Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1494 | 1495 | (Page 1496) | 1497 | 1498 | .... | 1903 | newer

  0 0

  WANACHAMA 139 wa Chadema wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Manyara Mosses Komba. 

  Akizungumza wakati wa kuwapokea na kuwakabidhi kadi za CCM wanachama hao wapya, Komba alisema wamefanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Komba alisema hawatajuta kujiunga na CCM kwani hivi sasa chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli kinawatumikia wananchi kwa kutatua kero na kuufanikisha maendeleo. 

  Alisema wanakaribishwa CCM kwa moyo mmoja hivyo washirikiane na wanachama wengine ili kuhakikisha wanalirudisha jimbo hilo na kata sita zinazotawaliwa na Chadema. "Kati ya makosa tuliyofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni kuachia jimbo la Simanjiro liende Chadema na kata za Mirerani, Naberera, Loiborsiret, Ruvu Remit, Loiborsoit na Endiamtu zichukuliwe na wapinzani," alisema Komba. 

  Alisema ushabiki wa kufuata mkumbo ndiyo uliowagharimu wananchi wa wilaya hiyo na kata hizo, hadi kusababisha wakapatikana madiwani na mbunge wa kutoka upinzani badala ya CCM."Nakuagiza Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel na wenyeviti UVCCM wa kata husika ambazo madiwani wao ni wapinzani, mkishindwa tena 2020 mjiuzulu," alisema Komba. 

  Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro Thomas Mollel alisema kwa kushirikiana na vijana wenzake wa Simanjiro, watahakikisha wanatekeleza agizo hilo la kurejesha jimbo na kata sita zinazoshikiliwa na wapinzani. "Hata hivyo, wananchi wengi wa Simanjiro wana imani kubwa na Rais John Magufuli kupitia CCM mpya, tunatarajia uchaguzi ujao wa mwaka 2020 tutarudisha jimbo na kata hizo sita," alisema Mollel. 

  Alisema vijana ndiyo nguzo kubwa ya ushindi kwenye chama hicho na wamepata mwamko wa kushiriki kuwajulisha wananchi kuwa CCM ndiyo chama cha kukimbilia. Mjumbe wa baraza la utekelezaji UVCCM mkoa wa Manyara, Elizah Ladis alisema tangu waanze ziara ya kutembelea wilaya za mkoa huo mwezi Desemba mwaka jana, hiyo ndiyo idadi kubwa ya wapinzani 139 kujiunga na CCM. 

  "Simanjiro wametupokea kwa wapinzani 139 kujiunga na CCM wilaya za Hanang na Mbulu, wapo waliojiunga ila siyo wengi kama hawa, tunaelekea Kiteto na Babati sasa tunatarajia kupata wapinzani wengine," alisema Ladis.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) msimamo wa serikali kwa Klabu ya Michezo ya Simba kuhusu suala la uwekezaji kwa vyama vya michezo vilivyoanzishwa na wanachama kwa kuzingatia wa sheria kuwa ni 49% kwa mwekezaji na 51% kwa wanachama kufuatia kutangaza kumpa mwekezaji wao 50% hivi karibuni kinyume na kanuni jana jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Salim Abdallah na Katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
  Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw. Salim Abdallah akieleza waandishi habari (hawapo pichani) kuwa msimamo wa serikali wameuelewa na watakwenda kuzungumza na mwekezaji wao Mohamed Dewji kuhusu kumpunguzia 1% na kumpa 49% badala ya 50% waliyokuwa wametangaza hivi karibuni kumpa jana jijini Dar es Salaam,pembeni yake ni Mwanasheria wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Evodius Mtawala.

  0 0


  Ili Kujiunga na Mtandao huu wa Elimika Wikiendi Bofya hapa
   www.elimika.co.tz 
  Kwa ufupi

  #ElimikaWikiendi ilianzishwa mnamo tarehe 15.01.2016 kama jamvi wazi kwa wapenda Kiswahili ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu jamii zao
   Kutafiti,kuhoji,kufahamiana,kujifunza mambo kadha wa kadha ikiwemo ubunifu wa Tehama, elimu juu ya afya, maendeleo jamii,ujasiliamali, mitindo, michezo na mengine mengi.


  #ElimikaWikiendi hufanyika kila jumamosi kwa njia ya Twitter kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana kupitia #tag #ElimikaWikiendi . Saa moja la kwanza huwa ni wakati wa kukienzi Kiswahili kwa misemo,nahau,mafumbo na methali tofauti, na ikifuatiwa saa nyingine kwa ajili ya elimu juu ya afya kutoka kwa wataalam mbalimbali, Ikimalizia na masomo mchanganyiko ikiwa ni pamoja na teknolojia,maendeleo ya jamii au mada tofauti zenye mlengo wa kuelimisha jamii. 

  Muonekano wa Tovuti ya Elimika Wikiendi  Baadhi ya Jumbe mbalimbali ambazo zilitumwa wakati wa kutambulisha rasmi Tovuti ya Elimika Wikiendi.Ili Kujiunga na Mtandao huu wa Elimika Wikiendi Bofya hapa www.elimika.co.tz 
   Twitter @EW_Tanzania


  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akitazama eneo la uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha Dangote wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote na Mathias Canal
  Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Dangote Ndg Hemendra G. Raithatha alipotembelea kiwanda hicho wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Dangote Ndg Hemendra G. Raithatha kuhusu uzalishaji Wa saruji kiwandani hapo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. 
  Kikao cha kazi kikiendelea 

  Na Mathias Canal, Mtwara


  Uongozi wa Kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha (DANGOTE CEMENT LTD) Mkoani Mtwara umeagizwa kuandaa  mikataba ya ununuzi wa jasi (Gypsum) na wachimbaji wadogo ili kuboresha Biashara ya wachimbaji hao sambamba na faida kwa kiwanda hicho kuliko ilivyo sasa ambapo kiwanda kinanunua Madini kutoka kwa wachimbaji wadogo bila kuwepo makubaliano maalumu yanayofanana kwa wote.


  Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa agizo hilo leo 19 Januari 2018 wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Dangote muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.


  Mhe Biteko alisema kuwa rasmi mikataba hiyo inapaswa kukamilika katika kipindi cha Siku 14 (Wiki mbili) kuanzia Leo 19 Januari 2018 hadi 2 Februari 2018  na kuwasilishwa kwenye ofisi ya madini kanda ambayo itawaita wadau wote kujadiliana vipengele vya mikataba hiyo ambayo itawafanya wachimbaji kuwa na bei ya pamoja na kutoa wajibu na haki kwa pande zote mbili.


  Alisema kuwa katika mkataba huo ni lazima kuwepo kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 wachimbaji Mara baada ya kiwanda kukusanya bidhaa zao jambo ambalo litaibua ufanisi na tija katika ukuzaji wa Biashara zao na kuaminika katika jamii.


  Mhe Biteko alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli inataka wawekezaji wafanye kazi kwa amani pasina kusumbuliwa huku kwa upande wa wananchi wakisalia kunufaika na uwepo wa wawekezaji hao.


  Alisema kuwa moja ya ajenda muhimu kwa serikali ni pamoja na kufanikisha ukuaji wa wachimbaji wadogo kufikia kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa hivyo ni lazima kuimarisha soko la ndani kwani wachimbaji wadogo hawawezi kukua kama soko la ndani halitaboreshwa.


  Awali wachimbaji wa Jasi, walitoa kilio chao kwa Naibu Waziri huyo kuwa kiwanda cha Dangote hakinunui Madini yao na hata kikinunua malipo huchukua muda mrefu sana hadi miezi minne na kwamba kiwanda kinawagawa wachimbaji hao na kununua bei tofautitofauti kwa bidhaa moja jambo ambalo linawafanya wachimbaji wa Jasi kuambulia hasara. 


  Aidha, Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko amewataka watanzania wote wanaofanya kazi kwenye migodi na kwingineko kuwa waaminifu mahali pa kazi kwani kumekuwa na malalamiko ya wizi hususani migodini jambo ambalo linapunguza imani kwa wawekezaji.

  0 0

  MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

  Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jackson Sipitieck alisema vipaumbele vya bajeti hiyo ni elimu, afya, maji na viwanda. 

  Sipitieck alisema suala la kupitishwa kwa bajeti ni jambo moja na utekelezaji ni jambo lingine, hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake ipasavyo wakiwemo madiwani na watumishi, ili kufanikisha hilo. Alisema kila mmoja kwa nafasi yake akisimama kwa nguvu zote, wilaya ya Simanjiro itapiga hatua kubwa ya maendeleo na wananchi wake watakuwa wanapata huduma zao za kijamii kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alisema bajeti hiyo ni kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwemo miradi ya maendeleo, ruzuku ya uendeshaji ofisi na mishahara. Myenzi alisema wilaya hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha wanaboresha vipaumbele vyao vya elimu, afya, maji na viwanda. Alisema mazao ya mifugo, ikiwemo maziwa, ngozi na nyama inapaswa kuboreshwa ili iwe chachu ya vichocheo vya uchumi. 

  Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary aliwapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kupitisha mpango huo wa bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa manufaa ya wananchi. "Pamoja na hayo tunapaswa kuhakikisha tunatekeleza agizo la kila mkoa kuwa na viwanda 100 kwa sisi Simanjiro kuanzisha viwanda 15 ambayo vitasambazwa kwenye kata zetu na vijiji," alisema Omary. 

  Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Komolo, Michael Haiyo aliipongeza bajeti hiyo na kusisitiza ikamilishwe kwa vitendo. Haiyo alisema bajeti hiyo imegawanywa bila upendeleo kwani kata zote zimepatiwa miradi ila umuhimu wake utaoneka endapo itatekelezwa kwa vitendo. Diwani wa kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka alisema bajeti hiyo inapaswa kujali suala zima la uboreshaji wa mifugo kwani asilimia kubwa ya wananchi wa eneo hilo ni wafugaji. 

  "Sisi kwetu kahawa ya Simanjiro ni mifugo ambayo ni roho ya uchumi, hivyo tunapaswa kulizingatia hilo kwenye utekelezaji wa bajeti yetu," alisema Ole Kinoka.
  Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kushoto ni Makamu Mwenyekiti Albert Msole na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yefred Myenzi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega (wa kwanza kulia) akiongoza shughuli ya kuteketeza nyavu haramu zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 400 zilizo salimishwa na wavuvi wa mwalo wa Igombe mkoa wa Mwanza.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na wanachi wa mwalo wa Igombe mkoa wa Mwanza kabla ya kuteketeza  nyavu haramu zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni  400 zilizo salimishwa na wavuvi.
    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameongonzana na watumishi wa mkoa wa Mwanza wakiwasili katika kiwanda cha Tanzania Fish Processors (TFP) mkoa wa Mwanza.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akipima urefu samaki kwa kutumia kipimo cha kisasa chenye urefu wa sentimita 50-85 kilicho ruhusiwa kisheria.  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akipatiwa maelezo juu maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya kutoka kwa Mkurugenzi wa tawi hilo Dkt. Heriel Nguvava ,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika.Waziri alitembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC.TPSC ina matawi sita.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa tawi la Mbeya wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt Heriel Nguvava (kulia) wakati Waziri alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita, kushoto ni Mkuu wa TPSC Dkt. Henry Mambo 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika kulia akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa tawi la Mbeya wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt Heriel Nguvava wakati Waziri huyo alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita 
  Mfanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya Nuhuman Iddy akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati Waziri huyo alipotembelea tawi hilo mwishoni mwa wiki ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuyatembelea matawi ya TPSC, TPSC ina matawi sita 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati aliyekaa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya, kulia kwake ni Mkuu wa TPSC Dkt. Henry Mambo , wengine ni viongozi waandamizi wa mkoa wa Mbeya

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Shedeli Mikole Mwenyekiti wa CCM kata ya Vigwaza wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua huduma za maendeleo na miradi mbalimbali inayotekelezwa jimboni humo, Mh. Ridhiwan Kikwete ametembelea kata na vijiji vya Visezi, Buyuni , kata ya Vigwaza. na Magulumatari, Kisanga Kata ya Talawanda, Bago na Msinune kata ya Kiwangwa.
  Sehemu ya Bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya Kimaendeleo. Kikundi cha Jipe Moyo ambacho ni moja kati ya vikundi vilivyofaidika na fursa za Mitaji Katika Halmashauri na Mfuko wa Jimbo ambao upo chini ya Mbunge wa Chalinze wakionyesha kazi zinazotokana na Mikono yao mbele ya Mbunge.
  Mmoja wa wananchi akizungumza mbele ya Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze .
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikagua Nguzo za umeme zipatazo 60 katika Kijiji cha Visezi. ambazo zipo hapo toka mwaka 2015 sasa ni miaka miwili toka Zilipoletwa hadi leo hazijaunganishwa. Serikali kupitia mradi wa Peri-Urban Enlightment Initiative watakuja waunganishia wananchi wa Visezi.
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa Mh. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha, Ajay Shah, akiongoza zoezi la kuchoma nyavu haramu za dagaa zilizo chini ya sentimita 8 (marobota 584) zenye jumla ya shilingi milioni mia moja zilizokamatwa kwenye Kiwanda chake na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina kwenye dampo la takataka nje kidogo ya jiji la Arusha leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akikagua chumba cha baridi cha kuhifadhia samaki (Cold room) cha kampuni ya Alpha Choice mjini Arusha leo akiwa katika operesheni maalumu ya kudhibiti uvuvi haramu kulia ni mmliki wa kampuni hiyo Yussuf Khatry. 
  Marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 wakitekea kwenye dampo nje ya jiji la Arusha leo. Marobota hayo alikamatwa na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina ambapo uteketezaji huo uliongozwa na mmliki wa kiwanda hicho Ajey Shah.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akisikiliza taarifa ya ukamataji wa marobota 584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka kwa kiongozi wa Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini West Mbembati aliye kulia, kushoto mwakilishi wa Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi.  Na John Mapepele

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekitoza faini ya Shilingi milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag Tanzania Limited cha jijini Arusha baada ya kukutwa na makosa mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzalisha na kuuza nyavu ambazo ziko kinyume na matakwa ya Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2009.

  Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ajay Shah, kiwanda kimekuwa kikitengeneza vyavu hizo haramu kwa miaka mitatu mfululizo sasa ambapo inakadiliwa kuwa tayari kimeshatengeneza tani 1296 nyavu hizo zenye thamani ya shilingi bilioni nne.

  Akitoa taarifa kwa Waziri Mpina, Kiongozi wa kikosi kazi cha kutokomeza uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria, West Mbembati amesema kuwa tarehe 17/1/2018 walifika kwenye kiwanda hicho na kukamata marobota 584 yenye thamani ya milioni mia kufuatia maelekezo ya Waziri Mpina yaliyotolewa Mjini mwanza hivi karibuni baada ya mfanyabiashara Dastan Venanti kukamatwa na nyavu hizo zenye thamani ya milioni sitini na tano ambazo nyaraka zilionyesha alinunua katika kiwanda hicho.

  Akipokea taarifa hiyo Waziri Mpina alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria ambapo amesema hatua za kali za kisheria dhidi yao zitatumika ili kudhibiti uvuvi haramu kwenye maji(mito,maziwa na bahari) ya nchi yetu.

  “Operesheni ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanya biashara wakuu wanaofadhili na kuendeleza biashara ya uvuvi haramu ni ya kudumu ambapo mkakati uliopo sasa ni kuwanyang’anya na kuwafutia lesseni zao za biashara” alisisitiza Mpina

  Aliwaonya wafanyabiashara wanaosafirisha samaki na mazao yake katika nchi za jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kongo wanaotishia kugoma ambapo amesisitiza kwamba hatua waliyoichukuwa ni ndogo badala yake waachane kabisa na biashara hiyo kwa kuwa wamekuwa wakikwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato yake kwa muda mrefu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ajay Shah alikiri kutenda makosa hayo na kueleza kuwa kiwanda kimekuwa kikiendelea kutengeneza vyavu hizo bila kujua kuwa kilikuwa hakizingatii sheria za Uvuvi ambapo alisema kimekuwa kinauza nje ya nchi hususan kwenye soko la Nairobi nchini Kenya na Mwanza

  Aliwataja baadhi ya wateja wake wakuu wa mkoani Mwanza kuwa ni pamoja na Dastan Venant, Morice Otieno na Majani Masagati ambao wote walikamatwa hivi karibuni na nyavu zisizoruhusiwa kisheria na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu kilichoundwa na Waziri Mpina na kutozwa faini ya jumla ya shilingi milioni 120 huku vyavu hizo zikitaifishwa na kuteketezwa mara moja.

  Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliongoza zoezi la kuteketeza nyavu hizo haramu kwa kushirikiana na Waziri na Watendaji mbalimbali wa Serikali katika dampo la kuwekea takataka nje kidogo ya jiji la Arusha huku akikiri kuwa atazingatia taratibu zote za Serikali katika kutengeneza nyavu zinazoruhusiwa kisheria ambapo alisema tayari wameshapeleka barua Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata kibali cha kutengeneza nyavu.

  Aidha Waziri Mpina ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara yake kumempatia kibali cha kutengeneza nyavu hizo kwa mujibu wa sheria za nchi. Kulingana na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 kibali hicho kinatolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi.

  0 0


  0 0


  TANZIA: Familia ya Bwana Sylvester Manase Matunda Lema, wa Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000 jijini Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, Bibi.Lulu Sylvester kilichotokea katika Hospitali ya Agha Khan tarehe 20/01/ 2018 majira ya saa 10;30 alfajiri.

  Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000. Mwili utaagwa Jumatano Januari 24, 2018 kuanzia saa 8 mchana Kanisani KKKT Usharika wa Sinza -Kumekucha.

  Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Alhamisi tarehe 25/01/2018 kuelekea Kijiji cha Nronga-Machame, wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira. Kikao hicho kimejumuisha pia wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo Mhe. Makamba amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kulia) akifuatilia hoja za wabunge  katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma.
   Sehemu ya waheshimiwa wabunge, Mhe. Mussa Ramadhani Sima na Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest wakifuatilia mawasilisho juu ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini, katika kikao cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira. Kikao hicho kimejumuisha pia wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo Mhe. Makamba amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kulia) akifuatilia hoja za wabunge  katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma.
   Sehemu ya waheshimiwa wabunge, Mhe. Mussa Ramadhani Sima na Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest wakifuatilia mawasilisho juu ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini, katika kikao cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini Dodoma.

  0 0

   Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kushoto, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa mara baada ya meli kuwasili bandarini hapo
   Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Ajuaye Msese kushoto, akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kulia, katikati kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa
   MV Njombe ilipowasili bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
  MV Njombe mara baada ya kutia nanga bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi


  Kuanza safari kwa Meli za kisasa za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ambazo zina uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,000 kumefungua fursa za kibiashara kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.

  Meli ya Mv Njombe ambayo imefanya safari yake kwa mara ya kwanza nchini Malawi imefika salama na kutia nanga katika bandari za Nkhata Bay. Meli ya Mv Ruvuma inayopakia shehena ya Clinker inatarajiwa kutia nanga katika Bandari ya Monkey Bay nchini Malawi siku mbili zijazo.MV Njombe ambayo ilibeba takribani tani 800 ya shehena ya saruji kutoka bandari ya Kiwira nchini Tanzania hadi bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi imetia nanga salama na imetumia muda mfupi zaidi kufika Malawi.

  MV Ruvuma ambayo ni pacha wa MV Njombe nayo imepakia takribani tani 800 za shehena ya ‘Clinker’ katika bandari ya Kiwira nchini Tanzania kuelekea bandari ya Monkey bay nchini Malawi.Akizungumzia ujio wa shehena hizo za Saruji na ‘Clinker’, Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye pia alikuja kushuhudia tukio hilo, Mheshimiwa Benedicto Mashiba amesema kwamba kuanza kwa safari hizo ni habari njema kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi .

  Balozi Mashiba amesema kwamba, ujio wa meli hizo ni ufunguo wa biashara kati ya Tanzania na Malawi kwani kusafirisha bidhaa kwa njia ya maji ni nafuu na salama zaidi ukilinganisha na barabara.

  “Usafiri huu ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi hizi mbili (Malawi na Tanzania) kwani utawezesha usafirishaji wa mizigo kwa wingi ukilinganisha na njia nyingine kama barabara,” amesema Balozi Mashiba.Mashiba amesema kwamba kuna biashara kubwa ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa hivyo kuanza safari kwa meli hizo kutasaidia kuongeza zaidi ukubwa wa shehena katika ya nchi hizo.

  Naye Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Bw. Ajuaye Msese amewasihi wananchi na wafanyabiashara wa Tanzania, Malawi na Msumbiji kutumia usafiri huo kwani ni wa uhakika, nafuu na salama.Msese amesema kwamba kusafirisha shehena ya bidhaa kama ‘Clinker’, saruji na makaa ya mawe pamoja na bidhaa nyingine kwa wingi ni salama zaidi ukitumia njia ya maji kuliko barabara.

  Amesema mbali na hilo na usalama na unafuu, lakini pia tukisafirisha bidhaa kwa kutumia maji tunaokoa uharibifu wa miundombinu yetu kama barabara na madaraja.Mkuu huyo wa bandari za Ziwa Nyasa alitolea mfano mzigo wa saruji ulioletwa na meli ya MV Njombe pekee, kama ungekuja kwa njia ya barabara, basi msafirishaji angelazimika kutumia malori 25.

  “Ukisafirisha mzigo kwa njia ya maji ni nafuu, salama na unakuwezesha kusafirisha mzigo mkubwa zaidi kwa wakati mmoja,” amesema Msese.Kwa mujibu wa Bw. Msese, ukisafirisha mzigo kwa njia ya maji na kwa wingi kama huu, itamsaidia mlaji wa mwisho kuja kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu.

  Ziwa Nyasa ni moja kati ya maziwa makuu yanayounganisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Songea na nchi za Malawi na Msumbiji kwa njia ya maji.

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Idadi ya watalii duniani imekuwa kwa kiwango cha 7% mwaka 2017 na kufikia idadi ya milioni 1,322, kwa mujibu wa matokeo ya hivi karibuni yaliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO). 
   
  Kulingana na takwimu zilizoripotiwa kutoka sehemu tofauti duniani, inakadiriwa kwamba idadi ya watalii waliowasili duniani kote imeongezeka kwa 7% mwaka 2017. Hii ni ishara nzuri au zaidi ya kiwango kilichokuwepo cha 4% kilichodumu tangu mwaka 2010, hivyo kuonyesha matokeo mazuri ndani ya miaka saba. 

  Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa Afrika ambazo Jumia Travel ingependa kukushirikisha, ukuaji katika mwaka 2017 ulikadiriwa kuwa wa 8%. Ilijiimarisha kama ilivyokuwa kwa mwaka 2016 na kuwa na matokeo mazuri yaliyofikia idadi ya watalii milioni 62 kutembelea kutoka mataifa tofauti duniani. Licha ya changamoto mbalimbali hususani za kisiasa, nchi za Kaskazini mwa Afrika zilirejea kuwa na matokeo mazuri kwenye sekta ya utalii ambapo idadi ilikuwa kwa 13%, wakati nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zenyewe idadi iliongezeka kwa 5%.

  Mwaka 2017 ulitawaliwa na ukuaji endelevu kwenye maeneo mengi na kwa maeneo yaliyokumbwa na changamoto miaka iliyopita yaliimarika na kurejea hali zao za kawaida. Kwa kiasi kikubwa matokeo haya yamepelekewa na mabadiliko kwenye uchumi wa dunia na uhitaji mkubwa kutoka kwenye nchi nyingine na masoko mapya ya kitalii, hususani kuongezeka kwa matumizi makubwa kwenye nchi kama vile za Brazili na Urusi ambazo kwa miaka michache iliyopita zilikuwa zimeshuka kidogo. 

  “Utalii wa kimataifa unaendelea kukua na thabiti, na kuifanya sekta ya utalii kuwa imara katika kuendesha shughuli za maendeleo ya uchumi. Ikiwa ni sekta ya tatu katika kuleta mapato ya kigeni duniani, utalii ni muhimu katika kutengeneza ajira na ustawi wa jamii duniani kote,” alisema Katibu Mkuu wa UNWTO Bw. Zurab Pololikashvili kwenye taarifa hiyo. “Bado tukiendelea kukua lazima tufanye kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha kwamba ukuaji huu unainufaisha kila jamii kwenye eneo walilopo, na tunakuwa sambamba kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu.” 

  Ukuaji unatarajiwa kuendelea kwa mwaka 2018 

  Kasi ya ukuaji imara uliopo hivi sasa inatarajiwa kuendelea mwaka 2018, tena katika kasi endelevu zaidi baada ya miaka 8 ya upanuzi wa kutosha kufuatia changamoto za kiuchumi na fedha mwaka 2009. Kulingana na mienendo ya sasa, matarajio ya kiuchumi na mtazamo kutoka kwa jopo la wataalamu wa UNWTO, UNWTO inatazamia idadi ya watalii kimataifa kwenye maeneo mbalimbali duniani kukua katika kima cha 4% mpaka 5% mwaka 2018. Kwa kiasi fulani hii ni juu kwa 3.5% ya ongezeko la wastani wa kawaida uliotazamiwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 mpaka 2020 na UNWTO katika utabiri wake wa Utalii Kuelekea 2030. Ulaya na Amerika zote zinatarijiwa kukua kwa 3.5% mpaka 4.5%, Asia na Pasifiki kwa 5% mpaka 6%, Afrika kwa 5% mpaka 7% na Mashariki ya Kati kwa 4% mpaka 6%.

   

  Utalii Tanzania katika mwaka 2017


  Mwaka 2017 ulikuwa ni wenye neema na mafanikio kwa upande wa Tanzania kwani ilishuhudia matukio makubwa kama vile kuja kwa watu mashuhuri kutembelea vivutio vya kitalii kama vile; Will Smith (mwanamuziki na mcheza filamu), David Beckham (aliyekuwa mcheza soka wa vilabu vya Manchester United, Real Madrid, AC Milan na PSG), Mamadou Sakho (aliyekuwa mchezaji wa Liverpool), Morgan Schneiderlin (mchezaji wa Everton) pamoja na ziara ya kikosi kizima cha timu ya Everton kutokea ligi kuu ya Uingereza.


  Ujio wa watu hao mashuhuri nchini Tanzania ulisaidia kuipaisha sekta ya utalii kwani katika matembezi yao waliweza kushirikisha dunia uzuri wa nchi na vivutio tulivyonavyo duniani. Na kwa kiasi kikubwa ulizaa matunda kwani wengi zaidi waliendelea kumiminika. 

  Mbali na watu hao mashuhuri pia viongozi mbalimbali wa kiserikali kutembelea kwenye vivutio vya kitalii nchini kulileta hamasa kwa wananchi pia. Mwezi Oktoba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu alipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Ngorongoro ambapo aliwahimiza watanzania kuendeleza juhudi za kuhifadhi na kutunza mazingira ya eneo hilo ili kuendelea kunufaisha kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. 

  Lakini katika mwaka huo pia tulishuhudia mabadiliko kwenye sekta ya utalii ambapo Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala aliteuliwa na Mh. Rais John Magufuli kuwa Waziri wa Utalii na Maliasili ambapo kupitia uongozi wake mpya tunaona mabadiliko na jitihada za dhati katika kuendeleza sekta hii ambayo ina mchango mkubwa katika pato la ndani la taifa na ajira. 

  Kwa upande wa miundombinu, serikali kwa kiasi kikubwa imeendelea kuimarisha sekta ya mawasiliano kama vile barabara, reli, maji na anga ambapo imefanya uwekezaji mkubwa. Sehemu nyingi nchini zimekuwa zinafikika kwa urahisi kutokana na maboresho ya barabara huku uwekezaji mkubwa ukiwekwa katika ujenzi wa reli na kuzifufua za zamani. 
  Yapo mengi ya kuvuna kutoka kwenye sekta ya utalii kama vile ajira na fedha ambazo zinasaidia kukuza pato la taifa. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Benki ya Taifa (BoT), mapato ya nje yaliyotokana na sekta ya usafiri, hususani sekta ya utalii, yameongezeka kwa zaidi ya ilivyokadiriwa na kufikia shilingi bilioni 128.8. Mapato hayo yamekuwa na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2,156.9 katika mwaka ulioshia mwezi Novemba 2017, kutoka Dola za Kimarekani 2,101.2 mnamo mwezi Novemba mwaka 2016, ambapo imechangiwa na kuongezeka kuja kwa watalii.

  0 0

  NA TIGANYA VINCENT

  VIONGOZI  mbalimbali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Serikali Mkoani Tabora wameahidi kutoa mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika eneo la Kipalapala kwenye Manispaa ya Tabora.

  Akizungumza jana mjini Tabora kabla ya zoezi hilo la harambee kuanza Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt Barnabas Mtokambali alisema kuwa Kanisa limeamua kujenga Shule mbalimbali ili kutoa mchango katika kupiga vita umaskini , maradhi na ujinga.

  Alisema kuwa Kanisa linachukua hatua hiyo kwa kutambua kuwa silaha kubwa ya kupambana na maadui hao watatu ni elimu ndio maana pamoja na kutoa huduma nyingine katika jamii kama vile afya na maji pia wawekeza katika kujenga kujenga ili kuelimisha jamii.

  Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt.Mtokambali alisema kuwa Viongozi wa Kanisa na watu wengine kama wazazi wanalojukumu la kuwasaidia watoto kuwapata elimu bora na yenye maadili itakayowasaidia kupiga vita umaskini, ujunga na maradhi.

  Alisema kuwa elimu bora na yenye maadili itamwezesha mtoto kuweza kutawala mazingira yake ambayo yatamasaidia kuondoa maadui hao watatu.Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa zoezi hilo , alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa madhehebu yote na wadau mbalimbali wanaungana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo elimu na afya.

  Alisema kuwa atahakikisha kuwa vikwazo vyote ambavyo vichelewesha upatikanaji wa huduma hizo kwa jamii vinaondolewa haraka ili wananchi waweze kunufaika haraka na huduma zilizopangwa kutolewa.Awali Mkurugenzi wa akielezea maendeleo ya ujenzi wa Seminari ya Ushindi alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha anawasaidia kuwatambulisha kwa uongozi wa elimu mkoani humo ili waweze kufanyakazi kwa karibu zaidi.

  Alisema kuwa  Idara ya Elimu ya TAG mkoani Tabora imekuwa haifanyi vizuri katika baadhi ya shule kwa sababu ya kukosa ushirikiano kwa watendaji wa sekta ya elimu.

  0 0

  Wananchi katika Wilaya ya Butiama mkoani Mara wameendelea kujitokeza kwa mamia kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa pamoja na changamoto ya umeme iliyopo kwa sasa katika kijiji cha Rwamkoma ambacho kwa sasa kinaendelea na hatua za Usajili.

  Aidha wamepongeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kuwajali na kuwasogezea huduma kwenye maeneo wanakoishi.Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Musa Luseke, amesema kuwa zoezi linakwenda vizuri na wananchi katika kijiji hicho kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa na kutambulika. 

  Kwa upande wake Afisa Usajili wa wilaya hiyo Bw. Paul Meela amesema kuwa zoezi la usajili kwa wilaya yake linatazamiwa kumalizika ifikapo katikati ya mwezi huu; na kuwataka wananchi katika Kata zote ambao bado kusajiliwa kujitokeza kwa wingi ili kumaliza zoezi kwa wakati.

  Amewataka wananchi katika Kata ambazo Usajili umemamalizi kujitokeka kwa wingi kwenye zoezi la uhakiki wa taarifa na mapingamizi kwa wale ambao siyo Raia ili zoezi la kuandaa vitambulisho liweze kwenda kasi ili kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho.
  Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Rwamkoma wakiwa katika kituo cha uandikishaji Vitambuisho vya Taifa wakishubiri kukamilisha zoezi la usajili.
  Bw. Ezekiel Midamo (mwenye koti jeupe) mzazi wa Bw. Jared Ezekiel (anayejaza fomu) wakazi wa kijiji cha Rwamkoma, akimuelekeza kijana wake namna ya kujaza fomu wakati wa zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa katika Kata ya Butiama wilayani Butiama.
  Baadhi ya akinamama wakazi wa kijiji cha Rwamkoma wakielekezana namna ya ujazaji wa fomu wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
  Bi. Dotto Wambura mkazi wa kijiji cha Rwamkoma akiwa katika hatua za kukamilisha zoezi la usajili kwa kuweka saini yake ya kielekroniki wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
  Afisa Usajili wilayani Butiama Bw. Paul Meena (katikati) akielekezana jambo na wasimamizi wa kituo cha kijiji cha Rwamkoma katika Kata ya Butiama. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Rwankoma na kulia ni Afisa Mtendani wa kijiji cha Rwamkoma Bw. Musa Luseke.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi ili wakague mali za Chama cha Ushirika cha mkoa wa Mara.

  Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya Ushirika nchini zikiwemo za chama cha Ushirika mkoa wa Mara.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

  Alisema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.“Kumekuwepo na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi.”

  Pia Waziri Mkuu aliitaka mikoa yote ikomeshe matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama butura na kangomba ili mkulima wapate tija.“Vipimo hivyo ni vya kinyonyaji na vinamwibia mkulima na kuwanufaisha wafanyabiashara jambo ambalo si sahihi.”Pia Waziri Mkuu aliziagiza Halmashauri zipunguze watumishi walio kwenye Makao Makuu ya Halmashauri na kuwapeleka maeneo ya vijijini ili wakawahudumie wananchi.

  Alisema watumishi watakaobaki Makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa nao waweke utaratibu wa usafiri ili kwenda vijijini kutatua kero za wananchi.Kwa upande wa kilimo, aliagiza Maafisa Kilimo wote wapelekwe vijijini kuwahudumia wananchi na watakaobakia Ofisini ni Mkuu wa Idara, Afisa Bustani na Afisa Utafiti tu.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATATU, JANUARI 22, 2018.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi ili wakague mali za Chama cha Ushirika cha mkoa wa Mara.

  Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya Ushirika nchini zikiwemo za chama cha Ushirika mkoa wa Mara.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

  Alisema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.“Kumekuwepo na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi.”

  Pia Waziri Mkuu aliitaka mikoa yote ikomeshe matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama butura na kangomba ili mkulima wapate tija.“Vipimo hivyo ni vya kinyonyaji na vinamwibia mkulima na kuwanufaisha wafanyabiashara jambo ambalo si sahihi.”Pia Waziri Mkuu aliziagiza Halmashauri zipunguze watumishi walio kwenye Makao Makuu ya Halmashauri na kuwapeleka maeneo ya vijijini ili wakawahudumie wananchi.

  Alisema watumishi watakaobaki Makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa nao waweke utaratibu wa usafiri ili kwenda vijijini kutatua kero za wananchi.Kwa upande wa kilimo, aliagiza Maafisa Kilimo wote wapelekwe vijijini kuwahudumia wananchi na watakaobakia Ofisini ni Mkuu wa Idara, Afisa Bustani na Afisa Utafiti tu.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATATU, JANUARI 22, 2018.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akimkabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Mil 2 mshindi wa kwanza wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini ,Hassan Kusaga ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akimkabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Mil 1 mshindi wa Pili wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini ,Mwakilishi wa kampuni ya Real Statonary ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.


  Washindi wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini  wakiwa katika picha ya pamoja  ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.


  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini  ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Januari, 2018 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi sita walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

  Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Konstantinos Moatsos – Balozi wa Ugiriki hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Fafre Camara – Balozi wa Mali hapa nchini mwenye makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia na Mhe. Dina Mufti Sid – Balozi wa Ethiopia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.

  Wengine ni Mhe. Elizabeth Taylor – Balozi wa Colombia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo – Balozi wa Argentina hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya na Mhe. Uriel Norman R. Garibay – Balozi wa Ufilipino mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.

  Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi wote kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na ameahidi kuwapa ushirikiano utakaowezesha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi zao kukua zaidi.

  Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia kuwa Tanzania inatambua uwepo wa fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi katika nchi hizo pamoja na ujuzi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, na kwamba ni matarajio yake kuwa ujio wao utasaidia kuongeza manufaa ya kiuchumi na kubadilishana uzoefu.

  Pia Mhe. Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha salamu zake kwa viongozi wa nchi zao na amewakaribisha kutembelea Tanzania.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  22 Januari, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi mteule wa Ugiriki hapa nchini Konstantinos Moatsos wakati alipokuwa akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Mali hapa nchini Fafre Camara Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa Balozi wa Ethiopia hapa nchini Dina Mufti Said Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Colombia hapa nchini Elizabeth Taylor mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Argentina hapa nchini Martin Gomez Bustillo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino hapa nchini Uriel Norman Garibay Ikulu jijini Dar es Salaam.


older | 1 | .... | 1494 | 1495 | (Page 1496) | 1497 | 1498 | .... | 1903 | newer