Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1492 | 1493 | (Page 1494) | 1495 | 1496 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakabidhi hati ya usajili wa chama viongozi wa chama cha ushirika cha Igembe Sabo cha Bunda , Malongo Mashimo ambaye ni Katibu (kulia) na Maria Nengwa ambaye ni Mwenyekiti wa Ujenzi baada ya kuzindua ushirika huo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfereji wa maji wakati alipozindua chama cha ushirika cha Igembe Sabo kinachojishughulisha na kilimo cha mpunga wilayani Bunda Januari 19, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ushirika wa Igembe Sabo wilayani Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. akikagua mashine za kusukuma maji wakati alipoembelea mradi wa chanzo cha maji Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 18, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Hunyari baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati hiyo wilayani Bunda Januari 19, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengti, Bw. William Mwakileme kutokana na mchango mkubwa wa hifadhi hiyo katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Robada wilayani Serengeti. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 19, 2017. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Kutoka Kushoto ni Mhandisi James Mitayakingi Kilaba Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Mary Sassabo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe wakikata utepe kuzindua Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Nawasiliano leo kwenye ukumbi wa JNCC)( jijini Dar es salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
  Kutoka Kushoto ni Mhandisi James Mitayakingi Kilaba Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Mary Sassabo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe wakionyesha Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Nawasiliano leo kwenye ukumbi wa (JNCC) jijini Dar es salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mara baada ya kuuzindua rasmi tayari kwa kutumika.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe akikaribisha wadau wa mawasiliano katika uzinduzi huo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika uzinduzi huo.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiyeakizungumza katika uzinduzi huo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) wakifuatilia uzinduzi huo (Kutoka) Kushoto ni Mhandisi James Mitayakingi Kilaba Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Mary Sassabo
  Mhandisi James Mitayakingi Kilaba Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akimkabidhi Bw. Rodney Thadeus Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Nawasiliano leo kwenye ukumbi wa (JNCC) jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
  Picha mbalimbali zikionyesha wadau wa sekta ya mawasiliano wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye ukumi wa (JNCC) jijini Dar es salaam.
    


  Msanii Mrisho Mpoto wa Bendi ya Mjomba akitumbuiza pamoja na wasanii wenzake katika uzinduzi huo.  Baadhi ya wasanii wa bendi ya Mjomba wakiimba katika uzinduzi huo.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Gari la Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke likiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke akishuka kutoka kwenye gari baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Ofisa Itifaki katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM Frank Uhahula. Katikati ni Kansela wa Ubalozi wa China hapa nchini Dai Xu.
   Balozi Wang Ke baada ya kushuka kutoka kwenye gari lake. Katikati ni Kansela wa Ubalozi wa China hapa nchini Dai Xu
   Ofisa Itifaki katikia Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM Frank Uhahula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Kansela wa Ubalozi wa China hapa nchini Dai Xu
   Uhahula akimwelekeza Balozi huyo kwenda Ofisini kukutana na Komredi Kinana
   Uhahula akiwa na Balozi Wang Ke wakati wakienda ofisini kwa Komredi Kinana.
   Balozi Wang Ke na Uhahula wakikaribia kufika ofisini kwa Komredi Kinana
   Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo

  Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akimkaribisha kuketi Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
  Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Mazungumzo yakiendelea
   Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akimsindikiza mgeni wake, Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
   Katibu Mkuu wa CCM Komredi Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   "Byeee" Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke, akimuaga Katibu Mkuu wa CCM Komredi Kinana wakati akiwa tayari kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Saslaam, leo. Kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
   Gari la  Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke likiwa tayari kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   "Byeeee, Karibu tena"Katibu Mkuu wa CCM Komredi Kinana akimpungia mkono Balozi wa China hapa nchini Tanzania Wang Ke ofisini kwake, Balozi huyo alipokuwa akiondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na kulia ni Stephen Msami ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

  0 0

  Mkoa wa Mtwara Umeanza Kufanya Uhamasishaji wa Kuondoa Mimba za Utotoni na Wanafunzi wanaoacha Shule kutokana na Sababu Mbalimbali zinazowakumba Wanafunzi wa Kike kwa Njia ya Sanaa ya Maigizo.

  Kupitia kituo cha Sports Development Aid (SDA) tayari kimefanya Mafunzo ya Sanaa ya Maigizo kwa Kuwatumia Waigizaji wenye Mafanikio kwa lengo la kutoa elimu kwa Wanafunzi wa Jinsia zote katika Shule ya Sekondari ya Shangani.

  Kituo cha SDA tayari kimeanza Kutoa Mafunzo ya Elimu ya Jinsia kwa shule za Mtwara mjini na Vijijini kwa Kutumia njia ya Michezo, ambapo imekuwa ikigawa Vifaa vya Michezo pamoja na Kukarabati Viwanja Michezo vya Shule.
   Msanii wa Maigizo Yvone Sherry (Monalisa)Akiongea na Wanafunzi wa Shangani Sekondari mkoani Mtwara pamoja kusimamia Igizo La Elim ya Jinsia kwa njia ya Maigizo.
   Viongozi wa Kituo cha Sports Development Aid (SDA) ambao ndio waandaaji wa Mafunzo hayo wakiongea na Wanafunzi wa Sekondari ya Shangani Iliyopo mkoani Mtwara.
   Pichani ni Afisa taalum wa Mkoa wa Mtwara Masalanga akiongea na Wanafunzi wa Sekondari ya Shangani katika Mafunzo kupitia Sanaa ya Maigizo.

  0 0

  Zoezi la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.

  Katika awamu ya pili iliyoanza jana zaidi ya Walemavu 108 wamepatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Shilling Million 324,000,000 lakini kwa jitiada za RC Makonda wamepatiwa Miguu hiyo Bure.

  Katika awamu ya Kwanza jumla ya Wagonjwa 35 wa kisukari walipatiwa miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya Shilling million 157 kutoka CCBRT na kufanya jumla ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo kufikia 143 yenye thamani ya Million 481 Bure.

  Baadhi ya Walemavu waliopatiwa Miguu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.

  Aidha wameishukuru kampuni ya Kamal Group kwa kumuunga mkono RC Makonda kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
   Baadhi ya Walemavu 108 wamepatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa kuwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Shilling Million 324,000,000 lakini kwa jitihada za RC Makonda wamepatiwa Miguu hiyo Bure.
   Iliuwa ni furaha kwa Walemavu hao kupatiwa miguu ya bandia bure
    Miguu ya kisasa ya Bandia ikiwa tayari kugaiwa kwa walengwa


  0 0

  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Waziri wake Mhe.Abdalah Ulega na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili yakutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina. Kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, Mashimba Ndaki.   WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.


  Pia Waziri Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuwakatalia wafugaji kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa sio wakazi halali wa maeneo husika jambo ambalo amesema halikubaliki na kusisitiza kuwa zoezi lisihusishwe na migogoro ya muda mrefu ya matumizi ya ardhi na hivyo kuagiza kuwa ng’ombe na punda wote nchini wapigwe chapa isipokuwa ya kutoka nchi jirani.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi upigaji chapa mifugo, Mpina alisema hadi kufikia Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo wameshapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali.

  Aidha amesema wafugaji wote nchini wataoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26 huku akizionya halmashauri ambazo zitashindwa kutekeleza kikamilifu hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wake.

  Alisema hadi sasa halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 huku halmashauri 9 zikiwa bado hazijaanza kabisa zoezi hilo.

  Waziri Mpina amezitaja Halmashauri hizo ambazo hadi sasa hazijaanza kupiga chapa ni Tandahimba, Nanyumbu, Mafia, Newala, Halmashauri za miji ya Newala, Nanyamba, Masasi na Manispaa za Kigamboni na Ilemela Mwanza ambapo amesema halmashauri 68 ambazo ziko chini ya asilimia 50 na ambazo haijaaanza kabisa tayari halmashauri hizo ameziwasilisha kwa Waziri Mkuu.

  Pia alisema halmashauri 6 zina ng’ombe wengi wa maziwa walio kwenye mpango wa kuvalishwa hereni pamoja na mikoa mingine ambapo jumla ya ng’ombe wote wa maziwa nchini 782,995 kwa sasa, aidha jumla ya punda 572,353 wanatarajiwa kupigwa chapa, taarifa kutoka mikoani kuhusu utekelezaji wa zoezi hili zinaendelea kukusanywa kila siku.

  Alisema kumekuwa na ongezeko la asilimia 20.8 katika muda wa kipindi cha wiki mbili tangu muda wa nyongeza kutolewa ongezeko hili ni kutokana na juhudi za pamoja za uhamasishaji uliofanywa kati ya Wizara na halmashauri pamoja na mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari .

  “Hivyo juhudi kubwa za pamoja baina ya Wizara, Halmashauri, vyombo vya habari na wafugaji zinahitajika ili kukamilisha zoezi la upigaji chapa kwa asilimia 100, kwa kuwa hadi sasa bado asilimia 40.7 ya ng’ombe hawajapigwa chapa “alisema

  Aidha Waziri Mpina amesema kipimo cha asilimia hakitakuwa kigezo cha mwisho cha uhakiki mifugo iliyopigwa chapa badala yake ni kuhakikisha kila ng’ombe na punda mwenye umri wa kuanzia miezi sita wamepigwa chapa.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, Mashimba Ndaki alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na wizara hiyo katika kusimamia zoezi la upigaji chapa ambalo limeungwa mkono na wafugaji wengi nchini.

  0 0

  Shirika lisilo la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) la Mjini Shinyanga limekutana na wanafunzi na walimu wa shule za msingi Didia,Mwanono,Bugisi,Mwamalulu ,Bukumbi na shule ya Sekondari Didia zilizopo katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuzuia ndoa na mimba za utotoni.
  Kikao hicho kimefanyika leo Ijumaa Januari 19,2018 katika shule ya msingi Didia na kuhudhuriwa na baadhi ya wanafunzi walioambatana na walimu wao kutoka shule hizo.
  Meneja Mradi wa Kuzuia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE,Mustapha Isabuda alisema lengo la kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Didia Felister Meli,Kaimu Mtendaji wa kata William Nkuya ni kupanga mikakati ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni ili wanafunzi waweze kumaliza masomo yao vizuri.
  Alisema wanafunzi waliohudhuria kikao hicho watakuwa viongozi wa wanafunzi wengine katika kupambana na ndoa na mimba za utotoni ambapo wataunda klabu kwa ajili ya masuala hayo zitakazopewa jina la “Tuseme Klabu”.
   
  “Hatutaki kuona mwanafunzi anakatiza masomo kwa sababu ya kupewa mimba ama kuolewa, ni wajibu wetu wanafunzi,walimu,serikali na wadau wote tushirikiane kupaza sauti ili watoto wetu watimize ndoto zao”,alieleza Isabuda.
  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE John Myola alisema bado jitihada kubwa zinatakiwa kufanyika ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto katika jamii kwani baadhi ya matukio yamekuwa yakifanywa na ndugu wa karibu huku kesi za watoto zikifanywa dili na baadhi ya watendaji wasio waaminifu.
  Kwa upande wake Secilia Kiza kutoka dawati la jinsia na watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga aliwataka wanafunzi kutofumbia macho vitendo vya ukatili na watoe taarifa katika vyombo vinavyotakiwa.
  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE,John Myola akizungumza katika kikao chao na wanafunzi na walimu kutoka shule za msingi Didia,Mwanono,Bugisi,Mwamalulu ,Bukumbi na shule ya Sekondari Didia zilizopo katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichofanyika katika shule ya msingi Didia leo Ijumaa Januari 19,2018 - Picha zote na Kadama Malunde
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE John Myola akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka wanafunzi kufichua vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na walimu kuwa wadadisi wa mambo mbalimbali wanayoambiwa na wanafunzi wao.
  Meneja Mradi wa Kuzuia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE,Mustapha Isabuda akielezea lengo la kukutana na wanafunzi na walimu kwa ajili ya kujadili namna ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni
  Meneja Mradi wa Kuzuia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE,Mustapha Isabuda akionesha picha ya watoto waliosaidiwa na shirika la AGAPE baada ya watoto hao kukatishwa masomo kwa kupewa ujauzito na wengine kuolewa wakiwa na umri mdogo
  Secilia Kiza kutoka dawati la jinsia na watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwasisitiza wanafunzi,walimu na jamii kwa ujumla kutoa taarifa pale wanapoona kuna matukio ya ukatili dhidi ya watoto.
  Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Didia,Hellena Mussa akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema wataenda kutoa elimu ya namna ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni
  Picha ya pamoja washiriki wa kikao hicho.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  NA TIGANYA VINCENT,RS-TABORA

  KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) linatarajia kufunga na kuomba kwa muda wa siku 21 nchini kote kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mihili mitatu ya Serikali kuanzia Jumatatu ijayo.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt Barnabas Mtokambali wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Biblia (Western Bible College) kilichojengwa Wilayani Uyui na Uzinduzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika Manispaa ya Tabora.

  Alisema kuwa kuanzia Jumatatu (22 January 2018) kitakuwa ni kipindi cha kuanza kufunga na maombi ya katika Makanisa ya TAG nchi nzima waumini wake watafunga na kuomba katika maombi yatakayojulikana kama maombi ya Daniel.

  Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt .Mtokambali alisema kuwa katika maombi hayo mojawapo ya ajenda ni kumwombea Rais Magufuli na Mihimili yote ya serikali ikiwa ni Serikali, Mahakama na Bunge ili aendelee kuwatumikia Watanzania vizuri kama alivyoanza.

  “Mkuu wa Mkoa umeleta ombi lako wakati muafaka la kutaka Kanisa limuombee Rais katika kazi nzuri anazowafanyia Watanzania…Majenerali wa Bwana Yesu wa Kanisa letu wapo hapa kuanzia Jumatau ya tarehe 22 Januari 2018, Makanisa yetu yote tutakusanyika makanisani kwa ajili ya kufunga na kuomba” alisema Askofu Mkuu huyo wa TAG.

  “Tutafunga na kuomba kwa siku 21 mfufululizo ambapo maombi hayo yatajulikana kama maombi ya Daniel…ambapo waumini wetu wote watakuwa wakikusanyika kila siku kuanzia saa 10 Makanisani kumwomba Mungu na siku ya Ijumaa tutakesha makanisani..moja ya item ni kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Bunge, Mahakama na Serikali kuu” alisema Dk. Mtokambali.

  Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa uzinduzi wa Chuo na shule hiyo ya Seminari aliwaomba waumini wa TAG na madhehemu mengine hapa nchini kutumia nguvu waliyonayo ya maombi ya kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika kupigania haki mza wanyonge wa nchi hii.

  Alisema kuwa maombi hayo yatasaidia kumwongezea nguvu katika mapambano aliyaanza ya kuwakomboa wanyonge dhidi ya watu wachache ambao wamekuwa wakichukua rasimali za nchi hii kwa maslahi binafsi.

  Mwanri alisema kuwa wakazi wa Tabora wanaungana na viongozi wa dini katika zote kumwombea na kuongeza Rais asonge mbele wao wako nyuma yake na hawawezi kumuacha pekee yake katika vita hivyo.

  0 0

  Na Jumbe Ismailly -SINGIDA.

  NAIBU Waziri wa maji,Juma Aweso amewaagiza wataalamu wa maji nchini kuwasimia kwa karibu wakandarasi waliopewa kazi za miradi ya maji katika suala zima la utekelezaji wa miradi hiyo na kuwaahidi kwamba wizara hiyo haitaweza kuwa kikwazo katika kuhakikisha wakandarsi hao wanalipwa fedha zao kwa wakati ili miradi hiyo isikwame.

  Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo mjini Singida wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Singida kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

  Aidha Aweso alisisitiza kwamba katika ziara zake anazoendelea kufanya amebaini kwamba matatizo ya upatikanajai wa huduma ya maji safi na salama haiwezi kupatikana kwa wataalamu wa wizara hiyo kukaa ofisini kwa kuchezea kompyuta,bali maji yanapatikana kwa wananchi kutokana na kuwatembelea wananchi na kubaini kero zao.

  “Na tunafanya ziara tukitambua kabisa maji hayapatikani kwa kukaa ofisini kwa kuccheze kompyuta,maji yanapatikana kwa wananchi kwa sababu anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo ya mgonjwa.”alifafanua Naibu Waziri huyo.

  Hata hivyo Aweso aliweka bayana kwamba akiwakatika ziara yake ya wiki moja Mkoani Shinyanga alibaini baadhi ya miradid iliyokuwa ikisuasua lakini baada ya kuisukuma imeanza kwenda vizuri na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaahidi wananchi wa Mkoa wa Singida kwamba anatarajia kurudi Mkoani hapa kufanya ziara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.

  Kwa mujibu wa Aweso lengo la ziara hiyo Mkoani Singida ni kuhakikisha kuwa miradi inayosuasua inapata msukumo ili mwisho wa siku ile azma ya wananchi kuhakikisha wanakwenda kutuliwa ndoo kichwani,inatekelezeka kama ambavyo Rais Dk.John Pombe Magufuli alivyoahidi.

  Akizungumzia changamoto alizokumbana nazo katika Mkoa wa Singida,Naibu Waziri huyo aliweka bayana kwamba katika mji wa Singida bado wananchi wanakabiliwa na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama,jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzi wa kina na wa haraka zaidi.

  Naibu huyo wa Waziri hata hivyo alibainisha kwamba kiwango upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katikaa Mkoa wa Singida ni asilimia 44 kwa wananchi wa mjini wakati azma ya rais ni kwamba ifikapo mwaka 2020,kiwango kifikie asilimia 95 kwa mjini na asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini.

  “Kwa hiyo serikali imetoa fedha sisi tunachoitaka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Singida (SUWASA) inatangaza tenda kwa haraka ili wananchi wa Singida waweze kupata maji lakini kikubwa uzingatie Mkandarasi atakayepatikana ni yule mwenye uwezo katika kuhakikisha mradi hausuisui ili wananchi hao waweze kupata maji safi na salama”alisisitiza Naibu Waziri huyo.

  Akimkaribisha Naibu Waziri huyo,Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alisama ziara ya Naibu waziri huyo imemuwezesha kuona namna miradi hiyo inavyotekelezwa pamoja na changamoto zilizopo.Changamoto hizo kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya huyo ni pamoja na baadhi ya miradi fedha zake kutotolewa na serikali na kuna baadhi ya miradi fedha zake zimepokelewa kilichobakia na utekelezaji na ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati.

  Katika taarifa ya Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) iliyosomwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Patrick Nzamba aliweka bayana kwamba Mamlaka hiyo imepokea zaidi ya shilingi milioni 700 kati ya shilingi bilioni 1,150,000,000/= kwa ajili ya kugharamia visima ambavyo havijawekewa miundombinu viweze kuwekewa ili uzalishaji wa maji uweze kuongezeka.

  Hata hivyo Mhandisi Nzamba alizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na deni kubwa la ankara za nyuma za nishati ya umeme kwa ajili ya uzalishaji wa maji.

  Kwa mujibu wa Mhandisi Nzamba Mamlaka hiyo inadaiwa shilingi milioni 475 katika kipindi cha kuanzia januri hadi sept,mwaka 2017 hali inayosababishiwa wakati mwingine kusitishiwa huduma ya umeme wakati Mamlaka hiyo pia ikizidai taasisi za serikali ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana,taasisi hizo zilikuwa zikidaiwa shilingi 243,065,937.07/=.
  Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso akiteta jambo na katibu wake mara baada ya kupokea taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Singida inayohusu sekta ya maji.
  kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Faustine Kiyui akisoma taarifa ya sekta ya maji ya Manispaa ya Singida kwa Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso.
  Naibu wazziri wa maji,Bwana Juma Awesso akiongozaa kikao cha watendaji wa Halmashauri ya wilaya na Manispaa ya Singida baada ya kupokea taarifa za Halmashauri hizo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)


  Ni baadhi ya watendaji wa serikali wa wilaya ya Singida wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Dr. Harrison Mwakyembe, Leo Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 16 Serengeti Boys iliyopo kambini kwenye hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na kuwaachia ujumbe wa Serikali. 

  Dr. Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia Vijana wanaounda timu hiyo kuwa serikali inawaamini na wanalo jukumu la kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania. 

  Amewataka kupambana kwa ajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa Vijana hao. 

  Aidha Dr. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia. "Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa".Alisema Dr. Mwakyembe. 

  Katika ziara yake hiyo Dr. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa kirafiki kati ya Serengeti Boys na Makongo Sekondari iliyomalizika kwa Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 4-1.

  Kabla ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara kumkamata na kumuhoji Mkurugenzi Mtendani wa Mamlaka ya Maji Musoma (MUWASA) Mhandisi Gantala Said kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji Bunda.

  Mbali na Mkurugenzi huyo pia TAKUKURU inawashikilia wakandarasi wanaojenga mradi huo ambao ni Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi Bw Mauza Mmangi ambaye ndiye mkandarasi anajenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenye eneo la Nyabehu hadi Bunda mjini.

  Wengine waliokamatwa ni pamoja na Mhasibu wa Kampuni ya Ujenzi ya Nyakirang'anyi Bw. Amon Gideon pamoja na viongozi wa kampuni nyingine ya ujenzi ya Fortrss Bw. Juvenari Chirianga na Ephraim Mpeko ambao nao walishiriki katika ujenzi wa mradi huo.

  Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo jana jioni (Ijumaa, Januari 19, 2018) baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kueleza sababu zilizosababisha mradi wa maji Bunda kutokamilika pamoja na Serikali kutoa fedha nyingi.

  Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Mara, alichokiitisha mjini Bunda, Waziri Mkuu alisema alimua kuitisha kikao hicho baada ya kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo hususan inayosimamiwa na MUWASA .

  Alisema kwa sasa Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo itawachukulia hatua wote watakaokwamisha miradi ya maji.

  Waziri Mkuu amesema malengo ya kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

  Pia Waziri Mkuu aliagiza kupitiwa upya kwa mradi huo kwa sababu hafurahishwi na ujenzi wake.” Kama Mkurugenzi wa MUWASA anasema mradi umekamilika kwa asilimia 98 sasa kwa nini wananchi walalamikie kukosa huduma hiyo.”

  Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa akimlipa mkandarasi fedha kabla ya kufanya kazi ambapo hadi sasa tayari mkandarasi anayenga mradi huo ameshalipwa zaidi ya sh. bilioni saba na mradi haujakamilika na wananchi wanaendelea kutumia maji ambayo siyo salama.

  Waziri Mkuu alisema viongozi hao wahojiwe na wakibainika kuhusika na ubadhilifuu wa fedha za mradi huo, wachukuliwe hatua kali za kisheria.”Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za maji, hivyo hatuhitaji mtu atakayeenda kinyume na mpango huo.”

  Mradi wa kupeleka maji kwenye mji wa Bunda maji kutoka ziwa Victoria katika eneo la Nyabeho ulisanifiwa mwaka 2006 na ulikuwa unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha za maendeleo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Adam Malima aliagiza kufungwa na ofisi za MUWASA na kuwataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kutoruhusiwa kuingia ofisini hadi hapo uchungi utakapokamilika.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAMOSI, JANUARI 20, 2018.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Maji Musoma, Mhandisi Said Gantala (kushoto) akitoka kwenye ukumbi wa Balili Rock Resort mjini Bunda baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuamuru kuwa akamatwe na ahojiwe na TAKUKURU Januari 19, 2018.Kulia ni Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mara, Alex Kuhanda.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, sehemu ya ujenzi wa barabara ya mchepuo kutoka Chimwaga-Ihumwa yenye urefu wa KM 10 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari yanayoingia mkoani humo.Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Chimwaga-Ihumwa KM 10 kwa kiwango cha lami, Mhandisi Nicholaus Mzeru, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi kwa waandishi wa habari ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.4 na KM 8 zimeshakamilika kujengwa, mkoani DodomaNaibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa KM 11.7, inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani humo.Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, athari za mvua eneo la katondo katika barabara za mji huo.Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, wakikagua athari za mvua eneo la Kibaigwa, katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana nae wakati akikagua athari za mvua eneo la Kibaigwa, katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.Muonekano wa sehemu ya barabara ya mchepuo ya Chimwaga-Ihumwa yenye urefu wa KM 10 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.

  ………………………………………………………………………….

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa (Km 11.7) na Chimwaga – Ihumwa (Km 10) utasaidia kupunguza msongamano kwa magari yanayoingia Dodoma mjini.

  Naibu Waziri huyo ameyasema hayo wakati akikagua barabara hizo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo amesisitiza kwa makandarasi wanaojenga barabara hizo kuhakikisha wanamaliza kazi hizo kwa muda uliopangwa na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.

  “Tutaendelea kujenga na kuboresha barabara hizi za mchepuo lengo ni kupunguza foleni katikati ya mji kwani Dodoma sasa inakua kutokana na uwepo wa watumishi wengi wa Serikali na ongezeko la magari, kwa hiyo sisi kama Serikali hatuna budi kuangalia namna ya kuboresha miundombinu yetu ili ikidhi haja ya ongezeko hili”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Aidha, amefafanua kuwa barabara hizo zikikamilika zitakuwa ni njia mbadala kwa watumiaji kwani sio lazima kwa magari yote kupita mjini na badala yake yatatumia njia nyingine za mchepuo kuendelea na safari zake.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua athari za mvua katika barabara za mji wa Dodoma na kuwataka wananchi na madereva kuchukua tahadhari ili kuepusha hatari zinazoweza kuwakabili wakati wakivuka ama kupitisha magari yao katika kipindi hiki ambacho baadhi ya sehemu za barabara zinajaa maji kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha. 

  Amewaomba viongozi mbalimbali wa Serikali kushirikiana katika kutoa ushauri kwa wananchi kuhusu utafutaji wa maeneo yanayowafaa kuishi ili kunusuru maisha yao na mafuriko ambayo yanaweza kuwakabili kutokana na kuchagua maeneo yasiyo sahihi kwa makazi ya binadamu.

  Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, amefafanua kuwa barabara ya Mbande- Kongwa yenye urefu wa KM 11.7, kwa sasa imejengwa kilometa Tano ikiwa ni awamu ya kwanza na kufikia mwezi ujao watajenga tena kilometa nyingine Tano.

  Naye, Msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Chimwaga – Ihumwa yenye urefu wa KM 10 kwa kiwango cha lami, Mhandisi Nicholaus Mzeru, amesema mradi ulianza mwaka 2013, ambapo kwa sasa umefika asilimia 92.4 na kilometa 8 tayari zimeshajengwa.

  Ujenzi wa Barabara ya Chimwaga- Ihumwa (Km 10), inajengwa na mkandarasi Nyanza Road Works kwa gharama ya takriban shilingi bilioni 15 ambapo ujenzi wake unaendelea na unategemewa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama.

  Amekagua shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari 20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama.

  Waziri Mkuu amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima zao hilo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo zinazozalishwa katika shamba hilo zitagawanywa kwa wakulima katika kata zote 18 za wilaya ya Butihama.

  Alisema mbali ya kuzalisha mbegu pia wanatarajia kuanzisha kiwanda cha kuchakata zao la mihogo ili kuweza kuliongezea thamani.Mbali na shamba la mbegu bora za mihogo pia kikosi hicho kina shamba lingine la pamba lenye ukubwa wa ekari 57, ambapo wanatarajia kuvuna tani 57 za pamba. Mwakani wanatarajia kuongeza ukubwa wa shamba na kufikia ekari 300.

  Awali, Waziri Mkuu alitembelea shamba darasa la mkoa wa Mara la zao la pamba lililopo Kisangwa wilayani Bunda akiwa njiani kuelekea wilayani Butihama, kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima alisema shamba darasa hilo ni moja ya jitihada za Mkoa wa Mara kuelimisha wakulima wa zao hilo mbinu bora za uzalishaji ili kuongeza tija katika uzalishaji.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakati alipotembelea shamba la kuzalisha mbegu bora ya mhogo  aina ya mkombozi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Rwmkoma wilayani Butiama, Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama  shamba la Pamba wakati alipotembelea shamba la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililopo Rwamkoma wilayani Butiama Januari 20, 2018. Shamba hilo  pia linazalisha mbegu bora za mhogo aina ya mkombozi.

  0 0

  Uongozi mpya wa Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mara baada ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro.


  SHIRIKISHO la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), litatekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania Bara, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mabonanza kila mwisho wa mwezi yatakayohusisha wachezajiw a michezo mbalimbali.

  Moshi Makuka, Katibu Mkuu wa SHIMIWI, alisema wamekubaliana katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hivi karibu, ambapo wataanza na bonanza kubwa litakalofanyika Februari mwaka huu mkoani Dodoma, ambapo sasa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali zimeshahamia mkoani hapo.

  “Hili bonanza litakuwa kubwa sana kwani ukiangalia tayari wizara, taasisi na Idara za serikali kwa asilimia kubwa zimeshahamia Dodoma, hivyo timu zianze kujiandaa na baada ya kukamilisha hili baadaye katika tarehe zitakazotangazwa tutafanya tena Jijini Dar es Salaam,” alisema Makuka.

  Makamu wa Rais, mwaka jana alitoa agizo kufanyike mazoezi ya kila mwezi kwa kuhusisha wafanyakazi ili kujijengea afya zao. Michezo inayochezwa SHIMIWI ni pamoja na soka, netiboli, kuvuta kamba, baiskeli, karata, bao na draft (wanawake na wanaume).

  Mbali na kuanza kwa mabonanza, pia Kamati hiyo ya Utendaji imeunda Kamati mbalimbali ikiwemo ya Habari na Mawasiliano ambayo itaongozwa na Itika Mwankenja (Mwenyekiti), Elias Malima (Katibu), huku wajumbe ni Bahati Mollel, Jane John, James Katubuka, David Kitila na Jessey John; kamati ya utendaji na nafasi zao ni Daniel Mwalusamba (Mwenyekiti), Ally Katembo (Makamu Mwenyekiti), Makuka (Katibu Mkuu), Alex Temba (Katibu Msaidizi), William Mkombozi (Mweka hazina), Frank Kibona (mweka hazina msaidizi) na wajumbe ni Appolo Kayungi, Damian Manembe, Seleman Kifyoga, Assumpta Mwilanga na Aloyce Ngonyani, huku wajumbe wa viti maalum ni Mariam Kihange na Mwajuma Kisengo.

  Wanaounda Kamati ya Mipango ni Mwalusamba Mwenyekiti), Mkombozi (Katibu) na wajumbe ni Makuka, Ngonyani, Kihange na John Jambele; huku kamati ya Ufundi inaundwa na Kayungi (Mwenyekiti), Manembe (Katibu) na wajumbe ni Kisengo na Joyce Benjamin; Kamati ya Nidhamu wapo Katembo (Mwenyekiti), Temba (Katibu) na wajumbe ni Marcel Katemba na Mwilanga.

  Kamati ya usajili itaongozwa na Temba (Mwenyekiti), Kibona (Katibu) na James Emmanuel (Mjumbe); nayo Sekretarieti ya Uendeshaji inaundwa na Kihange (mwenyekiti), Kifyoga (Katibu), na wajumbe ni Bahati Magambo, Buya Ndalija, Justo Mwandelile, Ahmed Chitagu, Peter Lihanjala, Gracia Kyelula, Peter Onono, Modesta Kaunda, Amina Kakozi, Ismail Ismail, Sophia Mkama na James Emmanuel.

  Nayo Kamati ya Huduma za tiba itaongozwa na Joakim Mwaipaja (Mwenyekiti), Magreth Mtaki (Katibu), na Wajumbe ni Richard Yomba, Haji Masasi, Jafari Chikoko na Gration Kaizirege.

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokea jumla ya Wanachma wapya 350 katika Kongamano Maalum lililoandaliwa na Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

  Kheri amewataka Vijana wanaopata nafasi za uongozi kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwakomboa wengine na kuacha kutumika na makundi ya watu.

  “Vijana wengi ambao wameaminiwa wameacha kushughulika na matatizo ya Vijana na yenye tija kwa taifa, wamekuwa wakiendeshwa na watu ambao wanamaslahi yao binafsi” amesema Kheri

  Amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweza kuwaamini Vijana, hivyo kila kijana wa CCM  anabudi kuwaunga mkono viongozi wote Vijana ambao wana nia ya dhati ya kutaka kulifikisha taifa hili pale linapotakiwa liwe.

  Alimaliza kwa kutoa wito kwa Vijana wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Chaguzi ndogo zinazoendelea na kuifanya CCM ishinde kwa kishindo.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James akizungumza na Wanachama wa Umoja huo Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika ukumbi wa Urafiki leo jijini Dar Es Salaam .
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James, akipokea Risala kutoka kwa Katibu wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka, akisalimiana na Mmoja ya Wanachama wapya waliojiunga na Chama hicho kupitia Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Sehemu ya Wajumbe wa Uvccm kutoka Wilaya Mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
  Sehemu ya wanachama wapya 350 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Wakila Kiapo cha Uaminifu.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James, akisalimiana wanachma wa CCM

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Edwin Kunambi akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (Press Club) wakifuatilia mkutano huo mapema leo mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Bw.Herbet Chidawali akitoa maelezo mafupi ya namna chama hicho kinavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na changamoto zinazokikabili kwa sasa.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Khalifa Kondo akizungumza na wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (Press Club) wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.  Na. Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

  Serikali kupitia Idara ya Habari ya MAELEZO imesema itatoa kipaumbele kwa waandishi wa habari wa Dodoma kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo kutokana na mkoa huo kuwa na matukio mengi ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na kutembelewa na wageni wa Kimataifa.

  Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Kanda ya Kati (The Central Press Club (CPC)).

  “Nawathibitishia kuwa Serikali sasa iko Dodoma, Dunia sasa inategemea kusikia mambo mengi kutoka Dodoma. Shughuli za Kitaifa na Kimataifa zitakuwa zikifanyika hapa Dodoma ,” alisema Dkt. Abbasi.

  Amesema mkoa huo utakuwa unapokea wageni mbalimbali wa Kimataifa hivyo ni lazima waandishi wa habari wa mkoa huo wawe na uelewa wa mambo ya Itifaki na diplomasia ili kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.“Lazima tubadilike hata katika uvaaji wetu, kwani sasa tunaenda kukutana na viongozi wakubwa wa nchi na wa Kimataifa,” aliongeza Dkt. Abbasi.

  Aidha amesema, Idara ya Habari MAELEZO itaandaa mafunzo mafupi katika maeneo mbalimbali ya tasnia ya habari ikiwemo masuala ya itifaki na mambo ya diplomasia ili kuwajengea uelewa waandishi hao.Hata hivyo, Dkt. Abbas amesema Idara yake itatafuta ufadhili kwa mabalozi mbalimbali yaliyopo hapa nchini ili waandishi hao wakajifunze namna vyombo vya habari vya Kimataifa vinavyofanya kazi.

  “Mwaka 2017 tulifanikiwa kupata ufadhili wa ubalozi wa China na waandishi Kumi walienda China, Bado hatujajua ni waandishi wangapi watafanikiwa kwenda mwaka huu, lakini tutao kipaumbele kwa waandishi wa habari walioko Dodoma,” alisisitiza Dkt. Abbasi.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CPC Habel Chidawali amesema waandishi wa habari walioko mkoani humo walikuwa na changamoto ya kutoweza kujiendeleza katika tasnia ya habari kutokana na vyuo vilivyopo mkoani humo kutokuwa na kozi ya masuala ya habari.

  “Kama viongozi wa CPC tumetembelea baadhi ya vyuo vilivyopo mkoani hapa na kuvishawishi kuanzisha kozi ya masuala ya habari katika vyuo vyao. Vyuo vitatu vimetuahidi kuanzisha kozi hiyo mwaka huu,”alisema Chidawali.Amesema kuwa ni mategemeo yao kuwa, waandishi wengi watajiendeleza kwa mwaka huu jambo ambalo litawaongezea weledi katika kazi zao za kila siku hasa kwa kipindi hiki ambapo sasa Serikali yote ipo mkoani humo.

  Mkoa wa Dodoma tayari umepokea viongozi wakuu wa nchi wawili yaani Makamu wa Rais mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri na Watumishi wa Serikali zaidi ya 3000. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kuhamia mkoani humo muda wowote mwaka huu.

  0 0

  Shirika lisilokuwa la kiserikali la faidika wote pamoja FAWOPA limetoa Elimu kwa Wadau Mbalimbali wa sekta hiyo Juu ya uandaaji wa Bajeti na kuweza kuwasilisha kwa kamati za Shule, ili kuzifanyia kazi Kwa lengo la kuondokana na migongano inayojitokeza baina ya Wazazi na Walimu.

  Mratibu wa shirika hilo Baltazar Komba amesema Bado viwango vya Bajeti mashuleni haijaainisha, matokeo yake Shule Nyingi wamekuwa wakitegemea wazazi kwa ajili ya michango kabla ya Mh. Rais John Pombe Magufuli kukataza Michango yoyote Mashuleni.

  Aidha katika Ufuatiliaji uliofanywa na Kamati ya FAWOPA ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani imebaini kuwa Halmashauri haina Bajeti maalum ya Elimu zaidi ya Bajeti kutoka Serikali Kuu.

  Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha manispaa hiyo inapiga hatua katika suala la elimu kutokana mkoa was Mtwara kuwa nyuma katika Ufaulu ukilinganisha na mikoa mwingine.
   Pichani ni mratibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la faidika wote pamoja FAWOPA iliyopo Mkoani  Mtwara  Baltazar Komba akizungumza na wadau mbali mbali wa elimu juu ya Uboreshwaji wa Elimu mkoani Humo.
  Mshauri wa Mambo ya Kisheria FAWOPA Marythereza Namangi akitoa mafunzo kwa Wadau Mbalimbali wa Elimu Juu ya uandaaji wa Bajeti katika mashule kama Moja ya dhana ya Uwazi na Uwajibikaji.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozana na Mama Maria Nyerere kuingia kwenye uwanja wa Mwenge katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018. Kulia ni mkewe Mary .
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama, Januari 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni mkewe Naima .
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Mkewe Mary na Mama Maria Nyerere wakiwapungia wananchi katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa Mwenge kijijini Butiama Januari 20, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2017
  Wananchi wa Butiama wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijijini hapo Januari 2018
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwengekijijini hapo Januari 20, 2018.
  Mama Maria Nyerere akiwasalimia wananchi wa Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwenge kijijini hapo Januari 20, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


   Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati), akishiriki katika maombi ya shukurani na kuikabidhi Nchi kwa Mungu yaliyofanyika leo Nyumba ya Huduma Abundant Blessing Centre  (ABC) Tabata  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa ABC,  na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.

  Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye Mratibu wa maombi hayo akizungumza kwenye ibada ya maombi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila, akimkaribisha Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwenye ibada hiyo mara baada ya kuwasili.
   Kwaya ya Haleluya Selebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu katika ibada hiyo.
   Maombi yakifanyika.
   Mtumishi wa mungu, John Kanafunzi kutoka Kanisa la KLPT Mbezi Mwisho akiongoza kuimba nyimbo za kusifu.
   Watumishi wa Mungu  wakiwa kwenye maombi hayo. Kutoka kushoto ni Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah na Askofu Mhina.
   Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Wanamaombi kutoka Kibaha mkoani Pwani wakiwa kwenye maombi hayo.
   Maombi yakiendelea.

  Mmoja wa waombaji  Baba Askofu, David Mwasota akiongoza maombi ya shukurani.
   Taswira ndani wakati wa maombi hayo.
   Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah, akifanya maombi.

  Askofu Emanuel Mhina akiongoza maombi hayo.
  Mtumishi wa Mungu akiomba katika ibada hiyo.
   Viongozi wa dini na waumini wakiwa kwenye maombi hayo.
   Utulivu wa viongozi wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa.
  Waziri Mwakyembe akizungumza na waumini wakati wa maombi hayo

  Na Dotto Mwaibale

  WAZIRI wa Habari Utamaduni, Sanaa  na Michezo,  Dk.Harrison Mwakyembe amesema maombi yaliyofanywa na viongozi wa dini wakati wa uchaguzi mkuu kuomba nchi ipate rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yaliyo mleta Rais Dk, John Magufuli.

  Mwakyembe ameyasema hayo wakati wa maombi maalumu ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yaliyofanywa na maaskofu na viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali katika Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre Tabata jijini Dar es Salaam leo.

  "Maombi yenu ya kumuomba Mungu atupe rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yalisababisha kumpata Rais John Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu ambaye anapigania maslahi ya wanyonge hasa maskini kwa kupambana na watu waliokuwa wakijineemesha wenyewe kwa kutumia fedha za umma vibaya" alisema Mwakyembe.

  Alisema katika hatua nyingine Rais Magufuli ni rais pekee ambaye amekuwa akiwaomba viongozi wa dini wamuombee kwa kuwa anafahamu bila ya maombi hawezi kufanya chochote na maamuzi yake yote yanatokana na maombi ambayo anafanyiwa na viongozi wa dini.

  "Serikali ina utambua mchango mkubwa mnaoufanya wa kumuombea Rais na nchi kwa ujumla hivyo mnapokuwa na malalamiko yenu msiyazungumzie chini chini tuelezeni tutayafanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine" alisema Mwakyembe.

  Akizungumza katika ibada hiyo ya maombi ya kuliombea taifa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alisema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayemsema rais vibaya wakati sasa anafanya mambo makubwa ya kuijenga nchi.

  "Kuna baadhi ya watu wanamnenea vibaya rais wetu kutokana na kazi nzuri anayoifanya nasema hatutakubali kuona rais akifanyiwa hivyo mtu yeyote atakayebainika tutamkamata bila ya kumuonea huruma" alisema Mshama.

  Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye mratibu wa maombi hayo alisema maombi hayo ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yameshirikisha viongozi wa makanisa mbalimbali na huduma za Kikristo na kuandaliwa na I GO Africa for Jesus Prayer Movement na kuwa maombi ya namna hiyo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara.

  Alisema maombi yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru wa Taifa letu ulipatikana pasipo kumwaga damu pamoja na ulinzi na neema na rehema katika nchi yetu.Alitaja eneo lingine la maombi ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya nchi yetu kuwa na utajiri na rasilimali nyingi kama dhahabu, almasi, uranium, mafuta ya petroli, ardhi nzuri, mbuga za wanyama, gesi, mito na milima.

  Alisema maombi mengine yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa viongozi ambao wameliwezesha taifa kupiga hatua mbalimbali za maendeleo licha ya kuwepo changamoto kama za umaskini, maradhi na ujinga.

  Askofu Ndabila alisema maombi mengine yalikuwa ni kuliombea Taifa, Kanisa na Afrika kwa ujumla.Alisema anashangaa kuwasikia watu wakilalamika kuwa eti vyuma vimekaza wakati nchi ina kila rasilimali.Maombi hayo yalihudhuriwa na maaskofu takriban tisa kutoka makanisa mbalimbali.


older | 1 | .... | 1492 | 1493 | (Page 1494) | 1495 | 1496 | .... | 1903 | newer