Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1521 | 1522 | (Page 1523) | 1524 | 1525 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  WAAJIRI  wa kampuni nne tofauti wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini  Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa kadhaa yakiwemo ya kushindwa kujisajili na kuwasilisha taarifa za shughuli wanazozifanya kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi [WCF].

  Washtakiwa hao, Malakkara Semis na Shafeek M. Purayil ni Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya SPASH  INTENATIONAL CO. LTD. Silas Shemdoe na Deusdedit Samwel Kibassa ambao ni  Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya ENCC CONSULTANTS.

  Wengine ni Wakurugenzi Watendaji wa LASAR LOGISTIC, Abshir Farah Gure na Farhiya Hersiwarsame, wakati Mshtakiwa mwingine ni Josephat Alexander ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KAMANDA SECURITY GUARDS CO. LTD.

   Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na waendesha mashtaka tofauti wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Emilly Kiria mbele ya Hakimu Mfawidhi Victoria Nongwa. Wanashtakiwa kinyume cha Kifungu  cha 71 (1) (a) na 71 (4) cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi Sura ya 263 marejeo ya mwaka 2015.

  Akisoma mashtaka yanayomkabili Joseph inadaiwa  Januari, mwaka 2018 walishindwa kujisajili na kutoa taarifa muhimu za shughuli zake na za wafanyakazi kwa Ofisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.

  Ilidaiwa Januari 11, mwaka 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kutoa taarifa mihimu za waajiriwa wake ikiwamo majina na mishahara ya wafanyakazi.

  Katika kesi ya jinai namba 33 ya mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi  alidai washtakiwa  Malakhara Semis  na Shafeek Purayil  wa kampuni ya Spash International Co.Ltd  Desemba 25,mwaka 2017 walishindwa kusajili na kutoka taarifa muhimu za shughuli za kampuni kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF.

  Pia walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi wao kwa Ofisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF ambapo Septemba 6,mwaka 2017  washtakiwa hao walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi ikiwamo majina na mishahara.

  Wakati kesi hiyo ikisomwa Malakhara hakuwapo mahakamani.

  Katika kesi nyingine, wakili wa Serikali, Emma Msofe amedai washtakiwa Abshir Gure na Farhiya Warsame wa kampuni ya Lasar Logistic Limited, walishindwa kusajili na kupeleka taarifa muhimu kwa Mfuko wa WCF.

  Alidai kuwa Oktoba 19,mwaka 2017 walishindwa kutoa taarifa muhimu zikiwamo majina na mishahara. Pia wanadaiwa Novemba 27,mwaka 2017 walishindwa kupelekwa taarifa za mfanyakazi wao, Lihikambo  Yunus ikiwamo kitambulisho cha Taifa, cha mpiga kura, leseni, mkataba wa ajira, taarifa za msharaha na taarifa ya polisi kwa afisa wa mfuko wa WCF.

  Wakati kesi hiyo ikisomwa Abshir alikuwapo mahakamani lakini Farhiya hakuwapo.

  Katika kesi namba 35,mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi Derrick Mukabatunzi alisisimama mahakamani hapo na Kuwaita washtakiwa Riziki Shemdoe na Deusdedit Kibassa ambapo wakili huyo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa mmoja hakuweza kumpata na kwamba mwingine alikuwa akiuguliwa na mkewe Dodoma.

  Hata hivyo, Mahakama imetoa hati za wito za Kuwataka mahakamani washtakiwa hao.

  Washtakiwa wote wamekana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika.

  Hakimu Nongwa alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo kila mdhamini atasaini ahadi ya Sh 50 milioni, washtakiwa wote, wako nje kwa dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Februari 22,mwaka 2018 ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali (PH).

  Akizungumza nje ya Mahakama Mwanasheria wa WCF, Deo Victor alisema kabla ya Mfuko  huo kuchukua hatua hii ya kuwafikisha  mahakamani, washtakiwa walipewa taarifa ya kutekeleza takwa hilo la kisheria katika tarehe mbalimbali, kati ya Septemba 2017 hadi Januari mwaka 2018 lakini walishindwa kutekeleza.
    Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya Spash International Co  Ltd  Shafeek Purayil (kulia) na Japhet Alexander  wa Kampuni ya Kamanda Security Guard Co. Ltd, wakipelekwa mahabusu ya Mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2018 baada ya kusomewa mashtaka mawili ya jinai kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na kuwasilisha taarifa za shughuli za Makampuni wanayoyaongoza kwa Mfuko huo. Washtakiwa wakipatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka mitano (5), jela au faini isiyozidi shilingi milioni hamsini au vyote kwa pamoja.


  Shafeek Purayil(mbele) na Japhet Alexander wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashtaka na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bibi Victoria Nongwa.  
   Shafeek  Purayil
  Meneja Matekelezo (Compliance Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Victor Luvena akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo. Alisema washtakiwa wengine Zaidi watapandishwa kizimbani Jumanne Februari 20, 2018 kwa makosa hayo hayo. Kulia ni Mwanasheria wa WCF, Bw. Deo Ngowi.
  Meneja Matekelezo (Compliance Manager),  wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Victor Luvena akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo. Alisema washtakiwa wengine Zaidi watapandishwa kizimbani Jumanne Februari 20, 2018 kwa makosa hayo hayo.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu 
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wanaofundisha katika kata ya Ihalimba katika jimbo la Mufindi Kaskazini 


  Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi. 

  Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

  “Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

  Mgimwa alieleza maeneo ambayo ametoa bati na mifuko ya saruji kuwa ni shule ya msingi Nundwe Bati 160 kwaajili ya nyumba ya walimu 60 na ukarabati wa paa la madarasa, bati 100. shule ya msingi Vikula bati 100 na saruji 50, shule ya msingi Mong'a bati 50,Zahanati ya Ugesa bati 30 na saruji 40 kwaajili ya nyumba ya mganga wa kijiji cha Wami, ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Mbalwe bati 100 na saruji 20,Ihalimba sekondari nyumba ya mganga bati 50 na fedha tshs 1,100,000 kwaajili ya dari jengo la maabara na kununua pampu ya maji.

  “Hizi ni gharama ni kata moja tu ya Ihalimba ambazo nimezitafuta nako kujua mimi hivyo lazima walimu mjue kuwa kuwa mbunge ni kazi kubwa sana na lengo la kuwa mbunge nikuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo ambayo yanatakiwa kwa wakati sahihi hivyo napenda kuwapa habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kata ya Ihalimba kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa

  Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.

  Aidha Mgimwa aliwataka walimu kumwambia changamoto ambazo wanakumbana nazo ili kuzitatua na kuhakikisha walimu wanafundisha katika mazingira mazuri.

  Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ihalimba wilayani Mufindi mkoani Iringa Award Mahanga amempongeza mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa kwa kuendelea kutatua changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu kwa kuchangia saruji mifuko 200 na bati 590 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule za msingi na sekondari za kata hiyo.

  Mahanga aliesema kuwa mbunge Mgimwa amekuwa akijitoa kwa kutatua changamoto za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika.Aidha Mahanga alisema kuwa mbunge huyo amechangia kwenye sekta ya afya ambapo amefanikisha ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji cha kata hii ya Ihalimba

  Lakini pia Mahanga alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kuahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneno ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.

  “Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Mahanga

  0 0

  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.
  Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio 
  Sehemu ya wanahabari mkoani Tanga wakifuatilia matukio katika mkutano huo  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi.

  Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.Alisema taarifa hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo taarifa zilizo pokelewa ni 174.

  Aidha alisema katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya ardhi 33,vyama vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari (TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu 1.

  Mkuu huyo alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.Aliongeza kuwa taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana na makosa chini ya kuzuia na kupambana na rushwa.

  Hata hivyo alisema katika uendeshaji wa mashitaka takukuru mkoa wa Tanga imefanya uendeshaji wa kesi 18 mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 9 zilifunguliwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2017 na kesi 9 ni za kabla ya Julai 2017.

  Alieleza pia katika kipindi hicho usikilizwaji wa kesi moja huko wilayani Lushoto kwa mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la Ally Mgovi ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Funta ambapo alifikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima.

  Alisema mshtakiwa huyo alipatikana na hatia alihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh Milioni 1.9 ambapo alishindwa kulipa faini hivyo alipelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

  Akizungumzia fedha ambazo zimeokolewa na kazi za uchunguzi na udhibiti ambapo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 kumekuwa na ongezeko la fedha walizookoa na kuzirejesha serikalini kutoka milioni 6,450,000 kwa miezi sita ya mwanzo hadi Milioni 52,508,260.

  Alieleza fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hewa ndani ya mpango wa elimu bila malipo katika shule za sekondari,mishahara hewa na gharama kwa ajili ya semina hewa(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, akifungua mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 19, 2018.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, amewataka madaktari na watoa huduma za afya, wanaohuduria Mafunzo ya siku tano, (5), ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, kuzingatia miiko ya kazi zao wanapotekeleza jukumu hilo.

  Mhe. Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo Februari 19, 2018, wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuwaleta pamoja madaktari zaidi ya 200 wa Kanda ya Kaskazini na kufanyika Mjini Moshi.

  Alisema, lengo la Mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo Madaktari ili hatimaye watoe huduma kwa weledi na kwa urahisi kwa wafanyakazi wanaopatwa na madhara wawapo kazini katika maeneo mbalimbali nchini.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, katika kipindi kifupi toka kuanzishwa kwa Mfuko kumekuwa na mafanikio kadhaa yaliyopelekea kutimiza malengo yaliyowekwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu katika masuala ya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

  Mafunzo haya ya siku tano, (5), yaliyoandaliwa na Mfuko ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madaktari wenye ujuzi katika kufanya tathmini ya ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yanayosababishwa na kazi.

  “Lengo ni kuwa na madaktari wa kutosha kwenye hospitali zetu wenye uwezo wa kufanya tathmini sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi,” alisema Bw. Mshomba.

  Alisema, Jukumu la utoaji mafunzo kwa madaktari nchini si dogo na linahitaji uwezo mkubwa wa kifedha. Hivyo, Mfuko utaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kutoa mafunzo kwa madaktari nchini kuhusu masuala ya tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi

  Bw. Mshomba pia alisema, Mfuko huu ni mkombozi mkubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa kwa ujumla, kutokana na ukweli kwamba matukio ya ajali, magonjwa ama vifo yanapotokea sehemu za kazi, licha ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa lakini pia huzorotesha shughuli za uzalishaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.

  “Hivyo, uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na utekelezaji wa majukumu yake unalinda nguvu kazi ya Taifa na kuchochea shughuli za uzalishaji na kuwa chachu katika kukuza uchumi wa viwanda na kuwa nchi ya kipato cha kati kufikia mwaka 2025.” Alisema.

  Alizishukuru Taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Ocean Raod, Taaisi ya Mifupa (MOI), MUHAS NA OSHA, kwa kuwaruhusu wataalamu wao kushirikiana na WCF katika kutoa mafunzo haya kwa Madaktari.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kwenye mafunzo hayo.
  Bw. Mshomba akitoa hotuba yake
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba za ufunguzi kabla ya kuanza kupata elimu juu ya tathmini kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
  Wawezeshaji (watoa mada), stari wa mbele wakisikiliza hotuba za ufunguzi.
  Mkuu wa Mkoa Mhe. mama Anna Mghwira (katikati), Mkuu wa wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, wakiwa meza kuu mwanzoni mwa mafunzo hayo.
  Kiongozi wa timu ya wataalamu, Dkt. Peter Mhina, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
  Mkuu wa kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akipitia machapisho ya kisheria kabla ya kutoa mada.
  Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia mbalimbali zinazosimamia Mfuko katika uendeshaji wake.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura George, (kulia), akiteta jambo na Dkt. Pascal kutoka kitengo cha Tiba na Tathmini.
  Dkt. Abdulsalaam, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu vigezo vinavyotumika katika kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, akitoa mada kuhusu uendeshaji wa Mfuko.
  Mshiriki akitumia laptop kunakili kilichokua kikizungumzwa.

  Bw. Mshomba, (kushoto) na Dkt.Hussein, (katikati), wakimsikilzia Bw.Anslem.
  Mhe. Mamam Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha wakati akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Lutheran Uhuru mjini Moshi, tayari kufungua mafunzo hayo.
  Mhe. Mamam Anna Mghwira, akipeana mikono na Dkt. Abdulsalaam, mara baaya ya kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba.
  Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.
  Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.
  Bw. Mshomba akiongozana na Dkt. Abdulsalaam wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.
  Piacha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
  Piacha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

  0 0  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.


  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akiangalia moja ya mradi wa maji.


  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amezitaka mamlaka zinazohusika na usambazaji wa huduma ya maji safi na taka (DAWASA na DAWASCO) kuendelea kusambaza huduma pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

  Kauli hiyo ameitoa Februari 19, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kuweza kujionea miradi mbali mbali iliyoanzishwa ili kuweza kuwafikia huduma ya maji kwa urahisi.

  0 0

  Kampuni ya Msama Promotiosn Ltd inaandaa tamasha la Pasaka kanda ya ziwa likalofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili,litakalohusisha waimbaji wa nyimbo za injili mbalimbali hapa nchini,na kwamba litakuwa tamasha lile lile ambalo limekuwa likifanyika jijini Dar Es Salaam kwa miaka yote. 

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema Tamasha la Pasaka Mwaka huu litafayika jijini Mwanza na mkoa wa Simiyu mnamo Aprili 1 na April 2 na baadaye kuendelea kwenye mikoa mingine. 

  “Tamasha la pasaka safari hii linaanzia mkoani Mwanza na baadae mkoa wa Simiyu,na pia mikoa mingine,tamasha hilo kwa jiji la Mwanza litafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, na baadae mkoani Simiyu katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi’’,alisema Msama. 

  Msama amesema kuwa tamasha hilo kwa Mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa,kwa maana ya eneo lakini mambo yote yaliyokuwa yikifanyika jijini Dar,yatahamia jijini Mwanza. 

  Msama anawakaribisha wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake,kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia utukufu wa Mungu kwa njia ya kuimba kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili . 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ,Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,alipokuwa akieleza kuhusu mwanzo wa maandalizi ya tamasha la pasaka 2018,litakaloanzia kanda ya ziwa.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (kushoto), alipomtembelea ofisini kwake katika ziara yake ya kikazi mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi ya ujenzi ya barabara iliyokamilika na inayoendelea. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Urambo, alipokutana nao katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
  Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akimshukuru Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), kwa kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwago cha lami, mkoani Tabora.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua za mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 na kusisitiza nia ya Serikali ya kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kutekeleza miradi ya ujenzi hapa nchini.
  Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akiagana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.

  Muonekano wa Daraja la Kasisi lenye urefu wa mita 54 lililopo katika barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30. Ujenzi wa barabara hiyo umefikiwa asilimia 80 na inajengwa na mkandarasi CICO kwa gharama ya shilingi bilioni 28.


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, na uongozi wa wilaya ya Tabora wakipita juu ya daraja la Wala lenye urefu wa mita 34 katika barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30, katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo, mkoani humo.

  …………………

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.  Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.

  “Nataka nione kazi za ujenzi zinafanyika kwa haraka, kwani uzoefu unaonesha baadhi ya makandarasi wazawa wamekuwa na kasi ndogo, hivyo mjipange vizuri ili barabara ikamilike kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.  Amesema kuwa nia ya Serikali ni kuwajengea makandarasi wazawa uwezo ili waweze kutekeleza miradi mikubwa mingine ya ujenzi hapa nchini lakini haitasita kuwanyima kazi hizo kama miradi hiyo itacheleweshwa, haitakidhi viwango vinavyohitajika na kama hawataonekana eneo la kazi kwa kipindi kirefu.

  “Mkandarasi mzawa atakayechelewesha mradi wowote wa ujenzi hatapewa kazi nyingine kwa sababu atakuwa amechelewesha maendeleo ya wananchi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.  Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuwalipa makandarasi wazawa kwa wakati ili waweze kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.  Naye Mbunge wa jimbo la Urambo, Magreth Sitta, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa wilaya yake na Kaliua na hata mikoa jirani kwani usafirishaji wa mazao na abiria utarahisishwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa amesema wamejipanga vyema kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wazawa hao, na kuahidi kumsimamia ili amalize kazi hiyo kwa wakati, lakini kwa kiwango.

  Awali akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo Mhandisi Damian Ndibalinze, amesema mkandarasi ameshapewa fedha za mradi hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha mradi huo na kuahidi kuwasimamia ili wakamilishe kabla ya mwaka 2020.

  Ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 37.6 na zote zikiwa zinafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.

  Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30 inayojegwa na mkandarasi CICO kwa gharama ya shilingi bilioni 28.6 na kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi wa sita.

  Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Tabora kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miundombinu ya barabara, mkoani humo

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0  0 0

  Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga (katikati mwenye kotI jeusi) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (wa pili kulia) wakikata utepe kuashiriki uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo,wengine ni wadau wa afya mkoani Kigoma. Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Thamini Uhai, Dk.Nguke Mwakatundu (katikati ) akizungumza wakati wa uzinduzi huo .


  Baadhi ya wadau wa afya mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi huo --- Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Shirika la Thamini Uhai imezindua kampeni ya “Mjamzito na Mtoto Salama ni Wajibu Wetu” kupitia radio na uhamasihaji jamii kwa lengo la kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mchanga mkoani Kigoma. 

  Kampeni hii ina lengo la kuhamasisha akina mama kwenda kujifungua katika vituo vya afya,kupanga na kujiandaa kujifungua, na kuweza kutambua dalili hatarishi kipindi cha ujauzito na kuweza kutafuta huduma ya haraka wakati dalili hatarishi zinapojitokeza. Kampeni pia inakuza mpango shirkishi wa uzazi katika vituo vya afya kadhaa vilivyochaguliwa Kigoma. 

  Mpango huu utahimiza akina mama kuja na msindikizaji wa kike atakayemsaidia mama mjamzito kipindi anapokuwa chumba cha kuzalia. Vikwazo vingi vya afya, na vingi vinavyohatarisha afya ya mama na mtoto huweza kutokea kipindi cha awali. Hivyo basi kujifungua katika vituo vya huduma za afya ni njia salama ya kulinda afya ya mama na mtoto. 

  Na hii sio kwa akina mama wenye ujauzito hatarishi pekee lakini pia kwa akina mama wajawazito wote kwa sababu matatizo yasiyotarajiwa yanaweza kutokea hatua yoyote wakati wa mchakato wa kujifungua. Kwa mujibu wa utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuhusu Idadi ya Watu na Afya,Tanzania asilimia 47 tu ya wanawake mkoani Kigoma hujifungua katika kituo cha huduma za afya. Thamini Uhai ni shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania ambalo linasaidia juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008.

  Inafanya kazi na serikali ya Tanzania na Thamini Uhai ni shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania ambalo linasaidia juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008. 

  Inafanya kazi na serikali ya Tanzania na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali Thamini Uhai hujenga uwezo wa kutoa huduma ubora, salama na upatikanaji wa huduma mtambuka ya dharura ya uzazi (EmonC), katika vituo vya serikali,i kwa sasa inasaidia vituo vya afya 50 katika mkoa wa Kigoma. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Brigadier Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga,alisema kwamba kampeni hii inaendana moja kwa moja na mpango wa serikali katika kupunguza na vifo vya akina mama na watoto wachanga. 

  "Katika juhudi za kushughulikia changamoto za afya ya uzazi na akina mama, Serikali inaendelea kujenga wodi za wazazi kwa ajili ya akina mama wajawazito katika vituo vya afya nchini kote mijini na vijijini ili kutekeleza kampeni za afya ya uzazi. Hivyo ninapongeza Thamini Uhai na wadau wengine wanaosaidia mpango huu na ninawaomba wananchi kutumia huduma hizi za afya. "Alisema. 

  Dr Paul Chaote, ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma, alisema kuwa ili kupunguza vifo vya uzazi, huduma mtambuka za dharura za uzazi zinapaswa kuwepo masaa ishirini nanne kwa siku saba za wiki (24/7). Kwa hiyo, wanawake na familia zao wanapaswa kujua kwamba huduma zipo kwa kuwa na ufahamu wa faida zake na kutumia huduma za msingi, bila kuchelewa. Kampeni itakuwa na matangazo ya redio na vipindi vya magazeti itatayojulikana kama“Mjamzito na Mtoto Salama ni Wajibu Wetu” ambavyo vitaruka hewani katika redio zifuatazo: redio Clouds.
   
  kupitia kipindi cha kila siku cha Leo Tena, Joy FM ya mjini Kigoma kila siku ya jumatatu, Jumanne, Alhamis na Jumamosi na redio Kwizera siku ya Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Kampeni pia itatumia vipeperushi, mabango, vibandiko, uhamasishaji jamii na mawasiliano ya kibinafsi ili kueneza ujumbe muhimu. 

  “Kampeni hii ina matumaini ya kuwafikia watu wengi mkoani Kigoma na kuwasaidia wanawake wajawazito na familia zao kuelewa vizuri haja ya kufahamu kuhusu afya ya uzazi na kupanga vizuri namna ya kujifungua. Hii itasaidia mkoa kuelekea kufikia malengo ya uzazi na watoto wachanga yaliyotajwa katika Mpango wa kitaifa wa afya (One Plan II) ", alisema Dk Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda wakati akeielekea kwenye ndege yake tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance  Mabeyo kabla ya kupanda ndege kuelekea nchini Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52) inayomkabikabili Meneja wa benki Khalid Mwinyi (33) bado haujakamikika.

  Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

  Wakili Mkini alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ili kuona kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

  Kabla ya Wakili huyo kueleza hayo, mshtakiwa Rahma Almas aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Mohammed Maganga anaumwa na yupo gerezani.

  Washtakiwa wengine  katika kesi hiyo ni Rahma Almas maarufu kama Baby (37)  Mfanyabiashara na Mohammed Maganga mwenye (61) ambaye ni mchimba makaburi.

  Kesi imeahirishwa hadi Machi 6,mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

  Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa, Agosti 16,mwaka 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walimuua Lotter.

  0 0
 • 02/21/18--01:29: TANGAZO


 • 0 0

  Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC) imeamua kusitisha mpango wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa halmashauri hiyo itakapopatikana. 

  Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika (Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu ya suala hilo. .

  Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao juu ya wapi pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo. Baadhi ya viongozi wanadai utaratibu wa fedha za manunuzi haukufuatwa katika kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la Kwehangala na kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya Sh. milioni 700.

  Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kikao kiliafiki kisitishe zoezi hilo mpaka maelewano yatakapopatikana." Wajumbe wameshauri suala la kuhamisha makao makuu lisitishwe hadi hapo utakapopatikana utangamano,kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao umeleta utengano kwa viongozi" Alisema Lugangika .

  Mbunge wa jimbo hilo, January Makamba alikiri kuwepo kwa mvutano huo ambao alisema hauna tija katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bumbuli.Makamba alisema ni vyema kama viongozi wakazungumzia suala la maendeleo mfano;maji,barabara,umeme,nyumba za watumishi badala ya kila siku kuzungumzia wapi kujengwe jengo la halmashauri. 

  Alishauri kuwa wananchi washirikishwe katika suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya kutosha juu ya hoja ya kuhamisha halmashauri kwa kuwa ndio wenye chombo chao badala ya viongozi kuamua wao pekee.

  "Suala hilo nakubaliana na maoni wa kikao cha DCC tulisitishe kwani kwa sasa hatuna shida na majengo ya halmashauri kwa sababu majengo tunayo ambayo hatulipii kodi ya pango. Sasa hivi tuzungumzie maendeleo kwani wananchi mwaka 2020 hawatatudai majengo ya halmashauri bali watatudai maendeleo juu ya huduma muhimu za jamii alisema Makamba.

  Hivi karibuni baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura ya kupitisha azimio la kujenga jengo hilo la halmashauri huku Madiwani nane wakigoma kupiga kura kwa madai kuwa hawawezi kupiga kura wakati kuna ukiukwaji wa kanuni na utaratibu ktk kitengo cha manunuzi.

  Madiwani hao nane ambao waligoma kupiga kura kupitisha azimio hilo mnamo January 18 mwaka huu walimuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuingilia kati mgogoro na kuzuia walichokiita ukiukwaji wa utaratibu wa manunuzi pamoja na maelekezo mbalimbali ya viongozi juu ya mpango huo.

  Pia walimuomba aingilie kati na kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma na ukiukwaji wa utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri na kudharau kwa makusudi maelekezo yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa serikali kuu.

  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amir Shehiza alisema kuwa baraza ni chombo chenye maamuzi sahihi hivyo alikitaka Kikao hicho cha DCC kuacha kuingilia Kazi za baraza .

  0 0

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

  Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

  Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

  Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

  Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.

  Februari 19, 2019 akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim Majaliwaalimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.Alichukua hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.

  Amesema Mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.

  Waziri Mkuu alisema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim. Alisema mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.

  Alisema Mwanasheria alimlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.Hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.
  Kikundi cha ngoma za Asili cha Masters of ground kutoka Wilaya cha Kyotera, Masaka nchini Uganda wakitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU


  0 0

  NA  YEREMIAS  NGERANGERA
  Upepo  mkali ulioambatana na mvua umeleta tafrani katika kijiji cha Njalamatata kata ya Mkongo Nakawale wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma .

  Tafrani  hiyo ilitokea siku ya  jumatatu  wiki hii  baada ya nyumba tano kuezuliwa na upepo na wananchi waliokumbwa na dhahama hiyo kubaki wakitafuta makadhi  ya kujihifadhi kwa majirani.

  Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Adelin Nchimbi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama  walifika eneo la tukio na kuongea na  waathirika wa tukio la kuezuliwa nyumba katika  kijiji cha Njalamatata.

  Aidha bwana Nchimbi alisema kuwa katika tukio hilo Nyumba tano ziliezuliwa na  upepo  lakini   hapakujitokeza  mwananchi yoyote kujeruhiwa au kuwepo kwa  maafa katika tukio hilo.

  Alitaja majina ya wananchi walioathirika katika tukio hilo ni  Clavery Ponera ,Donatus Kapinga,James Mdagi ,Sadiki Kapinga ,Rusti  Kimbili na Lotary Hongo wote ni wakazi wa kijiji hicho cha Njalamatata wilayani humo.
   Kamati  ya ulinzi na usalama  ya wilaya ya Namtumbo pamoja  na kutoa pole kwa waathirika wa tukio hilo ilifanya mahojiano na waathirika kubaini hasara iliyopatikana  kutokana na tukio hilo.
  Kamati ya ulinzi  na usalama ya wilaya ya Namtumbo pamoja na pole hizo iliwashauri wananchi wa kijiji hicho kujenga nyumba na kuziezeka kwa kuweka tengo za kushikizia kwenye ukuta baada ya kubaini baadhi ya nyumba hazikuwekwa tengo hizo.

  0 0  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanza kwa usajili wa mbio za km 21 za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi tarehe 4 Machi ya mwaka huu. Kulia ni Afisa wa Lipa kwa Tigo Pesa, David Chinguile.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanza kwa usajili wa mbio za km 21 za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi tarehe 4 Machi ya mwaka huu. Kulia ni Afisa wa Lipa kwa Tigo Pesa, David Chinguile.


  Usajili upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo

  21 Januari, 2018. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania leo imetangaza kuanza kwa usajili wa mbio ndefu za Tigo Tigo Kili Half Marathon kupitia namba *149*20#.

  Kwa mwaka wa nne mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mbio za KM 21 za Tigo Kili Half Marathon ambazo zitafanyika tarehe 4 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi. Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa shindano la Tigo Kili Half Marathon 2018 linaunga mkono juhudi za serikali za kuinua viwango vya michezo na kujenga afya bora za Watanzania kupitia ushiriki wao katika michezo.

  “Usajili wa mbio za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Kujisajili, piga simu namba *149*20#, kisha fuata maelekezo rahisi ya kuchagua mbio unazotaka kukimbia na kulipia ada ya usajili kwa mbio husika. Baada ya kutuma ada ya ushiriki, utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakaokujulisha kuhusu kukamilika kwa muamala wako. Utunze ujumbe huu mfupi wa maneno na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika kituo utakachojulishwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Moshi ili kuchukua namba yako ya ushiriki,’ Woinde alieleza.

  Tigo inatoa jumla ya TZS 11m kama zawadi kwa washindi kumi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanaume na wanawake. Pia kuna medali na vyeti vya ushiriki kwa watu 4,500 wa kwanza watakaomaliza mbio hizo.

  ‘Tunachukua fursa hii kuwakaribisha washiriki wote, ikiwemo wanariadha wa kimataifa, wa kitaifa, wapenda michezo na wanafamilia wote kuja kushiriki katika mbio hizi za Tigo Kili Half Marathon, ili waweze kutunza afya zao pamoja na kufurahia kumbukumbu za matukio yanayoendana na shamrashamra za mashindano,’ Woinde alisema.

  Naye Afisa wa Lipa Kwa Tigo Pesa, David Chinguile alisema kuwa Tigo imepanua huduma ya Tigo 4G kufikia miji 22 nchini Tanzania, ikiwemo katika mji wa Moshi na kanda yote ya Kaskazini. Uwekezaji huu mkubwa utahakikisha kuwa watakaohudhuria Tigo Kili Half Marathon 2018 watapata huduma bora na za uhakika za mtandao wa simu utakaowawezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa, na marafiki pamoja na kutuma picha na video za matukio na kumbukumbu nyingine muhimu kwa kasi ya juu kupitia mtandao wa Tigo 4G.

  Tigo inajivunia kuwa sehemu ya mbio za Tigo Kili Half Marathon 2018 ambazo zinazidi kujizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni mwaka hadi mwaka.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.


  Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.

  Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

  “Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”

  Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.

  Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.

  Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile alisema dawa za kulevya zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi na kifua kikuu.

  Pia alisema kwa sasa dawa za methadone zinazotolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya wanazipata kutoka kwa wahisani mbalimbali. Hata hivyo, Serikali imepanga kuingiza suala hilo katika bajeti ijayo ili ianze kuagiza yenyewe.

  Baadhi ya vijana waliokuwa wanatumia dawa za kulevya mkoani Mwanza akiwemo, Nyamizi Sospeter na Abdul Abdallah, waliishukuru Serikali kwa kuanzisha vituo vya methadone.

  Nyamizi alitumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka saba na muda wote huo alikuwa akiisumbua familia yake kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu aliyokuwa akiyafanya ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

  Naye Abdul Abdallah alisema alitumia dawa za kulevya aina ya heroine kwa takribani miaka 20 na muda wote huo alikuwa anakaba watu ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

  “Naishukuru Serikali kwa kuanzisha kliniki ya methadone na sasa nimeacha mimi pamoja na mke wangu. Najiona binadamu maana nilikuwa mwizi, mchafu kwani nilikuwa nakaa mwezi bila kuoga na hata kutengwa na jamii.”

  Kwa pamoja waathirika hao wa dawa za kulevya waliiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kufanya kazi na kupata kipato kitakachowasaidia kuendesha maisha yao.

  Awali, Waziri Mkuu alizindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses) ambao unalenga kuwawezesha wamiliki wa nyumba hizo kuziendesha vizuri na kuwasaidia ipasavyo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.

  0 0

  Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO kutoka China, Bw. li, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiwaonesha Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi na Mbunge wa Jimbo la Igalula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami itajengwa, mkoani Tabora.
  Tingatinga likikata miti kwa ajili ya kusafisha eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami utaanza, mkoani Tabora.   Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.

  Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara hiyo.

  Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 117.9 na utachukua miezi 24 mpaka kukamilika kwake."Serikali imeanza rasmi ujenzi wa barabara hii na sasa ni jukumu lenu kuhakikisha mnampa ushirikiano mkandarasi huyu ili mradi uwahi kukamilika mapema", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani. Ameongeza kuwa sasa Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka daraja la Kikwete mpaka Uvinza, mkoani Kigoma na hivyo itasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi kutoka mkoa wa Dar es Salaam mpaka mikoa ya katavi na Kigoma kupita kwenye lami njia nzima.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa yeye na timu yake watajitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutohujumu vifaa vya mkandarasi huyo.

  Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi, ameishukuru Serikali kwa mradi unaoendelea katika wilaya hiyo na kumuahidi Waziri kuwa yeye na kamati ya usalama itahakikisha mkandarasi hahujumiwi.

  Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi DamianNdibalinze, amemueleza Waziri kuwa kazi imeanza kwani Mkandarasi ameshaanza kuleta vifaa eneo la kazi na ujenzi wa kambi unaendelea.

  Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea mkoani humo .

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara  Wenye Viwanda  (TCCIA) mkoa wa Mwanza, Christopher Mwita Gachuma wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza  kuongoza kikao cha wadau wa zao la pamba alichokiitisha, Februari 21, 2018.Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula na kushoto ni Mbinge wa Sumve, Richard Ndassa.
   Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la pamba ulioitishwa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 21, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


older | 1 | .... | 1521 | 1522 | (Page 1523) | 1524 | 1525 | .... | 1897 | newer