wa sheria na maelekezo mbalimbali kutokana na baadhi ya viongozi kuingilia utekelezaji, hivyo ni vema hatua zichukuliwe.

  0 0

  Na-Jumbe Ismailly MANYONI  

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida imemuhukumu Musa Haruna (47) mkazi wa Kijiji cha Mtimkavu,kata ya Itigi,wilayani Manyoni kutumikia adhabu ya mwaka mmoja jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa bomba tatu za chuma zenye thamani ya shilingi milioni mbili laki mbili elfu na themanini mali ya Wakala wa barabara Tanzania(TANROADS).
  Mahakama hiyo ilimtia hatiani mshitakiwa baada ya kukiri na kukubaliana na hoja zote za mashtaka,ikiewemo kukamatwa na bomba tatu za chuma zilizopatikana kwa njia isiyo halali,kufikishwa polisi na kufikishwa Mahakamani.
  Awali Mwendesha Mashtaka wa serikali,Geofrey Luhanga alidai kwamba sept,23,mwaka jana saa 1;30 usiku katika eneo la mtaa wa Majengo,mjini Itigi,Musa Haruna alikutwa na bomba za chuma tatu zenye thamani ya shilingi milioni 2 na laki mbili elfu na themanini zilizopatikana kwa njia isiyo halali mali ya Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS).
  Aidha Luhanga alidai pia kwamba hakuna kumbukumbu za makosa ya nyuma hivyo aliiomba Mahakama hiyo kwamba adhabu zinazotolewa na Mahakama kwa makosa ya aina hiyo ziwe kali ili ziwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
  Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka huyo wa serikali mabomba hayo yalikuwa yakitumika kwa alama mbali mbali za barabarani na makosa hayo yamefanywa kwa makusudi na mshitakiwa huyo na kutokana na kukosekana kwa alama hizo imekuwa vigumu kwa watumiaji barabara kujua maeneo hatarishi kwa kuwa hakuna alama zinazoonyesha tahadhari hizo.
  Hata hivyo Luhanga alidai pia kwamba serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya alama za barabarani na alama hizo hutumika kwa raia wote,hivyo kuziondoa ni kuwanyima haki raia wengine.
  Katika maombolezi yake mshitakiwa kabla ya kusomewa adhabu hiyo,mshitakiwa alisema yeye binafsi hajaiba bomba hizo bali aliuziwa na mtu bila kujua kama bomba hizo ni mali ya serikali kwa ajili ya matumizi ya barabarani,hoja ambayo ilipingwa na Hakimu huyo kwamba haina mashiko kwa wakati huo.
  Hata hivyo Haruna alisema kuwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa presha ya kushuka hivyo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu na vile vile hilo ni kosa lake la kwanza hivyo Mahakama imfikiria na kumpunguzia na kumfikiria kumpa adhabu ndogo kutokana na matatizo hayo yanayomkabili.
  Kabla yaa kutoa hukumu ya adhabu hiyo,Hakimu   Mkazi Mfawidhi,Ferdinand Kiwonde aliweka bayana kwamba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili ameridhishwa kuwa mshitakiwa ni mkosaji  wa mara ya kwanza,ana presha ya kushuka lakini hakuwa na kielelezo chochote cha ushahidi wa kuthibitisha ugonjwa huo.
  Hivyo Hakimu Kiwonde alisisitiza kwamba kisheria adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha miaka mitatu jela,lakini kwa sababu hakuna kumbukumbu zozote za nyuma zinazoonyesha kuwa mshitakiwa huyo ni mkosaji mzoefu,hivyo Mahakama hiyo inampunguzia adhabu yake.
  Akitoa hukumu,Hakimu wa Mahakama hiyo Kiwonde alimuhukumu Haruna Musa kuanza kutumikia adhabu ya mwaka mmojaa jela kwa kosa la wizi huo wa bomba tatu za alama za barabarani na kwamba yeyote Yule ambaye hatakuwa ameridhishwa na hukumu hiyo ana haki ya kukata rufaa.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Gemen Engineering & Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori (kulia), alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti, Mkoani Mara.
  Muonekano wa Daraja la Mto Mara lenye urefu wa Mita 94 na kuunganisha Wilaya za Tarime na Serengeti likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Bertha Bankwa, wakati akikagua kiwanja hicho. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wa pili kulia) mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti, Mkoani Mara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), kuhusu eneo ambalo litachukuliwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, mkoani humo.
  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Bertha Bankwa, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa eneo ambalo litajengwa jengo la abiria, wakati akikagua maendeleo kiwanja hicho, Mkoani Mara.
  Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Musoma, ambacho kipo katika mpango wa upanuzina uboreshaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, taa pamoja na jengo la jipya la abiria.  Serikali imesema ujenzi wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 lililopo katika barabara ya Tarime-Mugumu-Nata litakamilika mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.

  Amezungumza hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya ya Tarime na Serengeti na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hizo kuwa endapo daraja hilo likikamilika litaondosha adha waliyokuwa wanaipata ya kuvuka hasa vipindi vya masika.

  “Niwahakikishieni daraja hili litamalizika mapema mwezi wa nne pia nimemuagiza mkandarasi huyu ambaye ni mzawa kuhakikisha anazingatia viwango na wakati” amesema Prof. Mbarawa.Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo itakuwa dira kwa wakandarasi wazawa kupewa miradi mikubwa kwani pamekuwa na changamoto kwenye utekelezaji wa miradi hususani kwa wakandarasi wazawa.

  Kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya M/S Gemen Engineering & Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori, amesema kuwa mradi umekamilika kwa sehemu kubwa hivyo kazi zilizobakia ni kutandika vyuma juu ya daraja ili likamilike na kuanza kutumika na hivyo kuiomba Serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapa miradi mingine mikubwa.

  “Nikuhakikishie Mhe Waziri mradi huu utakamilika kwa viwango hivyo naomba utuamini na hata zikitokea kazi nyingine naomba tupewe kipaumbele wa kuzitekeleza kwa kuwa tunaweza”, alisisitiza Mhandisi Nyamtori.

  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara Mhandisi Mlima Ngaile, amesema watahakikisha wanamsimamia vizuri mkandarasi ili aweze kutekeleza mradi huo kwa viwango vyote. 

  Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa, amekagua kiwanja cha ndege cha Musoma na kueleza kuwa Serikali tayari imeshatangaza zabuni ya upanuzi wa kiwanja hicho na kuwa wakati wowote zabuni zitafunguliwa ili mzabuni kuweza kupatikana.

  Naye Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma aliemaliza muda wake Bi. Bertha Bankwa, amesema kuwa tayari Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) imeshaainisha hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata mkandarasi ili upanuzi na uboreshaji uanze.

  Ameongeza kuwa wameshamaliza zoezi la kupitia tathimini za fidia za mali za wananchi watakaothiriwa na upanuzi wa uwanja huo ambapo jumla ya wananchi 135 wameashafanyiwa tathimini hiyo.Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ikiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0


  Afisa Masoko wa Umoja Swich,(Beatrice Emmanuel) akimkabidhi Nd, Muhunzi Kisome,(Kushoto) zawadi ya fedha taslim shil.Mil. 1 alizoshinda katika droo ya pili ya shinda na Umoja Swich

  Kapuni ya Umoja switch leo imewazawadia washindi wake zawadi walizoshinda kwenye droo ya pili ya Shinda na Umoja Switch iliyochezeshwa February 2 mwaka huuKatika droo hiyo ya pili ilitoa washindi katika vipengele vinne ambavyo ni, washindi wawili wa fedha taslimu Milioni moja, mshindi wa fedha taslim mara mbili ya muamala aliyofanya kwenye ATMs za UmojaSwitch, washindi wanne wa Simu za mkononi (Smart phones) na washindi zaidi ya 20 wa T-shirt za UmojaSwitch

  Akiwakabidhi zawadi hizo za afisa masoko wa Umoja Switch Umoja Beatrice Emmanuel amesema anawashukuru wateja wa Umoja Switch kwa kuendelea kutumia kadi za Umoja Switch na amewataka wale ambao hawajabadili kadi zao wafike kwenye Benki zao ili kubadilisha kadi zao na waingie kwenye droo ya Pili ya Promosheni hii ya Shinda na Umoja Switch
  Felister Japhet, akipokea zawadi yake ya simu ya mkononi(smart phone) toka kwa Afisa masoko waUmoja Swich Beatrice Emmanuel , aliyoshinda katika droo ya pili ya shinda na umoja switch

  Akizungumza na Fahari News kwa niaba ya washindi wenzake Bwana Muhunzi Kisome ambae ndio mshindi wa Milioni moja, mfanya biashara kutoka Chamanzi Jijini Dar es salaam amesema hakutegema kama angekuwa mshindi wa fedha hizo na wakati amepigiwa simu alipuuza mpaka alipoamua kujidhihirishia kwa kuangalia kama kweli kuna Droo ya Shinda na Umoja Switch inayochezeshwa kupitia Simu yake

  “kiukweli siku amini mara ya kwana mpaka nikaingia kwenye internet kuhakikisha, walivyonipigia simu mara ya pili ndo nikafika hapa na nimeamini baada ya kuona na waandishi wa habari wapo hapa, pesa yangu nitaifanyia kitu ambacho kitakua ni kukbukumbu na shukrani kwa kampuni ya UmojaSwitch” alisema Kisome
  fisa Masoko wa Umoja Switch, Beatrice William akiwa pamoja na baadhi ya washind wa droo ya pili ya shinda na Umoja.

  Kampuni ya umoja Switch imekua ikitoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na mabemki zaidi ya 20 nchini kwa njia ya kielectronic ili kuwarahisihia wateja wa mabenki njia rahisi za kufanya miamala kwa kutumia ATMs za Umoja Switch zilizosammbaa Tanzania Nzima

  0 0


  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe (kulia) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa Mamlaka inayotoa huduma bora za Maji Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) ,Prof. Faustine Bee. Kushoto ni Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa MUWSA, Joyce Msiru. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma juzi.
                                                                  ******************
  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,Aisack Kamwelwe ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuukagua mradi wa maji wa Buchosa uliopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kwani anazotaarifa kuna vifaa vimenunuliwa havina ubora kabisa.

  Maagizo hayo aliyatoa jana Mjini hapa wakati akizindua ripoti na utendaji wa Mamlaka za Maji za Miji na Mikoa na miradi ya kitaifa.

  Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo Mamlaka ya Maji ya Moshi ilichaguliwa kuwa ya kwanza kwa utoaji bora wa huduma za maji.

  Waziri Kamwelwe alisema alienda kuungalia mradi wa Buchosa na kutoridhishwa nao kutokana na mabomba yaliyonunuliwa kutokuwa na ubora hivyo ameiagiza Takukuru wakaungalie ili kujua ubadhilifu uliofanyika.

  “Bosi wa Takukuru upo hapa siwezi kukuagiza lakini kuna huu mradi wa maji wa Buchosa mabomba yaliyonunuliwa ni ya Class B wakati mabomba hayo yanatumika sehemu ambayo maji hayana ‘Pressure’ pamoja na kwenye majitaka,”alisema Kamwelwe.

  Aidha Waziri Kamwelwe ameziagiza Mamlaka za Maji kutafuta maeneo kwa ajili ya kutupa maji taka ili kupunguza magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu.

  “Hasa kwenye Mji Mkuu kama hapa Dodoma ni lazima tutenge maeneo kwa ajili ya maji taka,”alisema Kamwelwe.

  Katika hatua nyingine, Waziri Kamwelwe ametoa mwaka mmoja kwa Mamlaka za Maji za Lindi,Mpanda,Bariadi na Geita kujitathmini na kubadilika kwani haridhishwi na utendaji kazi wao.

  ‘Niwashauri msitukimbie wazee kwenye maamuzi yenu sio mtu anatoka Chuo miaka mitatu tu anapewa mradi lazima ataharibu kwani hana uzoefu,’alisema

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura,Profesa Jamidu Katima alisema utoaji wa huduma za maji taka ni tatizo nchini kutokana na kutolewa na sekta binafsi.

  ‘Lazima tuweke utaratibu ukiwemo wa kutibu maji ili kuondoa tatizo la ugonjwa wa Kipindupindu,”alisema

  Naye Mwenyekiti wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Moshi (MUWSA) Profesa FaustiNE Bee ambao ndio washindi wa wanaotoa huduma bora za maji,alisema usafi unaopatikana katika Mji huo unasababishwa na upatikanaji wa maji.

  “Kwa sasa maji upatikanaji wa maji ni kwa masaa 23.5 hapo tunakosa 0.5 ndani ya masaa 24, hivyo tumejipanga kuhakikisha hiyo 0.5 tunaiondoa na kuwa masaa yote maji yanapatikana katika Mji wa Moshi,”alisema

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa EWURA Mchami alisema uzalishaji wa maji safi kwa sasa umeongeza toka lita 248 hadi 276 kwa 2016/2017, jambo ambalo linatia moyo kutokana na hali hiyo.

  Alisema kutokana na hilo hata wateja pia wameongezeka kwa sababu lita za ujazo zimeongezeka kutokana na kuwa mamlaka zinafanya kazi kwa karibu na wateja wao wa maji hapa nchini.

  Hata hivyo Waziri aliwapongeza mamlaka hizo kutokana na utendaji uliashiria kwamba wanawajali wateja na kuwataka waongeze bidii zaidi.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wakutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

  Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam .Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

  “Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa, Balozi Slaa alifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga akiwa tayari kuelekea kwenye kituo chake kipya cha kazi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto aliyefika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo kipya cha kazi, katikati ni Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0


  Chama cha Urafiki wa Wananchi wa Nchi ya Tanzania Na Msumbiji TAMOFA Kimempa Ubalozi Bondia wa Kimataifa Francis Cheka Ili kuweza Kutangaza Chama Hicho kwa lengo la Kujipatia wafadhili ndani na nje ya nchi.

  Akiongea mara baada ya makabidhiano ya kadi ya ubalozi Mkoani Mtwara Francis Cheka anasema Urafiki wa msumbiji na Tanzania Umekuwa wa Muda Mrefu na hivyo kuhamasisha wananchii kujiunga na chama hicho hasa wale wanaofanya safari katika nchi hizo mbili.

  Hamza Lichete ni katibu mwenezi wa TAMOFA anasema kazi kubwa ya chama hicho ni kuimarisha Mahusiano pamoja na kulinda  Umoja  kati ya nchi hizi mbili kwa lengo la kuimarisha uchumi pamoja na amani.

  Cheka ambaye kwa sasa anaishi Mkoani Mtwara amezaliwa Nchini Msumbiji lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akiitangaza Tanzania katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa ambayo yamempatia umaarufu yeye pamoja  Na Nchi ya Tanzania

  Chama cha TAMOFA kiliasisiwa na marasi Hayati Jullius Kambarage Nyerere pamoja na Samora Mashel mwaka 1987.
  Bondia Francis Cheka akiwa amesimama Mbele ya Jengo la Ofisi ya TAMOFA maara baada ya Kupewa Ubalozi wa Chama Hicho Mkoani Mtwara.
   Bondia Francis Cheka akionesha Kadi ya Ubalozi wa TAMOFA kwa Waandishi wa Habari Mara Baada ya Kukabidhiwa Mkoani Mtwara.
  Picha1.Mwenyekiti wa TAMOFA Kanda ya Kusini Seleman Mstapha Akimkabidhi Kadi ya Ubalozi wa TAMOFS bondia Francis Cheka Mkoani Mtwara.

  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Makulunge iliyopo kata ya kiluvuya katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea shule na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili.
  Waziri wan chi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziaara yake ya kikazi aliyoifanya katika kaata ya Kiluvya kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
  Mmoja wa walimu wa shule ya sekondari Makuunge Ester Matemu akizungumza kuhusiana na changamoto ambayo ianwakabili ya ukosefu wa vyoo,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

  ……………………………………………………………………….

  VICTOR MASANGU, KISARAWE 

  WANAFUNZI wapatao 472 na walimu zaidi ya 25 katika shule ya sekondari Makulunge iliyopo katika kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa sasa wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo UTI,na kipindu pindu kutokana na vyoo ambavyo wanavitumia kwa sasa vipo katika mazingira hatarishi na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo wakati mwingine inawalazimu kwenda kujisaidia katika maeneo mengine.

  Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ambayo imefanyika katika kata ya Kiluvya na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambapo baada ya kutembelea shule hiyo ya sekondari ameweza kubaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya walimu wa shule hiyo kutokuwa na choo chao hivyo kuchangia na wanafunzi wao.

  Wakizungumza kwa masikitiko wanafunzi hao akiwemo Waziri Mwinjuma na Zuwena Mohamed wamebainisha kwamba kwa sasa wanapata shida kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu ya miundombinu ya vyoo na kwamba kunahatarisha usalama wa afya zao kutoka na kukithiri kwa uchafu pamoja na miundimbinu kuwa mibovu na baadhi ya vyoo hazina milango na sehemu za ukuta zimeanza kubomoka.

  Walisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya wanafunzi wengine hususan wa kike wanapata ugonjwa wa UTI kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na matundu ya vyoo yaliyopo hivyo wakati mwingine wanafunzi kujisaidia sehemu ambayo sio salama kabisa.

  “Kwa kweli shule yetu kwa sasa tunakabiliwa na chanagmoo ya vyoo kwani ukizingatia idadi ya wanafunzi tuliopo ni wengi sana, na matundu ya vyoo yaliyopo ni machache maana kwa upande wa wavulana matundu yapo manne tu, na kwa wasichana hivyo hivyo, kwa hiyo tunachangai vyoo vyetu pamaja na walimu na ukizingatia vipo katika mazingira machafu,havina milango na miundombinu yake ni mibovu, walisema wanafunzi hao.

  Nao baadhi ya walimu hao hususan wakike wakitoa kero hiyo akiwemo Merry Godfrey na Ester Matemu wamesema kwamba kwa upande wao hawana vyoo kabisa kwani vilivyopo ni vyawaanafunzi na vipo katika hali mbaya hivyo inawalazimu kuchangia na wanafunzi wao na wakati mwingine wanaogopa kuingia kujisaidia kutokana na kuwepo kwa wadudu wakali kama vile nyoka.

  Aidha walimu hao kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha wanawajengea vyoo ili waweze kuwa katika mazingira ambayo ni rafiki kwa upande wao kuliko ilivyo kwa sasa kwani ni hatari kwa usalama wa afya zao. 

  Kufuatia kuwepo kwa kilio hicho Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha wanaanza jitihada za ujenzi wa matundu ya vyoo mara moja kwa lengo la kuweza kuwaepusha wanafunzi na walimu wa shule hiyo wasiweze kupata magonjwa ya mlipuko na madhara mengine.

  “Hii hali kwa kweli mimi kwa upande wangu siwezi kuivumilia hata kidogo maana haiwezekani watendaji mpo na mnashindwa kutekeleza majukumu yenu ipasavyo, haiwezekana shule kama hiii ya sekondari ya makulunge walimu kukosa vyoo, hii ni hatari sana na wanafunzi vyoo vyao navyo vipo katika mazingira hatarishi hivyo namuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe kulifanyia kazi suala hili haraka iwezekanavyo kwa kujenga vyoo,”alisema Jafo.

  Pia Waziri Jafo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi wa ngazi zote hivyo asingependa kuona wanafunzi na walimu wanasoma katika mazingira magumu, na kuahidi kulivaia njuga sualaa hilo kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika suala zima la elimu.

  SHULE ya sekondari ya Makuiunge iliyopo katika halmasauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambayo ina jumla ya wanafunzi wapatao 472 inakabiliwa na uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo, pamoja na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo kunahatarisha usalama wa walimu na wanafunzi wao katika suala zima la afya zao kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko.

older | 1 | .... | 1519 | 1520 | (Page 1521) | 1522 | 1523 | .... | 1898 | newer