Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WAZIRI MPINA ATOZA FAINI YA MILIONI 180 VIWANDA VYA KUCHAKATA MINOFU YA SAMAKI

$
0
0


Meneja uchakataji wa Kiwanda cha kuchakata samaki Victoria cha jijini Mwanza, Endwin Okwong’o (aliyeshika kofia) akimuelezea Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani), namna ambavyo wanapokea samaki kutoka kwa mawakala na kuwachambua kabla ya hatua ya kuchakata kiwandani hapo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia), akimpima urefu samaki aina ya Sangara kwenye rula maalum ili kubaini kama ana urefu unaotakiwa kisheria kwenye kiwanda cha Nile Perch Limited jijini Mwanza, kushoto Dkt. Yohana Budeba Katibu Mkuu Uvuvi na kulia ni Bwana Gabriel Mageni Afisa Mvuvi Mkuu. Samaki chini ya sentimita 50 na mwenye zaidi ya sentimita 85 hawaruhusiwi kisheria kuvuliwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akimbeba samaki aina ya sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu alipokuwa katika ukaguzi wa mazao ya uvuvi katika Kiwanda cha Nature Fisheries Limited Jijini Mwanza, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Yohana Budeba na kulia ni Afisa Uvuvi Mkuu Bw. Boniface Shatila.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (Mwenye Kofia) akitoa tamko la Serikali la kuwataka wenye viwanda vya samaki kutofadhili uvuvi haramu alipotembelea katika gati la Kiwanda cha samaki cha Tanzania Fish Processing (TFP) jijini Mwanza leo, kulia ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba.

Samaki mzazi aina ya Sangara aliyevuliwa kinyume na taratibu(alikuwa na urefu wa sentimita 120), samaki ambaye akiachwa ziwani kwa muda wa miezi mitatu ana uwezo wa kuzaa samaki milioni tatu, na kuongeza idadi kubwa ya jamii hiyo ya samaki katika ziwa Victoria.





Na Mwandishi Maalum, Mwanza

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewaamuru wamiliki wa viwanda vitano vya kuchakata minofu ya samaki vilivyoko jijini Mwanza kulipa faini ya shilingi milioni 180 ndani ya saa 24 baada ya kubainika kupokea na kuchakata samaki wasioruhusiwa kwa kukiuka Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 sambamba na Sheria ya usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004

Pia Waziri Mpina amechukizwa na kitendo cha viwanda hivyo kufadhili uvuvi haramu na kueleza kuwa ni bora kutokuwa na kiwanda hata kimoja cha samaki kuliko kuendelea kuwa na viwanda vinavyofadhili uvuvi haramu na kutishia kuvifunga viwanda vyote sambamba na kutaifisha samaki, magari na boti zinazobeba samaki wasioruhusiwa.

Waziri Mpina amesema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara kutembelea viwanda vinavyochakata samaki jijini Mwanza ambapo pia amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuwasimamisha kazi maofisa watatu wa Kitengo cha Udhibiti wa Usalama na Ubora wa Mazao ya Uvuvi Kituo cha Mwanza kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kulisababishia Taifa hasara kubwa.

Maofisa hao ambao Waziri Mpina ameagiza wasimamishwe kazi na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ni pamoja na Philemon Mugabo,Dorina Mlenge na John Bosco Rubajuna

Waziri Mpina ametaja viwanda vilivyokutwa vikichakata samaki wasioruhusiwa wakiwemo samaki wazazi na samaki wachanga na idadi ya kilo zilizokamatwa kwenye mabano kuwa ni pamoja na Nile Perch Fish (920), Victoria Fish (131), Nature Fish (150), Omega Fish (580), Tanzania Fish Processing (842) huku magari 41, boti 15, Nyavu haramu 294 wakiwa na samaki wachanga na wazazi ambapo sheria inakataza kuvuliwa samaki chini sentimita 50 na juu ya sentimita 85 .

Majina ya viwanda hivyo na faini zao walizotozwa Nile Perch sh milioni 25, Tanzania Fish Processing sh. milioni 50, Victoria Perch Milioni 30, Nature Fish milioni 25, Omega Fish Ltd milioni 50 ambapo amesisitiza kuwa adhabu hiyo ni ya kwanza na ya mwisho na kwamba ikithibika tena wenye viwanda waendelea kufadhili uvuvi haramu hatua za kuvifunga viwanda na kutaifisha mali ikiwemo mitumbwi, boti na magari yatakayokuwa yanabeba samaki hao itafuata.

Waziri Mpina amesema ukanda wa Ziwa Victoria ulikuwa na Viwanda 13 vya kuchakata samaki vilivyokuwa na uwezo wa kuchakata tani 1,065 kwa siku lakini kutokana na kushamiri kwa uvuvi usiongatia sheria kumesababisha viwanda 5 kufa kutokana na kukosekana malighafi na kwamba viwanda 8 vilivyobaki sasa vinachakata tani 171 tu kwa siku huku ajira zikiwa zimeporomoka kutoka ajira 4, 088 na kufikia 2,179 tu.

Mpina amesema tayari Rais Dk John Magufuli ameshatoa maagizo kwa wavuvi kuachana na uvuvi haramu sambamba na wenye viwanda kutofadhili uvuvi huo huku pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye akisisitiza jambo hilo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikikemea vikali huku Sheria za nchi nazo zikikataza jambo hilo lakini wenye viwanda kwa makusudi wameamua kudharau maagizo ya viongozi wakuu wa nchi jambo ambalo Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya uongozi wake Waziri Mpina haliwezi kukubalika kamwe.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dk. Yohana Budeba amesema kama watumishi wa wizara yake wangesimamia majukumu yao kikamilifu mambo hayo aliyobaini Waziri Mpina yasingejitokeza huku akikiri kupokea maagizo yake yote na atayasimamia kwa haraka kuona yanatekelezwa.

Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC), Mhandisi Boniphace Guni amesema wenye viwanda hivyo wamekutwa na makosa ya kupatikana na samaki waliochini wa ukubwa, kukutwa na samaki wachanga kinyume cha Sheria ya Usimamizi Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 ambapo wamekiuka kifungu namba 58(I)(a) hivyo wamestahili adhabu hiyo ya kulipa faini ya milioni 180 ndani ya saa 24 .

WAFANYAKAZI WAPYA WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WAPIGWA MSASA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza leo na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa katika Taasisi hiyo kuhusu umuhimu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.
Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na vitengo vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupi pichani) wakati akinzungumza na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa katika Taasisi hiyo.
Afisa Tawala wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akiwaelekeza jinsi ya kujaza fomu watumishi wapya 57 wa Taasisi hiyo ambao wameajiriwa hivi karibuni.
Picha na JKCI


Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na kuepuka vitendo vya rushwa.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Prof. Mohamed Janabi, wakati alipokuwa akuzungumza na wafanyakazi wapya 57 wa kada mbalimbali walioajiriwa hivi karibuni.Alisema miongoni mwa wafanyakazi hao, wapo madaktari, maafisa uuguzi, wahasibu, maafisa Tehama, wahudumu wa afya, wataalam wa maabara na maafisa ustawi wa jamii.

“Mtumishi wa umma lazima ufanye kazi kwa kuzingatia maadili na sheria za kazi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yako.“Humu ndani ya taasisi kazi yetu inahitaji nidhamu ya hali ya juu kwa sababu tukikosea hata kidogo maana yake tunapoteza maisha ya mtu.

“Ukipangiwa zamu zingatia, msipokee rushwa, kwani ni kitu hatari sana ukimuona mwenzio anajihusisha na vitendo hivyo hatua ya kwanza ni kumkemea na kumshauri kuacha mara moja,” amesisitiza.Amewataka wafanyakazi hao kuzingatia kuvaa mavazi yenye staha wakati wote hususan wale ambao watakuwa hawavai sare maalum za kazi.

“Hakikisheni mnawahi kazini, kama unaishi mbali jitahidi kuwahi mapema kutekeleza majukumu yenu,” amewasihi.Prof Janabi hakusita kuwaeleza wafanyakazi hao baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ikiwamo ufinyu wa nafasi.“Ofisi tulizonazo ni chache, kwa kuanzia tutashirikiana hivyo hivyo hasa wale ambao si wataalamu wa afya,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Taasisi hiyo, Ghati Chacha alisema kati ya wafanyakazi walioajiriwa 23 ni wanaume na 29 ni wanawake.“Wameajiriwa JKCI baada ya kupatiwa kibali na Serikali kulikuwa na nafasi 57 zilizojazwa ni 56 na hadi sasa walioripoti kazini ni 52, wanne wameomba udhuru kwani wana dharura na hadi kufikia wiki ijayo tunatarajia nao watakuwa wameripoti kazini,” amesema.

Dkt KALEMANI ataka Kupitiwa upya Mikataba ya Gawio la Serikali Kutoka Songas

$
0
0

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameitaka kampuni ya kuzalisha umeme ya SONGAS, kupitia upya mikataba ya gawio kwa serikali ili kuhakikisha serikali inapata mgao sawa na Kampuni hiyo na kubadilisha mfumo wa sasa ambapo serikali inapata gawiwo la faida baada ya uzalishaji.

Ni katika ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipotembelea katika kampuni ya kuzalisha Umeme ya Songas, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo Dr. Kalemani akaitaka kampuni hiyo kupitia upya mikataba yao katika gawio na serikali.

Aidha Waziri Dkt kalemani amethibitisha mchango wa serikali katika uchangiaji wa uzalishaji wa sekta ya umeme sanjari na kampuni ya Songas pia lakini akakemea vikali tabia ya kutofautiana kwa mgao baina ya kampuni hiyo na Serikali.

Sebastian Kastuli ni meneja biashara wa kampuni ya Songas ambaye anaahidi kutekeleza maagizo ya Waziri na kupitia upya mikataba yao na serikali.

Aidha Waziri Dkt Kalemani amezitaka kampuni zote za uzalishaji nchini kuacha mara moja tabia ya kuagiza mitambo ya uzalishaji nje ya nchi na badala yake ipatikane hapahapa nchini.

HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE MAAFURU NYUMBA YA TEMBO YAZIDI KUVUTIA WATALII

$
0
0
Wanyamapori aina Tembo wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire inayopatika kwenye mikoa ya Manyara na Arusha ni kivutio kikbwa kwa wageni wanaotembela hifadhi hiyo.


Wanyamapori aina Tembo wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire inayopatika kwenye mikoa ya Manyara na Arusha ni kivutio kikbwa kwa wageni wanaotembela hifadhi hiyo.
Miti aina ya Mibuyu inaonekana kwa wingi na inaongeza mvuto kwenye hifadhi ya Taifa Tarangire.
Kundi la Tembo likinywa maji ndani ya Hifadhi ya TaifaTarangire.
Pundamilia ni sehemu ya kivutio cha watalii wa ndani na nje ya nchi .
Ndege aina ya Kanga
Msururu wa magari ya watalii ukisubiri utaratibu wa malipo kwa njia ya kadi kuanza safari ya kutembelea hifadhi hiyo
Watalii wakiwa ndani ya Hifadhi

IGP AKAGUA MIRADI KINONDONI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi. 
 Wananchi wa Kigogo Mburahati jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao. Picha na Jeshi la Polisi.






Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa  Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya  Jeshi hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

MBUNGE WA LUSHOTO AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuijali kata hiyo kwa kupeleka fedha milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kisasa katika Kata ya Mlola ambapo kati ya hizo milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa wakati kituo hicho kitakapomalika huku milioni 400 zikiwa tayari wameingiziwa tayari kwa ajili ya ujenzi huo
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuijali kata hiyo kwa kupeleka fedha milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kisasa katika Kata ya Mlola ambapo kati ya hizo milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa wakati kituo hicho kitakapomalika huku milioni 400 zikiwa tayari wameingiziwa tayari kwa ajili ya ujenzi huo
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara kushoto ni Diwani wa Kata ya Mlola
Diwani wa Kata ya Mlola (CCM) akizungumza katika mkutano huo kabla ya  kumkaribisha mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia aliyekaa kulia
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia aliyekaa kulia akiwa na diwani wa Kata ya Mlola wakifuatilia kwa umakini maswali ya wananchi katika mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia aliyekaa kulia akiandika baadhi ya kero alizoelezwa na wananchi hao ili kuweza kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wao
 Mkazi wa Kijiji hicho Kata ya Mlola wilayani Lushoto akimuuliza swali Mbunge huyo

 Mmoja kati ya wakazi wa Kijiji hicho akimuuliza Mbunge huyo swali kuhusu kuwasaidia vijana na ajira za mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga
 Mkazi wa Kijiji hicho akimuuliza swali Mbunge wa Jimbo hilo
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiagana na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Mlola wilayani Lushoto,Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Elmerick Joseph mara baada ya kumalia mkutano wa hadhara katikati ni diwani wa kata hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akisalimiana na wakina mama wa Kijiji hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara

 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kushoto akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa CCM kata ya Mlola
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiwasilikiliza wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akiteta jambo na wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara

Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wa pili kutoka kushoto akimuelza jambo diwani wa kata ya Mlola (CCM) mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Kijiji cha Lwandai Kaya hiyo(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

JK AONGOZA MAMIA MAZIKO YA ALIYEKUWA MPIGA PICHA WA MAGAZETI YA SERIKALI ATHUMAN HAMISI MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Athumani Hamisi wakati wa maziko yake yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.Athumani Hamis amefariki hivi karibuni katika hospital ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuugua ghafa nyumbani kwake Sinza Madukani.
 Dua ya kumuombea marehemu ikifanyika mara baada ya maziko 
Sehemu ya umati wa watu wakishiriki maziko ya Marehemu Athumani Hamisi jioni ya leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar
 Jeneza lenye Mwili wa  Marehemu Athumani Hamisi Msengi likiwa mbele ya Waombolezaji kabla ya kuelekeo mazikoni Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.Jim James Yonas akitoa salamu za pole za Kampuni ya TSN pamoja na za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaamu Mh Paul Makonda (pichani kulia) kwa wafiwa na waombolezaji ,baada ya mwili Marehemu  Athumani Hamisi kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadj Mussa Salum akitoa salamu za pole kwa Wafiwa na waombolezaji wote waliofika kwenye msiba huo,jioni ya leo nyumbani kwa marehemu Sinza Madukani.
Kaka mkubwa wa marehemu Dkt Ibrahim Msengi akizungumza jambo mara baada ya mwili wa mdogo wake Athumani Hamisi Msengi kumaliza kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.
Jeneza lenye Mwili wa  Marehemu Athumani Hamisi Msengi ukipandishwa kwenye gari maalumu tayari kuelekea mazikoni Makaburi ya Kisutu mara baada ya kuswaliwa swala ya Ijumaa Nyumbani kwake Sinza Madukani leo jijini Dar Es Salaam.

Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde

$
0
0
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tigo, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde. Amezingirwa na baadhi ya washindi 153 wa promosheni hiyo waliojinyakulia vitita vya shilingi milioni 15, TZS milioni 10, TZS milioni 5, TZS milioni moja na TZS 500,000 kila mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 5 milioni kwa Mariam Maligisa, mkulima kutoka Nagangu mkoani Lindi, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 10 milioni kwa Kulthum Salim , mkulima kutoka Tunduru mkoani Ruvuma, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 15 milioni kwa Lugano Thomas , ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde aliyekuwa mshindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (aliyeketi wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi washindi wa promosheni ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo jumla ya wateja 153 walijishindia zawadi tofauti za  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni, TZS tano milioni na zawadi za kila siku za TZS milioni moja na TZS  500,000 kila mmoja.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TFS

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia) akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana.


...................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameugiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kukabidhi eneo la Kilomita za mraba 25,000 kutoka kwenye Hifadhi ya Msitu wa Morogoro unaosimamiwa na wakala huyo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).


Ametoa agizo hilo jana akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Morogoro ambapo alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi kuzikutanisha taasisi hizo ndani ya siku saba zijazo ili kukamilisha mchakato wa kumega eneo hilo na kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili taratibu za ujenzi ziweze kuanza.


Aidha, ameuagiza uongozi huo wa TFS kuweka vigingi vya mpaka katika eneo la hifadhi hiyo ya msitu ndani ya siku 30 zijazo huku akitoa muda huo huo kwa wananchi wote waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.


Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Prof. Dos Santos Silayo kukabidhi mbao zaidi ya 400 zilizokamatwa hivi karibuni mkoani Morogoro baada kuvunwa kinyume cha Sheria kwa uongozi wa Mkoa huo ili zisaidie kutengeneza madawati ya shule za msingi.


Pamoja na mbao hizo amemuagiza pia mtendaji huyo kukabidhi kwa uongozi wa mkoa huo magunia 350 ya mkaa yaliyokamatwa katika kituo cha Tazara yakiwa yanasafirishwa kinyume cha Sheria ili yasambazwe kwenye shule za Sekondari mkoani humo.


Dk. Kigwangalla alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Steven Kebwe, ambapo alimuomba kusimamia zoezi hilo la ugawaji kikamilifu ili walengwa waweze kufikiwa.



Katika ziara hiyo ametembelea pia bonde la Kilombero ambalo ni chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stieglers Gorge ambapo Serikali ya awamu ya tano itajenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa megawatts 2100.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia) akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana.
Dk. Kigwangalla akizungumza na watumishi wa TAWA wakati wa ziara hiyo.

ZIARA YA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA UBUNGO LUCAS MGONJA, JANA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya UbungoLucas Mgonja akizungumza na viongozi wa Wilaya hiyo katika Mkutano wa ndani uliofanyika jana katika Kata ya Msigani wilayani humo, ikiwa ni sehemmu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Salum Kally
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akishauriana jambo na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Salum Kally wakati wa kikao hicho
 Katibu wa UVCCM Kata ya Msigani Reinhard Chicano akisalimia baada ya kutambulishwa
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msigani Godlove Mondo akifungua kikao hicho
 Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo Mbarouk Masoud akifanya utambulisho wa viongozi waliofuatana na Mwenyekiti Mgonja kwenye kikao hicho
 Wajumbe kwenye kikao hicho wakishangilia jambo kuliunga mkono.
 Diwani wa CCM Kata ya Manzese Manumbu Magafu akisalimia katika kikao hicho
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo Pili Mustafa, akiimba wimbo wa hamasa alipopewa nafasi ya kusalimia
 Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimbo huo 
 Mbunge wa Mbinga Vijijini ambaye pia ni Mweneyekiti wa Mtaa wa Msingwa Kata ya Msigani Martin Msuha akisalimia
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na kamati ya Siasa mkoa wa Dar es Salaam Issa Mtemvu akisalimia kwenye kikao hicho  katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Salum Kally akiimbisha wimbo wa hamasa kwenye kikao hicho
 Viongozi wa meza kuu wakishiriki kuimba wimbo huo wa hamasa. 
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo akihutubia kikao hicho kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mgonja kuhutubia.Mgonja akihutubia.
 Mgonja akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa Chadema Gatto John, ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
 Mgonja akimpa kadi ya CCM
 Gatto akionyesha kadi ya CCM baada ya kukabiodhiwa
 Mgonja akimpokea kadi kutoka kwa aliyekuwa katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya msigani Kerned Odera baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
Mgonja akimpokea kadi kutoka kwa aliyekuwa katibu Mwekiti wa Chadema Tawi la Msigani Benedict Mumbi baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
 Waliokuwa wanachama wa Chadema wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za CCM
 Kinamama wajasiriamali wakishangilia wakati wakipeleka zawadi na kujinadi kwa viongozi wa meza kuu kuhusu shughuli zao 
 Kiongozi wa Kinamama hao akitoa maelezo
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akikabidhiwa zawadi kutoka kwa Kinamama hao wajasiriamali
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akitazama bidhaa za kinamama wajasiriamali waliozkuwa wakionyesha nje ya ukumbi
 Mgonja akinunua bidhaa kwa kinamama hao wajasiriamali
 Mwenyekiti wa CCM Lucas Mgonja akiwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mbezi Othman Shaibu baada ya kuwasili katika kata hiyo kuendelea na ziara yake. 
 Wajumbe wakiwa wamesheheni ukumbini kwenye mkutano huo wa Kata ya Mbezi
 Wakiomba dua kabla ya kikao kuanza
 Baadhi ya vijana wa CCM waliofika kwenye kikao hicho Mbezi
 Baadhi ya vijana waliofika kwenye kikao hicho wakiwa nje ya ukumbi kwa kuwa siyo wajumbe.
 Vijana wakipata chakula nje ya ukumbi
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kally akimkaribisha Mwenyekiti kuzungumza kwenye kikao hicho cha kata ya Mbezi 
 Baadhi ya wajumbe ukumbini 
Mwenyekiyi wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akihutubia wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika Kata ya Mbezi Wilayani humo jana.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018

Na Mathias Canal, Mbeya


Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa amemuagiza Mrajis Mkuu wa Maendeleo ya Ushirika nchini kuanza uchunguzi mara moja kwenye SACCOS ya Wakulima wa mpunga Madibila iliyoko Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Watendaji waliohusika na upotevu wa fedha pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.


Mhe Mwanjelwa alitoa agizo hilo Jana Disemba 4, 2018 wakati akipokea taarifa ya kilimo ya Wilaya ya Mbarali akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilayani humo.


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune alimueleza Mhe Mwanjelwa kuwa katika SACCOS ya Madibila kumekuwa na hasara kubwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika.


Hivyo alimuomba Naibu Waziri kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka viongozi wote waliosababisha hasara kwenye vyama hivyo vya ushirika baada ya uchunguzi kufanyika katika kipindi cha siku 14.


Aliongeza kuwa taarifa ya ukaguzi iliwasilishwa kwa Mrajis wa vyama vya ushirika kwa barua Kumb Na. MDC/C.20/10/89 tarehe 23/01/2017 lakini mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kinidhamu jambo ambalo linafifihisha shughuli za wananchi kujipatia maendeleo endelevu.


Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa ametoa wiki mbili (siku 14) kwa Mrajis kufika katika SACCOS hiyo ya Madibira na kutoa majibu haraka ya matokeo ya uchunguzi huo katika kipindi tajwa.


Mhe Mwanjelwa alisema kuwa sekta ya ushirika ni moja kati ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Vikundi, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kukuza pato la mwananchi na kupunguza umasikini hivyo ni lazima kuwa na majibu ya haraka pindi kunapobainika uhujumu wa vyama hivyo.


Alisema kuwa Viongozi wa Wilaya zote nchini wana jukumu muhimu la kuhamasisha na kuhiza wanachama kuongeza thamani ya mitaji yao ili kuviwezesha vyama kukuza mitaji ya ndani badala ya kuwa tegemezi kwenye Taasisi zingine za kifedha.


Aidha, Kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ya Mazao ghalani ili mkulima apate bei stahiki ya Mazao yake.


MWISHO

MAKONDA AENDELEZA FARAJA KWA WAANDISHI WA HABARI.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda , Leo amehaidi Kuijengea Nyumba ya Vyumba Vinnie (4) Familia ya Mwandishi (mpiga picha) wa Magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News Marehemu Athumani Hamis ambae amezikwa Leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam. 

Ahadi hiyo Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Dkt. Yonaz kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ambae aliombwa kuisadia familia ya Marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma uku wakiwa wanaishia kwenye Nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya Miaka 10 na hivyo kushindwa kufanya kazi. 

 Dkt. Yonaz amesema Mhe Makonda kwa kutambua mchango wa tasnia ya Habari hususani waandishi wa Habari amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi Marehemu Athumani ambae katika Uhai wake alikuwa Mpiga Picha Mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini. 

 Hatua hii imepokelewa kwa Furaha na baadhi ya waandishi wa Habari ambao wamesema Kitendo cha Makonda kukubali Kuijengea Nyumba Familia ya Marehemu Athumani mbali na kuwafuta Machozi ya Huzuni, Bali kimekuwa ni fundisho Tosha kwa Baadhi ya waandishi ambao walikuwa Wakimchukia Mhe Paul Makonda pasipo sababu za Msingi, na kukifananisha Kitendo hiki na Ukamilifu wa Maandiko katika vitababu vitakatifu yanayotutaka TUWAPENDE ADUI ZETU.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda (katikati) akizungumza na Mhariri Mtendaji wa  Magazeti ya Serikali TSN Dkt. Jimmy Yonaz  kulia na Kaka wa Marehemu Athuman Hamis Dkt. Ibrahim Msengi nyumbani kwake Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam.

BALOZI MTEULE WA UFARANSA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier ambaye alifika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje leo kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier baada ya Mhe. Balozi kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao pamoja na mambo mengine walizungumzia masuala ya uwekezaji ambapo Ufaransa inahitaji kuongeza uwekezaji wa makampuni yake hapa nchini ili kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Ujumbe wa Wizara ulioshiriki mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga; Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. Jacob Msekwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi Mteule wa Ufaransa wakiendelea na mazungumzo yao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier mara baada ya wawili hao kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Naibu Balozi wa Ufaransa, Bw. Alexandre Peaudeau.

KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA

$
0
0
Diwani  wa kata ya  Mwangata Anjelus Mbogo kushoto   akizungumza na  wanahabari  leo  baada ya  kujiuzulu kwake wengine ni katibu kata  ya  Mwangata Tumaini Gwivaha  na aliyekuwa katibu wa mkoa wa Iringa Chadema Oscar Ndale  ambao  wote  wamejiuzulu  leo
Katibu wa  Chadema  mkoa wa Iringa Oscar Ndale  katikati  akiwa na diwani wa Mwangata  Anjelus Mbogo na katibu kata  ya  Mwangata  Tumaini Gwivaha  baada ya  kujiuzulu  leo

Na MatukiodaimaBlog.

IDADI ya  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia na  maendeleo  (chadema)  jimbo la  Iringa  mjini  kujiuzulu  imezidi  kuongezeka   na  kufikia madiwani  saba   sasa  baada ya watatu kujiuzulu ndani ya  wiki  hii pamoja  na katibu  wa chadema mkoa  wa Iringa  Oscar Ndale  .

wakati diwani wa Kwakilosa na Ruaha  walijiuzulu kwa pamoja    juzi diwani  wa Mwangata  Anjelus Mbogo alijiuzulu leo   pamoja na  katibu  wa mkoa  wa  chama  hicho  na katibu  kata  wa  Chadema Mwangata  Tumaini Gwivaha .


wakitangaza  azma  ya  kujiuzulu  kwao nafasi hiyo   mbele ya waandishi  wa  habari  Mbogo  na  Ndale  walisema   kuwa  kujiuzulu  kwao kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo  kwenye kata  yake pamoja na mabavu  ya  viongozi w juu wa Chadema .

kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.


"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "

Alisema  kuwa  mbunge Msigwa  amekuwa  akimfanyia  diwani  mwenzao Joseph Lyata figisu  figisu toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

Diwani  Mbogo alisema  kwa  sasa atabaki  mwanasiasa   huru  na  iwapo  mbunge  Msigwa na mstahiki meya  Alex Kimbe wataondoka  hata  leo  chadema basi atarejea  Chadema  ila  kama   wataendelea  kubaki hatarudi  kamwe .

Kwa  upande  wake aliyekuwa  katibu  wa Chadema  mkoa ,Ndale  alisema  kuwa kuyumba  kwa chadema  Iringa mjini  kumesababishwa na mbunge   kutokuwa na ushirikiano mzuri  na  wenzake na mara  kadhaa  wamekuwa  wakimuonya ila  bado  anaendelea  na kuwa  Mbowe pia  amesababisha  kujiuzulu kwake  nafasi hiyo  na  kwa  sasa  atajiunga na  CCM .

Ndale  alisema aliomba kujiunga na  CCM na amekubaliwa na  hivyo ataendelea na  Siasa  kupitia CCM huku akisema uhai  wa Chadema  Iringa  mjini  umefika  mwisho .

Kwa  upande  wake Joseph Lyata  aliyekuwa  diwani kata ya  Kwakilosa  alisema siasa ndani ya  Chadema kwake  imemshinda hivyo ameamua  kuondoka  ndani ya  chama  hicho na  kuwa  mwanasiasa  huru .

Msimamizi  wa  uchaguzi jimbo la Iringa  mjini  Omary  Mkangama ambae  ni kaimu  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa amethibitisha  kupokea  barua  za madiwani watatu ndani ya  wiki  hii  kutoka  Chadema  ambao  wamejiuzulu nafasi zao Tandesy  Sanga wa kata ya  Ruaha , Joseph  Lyata kata ya Kwakilosa na Anjelus Mbogo  wa kata ya Mwangata  .

"  Kwa  mujibu wa  sheria  nitamuandikia barua mstahiki  meya  ili  yeye  aweze   kumwandikia waziri mwenye   dhamana  ambae ataijulisha   tume  wa Taifa ya  uchaguzi  ili  taratibu  nyingine  zifanyike "

Alisema  jimbo la  Iringa  linazo kata 18   kati  ya  madiwani hao CCM  ina madiwani  watano  pamoja na yule wa  Kihesa  aliyepita  bila kupingwa  itakuwa na madiwani  sita   huku  Chadema   itabaki na madiwani  9.

WIZARA YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA FAMILIA YA NGUZA VIKING (BABU SEYA) KURUDI KWENYE ANGA YA MUZIKI WAO

$
0
0

 Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Studio ya Wanene na Wasanii Nguza Viking , Papii Nguza (Papii Kocha ) kwa ajili ya kurekodi mziki wa Live katika Studio Wanene.
 Msanii wa Muziki wa Dansi Nguza Viking akizungumza na Waandishi wa  Habari mara Baada ya kufanya Mazungumzo na Uongozi wa Wanene Studio na Naibu Waziri.
 Mwanamuziki wa Muziki wa Dansi Papii Kocha akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea Studio za Wanene na kufanya Mazungumzo  na mkurugenzi wa Studio na Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Juliana Shonza
  Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akiteta na Mkurugenzi wa Wanene  Studio wakati wa mazungumzo  ya Kufanikisha wasanii hao kurekodi katiKa Studio hizo
Wasanii   wa  muziki wa Muziki wa Dansi Papii Kocha na Gunza Viking wakiwa wanatoka katika Studio za Wanene Mikocheni Dar es Salaam
--

ZIARA YA MSEMAJI WA JESHI LA POLISI BBC LEO JIJINI DAR

$
0
0
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabasi Mwakalukwa akiagana na meneja wa ushirikiano wa BBC Media Action, Agnes Kayuni mara baada ya kumaliza mazungumzo na watendaji wa BBC Media Action leo alipo watembelea ofisini kwao kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.
Studio Meneja wa shirika la utangazaji la BBC, Peter Mfalila akimuonesha Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabasi Mwakalukwa namna studio ya BBC Dar es salaam inavyofanya kazi. Picha na Jeshi la Polisi

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA SOKO LA KONDE-PEMBA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongezana na viongozi wengine mara baada ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla fupi ya ufunguzi wa soko jipya la Konde lililopo Konde, Micheweni,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume Pemba tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakati alipowasili Konde tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamedmara baada ya kuwasili Konde tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na na Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na na Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. 

WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA KAHAWA

$
0
0

 *Asisitiza kahawa iuzwe kwa mfumo wa ushirika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la biashara.

Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.

“Limeni kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua uchumi wa Taifa”.

“Tumeamua kuweka mkazo kwenye mazao matano ya pamba, kahawa, chai, korosho na tumbaku kwa sababu yanaleta tija na kuliingizia Taifa fedha za kigeni,” alisema na kuongeza:

“Tumefanya tathmini na tumegundua udhaifu mkubwa mkubwa katika usimamizi wa mazao haya ndani ya Serikali kuanzia ngazi ya Halmashauri.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati alipotembelea Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma  kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa ufafanuzi wa miche ya Kahawa,  na mkulima wa zao hilo wakati akikagua kitalu cha miche ya kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma  kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi miche ya Kahawa, Mkulima wa zao hilo, Remigius Njovu,i nayotolewa bure na Kampuni ya Molam Tanzania Limited, kwa wakulima wa zao la Kahawa, baada ya kukagua kitalu cha miche ya kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma  kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati akikagua kitalu cha miche ya Kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma  kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC Wangabo aziagiza kamati za ulinzi na Usalama kusimamia usambazaji wa pembejeo.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wadau wa kilimo Mkoa wa Rukwa (hawapo kwenye picha) katika Kikao kilichowajumuisha Wataalamu wa kilimo ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Kamati za ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wao, Mawakala wa usambazaji wa mbolea wakubwa na wadogo pamoja na wakulima. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amezitaka kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa kushirikiana na za Wilaya kusimamia usambazaji wa mbolea ili kufikia malengo ya kuzalisha chakula kwa wingi katika mkoa baada ya kutokea upungufu wa mbolea za kupandia (DAP) na za kukuzia (UREA) katika Mkoa.

Ameagiza hayo katika kikao cha kutafuta suluhisho la upatikanaji wa mbolea Mkoani Rukwa baada ya taarifa za upatikanaji wa mbolea hizo kutoridhisha hasa katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo ambapo asilimia 80 ya wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanategemea kilimo kujipatia kipato cha kujiendesha Kimaisha.

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya kilimo ilichukua hatua za makusudi kubadili mfumo wa ruzuku uliokuwa ukiwafaidisha wakulima wachache kupitia vocha za pembejeo na hatimae kupitia mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) iliweka mfumo wa uuzaji na usambazaji wa mbolea kwa uagizaji wa pamoja na kutoa bei elekezi kwa kila Halmashauri.

Ameongeza kuwa hali ya upatikanaji wa mbolea Mkoani Rukwa si ya kurudhisha na kubainisha kuwa hadi kufikia tarehe 3/1/2018 Mkoa umepokea mbolea ya kupandia (DAP) tani 3,746.6 kati ya tani 47,869 upungufu ni tani 44,122.9 na mbolea ya kukuzia (UREA) tani 2,599.6 kati ya mahitaji ya tani 49,669 na kuwa na upungufu wa tani 47,069.4.

“Ndugu zangu hivi sasa tuko vitani, na adui yetu ni upatikanaji wa pembejeo, kwahiyo hapa Mkoa mzima tuungane tuwe kitu kimoja, tulidhibiti hili jambo, haya ni maagizo mbolea yoyote inayokuja hapa katika ngazi ya Mkoa, kamati ya ulinzi na usalama lazima isimamie, sio suala la Sekretariet hya Mkoa peke yake, lazima tujue kama mbolea hiyo imefika ama la,” RC Wangabo alisisitiza.

Aidha amewataka mawakala wa mbolea Mkoani humo kuhakikisha wanaagiza mbolea ya kutosha kutoka nje ya mkoa ili wasambazaji wadogowadogo waweze kuisambaza mbolea hiyo katika vijiji vya halmashauri zote nne za Mkoa wa Rukwa.

Akiwawakilisha mawakala wa usambazaji wa mbolea mkoani humo Mmiliki wa Kampuni ya usambazaji Ikuwo General Enterprises Sadrick Malila amesema kuwa upungufu mkubwa uliopo ni upatikanaji wa mbolea ya kukuzia (UREA) na sio mbolea ya kupandia (DAP) ambayo mpaka sasa ana tani 200 katika ghala lake peke yake, na kuiomba serikali kuongeza shilingi 1000 katika bei elekezi ili kufidia usafirishaji wa mbolea hizo.

Mmoja wa Wakulima waliohudhuria katika kikao hicho Godfrey John ameiomba serikali kwa kushirikiana na mawakala hao kuongeza kasi ya upatikanaji wa mbolea hiyo ili kunusuru maisha ya wanarukwa wanaotegemea kilimo kujikimu kimaisha.

Kwa msimu wa 2016/2017 Mkoa wa Rukwa ulilima Hekta zipatazo 556,975.9 na kuvuna tani 1,109,055.6 za mazao ya chakula kati ya hizo mahindi yalikuwa tani 710,602. Kwa msimu huu wa Kilimo wa 2017/18 Mkoa umelenga kulima jumla ya eneo la Hekta 554,310.6 na kuvuna tani 1,669,746.2 za mazao ya chakula

WAZIRI UMMY AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA KLABU YA AFRICAN SPORTS

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba 

Halfa ya makabidhiano ikiendelea 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed Kidiwa 



WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.

Aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.

“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema 

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na changamoto hiyo kwisha.

Alisema msaada uliotolewa na Waziri utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.

“Mh Waziri tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images