Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu. IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala amesema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa letu,sisi ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki

Hivi karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.Amesema kumekuwapo kwa watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.

Dkt. Anna Makakala amesema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra chanya kwa Taifa lao.Amesema ni vyema jamii kutambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo sahihi, amewasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi," 

Amesisitiza hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa mchakato huo.“Ni vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” amesema Dkt. Makakala.

Amesema kila nchi yenye kuhitaji maendeleo ni muhimu kutumia hati ya kusafiria ya kielektroniki ili kufikia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.“Mabadiliko ya kidunia katika maendeleo yanatuonyesha wazi kuwa Taifa hili limefikia kuwa na hati za kisayansi na kiteknolojia hivyo katika hati mpya,mtu yeyote hataweza kutumia ujanja au kughushi na kutumika kwa matumizi yasiyo sahihi,” amesema Dkt. Makakala.

Amesema anaamini idara hiyo haitashindwa na wachache wanaokubali kutumika kuhujumu mchakato huo kwa maslahi binafsi kwakuwa kushindwa kwa mchakato huo ni kupunguza hadhi ya usalama wa nchi.

“Pasipoti ndio kitu kinachotuwezesha kudhibiti wanaoingia nchini na kutoka hiki ni kitambulisho cha raia sehemu yoyote duniani wenye Pasipoti za Tanzania ni mabalozi wa Tanzania mfumo huu utawezesha kudhibiti ujanja wote unaotumika kutakuwa na cheap na security features nyingi sifa ya Taifa letu dunia imeharibika lazima kufanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa letu,” amesema.

Dk. Anna alisema kufanikiwa kwa mradi huo wa e-Immigration kwa gharama ya dola za Marekani milioni 57 imekuwa mwiba kwa vigogo walioondolewa Uhamiaji na sasa wanahaha kwa aibu wakidai kwamba gharama iliyotajwa ni kwa ajili ya mradi mradi mmoja tu wa e-Pasipoti.

“Ni wajibu wa kila mtanzania kuwa macho na wale wote wanaotumiwa na mafisadi kwa ajili ya kuichafua serikali kwakuwa imezuia na kupambana na uhujumu uliotaka kujitokeza,” amesema.

Amesema hati hizo zitawezesha waliopotelewa na hati zao kutumia mfumo wa kiteknolojia na kupakua app yake hata katika simu ya mkononi, hivyo kutambulika na kupewa msaada haraka kokote duniani.Amesema hati hiyo inaviwango vyote vya ubora wa kimataifa pia itatumika kama kitambulisho kwa nchi za Afrika Mashariki.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

WAZIRI JAFO AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO SERA YA ELIMU BILA MALIPO

$
0
0
     
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Wanafunzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo amewataka Wadau wote wa Elimu pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali  kutekeleza sera ya elimu Bila Malipo. 

Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya shule katika shule ya msingi Uguzi, iliyopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma. 

Vifaa hivyo vilitolewa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Dkt. Ombeni Msuya na Abdala Jacob kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.Amewataka wadau hao wasikate tamaa kuunga mkono Serikali kuhusu Elimu. “Japo changamoto ni nyingi lakini wanafunzi wenye uhitaji maalum wanahitaji msaada wao”. alisisitiza 

Amesema wanafunzi wengi wanakosa fursa ya vitendea kazi kama madaftari na kalamu hivyo ni jambo la  msingi kwa wadau wa elimu kuendelea kusaidia watoto hao na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza sera ya Elimu Bila Malipo.

Waziri Jafo pia alizindua mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.Waziri Jafo amesema ujumbe huo unamhusu mtoto mwenye uhitaji wa kupata elimu na kuwaomba  Watanzania kwa ujumla kuunga mkono jambo hilo.

Amewaomba wadau hao wasichoke na wasikate tamaa kuchangia kwani watoto wengi wamepotea kwa kukosa vitedea kazi hivyo ni vyema kuwaokoa watoto hao na kuwatoa kwenye mazingira hatarishi. "Hivyo ni vyema watanzania kuwaunga mkono wadau wa elimu kwani wameongeza nguvu kazi kwa serikali kuwapatia elimu watoto wenye uhitaji,"amesema

Ameongeza "Japo kuna changamoto kubwa lakini ni vyema kujikita zaidi kusaidia Umma  na kuunga mkono kutatua changamoto za elimu,".Amesema wengine ni yatima hawapati mahitaji maalum ya shule hivyo wakisaidiwa itakua ni jambo la muhimu sana. 

Amewashawishi Watanzania kushirikiana kwa pamoja kusaidia mpango huu ambao utawasaidia watoto wenye mahitaji maalum.

PESA ZA MAENDELEO HAZINA CHAMA-SALUM MWALIMU

$
0
0
 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu akihutubia katika Mkutano wa Wananchi uliofanyika katika Kata ya Kigogo akiomba kura hili aweze kupata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni katika Uchaguzi Mdogo wa Marudio utakaofanyika February 16, 2018
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akumuombea Kura Mgombea Ubunge wa CHADEMA Salum Mwalimu katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Raound abot ya Kigogo .
 Waziri Mkuu Mstaafu, na Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Chadema , Fredrick Sumaye akihutubia Wananchi wa kata ya Kigogo katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Raound abot ya Kigogo.
 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu , akiwa Juu ya gari  na kuwapungia mkono wakazi wa Kigogo mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuomba kura kwa Wananchi
Sehemu ya Wananchi wa kata ya Kigogo waliojitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu.

MZEE MWINYI ASHIRIKI KUPANDA MITI NA ROTARY INTERNATIONAL CLUB JANGWANI SEKONDARI

$
0
0
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa pili kushoto) na Mkewe Esther (wa nne kushoto) pamoja na viongozi wa Rotary Clubs wakimsubiri Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kushiriki nao zoezi la upandaji miti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani Februari 6 2018. Zoezi hilo linaunga mkono kampeni ya mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther Rassin (kulia) wakati District Governor Mteule, Sharmila Bhatt akifanya utambulisho alipowasili kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na District Governor, Kenneth Mugisha wakati Kiongozi wa Rotary Club, Harsh Bhatt akifanya utambulisho alipowasili kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akipungia mkono wananfunzi wa shule ya wasichana ya Jangwani alipowasili shule hapo kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakimkaribisha Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi alipowasili shuleni hapo kushiriki zoezi la kupanda miti. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitumbuiza wageni wakati wa hafla hiyo
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi kupanda miti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia kwake) District Governor, Bwana Kenneth Mugisha (kulia), Mkewe Esther (wa pili kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211. 
District Governor Kenneth Mugisha akipanda mti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia (kulia kwake) ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa pili kulia) na Mke wa Rais Rassin, Esther (kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitumbuiza wageni wakati wa hafla hiyo. 
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakiwakifuatilia matukio katika hafla hiyo
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) akiagana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti kwenye shule hiyo. Katikati ni District Governor, Kenneth Mugisha. 
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin alipowasili kwenye Wodi ya watoto wenye mahitaji maalum iliyodhaminiwa na Rotary Clubs kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (kulia) akitoa maelezo kwa RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) na District Governor, Kenneth Mugisha. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (kulia) akitoa maelezo kwa RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) na District Governor, Kenneth Mugisha walipotembelea majengo mapya ya hospitali hiyo ambayo Rotary Clubs zimechangia ujenzi wake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi wa Rotary Clubs.
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther Rassin wakiwaangalia watoto wagonjwa wanavyojifunza wakati wakiendelea na matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa ziara yake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs, walipotembelea walipotembelea majengo mapya ya hospitali hiyo ambayo Rotary Clubs zimechangia ujenzi wake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi wa Rotary Clubs na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (wa nne kushoto).
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na ujumbe wake wakiondoka baada ya kufanya ziara hospitali ya CCBRT. Anayewasindikiza (wa pili kushoto) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans.

DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA , ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) .Kushoto ni mwenyekiti wa TAHOSA wa halmashauri hiyo Leonard Laurent. Kulia ni Kaimu mkurugezi wa halmashauri hiyo Stewart Makali. picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine MatiroMatiro amewatahadharisha wakuu wa shule za sekondari wilayani humo kutothubutu kuchangisha pesa kwa wazazi na wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya shule na shule kwani ni kwenda kinyume cha agizo la rais John Pombe Magufuli linalokataza michango shuleni.
Matiro ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Februari 7,2018katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2018 cha Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kilichofanyika  katika ukumbi wa Mwalimu House Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu wa shule 27 za sekondari zilizopo katika halmashauri hiyo. 
Aidha aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutumia mapato ya ndani na juhudi za wafadhili au wadau wa elimu kufanikisha mitihani ya wilaya badala ya kuchangisha wazazi na wanafunzi. 
"Naomba mitihani mnayofanya ya Interschool Examination isihusishe michango yoyote kutoka kwa wazazi na wanafunzi, tukihusisha michango tunakuwa tumekwenda kinyume na kanuni, taratibu na matamko yanayotolewa na viongozi wetu”,alisisitiza . 
"Hakikisheni pia pesa za serikali zinatumika kulingana na kanuni na utaratibu uliopangwa,zisipotumika vizuri maana yake mmeshindwa kufanya kazi mtawajibishwa”,alieleza.Mkuu huyo wa wilaya aliwakumbusha kuwa wakuu wa shule ndiyo wasimamizi wakuu wa shule na mambo yanapoharibika wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuchukuliwa hatua. 
“Kwa mwongozo uliopo sasa mkuu wa shule ndiye mdhibiti ubora wa shule wa kwanza, yaani ubora wa shule unakutegemea wewe, ina maana shule yako ikiwa na matatizo msababishi ni wewe na mwalimu mwandamizi wa taaluma, tumieni vizuri vitabu vya mwongozo mlivyopewa, kiongozi cha mwalimu mkuu ili kujikita katika mazingira salama mnapotekeleza majukumu yenu", alisema Matiro. 
Mkuu huyo wa wilaya pia aliwataka wakuu hao wa shule kusimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi na kudhibiti utoro shuleni. 
Matiro aliwataka walimu kujituma katika kazi na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua walimu ambao shule zao kila mara zimekuwa zikifanya vibaya katika matokeo ya mitihani. 
“Mwalimu upo pale kila mwaka wanafunzi wanafeli, wanapata ziro, shule inakuwa ya mwisho halafu mnamuacha tu huyo mwalimu kwanini? tuna walimu wengine pelekeni wakajaribu Labda kuna tatizo linalosababisha hayo maana kuna mtu mwingine kapewa majukumu yanayomzidi uwezo, mwekeni pembeni aingie mwingine tuone mabadiliko”,aliongeza. 
Matiro aliwakumbusha pia wakuu wa shule kuwajengea wanafunzi hulka ya kupenda michezo na kuwapatia elimu ya kujitegemea badala ya kuwapa elimu ya darasani pekee na Kwa upande wake mwenyekiti wa wakuu wa shule za sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Leonard Laurent alisema pamoja na nia njema ya rais Magufuli kuzuia michango shuleni,jamii imelipokea agizo hilo tofauti ambapo wazazi na jamii kwa ujumla hawajishughulishi na chochote katika maendeleo ya shule. 
“Jamii sasa haijishughulishi na chochote,hata pale walipokuwa wameshaazimia wao wenyewe kuchangia gharama za samani (viti na meza),chakula na miundo mbinu kupitia kamati walizounda wenyewe hawashiriki tena”,alieleza. 
Aidha aliwaomba viongozi wa serikali kuzunguka kila kata ili kukutana viongozi wa kata na wenyeviti wa serikali za vijiji ili watoe fasiri sahihi juuu ya nafasi ya ushiriki wa jamii katika kuleta maendeleo ya shule zao. 
Imeandikwa na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatano. Aliwasisitiza kutumia pesa  zinazotolewa na serikali kama inavyotakiwa.
Wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Matiro aliwasisitiza wakuu hao wa shule kuwachukulia hatua watu wanaowapa mimba wanafunzi na kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu madhara ya ndoa na mimba za utotoni. 
Matiro pia aliagiza shule kutunza mazingira kwa kupanda miti na maua sambamba na kuimarisha usafi kwa walimu na wanafunzi 
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti wa wakuu wa shule za sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Leonard Laurent akisoma risala kwa mgeni rasmi katika kikao hicho, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Stewart Makali ambaye ni afisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo akizungumza katika kikao hicho. Alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa viti na meza 3000 katika shule za sekondari.Katibu wa Chama cha Walimu wilaya ya Shinyanga Victoria Laurent akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka walimu hao wakuu kuhakikisha wanajenga vyumba vya kujistiri kwa wanafunzi wa kike. Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Shinyanga Francis Mbonea akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka walimu wakuu kujituma kufanya kazi kwa bidii na kuondoa matokeo yenye sifuri shuleni kwao ili kuonyesha hamasa kwa serikali na hatimaye kushughulikia matatizo yao ikiwemo kuwalipa madeni na kuwapandisha madaraja Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde1 blog

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEKELEZA MWONGOZO WA HUDUMA KWA WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Bw. Abbas Mpunga kabla ya kumkabidhi Bajaji ili kumwezesha mtumishi huyo kutekeleza majukumu yake.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa tukio la kumkabidhi Bajaji kwa mmoja wa watumishi wa ofisi yake
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikabidhi nyaraka za umiliki wa Bajaji kwa Bw. Abbas Mpunga.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikata utepe kabla kumkabidhi Bajaji mmoja wa mtumishi wake Bw. Abbas Mpunga.
Bw. Abbas Mpunga akishuhudiwa na watumishi wenzake akiwa katika Bajaji yake mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Bw. Abas Mpunga akipongezwa na mtumishi mwenzie mara baada ya kukabidhiwa Bajaji na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Bw. Abbas Mpunga akiwa na watumishi wenzake kabla ya kukabidhiwa Bajaji na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) itakayomuwezesha kiutendaji.

MPINA APANGUA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU NAMNA WIZARA YAKE INAVYOPAMBANA KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU NCHINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Injinia Arcard Mutalemwa (Mwenye shati jeupe), kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akikabidhi ripoti ya kazi hiyo jana kwa Waziri Mpina na viongozi wakuu wa Wizara hiyo. Mhe. (Picha na John Mapepele).
Picha ya pamoja baina ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye suti nyeusi na miwani) kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) kushoto kwake ni Injinia Arcard Mutalemwa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Maria Mashingo Katibu Mkuu wa Mifugo, kulia ni Naibu Waziri Abdalah Ulega na Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa Philemoni Wambura
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Injinia Arcard Mutalemwa (aliyesimama), kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akisoma na kuwasilisha ripoti ya kazi hiyo jana kwa Waziri Mpina na Viongozi wakuu wa Wizara hiyo.
Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa Philemoni Wambura akichangia hoja kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kwenye kikao cha kukabidhi taarifa ya kamati ya kufanya tathmini ya uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) jana.(Picha na John Mapepele) 



Na John Mapepele, Dodoma

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepangua hoja zilizotolewa na wabunge kuhusu namna Wizara yake inavyopambana kutokomeza uvuvi haramu ili kunusuru kupotea kabisa kwa samaki na kuchochea kufa kwa viwanda vya samaki na kusababisha kupungua kwa ajira nchini.

Waziri Mpina alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge bungeni Mjini Dodoma ambao walikosoa hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo katika kupambana na uvuvi haramu hususan katika Ziwa Victoria pamoja na kudhitibi utoroshaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi.

“Mimi na Wizara yangu tutahakikisha hili tunalisimamia kwa nguvu zote, hizi ni rasilimali za taifa na haziwezi kugawanwa kwa ukanda, rasilimali hizi zinapashwa kunufaisha nchi nzima kwa hiyo kama Wizara inayosimamia Sheria zilizopitishwa na Bunge hili tutahakikisha kwamba hakuna kabisa uvuvi haramu katika nchi yetu, hakuna mfanyabishara atakayejihusisha na kuuza wala kusambaza nyavu haramu, hakuna kiwanda kitakachochakata samaki wasioruhusiwa, hakuna mtu yoyote atakayevua kwa vyavu haramu wala kufanya biashara haramu ya mazao ya uvuvi ni lazima mali zetu tuzilinde kwa nguvu zote” alisisitiza.

Akifafanua hoja hiyo alisema Wizara yake katika kupambana na suala la uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi inatumia Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009, Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998, na marekebisho yake ya mwaka 2007,Sheria ya Mazingira namba 20 ya Mwaka 2004, Sheria ya Uhujumu Uchumi (Economic and organized crime Act Cap 200 CE 2002 as amended by Act no 3 of 2016) na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994. 

Wabunge hao waliokuwa wakichangia taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ni pamoja na Joseph Msukuma wa Geita Vijijini, Constantine Kanyasu na Geita mjini na Dk Raphael Chegeni wa Busega

Mpina alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Wizara yake samaki aina ya Sangara wanaoruhusiwa kuvuliwa wenye urefu wa kati ya sentimita 50 mpaka 85 wamebaki asilimia 3 samaki wazazi wamebaki asilimia 0.4 samaki wachanga wasioruhusiwa kuvuliwa chini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 kwa mantiki hiyo hatuna samaki wanaofaa kuvuliwa katika Ziwa Victoria.

Alisema Kamati hiyo imezungumzia juu ya viwanda vya samaki kufungwa ambapo kabla uvuvi haramu haujashamiri kulikuwa na viwanda 13 vilivyokuwa na uwezo wa kuchakata tani 1, 065 na kutoa ajira 4,000 katika ukanda wa Ziwa Victoria lakini kutokana na kuendelea na uvuvi haramu vimepungua na kubaki 8 vyenye uwezo wa kuzalisha tani 171 na kusababisha kubaki na ajira 2,000 tu.

Mpina aliongeza kuwa Kamati ya Bunge imetoa msukumo mkubwa kwa Wizara hiyo kupitia katika ukurasa wa 32 wa taarifa yao kwamba Serikali iongeze bidii katika kupambana na uvuvi haramu sambamba na kuhakikisha wale wanaotorosha samaki na mazao yake wanawadhibitiwa vilivyo.

Aidha, Mpina alisema katika operesheni hiyo, maamuzi hayafanywi na mtu mmoja katika kutafsiri mambo mbalimbali ikiwa ya vipimo vya nyavu za ngazi mbili au tatu badala yake timu nzima ya wataalamu inachambua na kuishauri Serikali hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Aliongeza kwamba Kamati hiyo imejuisha Maafisa Uvuvi, Maafisa kutoka Baraza la Mazingira la Taifa(NEMC), Jeshi la Polisi,Ofisi ya Rais, Tamisemi, Idara ya Uvuvi .

“Lakini mheshimiwa Mwenyekiti mambo tuliyoyaona kwenye operesheni hii yanatisha zipo gari za waheshimiwa wabunge tumezikamata na samaki haramu,wapo wenyeviti wa halmashauri ,wapo wenyeviti wa vijiji, madiwani, watendaji wa Serikali tumewasimamisha kazi kwa hiyo katika operesheni hiyo tulipokagua viwanda tukakuta viwanda vyote vinachata samaki wasioruhusiwa, tumekamata viwanda vya nyavu haramu”alisema.

Aidha baadhi ya Wabunge akiwemo Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kwa nyakati tofauti walimtaka Waziri Mpina kutaja hadharani majina ya wabunge hao wanaotuhumiwa kufadhili uvuvi haramu. 

“ Waziri amesema katika shughuli hii ya kutokomeza uvuvi haramu kuna magari ya wabunge yamekamatwa na samaki ambao wamevuliwa kiharamu,kuna wenyeviti wa halmashauri ambao magari yao yamekamatwa na samaki ambao wamevuliwa kiharamu hawa watu ni wabaya wanaangamiza Taifa letu nakuomba mheshimiwa Waziri uwataje watu hawa ili tuwalaani” alisema Serukamba.

Aidha Waziri Mpina alisema kwa sasa timu yake inakamilisha taarifa ya awamu ya kwanza ya operesheni Sangara mwaka 2018 inayoendelea ambayo iko mbioni kumaliza na kwamba ataifikisha mbele ya kamati na baadae taarifa hiyo itaingia bungeni.

Kufuatia mjadala huo,Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu aliwataka wabunge kuacha kumpa taarifa Waziri Mpina kwani tayari ameshaeleza kuwa taarifa ikikamilika ataiwasilisha kwenye kamati. 

“Waziri ameeleza vizuri ,tuhuma za watu amezitaja taarifa inaandaliwa itawasilishwa kwenye muda muafaka end of the story sasa ninyi mnakataa nini hatupigi daku hapa kuanzia sasa hakuna taarifa yoyote mhe Waziri maliza..”alisema Zungu.

Aidha Waziri Mpina alisema Serikali imekamata zaidi ya kilo 133,000 ya samaki aina ya kayabo na dagaa zikitoroshwa kwenda Rwanda, Burundi, Kongo na Kenya, pia wamekamatwa samaki wachanga kilo 73,000 ambazo rasilimali hizi zote za nchi zinachezewa kwa kiasi huku operesheni hiyo ikiwakamata hadi raia wa kigeni kutoka Rwanda, Kenya na Burundi wakiwa ndani ya visiwa wakishiriki uvuvi na kununua samaki jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Pia walikamata viwanda vya mabondo 22 vinafanya biashara lakini vilivyokuwa na leseni halali ni viwili tu hivyo Serikali ikisema inapambana na uvuvi haramu inapambana kweli kweli huku akisisitiza kuwa operesheni hiyo haina mwisho hadi uvuvi haramu utakapomaliza hapa nchini

Kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu Waziri Mpina alisema tayari Serikali imeshapata meli ya kufanya doria kwani ilizoeleka meli hizo zinakuja kuvua na kuondoka huku taifa letu linaachwa halina chochote.

“Tunashindwa kukusanya chochote na ndio maana kwa mara ya kwanza tumekamata meli na kuipiga faini milioni 770 nilitegemea Bunge hili litapongeza jitihada hizi kubwa za Wizara ambazo zinalinda rasilimali hizi leo hii mkakati wa kulinda uvuvi wa bahari kuu tutazikagua meli zote zikiwa zinavua huko huko hakuna mtu atakayeondoka kwenye maji ya Tanzania akiwa amebeba rasilimali za watanzania”alisema. 

Alisema Serikali itaongeza meli mbili za doria katika ili kuhakikisha uvuvi wa bahari kuu pamoja na bahari nzima unalindwa kwa nguvu zote na kuhakikisha kwamba rasilimali nchini mwetu zinanufaisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hataruhusiwa mtu yoyote na niseme Mheshimiwa Mwenyekiti kama mtu atajishughulisha na uvuvi haramu aache mimi Mpina hata Mzee Mpina mwenyewe ninyi doria mkamateni kama anajishughulisha na uvuvi haramu hatuwezi kuongelea kwa maneno mepesi mambo makubwa ya mstakabali wa taifa letu’alisema.

Waziri Mpina alisisitiza timu yake ya doria kufanya kazi kwa weredi kwa kufuata sheria na kutokumwonea mtu yeyote wakati wa operesheni hii. Aidha alisema katika ulinzi wa rasilimali za taifa Serikali ni walinzi tu hivyo mlinzi ukikutwa mlango wa tajiri umevunjwa atakuwa na shida .

“Mimi ni kibarua wenu kazi yangu ni kuhakikisha katika wizara mliyonipa rasilimali zinalindwa kwa nguvu zote na kazi hiyo mimi na wizara yangu tutaifanya usiku na mchana lakini nasema kama kuna hoja ya msingi wabunge wasituhumu kwa ujumla yawezekana kuna mtendaji akakosea katika kuchukua hatua, unasema katika eneo fulani katika kijiji fulani kuna jambo hili na hili limefanyika Mpina lishughulikie hata sasa hivi ukiniletea nitafanyia kazi na kuchukua hatua mara moja ”alisema.

Alisema rasilimali za taifa zimetoroshwa vya kutosha na kwamba Bunge muda wote limekuwa likilia juu ya makusanyo hafifu yatokanayo na uvuvi ambapo Serikali inakusanya wastani wa bilioni 20 tu ukiwaondoa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivyo ni wakati sasa wa Bunge kuisaidia Wizara kuinua sekta hiyo .

Kuhusu Ranchi za Taifa (NARCO) Waziri Mpina alisema Kamati ilishauri Serikali ifanye tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika ranchi hizo unatija ili ije na mapendekezo sahihi ya namna bora ya kuwekeza katika ranchi hizo ambapo alisema tayari Wizara imeshaunda kamati hiyo inayoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mstaafu wa DAWASA, Arcard Mutalemwa.

TANO LADIES MAANDALIZI NA MKAKATI WAO

$
0
0
Katika sehemu ya pili ya kipindi cha Jukwaa Langu Jumatatu hii tumetembelewa na TANO LADIES.
"Wadada" walioamua kuwa sehemu ya msukumo wa maendeleo ya wanawake na mabinti zetu.
Wamezungumzia (pamoja na mambo mengine) nafasi na mchango wao kama Diaspora kwa Tanzania, na pia wanavyopanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake duniani.
Unaweza ona sehemu ya video yao hapa
https://vimeo.com/253461804

JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi na waalikwa wengine kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI NI HAKI YAKO, NI WAJIBU WAKO

TANESCO SUMBAWANGA YAPOKEA JENERETA YA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 10.

$
0
0
  NA SAMIA CHANDE, SUMBAWANGA
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila, Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.

“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.
Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon(wane kushoto), akipatiwa maelezo kuhusu jenereta hiyo na mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba

  Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon (watatu kushoto), akipta maelezo kutoka kwa mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba  kuhusu jenereta ujio wa jenereta yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 10 kwenye kituo hicho.

Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa.
 


JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dodoma.

08/02/2018 Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo
zote zinazotakiwa ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge
waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza
iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo
ilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na wananchi
kupitia mikutano ya hadhara wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto
wao katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa
wakati.

Aidha Waziri huyo alisema kuwa matibabu ya moyo pamoja na magonjwa
mengine yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao
kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao
utawasaidia kupata matibabu katika Hospitali zote nchini ikiwemo JKCI
na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa Taasisi
zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake
binafsi Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi
vizuri katika matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya watanzania
wengi.

“Katika utendaji kazi wa Taasisi hii tunaona juhudi binafsi za
kiongozi ambaye kwa jitihada zake amewatumia marafiki aliosoma nao
na kufanya nao kazi katika nchi mbalimbali kuja nchini kutoa mafunzo
kwa wataalam wetu na huduma za matibabu magumu ya moyo ambayo sisi
peke yetu tusingeweza kuyafanya kutokana na uchanga tulionao”, alisema
Waziri Ummy .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii
Mhe. Peter Serukamba aliomba katika kikao cha Bunge la Bajeti wabunge
wapewe semina kama hiyo ambayo itaenda sambamba na upimaji wa
magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, saratani za matiti na shingo ya
kizazi, tezi dume na kisukari.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
aliwasisitiza wabunge kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu kwa wakati,
kufanya mazoezi na kuepuka kula vyakula ambavyo vitawaepusha kupata
magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Katika semina hiyo ya siku moja mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni
pamoja na Shinikizo la damu na dalili zake na tiba , kiharusi, tezi
dume na wanawake kukoma kwa hedhi kwa wanawake.
 Mbunge wa Lupa Mhe. Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
 Mbunge wa  Bunda mjini  Mhe. Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa  na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam  hao wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye.
 Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu dalili za shinikizo la damu na tiba yake wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.Picha na JKCI

SERIKALI YAANDAA ENEO KWA VIJIJI VILIVYOATHIRIWA NA MVUA MKOANI DODOMA

LUSINDE AIBUKIA MAKUMBUSHO NA KUMNADI MTULIA

MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE

$
0
0


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.

Pia shida za wananchi ni shida zake, matatizo yao ni matatizo yake pia na kuongeza yeye in mtoto wa kimaskini.tulia amesema hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni kwenye uchaguzi huo wa jimbo hilo.Hata hivyo wakati Mtulia akiomba kura  kwa wananchi hao wa Kinondoni, mgombea ubunge wa Chadema Salum Mwalimu naye ameendelea kuomba kura.

Mwalimu amekuwa akitoa Sera mbalimbali zenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo na kwamba anaamini yeye ndio mgombea sahihi ,hivyo wamchague alete maendeleo.Wakati wagombea hao kila mmoja akiomba kura  za wananchi hao ,kwa Mtulia yeye ameendelea kusisitiza changamoto za jimbo hilo anazijua na anao uwezo wa kuzitatua.

"Niliguswa na matatizo yenu ya kubomolewa nyumba nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa nikafanikiwa."Nilipambana kuhakikisha watu waliobomolewa wanapata hifadhi Magomeni. Nimekuja CCM kuhakikisha hilo linatimia," amesema Mtulia. Ameongeza kuwa "Niliacha ubunge, mshahara, posho na kiinua mgongo changu kwa sababu nawajali wana Kinondoni. Ukiwa jiongozi wa upinzani hauwezi kufanya lolote.

"Maendeleo hayapatikani kwa kutukana, kukashifu, matusi. Maendeleo huja kwa ushirikiano na mahusiano mema," amesema.Amefafanua zaidi  ni kweli anampenda Rais,Dk.John Magufuli  na kuuliza ataachaje Rais ambaye anajenga reli ya kisasa, kununua ndege za kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme. Rais mkweli na muwazi.

Ameongeza atashirikiana na Meya na Mkurugenzi kugawa maeneo ya Mabwepande kwa ajili ya wana Kinondoni waliobomolewa nyumba."Mchague Mtulia arudi Bungeni kivingine akiwa Mtekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayoongoza dola," amesema Mtulia.Amesena akishinda atahakikisha vijana wanakopeshwa Pikipiki na akina Mama wanapewa mikopo ya biashara.

"Nikishinda nitahakikisha Zahanati ya Makumbusho inajengwa, fedha zipo."Nikishinda nitahakikisha kiingilio Hospitali ya Mwananyamala nakifuta, Wananchi wanapata Bima za Afya na Wazee wanapewa huduma bora,"amesema Mtulia.Pia atapunguza  mrundikano wa wagonjwa Hospitali ya Mwananyamala kwa kuhakikisha hospitali ya Mabwepande inakamilika ili kupunguza foleni, kujenga Maghorofa Hospitali ya Mwananyamala.

Amewaaambia wananchi wa jimbo hilo atahakikisha kupatikaba kwa njia mpya ya usafiri kutoka Makumbusho Mpaka Muhimbili, Makumbusho mpaka Posta."Tatizo la taka litakuwa bistoria. Nitahakikisha tunajenga kiwanda cha taka pale Mabwepande, pesa zipo."Kwa wale vijana wenye vipaji, nitashirikiana na Msanii Diamond Platnum kuhakikisha tunaunda timu itakayohakikisha inaibua, inakuza na inalinda kazi za Wasanii wa Kinondoni," amesema.

 Ameongeza maji hayatoki mara kwa mara lakini bili inayotoka ni kubwa, hivyo akishinda atakaa meza moja na Waziri na Dawasco kurekebisha hali hii mbovu iwe historia."Nimetoka kule na kujiunga na CCM ili niweze kupata nguvu ya kuwatumikia wakazi wa jimbo la Kinondoni."Nawaombeni sana itakapofika Februari 17 mkanipigie kura za ndiyo. Kumchagua Mtulia ni kuchagua maendeleo," amesema  Mtulia
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni jana jioni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho,Kinondoni jijini Dar. 
Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika kwenye kampeni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho Kinondoni jijini Dar
Baashi ya Wananchi wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni hizo.

PICHA ZA MATUKIO WAZIRI MKUU BUNGENI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Geita Upendo Penezanje ya jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma, Februari 7, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, bungeni mjini Dodoma Februari 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Tatu Mzuka yazidi kuwaneemesha Watanzania,wengi waendelea kujizolea mamilioni

$
0
0


Mwakilishi wa Kampuni ya inayochezesha mchezo wa kubahatisha,TatuMzuka,Kemilembe Mbeikya (katikati),akizungumza mbele ya Wanahabari mapema jana wakati wa kuwatambulisha washindi wa TatuMzuka,ambao kulia ni Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni aliyejishindia million 60 pamoja na Ummy Abraham kutoka Wazo hill, Tegeta alijishindia million 5.
Kemi alisema kuwa Tatu Mzuka jackpot ya wiki iliyopita imetoa jumla million 80 kwa washindi wa nne,wakiwemo wawili pichani na wengine ni Mathew Mtoni kutoka Songea aliyejishindia milioni 10 pamoja na Selemani Mkoko kutoka Nachingwea aliejishindia millioni 5.

Tatu Mzuka hadi leo imetoa billion 14 na kutengenza washindi million 6. Hawa washindi ni thibisho tosha kuwa Tatu Mzuka inabadilisha maisha ya watu.Kama unavyojua, Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda kila lisaa hadi million 6, na sasa hivi kwenye msimu wa Valentine, wewe na mpendanao mnaweza kushinda million kumi kila silku na bado una nafasi ya kushinda million 60 jumapili hii.
Ummy Abraham amabae ni wa Wazo hill, Tegeta jijini Dar Es Salaama akieleza namna alivyojishindia kitita cha shilingi million 5.Amesema kwa sasa fedha hizo zitamsaidia kuendelea kumsadia katika Matibabu ya Mumewe ambaye ni mgonjwa na pia Fedha nyingine amepanga kumaliza ukarabati wa nyumba zake mbili ili ziendelee kumuingizia kipato.Aidha Ummy ameishukuru TatuMzuka kwa kuleta mchezo ambao kwake umekuwa kama mkombozi kwa wakati aliokuwa nao kwa sasa.
Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni jijini Dar,ambaye ni Dereva wa taasisi ya UVCCM alijishindia milioni 60.Abraham ameishukuru Tatu Mzuka kwa kuuleta mchezo huo kwa Wananchi,kwani umekuwa na manufaa makubwa kwa baadhi yao kiasi hata ya kuyabadilisha maisha yao,anasema kwa sasa fedha hizo atazitumia kujiimarisha zaidi kiuchumi .
Mwakilishi wa Kampuni ya inayochezesha mchezo wa kubahatisha,TatuMzuka,Kemilembe Mbeikya (katikati),akiwa na Washindi wa washindi wa TatuMzuka,ambao kulia ni Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni aliyejishindia million 60 pamoja na Ummy Abraham kutoka Wazo hill, Tegeta alijishindia million 5 wakiwa sambamba na mfano wa hundi zao.

Airtel yawazawadia washindi 2,000 wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti

$
0
0
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akionesha moja namba ya washindi wakati wakuchezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intanetiambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB za SMATIKA Yatosha Intaneti. Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na mmoja kati ya washidi wakati Airtel Ilipochezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intanetiambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB. Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar



Kampuni ya simu za mkokoni Airtel Tanzania leo imewazadia washindi 2,000 wa kwanza wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti kwenye droo ambayo imechezesha jijini Dar es Salaam.

Promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ilizunduliwa mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine zikiwepo wakishinda simu za kisasa za smatiphone na moden.Akiongea baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiani Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wateja wa Airtel 2000 wameweza kujishindia bando ya 1GB.

Kama mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti inafanyika kwa uwazi kabisa na washindi. Ni ya promosheni hii ni kutoa shukrani kwa wateja wa Airtel kwa kuonyesha uaminifu wao kwa kuendelea kutumia mtandao bora kabisa hapa nchini, alisema Mmbando.

Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kambambe, alisema Mmbando.

Mmbando aliongeza kuwa promosheni ya Shinda na Yatosha SMATIKA intaneti ilizinduliwa mwanzo mwa wiki na itakuwa ni ya siku 30 huku kukiwa na droo 3 kila wiki – Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Kwa droo za kila siku, wateja 1000 watajishindia bando ya intaneti yenye 1GB kila mmoja wakati kwenye droo kubwa kutakuwa na washindi 10 huku watano wakishinda simu za smatiphone na 5 wakijishindia moden.

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YABOMOA NYUMBA YA SERIKALI

$
0
0
Na Emanuel Madafa-Mbeya 

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imetoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga nyumba ya serikali iliyoamuliwa na mahakama kuu kujengwa, kuibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Afisa habari wa halmashauri hiyo, John Kilua, amesema ofisi kupitia idara ya majengo ilitembelea eneo la nyumba hiyo inayojengwa kwa amri ya mahakama kuu na kubaini changamoto mbalimbali za ujenzi.

Amesema, kutokana na changamoto hizo wahusika wanaojenga nyumba hiyo wametakiwa kuibomoa na kuanza upya kwa kufuata kanuni za ujenzi na kwamba zoezi la kubomolewa kwa jengo hilo la nyumba linatakiwa kufanyika ndani ya siku saba.Nyumba hiyo yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini hapa, ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama
Muonekano wa Nyumba yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini Mbeya , ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya Mbeya. 

Serikali Yahamasisha Kilimo cha Mazao Makuu Matano ya Biashara.

$
0
0
 Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.

"Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu.

Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.

Pia, Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu amesema, Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.

"Baada ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu," alisema Mhe. Majaliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, amesema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.

Hata hivyo amesema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au pori, tathimini itafanyike na baadae watapewa elimu ya kutoingia ndani ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu.

Misitu yote ya Serikali Kuu inahifadhiwa kisheria na mipaka hiyo inaonekana ili kuondoa migogoro na wananchi.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images