Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

HABARILEO- TUNAKARIBISHA PICHA

$
0
0

Mpenzi msomaji, wa Gazeti la HABARILEO, tuletee picha za harusi, Kumuaga Bi Harusi, Uchumba, Ubatizo, Kipa imara, na nyinginezo, nasi tutazichapisha bureee katika Ukurasa huu.



Unaweza kutuletea moja kwa moja katika Ofisi zetu Zilizoko Jengo la Daily News Makao Makuu, Barabara ya Mandela Tazara (Tunatazamana na Ofisi za TAZARA), Dar es Salaam au kupitia anuani ya barua pepe habarizapicha@gmail.com–MHARIRI. 

PIA waweza kuzituma kwa barua pepe:- mrokim@gmail.comKWA MAELEZO ZAIDI PIGA +255 755 373999 AU +255 717 002303.


SEMINA YA MAKATIBU WAKUU WA SMZ

$
0
0



 Dkt Hassan Mshinda Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknologia COSTECH akitoa mada kwa Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusiana na Kazi na Wajibu wa Tume hiyo huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar.

  Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Amina Khamis Shaaban akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknologia hayupo pichani katika Semina ya Makatibu Wakuu wa Zanzibar kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume hiyo kwa Zanzibar huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Zanzibar Bakari Asseid akiuliza swali kwaMkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknologia hayupo pichani katika Semina ya Makatibu Wakuu wa Zanzibar kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume hiyo huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar.
  Makatibu wakuu wa Zanzibar wakiwa katika Semina yapamoja kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume ya Sayansi na Teknologia iliyotayarishwa na Tume hiyo huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar.
 Mratibu wa Tume ya Sayansi na Teknologia Dkt. M. Sheikh akiwasilisha mada katika Semina ya Makatibu wakuu wa Zanzibar kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume ya hiyo huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar
  Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akifunga Semina ya siku moja ya Makatibu wakuu wa Serikali ya SMZ kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume hiyo kwa Zanzibar huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
======  =====  ====== ========

Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar.
                   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari 19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari huko Gulioni katika Jengo la  ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha Sekta za Umma na Sekta Binafsi, ambao utajadili mada mbili muhimu ambazo ni Maendeleo ya uwekezaji katika viwanda na Ubiya unaohitajika katika viwanda vya Zanzibar.

Amesema wameamua kuzungumzia masuala hayo kutokana na Sekta ya Viwanda Zanzibar kuwa nyuma sana jambo ambalo pia huchangia ukosefu wa Ajira kwa vijana na mapato kwa maendeleo ya Zanzibar.

Ameongeza kuwa Zanzibar ina fursa nzuri ya kuanzisha viwanda vipya na kuvifufua vile vilivyokuwepo awali jambo ambalo litachochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa Zanzibar.

Vuai amefahamisha kuwa Viwanda vilivyokufa Zanzibar vilitokana na sababu mbalimbali na kwamba Mkutano huo utakuwa ni sehemu muafaka ya kuelezea chanzo cha kufa viwanda hivyo na kubuni mipango mipya ya kufufua sekta hiyo.

Alisema wamealika wadau mbalimbali wa Viwanda na Biashara kutoka ndani na nje ya Zanzibar kuja kujadili namna bora ambapo anaamini kuwa mwisho wa Mkutano huo Zanzibar inaweza kuja na fikra mpya ya juu ya Viwanda.

Aidha Katibu huyo alisema katika Mkutano huo Makala tatu zitawasilishwa mbili kutoka katika Sekta ya Umma na moja itawasilishwa na Sekta binafsi kuhusiana na mambo yanayohusu njia bora za kuimarisha sekta ya Viwanda Zanzibar.

Katibu Vuai pia amewaomba Wajasiriamali wa Zanzibarkuitumia fursa hiyo adhimu kwao kutangaza biashara zao kupitia Wageni na wenyeji ambao watashiriki katika mkutano huo wa Saba toka kuanzishwa Baraza la Biashara la Zanzibar.

Mkutano huo wa siku moja unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 350 kutoka ndani na nje ya Zanzibarambapo Mashirika kama UNIDO, TIDO, TMS, Tume ya Biashara ya Afrika ya Mashariki ni miongoni mwa waalikwa.

 

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR   17/01/2013


SERIKALI YABARIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

$
0
0

Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa
la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii,
Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na
Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya
kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa
kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.

Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda
zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye
sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka
huu,ambapo jumla ya warembo 60 wameingia rasmi kambini leo katika
hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji
hilo la Taifa.

Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika
mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism
World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism
University World, Miss Globe International n.k

Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya
Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss
Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality n.k

Fainali za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya
Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa umepewa
heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais

WASANII WA FILAMU BONGO KUPELEKWA NIGERIA

$
0
0

 Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jmahuri  ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba. 

Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.  

DAR ES SALAAM, Tanzania

KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (jana), Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.

 “Kwa muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili  kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.

“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.

Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa,  alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu,  kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi. 
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.

“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema 
Mwakifamba.

Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.

ILE CAMPAIGN YA KUPUNGUA BADO INAENDELEA 2013 @ AK COSMETICS!!

$
0
0





ILE CAMPAIGN YETU YA KUPUNGUZA MANYAMA UZEMBE BADO INAENDELEA TENA SAFARI HII TUMEIPIMP KWA KUWAONGEZEA MAMBO MENGINE MAKUBWA na YENYE KUFANYA SHUGHULI YA KUAMINIKA DUNIA NZIMA!!

PITIA www.akclassic.blogspot.com upate kuona mambo zaidi
Au Wapigie
0713468393/0753482909

wasanii wa filamu wapanga kugoma leo kisa kuambiwa hawana elimu.!

$
0
0

Aisee kauli hiyo ilimkasirisha sana Mboto mpaka akataka kuhakikisha kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu kujiuzulu na kutaka awakome kabisa wasanii nchini
Msanii wa Cloud "Ahaa!! Yani huyu mwanamama ndio anatuchanganya sisi yani hata Rais wetu Kikwete mwenyewe anatusadia katika mambo mengi,lakini huyu anatukatisha tamaa yani sisi eti hatujasoma.
Steve Nyerere akitaka kuhakikisha kuwa wasanii wanaandamana kama ambavyo wanavyofanya Chadema kwa kuwa kwa kufanya hivyo ndio heshima itakuja kwao.
Wasanii wa tasnia ya filamu na Maigizo nchini leo wameonesha kukerwa kwao na kauli iliyokuwa ikitolewa mara kwa mara na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joycee Fisoo kuwa hawana elimu ya kutosha.

Wasanii hao kwa pamoja wameamua kuendesha maandamano ya kutaka mama huyo aachie ngazi ili kupisha mtu anayejua sanaa na kuwatetea maslahi yao .Wakati huohuo wasanii hao wamepinga viwango vya malipo ambavyo vimewekwa na bodi ya filamu nchini vinavyotakiwa kulipwa na wasanii wa tasnia hiyo.

Wasanii hao waliokutuna juzi na jana katika ukumbi wa Vijana  Social Hall kwa pamoja walionekana kupinga viwango hivyo huku wengine wakisisitiza kuwa bodi hiyo imewasariti baada ya kuwasaidia.

Akisoma viwango mbalimbali kama vile ada ya ukaguzi wa mwongozo wa filamu (script) ambapo alisema kuwa kwa saa moja ni shilingi elfu 60 na kuongeza kuwa  iwapo zoezi hilo likichukua zaidi ya saa moja itawaumiza wasanii. Alisema kuwa iwapo msanii atakuwa akitaka script yake hiyo isomwe haraka haraka basi itatakiwa alipie laki moja.

Alisema kuwa pia iwapao mwandaaji wa filamu akitaka kutumia wasanii kutoka  nchi za Afrika Mashariki atatakiwa kulipia 120,000/= huku wasanii wa kigeni wa nje ya Afrika Mashariki watatakiwa kulipiwa dola 500.

Pia alisema kuwa kibali cha kutengeneza filamu imekuwa ni laki 5 huku kama mtayarishaji akiwa anataka kupewa kibali kwa haraka itabidi alipie milioni moja huku kama mtayarishaji ni mgeni kutoka nje ya nchi basi atatakiwa kulipia dola 3000.

Wakati Sangu akisoma maelezo hayo wasanii walikuwa wakizomea huku wengine wakitoa maneno ya kulalam akuwa viwango hivyo ni vikubwa. Sangu aliendelea kuwasomea wasanii hao viwango hivyo ambapo aliwataarifu kuwa kubandika barabarani tangazo la kutangaza ni shilingi 5000 kwa tangazo moja.

Alisema kuwa adhabu zitakazotolewa kwa watu watakaokiuka taratibu hizo watatozwa faini za hapohapo ya milioni moja ikiwa pamoja na amri ya kusitisha utengenezaji wa filamu hiyo. “ Mimi naona kuwa hii bodi inataka watu turudie hali zetu za wizi, kuzurura na tushindwe kupata hiki kidogo tunachokipata kwa sasa, na hii ni kinyume na Rais Kikwete atakavyo” alisema Sangu.

“ Yani kama ukipewa kibali cha kuitengeneza filamu kwa miezi mitatu ni shilingi laki tano lakini sasa iwpao miezi mitatu ikiisha na haujamaliza filamu yako basi itabidi ulipie tena laki 5 nyingine sasa hii ni adhabu na itapelekea watu kutengeneza filamu mbovu zisizokuwa na umuhimu” alisema Sangu.

Mbali na hayo lakini pia Sangu aliendelea kuishutumu bodi hiyo huku akiendelea kutupa lawama za wasanii hao kwa Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Joyce Fisoo kuwa amekuwa akiwakejeli wasanii kuwa hawana elimu.

Kufuatia kauli hiyo wasanii walipandwa na jazba huku wengine wakianza kutoa lawama zao kwa katibu mtendaji huyo kuwa anatakiwa kujiudhulu. 
Wasanii waliotoa mawazo yao ambao ni Cloud, Mpoto na wengineo walisikika kwa pamoja wakisisitizia kuwa katibu huyo ajiudhuru haraka iwezekanavyo na kusisitiza kuwa wataandamana kusisitiza jambo hilo.

Habari picha kwa hisani ya http://www.elimuboratanzania.blogspot.com

Shirika la ndege la Precision Air yazindua safari za Mbeya

$
0
0
 Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri wa Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu, akikata utepe kuzindua Safari za Ndege za Shirika la Precision Air za Mbeya kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael Shirima. 
  Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu, akishuka kutoka katika ndege ya shirika la Precision Air wakati wa uzinduzi wa Safari za Mbeya – Dar kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kabla ya kukata utepe kuzindua safari hizo. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Michael Shirima. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air (PW), Michael Shirima, (Kushoto) akiteta jambo na abiria wa kwanza kununua tiketi ya safari ya Mbeya wakati wa uzinduzi wa Precision Air wa  njia ya Mbeya – Dar, Bw. Alfred Mwambeleko Jumatano hii.  

 Mzee akisaidiwa kupanda ndege, ambaye ni mkazi wa mkoani Mbeya wakati wa uzinduzi wa Safari za Ndege za Shirika la Precision Air za Mbeya – Dar uliofanyika Jumatano hii kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uliofanyiwa marekebisho kutumika kwa safari za kimataifa.

=========  ===============  =========

Shirika la ndege la Precision Air yazindua safari za Mbeya

SHIRIKA la ndege la Precision Air (PW) jana lilizindua safari zake za mkoani Mbeya, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambao umekamilika kukarabatiwa hivi karibuni na kuuwezesha utumike katika safari za kimataifa.

Huu ni ujio mpya wa safari za shirika hilo ambapo walikuwa wanaruka kuenda mkoani Mbeya kati ya miaka ya 1997 hadi 2000 wakitua kastika uwanja mdogo uliopo katikati wa mji wa Mbeya.

Uzinduzi ambao ulifanywa na Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Peter Lupatu kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Songwe, ambapo wakazi wa Mbeya walielezea furaha yao juu ya uzinduzi huo.

Shirika hilo lilitumia ndege yake aina ya ATR-72 yenye uwezo wa kubeba abiria 70, katika kuzindua njia hiyo mpya, kwa kuanza na ratiba ya kuruka Mbeya mara nne katika wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili) kwa nauli ya shilingi 249,000/= kwa tiketi ya kwenda na kurudi na shilingi 165,000 /= kwa tiketi ya njia moja, zikijumuisha kodi na gharama nyinginezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Lupatu alisema kuwa hatua iliyochukuliwa na Precision Air itauwezesha mkoa wa Mbeya na majirani zake kuwa na fursa nyingi za kibiashara na maendeleo kwa upatikanaji wa usafiri wa anga katika eneo hilo.

"Natoa wito kwa wakazi wa Mbeya na majirani zake kutumia fursa hii kikamilifu iliyotolewa na Precision Air baada ya kuanzisha safari zake za kibiashara katika mkoa huu. Hii ni hatua kubwa kwa mkoa na sekta ya usafiri wa anga nchini.

"Uwepo wa usafiri wa uhakika wa ndege tunaouanzisha leo hii unaonyesha kwamba Mbeya na mikoa ya jirani sasa itapata fursa kubwa za kibiashara pamoja na kuunganishwa na miji mikubwa ya kibiashara na miji mingine duniani.

"Kuanzishwa kwa njia hii mpya itakuwa ni chachu ya ukuaji mkubwa wa shughuli mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huu ambazo ni pamoja na kilimo cha mbogamboga na maua, kwa kuwa sasa wakulima wanauhakika wakusafirisha mazao yao kwa wakati katika masoko yanayostahili," alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael Shirima, aliiomba serikali kutafuta mwekezaji ambaye atawekeza katika uuzaji wa mafuta ya ndege katika uwanja wa ndege wa Songwe ili kuwasaidia wawekezaji katika sekta ya usafiri wa anga kupunguza gharama za uendeshaji.


"Ombi langu kwa serikali ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na upatikanaji wa mafuta  ya ndege ya kutosha katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji kwa mashirika ya ndege. Kwa sasa, tunalazimika kubeba mafuta ya akiba ambayo huongeza mzigo katika ndege, hivyo inatulazimu kubeba abiria wachache na kuacha nafasi kwa ajili ya mafuta ya akiba, "alisema Bw Shirima.

Muasisi huyo wa PW pia aliiomba serikali kuhakikisha kuwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe unakuwa na vifaa bora vya kuongozea ndege kutokana na eneo lilikojengwa ili kulinda usalama wa ndege na abiria wake. Pia aliiasa serikali kufunga rada katika uwanja huo wa ndege, kama ilivyo katika viwanja vingine vya kimataifa.

Aliwahakikishia wakazi wa Mbeya kwamba shirika katika siku za usoni litaongeza idadi ya safari zake za Sogwe endapo abiria wa kwenda na marudio itaongezeka.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigala akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni alisema kuwa anafuraha na uamuzi wa Precision Air wa kufika mkoani Mbeya kwa kuwa jitihada hizo zitapunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa mkoa huo za usafiri hususani usafiri wa Dar es Salaam na kuungana na miji mingine duniani.

"Uzinduzi tunaoushuhudia leo ni wa baraka kubwa kwa Mkoa wa Mbeya na majirani zake. Napenda kuwahakikishia wakazi wa Mbeya kuwa Mbeya ya leo haifanani na Mbeya ya jana na ya siku zijazo. Kwa kuwa Precision Air imezindua safari zake kwa mkoa huu, utaona mashirika mengi ya ndege yakileta ndege zao hapa. Uwepo kwa usafiri wa anga sasa kutafanya ndoto zetu za kuendeleza kilimo cha mbogamboga na matunda katika mkoa wetu kufanikiwa. Shughuli zaidi za kiuchumi sasa zitafanyika katika mkoa na hivyo kuwainua watu wetu kiuchumi," alisema. 

INDOMA TOURS ZANZIBAR INAWALETEA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA

$
0
0
Kampuni ya Utalii ya Indoma Tours ya Mjini Zanzibar, inawaleate mchezo mkali wa Kirafiki wa Kimataifa wa Soka, kati ya timu ya Skonda Flota kutoka Barani Ulaya na Timu ya Sale Mdosi Hardware, ya mjini Zanzibar, mchezo utakaochezwa Februari 9, mwaka huu katika Uwanja wa Uzi Football Yard, kuanzia saa 10:00 jioni.

WASOMAJI WETU POLENI KWA USUMBUFU, KWA SASA TUPO HEWANI

$
0
0


Mtandao wako uupendao wa www.globalpublishers.info kwa sasa upo hewani baada ya kutopatikana kuanzia Jumatano asubuhi kutokana na matatizo ya kiufundi ambayo yameshughulikiwa ipasavyo na wataalamu wetu.  Ni matarajio yetu kuwa tatizo kama hili halitatokea tena.

Tunawaomba radhi wasomaji wetu pamoja na watu tunaotangaza nao kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hiki. Kwa sasa tunaendelea kuwapa habari motomoto kama kawaida wasomaji wetu.
Asanteni kwa uvumilivu wenu.
Web Master
Global Publishers Ltd

Sua freestyla Battle Toxic VS Kevoo

kikosi cha timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini yatua leo jijini dar,kumenyana na timu ya yanga uwanja wa taifa kesho.

$
0
0

 
 Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius kambarage Nyerere.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa shindano hilo,kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda,Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
 Nahodha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Waratibu kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Wachezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini dar.
 Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. kambarage Nyerere.Picha zote na JIACHIE BLOG.
======  ======= ======= =======
WAKATI mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa Black Leopards ametema cheche na kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na uzoefu wao wa mashindano ya Kimataifa.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki wengi kufika.
Mratibu wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na shs 7,000 na kuwa cha shs 3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona mechi hiyo.
Viingilio vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni shs 15,000 , VIP B shs 20,000 na VIP A shs 30,000
Dauda alisema kuwa Black Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo kutokana na uzoefu waliopata katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja na kombe la Shirikisho.
Kocha wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja ya faraja kwao.
“Ziara hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,” alisema Makhubela.
 Alisema kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao ambayo ipo katikati..

Rais Kikwete afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi

UFUNGUZI WA VISIMA 30 KATIKA MAENEO YA WILAYA 6 KAME TANZANIA VILIVYOCHIMBWA KWA MSAADA WA SERIKALI YA MISRI WAFANYIKA WILAYANI MASWA.

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akishirikiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed (kulia) kukata utepe kuashiria ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri uliofanyika jana katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kushoto kabisa ni Mhe. Pascal Mabiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Tanzania Jumanne Maghembe naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mbunge wa jimbo la Busega mkoani Simiyu  Titus Kamani naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mama Maria akiondoka kwenye eneo la bomba kuu la kutekea maji mara baada ya kutwishwa ndoo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed huku wananchi wengine wakipiga makofi kuashiria kufurahia tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. .

Jiwe la Msingi.

Ni burudani ya ngoma ya kabila la wasukuma na wala si mchezo wa vita.

Meza kuu ikifurahia yanayojiri ya kiburudani katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri .

 Kwa upande wake waziri wa Maji na Umwagiliaji Nchini Prof. Jumanne Magembe amesema kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inapunguza kama si kuondoa kabisa tatizo la uhaba wa maji nchini Tanzania.
Bofya Play usikilize ..
Takwimu za upatikanaji wa maji katika Wilaya zilizochaguliwa kwenye mradi huo hadi mwezi Disemba 2011 katika wilaya zilizomo kwenye miradi zinaonyesha kuwa na hali ni ya mvua zisizoridhisha, hivyo kipaumbele katika mradi huu ni kusaidia kwanza maeneo yaliyo upande wa mvua kidogo ambapo matarajio ya serikali kwa miradi yote ikikamilika hali ya upatikanaji wa maji katika vijiji vyote itakuwa bora, suala ambalo linawezekana.


Nae Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed amesema kuwa serikali yake inajivunia msaada iliyoutoa wa kiasi cha fedha Dola milioni moja za Kimarekani kusaidia kukamilika kwa miradi ya maji nchini Tanzania kwani Misri inaamini kuwa hiyo ni moja kati ya njia ya kudumisha na kuendeleza ushirikiano uliopo.  



Msaada huo wa Misri si suala geni hapa nchini kwani tangu enzi za hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, Tanzania na Misri zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja za siasa, maji, kilimo cha umwagiliaji, na Tanzania imekuwa ikipokea madaktari wakujitolea ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye hospitali za mikoa na kila mwaka Tanzania imekuwa ikipeleka wataalamu wake nchini Misri kupata mafunzo kujinoa katika taaluma hiyo.

Wananchi wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri 
Pamoja na mradi huu, huduma ya maji imeendelea kuboreshwa kote nchini kupitia Program ya maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ilianza kutekelezwa tangu mwaka 2006, kwa kushirikisha juhudi za wananchi wenyewe na washirika wengine wa maendeleo. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za programu wilayani Maswa ni ; Miradi ya maji ya bomba ya vijiji vya Sayusayu, malampaka na Mwasayi; Miradi mipya inayokaribia kuanza kutekelezwa ni ya vijiji vya Njiapanda na Jija.


Lengo la Programu ya Maji ni kuwa kufikia mwaka 2015,huduma ya maji vijijini iwe wastani wa asilimia 65.

Wananchi wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri 

Wito umetolewa kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo yote ya miradi nchini kuwa walinzi wa miundombinu ya maji. kutokomeza tatizo la miundombinu ya maji na vifaa vya maji kuhujumiwa na watu wabaya ambao huing'oa na kuuza kama chuma chakavu hivyo kila mwananchi awe mlinzi wa miundombinu hiyo kwa faida ya taifa na kwa kuzingatia maslahi ya walio wengi (kuwaepusha mama zetu na adha ya kusafiri umbali mrefu kusaka maji salama).

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, GERGORY TEU AFANYA ZIARA KONYAGI NA TBL

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa kuhusu picha ya watoto wa wakulima wa zao la zabibu wanaosomeshwa na kiwanda hicho, alipotembelea kuona utendaji wa kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Ofisa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Athuman Mkungu akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kiwanda cha Konyagi.
Naibu Waziri, Teu  (katikati) akitembelea kiwanda cha Konyagi
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (katikati) akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa bidhaa.


 Wafanyakazi wa kiwanda cha Konyagi wakifungasha viroba vya konyagi kiwandani hapo
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa alipotembelea kuona utenddaji wa kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi.. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtaalamu wa Upishi wa Bia, Kelvin Nkya akimuonesha kompyuta inatumiwa kupikia bia katika kiwanda cha TBL Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Martine Calvin (katikati) jinsi bia inavyopikwa kitaalamu alipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Martine Calvin (katikati) kuhusu uzalishaji wa bia unavyofannyika, alipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa wizara hiyo, Genoveva Kilabuko.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu
 Mena wa Kiwanda cha Bia cha TBL, Dar es Salaam, Martine Calvin (kulia) akimpatia zawadi Naibu Waziri
 Calvin akimpatia zawadi msaidizi wa waziri, Gregory Teu
 Naibu Waziri Gregory Teu (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBL
 Mkurugenzi wa Mauzo wa Kiwanda cha Konyagi cha TDL, Joseph Chibehe (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri, Teu.
Mkurugenzi wa Miradi Maalumu wa TBL, Phocus Lasway akielezea mafanikio na changamoto zinazoikabili kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa  Wizara ya Viwanda na Biashara, Kilabuko akizungumza na wafanyakazi wa TBL walipomaliza ziara.. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

ALLIANCE AUTOS YASAIDIA TIMU YA DAR LEOPARDS RUGBY CLUB

$
0
0
Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja akikabidhi jezi kwa timu mchezo wa raga (Rugby) ya Dar Leopards jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot. Minja amesema kuwa wameamua kuunga mkono mchezo wa raga(Rugby) kwani ni miongoni mwa michezo iliyosahaulika nchini. Alliance Auto wameshirikiana na HSE Solutions kudhamini jezi Dar Leopards Club. Wanaoshuhudia tukio hilo ni baadhi wachezaji wa Dar Leopards Rugby Club.
Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor (kushoto) akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo huku wakiwa wamevalia jezi hizo.
Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot.
Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo kwenye moja ya Brand ya magari ya Alliance Autos aina ya 'Volks Wagon AMAROK' huku wakiwa wamevalia Jezi walizokabidhiwa leo katika makao makuu ya kampuni hiyo.

Mstahiki Meya Jerry Silaa mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita shule ya Sekondari Azania

$
0
0
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita ya shule hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ambapo na yeye pia alikuwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliosoma shule hapo baada ya kuwasili kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita.

Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini daftari la wageni la Shule ya Sekindari Azania katika sherehe za mahafali ya Kidato cha sita shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Azania Bw. Bernard Ngoze akizungumza na mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa na kumwelezea changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo. Wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda na Makamu wa pili shuleni hapo Mwl. Joram Nkya.


Kutoka kushoto ni Mgeni maalum aliyewahi kusoma shuleni hapo Bw. Ali Said Mwema, Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo Bi. Hilda Luhanga na Msaidizi wa Meya Jerry Silaa Bw. Anthony William wakimsikiliza mkuu wa shule ya sekondari Azania (hayupo pichani) wakati akiongea na Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiongozwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Azania Bi. Elizabeth Ngoda kutazama baadhi ya picha zinazoonyesha hali ya utunzaji wa mazingira tangu awali mpaka sasa ambapo kwa kiasi kikubwa shule hiyo imeweza kuboresha na kutoa elimu ya mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo. Mstahiki Meya amepongeza juhudi zao na kuwataka shule nyingi za jijini zilizochini ya manispaa ya Ilala kuiga mfano wa shule ya Azania katika kutunza Mazingira.
Baadhi ya picha zikionyesha harakati za utunzaji wa Mazingira wa Shule ya Azania unaosimamiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze ambaye naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliosoma shule hiyo.
Vijana wa Skauti wa shule ya Sekondari Azania wakitoa heshima kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa alipowasili eneo maalum palipofanyika sherehe za mahafali ya kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wa shule hiyo.
Kiongozi wa gwaride la skauti la Azania akisalimiana na mgeni rasmi Meya Jerry Silaa.
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Azania wakiimba wimbo wa Taifa baada ya mgeni kuwasili.
Skauti wa shule ya Azania wakuupa heshima wimbo wa Taifa.
Meza kuu ikiimbia wimbo wa taifa.
Baadhi ya Wazazi na walezi waliohudhuria hafla ya watoto wao.
Vijana wa Skauti wakionyesha manjonjo yao mbele ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Binti Pekee wa kikundi cha Skauti cha Azania sekondari aliyeshangaza wengi kwa kutembea na kamba huku akijiamini vilivyo wakati wa sherehe za mahafali hayo.

Taarifa ya Msiba

$
0
0

Familia ya ndugu Demba Sow, inasikitika kutangaza Kifo cha mke wake mpenzi Monique Demba Sow Kasongo. Kilichotokea Burhani Hospital 14-1-13 saa 2 usiku. 

Habari ziwafikie watoto wa Marehemu, Yan Sow na Didy Sow walipo America na Canada, ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. 

Leo tunakesha nyumbani kwa Marehemu Mikocheni karibu na Clouds Fm. Mazishi ni kesho Jumamosi 19-1-13 ambapo Misa ya kumuombea Marehemu itafanyika nyumbani kwake Mikocheni kesho 19-1-13 saa 5 na kuagwa. 

Mwili utazikwa Katika makaburi ya Kinondoni saa 9 mchana. 

Kwa mawasiliano zaidi,Wasiliana na mwenye namba hii 0754280895

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.

-Amen.

Ihii ndiyo yanga,yainyuka 3-2 Black leopards ya sauzi jijini dar leo.

$
0
0

 Mkuu wa masoko na mawasiliano wa NMB Imani Kajula akimkabidhi kitita cha shilingi laki tano Frank Domayo,ambaye ameibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Yanga FC na Black Leopards ya Afrika Kusini,uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo jijini Dar.

 Golikipa wa timu ya Black Leopards,Ayanda Mtshali akijaribu kuokoa mpira uliotinga kimiani kwa njia ya penati na mchezaji wa yanga,Jerson Tegete,penati hiyo ilipatikana katika kipindi cha kwanza,katika kuoenesha Yanga wako fiti mnamo kipindi cha pili mchezaji Frank Domayo akaongeza goli la pili,haikutosha Tegete tena akapachika goli la 3-2 .Hii ndiyo Yangaa.Mpaka dakika 90 Yanga imetoka kifua mbele kwa magoli 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,Mtanange huo uliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar.
Hatari golini kwa timu ya Black Leopards,Golikipa wa timu ya Black Leopards,Ayanda Mtshali akiokoa hatari golini kwake.
 Mchezaji wa timu ya Yanga,Kabange Twite akimtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.Ama kwa hakika ihiiii ndiyo Yanga ya Uturuki iliotandaza kabumbu safi kabisa ndani ya Uwanja wa Taifa.
 Mchezaji wa timu ya Yanga,Haruna Niyonzima akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,kwenye mchezo wao wa kirafiki unaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.
 Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mtanange wa Yanga na timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
 Mashabiki wa yanga kibao
 Full Nginja ngijaaa

 Mashabiki kwa shangwe kila wakati wakiipa hamasa ya ushindi timu yao ya Yanga.
 Mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini akitaka kuwapangua wachezaji wa timu ya Yanga,aah iwapi kwa taabu sana kama uonavyo pichani.
 Baadhi ya wachezaji wa Black Leopards ya Afrika Kusini wakiwa kwenye benchi lao
 Baadhi ya makocha wa yanga na wachezaji wakiwa watulia tulii kwenye benchi lao la Ufundi
 Sehemu ya kikosi kazi cha Clouds TV kinachorusha mtanange huo live kupitia Clouds TV jioni ya leo
 Wachezaji wa timu ya Yanga wakiingia iwanja kuiana ngwe ya kwanza.
 Hiki ndiyo kikosi kazi cha Yanga
Kikosi cha Black Leopards ya Afrika Kusini.

Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika,mdau ajishindia king'amuzi cha dstv jioni ya leo.

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa Ving'amuzi vya DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani City jijini Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini Afrika ya Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha bahati nasibu kwa wapenzi hao wa Soka waliokuwepo hapo.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda King'amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano ya Kombe la Afrika.
 
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) akikabidhi King'amuzi hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyi,ambaye ni Mwanalibeneke wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh.....!! jamaa anazali huyu!).
Baadhi ya Wadau wa DStv wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika,kati ya timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.
Wadau kibao toka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha Samaki Samaki jijini Dar kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea nchini Afrika ya Kusini yanakofanyika Mashindano hayo.

Green Waste Pro Ltd yazindua kampeni ya usafi wilaya ya Ilala

$
0
0

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road, kampeni iliyozinduliwa leo ikiendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd. yenye zabuni ya kusafika maeneo yanayoizunguka manispaa ya Ilala ambapo amesema zoezi hilo litadumu kwa wiki tatu mfululizo kwa kila Jumamosi ya wiki.

Mstahiki meya Jerry Silaa amewataka wananchi wa manispaa ya Ilala kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika zoezi la kusafisha maeneo ya kata zao. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
Pichani Juu na Chini Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia), Mh. John Chiligati ambaye ni mkazi wa Kivukoni na mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi wakishiriki katika zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akishiriki katika zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo katika maeneo ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni kampeni maalum ya kuweka mazingira safi katika maeneo mbalimbali yanayoizunguka Manispaa ya Ilala ambapo Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. imechekuza Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala na kata zake tatu.
Picha Juu na Chini ni Baadhi ya raia wa kigeni kutoka taasisi ya Roots and Shoots wakiunga mkono zoezi hilo na kuhakikisha manispaa Ilala inaongoza kwa usafi.


Picha juu na chini niVijana wa Ilala Jogging Club waliokuwa wakifanya mazoezi katika fukwe hiyo wakati zoezi la kufanya usafi likiendelea na kuamua kusitisha mazoezi yao na kushiriki na kujumuika kusafisha fukwe hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiwajibika wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Greda likifanya kazi ya kubeba takataka ngumu katika fukwe ya Ocean Road ambazo hazizoleki kwa mkono.
Lori la kubebea takataka la Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. likiwa limesheheni uchafu uliokusanywa wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd. wakiwajibika wakati wa zoezi hilo.
Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kushoto) akiwa na mdau wakati za zoezi hilo.
Kutoka kulia ni Bw. Said Mazingira, Afisa Habari wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd Bi. Vidah Fammie, Meneja Mkuu Bi. Elizabeth, Operation Manager Bw. Abdallah, Cindy na Mdau wa kujitolea Joshua wakionyesha Umoja wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwashukuru vijana wa Ilala Jogging Club kwa kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hiyo na kuwataka waendelee na moyo huo kwa maana suala la usafi ni letu sote.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kivukoni walioshiriki zoezi la usafi wa fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (kushoto) akivuta pumzi na wadau waliojitokeza kushiriki zoezi la kusafisha fukwe za bahari ya Hindi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Green Waste Pro ltd, wadau na wananchi wakipangiana maeneo ya kufweka majani katika fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road.
Mmoja wa wakazi wa jijila Dar anayefanya shughuli za kukusanya chpa za maji akionekana kufurahia mazingira hayo kuwa safi na kuamua kuweka kiroba chake chini na kumpumzika katika fukwe hiyo.
Moja ya Sehemu ya Fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road iking'ara baada ya kufanyiwa usafi.
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live


Latest Images