Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1514 | 1515 | (Page 1516) | 1517 | 1518 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Yang wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya st Louis ya Visiwa vya Shelisheli katika mchezo uliochezwa leo Jijini Dar es Salaam.

  Mchezo huo wa kwanza katika hatua ya mtoano uliopigwa leo ilichukua takribani dakika 67 kwa Yanga kuandika goli la kwanza na la ushindi kupitia kwa mchezaji wake Juma Mahadhi aliyeingia kuchukua nafasi ya ibrahim Ajib.

  Yanga ilishinda kutumia nafasi walizozipata katika kipindi cha kwanza ikiwemo panati aliyoipiga Obrey Chirwa na kuitoa nje.St Louis imeweza kupoteza mchezo wao wa kwanza lakini walionekana wakijilinda kwa mda wote.

  Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema kuwa wameona wapi walipokosea ila katika mchezo wa marudiano  utakaofanyika wiki mbili zijazo.

  Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu hatua inayofuata ya Klabu Bingwa Afrika mechi itakayochezwa Februari 19 mwaka huu.

  0 0

  "Mimi ni wa hapa hapa, nimesoma shule hii ya Msingi ya Tandale. Naijua vyema Tandale, nazijua vyema shida zenu." - Mtulia

  "Leo nimekuja kuombewa kura na Watu wanaoongoza nchi, nimekuja kuombewa kura na Waziri ambaye namwambia shida zenu moja kwa moja. Huo ni usaliti?" - Mtulia."Nimetoka kwenye chama cha CUF kisicho na chochote chenye kuleta maendeleo, nimekuja kwenye Chama Cha Mapinduzi chenye Serikali, ilani ya uchaguzi na maendeleo." - Mtulia

  "Leo hii nipo kwenye chama ambacho napewa pesa Tsh. Bilioni 25 kwa ujenzi wa barabara; napewa Tsh. Bilioni 3.5 kwa ujenzi wa masoko. Bilioni 1 ya gharama ya uchaguzi kitu gani mbele ya maendeleo hayo?" - Mtulia."Nayajua matatizo yenu, mfereji wa Mwangosi utajengwa, mna matatizo ya barabara mbovu zote zitaenda kujengwa" - Mtulia

  "Najua akina Mama na Vijana hamjapata pesa za asilimia 10 za mikopo toka Manispaa, nipeni kura za ndiyo za kutosha nikasimamie mpewe mikopo hiyo" - Mtulia."Tsh. Bilioni 25 za ujenzi wa Barabara, Tsh. Bilioni 3.5 za kujenga masoko bora zipo tayari. Nichagueni niwe Mbunge wenu nikasimamie ujenzi huo" - Mtulia

  "Nawaombeni mambo mawili. Moja, muende mkaniombee kura kwa wale waliopo majumbani wamchague Mtulia awe Mbunge. Pili, muwahi vituoni mapema mkiwa na kadi zenu za kupigia kura mkanipigie kura za ndiyo niwe Mbunge wenu" - Mtulia."Mtulia ni mwenzenu, Mtoto wa kitaa mwenzenu, naombeni sana kura zenu za ndiyo tarehe 17 mwezi wa pili. Muwahi vituoni, mkanipigie kura za ndiyo." - Mtulia

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera kulia, akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 kutoka kwa  meneja mawasiliano wa Shirika la maendeleo la Petroli Nchini(TPDC) Marie Msellemu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo.
   Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera katikati na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya  hiyo Chiza Malando kulia,wakifurahia mfano wa Hundi ya shilingi milioni 25  iliyotolewa na Shirikala maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya ambacho kinatajwa mara kitakapokamilika kitasaidia kusogeza huduma za matibabu kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka  kituo hicho kushoto ni meneja mawasiliano wa TPDC Marie Msellemu.
   Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera,akimtembeza meneja mawasiliano wa Shirika la Petroli Nchini Marie Msellemu maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Nakayaya ambacho ujenzi wake umeibuliwa na kuanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kwa kutumia wafadhili mbalimbali.Picha na Muhidin Amri
   Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya Nakayaya kiendelea kengwa,kikiwa chini ya simamizi mkbwa wa DC Homera,kituo hicho kinataraiwa kukamilika Septemba mwaka huu 2018. 
   Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera kushoo akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Vinesh Mathew wa korosho Africa  Ltd kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo.


  Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma amepokea hundi ya fedha kutoka shirika la maendeleo ya petrol Tanzania TPDC ambayo ilikabidhiwa na Bi Marie Mselemu Mkurugenzi wa Mawasiliano TPDC .

  Bi Marie Mselemu aliongozana na wasaidizi wake akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya petroli Eng Musomba, hata hivyo Bi Marie Mselemu alisema walifikia maamuzi ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Nakayaya ili kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ndg Juma Zuberi Homera na pia waliandikiwa barua na  DC Homera ambaye aliibua wazo hili kwa lengo la kukabiliana na msongamano mkubwa wa wagonjwa ulioko hospital ya wilaya Tunduru.

  Kwa upande wake DC Homera alilishukuru shirika hilo na kaimu Mkurugenzi huyo kwa moyo wa kizalendo walioonesha kwa wananchi wa Tunduru na pia Homera alisema shirika limeunga mkono jitihada za Mhe Rais Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo .

  Aidha kwa upande wao kiwanda cha korosho cha Tunduru, Korosho Africa wamechangia fedha za kitanzania million 5 Kati ya million 10 walizoahidi kwa ajili ya kutengeneza madirisha ya chuma ya kituo hicho yani (gril) .kituo hicho mpaka sasa kinaendelea kusimamiwa na Mhe Homera na kinatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka huu 2018.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu wa ZATU Mussa Omar Tafurwa, alipowasili katika viwanja vya Wizara habari kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Walimu wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama cha Walimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar wakati wa ufunguzi huo
  BAADHI ya Walimu wa Chama cha Walimu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano wa Sita uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa viongozi wa meza kuu wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa solidariti foreva wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama cha Walimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar
  WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Kisiwandui wakicheza ngoma ya mwanandege wakati wa ufunguzi huo wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Zanzibar.
  RAIS w Chama cha Walimu Zanzibar Seif Mohammed akisoma risala ya Chama hicho wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama hicho wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
  BAADHI ya Wanachama wa Chama cha Walimu Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi ya ufungunguzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
  KAIMU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia ni Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kuufungua mkutano huo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha picha ya sura yake aliokabidhiwa zawadi na Chama cha Walimu Zanzibar wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania Bara. Leiya Ulaya, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar
  RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Walimu Uganda Tumuhimbise Zadock, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Walimu kutoka (DLF) Flemming Sorrensen, baada ya hafla ya uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Zanzibar.Picha na Ikulu

  0 0

  Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Nicholas O’Dwyer, Frank Lynham, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua ya maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha kisasa cha lami, wakati alipotembelea kambi ya mkandarasi, mkoani Morogoro.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akikagua eneo la Ruaha lililopo katika Wilaya ya Kilombero ambapo ujenzi wa daraja kubwa lenye urefu wa mita 130 linatarajiwa kujengwa katika barabara ya Kidatu-Ifakara KM 66.9, mkoani Morogoro. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga.
  Muonekano wa daraja la zamani katika eneo la Ruaha ambapo litajengwa daraja kubwa la Great Ruaha lenye urefu wa mita 130 katika barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9, mkoani Morogoro.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Morogoro.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo, wakisalimia wananchi wa kijiji cha Sululu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kukagua kambi ya Mkandarasi anayejenga barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa KM 66.9, kwa kiwango cha lami.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo (kulia), katika ziara yake ya kikazi wilayani humo, mkoani Morogoro.


  Serikali imesema imeanza ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 kwa kiwango cha lami ambapo kukamilika kwake kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya za mkoa wa Morogoro.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Reynolds Construction kutoka Nigeria anayejenga barabara hiyo kujenga kwa viwango na kukamilisha kwa wakati.

  “Mradi huu umesuburiwa kwa siku nyingi na wananchi wa wilaya hii na mkoa kiujumla, mategemeo ya Serikali ni kuwa mradi huu utaukamilisha mapema mwezi Aprili, 2020 kwa kuzingatia vipengele vya mkataba na kwa viwango stahiki”, amesema Prof. Mbarawa.

  Amesema kuwa ujenzi katika barabara hiyo unatarajiwa kuhusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili, madaraja madogo manne, makalvati makubwa na madogo 271 na unatarajiwa kudumu kwa miaka 20.

  Aidha, Prof Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itahakikisha wananchi wa mkoa huo wanapewa kipaumbele kwenye ajira mara tu kazi itakapoanza ili kuongeza kipato chao.“Mradi umeanza na nimemuelekeza mkandarasi kuajiri afisa mwajiri ili kuhakikisha nafasi nyingi za ajira zinapatikana kwa wazawa kwani nafasi 70 walizoajiri mpaka sasa ni za mwanzo tu, ila nafasi nyingine zitaongezwa”, amefafanua Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo, ameipongeza Serikali kwa jitihada inazozifanya kuboresha miundombinu ya barabara hapa nchini na amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kuwa wananchi na uongozi wa usalama wa Wilaya yake watatoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo ili waweze kunufaika na mradi huo mapema.

  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, amesema kuwa kazi halisi itaanza mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu na watahakikisha wanamsimamia mkandarasi kwa karibu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na viwango.

  Ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara KM 66.9 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kujengwa kwa miezi 30 na utagharimu kiasi cha shilingi

  bilioni 111.4 na unafadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (European Union), Shirika la Misaada la Uingereza (UK aid) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

   Kila jambo hakika huwa halikosi mwisho msemo huu huwa na ukweli ndani yake ilikuwa kama ndoto kwa Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin kutangaza kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red, lakini ndoto hiyo imetimia kabisa bila kipingamizi mbele ya hadhara kubwa ya watu usiku wa 9 Feb 2018 ndani ya King Solomon Hall.

  Lad in Red 2018 limekuwa ni Onyesho la Mwisho kwa  Designer mkongwe ambaye ndiye mwanzilishi wa Onyesho hilo Asya Idarous Khamsin. Kiukweli Jukwaa la mwisho la Lady in Red lilikuwa na mvuto, kwa taswira ya mbali inaonyesha kabisha ni jukwaa mabalo lilikuwa na ushirikiano mkubwa sana wa wadau na wanamitindo wengine toauti ilivyo zoeleka.

  Mwisho ni pongenzi kwa Asya kwa kuamua kuwaachia jukwaa wanae yaani Designers walio lelewa na Lady in Red, maana angekuwa na roho  mbaya pengine Onyesho lingeishia mitini Hongera sana Asya.
  0 0

  The UNESCO Dar es Salaam Office is conducting a 7-day training workshop for community radio practitioners on Editorial, Programming and Monitoring on Issues of Local Concern. The training which started on Tuesday February 06 has brought together 49 community media practitioners from 24 UNESCO supported community radios. The main objective of the training is to build capacity of community radio journalists and reporters on news formats. The move is meant to enable them report on issues of local concern through investigative journalism, sports news reporting and monitoring the quantity and quality of news bulletins.  Participant contributing her points.[/caption] Participants to the training comprise of journalists and reporters as well as monitoring focal points previously trained on M&E by UNESCO. UNESCO has localized Gender Sensitive Indicators for Community Radios to emphasize on “sex disaggregated participation list for workshops”. To put this into practice, selection of participants from community radios will adhere to gender balance aspects. Mentorship in journalism for local public interest, in particular investigative journalism will come after the training where 72 journalists are expected to gain knowledge through peer learning. Feedback session.[/caption] UNESCO with the financial assistance from the Swiss Development Corporation (SDC) supports community radios and the Community Media Network (Tanzania Development Information Organization- TADIO). The support is meant to ensure that people in Tanzania, especially the poor, women and girls, have the capacity to make informed decision on issues that affect their daily lives.  Above and below discussion groups of participants on news editing session.[/caption] Community radios in attendance under the SDC support with their regions in brackets are Nuru FM (Iringa), Pambazuko FM (Morogoro), Fadhila FM (Mtwara) Jamii Mtukwao FM (Mtwara), Loliondo FM (Arusha), Baloha FM (Shinyanga), Kahama FM (Shinyanga) Ileje FM (Songwe) and Tripple A FM (Arusha). In the list are Storm FM (Geita) and Sengerema FM (Mwanza), Kwizera FM (Kagera), Dodoma FM (Dodoma) and Kitulo FM (Njombe). Others are Uvinza (Kigoma), Mpanda (Katavi), Pangani (Tanga), Boma (Kilimanjaro), Mazingira (Mara), Mtegani FM (Unguja South,) Mkoani FM (Pemba South), Micheweni FM (Pemba North) Tumbatu FM (Unguja North), Ruangwa FM (Lindi) respectively. The training covers 77.4% of all regions in the United Republic of Tanzania.

  0 0

  MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam, John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.

  Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui kutokana na uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana wiki hii kupitia ripoti za makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

  Alitoa mchango mkubwa kwa Simba mwezi huo ikipata pointi tisa katika michezo mitatu iliyocheza na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za usaidizi wa bao.Pia kiwango cha mshambuliaji huyo aliyecheza dakika zote 270 za michezo mitatu ya Simba mwezi huo kilikuwa juu karibu kila mchezo.

  Kwa upande wa Okwi aliyecheza dakika 206 kati ya 270 ilizocheza timu yake, alitoa mchango mkubwa kwa Simba kupata idadi hiyo ya pointi na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku akifunga mabao manne. Simba iliifunga Singida United mabao 4-0,ikaifunga Kagera Sugar mabao 2-0 na kisha ikailaza Majimaji mabao 4-0.

  Awesu aliingia katika hatua hiyo kutokana na kung’ara katika michezo ambayo Mwadui ilicheza mwezi huo, akiibuka Mchezaji Bora katika mchezo wao dhidi ya Yanga, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam uliomalizika kwa timu hizo kutofungana, pia aliibuka mchezaji bora wa mchezo wo dhidi ya Njombe uliofanyika Uwanja wa Mwadui, Shinyanga na timu hizo kufungana mabao 2-2.

  Mshambuliaji huyo aliyecheza kwa dakika 322 kati ya 360 ilizocheza Mwadui alifunga bao moja na kuisaidia timu yake kupata pointi sita katika mechi nne ilizocheza mwezi huo, ikitoka sare tatu na kushinda moja, ikiendelea kubaki nafasi ya kumi.Kutokana na ushindi huo, Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi, Kampuni ya Vodacom Tanzania.

  Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba) na mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba).

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba.

  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetua Mjini Bukoba asubuhi hii ikitokea Jijini Dar es salaam. Tayari kwa mchezo wao na Wenyeji wao Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba kesho jumatatu. Azam FC katika mchezo uliopita ilifungwa na Simba bao 1-0. Msimu uliopita Kagera Sugar ilifungwa na Azam Fc bao 3-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba na msimu huo huo Kagera Sugar waliwafunga bao 1-0 Azam Fc na kuumaliza msimu huo wakiwa nafasi ya tatu.  

  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2013/2014, wataendelea kuikosa huduma ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja, aliyepewa mapumziko maalum kufuatia majeraha ya goti la mguu wa kulia yanayomsumbua, pamoja na mshambuliaji Wazir Junior na beki Daniel Amoah, ambao nao ni majeruhi.

   Aidha itamkosa nahodha wake msaidizi, Agrey Moris, aliyekusanya kadi tatu za njano, zinazomfanya kukosa mechi moja ijayo, lakini wachezaji wengine wote waliobakia wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, ukiondoa majeruhi wa muda mrefu Joseph Kimwaga, ambaye anaendelea na programu ya mwisho (recovery) ya kurejea dimbani kwenye ushindani. 

  Mpaka sasa Azam FC imejikusanyia jumla ya pointi 33 kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa sawa na Singida United iliyonafasi ya nne, ikizidiwa pointi nane na Simba iliyojikusanyia pointi 41 kileleni huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi zake 34.
  Walipowasili asubuhi hii kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
  Kocha wa Azam Fc Idd Nassor Cheche akiteta jambo na mwandishi wa habari(hayupo pichani) mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kaitaba. Kocha huyo  amesema kilichowaleta ni pointi tatu hakuna kingine huku akiwamiminia sifa wenyeji wao kuwa ni timu nzuri na kwa sasa ipo kwenye sehemu mbaya hivyo mechi hiyo itakuwa  ngumu lakini watafanya jitihada na hatimae wazoe pointi zote tatu.
  Mshambuliaji wa Timu ya Azam Fc Mbaraka Yusuph nae ameambatana na kikosi hicho. Mbaraka Yusuph alikuwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Kagera Sugar.
  Wachezaji wa Azam Fc wakiteta Jambo na Kocha wao Idd Nassor Cheche mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba.

  0 0

   Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijiandaa  kupima Kisukari leo aliposhiriki kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha .
  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata kipimo cha Presha kutoka kwa Dokta Mahmod Shahamati ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Iranian kilichopo jijini hapa.

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameungana na wakazi wa jijini hapa katika kongamano la  kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania  kilichopo jijini hapa.

  Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji  na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

  Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti  kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

  "Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu, angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila  mwananchi anahitaji kuipata" amesema Meya Mwita.

  Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa  wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha  Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao.

  Imetolewa leo Februali 11 na  Christina Mwagala Afisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji.

  0 0

  Mbunge wa Mtela ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde ‘Kibajaj’ akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)
  Mbunge wa Mtela ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde akihutubia wananchi wakati akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Akson akimuombea kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kinondoni Said Mtulia katika Mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akimuombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kinondoni Saidi Maulidi Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya shule ye msingi Tandale jijini Dar es Salaam

  Mbunge wa Mtela ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde ‘Kibajaj’ akipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Said Mauli Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam
  Wananchi wakishangilia kwa hamasa wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam
  Mbunge wa zamani wa Kinondoni ambaye ni Meneja wa kampeni za uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo Iddi Azani akisalimia wananchi baada ya kuitwa jukwaani na Msemaji Mkuu katika mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Kinondoni Saidi Mtulia uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Tandale
  Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni za ubunge za CCM uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Tandale jijini Dar es Salaam, leo
  Baadhi ya wabunge wa CCM na wageni waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kate Kamba (katikati) akiwa na baadhi ya wabunge wa CCM waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mtulia katika viwanja vya Sule ya msingi Tandale
  Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni katika Mkutano wa kampeni hizo za kumnadi mfgombea ubunge jimbo la Kinondon Said Mtulia (kushoto)
  Baadhi ya Wabunge wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo


  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCm katika Jimbo la Kinondoni said Mtulia akipanda jukwaani
  Mgombea ubunge katika jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM said Mtulia na Msemaji Mkuu katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya shule ya Tandale Mbunge wa Mtela na Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Livingstone Lusinde ‘Kibajaj) akicheza wimbo wa CCM baada ya Mtulia kupanda jukwaani
  Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Akson (kushoto) akiungana na Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM said Mtulia (katikati) wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea huyo zilizofanyika kwenye Viwanja vya shule ya msingi tandale jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mbunge wa Mtela na mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Lusinde
  Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbea wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde akihutubia wananchi wakati akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.

  Mbunge wa Mtela ambaye pia ni Mjumbea wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde akihutubia wananchi wakati akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na tani moja ya sukari na chumvi, majani ya chai mifuko 18, mirungi kilogramu 16, vifaranga vya kuku 5000 na mayai kasha 416 katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha zikitokea nchini Kenya kupitia njia zisizo rasmi.
  Akizungumza mara baada ya kukamata bidhaa hizo, Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapo Edwin Iwato alisema bidhaa hizo ni mali ya Joseph Sekino, Innocent Minja na Andrew Lyimo wote wakiwa ni wafanyabiashara kutokea Tanzania na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
  "Tumewakamata wafanyabiashara watatu ambao ni Joseph Sekino akiwa amepakia tani moja ya sukari na chumvi na majani ya chai mifuko 18 kwenye gari Na. T 785 AWV, Innocent  Minja akiwa na mayai kasha 416 na mirungi kilo 16 kwenye gari Na. T 443 CQU na Andrew Lymo akiwa na vifaranga vya kuku 5000 kwenye gari Na. T 441 DHW wote wakitokea nchini Kenya kuja mkoani Arusha," alisema Iwato.
  Iwato alieleza  kwamba, wafanyabiashara hao waliingiza baadhi ya bidhaa hizo kwa kutumia vifungashio vya bidhaa nyingine za nchini Tanzania ili kuficha uhalisia wake huku wakiwa hawana vibali wala kulipa ushuru wa Serikali kama inavyotakiwa.

  Alifafanua kuwa, mirungi ilikamatwa ndani ya mifuko ya plastiki maarufu kama Rambo ikiwa imefichwa kwenye boneti ya mbele ya gari aina Noah Na. T 443 CQU sehemu ya injini.
  Naye, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Richard Kayombo alisema, tabia ya wafanyabiashara hao siyo tu inawahujumu wafanyabiashara wenzao bali inakwamisha azma ya Serikali ya kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya kila mwananchi.
  "Tabia ya wafanyabiashara hawa siyo nzuri kwa kuwa inakwamisha ukusanyaji mapato ya Serikali na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine wanaofikiria kufanya biashara pasipo kutumia njia rasmi na kulipa ushuru ipasavyo", alisema Kayombo.
  Aidha, Kayombo aliongeza kuwa, bidhaa zote haramu zilizokamatwa zitateketezwa kwa mujibu wa Sheria, zile zinazofaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA na magari yote yaliyotumika kusafirisha bidhaa hizo yametaifishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Utaifishaji wa magari na bidhaa ambao usafirishaji wake haufuati sheria na taratibu, unalenga kukomesha shughuli za magendo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa zinakwamisha juhudi za Serikali katika ukusanyaji wa mapato.


  0 0

   Boti ya kisasa yenye injini na maboya ikiwa na thamani ya shilingi milioni 47  imekabidhiwa kwa kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria.

  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kikumbaitale  kata ya Kigongo wakiwa kwenye hafra fupi ya makabidhiano. 

   Vyumba vya madarasa ambavyo vimejengwa na  TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo kwa kushirikiana na  wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6.

  Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi akizungumza na wananchi namna ambavyo wameweza kutekeleza miradi yote miwili na kutoa kwa wananchi ambao wanazunguka kisiwa cha hifadhi ya Rubondo.

   Mwenyekiti  wa Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara akizungumza na wananchi ambapo aliwasisitiza   kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi  pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Dkt,Allan Kijazi wakitia saini hati za  makabidhiano.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akitoa hati kwa mwenyekiti wa Kijiji cha Mwelani.

  Na,Joel Maduka,Geita

  Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhamini ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.


  Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi alisema mradi wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6.
  "Madarasa haya yatapunguza tatizo la upungufu wa vyumba kusomea ambalo lipo katika shule za sekondari ya Kigongo .Kukamilika kwa madarasa haya kutasaidia kuanzishwa kwa shule ya sekondari ya Kikumbaitale ikiwa ni sehemu ya shule ya Kigongo mpaka itakapopata usajili wa kudumu",alisema Kijazi.

  Aidha Dkt. Kijazi alisema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya ikiwa na thamani ya shilingi milioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ ni kutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi kisiwa cha Rubondo ilipokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelanina kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa itasimamia vyema miradi hiyo na pia  amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusiana na uvuvi haramu na kwamba wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Ihongole Mafinga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mgololo, Mufindi mkoani Iringa mara baada ya kulifungua ,pembeni yake ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Rai wanaomiliki kiwanda cha Mufindi Paper Mills Bw. Jaswant S. Rai na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.

  Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

  Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .

  Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.

  Makamu wa Rais alisema “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa yale yanayohitajika”.Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.

  Mapema leo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu shilingi milioni 450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.

  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kipunguni A na Mashariki, Dar es Salaam kuhusu ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao, ili kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongele.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo, akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kipunguni A na Mashariki, Dar es Salaam kuhusu ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
  Mkazi wa Kipunguni Mashariki Dar es Salaam leo akichangia mada katika mkutano wa ulipwaji wa fidia kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

  Mkazi wa Kipunguni Mashariki, Bw. Daudi Peter, akichangia hoja katika mkutano wa ulipwaji wa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayon gela, akizungumza na wanannchi Kipunguni A na Mashariki, kuhusu ulipwaji wa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege.

  0 0


  Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari. 

    Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo, usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo. Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni, Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo. 

    Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani. Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio. 

    Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki. Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi. 

    Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika. Si tu redio inatumika kubadilishana Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika. Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii. 

  Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO. 

    Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo. Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii, kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na kuboresha uwezo wao katika kazi.

  0 0

   NA SAMIA CHANDE, KATAVI

  Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesaidia kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 2.5 ambazo zimesaidia  kumaliza tatizo la umeme Wilaya ya  Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani  Katavi, Mhandisi Julius Sabu, kituo hicho kimesaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo, na kutoa umeme wa uhakika na wenye ubora.“Kituo hicho kinahudumia Wilaya za Tanganyika, Mpanda mjini, maeneo ya Starlike na Kakese”. Aliainisha Mhandisi Sabu.Lakini pia Kituo kimepunguza gharama za uzalishaji umeme ukilinganisha na Kituo cha zamani.
  Wakaazi wa Wilaya ya Tanganyika wameishukuru Serikali na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kuwaletea umeme kwani umekuwa mkombozi katika shughuli zao za kiuchumi, kama vile kuchomelea, "saloon",  na biashara ya maduka.
  “Nawashauri Wananchi wenzangu, sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa hii inayotokana na kupata umeme wa uhakika katika kukuza shughuli zetu za kiuchumi.” Alisema Mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maneno Mtogwa mkazi wa Wilaya ya Tanganyika.
  Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi ametoa rai kwa Wananchi wa Wilaya za Tanganyika, Mpanda Mjini, maeneo ya Kakese na Starlike kujitokeza kwa wingi kwenye madawati ya huduma kwa Wateja na Ofisi za TANESCO ili kupatiwa huduma kwani TANESCO imejipanga kuwahudumia Wananchi popote walipo na kwa viwango vya hali ya juu.
   Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu kiwa anakagua mashine kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda mkoani Katavi


   Kituo cha kufua umeme cha Mpanda Mkoani Katavi
  Vijana wa Wilaya ya Tanganyika wakiwa wanachomelea mageti

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dr. Mwiguli Lameck Nchemba awewataka watanzania kuwa wazalendo wa kweli kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye mikoa 19 ya Tanzania kwa kuwafichua wale wote wanaojipenyeza kutaka kusajiliwa kama Raia.

  Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizindua shughuli za Usajili na Utambuzi wa Watu katika Mkoa wa Morogoro Jumamosi katika viwanja vya Shujaa mkoani humo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew Massawe akisoma taarifa ya zoezi la Usajili na Utambuzi  wa Watu kwa mikoa 19 inayoendelea na Usajili; amesema mkoa wa Morogoro unakusudiwa kusajiliwa zaidi ya wananchi 960,000 wenye umri wa miaka 18  na kuendelea. Zoezi ambalo limepangwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,2018.
  “ Mkoa wa Morogoro zoezi litahusisha Wilaya zote isipokuwa Kilombero ambayo ilikuwa Wilaya ya kwanza ya mfan kufanyiwa usajili mwaka 2012 na hivyo idadi kubwa ya wananchi wake tayari wana Vitambulisho vya Taifa na kwasasa wanaosajiliwa ni wale wanaotimiza umri wa miaka 18 na wanaohamia “ asisisitiza
  Aidha ndugu Massawe amemweleza Mhe. Waziri mbali na Usajili Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza matumizi ya Vitambulisho vya Taifa ikiwemo Usajili wa Makampuni unaofanywa na Brella ambao kwa sasa unataka kila anayesajili Kampuni kuwa na Kitambulisho cha Taifa. Huduma nyingine ambazo kwa sasa huwezi kuzipata bila kuwa na Kitambulisho cha Taifa ni upatikanaji wa Hati za kusafiria(Passport), Usajili wa namba za simu na huduma nyingine za kifedha n.k
  Katika hotuba yake Mhe. Waziri amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kudai posho au kuhusisha michango na tozo mbalimbali wakati wa kuwasajili wananchi wakati zoezi hilo ni bure. Amesisitiza Mamlaka  zote za Serikali kuhakikisha zinasisimia na kutoa ushirikiano kwa NIDA kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa kwa wakati wakiwemo Wageni na Wakimbizi kwani shughuli ya usajili kwa sasa inahusisha makundi yote.  Pindi wakati utakapofika kwa wale wote ambao watakuwa hawakusajiliwa watakuwa na cha kujieleza kwanini hawakusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakati Serikali imewekeza fedha nyingi kukamilisha zoezi hili.
  Amesisitiza Usajili Vitambulisho vya Taifa si hiyari ni wajibu wa kila Raia, Mgeni na Mkumbizi kusajiliwa kwa kufuata taratibu, sharia na kanuni za Usajili zinazosimamiwa wakati wa utekelezaji wa Usajili.
  “ Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano chini Mhe. Dr. John Pombe Magufuli ina vipaumbele vingi na mahitaji kwa wananchi ni mengi. Sasa Rais ameacha mambo mengine akaamua kuwekeza kwenye Vitambulisho vya Taifa mradi unaoigharimu Serikali fedha nyingi sana; sasa ole wao ambao hawatasajiliwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi” alisisitiza.
  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe amewataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kusisitiza hatowafumbia macho wale wote watakao husisha zoezi hilo na itikadi za vyama au dini, au kudai rushwa kuwahudumia wananchi pindi wanapojitokeza kwenye vituo vya kusajiliwa.
  Zoezi la Usajili wanachi Vitambulisho vya Taifa linakusudiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kuwa wamesajiliwa na kupata namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) wakati hatua za Uzalishaji zikiendelea sambamba na kuvigawa kwa wananchi.
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe akisoma taarifa kuhusu mkakati wa mkoa kuwasajili wananchi zaidi ya 960,000 wakati wa sherehe za Uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
   Mbunge wa Morogoro Mjini  Mhe. Aziz Abood akitoa salamu kwa wananchi waliofurika kushuhudia sherehe za Uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa Morogoro.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Dr. Mwigulu Lameck Nchemba akihutubia wananchi wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu wenye lengo la Kutoa Vitambulisho vya Taifa Morogoro.

    Mhe. Waziri (Katikati)  akizindua rasmi kuanza kwa Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro. Wengine ni  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven Kebwe (Wa kwanza kulia), Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood (Wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndugu Andrew  Massawe (watatu kulia), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kiyanga ( wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo (wa kwanza kushoto).
   Mhe Waziri wa Mambo ya Nchi pamoja na viongozi wengine wakishuhudia mmoja wa wananchi Bi. Rehema Abdallah akisajiliwa kwa mara ya kwanza na taarifa zake kuingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa NIDA wakati wa sherehe za Uzinduzi Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro.
  Pamoja na kuzindua kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho mkoani Morogoro Waziri Mwigulu pia alizindua kuanza kutolewa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu za Usajili.  Hapa anamkabidhi Bi. Jackline Kayombo kitambulisho chake.

  0 0


  0 0

  Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende, akibadilishana na mawazo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisiwani, Peter, Mwasingi (wa pili kushoto), kada wa CCM, Ebeneza Emmanuel (kulia) na kushoto ni kada wa chama hicho, Willy Kamwela,
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Bonyokwa, Nuhu Mwambuma (kulia), akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Kata ya Bonyokwa na Mjumbe wa Baraza UWT, Tumike Malilo (kushoto), kabla ya kuanza kwa semina hiyo. Katika ni kada wa chama hicho.
  Katibu wa CCM Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende, akibadilishana na mawazo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Bonyokwa, Nuhu Mwambuma.
  Katibu wa CCM Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende, akitoa hotuba yake wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa CCM Kata ya Bonyokwa.
  Washiriki wa semina hiyo.
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Abdulaziz Chuma, akifungua semina elekezi kwa viongozi wa CCM Kata ya Bonyokwa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende.
   Semina ikiendelea.
  Kada wa CCM, Ebeneza Emmanuel akitoa mada katika semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Meza Kuu.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Kata ya Bonyokwa na Mjumbe wa Baraza UWT, Tumike Malilo (kushoto), akiwa ukumbini kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisiwani, Peter, Mwasingi (kushoto), akifuatilia mada katika semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Katibu wa CCM Kata ya Bonyokwa, Mohamed Chende (kushoto), Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisiwani, Peter Mwasingi (kulia) pamoja na kada wa chama hicho, Willy Kamwela, wakiwa katika picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 1514 | 1515 | (Page 1516) | 1517 | 1518 | .... | 1904 | newer