Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

SERIKALI YASISITIZA UWAZI SHUGHULI ZA MADINI

$
0
0
Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam Januari 29, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kwenye mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles aliyeambatana na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.

Ujumbe huo ulimtembelea Katibu Mkuu Msanjila kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kwenye Sekta ya Madini ikiwemo suala la Sheria ya Madini, masuala ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) yanayofanywa na kampuni mbalimbali zikiwemo za kutoka nchini Canada na matarajio ya Serikali kwa kampuni (wawekezaji).

Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazofanya shughuli zake nchini zinalazimika kufuata taratibu na sheria za nchi ili kujijengea mazingira rafiki ya utekelezaji wa shughuli husika.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha Taifa kwa ujumla sambamba na wawekezaji na alibainisha kwamba lengo hilo litafikiwa ikiwa kampuni husika zitatekeleza wajibu wake kwa uwazi kulingana na matakwa ya sheria.

“Kampuni zinazojihusisha na shuguli za madini zinapaswa kufanya shughuli zake kwa usahihi na uwazi,” alisisitiza Profesa Msanjila.

Aidha, Profesa Msanjila alisisitiza kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za madini nchini, zinapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwa Wataalam waliopo Serikalini ili kupata mwelekeo sahihi wa dhamira ya Serikali.

“Kampuni zinatakiwa kupata taarifa sahihi kutoka kwa vyanzo sahihi ili kufanya shughuli zake kwa usahihi,” alisisitiza Profesa Msanjila.

Profesa Msanjila vilevile alizungumzia dhamira ya Serikali ya kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa nje ili kukuza uchumi wa Taifa.

“Madini yakiongezwa thamani hapa nchini, faida ni nyingi ikiwemo ajira na pia mapato yataongezeka kwani tutakuwa tumeelewa thamani halisi ya madini husika, kabla hayajasafirishwa,” alisema.

Ili kufikia dhamira hiyo, Profesa Msanjila alisema Serikali ipo kwenye mazungumzo na kampuni zilizoonyesha nia ya kujenga viwanda vya kuyeyusha na kusafisha madini (smelting and refining).

Mbali na hilo, Profesa Msanjila alizungumzia suala la uwezeshaji wachimbaji wadogo wa madini ambapo alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba wananufaika ipasavyo na shughuli zao sambamba na mchango wao kwenye pato la Taifa kuonekana.

Alielezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuwawezesha wachimbaji wadogo ikiwemo uanzishaji wa vituo vya mafunzo vya mfano (centre of excellence) ambavyo alivitaja baadhi yake kuwa ni Kituo cha Tanga, Geita na Mtwara.

Kwa upande wake Balozi Myles alisema ni muhimu Serikali, Wawekezaji na Jamii kwa ujumla kushirikiana na pia kuwa na lengo la wazi la namna ya kunufaika kutokana na Sekta ya Madini.

Naye Davidson aliahidi kuzungumza na kampuni za Canada kuelezea matarajio ya Serikali kwao kwa namna mbalimbali ikiwemo suala la sheria, uwajibikaji kwa jamii, mazingira na michango mbalimbali ya kampuni kwa maendeleo ya jamii.

“Nitawakumbusha kwamba wanawajibika si kwa wanahisa wao peke yake bali pia kwa jamii wanapofanyia shughuli zao,” alisema Davidson.

Mkutano wa Katibu Mkuu wa Madini na Balozi wa Canada nchini ulihudhuriwa na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini akiwemo Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (katikati) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia) na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (kushoto).
 Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Madini na Balozi wa Canada (hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kulia ni Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy. Wengine ni Maafisa kutoa Wizara ya Madini.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia) akimsikiliza Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson (katikati). Kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles (kulia). 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles (katikati). Kulia ni Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini, Profesa Shukrani Manya. Kutoka kushoto ni Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson na Kamishna wa Biashara Ubalozi wa Canada nchini, Anita Kundy.

SERIKALI, MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WAJADILI MPANGO UTEKELEZAJI SERA IDARA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba (wa tatu kulia)akifungua kikao baina ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs ) na Serikali kilicholenga kujadili mpango wa pamoja katika utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kilichofanyika Makao Makuu Dodoma tarehe 30.1.2018.
 Katibu wa kikao cha ushirikiano baina ya Serikali na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Bi. Tausi Mwilima (kulia)akisoma Muhtasari wa kikao kilichopita kwa wajumbe wakati wa kikao cha pamoja moja kilicholenga kujadili mpango shirikishi wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ili kuharakisha Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike(kulia) akiwasilisha taarifa fupi juu ya Mpango wa Kuamsha Ari ya wananchi kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo wakati wa kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali(NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili mpango shiriki na endelevu wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya  Maendeleo ya Jinsia Bi. Slyvia Siriwa(kulia) akiwasilisha mada kuhusu uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi na utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao kati Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Serikali kilicholenga kujadili mpango ushiriki wa utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai(kushoto) akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili utekelezaji shirikishi wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Twaha Kibalula  akiwasilisha mada kuhusu uimarishwaji wa mifumo ya Ustawi na utolewaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mwakilishi wa Shirika la World Vision Bi. Janeth Edison akitoa mrejesho kutoka katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilichofanyika makao Makuu Dodoma kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
  Mwakilishi wa Kigamboni Community Bw. Rashid Kombo(katikati) akitoa mrejesho kutoka katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Serikali kilichokutana mjini Dodoma kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi wa Shirika la REPSSI Bibi Edwick Mapalala akitoa mrejesho kutoka katika shirika lake kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs)na Serikali kilicholenga kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
 Mwakilishi wa Shirika la JSI Bi Victoria Munisi(katikati) akitoa mrejesho kutoka katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya pande hizo mbili kilicholenga kujadili ushirikiano wa pamoja na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili utaratibu bora wa ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeendesha warsha kwa WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

WAVIU washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa,kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

Warsha hiyo ya siku tatu imeanza Jumatatu Januari 29,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja WAVIU Washauri takribani 75 kutoka halmashauri za wilaya za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga, Kahama Mji, Ushetu na Msalala.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma.

“Kupitia warsha hii tutapeana mikakati mbalimbali jinsi ya kuwatafuta wateja waliopotea katika huduma na kujadili namna ya kuboresha zaidi huduma katika vituo vya tiba na matunzo lakini pia kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU Washauri”,alieleza Tesha.

Naye Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya Mwanza, Veronica Joseph aliwasihi watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kujiweka wazi kwani itawasaidia kupata msaada kwa watu wanaowazunguka ikiwemo familia zao.

“Wale ambao hamjapima nawashauri mpime ili mjue afya zenu na ukibainika una maambukizi ya VVU jiweke wazi ili usaidiwe,kujiweka wazi kutakusaidia kuondoa matatizo na utaweza kupata fursa mbalimbali kutoka wafadhili”,alileleza.

Katika hatua nyingine alisema shirika la AGPAHI linatekeleza miradi ya Ukimwi katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,Mwanza, Tanga na Mara kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and Preventation (CDC).
Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya WAVIU Washauri halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Aminael Tesha akielezea malengo ya warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha hiyo, Veronica Joseph ambaye ni Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya Ziwa, akielezea kuhusu umuhimu wa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU na kujiweka wazi.
MVIU Mshauri, Joyce Philimon kutoka mkoani Simiyu ambaye anaishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 1997 akielezea umuhimu wa kujiweka wazi pale unapobaini kuwa umepata maambukizi ya VVU. Kujiweka wazi kwa Joyce kumfanya aishi salama na kwa amani na kupata fursa za kushiriki shughuli mbalimbali kutoka kwa wadau. 
MVIU Mshauri Seleman Habibu kutoka Kahama akielezea namna alivyoweza kuishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 2000 na ana watoto wawili ambao hawana maambukizi ya VVU na mke wake pia hana maambukizi ya VVU.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na VVU katika Manispaa ya Shinyanga,Vedastus Mutangira akizungumza katika warsha hiyo ambapo akiwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
WAVIU Washauri wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yanajiri ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika warsha hiyo,Vedastus Mutangira akitoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi. Aliwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
MVIU Mshauri Neema Anthony kutoka kutoka CTC ya Segese katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly- IRAMBA

KITUO cha Msaada wa sheria kwa Wanawake( WLAC) kimeanza kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili kwa kijinsia na ukeketaji pamoja na madhara yake kwa watoto wa shule za msingi za Nguvumali,Songambele na sekondari ya Ndago wilayani Iramba,Mkoani Singida ambapo katika kipindi cha wiki moja jumla ya wanafunzi 600 kutoka katika shule za msingi na sekondari walinufaika na mafunzo hayo.

Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa sheria na Wanawake (WLAC) Abia Richard aliyasema hayo kwenye mafunzo waliyotoa kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Tarafa ya Ndago,wilayani Iramba.

Aidha Mwanasheria huyo wa WLAC alifafanua kwamba katika kipindi hicho cha wiki moja zaidi ya watu 1000 wameshapatiwa mafunzo hayo ambayo kati ya hao wanafunzi wa darasa la tano mpaka la saba wa shule za msingi na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni 600 na watu wazima ni 500.

Akizungumzia sababu za kwenda kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi,Abia amezitaja kuwa  ni kizazi na taifa la kesho,jambo ambalo endapo wakifahamu madhara yake mapema watakapokuwa wakubwa itakuwa rahisi kuepukananavyo.Kwa mujibu wa Abia kituo cha msaada wa sheria na Wanawake na watoto kikifadhiliwa na The Foundation For Civil Society kimekuwa kikiendesha mradi wake wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa wanawake.

“Kwa hiyo tumefika katika wilaya ya Iramba,kata ya Ndago katika Kijiji cha Zinziligi kwa ajili ya kuongea na wanakijiji wa Zinziligi kujua ni aina gani ya ukatili wa kijinsia ambao unakumbana na wananchi wa Kijiji hicho pamoja na kupanga mkakati ni kwa namna gani wananchi hao wataepukana na ukatili huo”alisisitiza Mwanasheria huyo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndago,Abeli Philipo Shalua alithibitisha kwamba asilimia 85 ya wanawake ndiyo wanaonyanyasika sana kwa waume zao na kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka jana mpaka sasa kuna matukio ya ukatili wa kijinsia 13 waliyofanyiwa wanawake.

Naye Mchungaji wa Kanisa la EAGT Zinziligi,Rejina Matoke huku akinukuu maandiko matakatifu aliweka bayana kuwa kitu kinachouwa nyumba za familia nyingi na kushindwa kuendelea ni tamaa ya uzinzi kwani hivi sasa suala la uzinzi limekamata watu wengi.“Zinziligi imekamatwa na uzinzi nasema ile kweli halafu kuna magonjwa ya kutisha hapa,hata kama leo daktari ataleta kipimo watakaopona ni wachache,idadi kubwa hapa ni taabu tu,watu hawajiheshimu”alisisitiza Mchungaji huyo.
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba wakiwa kwenye viwanja vya mikutano ya Kijiji hicho wakipatiwa mafunzo na Kituo cha Msaada wa sharia kwa wanawake (WLAC) juu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji pamoja na madhara yake.
Bi Esther Kileee (aliyemshikilia mkono ni Afisa mtendaji wa kata ya Ndago) kwanza    akitoa ushuhuda wa kuacha kujishughulisha na vitendo vya ukeketaji baada ya kuokoka na kwamba kabla ya kuokoka alikuwa akinufaika na shughuli hizo kwa kumpatia kipato chake na alaikuwa akiwakeketa wanawake wasiopungua 50 kwa mwezi.
  Mwanasheria wa WLAC,  Abia Richard akiwasilisha mada kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Kata ya Ndago,wilayani Iramba ambapo pamoja na mambo mengine alisema katika kipindi cha wiki moja zaidi ya watu 1000 walipatiwa mafunzo na kati yao,wanafunzi ni 600 na watu wazima ni 500.
 Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard ajiteta jambo na afisa mtendaji wa kata ya Ndago, Abeli Philipo Shaluo.
Igizo linaloashiria mwanaume anayemnyanyasa mkewe kwa kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia.(Picha  zote Na Jumbe Ismailly)

RC MNYETI AMTUMIA MBUNGE OLE MILLYA, SALAMU ZA KUACHA JIMBO LA SIMANJIRO

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro kwenye ziara yake ya siku saba ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza kero zao na kuzungumza nao kwa kutoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa wananchi na viongozi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizindua ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya kidato cha sita ya sekondari Emboreet, Wilaya ya Simanjiro iliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation kwa kuchimba msingi kwa kutumia jembe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (mwenye shati la maua) akimsikiliza Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Peter Kiroiya Toima, juu ya ujenzi wa chuo cha ufundi cha Veta, ambacho kimejengwa na shirika hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, amemtumia salamu mbunge wa Jimbo la Simanjiro James Ole Millya (Chadema) kutumia nafasi hii kuagana na wananchi wake kwani hawezi kushinda tena ubunge wake mwaka 2020.

Mnyeti aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya sekondari Emboreet kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation.

Alisema Ole Millya anapaswa kuanza kupita kwenye vijiji vya jimbo hilo kwa ajili ya kuaga wananchi wake sababu hivi sasa wanataka kuongozwa na mbunge wa CCM.

"Mfikishieni salamu zangu rafiki yangu Ole Millya kwani tulikuwa naye CCM na namuhakikishia hawezi kuwa mbunge wa jimbo la Simanjiro mwaka 2020 kwa sababu CCM italirudisha hivyo aanze kuaga kabla hajaondoka," alisema Mnyeti.

Hata hivyo, Ole Millya alisema Mnyeti ni kijana mwenzake wanayeheshimiana na waliyefahamiana kwa muda mrefu tangu wakiwa UVCCM, hivyo haamini kama maneno hayo yametoka kinywani mwake.

Alisema Simanjiro aliyoikuta wakati anachaguliwa mwaka 2015, ilikuwa imeharibiwa kwa siasa za maji taka, rushwa zinazodhalilisha utu wa watu na uuzaji wa ardhi uliokithiri.

"Kama nia yetu ni maendeleo kwa wananchi tunaowaongoza ni muhimu kushirikiana ili lengo litimie na Mungu akitufikisha mwaka 2020 wananchi waamue nani wa kumpa kura kwenye nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Ole Millya.

Mnyeti alitumia nafasi hiyo kumpigia debe mkuu wa wilaya mstaafu Peter Toima ambaye pia ni Mwenyekiti wa shirika la ECLAT lililowekeza kwenye shule ya sekondari ya kidato cha sita Emboreet.

"Hili jimbo lipo wazi kwani linashikiliwa na upinzani, hivyo ndugu yangu Toima anza kupitapita huku na huku ili uchukue ubunge na mimi nitakuunga mkono kwa asilimia 100 kwani wewe ni mtu wa maendeleo," alisema Mnyeti na kuongeza:

"Wana Simanjiro mkiwa na mtu kama Toima ni sawa na kuwa na wabunge 20 hivyo msimuache kwani yeye hana ubalozi hata wa nyumba 10 lakini amefanya maendeleo mengi, nami nitamuunga mkono kwani siyo mbabaishaji," alisema Mnyeti.

Alisema Toima anapenda kunyanyua jamii yake kielimu kwani ipo nyuma mno ndiyo sababu anapaswa kuungwa mkono na kupongezwa kutokana na mchango mkubwa wa elimu alioutoa kwenye eneo hilo.

Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima alisema shirika hilo lilianza shughuli za ufadhili wilayani humo na kwenye shule ya sekondari Emboreet kwa mwaka 2015 hadi mwaka 2019 wametumia bajeti ya sh2.8 bilioni na mradi ukikamilika baada ya miaka sita zitakuwa zimetumika sh3.5 bilioni.

Toima alisema shule hiyo ya sekondari Emboreet ndiyo pekee wilayani Simanjiro yenye kidato cha sita na kwenye matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka huu shule hiyo imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya.

"Tuliona eneo hili la wafugaji linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu bora ndiyo sababu tukajenga shule hii ambao sasa hivi zaidi ya wanafunzi 200 wanalala kwenye mabweni ikiwemo wanafunzi 40 wa kidato cha sita," alisema.

Alisema wamepanga bajeti ya sh480 milioni, kwa ajili ya ukamilishaji wa chuo cha ufundi stadi Veta ambacho ni pekee kilichopo wilayani humo ili kuwapatia vijana mafunzo ya ufundi.

Alisema hadi kufikia mwezi Octoba mwaka huu, mradi wa chuo hicho cha Veta, utakuwa tayari na utaanza kwa wanafunzi 24 watakaojihusisha na masomo ya ufundi uashi.

NAMNA MAHABUSU,WAFUNGWA WANAVYOTUMIA SEHEMU ZA SIRI KUINGIA NA SIMU, SIGARA GEREZANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

WAMETAFUTA mbinu mbadala! Ndivyo unavyoweza kuelezea kinachoendelea kwenye baadhi ya magereza yaliyopo nchini kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kwa ajili ya kuingia na simu za mkononi pamoja na sigara.

Sheria za magereza kuna baadhi ya vitu vimepigwa marufuku ikiwamo simu ya mkononi, dawa za kulevya, visu ,nondo na sigara lakini baadhi ya mahabusu na wafungwa wamekuwa wakiingia nazo kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Magereza, makao makuu kitengo cha sheria Absalom Mokily ameiamba Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika leo alipokuwa kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria inayoendelea jijini Dar es Salaam kuwa kuna mbinu nyingi wanazozitumia mahabusu na wafungwa kuingia na vitu hivyo.

SEHEMU ZA SIRI ZINATUMIKAJE? IKO HIVI .

Akielezea zaidi kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kuingia na vitu ambavyo vimepigwa marufuku , Mokiry amesema wenye tabia hiyo wamekuwa wakijaza mizigo kupitia njia  za haja kubwa na njia ya mkojo.

Amesema kuwa wanaoingia na vitu hivyo hata askari Magereza wanashindwa kubaini kutokana na utaalamu wanautumia kificha vitu hivyo vilivyopigwa marufuku kuingizwa magerezani.

"Unaweza kuwapekua na usione chochote, hivyo unapomruhusu aondoke, anachokifanya anakwenda chooni na kisha kutoa vitu alivyoficha kwenye  sehemu zake za siri,"ameeleza.

Mokily amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Magereza namba 149 ya mwaka 2003 imezuia baadhi ya vitu kuingizwa magerezani.Ametaja baadhi ya vitu hivyo ni ni silaha, simu, visu, nondo, bangi, tumbaku na simu za mkononi."Ni marufuku kuingia na vitu,"amesema.

Amesema kuwa tabia hiyo si tu kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wa kiume tu bali hata wanawake nao wanatabia hiyo kwa kuchukua vitu hivyo na kuficha sehemu zao za siri.

"Wanawake wenye tabia ya kuficha vitu wanachokifanya ni kukimbilia chooni na kisha huvitoa na baada ya hapo utashangaa kuona wanawasiliana na watu walioko nje kwa kutumia simu ambazo wameingia nazo kwa mtindo huo,"amesema.

Amefafanua kuna watu magerezani wamekuwa wakiingia na kutoka , wengine wazoefu magerezani hasa mahabusu.Wanapokwenda mahakamani inakuwa ndio njia ya wao kupata vitu hivyo na kisha kuingia navyo magarezani.

WASHINDWA KUTHAMINI UTU WAO

Wakati huohuo, Mokiry anasema mfungwa anachukuliwa kama binadamu na kubwa zaidi askari magereza wanathamini sana utu wa watu wote lakini baadhi ya wafungwa na mahabusu wameshindwa kuthamini utu wao hasa wakiwa magerezani.

"Unapawakagua huoni chochote lakini ukienda chooni utagundua wameingia na pakiti za sigara na simu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi.Tunashindwa kuwapekua sana kwani unaweza kuambiwa unadhalilisha utu wa mtu lakini wenyewe wamekuwa wakwanza kutothamini utu wao,"amesema.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Mokiry ameongeza mahabusu au mfungwa atakayekamatwa akiwa na vitu hivyo huchukuliwa hatua za kisheria ikiwamo ya kupelekewa mahakamani na ikitokea kuna mtumishi asiye mwaminifu na anayekiuka kanuni huchukuliwa hatua na ikiwezekana anafukuzwa kazi ikibainika ni kweli amehusika kusaidia kuinga kwa vitu hivyo.

MIMBA GEREZANI

Kwa upande wa Mrakibu wa Magereza, Amina Kavirondo  alipoulizwa kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kupata mimba wakiwa magerezani, amejibu haijawahi kutokea mwanamke akapata ujauzito akiwa gerezani.

"Kinachotokea wapo baadhi ya mahabusu na wafungwa wanaoingia wakiwa na mimba gerezani na hivyo hujifungulia huko huko na kupata watoto,"amesema.

Amefafanua wafungwa na mahabusu wanawake wanaipongia gerezani wanapimwa afya ili kubaini hali zao na kama mjamzito ripoti hupelekwa Makao Makuu ya Magereza na usimamizi wake kuanzia mwanzo hadi mwisho.

"Mfungwa wa kike akibainia ni mjamzito humpokea na kumtunza  ili kuhakikisha anakuwa salama yeye na kiumbe kilicho tumboni mpaka pale atakapojifungua salama,"amesema Kavirondo.
Mrakibu wa Magereza Kitengo cha Sheria, Absalom Mokiry akifafanua mambo mbali mbali juu ya wafungwa na mahabusu waliopo mahakamani ikiwemo kuingiza simu na vitu vilivyokatazwa gerezani kwa kutumia njia zisizostahili.

MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali.

Jengo hilo pamoja na kuendeleza ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na kufunzia na Dk Mengi amesema amelitoa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo yalifuatana na ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko aliyetaka jengo hilo kupewa wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na kimafunzo.

 Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi aliwataka wanawake kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha kiuchumi. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Aliwataka wanawake kuthubutu na kuwa wajasiri katika kuangalia na kuzitumia fursa zilizopo sasa nchini badala ya kuzipita bila kuziona. Aidha Dk Mengi aliwataka wanawake wajiamini na kujihakikishia kwamba wanaweza kujiletea maendeleo, wawe wanyenyekevu katika biashara zao, na wawe na ndoto kubwa ya maendeleo huku wakianza kidogo kidogo badala ya kusubiri mtaji mkubwa. 

Katrika mkutano huo Dk Mengi alitoa ushuhuda wa jinsi yeye alivyoanza biashara zake na kusema alitumia fursa alizoziona kutengeneza dawa ya kung’arisha viatu baada ya kuchukua mkaa Kariakoo na kuusaga na kuchanganya na mafuta. Alisema alitengeneza dawa iliyoitwa ‘Sunshine’ na alivuna mapesa.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.


Aidha alisema kwamba alianzia kutengeneza kalamu ndani ya sebule kabla hajaondoka na kutumia maeneo ya nje kutengeneza kalamu na kasha kuwa na kiwanda kikubwa. Alisema yeye alizaliwa katika umaskini akiishi katika nyumba ya msonge pamoja na wanyama na kuamua kuukataa umaskini. Alisema kilichomsaidia yeye ni kuwa na macho yanayoona Fursa na kuitumia vilivyo kwa kujiamini na kuthubutu. 

Alisema Mungu aliumba kila mtu kuwa namba Moja na ni vyema watu wote wakajiona kuwa namba moja na katika hilo kuthubutu huku wakihakikisha kwamba wanatumia vyema teknolojia iliyopo kwa kufanya matangazo ya biashara zao. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi. Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.

Aliwataka kutumia simu zao kuhakikisha kwamba wanauza na kuzitangaza bidhaa zao huku akiwataka wakue na kuacha kuogopa kuanzisha viwanda. Pia aliwataka kuwa wanyenyekevu katika biashara zao kwani ndio namna bora ya kuendeleza urafiki wa kibiashara kati yao na wadau wanaohitaji huduma au bidhaa zao. 

Alisisitiza utoaji wa bidhaa bora hata kama bidhaa hizo zimelenga kuwasaidia watu maskini na kuwataka kila senti wanayoipata katika biashara kuhakikisha inabaki hukohuko na isichanganywe na matumizi binafsi. Mapema akimkaribisha mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti TWCC, Jacquiline Maleko alipendekeza Chama chake kiwe na ushirikiano na uwakilishi mkubwa kwenye taasisi muhimu za biashara na kuyataka makampuni binafsi nchini yawe yananunua bidhaa za wanachama wao kabla ya kupendelea bidhaa za nje.  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr. Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Maleko pamoja na kumuomba Dk Mengi, kuipatia TWCC jengo lililopo Sabasaba pia aliitaka TPSF (sekta Binafsi) kuhakikisha kwamba inawazungumzia wanawake na kuwapa nafasi katika vikao vya maamuzi. Pia alifafanua kwamba chama hicho kinataka kushirikishwa katika baraza la biashara la kitaifa na mikoani kwa lengo la kutetea wanawake ambao asilimia 50 ya wafanyabiashara nchini ni wao. 

Maleko alisema chama hicho kilichoundwa mwaka 2005 na kwa sasa kikiwa na majukwaa 11 pote nchini, kimelenga kuunganisha nguvu za wanawake katika kuhakikisha wanashika uchumi kwa kutumia fursa zilizopo za nafasi mbalimbali za wanawake zilizowezeshwa kitaratibu, kama asilimia 5 ya mapato ya halamashauri kusaidia makundi maalumu na asilimia 30 ya zabuni ya manunuzi ya serikali kupewa makundi maalumu. Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Louis Accaro akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es Salaam.

Alishauri asilimia hiyo tano kukopeshwa SACCOS yao wanawake ili waweze kukopa na kuendeshea biashara zao, akiamini kwamba fedha hizo zikifikishwa zitawatoa wanawake kiuchumi. Alisema kwa sasa wanawake wafanyabiashara wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya mila, desturi na taratibu za kisheria na hivyo wao ni kazi yao kuhakikisha kwamba sauti ya mwanamke inafika kila mahali ili mazingira ya biashara yaboreshwe. 

Maleko pia alisema kama serikali inaweza kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa kwanini na wao wasipewe ruzuku hiyo ili waweze kuinua uchumi wa taifa. Pia waliomba nafasi katika maeneo ya Taasisi ya viwanda vidogo SIDO kutumiwa na wanawake kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula ambapo pia wanaweza kufundishwa na watalamuwa SIDO wakiwa palepale. Meneja mikopo ya wanawake na uwezeshaji wanawake wa benki ya CRDB nchini, Rehema Shambwe akitoa salamu za benki hiyo kwa wajumbe wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.


Mkutano huo wa mwaka ulifadhiliwa na Mamlaka ya Kodi na Mapato TRA, uilikuwa na wageni wengi wakiwemo watu wa CRDB ambao wanampango wa kuanzisha kituo cha kusaidia wanawake katika masuala ya biashara na ujasiriamali na Trade Mark ambao tayari wanaushirikiano na TWCC. 

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga alisema Asasi yake ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na Chama hicho, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa. Mkataba huo wa mwanzo ulishughulika na mafunzo kwa wajasiriamali katika nyanza zote kuanzia uzalishaji na ufungashaji na matumizi ya hati mbalimbali zinazogusa ujasiriamali.  Mwakilishi wa TRA ambao ndio wamefanikisha kufanyika kwa mkutano huo, Bi. Rose Mahendeke aktioa salamu za TRA kwa wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga akitangaza kuhusiana na hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wa thamani ya shilingi bilioni mbili na TWCC, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akishuhudia Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akiweka kwa maandishi kukabidhi jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam.   Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko (katikati) kibali cha jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wake kuendeleza ujasiriamali. Kulia Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akisalimiana na wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD katika picha ya pamoja na wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Saalaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Noreen Mawalla.

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA

$
0
0

Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.



Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati.

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero
Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO LEO KWA WAZIRI MPINA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Dereva wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.

Na John Mapepele-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali  inakadiliwa kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje ya nchi.

Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo kali.

Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa Desemba 31 Mwaka jana .

Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.

DK. KIGWANGALLA AELEZA HATMA YA WAVAMIZI KATIKA HIFADHI YA BONDE LA MTO KILOMBERO

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2018 amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Uzinduzi wa mfumo huo umefanyika katika ofisi kuu ya uhamiaji Jijini                 Dar es salaam na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti     wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Ali Iddi, na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu    wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi     Mhe. Zubeir Ali Maulid, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano             wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume.
Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Mhe. Rais Magufuli amekagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielektronikia (e-Passport) ambayo pia imeanza kutolewa leo.
Pasipoti mpya za kielektronikia pia zimetolewa kwa viongozi wengine wakuu         wa Serikali, Bunge na Mahakama wa Tanzania Bara na Zanzibar, waliohudhuria uzinduzi huo.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi              Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Idara ya Uhamiaji kwa kufanikisha mradi wa kuweka mfumo wa uhamiaji mtandao na kuanza kutoa pasipoti mpya                ya kielektronikia kwa gharama nafuu ya Shilingi Bilioni 127.2 ikilinganishwa           na makadirio yaliyowekwa awali ya Shilingi Bilioni 400.
“Hapa tumeokoa fedha nyingi za Watanzania, kuna watu walikuwa wamejiandaa kutupiga na kuchukua hizo Shilingi Bilioni 400, lakini tukatumia vyombo vyetu mbalimbali, tukafanya uchunguzi                na tumefanikiwa kutekeleza mradi huu kwa gharama nafuu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na idara ya uhamiaji baada                ya kupokea maelekezo yake ya kutakiwa kufanya mabadiliko makubwa, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kutoa Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kujenga ofisi ya makao makuu ya idara hiyo Mjini Dodoma.
“Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala na timu yako mnafanya kazi nzuri, ndio maana nimewanunulia nyumba 103 kwa ajili ya wafanyakazi kule Dodoma na leo nitawapa fedha nyingine Shilingi Bilioni 10 mkajenge ofisi nzuri ya makao makuu, nyinyi endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kukamata wahamiaji haramu na endeleeni kukusanya mapato vizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mapema akitoa taarifa ya mfumo wa uhamiaji mtandao, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amesema mfumo huo ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja, kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji na kwamba kupitia mfumo huo idara ya uhamiaji inatarajia kutoa pasipoti za kielektronikia (e-Passport), viza           za kielektronikia (e-Visa), vibali vya ukaazi vya kielektronikia (e-Permit) na udhibiti wa mipaka wa kielektronikia (e-Border Management) kwa awamu nne hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu 2018, pamoja na kutoa pasipoti ya kielektronikia ya Afrika Mashariki ya Tanzania.
Balozi wa Ireland hapa nchini Mhe. Paul Sherlock ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha mradi huu na kueleza kuwa mfumo huu wa uhamiaji mtandao ni alama muhimu ya Taifa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Januari, 2018



















































BIMA YA AFYA NHIF WASHIRIKI MAONYESHO WIKI YA SHERIA NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Mfuko wa taifa wa bima ya Afya (NHIF) umeshiriki katika wiki ya sheria kwa kutoa ushauri na kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi waliofika kutembelea mabanda hayo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Katika kuelekea wiki ya sheria Februar Mosi, maonyesho hayo yaliyoanza siku ya Jumapili NHIF waliweza kutoa huduma ya upimaji magonjwa yasiyoambukizwa sambamba na ushauri nasaha kwa wananchi mbalimbali.


Mtaalamu wa Kisukari kutoka Hospitali ya Amana Dr Natalius Kapilima amesema kuwa takribani wananchi wengi waliojitokeza kupata huduma ya vipimo wamekutwa wana uzito mkubwa unaotokana na ulaji usiofaa na kutokufanya mazoezi ya viungo vya mwili


Magonjwa yaliyokuwa yanapimwa katika banda la NHIF ni kisukari, presha (BP), uwiano wa uzito na urefu wa mtu pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) na takribani wananchi 170 waliweza kupata huduma hiyo.


NHIF waliweza kuandikisha wanachama wapya wanaotaka kujiandikisha na mfuko huo wa bima hususani kwa TOTO afya Kadi kwa ajili ya watoto wadogo chini ya miaka 18.


Nesi Catherine Moshi akiwa anachukua kipimo cha damu kutoka kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya Sheria nchini.

Afisa wa Sheria kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Tamasha Magongo akimuelekeza mwananchi aliyefika kwenye band lao alipoleta malalamiko yake


Mfanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Victor Wanzagi akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya Sheria nchini.

Mtaalamu wa Kisukari kutoka Hospitali ya Amana Dr Natalius Kapilima akimsikiliza mwamachi aliyefika kwenye banda la Mfuko wa Taifawa Bima ya Afya (NHIF) katika maonyesho ya wiki ya sheria nchini.

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA MFUMO UHAMIAJI MTANDAO

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI MSANII MKONGWE KING MAJUTO HOSPITALINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama  King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali msanii mkongwe King  Amri Athumani maarufu kama Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018

Wafanyakazi JKC Wapewa Mafunzo na kampuni ya Medtronic ya Mfumo wa Umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG)

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (pace maker) ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram –ECG) kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Medtronic ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG) kwa wafanyakazi wa JKCI yaliyoandaliwa na kampuni hiyo.
Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram –ECG) unavyofanya kazi mwilini wakati wa mafunzo hayo yanayoenda sambamba na vitendo ya siku tano yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
 
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Ahmed Osman (hayupo pichani) kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG) unavyofanya kazi mwilini.Picha na JKCI

ILANI aliyosaini Dk. Kigwangalla waliovamia kiwanja hati namba 4019 kilichopo Njiro, Jijini Arusha

LYATONGA MREMA KUUNGURUMA LEO STENDI YA MABASI MWENGE JIJINI DAR

$
0
0
KATIBU MKUU WA TLP, Mhe Nancy Mrikaria,anapenda kuwataarifu  akina mama na akina baba  kuwa Mhe.Augustino Lyatonga Mrema Mwenyekiti Wa Taifa wa bodi ya Parole na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa TLP atafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika leo tarehe 01/02/2018  muda saa nane kamili mchana (8:00) katika viwanja vya stendi ya zamani ya mwenge.

Mhe Mrema,atamwaga sera na kumnadi mgombea Ubunge wa chama cha Tanzania Labour paty(TLP) Dr. Godfrey Malisa, watasikiliza shida ,KERO na changamoto za wananchi na kutoa suluhisho la matatizo ya wananchi wa jimbo la kinondoni,anawaomba wanakinondoni bila kujali chama kufika kwa wingi tusikilize sera za mgombea wao ,amekumbusha kuwa hii ni fursa ya wanakinondoni kusikiliza na kupima uwezo na sera bora ili kupata muelekeo wa kujua nani anastahili kuchaguliwa na nani anaweza kuwa mwakilishi wao makini na anayeweza kumaliza shida ZAO.

ikumbukwe kuwa UCHAGUZI NI tendo na utashi na itakuwa makosa IKIWA mwananchi atabaki nyumbani akiamini ATAKAYECHUGULIWA NI CHAGUO LA WOTE BILA YEYE BINAFSI KUPIMA NA KUJIRIDHISHA ATAKUWA ANAJINYIMA HAKI YAKE YA MSINGI.
KARIBUNI.
Imetolewa na ofisi ya Katibu MKUU,
chama cha TLP
MAKAO MAKUU - MAGOMENI 
DAR ES SALAAM

WITO WATOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA KUTII SHERIA WAKATI WA UCHAGUZI.

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevikumbusha vyama vya siasa kutii Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchaguzi.

Wito huo umetolewa kupitia barua aliyoviandikia vyama vya siasa yenye kumbukumbu HA.322/362/01/165 ya tarehe 30 Januari, 2018.

“…natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za Ubunge na Udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata. Hivyo, natumia fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika chaguzi hizo, kwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kidemokrasia. 
 
Aidha, naviasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kuheshimu na kufuata sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kanuni zake, kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi” imenukuliwa barua hiyo. 

Jaji Mutungi pia ametoa wito kwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko kujichukulia sheria mkononi, endapo kitashuhudia kwa kuona ama kusikia uvunjifu wa Sheria unaohusu chaguzi zinazofanyika.

Msanii Wastara awatoa hofu watanzania kuhusu matibabu yake

$
0
0







Msanii wa Filamu nchini Bibi. Wastara Issa (wapili kulia waliokaa chini) akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu maandalizi ya safari yake ya matibabu kuelekea Mjini Mumbai walipofanya naye mazungumza leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Msanii wa filamu nchini Bibi. Wastara Issa ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tatizo linalomsumbua na kuweza kumpatia kiwango cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya mguu pamoja na mgongo.

Bibi. Wastara ametoa shukrani hizo jana  Jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa awali ilikua aondoke nchini tarehe 28 mwezi januari mwaka huu kwenda mjini Mumbai kwa ajili ya matibabu lakini kutokana na baadhi ya mipango kutokaa vizuri safari hiyo ilisogezwa hadi jumapili tarehe 4 Februari 2018 ambapo anatarajia kuondoka mida ya jioni na kufika Mumbai mapema alfajiri siku ya jumatatu ambapo ataanza matibabu siku hiyo hiyo.

Bibi. Wastara amesema kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya TMJ pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake yatafanyika katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia matibabu hayo kuchukua takribani wiki tatu na zaidi.

Aidha msanii Wastara Issa ameishukuru wizara inayosimamia tansia ya filamu kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru Waziri mwenye dhamana na tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na watanzania wote kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake.

“Asanteni sana watanzania mmeonyesha moyo wa dhati kwangu kwa muda mrefu sasa, mmekua pamoja nami tangu kipindi cha matibabu ya Saduki hadi sasa, uzito wa neno asante kutoka kwangu leo hauwezi kulipa fadhila kwa dua na michango yenu kwangu, mwenyezi mungu aendelee kuifanya nchi yetu kuwa na amani na upendo” amesema msanii Wastara Issa

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa serikali kupitia bodi ya filamu inashukuru kwa kupata taarifa kamili ya safari ya msanii Wastari Issa ilipofikia kwani bodi ya filamu inapenda kumuona Wastara akiwa katika afya nzuri na kurudi katika hali yake ili aweze kuungana na wanatasnia wenzake kuendeleza tasnia ya filamu nchini.

Bibi. Fissoo amesema kuwa Watanzania wengi wamekua wakiwasiliana na Wastara kwa njia mbalimbali, kumchangia na hata kufika kumuona, hivyo serikali inatambua kuwa msanii Wastara Issa yupo katika maandalizi ya safari ambapo awali alikua asafiri tarehe 28 mwezi januari mwaka 2018 lakini kutokana na taratibu za safari kutokukamili kumepelekea safari hiyo kusogezwa hadi tarehe 4 februari mwaka huu.

MFANYABIASHARA WA NGUAO KARIAKOO AJISHINDIA MILIONI 60 ZA TATUMZUKA

$
0
0

Mwakilishi wa TatuMzuka,Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi Neema  Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,aliyeibuka na kitita cha shilingi milioni 60 za TatuMzuka mwishoni mwa wiki.
Neema  Mtewele (38),ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za akina mama Kariakoo jijini Dar Es Salaam,akifafanua mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda mamilioni hayo ya Mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka.Neema alisema kuwa amekuwa akiucheza muda mrefu mchezo huo bila mafanikio,lakini hakukata tamaa,alindelea kucheza na hatimae akabahatika kuibuka mshindi wa milioni 60.

"Hizi fedha kwakweli matumizi yake makubwa yatakuwa ni kuendeleza na kuunyanyua zaidi mtaji wangu niliokuwa nao kwenye biashara yangu,bado nahitaji kuikuza zaidi biashara yangu",alisema Neema huku akionesha furaha ya wazi kwa kushinda kitita hicho cha milioni 60.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images