Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 14 | 15 | (Page 16) | 17 | 18 | .... | 1898 | newer

  0 0  MSAMA AUCTIONMART & DEBTS COLLECTOR INAHITAJI VIJANA WENYE SIFA ZIFUATAZO KUJAZA NAFASI ZILIZOWAZI:-

  MENEJA (1)
  SIFA:

  λELIMU KIDATO CHA SITA NA KUENDELEA
  λUZOEFU USIOPUNGUA MIAKA 2 KATIKA SHUGHULI ZA UDALALI NA MINADA
  λUZOEFU KATIKA MASUALA YA UKUSANYAJI MADENI SUGU KUTOKA TAASISI, MABENKI, MAKAMPUNI NA WATU BINAFSI
  λUMRI USIOZIDI MIAKA 50

  MAAFISA UDALALI NA UKUSANYAJI MADENI (5)
  SIFA:

  λELIMU KUANZIA KIDATO CHA NNE NA KUENDELEA
  λUZOEFU USIOPUNGUA MIAKA 2
  λAWE MWAMINIFU NA MCHAPAKAZI
  λUMRI KUANZIA MIAKA 25 NAKUENDELEA.

  MSAMA AUCTIONMART & DEBTS COLLECTOR INAJISHUGHULISHA NA SHUGHULI ZIFUATAZO:-

  1.KUPIGA MINADA NA KUUZA SAMANI ZA MAJUMBANI NA MAOFISINI KAMA VILE MAGARI, PIKIPIKI, MAJENGO, MASHAMBA, MAGHALA, VITI, MEZA, MAKABATI N.K.
  2.KUDAI MADENI SUGU (YALIYOSHINDIKANA).
  3.PIA KUTOA USHAURI KWA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI, MASHIRIKA, MAKAMPUNI, WATU BINAFSI JINSI YA KUFUATILIA MADENI SUGU (YALIYOSHINDIKANA).
  4.KUTOA WAPANGAJI WASUMBUFU NDANI YA NYUMBA.
  5.KUTOA ULINZI KATIKA MATAMASHA, MIKUTANO, SHEREHE MBALIMBALI NK.
  6.KUKUSANYA USHURU NA KODI MBALIMBALI KWA NIABA YA TAASISI MBALIMBALI.
  7.KUSIMAMIA UTEKELEZAJI AMRI ZA MAHAKAMA KWA KUWA KAMPUNI YETU IMESAJILIWA KISHERIA KAMA WAKALA WA MAHAKAMA YAANI COURT BROKERS.
  8.KUTOA USHAURI WA KISHERIA KUHUSU MASUALA MAZIMA YA USIMAMIZI WA MIRATHI.
  9.KAMPUNI YETU KWAKUTUMIA WATALAMU WALIOBOBEA NA WANAOZINGATIA WELEDI (PROFESSIONALISM) INAUWEZO MKUBWA KUFANIKISHA KAZI KIDIPLOMASIA NA KUTUMIANGUVU KIDOGO PALE INAPOBIDI TU ILI KUEPUSHA MADHARA YA KIUCHUMI NA KISHERIA KWA WATEJA WETU.
  10.KAMPUNI YETU KWA KUJALI NA KUTHAMINI WATEJA WETU IMEJIPANGA KULIPA FIDIA KWA WATEJA WETU KWA HASARA ITAKAYOSABABISHWA NA UZEMBE WETU IKITHIBITIKA HIVYO.
  11.KAMPUNI INAVITENDEA KAZI VYA KUTOSHA KAMA MAGARI, PIKIPIKI, OFISI KUBWA NA YA KISASA,ENEO KUBWA(GODOWN) KWAAJILI YA KUHIFADHI MALI ZA AINA NA UKUBWA WOWOTE HUKU LIKIZIACHA ZIKIWA SALAMA WAKATI WOTE.

  KWA UTOAJI WA HUDUMA YA HARAKA NA UHAKIKA ZAIDI FIKA SASA OFISINI KWETU KINONDONI BIAFRA-BLOCK41, MTAA WA KUMBUKUMBU JIJINI DAR-ES-SALAAM AU WASILIANA KWA NAMBA 0222 669066, 0713 972615 au 

  tuma kwenda S.l.p. 105497
  Barua pepe: msamaauctionmart@yahoo.com 
  Nukushi: 0222 667900

  “TUTUMIE TUKUTUMIKIE”

  0 0


  Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.Picha na Mo Blog


  Mgeni rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.
  Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.
  Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
  Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
  MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.
  Mgeni rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akipokea shada la maua kutoka kwa watoto Ilsa na Alaisa ikiwa shukrani kwa kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights. Kushoto ni Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed.  Ilsa na Alaisa wakiimba wimbo wa Taifa kubariki sherehe za ufunguzi wa jengo hilo.

  CEO wa VFX Dubai Yusuf Thakur akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed akielezea wageni waalikwa jinsi watakavyoweza kufaidika na mikopo itakayotolewa na Benki hiyo ikiwemo kupata kipindi cha marejesho ya mkopo kwa miezi 120, viwango nafuu vya riba, kiwango cha juu cha umri wa mkopaji ni miaka 60 kufikia kipindi mkopo unapotolewa na mkopo huo unapatikana kwa hela za madafu na dola za Marekani.

  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant akifafanua namna wateja wa Benki ya Exim watakavyoweza kunufaika na mkopo kwa ajili ya kununua nyumba zilizopo katika jengo la Uhuru Heights.

  Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.

  CEO wa VFX Dubai Yusuf Thakur akiendesha zoezi la mauzo ya nyumba katika jengo la Uhuru Heights ambapo mteja wa kwanza Samantar Abdinur Iusuf (kulia) aliyejitokeza kununua makazi katika jengo hilo.

  Mgeni rasmi Mh. Tajammul Altaf akimpongeza mteja wa kwanz baada ya kununua moja ya nyumba kuashiria uzinduzi wa idara ya mauzo na wageni wengine pia kuendelea na manunuzi wakati wa uzinduzi huo.

  Balozi wa Japan nchini Tanzania Salome Sijaona ( wa pili kushoto) akizungumza jambo la msingi wakati wakitembelea maeneo mbalimbali ya jengo hilo na Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi. Kushoto ni mgeni rasmi Balozi Tajammul Altaf.

  Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Safi Theatre wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la kisasa la biashara na makazi la Uhuru Heights jijini Dar.

  Waziri wa zamani Mh. Juma Ngasongwa akizungumza jambo na baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi huo.

  Mh. Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na Waziri wa zamani Mh. Juma Ngasongwa na wageni wengine wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights.

  Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamililki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.

  Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wageni, viongozi wa Serikali na wafanyabiashara wakubwa nchini waliohudhuria uzinduzi wa Jengo la Uhuru Heights.

  Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya ICB wakitoa maelezo ya jinsi ya kupata mikopo ya nyumba kupitia benki hiyo.
  Mgeni rasmi Balozi Tajammul Altaf na mwenyeji wake wakiwa ndani ya moja ya vyumba vya makazi ndani ya jengo hilo.
  Balozi Tajammul Altaf akingalia muonekano wa mandhari ya jiji la Dar akiwa gorofa ya 12 ndani ya jengo jipya la Uhuru Heights.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
  Wasichana warembo na watanashati wa Kitengo cha Mauzo cha Uhuru Heights wakipozi na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
  Pichani Juu na Chini ni Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamililki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na waandaji wa uzinduzi huo.

  0 0

  Pichani Juu na Chini ni Lundo la matawi ya miti yanayodaiwa kukatwa na Shirika la Umeme Tanesco nakuachwa chini ya kizagaa hovyo bila kujulikana utaratibu wa kuyazoa. Eneo hili ni karibu na Hotel ya Southern Sun kuelekea jengo la Pam Residence maeneo ya Ocean road jijini Dar.

  ====== ====== ======  =========  ======

  Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie akizungumzia changamoto kampuni hiyo inayokumbana nazo wakati wa kutekelezaji wajibu wao wa kufanya usafi na kutolea mfano kubwa likiwa la matawi ya miti kuachwa hovyo barabarani.

  Amesema Kampuni yake inashughulika na Domestic Garbage lakini swala la miti liko nje ya kazi za kampuni hiyo na kuashauri kuwa ingekuwa vizuri mtu anapotaka kukata miti awasiliane nao waweze kushauriana juu ya uzoaji wa taka hizo.

  Amesema taka za aina hiyo zinazongeza gharama kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kuwa magari yake ni maalum kwa ajili ya kubeba Domestic Garbage hivyo yoyote atakayetaka kufanya zoezi la kukata matawi ya miti pembezoni mwa barabara za jiji anapaswa kutoa taarifa mapema.

  Kampuni ya Green Waste Pro Ltd imekuwa ikilishitumu shirika la Umeme Tanesco kwa kukata matawi ya miti na kuyaacha yakizagaa katika barabara na kuwa hiyo si mara ya kwanza shirika hilo limekuwa likifanya hivyo mara kadhaa, kwani kipindi cha nyuma waliwahi kuacha matawi barabarani na kampuni hiyo ikawajibika kuingia gharama ya kuzoa taka hizo na ilipowaandikia Invoice ya kwamba wamechafua mji na kampuni hiyo imechukua jukumu la kufanya usafi hivyo inawadai walikaidi kulipa.

  Leo kampuni hiyo imeendelea na zoezi la kukata matawi ya miti na kuyaacha katika barabara tofauti za jiji yakizagaa hovyo huku haijulikani nani anawajibika kwenda kuzoa.  Lundo la matawi ya miti lilotelekezwa na Tanesco katika maeneo ya karibu na ofisi za Shirika la Afya duniani WHO.

  Hapa ni ukuta wa Chuo cha usimamizi wa fedha IFM.  0 0


  0 0


   Rais Kikwete akiongea na wadau

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akihutubia.

   Waziri wa Ujenzi Dkt John Pome Magufuli akiongea na wadau

   Mwenyekiti wa Jumuiya wa Watanzania waishio Ufaransa Deli Makombe akisoma risala meza kuu
   Wadau mkutanoni.
   Wadau oye!


   wadau
   JK akiongea
   Mdau Collins Mtita wa Daily News na wadau
   Wadau wa Diaspora wa Ufaransa
   Wadau zaidi
   Wadau


   Balozi Dorah Msechu na mdau
   Wadau hawana mbavu
   Mama Salma Kikwete akisalimia kadamnasi

   Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akiongea


   Waziri na Nishati na Madini Profesa Sospeter  Muhongo akiongea
   Wadau


   JK akifurahi na watoto na wadau
   JK na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Ufaransa
   JK na Balozi na maafisa wa ubalozi
   JK na wadau
   Dkt Magufuli
   Prof Muhongo akiongea na wadau
   JK akiongea na wadau
   Profesa Mohamed Sheya, Naibu Mwakilishi wa kudumu Unesco na wadau
   Haloooo tootoooooo juriiii...
   Wadau mkutanoni
   Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akisema machache
   Wadau mkutanoni
  Baadhi ya maofisa walioongozana na JK Ufaransa

  0 0


  MWENYEKITI wa kamati ya kuratibu Tamasha la kila mwaka la Pasaka, Alex Msama, amesema tukio hilo linalohusisha onyesho la muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi, ni la kila mtu kwani litaendelea kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza na walemavu. 

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Msama alisema ingawa wao ni waratibu, lakini lengo hasa la tamasha hilo ni kupata kiasi cha fedha za kuwapatia watu wanaohitaji msaada, kama vile watoto yatima, walemavu wa aina mbalimbali na wale wanaokumbwa na majanga makubwa. “Hili ni tamasha lao, wao ndiyo wadau wakubwa kwa sababu wananufaika nalo. Kila mtu ni shahidi kuwa tumekuwa tukitoa misaada ya aina mbalimbali kwa makundi maalum ya watu. 

  Hata hivyo, ni vyema pia tukaweka wazi kuwa wanaowezesha haya yote ni watu wanaokuja kuunga mkono tukio hili linalofanyika kila mwaka,” alisema Msama. Kuhusu tamasha la mwaka huu, Msama alisema hawezi kulizungumzia kwa undani kwa sasa kwa vile bado wanaendelea na taratibu za kupata kibali chake na wakishafanikisha suala hilo, wataweka wazi kwa umma ili ujue. Katika tamasha la mwaka jana lililofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, waimbaji mbalimbali maarufu walipanda jukwaani na kutoa burudani safi. 

  Miongoni mwao walikuwa ni Rose Mhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival. Waimbaji wan je walioshiriki tamasha hilo ni pamoja na Rebeca Malope wa Afrika Kusini, Maryanne Tutuma, Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa (Kenya), Faraja Ntaboba (Congo) na Ephraim Sekeleti.

  0 0


  Sauti za Busara music festival is taking a step back on the first day of the festival, February 14, in order to let Stone Town to shine. 

  This is the first day of ‘Busara Xtra’ - a day where Stone Town businesses throw open their doors to display shows of art, drumming and dance classes, music, and a sunset reggae party.  The Sober House will hold a daily art exhibition at Livingstone’s Restaurant, starting on 14 February and continuing throughout the festival.  The artwork of recovering addicts and alcoholics will be displayed at the exhibit, starting at 10:00 am. 

  The toughest choice visitors will have to make is not whether to come a day early, but which event to go to first! The sunset reggae cruise starts at 4:00 pm at Kae Funk Michamvi. Zanzibar’s popular Nadi Ikhwan Safaa will be performing at NIS Club House at 4:00 pm the same day.  No matter if your music style is old Taarab or new Sinachuki Kidumbak or anywhere in between, Stone Town has something for you with Busara Xtra. 
  Festival Director Yusuf Mahmoud says that the festival has always made it a point to benefit Zanzibaris. Since the festival began in 2004 the number of visitors to Zanzibar in February has gone up by 500%.  By training and employing local people and drawing so many visitors to the island each year, Sauti za Busara helps the people of Zanzibar. Busara Xtra is another way the festival contributes to the economic and cultural life of the island.“Busara Xtra increases opportunities for regional artists to showcase their work, for visitors to see different parts of the island, meet local people and widen participation in the festival by local communities in Zanzibar,” said Mahmoud.

  After warming up for the festival with Busara Xtra, Sauti za Busara’s main stage opens on 15 February and hosts performers until 17 February, 2013.  The Busara Film Programme will show three films that complement the music on the main stage.  The amphitheatre of the Old Fort will be transformed into an open air cinema where popular music videos will be displayed as well as the three feature length films.  For more information or to purchase tickets online, please visit www.busaramusic.org or purchase tickets at the door starting on 13 February, 2013. Tickets are Tsh 3,000/- for Tanzanians with special rates for East African residents.

  With special thanks to Sauti za Busara sponsors: HIVOS, Goethe Institute, Grand Malt, Memories of Zanzibar, Diamond Trust Bank, ChemiCotex, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., Southern Sun, Embassy of France, Alliance Française, SMOLE II and all of our sponsors and supporters

  0 0

   Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika katika onesho lake maalumu la kumtambulisha mwimbaji mpya wa bendi hiyo Othumani Kambi wa pili kulia wengine ni Hassani Moshi kushot Eddo Sanga na Juma Katundu onesho lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni
  Mashabiki wa bendi ya msondo music wakicheza kwa furaha wakati wa onesho maalumu la kumtambulisha mwimbaji mpya wa bendi hiyo Othumani Kambi Picha na www.burudan.blogspot.com

  0 0

  The Exim Bank Managing Director Anthony Grant (left) shakes hands with the Cosmos Group Chairman Muhammad 0wais Pardesi during the launch of Uhuru Heights building in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the right is the International Commercial Bank (ICB) CEO Basser Mohammed.


  Exim Bank Tanzania has pledged to offer mortgage facilities to individuals and corporate companies seeking to acquire property at Uhuru Heights building in Dar es Salaam. This was revealed by the Exim Bank Managing Director during the launch of the magnificent building in Dar es Salaam at the weekend.

   The Exim Bank Managing Director Anthony Grant gives a speech during the launch of Uhuru Heights building in Dar es Salaam at the weekend. The bank is set to offer mortage facilities to facilitate buying of space in the new building. 
   he Exim Bank Managing Director Anthony Grant (right) shares a light moment with the Pakistan High Commissioner to Tanzania H.E Tajammul Altaf (left) during the launch of Uhuru Heights building in Dar es Salaam at the weekend.
   The Exim Bank Sales Executive Annette Kondoro explains a point to Former Tanzania Investment Centre (TIC) Executive Director Emmanuel Ole Naiko (left) on the bank’s mortgage facility during the launch of Uhuru Heights Building in Dar es Salaam at the weekend.
   he Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (left) shares a light moment with the Singida Urban Legislator Mohammed Dweji (right) during the launch of Uhuru Heights building in Dar es Salaam at the weekend.
  The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (left) shares a light moment with the Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Harry Kitilya (centre) during the launch of Uhuru Heights building in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the right is the Alexander Forbes Tanzania Limited Managing Director Sanjay Suchak .

  0 0

  Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida. 

  Matengenezo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani.

  Uongozi wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013. 


  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana  kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa jijini Harare,  walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo yaliyofanyika jana  jijini Harare Zimbwabwe. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea  Ikulu ya Harare  jana  kwa lengo la  kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt.  Landa John Nkoma kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati  ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe  Adadi Rajabu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare  baada ya kumaliza  mazungumzo yao.  Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la  kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita.  Dkt. Nkomo   alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare . Picha na OMR.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa Rais wa Seneti ya Ufaransa Mhe. Jean Pierre Bel, alipotembelea makao makuu yake jijini Paris.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiongea na Rais Mstaafu wa Ufaransa Mhe Valery Giscard d'Estaing na ujumbe wake katika hafla ya chakula cha usiku alichoandaa Rais huyo Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tanzania Wildlife Foundation jijini Paris.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa jumuiya ya Ismailia duniani,HH The Aga Khan alipomtembelea kwenye Hotel ya le Meurice jijini Paris. PICHA NA IKULU.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Seneti ya Ufaransa Mhe. Jean Pierre Bel, alipotembelea makao makuu yake jijini Paris.

  0 0

  Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Hair Industry ltd James Walwa - Jimmy akimkabidhi mbunifu wa mavazi nchini Ally Rehmtullah tiketi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Afrika Mashariki katika mkutano wa 'The Economics of the Africa Fashion Industry' utakaofanyika nchini Marekani mwezi wa Februari. Tanzania Hair Industry ltd ambao ndio watengenezaji wa nywele maarufu aina ya Darling ndio wadhamini wa safari ya mbunifu huyu kwenye mkutano huo wa kihistoria utakaofanyika katika Kikuu cha Havard nchini Marekani.

  Mbunifu mahiri wa mavazi nchini Tanzania Ally Remtullah amechaguliwa kuiwakilisha Africa Mashariki katika ‘East Africa Fashion Industry’ kuongea katika mkusanyiko wa Afrika Business Conference utakaofanyika Harvard Business School nchini Marekani.

  Akizungumza na Mo Blog jijini Dar es Salaam leo, Mbunifu huyo Remtullah amesema shughuli hiyo itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Marekani cha Harvard ambacho ni kikubwa kuliko vyote duniani itafanyika Februari tarehe 15 mwaka 2013.

  Akifafanua amesema kuwa kila mwaka Chuoni hapo kunafanyika mikutano ya ‘Africa Business Conference’ ikiwa na kauli mbiu tofauti na sasa mwaka huu yeye amechaguliwa kuwa mmoja wa wazungumzaji kuhusiana na ‘The Economic of Africa Fashion’.

  Ally Remtullah amesema kwa ujumla anaiwakilisha Afrika Mashariki katika kategori hiyo ambapo anatarajiwa kuzungumzia changamoto zinazoikabili na fursa zinazopatikana katika tasnia ya fasheni Afrika Mashariki, ikiwemo tatizo la umeme na gharama za manunuzi ya vitambaa vya Pamba ambayo kimsingi huzalisha katika ukanda huu.

  Amesema anafurahi kuchaguliwa na wandaaji hao kuziwakilisha nchi za Afrika Mashariki na sasa si kwenda tena kuonyesha mavazi, bali ni kuzungumza mbele ya wadau wakubwa wa kidunia kuhusu nafasi ya masuala ya ubunifu na uchumi.Wazungumzaji wengine katika mkutano huo ni pamoja na mbunifu maarufu wa Afrika Magharibi Ituen Basi kutoka Nigeria.

  Katika maandalizi hayo Ally amesema pamoja na kusoma vitu vingi kuhusiana na uchumi katika tasnia ya fasheni na gharama za uzalishaji za viwanda vya nguo, pia amekutana na wafanyabiashara wakubwa wa viwanda vya kutengeneza nguo hasa za kiafrika akiwemo Mfanyabiashara Mkubwa nchini Mh. Mohammed Dewji ambaye kwa namna moja ama nyingine amempa ushirikiano wa kutosha.

  Safari hiyo ya mbunifu wa mavazi nchini Ally Remtullah katika mkutano mkubwa wa kihistoria wa Boston nchini Marekani, imedhaminiwa na kampuni ya Tanzania Hair Industry Ltd, ambao ni wazalishaji wa nywele maafuru aina ya Darling.

  0 0


   Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu (Kushoto), akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Morogoro Amir Nondo (Kulia) na Mratibu wa mradi wa afya ya mama na mtoto wa Aga Khana Sisawo Konteh (Kushoto) , wakinyanyua mikono ikiwa ni ishara ya kushikana mikono pamoja  katika kuunga mpango wa huduma bora ya Afya ya mama na Mtoto kwa Mkoa wa Morogoro.

   Mratibu wa mpango wa kuboresha afya ya Mama na mtoto ( JHI)  wa Aga Khan, Sisawo Konteh, akizungumza na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunga mkono huduma bora za afya kwa mama na mtoto kwa mkoa wa morogoro. 

  Mratibu wa Mpango wa kuboresha afya ya mama na mtoto, (JHI)  wa Aga Khan, Sisawo Konteh, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa afya ya mama na mtoto kwa Mkoa wa Morogoro. Mradi utakao wezesha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa mama na mtoto, Pamoja nae ( Katikati) Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo, na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu.

  Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akifungua Shampeni katika uzinduzi wa Mpango wa Afya bora kwa Mama na mtoto kwa Mkoa wa morogoro. Pamoja nae ni Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan Morogoro, Dr Hugo Yeste.

  =========  ===========  ===========
  Kituo cha huduma ya Afya cha Aga Khan chazindua Mradi wa kuboresha  Afya ya mama na mtoto Morogoro
  •        Ni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
  •        Mradi umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Canada
  •        Hii ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia 4 na 5

  Morogoro, Januari 2, 2013 – Kituo cha Huduma za Afya cha AKHS kimezindua mradi ambao utachangia kuboresha huduma ya afya ya  mama mjamzito na mtoto nchini Tanzania uzinduzi uliofanyika mkoani morogoro.

  Mradi huo unaojulikana kama Tushikane Mikono Kuboresha huduma kwa Wajawazito, na Afya ya Mtoto (Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI), umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Canada (CIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania.

  Mradi huo wa JHI ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs 4 na 5, ambao umelenga kuchangia kuboresha uzazi kwa wajawazito na watoto wachanga, (MNCH) katika mikoa mitano ya Tanzania.

  Mradi huo utatekelezwa kupitia Kituo cha Huduma ya Afya cha Aga Khan nchini Tanzania (AKHST) na vituo vyake vitano vya afya ya awali (PMCs) kwenye mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, na Morogoro ikiwa na lengo la kujenga uwezo wa huduma za Afya kwa jamii na kuimaimarisha uhusiano na huduma ngazi ya rufaa.

  Aidha, Mradio huo wa JHI unajivunia Shirika la Kimataifa la CIDA juu ya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania na mtazamo wake juu ya nia yake ya kipaumbele kwenye sekta ya afya nchini. Mradi huo pia utatumika kwa kuinua uwekezaji mkubwa uliofanywa na CIDA pamoja na serikali katika kutekeleza mikakati yake.

  Malengo ya mradi huo wa JHI ni pamoja na: kuboresha ubora wa huduma kwa wajawazito, Afya ya Mtoto na kulenga kuongeza uwezo wa maeneo ya mradi; kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za Wajawazito, Watoto na Afya ya Mtoto na kulenga watu wa kipato cha chini na makundi ya wakazi maskini, na hasa katika kuongeza uwezo wao wa kupata nafuu wa kupata huduma, ubora wa huduma za Afya ya uzazi na Wajawazito, Watoto na huduma ya Afya kwa mtoto katika ngazi ya kwanza ya vituo vya Afya; na kuboresha njia za afya, usafi na lishe ya familia kwa walengwa husika (MNCH) kuongeza mahitaji ya huduma (MNCH) ubora kwa walengwa; na kuongeza maarifa uhamisho na kubadilishana juu ya masuala muhimu katika Ushirikiano MNCH Umma muktadha (PPP).

  Mradi wa JHI wa kuboresha  Afya ya mama na mtoto ulizinduliwa Julai 2012 nchini Tanzania na unatarajiwa kuendelea hadi mwaka 2015.

  Mhina Shabani.

  Media Executive GDCC

  0 0


  Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar                       

  Jumla ya Shilingi Bilioni 12 zimetumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo 820 inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeo ya Jamii TASAF kwa Awamu ya Pili ya Mfuko huo  Unguja na Pemba.

  Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Khalid Suleiman ameyasema hayo leo katika Warsha ya siku mbili ya kuwajengea uelewa wa Awamu ya Tatu ya TASAF juu ya ‘Mpango wa Taifa wa kunusuru Kaya Maskini’ kwa Wajumbe wa Kamati za uongozi na menejiment za TASAF –Zanzibar huko ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.

  Amesema katika Miradi hiyo jumala ya Miradi 433 imetekelezwa kwa upande wa Unguja na Pemba imetekelezwa 387 ambapo Wananchi wa Zanzibar kwa ujumla wao waliweza kuchangia Shilingi Bilioni 1.3 za Miradi hiyo.

  Aidha amefahamisha kuwa Zanzibar kwa ujumla iilifanya vyema katika kutekeleza Miradi hiyo licha ya changamoto mbalimbali zilizojitekeza kwa kipindi hicho cha Awamu ya pili ya TASAF.

  Akifungua Warsha hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amewataka wasimamizi wa TASAF kuhakikisha kuwa Fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi hiyo zinatumika ipasavyo ili kutimiza maelengo ya Mfuko huo.

  Amesema licha ya Zanzibar kufanya vyema katika Awamu ya Pili ya TASAF viongozi hao wanapaswa kuyaendeleza mema yote yaliyofanywa katika Awamu mpya ikiwa ni pamoja na kuziba mianya yote ya ubadhirifu wa pesa za miradi hiyo.

  Balozi Seif ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kuunga mkono utekelezaji wa Mpango huo katika Shehia za Unguja na Pemba ili kuondoa umasikini kwa manufaa ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

  Amefahamisha kuwa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini utaimarisha uwazi, uwajibikaji na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa kubaini Walengwa katika Shehia.


  Balozi Seif amewataka Washiriki wa Semina hiyo kushiriki kikamilifu na kuwa makini ili kufahamu vyema taratibu na miongozo ya utekelezaji wa Awamu hiyo ya Tatu ya Mfuko huo na hatimaye kufanyia kazi kikamilifu.

  Awali akitoa Shukrani zake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga ameishukuru Serikali na Wananchi kwa ujumla kutokana na ushirikiano walioutoa katika Awamu zilizopita na kuomba mashirikiano hayo yaendelezwe kwa Awamu ya Tatu.

  Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa akitoa shukrani kwa niaba ya Washiriki amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif kuwa watatumia uwezo wao wote kuhakikisha Miradi ya maendeleo ya TASAF inasimamiwa vyema na kufikia lengo lililokusudiwa.

  Warsha hiyo ya TASAF Awamu ya Tatu inaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi na kuwashirikisha Wakuu wa Mikoa ya Unguja na Pemba,Wakuu wa Wilaya na Menejiment za TASAF –Zanzibar ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu awamu hiyo Mpya. 

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR  22/01/2013


  0 0

   Marubani   wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo asubuhi.

  Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
   Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam. 

  Kapteni  Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8 Q300 Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22.Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.

  0 0

   -Profsa wa Kitivo cha Sheria  Chuo kikuu Dar es Salaam Palamagamba Kibudi akiwaelezea jambo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charlzi Kitwanga kabla ya Semina ya Kukuza Uelewa Juu ya Masuala ya Matumizi y Bioteknolojia ya Kisasa Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula kushoto Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu waRais Eng Ngosi Mwihava'

  Dk Emmarold Mnemeya akitowa Mada ya Kukuza Uelewa juu ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa kwa Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamu wa Rais JIji Dar es Salaam.{Picha na Ali Meja].
   Baadhi ya washiriki wa Semina ya Kukuza Uelewa juu ya Masuala ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia wakimsikiliza Mtoa Mada Profesa Palamagamba kabudi alipotoa sheria ya Mazingira kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani akiuliza masuala mara baada ya kutolewa Mada Kuhusu Masuala ya Bioteknolojia ya kisasa kwa uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya mtaa wa :Luthuli Jiji Dar es Salaam. 

  Profesa Kitivo cha Sheria chuo Kikuu Palamagamba Kibudi akitoa Mada ya Sheria ya Mazingira kwenye Semina ya Kukuza Uelewa Juu ya Masuala ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa kwa Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jiji Dar es Salaam. 

  0 0


  Na Kambi Mbwana,
   Dar es Salaam.

  HALI ya mkoani Mtwara ni dhahiri inatishia amani, hivyo kuna kila sababu ya serikali na wadau wote kukaa na kuliangalia suala hilo kwa marefu.

  Nikiwa kama Mtanzania, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mno sakata hilo la gesi inayopingwa na wadau kuletwa jijini Dar es Salaam, badala yake wanataka ibaki mkoani Mtwara, ingawa wenye akili ndogo wanapinga au kutukashifu kadri ya uwezo wao, wakijidanganya kuwa sipaswi kufuatilia mambo ya Mtwara na Lindi.

  Huu ni udhaifu na hauwezi kuchekewa, maana ni dhahiri Mtwara, Lindi ni sehemu ya Tanzania kama ilivyokuwa Tanga, Arusha, Kilimanjaro na kwingineko. Wananchi hao waliojikusanya kwa ajili ya kupigania sakata hilo, wamefikia kubadilisha kabisa hisia zao, bila woga wowote katika kulizungumzia suala la gesi.

  Kama nilivyowahi kuhoji hapo nyuma, kuwa tatizo ni gesi, choyo, siasa au ubaguzi? Makala haya yalitoka katika blog hii ya Handeni Kwetu na kupokea maoni mbalimbali.

  Na haya ndio maoni ya Watanzania hao wanaoishi mkoani Lindi na Mtwara.

  Mwanzo wa ugaidi Tanzania ni mwisho wa amani. Kusini hawaogopi jeshi. Kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ipo kwenye mioyo yao. Leo nasema, ila wana Mtwara watasema kwa sauti zao, maana vitisho kwao ni kama kuitukana maiti. Chochote kitatokea iwe ni vita vyovyote vile 2015 hatutaki uchaguzi na hatutaki pia tuletewe kiongozi na ole wenu, +255712897794.

  Kaka nimefurahishwa na makala yako isemayo Tatizo ni ni gesi, siasa, choyo au ubaguzi? Inaonekana na wewe pia umeandika makala hii kwa lengo lako binafsi. Umeshindwa kutoa uhalisia wa jambo lenyewe, badala yake umeandika kwa lengo la kutaka kumfurahisha ama kuwafurahisha watu fulani.

  Rudi nyuma angalia wanachofanyiwa wakulima wa korosho wa Mtwara je ni sahihi? Lile zao halisaidii kuinua pato la Taifa? Angalia hali ya maisha ya wakazi wa Mtwara. Nadhani umekurupuka na si mawazo yako kuna mkono wa mtu nyuma yako.

  Nenda kazunguuke na kufanya utafiti wa kina utapata majibu sahihi kwa wenyeji.+255657614354 Tatizo la mikoa ya Kusini sio gesi bali ni kusahauliwa kwa miaka 51 ya Uhuru. Korosho, reli, Bandari, miundo mbinu, tatizo la elimu na kuwa waanga wa ukombozi wa nchi zilizopo kusini mwa Afrika.

  Wanasiasa kujiingiza katika hoja si ajabu kwasababu duniani kote wanasiasa ndio huibua matatizo ya wananchi , maana wasomi wetu wengi hawana meno ya na ndio wanaopitisha mikataba mibovu . Sio choyo, lakini tunafikia wakati tunajuta kwa nini sisi Mtwara Lindi tumekuwa sehemu ya Tanzania. Tuna rasilimali tosha za kuweza kuitwa, kama vile Bandari, Bahari, Ardhi yenye rutuba, watu, mito, madini, korosho, ufuta, mhogo na nyinginezo.
  Kusini tuna haki ya kumdai mume wetu Tanzania haki zetu za msingi, maana tumevumilia mno hadi kilio cha kwi kwi. Ni mimi mwanaharakati,  Amoni, wa Kata Msangamkuu, Mtwara Vijijini. +255652221100.
  Ninaomba uelewe lengo la wananchi wa Mtwara na Lindi sio kwamba hawataki gesi isitumiwe na wengine hapana, wao wanataka kiwanda kitengenezwe Mtwara.
  Kule itoke gesi safi, maana wanakataa mambo yasijekuwa kama ya madini ya Geita ambayo mwekezaji anachimba anaenda kuhakiki Mwanza na kulipa kodi ya uwongo na kuiibia nchi na kuwa masikini, huku wakifaidi watu kutoka nje.
  Nimesoma makala yako, inayosema tatizo ni gesi, siasa, choyo au ubaguzi? Mimi nimeisoma na kwa utafiti wangu, nimegundua kwamba wewe ni CCM na ndio maana ukaona eti ni siasa. Hapana, ni kwasababu vyama vya upinzani vinapenda maendeleo ya Watanzania.
  Mbona hawakuhamisha miwa kutoka Kagera na kuileta Dar es Salaam ili itengenezwe hapa? Pili, hebu fikiria gharama za kuweka bomba ni kiasi gani?
  Tatu, kumbuka msongamano mkubwa wa watu, ina maana wakiongeza viwanda wanazidisha msongamano. Nne, kwanini wasiwaachie watu wa Mtwara na Lindi na wao wapate ajira?
  Tano, kila kilichokuwapo Dar es Salaam, Mtwara kipo kama vile Bandari na mengineyo.+255713221244.
  Ingawa hujaonyesha wazi ujumbe unaopeleka kwa wana Mtwara, lakini ninachofahamu, Taifa halina rasilimali. Mikoa, wilaya, vijiji, ndivyo vyenye rasilimali, kama vile mbuga za wanyama, madini, mazao na mengineyo ambayo mapato yake hukusanywa na kuwa pato la Taifa.
  Gesi ni kama rasilimali nyingine tu. Ikiwa Mtwara, Lindi, Kigoma, Mbeya au popote nchini, tueleze ni vipi italinyima Taifa letu pato? Au italigawa vipi Taifa? +255717757797.

  Hongera bwana Kambi Mbwana kwa makala yako. Endelea kuwapa elimu Watanzania wenzetu wasioelewa. Naitwa Moi, +255757295249.

  Unajua sisi tunaotoka Mtwara tunafananishwa na nyani katika Taifa hili. Hatuna thamani mbele ya makabila mengine toka Uhuru.

  Barabara haijaisha, mazao yetu hayana usimamizi na hatuna huduma za jamii zilizo bora. Tukipata wakarimu, sio bora pamoja na watumishi wote.

  Sisi ni jamii ya mwisho katika Taifa hili, hujiulizi gesi na mafuta aliyotupatia Mwenyezimungu ingekuwa sehemu nyingine ingehamishwa?

  Kwakuwa sisi nyani, hatuna thamani, gesi itaondoka na mafuta pia yataondoka, maana hawa hawatatuthamini milele. +255712848839.

  Asante kwa makala yako, lakini usiwe mwandishi mwoga anayeogopa watawala walioshindwa kuwaondolea wananchi umasikini na kuligawa Taifa, kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho. Jitahidi kuwa mkweli ili upate mafanikio maishani mwako.+255755045295.

  Kijana mbona unakuwa kama popo asiyejulikana kama ni mnyama au ndege. Ya Handeni Kwenu yamekushinda sasa umehamia kwenye gesi.

  Nasikitika ujumbe huu uliotumwa kwa namba +255757602075. nimeufipisha kwa sababu za kimaadili, maana ulijaa matusi na kashfa kutoka kwa mtumaji, ambaye pia hakujitambulisha jina lake.

  Kaka nimesoma makala zako nyingi, nimegundua wewe ni kada wa CCM na usiyejua nini wanachokitaka Watanzania.
   Hata hujui huko vijijini watu wanaishi vipi. Unaogopa ya Daudi Mwangosi na Amina Chifupa na huo sio uzalendo, hivyo hupaswi kuwa mwandishi.

  Hivi unajua CCM wanaiendashaje nchi hii? Umeshahoji wananchi wangapi kuhusu maisha yao badala yake unamfuata Nape Nnauye, unataka CCM ndio waiongoze nchi milele na milele kwakuwa wewe si mzalendo. Ujumbe huu ulitoka kwa namba +255652273836.

  Nashukuru brother kwa kuweza kupata fursa ya kuweza kusoma makala yako. Ni kweli hoja zako ulizozisema zinaweza kushabihiana na ukweli,  ila kutokana na vile hali ilivyo naweza (kudetermine ya words) nazo yanatokana na siasa pia.

  Hebu nambie kaka angu, umaskini uliopo katika mikoa ya kusini, moja kwa moja tumekuwa maskini na hii ilikua nafasi pekee ya kuweza kupata ahueni.

  Hebu jamani isifike wakati tukawa tunaangalia swala hili kijuu juu, hali ni mbya kusini hatuna pa kushikia, serikali ilibidi iangalie gesi hii pia katika kutafuta namna ya kuikomboa miji hii ya kusini.

  Ni wazi kuwa serikali imekua ikifurahia tu kupata neema hiyo kuendesha mambo yao na si kusaidia kuondosha umaskini.
  Nyinyi waandishi tunawategemea kutoa hoja za kusaidia kuondokana na majanga ya kimaskini. Ujumbe huu ulitumwa kwa njia ya barua pepe kutoka kwa Raya Juma, 

  Nashkuru
  Haya ni baadhi ya maoni yaliyoingia mara baada ya kuandika makala ile, huku watu wakiingia moia kwa moja katika hoja yangu ya siasa, ubaguzi na choyo nilizokemea.

  Kwanini nasema siasa? Ukiangalia hapo, wapo waliotuma ujumbe huo wakiwa na chukia serikali ya CCM. Hata hivyo, kuyaanika maoni yao si kuwaletea matatizo, bali kusoma mawazo ya watu wa Mtwara.

  Wao ndio wahusika. Ndio wenye kupigania suala la gesi, hivyo inaweza kuwa njia muafaka ya kuepusha shari inayozidi kujengeka mioyoni mwa Watanzania, hususan wale wanaoishi mkoani Lindi na Mtwara.

  Watu wamekuwa na mawazo tofauti juu ya sakata hilo. Wapo wale wanaofikia kutamani Mtwara iwe na utawala wake, jambo ambalo hakika si la kuchekea.
  Rasilimali za Tanzania zinaanza kutugawa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, ndio maana nikaamua kuyaanika mawazo ya ndugu zetu hao.
  Kwa kumalizia tu, sakata la gesi linaweza kujadiliwa upya kwa kuwashirikisha wadau na wananchi wa Mtwara, hasa kwa kupewa mikakati ya namna ya serikali kuwapelekea maendeleo maana ni wajibu wao.

  Masuala ya chokochoko ya gesi yasiachwe tu kwa wanasiasa ambao wamekuwa wabunifu kuingia kwenye hoja zinazoshirikisha watu kwa ajili ya kujijenga kisiasa, jambo ambalo si zuri.
  Na sisi tunaofikia kujadili suala la gesi, wakiwamo wana harakati, wasitumie maneno makali, maana siku zote jazba inaondosha maana husika.

  Maoni mengi ya Watanzania nimeshindwa kuyaandika kwa kwasababu hayajatolewa kiungwana, huku niliyoaandika nikiyafanyia marekebisho mengi mno.

  Katika hili, serikali kwa kupitia Waziri wake wa Nishati na Madini, Professa Sospeter Muhongo, anapaswa kukaa na kulijadili jambo hili kwa mapana yake.
   

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU),Dr. Salim Ahmed Salim ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, mara baada ya Mh. Lowassa kutoa maonai yake mbele ya tume hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba mpya,mara baada ya kutoa maoni yake.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Mjumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya,Dk. Senkondo Mvungi mara baada ya kutoa Maoni yake.

  YAFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASAA:

  Kwanza ningependa kukupongeza wewe mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume nzima kwa imani kubwa ambayo Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu hilo zito na muhimu kwa nchi yetu.

  Wananchi pia wamekuwa na imani kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa tume hii. Kutokana na hilo wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine hayahusiani na katiba, yaani siyo ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa miongoni mwao, kwa hiyo naomba radhi mapema, iwapo maoni yangu haya mengine , yataonekana si ya kikatiba.

  Katiba yetu ya sasa ni nzuri, imetuongoza katika umoja na mshikamano wa kitaifa kwa muda wote huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni vyema kuwepo na katiba mpya ili kuendana na hali halisi.

  Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.

  1.ELIMU BURE

  Moja ya haki za mtoto ni kupata elimu. Ningependa suala la elimu bure ya sekondari liwemo kwenye katiba yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya sekondari ni bure.Nchi yetu bado ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni masikini.

  Uwezo wao wa kipato ni mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali inaweza kugharimia elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya kujenga taifa lijalo lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata elimu ya sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.

  Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa  watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo, kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.

  2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT

  Katiba ya sasa haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 inatamka kiujumla tu kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI WAKE KULINDWA.

  Lakini , haki hiyo inanyang'anywa na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16(penal code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya kifo(death penalty or capital punishment) kwa kosa la mauaji ya kukusudia.

  Adhabu hiyo hiyo pia utolewa kwa kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA NA ADHABU YA KIFO HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.

  3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI

  Katika sehemu nyingi hapa nchini mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni kiasi gani cha fedha ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika kampeni.Iainishe ni matumizi gani ya lazima ambayo mgombea hawezi kukwepa kutumia fedha katika kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura kwenda kupiga kura gharama hizo nani azibebe.

  Katiba ifafanue rushwa ni nini kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa PROPORTIONAL REPRESENTATION ,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi kuwania majimbo na siyo wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama chake kupata kura nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii itasaidia kuondoa kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze kuwania uongozi.

  4.ARDHI

  Kwa mwanadamu, kunyang'anywa haki ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni sawa na kunyanng'anywa haki ya uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa nguvu wakulima katika suala la ardhi, na kuwasahau wafugaji.

  Wafugaji wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao, ile ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka kutafuta malisho huku nyuma imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima au wawekezaji, hili kwakweli si jambo jema .

  Tumeshuhudia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi ningependa katiba hii mpya impe mfugaji haki katika suala la ardhi kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe, ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe na hali ya 50,50 situation kati ya mfugaji na mkulima katika suala zima la umiliki wa ardhi,kikatiba!

  0 0
 • 01/22/13--20:19: taarifa ya chadema

 • NDUGU waandishi wa habari,

  Kuna mambo mengi yamezungumzwa kuhusu CHADEMA. Nanyi waandishi wa
  habari mmekuwa mkitupigia simu, mmoja mmoja kutaka ufafanuzi na
  msimamo wa chama chetu kuhusiana na masuala hayo. Leo tumeamua kuwaita
  hapa ili kuwapa ufafanuzi mkiwa pamoja badala ya kila mmoja kuuliza
  akiwa kwenye chumba chake cha habari.

  Kwanza, CCM kupitia kwa viongozi wao waandamizi, akiwemo Nape na
  Mwigulu, wanazunguka zunguka huko, kuwaambia Watanzania kuwa CHADEMA
  inakufa, tena wanatengeneza hata sababu za kifo, wanasema ni ubaguzi
  na kutokana na laana ya Mwalimu Nyerere.

  Tunataka kuwaambia hivi: Kwamba CHADEMA haina ubaguzi na hivyo haiwezi
  kufa leo wala kesho, mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa
  Watanzania. Na bahati mbaya, CCM wanaona CHADEMA kitakufa, wanasahau
  kuona kuwa chama chao tayari kinakufa tayari sasa.

  Kama suala ni laana ya Nyerere. Laana hiyo haiko CHADEMA; iko ndani ya
  CCM kwa sababu tatu.

  (i) Mwalimu wakati wa uhai wake, kwa kushirikiana na waasisi wengine,
  alijenga misingi ya utaifa wetu, ambapo CCM wameamua kuivunja kwa
  maslahi ya wachache. Akiwa bado hai, Mwalimu alitunga hata kitabu
  akasema CCM kimeoza na kinakuka rushwa. Akaongeza CCM kuna kansa ya
  uongozi na uchaguzi ndani ya chama hicho, ni gulio la wala rushwa.
  Maneno hayo ni laana tosha.

  (ii) CCM kinapata laana ya Mwalimu kwa sababu kimerasimisha ubaguzi
  kwa wanachama wao, viongozi wao na Watanzania kwa ujumla. Ni hawa hawa
  CCM wanaoeneza uongo wa hatari, wakiwatisha wananchi kwa kusema
  CHADEMA kina ukabila, mwaka 2005 walimzushia Dk. Salim Ahmed Salim
  uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa
  wasisi wa taifa hili, Abeid Amani Karume. Uchafu ulifanywa na wana CCM
  wa kundi la wanamtandao ambao leo ndiyo wanaongoza chama na serikali
  na ubaguzi huu dhidi ya Dk. Salim ndiyo uliowafanya washinde.

  (iii) CCM kinakufa pia kwa sababu ya laana ya ubaguzi wa kukiuka haki
  za raia. Ninyi ni mashahidi namna ambavyo baadhi ya makundi ya
  wafanyakazi yamekuwa yakibaguliwq katika kupata stahiki zao. CCM na
  serikali yake, imekuwa ikijibu kwa kauli za kejeli na vitisho, ikiwemo
  kutekwa na kuteswa kwa viongozi wa wafanyakazi na kisha kutupwa katika
  Msitu wao wa Mabwepande na baadaye kulinda wahalifu kwa visingizio
  vingi vya kulindana huku wakichezea maisha na uhai wa Watanzania
  wenzetu.

  Hivi unaweza kuielezea vipi hali ya serikali ya CCM kutowalipa wazee
  wastaafu waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama si
  ubaguzi! Wazee ambao wametumikia taifa hili kwa uwezo wao, akili zao
  na miili yao, wenzao wote katika nchi nzingine zilizokuwa zikiunda EAC
  wakati ule, walishalipwa, isipokuwa hapa Tanzania ambapo chama
  kinachotawala kimeamua kufanya ubaguzi wa haki za watu, nani apate na
  yupi asipate.

  Itakumbukwa kuwa wazee wale kutokana na kuyumbishwa na kubaguliwa
  katika kupata haki zao, waliamua kuvua nguo barabarani, pia kwa kiburi
  na ukosefu wa heshima ya serikali ya CCM kwa wananchi, wakawachapa
  viboko wazee wale! Laana ya wazee hawa inakiua CCM.

  Hivyo basi, CCM kinakufa kutoka na laana hiyo na uongo uliosababisha
  na kushindwa kutekeleza ahadi zake za maisha bora, ajira kwa vijana na
  kuwezesha wanawake.

  CCM wajiandae kufuata njia za vyama vya KANU ya nchini Kenya, UNIP ya
  Zambia na chama cha ukombozi nchini Malawi.

  Ndani ya CHADEMA kuna baraka za Mwalimu Nyerere. Hakuna laana. Ninyi
  ni mashahidi kuwa kabla ya Mwalimu kufariki dunia, alikimwagia sifa
  CHADEMA kwa kusema ni chama makini.

  Tofauti ya CCM na CHADEMA

  Kwenye mikutano yao, sasa CCM wamejipatia majukumu wasiyoyamudu ya
  kujifanya ni maofisa waenezi wetu na moja ya majukumu waliyoamua
  kujipachika na kuyafanya ni kuwaonesha Watanzania, moja ya tofauti
  kati yetu na wao, ambazo ni uwezo wa kuchukua hatua na kuwa na sera
  sahihi mbadala kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Watanzania.

  Kwenye mkutano wao uliomalizika hivi karibuni na kwenye shughuli zao
  za kila siku, CCM sasa wameamua ‘kuimba’ sera za CHADEMA, hasa zile za
  elimu bure na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi. Mambo ambayo miaka
  miwili tu iliyopita walikuwa wakiimba kinyume chake. Bahati mbaya
  hawana uwezo wa kuzitekeleza, kwa sababu si mawazo yao na hawana
  utashi huo.

  Hili la pili la kuchukua hatua…bahati mbaya kwa sababu ya kuelemewa na
  kansa ambazo tumezitaja hapo juu, CCM wanaona kuchukua hatua ni
  ‘kufukuzana’, maneno ambayo hata jana wakati wakizungumza na waandishi
  wa habari wameyarudia. Hawawezi kuona kwa sababu wote ni wachafu,
  wanaishi hivyo kwa kukubaliana.

  Ndugu wanahabari, hii ni moja kati ya tofauti nyingi zilizopo kati ya
  vyama hivi viwili, ambazo zimeifanya leo CHADEMA ndiyo tumaini la watu
  wanaodai haki na uwajibikaji, tumaini la watu katika kupigania uhuru
  na mabadiliko ya kweli nchini, kimbilio la watu wasafi dhidi ya
  ufisadi, wanaopinga ubadhirifu na dhuluma ya CCM, ni tofauti hizo
  zinakifanya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani na mbadala
  kinachoaminiwa na Watanzania kukabidhiwa dola.

  Tukiwa chama imara na makini kinachoaminiwa na kubeba matumaini ya
  Watanzania, tutachukua hatua mbalimbali, dhidi ya makosa tofauti
  tofauti, kulingana na uzito wake, kama vile uzembe, udhaifu,
  ubadhirifu, ufisadi na usaliti.

  Tuwachukulia hatua hata wale ambao wametumwa na CCM kuja kufanya kazi
  ya chama hicho kupitia kwa jina la CHADEMA.

  Ni uwezo na uthubutu wa kuchukua hatua mbalimbali, ndiyo umekuwa moja
  ya sababu kubwa ya Watanzania kuiunga mkono CHADEMA kila tunaponyoosha
  mkono kuikemea CCM na serikali yake juu ya ufisadi, ubadhirifu na
  uminyaji wa haki za Watanzania.

  Zamani, CCM kilipokuwa bado chama cha siasa hasa, ambapo kilikuwa
  kinasimamia misingi ya umoja wa kitaifa bila kujali dini ya mtu,
  kabila au rangi; kilipokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi
  rushwa na ufisadi, yaani CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere na waasisi
  wengine waadilifu, hakika kilikuwa na uwezo wa kufukuza kila
  aliyeonekana kwenda kinyume na misingi yake.

  Ni katika kipindi hicho, CCM kiliwavua uongozi na uanachama baadhi ya
  waliokuwa viongozi wake. Kwa mfano, Maalim Seif Shariff Hamad, Hamad
  Rashid Mohammed, Sudi Yusuf Mgeni, Fortunatus Lwanyantika Masha na
  wengineo. Baadaye mwaka 1984 kilimfukuza uongozi (msisitizo uongozi)
  aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
  Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, kwa kukiuka misingi yao.

  Lakini leo hii, CCM hakiwezi kuchukua hatua hiyo hata kwa katibu wa
  tawi. Kwa sababu, hiki si chama cha siasa tena. Hili ni genge la
  wahuni, waliojikusanya pamoja na kujiita chama cha siasa. Ni wezi wa
  raslimali za taifa, waliotayari kulirejesha taifa kwenye utumwa kwa
  maslahi yao binafsi.

  Ndiyo maana wameshindwa kuwafukuza mafisadi, badala yake ndiyo
  wanaoongoza chama na kuwatawala. Walisema wanataka kujivua gamba (la
  nyoka) baadae wakagundua kuwa gamba lao halisi (ufisadi) ni gamba la
  kombe, ambalo ili livuke ni lazima kobe afe!

  CCM ya sasa, hakiwezi siyo tena kutetea wafanyakazi na wakulima.
  Hakitetei tena maslahi ya wanyonge. Kimebeba na kukumbatia ufisadi na
  mafisadi wa kila aina, na wabadhirifu wa mali za umma, ambao
  wameyafikisha maisha ya Watanzania na nchi yao hapa yalipo.

  Lakini CHADEMA inachukua hatua kwa sababu hiki ni chama sikivu na
  kinachobeba matumaini ya wananchi. Hivyo, hatuko tayari kumuacha mtu
  yeyote ambaye anafanyakazi za CCM ndani ya CHADEMA, kisha kujiita yeye
  ni mwana-Chadema. Tutamfukuza.

  Huwezi kuzusha uongo kwa viongozi wako na chama chako, kisha ukataka
  uachwe. Usijadiliwe. Usiguswe. Tutakujadili na tukibaini kuwa una
  makosa, tutakuomba ujirekebishe. Ukikataa, tunakuambia hutufai.
  Ondoka. Ukishindwa, tunakufukuza.

  CCM kupitia mawakala wao wanasema: CHADEMA kinapokea ruzuku kubwa,
  lakini kimepanga ofisi. Hii nyumba ni mali ya Chadema. Lakini mbona
  hao mawakala wa ‘status quo’ hawasemi kuwa CCM haina ofisi? Maana ile
  inayoitwa ofisi ya CCM Makao Makuu Dodoma, ni mali ya Mamlaka ya
  Ustawishaji Makao Makuu (CDA).

  Huyu Nape hana hata maadili ya uongozi. Alifukuzwa kwenye UV-CCM baada
  ya wenzake kumwambia amezusha uongo. Baada ya kuitwa kujitetea,
  akasingizia kuwa alilishwa maneno na waandishi wa habari. Kumbe
  wenzake walikuwa na mkanda wa hotuba yake aliyoitoa pale Peacock
  Hotel. Wakampa aisikilize. Eti ndipo akakiri na kuomba radhi. UV-CCM
  chini ya Emmanuel Nchimbi, ikamwambia hutufai. Muongo wee. Ikamfukuza.
  Sasa mtu ambaye amethibitishwa na chama chake kuwa muongo, atawezaje
  kutusumbua CHADEMA?

  Wala tunachofanya hapa siyo kujibu maneno yake, bali tunaweka rekodi
  zake sawasawa. Tunataka umma umfahamu vizuri, kwa sababu wasiomjua
  wanaweza kuamini maneno yake.

  Kauli za Mwigulu Nchemba

  Tunataka kuwaambia wahusika wa usalama na ulinzi nchini, hususan Rais
  Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na
  Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid, nini maana ya tafsiri
  ya habari za kutunga, lakini za hatari sana za Mwigulu Nchemba;

  (i) Kwamba suala la yeye kusema CHADEMA inapanga mauaji, tunataka
  kumwambia Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said
  Mwema na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othuman Rashid kuwa, kwa
  sababu wamekuwa kimya na kukubaliana na uzushi wa hatari wa Mwigulu,
  tafsiri yake ni kwamba Jeshi la Polisi limeasi na sasa linafanya kazi
  kwa maelekezo ya CHADEMA. Linatekeleza amri za CHADEMA!

  Kwa sababu, iko wazi. Watanzania na dunia inajua kuwa mauaji yenye
  utata yanayohusishwa na siasa, yamefanywa na Jeshi la Polisi. Ushahidi
  upo. Polisi wameua watu Arusha, polisi wameua watu Songea, polisi
  wameua mtu Morogoro, polisi wameua mwandishi wa habari, Daudi
  Mwangosi.

  Orodha ya mauaji ya vitendo vya mauaji vinavyofanywa na Jeshi la
  Polisi nchini ni ndefu, kwa malengo ya kisiasa ya CCM. Lakini kama
  Mwigulu anasema, hiyo ni mipango ya CHADEMA, maana yake ni kwamba
  Jeshi la Polisi linatekeleza mipango ya chama hiki, tafsiri ya haraka
  hapo, Mwigulu anamaanisha, “basi jeshi limeshaasi.”

  Sasa mtu anayetangaza ‘uasi’ wa jeshi kwa kiwango cha kutekeleza
  mipango ya chama cha siasa badala ya kumsikiliza Amri Jeshi Mkuu,
  serikali inamnyamazia na kumchekea!

  Tumeitaka serikali kufanya uchunguzi huru kwenye matukio ya mauaji
  yanayohusishwa na siasa, ikiwemo tukio la kifo cha kada na kiongozi wa
  CCM huko Ndago, Singida, lakini wamekaa kimya. Badala yake wanatunga
  uongo na kumtuma Mwigulu atangaze na kueneza.

  (ii)Tafsiri nyingine ya maneno ya kutungwa hayo kisha anatumwa Mwigulu
  kutangaza, ni kwamba vyombo vinavyohusika katika ulinzi na usalama,
  vimeshindwa kazi. Ni maneno ya aibu kwa IGP Mwema na Othman Rashid,
  kwamba wao wameshindwa kazi zao na sasa wamemkabidhi Mwigulu, ambaye
  anaweza kuingia kwenye vikao vya CHADEMA, akarekodi, kisha badala ya
  kuwapelekea hao wenzake, ili serikali ya chama chake ichukue hatua,
  anazunguka nao kulia kwenye vyombo vya habari! Na wahusika wamekaa,
  wanamsikiliza na kumchekea!

  Tunaomba tuwaambie, tuko makini sana. Hiki ni chama kinachojiandaa
  kushika dola, kuwatumikia wananchi. Tunajua mipango yao katika hayo
  maneno ya Mwigulu. Tunaelewa wanachotaka kufanya. Tunafahamu hata
  kesho wanataka kufanya nini. Tuko imara. Tunawaambia Watanzania
  waendelee kutuunga mkono, katika harakati hizi za ukombozi wa nchi
  yetu.

  Asanteni sana kwa kunisikiliza.


  Imetolewa leo tarehe 22 Januari 2013 na:

  …………………………………………………

  Benson Singo Kigaila,

  Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo (CHADEMA).

older | 1 | .... | 14 | 15 | (Page 16) | 17 | 18 | .... | 1898 | newer