Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 13 | 14 | (Page 15) | 16 | 17 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Eng. Dr. Richard Masika wakiwa wameshikia mfano wa Hundi ya Sh. mil 10 kwa ajili ya Wanafunzi 10 bora . Fedha hizo ni Ahadi ya Mh. Mizengo Peter Pinda wakati wa mahafali ya mwaka 2012. Pembeni kushota ni baadhi ya wanafunzi bora.

  Kushoto ni Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo wakiwa na Mkuu wa Bodi ya Chuo cha ufundi(Katika), Bw. Abraham Nyanda pamoja na Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng.Dkt. Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mahafali ya Chuo.
  Mgeni Rasmi, Mh. Philipo Mulugo akihutubia wahitimu na wageni waalikwa.
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng. Dkt. Richard Masika akitoa Hotuba wakati wa mahafali ya Nne ya Chuo.
  Mkuu wa Bodi ya chuo cha Ufundi Arusha, Bw. Abraham Nyanda alitoa Hotuba wakati wa Mahafali.
  Baadhi ya Wahitimu wakiwa na sura za furaha wakati wa mahafali ya Nne ya Chuo cha Ufundi Arusha.

  0 0

   Mtoto Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda inabidi abadilishiwe damu.

  MATIBABU

  Matibabu ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia.

  Matibabu yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu iligharimu dola 10,000. Mwisho wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na Hanifa kurudishwa Tanzania.

  Ripoti za madaktari India zilipelekwa Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh. milioni 2 kwa mwezi.


  Hakuna pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.


  Hadi sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.

  MICHANGO

  Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi

  Kwa walio Tanzania

  Jokha Khamis Issa
  Akaunti Namba: 041212000428
  People Bank of Zanzibar
  Kwa mawasiliano namba ya simu ni: +255 777 462587

  Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii

  Suleiman Maadini
  Account Number: 15092968
  Sort Code: 30-67-99
  Bank: Lloyds TSB
  Country: United Kingdom
  Kwa mawasiliano na Bwana Maadini: +44 78 18674305

  0 0

  Mashabiki wa soka wa jiji la Arusha, wamepata fursa ya aina yake ya kushuhudia uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka huu wa 2013, katika kiota maarufu cha Babylon Club kilichopo katika eneo la Metropole sambamba na wadau kutoka DStv ambao ndio waonyeshaji wa uhakika wa mashindano haya kupitia Channels zao za SuperSport. Hizi hapa ni picha na maelezo kutoka katika tukio hilo la uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yataendelea mpaka tarehe 10 Februari.
  Wadau wa Babylon Club,Arusha katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa ulioletwa na DStv kupitia channels zao za Super Sports. Experience The Spirit Of Africa...
  Ndani ya Babylon Club, kama unavyoona kuna screens kubwa na nyingi...Zote zimeunganishwa na DStv
  Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu(kulia) akiwa na mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo, wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ndani ya Babylon Club. DStv wanaonyeshaji mashindano hayo Live na katika HD kupitia Channels zao za SuperSport.
  Sales Coordinator wa DStv Kanda ya Kaskazini, Christopher Mbanjo, akiteta jambo la Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo(www.millardayo.com) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ndani ya Babylon Club,Arusha.
  Macho yote kwenye screens mbalimbali zilizotapakaa ndani ya Babylon Club
  Baadhi ya mashabiki waliohudhuria kutizama mechi za ufunguzi za AFCON 2013 wakishuhudia mchezo wa kwanza wa mashindano hayo baina ya South Africa na Cape Verde. Timu hizo zilikwenda sare ya kutofungana.
  Panapo watu haliharibiki jambo.Lakini...endapo lingeharibika basi hawa jamaa walikuwa tayari kabisa kurekebisha au kutatua.Ndani ya Babylon Club,Arusha.
  Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu, akiwa na mdau wa soka ambaye alikiri kwamba yeye huwaamini DStv pekee linapokuja suala la burudani kupitia mchezo wa soka.
  Soccer and Dance....Experience The Spirit Of Africa.

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baad ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu
   Mama Salma Kikwete akiongea na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa  Mhe Begum Taj na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania,wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa,  tayari kuanza ziara ya yake ya kiserikali ya siku tatu.

  0 0  Ndugu zangu,

  Nimepata kuandika, kuwa ni heri kufa na kuacha fikra zinazoishi kuliko kuishi bila kufikiri. Na hakuna njaa mbaya kwenye dunia hii kama njaa ya akili. Kwa mwanadamu, ukiwa na shibe ya akili unaweza kumaliza njaa ya tumbo.
  Ninachoandika hapa kinakutaka msomaji sio tu ufikiri, bali ufikiri kwa bidii. Kwenye sakata hili la gesi ya Mtwara na Lindi ambayo kimsingi ni gesi ya Watanzania nauona mkanganyiko wa fikra. 

  Tulipo sasa ni sawa na mwili uliohangaika kubeba mzigo mkubwa, na kusafiri nao umbali mrefu. Mzigo uko begani. Maungo ya mwili yamechoka sana. Safari imekaribia mwisho. Mzigo ukifika sokoni utauzwa kwa shilingi elfu mbili tu. Kitakachopatikana kitakuwa ni faida ya mwili mzima.

  Ghafla kichwa kinadai mzigo ubebwe kichwani, na si begani. Na faida itakayopatikana sokoni iwe ni ya kichwa tu. Mikono na mabega imegoma kuinua mzigo kuufikisha kichwani. Kichwa kinasema kiko tayari kumlipa mpagazi atakayesaidia kuufikisha mzigo kichwani. 

  Gharama ya kumlipa mpagazi ni shilingi mia tano tu. Hivyo, kazi yote iliyofanya mwili kuufikisha mzigo mpaka hatua hii ya safari ni ya bure tu. Kwanza mwili ulichoka, maungo yakalegea. Lakini ghafla, mwili umeanza kuchemka, umekuwa mgumu. Naam, mwili umegoma. Unakataa mzigo usifike sokoni. 

  Je, kichwa kifanye nini?

  Jibu, hakuna jinsi. Kichwa kina lazima ya kukaa chini na kufanya mazungumzo na mwili. Kuna lazima ya kupatikana muafaka, kwa mazungumzo. Hasara ya kichwa na mwili kuingia kwenye mgogoro ni hasara ya wote; kichwa na mwili.

  Ndugu zangu,
  Kuna ishara mbaya naziona mbele yetu. Maana, sakata hili la gesi ni jambo kubwa na laweza kuwa la hatari pia. Kwenye msafara huu wa hoja ya gesi nayaona mafuta ya taa . Kuna miongoni mwetu, wawe wanasiasa, wanaharakati na hata viongozi wa dini, kwao ya Mtwara na gesi ni ‘ Mtaji katika harakati zao’.

  Hata wale Wabunge waliokuwa wakitetea ongezeko la posho zao bungeni sasa wako mstari wa mbele , eti, kuwashawishi Watanzania wa Mtwara kujitenga na kuunda taifa lao. Kama kweli walikuwa na uchungu na wananchi wa Mtwara na Lindi kwanini hawakugoma kuchukua ongezeko la posho zao bungeni? 
  Ndugu zangu,

  Hii ni nchi yetu. Tunajivunia Tanzania yetu. Kamwe tusizichekee fikra za kihaini za kutaka Watanzania wenzetu wajitenge kutoka kwenye nchi yetu tuliyorithi kutoka kwa mababu zetu. Maana, hatari ya kuzichekea fikra kama hizo ni kupelekea nchi yetu kumegeka vipande vipande. Kuna haja ya haraka kwa Serikali kutoa elimu kwa umma na si vitisho juu ya hoja hii ya gesi. Vinginevyo itatoa nafasi kwa wachache wenye dhamira ya kupotosha umma wakaendelea kuifanya kazi hiyo. 

  Chukulia mfano wa mwanasiasa kijana niliyemsikia kwenye taarifa ya habari ya Star Tv hivi majuzi akitamka; kuwa kama gesi ya Mtwara ikichimbwa na kuuzwa yote, Watanzania milioni 45 , kila mmoja atakuwa akikaa tu, na mwisho wa mwezi analipwa mshahara kwa miaka 200!

  Lakini mwanasiasa yule kijana alishindwa kuwaambia Watanzania wangelipwa kiasi gani kwa mwezi. Huu ni upotoshaji mkubwa na wa hatari na ndio maana ya kuhitajika jitihada za makusudi za kutoa elimu juu ya suala hili la gesi.

  Hoja ya msingi juu ya gesi ya Watanzania iliyogunduliwa Mtwara na Lindi ni kwenye usimamizi na mgawanyo wa faida itakayopatikana kutokana na rasilimali hiyo ili iwanufaishe Watanzania wote, wakiwemo wana Mtwara na Lindi. 
  Kuna hoja za msingi pia juu ya mikataba inayoingiwa baina ya wawekezaji na nchi yetu, kama ina maslahi kwa nchi yetu na watu wake au la. 

  Naam, kwenye msafara huu wa hoja ya gesi kuna mafuta ya taa pia. 

  Tukiyadharau, yana uwezo wa kusababisha mlipuko mkubwa utakaoangamiza nchi yetu. Tumeshaziona ishara.
  Na hili ni Neno La Leo.

  0 0

   Wanachama wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini  katika mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.
   Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
   Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
   Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
  Pichani kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.

  Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
   Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement Sanga wakifatilia jambo kwa  makini ukumbini humo.
   Pichani baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
   Baadhi ya Wazee wa baraza wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo mkuu wa Kihistoria.
   Kocha mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.
   Pichani ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo. 
   Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
  Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.

  0 0

  Mtwara : Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi.

  Kwa wiki ya tatu mfululizo kumekuwa na malumbano kuhusiana na suala la ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Kumekuwa na madai yenye nguvu ya hoja kutoka kwa wananchi wa Mtwara dhidi ya porojo kutoka kwa viongozi wenye dhamana ya kujibu madai haya ya watu wa Mtwara. Watu wa Mtwara kwa umoja wao na kwa kuungwa mkono na viongozi wa dini zote wamekuwa wakitaka Serikali ifikirie upya suala la mradi wa ujenzi wa Bomba la gesi na badala yake kujenga mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara na kusafirisha umeme huo kwenda maeneo mengine ya nchi. Kwenye moja ya maandishi yangu (Serikali iwasikilize watu wa Mtwara) nimeshauri kuwa Taifa liwe na gridi nyingine ya Taifa ambayo itatokana na Gesi tu na ianzie Mtwara.
  Ikumbukwe kwamba katiba ya nchi, ibara ya 9 katika mabano J inataka mamlaka ya dola na vyombo vyake vyote kuhakikisha ya kwamba shughuli zote za kiuchumi zinaendeshwa kwa namna ya kwamba pasiwe mrundikano wa utajiri au shughuli za uzalishaji kwa watu wa chache. Katiba inaendela kwa kuelekeza kwamba uchumi wa nchi upangwe katika uwiano sawia (9, d). Watu wa Mtwara wanatekeleza matakwa haya ya katiba kwa kukataa mrundikano wa shughuli za kiuchumi wa nchi na utajiri wa nchi kua kwenye mikoa michache na hasa mkoa wa Dar-Es-Saalam.
  Serikali imekuwa ikitoa majibu ya porojo na kuwatusi watu wa Mtwara na kama ilivyozoeleka Rais Jakaya Kikwete na Mawaziri wake wamekuwa wakisema suala la Mtwara linatumika na wanasiasa kujitafutia umaarufu. Inasikitisha sana kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaambia mabalozi wa nchi za kigeni waliopo hapa nchini kuwa yanayoendelea mkoani Mtwara yanachochewa na Wanasiasa tuliosimama na wananchi wanaodai haki ya kufaidi utajiri wa nchi yetu. Rais Kikwete na Mawaziri wake wameshindwa kabisa kuonyesha uongozi katika suala hili na hatimaye kuhatarisha umoja wa kitaifa.
  Kwa udhaifu wa serikali na tabia ya kutafuta mchawi badala ya kutatua tatizo la msingi, wananchi wameendelea kukutana na hata wengine sasa kuanza kusambaza ujumbe wa kukata kipande cha nchi na kuanzisha Jamhuri ya Kusini. Nimeona kwenye mabango ya mkutano wa hadhara uliofanyika 19/1/2013 wananchi wakibeba mabango yanayoaishiria kuchoka kuwa sehemu ya Tanzania na kuanzisha Jamhuri ya Makonde kuanzia jiwe la Mzungu wilayani Kilwa mpaka mto Ruvuma. Haya yanatoka na kiburi cha Serikali kujishusha na kuwasikiliza wananchi wanao dai haki yao ya kikatiba.

  Ni Serikali iliyokosa uhalali wa kutawala inayoweza kudharau hisia hizi za wananchi. Serikali ielewe kwamba kamwe haitaweza kulinda kila nchi ya bomba hili iwapo italijenga kwa nguvu. Badala ya kuzungumza na vyombo vya habari Serikali ifanye mazungumzo na wananchi wa Mtwara na kukubaliana na matakwa yao. Kitendo cha Serikali kung’ang’ania msimamo wake dhidi ya watu wa mtwara ni kitendo kinacho weza kuipasua nchi na hivyo kwenda kinyume na masharti ya katiba ibara ya 28 ambayo inasema: “kila raia ana wajibu wa kulinda uhuru wa nchi, uhuru mamlaka na umoja wa taifa.”ibara ya 28, 1.
  Inawezekana Serikali inaogopa kuvunja makubaliano na Wachina ya mkopo wa dola za kimarekani 1.2 bilioni ambao imeuingia bila hata kushirikisha Bunge. Inawezekana Serikali na hasa watendaji wa Serikali waliojadili mkopo huu wameshapata chao na hivyo kuogopa kusikiliza madai halali ya wananchi. Lakini yote hayo hayawezi kuwa zaidi ya Umoja wa nchi yetu. Hatuwezi kukubali nchi yetu ipasuke vipande vipande kwa sababu tu ya kulinda mkataba wa bilioni 1.2 tuliokopa China, ambayo serikali inang’ang’ania.
  Tunafahamu kwamba ubalozi wa China umeandika barua serikalini kuwaondoa raia wa China waliopo Mtwara kwa hofu ya maisha yao. Serikali inaficha ukweli huu kama ilivyoficha ukweli kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini bwana George Simbachawene alifukuzwa na wananchi wa Mtwara alipokwenda hivi majuzi. Serikali itaficha ukweli mpaka lini? Lazima tupate majawabu.
  Kwanza Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa Bomba hili. Kamati ya Bunge ya POAC ilipokuwa inapitia mahesabu ya TPDC iliomba mkataba na kwa mshangao mkubwa wabunge wakaambiwa Mkataba haupo TPDC bali upo Wizarani. Kwa nini Mkataba huu wa matrilioni ya Fedha unafichwa? Mkataba huu ulisainiwa pamoja mikataba mingine 2, mmoja wa kujenga nyumba za wanajeshi wa thamani ya dola za kimarekani 400 milioni na mwingine wa mawasiliano jeshini wa dola za kimarekani 110 milioni, na mikataba yote mitatu imesainiwa kimya kimya bila kushirikisha wananchi kupitia Bunge. Lazima mikataba yote hii iwekwe wazi.
  Pili, Mkataba huu uchunguzwe kama unalingana na thamani ya fedha maana kwa utafiti wa awali inaonyesha kuwa bei ya ujenzi wa bomba imepandishwa maradufu. Wastan wa kujenga bomba la gesi duniani ni dola za kimarekani 1.2 milioni kwa maili moja. Mradi huu wa Tanzania utagharimu dola za kimarekani 2.2 milioni kwa kilomita moja (maili 1 ni sawa na kilomita 1.6).
  Tatu, Serikali ibadilishe Mkataba huu kuwa wa mkopo wa kujenga Mitambo ya kufua umeme Mtwara na ujenzi wa Msongo wa Umeme kama gridi ya pili ya Taifa. Kwa sasa Tanzania ina gridi moja ambayo inabebwa na bwawa la Mtera linalo tegemea mto Ruaha ambao hivi sasa unakauka miezi 5 katika miezi 12 ya mwaka. Ni dhahiri kwamba kwa usalama wa Taifa na hata kwa gharama Nchi itafaidika zaidi kwa kujenga gridi nyingine kutokea Mtwara badala ya kusafirisha gesi kuja Dar-Es-Salaam.
  Serikali haitashinda vita hii kwa kuzusha kwamba ama wanasiasa wanaopinga wanatumika na makampuni mengine au kwa mataifa ya magharibi kutaka kuvuruga nchi. Serikali ijitazame yenyewe. Bila kufanya hayo tunayo pendekeza hapo juu, wananchi wataendelea kupigania hako yao. Hii ni vita ya uwajibikaji. Wananchi wanataka kufaidika na rasilimali za nchi yao. Kwa vyovyote vile upande wa wananchi utashinda. Vita ya uwajibikaji kwenye rasilimali za nchi sio ya vyama vya siasa, ni vita ya wananchi. Chama cha siasa kitakachokwenda kinyume na matakwa ya wananchi, kinajichimbia kaburi.
  --
  Zitto Kabwe
   

  0 0  0 0

  0 0
 • 01/21/13--00:34: House for Rent-KIJITONYAMA
 •  A two bedroom house is available for  immediate lease. The house is located at Kijitonyama and asking rent is USD 1,000 per month.
  If interested please send text with your name to +255786223333 or email at neemashau@gmail.com 

  0 0
 • 01/21/13--01:30: Viwanja vinauzwa
 • Viwanja vinauzwa,vimepimwa na vina hati,vipo eneo la Viwanda Mwanambaya Mkuranga barabarani na vimezingatia hifadhi ya barabara,vimepakana na kiwanda cha Cement,kiwanda cha Gypsum na Yad ya Scania used,Heka 4 bei yake ni sh mil.700,zipo heka 28 nyuma ya hicho mil 700,zipo heka 4 zinapakana na ukuta wa kiwanda cha Cement Mil.600.

  Zipo heka 6 hazijapimwa zipo barabarani  eneo hilo hilo mil 500. Mwandenga  zipo heka 67 Mil. 700,Zipo nyumba eneo la Gerezani  kariakoo Mil. 700 kwa Mil.900,Round about ya Kariakoo bilioni 1 na 200 milioni.Kariakoo stendi ya Kawe ni bilioni 1 na 200 mil. Ipo beach gezaulole Kigamboni Mil.600,pia vipo viwannja vya Mil.10 na vilivyopimwa kwa mil 25 Gezaulole-Kigamboni.

  Kwa mawasiliano piga namba 0652020343 

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpa pole mfiwa,Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam jana.


  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa jana Jumapili jioni alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga,Nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam.

  Marehemu Sufiani Bakari Kusaga alikuwa ni mume wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Temeke ambaye sasa hivi ni Katibu wa CCM Kishapu,Mh. Khadija Kusaga.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimfariji mfiwa,Mama Khadija Kusaga.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Temeke,Mh. Abbas Mtemvu wakati walipokuwa kwenye msiba huo jana jioni.

  0 0  Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal  umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji  tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo  ambalo hutumika kupaki  wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezaa kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa  akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.

  Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
  Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
  Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, KinondoniAfande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi
  Mmoja wa Maofisa wa Polisi akitazama moja ya gari lililoharibiwa vibaya mara baada ya kuangikwa na ukuta.
  Baadhi ya watu wakiwa kwenye eneo la tukio wakishuhudia namna magari yalivyoharibika vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta.
  Mmoja wa watu,ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliyeathiriwa na tukio hilo pichani kati akiwa amezungukwa na Maofisa wa jeshi la Polisi,akielezea namna hali ilivyokuwa.
  Sehemu ya ukuta ambao umebaki ukiwa umewekwa alama ya hatari

  Baadhi ya watu wakishuhudia hali halisi ya tukio hilo lilivyokuwa mara baada ya kutokea mapema alfajiri ya leo.

  0 0

  Mimi Na Tanzania‚ ni kipindi kinachohusu masuala yanayoigusa jamii kwa namna moja au nyingine haswa katika siasa, uchumi,michezo,na vikwazo na vimbwangwa vinavyoikumba jamii ya kitanzania.

  Mimi Na Tanzania ni kipindi kisicho na upendeleo katika kumsaidia mwananchi wa kawaida haswa unyanyasaji unaofanywa na wanaodhani wana nguvu kuliko aliyewaumba.

  Tunamulika Kaskazini hadi Kusini, Magharibi hadi mashariki ili kujenga jamii yenye amani, haki na upendo. Mimi Na Tanzania ni kipindi pekee kinachofunga safari kutafuta habari za kijamii popote pale Tanzania.

  Usikose kutazama kipindi hiki kila siku ya Jumapili Saa moja na nusu jioni katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten. Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' kinaongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.

  Pia unaweza kupata vipindi vipya vinavyoigusa jamii kwa kuetembelea libeneke lake hapa http://www.miminatanzania.co.tz/ Unaweza pia kulike page kwenye mtandao wa facebook humu http://www.facebook.com/miminatanzania
  Fuatilia moja ya kipindi cha madhara ya madawa ya kulevya hapo chini.

  0 0


  KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini iliyopangwa kufanyika siku ya Jumatano mjini Mwanza.
  Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

  Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
  “Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango  vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
  Kuhusiana na mabacha wawili, Mbuyu Twite na Kabanga Twite  kucheza upande wa kulia, Brandts alisema kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika timu yake na uamuzi huo ulikuwa na faida kwa Yanga.
  “Kabanga anauwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu ana uwezo huo, hivyo uwepo wao katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na mipango ya mechi na wala si vinginevyo,” alisema.
  Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.
  Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwapa waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
  “Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

  0 0

  Mmoja wa washiriki, Ally Kawina, akichana mistari.


  Ibrahim Jackson akiwaonyesha mashabiki hazina yake katika mpambano huo.
  Arnold Mathias akikamua ‘vipande’ vyake.
  Ally Zuberi akionyesha vitu vyake.
  Baraka Daniel akifanikisha zamu yake katika ‘microphone’.
  Bahati Charles naye akifanya vitu vyake.


  SHINDANO la kumtafuta mkali wa kuchana mistari ya ‘hip hop’ la The Mic King linalofanyika ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live ulioko Mbagala jijini Dar es Salaam kila Jumapili, limezidi kuchanja mbuga na kuwachengua mashabiki wengi wanaojitokeza katika ukumbi huo.


  Shindano hilo hurushwa moja kwa moja kila Jumanne saa 4 usiku na kurudiwa siku ya Jumamosi saa 8 mchana katika kituo cha televisheni cha DTV.
  (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)

  0 0

  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akizungumza na wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni ya Simu ya TTCL na migogoro iliyopo kwenye Kampuni  hiyo. Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said (kushoto) akitoa muongozo kwa wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo ya TTCL na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Karim Bablia akitoa kero mbali mbali alizokumbana nazo kwenye kampuni hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.


  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TTCL,Shaban Mrisho wakisikiliza kwa makini kero mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam,leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Injinia Clarence Ichwekeleza wakati wa Mkutano wa Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye Mkutano wao na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akiendelea kuongea na Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye Mkutano wao na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.Picha na http://othmanmichuzi.blogspot.com

  0 0


  Dira Media Group wachapishaji wa Gazeti la Dira ya Mtanzania linatangaza nafasi 5 za Kazi, Afisa Mauzo (Sales Executive).


  SIFA:
  1.Awe amemaliza kidato cha sita na kuendelea
  2.Awe kijana / Msichana mwenye umri usiozidi  miaka 35.
  3.Mwenye uzoefu usiopungua mwaka mmoja katika tasnia ya habari upande wa matangazo.
  4.Awe tayari kufanya kazi katika mazingira yoyote.
  5.Awe anajua kutumia Computer
  6.Awe anajua kuongea na kuandika Kiingereza vizuri.

  MAOMBI YATUMWE KATIKA ANUWANI IFUATAYO:
  Meneja Utawala na Fedha Dira Media Group S.L.P 105497 Dar es salaam yafike kabla ya tarehe 31/01/2013 au Alete kwa mkono katika Ofisi za Dira Media Group zilizopo Kinondoni Block 41 karibu na shule ya Msingi Kumbukumbu, simu namba 0222669066 au 0658 – 824 723 Email-diramatangazo@yahoo.com.


  Dira Media Group in Tanzania, invites applications from highly competent individuals for the post of  FINANCE AND ADMINISTRATION MANAGER.

  Duties and Responsibilities:
  λManage financial and administration activities to achieve financialgoals.
  λDevelop the overall corporate financial goals and objectives.
  λDevelop and maintain standard financial and administrative procedures.
  λWork closely with the CEO in preparation of business plan and operational budget.
  λEnsure preparation and maintenance of financial records.
  λSupervise and manage payroll processing and tax filing activities.
  λDevelop overall goals for the finance and administration departments.
  λIdentify and resolve invoicing issues, accounting discrepancies and other financial related problems
  λAny other duties as may be assigned by the CEO

  Qualifications:
  Minimum of Bachelor’s Degree in Accounting, CPA qualifications, master’s Degree in Business Administration is an added advantage.

  Experience:
  Two to Three years experience working in the Finance and Administration role preferably in Media industry

  Age: Not above 50 years
  Remuneration: An attractive package awaits the right candidate.
  To apply: Send your application and CV with copies of your certificates with 3  reliable references before 31th January  2013 to:

  Managing Director,
  Dira Media Group,
  P.O. Box 105497
  Dar es Salaam


  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
   Gari iliyomchukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiondoka Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika maongezi rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake  katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.PICHA NA IKULU
   

  0 0


older | 1 | .... | 13 | 14 | (Page 15) | 16 | 17 | .... | 1896 | newer