Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini


MBUNGE MGIMWA:WATENDAJI KAMATENI WAZAZI WOTE AMBAO HAWAWAPELEKI WATOTO WAO SHULE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo 
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini


Na Fredy Mgunda,Mufindi. 


Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari. 

Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ilogombe Pastor Haonga alisema kuwa wazazi wengi wa kata ya Kibengu wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Haonga

Haonga alimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kata ya Kibengu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Haonga.

Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu

Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi
Nao watendaji wa vijiji vitano vya kata ya Kibengu ambao ni Dominicus Nyaulingo,Saifod Mwengwa,Haruna Kalenga, Richard Mandili na Demetus Kanyika walisema kuwa wamepokea agizo la mbunge na watalifanyia kazi kwa ukamilifu kwa kufuata sheria ili kuhakikisha watoto wa kata hiyo wanapata elimu kama inavyotakiwa.

Na kata ya Kibengu inajumuisha vijiji vitano ambavyo ni kijiji cha Kibengu,kijiji cha Igereke,kijiji cha Ilogombe,kijiji cha Usokami na kijiji cha Kipanga

MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia aliyesimama) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Mtinika (aliyesimama) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto waliokaa) ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiagana na Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia) mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati.


Shirika la Umeme Tanzania limeagizwa kumchukulia hatua Mkandarasi ambaye ni kampuni ya wazawa ya JV State Grid Electrical & Technical Works Ltd aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kushindwa kukamilisha katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa makubaliano.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo Januari 5, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Umeme Vijijini.

Mgalu alitoa agizo hilo kufuatia taarifa ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati ambaye alimueleza kuhusu kampuni hiyo iliyokuwa ikitekeleza Miradi katika Wilaya za Mbarali, Rungwe, Kyela na Ileje kushindwa kukamilisha miradi yake kama ilivyopaswa kulingana na mkataba. 

Alisema Serikali haitowafumbia macho Wakandarasi walioshindwa kukamilisha utekelezaji wa Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano na aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha Mkandarasi huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa makubaliano ya awali.

“Serikali haijaribiwi, tutachukua hatua kwa Wakandarasi wote walioshindwa kutekeleza Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa Sheria; TANESCO na REA, hakikisheni Mkandarasi huyu anapatikana na hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi yake,” alisema Mgalu.

Mgalu aliagiza Mkandarasi huyo apatikane ndani ya Siku Saba ili aeleze sababu za kushindwa kutekeleza mradi huo kwa kiwango kilichokubaliwa na kwa muda wa makubaliano. “Nataka ndani ya Siku Saba tukutane nae aeleze kwanini hajakamilisha mradi kwa mujibu wa mkataba wake,” alisema.

Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwainua Wakandarasi wazawa hata hivyo katika utekelezaji wa miradi hiyo ya REA, imedhihirika kwamba walio wengi wameshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano.Aidha, Naibu Waziri Mgalu alionya Wakandarasi waliopewa jukumu la kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuhakikisha wanatekeleza kwa mujibu wa mkataba na kwamba Serikali haitomvumilia Mkandarasi atakayekwenda kinyume.

“Wakandarasi mnaotekeleza mradi wa REA III; anayeona hawezi kazi atupishe; hatutomvumilia Mkandarasi anayeharibu kazi,” alionya Naibu Waziri Mgalu.Alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Miradi ya Umeme Vijijini inakamilika kwa kiwango kinachokubalika na kwa wakati kama inavyoelekezwa kwenye mikataba waliyoingia na Serikali.

Naibu Waziri Mgalu yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kukagua na kujiridhisha utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini hususan ya REA pamoja na kuzungumza na Wananchi na Wakandarasi kuhusiana na utekelezaji wake.

WANANCHI WA BUCHI-BWERA KUPATA DARAJA LA KUDUMU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.Evarist Ndikilo na viongozi wengine wa Mkoa huo wakati wa ziara yake ya kuweka jiwe la msingi katika Daraja la Mbuchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimpa MKandarasi maelekezo juu ya umuhimu wa daraja la Mbuchi kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu kutokana na hali adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo kwa hivi sasa.
Hawa ni wananchi wa kijiji cha Mbwera wakivuka kwa kutumia Mtumbwi kuja kijiji cha Mbuchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali hii ni kutokana na kukosekana kwa daraja linalounganisha vijiji hivyo lakini kwa sasa Ujenzi wa daraja hilo umeanza na utakamilika baada ya mwaka mmoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akimskiliza Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibiti kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Mbuchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbuchi na Mbwera kwenye Mkutano wa hadhara wakati alipokuwa anaweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Daraja la Mbuchi.


Nteghenjwa Hosseah,Kibiti.

Wananchi wa Kata ya Mbuchi Tarafa ya Mbwera Wilayani Kibiti kwa kipindi kirefu wametaabika na adha ya kukosa Daraja linalounganisha vijiji hivyo viwili vyevye wakazi zaidi ya elfu 24.

Kukosekana kwa Daraja hilo kumepelekea kukatika kwa mawasiliano ya Uhakika baina ya wananchi wa Mbuchi na wale wa upande wa Pili wa Bwera, kuongeza gharama za maisha na hata kupelekea maafa kwa wakina mama wanaojifungua na wagonjwa kwa sababu ya kukosa njia rahis na nafuu ya kuwafikisha katika huduma za Matibabu.

Vijiji hivyo ambavyo vimetengenishwa na Mto Mberambe ambao ni Tawi la Mto Rufiji na kutengeneza Delta ya Kaskazini tangu kuanzishwa kwake havijawahi kuwa na Daraja la kuwaunganisha katika shughuli zao za kila siku za kila siku za kujiletea Maendeleo.

Wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakitumia Mitumbwi kuwavusha kutoka eneo moja hadi Lingine na huku wakitozwa Tsh 200 kwa safari moja na Pikipiki kutozwa Tsh 1000 kwa safari; Huduma hiyo hupatikana kuanzia saa kumi ba mbili asubuh hadi saa kumi na mbili jioni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani JJafo akiwa ndiye mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa alitembele Tarafa hii miezi kadhaa iliyopita na kuona changamoto hii iliyompelekea kuwaagiza Tarura kuchukua hatua za haraka kwa kujenga Daraja la kudumu litakalounganisha wananchi hao wa maeneo hayo na huduma za kibinadamu.

Na Leo January 05,2018 Waziri Jafo amezuru tena katika vijiji hivyo kukagua Ujenzi wa Daraja la Mbuchi-Mbwera halkadhalika kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi huo utakaotatua changamoto kubwa ya mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wakati wa ukaguzi Daraja hilo Waziri Jafo alisema alitegemea kuona Mkandarasi amepiga hatua lakini ujenzi unaenda polepole sana ukiachilia mbali sababu zilizotolewa na Mkandarasi kuwa wa amechukua muda mrefu kutokana na ubovu wa barabara hivyo imekua ngumu kwake kufikisha materio.

“Nimepita katika barabara hii na nimeona Ubovu wake lakini haya yote ulitakiwa uyafahamu tangu mwanzo wakati unaomba kazi hii, sasa mpaka leo hakuna kazi ya maaa iliyofanyika hapa kama unahisi huwezi bora useme mapema ili tutafute Mkandarasi mwingine mwenye uwezo mkubwa” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa wananchi hawa wamepata tabu kwa kipindi kirefu, wameteseka sana,wamenyanyasika siwezi kuvumilia kuona hali hii inaendelea hawa ni wananchi kama walivyo wananchi wengine wa Nchi hii wana haki sawa wanahitaji huduma muhimu kama Daraja hili liweze kuwaunganisha, katika hili Mkandarasi utaniona mbaya na nitakua narudi mara kwa mara kukagua maendeleo ya ujenzi.

Akielezea maendeleo ya Ujenzi Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibiti amesema ujenzi wa Daraja hilo ulikua uanze Mwezi March,2017 lakini kutokana na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha iliyompelekea Mkandarasi kushindwa kupeleka vifaa na material kwenye eneo la kazi hivyo kuomba tupitia Mkataba na baada ya kufanya hivyo kazi ilianza rasmi mwezi Septemba,2017 na itachukua miezi 15

Daraja hilo ambalo litabadilisha maisha ya wananchi wa Mbuchi-Mbwera litagharimu Tsh Bil 2.4 na litakamilika mwezi Novemba 2018 na linasimamiwa na Wakala wa barabara Wilaya ya Kibiti

SERIKALI YA KUTANA NA WADAU WA SANAA KUJADILI KUHUSU SUALA LA MAVAZI KWA WASANII

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wadau wa Sanaa (hawapo pichani) kuhusu nini kifanyike kwa mavazi ya wasanii sababu ya kuwepo kwa wasanii wengi wanaovaa mavazi yanayokiuka na maadili ya kitanzania katika kikao chake na wadau mbalimbali wa Sekta ya Saana nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (kulia).
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Sanaa (hawapo pichani) kuhusu Sheria ya Filamu nchini inayosema lolote linalotoka nje ya nchi,Michezo ya kuigiza na kazi yoyote ya kisanii inayotengenezwa hapa nchini kusawili hali halisi ya kitanganyika, katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) kujadili nini kifanyike kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa maadili katika mavazi kwa wasanii.

Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania ambaye ni Mwanamuziki Mkongwe John Kitime akisisitiza kuwepo kwa Kampeni ya Kitaifa kusisitiza suala la mavazi yenye kulinda utamaduni wetu katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kujadili suala la mavazi kwa wasanii na taifa kwa ujumla.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Stara Thomas akichangia mada ya kuhusu mavazi ya heshima kwa wasanii nchini katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani).Na Anitha Jonas – WHUSM

WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA KILIMO WASAMBAZWE

$
0
0
*Ataka takwimu za kahawa ziwe tayari ifikapo Feb. 28

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji na Wilaya za Mbinga wahakikishe kuwa wanaunda kanda za kilimo na kuwasambaza maafisa kilimo wao badala ya kuwaacha wakae maofisini.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Januari 5, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga, kwenye ukumbi wa Jumba la Maendeleo, mjini Mbinga.

“Mkurugenzi wa TC na DC chuja maafisa kilimo ulionao na uhakikishe wanabakia watatu tu. Abaki DALDO, mtu wa horticulture na mthamini, wengine wote wasambaze kwenye kanda ili wasimamie wakulima wakiwa huko huko. Hili litekelezwe na Mkuu wa Wilaya ulisimamie” alisema.

Aliwataka maafisa kilimo wa zao la kahawa waende vijijini na kufanya sensa ili waweze kubaini wana wakulima wangapi wanaozalisha kahawa. “Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue kijiji kina wakulima wangapi wa kahawa, na wana ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi? Hii itaisaidia Serikali ijue inahitaji dawa za aina gani, mbolea kiasi gani na miche mingapi kwa wakulima wake,” alisema.

“Ninataka hizi takwimu ziwe zimekamilika ifikapo tarehe 28 Februari, mwaka huu,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mche wa Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha miche ya Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Januari 5, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia kahawa kwenye mashine ya kusagia kahawa, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kushoto ni Meneja Uzalishaji Rabiel Ulomi na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Januari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia sampuli za kahawa kwenye, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kulia ni Meneja Uzalishaji Rabiel. Januari 5, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya Mbinga, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma. Januari 5, 2018.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU PAMOJA NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wapishi wanaofanya kazi ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati akitoka kuona wagonjwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na manesi wanaohudumia wagonjwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Nasoro Rashid aliyelazwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mzee Hamadi Lila aliyekuwa akilia kwa furaha mara baada ya kumuona Rais alipofika katika wodi ya Sewahaji.
PICHA NA IKULU

CCM YATEUA WAGOMBEA UBUNGE KINONDONI NA SIHA

$
0
0
UCHAGUZI WA MARUDIO KATIKA KATA NNE ZA MANZASE (CHAMWINO), KIMAGAI (MPWAPWA), ISAMILO (MWANZA) NA MADANGA (PANGANI)
PAMOJA NA MAJIMBO YA SIHA (KILIMANJARO) NA KINONDONI (DAR ES SALAAM)
____________________

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wanachama wa CCM kuwa kimepokea taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa kutakuwa na uchaguzi wa marudio katika Kata na Majimbo yaliyotajwa hapo juu.

Wanachama wote wenye sifa za msingi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na waliokidhi vigezo vya uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM na Kanuni zake wanahamasishwa kujitokeza ili kuomba ridhaa ya Chama kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi huu wa marudio isipokuwa na kama inakavyoelekezwa na taarifa hii.

Aidha Chama kimejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na kisayansi, na zilizosheheni siasa za hoja na zinazojikita katika kushughulika na shida za wananchi na hatimaye kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huu wa marudio. Kwa maana hii, msisitizo unawekwa kwa wanao omba ridhaa ya kugombea, vikao vya uchujaji na mapendekezo, na vikao vya uteuzi kuzingatia Misingi ya Maadili na kuhakikisha waombaji wana akisi uaminifu, uadilifu, uchapakazi, heshima kwa watu, ukubalifu wa imani, siasa na itikadi ya CCM, nidhamu kwa chama na wawe watu ambao umma wa wananchi unawatambua kwa nafasi yao katika jamii inapokuja katika kushughulika na shida zao.

KWA WAOMBA DHAMANA YA UDIWANI

Wana CCM ambao wamejipima na kujitafakari na kuona wanatosha, wanakumbushwa kwamba kuchukua fomu ya ugombea udiwani katika Ofisi za Kata tajwa hapo juu ni tarehe 8-11 Januari 2018. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 11 Januari 2018 saa 10:00 jioni. Gharama ya fomu ni Shilingi 10,000/- tu za Kitanzania.

Wajumbe wa Mikutano Mikuu ya Kata watapiga kura za maoni tarehe 12 Januari 2018. Kamati za Siasa za Kata zitajadili na kutoa mapendekezo kwa Kamati za Siasa za Wilaya tarehe 13 Januari 2018.

Kamati za Siasa za Wilaya zitajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mkoa tarehe 14 Januari 2018. Kamati za Siasa za Mikoa zitajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Mikoa tarehe 16 Januari 2018. Halmashauri Kuu za Mikoa zitajadili na kufanya uteuzi wa mwisho tarehe 17 Januari 2018

Wagombea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushiriki katika uchaguzi wa Udiwani katika Kata nne watachukua fomu kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata katika kata husika tarehe 18-19 Januari 2018 na zoezi hili litafanyika chini ya usimamizi wa Katibu wa CCM wa Wilaya.

UCHAGUZI WA MARUDIO KWA MAJIMBO YA SIHA NA KINONDONI

Baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Ndg. Dkt. Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na Ndg. Maulid Mtuliakusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidhawagombea wa Ubunge wanaelekezwa kufika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo Uchaguzi kutoka kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa hiyo siku ya Jumanne, tarehe 9 Januari 2018 bila kukosa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
 
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

06 Januari 2018


WAZIRI UMMY AKABIDHI MIFUKO 200 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI MAWENI.

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akichimba msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwenye shule ya sekondari ya Maweni Jijini Tanga wakati alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo  
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akichimba mtaro huo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni Jijini Tanga leo Ambapo WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo .
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akichimba msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu kwenye shule ya sekondari ya Maweni Jijini Tanga wakati alipokwenda kushiriki msaragambo na kukabidhi mifuko 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo 
Sehemu ya mifuko ya Saruji iliyotolewa na WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga katikati akipokea cheti cha kutambua mchango wake kusaidia maendeleo ya Jiji la Tanga kutoka kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi kushoto ni Diwani wa Kata ya Maweni,Joseph Calvas 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi kulia akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wao katika kuinua sekta ya elimu kwenye Kata ya Maweni Diwani wa Kata hiyo kushoto Joseph Calvas 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi katika akimshukuru  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kulia kwa kusapoti elimu katika Jijini hilo baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni 
Afisa Elimuy Sekondari Jiji la Tanga,Lusajo Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari ambapo walimshukuru WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kulia kwa kusapoti elimu katika Jijini hilo baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Maweni 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akisaini kitabu cha wageni katika shule ya Sekondari Maweni Jijini Tanga katikati Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Ramadhani Posi
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Ramadhani Posi
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akipiga picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Maweni Jijini Tanga 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga katikati akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Maweni Zawadi Ponera kulia 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akitembelea maeneo mbalimbali katika shule hiyo kushoto ni diwani wa Kata ya Maweni,Joseph Calvas na kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zawadi Ponera
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga akimsikiliza kwa umakini Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaji Mustapha Selebosi kulia ni Kaimu Mhandisi wa Jiji la Tanga Mussa Mkomola (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

WAZIRI JAFO ASABABISHA SHANGWE KWA WAFANYABIASHARA WA MABIBO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.
Wafanyabiashara wa Mabibo wakimskiliza Mhe.Waziri Selemani Jafo
Wafanyabisara wa Mabibo wakifuatilia Mkutano wa Waziri Jafo kuhusu suluhisho la wao kuondolewa katika kiwanja cha Soko hilo.
Wafanyabisara wa Mabibo wakifuatilia Mkutano wa Waziri Jafo kuhusu suluhisho la wao kuondolewa katika kiwanja cha Soko hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.


Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekutana na wafanyabiashara wa Soko la Mabibo Jijini Dar es Salaam na kutoa Tamko la Serikal kuhusu wafanyabiashara hao kuhamishwa na kuachia eneo hilo ambalo ni Liko chini ya miliki ya Kiwanda.

Wazii Jafo amesema nimekuja hapa baada ya kupata malalamiko kupitia wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba mnataka kutolewa kwa sababu kiwanja hiki sio kiwanja cha Soko halali na Mahakama imetoa hukumu abayo inaonyesha eneo hili liko chini ya Miliki ya Kiwanda.

“Sisi hatuna Mamlaka ya kuvunja hukumu ya Mahakama lakini katika hili kuna maslahi mapana ya wafanyabiashara ambao ni wanyonge wanaofanya biashara katika eneo hili lazima tuwaangalie kwa namna tofauti na kuangalia namna ya kuwasaidia ili waweze kuendesha maisha yao”

Aliongeza kuwa Agenda ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufu ni kuhakikisha wanyonge wanapata haki zao hivyo ameniagiza nije kuwasikiliza na kutafuta suluhisho la haraka dhidi ya wafanyabiashara wa Mabibo.

“Baada ya kufika hapa nimetoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kukutana na Yono Auction Mart, Uongozi wa Kiwanda na wote wanaohusika ili tupate njia muafaka ya kuhakikisha wafanyabishara wa eneo hili wanaendelea kufanya biashara zao vizur kama walivyokuwa wanafanya hapo awali”.

Naomba muwe watulivu muendelee na biashara zenu, suala hili Serikali inalishughulikia kwa umakini na haraka zaidi ukizingatia hiki ni kipindi cha mwezi January ambapo Fedha zinahitajika kwa ajili ya ada za watoto, kodi za nyumba nk mkibugudhiwa mtashindwa kukidhi mahitaji ya Familia alimalizia Mhe.Jafo.

Soko la Mabibo lenye wafanyabiashara zaidi ya elfu mbili limekubwa na mgogoro huu miezi kadhaa iliyopita kufuatia Kiwanda cha Urafiki kuwataka waondoke hapo ili kupisha eneo hilo kwa matumizi ya kiwanda ilihali eneo maalumu la kuwahamishia wafanyabiashara hao bado halijakamilika lakini pia wafanyabishara wamekuwa wakionyesha hisia zao kuwa eneo hilo walilopo sasa ni la Kimkakati kwa biashara zao kutokana kuwa katikati ya Mji hivyo kuwa rahisi kufikika kwa wateja wa aina zote.

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI AFANYA ZIARA MKOANI MOROGORO.

$
0
0
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel afanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro na kutembelea kiwanda cha 21 Century pamoja na kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd vyote vya mjini Morogoro.

katika hotuba yake Prof. Elisante amesifu utendaji wa kazi wa viwanda hivi na kluwataka kuongeza juhudi ya uzalishaji wenye tija na kuthamini wafanyakazi.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa Serikali inapenda kuona muelekeo mzuri wa Viwanda kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 hivyo ni jukumu la wenye Viwanda kuongeza uzalishaji wenye tija ambapo kwa upande wa serikali kazi yetu ni kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuondoa vikwazo vya kufanya shughuli.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akipokelewa na mtendaji mkuu wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia pamba iliyosokotwa kushoto kwake ni ndugu Gevaronge Miyombe, Mchumi Wizara ya Viwanda na kulia kwa katibu mkuu ni ndugu Deus Rwegasira Msimamizi Mkuu, Idara ya Usokotaji katika kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia mashine ya usokotaji wa nyuzi pembeni ni ndugu Deus Rwegasira, Msimamizi Mkuu -Idara ya Usokotaji katika kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
Wafanyakazi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akizunguka katika kiwanda cha ABOOD SEED OIL INDUSTRY LTD akiangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho mapema hii leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza mwekezaji wa kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd Mbunge jimbo la Morogoro Mjini ndugu Abdulaziz Mohamed Abood wakati wa majadiliano mara baada ya kutembelea kiwanda hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd. cha mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akizungumza na wamiliki wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro (Hawapo pichani) pembeni ni ndugu Ernest R. Mkongo – Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya uchumi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

WANANCHI WA GAIRO WAFURAHIA UJENZI WA BARABARA YA LAMI

$
0
0


Mkuu wa Wilaya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (aliyevaa kiti jekundu la drafti) akimuonyesha Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby madhara ya miundombinu kwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo.
Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby, akielezea hali ya barabara kwasasa na jinsi ilivyokuwa zamani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Agnes Mkandya akifafanua jambo.
Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Kilian akielezea jambo mbele ya viongozi wa wilaya ya Gairo walifika kutembelea barabara hiyo kujionea eneo lililoadhiriwa na mvua..

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA), Gairo Bw. Simon akielezea jambo wakati wa ziara hiyo. Pembeni kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe na (wa kwanza kulia) ni Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby wakiwa na viongozi wengine.

Wananchi wa Wilaya ya Gairo wametoa shukrani zao za pekee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwawezesha kupata barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 3.5.

Hayo yamezungumzwa na Kata ya Magoweko mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ziara ya viongozi wa wilaya ya Gairo walipofanya ukaguzi wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua za mwisho kumalizika.

"Wana Gairo tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwani barabara ya lami ni muujiza hatukuwahi kuota kama itatokea," walisema wakazi hao.

Viongozi hao ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Bw. Shabani Sajilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Meneja TARURA. Bw. Simon, Wajumbe KUU (W) nk walifanya ziara hiyo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea Wilayani.

Aidha dhumuni rasmi la ukaguzi huo ilikuwa ni kuhakikisha ujenzi huo unaisha kwa wakati ambapo barabara inatakiwa kukabidhiwa Januari mwaka huu.

Barabara hiyo ni matokeo ya ahadi ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambaye kwa sasa ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Gairo miaka mitatu iliyopita kwenye mkutano wa hadhara ambao Mgeni Rasmi alikuwa rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZINDUA UMEME KISIWA CHA FUNDO PEMBA LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akibonyeza kitufe kuashiria kuuzindua Umeme katika Kisiwa cha Fundo Wilaya ya Wete Pemba ikiwa na shamrashamra za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika kisiwa hicho leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika Kisiwa cha Fundo kisiwani Pemba ikiwa katika shamra shamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika kisiwa hicho huko Fundo Wilaya ya Wete.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika kisiwa cha Fundo kwa ajili ya Uzinduzi wa Umeme leo mchana.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Maji Ardhi Mazingira na Nishati Mhe. Salama About Talib alipowasili katika Kisiwa cha Fundo kwa ajili ya Uzinduzi wa Umeme.(Picha na Ikulu)
 
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi wa Kisiwa cha Fundo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umeme.(Picha na Ikulu)

WANAFUNZI wa Madrasatul Hidaya Islamia ya Tumbe wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kisiwa cha Fundo kwa ajili ya uzinduzi wa Umeme leo.(Picha na Ikulu)

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AFUNGUA BARABARA YA FUONI MELI TANO KWARARA ZANZIBAR WAFANYIKA

$
0
0
Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Muhammed Gharib Bilal alipokata utepe kuashiria kufungua Barabara ya Kilomita Mbili ya Fuoni Meli Tano Kwarara.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Baloz Ali Abeid Karume.
Barabara ya Fuoni Meli Tano Kwarara yenye urefu wa kilomita mbili iliofunguliwa na Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Muhammed Gharib Bilal.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Muhammed Gharib Bilal akikunjuwa kitambaa kuashiria kufungua Barabara ya Kilomita Mbili ya Fuoni Meli Tano Kwarara.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Ufunguzi wa Barabara ya Kilomita Mbili ya Fuoni Meli Tano Kwarara.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Baloz Ali Abeid Karume akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Barabara ya Kilomita Mbili ya Fuoni Meli Tano Kwarara.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Muhammed Gharib Bilal akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya ufunguzi wa Barabara ya Kilomita Mbili ya Fuoni Meli Tano Kwarara.Ikiwa Shamra Shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

CCM YAWAHAMASISHA NA KUWAUNGA MKONO WANAFUNZI WA UALIMU (DUCE) WANAOJITOLEA KUFUNDISHA KATIKA SHULE ZA SERIKALI

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Kamati ya Wanafunzi wanaojitolea kufundisha katika shule za Serikali na wanaosomea Masomo ya Ualimu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) pamoja na Uongozi wa Tawi la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chuoni hapo.

Kamati hiyo ya Wanafunzi wanaojitolea kufundisha katika shule za Serikali imekuwa na utaratibu wake mahususi ambapo wanafunzi wanaosomea ualimu Chuoni hapo hufundisha masomo mbali mbali ikiwamo yale ya Sayansi, Hisabati, na Uchumi katika shule za Serikali kuanzia shule za msingi na sekondari.

Awali akitoa neno la utambulisho na ufunguzi Mwenyekiti wa Kamati ya Wanafunzi wanaojitolea Ndg. Emijidius Cornel alieleza ushirikiano ambao wameupata kutoka kwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na kwamba walichukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa Taifa katika sekta ya elimu zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Uongozi wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naye Mwenyekiti wa Tawi la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Tweve Enock la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) alipongeza Kamati ya Vijana wanaojitolea na kufafanua programu hiyo ya kujitolea ni sehemu ya mipango ya Tawi la Chama chuoni hapo kuunga mkono uharakishaji wa utekelezaji wa Sera za CCM na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015-2020.

Katika nasaha zake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi amesema kitendo cha kutoa elimu na kupeleka maarifa kwa kujitolea ni kitendo cha Kijamaa na kinakwenda sambamba na misingi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiifafanua baadhi ya misingi hiyo amegusia Ahadi za mwanachama wa CCM zinazosema nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondosha umasikini, ujinga, magonjwa na dhuluma na nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

Aidha ndugu Polepole amesisitiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuunga mkono jitihada na harakati za watu na makundi ambayo yanatumia muda wao kushughulika na shida za watu kwa sababu kufanya hivyo ni sehemu ya utume wa mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM katika Uongozi wake wa awamu ya Tano.

Katika Mkutano huo, aliyekuwa Mshauri na Mlezi wa Taasisi ya CHASO-DUCE Ndg. Gracious Mwanguya ameomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, na ameshauriwa kufuata utaratibu katika Tawi lililo karibu naye.

Wakati uo huo, Seneti ya Mkoa wa Dar es Salaam imekuwa na kikao chake cha kazi kwaajili ya kupanga mikakati ya ujenzi wa Chama mwaka 2018. Akizungumza na Seneti hiyo Ndg. Polepole amewakubusha umuhimu wa kuwa mabalozi wazuri wa CCM na kuyaishi masharti ya Uanachama

Mwanachama mwaminifu ni yule anayeyaishi masharti ya uanachama kama yalivyoainishwa katika Katiba ya CCM Ibara ya 8(2) Kuwa awe mtu anayefanya juhudi ya kuielewa, kuielezea, kuitetea na kutekeleza Itikadi na Siasa ya CCM na awe mtu 8(4)… anayependa kushirikiana na wenzake na 8(5) kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma kulingana na Miongozo ya CCM, alisema Ndg. Polepole akinukuu vifungu hivyo vya Katiba.

Shughuli hizi mbili ni mwendelezo wa vikao vya ndani na sehemu ya kazi ya Ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo zimeshaanza kwa mwaka 2018 na zitaendelea katika Mikoa na Wilaya zote nchini huku msisitizo ukiwa ni kufanya kazi kwa bidii ikiwamo kwa kujitolea, kuendelea kushughulika na shida za watu na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM

Imeandaliwa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA





MBUNGE UNGANDO KUTATUA KERO YA KITANDA CHA KUJIFUNGULIA HUKO MUYUYU

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti

MBUNGE wa jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani ,Ally Ungando ameahidi kuitatua kero ya kitanda cha kujifungulia akinamama wa kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda,kero ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.

Pamoja na hilo amesema atatoa fedha kiasi cha sh.mil.nne ambapo mil.mbili itakuwa kwa ajili ya kujenga choo kwenye nyumba ya mganga wa zahanati ya Muyuyu na milioni mbili nyingine kwa lengo la kumalizia choo katika shule ya msingi Muyuyu.

Ungando alibaini kero hiyo wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya siku 21 jimboni humo .Hata hivyo Ungando ,alisema ataendelea kwenda sambamba na kauli mbiu yake yake ya mwendo kasi katika maendeleo ya Kibiti .

Alieleza ,jukumu lake kubwa ni kushirikiana na wananchi kutatua kero mbalimbali zinazowakabili ,kuzisimamia kwenye idara husika na kufuatilia yale yanayoendelea kufanyiwa kazi .Ungando ,aliwataka wananchi wa Kibiti kushirikiana nae kuchangia pia shughuli za kimaendeleo badala ya kuisubiria serikali pekee ama wafadhili suala ambalo litawachelewesha kupiga hatua na kutoka walipo sasa .

"Ninafanya ziara hii ,sio kujua changamoto zilizojitokeza na kuwaeleza nilipofikia kwenye ufuatiliaji kwa zile nilizoanza nazo " serikali inafanya yale ambayo yapo kwenye taratibu zake hivyo na sie jamii tuiungr mkono kwa kuendeleza yale ambayo yapo kwenye uwezo wetu "alisema Ungando.

Mbunge huyo ,alipokuwa kata ya Kiongoroni alitembelea visiwa vya Pombwe,Jaja,Kiongoroni na Ruma aliwaasa wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na kuacha tabia ya kuwaacha majumbani jambo ambalo linawakosesha haki ya kielimu.

Ungando alitaka wananchi wa visiwa hivyo ,kuwachunguza watu ambao wana mashaka nao kwakuwa wahalifu wakitokea Gongoni wanaweza kukimbilia visiwani.Alisema ulinzi na usalama upo mikononi mwa kila mmoja hivyo wachunguzane wao kwa wao kwani wanajuana.

Akiwa visiwani hapo,alipokea changamoto za uchache wa watumishi wa idara ya afya,elimu ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu na miundo mbinu ya barabara na kuahidi atazisimamia .Wananchi wa vijiji hivyo walimshukuru Mbunge wao Kwa juhudi anazozionyesha kwa kuwatumikia na walimuomba akafanyie kazi changamoto walizomueleza ili kuondokana na adha walizonazo.

Katika ziara hiyo ,Ungando alitoa mifuko ya saruji 100 kwenye kata alizopitia ili kusaidia masuala ya maendeleo ambapo ameshatembelea kata ya Mtunda,Mtawanya,Ruaruke na Kiongoroni.
Mbunge wa jimbo la Kibiti, mkoani Pwani Ally Seif Ungando ,wa kwanza kulia akisafiri na msafara wake ,kwa kutumia njia ya majini kuelekea kwenye visiwa vilivyopo kata ya Kiongoroni, kwenye muendelezo wa ziara yake jimboni humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)

KAULI YA MBUNGE YADAIWA KUCHOCHEA WANANCHI KUUA TEMBO

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KAULI za baadhi ya wanasiasa za kuhamasisha wananchi kuua tembo katika Jimbo la Serengeti mkoani Mara zinadaiwa zimeanza kuleta athari baada ya watu wanne kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuua tembo.

Baadhi ya wananchi ambao wameomba majina yao kutoandikwa kwenye habari hii, wameiambia Michuzi Globu kwa njia ya simu kuwa kuna mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Chacha(Chadema) akiwa kwenye msiba wa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 aliyeuliwa na tembo katika kijiji cha Kenoku kwa Mfano aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali imeshindwa kuweka uzio ili tembo wasilete madhara, hivyo nao wawaue tembo tu.

Kwa mujibu wa watoa taarifa hizi wamedai baada ya kauli hiyo imeonekana kuchochea watu kufanya ujangiri kwa kuua tembo na Jumatano ya wiki hii kuna watu wanne katika kijiji cha Robanda wamekamatwa kwa tuhuma za kuua tembo.

"Ni vema Mbunge akawa makini na kauli zake kwani baada ya kuwaambia wananchi waue tembo wanapokuja kijijini, tayari kuna watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kuua tembo eneo la kijiji cha Robanda jimboni Serengeti."Hili si la kulifumbia macho kwa mbunge wetu amekuwa na utamaduni wa kutoa kauli ambazo zinachangia wananchi kuua tembo"amedai moja ya watoa taarifa hizi.

MBUNGE AFAFANUA

Akizungumza na Michuzi Globu, Mbunge wa Serengeti Chacha Marwa amesema madai ya wananchi hao ambao wametoa taarifa hizo hayana ukweli wowote.

Kwani amesema hakuna mahali ambako amewaambia wananchi waue tembo na badala yake amekuwa akiiomba Serikali kufanya jitihada za kuweka uzio ili tembo wasiingie vijijini kwa wananchi kwani watu wanakufa na mazao yanaharibiwa kila kukicha.Marwa amesema amefuatilia suala hilo muda mrefu Wizara ya Maliasili na Utalii tangu Waziri akiwa Profesa Jumanne Maghembe lakini hakuna uzio hadi leo hii.

Ameongeza amewahi kuandika barua kwa Spika wa Bunge ya kulalamikia tembo kuingia maeneo ya wananchi na kuleta madhara hakuna ambacho kimefanyika."Nikweli nilienda kushiriki kwenye msiba wa kijana mmoja aliyeuliwa na tembo siku za karibuni, ila sijahamasisha wananchi kuua tembo na siwezi kufanya hivyo.

"Kwanza kijiji ambacho msiba umetokea ni kilometa 50 na kijiji cha Robanda, sasa kwanini wanizushie hayo maneno.Hayo ni mambo tu ya siasa za huku kwetu."Pia tuseme ukweli, wananchi wamekuwa wakiteseka sana kutokana na tembo kuja kwenye makazi ya watu na kuleta madhara, kila siku wananchi wanalia na ipo siku watachoka kweli.

"Hivyo niiombe Serikali itusaidie kuondoa tatizo hili huku kwetu kwa kulinda usalama wa wananchi wake,"amesema Marwa.

POLISI YATAJA WANAOSHIKILIWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limekiri kukamatwa kwa watu hao baada ya kupatikana kwa taarifa za kuua tembo hao ambapo kwa sasa jeshi hilo linawashikilia. 

Limewataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kutuhuma hizo za kuua tembo na kukutwa wakiwa na meno yake ni Kirihena Bwanana(34),mkazi wa Bwitenga.Wengine ni Kasimu Mussa(40),mkazi wa Robanda, Hamisi Gamuhu(37),mkazi wa Robanda na Hamisi Mabula(52) mkazi wa Kitembele.
 Watuhumiwa wa pembe za ndovu wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mara baada ya kunaswa wakituhumiwa kuua tembo.
 Mtuhumiwa wa pembe za ndovu akiwa amewekwa chini ya Ulinzi na Askari Wanyama Pori  

Mtuhumiwa wa pembe za ndovu akiwa amewekwa chini ya Ulinzi na Askari Wanyama Pori  

KAMANDA WA POLISI TANGA AZUNGUMZIA BASI SIMBA COACH KUCHOMWA MOTO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa ufafanuzi kuhusu tukio la kuchomwa moto kwa basi la Simba Coach.

Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza basi hilo limechomwa leo na wananchi wenye hasira kali baada ya dereva wake kumgonga dereva wa bodaboda.

Akizungumza na Michuzi Globu kwa njia ya simu muda huu, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amefafanua ni kweli amesikia taarifa za kuchomwa moto basi hilo lakini halijachomwa mkoani Tanga kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

Amesema baada ya kuona taarifa za kuchomwa basi la Simba Coach waliamua kufuatilia lakini wamejiridhisha haikutokea kwenye mkoa wao ila  basi hilo limechomwa nchini Kenya.

Kamanda Bukombe ameiambia Michuzi Globu kuwa basi hiyo ilikuwa inatoka Mombasa nchini Kenya na taarifa walizonazo limechomwa huko huko nchini Kenya kwani lilikuwa halijaingia kwenye mipaka ya nchi yetu ya Tanzania na hasa mkoani Tanga.

Alipoulizwa iwapo anafahamu namba za basi hilo linalodaiwa kuchomwa moto na dereva aliyekuwa analiendesha ,amejibu wanaendelea kufuatilia kwa polisi wa nchini Kenya na kisha atatoa taarifa kuufahamisha umma.

"Tunaendelea kukusanya taarifa na kwa kuwa limechomwa huko Kenya tunawasiliana na polisi wa huko ili tuwe na uhakika wa taarifa Kamili za tukio hilo.Hatujapata namba za basi.Wananchi wasubiri tutaeleza kwa usahihi tutakapokamilisha kupata ukweli zinazohusu tukio hilo, "amesema Kamanda Bukombe.

TAARIFA KUCHOMWA MOTO SIMBA MTOTO

Mapema asubuhi ya leo katika mitandao ya kijamii zilianza kuzagaa picha zinazoesha basi linaungua moto, na vyanzo vya moto huo ikawa inaelezwa ni wananchi wenye hasira wamechoma moto basi la Simba Coach.

Taarifa hizo zikawa zinadai tukio hilo limetokea Mkoa wa Tanga lakini haikuwa inaonesha ni wananchi wa eneo gani walioamua kuchoma basi hilo.

Pia taarifa hiyo imedai basi limochomwa moto kutokana na dereva wake kugonga dereva wa pikipiki na hivyo wananchi wakaonesha hasira zao kwa kulichoma moto basi hilo. 


 

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (MIFUGO) DK MARIA MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili kuepuka kuiraribu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi mapema leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.



Na Kumbuka Ndatta, WMUV

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dk. Maria Mashingo amewataka wafugaji kuhakikisha wamekamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo yao kabla ya muda ulioongezwa na Serikali wa hadi Januari 31 mwaka huu kwani baada muda huo kupita haijulikani Serikali itaamua nini kuhusu mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Igalula Kata ya Mpanda ndogo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Dk. Mashingo alisema zoezi hilo la upigaji chapa linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 .

Dk. Mashingo alisema upigaji chapa umelenga kudhibiti magonjwa ya mifugo,wizi wa mifugo, uimarishaji usalama wa afya na mazao ya mifugo sambamba na kudhibiti usafirishaji na uhamaji wa mifugo kiholela na kuimarisha biashara ya mifugo na mazao yake kitaifa na kimataifa.

"Wafugaji hakikisheni mifugo yenu yote inapigwa chapa kwani baada ya Januari 31 mwaka huu hatujui Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa "alisema.

Dk. Mashingo alisema pamoja nia njema ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwatetea wafugaji wanaofanyiwa vitendo vya uonevu na mamlaka nyingine za Serikali pia aliwahimiza kutii sheria za nchi kwa kutoingiza mifugo yao kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Pia aliwakumbusha wafugaji kutambua kuwa rasilimali ya mifugo waliyonayo ina thamani kubwa na kwamba wao pia ni sehemu ya wawekezaji hivyo ni vyema wakatengeza miundombinu bora kwa ajili ya mifugo yao kuliko kuisubiri Serikali pekee kujenga miundombinu hiyo.

“Wafugaji ni wawekezaji muhimu sana katika nchi yetu kwani kama wasingekuwepo nchi ingelazimika kuagiza mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi na tungelazmika kutumia sh. trioni 17 kwa mwaka”alisema Dk. Mashingo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Cresencia Joseph amemweleza Dk. Mashingo kuwa mkoa huo unajumla ya ng'ombe 570,758 ambapo kati ya hao 423,767 wameshapigwa chapa.

Dkt KALEMANI akagua maeneo ambayo Waziri Mkuu ataweka Jiwe la Msingi

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametembelea maeneo mawili anayotarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 7/01/2018 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.

Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.

Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi. Meneja wa Mradi Mkubwa wa Usafirishaji wa Umeme wa Makambako - Songea Mhandisi Didas Lyamulya akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo la ujenzi wa mitambo ya kupoozea umeme unaoendelea kujengwa wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirirka la Umeme Tanzania (Tanesco) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioambatana na Waziri wa Nishati ili kukagua eneo litakalowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kupoozea Umeme katika mradi wa Kusafirisha umeme wa Makambako Songea.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto ) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme katika mradi wa Kusafirisha Umeme wa Makambako-Songea wilayani Songea tayari kwa ajili ya kuwekwa kwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Tarehe 7/01/2018.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka akimweleza jambo walipotembelea eneo la uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako-Songea ili kujionea maandalizi ya uzinduzi huo.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images