Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1481 | 1482 | (Page 1483) | 1484 | 1485 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu, akizungumza na Naibu Spika, Tulia Akson alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kutembelea MSD kuona shughuli mbalimbali za uhifadhi dawa na Vifaa tiba jijini Dar es Salaam jana.
  Hapa Naibu Spika, Tulia Akson akitembelea ghara la kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
  Naibu Spika akipata maelezo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu, akiagana na Naibu Spika, Tulia Akson baada ya kumaliza ziara hiyo ya kikazi.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akimsindikiza Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA IKULU

  0 0

  Na Gideon Mwakanosya-Songea

  MBUNGE wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kukihama chama cha mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wakiwemo wa vyama vya upinzani kwa kile alichodai kuwa magari ya upinzani yanaenda kuzama na hayajulikani yataibuka lini.

  Uwazi huo ameuweka jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma kwa tiketi ya CCM Dk, Damas Ndumbaro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bombambili Manispaa ya Songea.

  Nnauye ambaye aliwahi kuwa katibu wa hitikadi na uenezi CCM taifa na Waziri wa Habari, Michezo na Sanaa katika serikali ya awamu ya tano alisema kuwa kama kuna watu walidhani atakihama chama cha mapinduzi (CCM) na kwenda upinzani wasahau kabisa .

  Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa bombambili alisema kuwa kama kuna kuwa na matatizo ndani ya CCM tunaonyana ndani ya chama na kuyamaliza na siyo kuhama chama.
  “Naikubali serikali ya awamu ya tano inayongonzwa na jemedali Dk. John Magufuli pamoja na makamu wa Rais na waziri mkuu wake kuwa ipo imara na mimi naapa kufia CCM na siyo vinginevyo” alisema Nape Nnauye.

  “Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo” alisema mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
  Katika kampeni hizo ambazo uchaguzi wake utafanyika Januari 13 mwaka huu Nape Nnauye na Moses Machali aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kasulu mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya NCCR Mageuzi wamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jimbo la Songea hasa wanapokuwa majukwani.

  0 0  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akiwaeleza na wafugaji wa Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umuhimu wa zoezi la kupiga chapa ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.  Na Kumbuka Ndatta, KASULU

  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo ameagiza ng’ombe wote wenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea kuhakikisha wamepigwa chapa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya upigaji chapa Januari 31 mwaka huu, kwani zoezi hilo sio la hiari bali ni la lazima na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

  Dk. Mashingo ametoa kauli hiyo wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa Wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.

  Dk Mashingo aliwaambia wafugaji hao kutambua kuwa zoezi hilo linasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 na kuwasititiza kuwa haijulikani Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Januari 31 mwaka huu.

  Aidha Dk. Mashingo alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wafugaji sehemu maalum ambayo ng’ombe anapotakiwa kupigwa chapa mwilini mwake ili kutoharibu ngozi yake inayotegemewa kwa matumizi mengine.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amesema zoezi la upigaji chapa linaendelea vizuri na mwitikio ni mkubwa kutoka kwa wafugaji ambapo jumla ya ng'ombe 93,182 wameshapigwa chapa kati ya ng'ombe 345,469 waliotambuliwa ambao ni sawa na asilimia 27.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Fatima Laay amemweleza Katibu mkuu kuwa jumla ya ng'ombe 7,552 kati ya 10,000 wenye umri wa zaidi ya miezi sita na kuendelea tayari wameshapigwa chapa ambao ni sawa na asilimia 75.52.

  Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alikiri kuwepo tatizo la Ng'ombe kupata vidonda vikubwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo jambo lilochangiwa na wafugaji kutoelimishwa sehemu sahihi ya kupiga chapa mifugo.

  "Mimi ng'ombe wangu bado hawajapigwa chapa,waliopigwa chapa walipata vidonda vikubwa kwa hiyo kama wataalam wetu ngazi ya vijiji wameelimishwa vizuri jinsi ya kupiga chapa basi haina shida nitawapeleka ng'ombe wangu wakapigwe chapa na kuhamasisha wananchi wengine kuunga mkono zoezi hili "alisema Nsanzugwanko.

  0 0

  Waziri mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA, amewaagiza viongozi wa halimashauri ya NYASA akiwemo mbunge wa jimbo hilo, mkuu wa wilaya na mkurugenzi, kumaliza tofauti zao na madala yake wawaletee wananchi maendeleo. Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na watumishi na wakuu wa idara mbalimbali wa halimashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

  0 0

  Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kushoto) akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini ndg:Justine Monko (kulia) wakati wa mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini  Bi Grace Shindika Akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
  .Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (katikati) akizungumza na Mgombea Ubunge Jimbo ;la Singida Kaskazini ndg: justine Monko (kwanza kushoto) pampoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg:Juma Kilimba.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe: Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida mhe: Martha Mlata  akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida ndg:Juma kilimba akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kumnadi Mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
   Viongozi wakifurahia jambo
  Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Justine Monko akijinadi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


  0 0


  *NI kamati maalum itakayochunguza athari za bonde hilo na kumpatia majibu
  *Akagua maeneo mbalimbali ya bonde hilo na kuhushudia athari zaidi

  Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ameteua Kamati maalum ambayo itaishahuri Serikali namna ya nini kifanyike katika kushughulikia athari za bonde la Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.

  Waziri Dk Kigwangalla amebainisha kuwa Kamati hiyo aliyoiteua, ndio itamshahuri juu ya bonde hilo litasimamiwa vipi pamoja na namna bora ya hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina mahitaji makubwa ikiwemo chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme unaotarajiwa kufikia megawatts 2100 huku pia bonde hilo likiwa na utajiri wa kuwepo na aina zaidi ya 400 ya ndege pamoja na mnyama anaina ya Puku ama Sheshe ambaye hapatiani duniani kote zaidi ya Tanzania pekee.

  "Hii ndio Kamati yangu, itakayonishahuri juu ya bonde ili litasimamiwa vipi. Hii ndio Kamati ambayo itanishahuri mimi na kwamaana hiyo Serikali kwa ujumla wake juu ya namna bora ya uhifadhi hususani katika eneo lile la Pori tengefu.

  Hapa kuna vitu viwili vya kuzingatia: Ardhi Ohevu (Ramsar site) ambalo lina eneo lake huku pia eneo la pori tengefu nalo kichukua nafasi kubwa zaidi" Amesem Waziri Dk Kigwangalla wakati wa kuteua Kamati hiyo.

  Kamati hiyo inaundwa na wajumbe mbalimbali ambao wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndugu Andrew Napacho, Pia wajumbe ni Brig. Gen. (Mst.) Edmund Mndolwa, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Mstaafu, Suleiman Kova, Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha wafugaji Bwana Semkae Kilonzo (Policy Forum).

  Wengine ni Dk. Simon Mduma, Prof. Jaffar Kideghesho, Ruzika Muheto, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, MKuu wa Wilaya ya Kilombero na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.

  Wemgine ni Mwenyekiti Halmashauri Ulanga, M/Halmashauri Kilombero, M/Halmashauri Malinyi na M/Halmashauri Ifakara.

  Pia yupo Mtendaji Mkuu wa KPL, Mtendaji MKuu wa Illovo, Mkuu Kikosi JKT Chita. Wengine ni Dk. Aggrey Mlimuka, Mwakilishi kutoka mamlaka ya maji Bonde la Kilombero, Mwakilishi kutoka Wizara ya ardhi.

  Wajumbe wengine ni Ndugu. Innocent Kylogeris, Dk. James Wakibara pamoja na Mkurugenzi Mkuu TAWA ambaye atakuwa Katibu wa Kamati hiyo.

  Hatua hiyo inafuatia Waziri Dk Kigwangalla kufanya ziara maalum kwenye bonde hilo la kilombero ambapo ameweza kushuhudia athari kubwa zaidi zilizofanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji ambao wameonekana kuvamia maeneo makubwa ndani ya pori tengefu la bonde pamoja na Kwenye eneo ohevu ndani ya bonde hilo.


  Waziri wa Maliasili na Utali Dkt Hamis Kigwangalla

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kulia), akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ziara ya kikazi ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa, anayefuatia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, pamoja na Maofisa wa Jeshi hilo wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (katikati), akitoa neno wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia) na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele (kulia) wakiteta jambo wakati walipokuwa kwenye moja ya ofisi ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana, ili kuona namna Kamisheni hiyo inavyofanyakazi zake.

  Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji, Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
  Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
  Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
  Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima
  Mbolea ikibebwa kuingizwa kwenye malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
  Malori yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
  Maghara ya kampuni ya Premium Agro Chem Limited yenye mbolea hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo.

  Waandishi wa Habari jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo.

  Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  “Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba.

  Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa.

  Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika wanatulia kwa kupokea mbolea.

  “Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba.

  Mkumba alisema wameamua kuingia makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji, lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali.

  Meneja Biashara wa Primium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji. 

  Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50.

  Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi.

  “Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.

  0 0  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipata maelezo ya hali ya sekta ya mifugo na Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwila (mwenye suti nyeusi) alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipokea maelezo ya changamoto za ukaguzi mazao ya mifugo na Uvuvi kutoka kwa Afisa Uhamiaji Konstabo, Rahabu Joel alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula leo.  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akiangalia mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokamatwa katika kituo cha mpaka cha Mutukula mkoani Kagera. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Uvuvi Mwanaidi Mlolwa katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Missenyi Limbe Maurice. Kilo120 zilikamatwa katika kituo hicho.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifungua mlango wa gari lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato zenye thamani ya shillingi 20,850,000/= kwenye mpaka wa Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017

  Na John Mapepele

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuhakikisha inafufua mara moja mnada wa Mlusagamba ifikapo mwezi Februari mwaka huu ili kudhibiti zaidi ya milioni mia moja zinazopotea kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali ya kusafirisha mifugo nje ya nchi kwa kupita njia za panya.

  Waziri Mpina aliyasema haya leo alipokutana na uongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara katika kituo cha mpaka cha Rusumo baina ya Tanzania na Rwanda kukagua shughuli mbalimbali za sekta za Mifugo na Uvuvi baada ya kutokea katika kituo cha Mutukula mkoani Kagera ambapo pia alifanya ukaguzi kama huo na kukamata kilo 120 za mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokuwa yakitokea nchi jirani ya Uganda bila kufuata utaratibu.

  “Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya sekta ya mifugo na uvuvi naelekeza kwamba ifikapo Februari mwaka huu nataka miundo mbinu yote iwe imeboreshwa na mnada wa Mlusagambo uwe unafanya kazi katika kiwango cha mnada wa upili na mimi mwenyewe nitahakikisha ninakuja kuuzindua”lisisitiza Mpina

  Waziri Mpina alisema kutokuwepo kwa Mnada wa Mlusagambo kunaipotezea Serikali mapato makubwa ambapo mifugo mingi imekuwa ikiuzwa katika nchi jirani na Serikali kuambulia kiasi kidogo cha fedha kutokana na wafanyabiashara kupita njia za panja na kufanikiwa kukwepa kulipa kodi malimbali za Serikali.

  Alisema taarifa inaonyesha kuna idadi kubwa ya Ng’ombe wanaopita njia za panya ambao hawatozwi ushuru wa kushafirishwa jambo ambalo amelilalamikia kuwa ni hujuma na kuendekeza rushwa baina ya watendaji wa Serikali.

  Aidha amesema Wizara inakusudia kuomba Serikali kupandisha ushuru wa kusafirisha mifugo (movement permit) kufikia shilingi 50,000/= badala ya shilingi 20,000/= ya sasa kwa kuwa hailingani na hali halisi ya soko na gharama za utunzaji wa mifugo hiyo.


  “Tutahakikisha tunaiomba serikali ibadili ushuru huu kwa kuwa mfugaji anatumia gharama kubwa za kumfuga na kumnenepesha mfugo kwa zaidi ya miaka mitano halafu anakuja kupata shilingi 20000 tu ni jambo lisilokubalika” alisisitiza Mpina

  Aliongeza kwamba baada ya kukamilika kwa mnada huo Serikali itaweka vizuizi katika njia zote za panya ambapo pia alisisitiza watendaji wa Serikali na wananchi kwa ujumla kuwa waadilifu na kuwa walinzi badala ya kutegemea viongozi wa kitaifa wa Serikali kulinda utoroshaji wa raslimali za taifa ikiwa ni pamoja na mifugo, samaki na mazao mbalimbali yatokanayo na sekta hizo.

  Aidha alisema katika njia zote za panya inashangaza kuona kuna wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, kata, vyombo vyote vya serikali vya ulinzi na usalama pia kuna Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya lakini utoroshaji unaendelea bila wahalifu hao kukamatwa, ambapo aliwataka watendaji wote kuwa waaminifu na kumwagiza Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua za mara moja watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na rushwa.

  Akitolea mfano wa jinsi alivyokamata kilo 65,600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia hivi karibuni, alisema zoezi hilo lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.

  “Naomba kusema raia mwema huyo alitoa taarifa siyo kwa sababu alilipwa fedha bali alikuwa na uchungu na uzalendo wa dhati kwa taifa lake baada ya kuona kwamba raslimali ya taifa inatoweka” alihoji Waziri Mpina

  Aidha, Waziri Mpina alisema Wizara inapambana kuhakikisha kwamba kunakuwa na kodi ya mifugo ambapo kila mfugo utatakiwa kulipiwa kodi tofauti na mfumo wa sasa ambapo hakuna kodi ya moja kwa moja inayotozwa kwa mifugo.

  Alisema uanzishwaji wa kodi ya mifugo utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya mifugo katika kipindi kifupi kijacho kwa kuwa fedha itakayokusanywa itatumika katika kununua madawa ya ruzuku kwa mifugo, chanjo, kuboresha malisho na miundombinu mbalimbali ya mifugo ikiwa ni pamoja na majosho na malambo ya kunyweshea maji mifugo hiyo.

  Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya mifugo yote nchini inateketea nchini wakati wa jua kali kipindi cha kiangazi kwa sababu ya kukosa maji na malisho bora jambo ambalo ni hasara kubwa kwa taifa.
  Mbunge wa jimbo la Ngara, mheshimiwa,Alex Raphael Gashaza alipendekeza wafugaji kutambuliwa kwa kulipa kodi ya mifugo na kuanzisha vitalu maalumu vya ranchi za mifugo ili kuthibiti magonjwa na kuinua ubora wa mifugo.

  Alisema utaratibu huo pia utapunguza migogoro mingi inayojitokeza sasa baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ambapo ambapo pia ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya katika zoezi linaloendelea la kupiga chapa mifugo.

  Akitoa ufafanuzi Waziri Mpina alisema Serikali inaruhusu uanzishwaji wa ranchi ndiyo maana suala hilo limezingatiwa katika sheria mbali mbali za tasnia ya mifugo ikiwa ni pamoja na Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010, Sheria ya Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo Namba 13 ya Mwaka 2010, na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo namba 4 ya Mwaka 2012.

  Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele alimweleza Waziri kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2017 jumla ya kilo 903,018 za mazao ya uvuvi kutoka katika maeneo ya Mwanza,Mganza,Kagera, Kigoma na Dar es Salaam yenye thamani ya shilingi bilioni mbili yalikaguliwa na kuhakikiwa na kuruhusiwa kusafirishwa kupitia kituo cha mpakani cha Rusumo.


  Aidha alisema kituo cha Rusumo katika kipindi hicho kimekusanya shilingi 7,058,300 kama mrahaba kwa mazao ya uvuvi yanayokwenda nje ya nchi.

  Akiwa katika ziara hiyo Waziri Mpina alipata fursa ya kuliona na kukagua gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato zenye thamani ya shillingi 20,850,000/= kwenye mpaka wa Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017 saa tatu asubuhi ambapo aliwaelekeza watendaji kuhakikisha taratibu zote za kisheria zinafuatwa ili kuweza kulitaifisha gari hilo kulingana na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2012 na 2015.

  Katika tukio hilo Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma na dereva wa gari hilo Ayoub Sanga walishikiliwa na polisi ambapo Ngoma alisimamishwa kazi mara moja kupisha uchunguzi.

  Aidha Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B CHRISTINA MNDEME amefanya ziara ya kushitukiza katika maghara ya SONAMCU ya kuhifadhia mbolea huku akikuta uchache wa mbolea katika maghara hayo habari kamili hii hapa video yake.

  0 0


  Malori ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yakiwa tayari yamepakia mbolea kutoka maghala ya Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd Dar es Salaam jana tayari kuisafirisha kwenda vijijini kwa wakulima ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati.
  Mbolea ikipakiwa kwenye magari.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo,  Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji,  Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
  Malori yakisubiri kupakia mbolea hiyo.


  Na Dotto Mwaibale 

  KAMPUNI ya Mbolea ya Premium Agro Chem Limited, imeeleza kwamba katika kipindi cha miezi mitano sasa imevuka malengo ya usambzaji wa mbolea kwenye vituo vyake tisa nchini kote, kwa kusambaza zaidi ya tani 19,500 mpaka mpaka Januari sita mwaka huu.


  Kampuni hiyo, ilisema ilipewa mgawo wa tani 3,500 na serikali wa kuuza mbolea hiyo kwa wakulima kwa bei elekezi, mbolea ambayo ilinunuliwa kwa utaratibu maalum uliowekwa na serikali. 

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Sargar Shah, alipozungumza na waandishi wa habari waliotembelea maghala yao kujionea utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli, alilolitoa juzi wakati akimwapisha Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko. 

  Sargar alisema wameamua kutoa taarifa kuhusu utendaji wa kazi zao, ambapo kuanzia mwezi Septemba walisambaza zaidi ya tani 1,040 ikiwa ni sawa na mifuko 22,603 yenye ujazo wa kilo 25,na Kilo 50 kwenye vituo vyao nchini kote. 

  Vituo vya kampuni hiyo vinavyotumiwa kwa ajili ya usambazaji wa mbolea kwa wakulima vipo Makambako, Njombe, Iringa, Kahama, Moshi, Songea, Mbinga na Dar es Salaam. 

  Aidha, Sargar alisema kwamba mwezi Oktoba, kampuni yake ilisambaza kwa mawakala zaidi ya tani 3,202 sawa na mifuko 76,030 yenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50 kila mmoja, ambazo ziliendelea kuuzwa kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali na kusimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA). 

  “Mwezi Novemba kampuni ya Premium Agro Chem Limited, ikionyesha uzalendo wa hali ya juu iliendelea kusambaza zaidi ya tani 4,250 sawa na mifuko 92,761 yenye ujazo wa kilo 25 pamoja na kilo 50,” alisema Sargar na kuongeza yote hiyo wanafanya kumuunga mkono Rais.

  Aliongeza kusema kuwa mwezi Desemba, wamesambaza zaidi ya tani 8,800 kwa mawakala wao nchini kote, ikiwa ni sawa na mifuko 186,138 yenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50, kulingana na mahitaji ya wateja na wakulima nchini. 

  Sargar, alisema mwezi Januari, walianza kusambaza mbolea kwa mawakala hao mikoani na hasa katika mikoa ambayo kuna mawakala wao, ambapo jumla ya tani 2,127 zilisambazwa kwa wadau wao nchini kote mpaka kufikia Januari 06, sawa na mifuko 42,692. 

  Mkurugenzi huyo alisema kwamba makubaliano na Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) ni kupakiwa na kusambaza zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wao hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali. 

  Meneja Biashara wa Premium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo,  Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji. 

  Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50. 

  Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi.  

  “Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi  ili kuwakomboa kiuchumi kupitia mazao watakayopata kwa kuyauza na ziada kwa matumizi ya chakula,” alisema Barot.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akionesha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa watendaji wa Wilaya ya Liwale (hawapo pichani), ambapo utekelezaji wa miradi yote ya barabara hapa nchini umeanishwa humo wakati alipowatembelea kuona hali ya mtandao wa barabara katika wilaya hiyo, mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Sara Chiwamba.
   Mkuu wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Bi. Sara Chiwamba akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu hali ya mtandao wa barabara wilayani humo katika ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo, mkoani humo kukagua miundombinu hiyo.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango kuhusu nia ya Serikali ya kuhakikisha inafungua wilaya hiyo na wilaya jirani ya Liwale kwa kuwajengea barabara kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akisisitiza jambo kwa uongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakati alipofanya kikao nao wilayani hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Joseph Mkirikiti.
   Muonekano wa sehemu ya barabara ya Ruangwa- Namichiga KM 22 ambapo Wakala wa Barabara mkoa wa Lindi wamepewa jukumu la kuhakikisha inapitika wakati wote.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Mzawa kutoka Kampuni ya Southern Link, Mhandisi Felix Aminieli, anayejenga Daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Joseph Mkirikiti.
   Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo katika mto wa Lukuledi, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
  Muonekano wa daraja la Nandanga ambalo lipo katika barabara ya Wilaya ya Luchelegwa-Ndanda inayounganisha wilaya za Ruangwa mkoa wa Lindi na Masasi mkoani Mtwara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.

  Wananchi wa wilaya ya Liwale na Nachingwea mkoani Lindi wameiomba Serikali kuhakikisha inaanza ujenzi wa barabara ya Liwale - Nachingwea (Km 129) kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mazao katika wilaya hizo. 

  Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, Mkuu wa wilaya ya Liwale Bi. Sarah Chiwamba amesema kuwa wanachi wake wanaamini kuwa Liwale itafunguka kibiashara na kiuchumi endapo itakuwa imeimarishwa katika mtandao wa barabara ambazo zitaiunganisha wilaya hiyo na wilaya jirani pamoja na nchi kwa ujumla.

  "Naamini barabara hizi zikikamilika wilaya hii na mkoa wetu utaendelea kiuchumi kwani suala la miundombinu ya barabara imekuwa ni kilio cha muda mrefu katika wilaya yetu", amesema Mkuu wa Wilaya.
  Aidha, Bi. Sarah amefafanua kuwa wananchi wengi katika wilaya hiyo ni wakulima, hivyo wamekuwa wakitumia miundombinu ya barabara kusafirisha mazao ya korosho na ufuta yanayozalishwa kwa wingi kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo anayeshughulikia masuala ya Ujenzi, amewataka wataalamu wote wa masuala ya ujenzi nchini kupitia Sera ya Ujenzi ya mwaka 2003 ambayo itawasaidia kuwapa mwongozo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma bora kwa jamii.

  Ameongeza kwa wataalam wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuwa wabunifu katika ujenzi wa barabara zao ili kuondoa dhana potofu iliyopo dhidi ya usimamizi wa barabara kati yao na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

  "TANROADS na TARURA shirikianeni katika kuhakikisha mnawajengea wananchi miundombinu iliyobora, kusiwepo na utofauti kati ya barabara mnazozisimamia", amesema Naibu Waziri huyo.

  Ametoa wito kwa uongozi wa TANROADS mkoani Lindi kuhakikisha kuwa wanaboresha maeneo yote ya barabara ambayo ni korofi ili yaweze kupita kiurahisi katika kipindi chote cha mwaka. Naye, Meneja wa TANROADS mkoani Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima, amemhakikisha Naibu Waziri Kwandikwa kuendelea na mpango wa matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.

  Naibu Waziri Kwandikwa yupo katika ziara ya kikazi mkoani Lindi kujionea hali halisi ya mtandao wa barabara katika mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua daraja la Nandanga lenye urefu wa mita 30 ambalo lipo kwenye mto Lukuledi katika barabara ya wilaya ya Luchelegwa- Ndanda inayounganisha wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi na Masasi mkoa wa Mtwara ili kujionea miundombinu yake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, ameziagiza halmashauri zote nchini kutowapa kazi za utekelezaji wa miradi ya maji wakandarasi wasiojali maslahi ya taifa na kusisitiza kuwa Serikali haitavumilia wakandarasi wazembe, ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza kwa muda uliopangwa.

  Aweso alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Shinyanga na wakazi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga na  kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa mradi wa maji kijijini hapo.

  ‘‘Nikuombe sana Mkurugenzi wa Halmashauri, hakikisha mnawapa kazi wakandarasi watakaohaikisha miradi inakamilika kulingana na mikataba yao, miradi mingi ya Serikali imekua haina manufaa kwa wananchi na kukosa tija kwa taifa kwa sababu tunawapa wakandarasi wazembe, wanaokosa uzalendo na kutokujali maslahi ya taifa.’’

  ‘‘Mfano mzuri ni mradi huu wa Mendo ulioanza kutekelezwa tangu Aprili 2014 na ulitakiwa kukamilika Disemba 2017, lakini bado haujakamilika wakati Serikali imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh. mil 300. Jambo ambalo si sahihi, hivyo naagiza ifikapo mwisho wa mwezi huu uwe umeshakamilika na wananchi wapatao 2199 waanze kupata maji,’’ aliagiza Naibu Waziri Aweso.

  Naibu Waziri Aweso ameanza ziara ya siku 5 mkoani Sinyanga inayolenga kukagua maendeleo ya miradi ya maji na kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa  mkoa huo wanapata huduma ya maji  ya uhakika kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitembelea Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga 
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga 

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mtambo wa maji Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga.


  0 0

  Serikali imewataka  watendaji   ngazi  ya   wilaya  na  mkoa  kusimamia kwa umakini zoezi  la  upigaji  chapa   mifungo  linaloendea hapa nchini.

  Agizo hilo amelitoa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah   Ulega wakati alipokuwa anazungumza na baadhi ya watendaji  wa mkoa wa Lindi kwenye ziara  yake ya kikazi  ya siku mbili  mkoani humo.

  Ulega  alisema mtendaji  yeyote  atakaye bainika kukwamishwa  zoezi hilo  hata vumiliwa  na kueleza kuwa kuna baadhi    wanaonekana kukwamisha zoezi hilo kwa madai ya kukosa  bajeti ya kuendesha zoezi.

  Wapo watendaji wanaodharau zowezi hili kwa kweli serikali haita waacha salama  alisema   Ulega.Kwa upande  wake  mkuu wa mkoa wa Lindi  Godfrey Zambi  amesema kuwa kunachangamoto kadha zilizosababisha  baadahi  ya  Halmshauri kushindwa kutekeleza  jukumu  hilo  kwa wakati.

  Zambi alisema   Halmshuari  ya wilaya Ruangwa ngo’mbe  268 kati  3000  wamepigwa chapa wakati wilaya   ya  Nachingwea  ngombe  328 tayari wamekamilisha zoezi  hilo.
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega na akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Lindi mara baada ya kupokea  ripoti ya ya mkoa huo.
   Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo katika mkoa wa Lindi.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Lindi.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizungumza na  viongozi mbalimbli,wafungaji  juu ya  kuhamasisha zowezi la ubikaji chapa mifugo mkoa wa Lindi.

  0 0

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nyingine sita utafanyika Februari 17 mwaka huu.

  Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage alisema jana kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalibali zikiwemo kifo na baadhi ya madiwani kujiuzulu.

  Alizitaja kata ambazo zitafanya uchaguzi huo mdogo kuwa ni Kata ya Buhangaza iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Kata ya Kanyelele iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kata ya Mitunduruni iliyoko katika Manispaa ya Singida.

  Kata zingine ambazo zitafanya uchaguzi ni kata ya Kashashi, Gararagua na Donyomuruak ambazo madiwani wake wamejiuzulu hivi karibuni.“Napenda kutumia nafasi hii kutoa tarifa kwa umma kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hizo februari 17, 2018,”alisema Jaji Kaijage.

  Uchaguzi huo unafanyika sambamba na uchaguzi mwingine mdogo wa wabunge ambao utafanyika katika majimbo mawili ya Songea Mjini ambako mbunge alifariki na Longido mbunge wake alivuliwa ubunge na mahakama.
  Aliongeza kuwa kutokana na uchaguzi huo mdogo, ratiba ya uchaguzi huo itaanza tarehe 18 hadi 24 Januari ambako tume itatoa fumu za uteuzi, uteuzi wa wagombea utafanyika januari 24 na kampeni zitaanza Januari 25 hadi Februari 16 na uchaguzi wenyewe utafanyika Febuari 17.

  Kaijage alitoa mwito kwa vyama vya siasa, wadau wa uchaguzi na wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo. “Tume inaviasa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya katiba, sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi na serikiali za mtiaa za mwaka 2015, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo yaliyotolewa na tume katika kipindi chote cha uchaguzi mdogo,”alisema Jaji Kaijange.

  0 0

  Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amekutana na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi ya Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya urithi wa Taifa la Tanzania ili kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania

   Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo ya kitaifa inategemewa kuandaa utaratibu maalam kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi kushiriki kikamilifu  kupitia midahalo na programu mbalimbali za kielimu; matamasha mbalimbali yakiwemo michezo ya jadi; vyakula vya asili na vazi la Kitaifa.

  Dk.Kingwangala amkutana na kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizundua rasmi kamati hiyo ya maandalizi ambapo pia wameamua kwa pamoja jina la maadhimisho hayo ambapo tayari wamekubaliana yatakuwa yanafanyika kila ifikapo Septemba ya kila mwaka.

  Ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa lengo la mwezi wa urithi huo wa taifa la Tanzania ni kutoa nafasi ya kuiweziwezesha jamii kuutumia urithi ambao taifa limejaliwa nao kama zao la utalii na hivyo kuchangia kiuchumi katika jamii na taifa kiujumla.

  “Pia maadhmisho hayo yatatumika kuelimisha jamii kuhusu kumbukumbu tulizonazo na namna ya kuzitumia kikamilifu katika kuendeleza Taifa na kuboresha maisha yao. Kuzikumbusha jamii chimbuko la tabia, mila na desturi za watanzania

  “Na kuzitambua na kuzienzi mila na desturi za makabila mbalimbali ya nchi hii pamoja na kuhakikisha kuwa matamasha yote ya utamaduni yanafanyika katika mwezi husika (mwezi wa urithi) ambao tumekubaliana iwe Septemba ya kila mwaka,”amesema Dk.Kigwangala.

  Amefafanua kuwa lengo la wizara yake ni kuhakikisha wanaunganisha wadau katika kuthamini, kuendeleza na kuhifadhi uritihi wa taifa.Hivyo amehimiza taasisi zote za umma na binafsi zinazojihusisha na masuala ya urithi kujiandaa kikamilifu na kuunga mkono dhamira hiyo ili kufanikisha lengo hilo kwa manufaa ya Taifa letu.

  “Nichukue fursa hii kuwaomba wajumbe wateule kushirikiana ili kutekeleza lengo hili ili kuendeleza juhudi za kukuza sekta ya utalii kwa manufaa ya Taifa letu. “Ingawa najua kuwa sote tuna majukumu mengine ya kitaifa, ushirikiano wa wanakamati wote pamoja na watendaji wa Wizara yangu ndio utarahisisha ufanisi wa kazi hii. Niwahakikishie mimi na watendaji wa Wizara yangu tutakuwa nanyi bega kwa bega ili kufanikisha kazi hii,”amesisitiza.

  Amefafanua urithi huu wa Taifa ni miongoni mwa vivutio vya utalii kwa kuwa ni vielelezo vya historia, utamaduni na ustaarabu wa jamii katika hatua mbalimbali za maisha. “Urithi huu huonesha na kuikumbusha jamii husika chimbuko la tabia, mila na desturi ambazo inazitumia katika nyanja za uchumi, siasa, teknolojia na elimu.

  “Jamii yoyote ile inatambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa kutokana na urithi wake. Kwa sababu hiyo, tuna kila sababu ya kuendeleza urithi huu tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu,amesema.

  Hivyo kwa kutambua umuhimu huo wa kuuenzi, kuutangaza na kuutumia uritihi wa Taifa la Tanzania kama kivutio cha utalii na kumbukumbu za Taifa, Wizara yake imeona ni vema kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania .
   Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo  akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania katikati ni Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG.
   Waziri wa Maliasili na Utalii  Dkt.Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye chuo cha Utalii cha Taifa Posta jijini Dar es salaam leo kushoto ni Dkt. Aloyce Nzuki Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasoli na Utalii.
   Mjumbe wa Kamati hiyo  na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Jokate Mwegelo.
   Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu Anthony Mtaka akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania wanaofuatia katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa mama Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Jokate Mwegelo na Imani Kajula
   Wajumbe wa kamati hiyo kutoka kulia ni Wema Sepetu na Dkt. Sebastian Ndege pamoja na wajumbe wengine

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kupitia Bia ya Serengeti Lite.

  Mkataba huo wa wenye thamani ya Shilingi Milioni 450 unaifanya Serengeti Lite kuwa bia ya kwanza kuidhamini Ligi ya Wanawake.Serengeti Breweries ambao pia wanaidhamini timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kupitia Bia yao ya Serengeti Premium Lager kupitia Mkurugenzi Mtendaji Hellen Weesie wanaamini udhamini huo utatoa msukumo kwa timu zote nane zilizofanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika msimu huu wa pili wa ligi hiyo.

  Weesie amesema siku zote Serengeti wanaamini katika kuendeleza vipaji hasa inapokuja katika michezo ambayo inawaleta pamoja wadau mbalimbali na wanaamini udhamini huo utawavutia mashabiki wa rika mbalimbali.
  Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura akizungumzia udhamini huo amesema Serengeti Breweries wanafungua milango kwa wadhamini wengine kupitia udhamini huo wa Bia yao ya Serengeti Lite.

  Amesema SBL wameangalia mbali zaidi kuingia kwenye soka la Wanawake kwakuwa hata mkutano mkubwa wa FIFA wa maendeleo ya mpira(FIFA Football Executive Summit) utakaofanyika Tanzania February 22 moja ya ajenda zake ni soka la Wanawake .

  “Udhamini huu utakuwa kichocheo kwa soka la Wanawake kukua na tunaamini soka la kina mama litajulikana kama inavyojulikana bia yao na udhamini huu fedha tunayoipata tutaitumia vizuri ” Alisema Wambura.
  Kwa upande wa Serikali kupitia Afisa Mkuu wa Michezo Henry Lihaya wamesema Makampuni mengine yaige mfano wa SBL kuingia kwenye michezo ambako ni chanzo cha ajira.

  Naye mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania(TWFA) Amina Karuma amesema udhamini huo wanaupokea kwa furaha kubwa kwakuwa utasaidia kutimiza lengo kwa mpira wa Wanawake kuchezwa kwa ufanisi.
  Ofisa mkuu wa michezo wa wizara ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama) akishuhudia tukio la kudhaminiwa rasmi kwa ligi ya Soka la Wanawake kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL (Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na 

  Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie wakipongezana mara baada ya tukio hilo kufanyika mbele ya Waandishi wa habari,jioni ya leo jijini Dar.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Mohamed Shein amefungua  Soko Jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ili kutatua changamoto za kukosekana kwa soko la kisasa katika Mkoa wa Kaskazini litakalowasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuendesha biashara zao.

  Mhe. Rais Shein amesema soko hilo litawagusa na kuwafikia  watu wenye kipato cha chini kuinuka kiuchumi kwa kuwanufaisha   Wajasiliamali wadogo wadogo vijijini pamoja na wafanyabiashara; Asasi ndogo ndogo za kifedha zinazotoa huduma vijijini; Vyama vya Msingi vya Ushirika/ Asasi za vijijini zinazojishughulisha na usindikaji wa mazao na masoko ya mazao kwa kushirikisha wanawake katika  makundi yote.

  Katika uzinduzi huo uliofanyika Januari 09, 2018 Mkoa wa Kaskazini katika eneo la Kinyasini, Mhe.Rais alisema kujengwa kwa   soko hilo kuna manufaa makubwa kwa wakulima wadogo wakiwemo wafugaji, wavuvi na wafanya kazi za mikono.

  “Soko hili litakuwa lenye tija kubwa kwa wananchi wa Zanzibar bila kujali maeneo wanakotoka. Soko hili ni letu sote, lisingeweza kujengwa kila mahali, au hewani lazima lingewekwa mahali, hivyo eneo hili la Kaskazini lilipata fursa hii, hivyo niwaombe liwe la wananchi wote wa Zanzibar.”Alisema Mhe.Rais

  Sambamba na hilo Mhe. Rais alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo ni moja ya matunda ya Muungano na kuwataka Wananchi kuuenzi na Kuulinda Muungano huo.

  “Miradi hii inayohusisha Bara ni moja ya mafanikio na matokeo makubwa ya Muungano wetu na hatuna budi kuuenzi”Alisisitiza Dkt.Shein

  Katika hatua nyingine,Mhe. Rais aliitaka Halmashauri husika kuendelea kuweka mikakati mizuri ya kulitunza na kuliendeleza ili liweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa Wazanzibar wote.

  “Niwaombe Halmashauri Kuona njia nzuri za kuendeleza kazi hii iliyofanywa na Programu hii na kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi kama ilivyokusudiwa”Alisisitiza Mhe.Rais

  Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwataka wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzingatia mafanikio ya mradi huu ikiwemo kusaidia kupambana na umasikini na kuleta tija.

  “Kuwepo kwa soko hili kutasaidia kupambana na umasikini na kuongeza mapato, hivyo washiriki watunze miundombinu hiyo pamoja na kuongeza thamani ili kuleta tija.”Alieleza Mhe.Mhagama .

  Naye Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohamed alimalizia kwa kuishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya MIVARF kuona umuhimu kuwajengea soko lenye ubora na litakalo tatua changamoto za kukosa soko la uhakika.

  “Soko hili la Kinyasini  moja kati ya masoko 16 yaliyojengwa na Programu hii katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo litasaidia kuondokana na umasikini na wananchi kujikwamua kiuchumi”   

  Programu hii ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) inatekelezwa katika Halmashauri 62 za Tanzania Bara na Wilaya 10 za Zanzibar, ikiwa  imegharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo,  na Uvuvi Zanzibar.Programu ilianza utekelezaji wake Mwaka 2012.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 09, 2018 eneo la Kaskazin ‘A’ Zanzibar.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu),  Mhe.Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
   Mhandisi wa Kampuni ya ZECCON Bw.Ali Mbarouk Juma akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Soko la kinyasini kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa Soko hilo lililojengwa eneo la Kaskazin ‘A’ Unguja, Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Soko la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelezo mafupi ya Soko la Kinyasini wakati wa uzinduzi wa Soko hilo Januari 09, 2018 Lililojengwa katika mkoa wa Kaskazin ‘A’ Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama mara baada ya kuwasilisha maelezo mafupi kuhusu soko la Kinyasini lililozindulia Januari 09, 2018.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Soko jipya la Kinyasini mara baada ya Uzinduzi Januari 09, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii Posta jijini Dar es salaam leo. 

   WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amezindua kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania.
   Kamati hiyo inahusisha Wakuu wa Mikoa ambao pia ni wajumbe wateule wa Kamati ya kitaifa ya kuratibu shughuli za maandalizi ya Mwezi Maalum wa Maadhimisho ya urithi wa Tanzania.
   Akizungumza Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo, Dk.Kigwangala amesema anawapongeza  wajumbe wote wa Kamati ya Maadhimisho wa Mwezi wa Urithi wa Tanzania kwa kuteuliwa kwao kwa ajili ya shughuli hii muhimu katika kuhimiza urithi wa Tanzania kwa maendeleo ya sekta ya utalii katika Taifa letu.
  Amesema sekta ya utalii imekuwa mhimili muhimu katika ukuaji wa uchumi  wa Tanzania ambapo kwa mwaka 2017 sekta ya  utalii imechangia dola za kimarekani Bilioni 2.1 takriban asilimia 25  ya  fedha za kigeni.
  Amesema takwimu zinaonesha mwaka 2016 idadi ya watalii waliotembelea nchi yetu walifikia 1,284,279. Katika taarifa yake ya 6 ya maendeleo ya uchumi, inayoitwa “Unlocking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians” Benki ya Dunia inaonesha kuwa mapato ya utalii yatakua kila mwaka na kufikia Dola za Marekani 16 bilioni ifikapo 2025. 
  “Hata hivyo, mpaka sasa sekta ya utalii Tanzania imekua ikijikita zaidi katika utalii wa wanyamapori ili kuvutia watalii ambapo takriban asilimia zaidi ya 80 ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Tanzania bara huja kuona wanyamapori.
  “Nchi yetu imejaliwa kwa kuwa na rasilimali mbalimbali za urithi wa Taifa nje ya zile za wanyamapori. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaliwa kuwa na rasilimali za kipekee duniani zinazobainisha harakati za maendeleo ya binadamu kama vile chimbuko lake, teknolojia alizotumia.
  ”Na namna ambavyo binadamu amekuwa akitumia mazingira yake ili kumwezesha kuishi kwa zaidi ya miaka milioni tatu iliyopita. Mfano wa rasilimali hizo ni masalia ya Binadamu wa Kale (Zamadamu) walioishi Bonde la Olduvai zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyopita na nyayo za Zamadamu aitwaye Australopithecus afarensis aliyeishi Laetol miaka milioni 3.6   iliyopita”amesema.
  Pia miji ya kihistoria kama vile Bagamoyo na Kilwa, michoro ya miambani, Kondoa na mapango ya Amboni.Aidha Tanzania ikiwa na zaidi ya makabila 120 imejaliwa kuwa na anuaia za mila, desturi, vyakula, misemo, imani, mavazi, nyimbo, ngoma za aina mbali mbali na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuunganisha Watazania. 
  Dk.Kigwangala amesema kutokana na kuona hayo yote wizara yake imeamua kuwepo na mwezi maalumu kwa ajili ya kusheherekea Urithi wa Taifa la Tanzania.
   Amesema Urithi huo wa Taifa ni miongoni mwa vivutio vya utalii kwa kuwa ni  vielelezo vya historia,  utamaduni na ustaarabu wa jamii katika hatua mbalimbali za maisha.
  Ameongeza urithi huo huonesha na kuikumbusha jamii husika chimbuko la tabia, mila na desturi ambazo inazitumia katika nyanja za uchumi, siasa, teknolojia na elimu.
  “Jamii yoyote ile inatambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa kutokana na urithi wake. Kwa sababu hiyo, tuna kila sababu ya kuendeleza urithi huu tuliojaliwa na mwenyezi Mungu.
  ” Kwa kutambua umuhimu huo,kuuenzi, kuutangaza na kuutumia urithi wa Taifa la Tanzania kama kivutio cha utalii na kumbukumbu za Taifa, Wizara yangu imeona ni vema kukwepo na mwezi maalum wa kusherehekea Urithi wa Taifa la Tanzania (Tanzania National Heritage Month).Tumekubaliana mwezi huo utakuwa ukiadhimishwa kila ifikapo Septemba ya kila mwaka,”amesema.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza katika mkutano na  Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania uliofanyika leo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii Posta jijini Dar es salaam leo. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akizungumza katika mkutano huo.
  Imani Kajula Mjumbe wa Kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania akizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye chuo cha Utalii cha Taifa Posta jijini Dar es salaam kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo na katikati ni Jokate Mwegelo mjumbe pia.
   Kutoka kulia ni Wajumbe wa kamati hiyo WEma Sepetu, Dkt. Sebastian Ndege, Dk. James Wakibara na Dk. Fredy Manongi na Devotha Mdachi
   Mjumbe wa kamati hiyo Ritha Paulsen akichangia mada katika mkutano huo uliofanyika kwenye chuo cha Utalii cha Taifa jijini Dar es salaam.
   Mjumbe wa Kamati hiyo Jokate Mwegelo akitoa mchango wake wa mawazo katika mkutano huo kulia ni Mjumbe Imani Kajula na kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. 
   Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. John Mtaka (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki (kulia)
   Picha ya pamoja
    Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla na wajumbe wa kamati hiyo.
  Baada ya kuhitimisha uzinduzi na picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 1481 | 1482 | (Page 1483) | 1484 | 1485 | .... | 1897 | newer