Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1516 | 1517 | (Page 1518) | 1519 | 1520 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Mwanasheria wa Kituo cha Usuluhishi–CRC, Suzan Charles (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jana jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam.

  Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma.
  Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

  Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

  BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huza huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na msaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogeza huduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.

  "...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa na kesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.

  Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa na muitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

  Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili za matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikia muafaka juu ya mvutano wao.Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapo huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na ushauri wa kisheria utatolewa.

  "...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji huduma hizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa kuja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwa pia," alisema Bi. Chonya.

  0 0


   Barnaba


   Dulla Makabila


   Manfongo


   Amigo


  Joh Makini
  Inspector Haroun

  Uhuru FM kwa kushirikiana na Darlive inakuletea tamasha la Muziki  lijulikanalo kama MIC TATA litakalokutanisha miamba ya Muziki hapa  nchini litakalofanyika katika ukumbi wa Darlive-Mbagala Zakyeem Februari 24 Mwaka huu.

  Mratibu wa show hiyo Said Ambua , amesema Wasanii watakaokutanishwa katika tamasha hilo la MIC TATA ni wa Bongo Flava, Singeli, Taarabu na Hip Hop.

  Katika tamasha hilo la Muziki wasanii watakaokuwepo ni Barnaba, Inspector Haroun, Manfongo, Dula Makabila, Joh Makini kutoka Weusi na  kwa upande wa taarabu ni Amigo.

  Tamasha hilo ambalo kiingilio chake ni shilingi 5,000 litafanyika kuanzia Saa Mbili usiku.

  0 0


   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso, (aliyesimama), akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara yake aliyoifanya kuangalia hali ya upatikanaji wa maji kwenye wilaya ya Ilala hususan jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam Februari 12, 2018.


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso, ataongoza kikao baina ya uongozi wa Manispaa ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafuta njia ya kupata fedha za kukamilisha mradi wa maji wa Kimbiji ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye maeneo kadhaa ya jiji ikiwemo wilaya hiyo.

  Naibu Waziri ameyasema hayo Februari 12, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bonyokwa huko Kinyerezi Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, baada ya kuambiwa kuwa awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu 20, umekamilika na unakusudia kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji maji kwenye maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.
  “Mamlaka ya DAWASA ndio iliyopewa jukumu kusimamia awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu vilivyo kwenye takriban mita 405 hadi 600 na viko 20 kilichobaki ni awamu ya uendelezaji wa visima (kuweka mtandao wa usambazaji maji ili maji yaweze kuwafikia wananchi wa jiji la Dar es Salaam likiwemo eneo hili.” Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, (DAWASA) Bi. Modester Mushi.
  Bi. Mushi alifafanua kuwa sababu ya kutenga mradi huo kwa awamu ni kutokana na gharama na upatikanaji wa fedha lakini akabainisha kuwa Mamlaka iko kwenye hatua nzuri kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ambapo nyaraka ziko kwa Mwnaasheria Mkuu kwa ajili ya mapitio na kupitia Wizara wanategemea kuanza mradi huo kwa wakati katika mwaka wa fedha ujao, alisema.

  Baada ya maelezo hayo ndipo Naibu Waziri ambaye alifuatana na Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Bonna Kalua, aliagiza mkutano wa dharuara ufanyike Jumanne baina yake, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafutia ufumbuzi mkwamo huo kwani wananchi wanataka maji na si vinginevyo.
   Mhe. Aweso, akisikiliza kwa makini kero za wananchi kuhusu maji.
   Baadhi ya wananchi wa jimbo la Segerea waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Bonyokwa Februari 12, 2018.
   Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
   Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
   Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam, (DAWASA), Bi. Modester Mushi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dar es Salaam ikiwemo jimbo la Segerea.
   Mwakilishi kutoka DAWASCO, akizungumza kwenye hadhara hiyo.
   Meneja Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Neli Msuya, na wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia hotuba.
  Mhe. Aweso na Mhe. Bonna Kalua, wakijadiliana jambo mwishoni mwa mkutano huo.

  0 0

  Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele.


  Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeendesha mafunzo kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri za wilaya mkoani Mwanza. 

  Mafunzo hayo ya siku tano yanayokutanisha wahudumu wa jamii kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba, Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana yanafanyika kuanzia Jumatatu Februari 12,2018 hadi Ijumaa 16 Februari ,2018 katika ukumbi wa Midland Hotel jijini Mwanza.

  Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele alisema mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma ngazi ya jamii kuboresha huduma katika vituo vya afya kwenye maeneo yao.

  “Kupitia mafunzo haya mtaweza kuwaunganisha wateja na huduma mbalimbali za kijamii ili kuhakikisha kunakuwepo uendelevu wa huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo ikiwa ni pamoja na kuwarudisha kwenye huduma wateja waliopotea”,alisema Dk. Masele.

  “Naomba mkafuatilie wateja waliopotea, muwaelimishe kuzingatia ufuasi mzuri wa dawa na kuhakikisha hawapati maambukizi mapya na magonjwa nyemelezi kwani hatutaki kuona mgonjwa anakuwa wa kulala kitandani, sisi tunataka watu washiriki katika shughuli za maendeleo”,aliongeza Dk. Masele.

  Aidha alilishukuru shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC) kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.

  “Juhudi za mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi zitafanikiwa zaidi pia kama tutaboresha kamati za Ukimwi za ngazi ya kijiji na kata kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu ili kupunguza maambukizi ya VVU katika mkoa wetu ambao maambukizi yameongezeka kutoka asilimia 4.2 hadi 7.2”,alisema Dk. Masele.

  Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona alisema lengo la mafunzo hayo ya msaada wa kisaikolojia ni kuwezesha upatikanaji wa huduma rafiki kwa watoto, vijana na watu wazima wanaoishi na VVU ili watambue umuhimu wao katika taifa na jamii zao.

  “Mafunzo haya pia yatasaidia katika kutoa ushauri na mafunzo sahihi kwa watoto na vijana kuhusiana na majibu ya changamoto zinazowakabili, matumizi ya dawa/ARV na ufuasi mzuri wa dawa lakini pia kuboresha mawasiliano kati ya watoa huduma,wazazi, walezi, vijana na watoto”,aliongeza.

  Aliyataja baadhi ya madhara yanayompata mtu iwapo atakosa msaada wa kisaikolojia kuwa ni pamoja na kukata tamaa ya maisha, kuacha dawa, kuchanganyikiwa, kujitenga ama kuwa na hali ya upweke na kupoteza maisha.

  Shirika la AGPAHI linatekeleza miradi ya VVU na Ukimwi katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,Mwanza, Tanga na Mara likishirikiana na serikali ya Tanzania kupitia ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia CDC katika kutekeleza mradi wa “Boresha” ambao unatoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi.
  Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele akifungua mafunzo kuhusu msaada wa huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii. Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona.
  Dk. Masele akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo watumie mafunzo wanayopewa ili wakaboreshe huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo.
  Dk. Masele akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia mbinu mbalimbali kurudisha wateja waliopotea.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini.
  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea malengo ya mafunzo ya huduma na msaada wa kisaikolojia na maana yake kwa wahudumu wa jamii.
  Cecilia Yona akielezea shughuli zinazofanywa na shirika la AGPAHI katika kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
  Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Gaston Kakungu ambaye ni Afisa Muuguzi Mstaafu akitoa mada wakati wa huduma na msaada wa kisaikolojia.
  Kakungu akiwaasa washiriki wa mafunzo hayo kuwa daraja muhimu la kuunganisha wateja katika huduma za tiba na matunzo.
  Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Dk. Joseph Musagasa akielezea juu ya ukweli kuhusu VVU na Ukimwi.
  Dk. Musagasa akiwasihi washiriki wa mafunzo hayo kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita imani potofu zinazochangia kuendelea kuwepo kwa maambukizi ya VVU, ikiwemo kuendekeza waganga wa kienyeji ambao baadhi yao hawana elimu ya kutosha kuhusu VVU na Ukimwi.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0


  Na John Nditi, Kilombero.

  HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro wamewakatia  kadi za   Mfuko wa Afya ya Jamii  (CHF ) iliyoboreshwa  wazee wasiojiweza zaidi ya 7,800 waliopo katika  kata  26  ili kuwawezesha kupata  huduma bora za matibabu katika vituo vya  Afya, Zahanati na hospitali na wategemezi wao.

  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri  hiyo , Dennis Londo   alisema hayo  mbele ya  Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa baadhi ya wazee wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.

  Londo  alisema   kuwa , hadi sasa  kiasi cha Sh milioni 13.3 zimetumika  kwa ajili ya mpango wa kuwakatia wazee wasiojiweza  bima  ya  afya ya CHF Iliyoboreshwa.

  Hata hivyo alisema , halmashauri hiyo imejipanga  kuhakikisha wazee wanapatiwa bima ya Afya CHF iliyoboreshwa na lengo  ni  kuwafikia  wazee wasiojiweza  zaidi ya  15,000  katika kata zote 26.

  “ Halmashauri ya wilaya hii imejipanga vyema na inatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM  na miongoni mwa mam ohayo ni kundi la wazee wasiojiweza wamenufaka na huduma ya bima  ya afya” alisema Londo.

  Naye Mwenyekiti wa halmashauri  hiyo , David Ligazio aliwataka watendaji wa vituo vya afya, zahanati na hospitali  ambaki madirisha ya wazee hayajaanzishwa waanzishe mara moja   ili  wazee hao wapate  unafuu wa huduma kulingana na lengo lililokusudiwa .

  Kwa pande wake  mkuu wa wilaya ya Kilombero , James Ihunyo  alisema  , halmashauri hiyo inaendelea kufanya vizuri kutokana na  sehemu ya fedha zinazopatikana za   makusanyo ya ndani  kuelekezwa  kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kuwakatia  bima  ya afya wazee wasiojiweza sambamba na kwa halmashauri ya mji Ifakara.

  Awali  akisoma taarifa ya ugawaji wa kazi hizo ,  Ofisa Elimu Kata Kalengakelu,  Zainab Said  alisema,  wazee wasiojiweza walionufaika na mpango huo ni wa kutoka kwenye vijiji 23 vya  kata ya Chisano, Kalengakelu, Mlimba, Kamwene, Utengule , Masagati na Uchindile .

  Akizungumza katika halfa hiyo katibu tawala wa mkoa huo, Tandari alizitaka halmashauri nyingine ndani ya mkoa huo  kuiga mfano wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero  ili kuhakikisha wazee wote wanakuwa bima ya afya.

  Nao baadhi ya wanufaika na mpango huowa CHF iliyoboreshwa ,Nelasi Nyingi  na Petro Karubandika kwa nyakati tofauti waliipongeza Serikali na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero  kwa kuwawezesha kuingizwa kunufaika na huduma za afya hasa ikizingatiwa wao wanahauwezo wa kifedha na wategemezi wao.
   Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( wapili  kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa mzee  Petro Karubandika mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero  wakati wa zoezi la ugawaji  kadi  hizo kwa wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba na (  kushoto) ni  mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
   Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa   Nelasi Nyingi , mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero  wakati wa zoezi la ugawaji  kadi  hizo kwa wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba (  kushoto ) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri   ya Kilombero , Dennis Londo  ( kulia) akitoa maelezo mafupi ya mapango wa kuwakatia bima ya afya wazee  wasiojiweza kwa  Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kutoka kushoto) wakati wa  zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa  wazee wapatao  2,100 wa  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
  Baadhi ya wazee wa kata saba za tarafa ya Malimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( hayupo pichani) wakati wa  zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa  wazee wapatao  2,100 wa  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.  ( Picha na John Nditi).

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam alipotangaza washindi wa kwanza wa simu za Tecno R6 zenye uwezo wa 4G katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo inatoa bonasi ya hadi GB1 ya intaneti kwa wateja wanaonunua bando za data kuanzia TSh 1,000 kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00# pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu za smartphone kila saa. Kushoto ni Mtaalam wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
   Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimzawadia  Saidi Abdallah Popote wa Tabata, Dar es Salaam simu aina ya Tecno R6 yenye uwezo wa 4G aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus, huku akishuhudiwa na baadhi ya washindi wengine. Tigo inatoa bonasi ya hadi GB1 ya intaneti kwa wateja wanaonunua bando za data kuanzia TSh 1,000 kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00# pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu za smartphone kila saa.
   Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kati) akimzawadia  Advera Revelian Kyaruzi wa Tegeta, Dar es Salaam simu aina ya Tecno R6 yenye uwezo wa 4G aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus, huku akishuhudiwa na baadhi ya washindi wengine. Tigo inatoa bonasi ya hadi GB1 ya intaneti kwa wateja wanaonunua bando za data kuanzia TSh 1,000 kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00# pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu za smartphone kila saa.


  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 36 wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G. 

  Akitangaza washindi hao wa kwanza 36 waliopatikana katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu, Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alibainisha kuwa washindi 13 wanatoka Dar es Salaam, na wengine ni wakaazi wa mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dodoma, Mtwara, Iringa, Mwanza na Arusha. 

  ‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema. 

  Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zaidi ya elfu moja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo kila saa.

  ‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki. Pia sasa nitaweza kupiga picha za kazi zangu na kuwatumia wateja kwa kasi zaidi kupitia mtandao wa Tigo 4G,’ Said Abdallah Popote ambaye ni fundi wa kupaua nyumba na mkaazi wa Tabata, Dar es Salaam alisema. 

  Advera Salum Abdallah, ambaye ni muuguzi na mkaazi wa Tegeta alisema kuwa simu aliyoshinda itamwezesha mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi kutafiti mambo mbali mbali ya kielimu kupitia mtandao wenye kasi ya juu wa Tigo 4G. 

  “Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00#  ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Woinde alisema.

  Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikagua bomba la DAWASCO linalosambaza Maji ya Ruvu Juu iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikagua Mradi wa visima 20 eneo la Kisarawe II katika mji wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso aendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya Miradi ya Maji Mji wa Kigamboni Jijini Dar es salaam.

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari  (hawapo pichani) kuhusu Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambao utakuwa ukikusanya na kuhifadhi historia ya ukombozi wa bara la Afrika alipotembelea yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam leo,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Wiliam.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaeleza waandishi (hawapo pichani) kuhusu historia ya pikipiki aliyoshika kuwa ilikuwa ikitumiwa na Rais wa awamu ya kwanza wa Msumbiji Hayati Samora Machel katika kipindi cha kupigania uhuru wanchi yake, alipotembelea yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa kukomboa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam. 
   Mkurugenzi wa Idara ya Historia na Makumbusho (JWTZ) Kanali Robert Mjange (wa pili kulia) akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu hali ya jengo ambalo lilikuwa ni  Makao Makuu  yaliyokuwa yakitumiwa na viongozi mbalimbali  wa Afrika ambao walikuwa wanakamati wa kupigania Ukombozi wa Bara la Afrika hapo zamani, alipotembelea Ofisi zinazoratibu Programu ya Ukombozi  Bara la Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.
  Mratibu wa Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiahedi Mduma (katikati) akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) jengo ambalo lilikuwa ni  Makao makuu ya Viongozi wa Kamati ya kupigania uhuru wa bara la afrika  hapo zamani ambalo linahitaji ukarabati kwa sasa  alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo leo jijini Dar es Salaam.

  Na Anitha Jonas – WHUSM.

  Serikali yatao Milioni Mia saba kwa ajili ya ukarabati wa Jengo lilokuwa Makao Makuu ya Wanakamati wanaopigania Uhuru wa kulikomboa Bara la Afrika ikiwa ni sehemu ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.

  ‘’Tumepewa dhamana na heshima kubwa na Umoja wa Afrika ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika sababu ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alivyopigania uhuru wa bara la afrika na kutoa ofisi jijini Dar es Salaam ambayo ilikuwa Makao Makuu ya wapigania Uhuru kutoka nchi mbalimbali za Afrika kukutania na kupanga mikakati hivyo ni vyema tuhifadhi historia hii,’’ Dkt.Mwakyembe.

  Akiendelea kuzungumza katika ziara yake ofisini hapo Waziri Mwakyembe alisema serikali inampango wa kujenga ofisi kubwa na za kisasa katika maeneo ya Bunju Mwabepande jijini Dar es Salaam ambazo itahifadhi historia yote na hapo patakuwa ni kituo cha Kimataifa ambacho watalii na wageni mbalimbali watatembelea na kupewa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

  Kwa upande wa Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiedi Mduma alieleza kuwa kituo hicho kitakachojengwa kitakuwa ni moja kivutio cha utalii na kitasaidia kuiingizia serikali mapato  kutoka na wageni watakao kuwa wakitembelea kituo hicho na eneo lake linakaribia ekari hamsini.

  Pamoja na haya Mheshimiwa Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania kuhifadhi na kutunza maeneo yaliyotumika na mashujaa hao waliyokuwa wakipigana kukomboa bara la Afrika pamoja na kutoa taarifa za maeneo wanayojua yalitumika na mashujaa hawa kwa lengo ya kuisaidia serikali ili iweze kuhifadhi historia hiyo adhimu yenye kulipa Taifa heshima kubwa.

  Hata hivyo serikali imeanda muswada utakao pelekwa bungeni kwa ajili ya kupatikana kwa sheria itakayosimamia vyema historia mbalimbali za taifa letu.

  0 0


  Na Mwandishi Wetu

  JUKWAA la Nishati Tanzania linatarajia kutoa semina kwa wabunge ili wapate uelewa wa nishati na changamoto zake, watakapokuwa wanajibu maswali ama kuuliza wafanye hivyo kwa manufaa ya taifa.

  Mratibu wa Jukwaa hilo nchini ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Hudson Nkotagu alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli wanazozifanya.

  Profesa Nkotagu alisema wanaamini wabunge wakipata uelewa kuhusu nishati pale watakapokuwa wakijadili masuala hayo bungeni watakuwa na uelewa mpana, na maamuzi yake yatakuwa kwa manufaa ya taifa.

  Pia alisema semina hizo zitatolewa kwa viongozi wakuu, watendaji wa serikali kutoka sekta za viwanda, mazingira, serikali za mitaa, wawekezaji pamoja na wafanya biashara mbalimbali.

  Alisisitiza kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa nishati kwamba kuna za aina mbili, aina ya kwanza inatokana na vyanzo vya nishata ambavyo vikitumika vinapoisha havirudi tena mfano gesi, mafuta, mkaa wa mawe pamoja na urani.

  Na aina nyingine ni ile inayotokana na vitu ambavyo vinajiendeleza vyenyewe kiasili kwa mfano nishati ya sola, upepo, maji, mawimbi ya bahari na kuni.

  “Nishati hizi zinajiendeleza kiasili. Kwa bahati nzuri zote tunazo katika nchi yetu. Tanzania imejaliwa kuwa na vyanzo vyote vya nishati, vinahitajika tu kuendelezwa,” alisema.

  Alisema jukwaa hilo linashirikisha UDSM, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), pamoja na vyuo vikuu vine kutoka nchini Uholanzi ambavyo ni Twente, Ultreacht, Hanze na Delft.

  0 0
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam  kuhusu utaratibu wa ujio wa Rais  FIFA na CAF nchini mwezi huu kwa ajili ya kufanya mkutano wa kujalili agenda za mkutano mkuu wa FIFA,na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
  PIX 2
  Mjumbe wa CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Leodger Tenga (katikati) akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) kuhusu mambo ambayo uongozi wa FIFA utapenda kujua katika soka la Tanzania ambapo moja wapo ni Maendeleo ya Soka la Wanawake,Kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
  PIX 3
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wallace Karia  (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa waandishi watakao shiriki kuripoti habari wakati wa ujio wa Rais wa FIFA na CAF nchini kwa Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo vya habari nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
  PIX 4
  Baadhi ya Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kikao cha maandalizi ya ujio wa rais wa FIFA NA CAF mwezi huu nchini kilichokuwa kikiendeshwa na Waziri wa Habari     Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi leo amezindua rasmi bodi ya wathamini ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya uthamini na usajili wa wathamini ya mwaka 2016 ambayo imeanza kutumika rasmi Januari mwaka huu. 

  Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria wajumbe wa bodi ni lazima kutoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ofisi ya rais TAMISEMI, vyuo vikuu, vyama vya kitaluma vya wathamini, ofisi ya mwanasheria mkuu, taasisi ya mabenki, na bodi ya wakaguzi na wahasibu(NBAA) na kuongeza kuwa kwa muundo huo bodi inahitaji mpana mkubwa wa uwakilishi ili kutekeleza majukumu yake kwa urahisi. 

  Pia amesema kuwa serikali iliona umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti kwa ajili ya kusimamia taaluma ya uthamini baada ya kuonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la udanganyifu katika kazi ya uthamini hasa kwenye miradi ya serikali na ya mikopo katika mabenki baada ya Kazi hiyo ya uthamini kuwa chini ya Baraza la wapima ardhi na wathamini (NCPS). 

  Aidha ameweka wazi kwamba tasnia ya uthamini ni ya muhimu sana kwa ustawi wa uchumi kwa ujumla kwani Kazi za wathamini zunahusiana na ukadiriaji wa Mali kwa malengo mbalimbali ikiwemo kuweka rehani za mikopo kwenye mabenki, kodi za ardhi na majengo, mahesabu ya makampuni binafsi na taasisi za serikali hivyo kama Kazi hiyo haitafanywa kwa umakimi na uadilifu inaweza kuchangia kuanguka kwa uchumi na hata watu kupoteza mali sambamba na kusababisha migogoro ya ardhi. 

  Pia amebainisha masuala ambayo yanatakiwa kufanyiwa Kazi kwa haraka ili kufuta dosari zilizopo na kusema kuwa ni kudhibiti kazi ya uthamini kufanywa na watu wasiosajiliwa na bodi na wale wasio ma taaluma ya uthamini, kudhibiti udanganyifu wa thamani kwa ajili ya uthamini kwa ajili ya fidia, kodi na mikopo ya benki, kutoa na kusimamia mafunzo ya Mara kwa Mara kwa wathamini pamoja na kuandaa viwango na miongozo ya uthamini. 

  Pia Waziri ametoa onyo kwa wathamini wanaotumia udanganyifu pindi wanapofanya tathimini pamoja na wale wanaofanya kazi ya uthamini nje ya kazi au miradi ya serikali na kuwaomba wathamini wote kujisajili kwenye bodi ya wathamini ili watambulike na kupata usajili unaotambulika. 

  Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wathamini Dkt.Cletus E.Ndjovu amesema kuwa bodi ya wathamini ni muhimu sana katika suala la maendeleo na kuahidi kwamba watafanya kazi kwa weledi na kwa kufuata sheria ya bodi ya uthamini bila kumwonea mtu aibu ili kuleta heshima katika taaluma ya uthamini.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiongea na waandishi wa habari na watangazaji wa Radio katika hafla ya kuazimisha siku ya Redio Duniani ambapo aliwataka kuzingatia maadili ya utangazaji kwa kudumisha,amani,upendo na mshikamano.
  Pix 1
  Mwakilishi kutoka  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) Bi. Faith Shayo akiongea wakati wa kuadhimisha siku ya Redio Duniani  leo Mkoani Dodoma, katikati nia Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge .
  Pix 2
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge (wa kwanza kulia) akiongea kwa ajili ya kumkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)  katika hafla ya kuadhimisha siku ya Redio Duniani ambayo kitaifa imefanyika leo Mkoani Dodoma, kushoto ni Mwakilishi kutoka  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) Bi. Faith Shayo.

  Pix 6
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walihudhuria maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika leo Mkoani Dodoma, kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge.
  Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
  …………….
  Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili kwa kuandika habari zenye ukweli na uhakika kwa manufaa ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.

  Mhe. Shonza ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Redio Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi na watangazaji wa redio za jamii kutoka mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro, Mtwara, Shinyanga, Songwe, Geita, Mwanza, Kagera, Dodoma, Pemba, Unguja, Lindi na Songwe.

  “Redio za jamii zimekuwa tegemeo kubwa la kupata habari kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini hasa pembezoni mwa nchi. Mwananchi haitaji kuwa na umeme anapotaka kusikiliza Redio,” alisema Shonza.
  Amesema, ni vyema waandishi wawe wa kweli wanapotoa habari mbalimbali kwa wananchi ili kuepuka machafuko ya nchi kama ilivyotokea nchini Rwanda, ambapo chanzo cha machafuko hayo kilitokana na habari zilizotangazwa kupitia Redio.

  “Wananchi wanategemea habari toka kwenu ili kujua namna Serikali inavyotekeleza majukumu yake pamoja na kutatua changamoto zao,” alisema Mhe. Shonza.Vile vile kupitia Redio za Kijamii, wananchi ambao ni wakulima wanaweza kujua maeneo yalipo masoko kwa ajili ya mazao yao.
  Naye,  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge amewata waandishi wa habari kuitangaza Dodoma pamoja na fursa zilizomo mkoani humo kwa kuwa ni ya Serikali ni kuifanya Dodoma kuwa kituo cha mji wa kiuchumi.

  “Mpaka sasa jumla ya watumishi 3000 wamehamia mkoani humu na kufikia Juni mwaka huu jumla ya watumishi wa Serikali 7000 watakuwa wamehamia. Hivyo fursa nyingi zitahamia mkoani humu,” alisema Dkt. Mahenge.Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Faith Shayo amewataka waandishi wa habari hao kutumia vizuri vipaza sauti vyao katika kudumisha amani ya nchi, kuchochea maendeleo, kupinga unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kuweka msisitizo wa  usawa wa kijinsia.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa, Wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas
  8
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  ………………..

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza
  Kuwasaidia wananchi.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi ambako kote alishiriki shughuli za kimaendeleo ikiwa kuzindua Vituo vya Afya Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya Sekondari Kilolo,Pia aliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Maabara na Madarasa katika shule ya sekondari Mgololo na kuweka jiwe la Msingi katika upanuzi wa Kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

  Makamu wa Rais pamoja na kutembelea miradi hiyo ya kimaendeleo pia alitembelea Kiwanda cha Ivori kinachotengeneza pipi na Chocolate na alitembelea kampuni ya GBRI inayoshughulika na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za mboga mboga.Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Iringa kwa mapokezi mazuri waliompa kipindi chote cha ziara .

  Makamu wa Rais alisisitiza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na utunzaji mazingira, Aidha Makamu wa Rais aliwataka viongozi wa mkoa huo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya mazingira na elimu juu ya ugonjwa hatari wa ukimwi ambao unaonekana kuenea kwa kasi mkoani humo.

  Makamu wa Rais aliwataka viongozi kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii.
  Makamu wa Rais alitoa rai kwa Viongozi na Wananchi kuunga mkono mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) aliouzindua jana kwani pamoja na kufungua fursa mkoani humo lakini pia utasaidia katika kutunza mazingira.

  Mwisho Makamu wa Rais aliwaahidi kubeba changamoto zote kubwa zikiwemo za barabara na huduma za afya ambazo bado ni kilio kikubwa mkoani humo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa azindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini ni  lenyelengo  katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa mahala safi na salama kwa kuishi na kufanya kazi za kimaendeleo.kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama.na kushoto ni Waziri wa kilimo kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hamadi Rashid Uzinduzi hou umefanyika leo Februari 13 /2018 jijini Dar es salaam.


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa mahala safi na salama kwa kuishi na kufanya kazi za kimaendeleo.

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 13, 2018) wakati akizindua mpango mkakati huo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo amesema dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea.

  Waziri Mkuu amesema mbali na mpango kufaa kutumika katika nchi zinazoendelea pia hata kwa nchi zinazokaribia maeneo ya wanyama pori kama Tanzania kutokana na kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa rasilimali.

  Amesema kwa upande wa nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa kuwa Bara hilo, lina sehemu nyingi zinazokaribia mapori makubwa ya wanyama kama Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.

  Waziri Mkuu amesema kwa kutambua hilo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) na wadau wengine wa Maendeleo, imeendelea kutekeleza agenda ya Afya Moja nchini tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mjini Arusha na  Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

  “Utekelezaji wa Mpango huu unakwenda sambamba na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2015-2020) ya kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora itakayowawezesha kuzalisha mali na kutoa huduma mbalimbali ambayo ni muhimu sana katika kufikia azma ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda.”

  Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema uzinduzi wa mkakati huo ni ngao tosha kwa nchi katika kuzuia na kudhibiti magonjwa.

  Alisema pamoja na kutekeleza kanuni za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ambazo zinahitaji ushirikiano  wa sekta mbalilmbali kwa kutumia dhana ya afya moja, mpango mkakati huo unaleta msukumo katika Ofisi ya Waziri Mkuu  kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali kudhibiti magonjwa.

  Bibi Jenista alisema uratibu wa afya moja unakwenda sambamba na matakwa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (IOE) na Shirika la Kimataifa la Chakula la Kilimo (FAO) ambayo yanashirikiana katika kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na usugu wa dawa.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa( Aliye vaa miwani)leo (Jumanne, Februari 13, 2018) amekabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga kwa ajili ya Mamlaka hiyo. Makabidhiao hayo yamefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU


  BAHARI KUU, VIWANJA VYA NDEGE VYABAINIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA-MAJALIWA

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini kwamba maeneo ya bahari kuu, bandari, vituo vya mabasi na viwanja vya ndege yanayotumika sana katika kupitisha dawa za kulevya.

  Hata hivyo Waziri Mkuu amesema wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya wameendelea kukamatwa, lengo ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika nchini.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 13, 2018) wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Amesema mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya sambamba na watumiaji, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali.  

  Waziri Mkuu amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulenya, ambapo hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ilikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.

  “Niwakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili iweze kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo.”

  Pia Waziri Mkuu amewataka Watanzania waachane na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na  kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nayo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Amesema kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata.

  Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo. Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya.

  Kwa upande wake Siyanga aliishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara ya dawa za kulevya. Alisema wanapambana kuhakikisha dawa za kulevya ili zisiingie nchini.

  Alisema mbali na kudhibiti biashara hiyo, pia wanatoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya vikiwemo vitendo viovu vinavyofanywa na watumiaji ili wachukie na waache kutumia dawa hizo.

  Pia wanafanya kazi ya kuwahudumia watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya, hivyo aliwaomba wananchi kutowanyanyapaa waathirika na badala yake wawapeleke katika vituo maalumu vya kutolea huduma za methadone.

   (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, FEBRUARI 13, 2018.  0 0

   Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt.  Mwigulu Nchemba akiongea na vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliyopo stand kuu ya mabasi iramba kuhusu usalama wao waendeshapo pikipiki
  …………………………………………………………………
  …………..
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt. Mwigulu Nchemba leo amewatembelea wafanyabiashara ndogondogo katika soko kuu la wilaya ya Iramba, Madereva wa pikipiki na madereva wa daladala na makodakta waliopo stendi kuu ya mabasi Kiomboi ili kusikiliza changomoto wanazokutana nazo katika utendaji wao wa kazi za kila siku na kuwasilisha katika balaza la madiwani.

  Kwa upande wa madereva wa bodaboda Dkt. Mwigulu amewashauri waendeshe bodaboda zao kwa usalama na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kukamatwa mara kwa mara na askari polisi pale wanapofanya  makosa.

  Wafanyabiashara ndogondogo wa soko kuu la mji wa Kiomboi wamemuomba mbunge wao kuwasaidia kupunguza kodi nyingi ambazo wanakutana nazo wakati wanafanya biashara katika soko hilo, ombi lao limepokelewa na Dkt. Mwigulu na ameahidi kukaa nao ili kuona njia nzuri za kutatua changamoto zao.

  Baraza la madiwani linatarajia kukutana  mchana  leo ambapo changamoto mbalimbali alizozipokea  ataziwakilisha kupata utatuzi katika kikao hicho.

  0 0

  Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akihutubia wakati akiongoza harambee ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana usiku.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama akihutubia katika harambee hiyo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi,Bw.  Godfrey Simbeye akihutubia.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akihutubia.
  Wasanii wakitoa Burudani katika harambee hiyo
  Wadau wakiwa kwenye harambee hiyo.
  Makofi yakipigwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi,  Bw. Godfrey Simbeye na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM), Bw. Tenga B. Tenga.
  Wadau wakiwa kwenye harambee hiyo.
  Harambee ikiendelea.
  Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akitoa zawadi ya picha iliyonunuliwa kwa sh. milioni moja katika harambee hiyo.
  Rais Mkapa akimkabidhi picha  Salama Mussa kutoka Benki ya NBC baada ya kuinunua katika harambee hiyo. Kulia ni Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama na wa pili kushoto ni Mdau Teddy Mapunda mratibu wa harambee hiyo.
  Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez baada ya kuinunua katika harambee hiyo.
  Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha ya simba Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena, Bw. Seraphin Lusala baada ya kuinunua kwenye harambee hiyo.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM),  Bw. Tenga B. Tenga akimkabidhi Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 zilizo tolewa na mgodi huo kuchangia mfuko huo.


  Na Dotto Mwaibale

  RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amewataka wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini ambapo zaidi ya sh.milioni 200 zilipatikana.

  Mkapa alitoa ombi hilo wakati akiongoza harambee ya kuchangia mfuko huo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya nje na ndani pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

  "Ni wajibu kwa kila mwananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia mfuko huu ili kusaidia mapambano ya Ukimwi hapa nchini na kuwa mapmbano hayo si ya mtu mmoja" alisema Mkapa. 

  Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mkapa ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha za Ukimwi katika bajeti zake.

  Akizungumza katika harambee hiyo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema kwamba Serikali itaendelea kusimamia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika matumizi ya  fedha hizo.

  Mhagama alisema asilimia 60 ya fedha hizo zitatumika kununulia madawa, asilimia 25 itatumika katika kutoa huduma za kinga pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi na asilimia 15 zitatumika  kwa ajili ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa programu za Ukimwi.

  Mhagama aliongeza kuwa matumizi ya dawa za kufubaza VVU kwa wanawake ni asilimia 92.9 wakati wanaume ni 86.1 na kuwa katika tisini ya tatu kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15-64 ambao wametoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU asilimia 87.7 ya watu hao inaonyesha kiasi cha VVU kimefubazwa wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84.

  Alisema utafiti huo pia umeonyesha kuwa maambukizo mapya ya VVU (HIV incidence) kwa mwaka kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 Tanzania Bara ni asilimia 0.29 ambayo ni sawa na watu 81,000.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Bw. Godfrey Simbeye alisema sekta binafsi imeunga mkono kwa kiasi kikubwa katika kuchangia mfuko huo na kuwa hakutakuwa na matumizi mabaya ya fedha hizo na zitakwenda kutumika kwa kile kilichokusudiwa.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alimshukuru Rais Mstaafu Mkapa kwa kukubali kushiriki kuongoza harambee hiyo na kueleza kuwa Tacaids imekuwa ikiendesha harambee mbalimbali pamoja na kuandaa mashindano ya michezo na viingilio vyake vimekuwa vikiingia katika mfuko huo.  0 0

  Mtendaji-Mahakama ya Hakimu Mkazi-Musoma, Bi. Zilliper Geke akiongea jambo katika mahojiano maalum. (Picha na Mary Gwera, Musoma-Mara) 
  Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Musoma likiendelea kujengwa. 
  Mafundi wakiendelea na ujenzi. 
  Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa katika ujenzi wa jengo hilo. 
  Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo litakalokuwa na ghorofa mbili. 
   
  Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa katika ujenzi wa jengo hilo.   Na Mary Gwera 

  KAMA ilivyo kwa huduma nyingine katika jamii, huduma ya upatikanaji wa HAKI ni miongoni mwa huduma ambazo wananchi wanahitaji kwa wakati bila longolongo, kufuatia uhitaji huu wa Wananchi, Mahakama ya Tanzania imekuwa na inaendelea katika jitihada za kuboresha huduma ya upatikanaji wa haki kwa kujenga na kukarabati miundombinu bora na wezeshi ya kutolea haki. 

  Tukiangazia Mkoa wa Mara ambapo kwa kipindi kirefu wananchi wake wamekuwa na wanaendelea kupata shida hususani katika upatikanaji wa huduma ya haki kwa ngazi ya Mahakama Kuu ambapo Mwananchi mwenye kesi anatakiwa kusafiri kwa kilomita zipatazo 218 kwenda Mahakama Kuu Mwanza ili kutafuta haki yake. 

  Kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma ya Haki nchini, Mahakama ya Tanzania imekuwa ikifanya ujenzi na matengenezo ya majengo yake kwa awamu kulingana na hali ya bajeti, kwa sasa Mahakama ya Tanzania imeanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa miwili ambayo ni Mara na Kigoma. 

  Katika mahojiano maalum na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Bibi. Zilliper Geke yaliyofanyika ofisini kwake Mahakama ya Mkoa-Musoma, Februari 13, Bi. Zilliper anasema kuwa ujenzi wa Mahakama Kuu unaoendelea katika Kanda hiyo umeleta faraja na ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kwani wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kusafiri kilometa kadhaa kwenda mkoani Mwanza kutafuta haki zao kwa ngazi ya Mahakama Kuu. 

  “Kwakweli wananchi wa Mkoa huu na hata wateja wanaokuja katika Mahakama ya Mkoa, wanaonekana kufurahia ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambapo pindi itakapokamilika itawaondolea usumbufu wa kusafiri hadi Mwanza kupata huduma” alieleza Mtendaji huyo. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya D.F MISTRY& CO (1974) LTD, Kampuni ambayo imepata tenda ya ujenzi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma, Eng. Bhavesh anasema ujenzi wa Mahakama hiyo ulioanza rasmi Novemba 11, 2017 unaendelea vizuri kama ratiba ilivyopangwa. 

  “Ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma umepangwa kumalizika ndani ya miezi 18 ambao ni sawasawa na mwaka mmoja na nusu, hivyo kwa hatua tuliyofikia sasa tuko mbele zaidi hali ambayo inaridhisha kuwa ujenzi huu tutamaliza ndani ya muda kama hakutakuwa na changamoto yoyote,” alisema Mkurugenzi huyo. 

  Aidha Eng. Bhavesh anabainisha juu ya hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa sasa kuwa ni ujenzi wa ghorofa ya kwanza ‘first floor’ ya jengo hilo ambayo anasema kuwa itachukua muda wa takribani mwezi mmoja hadi kukamilika kwa hatua hiyo. 

  “Hatua hii ya ujenzi itatuchukua takribani mwezi mmoja toka sasa, kwa sasa tunakwenda vizuri, hivyo mara baada ya kukamilika kwa hatua ya ujenzi ya ghorofa ya kwanza tutaendelea na ghorofa ya pili, na kazi hii ya ujenzi wa jengo zima la Mahakama Kuu Musoma inatakiwa kukamilika ifikapo Aprili 19, 2019,” alieleza Eng. Bhavesh. 

  Akionyesha kufurahishwa na ujenzi wa Mahakama hiyo, kwa upande wake Wakili wa Kujitegemea-Mkoani Mara, Bw. Thomas Makongo anaeleza kuwa uamuzi wa Mahakama ya Tanzania kujenga Mahakama Kuu-Musoma utasaidia kuharakisha ‘speed up’ mashauri na kuipunguzia mlundikano wa Mashauri Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza. 

  “Hata hivyo naweza kusema kuwa, ujenzi wa Mahakama Kuu Mara umechelewa sana kwa sababu mkoa huu una mashauri mengi ya Jinai hususani ya mashauri ya Mauaji, kwahiyo kukosekana kwa Mahakama Kuu katika Mkoa huu kumechangia ucheleweshaji wa mashauri haya kusikilizwa na kumalizwa kwa wakati,” alisema Wakili Makongo. 

  Aidha, Wakili huyo anaendelea kusema kuwa kuwepo kwa Mahakama Kuu Mara kutasaidia pia kushughulikia migogoro dhidi ya Watendaji wa Mahakama kwa ukaribu zaidi. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi, Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi amesema kuwa ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambao unasimamiwa na ‘HAB Consult’ na ‘Mbega Associates’ unaenda sambasamba na Ujenzi wa Mahakama Kuu Kigoma. 

  “Kukamilika kwa Mahakama Kuu hizi mbili kutafanya idadi ya kuwa na jumla ya Kanda za Mahakama Kuu 16 kati ya mikoa 26, na hivyo uhitaji utakaobaki ni wa Majengo 10 tu,” alieleza Mhandisi Kitunzi. 

  Hata hivyo, Mhandisi Kitunzi anasema kuwa taratibu za ujenzi wa Mahakama Kuu katika baadhi ya mikoa iliyobaki zinaendelea, na Mahakama hizo zitajengwa chini ya Fedha za Mradi wa Benki ya Dunia (WB) Mikoa itakayojengewa Mahakama Kuu/Vituo vya Haki ‘Justice centre’ ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Mwanza na Arusha. 

  Aidha; kwa upande wa ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi, Mhandisi Kitunzi anabainisha kuwa ujenzi wa Mahakama hizo pia unaendelea katika mikoa ya Geita, Njombe, Lindi, Katavi na Simiyu. 

  Azma ya Mahakama ya Tanzania ni kusambaza huduma za Mahakama nchi nzima ili hata mwananchi aliyepo katika ngazi ya Kata aweze kupata huduma ya Haki. 

  Mbali na ujenzi pia kumekuwa na ukarabati wa majengo ya Mahakama ya mara kwa mar azote zikiwa ni jitihada za kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya majengo bora ya kutolea haki. 

  Hivi karibuni katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini jumla ya Majengo mapya matano (5) ya Mahakama yalizinduliwa rasmi; majengo hayo ni pamoja na Kituo cha Mafunzo na Habari za Mahakama kilichopo Kisutu Dar es Salaam, Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mahakama ya Wilaya Mkuranga pamoja na Mahakama ya Mwanzo Kawe.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu pajini wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018
  Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na waumini wenzao baada ya ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Padri Venance Tegete baada ya kujiunga baada ya ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.Picha na IKULU

  0 0

  Meneja wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Pwani ,mhandisi Yudas Msangi akizungumza jambo ofisini kwake ,kuhusiana na masuala ya barabara Mkoani hapo ( picha na Mwamvua Mwinyi)
  ……………………………………………………………………………….
  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  KIASI cha sh. bilioni 23.061 zimepangwa kutumika kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya miradi ya matengenezo mbalimbali ya barabara ,mkoani Pwani, katika kipindi cha mwaka 2018/2019 .Aidha katika kipindi hicho kiasi cha shilingi bilioni 10.4 zimepangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 518 za barabara kuu madaraja madogo 23 na makubwa mawili.

  Hayo yamesemwa mjini Kibaha na meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani, Mhandisi Yudas Msangi wakati wa kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo.Pamoja na hayo ,alisema kiasi cha shilingi bilioni 14 zitatumika kutengeneza barabara zinazounganisha maeneo muhimu ya kiuchumi ili kurahisisha mawasiliano kwenye maeneo hayo.

  Hata hivyo ,Msangi alielezea shilingi bilioni 12.5 zitatumika kwenye matengenezo ya barabara za mkoa huo .“Matengenezo ya kawaida lami kilometa 501.7 yametengewa shilingi bilioni 3.1, matengenezo maalumu lami kilometa 15.6 yametengewa kiasi cha shilingi bilioni 7 huku matengenezo ya sehemu korofi 0.7 kilometa yametengewa kiasi cha shilingi milioni 57.9,”alifafanua Msangi.

  Alibainisha matengenezo madogomadogo ya madaraja 23 yametengewa kiasi cha shilingi milioni 74 na matengenezo makubwa ya madaraja mawili yametenegewa kiasi cha shilingi milioni 200.4.Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema katika kuelekea kwenye ukanda wa viwanda ,ni lazima miundombinu ya barabara iboreshwe na kujengwa ili kuvutia wawekezaji.

  Aliitaka Tanroads kutekeleza miradi hiyo kama ilivyoomba ili kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara.Ndikilo ,aliwaasa pia wananchi kulinda na kuacha kuharibu alama zinazowekwa barabarani .

  Wakati huo huo mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka ,aliomba ufafanuzi juu ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kwamatias hd Nyumbu.
  Meneja wa TANROADs Pwani ,alimtoa hofu Koka kuwa barabara hiyo itajengwa mita 300 kwa mil.200.9 na ujenzi utaanza wakati wowote kuanzia sasa.

older | 1 | .... | 1516 | 1517 | (Page 1518) | 1519 | 1520 | .... | 1904 | newer