Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

SIXTUS MAPUNDA AMNADI KWA KISHINDO MTULIA, KINONDONI SHAMBA

$
0
0
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam.( PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam
Sixtus na Mtulia wakiselebuka Singeli baada ya Mtulia kupanda jukwaani kinadiwa
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam

Mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Kinondooni Said Mtulia akisalimia wananchi wakati akinadiwa na Mbunge wa mbinga mjini Sixtus Mapunda katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika kata ya Kinondoni Shamba, jijini Dar es Salaam
Mbombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni Sad Mtulia akiomba kura kwa wananch katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam, leo Feb 213, 2018
Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda akitamba jukwaani kumuombea kura kwa wananchi mgombea wa CCM Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kata ya Kinondoni Shamba, Dar es Salaam, leo Feb 13, 2018.
Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda akisisitiza jambo jukwaani kumuombea kura kwa wananchi mgombea wa CCM Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kata ya Kinondoni Shamba, Dar es Salaam, leo Feb 13, 2018
Baadhi ya Wabunge wakiwa jukwaaani kumuombea kura mgombea ubunge wa CCM Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Kata ya Kinondoni Shamba, leo Feb 13, 2018
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate kamba akimkaribisha jukwaani sixtus Mapunda
Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akimuombea kura mgombea ubunge wa CCM Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018 katika Kata ya Kinondoni Shamba Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa akimuombea kura mgombea Ubunge wa CCm Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018 katika Kata ya Kinondoni Shamba Dar es Salaam,.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Sophia Simba akiwasili kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM uliofanyika leo katika Kata ya Kinondoni Shamba dar es Salaam, leo Feb 13, 2018
Mweneyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba (kulia) akijadili jambo na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kinondoni Said Mtulia, wakati wa mkutano wa kampeni za CCm uliofanyika leo Feb 13, 2018 katika kata ya Kinondoni Shamba Dar es Salaam. katikati ni Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda
Mweneyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba (kulia) akiwa na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kinondoni Said Mtulia (kushoto) baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni za CCm uliofanyika leo Feb 13, 2018 katika kata ya Kinondoni Shamba Dar es Salaam. katikati ni Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda


Kijana Amina Mohammed akionyesha umahiri wa kucheza danadana wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM Said Mtulia uliofanyika leo Feb 13, 2018 katika kata ya Kinondoni Shamba dar es Salaam.


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Kinondoni Said Mtulia akisalimiana kwa furaha na Mzee Maarufu wa Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam, Shaaban Uledi wakati akiingia kwenye eneo la mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo leo Feb 13, 2018. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea Jaji Costa Mahalu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea Jaji Costa Mahalu mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAKULIMA WA KOROSHO PWANI WANEEMEKA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha 

Wakulima wa zao la korosho Mkoa wa Pwani wamefanikiwa kupata kiasi cha sh. bilioni 57.7 kutokana na mauzo ya zao la korosho ,msimu huu. Mafanikio hayo yametokana na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umetumika miaka mitatu iliyopita tangu kuanzishwa kwenye Mkoani hapo. 

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC). Alisema fedha hizo zimepatikana kutokana na minada sita hadi kufikia Januari mwaka huu ambapo minada hiyo ilianza Novemba mwaka jana. 

Ndikilo alifafanua ,kilo zilizouzwa ni 20,399,325 za daraja la kwanza ni kilo 11,554,380 na daraja la pili ni kilo 8,814,945. “Kilo hizo kwa daraja la kwanza ziliingiza kiasi cha shilingi bilioni 35.8 na daraja la pili shilingi bilioni 21.4 kwa wakulima wa mkoa huo” 

“Wilaya ya Mkuranga imeweza kuongoza kwa kuuza na kupata mapato makubwa ikiwa imeingiza kiasi cha bilioni 13 ikiwa imeuza kilo milioni 4.1, Kibiti waliingiza bilioni 4 kwa kuuza kilo milioni 4,Rufiji bilioni 2.8 kwa kuuza kilo milioni 1.5,” alisema Ndikilo. Awali katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Shangwe Twamala alieleza, bei ya juu kwa korosho daraja la kwanza ilikuwa ni shilingi 3,817 kwa kilo na daraja la pili ni shilingi 2,950. 

Twamala alisema baadhi ya changamoto ni pamoja na mfumo huo umepata changamoto za malalamiko ya wanunuzi juu ya kushuka ubora na upungufu wa uzito. Alisema baadhi ya wanunuzi kushindwa kuwalipa wakulima kwa wakati, uhaba na ubora wa maghala,baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kutokuwa waaminifu. 

Pamoja na hayo, mkoa huo umetoa mapendekezo ya mpango wa bajeti wa shilingi bilioni 296.7 kwa mwaka 2018/2019. Akitoa mwelekeo wa bajeti ya mkoa katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Edward Mwakipesile alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo. 

Mwakipesile alisema kuwa ili kutekeleza mpango na bajeti ya sekretarieti ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa kwa mwaka huo wa fedha. Alisema kuwa kati ya fedha hizo bilioni 222.4 zitatumika kwa ajili ya malipo ya mishahara ya watumishi, bilioni 32.4 kwa ajili ya miradi ya aendeleo,bilioni 23.8 ni mapato ya ndani bilioni 18 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo. 

“Katika fedha za miradi ya maendeleo za ndani ni bilioni 25 na za nje bilioni 7.3 kwa ajili ya miradi mbalimbali,” alisema Mwakipesile.
 
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC)kuhusiana na mipango na mkakati mbalimbali ya kuendeleza maendeleo ya kimkoa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Naibu Waziri awasha Umeme Gongolamboto

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyekaa) akiwasha umeme katika kituo cha Gongolamboto kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya Kompyuta.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya uendeshaji wa kituo cha Gongolamboto , kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James,(mbele) wakati akikagua mitambo ya kituo hicho kabla ya kuwasha kwa mtambo huo.kushoto ni Kaimu Meneja Miradi , Mhandisi Emmanuel Manirabona.
Baadhi ya watendaji katika kituo cha Gongolamboto, wakikamilisha kazi kabla ya kuwasha umeme katika kituo hicho.
Transfoma iliyofungwa mwaka 57, ( kulia) iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza umeme katika kituo cha Gongolamboto,na mpya zilizowekwa sasa( kushoto).
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wapili kushoto) akizungumza na mkandarasi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala. kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James

……………………………………………………………..

Na Zuena Msuya, Dar es salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolamboto chenye uwezo wa MVA 65 na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mgalu alisema Kituo hicho kinapokea umeme kutoka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi katika line ya 132 kV.

Mgalu alifafanua kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumewezesha uboreshaji wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kurasini, Kipawa, Kitunda, Chanika na Kisarawe, Ubungo, Mbagala na GongolaMboto.

“Kwa sasa hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yakisambaziwa umeme kutoka katika kituo hiki haitakuwepo tena, hivyo Serikali itaendelea na juhudi kuwasha umeme katika vituo vingine vilivyosalia,” alisisitiza Mgalu.

Kituo cha Gongolamboto ni miongoni mwa vituo 19 vya kupoza na kusambaza umeme nchini vilivyo katika mradi wa uboreshaji wa vituo hivyo unaofadhiliwa na TEDAP ambapo Jiji la Dar es salaam lina vituo 11, Arusha vituo Sita (6) na Kilimanjaro vituo viwili (2

KWANDKWA: SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA UJENZI NA UCHUKUZI MKOA WA TANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighella mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya Naibu Waziri huyo ajaanza kukagua miradi ya barabara katika Wilaya za Pangani na Muheza jana Jumanne Februari 13, 2018. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiaino, Elias Kwandikwa akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara katika Wilaya hiyo jana Jumanne Februari 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Bi. Zainab Issa. 
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbaro akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (wa pili kulia)kuhusu ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa kilometa 550 linalotarajia kujengwa na Serikali katika Mto Pangani wakati wa ziara yake Wilayani humo jana Jumanne Februari 13 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi. Zainab Issa. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu ufafanisi wa utendaji kazi wa kivuko cha MV Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya barabara na vivuko katika Wilaya ya Pangani na Mkoa wa Tanga kwa ujumla katika ziara yake jana Jumanne Februari 13 2018. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA), Mhandisi Magreth Ginna. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika kivuko cha MV Tanga iliyopo Pangani wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara na vivuko katika Wilaya za Mkoa wa Tanga jana Jumanne Februari 13, 2018. Anaongoza nao Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi, John Semhande na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Magreth Ginna na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Issa. (PICHA NA MAELEZO 

………………… 



Na Ismail Ngayonga -MAELEZO 


NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema Serikali imekusudia kuimarisha sekta ya ujenzi na uchukuzi katika Mkoa wa Tanga ikiwemo Ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa Mita 550 katika Wilaya ya Pangani, hatua inayolenga kufungua fursa na kuinua pato la kiuchumi kwa wanachi wa Mkoa huo. 

Akizungumza katika mkutano wake na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Sheghela jana Jumanne Februari 12, 2018, Naibu Waziri Kwandikwa aliyopo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara Mkoani humo, alisema lengo la Serikali ni kuimarisha miundombinu ya barabara, bandari na uwanja wa ndege katika Mkoa wa Tanga. 

Kwandikwa alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imekusudia kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo yenye urefu urefu wa kilometa 242, ambapo tayari kazi ya usanifu wa barabara hiyo tayari umeaanza, ambapo wakati wowote kutoka sasa Serikali inatarajia kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo. 

“Kwa kipande cha barabara ya Tanga-Pangani ambayo imekuwa kilio cha wananchi wa Pangani kwa kipindi kirefu, tayari tumeanza hatua ya usanifu wa barabara hiyo, ambapo Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo” alisema Kwandikwa. 

Aliongeza kuwa Serikali pia imepanga kuharakikisha ujenzi wa Barabara ya Handeni-Kilindi-Nchemba-Mkoro yenye urefu wa kilometa 461 ambayo inatarajia kuunganisha Wilaya ya Kondoa na Mkoa wa Singida, hatua inayolenga kuongeza fursa ya shughuli za uzalishaji mali kwa kuzingatia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta linloatarajiwa kuanza ujenzi wake mwaka huu. 

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege na uimarishaji wa bandari ya Mkoa wa Tanga, Naibu Waziri Kwandikwa alisema uwezeshaji na utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wake upo katika miradi ya Afrika Mashariki, ambapo kukamilika kwake kutasaidia kuzalisha ajira na kuongeza mvuto wa Mkoa wa Tanga kwa wawekezaji mbalimbali. 

Kwa mujibu wa Kwandikwa alisema mbali na Mkoa wa Tanga, Serikali imekusudia kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini kwa wakati hatua inayolenga kuwapunguzia gharama wananchi na kuokoa muda wa kusafirisha bidhaa na malighafi. 

“Ujenzi wa Barabara ya Handeni-Kilindi-Nchemba-Mkoro ukikamilika unatarajia kuokoa zaidi ya kilometa 150 kwa abiria wanaosafiri kutoka Dar Es Salaam hadi Singida, huu ni mradi muhimu na hivyo tutaupa kipaumbele cha pekee” alisema Kwandikwa. 

Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Tanga, Martin Sheghella alisema ujenzi wa miundombinu ya uhakika ikiwemo uimarishaji wa bandari ya Tanga katika Mkoa huo utasaidia kuongeza pato la wananchi na mapato ya Serikali kwa kujenga ushawisihi wa Nchi jirani ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutumia Bandari hiyo. 

“Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Shehena za mizogo Milioni 28 zinasafirishwa katika nchi jirani za Burundi, Rwanda, Uganda na DRC lakini iwapo tutaimarisha bandari ya Tanga tutaweza kukifanya nchi hizi zikatumia bandari yetu” alisema Sheghella.

ETIHAD AVIATION GROUP LAUNCHES HUMANITARIAN AID MISSION FOR ROHINGYA REFUGEES

$
0
0

Etihad team visiting the Rohingya camp in Bangladesh.
Abu Dhabi, United Arab Emirates - Etihad Aviation Group (EAG) has launched a humanitarian aid mission in support of Rohingya refugee families. The campaign commenced with the distribution of garments, dry food packages, and blankets to more than 3,000 Rohingya families in Bahukhali Bazar in Bangladesh.

The initiative is funded by the generous miles donations of Etihad Guest members, in addition to donations made at various Abu Dhabi-based sporting and social events, as well as the electronic Dirham initiative.

The mission also included humanitarian aid distribution at a hospital jointly operated by Malaysia, the United Arab Emirates and the Kingdom of Saudi Arabia.

The EAG delegation included Khaled Al Mehairbi, Senior Vice President & General Manager of Etihad Airport Services - Ground, and CSR Strategy, Ali Al Shamsi, Vice President Global Airports, and Dougie Douglas, General Manager, commercial activities in Bangladesh, Sri Lanka and Nepal.

Earlier this year, EAG announced a year-long programme of activities and humanitarian initiatives to mark 2018 as the Year of Zayed.

Al Mehairbi said: “Today, the Rohingya are in dire circumstances and it is incumbent upon us to do all we can to support them. Driven by our founding father, the late Sheikh Zayed’s decades-long charitable activities, Etihad Aviation Group is hoping to play a small role in alleviating the Rohingya’s current conditions.”

In recent months, hundreds of thousands of Rohingya have fled violence to Cox's Bazaar - a district in Bangladesh. The vast majority are women and children, including new-born babies. It is known as the fastest-growing refugee emergency in the world. Many refugees have experienced extreme trauma, both from the attacks and the difficult journey to the Bangladeshi border. They arrive hungry, in poor physical condition and in desperate need of life-saving support.

Implemented via an agreement between EAG and the UAE Embassy in Bangladesh, this humanitarian mission was undertaken in cooperation with the Emirates Red Crescent and the Bangladeshi Red Crescent.
  
The UAE government has already pledged US$7 million in support of the Rohingya community.

During the past five years, EAG has also supported refugees in Greece, Serbia, Lebanon and Jordan.

Barclays hosts an economic forum for its corporate clients

$
0
0
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left), addresses participants during the bank’s Economic Forum hosted for its corporate and investment banking clients in Dar es Salaam over the weekend. Far from right are Absa Capital economic researcher, Samantha Singh, Barclays Tanzania CFO, Obedi Laiser and banks Corporate Director, Esther Maruma. 
 Barclays Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser (left), highlights the BBT performance during the bank’s economic forum hosted for its corporate and investment banking clients.
 Barclays Bank Tanzania Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (right), chats with South Africa’s Absa Capital economic researcher, Samantha Singh (left), during the bank’s economic forum hosted for its corporate and investment banking clients in Dar es Salaam. Second left is BBT Corporate Director, Esther Maruma and the bank’s Marketing Officer, Nasikiwa Berya.
 It is all similes for Barclays staff as they share a light moment with customers during the forum.
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (centre), talks to a customer during the bank’s economic forum organized for its corporate and investment banking clients in Dar es Salaam.

 Some Barclays officials and the bank’s customers socialise during the function.
Barclays Bank Tanzania senior officials exchange views during the forum. From left: Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga, Chief Financial Officer, Obedi Laiser and Marketing and Communications  Manager, Joe Bendera.


Barclays Corporate and Investment Banking (CIB) clients were invited for an evening hosted by the bank, whereby the main agenda for the evening was to present the banks 2017 financial performance, future ambitions and the 2018 economic outlook for Tanzania. 

Speaking during the event, which took place at the Serena Hotel, Barclays Managing Director, Abdi Mohamed said “We had a tremendous year in 2017, and look forward to exceeding our own expectations in 2018. Our ambition is to create a business that is modern, agile and fit for purpose. 

Our focus will still be on ensuring we make our customers’ and clients’ lives easier by simplifying our business processes to better serve our customers and clients, by sustainably reducing costs and improving efficiencies. Our continued investment in people, our technology and digital innovation will still be a key component to our success and our commitment to our communities in which we serve will continue to be an area of focus”

In 2017, Barclays was awarded the Best Commercial Bank in Tanzania by the Banker Africa. Abdi continued, “The award received was based on ‘peer voting’, and such, we were proud of this recognition by the industry in Tanzania”. 

Also in attendance, was Barclays Chief Financial Officer, Mr. Obedi Laiser, who commented on the banks performance. “As a total bank, our performance in 2017 was the best in the last five years. Our Profit Before Tax (PBT) was TZS 11.3 Billion, which positions Barclays as the ‘Best Performer of the year’. Even though there was an indication that banks would struggle to maintain a favourable NPL ratio, Barclays was able to reduce NPL ratio to 8.5% which is below the industry average.”. He continued, “In 2018 we have set new challenges and goals for ourselves, and we are working harder than ever to ensure that we replicate and surpass our 2017 performance”. 



On the economic outlook, Sam Singh an economic researcher from Absa Capital commented “In 2018, Tanzania’s GDP is expected to improve, given the recovery in the Agriculture sector and its long term commitment in the development of industries in the country will help propel further economic developments”

MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.

Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.

Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.

Alisema umeme unaozalishwa nchini humo kwa sasa ni Megawati 140 pekee huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 17 kiasi ambacho alisema kimeshindwa kukidhi mahitaji.

“Sasa hivi tumebaki na megawati 140 peke yake, hali siyo shwari; suluhisho la haraka linahitajika ili kuweka mambo sawa. Imani yetu ni kwa Tanzania kutazama namna ya kusaidia katika hili,” alisema.

Alibainisha kwamba chanzo kikuuu cha uzalishaji wa umeme nchini humo ni maporomoko ya maji na kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, chanzo hicho kimeshindwa kuzalisha umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.

Aliongeza kwamba Serikali ya Malawi imeamua kuwa na vyanzo mbadala vya kuzalishia umeme ikiwemo Gesi Asilia hata hivyo alisema hakuna Gesi Asilia inayozalishwa nchini humo na kwamba matarajio yao ni kupata Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.

“Tumefarijika, tumepokelewa vizuri, lengo la ujio wetu ni kubaini uwezekano wa kupata Gesi Asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme,” alisema Masi.

Alisema kwamba baada ya tathmini waliyoifanya wamebaini kwamba chanzo cha haraka kinachoweza kuwasaidia kuvuka kwenye upungufu mkubwa wa umeme uliyoikumba nchi hiyo kwa sasa ni Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa tayari mwekezaji amepatikana ambaye atazalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kwamba atajenga mitambo yake kwenye eneo la Kalonga mpakani mwa Tanzania na Malawi.

Kwa upande wake Waziri Kalemani alisema suala hilo linaweza kujadiliwa baada ya wataalam wa Tanzania kujiridhisha uwezekano wake.

“Tupo tayari kushirikiana, kinachohitajika hapa ni majadiliano ya kitaalam na wataalam wetu waliopo hapa ili kuelewa mwelekeo,” alisema Waziri Kalemani.

Dkt. Kalemani aliwasisitiza wataalam hao kabla hawajafanya majadiliano wanapaswa kuelewa mambo makuu matatu ambayo wingi wa Gesi Asilia iliyopo kwa sasa, matakwa ya Sera ya Nishati na namna ambavyo Gesi hiyo inaweza kusafirishwa hadi huko Kalonga.

“Je tunayo gesi ya kutosha kugawana ama ni ya kutosha kwa matumizi yetu tu? Je Sera inaruhusu suala hilo? Na kama masuala hayo yanakubalika, Je ni vipi tutaifikisha hiyo Gesi huko mpakani?” alihoji Dkt. Kalemani.

Aliueleza ujumbe huo kuandaa mpango wa ombi lao kimaandishi pamoja na kuandika ombi rasmi na kuwasilisha katika utaratibu maalum wa Kiserikali ili majadiliano yafanyike.

Aidha, suala la Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe, Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana kupitia taarifa ya Tume ya Uendelezaji wa Bonde hilo ambayo inaundwa na nchi hizo mbili ili kubaini hatua za kuchukua kwenye kipengele cha kuzalisha umeme.

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika bonde hilo ni pamoja na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 180 ambazo zitagawanya sawa kwa nchi hizo, kilimo cha umwagiliaji, (hekta 6,200) usambazaji wa maji kwa wananchi, ujenzi wa miundombinu ya jamii (bararabara, shule, na vituo vya afya).

Miradi mingine ni uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, uvuvi, utalii na uboreshaji wa mazingira, hususan kuimarisha kingo za mto ambao ni mpaka wa Tanzania na Malawi.
 Mawaziri kutoka Malawi mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa ajili ya majadiliano kuhusu masuala ya Nishati na mwenyeji wao Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kushoto ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa.
 Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Mawaziri kutoka Malawi (hawapo pichani).
 Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Mawaziri kutoka Malawi. Kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini wa Malawi, Aggrey Masi.
 Viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake wakiendelea na majadiliano. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ally Ubwa, Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi. Kutoka kulia ni Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Tanzania, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi mara baada ya kumalizika kwa majadiliano ya masuala ya Nishati.
Ujumbe kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).

BIL. 161.9 ZIMETUMIKA KUBORESHA VITUO VYA AFYA 170-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9 kuboresha vituo vya afya 170 nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa maisha yao.

Amsema Serikali itaendelea kukarabati na kupanua miundombinu ya kutolea huduma pamoja na kununua vifaa vya kisasa katika Hospitali za Mloganzila, Benjamini Mkapa, Dodoma na Hosptali za Rufaa katika Mikoa na Kanda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) wakati akizindua jengo  jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Amana iliyopo wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo la ghorofa mbili limejengwa kwa ufadhili wa kundi la kampuni za AMSONS na lina thamani ya sh bilioni 1.2.

Amesema uzinduzi wa jengo hilo  unakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt. John Magufuli za kuimarisha sekta ya afya na kuifanya kuwa miongoni mwa sekta za kipaumbele.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi. “Mfano, Hospitali za Rufaa za Amana, Mwananyamala na Temeke, zimeendelea kuhudumia wagonjwa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya vya Serikali, binafsi na vya dini kutoka mikoa jirani ya Pwani, Morogoro na Lindi.

Pia amesema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, kuhusu kuwapatia wananchi huduma bora za afya pamoja na kujenga hospitali nyingine za Rufaa kwa ajili ya Kanda ya Kusini, Kati na Magharibi.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya idadi ndogo ya watumishi na ukosefu wa huduma za uangalizi maalumu (ICU) katika hospital ya Amana, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto zote zilizopo katika sekta ya afya zikiwemo n aza hospital hiyo.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wadau mbalimbali pamoja na kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa huduma za afya nchini zinaboreshwa.

Hivyo, alitumia fursa hiyo  na kulipongeza kundi la kampuni za AMSON’s lililoamua kujenga jengo la mama na mtoto katika hospital hiyo kwa ushawishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda.

Awali, Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana, Dkt. Meshack Shimwella alisema wazazi wanaolazwa katika hospitali hiyo kwa siku ni 180 hadi 250 na uwezo wa hospitali ni vitanda 353, ambapo vitanda 250 vinatumika wodi ya wazazi.

Alisema idadi hiyo hailingani na idadi ya wagonjwa, hivyo kusababisha wakati mwingine wagonjwa kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kutokana na kasi ya ongezeko wa wagonjwa wanaolazwa hususani wodi ya watoto na akinamama.

Dkt. Shimwella alisema wamefanikiwa kuongeza jingo la kutolea huduma ya mama na mtoto lenye ghorofa mbili ilililojengwa kwa ufadhili wa AMSONS lenye uwezo wa vitanda 100, ambalo ndilo liliongeza idadi ya vitanda kutoka 253 hadi kufikia 353.

“Kutokana kukamilika kwa jengo hilo kwa sasa akinamama wanaonyonyesha wanalala wakiwa mmoja mmoja, watoto wachanga wanahudumiwa katika mazingira mazuri yanayofanana na viwango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Makonda aliwashukuru wafadhili waliojenga jengo hilo kwa sababu si kila mtu anayekwenda hospitali na kukuta changamoto na akaamua kuzifanyia kazi.

Bw. Makonda alisema awali akinamama walikuwa wanalala hadi watatu katika kitanda kimoja, hivyo madhumuni ya ujenzi wa jego hilo ni kupunguza msongamano katika wodi ya wazazi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 14, 2018.

SERIKALI YAPOKEA ZANA ZITAKAZOTUMIKA KUKUSANYA NA KUTOA TAARIFA ZA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

$
0
0
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA.
Serikali imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.

Zana hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).

Wakati wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.

Dkt. Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.

“ Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema Dkt. Ng’ondi.

Nae Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la John Snow Inc (JSI) Dkt. Tulli Tuhuma amesema kuwa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii unaosimamia na JSI unalengo la kuimarisha mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii.

“Zana hizi tisa ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani USAID na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI na zitawasaidia wasimamizi wa mashauri ya watoto kuweka kumbukumbu na kufuatilia mashauri ya kiulinzi, ustawi wa jamii na afya katika halmashauri na kutoa huduma pamoja na rufaa kwa watoto walio katika mazingira hatarishi”alisema Dkt. Tulli.

 Aidha, Dkt. Tulli ameongeza kuwa awali kulikuwa na muingiliano wa katika utoaji wa huduma na kusababisha ugumu katika kufanya ufuatiliaji wa huduma na upatikanaji wa takwimu.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akifungua  kikao cha makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kulia) akimpongeza Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi (kushoto)baada ya kufungua  kikao cha makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi  kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Meneja Miradii wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw. Grey Saga akizungumzia miradi inayofadhiliwa na Shirika hilo wakati wa  Kikao cha Makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Miradi JSI Dkt. Tulli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika makabidhiano ya zana hizo katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika  Kikao cha makabidhiano ya  zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akikata utepe kuzindua zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika hafla ya makabidhiano ya zana hizo katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14, 2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi pamoja na wadau wakionesha zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya Kikao cha makabidhiano ya  zana hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

kwamkonga yakabidhiwa vifaa vya afya kuboresha huduma ya zahanati hiyo

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigela akizungumza na watumishi na wananchi wa Komkonga juu ya utunzaji wa vifaa hivyo na kupongeza uongozi wa Halmashuri kwa ujenzi wa maabara ndogo.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe aki shukuru Rais kwa fedha alizozitoa na kufikia hatua ya kupokea Vifaa hivyo kwenye Zahanati ya Komkonga.
 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dk. Credeanus Mgimba akisoma taarifa ya vifaa vilivyonunuliwa.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa akishukuru kwa kuletewa vifaa vitakavyosaidia kuboresha huduma ya Afya kwa wananchi wa Komkonga na kupunguza adha ya kufata hudduma hizo maeneo ya Mkata na Handeni.
 Baadhi ya Wananchi wa Komkonga waliofika kushuhudia makabidhiano.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akisaidiana na mganga mkuu katikati na mkuu wa Mkoa kutoa hadubini tayari kwa kuikabidhi kwa viongozi wa Komkonga.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigela(kulia) akikabidhi hadubini kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Komkonga Bw.Omary Mngazija ikiwa ni moja ya kifaa kwaajili ya kuboresha huduma za Zahanati ya Komkonga.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Komkonga Bw.Omary Mngazija akishangilia kupokea hadubini ikiwa ni moja ya kifaa alichokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella mwenye suti ya kijivu kwaajili ya kuboresha huduma za Zahanati ya Komkonga.

WAPIGA DILI,WALA RUSHWA HAWATAKIWI CCM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kiwalani,Mathias Kahinga kulia)akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake,leo jijini Dar es Salaam.


MWENYENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya kiwalani Mathias Kahinga Amesema katika kipindicho chote cha uongozi wake wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake nakudai mbeleko za kuwabebea zimechanika.

Amesema kwake ni kuchapa kazi aliyotumwa na wanachama wa Chama chake kwa lengo kuu la kutatua na kuisimamia Serikali huku akitoa rai kwa viongozi wezake ndani ya chama hicho kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wenye unyenyekevu kwa wananchi na kutatua kero zao.

Mwenyekiti na kada huyo wa Chama ameyasema haya jijini Dar es salaam katika ofisi za Chama hicho Kata zilizopo Kata hiyo ya kiwalani ndani ya manispaa ya Ilalat. Ambapo amesema kwake wapiga dili na wezi hawana nafasi kabisa.

"Nilikuwa na mambo kadhaa ambayo nilihaidi kwa wanaccm wakati nautaka uwenyekiti na moja ya kazi yangu kubwa ni kurejesha mtaa mmoja wa serikali ya mtaa ambao unatawaliwa na CUF kwa miaka 15 sasa na hakuna maendeleo yeyote ndani ya mtaa huo wa kigilagila. "amesema Kahinga

Pia alisema jambo lingine ambalo alihaidi nikuona ofisi za Chama hicho zinakuwa katika mwenekano iliobora kabisa tofauti na ilivyo sasa na tayari kuna hatua mbalimbali ambazo amezichukuwa na anasubiri maombi yake ambayo ameyapeleka ngazi za juu za chama hicho.

Mwenyekiti huo ameongeza kuwa amepanga safu yake vilivyo ambayo lengo lake kubwa nikufanya kazi karibu na wananchi wa Kata hiyo ya kiwalani kwa maana ya kuisimamia serikali vilivyo ili 2019 waweze kurudisha mtaa ambao umekwenda upinzani.

Amesema inawezekana utendaji mdogo wa huko nyuma Kwa kiasi kikubwa ulichangia mtaa kwa miaka yote kuendelea kuwa chini ya Chama cha upinzani pamoja na ngazi ya udiwani."kimsingi sina muda wa kubeba wezi, na kila mmoja afanye kazi kwa moyo kama jinsi akivyoomba nafasi aliyopo na kamwe hatahitaji watu ambao hawatimizi wajibu wao. "amasema Kahinga.

Naye Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani  Eva Malenga Amewatoa hofu wanachama wa hicho kuhusu uwepo wa tetesi ya baadhi ya maeneo yao kudaiwa ni maeneo ya wazi ya serikali nakudai kuwa madai hayo hayana hoja nakwamba wao wamefuata taratibu zote za kumiliki maeneo hayo.

Amesema kila eneo ambalo wanajuwa ni mali ya Chama chao basi wamehakikisha kila nakala inyohusu maeneo  wanafanyia kazi na kwamba taarifa zote zipo kwa viongozi husika.

Aidha akizungumzia ukakasi wa utoaji wa mikopo kutoka ngazi ya halmashauri lakini hali hiyo imeshaghulikiwa na hivi sasa mikopo hiyo inapitia ofisi za watendaji wa Mitaa ikilinganishwa na huko nyuma jinsi ilivyokuwa inatolewa huku kiongozi mmoja ngazi ya Kata akijanasibu kwamba mikopo hiyo nijitahada zake.

Akizunguzia mikakati yao kama viongozi amesema kubwa kuliko ni kuhakikisha wanashikamana ili kuweza kufanya vyema ambapo pia watendaji wanatakiwa kutimiza wajibu wao nakuona kwamba wapo kwa ajili watanzania.


Pia katibu huyo Amezungumzia kero ya maji taka ambayo yanatililika kutoka Ndani ya ujenzi wa kiwanja cha Ndege  (Airpot)unaondelea nakudai kwamba eneo hilo wameshapigia kelele sana ikiwa pamoja na kumshirikisha Mbunge lakini hadi sasa kero hiyo bado ipo.

Kwaupande wake Mwenezi wa Chama hicho kata, Haroun Muhajir. Amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu na kwamba watambue kuwa CCM ipo kazini nakudai wale watendaji wapiga dili na wala rushwa hawatafumbiwa macho.nakudai baadhi ya walimu walitaka kwenda kinyume na agizo la elimu bure kwa kuwatoza wanafunzi fedha sh. 500 Lakini jambo hilo wameshalimaliza.

"Tumejipanga vizuri kama Kata na kubwa nikuona kila jambo linakwenda kama linavyotakiwa japo kuna kero ya baadhi ya mitaa yetu miwili kukosekana kwa watendaji kwa maana mtaa wa kiwalani na kigilagila japo ambalo linafanya Wananchi kukosa huduma ya kiserikali kutoka kwa watendaji. ."  Amesema
Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani,Eva Malenga Amewatoa (kushoto) akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 


WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI

$
0
0


Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.
Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.
Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.


Na Joel Maduka ,Chato

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato.Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.

Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara zao.

Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.

“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi wa Shirika la White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi 16 kwenye jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni Sh Bilioni 78.56.

WABUNGE CCM WAMIMINIKA KUMUOMBEA KURA MTULIA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wameendelea kunadi sera za maendeleo na kumuombea kura mgombea wao wa ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam huku baadhi yao wakisema uchaguzi huo ni sawa na usajili wa dirisha dogo.

Hivyo wanatumia usajili huo kwa ajili ya kumpata Mtulia ambaye wanaamini ni mtu sahihi kwa maendeleo ya wananchi wa Kinondoni kwani alikokuwa awali hakuwa nafasi ya kushirikiana na Serikali ya Rais ,Dk.John Magufuli kufanya maendeleo.

Wakizungumza kwenye kampeni za uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Februari 17(Jumamosi ya wiki hii), viongozi wa CCM wakiwamo baadhi ya mawaziri ambao wamefika kwenye kampeni hizo kwa nafasi zao za ubunge,wamewaambia wananchi hao Mtulia ndio mtu sahihi kwao.

Mgeni rasmi kwenye kampeni zilizofanyika leo Kata ya Ndugumbi ambaye pia ni mbunge wa Mbinga Sixtus Mapunda amesema anatambua uwezo wa Mtulia na hivyo ni vema wananchi wakamchagua ili awatumikie kikamilifu.

Amewaeleza wananchi kuwa uchaguzi mkuu ulishafanyika mwaka 2015 na sasa ni uchaguzi mdogo ,hivyo Chama ambacho kimepewa dhamana ya kuongoza ni CCM na kwa maana hiyo Mtulia akiwa mbunge atashirikiana na viongozi wengine kuleta maendeleo ya wananchi.

Amefafanua anaufananisha uchaguzi huo na usajili wa dirisha dogo ambapo tayari CCM wanayo timu nzuri yenye ushindani wa hali ya juu na iliyokuwa na ari ya kuwatumikia wananchi,hivyo kwenye usajili huo wanamtaka Mtulia kuboresha timu yao.

 "CCM ni timu ambayo inawachezaji wazuri na waliotumia kwenye kila idara na kama mnavyojua kwenye usajili mdogo lazima msajili mchezaji ambaye atakuwa na uwezo na anaendana na kasi na timu ambayo tunayo.Hivyo Mtulia ni mtu sahihi kwetu.

"Kule alikokuwa mwanzoni hakuwa na uwezo wa kufanya maendeleo kwani kila akitaka kufanya wenzake wanamzuia kwa kigezo kuwa yakipatikana maendeleo ya Kinondoni upinzani hautakuwa na nafasi mwaka 2020.Hivyi akiwa CCM atafanya maendeleo kwa kasi kubwa na tutampa ushirikiano kadri ya uwezo wetu,"amesema Mapunda.



TANZANIA YASHINDA TUZO YA TEKNOLOJIA KATIKA MKUTANO WA DUNIA WA SERIKALI (WORLD GOVERNMENT SUMMIT 2018)

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshinda Tuzo za Kilele cha Serikali duniani (World Government Summit Awards) katika kundi la Tuzo ya Teknolojia bora inayoibuka Serikalini (Winner of the Best Government Emerging Technologies Award).

Tuzo hiyo ilitolewa na Mtukufu Shaikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais ya Umoja wa Falme za Kiarabu) (UAE) na kupokelewa na Balozi wa Tanzania, UAE, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk kwa niaba ya Serikali, wakati wa kilele cha Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Government Summit) uliohitimishwa jijini Dubai tarehe 13 Februari 2018.

Tuzo hiyo ilitokana na juhudi za Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kilimo ya Mikocheni (Mikocheni Agricultural Research Institute kufanikiwa kulipatia ufumbuzi tatizo la maradhi ya zao la muhogo “Cassava Brown Creek Disease,” na “Cassava Mosaic Disease,” kwa kutumia chombo cha kisasa kinachoitwa “Portable DNA Sequencer”.  Maradhi hayo yanasumbua sana zao la muhogo ambalo ni zao muhimu kwa Tanzania na nchi mbalimbali Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwa kutumia teknolojia hii mpya wataalamu wanaweza kugundua magonjwa mbalimbali ya zao la muhogo yanayosababishwa na wadudu, virusi, bacteria na fangasi (pathogens) kwa muda wa siku 2 tu kulinganisha na teknolojia ya zamani ambayo huchukua miezi kadhaa na ina gharama kubwa.

Zao la muhogo ni zao muhimu la chakula na biashara linalotegemewa sio tu na  Tanzania bali na nchi nyingine nyingi duniani.  Inakadiriwa kuwa watu wapatao millioni 800 duniani wanategemea zao la muhogo kwa chakula na biashara. Hivyo, teknolojia hii mpya itanufaisha nchi mbalimbali duniani katika kusaidia na kuendeleza zao hilo.

Nchi nyingine zilizopata Tuzo hiyo ni India na Australia.

Wakati huo huo, Watanzania wenye sifa wanahimizwa kuomba nafasi ya kazi iliyotangzwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya mazingira (UNEP). Nafasi inayotakiwa kujazwa ni ya Chief Biodiversity Unit. Maelezo kuhusu nafasi hiyo yanapatikana katika mawasiliano http://careers.un/bw/jobdetail.aspx?id=88749 na siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni tarehe 25 Februari 2018.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 15 Februari 2018.


BALOZI WA JAPAN AKABIDHI SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI KASENDA

$
0
0



Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa na mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi baada ya kukabidhi soko la samaki la kimataifa la Kasenda lililopo kata ya Mganza Wilayani Chato lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizindua kwa kuweka jiwa la msingi kwenye mradi wa soko la samaki la kimataifa la kasenda pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato ,Mhandisi Joel Hari.
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakati wa hafra fupi ya kukabidhi soko la kimataifa la Samaki.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida pamoja na mbunge wa jimbo la Chato Dk,Medard Kalemani.
Jiwe la msingi ambalo limewekwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida kwenye soko la samaki la kimataifa la Kasenda.
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi(CCM)
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi baada ya shughuli ya kukabidhi na kuweka jiwe la msingi kwenye soko la samaki la kimataifa.
Muonekano wa soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilaya ya Chato mkoa wa Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida wakiweka saini kwenye vitabu vya wageni.





Na,Joel Maduka,Chato.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaharu Yoshida kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita amezindua rasmi soko la kimataifa la uuzaji samaki la kasenda lililojengwa kata ya mganza wilayani chato mkoani hapa kwa hisani ya watu wa Japani.

Soko hilo lililopo kata ya Muganza lina jumla ya wafanyabiashara wa samaki zaidi ya 240 limegharimu jumla cha Shilingi milioni 320 za kitanzania hadi kukamilika kwake ukarabati uliohusisha pia ukarabati wa soko la zamani.

Akikabidhi soko hilo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Balozi wa Japan nchini Tanzania mhe. Masaharu Yoshida amesema kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhia samaki na dagaa kutasaidia kuokoa mazao mengi kutoka ziwani hususan samaki na dagaa.

“Soko la samaki la Kasenda halikuwa na miundombinu ya kuhifadhia samaki ambapo zaidi ya tani 200 za samaki zilitupwa kila mwaka kutokana na kuharibika ambapo serikali” alisema Mhe Masaharu.

Wakati huo huo serikali ya Japan imesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Chato ya ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa moja kutoka Muganza hadi Kasenda mahali lilipo soko hilo kwa thamani ya shilingi milioni 197.

Waziri wa Nishati mhe.Dkt. Medard Kalemani ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chato ameishukuru serikali ya Japan kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania. Alisema serikali ya Japan kwa muda sasa imekuwa ikishirikiana na Wilaya ya Chato na hii inatokana na uhusiano mzuri ulioanzishwa na mbunge wa Chato kwa wakati huo mhe. John Pombe Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel amewataka wananchi pamoja na uongozi wa soko kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ili kuhakikisha malengo ya uanzishwaji wa soko hilo yanatimia likiwemo suala zima la ukusanyaji wa mapato.

Mbali na kuhudumia soko la ndani ya nchi, soko hilo la kimataifa la Kasenda limekuwa likihudumia baadhi ya nchi za jirani kama vile Congo DCR, Rwanda, Burundi na Uganda.Ambapo linakadiriwa kukusanya Zaidi ya shilingi milioni 140 kwa mwaka.

WATUMISHI FANYENI KAZI KWA UHAKIKA NA MJIAMINI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Anthony Diallo wakiwa ndani ya pantoni ya Orion wakivuka ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenda Kamanga wilayani Sengerema kwa Ziara ya Kazi Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole kuelekea kwenye eneo inapojengwa hospitali ya Halmashauri ya Buchosa, Februari 15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma watumie utalaamu wao vizuri na wafanye kazi kwa uhakika na kwa kujiamini ili matokeo ya utendaji wao yaonekane.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Februari 15, 2018) mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza alipowasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku saba.

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa watumie utalaamu wao vizuri na wafanyekazi kwa kujiamini pamoja na kuwa na taarifa za kutosha za idara wanazoziongoza ili wananchi waweze kupata tija.

Pia amewataka watendaji kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika ipasavyo. “Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe na vitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”

Pia Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongela alimueleza Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanafanya kazi kwa bidii na fedha zote za miradi zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Hata hivyo Bw. Mongela alizungumza kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika mkoa huo kuwa ni ya kuridhisha na imefikia asilimia 80, pia wameboresha huduma ya mama na mtoto.

MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV. Clarias inayotoa huduma kati ya Mwanza na Ukerewe.????????????????????????????????????
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata tiketi ya kieletroniki mara baada ya kuzindua mfumo wa tiketi hizo katika Meli ya MV Clarias, mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamis, wakati akikagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias, mkoani Mwanza.
……………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha inafunga kamera katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi ili kudhibiti vitendo vya hujuma katika mifumo ya kampuni hiyo hususani kwenye Mapato. 
Ametoa rai hiyo jijini Mwanza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV Clarias na kusisitiza kuwa matumizi ya mfumo huo mpya yaende sambamba na elimu stahiki kwa watumishi wanaoutumia mfumo huo katika kukatisha tiketi. 
“Niwapongeze sana kwa hatua hii ya kuingia kwenye mfumo wa kielektroniki katika utoaji huduma lakini niwatake sasa kuongeza kamera kwenye maeneo yote unapofanyika ukaguzi ili kudhibiti mianya yote inayoweza kujitokeza ya kuhujumu mapato ya kampuni” amesema Prof. Mbarawa. 
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye shirika hilo ili liweze kupata faida na liweze kujitegemea na kuagiza kuwa kwa sasa kila fedha inayopatikana itumike vizuri sababu Shirika limeanza kupata faida. 
Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), kutengeneza mfumo kama huo kwa ajili ya Shirika la Reli Nchini (TRL), ili kudhibiti uvujaji wa mapato. 
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Kuwe, amesema mfumo huo umetengenezwa na Wakala ili kuiwezesha taasisi hiyo kuthibiti mapato kwani mfumo huo utarahisisha Huduma kwani abiria ataweza kukata tiketi akiwa sehemu yoyote nchini. 
Naye Kaimu Meneja Mkuu wa MSCL, Bw. Erick Hamis, amesema mfumo wa kielektroniki umeanza kwa meli moja ya MV Clarias inayofanya Safari zake kutoka Mwanza kuelekea kisiwa cha Ukerewe ambapo katika mpango wa baadae Kampuni inategemea kutumia mfumo huo kwenye meli zote za kampuni hiyo. 
“Toka tuanze kutumia mfumo kumekuwa na ongezeko la mapato kwa zaidi ya asilimia 20, pia na kwenye matumizi ya mafuta hii inatupa ishara kuwa mfumo huu utatusaidia kidhibiti mapato mengi yaliyokuwa yakipotea kwenye tiketi”amesema Hamissi. 
Ameongeza kuwa kampuni imejiwekea mpango wa miaka miwili wa kukarabati meli Tisa za kampuni hiyo ambapo mpaka sasa meli Tatu zimeshakarabatiwa na kuanza kazi wakati hatua ya kuanza ukarabati kwa meli zilizobaki uko kwenye hatua mbalimbali za manunuzi. 
Mfumo huo mpya wa kielektroniki wa ukatishaji tiketi katika kampuni hiyo umegharimu kiasi cha shilingi takriban milioni 50.

MSD YATUNUKIWA ITHIBATI YA JUU YA UBORA

$
0
0


Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).

Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uliofanywa na kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED mweziAgosti 2017, na kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozoya ya juu ya kimataifa katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na kuboresha masuala yote yanayo husiana na mnyororo wa ugavi ilikuwapa wananchi huduma bora, zenye viwango, bei nafuu na kuwafikishia kwa wakati.

Bwanakunu ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa ugaviwa MSD  kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wamwaka 2017 - 2020. 

Mara ya kwanza MSD ilipataIthibatiya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, tunzaji na Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza kuishikilia  ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa. 

MSD imekuwa  miongoni mwa taasisi za kwanza nchinikupataithibatiyauborayakiwango cha ISO 9001:2015 kutokakiwango cha ISO 9001:2008 na imethibitisha umahiri wa utendaji wake.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AKIKAGUA MIRADI YA UJENZI MKOANI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akikagua ujenzi wa nyumba ya makazi ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyopo eneo la Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi inayotekelezwa na Wizara yake jana Jumatano Februari 14, 2018. Nyuma yake ni Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Mkoa wa Tanga, Edward Ngowi.2.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua  miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi  inayosimamiwa na Wizara katika Mkoa wa Tanga hapo jana Jumatano Februari 15, 2018.3.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua  miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi  inayosimamiwa na Wizara katika Mkoa wa Tanga hapo jana Jumatano Februari 15, 2018.
4.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Luiza Mlelwa (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Wilaya kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  (mbele) wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018.
5.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Luiza Mlelwa akimakabidhi taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018.
6.Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (mbele) aliyefika katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018
7.
Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (shati nyeupe) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Muheza-Amani kwa kiwango cha lami wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara inayosimamiwa na Wizara yake.
8.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Kata ya Zirai iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara juzi Jumanne Februari 13, 2018.
9.Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Zirai iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakifuatilia kwa makini mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Viongozi na wananchi wa Kata hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara juzi Jumanne Februari 13, 2018.
11.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa mwenye (shati nyeupe) akisalimiana na Madiwani wa Kata ya Mombo iliyopo katika Halmashauri ya Korogwe  Vijijini wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Stephen Ngonyani (katikati) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara jana Jumatano Februari 14, 2018.
12.Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mombo ikiwemo stendi ya Mombo jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyan
13.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (katikati) akiongozwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa (kushoto) kukagua kipande cha barabara kilichopo katika stendi ya Mombo ikiwa ni sehemu yake ya kukagua miradi ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga jana Jumatano Februari 14, 2018.
14.Diwani wa Kata ya Mombo iliyopo Korogwe Mkoani Tanga, Halima Mussa akimpa maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kulia) kuhusu kuharibika kwa mtaro wa kupitisha maji machavu na uchakavu wa miundombinu ya barabara katika eneo la soko lililopo katika stendi ya Mombo Wilayani Korogwe jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images