Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea kuhusu mikakati ya utendaji kazi kwa mwaka 2018 moja ya mkakati huo ukiwa ni kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Kulia ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo. 
 Wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alielezea kazi zilizofanyika katika Taasisi hiyo kwa mwaka 2017  katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kilichofanyika hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa  1025  walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kwa mwaka 2017 na hivyo Taasisi kuokoa  zaidi ya bilioni 29 ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi.
 Kikao cha kwanza cha Manejimenti  cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka  2018 kikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akisoma  taarifa za utendaji kazi wa idara yake kwa kipindi cha miezi mitatu katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kwa mwaka 2018 kilichofanyika hivi karibuni. Picha na JKCI


Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umewaahidi watanzania kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa  kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. 

Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea katika kikao cha kwanza cha Menejimenti  kwa mwaka 2018.

Prof. Janabi ambaye  pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho alizitaja ahadi zingine ni pamoja na kuendeea kupunguza kupeleka wagonja nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi katika Hospitali na kuendelea  kushirikiana na wananchi.

Mwenyekiti huyo alisema kwa mwaka 2018 wamejipanga  kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 64,093 walitibiwa katika Taasisi hiyo kati ya hao wagonjwa wa nje walikuwa 60796  na waliolazwa 3297.

RC MAKONDA AWAPIGA STOOP YONO KUWAONDOA WAFANYABIASHARA SOKO LA NDIZI MABIBO (MAHAKAMA YA NDIZI)

0
0

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni tayari wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiongozana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Khamis Rashid Kheri. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar.
 Sehemu ya waliohudhuria uzinduzi wa baraza la vijana Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihamasisha vijana wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiwa pamoja  na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Khamis Rashid Kheri.
 Sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana uliofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

JK, VIONGOZI MBALIMBALI WAMFARIJI MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

0
0
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya leo.
 Huzuni ilitawala pale mwili wa Marehemu ulipowali Nyumbani.
 Ibada ya kumuombea Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ikiendelea nyumbani.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Mzee Ally Mtopa.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwa ameambatana na viongozi Wengine wa Chama hicho waliofika nyumbani wa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kumfariji kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru.


 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam leo. 



















MKUU WA MKOA WA RUVUMA AIFAGILIA KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD KWA KAZI NZURI YA KUSAMBAZA MBOLEA

0
0

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme, ameipongeza kampuni ya Premium Agro Chem Limited, kutokana na kazi nzuri iliyofanya ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea za kupandia aina ya Urea kwa wakulima wa mkoa wake na wilaya zake kwa ujumla.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mazingira ya mkoa huo na mahitaji yaliwafanya viongozi kuwa katika changamoto kubwa, lakini kampuni hiyo imefanyakazi kubwa ya kuwafikishia wakulima hao mbolea.  

Alisema mahitaji ya mkoa wake kwa sasa ni zaidi ya tani 52,700, lakini wamepokea kiasi cha tani 15,200, na kutaka juhudi zaidi zifanyike kwani mbolea ya kupandia inahitajika kwa wakulima hao kabla ya Januari 15 mwaka huu.

"Ninawashukuru sana wadau wa mbolea na kilimo kwenye mkoa wetu, lakini kipekee naomba niwashukuru sana Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd, kutokana na kazi nnzuri ya kutusambazia kupitia mawakala wao na hata matawi yao hapa Songea na Mbinga, ninawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi nzuri, wameonyesha uzalendo mkubwa," alisema RC Mndeme.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri ndani ya mkoa wake, kufuatilia suala la upatikanaji wa mbolea kwa wakulima kwenye maeneo yao na kazi hiyo inatakiwa kufanyika masaa 24 bila kuchoka.

Kwa upande wake Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo ya Premium Agro Chem Ltd, Brijesh Barot, alisema kwamba wamesambaza zaidi ya tani 8,200 kwa mkoa wa Ruvuma na bado wanaendelea kusambaza kupitia kwa mawakala wengi zaidi.

"Tunaendelea kusambaza mbolea kwa mikoa yote, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe na Katavi, kupitia kwa mawakala pamoja na kuwatumia maafisa wetu walio katika vituo vya matawi yetu huko kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima vijijini," alisema Barot.

Alisema kampuni yao inafanyakazi kazi hizo kizalendo na ndio maana wamekubali kuuza kwa bei elekezi mbolea ambayo wao walikuwa wameinunua muda mrefu kabla ya kutolewa kwa maagizo ya kununua kwa mfumo maalum wa serikali, na hili linafanywa kwa kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

MPINA ATAKA KUHAKIKI USHURU WA MIAKA MITANO KATIKA MASOMO YA SAMAKI YA KIMATAIFA.

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Chato Shabani Ntarambe (aliyesimama) akimweleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) wakati wa mkutano wa hadhara kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ambapo Waziri ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.Kulia ni Diwani wa kata ya Kasenda Muganza Mwita.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia katikati) akiwa kwenye moja ya boti inayotumika kwa Uvuvi wa samaki kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Bathromeo Christiani, Kushoto ni Diwani wa kata ya Kasenda Muganza Mwita. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwahutubia wananchi kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) akikagua ofisi za soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi bi Mwanaidi Mlolwa. Nyumba niYohana Mikumbe Mtekinolojia wa samaki katika soko la Kasenda. . (Picha na John Mapepele)
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa Waziri Luhaga Mpina kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha na John Mapepele)

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Masoko hayo yatakayohusika na ukaguzi huo ni pamoja na Kirumba Mwanza, Nyakalilo Buchosa Mwanza ,Kasenda Chato Geita, Magalini Muleba Kagera, Kemondo Bukoba Kagera na Mwigobero Musoma Mara ambapo wafanyabiashara watakaobainika walihusika kufanya udanganyifu wa mapato watatakiwa kurejesha fedha hizo walizoiibia Serikali kwa kipindi hicho ambapo Watumishi wa Umma nao waliohusika kuhujumu mapato hayo watasakwa popote walipo na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kukabiliana na mashtaka ya kuhujumu wa rasimali za nchi .

Hatua hiyo ya Waziri Mpina imekuja kufuatia kubaini kuwepo udanganyifu mkubwa katika biashara ya samaki, dagaa,mabondo, na mapanki akibainisha kuwepo tabia ya kupunguza uzito na idadi ya magunia,kubadilisha matumizi ya vibali,kuchanganya mizigo ya ndani na nje ya nchi kwenye malori, kuanzishwa kwa masoko ya kimataifa yasiyo rasmi na wafanyabiashara wakubwa wa mazao ya uvuvi kutolipa kodi za mapato kutoka TRA.

Pia Waziri Mpina ameamuru kufutwa kwa masoko yote yasiyo rasmi yaliyopewa hadhi ya kimataifa ikiwemo soko la Nyakalilo na Magalini ambapo amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuwaondoa na kuwapangia vituo vingine vya kazi watumishi waliokuwepo kwenye masoko hayo.

Waziri Mpina ametolea mfano udanganyifu mkubwa uliofanywa na wafanyabiashara na watumishi wa umma wasio waaminifu likiwemo tukio la Disemba 16 mwaka jana ambapo mfanyabiashara mmoja (jina tunalo)huku akitumia gari lenye usajili ya nchi ya Rwanda lenye namba za usajili RB 9591 alipewa kibali cha kusafirisha magunia 258 kwenda Ngara mkoani Kagera na badala yake aliyapeleka nchini Rwanda na kuisababishia Serikali hasara ya sh. Milioni 3.

Pia kupunguza uzito na idadi ya magunia ili kulipia kidogo mapato ya Serikali akitolea mfano mfanyabiashara mwingine (jina tunalo) ambapo Disemba 2 , 2017 kutoka soko la Kasenda alisafirisha magunia 300 ya dagaa lakini yaliyolipiwa mrabaha wa Serikali ni magunia 200 tu huku Serikali ikipoteza mapato ya magunia 100 .
Waziri Mpina amesema matukio hayo ya udanganyifu aliyotolea mfano ni ya siku moja tu huku wafanyabiashara hao wakiwa na utamaduni wa kusafirisha zaidi ya safari nane kwa mwezi ambapo Serikali hupoteza mabilioni ya fedha za mapato kwa mwaka ambapo Samaki, dagaa, kayabo, mabondo, mapanki,furu wamekuwa wakiroroshwa kupitia mipakani na njia ya panya kwenda nchi za Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi, Uganda na Kenya.

Amesema wafanyabiashara waliopewa leseni za kusafirisha mazao ya uvuvi nje ya nchi wamekuwa mawakala wa raia wa kigeni ambapo kazi ya kununua, kukusanya na kusafirisha hufanywa na wageni jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 13 (14).

Kuhusu kasi ya Uvuvi haramu katika Wilaya ya Chato Waziri Mpina amesema taarifa zinaonesha kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2017 zana haramu zikiwemo Timba, Kokoro,Katuri,Mitumbwi, yenye thamani ya sh milioni 525,207,000 vilikamatwa, kutaifishwa na kuteketezwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi kuacha uvuvi haramu huku akieleza kusikitishwa na namna watanzania hao wazawa walivyopoteza mitaji yao lakini akatangaza msimamo mzito.

“Nimesononeshwa sana na taarifa ya kuteketezwa kwa mitaji ya wafanyabiashara hao wazawa kwa sababu ya kujihusisha na uvuvi haramu lakini nataka kuwakikishia kuwa vita dhidi ya uvuvi haramu haina suluhu na kwamba sitamuonea haya wala huruma mtu yoyote atakayejihusisha na uvuvi haramu tutawashughulikia wote bila huruma kwani Serikali ya awamu ya tano imejidhatiti kukabiliana na uvuvi haramu kwa nguvu zote na bila kuchoka”alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwanaidi Mlolwa alisema jukumu la kulinda rasilimali za nchi liko kikatiba hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kusaidia kulinda rasilimali hizo zisitoroshwe kwa manufaa ya nchi ya nyingine.

Amesema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) na kanuni zake za mwaka 2009 zinawapa mamlaka wasimamizi wa Sheria hiyo kumkamata mtu yeyote anayekutwa na samaki na mazao yake waliovuliwa kwa njia haramu na kutaifisha mali zote ikiwemo samaki, boti, mitumbwi na magari yaliyobeba samaki hao.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shabani Ntarambe amesema katika kukabiliana na uvuvi haramu wilaya kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2017 imefanikiwa kukamata ,kutaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zikiwemo Timba, Kokoro,Katuri,Mitumbwi, yenye thamani ya sh. milioni 525.2 na kumhakikishia Waziri Mpina kuwa mapambano bado yanaendelea kukomesha kabisa uvuvi haramu

LAND TENURE SUPPORT PROGRAMU YADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGO YA ARDHI MKOANI MOROGORO

0
0
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika amefanya ziara kwenye Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga ni wilaya tatu zilizochaguliwa kutekeleza zoezi la upimaji na urasimishaji wa ardhi kwa majaribio katika mkoa wa Morogoro lengo kuu likiwa ni kupanga matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro na ugomvi  baina ya wakulima na wafugaji.

Akihutubia wananchi hao, Katibu mkuu aliwataka wanavijiji hao kutumia fursa mbalimbali zilizo sanjari na mradi wa upimaji na urasimisha ardhi ili kujiletea maendeleao katika ngazi ya familia, Kijiji na taifa kwa ujumla.

Alisema migogogo ya ardhi ni imekuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa maendeleo maeneo husika kutokana na muda mwingi kutumika kukashughulika kutatua migogoro hiyo na kutumia muda mchache kwenye  shughuli za maendeleao.

Katibu Mkuu pia amewashuru wananchi kwa utayari wao wa kumaliza migogoro na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali ili kujiletea maendeleo yao na Taifa letu.  
AFISA Mipango wa Miji na Vijiji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nickson mjema akimpatia muhtasari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doroth Mwanyika kuhusu elimu na mikakati ya kuwahamasisha na kutoa elimu kwa wna Kijiji wa Nakafulu, wakati wa ziara ya Katibu huyo Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro Januari 10 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika akijaliana jambo na mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakati wa ziara yake kwenye Kijiji cha Nakafulu, Wilayani humo Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

MPIMAJI wa Ardhi wa Land Tenure Support Programu (LTSP), Gilbert Utama akimfafanulia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika jinsi tekiolojia ya mtandao wa simu inavyorahisha upimaji ardhi wakati wa upimaji ardhi kwenye Kijiji cha Ipunguo Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018. Kushoto (kwa katibu Mkuu) ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jacob Kassema, Katibu Tawala, viongozi wa wizarani na watendaji wa serikali za mtaa  wa Mkoa huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili Mlima Ndororo na Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.
MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Yusta Makoto akionesha Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Dastan Kaweza akionesha pia Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika (wa nne kulia) na mwenyeji wao, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili wilayani hapo Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akiongea na kuwapongeza wana Kijiji cha Nakafulu baada kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

SEHEMU ya wananchi wa vijiji vya Signali, Sululu na Sakamaganga wilaya ya Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Doroth Mwanyika.
SEHEMU ya wananchi wa vijiji vya Signali, Sululu na Sakamaganga wilaya ya Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Doroth Mwanyika.

MWANA Kijiji cha Ipungua ambaye ni mmoja wa walionufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Diana Mbangayao akionesha kitambulisho chake cha kupigia kura ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

MPIMAJI wa Ardhi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Gilbert Utama akimmwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika jinsi  mtandao wa simu inavyotumika kufanya kazi katika kupima ardhi wakati wa zoezi la upimaji ardhi kwenye Kijiji cha Ipunguo Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mmiliki wa ardhi hiyo, Diana Mbangayao.
SEHEMU ya msafara wa Katibu Mkuu huyo na watendaji wa serikali wakitembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Kijiji cha Idunda Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akiongea na kuwapongeza wana Kijiji cha Nakafulu baada kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.
WANAKIJIJI cha Nakafulu wakimsikiliza katibu Mkuu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika alipowasili kijijini hapo baada ya kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akipata maelezo ya alama maalum zinazotumiwa kwenye mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP) kutoka kwa watendaji wa serikali wa wizara hiyo alipotembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akipata maelezo ya eneo la makaburi kwenye kijiji cha Idunda kutoka kwa watendaji wa serikali wa wizara hiyo alipotembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATEUA MABALOZI WAWILI

0
0


WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD KWA KUSAMBAZA MBOLEA KIASI KIKUBWA NCHINI

0
0
Na Dotto Mwaibale

WAZIRI Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, ameipongeza Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayojihusisha na mbolea, kutokana na kazi nzuri na kutia ya kusambza kiasi kikubwa cha mbolea kwa wakulima nchini na hivyo kusaidia kupunguza adha iliyokuwa ikiwasumbua baadhi ya wadau wa sekta hiyo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo ya pongezi jana alipokuwa akikagua zoezi la upakiaji wa mbolea na usafirishaji ili kufikia malengo ya kutekeleza agizo la hivi karibuni lililotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli, alimuagiza Waziri Mkuu kusimamia zoezi hilo kwa ajili ya kumaliza malalamiko ya wakulima wa mazao ya chakula na biashara kwa mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.

Mikoa maarufu kwa uzalishaji huo inafahamika kama The Big  ni Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma.

Akizungumza na watendaji wa kampuni hiyo, Waziri Mkuu aliipongeza kutokana na uamuzi wao wa kukubali kufanya kazi hiyo usiku na mchana na kusaidia kupunguza malalamiko ya wakulima.

"Kwa kweli ninawapongeza kwa kazi nzuri, mmetusaidia kwa kiwango cha juu, tunawashuru kwa kazi mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya kwa nia njema, huu ni uzalendo mkubwa na unaostahili kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Alisema wakulima wa mazao ya chakula wanahitaji huduma ya kufikishiwa mbolea kwa wakati, lakini kwa taarifa nilizozipata, kazi kubwa imefanywa na kampuni yenu ndani ya siku mbili hizi, yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kama sio kumaliza kabisa malalamiko ya wadau wenu.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, alitumia muda huo kumweleza Waziri Mkuu, kwamba kampuni hiyo imefanyakazi kubwa usiku na mchana kupakia mbolea kwa ajili ya mikoa iliyokuwa na changamoto nyingi.

Alisema mpaka jana usiku, magari makubwa ya kubeba migizo mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yalipakiwa kwa ajili ya kusambaza mbolea zaidi ya tani 600 kwa mikoa ya Rukwa na Katavi.

Lakini pia Mheshimiwa Waziri Mkuu, mawakala wa kampuni hii ya Premium wameendelea kuja hapa na kuchukua mbolea kwa ajili ya kukabilia na hali ya mahitaji makubwa yanayowakabili wakulima vijijini," alisema Waziri Tizeba na kuongeza kwamba kampuni hiyo imeendelea kushirikiana bila masharti na Kampuni ya Taifa ya Mbolea kusambaza mbolea hizo katika maeneo ambayo wao hawana mawakala ama hawana matawi ya kuuzia.

ELIMU BURE YAWABANA WAZAZI WALIOKUWA WAKIOZESHA WATOTO KATIKA UMRI MDOGO WILAYANI BAHI

0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

Serikali Wilaya ya Bahi  imeahidi kuendelea kushirikiana na Tasisi ya Msichana Initiative katika Mapambano yake ya kupinga ndoa za utotoni na  ukatili wa kijinsia kwa watoto wa Wilaya hiyo,ili kufikia malengo kama ilivyo katika sehemu zingine hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa  Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma , Daudi Kisagure alipotembelea mradi Msichana Cafe unaoendeshwa na taasisi ya Msichana Initiative katika kata kumi za wilaya hiyo.

"lazima niwaeleze ukweli tangu mradi huu wa Msichana Cafe uanzishwe na Msichana Initiative umesaidia kwa kiasi kikubwa sana, kwani tangu mwaka jana mara baada ya watu kupata elimu na kuelewa kesi za watoto kuolewa katika umri mdogo zimepungua sana,tathmini ya awali kutoka kwa walimu wakuu wanasema elimu iliyotolewa imepunguza kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni "amesema Kisagure.

Ametaja kuwa hivyo uwepo wa tasisi hiyo kumesaidia sana kutoa uelewa kwa wazazi juu ya elimu kwa mtoto na kuwaelimisha juu ya haki za mtoto kuliko ilivyokuwa hapo awali, ambapo watoto wengi walikuwa wakiripotiwa kuolewa na kushindwa kuendelea na masomo.

Ametaja kuwa taasisi hii imefanikiwa zaidi kutokana na mpango wa elimu bure ulioanzishwa na Rais Dk John Magufuli na umeondoa visingizio ambavyo hapo awali vilikuwa kikwazo kwa watoto wa kike kwenda shule na badala yake kuozeshwa ili wazazi wapate mali.

kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Msichana Cafe, Paulina Mbabala amesema kuwa mradi huo wa kupinga mimba za utotoni umewasaidia sana mara baada ya kufanyiwa semina na kuchaguliwa kama wawakilishi wa kutoa elimu hivyo wameweza kuifikia jamii kubwa na kwasasa wameanza kupata kuelewa umuhimu wa mtoto wa kike kuendelea na masomo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Daudi Kisangire akizungumza jambo na wajumbe wa Msichana Cafe alipowatembelea katika eneo lao la kukutana kwa ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili katika mapambano ya ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni katika kata ya Kigwe.
Katibu wa mradi wa Msichana Cafe katika kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma,Miraji Adam akisoma taharifa kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo namna walivyofanikiwa kuwafikia wanafunzi na taasisi mbalimbali kutoa elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni.
Baadhi ya Wajumbe wa Mradi wa Msichana Cafe kutoka kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi wakisikiliza kwa makini Nasaha kutoka kwa afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo.

TUNATAKA ARUSHA YENYE MAAMUZI-HERRY JAMES

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James akisalimiana na baadhi ya viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha mara baada ya kuwasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha Na Mathias Canal

Na Mathias Canal, Arusha


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James amesifu ushirikiano wa wananchi Mkoani Arusha kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kusimamia rasilimali za Taifa.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ameeleza hayo Mara baada ya kuwasilia Mkoani Arusha leo 10 Januari 2018 katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Longido katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.


Akizungumza na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi waliozuru kumlaki katika Mtaa wa Tengeru, Wilaya ya Meru, Herry aliwasisitiza Vijana hao kuendeleza mahusiano mazuri kwa Chama na serikali ili kuwa na jamii yenye nidhamu, weledi na mtazamo chanya katika utendaji.


Alisema pia mahusiano mazuri ndio msingi wa ushindi wa ngazi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mdogo wa udiwani uliomalizika hivi karibuni na CCM kuibuka kidedea kwa zaidi ya asilimia 97%.


Aidha, Herry amewafikishia vijana hao salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kuwa amemuelekeza kushiriki kampeni za Uchaguzi mdogo ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli anatarajia matokeo ya ushindi wa kishindo katika chaguzi zote za marudio nchini.


Aliongeza kuwa katika kipindi kirefu Mkoa wa Arusha umekuwa na viongozi wasiokuwa na maamuzi lakini kupitia serikali ya awamu ya Tano viongozi wengi wamekuwa na maamuzi muhimu na mazuri kwa wakati sahihi huku akisifu uwajibikaji wa Kamishna wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo.


Sambamba na hayo pia amewasihi Vijana wote nchini kusimamia kile wanachokiamini kwa maslahi ya wengi na kuwa na maamuzi yakinifu kwa wakati sahihi.

WAFANYABIASHARA WA WANYAMAPORI HAI NJE YA NCHI WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akifungua kikao cha Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina
Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Enock Balilemwa akizungumza kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao cha Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Fatuma Hamisi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani) kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
Baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma kati ya Wizara na wadau hao lengo likiwa ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
Mjumbe wa Halmashauri wa TWEA, Paul Madinda ambaye pia ni mmiliki wa shamba la viumbe hai jijini Arusha, akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani) jinsi alivyoathirika tangu zuio hilo la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi lilipotelewa kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma. (
Picha na Lusungu Helela-MNRT


Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA) kimeiomba serikali isitishe zuio la kusafirisha nje wanyamapori hao ili wanachama wake waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha inayaowakabili.

Wakizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kwenye kikao cha Wizara na wawakilishi wa Wafanyabiashara hao waliiomba serikali isikilize kilio chao.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Chama hicho, Enock Balilemwa alisema baadhi ya wanachama wakiwemo walemavu waliokuwa wamechukua mikopo benki wamefukuzwa kwenye nyumba zao baada ya kushindwa kufanya marejesho ya mikopo hiyo kufuatia zuio la biashara hiyo.

Alieleza kuwa baadhi ya wanachama wake wamejikuta kwenye hali ngumu ya kupoteza mali zao na kuingia kwenye mifarakano na wateja wao kwa vile wafanyabiashara hao walichukua pesa toka kwa wateja kama malipo ya awali hivyo wakati wa zoezi la kusimamisha biashara linafanyika liliwakuta wafanyabiashara hao wameshachukua pesa za wateja wao kama malipo ya awali.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa TWEA, Fatuma Hamis alimweleza Naibu Waziri kuwa zuio hilo lilifanywa ghafla mno bila kutoa muda kwa wafanyabiashara hao ukizingatia kuwa walikuwa wakimiliki leseni halali walizokuwa wamezilipia pesa bila kuzifanyia kazi ya kuwaingizia kipato.

Aidha, alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa zuio hilo limepelekea wafanyabiashara hao kupoteza uaminifu kwa wateja wao na kuwaweka kwenye mazingira magumu ya ushindani kibishara kwani biashara hiyo haifanywi na Tanzania pekee.

Wakati akijibu hoja za Wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA) ,kuyafanyia kazi malalamiko yao kadri itakavyowezekana na kuja na kauli moja ya serikali.

Amesema lengo la serikali la kuzuia usafirishaji wanyamapori hao lilikuja baada ya wafanyabishara ambao sio waaminifu kukengeuka kwa kuanza kujihusisha na ujangili pamoja na kusafirisha wanyamapori ambao hawamo kwenye orodha ya vibali walivyopewa.

‘’Dhumuni la serikali la kusitisha biashara hii ilikuwa ni njema tu baada ya kuona wajanja wachache wananufaika huku wanyonge wakibaki watazamaji kwenye rasilimali zao’’ alisema Hasunga

Hata hivyo, Naibu Waziri Hasunga alisema lengo la serikali halikulenga kuwakomoa bali ni kutaka kuweka mfumo mzuri utakaomsaidia kila Mtanzania aone ananufaika na rasilimali za nchi yake.

‘’Nimewasikiliza kwa umakini wa hali ya juu lakini hata hivyo Serikali ina utaratibu wake wa kutoa majibu, tupeni muda ili tukitoa majibu kuhusu hoja zenu kuwe na jibu moja kwa kila mmoja wetu’’ alisema

Katika hatua nyingine, Hasunga aliwataka wafanyabishara hao wasisite kuonana nae muda wowote ule kwa kumpigia simu au kwa kuonana nae pindi wanapokuwa na jambo la kutaka kuzungumza nae kwa ajili ya manufaa mapana ya Wizara na nchi kwa ujumla.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina aliwahakikishia wafanyabiashara kufanyia kazi malalamiko yao kutokana na hoja za msingi zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao.

‘’Nimesikia baadhi ya malalamiko yenu ambayo kwa nafasi yangu niliyo nayo kwa kushirikiana na watumishi walio chini yangu nitayashughulikia’’ alisema.

SUMATRA PWANI YAKEMEA KUPANDISHWA NAULI KIHOLELA KWA MABUS YAENDAYO MIKOANI-AYOUB

0
0
OFISA mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)Mkoani Pwani,Omary Ayoub ,akizungumza jambo kuhusu masuala ya usafirishaji ,katika ukaguzi wa magari stand ya Mailmoja ,Kibaha ,ukaguzi unaofanywa kati ya ushirikiano wa Sumatra na kamati ya usalama barabarani Mkoani hapo.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoani Pwani Josephine Protas,akizungumza jambo kuhusu masuala ya usalama barabarani,katika ukaguzi wa magari kwenye stand ya Mailmoja ,Kibaha ,ukaguzi unaofanywa kati ya ushirikiano wa Sumatra na kamati ya usalama barabarani Mkoani hapo.

kaguzi wa kipimo cha ulevi kwa madereva mbalimbali wa magari madogo na mabasi ya abiria yaendayo mikoani ,unaofanyika kwenye ukaguzi unaoendelea kwenye stand ya Mailmoja Kibaha na maeneo mengine ya Mkoa wa Pwani.Picha na Mwamvua Mwinyi



Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

OFISA mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)Mkoani Pwani,Omary Ayoub amekemea tabia ya kupandishwa kwa nauli inayofanywa na baaadhi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani .

Aidha mamlaka hiyo ,imetoa wito kwa abiria kufunga mkanda pasipo kudharau kwa ajili ya usalama wao.Ayoub aliyasema hayo ,wakati wa ukaguzi wa magari ya abiria yaendayo mikoani katika stand kuu ya Mailmoja,Kibaha ,ukaguzi ambao unafanyika kwa ushirikiano kati ya Sumatra na kamati ya usalama barabarani mkoani humo .

Alisema changamoto kubwa waliyonayo katika mkoa huo ni baadhi ya abiria waendao mikoani kuzidishiwa nauli tofauti na nauli halali.Ayoub ,alielezea wamepokea taarifa kutoka kwa abiria hao kuwa kuna wahusika wa mabasi ambayo yamekuwa yakipandisha nauli huku kwenye tiketi zao wakiwa wanaandikiwa nauli halali jambo ambalo linawakandamiza abiria.

Alisema hawatamvumilia dereva ,kondakta wala mmiliki yoyote anayehusika kukiuka taratibu za usafirishaji .Ayoub alieleza,wanapobaini kuwa madereva au wamiliki wamekiuka taratibu zilizopo kisheria huwachukulia hatua mbalimbali ikiwemo kuwatoza faini ama kuwashtaki mahakamani.

Aliwaomba wananchi na abiria kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa taratibu za usafirishaji kwa wale wanaopandisha nauli na kuandika nauli zisizo sahihi kwenye tiketi zao.“Tunaomba ushirikiano juu ya suala hili ,tunafuatilia na kusimamia ili kuwasaidia wananchi ambao hawajui haki zako na wapi waende kufikisha kero hizo”

“Msiogope kusema na kuwataja hawa wanaopandisha nauli ,;:Msilipe nauli zaidi ya iliyoandikwa kwenye tiketi ” alisema Ayoub.Akizungumzia umuhimu wa kufunga mkanda wakati wa safari ,Ayoub alisema abiria wanaona hakuna umuhimu wa kufunga mikanda lakini waelewe ni muhimu kwao.

Alisema kufunga mikanda ipo kisheria ya mwaka 2007 ya Sumatra inayotakiwa abiria wafunge mikanda kwa usalama wao.“Inastaajabisha unakuta abiria wanafunga mkanda wakiona askari wa usalama barabarani ama Sumatra wakikagua magari hayo ” alisema Ayoub.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Pwani ,Josephine Protas aliwataka madereva na wamiliki kufuata sheria na taratibu .Aliwaasa pia madereva kuacha kuendesha kwa mwendo kasi na kutumia vileo wakati wakiendesha.

Josephine alisema ,kuendesha pasipo kuwa makini na tahadhari ukiwa barabarani kunasabababisha ajali zembe na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia.

Aliyataka magari madogo ya abiria yanayofanya safari zake Mbezi-Mlandizi-Chalinze kutoa tiketi kwa abiria ili kuondoa usumbufu kwa abiria

Serengeti Lite mdhamini rasmi Ligi ya soka la Wanawake

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.




Ofisa mkuu wa michezo wa wizara ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama) akishuhudia tukio la kusaini Mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya Wanawake kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL (Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu .
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.


Bia pendwa ya Serengeti Premium Lite, ambayo inazalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), leo imetangaza kuwa mdhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake (Women Premier League). Katika Mkataba uliosainiwa kati ya SBL na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kama mdhamini rasmi wa ligi hiyo, Serengeti Premium Lite itatoa msukumo kwa timu zote nane za wanawake kwenye ligi ambapo mshindi atakuwa mwakilishi wa taifa katika mashindano ya kikanda na ya kimataifa. Kupitia udhamini huo, SBL ina matumaini makubwa kwamba itaweza kuwazindua wananchi na hasa mashabiki wa soka na kuwaunganisha pamoja ili kuongeza hamasa katika ligi ya taifa ya wanawake kupitia bia hiyo kipenzi cha watanzania ya Serengeti Premium Lite.

“Tunayo furaha kubwa kuwa wadhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake kupitia bia yetu maarufu ya Serengeti Lite. Siku zote tumekuwa tukiamini katika kuendeleza vipaji katika sehemu mbali mbali za nchi na haswa inapokuja katika michezo inayotuleta pamoja. Tunaamini udhamini wetu utawavutia mashabiki wa rika mbali mbali kuiunga mkono ligi ya wanawake na kufikia mafanikio makubwa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, SBL inaamini katika nguvu ya mpiga wa miguu ambayo inawaunganisha watu.

Udhamini wa Twiga Stars unafuatia historia ndefu ya udhamini wa timu ya soko ya wanaume, Taifa Stars ambayo mpaka hivi sasa inaendelea kupata udhamini wa SBL kupitia bia yake mama ya Serengeti Premium Lager. SBL ni sehemu ya kampuni ya Diageo ambayo inauhusiano mkubwa na masuala ya soka duniani ikiwa ni pamoja na udhamini wa Ligi Kuu ya Uingereza kupitia bia ya Guinness

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura alisema; “Leo kwa mara nyingine tunashuhudia ushikiano muhimu kati yetu na SBL, kampuni maarufu ya bia na ambayo imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia maendeleo ya michezo nchini. Ushirikiano huu utasaidia sana katika kuendeleza soka letu la wanawake pamoja na mashindano tutakayokuwa tunaandaa. Tunafurahia udhamini huu kupitia bia ya Serengeti Lite na tunaamini utakuwa wa mafanikio makubwa,”

Utiaji saini kati ya pande hizo mbili ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Bw, Yusuph Singo ambaye aliipongeza SBL kwa kujitolea kwake katika kuunga mkono sekta ya michezo nchini na pia kuwataka Watanzania wenye mapenzi mema pamoja na makampuni mengine kuiga mfano mzuri wa kampuni ya SBL.

ETIHAD AVIATION GROUP APPOINTS NEW GROUP CHIEF FINANCIAL OFFICER

0
0

Mark Powers, Etihad Aviation Group's Chief Financial Officer.
Abu Dhabi, UAE – Etihad Aviation Group (EAG) today confirmed the appointment of Mark Powers as its new Group Chief Financial Officer. Mr Powers will join EAG in January 2018.

In his new role, Mr Powers will be responsible for the finance function across the Abu Dhabi-based group’s five divisions, which comprise UAE national airline Etihad Airways, Etihad Airways Engineering, Etihad Airport Services, Hala Group and Airline Equity Partners. 

Mr Powers joins Etihad Aviation Group from Tulane University’s A.B. Freeman School of Business, where he was Professor of Finance. He brings with him significant industry experience, having held senior leadership roles at major airlines including JetBlue, where he most recently held the position of Chief Financial Officer.

He also worked for Northwest Airlines, where he held the position of Vice President Treasury, Corporate Finance; for Continental Airlines, where he was Treasurer and Associate General Counsel; and for GE Aviation, where he was Director Customer Finance and Commercial Engine Programs.

Tony Douglas, Group Chief Executive Officer of Etihad Aviation Group, who officially assumed his role on 3 January, said: “We are delighted that Mark will be joining the executive leadership team at Etihad Aviation Group. His corporate finance knowledge of aviation is unrivalled and he is extremely familiar with the challenges and opportunities that face our industry.

“The Etihad Aviation Group Board believes Mark and the wider finance team will play a pivotal role in helping to guide Etihad onto the next stage of its development.”

Mr Powers commented: “I am looking forward to joining Etihad Aviation Group and taking on this unique opportunity to lead the financial development of the group’s divisions at this exciting moment in its history.”

Mr Powers will report directly to Mr Douglas. Ricky Thirion, who has been Interim Group Chief Financial Officer, will resume his position as Group Treasurer.

Mr Douglas added: “I would like to thank Ricky for his dedication and focus during his interim tenure in one of the group’s most important corporate functions.”

TANESCO YATOA SIKU NNE (4) KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME WAWE WAMELIPA, VINGINEVYO HUDUMA ZINASITISHWA

0
0
 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.
mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
JANUARI 11, 2018

SALAMU ZA RAMBI RAMBI

0
0

KAZI ZA MIKONO ZAWASAIDIA WAKIMBIZI WANAWAKE KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KAMBINI

0
0

Baadhi ya wanakikundi Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakifinyanga vyungu mara baada ya kupata mafunzo kutoka shirika la IRC Ambalo linafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Wanawake hao licha ya kufanikiwa kufinyanga vyungu hivyo, huviuza kwa shilingi 200 kwa kila kimoja, hali ambayo imekuwa haileti tija na faida katika kazi yao.
Mmoja wa wanakikundi wa ufinyanzi katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma,ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), ambayo yanamuwezesha kutumia muda wake katika shughuli za mikono za uzalishaji. 
 
Ili kuhakikisha uendelevu wa vikundi mbalimbali vya wajasirimali ndani ya Kambi za wakimbizi, kipato hafifu wanachopata baada ya kuuza bidhaa huingizwa katika mfuko wa kuweka na kukopa (VICOBA) wa kikundi ambao umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanakikundi kujiwekea akiba pamoja na kugawana faida inayopatikana kila mwisho wa mwezi. Kutokana na wateja kuwa ni watumishi/wadau mbalimbali wanaotembelea kambi hizi faida yao huwa ni finyu.
Mmoja wa Wakimbizi katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma Ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR). Wanawake hawa wenye uwezo wa kufinyanga vyungu hutumia baadhi ya siku kuwafundisha wanawake wenzao waishio ndani ya kambi hii ya wakimbizi na kwa njia hii elimu inawafikia wanawake wengi. Shughuli za uzalishaji mali/ujasiriamali husaidia kuwajengea wanawake uwezo wa kujikimu kimaisha. Elimu hii itawasaidia hata watakaporejea nchini mwao.

Wanawake wa Kambi ya wakimbizi Mtendeli wakionesha baadhi ya nguo za Watoto ambazo wamezifuma kutokana na uzi kwa kutumia mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka IRC. “Kabla hatujapata haya mafunzo kutokana na mazingira tnayoishi kwa sasa shughuli pekee tuliyoweza kufanya ni kupika na kufanya usafi wa maeneo ya nyumba/mahema lakini sasa tunatumia muda katika kujifunza vitu vya maendeleo.”

Wanawake kutoka Kambi ya Wakimbizi Mtendeli wakifuma Vitambaa kwa uzi kutumia sindano ya mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka Taasisi ya IRC.

Beatrice Emmanuel - Muwezeshaji wa Wanawake kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR, akimvisha mtoto Kofia iliyofumwa na mwanakikundi ndani ya kambi ya Mtendeli.

TATU MZUKA YAKABIDHI MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA KITUO CHA POLISI MBANDE

0
0
Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka  kupitia mshindi wa wiki iliyo pita kutoka Temeke Erinisha Kilango aliyeshinda milioni 50,wamezawadia Wilaya ya Temeke mabati ya thamani ya milioni 5 kusaidia kujenga kituo cha polisi cha Mbande.

 Tatu Mzuka inasemaga kuwa "ukishinda na Tanzania inashinda. Kwenye wilaya ambayo mshindi anatoka, Tatu Mzuka wanazawadia wilaya milioni 5  kusaidia maendeleo ya wilaya hiyo. 

Ukicheza Tatu Mzuka , unaweza kushinda hadi milioni 6 kila lisaa, milioni 10 kila siks na jumapili hii kuna jackpot ya milioni 70 ya kuzawadia. 
  Afisa wa mawasiliano Bi. kemi Mutahaba akikabithi mabati ya thamani ya millioni 5 kwa Katibu Tawala wa Temeke Mh.  Hamisi Komba kusaidia kujenga kituo cha Polisi Mbande, wilaya ya Temeke.
 Mafundi wa ujenzi  wakiwa wana kabidhiwa mabati yenye thamani ya milioni 5 na Afisa ya Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Kemi Mutahaba.
Mhe Hamisi Komba, Katibu tawala wa wilaya ya Temeke akikabidhiwa fedha tasilimu milioni 5 na Bi . Kemi Mutahaba  wa Tatu Mzuka kwa ajili ya kununua  mabati yatakayo tumika kujenga kituo cha Polisi Mbande, Temeke.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUPELEKA KIVUKO LINDI

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandika, kuhusu hali ya miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, pamoja na viwanja vya ndege katika mkoa huo. Naibu Waziri huyo yupo katika ziara ya kikazi ya siku 3 mkoani humo.
 aibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Lindi katika kikao kazi, kuhusu umuhimu wa wataalamu wote kushirikiana katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima akisikiliza.
 Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Lindi, Mhandisi Grayson Maleko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, alipokuwa akikagua ujenzi wake mkoani humo.
 Muonekano wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, ambapo mkataba wa kukikokota Kivuko hiko kutoka Pangani mkoani Tanga kuja Lindi upo katika hatua za mwisho.
 Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Lindi,, Hamida Abdallah akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa kufika mkoani hapo kwa ajili ya kutazama hali ya miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko na viwanja vya ndege.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Mhe. Hamida Abdallah, wakikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Lindi inayojegwa na SUMA JKT chini ya uangalizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika ziara ya kikazi mkoani humo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko kipya  kutoka eneo kinapotengenezwa wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.

Akizungumza mara baada ya kukagua maegesho ya kivuko hicho ambacho kinatarajiwa kutoa huduma za usafiri kutoka Lindi Mjini - Kitunda mkoani humo, Naibu Waziri huyo amewahakikishia wananchi kutegemea kupata huduma nzuri za usafiri kwani ujenzi wa kivuko na  maegesho  yake  kwa sasa umefika katika hatua nzuri.

"Naagiza Mamlaka husika kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko hiki kutoka Tanga hadi hapa ili wananchi waone kwamba kivuko kimefika na kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo ameridhishwa na ujenzi wa maegesho hayo ambayo kwa sasa ujenzi wake umebakia asilimia 10 na hivyo kutarajiwa kukamilika muda wowote.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa, ametembelea na kukagua uwanja wa ndege wa Lindi ambapo amesema Serikali inaendelea na mpango wake wa kuboresha viwanja vya ndege nchini ili kuimarisha huduma katika usafiri wa anga.

Amefafanua kuwa Serikali kupitia mwaka wa fedha 2018/19 licha ya kuwa na mpango wa kuboresha uwanja huo pia itaboresha Uwanja wa ndege wa Kilwa Masoko lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa TEMESA mkoani Lindi, Mhandisi Greyson Maleko, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kujipanga katika kuhakikisha wananchi wa Lindi wanapata huduma bora za kivuko.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo Mheshimiwa Hamida Abdallah, ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusogeza maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Naibu Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi ya siku Tatu mkoani humo ambapo ametembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake ili kujionea maendeleo na changamoto zake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images