Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

0
0
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, limepitisha shilingi bilioni 43.983 za mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akizungumza baada ya kupitishwa bajeti hiyo, alisema vipaumbele vyake ni elimu, afya, maji, kilimo na mifugo. Kamoga alisema bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya vijiji, kata, halmashauri, mkoa, mpango wa pili wa maendeleo ya Taifa na dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

Alisema vipaumbele vingine ni mikakati na sera mbalimbali za kisekta, maelekezo mbalimbali ya viongozi wakuu wa kitaifa, na ahadi ya Rais John Magufuli alizozitoa wakati wa kampeni wilayani Mbulu. Alisema halmashauri hiyo imejikita katika kuongeza mapato ya ndani kwa kuimarisha vyanzo vilivyopo, kubuni vyanzo vipya na kuimarisha mfumo wa kielectroniki. 

"Halmashauri imejikita katika mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa makazi, biashara, viwanda vidogo, maeneo ya malisho ya mifugo, kilimo, hifadhi ya mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji," alisema Kamoga. Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay alipongeza kupitishwa kwa bajeti hiyo ambayo imekidhi kuondoa changamoto mbalimbali. 

Massay alisema bajeti hiyo imegusa sekta mbalimbali ikiwemo elimu ya msingi, sekondari, kilimo, mifugo, ushirika, umwagiliaji, afya na maji. Alisema anatarajia wananchi wa jimbo hilo watapiga hatua kubwa ya maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi ya mpango wa bajeti iliyopishwa na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. 

Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Honoratus Mulokozi alisema bajeti hiyo kabla ya kupitishwa imezingatia sheria namba 9 ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.Mulokozi alisema sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Januari mosi mwaka 2000 inayotaka kufuata sheria, kanuni na taratibu, wakati wa kuandaa bajeti. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza baada ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 43.983 za mwaka wa fedha wa 2018/2019. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akielezea vipaumbele vya mpango wa bajeti ya Halmashauri hiyo. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Joseph Mandoo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 43.983 za mwaka wa fedha wa 2018/2019.

MSEMAJI WA JESHI LA ZIMAMOTO,UOKOAJI NCHINI ATEMBELEA CHANNEL TEN

0
0
 Mwandishi wa habari na mtangazaji mwandamizi wa African Media group Ltd inayosimamia Vyombo vya utangazaji Channel ten na Magic Fm, Bw. Kibwana Dachi akifafanua jambo kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja (katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtangazaji mwandamizi wa Channel Ten na Magic fm, Kibwana Dachi katika studio za Channel Ten, (kushoto) ni Damian Muheya na Nasibu Mgosso (kulia) wakiwa ni Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Mkuu wa Kitengo cha kurusha matangazo Channel Ten, Bw. Abdallah Lugisha akitoa ufafanuzi jinsi mitambo ya kurusha matangazo inavyofanya kazi kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akiwa ameambatana na Maafisa habari wa Jeshi hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018.
 Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja akijibu swali kutoka kwa mtangazaji wa Magic Fm Salma Msangi katika kipindi cha Busati wakati wa ziara yake ya kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 29/01/2018. Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji).
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe

0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halamshauri zote nchini kuhakikisha wanajenga madarasa yenye ubora na Viwango kuondokana na tatizo la baadhi ya Wilaya kuwa na majengo ya udongo na tembe.

Jafo ametoa agizo hilo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya uongozi ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi toka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara yanayondelea katika ukumbi wa Hazina mkoani humo.

"Sitaki kuona madarasa ya udongo, tembe na watoto kusomea nje, hakikisheni matumizi ya mapato ya ndani yanagusa na kujibu matatizo ya wananchi," alisisitiza Jafo.Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha matumizi ya mapato ya ndani katika Halmashauri zao yanatumika katika miradi mbalimbali ya wananchi ikiwemo ujenzi wa madarasa ili kuondokana na uwepo wa madara ya udongo na tembe katika halmashauri zote hapa nchi.

Aidha amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya maamuzi ya haraka mara wanapopokea fedha za miradi ya maendeleo, kauli hii imetokana na baadhi ya wakurugenzi kuwa na uzembe katika kufanya maamuzi hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya zao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Naibu Waziri TAMISEMI Josephat Kandege amesema anaamini Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wataenda kutekeleza yale ambayo watajifunza katika mafunzo hayo."Naamini kwa fursa hii ya mafunzo mtakuwa vinara mara mbili au tatu ya mlivyokuwa katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)," alisema Kandege.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri katika kufanya maamuzi ya kimkakati, kuwapa uwezo wa kuongoza watu na rasilimali nyingine pamoja na kuimarisha uwezo wao katika sifa zao binafsi.

Prof. Semboja amesema awamu hii ya nne ya mafunzo ya Uongozi kwa viongozi hao inakamilisha idadi ya viongozi 324 wa Wilaya na Mamlaka ya Serikali za Mitaa waliotarajiwa kupata mafunzo hayo kwa nchi nzima.

Mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri yalizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 9/5/2017 ambapo yameendeshwa kwa awamu tatu tofauti na awamu hii ya nne ndio awamu ya mwisho inayofunga mafunzo hayo kwa viongozi hao wa Wilaya na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MTEULE DKT. WILBROD,MAAFISA WAKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuzungumza na wanahabaari Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita)  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael Isamuhyo watatu kutoka (kulia) Brigedia Jenerali Aron Robert Lukyaa wapili kutoka (kulia), Kanali Peter Samuel Sameji wa kwanza (kulia).  Wengine katika picha ni Brigedia Jenerali William Ephraim Kivuyo wapili kutoka kushoto na Brigedia Jenerali Elizaphani Lutende Marembo. PICHA NA IKULU

Rais Shein Afungua Warsha ya Uelewa Juu ya Mamlaka ya Viwanda Vidog Vidogo Zanzibar.( SMID )

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulifungua Kongamano la Warsha ya Uelewa Juu ya Mamlaka Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogona Vya Kati (SMIDA) hafla hiyo imewashirikisha Wajasiriamali mbalimbali wa Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.(Pcha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Viwanda na Masoko Zanzibar Juma Ali Juma akizungumza kitaalamu juu ya Uelewa Juu ya Mamlaka ya Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogo Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Tanzania Profesa Sylvester M Mpanduji, akitowa maelezo juu ya umuhimu wa uaznzishaji wa Viwanda Vidogo vidogo kwa wajasiriamali wakatikwa warsha hiyo ilioandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Kikwajuni.
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kulifungua Kongamano hilo.

BAADHI ya Wajasiliamali wa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifufunga Warsha hiyo ililofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.


BAADHI ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Kongamano la Warsha la Kutoa Uelewa Juu ya Mamlaka Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogo na vya Kati (SMIDA) lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Watoa Mada wa Warsha Hiyo baada ya kufunguliwa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, na kulia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali wenye viwanda Zanzibar .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, na kulia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali.Picha na Ikulu)

NAIBU SPIKA AONGOZA KIKAO KAMATI YA UONGOZI MJINI DODOMA.

0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo, kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya uongozi, Mheshimiwa Mwanne Mchemba akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo. kulia ni Mjumbe Mheshimiwa Naghenjwa kaboyoka na kushoto ni Mjumbe pia Mheshimiwa Najma Giga, ​​katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa kumi wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo, kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ajali ya basi la tahmeed kuungua moto.

0
0

Basi la kampuni ya Tahmeed lenye namba za usajili T483 BFL limeungua moto katika Kijiji cha Kabuku wilayani Handeni. 

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, SACP Edward Bukombe alisema basi hilo ambalo lilikuwa na abiria 9 tu kutoka Dar es salam liliungua moto kutokana na hitilafu za umeme. 

Alisema Dereva wa bus hilo Bakari Said (34) alihisi halipo vizuri katika mfumo wa engine akasimamisha gari kisha kuwaomba abiria washuke.

Hata hivyo hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo. Hii ni mara ya pili kwa basi la kampuni hiyo kupata hitilafu Kwenye mfumo wa injini na kuungua moto.

Bodi ya Filamu Yamaliza Mzozo Malipo Filamu ya Utu Wangu

0
0
Na: Mwandishi Wetu
Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.
Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Dilesh Mkurugenzi wa Steps kwa kukubali wito lakini pia kukiri kuwa msanii huyu haja;ipwa stahiki zake na kuamua kumaliza suala hili kwa kumlipa kwa jasho lake Bibi. Sikujua” alisema Mama Fissoo.

Mama Fissoo ameishukuru Kampuni ya Steps kwa hatua ilizochukua na kusema kuwa huo ni muendelezo way ale ambayo walikubaliana huko awali ikiwemo kuwalipa wale wote wanaoidai Kampuni hiyo jambo ambalo wameanza kulitekeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki amesema kuwa wao kama kampuni inayojihusisha na mambo mbalimbali ikiwemo usambazaji wa filamu hawafurahishi na kuona wana ingia migogoro na wasanii kwa hao ndio wateja wao muhimu.

Aidha amesema kuwa shida ambayo ilipelekea kutoka kwa tatizo la malipo kwa msanii huyo ni kitendo cha kuwepo kwa mtu wa kati ambaye kwa kiasi kikubwa bndiye amekuwa akifanya mawasiliano nao tofauti na mhusika mkuu.

Kwa upande wake Msanii Sikujua Mbwembwe ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kusema kuwa ameamini kweli kwamba Awamu ya Tani ni Serikali ya kutetea wanyonge ndiyo maana leo hii haki yake anaenda kuipata kwani ameangahika kwa muda mrefu sana.

“Binafsi nipende kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Ofisi yetu ya Bodi ya Filamu Tanzania, nimeleta malalamiko yangu tumekaa vikao vitatu haki yangu imepatikana keli Mungu ni mwema sana” alisema Bi. Sikujua.

Sikujua Mbwembe ni msaani mwenye ulemavu wa miguu ambaye alitayarisha filamu yake ya Utu Wangu na kuingia mkataba na Kampuni ya Steps Entertainment na kukutana na misukosuko katika malipo yake hata hivyo hii inaonyesha alipita katika njia zisizo sahihi, pamoja na yote hayo baada ya kuwasilisha madai yake katika mamlaka husika suala lake limeshughulikiwa na sasa anataraji kulipwa fedha zake na kunufaika na jasho lake mwenyewe.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo akipitia nyaraka za makubaliano ya mauziano ya Filamu ya Utu Wangu baina ya Mtayarishaji wa Filamu hiyo Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) na Kampuni ya Steps Entertainment wakati wa kikao cha usuluhishi leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu kufuatia mlalamikaji ambaye ni mtayarishaji wa filamu hiyo kufikisha malalamiko ya kutolipwa haki yake tangu mwaka 2015.

 Mwenyekiti wa Kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa Filamu ya Mtu Wangu, Bw. Andrew Makungu ambaye pia ni mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kikao hicho kilichohudhuriwa na uongozi wa Kampuni ya Steps Entertainment pamoja na upande wa mdai ambaye ni Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps  Entertainment Dilesh Solanki akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Madai hayo yanahusi kutolipwa kwa haki za mauziano ya filamu hiyo waliyokubaliana tangu mwaka 2015, hata hivyo suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya Steps kuamua kulipa deni hilo. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Steps ambaye ni mtumishi wa zamani wa Cosota Bw. Yustus Mkinga na kulia ni Mtayarishaji wa Filamu John Lister.
Mwanasheria wa Kampuni ya Steps  Entertainment inayojishughulisha na usambazaji wa Filamu Bw. Yustus Mkinga akifafanua jambo wakati wa kikao cha usuluhishi usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 Kampuni ya Steps iliingia mkataba wa kumiliki filamu hiyo kwa makubaliano ya kulipa sh. 7.5 milioni ambazo mpaka leo hawajalipa hali iliyopelekea madai hayo kufikishwa katika Ofisi za Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kutoka kulia ni Watayarishaji wa Filamu Suleiman Omary (Suleshi) na John Lister, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainments Dilesh Solanki. Mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembwe akiwa ndani ya Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) alipohudhuria kikao cha usuluhishi wa madai yake dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Dilesh Solanki akibadilishani mihutasari ya kikao cha usuluhi wa madai ya msanii wa filamu Bi. Sikujua Mbwembwe ambaye aliilalamikia Steps kutomlipa stahiki yake kufuatia kuwauzia kazi yake ya filamu ya Utu Wangu mara baada ya kumaliza kikao na kufikia muafaka wa Steps kumlipa msanii huyo pesa zake kuanzia tarehe 5 Februari 2018. Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO KATIKA PICHA ETHIOPIA ADIS ABABA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

GLOBAL FUND YATOA TRIONI MOJA KWA TANZANIA KUSAIDIA UKIMWI, TB NA MALARIA

0
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.
Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.



SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh.bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.

"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu" alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.

MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAKUTANA KUJADILI MRADI WA UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI

0
0
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na kutoka Rwanda ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakibadilishana taarifa walizosaini za maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango


Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano kuhusu upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugene Kayihura (kulia) wakiwa katika majadiliano ya pamoja kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu namna ya kupata fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.


Benny Mwaipaja, WFM


Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania na Rwanda wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.

Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.

Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na wajumbe wengine.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.

Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.

Zawadi kem kem promosheni ya Jero Yako ya Zantel.

0
0
 Meneja Masojo wa Zantel, Bi.  Rukia Mtingwa (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kwa Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali  mmoja wa washindi wa wiki wa promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambayo mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki. Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu hutolewa kila wiki.
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi huyo Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali .
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa (kulia) akipiga simu kwa  kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako ya Zantel huku mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuabahatisha Jehud Ngolo (kushoto) akisikiliza pamoja na mfanyakazi mwingine wa Zantel katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Zantel mjini Zanzibar, Mohammed Mussa Baucha (kulia), akikabidhi zawadi ya simu kwa Taimur Mohamed Hussein  mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako, kisiwani humo juzi.

AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, alisema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. “Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita.Alisema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

“Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi jirani pamoja na Jumuia zake.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 30, 2018.

Wajasiliamaji watakiwa kuendelea kutengeneza bidhaa bora kujenga uchumi wa Tanzania

0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akiwa ameshika chaki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeswa mafuta na sabuni walizotengeneza wajasiliamali waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. 
Mjasiliamali Suleiman Nassoro Mohamed ambaye ni Katibu wa BAKWATA akisoma risala wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo.
Baadhi ya wajasiliamali wakipatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo. 
Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.

. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni wakati akifunga mfunzo ya Sido yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wajasiliamali kuendelea kuwa wabunifu kwa kutenegeza bidhaa zenye ubora.

 "Nawaomba wajasiliamali mtengeneze bidhaa zenye ubora na nzuri zitakazowavutia wateja ili mtakapoziuza zitachangia pato la taifa kukua zaidi," alisema Mmuni. Aliongeza kuwa kwa sasa NSSF wamejipanga kurudi kuanza kuwasaidia wajasiliamali ili kukuza kipato chao ili waweze kuendeleza uchumi wa viwanda. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sido- Dar es Salaam, MacDonald Maganga aliwaomba wajasiliamali wote walipo mtaani kuchangamkia mafunzo ya Sido ili yaweze kuwaongezea ujuzi na kuzifanya bidhaa zao zikawa na thamani zaidi.

"Wajasiliamali jitokezeni kokote pale mlipo mchangamkie mafunzo tunayoyatoa maana yamekuwa yakiwajenga zaidi kwa kuongeza ubora wa bidhaa mnazozitengeneza, ukiangalia katika kundi lenu hili kuwa watu wameshaanza kutengeneza bidhaa ila wamekuja kujiongezea ujuzi zaidi jambo ambao ni jema zaidi maana unapopata cheti cha Sido kitakusaidia kuweza kupenya katika soko," alisema Maganga.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA AFYA NCHINI KATIKA KUBORESHA SEKTA HIYO

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Watumishi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Afisa Uuguzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Jane Mazigo akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa akipokea Cheti kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uuguzi na Wakunga, Kulia ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Lena Mfalila
Mwenyekiti aliyeingia kuliongoza Baraza la Uuguzi na Ukunga Abner Mathube akiahidi kuchapa kazi mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Uuguzi na Ukunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.



Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuendelea kutatua changamoto za zinazowakabili watumishi wa Kada ya Afya nchini ikiwemo kuboresha miundombinu inayowazunguka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akizindua Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

“Asilimia 80% ya Kazi zote za kutoa huduma za Afya, zinafanywa na Wauguzi na Wakunga, kwaiyo wakati tunazungumzia kuboresha huduma za, Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzifanyika kazi changamoto hizo ikiwemo suala la watumishi” alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Mh. Ummy aliendelea kusema kwamba, sambamba na changamoto Wauguzi na Wakunga wanazoendelea kukumbana nazo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kutatua changamoto hizo katika kuboresha Huduma za Afya.

Kwa upande mwingine Mh. Ummy alimwagiza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Bw. Abner Mathube Kusimamia mabadiliko ya kanuni za maadili ya Baraza hilo ambazo zimeonekana kupitwa na wakati, hivyo kutofanya kazi kwa ufanisi unaostahili na kushindwa kuendana na wakati huu.

“Nimeelekeza zile kanuni za maadili za mwaka 2007 ni lazima zifanyiwe marekebisho, kwani zimepitwa na wakati, ili tuweze kusimamia taaluma hii vizuri ya Uuguzi na Ukunga.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Pia Mh. Ummy Mwalimu amelitaka Baraza hilo kujizatiti katika kutoa taarifa za Baraza mbele ya umma katika kueleza shughuli za kila mara za Baraza hilo, jambo litakalosaidia kuwafahamisha wananchi juu ya majukumu ya baraza hilo.

“Jamii haipati taarifa kuhusu utendaji kazi wa Baraza, tunatakiwa kuliona Baraza linakuja mbele, angalau kila robo mwaka katika kila kipindi, kukaa kimya kunafanya wananchi waone Baraza halina meno wala maamuzi” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Kwa upande mwingine Mh. Ummy amelitaka Baraza hilo kuwachukulia hatua Waauguzi na Wakunga wanaenda kinyume na maadili ya kazi yao, huku akikemea matumizi ya lugha chafu yanayofanywa na baadhi ya wauguzi wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanaitia doa kada hiyo.

Aidha, Mh. Ummy amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuliongoza Baraza hilo ikiwemo kusimamia wauguzi na wakunga nchini, kusimamia vyuo na vituo vya kutolea huduma za Afya na kuweza kukamilisha jengo la kuwaendeleza Wauguzi na Wakunga, huku akiwataka waamishe kazi zote za Baraza hilo katika jengo hilo lililopo Kibaha.

Mwisho Waziri Ummy aliahidi kuvifungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havitakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa jamii, huku akiwataka Wakurugenzi kujenga tabia ya kuvitembelea vituo hivyo ili kujionea mahitaji ya Vituo hivyo.

“Tutafungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havikidhi vigezo, kwa hili hatutooneana aibu, wala kujali hiki ni kituo cha Afya cha serikali au chabinafsi, wakishindwa kutoa Huduma Bora hatutasita kuvifungia” alimaliza Mh. Ummy Mwalimu.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/18 HAYA HAPA

JPM Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki

0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kesho atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).Mtanda amesema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.

Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti. Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.

Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.

WAZIRI MKUU AREJEA NCHINI AKITOKEA ETHIOPIA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa, wakati akiondoka kurejea Dar es salaam, kushoto ni Mke wa Salim Ahmed salim, Amne Salim.Waziri Mkuu alikua Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiagana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, ndani ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa wanarejea kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, nje ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakati akiwasili kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WABUNGE WATEULE WALA VIAPO BUNGENI LEO

0
0
  Mbunge wa Songea Mjini (CCM) Mhe.Dkt.Damas Daniel Ndumbaro akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson (hayupo pichani)  wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulionza leo Mkoani Dodoma. 
 Mbunge wa  Singida  Kaskazini Mhe.Monko Justine Joseph  akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt.Tulia Ackson wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulionza leo Mkoani Dodoma. 
Mbunge wa Longido Mhe.Dkt.Stephano Lemomo Kiruswa akila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi ulioanza leo Mkoani Dodoma.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO

St Anne Maria yazawadia walioipaisha kitaifa

0
0
SHULE ya St Anne Maria ya Mbezi jijini Dar es Salaam imewazawadia wanafunzi wake waliofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni na kuipaisha kitaifa.

Akizungumza na wakati wa hafla hiyo shuleni hapo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura, alisema shule yake imeweka utaratibu wa kuwazawadia wanafunzi hao vitu mbalimbali kama vitabu na madaftari kama motisha wa kuendelea kufanya vizuri kwenye masomo.

Alisema wanafunzi wa darasa la nne wamefanikiwa kuitoa kimasomaso shule hiyo kwa kuiwezesha kuwa ya pili kiwilaya kati ya shule 90 na ya pili Mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 497.Alisema mbali na kuiwezesha shule hiyo kupata mafanikio hayo kiwilaya na kimkoa pia wanafunzi wote wa darasa la nne wamefanikiwa kupata wastani wa wa ufaulu wa alama A mtihani wa kitaifa.

“Mafanikio yameanzia msingi hadi sekondari maana kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017 shule ilikuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ubungo na ya  tano Mkoa wa Dar es Salaam tulitoa daraja la kwanza wanafunzi 15, daraja la pili 48, daraja la tatu 23 na daraja la nne mmoja tu na hatuna aliyepata 0,” alisema

Alisema hivi karibuni Mkoa wa Dar es Salaam uliipatia Ngao Maalum shule hiyo kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini na kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma.

Alisema shule yake ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, Best Performing Primary School in Tanzania.Alisema ngao hiyo imewapa changamoto ya kuendelea kufundisha kwa bidii ili hatimaye wapate matokeo mazuri zaidi ya mwaka huu.

Alisema ingawa shule yake imefanikiwa kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, lakini hawajabweteka na badala yake wanafanya jitihada za kuwa namba moja.“Kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu tumefanikiwa kuwa wa kwanza Wilaya ya Ubungo, tumekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na tumekuwa wanane kitaifa sasa hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,” alisema 
 Mwalimu Mkuu wa shule ya St Anne Maria Academy ya Mbezi, Gladius Ndyetabura, akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye mtihani wa darasa la nne mwaka 2017 Charles Lusato, ambaye alipata alama A kwenye masomo yote na kuwezesha shule hiyo kuwa ya pili Wilaya ya Ubungo kati ya shule 90 na ya pili pia kwa Mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 497.
Mwalimu Mkuu wa shule ya St Anne Maria ya Mbezi, Gladius Ndyetabura akiwasomea matokeo ya kidato cha pili wanafunzi wa shule hiyo ambayo yanaonyesha wanafunzi 48 kupata daraja la kwanza, 31 daraja la pili, 27 daraja la tatu na 13 daraja la nne na hakuna aliyepata 0.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images