Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1515 | 1516 | (Page 1517) | 1518 | 1519 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta mpakato na Printa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto). Vifaa vitakavyosaidia kutunza kumbukumbu za takwimu za majanga mbalimbali yanayotokea nchini, msaada huo umepokelewa Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo.
   Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe (kushoto) akimkabidhi Kompyuta mpakato (Laptop) Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya (kulia) (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

  Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi (ACF) Maria Kullaya wa nne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.ltd Bw. Rigobert Massawe wa tano kutoka (kulia), Meneja rasilimali watu wa Kampuni hiyo Bw. Danial Mbonea wa tatu kutoka (kulia) na Maafisa wa Jeshi hilo wakati wa makabidhiano ya msaada wa Komputa mpakato na Printa, mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo.

  Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Takwimu Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (ACF) Maria Kullaya amepokea msaada wa Kompyuta mpakato moja na Printa moja kutoka katika Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd, kwa ajili ya kuboresha kitengo cha Takwimu cha Jeshi hilo.

  Msaada huo wenye thamani ya sh.1.5 million ambao umetolewa na Kampuni ya Tanzania Tooku Garment Co.Ltd umepokelewa mapema leo Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliopo barabara ya Ohio Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati akipokea msaada huo Kamishna Msaidizi Maria alisema, msaada huu umetolewa wakati muafaka kwani utasaidia kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi katika ukusanyaji wa taarifa na utunzaji wa kumbukumbu tofauti na hapo awali.Tunatarajia kuvitumia vifaa hivi kwa lengo mahususi pamoja na kuvitunza vizuri “Vifaa hivi vitakuwa chachu kwa kitengo cha takwimu kwani tulikuwa na uhaba wa vitendea kazi” alisema Kamishna Msaidizi Maria.

  Naye Meneja wa Kampuni hiyo Bw. Rigobert Massawe, akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, alisema “lengo ni kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutimiza majukumu yake kwa ufanisi kwani kwa kufanya hivyo tunatimiza wajibu wetu wa kurudisha huduma kwa jamii”.

  Kamishna Msaidizi Maria anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada wa vitendea kazi hivyo, pia kupitia nafasi hii naomba wadau wengine waige mfano huu kwa kulisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Nyanja mbalimbali ili liweze kutimiza majukumu yake ya kuokoa Maisha na Mali za Watanzania.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

  Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .

  Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.

  Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija

  “Kama nilivyosema hapo awali mradi huu utajulikana kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW) na utaanza kutekelezwa katika maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous “

  Makamu wa Rais ameiagiza Baraza la Mazingira lililokuwa chini ya Ofisi yake kuharakisha tathmini ya mazingira ya bonde la mto ruaha mkuu ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi bila athari zozote baadaye za mazingira.

  Makamu wa Rais alielekeza taasisi zote zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za mikoa, Halmashauri za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.“Tuhakikishe sheria zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya maji na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako yakutunze”.

  Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia kwa kukubali kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .Aidha kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya Utalii ni moja ya sekta za kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo takribani asilia 20 ya pato la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za kigeni zinatokana na Utalii.

  0 0

  Na Jumbe Ismailly -HANANG        
  PAMOJA na serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini wazazi na walezi wa wanafunzi katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang bado wamekuwa kikwazo cha watoto wao kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Brycosen Kibassa aliyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na kituo hiki alipokuwa akizungumzia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya hiyo kutokana na wazazi au walezi kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani yao ya kumaliza masomo yao.
  Aidha Mkurugenzi huyo aliweka bayana kwamba mwaka 2017 Halmashauri hiyo iliweka mpango na wakakubaliana kwamba kiwango cha ufaulu kwa wastani uwe asilimia 80 kwa wilaya na licha ya kufanya majaribio mengi kabla ya kufikia mtihani wa taifa,ambapo katika mtihani wa majaribio walipata wastani wa asilimia 75.
  Kwa mujibu wa Kibassa baada ya kufanya mtihani huo wa kitaifa wamepata asilimia sita hali ambayo ni dhahiri kwamba iliwashitua sana na kuanza kuangalia kilichosababisha hali hiyo na katika taarifa za awali walizonano inaonekana wazazi wenye mwamko mdogo wa elimu katika eneo hilo waliwatuma kwa makusudi kabisa watoto wao kwamba wahakikishe hawafanyi vizuri katika mitihani yao.
  Akizungumzia mikakati waliyojipanga kukabiliana na hali hiyo,Kibassa pamoja na kukiri kwamba kuna baadhi ya maeneo ya usimamizi kwa upande wa ngazi ya wilaya hawakuwa wamejipanga vizuri sana na kutolea mfano kitengo cha udhibiti ubora wa elimu ambacho kinahusika na ukaguzi wa elimu kuwa kwa mwaka huu watafanya kazi kama timu kuanzia idara ya elimu,wadau wa elimu sambamba na kuwatumia maafisa elimu kata kuhakikisha wanasimamia kwa karibu kwenye maeneo yao.
  Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wakizungumzia changamoto hiyo,Mary Gwau aliwashauri wazazi kuona umuhimu wa elimu kwani ni maisha kwa watoto wao na kwamba mtu anapokuwa na elimu huweza kujisaidia katika maisha yake na anaweza kuwa mtu wa maana katika siku za baadaye na ataweza kuwasaidia wazazi wake.
  “Hivyo kama wazazi tuchukue jukumu la kuwasogelea watoto wetu na kupata elimu kwamba tuwasaidie hawa watoto wasome wapate elimu ili nao wajiwezeshe  tusijiunge na yale makundi ya watu ambao wamekata tamaa,kusomesha watoto hawataki kuwatia moyo hawataki kabisa”alisisitiza Mzazi huyo.
  Naye Mzazi Eliasi Kaila aliwatahadharisha wazazi na walezi wa wanafunzi kutokuwa chanzo cha kukwamisha elimu kwa watoto wao na badala yake wawe chachu ya watoto kupata elimu na kushauri kwamba wajenge utamaduni wa kuwafundisha nyumbani badala ya kuwategemea walimu peke yao.
  “Mzazi asiwe chanzo cha kumkwamisha mtoto kupata elimu kwa sababu hivi sasa elimu ni bila malipo na rais mwenyewe amesema na mwananchi asichangishwe mchango wa aina yeyote kuhusu mtoto wa shule”.alifafanua Kaila.
   Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara wakiwa wamesimama kwa muda wa takribani dakika tano kuashiria kumkumbuka mmoja wa madiwani hao aliyepoteza maisha katika siku za hivi karibuni.
   Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nangwa waliohudhuria mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo wasikiliza kinachojadiliwa na wawakilishi wao waliowachagua.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
    Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,CharlES Yona akisisitiza juu ya umuhimu wa kudumisha ushirikiano katika utendaji wa shughuli zote za Halmashauri ya Hanang,lengo likiwa ni kuisogeza mbele kimaendeleo Halmashauri hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Bryceson Kibassa (wa kwanza kulia) akimpongeza diwani wa kata ya Nangwa,Portagia Baynet muda mfupi baada ya kuapisha na kula kiapo cha uadilifu.

  0 0


  0 0
 • 02/12/18--04:28: Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus ambapo wateja wa Tigo wanapata bonasi ya hadi GB 1 ya data pamoja na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G aina ya TECNO R6 kila saa wanaponunua bando za intaneti kupitia namba *147*00# . Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf pamoja na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia). Bonasi Kemkem Kwa Wateja Wa Tigo Watakaonunua Bando Kupitia *147*00# Pata hadi GB 1 bure na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G kila saa! Dar es Salaam, Februari 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wake wote watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia watapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zaidi ya elfu moja ambazo zinatolewa na Tigo katika promosheni hiyo kabambe ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’. Akitangaza ofa hizo jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema kuwa ofa hizo murwa ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaolenga kukutana na mahitaji ya wateja na kuwezesha kila mtu afurahie huduma za kidigitali katika mtandao ulioboreshwa wa Tigo. “Kupitia mtandao wetu mathubuti wa 4G wateja wetu tayari wanafurahia huduma bora zaidi za intaneti. Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inatoa fursa kubwa kwa wateja wengi zaidi kumiliki simu janja zenye uwezo wa 4G na kupokea bonasi kubwa za data zitakazowawezesha kuwa sehemu ya mageuzi makubwa ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ alisema. Tigo ndio mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake ambapo katika soko la simu za mkononi nchini, ni wateja wa Tigo pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila kifurushi wanachonunua. Tigo pia imejizolea umaarufu mkubwa kwa promosheni zake bunifu. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kupitia promosheni mpya ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inalenga kuongeza matumizi ya data pamoja na kuongeza matumizi ya simu janja za kisasa (Smartphone) nchini, hivyo kuisogeza Tanzania hatua moja mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali. ‘Tunafahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma za mtandao na ndio maana Tigo inazidi kuwekeza katika kupanua na kuboresha huduma zake za mtandao. Kupitia promosheni hii tunalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini,’ alisema. “Tunawakaribisha wateja wetu wote kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00# ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Tarik alisisitiza.
 • Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus ambapo wateja wa Tigo wanapata bonasi ya hadi GB 1 ya data pamoja na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G aina ya TECNO R6 kila saa wanaponunua bando za intaneti kupitia namba *147*00# . Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf pamoja na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia).

  Bonasi Kemkem Kwa Wateja Wa Tigo Watakaonunua Bando Kupitia *147*00# Pata hadi GB 1 bure na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G kila saa!

  Dar es Salaam, Februari 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wake wote watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. 

  Pamoja na haya, wateja hao pia watapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zaidi ya elfu moja ambazo zinatolewa na Tigo katika promosheni hiyo kabambe ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’. 

  Akitangaza ofa hizo jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema kuwa ofa hizo murwa ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaolenga kukutana na mahitaji ya wateja na kuwezesha kila mtu afurahie huduma za kidigitali katika mtandao ulioboreshwa wa Tigo. 

  “Kupitia mtandao wetu mathubuti wa 4G wateja wetu tayari wanafurahia huduma bora zaidi za intaneti. Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inatoa fursa kubwa kwa wateja wengi zaidi kumiliki simu janja zenye uwezo wa 4G na kupokea bonasi kubwa za data zitakazowawezesha kuwa sehemu ya mageuzi makubwa ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ alisema. 

  Tigo ndio mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake ambapo katika soko la simu za mkononi nchini, ni wateja wa Tigo pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila kifurushi wanachonunua. Tigo pia imejizolea umaarufu mkubwa kwa promosheni zake bunifu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kupitia promosheni mpya ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inalenga kuongeza matumizi ya data pamoja na kuongeza matumizi ya simu janja za kisasa (Smartphone) nchini, hivyo kuisogeza Tanzania hatua moja mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali. 

  ‘Tunafahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma za mtandao na ndio maana Tigo inazidi kuwekeza katika kupanua na kuboresha huduma zake za mtandao. Kupitia promosheni hii tunalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini,’ alisema.

  “Tunawakaribisha wateja wetu wote kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00# ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Tarik alisisitiza.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  SERIKALI mkoani Pwani,imewaasa wafanyabiashara, wawekezaji na wenye viwanda ,kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoani humo, ifikapo machi 30 mwaka huu.

  Hatua hiyo itasaidia mkoa huo kunufaika na wafanyabiashara hao ambao wengi wao kwasasa wanalipa kodi katika maeneo ya mikoa waliojisajili .Mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alitoa agizo hilo ,mjini Kibaha wakati wa mkutano wa baraza la biashara la mkoa .

  Alisema kutokana na wafanyabiashara wengi mkoani hapo kulipia kodi nje ya Mkoa kunasababisha kudidimiza uchumi wa mkoa."Kila mmoja abebe mzigo wake,mchango wetu kama mkoa hauonekani,na hatunufaiki ,unakuta tuna miviwanda mingi lakini wamekata TIN no.Kinondoni, Ilala ,jijini Dar es salaam ,mapato yake yote yanahesabika huko"

  "Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa mkoa wa Pwani unachangia asilimia 1.6 ya pato la taifa ambalo liko chini, kumbe wafanyabiashara na makampuni hawatulipi kodi kwenye mkoa jambo ambalo sio sawa," alisema Ndikilo.

  Ndikilo alisema makampuni na wafanyabiashara hao, wamekuwa hawalipi malipo mbalimbali kwa kudai wanalipia Dar es Salaam.Aidha Ndikilo ,aliwaasa wawekezaji kuwa na lebo kwenye bidhaa zao zinazoonyesha zinazalishwa Mkoani Pwani ili kuutangaza mkoa .Pamoja na hayo ,alizitaka taasisi wezeshi kushirikiana na jumuiya ya wafanyabiashara (TCCIA), ili kuona kama kuna urasimu katika idara mbalimbali ikiwemo maji ,umeme na kuangalia namna ya kuondoa ama kupunguza urasimu uliopo.

  Ndikilo alisema ,kila mmoja apambane na rushwa pasipo kuiachia TAKUKURU pekee ,kwani kwa kuiachia TAKUKURU peke yake kamwe rushwa haitoisha.Aliwasisitizia wakuu wa wilaya na wakurugenzi kwenda kuundwa mabaraza ya uwekezaji ndani ya wilaya zao.

  Nae mkuu wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo alieleza kuna baadhi ya makampuni hasa yale yanayomiliki mahoteli yamekuwa hayalipi kodi kwa madai wanalipa Dar es Salaam.Njwayo alisema hakuna budi kuwasiliana na kamishna wa TRA ili kubadilisha utaratibu wa usajili kwa wahusika walipie kwenye maeneo ya biashara zao.

  Awali meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Pwani, Euvensia Lwiwa alieleza wanakabiliwa na changamoto hiyo ambayo inasababisha kukosa mapato.Lwiwa alisema alifanikisha makampuni matano kati ya 36 kulipa kodi na tozo mbalimbali lakini bado wanaendelea na mikakati kuhakikisha wanalipa ndani ya mkoa.
   Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mkutano wa baraza la biashara la Mkoa  wa Pwani
   Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amekizungumza wakati wa mkutano wa baraza la biashara la mkoa ,mjini Kibaha. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

  Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka ,akionekana pichani akizungumzia masuala mbalimbali ya kibiashara katika mkutano wa baraza la biashara la Mkoa huo.(picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya mazungumzo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Waziri Kindamba aliyefika Ikulu pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Waziri Kindamba Ikulu jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari kuhusiana na Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Waziri Kindamba

  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu akizungumza kuhusu Shirika hilo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano la Tanzania TTCL-Corporation Omary Nundu (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Waziri Kindamba Ikulu jijini Dar es Salaam.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Reli (TRL), Mhandisi Nelson Ntejo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) kuhusu maendeleo ya kazi ya ukarabati wa eneo lililoathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka, katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipokagua reli hiyo Mkoani humo, hivi karibuni.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu kutoka Shirika la Reli (TRL), Mhandisi Nelson Ntejo, alipokagua ukarabati wa njia ya reli ya kati ya eneo la Kilosa mkoani Morogoro iliyoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kazi zinazoendelea katika eneo la Kilosa, ambapo ukarabati umekamilika na treni za mizigo zimeanza kupita.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akishiriki katika kazi za kujaza mchanga kwenye viroba vinavyotumika kama kingo za kudhibiti maji ya mto Mkondoa yasifike kwenye miundombinu ya reli katika eneo la kilosa, mkoani Morogoro.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe, akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), na wakazi wa Kilosa, wakati alipokagua ukarabati wa njia ya reli ya kati eneo la Kilosa karibu na mto Mkondoa, mkoani humo.
  Muonekano wa sehemu ya njia ya reli ya kati eneo la Kilosa iliyokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha, mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwaka huu.
  Muonekano wa treni ya mizigo ikianza safari zake katika stesheni ya Kilosa, mkoani Morogoro kuelekea mkoani Mwanza mara baada ya njia hiyo kukarabatiwa.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adamu Mgoyi, alipokutana nao katika ukaguzi wa ukarabati wa njia ya reli ya kati kutoka eneo la Kilosa.

  …………………………………………………………………………………

  Shirika la Reli Tanzania (TRL) limepata hasara ya takribani shilingi bilioni tano katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya njia ya reli ya kati kusombwa na mafuriko katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ya reli hiyo na kusema kuwa Serikali imejipanga kupata suluhisho la kudumu la uharibifu katika maeneo hayo ambapo mara kadhaa yamekuwa yakiathiriwa na mvua kutokana na mabwawa yaliyopo kujaa mchanga na hivyo kusababisha uharibifu huo.

  “Serikali kwa sasa inayafanyia kazi mapendekezo matatu yaliyowasilishwa na RAHCO ikiwemo kuihamisha reli kwenye milima jirani, kuihamishia eneo ambapo inajengwa reli ya kisasa ya SGR ama kujenga tuta kubwa, huku tukizingatia gharama halisi za kazi hiyo kabla ya kufanya maamuzi”, amesema Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa mbali na Serikali kuja na suluhu ya muda mfupi ya kurejesha safari za treni pia amewatoa hofu wafanya biashara kwa kuwahakikishia kuwa mizigo yao iko salama na itasafirishwa kwa wakati.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Mkoa umejipanga kuhakikisha unatoa elimu kwa wananchi kwenye utunzaji wa mazingira ili kunusuru uharibifu unaotokea kutokana na shughuli za kibinadamu.

  “Kama Mkoa tumejipanga kuwa kuanzia sasa Sheria zilizopo zinazokataza kulima kandokando ya mito na kando ya reli sasa zitafuatwa na tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili miudombinu hiyo isiathirike kwa sababu ya shughuli za kibinadamu zinazofanywa kupitia kilimo”, amesisitiza Dkt. Steven Kebwe.

  Ameongeza kuwa kuanzia mwakani mkoa umejipanga kutenga fedha kwa ajili ya kutumia njia za asili kulinda miundombinu hiyo kwa kupanda miti na kuotesha matete ili kulinda miundombinu.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Massanja Kadogosa, amesema kazi ya ukarabati imekamilika kwa sehemu kubwa kwani tayari treni tano za mizigo zimepita salama na kuongeza kuwa kazi zinazomaliziwa kwa sasa ni kujaza mchanga kwenye matuta ya reli hiyo na kumalizia kingo ili kuilinda reli.

  0 0

  WaziriAfya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika unaofanyika Jijini DaeEs Salaam na kuhudhuliwa na n chi zipatazo 17 za Afrika.
  Dkt. Ndugulile akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuifungua mkutano huo.

  Pichani Naibu Waziri Dkt.Ndugulile akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bi.Agnes Kijo kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa siku tano na kujadili mfumo wa pamoja wa kudhibiti ubora wa dawa barani Afrika.
  Dkt.Ndugulile akifuatilia mada (mwasilishaji hayupo pichani) katika mkutano huo
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.Agnes Kijo akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa Mamlaka za Kudhibiti Chakula na Dawa Barani Afrika
  Msimamizi wa kitengo cha Afya katika Shirika la Maendeleo ya Afrika (NEPAD) yenye makao makuu yake nchini Afrika ya Kusini Bi.Margareth Ndomondo akiongea wakati wa uzinduzi huo.Shirika hilo katika afya linasaidia kupunguza magonjwa yanayoikabili nchiza Afrika.
   
   


  TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA

  Na.WAMJW-DAR ES SALAAM

  TANZANIA ni miongoni mwa nchi inayotumia dawa zilizo salama na ubora wa hali ya juu barani Afrika kutokana na udhibiti na umakini unaofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA.

  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mamlaka wa Udhibiti na ubora wa dawa barani afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam.

  ”Sisi kama Tanzania tunafanya vizuri sana katika udhibiti wa madawa yanayoingia,nataka niwathibitishie kwamba Tanzania dawa zetu tunazozitumia ni salama na zipo salama kwa uhakika mkubwa” alisema Dkt. Ndugulile  Aidha ,Dkt. Ndugulile alisema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa ambayo hayana kiwango na kutumika katika mfumo wa tiba umeleta changamoto katika kuongeza gharama za matibabu nchini na barani Afrika

  Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema changamoto hizo zinasababisha wagonjwa wengi kukaa hospitalini,kuongeza gharama, kuathiri matokeo ya mgonjwa na hatimaye vifo pamoja na kuleta usugu wa dawa kwa kutumia dawa zisizo na kiwango

  Hata hivyo Dkt. Ndugulile alisema mkutano huo utajenga utaratibu na mfumo wa pamoja wa kuona ni jinsi gani wanaweza kudhibiti matumizi ya madawa yasiyo na kiwango barani afrika.

  “Nataka niwathibitishie Watanzania kwamba tuna dawa za kutosha na dawa zote zinazoingia zina ubora unaotakiwa,Taasisi yetu ya TFDA inatambulika Kimataifa, ina viwango vya Kimataifa na tumeboresha maabara zetu kuwa za kisasa na kutumika katika bara la afrika katika udhibiti wa madawa”. Alisema Dkt. Ndugulile.

  Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi.Agnes Kijo alisema mamalaka hiyo imejidhatiti katika masuala ya udhibiti wa dawa hivyo kupelekea mkutano huo kufanyika Tanzania

  “Maabara yetu hivi sasa imewekewa vifaa vya kisasa ambapo mwaka huu wa fedha ilitengewa shilingi bilioni tano nukta moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya maabara ya Dar es Salaam na kanda ya ziwa ambapo itasaidia kufanyiwa uchunguzi wa dawa katika ukanda uliopo na hivyo kutoa majibu kwa wakati na mamlaka kufanya maamuzi sahihi” alisema Bi. Kijo.

  Mkutano huo ambao una lengo la kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali yanayo uhusiana na udhibiti na ubora wa dawa ambapo kumekuwa na changamoto za matatizo ya madawa yasiyo na kiwango umekutanisha nchi zipatazo 17 na utafanyika kwa siku tano.

  0 0

   Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (wapili kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Willium (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam
  Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi Februari. 

  Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia ujio wa viongozi wa FIFA na CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili nchini na kufanya mkutana wao tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari mwaka huu. 

  Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote. 

  “Ugeni unaokuja kwa kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe 

  Naye Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema kuwa hii ni fursa ya aina yake kwetu sisi kwani itatupa nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuona ni namna gani michezo inaweza ikasaidia katika kukuza na kuongeza uchumi kupitia utalii. 

  “Tunaamini kuwa wageni hao watakua mabalozi wazuri kwa kutuletea watalii kupitia michezo na kuitangaza nchi katika mataifa mbalimbali” amesema Mhe. Juma 

  Ujio wa viongozi wa FIFA na CAF ni bahati kubwa kwa nchi yetu na unatokana na matokeo chanya ya utendaji kazi mzuri unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Serikali lakini pia upigaji vita wa masuala ya rushwa na upangaji wa matokeo wakati wa mechi. 

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi Februari. 

  Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia ujio wa viongozi wa FIFA na CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili nchini na kufanya mkutana wao tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari mwaka huu. 

  Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote. 

  “Ugeni unaokuja kwa kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe 

  Naye Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema kuwa hii ni fursa ya aina yake kwetu sisi kwani itatupa nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuona ni namna gani michezo inaweza ikasaidia katika kukuza na kuongeza uchumi kupitia utalii. 

  “Tunaamini kuwa wageni hao watakua mabalozi wazuri kwa kutuletea watalii kupitia michezo na kuitangaza nchi katika mataifa mbalimbali” amesema Mhe. Juma 

  Ujio wa viongozi wa FIFA na CAF ni bahati kubwa kwa nchi yetu na unatokana na matokeo chanya ya utendaji kazi mzuri unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Serikali lakini pia upigaji vita wa masuala ya rushwa na upangaji wa matokeo wakati wa mechi. 

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei (Kulia). na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) . Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.Nchini Tanzania.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam


  WAZIRI MKUU. Kassim Majaliwa. amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Viongozi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao kwa pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.

  Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno mengi.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi kwa sababau mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya Serikali kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

  Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa maelekezo ya uhamasishaji wa kilimo hasa mazao makuu ya biashara, tayari tija imeanza kuonekana ambapo zao la korosho limepata mafanikio makubwa na sasa linafuatia zao la pamba.

  Waziri Mkuu amesema Serikali inashiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba kwa wakulima kuelekezwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko, hivyo amewaalika viongozi hao kushiriki katika mkutano utakaowakutanisha wafanyabiashara wote wa zao hilo.

  “Mimi mwenyewe mwezi huu nitakuwa na ziara ya kikazi mkoani Mwanza, kwa hiyo tarehe 21, Februari, nimeitisha mkutano wa wafanyabiashara wote wa pamba nchini iwe ni wanaosokota nyuzi, kuchambua pamba au kukamua mbegu za pamba, ili mradi wanajihusisha na pamba nanyi naomba muwepo”.

  Waziri Mkuu amesema Serikali imefurahishwa na uamuzi wao wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu kwani ni faraja kwa Taifa kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika.Kwa upande wao, Bw. Pardesi na Bw. Qin wamemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni zao zinauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nyuzi na nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, FEBRUARI 12, 2018.

  0 0

   Dkt Omari Rashid Nundu

  0 0

  Na Said Mwishehe, Glogu ya jamii

  WABUNGE kutoka majimbo mbalimbali nchini kupitia Chama ChaMapinduzi (CCM), wamewaomba wananchi wa jimbo la Kinondoni jijiniDar es Salaam kuhakikisha Februari 17, mwaka huu wanamchaguamgombea ubunge wa chama hicho, Abdallah Mtulia katika uchaguzi
  mdogo jimboni humo.

  Wamesema Mtulia ndio chaguo sahihi kwa wananchi wa Kinondoni nakwamba akiwa mbunge watashirikiana naye katika kufanikishachangamoto za wananchi zinapata ufumbuzi wake.Pia wameeleza namna ambavyo wabunge wa CCM  wamekuwa wamojabungeni katika kupigania maendeleo ya wananchi tofauti na wabungewa upinzani ambao kila kitu wao ni kupinga hata liwe jambo lamaendeleo.

  Wakizungumza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika wanja wa People Kigogo wilayani Kinondoni jijini, wabunge hao waCCM wamewaomba wananchi kutofanya makosa kwenye uchaguzi huohuku wakitoa sababu mbalimbali za kwanini Mtulia anastahili kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Mgeni rasmi  kwenye kampeni hizo ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amewaomba wananchikumchagua Mtulia kwani ndio mgombea sahihi na wanaamini akiwambunge watashirikiana naye kutatua kero za wananchi.
   
  "Nimekuja kuzungumza na ninyi kuwaomba tarehe 17,siku yaJumamosi wote mkamchague Mtulia, lakini si tu kumchagua lazimatuseme kwanini mumchague Mtulia.Ndio mgombea mwenye sifa zoteza kuwa mbunge wa Kinondoni,"amesema Bashe.

  Pia amesema kwenye kampeni hizo wapo wanaotoa hoja kuwa Serikali ya CCM haitaki mfumo wa vyama vingi, ambapo amefafanua hoja hiyo haina maana yoyote kwani mwaka 1992 licha ya watanzania wengi kutaka mfumo wa chama kimoja uendelee lakini uamuzi ulitolewa wa kuingia mfumo vyama vingi.

  "Mwaka 1992, watanzania walipata fursa ya kuchagua tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi au laa.Waliotaka vyama vingi walikuwa asilimia 20 na waliosema chama kimoja kiendelee walikuwa asilimia 80."Mwaka 1995 tukafanya uchaguzi wa vyama vingi na CCM ikashinda, hivyo CCM hatuna hofu na mfumo wa vyama vingi na ndio maana tumeendelea kushinda katika kila chaguzi.

  "Pia wapo wanaotoa hoja CCM hakuna demokrasia hili nalo halina ukweli.CCM demokrasia ipo tena ya kutosha.Ndani ya CCM tunaweza kutofautiana kimtazamo, tunaweza kutofautiana kwa hoja na wakati mwingine tukashikana mashati lakini ukweli utabaki tunafanya hayo yote kwasababu ya demokrasia tuliyonayo,"amesema Bashe.

  Kuhusu hoja uchaguzi ni gharama, Bashe amesema wanaona ni gharama wanayo fursa ya kupeleka muswada wa sheria bungeni ili kubadilisha sheria ambayo itaelekeza hakuna uchaguzi mdogo hata mbunge anapoamua kuondoka chama kimoja na kujiunga na chama kingine.Pia njia nyingine ni kubadilishwa kwa sheria ili kurudi kwenye mfumowa chama kimoja ambao hautakuwa na gharama.
   
  "Kuna hoja nyingine hazina maana mbunge akitoka upinzani kwendaCCM wanasema kanunuliwa ila akitoka CCM kwenda upinzani huyohajanunuliwa.Hii hoja haina mantiki yoyote.

  Bashe amesema Mtulia ameamua kujiunga CCM ili aweze kuleta maendeleo ya wananchi kwani alikokuwa hakuko salama."Mtulia mwaka 2015 alikuwa kwenye gari ya Ukawa na sasaameamua kuwa kwenye gari la CCM.Tatizo liko wapi hasa kwakuzingatia kule alikokuwa hakuko salama.CUF imegawanyika vipande viwili kwani Katibu Mkuu wao, Maalim Seif Sharif Hamad anafanya 

  kazi kivyake na Mwenyekiti Lipumba naye yupo kivyake."Mtulia alikuwa anapata posho bungeni, analipwa mshahara lakini ameamua kujiuzulu kutokana na hali iliyopo kwenye chama chake kwani hakuwa anapata muda wa kutosha kushughulikia changamoto za jimbo lake.Akaona ni bora ajiuzulu kule na kisha aje huku,"amesema Bashe.

  Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, Salma Kikwete amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua Mtulia ili washirikiane naye kutatua changamoto za wananchi wa Tanzania wakiwamo wa Kinondoni.Amesema Rais ,Dk. John Magufuli anafanya kazi nzuri ya kuleta maendeleo ya wananchi ,hivyo ni vema Kinondoni wakamchagua 

  Mtulia ili awe sehemu ya kiunganishi kati ya Rais na wananchi."Kazi iliyopo mbele yenu ni kumchagua Mtulia ili awe mbunge wa Kinondoni. Wabunge na viongozi wa ngazi mbalimbali ndio maana wapo hapa kumuombea kura Mtulia awe mbunge kwani wanaamini atashirikiana nanyi katika kupigania mamboyanayowahusu,"amesisitiza Mama Salma. 

  Kwa upande wake Mbunge Geita Vijijini, Joseph Kasheku mbali ya kumuombea kura Mtulia ametumia nafasi hiyo kuwaeleza baadhi ya viongozi wa Chadema kuwa hawana tofauti na watu matapeli.Amemtolea mfano Frederick Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 lakini hakuna hata siku moja ambayo amekwenda kuhutubia wananchi wa Kigogo lakini baada ya kuona kuna uchaguzi wa ubunge ndio anakwenda.

  "Sumaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 lakini hajawahi kufika kuhutubia wananchi na leo maisha yamempiga ndio anakuja kwenu.Wananchi msihangaike ikifika siku ya uchaguzi Februari 17 
  nendeni mkamchague Mtulia aje bungeni."Tena akifika bungeni nitamwambia akamuombe Spika wa Bungetuwe tunakaa karibu ili niwe namuelekeza ... mimi ni darasa la saba lakini mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi hayana nafasi,"amesema.

  Pia amesema upinzani wanazungunzia namna ambavyo viongozi wa CCM wanapiga magoti wakati wa kumuombea kura Mtulia na kueleza hiyo ni ishara ya heshima na ndio sifa ya wanaCCM ya kuheshimu wananchi.Wakati huo huo, Mbunge wa Mtela, Livingston Lusinde naye ameendelea kumuombea kura Mtulia huku akitumia nafasi hiyokuwapiga  vijembe wapinzani kutokana na hoja mbalimbali wanazozitoa kwenye kampeni hizo.

  CCM kwenye kampeni hizo wamekuwa wakitumia wabunge wake mbalimbali pamoja na viongozi ambao wamekuwa wakimuombea kura  Mtulia na kwa kampeni za leo zilizofanyika Kigogo wabunge zaidi ya10 wamemuombea kura mgombea wao.

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la Aslay akimhoji mmoja wa wapendanao Mwanaidi Msangi ambaye alikuwa ni mmoja kati ya Washindi na Mpenzi wake Kelvini Gibson pichani kulia.Wakazi hao wa Buguruni malapa walijinyakuliwa milioni kumi na kugawana kila mmoja milioni tano,kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy
  Kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy akimhoji mmoja wa wapenda nao Kelvini Gibson,wakazi wa Buguruni malapa waliojinyakuliwa milioni tano tano kwa kila mmoja mwishoni mwa wiki,katika kushiriki kampeni ya Wapendanao ilionzishwa na mchezo huo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka,uliobeba kauli mbiu iliyojulikana kwa jina la 'Ukishinda na umpendae anashinda' ,kushoto ni  Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina Aslay
  Pichani kati ni Wawili wapenda nao Mwanaidi Msangi pamoja na Kelvin Gibson wakiwa sambamba katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika mfano wa hundi ya shilingi milioni Kumi waliojishindia kwenye muendelezo wa kampeni ya Wapendanao ilioanzishwa na Tatu Mzuka, Kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Nandy pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la Aslay,ambao kwa pamoja wanatarajiwa kutumbuiza jumamosi hii katika ufukwe wa kiota cha maraha cha Escape One,Mikocheni jijini Dar.


  0 0

  Mchezaji wa Lugalo Golf Club Angel Eaton akishangilia mara baada ya kucheza mpira mzuri katika shimo namba Tisa katika mashindano ya wazi ya wanawake ya IBB ladies Championship yaliyomalizika Jumapili nchini Nigeria
  Mchezaji wa Lugalo Golf Club Angel Eaton akishangilia akiwa na wechaji wenzie mara baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya wazi ya wanawake ya IBB ladies Championship yaliyomalizika Jumapili nchini Nigeria
  Mchezaji wa Lugalo Golf Club Angel Eaton akinyenyua kikombe mara baada ya kushinda katika mashindano ya wazi ya wanawake ya IBB ladies Championship yaliyomalizika Jumapili nchini Nigeria
  Mchezaji wa Lugalo Golf Club Angel Eaton akishangilia kwa kujifunika bendera ya taifa mara baada ya kucheza mpira mzuri katika shimo namba Tisa katika mashindano ya wazi ya wanawake ya IBB ladies Championship yaliyomalizika Jumapili nchini Nigeria.Picha na Luteni Selemani Semunyu

  Angel Eaton Mchezaji Watimu Ya Golf Ya Wanawake Ya Klabu Ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Ya Lugalo Ametekeleza Agizo La Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Jenerali Mabeyo La Kulinda Heshima Ya Jeshi Katika Mashindano Nchini Nigeria

  Mchezaji Huyo Nyota Wa Klabu Ya Lugalo Amefanikisha Hilo Baada Ya Kuibuka Na Ushindi Wa Jumla Baada Ya Kushinda Siku Tatu Mfululizo Kwa Mikwaju 76 Katika Siku Ya Kwanza Ya Pili Na Tatu Ya Mashindano Ya Wazi Ya Wanawake Ya Ibb Ladies Open Championship Yaliyofanyika Abuja Nchini Nigeria.

  Tanzania Iliyowakilishwa Na Wachezaji Saba Kutoka Klabu Ya Lugalo Imefani9kiwa Kushika Nafasi Ya Nne Iliyonyakuliwa Na Mchezaji Wake Hawa Wanyeche Akiwa Nyuma Ya Wachezaji Kutoka Kenya Na Nigeria Huku Nafasi Ya Sita Ikinyakuliwa Na Nahodha Ayne Magombe

  Hivi Karibuni Wakati Akiwaaga Wachezaji Hao Kwenda Nchini Nigeria Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Jenerali Mabeyo Aliwataka Kuhakikisha Wanalinda Heshima Ya Klabu Jeshi Na Nchi Kwa Ujumla Katika Mashindano Hayo

  Mashindano Hayo Ya Siku Tatu Yaliyoshirisha Wacheza Ji 187 Kutoka Nchi 10 Zilizoshiriki Michuano Hiyo Ambapo Nahodha Wa Timu Hiyo Ayne Magombe Alisema Walikuwa Na Timu Nzuri Iliyokuwa Na Wachezaji Wazuri.

  Timu Ya Lugalo Iliwakilishwa Na Wachezji Ayne Magomba,Sophia Mathias, Hawa Wanyeche,Christina William, Rehema Athumani Na Angel Eaton Ambaye Pia Alishinda Longest Drive.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa Maafisa Utumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa Maafisa Utumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za  Mitaakilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
   Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathias Kabunduguru akizungumza wakati wa ufunguzi Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ,Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
      
      ....................................................................................
  Maafisa Utumishi Waaswa Kuzingatia Weledi Katika Kutekeleza Majukumu Yao. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewataka Maafisa Utumishi wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza ari ya watumishi wa umma katika kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi.

  Akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi cha Siku mbili kilichowahusisha
  Wakurugenzi wa Rasilimali watu wa Wizara zote, Idara zinazojitegemea na Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote hapa nchini mapema leo mjini Dodoma Waziri Jafo amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuona changamoto za Watumishi wa Umma zinatatuliwa kwa wakati.

  “Maafisa Utumishi mnalo jukumu kubwa lakuwasaidia watumishi katika maeneo yao kwa kufanya kazi zenu kwa kuzingatia weledi, kuepuka rushwa, vitendo vya upendeleo na mambo yote yanayoweza kuchafua taswira ya Serikali kupitia huduma mnazotoa” Alisisitiza Mhe. Jafo

  Akifafanua zaidi Waziri Mhe. Jafo amesema kuwa wajibu wa Maafisa Utumishi ni kuwa Kiungo kati ya Wakurugenzi na watendaji wa Taasisi hali itakayosaidia kupunguza au kuondoa malalamiko yanayofikishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

  Aliongeza kuwa Maafisa Utumishi wanajukumu kubwa katika kuhakikisha watumishi wanapandishwa madaraja kwa wakati, wanathibitishwa kazini kwa wakati ili kuwaongezea morali kwa watumishi hali itakayoongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

  Pia aliwaasa Maafisa Utumishi kuhakikisha kuwa Wanatunza taarifa zote za
  Watumishi kwa kuzingatia sheria , Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma ili kulinda maslahi mapana ya nchi. Kwa upande Wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe amewataka Maafisa Utumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia kuwa Serikali ya
  Awamu ya Tano inalenga kuleta mabadiliko kwa wananchi kwa kuwapa huduma bora.

  Aidha, Mhandisi Iyombe aliwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali inayopelekea kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa watumishi na hivyo kuzorotesha kasi yakuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bw. Mathias Kabunduguru akizungumza katika Kikao Kazi hicho amesema kuwa baadhi ya masuala yanayoleta kero kwa watumishi wa Umma ni pamoja na Mamlaka za Ajira kukataa kuidhinisha au kupitisha barua za watumishi kuhama, hivyo aliwaasa Maafisa hao kutozuia maombi ya watumishi wanaoomba kuhama.

  “Mamlaka husika inaweza kuweka maoni yakuomba mbadala wa Mtumishi
  anayeondoka na sikuzuia barua yake yakuomba uhamisho kwa kuwa uhamisho wa watumishi unajengwa kwa Misingi ifuatayo, kwanza mtumishi anayohaki ya kufanya kazi popote,Uhamisho hujenga Afya ya Utumishi kwa ujumla na pia swala hilo husaidia Kujenga umoja wa Kitaifa.

  Aliongeza kuwa Kikao Kazi hicho kitakuwa chachu ya kuimarisha
  Uadilifu,Uwajibikaji,Uwazi, na misingi mingine ya Utawala Bora.

  ’’Pamoja na Kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa Vyeti vya Kidato cha nne, Sita, Ualimu na Vyuo Vikuu bado wapo waajiri aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya wameendelea kuwafumbia macho watu wenye vyeti bandia ambapo wiki iliyopita tulilazimika kuchukua hatua kali dhidi ya Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kutokana na kuficha watu wenye vyeti Bandia” Alisisitiza Bw. Kabunduguru.

  Akizungumzia swala la kutambua mchango wa watumishi wanaofanya kazi kwa bidiivBw. Kabunduguru amesema linaongeza ari yao katika kutekeleza majukumu yao hivyo ni vyema utaratibu wa kuwatambua hata kwa kuwaandikia barua za kutambua mchango wao na pia kuwaadhibu watumishi wazembe wasiotekeleza majukumu yao.

  Kikao Kazi hicho cha siku Siku mbili kilichowahusisha Wakurugenzi wa Rasilimali watu wa Wizara zote, Idara zinazojitegemea na Maafisa Utumishi wa Mikoa, Halmashauri zote hapa nchini kinafanyika mjini Dodoma kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora na Ofisi ya Rais TAMISEMI kikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuimarisha utendaji na huduma zinazotolewa
  kwa wananchi.

  0 0


  • Washindi wengine 3,000 wajishindia kifurushi cha intaneti 1GB kila mmoja
  Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone Airtel Tanzania imewazadia washindi wa droo ya tatu ya promosheni yaSHINDA NA SMATIKA Intaneti katika droo iliyochezwa leo jijini Dar es Salaam.

  Katika droo hiyo ya leo, washindi 10 wameweza kujishindia simu za kisasa  za smartphone pamoja na modem huku wengine 3,000 wakijishindia kifurushi cha intaneti cha 1GB BURE. Hii ni droo ya tatu tangu kuzinduliwa kwa promosheni hiyo ambapo mpaka leo jumla ya washindi 8,000 tayari wamezawasiwa  zawadi ya kifurushi cha intaneti cha 1GB BURE.

  Akizungumza baada ya droo ya leo, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa promosheni ya SHINDA NA SMATIKAIntaneti ni maalum kwa  wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Yatosha Intaneti nchi nzima.

  ‘Promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti bado inaendelea, ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kambambe’, alisema Mmbando.
   Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akionyesha baadhi ya simu za smartphone ambazo ni zawadi kwa washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Jumla ya wateja 3000 walijishindia 1GB ya intaneti bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.


   Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti wakati wakuchezesha droo leo jijini Dar es Salaam ambapo washindi 3000 walijishindia 1GB bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.

  Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na washindi wa SHINDA NA SMATIKA Intaneti wakati wakuchezesha droo leo jijini Dar es Salaam ambapo washindi 3000 walijishindia 1GB bure, watano simu tano za smartphone na tano modem.


  0 0

  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara,Raphael Joseph Nyanda akifungua Semina kwa Maafisa hao wa Mkoa wa Mara na Arusha.
  Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo anayeshghulikia Habari na picha akitoa Salama za Idara wakati wa Semina hiyo
  Bibi Rebecca Kwandu, Mkuu wa Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, akitoa Malengo ya Mafunzo hayo kwa Mikoa ya Mara na Arusha.
  Baadhi ya Wakufunzi wa mafunzo wakifatilia kwa Makini Hotuba ya Ufunguzi.
  Athuman Pemba Mmoja ya Watoa mada, akiwa anaendelea na Utoaji mada mara baada ya Ufunguzi.
  Mkuu wa Mawasiliano kutoka OR TAMISEMI, Bibi Rebecca Kwandu, akiteta jambo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa muda mfupi kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.

  ………………

  Na. Atley Kuni OR TAMISEMI.

  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda amewataka Maafisa habari na TEHAMA nchini kutekeleza majukumu yao kwakuzingatia Weledi, maarifa na ubunifu kwakuwa wao ni Mawakala wa mabadiliko.

  Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilicho andaliwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwakushirikiana na Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya umma PS3, na kushirikisha maafisa habari na TEHAMA kutoka mikoa ya Mara na Arusha, amewatahadharisha maafisa hao kuwa endapo watazembea kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa weledi basi watu wengine watapotosha umma.

  “Kila mmoja miongoni mwenu anayo dhamana yakutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu watu wasio wema watapotisha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya serikali” amesisitiza Nyanda.

  Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, Rebbeca Kwandu, akizungumza kabla yakumkaribisha Mgeni rasmi, amewataka maafisa hao kubadilika katika utendaji wao mara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.

  “Mwanzoni tulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na muongozo ambao ni dira ya uendeshaji lakini mara baada ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuandaa muongozo huu kwakushirikiana na wadau wetu PS3 ni imani yangu tutabadilika” amesema Kwandu na kuongeza kuwa uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.

  Akizungumza kwa niaba ya Mradi wa PS3 Mkurugenzi anayeshughulia utawala bora na Ushirikishwa wa wananchi Dkt. Peter Kilima, amekiri kuwa Maafisa habari na Maafisa TEHAMA ndio roho ya taasisi, hivyo ushirikishwa hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursa kwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.

  Awali akitoa Salaam za Idara ya habari maelezo, Mkurugenzi Msaidizi wa habari na picha Thadeus Rhodney, amesema kuwa ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali lazima maafisa habari wawe na zana (tools) za utendaji kazi na zana yenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa ni Tovuti.

  “Wafadhali PS 3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Fremwork (GWF) tumieni hizi tovuti kama tools ya kuujuza umma.

  Ofisi Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji mifumo ya umma chini ya mradi wa PS3 wanaendesha Mafunzo ya nanna bora ya uendeshaji wa tovuti za serikali ambapo Maafisa habari pamoja na Maafisa TEHAMA wapatao 418 nchini kote watapatiwa mafunzo

  0 0

  Baadhi ya eneo ambalo linalalamikiwa na Sizya Mashirungu kuvamiwa na kujengwa shule na serikali kinyume na makubaliano kati yake halmashauri ya Mji wa Geita. 
  Mwenyekiti wa mtaa Shinde Bw Makoye Mumilambo akizungumza juu ya malalamiko ambayo yametolewa na Bw,Sizya Mashirungu juu ya kutaka kutahifishwa eneo la familia na serikali ya mtaa huo. 
  Eneo linalolalamikiwa likiwa tayari limeshaanza kuchimbwa Msingi kwaajili ya ujenzi wa shule ya Msingi ya Shinde. 


  Na Joel Maduka ,Geita.

  Familia ya Bw Mlelemi Mashirungu inayoishi mtaa wa Mkolani Kata ya Nyankumbu wilayani Geita imeilalamikia serikali kwa kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi Shinde kwenye shamba la ukoo huo lenye ukubwa wa ekari 20 bila makubaliano na serikali ya Halmashauri ya mji wa Geita .

  Msimamizi wa eneo hilo Bw Sizya Mashirungu amesema eneo la ujenzi wa shule hiyo lilitengwa na serikali ya kijiji kabla ya kubadilishwa na kuwa mitaa lakini ameshangazwa na kitendo cha serikali kuanzisha ujenzi katika eneo lake bila makubaliano.

  Bw Mashirungu alisema eneo hilo limeanza kumilikiwa na ukoo tangu mwaka 1991 baada ya Baba yao mzazi kufariki na kwamba limekuwa likitumika katika shughuli za kilimo.

  “Anayezungumza kuwa hii ni hifadhi akuna ofisi yoyote ambayo ilishawai kufika kuweka pingamizi juu ya eneo hili na mshangaa mwenyekiti ambaye anangangania kuwa eneo hili ni la hifadhi yani huu ni utapeli kabisa na mimi sitakubaliana na maamuzi ambayo yanataka kuchukuliwa na serikali juu ya matumizi ya eneo hili”Alisema Mlelemi.

  Aidha kutokana na malalamiko kumuelekea Mwenyekiti wa mtaa huo Bw Makoye Mumilambo kutaka kuhujumu eneo la ukoo huo, Kwa upande wake amesema eneo hilo lipo ndani ya hifadhi ya halmashauri ya mji wa Geita na kwamba watu wamekuwa wakimiliki maeneo hayo kinyume na utaratibu tangu mwaka 1978 na kwamba hata yeye ni mvamizi kutokana na miti iliyokuwepo kukatwa hivyo serikali imeamua kubadili matumizi ya eneo hilo.

  Diwani wa kata hiyo Bw Machael Kapaya alisema madai ya Bw Masirungu sio ya kweli kwa kuwa miradi inayoanzishwa michakato huanzia kwenye ngazi ya chini ambayo ni wananchi ambao wanapendekeza mahitaji yao na kwambe yeye ni moja kati ya viongozi wa mitaa na anajua utaratibu.

  “Huyu ni kiongozi kabisa wa mtaa na anajua taratibu zote ambazo zinafanyika kuibua miradi kwenye mitaa na wakati tunapendekeza eneo hilo alikuwepo kwenye kikao cha kamati ya maendeleo ya kata na tulikwisha mwambia kama anamadai alete vielelezo ambavyo vinathibitisha kuwa ni eneo lake lakini hadi sasa ajaleta na tukimwambia aje kwa mkurugenzi anachenga chenga”Alisema Kapaya.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modesti Apolinary alisema eneo linalotumika katika ujenzi wa shule ni eneo la hifadhi na kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kumiliki eneo lililo ndani ya hifadhi ya serikali.

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa.
  Sehemu ya Wakazi wa Iringa mjini waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

  ……………..

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaambia watendaji kuwa huu si wakati wa kuambiwa kufanya kazi ni wakati wa kujituma mwenyewe.

  Makamu wa Rais aliyasema haya wakati akihutubia wakazi wa Iringa mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa.

  Makamu wa Rais aliwataka watendaji watoke wakajionee wenyewe miti inavyokatwa na vyanzo vya maji kuharibiwa.

  “Sijaridhika na jinsi wananchi wanavyofanya shughuli zako kule kwenye vyanzo vya maji, sijaridhika na namna waheshimiwa wabunge na viongozi wengine wanavyolinda wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji na hili nimesema niliseme hapa tupo sote, kwenye vyanzo vya maji hakuna mbadala, hakuna mswalie mtume tunapodai tupate maji safi na salama haya maji hatutengenezi sisi serikali kuu haya maji yanatoka kwenye vyanzo vyanzo ambavyo vinataka vitunzwe”

  Makamu wa Rais aliwataka Viongozi kusimamia haki za wanyonge na kuhakikisha haki inatendeka kwa wanyonge ambao wengi wamedhulumiwa mali hasa ardhi.

  Makamu wa Rais aliwataka wananchi kuzidai halmashauri zipeleke pesa kwenye miradi ya maendeleo ,pia alizitaka Halmashauri kuzisimamia zile pesa asilimia 10% kwa ajili ya Wanawake na Vijana zinatoka lakini pia kusimamia zinavyotumika.

  Makamu wa Rais aliwaasa wakazi wa Iringa mjini kuwa makini na Viongozi ambao hawapendi maendeleo kwa kuwazuia kushiriki kwenye miradi ya maendeleo, aliwaambia wananchi hao maendeleo hayana chama.

  Makamu wa Rais aliwaagiza uongozi wa mkoa kuanza kurasimisha biashara zisivyo rasmi kwa kuanza kuwatambua wamachinga, kuwasajili na kuwapa vitambulisho na kuwaunganisha kwenye mifuko ya jamii na bima ya afya pia kuwawekea maeneo ya biashara yenye mahitaji yote muhimu.

  Makamu wa Rais ambaye amekuwa mkoani Iringa kwa siku nne akihamasisha shughuli za maendeleo alisema Serikali itaendelea kuboresha na kutanua vituo vya afya kwa kuviwekea huduma bora za mama na mtoto, vyumba vya upasuaji na vyumba vya kuhifadhia maiti.

  Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Iringa barabara zote ambazo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 iliekeza ,zitajengwa kwa kiwango cha lami.

older | 1 | .... | 1515 | 1516 | (Page 1517) | 1518 | 1519 | .... | 1903 | newer