Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1513 | 1514 | (Page 1515) | 1516 | 1517 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila (kushoto), akikwagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa hafla ya kumuaga akistaafu utumishi wa jeshi hilo, Hafla hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila , akipunga mkono wa kwaheri wakati wa hafla ya kumuaga akistaafu utumishi wa jeshi hilo. Hafla hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Gwaride la heshima likipita mbele ya Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila, wakati wa hafla ya kumuaga kamishna msaidizi huyo iliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila (kulia),akipongezwa na maafisa wa jeshi hilo baada ya kustaafu utumishi wa jeshi hilo katika hafla iliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila, akipongezwa na mkewe Yunisi Mwaisabila (kulia), baada ya kustaafu utumishi wa jeshi hilo wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo Cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila (kushoto) akipongezwa na mjukuu wake baada ya kustaafu utumishi wa jeshi hilo wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo Cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Dodoma

  Serikali imeeleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kama zilivyo taasisi nyingine kimefuata taratibu za ujenzi na umiliki wa viwanja vya michezo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni zilizopo.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza leo Mkoani Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa, lililohoji kuhusu viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na Chama hicho.

  “Ni vizuri ikafahamika kwamba mpaka sasa viwanja hivyo vinaendelea kutumika na umma wa watanzania kwa shughuli mbalimbali za kimichezo, kijamii na kiserikali sawa kabisa na Mipango ya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995, Sura ya 4 (i)-(ii)”

  “kwa hiyo kuhusu suala la uporaji wa viwanja hivyo, CCM hakijafanya uporaji wowote kwa kuwa kinamiliki viwanja hivyo kihalali kwa mujibu wa sheria zilizopo hivyo ushiriki wa wananchi wenye mapenzi mema katika ujenzi wa viwanja hivyo hauondoi uhalali wa Chama cha Mapinduzi kumiliki viwanja hivyo”amefafanua Shonza.

  Aidha Naibu Waziri Shonza amesema kuwa, Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1955, sura ya 7(vi) inaeleza wajibu wa Mamlaka ya Serikali za mitaa kushirikiana na wadau kujenga, kulinda na kutunza miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja.

  Akizungumzia kuhusu mpango wa serikali katika kusaidia kukamilisha ujenzi wa uwanja wa chunya Shonza amesema kuwa, ujenzi wa viwanja vya michezo ni jukumu jumuishi ambalo linawapa fursa wadau na wananchi kujenga na kuendeleza miundombinu ya michezo katika maeneo yao kwa manufaa ya jamii.

  Hata hivyo, Mhe. Shonza amepongeza juhudi za wananchi wa Chunya kwa jitihada za kuanza ujenzi wa uwanja wa kisasa wenye thamani ya bilioni 8 huku Halmashauri ya Chunya ikiwa imetenga kiasi cha shilling Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi huo.

  Mhe. Shonza amezidi kufafanua kuwa Serikali katika awamu zote tokea kupatikana kwa uhuru imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza watu binafsi, mashirika na Taasisi kuchangia katika kujenga na kuendeleza viwanja vya michezo nchini.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo Bw. Richard Mkumbo (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (Hawapo Pichani)kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)

  …………………………………………………………………………….
  TAARIFA YA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI
  Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze kuufikishia umma wa Watanzania.
  Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23  sawa na asilimia 42.27 ya madai yote,   na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
  Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.
  MATOKEO YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
  1. Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi  43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81  yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
  1. Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu  11,470
  1. Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
  Kwa matokeo hayo ya uhakiki, mazoezi yaliyofanyika likiwemo  zoezi la kuwaondoa kwenye Mfumo wa malipo ya mshahara (“payroll”) watumishi hewa, vyeti feki na wasio kuwa na sifa na  uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo ambazo bila zoezi  la uhakiki kufanyika zingelipwa wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
  Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.

  0 0

  Inline image 1

  Mkuu wa wilaya ya songea pololeth mgema amemtaka mkandarasi anayejenga miundo mbinu ya shule ya sekondari GUMBIRO iliyopo katika halimashauri ya madaba mkoani ruvuma kumaliza kwa wakati

  Rai hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika halimashauri hiyo HBARI KAMILI HII VIDEO YAKE

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kurejesha mali tisa kati ya 10 za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU) ambazo zilichukuliwa kinyume cha taratibu na kuagiza watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria.

  Amesema mali moja iliyobakia bado inafanyiwa uchunguzi na mali mbili za Chama Kikuu cha Ushirika cha Shinyanga (SHIRECU) nazo pia zimepatikana lakini bado ziko kwenye hatua ya makabidhiano.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Februari 9, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 10 wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amezitaja mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU) zilizorejeshwa kuwa jengo la Nyanza Cooperative Union (1984) Ltd. maarufu kwa jina la “Transport House” au KAUMA House, lililopo katika kiwanja namba 242, Kitalu T, Mtaa wa Stesheni; kiwanda cha kusindika mafuta cha New Era Oil Mill, kilichopo katika eneo la Igogo; na jengo na viwanja vya Ashock Industries vilivyopo eneo la viwanda Igogo.

  Nyingine ni majengo ya kilichokuwa kiwanda cha mkonge na dengu kilichopo eneo la Igogo kwenye kiwanja namba 41 na 79; jengo lililopo katika kiwanja kilichopo Isamilo namba 80, kitalu “D”; jengo lililopo katika kiwanja kilichopo Isamilo namba 110, kitalu “D” na ghala moja katika kiwanja namba 104, kitalu “A” kilichopo eneo la Igogo.

  “Mali nyingine zilizorejeshwa ni jengo moja lililopo mjini Geita katika kiwanja namba 8 Kitalu “K”; jengo moja lililopo mjini Geita, katika kiwanja namba 24, Kitalu “K” na jengo lililopo Isamilo katika kiwanja namba 89 Kitalu “D”,” amesema Waziri Mkuu.

  Kwa upande wa mali za SHIRECU, Waziri Mkuu amezitaja mali zilizopo kwenye hatua ya makabidhiano kuwa ni ghala lililopo Kurasini, Dar es Salaam na nyumba ya ghorofa tatu iliyopo kiwanja namba 1001 “BB” Ilala, jijini Dar es Salaam.

  “Katika kusimamia misingi ya utawala bora na uwajibikaji wa watendaji wa vyama vya ushirika, Serikali inaendelea kufanya uchunguzi maalum kuhusu mikataba mibovu ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU), Chama Kikuu cha Ushirika cha Shinyanga (SHIRECU), Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera (KCU) na Chama Kikuu cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU). Vilevile, tunachunguza kushikiliwa kwa mali za ushirika bila kufuata utaratibu,” amesema.

  Amesema Serikali itaendelea kuviamsha vyama vya ushirika vya msingi na vyama vikuu vilivyosinzia katika mikoa yote ili kujenga ushirika imara na kwamba juhudi na hatua hizo zinazochukuliwa na Serikali, zinalenga kuongeza imani, hamasa na uzalishaji wa mazao na kusimamia masoko yake, na hivyo, kuinua kipato cha wakulima sambamba na kuwapatia fursa ya kujiajiri wenyewe katika sekta ya kilimo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha bunge mjini Dodoma Februari 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati wa mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia) akisaini baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. Wanaoshuhudia ni Mawaziri wa Mazingira kutoka Uganda na Kenya.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa pili kulia) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Bi. Katerina Rangnitt wakiangalia baadhi ya michoro ya katuni za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mradi huo ya katuni unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakimsikiliza mmoja ya wachora katuni za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. 
   Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
  (PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WMU)

  0 0

    Mudumu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kulia,  akiwahudumia  wanakijiji wa Kirando, Wilayani Nkasi katika Madawati ya dharura Mkoani Rukwa Februari 8, 2018


  WAKAZI wa Mkoa wa Rukwa wamesema mpango wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kufungua madawati ya Kuhudumia na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zitolewazo na Shirika hilo umekuwa na faida kubwa.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mahojiano yaliyofanyika kwenye baadhi ya maeneo ya Mkoa huo, wakazi hao wamesema, hivi sasa wanauwezo wakupata huduma kwa haraka na kujua masuala mbalimbali yahusuyo umeme na hata wanapohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme kwenye majumba yao imekuwa rahisi kwani wanaelewa ni hatua gani za kufuata ili kupatiwa huduma hiyo muhimu katika maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
  Uongozi wa TANESCO Mkoa wa Rukwa umefungua jumla ya
  madawati matano ya kusikiliza na kutoa elimu kwa wananchi katika wilaya za Sumbawanga mjini, Nkasi na Laela, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Herini Mhina amesema Februari 8, 2018.
  Katika mahojiano, mkazi wa Kirando, Bi. Veronica Ndenje alisema kupitia madawati hayo yamewawezesha kupata huduma kwa haraka kwani kabla ya utaratibu huo iliwabidi wasafiri umbali  mrefu  kupata huduma za TANESCO.
  “Madawati hayo yamesaidia kupunguza gharama kwani zamani ilibidi kutumia nauli  kuafata huduma wilayani na kupoteza muda mwingi kufuata huduma.” Alisema.
  Kupitia madawati hayo wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali za TANESCO kama vile huduma ya kujua namna gani wanaweza kuunganishiwa umeme kwa mara ya kwanza, huduma za dharura pia kupata elimu mbalimbali zinazohusu umeme na shughuli za TANESCO.
  Naye mkazi mwingine Bw. Mohmmedi Waziri toka Kalambo alisema madawati haya yamesaidia wananchi kuachana na vishoka na matapeli kwani kipindi cha nyuma kabla ya madawati vishoka ambao hujitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa TANESCO kitu ambacho sio kweli walikuwa wakiwatapeli wananchi kwa kuwaahidi wangewasaidia kupatiwa huduma za umeme kwa haraka.
  Madawati hayo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alilolitoa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo mwishoni mwa mwaka jana.
  Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani humo, Mhandisi Mhina, Waziri Dkt. Kalemani aliuagiza uongoizi wa Shirika hilo Mkoani Rukwa kusogeza ofisi zake karibu na wananchi kupitia madawati ya huduma kwa wateja.
  “Madawati haya sio tu yamesaidia kuwasogezea karibu huduma wananchi bali pia yameongeza makusanyo ya fedha zitokanazo na huduma mbalimbali na ikiwa ni pamoja na kutokomeza tatizo la vishoka wanaojifanya ni wafanyakazi wa TANESCO”. Alisema Mhanidsi Mhina.

  Aidha Mhandisi Mhina alisema, Shirika lina mpango wa kuongeza madawati kutoka matano hadi kumi na sita ili kupanua mtandao wa huduma kwa wananchi, katika awamu ya REA awamu ya Tatu ya kuwafikishia umeme wananchi vijijini.
  Wanakijiji wa Kirando, Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa wakiwa kwenye foleni ili wapatiwe huduma kwenye dawati la dharura la huduma kwa wateja.
  Wananchi wakisoma vipeperushi vyenye maelezo ya huduma zitolewazo na Shirika la Umeme Nvchini (TANESCO), kwenye dawati la dharura la huduma kwa wateja Wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa Februari 8, 2018.
  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kising’a tayari kwa ufunguzi wa wodi katika Zahanati ya Kising’a. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Sehemu ya Wakazi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa mgeni Rasmi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda cha Ivori Food & Bevarage cha Iringa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Suhail Esmail Thakore. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya utengenezaji wa viungo katika kampuni ya GBRI inayozalisha bidhaa za mboga mboga zinazojulikana kama Eat Fresh mjini Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa baadhi ya bidhaa za mboga mboga za Eat Fresh na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBRI Bi. Hadija Jabir


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku nne mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania – REGROW.

  Mara baada ya kuwasili mkoani Iringa , Makamu wa Rais alifungua wodi mpya katika Zahanati ya Kising’a ambapo aliwaomba wananchi wote wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ili waweze kunufaika na huduma bora za afya.“niwaombe sana ndugu zangu kila mmoja ahakikishe ana bima ya afya, bima ya afya ndio mkombozi wako, unapopata mavuno yako weka pesa ya bima ya afya”

  Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Wananchi hao kwa mwamko wa kuchangia ujenzi na kutoa eneo lakini pia pongezi kwa umoja wa makampuni ya Asas kwa ufadhili wa shilingi za kitanzania milioni 125.Makamu wa Rais alisema Ilani ya CCM inatuagiza kujenga zahanati katika kila kijiji hivyo ujenzi wa Wodi hii katika Zahanati ya Kising’a ni utekelezaji wa maagizo ya Ilani hiyo.

  Makamu wa Rais aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ukimwi kwani unapoteza nguvu kazi ya Taifa kwani mpaka sasa wastani wa maambukizo umeongezeka mpaka kufikia asiliamia 22.3 kwa mwaka 2016/17 toka asilimia 9.1 mwaka 2011/ 2012.

  Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea kiwanda cha Ivori Food & Bevarage na kujionea namna kiwanda hicho kinavyozalisha bidhaa zake kwa kutumia malighafi kutoka ndani ya nchi ikiwemo Cocoa toka Kyela,Nyanya toka Ilula, mahindi toka kwa wakulima wa Iringa, Rukwa na Ruvuma.

  Aidha Makamu wa Rais alitembelea kampuni ya GBRI Business Solutions inayozalisha bidhaa za mboga mboga za EatFresh na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Hadija Jabir

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Hafla ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 kwa mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu.
    
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
  Baadhi ya Mabalozi hao wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

  0 0

  *Asema rekodi hiyo haijawahi kufikiwa kwa miaka minne

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema akiba ya fedha za kigeni imeongezeka na kufikia dola za Marekani bilioni 5.91 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa kwa takriban miaka minne kuanzia mwaka 2013 hadi 2016.

  Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 9, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 10 wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amesema mbali na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni, pia thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi imekuwa takriban dola za Marekani bilioni 8.695 ikilinganishwa na wastani wa dola bilioni 8.828 kwa miaka mitatu iliyopita.Hata hivyo Waziri Mkuu ameongeza kuwa utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka ni wa kuridhisha ambapo ukusanyaji wa mapato ulifikia Sh. trilioni 12.95 sawa na asilimia 82.8 ya lengo lililopangwa katika kipindi hicho. 

  Amesema matumizi ya fedha hizo yameelekezwa katika kugharamia shughuli mbalimbali za Serikali za kuhudumia wananchi na miradi ya kipaumbele ambayo ni kuanza kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Standard Gauge.Pia kugharamia Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo, kugharamia Mpango wa Ununuzi wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi na utekelezaji wa miradi ya usambazaji maji vijijini na mijini na usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA.

  Miradi mingine ni ununuzi wa meli za abiria na mizigo katika maziwa, ukarabati na ujenzi wa baadhi ya viwanja vya Ndege na kujenga na kuendeleza maeneo ya uwekezaji wa viwanda katika mikoa mbalimbali nchini.“Hakika kwa mafanikio haya tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa uongozi wake mahiri na juhudi anazofanya za kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma muhimu na maendeleo ya haraka.”

  Waziri Mkuu amesema  Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha kuwa inatekeleza ahadi zake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba malengo yaliyowekwa kwa mwaka 2017/2018 yanafikiwa kwa kiwango kikubwa. Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha na kujenga misingi na mifumo imara ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kuwa na mapato endelevu kwa ajili ya kugharamia matumizi yake. 

  Vilevile, kuwa na usimamizi madhubuti wa ukusanyaji wa mapato ambao utasaidia kupanua wigo na kudhibiti ukwepaji wa kodi kupitia urasimishaji wa shughuli za uchumi kwa kuwezesha ukuaji wa biashara katika sekta ndogo na za kati ambazo ndiyo mihimili wa kuzalisha ajira na kukuza uchumi.Akizungumzia kuhusu viashiria mbalimbali vya kiuchumi, Waziri Mkuu amesema vinaonesha kwamba hali ya uchumi ni nzuri na pato la Taifa katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2017 lilikua kwa wastani wa asilimia 6.8. 

  “Hali hii inaashiria kwamba tuna matarajio makubwa ya kufikia lengo la mwaka la ukuaji wa asilimia 7.0. Sekta zilizochangia kwa kiwango kikubwa katika ukuaji huo ni habari na mawasiliano, uchimbaji madini, biashara, ujenzi na uzalishaji viwandani.”


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.
  IJUMAA, FEBRUARI 9, 2018.

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

  Akiwa hospitalini hapo leo (Jumamosi, Februari 10, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa vizuri.

  Pia Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti pacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba Serikali inadhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku

  Kwa upande wake, Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

  Kwa upande wao Maria na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za matibabu wanazozipata na kwa sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kuwajulia hali na kumtakia kheri katika shughuli zake


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, FEBRUARI 10, 2018.

  0 0

  Dawa za kuuwa wadudu wa Pamba.
  Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe (mwenye miwani) akimsikiliza mkulima wa pamba Tindigwe Masuke wa kijiji cha Mbiti alipokuwa akiongelea juu ya uhaba wa dawa, unaowakabili wakulima hao.
  Meneja wa Bodi ya Pamba kanda ya ziwa Jones Bwahama akitoa maelezo kwa katibu mkuu wizara ya kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe namna walivyojipanga kuhakikisha wanasambaza dawa zilizotolewa na selikali ili kukabiliana na wadudu wanaoshambulia zao hilo.
  Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo namna wadudu wanavyoshambulia zao la pamba toka kwa Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi Alfred Chagula, walipotembelea mashamba ya wakulima jana huko mbiti.PICHA NA COSTANTINE MATHIAS  NA COSTANTINE MATHIAS, SIMIYU.

  SERIKALI imewahakikishia wakulima wa Pamba Mkoani Simiyu kuwapatia pembejeo za kilimo ili kukabiliana na wadudu waharibifu ambao wameanza kushambulia zao hilo.

  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe alipofanya ziara ya kukagua mashamba ya wakulima na kujionea changamoto zinazowakabili, ikiwemo mazao yao kushambuliwa na wadudu katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

  ‘’tumeanza kusambaza pembejeo kwa wakulima mkoani Simiyu baada ya kuona mahitaji ya dawa ni makubwa…awali tulipanga kusambaza chupa milioni 1.8, Lakini mahitaji yamekuwa ni makubwa tumeongeza na kufikia chupa milioni 2 ili kusuru zao hilo’’ alisisitiza Katibu Mkuu.

  Aliongeza kuwa wizara ya kilimo imesambaza watalamu 30 nchini ili kusaidiana na wataalamu kilimo ngazi ya mkoa, wilaya na kata katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya dawa, pia namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.

  Mtigumwe aliwataka wataalamu wa kilimo kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ili kuhakikisha dawa zinazosambazwa zinatumika ipasavyo.Tindigwe Masuke mkulima wa Pamba kijiji cha Mbiti alisema kuwa dawa zinazosambazwa na serikali hazitoshelezi mahitaji ya wakulima ambao wahamasika kulima, wamekuwa wakipata kidogokidogo hali inayowafanya kushindwa kuwakabili wadudu wa pamba.

  Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba kanda ya Ziwa, Jones Bwahama alisema kuwa serikali kwa kusirikiana na bodi ya Pamba imeleta timu ya wataalamu saba katika mkoa wa simiyu ili kusaidia na maafisa ugani kuelimisha wakulima jinsi ya matumizi sahihi ya pembejeo.

  Mkoa wa Simiyu unahitaji chupa za dawa 1,810,839 huku kukiwa na jumla ya wakulima wa pamba 309,511 ambao wamelima ekari 602,409 likitarajiwa kuzalisha tani 421,686.3 za pamba kwa wastani wa kilo 700 kwa ekari moja

  0 0


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akikagua moja ya jalada la mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akimhoji Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba sababu za kutomchukulia hatua mmoja wa watumishi mwenye tatizo la cheti licha ya kuwepo taarifa ambazo zinamuwezesha kuchukua hatua.
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao na Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
  Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga (katikati) akipitia orodha ya watumishi waliohakikiwa vyeti vya ufaulu wa kidato cha nne na cha sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika mazungumzo ya kikazi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi, Bw. Clodwing Mtweve alipomtembelea Ofisini kwake Katibu Tawala huyo. Katikati ni Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga akifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.


  0 0

   
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamonga wakati akitoa maelezo kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya uboreshaji Kituo cha Afya Chamwino.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kujionea eneo litakalotumika kuongeza majengo ya Kituo cha Afya Chamwino.  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kuagiza Wakala wa Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya jengo hilo liweze kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.


  Watumishi wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na jengo lao kutokamilika.


  Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu.Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa zilizofanya kukwama kukamilishwa kwa jengo hilo.


  “Jengo hili awali lilikuwa linajengwa na mkandarasi mwingine lakini kutokana na utendaji wake kutoridhisha tuliamua kumpatia Suma JKT na niliagiza jengo likamilike Januari mosi mwaka huu, lakini bado halijakamilika,”alisema


  Amesema sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa.Waziri Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.


  Awali, Mkandarasi kutoka Suma JKT, Mhandisi David Pallangyo amesema ukamilishaji umekwamishwa kutokana na hali ya hewa na pia makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali.“Hapa hii flow ya chini tuliona tuikamilishe lakini hali ya hewa na hizi mvua maji yanajaa hivyo tunafanya tathmini kama tutaweza ni vyema tukaweka water proof,”amesema


  Aidha Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Mhandisi Vilumba Sanga amesema wanafanya tathmini katika jengo hilo kuangalia namna ya kulikamilisha kwa kushirikiana na Suma JKT.“Tunafanya ‘estimate’ ya water proof maana maji yanajaa, hii inatokana na makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali, huyu mkandarasi wa sasa anakutana nayo site,”amesema Sanga


  Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo Cha Afya cha Chamwino Ikulu kuangalia uboreshaji wa kituo hicho ambacho kimeingiziwa Sh.Milioni 500 kwa ajili ya kujenga Wodi ya akina mama na watoto, maabara, Chumba cha Kuhifadhia maiti.


  Hata hivyo, amekuta ujenzi huo haujaanza kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa kuwa dogo na hivyo kuahidi kufanya tathmini halisi kwa kushirikiana na wataalam kuangalia uwezekano wa kujengwa jengo la ghorofa.


  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake leo
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake leo
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) walioshiriki ziara ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI Mha. Mussa Iyombe wakiwa katika chumba cha mikutano Babati leo
  Katika picha ya pamoja ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Misaile Mussa wakisikiliza taarifa ya Halmashauri ya Mji Babati
  Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkoa wa Manyara, Babati Mji na Halmashauri ya Wilaya Babati wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa akiongea nao mjini Babati leo
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipowasili katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Babati kuongea na watumishi leo


  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe amewaasa watendajii wa mkoa wa Manyara kuchukua hatua stahiki zinazohusu masuala ya watumishi ili kupunguza au kuondoa migogoro mkoani Manyara.

  Katibu Mkuu Mhandisi Iyombe ameyasema hayo mjini Babati wakati akiongea na watendaji na watumishi wa Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya Babati kwamba kiwango kikubwa cha migogoro hasa ya ardhi mkoani humo inatokana na baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu wao ipasavyo hali wakizingatia sheria na taratibu za nchi.

  “migogoro mingi inaanzia Sight (sehemu wanazotwaa ardhi ili kupima) kwa kuleta taarifa iliyo na mapungufu na pia zingatieni sheria za ardhi, migogoro ipungue kwa kwa kutenda”
  Pia Mhandisi Iyombe amesema wapo Watendaji ambao wanashindwa kutumia Mamlaka waliyopewa na kuzuia migogoro ya ardhi ambayo inazuilika lakini pia amehoji mbona mipaka ya mikoa na wilaya ipo wazi na kwanini sehemu nyingine za kiutawala, “msilazimishe migogoro ya ardhi kwani tumewapa mamlaka kwa kufanya Ugatuaji wa madaraka (D by D) hivyo amueni”

  Akipokea taarifa ya elimu kuhusu kuwashusha vyeo walimu wakuu zaidi ya 250, ametoa angalizo kuwa mamlaka na Uongozi wa mkoa mzima unapaswa kushauriana katika masuala mbalimbali kama hilo la elimu kabla ya kuchukua maamuzi magumu ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina kwani yanaleta athari kiutendaji na kisaikolojia kwa watumishi. Mhandisi Iyombe amewataka watendaji wa mkoa kuepuka suala la kuwa na Maafisa wengi wanaokaimu hali sheria zipo wazi kwani kufanya hivyo kunapunguza hamasa ya utendaji na kuongeza gharama zisizo za lazima. 

  “suala la kukaimu lisizidi miezi sita ili kuboresha utendaji, kwanini Halmashauri zingine wanakaimu hadi miaka mitatu” amewataka kufuata sheria za kazi ili kupunguza hoja zisizo na msingi.Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Misaile Mussa amesema mkoa wa manyara una upungufu wa watumishi wapatao 6644 kwa mkoa mzima ambapo watumishi 2,076 wapo Halmashauri ya wilaya ya Babati. 

  Lakini pia mkoa unakabiliwa na Maafisa wengi wanaokaimu kuanzia ngazi ya mkoa na Halmashauri za mkoa huo.Naye Mkuu wa wilaya ya Babati, Mhe.Raymond Mushi amesema kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji na hasa ya miundombinu ya kupeleka maji na pia mipaka ya wilaya ya Babati na Monduli, na Babati na Kondoa anaendelea kufuatilia kuona mipaka halisi mahali ilipo.

  Katibu Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Manyara ambapo leo hii ameongea na watumishi hali akisikiliza kero zao na kuzitolea majibu papo hapo na kesho atatembelea miradi ya maendeleo kujionea jinsi inavyotekelezwa
   


  0 0


  Na Jumia Food Tanzania

  Mbali na mwezi Februari kuwa mfupi, kitu kingine kinachoupa umaarufu mwezi huu ni kujawa na shamrasharma za sikukuu ya wapendanao au ‘Valentine’s Day.’ Sikukuu hii huadhimishwa kila ifikapo Februari 14 ya kila mwaka, ambapo shughuli na matukio mbalimbali ambayo huonyesha ishara ya upendo hutawala. 
  Umaarufu wa sikukuu hii umeendelea kushika kasi kote duniani kutokana na uzito wa maana halisi ya neno ‘upendo’ ambalo ndilo hutawala miongoni mwa washerehekeaji.  

  Miongoni mwa matukio maarufu yanayofanyika katika kipindi hiki ni pamoja na watu kuwatumia wapendwa wao kadi zenye jumbe za upendo au mapenzi, kutuma zawadi kama vile maua au chokoleti kwa wapenzi wao, pamoja na kuandaa mitoko kwenye sehemu ambazo zimeandaliwa kwa mandhari ya wapendanao. 

  Ukiachana na shughuli hizo, Jumia Food wamekuandalia orodha ya mambo ambayo unaweza kuyafanya kwa mpendwa/wapendwa wako katika msimu huu. 

  Andika ujumbe mfupi. Unaweza ukaandika ujumbe mfupi wa upendo na kisha ukauweka kwenye mkoba au begi la mpendwa wako ambao ataupata pindi akifika kazini. Hakuna jambo zuri kama kuanza shughuli za asubuhi kama kukutana na ujumbe utakaoufanya moyo wako kujisikia vizuri, kupendwa na kuthaminiwa.
  Tuma kadi, maua au chakula. Ingawa unaweza kuwa sio utamaduni wa watanzania wengi au dhana hii kuonekana kupitwa na wakati, lakini unaweza ukamtumia mpenzi wako kadi nzuri yenye ujumbe wa mapenzi na maua ya kuvutia, au chakula anachokipenda mpaka mahali alipo. 

  Mtembelee ofisini mpenzi/mpendwa wako ofisini. Unaweza ukamshangaza mpendwa wako kwa kumtembelea muda wa mchana, ukiwa na chakula anachokipendelea sana.  
  Panga mtoko kwa kushtukiza. Ili kunogesha siku hii unaweza ukaamua kwenda kwenye hoteli au mgahawa na kuutumia muda wenu vizuri bila ya kumuambia kabla. Inaweza kuwa baada ya kumaliza shughuli zenu za siku nzima.

  Endesha gari mkiwa pamoja. Inawezekana kila mtu hutumia gari lake kwenda na kurudi kazini, lakini unaweza kuitumia siku hii kwa kuamua kumpeleka na kumrudisha. Hii itawapatia fursa ya kutumia muda mwingi mkiwa pamoja.
  Mjazie mafuta gari lake. Kama huwa haufanyi hivi mara kwa mara basi kipindi hiki unaweza ukamshangaza mpenzi wako kwa kumjazia mafuta gari lake ‘full tank.’  

  Fanya jambo zuri kwa mama yake, baba, kaka au dada. Unaweza kwenda mbali zaidi kwa kuwafanyia matendo ya upendo ndugu na jamaa wa mpenzi wako. Kama vile kujumuika kwa pamoja kwa chakula, kulipa karo ya shule au hata kuwanunulia kitu ambacho wazazi wake wanakipendelea.

  Mpikie chakula cha usiku. Ni mara chache wanaume huingia jikoni kuipikia familia au wapenzi wao. Utumie msimu huu kwa kumshangaza mpenzi wako kwa kupika chakula cha jioni ili naye aonje mapishi yako.
  Itumie siku hiyo kwa kuzungumza kuhusiana na mipango ya maisha yenu. Inawezakana huwa mnapata muda mchache wa kuzungumza mustakabali wa maisha yenu au hampati kabisa. Itumie siku hiyo kwa kutulia sehemu tulivu pamoja na kujadili au kutafakari kwa pamoja mwenendo wa maisha yenu.

  Mfulie nguo zake, kama huwa hufanyi hivyo. Hakuna shughuli ambayo watu wengi hawaipendi (hususani wanaume) kama kufua. Endapo mpenzi wako huwa anakufulia mara zote, basi mshangaze siku hiyo kwa kumfulia nguo zake.

  Itenge siku maalum kwa ajili yake, panga kufanya vitu anavyovipendelea. Kuna vitu vingi ambavyo wapenzi huvifanya ambavyo siyo lazima hupendelewa na wote. Unaweza ukaitenga siku hiyo kwa kufanya vitu ambavyo mpenzi wako anavipendelea sana.

  Mchumbie. Inawezekana mmekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini hamkupata fursa ya kufanya jambo hilo kuwa rasmi. Itumie siku hiyo kumchumbia mpenzi wako na kumjulisha kwamba unataka kuishi naye milele.

  Mtambulishe mpenzi wako kwa familia, ndugu, jamaa na rafiki zako. Huchukua muda kidogo mpaka wapenzi wakaamua kutambulishana kwa ndugu zao au watu wa karibu. Kama mmetumia muda wa kutosha na mnapendana kwa dhati, itumieni siku hiyo kutambulishana kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
  Jumia Food kwa upande wao katika kuutambua umuhimu wa msimu huu wa wapendao, wanaendesha kampeni ambayo inawapatia fursa wateja wao kujishindia mtoko uliogharamiwa kwenye mgahawa wa Thai Kani pamoja na fursa ya kulala usiku mmoja bure kwenye hoteli ya Slipway. Ili kuweza kushinda fursa hiyo wewe pamoja na mpenzi wako, agiza chakula kupitia mtandao wao kwa kutumia nenosiri ‘LOVE.’ Mshindi atatangazwa siku moja kabla ya sikukuu ya wapendao, yaani Februari 13. 

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa
   Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
   Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

  0 0


  Na: Sekela Mwasubila - Kondoa

  Mamlaka ya Elimu Tanzania imekabidhi rasmi mradi wa ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa tukio lililofanyika katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.

  Akikabidhi mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima alisema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekae kwani iliyotolewa ni nyingi.

  Aidha aliongeza kuwa lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha kuwa shule inakuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kupata elimu iliyokusudiwa na kuongeza ufaulu kwani miundombinu ya maabara, maktaba na madarasa vyote vitakarabatiwa na kuwa na mwonekano mzuri kwa mwanafunzi kusoma.

  “Tuna imani uongozi wa Halmashauri ya Mji na Bodi ya Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa na hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwenda kinyume na taratibu za manunuzi sababu mradi huu force akaunti ambayo inatumia jamii zaidi” Alisema Bi Graceana

  Akiongea kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mh. Hamza Mafita alisema wanaishukuru serikali kwa kuwaletea fedha zote za mradi kwani fedha hizo zitabakia kwa wananchi wa Kondoa kwani mafundi watanunua vifaa vyote Kondoa na mafundi ni wenyeji wa Kondoa na kuwataka mafundi kumaliza mradi huo kwa wakati na haoni sababu ya kuchelewa ikiwa fedha zote zipo.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Khalifa Kondo akipokea mradi huo alisema kuwa anashukuru kupata mradi huo sababu ingekuwa ni jukumu la Halmashauri kukarabati kwa kutumia mapato ya ndani na kuahidi kuzisimamia fedha hizo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri na Bodi ya shule ili kuhakikisha lengo la mradi linakamilika.

  Mamlaka ya Elimu Tanzania imetoa kiasi zaidi ya bilioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Tanzania ikiwemo Shule ya Wasichana Kondoa ambapo imepewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo.
  Sehemu ya Mabweni yanayoendelea na ukarabati katika shule ya Wasichana Kondoa
  Kaimu Mkurugenzi wa Malmaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo orodha ya vifaa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa. 
  Mafundi wakiendelea na uchimbaji wa shimo la maji machafu ikiwa ni sehemu ya ukarabati wa mfumo wa miundombinu ya maji machafu katika shule ya wasichana Kondoa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Wasichana Kondoa.
  Picha ya Uongozi wa Mamlaka ya Elimu na Halmashauri ya Mji katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Kondoa.

older | 1 | .... | 1513 | 1514 | (Page 1515) | 1516 | 1517 | .... | 1903 | newer