Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MTANDAO WA DEIPLACES KUKUZA UTALII NCHINI TANZANIA

0
0

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI MABEYO AKAGUA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA RELI KILOSA MKOANI MOROGORO

0
0
Na. Andrew Chimesela – Morogoro

Hali mbaya ya mafuriko yanayoendela kuathiri wananchi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro yamemfanya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Generali Venance Mabeyo kufika Kilosa na kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika ili kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa kuokoa maisha ya wananchi wa maeneo hayo na mali zao.

Generali Mabeyo aliwasili Kilosa Januari.19, 2018 majira ya jioni na kuungana na mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyepiga kambi Wilayani humo kwa ajili ya mafuriko hayo kisha bila kujali mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha muda wote wakatembelea baadhi ya maeneo yaliyoakuwa yamethiriwa ili kuona hali halisi ya mafuriko hayo.

Kwenye kikao cha majumuisho Mkuu huyo wa Majeshi nchini alishauri kuwa ili kutatua changamoto hiyo inatakiwa nguvu ya ziada na ya pamoja kwa taasisi zote kuungana, Ikiwa ni pamoja na taasisi mbali ili kuweza kuokoa maisha ya watu, mali zao pamoja na miundombinu iliyoathiriwa.

Hata hivyo alisema changamoto hiyo inatakiwa kuwe na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Amesema suluhisho la mpango wa mda mfupi ni kuwa na kazi ya dharura, na kazi hiyo ya dharura inahitajika kuwepo na mpango wa dharura ambao ni kuokoa maisha ya watu waliozingirwa na maji ili wasiendelee kukosa huduma za kijamii na pia kuathiri afya zao kwa kunywa maji ambayo si salama.Pamoja na kuwepo kwa wazo la kurekebisha tuta la mto Mkondoa ikiwa ni mpango wa muda wa kati ili maji hayo yafuate mkondo wake lakini pia Generali Mabeyo ameshauri kuangalia namna ya kupunguza kasi ya maji hayo kuanzia yanakotoka kwa kujenga mabwawa ikiwa ni mpango wa muda mrefu.

“Maji haya yanakuja huku ni kama sisi ni waathirika zaidi lakini yanakoanzia hatujui hali iko namna gani, pengine katika mpango wa muda mrefu ingetazamwa namna ya kuyapunguza haya maji kasi yake.Sasa katika kuyapunguza, taasisi mablimbali zina wataalamu ambao wanaweza kusaidia kuweza kujenga mabwawa makubwa huko yanakoanzia ili haya maji kupunguza kasi yake kabla hayajafika huku” alisema Generali Mabeyo.

Akitoa maelezo ya awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema tuta hilo la mto Mkondoa lilijengwa enzi za Mkoloni kama kinga kwa mji wa Kilosa na kwa mara ya kwanza lilipasuka mwaka 2010. Ujenzi wake kuanzia hapo haukukamilika vizuri kutokan na hali ya kifedha na sasa limepasuka baada ya Mvua nyingi kunyesha kuamkia Jan,11 mwaka huu.

Hata hivyo Dkt. Kebwe ametoa Ombi kwa Mkuu huyo wa Majeshi, kupata nguvu kazi ya wananjeshi, vifaa na utaalamu wao ili baada ya mvua hizi kupungua waendelee na kutafuta mbinu ya kuuongozo mto Mkondoa uweze kupita katika sehemu yake ya awali na hivyo kutoathiri wananchi, mali zao na miundombinu iliyopo eneo hilo .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe akimuongoza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Adam Mgoyi katikati wakati walipokagua athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za wananchi kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe akitoa maelezo kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo katikati na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Adam Mgoyi kushoto wakati walipokagua athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za wananchi kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro
Maji yakiwa yametapakaa kandokando ya Reli ya kati na kusababisha uharibifu mkubwa wa reli, Mashamba pamoja na nyumba za wananchi.
Madaraja yakiwa katika hatari ya kusombwa kutokana na mvua hizo

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA DAWASA/DAWASCO KWA KAZI NZURI YA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI

0
0


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, RUVU

KAMATI ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa wa Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati imeona jinsi gani fedha za serikali zimetumika.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila kitu kinafanywa na makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.“Inawezekana kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye component ya huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.” Alisema Mhe. Papian.

Aidha Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani (Wakandarasi) wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima wawe wameshajua na kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze kuendesha miradi hii kikamilifu.

Ziara ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya kutembeela baadhi ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji ya Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya Makongo na Salasala.

Kamati pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu chini na Ruvu Juu.Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema, Mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika Miji ya Bagamoyo na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2 kukamilika.

“Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.Akifafanua zaidi kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi Mwang’ingo alitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi milioni 6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.

Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilomita zipatazo 477.“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.” Alifafanua.

Aidha maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na Msigani na maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston T. Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya ya Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.

“Tayari tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji mengi ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni uhaba wa fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema Bw.Msongole.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo(kushoto), akifafanua jamnbo mbele ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kulia) na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, walipotembelea ujemnzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji la Salasala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo Januari 20, 2018. 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel; Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
Kaimu Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, (katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
Modester Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya. 
Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.

SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI YA UMWAGILIAJI NCHINI

0
0
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(kushoto) akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaharu Yoshida baada ya kuweka jiwe la msingi katika shamba la mafunzo ya Uandisi,Ujenzi na Umwagiliaji.
Miundombinu ya umwagiliaji kwenye shamba lenye ukubwa wa eka 150 litawezesha kupata wahitimu walioiva kivitendo 
Baadhi ya wanachuo wakitoka kwenye darasa la mafunzo kwa vitendo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaharu Yoshida(katikati) akifatiwa nyuma na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia kukagua bwawa linalotumika kwaajili ya kukinga maji ya mvua na kuyatawanya kwenye mashamba ya mafunzo.
Mkurungezi wa Elimu ya Ufundi nchini,Mhandisi Thomas Katebelirwe akizungumza katika halfa hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha ATC anayeshughulikia Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya akizungumza umuhimu wa shamba hilo ambalo litasaidia kuwapata wataalamu waliobobea nchini katika fani ya umwagiliaji.

soka la bongo figisu figisu zitaisha lini?

0
0
 Na Hafidh Kido, Moshi.

KWA nafasi yangu ya msemaji wa timu ya Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' ninatakiwa kusafiri na timu popote iendapo lakini kutokana na majukumu mengine nashindwa kutenda haya.

Lakini nilijiapiza mechi baina ya Wagosi na Polisi Tanzania iliyochezwa mjini Moshi katika uwanja wa Chuo cha Ushirika lazima niende. Kwa bahati ikatokea dharura ya kifamilia nikapata ruhusa kibaruani nami nikahudhuria.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na maneno kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), anaikingia kifua Coastal Union kwa sababu ni mwenyeji wa Tanga lakini pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi kwenye klabu hiyo kongwe ya jijini Tanga iliyoanzishwa mwaka 1948.

Kama hiyo haitoshi ikaelezwa kuwa kikosi cha Coastal Union kinacheza soka kwa kubebwa waamuzi ambao wanapokea maagizo kutoka TFF.

Yamezungumzwa mengi, itoshe tu kusema baadhi ya klabu zinazoshiriki Ligi ya soka Daraja la kwanza wamekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kudai Coastal Union inabebwa.

Nimeamua kuja kushuhudia 'kubebwa' kwa Coastal Union. Naomba nitangaze maslahi kabla sijaendelea na andiko hili nililoliandika saa nane usiku wa kuamkia Jumapili Januari 21, 2018 nikiwa chumba cha hoteli Mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Mimi ni shabiki wa Coastal Union lakini pia ni mwanahabari. Hivyo naandika kwa jicho la kihabari lakini naweza kuteleza nikaweka unazi katika andiko hili. Nipo tayari kukosolewa na hata kuzodolewa ikiwa nitaandika uongo au kuongeza chumvi.

Hadi naandika haya msimamo wa kundi B inayojumuisha timu nane yaani Coastal Union, Polisi Tanzania, JKT Mlale, Kinondoni Manicipal (KMC), Mbeya Kwanza, Mufindi United, Mawenzi Market na Polisi Dar es Salaam.

Coastal Union ilikuwa inaongoza kundi kwa jumla ya alama 22, ikifuatiwa na Polisi Tanzania (21), JKT Mlale (21), KMC (19), Mbeya Kwanza (16), Mufindi Utd (12), Mawenzi Market (7) na Polisi DSM (3).

Kwa namna yoyote ile Polisi Tanzania wameumizwa na suluhu tuliyowalazimisha katika uwanja wao. Hivyo walijiandaa kwa hali yoyote iwayo kuhakikisha tunawaachia alama tatu muhimu kwao ili kujihakikishia kupanda Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Hata hivyo, mbinu walizotumia nje ya uwanja hazikuwa sahihi. Nasema nje ya uwanja kwa sababu ndani ya uwanja soka lililochezwa ni la uhakika na wala mwamuzi hakuwa na upendeleo wa aina yoyote ile. Na wachezaji pia walicheza 'Fair Game' ya kuheshimiana.

Tatizo lilianza siku moja kabla ya mechi, yaani Ijumaa ya Januari 19, 2018. Baada ya Katibu wa Coastal Union Bwana Kibabedi kukamatwa na askari polisi kwa kosa ambalo hata hao waliomkamata hawakumudu kulieleza.

Nilipowasiliana na askari ninaowafahamu hapa Moshi kuwauliza sababu za kukamatwa kiongozi wangu hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kunipa ushirikiano.

Askari Polisi wanadai wamemkamata kwa kosa la kutishia kumuua mtu kwa kisu. Kwanza sidhani kama kosa hilo lipo bali ni kosa la kumdhuru au kumshambulia au kutishia mtu kwa silaha au kitu chenye ncha kali. Sheria hazitambui kisu. Wanasheria watanisaidia.

Mwenyewe Kibabedi anasemaje: "Wallah Wabillah hapa mfukoni hata wembe wa kukatia kucha sina halafu naambiwa nataka kumuua mtu kwa kisu? Maajabu haya.

"Ninachokumbuka nilikua nimekaa sehemu nazungumza na simu ghafla naona watu wanakuja wananikamata wananiambia twende kituoni umetishia kutaka kumuua mtu kwa kisu."

Kwa bahati hakulala ndani bali juhudi zilifanyika akatoka salama kwa dhamana. Lakini si dhamana bali alitoka moja kwa moja. Ajabu kidogo mtu aliyetishia kuua anatoka tu hivihivi.

Tuachane na hilo. Niliingia uwanjani na Bus la timu nikiwa na wachezaji. Uwanja ulikua mtupu tukajiandaa kwa mechi. Baada ya kusikiliza mawili matatu ya kocha Juma Mgunda nikaamua niungane na mashabiki wenzangu jukwaani.

Tukiwa tumestarehe tukasikia ving'ora vikali vikiingia uwanjani. Lilikua basi la Jeshi la Polisi, ndani kuna maofisa wa polisi likazunguka uwanja mara tatu na kutimua vumbi huku wanapiga kelele za shangwe. Kisha geti likafunguliwa wakatoka nje.

Hatujakaa sawa likaingia gari la wazi lenye askari takriban 40 wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ambao kimsingi wapo chini ya Jeshi la Polisi, wamevalia kimapambano. Wapo waliobeba mitutu ya bunduki na wapo waliobeba zana za kufyatulia mabomu ya machozi.

Baadhi ya askari walikua wananin'ginia kwenye gari wengine wanachupa huku gari inaenda kasi na kupanda tena. Nayo ilizunguka uwanja mara tatu ikamkosakosa kumgonga Meneja wetu wa timu Bwana Hilal. Lakini hatukujali wala kutishika nayo ikatoka nje ya uwanja kwa shangwe.

Baada ya rabsha hizo kuisha neno la kwanza kusikia baada ya kukaa ni maofisa wa polisi waliovalia fulana za timu ya Polisi Tanzania kutoa agizo kwa mlinzi wa mlangoni kuwa asiruhusu mtu yeyote kuingia na ngoma uwanjani.

Alisema ngoma ni silaha hatari sana, hivyo zisiingie ndani kwa kulinda usalama wa raia na mali zao. 

Niliona ajabu sana kwa sababu ikiwa Old Trafford ya Uingereza ngoma zinaruhusiwa kuingia pamoja Uwanja wa Taifa Dar es Salaam zinaruhusiwa vilevile; itakua uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi?

Zogo la mashabiki wa Coastal Union kupinga hili lilikua kubwa. Amani ikaanza kupotea na dalili za vurugu zikanukia. Nikaona askari waliovalia kijeshi tayari kwa lolote wakianza kusogea karibu tayari kwa mapambano au kudhibiti 'vurugu'.

Nilipoona hivyo nikawaza akilini kuwa hawa wanatumia mbinu za kijeshi kutuchokoza ili tuonekane wakorofi. Ghafla tukakubaliana tuachane na hilo suala tusubiri hatma ya Mungu.

Mungu yupo na yu hai daima. Kabla vurugu hazijaisha wakaingia mashabiki wa Polisi Tanzania huku wamebeba ngoma wanapiga kwa kelele. Yule afisa aliyetuzuia ngoma alikua amesimama palepale mlangoni anawatazama huku akitabasamu.

Tukamuuliza je ile si silaha inaingia uwanjani? Hakujibu kitu. Akaondoka na kupotea machoni mwetu. Watu wa Tanga tunasema alitahayari.

Ngoma zetu zikaingizwa na kuanza kupigwa kwa madaha. Uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe, ngoma haina uadui. Moyo ndio unaopenda. Hata baadhi ya askari nikawaona wanafuatisha midundo huku wakicheka kwa pumbao.

Timu zikaingia uwanjani na mechi ikaanza. Hafla nyuma ya mgongo wangu nikasikia vurugu. Kutazama nyuma ni kijana wa makamo ameshikilia sumu ya kuua mbu. Ni ya kupulizia.

Lengo lake alitaka kumdhuru shabiki wa Coastal Union katika jukwaa letu. Ameshika chupa ya sumu hiyo huku ameshika kibiriti. Kimsingi hilo ni bomu. Lakini askari wakawa wanamwangalia na kusema mwacheni huyo ni mwendawazimu.

Tukamuuliza mwendawazimu ambaye ni shabiki wa timu pinzani anafanya nini jukwaa letu, kama hiyo haitoshi ameshika silaha mkononi ambayo muda wowote atamdhuru mtu. Katika hali ya kawaida naye atashambuliwa na pengine apoteze maisha. Kwanini wasimuondoe?

Utaona kama nasema uongo. Suala la kumuondoa pia ulikua ubishani baina ya polisi na mashabiki. Polisi wanasema mwacheni huyu kijana hana neno huku mashabiki wakisema muondoeni. Zaidi ya nusu saa tunalumbana hatimaye akaondolewa. Ajabu sana hii.

Tukiwa bado kwenye taharuki hiyo nikasikia mpira ni mapumziko. Hata sikuufaidi lakini waliofuatilia wanasema mechi ilikua ngumu ya piga nikupige.

Ikiwa imebaki dakika mbili kipindi cha pili kianze nikasikia mchezaji wetu Abubakar Kinanda, beki wa kulia ameshambuliwa na shabiki wa Polisi Tanzania tena mbele ya askari waliovalia kimapambano, kuzuia ghasia.

Kwa macho yangu nimemshuhudia Abuu akilalamika huku amefunika uso wako wakati askari wanamwangalia miguu 10 kutoka alipo. Halafu huyo aliyemshambulia kwa sumu ya mbu anaondoka taratibu bila kukimbia akizunguka uwanja watu wanamnyooshea kidole. Yuko peke yake.

Askari wamejaa uwanja mzima wanashindwa kulinda wachezaji 22 uwanjani. Je wangeweza kutulinda mashabiki 3000 tuliohudhuria?

Kama hiyo haitoshi tukiwa jukwaani ambapo pia ilikua ajabu mashabuki wa Polisi Tanzania walikuja jukwaani kwetu kukaa na sisi wanashangilia kwenye migongo yetu. Mmoja wa mashabiki hao akachana fedha halali ya Tanzania. Noti ya Sh 1000/- ya Benki Kuu.

Zikaanza kupigwa kelele. Kwa macho yangu nilimuona askari kanzu akienda kumkamata. Lakini wakatokea watu wakamwambia muache. Akamuacha.

Askari waliovalia sare walikuja kuangalia kelele hizi ni za nini? Shabiki mmoja wa Coastal Union akamweleza kuna mtu amechana pesa. Akamuuliza anatoka wapi akamjibu ni shabiki wa Polisi Tanzania. Askari yule akatabasamu na kuondoka huku anawaelezea wenzie ambao nao walikuja kusikiliza huo 'umbea'.

Hadi mpira unaisha dakika 90 mabao hayakupatikana ilikua Polisi Tanzania 0-0 Coastal Union.

Haya ndiyo waliyofanyiwa Coastal Union timu iliyobatizwa kumilikiwa na Rais wa TFF, Wallace Karia. Je hizo zisizojulikana zinafanyiwa vipi.

HAFIDH 
Moshi, Kilimanjaro Tanzania

SEKTA BINAFSI YARIDHISHWA NA UHUSIANO WAKE NA SERIKALI

0
0
 
Baadhi ya Wawekezaji na wageni kutoka Taasisi za Kimataifa walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, akizungumza wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kuboresha masuala ya biashara na uwekezaji nchini, mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Maafisa wengine kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Sehemu ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wawekezaji na viongozi wa Serikali walioshiriki mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa tatu wa wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma

MAAFISA WA BUNGE WATOA ELIMU KWA SHULE ZA SEKONDARI ZILIZOPO MUSOMA MJINI.

0
0
Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge, Ndg. Lawrence Makigi, akisisitiza jambo wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule za Sekondari za Musoma Mjini, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Musoma Sekondari iliyopo Musoma Mjini. Kulia ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Musoma Mjini, Ndg. Exavery Ntambala na kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Musoma, Mwl. Kilonda Salum
Katibu Msaidizi Uhusiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Bunge Ndg. James Sapali, akizungumza wakati akitoa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania kwa Shule ya Musoma Sekondari pamoja na Shule ya Sekondari ya Songe, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Musoma Sekondari iliyopo Musoma Mjini.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songe iliyopo Musoma Mjini akiuliza swali kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Bunge pale Maafisa hao walipotembelea Shule ya Sekondari ya Musoma kwa ajili ya utoaji wa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Musoma Sekondari iliyopo Musoma Mjini.
Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Musoma na Songe wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Dawati la Bunge la Afrika kutoka Ofisi ya Bunge, Ndg. Lawrence Makigi (katikati) akizungumza wakati wa utoaji wa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania, katika tukio lililofanyika leo katika Shule ya Musoma Sekondari iliyopo Musoma Mjini.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songe pamoja na Shule ya Sekondari ya Musoma wakifuatilia maada inayotolewa na maafisa kutoka Ofisi ya Bunge wakati wa utoaji wa Elimu kwa Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Tanzania uliofanyika leo katika Shule ya Musoma Sekondari iliyopo Musoma Mjini.

Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara kuweza kupata matibabu

0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa Filamu Wastara Issa ili aweze kwenda kupatiwa matibabu India ya mguu wake unaomsumbua.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu nyumbani kwake leo Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu wake uliyokatwa mpaka kufikia kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.

“Ndugu zangu watanzania najua kutoa ni moyo na siyo utajiri ninawaomba mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani mpaka sasa anahitaji kiasi cha milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha safari yake hiyo ya kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye matibabu hayo mwezi ujao,”Dkt.Mwakyembe.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa wito kwa wasanii wote wa filamu nchi kujitokeza na kumsadia mwanatansia mwenzao wa filamu katika kufanikisha anapata matibabu ili aweze kurudi na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .

“Bodi ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa laTaifa tumetoa kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya kumchangia katika kufanikisha safari yake ya matibabu na serikali kwa ujumla inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha msanii huyu anapata kiasi hicho cha pesa kilichobakia,”Bibi Fissoo.

Pamoja na hayo Katibu Mtendaji BASATA Bw.Godfrey Mngereza alitoa wito kwa wasanii wote nchini kwa nao kijitokeza kumchangia msanii huyo kwani wasanii wote ni wamoja kwa maana wote ni wanafanya kazi ya sanaa hivyo ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.

Kwa upande wa msanii Wastara Issa aliishukuru serikali kwa kumtembelea na kumjulia hali pamoja na kumchangia na kusema imekuwa nifaraja kubwa kwake kuwaona na alitoa akaunti namba anayotumia kwa ajili ya kukusanyanyia michango ambayo ni EQUITY BENKI – 3007111415583 na namba za simu anazotumia kuchangisha ni 0768 – 666 113 na 0713 666 113 na alieleza amesajiliwa kwa jina la Wastara Issa katika namba hizo za simu pamoja na akaunti namba yake.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo (kushoto) akimkabidhi mchango Msanii wa Filamu Wastara Issa aliyeketi chini kiasi cha shilingi milioni moja kilichotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kwa Kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa kitakacho msaidia kwa matibabu ya mguu wake walipomtembelea jana nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kumjulia hali ,katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimsikiliza kwa makini Msanii Wastara Issa aliyeketi chini alipokuwa akimweleza namna mguu wake huo unavyomuuma na ni kwa muda gani amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo jana alipomtembelea nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kumjulia hali na kufahamu ni kiasi gani cha pesa bado kinahitajika kumwezesha kwenda kwenye matibabu yake nchini India, wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) akitoa wito kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa filamu Wastara Issa ili aweze kupata matibabu ya mguu wake huko nchini India alipomtembelea msanii huyo nyumbani kwake jana Tabata Sanene jijini Dar es Salaam, na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Godfrey Mngereza na anayefuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo,na aliyeketi chini ni Msanii huyo wa Filamu Wastara Issa.
 

MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Agaustine Vuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea vijijini vyote vya jimbo hilo kwa lengo la kuangalia changamoto na kero zinazo wakabili wananchi.

Amefafanua changamoto atakazokutanazo baada ya kuwasikiliza wananchi wake hatua itakayofuata ni kuzifikisha Serikali zitatuliwe ili waendelee kufurahia uongozi wao uliopo madarakani.

Vuma amesema hayo jana wakati akikagua miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha Afya cha Nyakitonto kilichotengewa Sh. milioni 500." Ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 70 mpaka sasa na fedha Ilizo tumika ni Sh.milioni 290,"amefafanua Vuma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na ndio maana Rais,Dkt.John Magufuli ameanza kuboresha sekta za afya kwa kutoa fedha katika vituo vya afya.Ameongeza lengo la fedha hizo ni kuhakikisha wananchi huduma za afya vizuri pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na afya njema." Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kuendelea kuwasaidia wananchi na sisi kama wawakilishi kazi yetu ni kuibua matatizo na kumpelekea aweze kuyatatua.

"Mpaka sasa tunaendelea kuboresha huduma za afya na nimeahidiwa kupewa fedha nyingine kwaajili ya kituo cha afya Rusesa na fedha hizo zitaendelea kutolewa kwa kuwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)", amesema Vuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini ambae pia ni Diwani wa kata ya Nyakitonto , Yohana Mshita amesema wananchi wa vijiji vilivyo karibu na kata hiyo walikuwa wakiteseka kupata huduma.Amesema wananchi wengine walikuwa wakilazimika kufuata huduma Kasulu Mjini na kusababisha kupoteza nguvu kazi lakini kwa sasa wataendelea kupata huduma karibu.

Ameongeza fedha zilizotolewa zimetumika kujenga chumba cha upasuaji, wodi za Wagonjwa, nyumba ya Mganga na chumba cha kuhifadhia maiti.Amesema mpaka sasa kuna fedha nyingi zimebaki, na wataendelea kuzihifadhi ili zitumike katika miradi mingine itakayo ibuliwa na wananchi

Nao baadhi ya wananchi, akiwamo Happynes Dastan amesema wamekuwa wakililia kupata kituo cha afya karibu kwani walikuwa wakilazimika kufuata huduma za upasuaji Wilaya ya Kasulu."Sasa tunauhakika wa kupata huduma za afya hapa hapa na kuendelea kufurahia huduma hiyo kwa karibu,"amesema. 

Amesema wanampongeza sana Rais wa Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya na shughuli ya kuwahudumia wananchi wanyonge kwa shida walizokuwa nazo.


 Mbunge wa Kasulu Vijijini Agaustine  Vuma akikagua miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha Afya cha Nyakitonto kilichotengewa Sh. milioni 500." Ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 70 
MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Agaustine Vuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea vijijini vyote vya jimbo hilo kwa lengo la kuangalia changamoto na kero zinazo wakabili wananchi.

UBA Tanzania yahamasisha watanzania kushiriki fursa ya wajasiliamali Tony Elemelu

0
0
Mkuu wa Idara ya Masoko na Habari wa UBA Tanzania, Ms Brendansia Kileo akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Mmoja wa wanufaika wa USD 5,000 kutoka Tony Elemelu Foundation akizungumza katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Jagrin Agriculture Co. Ltd, Riziki Messa akizungumza katika mkutano huo.

Mkutano huo ukiendelea na wanahabari.

Washiriki katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo ulioandaliwa na UBA Tanzania.


BENKI ya UBA Tanzania yahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika kutumia fursa ya kupewa mitaji kwaajili ya wajasiliamali ambayo inatolewa na taasisi ya Tony Elemelu Foundation.

Katika Semina iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana Mkuu wa idara ya Masoko na Habari wa UBA Tanzania, Ms Brendansia Kileo amesema kuwa kwa sasa maombi bado yanaendelea na wale wote wenye wazo la biashara wanaweza kushiriki kwa mujibu wa waelekezo.

Aliwataka wenye wazo na ndoto za biashara kuzitimiza kwa kuomba nafasi ya kupewa mtaji kupitia asasi ya 'Tony Elemelu Foundation' ambayo watakaofanikiwa kupata watapewa USD 5,000 ikiwa ni mtaji wa mawazo ya biashara yao.

Alisema maombi kuhusiana na kuomba na kupata mtaji yanafanyika kupitia tovuti ya Tony Elemelu Foundation http://www.tonyelemelufoundation.org.

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa USD 5,000 kutoka Tony Elemelu Foundation walioshinda kutokea Tanzania katika miaka ya nyuma wamewataka idadi kubwa ya Watanzania kushiriki katika fursa hiyo ili waweze kufikia malengo yao.

Akizungumza mmoja wa wanufaika Mkurugenzi wa Jagrin Agriculture Co. Ltd, Riziki Messa alisema yeye pamoja na wenzake waliowahi kunufaika na fursa hiyo ya ujasiliamali amesema wamedhamiria kuhamasisha Watanzania wengi kushiriki katika fursa hiyo kutoka taasisi ya Tony Elemelu Foundation.

Aliwataka wanahabari kutumia fursa hii kwa ajili ya kuutangazia umma wa Watanzania kuomba kwa wingi ili kusudi Tanzania iweze kuwa na vijana wengi watakaonufaika na programu hii ya kutoa mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara au kuanzisha biashara.

SIMANJIRO KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA

0
0
Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo haina hospitali ya Wilaya imejipanga huhakikisha inaanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo. 

Wilaya ya Simanjiro iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya kugawanywa kutoka wilaya ya Kiteto, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ina wananchi 178,693 lakini hadi hivi sasa haina hospitali ya wilaya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yefred Myenzi aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. 

Myenzi alisema viongozi na wananchi wa wilaya hiyo kwa pamoja wanapaswa kushikamana ili kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa hospitali hiyo ya wilayani. 
Alisema ameshakutana na wataalamu wa idara ya afya waliotoka ofisi ya Rais Tamisemi, waliofika ofisini kwake na kupanga mipango ya kuanzisha hospitali ya wilaya hiyo. 

"Sikubaliani na pendekezo la kukipandisha hadhi kituo cha afya Orkesumet ili kiwe hospitali ya wilaya, hapana tunapaswa kujenga hospitali ya wilaya na kituo cha afya Orkesumet kitaendelea kufanya kazi yake kama kawaida," alisema Myenzi. 
Alisema tangu wilaya hiyo ya Simanjiro ianzishwe haijawahi kuwa na hospitali ya wilaya, hivyo huu ni wakati muafaka wa kuanza mchakato wa ujenzi wake. 

Diwani wa Kata ya Orkesumet, Sendeu Laizer alisema anaunga mkono hatua ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yefred Myenzi kuanza ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya na kutopandisha hadhi kituo cha afya cha Orkesumet. 
Laizer alisema suala hilo ni maendeleo makubwa kwa wananchi wa kata ya Orkesumet na Wilaya ya Simanjiro kwa ujumla kwani wilaya hiyo haijawahi kuwa na hospitali ya wilaya tangu ianzishwe. 

Mkazi wa wilaya hiyo Meshack Tureto alisema ujenzi wa hospitali hiyo, itakuwa ni maendeleo mazuri kwa wananchi wa eneo hilo, ambao hawana hospitali ya wilaya. 
Tureto alisema uanzishwaji wa hospitali ya wilaya itakuwa ni muendelezo mzuri wa maendeleo kwenye eneo la afya, kwani mgonjwa ataweza kupata rufaa ya ugonjwa kwa ukaribu zaidi tofauti. 

Mkazi wa Orkesumet, Baraka John alipongeza jitihada za Myenzi kuanzisha mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo kwani anaamini mikakati hiyo itafanikiwa. 
"Tunaposema uongozi wa ubunifu na unaoacha alama ni huu alioufanya mashine ya kazi Myenzi kwani hospitali ya wilaya ni hitaji la muda mrefu kwa jamii ya eneo hili," alisema John.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Yefred Myenzi akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary. 
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Albert Msole akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yefred Myenzi. 

WALIMU WAWILI KIBAHA WASHUSHWA VYEO KWA KUKAIDI AGIZO LA ELIMU BURE

0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MKUU wa wilaya ya Kibaha,Mkoani Pwani, Assumpter Mshama ameamuru walimu wawili wa shule za msingi washushwe vyeo kutoka nafasi ya mwalimu mkuu na kuwa walimu wa kawaida ,kutokana na kosa la kuchangisha michango wazazi.

Hatua hiyo ,ameichukua siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,kukemea tabia inayofanywa na baadhi ya walimu wakuu na bodi za shule kuchangisha wazazi na walezi michango ambayo serikali imeizuia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha ,alisema walimu hao wamekiuka agizo la serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk .John Magufuli .

Mshama aliwataja walimu hao kuwa ni mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembesaba, Rashinde Kilakala ambaye alikuwa akipokea sh.1,000 kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya mitihani jambo ambalo ni kinyume cha agizo la serikali.

Mwalimu mwingine ni wa shule ya msingi Jitegemee, Sapiensia Kilongozi ambae aliweka kikao na kuita wazazi na kuwataka wazazi wenye watoto watoe shilingi 2,000 kwa wiki kwa ajili ya masomo ya ziada na mitihani.

Mshama alisema,huo ni mwanzo kwani ataendelea kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali ili iwe fundisho kwa walimu wanaokaidi mipango ya serikali hiyo.Alieleza atakaeendelea kufanya hivyo akibainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi .

"Nilipata malalamiko kutoka kwa wazazi kwamba kuna walimu wakuu wa shule hizo wanachangisha wazazi fedha kwa ajili ya michango mbalimbali ambayo imekatazwa na siku chache zilizopita" alisema Mshama.

“Mwalimu huyu wa shule ya Miembesaba hana kibali wala hajapeleka barua na hakuwa na sababu wala kibali cha kufanya hivyo ambapo mtihani wa mwisho wa mwaka kila mtoto hutoa 1,000 na alikuwa hatoi risiti,” 

“Lazima tumheshimu Rais kwani juzi tu kaongelea suala la elimu bure,hata kama umechangisha risiti ulitoa hivyo mpumzike nafasi hizo mbaki walimu wakawaida,” alisema Mshama.Aidha anashangaa walimu hao walipata wapi nguvu ya kuwashawishi wazazi na kupokea fedha hizo wakati Rais alishazuia mambo hayo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jeniffer Omollo alisema suala la kuchangisha michango mashuleni lilipigwa marufuku na walimu waliaambiwa kuwa hawaruhusiwi kuwachangisha wazazi .Alisema kuanzia sasa watawachukulia hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Kwa upande wake mwalimu Kilakala alisema anashindwa kueleza kwani walikubaliana na wazazi lakini wakamgeuka kuwa walikuwa wakichanga kinyume cha taratibu hata hivyo hawezi kusema zaidi.

Mwalimu wa shule ya msingi Jitegemee Sapiensia Kilongozi yeye alijieleza":niliitisha kikao cha wazazi na kujadili masuala ya taaluma na wazazi wenyewe waliingiza kipengele wanahitaji watoto wao wasaidiwe kwenye masomo ya ziada na mitihani,” alisema Kilongozi.

Alisema walikubaliana baada ya hapo wakaandika muhutasari lakini baadhi ya wazazi walikuja huku kueleza lakini nia na madhumuni ilikuwa ni kufuata taratibu kwani asingeweza kutoa maamuzi ya kupitisha jambo hilo ,maamuzi lazima yapelekwe kwa ofisa elimu kata na baadaye kwa mkurugenzi.

Kutokana na hali hiyo ,Mshama alisema ni lazima wapate fundisho kwa kushushwa nafasi zao za kazi ili wabaki walimu wa kawaida.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ,Assumpter Mshama ,aliyesimama akizungumza jambo kuhusiana na masuala ya Elimu bure .(picha na Mwamvua Mwinyi)

Maandalizi ya Ujio wa FIFA YAANZA

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) (hawapo pichani) unaotarajia kufanyika nchini mwezi Februari 2018 kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri ili ujio huo uwezekuletea manufaa kwa taifa katika kikao kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wakisililiza maagizo ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliyokuwa akitoa katika kikao hicho kwa lengo la kufanikisha ujio huo wa Kimataifa kuwa unaleta manufaa kwa taifa jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe katika kikao cha maandalizi ya ujio huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam,wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Yusuph Singo.

ELIMU YA AFYA YA UZAZI YASISITIZWA KUOKOA VIJANA KISIWANI PEMBA

0
0
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetakiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kisiwani Pemba ili kuokoa kizazi kutokana na kukua kwa wimbi la kuingiliana kinyume cha maumbile.

Kauli hiyo imetolewa na washiriki wa mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendelea Micheweni, Kisiwani Pemba .

Wakichangia mada ya afya ya Uzazi, iliyotolewa na Mkuu wa Elimu ya Afya Wilayani Micheweni, Sulemani Faki Haji, mshiriki kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali anayeratibu masuala ya Jinsia, Hidaya Khamisi amesema kwamba takwimu za udhalilishaji za hivi karibuni zinaonesha Kisiwa cha Pemba hususan wilaya ya Wete inaongoza kwa asilimia 70 kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji.
 Kikundi kazi cha wanafunzi na akina mama kikifanya zoezi la kuwapima uelewa wao kuhusu somo walilopewa na malengo ya mafunzo hayo katika shule ya Sekondari ya Chwaka Tumbe, Micheweni kisiwani Pemba.

Amesema vitendo hivyo vinasababisha fedheha katika jamii na kukatisha ndoto za mtoto kufikia malengo yake maishani.

Wakionyesha ukubwa wa tatizo washiriki wamesema kuwa kwa hivi sasa si shuleni, kwenye madrasa wala nyumbani ni mahali salama kwa watoto wa kiume na wa kike kwani kwa sababu si ajabu kumwona mtu anayeheshimika katika jamii hususan mzazi wa kiume akifanya mapenzi na watoto wake wa kuwazaa na kuwapa mimba huku walimu wa dini kuwadhalilisha watoto.

Hivi karibuni mkazi mmoja wa shehia ya Kiungoni Kimango, Hamad Omari Hamad mwenye miaka 56 alikamtwa na polisi kutokana na vitendo vya ubakaji alivyowafanyia watoto wake watatu akiwemo mtoto mdogo wa miaka minne na mmoja wao kupewa mimba na baba huyo.Kipindi cha mazoezi cha kuendesha mahojiano kwa ajili ya kupata habari kati ya Mtangazaji wa Redio Jamii Micheweni, Time Khamis na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya ya Kujamiiana na Uzazi wa Mpango Wilaya ya Micheweni, Pemba Dk. Suleiman Faki Haji. Mahojiano hayo ni miongoni mwa vielelezo katika mafunzo ya Elimu ya Kujamiiana na Uzazi iliyofanyika Micheweni, Pemba yenye lengo la kuwapa ujuzi stadi wanafunzi wa shule nne za sekondari na kikundi cha akina mama Wilayani Micheweni Kutayarisha Vipindi vya redio vinavyohusu masuala yao.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Masuala ya Jinsia, Hidaya Khamisi, kuna mtandao ujulikanao kama cheni ridhia unaendelea katika baadhi ya shule Kisiwani Pemba wa watoto kwenda kufanya vitendo viovu iwe kupiga punyeto, kufanya ngono au kulawitiana.

Utafiti uliofanyika wilaya ya Wete mwaka 2016 kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa watoto iligundulika kwamba darasa zima lenye watoto 60 walisema kwamba wanataka wawekewe mazingira ili wasidhalilishwe kwa sababu watoto wote darasa hilo wamefanyiwa vitendo vya udhalilishaji hususan kulawitiwa.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Afya ya Kujamiiana na Uzazi iliyofanyika Tarehe 18 hadi 23 Desemba 2017 katika shule ya Sekondari Chwaka Tumbe, Micheweni kisiwani Pemba. Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Salma Khatib Mbarouk (pichani mwenye gauni jeusi na kitambaa cheupe).

Aidha ripoti nyingine kutoka shule moja wilayani Micheweni kwa mujibu wa Meneja wa Kituo cha Redio Jamii Micheweni, Ali Kombo imeonyesha kwamba kati ya wanafunzi 60 ni wanafunzi 10 tu ambao walikuwa bado hawajafanyiwa udhalilishaji wa kingono.

Mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na UNESCO yana lengo la kuunda Vikundi vya Vijana Shuleni na Akina Mama Watayarishaji Vipindi vya redio kwa kushirikiana na Redio Jamii Micheweni, ambavyo vitasambaza Elimu rika kwa Vijana na Akina Mama.

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

0
0
Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . 
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu. 
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo. 
Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu .

Na Joel Maduka,Geita.

Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.

Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"

Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.

Aidha Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa mapato.

Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.

Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.

Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.

SIMBA WAJIFUA KAITABA, KESHO KUPAMBANA NA WENYEJI KAGERA SUGAR

0
0


Na Faustine Ruta, Bukoba .


Kikosi cha Timu ya Simba kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, yakiwa ni maandalizi ya kukabiliana na kikosi cha Timu ya Kagera shugar hapo kesho jioni.

Kikosi hicho ambacho kinaongozwa na Kocha Masoud Djuma ambacho kilitua katika ardhi ya Kagera siku ya Ijumaa kimefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Kaitaba, huku kocha wa kikosi hicho akisema mechi yao na Kagera sugar itakayopigwa hapo kesho inahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kuibuka kidedea.
Nacho Kikosi cha timu ya kagera sugar kilifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana asubuhi kabla ya kukutana na wekundu wa msimbazi, mchezo utakao chezwa siku ya jumatatu katika dimba la Kaitamba.


Kagera sugar wanakutana na Simba wakiwa na taadhali kubwa baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Njombe mji huku Simba wakiwaadabisha matajiri wa Arizeti Singida United kwa mabao 4-0 wiki hii.


Katika mazoezi ya hayo kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Meckime amezungumzia maandalizi ya mchezo huo na kueleza kuwa kikosi chake kiko imara licha ya kutokuwa na matokeo mazuri tangu Ligi hii ianze msimu 2017/2018.
Emmanuel Okwi akiwa kati walipokuwa wanafanya mazoezi hii leo asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba.

Mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burudi nae alikuwepo katika mazoezi hayo.
Emmanuel Okwi
Wakati huo huo nao waamuzi nao walikuwepo wanafanya mazoezi
Walinda mlango wa Timu ya Simba Sc(kulia) ni Aishi Manula ambaye amejifunga kwa miaka miwili Simba. (kushoto) ni Said Mohammed Nduda
Wakijiuliza kuhusu mechi ya Kesho Kaitaba
Kocha wa Simba Masoud Djuma nae kapasha na Wachezaji wake
(kulia) ni Shabani Kapombe
Kocha wa Simba Masoud Djuma(kushoto)
Mavugo






kushoto ni Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya





Kesho Hapatoshi!!
Kocha wa Simba Masoud Djuma akiteta jambo na mwandishi(hayupo pichani) kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo wakati wa Mazoezi ya Mwisho kabla ya kukutana na Timu wenyeji Kagera Sugar.
(Kulia) ni Willy O. Ruta akiwa na Kiongozi wa Timu ya Simba
Makipa wakipimana

Taswira kamili za Mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kaitaba

Babu Seya na Papii Kocha waanza kupika kazi mpya

0
0
​Muimbaji nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.

Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.

Kwenye photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.

Unaweza kufuatilia kila hatua ya safari yao kuelekea kuachia kazi mpya kwa kulike ukurasa wao rasmi wa Instagram@babanamwana, Facebook: baba na mwana. Pia subscribe kwenye channel yao ya Youtube iitwayo Baba na Mwana kuona video mbalimbali za behind the scenes.
​​​​​​​​​​​​​​​
Unaweza kuangalia video ya behind the scenes ya upigaji picha kwa kufuata link hii >> https://youtu.be/h-Kdp87now4

Rais Dk. Shein Awasili Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Kuanza Ziara Yake

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai, kuanza ziara yake ya wiki moja kulia ni Balozi wa Tanzania Katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuanza ziara yake ya Wiki moja.(Picha na Ikulu)MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Mke wa Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa ngazi za Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,alipowasili katika Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Kiserikali ya Wiki moja. kushoto Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowaili katka Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Al Maljis Dubai kuaza ziara yake ya Wiki moja, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.

RC LUHUMBI ATANGAZA KIAMA KWA WAZAZI NA WALEZI AMBAO AWAJAWAANDIKISHA SHULE WATOTO WAO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na waandishi wa habari na baaadhi ya wakuu wa idara mbali mbali pamoja na kati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo wakati alipokuwa akielezea mikakati ya Mkoa huo na shughuli ambazo zimefanyiika. 
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitoa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha kila eneo linatatuliwa changamoto zake. 




Na,Joel Maduka,Geita

Serikali mkoani Geita imetangaza oparesheni ya kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba hadi sasa bado awajawapelekwa shuleni na pindi watakapobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria .

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa seekondari hali sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa kuingia kidato cha kwanza kwani hadi sasa asilimia 46 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni. 

Luhumbi ameongezea kwamba suala la elimu ni haki ya mtoto na hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri kwenye shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa kwenda shule na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.

Ameendelea kusema anafuatilia taarifa ya walimu ambao wameonekana kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo wakibaini hatua kali zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule walimu wameendelea kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.

katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na asilimia 54 .

Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha wilaya ya Bukombe walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620 sawa na asilimia 41,Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia 57,Geita mji walichaguliwa 4,286 walioripoti ni 2,751,sawa na asilimia 64 huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni 1,924 sawa na asilimia 64.

Halmashauri ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na asilimia 50,wilaya ya Nyanghwale 2,601 walioripoti ni 1,344 sawa na asilimia 52

TAMASHA LA BUSARA KUENZI SANAA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA

0
0
. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. 

Hayo yamesema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.

 “Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.

Anaongeza kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.” Likisifika kuwa miongoni mwa matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar.

Likiwa ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine, ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuutanganza muziki wao duniani.

 “Kila mwaka, kila mwanamuziki anayepata fursa ya kutumbuiza katika jukwaa la Sauti za Busara, hualikwa kuzunguka katika miji mbalimbali duniani na kufanya maonesho kwenye matamasha yanayofanyika katika nchi hizo.

 Wanamuziki ambao hupata fursa ya kualikwa aghalabu, ni wale ambao wamethibitika katika maonesho yao kuwa wabunifu, wenye kuzungumza ujumbe fulani, na wanaocheza muziki wenye utambulisho fulani,” anasema Yusuf, akiwataja Msafiri Zawose, Jagwa Music, Leo Mkanyia, Tausi Women’s Taarab na Maulidi ya Homu ya Mtendeni kama mifano ya vikundi vya Kitanzania ambavyo tayari vimekwishaitwa katika safari za kimataifa baada ya kuonekana katika Tamasha la Sauti za Busara. 

Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, Tamasha la Sauti za Busara ni fursa adhimu ambayo wanamuziki kutoka Tanzania hawatakiwi kukosa, kwa kuwa fursa kama hizi ni chache na ngumu kuzipata ndani ya Afrika.

 “Watu wa rangi tofauti huungana kwa pamoja kusheherekea muziki wa Kiafrika. Matarajio na msisimko ni mkubwa, hoteli zinazopatikana Stone Town huwa zinajaa katika wiki ya tamasha zikiwahudumia watu wanaotoka katika kila kona ya Tanzania, Afrika na Ulaya,” anasema Yusuf. Kwa makadirio ya haraka, tamasha linachangia kiasi cha Dola za Marekani 7 milioni katika uchumi kila mwaka, kikiwa ni kipindi cha mavuno kwa biashara nyingi zinazofanyika kwenye kila pembe ya Zanzibar na sehemu zingine, na kulifanya Tamasha la Sauti za Busara kuwa zaidi ya ‘Tamasha la Muziki’. 

Hata hivyo, licha ya kuwa na mafanikio hayo yote, lakini changamoto kubwa inayolikumba tamasha hili ni ufadhili, na ndiyo sababu hata tamasha la mwaka 2016 lilifutwa na kusababisha hasara kubwa sana kwa biashara nyingi visiwani Zanzibar. “Tunaendelea kutegemea fedha za wafadhili kutoka katika balozi mbalimbali, ambapo balozi za Norway na Uswisi zikiwa miongoni mwa wafadhili wakubwa, zikisaidia mafunzo na jitihada za ujengaji uwezo,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud. 

Tamasha la Sauti za Busara 2018 linafadhiliwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Africalia, Mozeti, Zanlink, Memories of Zanzibar, Zenj FM, Chuchu FM, Tifu TV, Music In Africa, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Emerson Zanzibar, Coastal Aviation, 2Tech Security, Ubalozi wa Ujerumani, Golden Tulip Dar City Centre.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images