Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1495 | 1496 | (Page 1497) | 1498 | 1499 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Elizabeth Masao akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, katika hafla ya kukabidhi vya kula kwa watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre vilivyotolewa na kikundi cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni. (Na Mpiga Picha Wetu).
  Mwenyekiti wa Jogging Club Kinondoni Majani Mrope akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, katika hafla ya kukabidhi vya kula kwa watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre.
  Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Kinondoni Elizabeth Masao, akikabidhi baadhi ya vitu kwa mtoto anaelelewa na kituo cha yatima cha Maunga Centre Thabiti Amili, vilivyotolewa na kikunda cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni.
  Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Kawawa Kata ya Hananasifu Kinondoni Elizabeth Masao, akikabidhi baadhi ya vitu kwa mtoto anaelelewa na kituo cha yatima cha Maunga Centre Thabiti Amili, vilivyotolewa na kikunda cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni.
  Baadhi ya wana kikundi cha Hananasifu Jogging Club Kinondoni, wakimkabidhi vitu.
  Picha ya pamoja.
  0 0

  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akiongea na wajasiliamali mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifunga mafunzo yaliyokuwa yameandaliwa na SIDO jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuzipa thamani bidhaa wanazozitengeza. Pembeni yake ni Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna -KAJUNASON/MMG.
  Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga akitolea ufafanuzi mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wajasiliamali mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa kuzipa thamani bidhaa zao wanazozitengeneza. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga anayemfuatia wakifurahia jambo na wajasiliamali mara baada ya kuhudhuria sherehe ya kufunga kwa mafunzo yao.
  Wajasiliamali wakifurahia bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo.
  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akipata maelekezo ya bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo. 
  Wajasiliamali wakipokea vyeti.
  Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle akiwa katika mazungumzo na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror kabla ya wawili hao hawajasaini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror wakiweka saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel. Makubaliano hayo yataanza kwa kuijengea uwezo hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma ambapo Israel itasaidia ujenzi wa Kitengo cha dharua na mifupa pamoja na ujenzi wa Kitengo cha kisasa cha wagonjwa mahututi (ICU).
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini. Watatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda.

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo jioni.
  Bao za Simba Sc leo hii zimefungwa kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 timu zote mbili zikiwa 0-0. Bao la kwanza limefungwa na Said Ndemla na bao la pili limefungwa na John Bocco baada ya mabeki wa Kagera Sugar kujichanganya.
  Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.  
  Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.
  Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) akipeta baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya timu ya Kagera Sugar.
  Mara baada ya Mchezo huo kumalizika Msemaji wa klabu ya Simba Sports Club, Haji Manara ambaye ameshuhudia mchezo huu Mbashara akiwa  jukwaa kuu ameipongeza Timu ya Kagera Sugar japo pamoja na kupoteza mchezo huo amesema waendelee hivyo hivyo ili waweze kuumaliza msimu huu wakiwa nafasi za juu kama msimu uliopita. hapo hapo ameimwagia sifa kemukemu Timu yake Simba kwa kurejea kileleni.
  Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya Simba SC hii leo kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba jioni hii kwenye Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara. 
  Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Timu Kagera Sugar.  
  Mwamuzi akiwa na Manahodha wa Timu zote mbili Kagera Sugar vs Simba Sc muda mfupi kabla ya Mechi kuanza, akiwaonesha ni yupi anafunga huku na yupi anafunga kule.Nohodha wa Timu ya Simba John  Bocco(kulia) akielezwa jombo na Mwamuzi.
  Picha ya pamoja
  Timu zote mbili zikisalimiana kabla ya mtanange kuanza.
  Wachezaji wakimsikiza Mgeni ramsi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.
  Wachezaji wa Timu ya Simba Sc wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati anawapa neno kabla ya mtanange kuanza. 
  Wachezaji wa Timu ya Kagera Sugar nayo wakimsikiza kwa Makini.
  Wachezaji wa Akiba wa Timu ya Kagera Sugar wakiwatazama wenzao uwanjani hii leo kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba.
  Msemaji wa klabu ya Simba Sports Club, Haji Manara akiutazama mchezo huo akiwa meza kuu sambamba na mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu na Viongozi wengine.
  Raia wa Kigeni nao walikuwa macho Kaitaba kuucheki mchezo huo uliokuwa wa kukata na Shoka ambao Simba wameitafuna Miwa ya Kagera Sugar.
  Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.
  Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.
  Kapombe akipongezana na mshambiliaji wa Simba Emanuel Okwi (nyuma) ni Kichuya.
  Mchezo ukiendelea kaitaba John Bocco akigombea mpira wa kichwa na Mchezaji wa Kagera Sugar.
  Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso akikimbiza mpira akiwa sambamba na mshambuliaji wa Kagera Sugar Emmanuel Okwi.
  Kadi ya Njano ilitolewa kwa mchezaji wa Kagera Sugar Fakhi
  Emmanuel Okwi akiwa Chini chaliii!!
  Mshambuliaji wa Kagera Sugar akimwangalia Mwamuzi juu ya rafu aliyotendewa na Mchezaji wa Kagera Sukari.
  Okwi akiwa chini
  Mlinzi wa Kagera Sugar Asante Kwasi akijutia kukosa nafasi ya kufunga bao
  John Bocco akiwa chini na mwezake wa Kagera Sugar baada ya patashika kutokea...kipindi cha pili.
  Jukwaa kuu wakiutazama mchezo
  Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakiutaza mchezo Kagera sugar dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.
  Hakuna kupita!! hapa!
  Mchezaji wa Kagera Sugar alimdhibiti mchezaji wa Simba kupita hapa!
  Kichuya akijiandaa kupiga kona.
  Mavugo wakati huo akipiga jalamba
  Wakisubiri mpira wa kona
  Patashika kwenye lango la Kagera Sugar kipindi cha pili
  Juma Kaseja akimcheki John Bocco
  John Bocco akimtoka Mohamed Fakhi wa kagera Sugar
  Baada ya kumtoka aliachia pasi kwa Mdemla aliyemalizia nyavuni na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwenye Viti kwenye Uwanja wa Kaitaba.
  Shangwe kwa Ndemla
  Kapombe akiambaa na mpira kumsonga kipa wa Kagera sugar Juma Kaseja.
  Wakipongezana kwa bao
  Mashabiki wakishangilia nao wa Timu ya Simba baada ya kufunga bao
  Raha kwa Mashabiki wa Simba  Mwinyi Vehicle(kushoto) akiwa na Mwinyi mwenzake (kulia) wakati wa Mtanange huo ukiendelea jioni ya leo, Simba Kashinda bao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
  Mashabiki wa Timu ya Simba leo wameingia kwa wingi kwenye Dimba la Kaitaba kuwapa sapoti wenzao wakati wa mchezo huo wa Kagera Sugar vs Simba SC.
  Wachezaji wa Kagera Sugar baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamepoteza mchezo huo wa bao 2-0 mbele ya timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Etihad Airways senior executive, Andrew Fisher, jets off from Abu Dhabi International Airport to Shanghai ahead of his round the world record-breaking attempt.

  Abu Dhabi, UNITED ARAB EMIRATES – Senior Etihad Airways executive, Andrew Fisher, embarks on a journey of a lifetime on 21 January when he attempts to break the world record by flying around the globe in the shortest time frame on scheduled flights, and with the fewest number of sectors.

  Fisher, who works as the airline’s Vice President Fleet Planning, hopes to shave three hours off the current record of over 55 hours by completing the journey in only four sectors.

  His flight path begins in the early hours of Sunday morning in Shanghai, taking him to Auckland, Buenos Aires and Amsterdam before returning to the Chinese city in the early hours of Tuesday morning, 23 January.

  A self-proclaimed ‘aviation geek’ with a love of studying airline networks and schedules, Abu Dhabi-based Andrew is well placed to chart his journey and fulfill a dream he has been keen to attempt for over 20 years.

  “It’s about time the job was done,” he said. “The planning has taken a long time, essentially to ensure the flight timings, routings and transits are kept as tight as possible and there is only a short window of opportunity for this to happen.”

  The progress of Andrew’s record-breaking attempt can be followed on Twitter at @AndrewFisherNZ

  0 0

  VIJANA wajasiriamali wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamefanikiwa kujinyanyua kiuchumi kwa kukusanya sh40 milioni, kupitia kikundi cha kuweka na kukopa (SACCOS) waliyoianzisha kwa vikundi 68 kujiunga nayo, kati ya vikundi 97 vya ujasiriamali vilivyosajiwa. 

  Kati ya vikundi hivyo 68, vilivyojiunga na SACCOS, hadi sasa vikundi 12 vimepata mikopo, ambapo kila kikundi kina wanachama 30 sawa na watu 360 wameanza kunufaika kupitia sh40 milioni kwenye mikopo wanayokopeshana. 

  Katibu wa UVCCM wilayani Simanjiro, Bakari Mwacha aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa wa Manyara Mosses Komba alipofanya ziara ya siku moja. Mwacha alisema kupitia SACCOS hiyo vijana hao wanachukua mikopo na kurudisha kwa wakati na uaminifu kupitia shughuli za ujasiriamali wanazozifanya. 

  Alisema wanatoa ombi kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutoa kipaumbele kwa vijana hao kuwapatia ile mikopo ya asilimia 5 ya mapato ya ndani kwani wataweza kuirejesha kwa wakati tofauti na vijana wengine. "Hawa wana uzoefu hata wakipewa mikopo inakuwa kwenye mikono salama tofauti na wengine ambao wakipewa wanasuasua kurejesha ila vijana wetu watakuwa na uhakika kwani wana SACCOS yao," alisema Mwacha 

  Alisema vijana wengi wanajiunga na uanachama kwenye jumuiya hiyo ambapo hadi sasa wapo 9,205 na wengine wapya 139 wamejiunga mji mdogo wa Mirerani. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Mosses Komba aliupongeza uongozi wa UVCCM wilaya ya Simanjiro, kwa kusimamia ipasavyo vikundi hivyo hadi kupatikana kwa fedha hizo na kujinufaisha kiuchumi. 

  "Mmekuwa mfano bora kwa vijana wa mkoa wa Manyara, kwani wilaya nyingine zinapaswa kuiga mfano wenu wa kuchangamkia fursa za kuongeza kipato," alisema Komba. Alisema baada ya kuwa na vikundi hivyo suala la kupatiwa mikopo na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, litakuwa rahisi kwani ninyi mtakuwa na uzoefu wa kufanya ujasiriamali. 

  Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel alisema atahakikisha anapigania upatikanaji wa asilimia tano ya mikopo kwenye halmashauri ya wilaya ili vijana wapate mikopo. Mollel alisema vijana wa Simanjiro wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kujijenga kiuchumi na kujitolea nguvu kazi ili kutekeleza ilani ya CCM. 
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara Mosses Komba akipokewa na wanachama wa CCM wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro alipoanza ziara yake ya siku moja.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewataka mahakimu wa mkoa huo kutekeleza wajibu wao ipasavyo wakati wanaposikiliza kesi na kutoa hukumu kwa haki ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi. 

  Akizungumza kwenye ziara yake ya kwanza ya siku saba katika Wilaya ya Simanjiro, Mnyeti alisema kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya maadili, hatakubali kuona wananchi wanalalamikia kukosa haki. 

  Mnyeti alisema baadhi ya mahakimu wanajigeuza kuwa miungu watu na kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hivyo kusababisha malalamiko kwa wananchi. "Hatuwezi kukubali kuona mambo kama hayo, yakifanyika kama kuna mtu anaona kuna mahakimu siyo waadilifu wanakula rushwa na kushindwa kutoa haki nijulisheni," alisema Mnyeti. 

  Awali, mkazi wa mtaa wa Njiro, Theopista Paulo alisema amekuwa akinyanyasika wakati akidai haki yake. Theopista alisema mmoja kati ya mahakimu wa eneo hilo alikuwa anamwambia hata kama akimkataa na kesi yake kuhamishwa kwenye mahakama nyingine hawezi kushinda chochote. 

  Hata hivyo, Mwanasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Peter Mangala alisema mwananchi yeyote ana haki ya kumkataa hakimu endapo atakuwa na sababu za msingi. Mangala alisema endapo mwananchi akiwa na hoja za msingi anazozipinga anaweza kumkataa jaji au Hakimu atakapobaini kuwa hawezi kutendewa haki. 
   Wananchi wa Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakitoa kero kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Pastory Mnyeti. 
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
  Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
  Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe. 
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo. 
  Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe. 

  NaJoel Maduka-Geita.

  Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .

  Mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Japhet Simeo alisema lengo kuu la hizo fedha ni kuboresha miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.

  Simeo alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500 kwenye kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga majengo manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.

  Juma Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .

  Aidha amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
  Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.


  Na Fredy Mgunda-Iringa


  Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

  Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

  Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

  Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao kwa ajili ya faida ya maisha yao.

  “Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa

  Aidha Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

  “Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

  Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

  “Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

  Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

  “Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

  Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.

  “Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

  nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

  “Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema walimu

  Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.

  Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu.

  Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

  “Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

  Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

  “Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(wa pili kuli) akiwapongeza wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kozi walizosomea 
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(katikati),Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(wa pili kulia),Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wasichana. 


  Arusha.Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameuagiza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) uwe umefunga vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Sh 14 bilioni ndani ya wiki nne badala ya siku 67 ili vianze kutumika mara moja.

  Ametoa agizo hilo kwenye mahafali ya tisa ya wahitimu 465 wa fani mbalimbali za ufundi jijini hapa kuwa ukarabati na upanuzi wa karakana ufanyike ndani ya muda alioutoa ili vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

  "Nilipotembelea Chuo hiki Desemba 2,mwaka jana nilitoa maagizo mharakishe ujenzi na ukarabati wa miundombinu itakayotumika kufunga vifaa hivyo kutoka Austria,nafarijika kusikia kuwa utaanza mara moja kwani Wizara ilishatoa kibali cha kutumia watalaam wenu wa ndani na fedha mnayo,"alisema Ole Nasha

  Alisema sekta ya elimu ya ufundi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2015 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate maendeleo.Ole Nasha aliongeza kuwa elimu ya ufundi ina mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda na nchi zilizoendelea kama Japan na China zimefikia hapo zilipo kwa kutilia mkazo elimu ya ufundi.

  "Katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 hadi 2020/21 tunalenga kuongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi(Veta) kutoka 150,000 hadi 700,000 na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyotoa elimu ya Kati kutoka 40,000 hadi 80,000,"alisema 

  Kuhusu idadi ya wasichana wanaosoma elimu ya ufundi kuwa ndogo alivitaka vyuo vyote vya ufundi nchini kuweka mikakati ya kuongeza udahili ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele maalum kwa kwa wanafunzi wa kike wanaomba kujiunga.

  Pia aliagiza Mamlaka ya Elimu nchini(TEA)kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi cha Sh 1.7 bilioni kilichotengwa kwaajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana katika Chuo hicho ili kupunguza pengo katika wavulana na wasichana.

  Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Masudi Senzia alisema wahitimu 465 wamemaliza katika ngazi za Astashahada ya awali,Astashahada ,Stashahada na Shahada huku wahitimu wa kike ni 101 sawa na silimia 21 na wahitimu wa kiume ni 364 sawa na asilimia 78.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi-Bagamoyo

  NAIBU Waziri Wa Nishati Subira Mgalu, ameridhishwa na kasi na kazi anayoendelea nayo ,mkandarasi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya III, Sengerema huko kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wilaya ya Bagamoyo ,Mkoani Pwani.

  Aidha amelitaka shirika la umeme (Tanesco) wilaya ya Bagamoyo, kukimbizana na wakati kwa kuwapa wananchi fomu za kujaza ili kupatiwa umeme wakati zoezi la kuweka nguzo likiendelea katika baadhi ya vijiji.

  Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kijiji cha Kongo ,kata ya Yombo na Visezi kata ya Vigwaza na kujiridhisha na kazi ya mradi huo inavyoendelea .Mgalu alisema mkandarasi huyo ameahidi kumaliza kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao na kwa uhakika anakwenda vizuri.

  Alieleza kwasasa amekuta wanaendelea na kazi ya kusimamisha nguzo na maeneo mengine yanatarajiwa kutandaza nyaya ."Mkandarasi Sengerema yupo Mkoa wa Iringa na Pwani ,ameanza kazi vizuri na ndivyo tunavyohitaji ,tunaomba aendelee na kasi hii ili wananchi wapate huduma hii ya umeme haraka" alisisitiza Mgalu.

  Naibu waziri huyo,alitoa tahadhali kwa wakandarasi wengine wa mradi wa REA kwenda na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano,na atakaefanya kazi chini ya kiwango hatakuwa na masihala nae.

  Pamoja na hayo ,alilitaka Shirika la Umeme (TANESCO) mkoani Pwani,kwenda kuhakiki nguzo 120 zilizotelekezwa chini miaka mitatu mfululizo,.kwenye vijiji hivyo ,ili kujua kama bado zinauwezo wa kutumiwa

  Mgalu alisema, nguzo 60 zilizopo kijiji cha Visezi na nguzo nyingine 60 kijiji cha Kongo ,zilipelekwa na mkandarasi MBH kwa maelekezo ya umeme vijijini (REA)awamu ya II ,ambae alifanya uzembe .

  Alieleza ,Tanesco ihakikishe inahakiki nguzo hizo bila kufanya ajizi kwani serikali ilishamlipa fedha mkandarasi huyo awamu iliyopita ,hivyo itakuwa ni hasara kubwa kuziacha nguzo hizo pasipo kuzifanyia kazi .Mgalu alisema mkandarasi huyo ,hatoshi na amechelewesha huduma ya umeme kwa wananchi na atachukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wakandarasi wababaishaji na wazembe.

  ”Ninaomba zikaangaliwe kama zinawezekana kufanyiwa kazi ,zitumike katika maeneo ambayo zitafaa kupelekwa ,kuliko kuendelea kukaa chini na kusababisha maswali ’alisema.

  Mgalu aliwaeleza wakazi wa Visezi kuwa kijiji hicho kinatarajia kupata umeme kupitia mradi wa umeme unaotekelezwa katika mkoa wa Pwani na baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam ikiwemo Kigamboni (PERI-URBAN).

  Nae mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,alisema anaimani na wizara ya nishati na nia nzuri ya serikali kwa kupeleka umeme katika vitongoji vyote na hakuna kitongoji kitakachoachwa.

  Alisema ,kijiji cha Visezi kimezungukwa na fursa za chama cha ushirika cha umwagiliaji,gesi,ukaribu wa bandari kavu ya Kwala ,hivyo kinapaswa kupatiwa huduma ya umeme ili kunufaika na kuinua uchumi wake.

  Ridhiwani ,alieleza ni wajibu wa wakandrasi na Tanesco kufanya kazi inayotarajiwa na jamii ili kuwaletea maendeleo wanayoyategemea .Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kongo,waliipongeza serikali kwa kuwasogezea huduma ya umeme karibu na wanaamini maendeleo yataongezeka.

   Naibu Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu mwenye kitambaa chekundu kichwani ,akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo la Bagamoyo.dk.Shukuru Kawambwa wa pili kushoto na wengine ni viongozi mbalimbali wa kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wakati alipokwenda kutembelea maeneo yanayotekelezwa mradi wa umeme vijijini (REA )awamu ya III ,ambapo amejiridhisha na kasi anayoendelea nayo mkandarasi Sengerema.(picha na Mwamvua Mwinyi)
   Nguzo 60 za umeme zilizotelekezwa ndani ya miaka mitatu huko kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza pasipo kufanyiwa kazi ,jambo linaloelezwa ni uzembe uliofanywa na mkandarasi MBH aliyepewa kazi awamu ya pili ya mradi wa umeme vijijini (REA )ambapo ameitia hasara serikali na kuchelewesha huduma ya umeme kwa jamii(picha na Mwamvua Mwinyi)
  Naibu Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza kuhusiana na masuala ya huduma ya umeme.
   Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo kuhusiana na changamoto ya nishati ya umeme huko kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
  VIONGOZI wa Ngazi za juu wa Serikali ya Abu Dhabi wakihudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa makaazi wa Mfalme wakati wa mkutano huo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi. kulia Balozi wa Tanzania Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nossor Mbarouk.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mwenyeji wake , Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE), baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
  Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)akimtambulisha Mtoto Aaliyah Al Mansoori kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohahed Shein, wakati wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) wakitoka katika Jumba la Kiongozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi ya Kiongozi hiyo Nchini Abu Dhabi.

  Picha na Ikulu

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, Tarime

  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Comrade Ngemela Lubinga jana (22/01/2018) ameanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

  Ziara hiyo ni sehemu ya kufuatilia (monitoring) utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika mkoa wa Mara.Comrade Lubinga ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Tarime ambapo alikutana na wanufaika wa Mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya masikini katika Vijiji vya Gamasala Kata ya Nyandoto na Remagwe katika Kata ya Regicheri.

  "Watendaji wa TASAF na wote wenye dhamana Serikalini, timizeni wajibu wenu na jitumeni zaidi katika kutatua changamoto za Wananchi wanyonge hawa na masikini ili nao wapate nafuu ya maisha," alisisitiza.

  Vilevile, Comrade Lubinga amekemea tabia za ubadhilifu wa mali ya umma na kuonya kuwa watendaji wa aina hiyo hawana nafasi katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari, Rais Dk John Magufuli."Serikali ya awamu tano iliyoundwa na CCM imedhamiria kuleta mabadiliko makubwa ya utumishi na kujenga nidhamu ya kazi katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania na hasusan wanyonge," alisema.

  Ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa CCM katika kuisimamia Serikali yake kutekeleza Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015. "CCM katika utaratibu wake wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani yetu, tumebaini changamoto katika mpango wa kupunguza umaskini na tumekuja kusikiliza kero za wananchi wetu ili kuzipatia majawabu," alisema Lubinga.

  CCM mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk John Pombe Magufuli, imeazimia kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wake wakiokipa dhamana ya kuwaongoza, alisema. Ziara hiyo inaendelea leo.

  0 0

  Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe, Sylvester Mabumba (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji wa Comoro, Bw. Said Mohamed Omar (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group pamoja na wajumbe waliofuatana nao katika ziara maalum ya kufungua na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania na Comoro.
  Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya comoro pamoja na Wajumbe kutoka clouds Media Group wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Comoro, Bw. Mouzamildine Youssouf.


  BALOZI wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro,  Sylvester Mabumba ameupokea ujumbe wa Clouds Media Group uliowasili visiwani humo Januari 20 mwaka 2018.

  Upo kwenye ziara maalumu ya siku tatu ikiwa na lengo la kushirikiana na ubalozi kuzitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana visiwani humo kwa Watanzania. Ujumbe huo wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba uliwasili Comoro kutokana na mualiko wa Ubalozi wa Tanzania hapa Comoro

  Ambapo lengo lake lilikuwa ni kuja kufanya tathamini ya kuzindua Jukwa la Fursa (FURSA EXPO) Visiwani Comoro kama sehemu ya kuendeleza kampeni za kuwapatia vijana wa kitanzania taarifa muhimu kuhusu fursa za uwekezaji na biashara.

  Ubalozi wa Tanzania Visiwani Comoro kwa kushirikiana na Ujumbe wa Clouds Media Group umelenga ifikapo Aprili mwaka 2018 kupanua mianya ya uwekezaji nchini Comoro na kuhakikisha masoko ya uhakika yanapatikana kwa ajili ya bidhaa za Tanzania hasa katika kipindi hiki ambapo Uchumi wa Tanzania unaelekea kuwa ni uchumi wa Viwanda. 

  Aidha, Balozi akiwa ameambatana na ujumbe wa Clouds Media Group amepata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na wadau kutoka sekta mbalimbali za Serikali ya Comoro, Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi. “Serikali ya Tanzania itaendelea kufungua maeneo mapya ya ushirikiano sambamba na kuhakikisha vijana wananufaika na ushirikiano baina ya nchi na nchi ulioanzishwa na mataifa yao” mesema Balozi

  Aidha, Mhe. Balozi alielezea anataraji ziara hiyo italeta matokeo chanya na kwamba kuzinduliwa kwa jukwaa la FURSA EXPO ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ambayo inalenga kwenye Diplomasia ya Uchumi na kwamba kupitia jukwaa hilo bidhaa za Tanzania zinauhakika wa kuingia kwenye Soko la Comoro kwani nchi ya Comoro inaitegemea Tanzania kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yake mbalimbali. 

  Pia ujumbe wa Clouds Media Group ulitumia nafasi hiyo kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Visiwani Comoro, Ndg. Said Mohamed Omar, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Kitaifa ya Utalii, Ndg. Mouzamildine Youssouf pamoja na Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Vijana. Katika mazungumzo hayo, wajumbe walionesha nia ya kutaka kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha kampeni itakayoibua maeneo muhimu ya kimkakati ambayo Vijana wa Kitanzania na wale wa KiComoro wanaweza kushirikiana.

  Naye Bw. Ruge Mutahaba kwa upande wake alieleza kufurahishwa na fursa mbalimbali zinazopatikana Comoro na kuahidi kuendelea kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Visiwani hapa kuhakikisha kwamba FURSA EXPO Comoro inafanikiwa na kuleta matokeo chanya kwa lengo la kuinua uchumi wa vijana wa Kitanzania na wa KiComoro.

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31,Januari 2018.  Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Hussein Kattanga.
   Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (kulia) kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi  31, Januari 2018. Kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Catherine Revocati.
  Msajili Mkuu wa Mahakama Catherine Revocati akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (wapili kutoka kulia) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga na Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali.(Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

  Rais Magufuli Mgeni Rasmi Siku ya Sheria nchini

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria itakayofanyika Februari Mosi mwaka huu.

  Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yenye maudhui ya ‘Matumizi ya TEHAMA katika utoaji haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili’.

  “Kila mwaka Mahakama ya Tanzania huadhimisha Siku ya Sheria ambayo huashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama, kwa mwaka huu maadhimisho hayo yatafunguliwa rasmi na Rais Magufuli katika viwanja vya Mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es Salaam,” amesema Jaji Mkuu Juma.

  Jaji Mkuu amesema kuwa kabla ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria, Mahakama ya Tanzania pamoja na wadau muhimu katika Sekta ya Sheria watatumia siku tano kuanzia tarehe 27 hadi 31 Januari mwaka huu kwa ajili ya kufanya maonesho yatakayotoa elimu kwa wananchi watakaopata nafasi ya kuhudhuria katika viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo jijini humo.

  Maonesho hayo yatatanguliwa na matembezi maalum ya kuadhimisha Wiki ya Sheria yatakayofanyika Januari, 28 mwaka huu ambayo yataongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yatakayoanzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mpaka viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo Rais Mstaafu Kikwete atazindua rasmi Wiki ya Sheria.

  Aliongeza kuwa Wiki ya Sheria inatoa nafasi nzuri kwa wananchi kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama pamoja na wadau wa sekta ya sheria ili kufanikisha maboresho endelevu ya Mahakama.

  Aidha, Jaji Mkuu Juma amewahakikishia wananchi kuwa Mahakama itaendelea kupokea malalamiko na mawazo kutoka kwa wananchi na kuyafanyia kazi hata baada ya Wiki ya Sheria kuisha.

  Wiki hiyo ya Sheria itaenda sambamba na uzinduzi wa majengo ya kisasa ya Mahakama yaliyokamilika yakiwemo ya Mahakama ya Mwanzo Kawe, Kituo cha kisasa cha mafunzo Kisutu pamoja na Mahakama ya WIlaya ya Bagamoyo, Mkuranga na Kigamboni.

  Wadau wengine watakaoshiriki katika wiki ya sharia pamoja na Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Taasisi ya Mafunzo ya Uanansheria kwa Vitendo Tanzania, Tume ya Kurekebisha Sheria, Chama cha Mawakili Tanganyika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi, na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega ameteketeza zana haramu katika Ziwa Victoria.Baadhi ya zana hizo zipo nyavu za Makila zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia katika kusafirisha Samaki haramu.

  Akizungumza leo na wananchi wa Mwembeni wilayani Chato mkoani Geita, Ulega amewata kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kuwafichuwa waharifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini au kwenda jela.''Serikali haitamuonea mtu huruma awe kiongozi au raia wa kawaida sheria itachukuwa mkondo wake.

  "Nia yetu ni kuona samaki wanaongezaka ziwa Victoria na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa lipate mapato pamoja na ajira kwa wananchi mbalimbali" amesema Ulega.Aidha amewaonya baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Lubondo kuacha tabia ya kupewa rushwa na wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua na kuwapatia fedha laki mbili hadi tatu.

  Amefafanua kuwa kwa sasa kuna oparesheni ya kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea maeneo ya Ziwa Victoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

  Aidha kiongozi wa oparesheni Gabriel Mageni ameongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku 13 baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa pamoja na madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato

  Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Chato,Shaban Ntalambe ,amewatahadharisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu akibainika na kitendo hicho Serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja anayejihusisha na shughuli hizo awe kiongozi mkubwa ama mtu wa kawaida.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega  akiteketeza nyavu haramu  zilizounganishwa zipatazo 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.
   Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi wilayani Chato mkoani Geita.
   Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akisisitiza jambo kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
   Mkuu  wa Wilaya Chato,Shaban Ntalambe akishiriki zowezi  la kutekeeza nyavu haramu
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameambatana na  Mkuu  wa Wilaya chato,Shaban Ntalambe wakielekea katika kisiwa cha hifadhi ya Lubondo.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha kushirikiana na wavuvu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 mshindi wa promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa, Roida Kipinya mkaazi wa Newala, Mtwara katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Tigo Pesa,  Hussein Sayed. Jumla ya mawakala 73,000 wa Tigo walishiriki  katika promosheni hiyo.

  Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (katikati) akimkabishi mfano wahundi ya shilingimilioni 10 mshindi wa pili katika promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa,Mojelwa Mlinga  mkaazi wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed. Jumla ya mawakala 2,281 wa Tigo Pesa walipata zawadi mbali mbali katika promosheni hiyo iliyodumu kwa kipindi cha mwezi  mmoja.

  Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani, George Lugata akimkabidhi mfano ya hundi ya shilingi milioni  2 mshindi wa kanda katika promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa, Vicky Ibrahim katika hafla iliyofanyika  katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari. Jumla ya Mawakala nane (8) wa Tigo Pesa walipata zawadi za TSH 2 milioni na shilingi 1  milioni kila mmoja baada ya kuibuka washindi katika kanda zao. 

  Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (aliyevalia tai katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa  promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa pamoja na wafanyakazi  wengine wa Tigo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni hiyo. Roida Kipinya wa Newala, Mtwara aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni 15, huku Mojelwa Mlinga wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam akijinyakulia shilingi milioni 10 katika promosheni hiyo iliyojumulisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa nchi nzima.  

  Wakala wawili wa Tigo Pesa wajinyakulia TZS 15 milioni na TZS 10 milioni kila mmoja.
  Tigo pia yatoa mamilioni ya fedha kama bonasi na zawadi kwa mawakala 2,281.  

  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tanzania, Tigo leo imegeuza mawakala wawili wa Tigo Pesa kuwa mamilionea katika promosheni yake iliyofika tamati leo.

  Roida Kipinya, Wakala wa Tigo Pesa kutoka wilaya ya Newala, mkoani Mtwara aliyepokea kitita cha TZS 15 milioni kutoka Tigo amesema, ‘Nimejawa furaha kubwa kwa kupokea zawadi hii kubwa kutoka Tigo Pesa kama shukrani kwa juhudi zangu za uwakala. Sasa nitaweza kukamilisha mahitaji yangu muhimu ya nyumbani pamoja na kupanua biashara zangu.’

  Kwa upande wake, Mojelwa Mlinga wa Pugu Mnadani jijini Dar es Salaam ambaye ameshinda TZS 10 milioni katika promosheni hiyo iliyodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja, aliielezea promosheni hiyo kama ya kwanza na ya kipekee kuwahi kutolewa na mtandao wowote ule wa simu kwa mawakala wake nchini.

  Akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bw Simon Karikari alisema kuwa nia kuu ya promosheni hiyo ilikuwa ni kurudisha shukrani kwa mawakala wa Tigo Pesa katika kipindi cha sikukuu na Mwaka Mpya.  ‘Nina imani kuwa tumefanikisha malengo na ndoto za mawakala wetu katika kipindi,’ alisema.

  Naye Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema kuwa Tigo imetoa zawadi na bonasi kwa mawakala 2,281 kutoka sehemu mbali mbali za nchi. ‘Pamoja na bonasi hizi kubwa, leo  Tigo pia inatoa zawadi za shilingi milioni mbili na shilingi milioni moja kwa mawakala nane kutoka sehemu mbali mbali za nchi,’ aliongeza.  

  Hussein alibainisha kuwa jumla ya mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walishiriki katika promosheni hiyo kote nchini. ‘Tunajivunia mchango wetu mkubwa katika kurahisisha upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha kwa watu wote nchini. Kupitia mtandao wetu mpana na uhakika wa mawakala wa Tigo pesa, tunaiwezesha jamii kutuma, kupokea na kufanya miamala ya fedha yenye mchango mkubwa katika uchumi wa watu binafsi, biashara, nchi na jamii yote kwa ujumla. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea pesa. Ni sehemu ya maisha.’

  Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.

  Kampuni ya Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini.  Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.

  Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.

  0 0

  Na Hamza Temba - WMU- Dodoma

  *Wanunuzi wataruhusiwa kuyakagua (Januari 25 na 26) kabla ya mnada
  *Watakaovuruga mnada kukiona cha mtemakuni

  SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) itafanya mnada wa hadhara wa meno ya viboko vipande 12,467 vyenye uzito wa kilo 3,580.29.

  Mnada huo utakaosimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango umepangwa kufanyika tarehe 29 Januari, 2018 kuanzia saa nne asubuhi katika Jengo la Mpingo, Barabara ya Nyerere Jijini Dar es Salaam, zilipokuwa  ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii (Ivory Room).

  Kupitia taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara amesema  mnada huo utawahusisha wafanyabiashara wa Nyara waliopewa leseni ya Nyara Daraja la Kwanza mwaka 2017.

  Amesema wafanyabiashara hao wataruhusiwa kukagua meno hayo kati ya tarehe 25 na 26 Januari, 2018 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa na nusu jioni kabla ya siku ya mnada huo.Aidha, amesema wanunuzi watakaoshinda mnada huo watatakiwa kulipa asilimia 25 ya malipo yote papo hapo na asilimia 75 itakayosalia itatakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne zijazo baada ya mnada huo.

  “Mtu yeyote atakayekuwa ametamka bei ya juu, kisha akashindwa kulipa asilimia 25 ya bei aliyotamka, atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga mnada na hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” ameonya Mkurugenzi huyo.

  Amesema meno hayo yatauzwa kwa wastani wa uzito wa nusu kilo bila kugawanywa au kuchambuliwa wakati wa mnada na wanunuzi wataruhusiwa kuondoa bidhaa kwenye eneo la mnada baada ya kulipia ada na kodi husika kikamilifu na kupewa hati ya kumiliki nyara hizo.
  Mnada huo utafanyika katika Jengo hili la Mpingo (Mpingo House) ambalo awali lilikuwa Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma. 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Dk. James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya 15 ya Jeshi Usu kwa kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro hivi karibuni Mkoani Katavi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.

  0 0

  Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa
  Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
  Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
  Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa 
  Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
  Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu  Na Fredy Mgunda,Kilolo

  MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi majengo kwenye shule nne za sekondari ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.

  “Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza

  Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.

  “Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza

  Masenza aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.

  “Jamani Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu wanakwenda shule” alisema Masenza

  Lakini mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000) na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000) pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.

  Aidha Masenza alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa mkoa wa Iringa kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

  “Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Masenza

  Sipia Kinyowa ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyanzwa, Amidu Kilamba diwani wa kata ya Nyanzwa,Hemerd Wiliamu diwani wa kata ya Ibumu na Justine Mgina mtendaji wa kata ya Ibumu ni baadhi ya viongozi waliompungeza mkuu wa mkoa kwa ziara aliyoifanya ya kimaendeleo na kimkatikati kuhakikisha wanafunzi wote wanatakiwa kufika shule na kusoma bila kubuguziwa na mtu yeyeto.

  “Leo tumefarijiaka sana kuona mkuu wetu kaja na mikakati hasa ya kusaidia kukuza maendeleo kwenye sekta ya elimu hivyo hatuna budi kumuunda mkono kuhakikisha kuwa mambo aliyoyaongea tunayafanyia kzi ili kuhikisha wanafunzi wanasoma” walisema vingozi

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  WATU saba wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam,wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuiba roli nne za waya za umeme zenye thamani ya Dola za Marekani 52268.78 sawa na Sh.116,872,813 mali ya  Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

  Mwendesha mashtaka wakili wa Serikali, Herieth Lopa amewataja washtakiwa hao kuwa ni Mbatia Mhando (35), Abdallah Tambwambwa (39),  Willy Mgimbudzi (32), Francis Nchimbi (50), Ally Mohammed (42), Hassan Haji (29) na Misana Selestine (27).

  Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wakili Lopa amedai, Desemba 16 mwaka 2017 huko Tabata Kinyerezi washtakiwa hao waliiba roli hizo nne za nyaya za umeme zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

  Wakili huyo wa Serikali alidai katika kipindi hicho,washtakiwa kwa vitendo vyao na kwa makusudi walisababisha hasara ya Sh 116,872,813 mali ya Tanesco.Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuzungumza chochote kwa sababu Mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

  Kesi imeahirishwa  hadi Februari 7, mwaka 2018.Katika kesi nyingine, Peter Mdegera na Ali Mayumba wamefikishwa mahakamani hapo,kujibu tuhuma za kukutwa na kilo 192.46 za dawa za kulevya aina ya bangi.

  Wakili wa Serikali, Lopa amedai mbele ya Hakimu Shaidi kuwa  Septemba 7, mwaka 2017 katika Mtaa wa Tarangile Mbezi Beach washtakiwa hao walikuwa wakiwa bangi hizo.

  Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ali alieleza mahakamani hapo kuwa anaumwa mguu kwa kuwa alipigwa na askari na kwamba kutokana na kipigo hicho sehemu zake za siri za kiume azisimami hivyo anahitaji msaada wa matibabu.

  Mbali na Ali na mshtakiwa mwenzake Peter anaye alilalamika kuwa naye alipigwa.Baada ya kuwasikiliza washtakiwa hao, Hakimu Shaidi aliwaeleza wakipelekwa gerezani watapatiwa matibabu na kama hawatapatiwe tarehe ijayo watoe taarifa.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februairi 7,2018 washtakiwa walipelekwa rumande. 

older | 1 | .... | 1495 | 1496 | (Page 1497) | 1498 | 1499 | .... | 1903 | newer