Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM WAIPONGEZA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga  na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa za Sugar Free zisizo na sukari wakati wa uzinduzi  wa bidhaa hizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

 Muonekano wa keki hiyo iliyotengenezwa kwa bidhaa hizo zisizo na sukari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza bidhaa hizo.
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale


WANANCHI jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wameipongeza  Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kwa kuwaletea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam walisema kampuni hiyo haina budi kupongezwa kwa kuzileta bidhaa hizo katika soko la Tanzania ili kukabiliana na changamoto ya matumizi kupitia vyakula.

"Hivi sasa kila pembe ya nchi yetu kumekuwa na changamoto ya ugonjwa wa kisukari ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari kupita kiasi kwa bidhaa hizi mpya zinazosambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD hakika itasaidia sana" alisema Frank Erasto mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.

Erasto alisema yeye ni mihongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa kisukari lakini tangu bidhaa hizo ziingie katika soko la Tanzania amekuwa akitumia bidhaa hizo ili asiongeze sukari mwilini mwake baada ya kupata matibabu.

Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina moaja la Reuben alisema familia yake imeanza kutumia bidhaa hizo ambazo hazina gharama kubwa.

"Familia yangu na marafiki zangu tumeanza kutumia bidhaa hizi za Sugar Free kusema kweli ni nzuri na zina radha kama ile zilizopo kwenye chakula halisi" alisema Reuben.

Mkazi wa Kariakoo Happyness Kimaro alisema kwake anaona bidhaa hizo ni mkombozi kwani ameanza kuzitumia baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari na hapendi kuongeza sukari mwilini mwake.

"Sisi wagonjwa wa kisukari tumekuwa na changamoto kubwa ya ulaji wa vyakula mara tunaambiwa tusile hiki na kile tule vyakula ambavyo havina sukari ambavyo havina ladha sasa kwa kuletewa bidhaa hizi tunasema ni nafuu kwetu" alisema Kimaro.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 

Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.

Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 

Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.


TANESCO YAFURAHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KULINDA VYANZO VYA MAJI YA KUFUA UMEME

$
0
0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
INAELEZWA kuwa umeme wa maji, (Hydro power) ndio umeme wenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, matumizi ya juu ya umeme nchini kwa sasa ni Megawati 1,060, kati ya hizo, TANESCO kwa kutumia mitambo yake, huzalisha Megawati zaidi ya 1,000, na kati ya hizo, Megawati 381 zinatokana na umeme unaozalishwa kutokana na maji, (Hydro powere) kutoka vituo vinne vya umeme wa maji vya Kidatu, Mtera, New Pangani Falls, Hale na Nyumba ya Mungu.
Hata hivyo katika siku za karibuni shughuli za kibinadamu zimekuwa zikiongezeka kwenye vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye vituo vya kufua umeme, na hivyo kutishia shuhghuli za uzalishaji umeme kwenye vituo hivyo.
Mhandisi Ikwasa alitoa mfano Mto Pangani ambapo yapo maeno ambayo shughuli za kilimo zinaendelea karibu na mto, na madhara yatokanayo na shughuli hizo hupelekea kingo za mto kuwa dhaifu na wakati wa mvua maji yanachukua udongo na kuingiza kwenye mto na hivyo kina cha mto kinakuwa kifupi.
“Sasa kipindi ambacho mvua zinanyesha unatarajia maji mengi yatiririke kwenye mto lakini kwa sababu kina kimepungua mto hauwezi kubeba yale maji na badala yake maji yanasambaa na kusababisha mafuriko na mbaya zaidi hayafiki kwenye mabwawa kwa kiwango kinachohitajika.” Alisema Mhandisi Ikwasa.
Alisema TANESCO kama wadau wakubwa wa maji wamekuwa wakishirikiana na mamlaka zinazosimamia mabonde, ili kuelimisha watumiaji wengine wa  maji.“Tunataka kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji, tunatambua wananchi wanahitaji maji kwa kilimo na sisi tunayahitaji kwa uzalishaji umeme kwa hivyo yakitumika vizuri yanaweza kufanya kazi zote.” Alisema.
Mhandisi Ikwasa aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.“Makamu wa Rais aliunda kikosi kazi cha kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.” Alisema.
Ili kuhakikisha wananchi wanajenga dhana ya umiliki wa miundombinu ya TANESCO, Shirika limekuwa likishirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia kutoa huduma za afya, elimu ya awali na usafiri katika maeneo yanayozunguka vituo vya kuzalisha umeme.

“Tunataka wananchi wafahamu kuwa pamoja na kwamba kazi yetu ni kuzalisha umeme, lakini tunataka tuwe sehemu ya maisha yao, kwa kusaidia mambo ya kijamii kama vile kutoa elimu bure ya awali, zahanati, na usafiri wa basi unaosaidia wananchi kusafiri kuelekea kwenye shughuli zao, tunadhani kwa ushirikiano huu, wananchi watakuwa wakwanza kulinda miundombinu yetu na pia kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwenye vyanzo vya maji.” Alisema Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
Ili kuhakikisha ujumbe huo pia unawafikia wananchi wote kupitia vyombo vya habari, wahariri wa vyombo vya habari walipata fursa ya kutembelea vituo vya kufua umeme wa maji vya Hale, New Pangani na Nyumba ya Mungu, vilivyoko mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, kituo cha Mtera kilichoko mkoani Iringa na Kidatu mkoani Morogoro ili hatimaye watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya vyanzo vya mito ambayo maji yake ndio huelekea kwenye vituo vya kufua umeme.
 Meneja wa kituo cha kufua umeme wa maji cha Kidatu, Mhandisi Anthony Mbushi, (kushoto), akizungumza kuhusu jinsi mageti ya kuruhusu maji kwenye mabwawa kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yanavyofanya kazi. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme. Mhandsisi Abdallah Ikwasa.
 Wananchi wa Kidatu, wakisubiri usafiri wa basi la Shirika la Umeme TANESCO, kuwapeleka kwenye mnada ili kuuza mazao yao. Usafiri huo hutolewa bure na Shirika katika mpango wake wa Corporate Social Responsibility (CSR) ili kujenga uhusiano mwema.
 Moja ya mashine za kufua umeme wa maji, (turbine), kituo cha Hale.
 Wasimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtera.
 Bwawa la New Pangani Water Falls.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza jambo.
Mhandisi Mahenda S.Mahenda, Meneja vituo vya kufua umeme vya Pangani Hydro Systems, akifafanua jambo.

TAARIFA KWA UMMA

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAVIPIGA JEKI VITUO VYA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
 
 Mkurugenzi wa Msama Promotions,Bwa Alex Msama akishiriki kushusha vifurushi vya mchele,ambavyo baadae alivitoa kwa vituo vya watoto waishia katika mazingira Magumu,makabidhiano ya msaada huo yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi zake Kinondoni jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Msama Promotions,Bwa.Alex Msama akikabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta. 
Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaada wa vyakula mbalimbali  kwa baadhi ya vituo vya watoto waishio katika mazingira magumu,vilivyopo jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari wakati wa makabidhiano ya msaada huo mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama alisema kuwa kama ilivyo ada ya kampuni yake,kila ifikapo mwishoni mwa mwaka hutoa sadaka kwa vituo mbalimbali vya watoto waishio katika mazingira Magumu.

"Nimeamua kufanya hivi pia kuwakumbuka wototo wetu wanaoishi katika mazingira magumu,na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao,kwa hiyo nimetoa unga,mchele,mafuta,viywaji mbalimbali na vingine ili watoto hao nao kwa pamoja wafurahie msimu wa siku kuu",alisema Msama.

Nae mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta ameishukuru Kampuni ya Msama Promotions na Uongozi wake kwa kuwakumbuka katika msimu huu,wamemshukuru na kumuombea Heri zaidi afanikiwe katika mambo yake ili azidi kuwakumbuka na kuwasaidia wasiojiweza katika maeneo mbalimbali.

 Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akimkabidhi msaada wa vyakula mmoja wa Viongozi wa kituo hicho cha watoto waishia katika mazingira Magumu cha Maunga,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu.
Mwakilishi wa kituo cha TOVICHIDO,Bi Honoratha Michael akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama ,hafla hiyo fupi ilifanyika ofisini kwake Kinondoni Jiini Dar

WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kulia akitazama mifugo ya ng'ombe aina ya Borani waliyopo kwenye ranchi ya mzeri wilayani Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe kushoto akimueleza jambo WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kulia ambaye alifanya ziara ya kikazi wilayani humo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati alipoitembelea ranchi ya mzeri wilayani humo 


NA MWANDISHI MAALUM, HANDENI


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa kukamata mifugo kiholela na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria huku akisifu utendaji kazi ya wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa sheria za mifugo nchini.

Mpina ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Handeni ambapo alitumia fursa hiyo kupiga marufuku ukamataji mifugo kiholela huku akimtaja Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Gondwe kama kielelezo cha kuwa kiongozi wa kwanza kitaifa anayezifahamu vizuri na kuzisimamia kikamilifu sheria za mifugo na kuleta tija katika ukuaji wa sekta hiyo ikiwemo kuanzisha kijiji cha wafugaji,kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na utoaji huduma bora za mifugo wakati wote.

Akizungumzia tatizo hilo la ukamataji holela wa mifugo nchini, Waziri Mpina amesema kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na Serikali kuamua kuagiza kutoka nje ya nchi basi ingezilazimu kutumia kiasi cha sh. Trilioni 17.8 huku kaya milioni 4.49 za kilimo nchini zinajishughulisha na ufugaji mifugo aina mbalimbali.

“Watendaji wa Serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki salama, tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria”alisema.

Amesema Sheria ya misitu na. 14 ya mwaka 2002 kifungu cha 26 kinazuia mifugo kuingia kwenye hifadhi za misitu ya kitaifa au iliyo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo pamoja na wafugaji kuvunja sheria hiyo bado wanahitaji kutendewa inavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuweka ulinganifu wa watanzania wote mbele ya sheria za nchi.

Waziri Mpina amebainisha kuwa kumekuwa na mazoea mbalimbali ya ukamataji holela wa mifugo yanayoendelea nchini ambayo yanatekelezwa bila kuzingatia sheria ya ustawi wa Wanyama (Animal welfare Act No.19 of 2008) na Kanuni zake za mwaka 2010 kifungu cha 7 na 8 na Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Na 17 ya mwaka 2003 (Animal Disease Act No.17 of 2003) hivyo mifugo imekuwa ikishikiliwa kama kidhibiti kwa muda mrefu na mingine kufa kutokana na magonjwa na ukosefu huduma ikiwemo matibabu,chanjo na kuogeshwa ili kuepuka magonjwa ndorobo na kupe.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema wao kama Serikali ya wilaya katika sheria ndogo yao ikiwa kundi la mifugo litaingia kwenye maeneo yasiyoruhusiwa wameweka faini isiyozidi sh 300,000 kwa kundi la ng’ombe ambapo alisema pamoja na pongezi za Waziri Mpina bado wataendelea kubuni mbinu mbalimbali za kuboresha sekta ya ufugaji ikiwemo uimarishaji wa majosho, malisho na uzuiaji uuzaji nyama kiholela barabarani.

WANANCHI WAITAKA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA UMEME KWENYE VITUO VYA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA- MTWARA

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa mkoani Mtwara ambapo katika Wilaya ya Mtwara Idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza kushiriki zoezi hilo huku baadhi wakilalamikia kukaa muda mrefu kwenye vituo vya Usajili na baadhi ya mashine kutokufanya kazi.

Bwana Athumani Salum mkazi wa Kata ya Magomeni amesema “zoezi kama zoezi ni zuri ila changamoto kubwa ni kukatika kwa umeme na hivyo kusababisha wananchi tusubiri muda mrefu kiasi cha kukatisha tamaa. Kwakuwa hili ni zoezi la kiserikali kwanini Serikali isisaidie umeme kutokatwa kwenye vituo? ”

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi Rose Mdami ambaye alikuwepo kituoni hapo ameeleza changamoto ya umeme ni kubwa katika vituo vingi vya usajili hata hivyo kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya wameshachukua hatua za kutafuta magenereta ili kazi ziendelee kama kawaida.

“ si kweli kwamba mashine zote hazifanyi kazi katika mashine tulizonazo zipo baadhi ambazo zinatunza umeme muda mrefu na kwahizi ambazo hazifanyi kazi kwa kukosa umeme tunaendelea kuharakisha kupata magenereta ili kuamsha mashine ambazo zimeshindwa kufanya kazi ili wananchi wasisubiri muda mrefu” alisisitiza

Katika kituo cha Magomeni kilichopo shule ya Msingi Lilungu wananchi pia wamekutwa wakihangaika kutafuta fomu zao za usajili walizosajiliwa mwaka 2014 ambapo zoezi hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza kwa hatua ya kujaza fomu tu bila kupigwa picha.

Akifafanua kuhusu wananchi hao Bi. Rose amesema kwa wale wananchi wanaofika kwenye vituo vya Usajili na ambao walisajiliwa mwaka 2014 na kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa, pindi wanapofika kwenye vituo vya Usajili wanachukuliwa alama za kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki na kisha kuruhusiwa kuondoka kwakuwa taarifa zao msingi tayari zilishaingizwa kwenye mfumo tofauti na wale ambao ndio kwanza wanaanza Usajili.

Mkoa wa Mtwara unakusudiwa kusajili wananchi zaidi ya 800,000 kwa Wilaya za Mtwara, Tandahimba, Nanyumbu, Masasi na Newala. Usajili ambao unakusudiwa kumalizika mapema mwezi Machi, 2018 na kuwezesha wananchi katika mkoa huo kuanza kutumia Vitambulisho vitakavyozalishwa katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali.
Hawa ni baadhi ya wananchi wa Mbaya Mashariki wakisubiri kujaziwa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa ili wakapigwe picha, kuchukuliwa alama za kibaiolojia na saini ya kielektroniki wakati zoezi la Usajili likiendelea kwenye Kata yao. Wakitoa huduma hiyo ni Bi. Moza Mohamedi Lukwekwe (kulia) Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbaya na Bi. Asia Abdallah Nachuma (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtaa wa Mbaya. Huduma hiyo ya kuwajazia wananchi fomu za maombi ya Vitambulisho imekuwa ikitolewa kwa wananchi wote wanaofika kwenye vituo kusajiliwa na hawajui kusoma na kuandika ili kurahisha zoezi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Chiputaputa Bw. Juma Hamisi Chambeya akiwagongea muhuri wakazi wa eneo lake kwenye fomu za maombi ya Vitambulisho kuthibitisha makazi ya wananchi hao wakati wa zoezi la kuwasajili Vitambulisho vya Taifa likiendelea. Kabla ya wananchi kugongewa muhuri wa Serikali ya Mtaa wananchi kwanza wanatakiwa kujaza fomu ya maombi yenye vipengele 72 na kutoa nakala ya viambatisho vyao msingi vinavyowatambulisha kabla fomu hiyo haijapitiwa kugongwa muhuri wa Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi.
Sharifa Said (kushoto), Zubeda Abdallah (katikati) na Rahma Ally (kulia) wakijaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa katika kituo cha Usajili kilichopo Shule ya Msingi Lilungu mkoani Mtwara, wakati zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye kulenga utoaji wa Vitambulisho vya Taifa likiendelea Wilaya ya Mtwara.
Bi. Asha Bakari (kushoto) na Bi. Asha Yasini (mwenye mtoto) wakazi wa Kata ya Mbaya Mashariki wakitafuta fomu zao walizojaza mwaka 2014 waliposhiriki zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa; ili wakakamilishe hatua ya mwisho ambayo ni kuchukuliwa alama za kibaiolojia, Picha na Saini ya Kielektroniki. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI WA AZAM TV

$
0
0
 Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa marehemu Idd Salum wakielekea makaburini wakati wa mazishi yake Desemba 26 2017. (Picha na Francis Dande)
 Meya wa zamani wa Kinondoni, Alhaji Salum Londa akiwa ni miongoni mwa waombolezaji.
 Wanahabari pamoja na ndugu wakielekea makaburini.
 Mwandishi wa habari wa Kituo cha Runinga cha ITV, Hemed Kivuyo akielekea makaburini
 Kuelekea makaburini.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Idd Salum wakati wakielekea makaburini.
Safari ya mwisho hapa duniani ya marehemu Idd Salum.
 Shughuli za mazishi zikiendelea.
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa makaburini.
 Waombolezaji.
 Mwili wa marehemu ukihifadhiwa kaburini.
 Taratibu za mazishi zikiendelea.
 Shughuli za mazishi zikiendelea
 Waombolezaji wakishiriki maziko ya Idd

ATAKAEFUNGA BARABARA NA KUCHOMA MATAIRI MKESHA WA MWAKA MPYA KUKIONA-RPC SHANNA

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna wa kwanza kutoka kushoto ,akizungumzia hali ya usalama wakati wa kuelekea sikukuu ya mwaka Mpya na kuelezea matukio ya kiuhalifu katika kipindi cha mwezi Jan -disemba mwaka huu,ukumbi wa mikutano ofisini kwake.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi mkoani Pwani ,pamoja na waandishi wa habari mkoani hapo wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna (hayupo pichani)wakati akizungumzia hali ya usalama wakati wa kuelekea sikukuu ya mwaka Mpya na kuelezea matukio ya kiuhalifu katika kipindi cha mwezi Januari na Disemba mwaka huu.


Na Mwamvua Mwinyi,Pwani.

KAMANDA wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara kuacha kufanya kitendo hicho .

Amesema atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoendelea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu ya mwisho wa mwaka ,kamanda Shanna alisema wanazidi kuimarisha doria katika pande zote za mkoa huo.

Alisema kipindi cha sikukuu ya x-mas hali ilikuwa shwarii hivyo wanaendelea na misako ya miguu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na doria hizo zitakuwa mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha watu waishi kwa amani .Akielezea kuhusiana na hali ya uhalifu katika kipindi cha Januari hadi disemba mwaka huu ndani ya mkoa huo ,kamanda Shanna alisema wamefanikiwa kupunguza idadi ya makosa kwa kiwango kikubwa.

Kamanda huyo alisema,matukio ya makosa ya uvunjaji yamepungua kutoka 771 kipindi kama hicho 2016 na kufikia 233 mwaka huu ikiwa ni tofauti ya matukio 538.Makosa mengine ni yale ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo yamepungua kutoka 31 mwaka jana hadi nane kwa mwaka 2017 tofauti makosa 23.

“Unyang’anyi wa kutumia nguvu yameripotiwa makosa 43 ,kipindi kilichopita ilikuwa 112 tofauti makosa 69,:;na mauaji makosa yaliyoripotiwa januari hadi disemba mwaka huu ni 34 ,mwaka uliopita ilikuwa 126 tofauti ni makosa 92.” alifafanua kamanda Shanna.Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo mara wanapotilia shaka kundi ama mtu ni mhalifu ,kwani kila mmoja ana wajibu wa kudhibiti vitendo vya uhalifu .

Kamanda Shanna ,alisema Pwani yenye utulivu,amani ,yenye kushikamana inawezekana endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.

MBUNGE WA KIBITI AWATAKA WANANCHI NA VIJANA KUJITUMA ILI KUJIPATIA KIPATO

$
0
0
MBUNGE wa jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani Ally Ung’ando wa katikati akiwa kwenye ziara yake ya jimbo ya siku 21 ambayo ameianza katika kata ya Rualuke
MBUNGE wa jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani Ally Ung’ando akizungumza na wakazi wa vijiji vilivyopo kata ya Rualuke wakati wa ziara yake ya jimbo ya siku 21 ambayo ameianza katika kata ya hiyo.Picha na Mwamvua Mwinyi

Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti

MBUNGE wa jimbo la Kibiti mkoani Pwani ,Ally Ung’ando amewataka wananchi jimboni hapo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kujishughulisha kimaendeleo ili kupiga hatua kiuchumi.

Amewaomba kushirikiana kwenye miradi ya maendeleo badala ya kuiachia serikali ama viongozi pekee suala ambalo linakwamisha jitihada mbalimbali zinazoendelezwa.Ung’ando aliyasema hayo kijiji cha Rungungu kata ya Rualuke katika ziara yake ya siku ya kwanza aliyoianza kwenye kata hiyo ambapo anatarajia kuendelea na ziara hiyo kwa siku 21 katika kata Tisa na vijiji vyote jimboni hapo.

Aliwataka vijana kuacha kujisahau kufanya kazi na kujiunga vikundi ili waweze kuwezeshwa kirahisi.“Vijana mjitume ,acheni kuishi kimazoea kwani maendeleo yoyote yanaletwa kwa kujituma ” alisema mbunge huyo.Hata hivyo ,alikemea tabia inayofanywa na baadhi ya wakulima wa korosho ambao wanauza korosho zao kwa mfumo usio rasmi wa kangomba .

Ung’ando alisema mfumo unaotambulika ni mfumo wa stakabadhi ghalani lakini wakulima wamekuwa wakiuza korosho zao kiholela .“Niwaombe muache kuuza korosho zenu kwa madalali ,hawawasaidiii,mtakuja kupata hasara na mkumbuke serikali haitohusika na mtu anauza korosho zake kiholela,msije kuipa lawama serikali wakati wenyewe mnataka njia nyepesi zinazowakandamiza ” alisema.

Pamoja na hayo ,aliwasihi wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule kupata haki ya elimu .Ung’ando alisema serikali chini ya Rais John Magufuli inatoa elimu bure kwa wanafunzi wa msingi hadi kidato cha nne lakini wazazi wamekuwa wakiwanyima fursa hiyo watoto wao.Katika ziara hiyo pia anatoa mifuko ya saruji 100 kwa kila kata,ambayo itakayosaidia kusukuma maendeleo ya kata hizo.

Ung’ando alianza ziara yake ya jimbo desemba 26 kwa kuzungumza na kusikiliza kero kwa wapiga kura wake katika vijiji vya Rungungu,Kilola Tambwe na Nyamatanga kata ya Rualuke,Ziara itaendelea desemba 28 kupisha ziara ya naibu waziri wa Nishati Mh,Subira Mgalu ambae yupo jimbo la Kibiti kwa ajili ya kuangalia changamoto ya nishati ya umeme .

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu Dar es Salaam akiangalia vitalu vya miche ya miti wakati alipowatembelea wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam wakioneshwa ramani ya Msitu wa Hifadhi Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo ( wa tatu kushoto) kuhusiana na“eneo la msitu huo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kisarawe, Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiwemo watumishi wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea eneo kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara jana ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto) akioneshwa eneo la msitu Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.

Picha na Lusungu Helela-MNRT



……………………

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.

Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Misitu Kisarawe, Mathew Mwanuo alisema wilaya hiyo ina misitu minne ya hifadhi ya serikali Kuu ambayo ni Ruvu Kusini, Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi.Alisema msitu wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na watu kutoka maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam.

“Msitu huu ulikuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014. Hata hivyo wavamizi hao waliendelea kuvamia kwa nyakati tofauti hadi mwaka huu,” alisema.

Alisema walianza kuwaondoa mwishoni mwa Agosti mwaka huu, Kamati ya Ulinzi na Usalam ya wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na maofis wa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania walianza kutembelea eneo la msitu kuangalia uvamizi na uharibifu uliofanyika katika Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi ikiwa ni pamoja na kuona ukubwa wa uharibifu na namna ya kutekeleza zoezi.

NI USIKU WA JUMA NA MKEWE FLORA BAADA YA KUFUNGA NDOA

$
0
0
 Bwana harusi, Juma katika pozi na mkwe Frola baada ya kufunga pingu za maisha na kufatiwa na tafrija katika ukumbi wa Makonde Kuringe Hall,  Dar es Salaam  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Bwana harusi Juma (kulia) akiwa katika pozi na mpambe wake Jacob
Biharusi Flora (kushoto) akipozi na mpambe wake Mariam kabla ya kuingia ukumbini

Bwana haruzi Juma katika pozi akifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya kupongezwa na mkewake Flora katika Ukumbi wa Makonde Kuringe Hall,  Dar es Salaam 
Bi harusi Mtarajiwa Flora akipambwa na mpambaji maarufu Sanura Beauty Artist
Mpambe wa Bi harusi Mtarajiwa Mariam akipambwa na mpambaji maarufu Sanura Beauty Artist




Bi harusi katika pozi

Bi harusi akiwa na mpambe wake katika pozi

Mnaniona katika pozi



Bi harusi Flora akilidaka ua baada ya kulirush juu
Bi harusi katika pozi kabla ya kuingia ukumbini




Mc na mtaalamu wa mapambo na chalula akiweka mambo sawa kabla ya kuingia maharusi na wageni waalikwa


Asante mume kunipokea UA pokea na wewe
Mama wa biharusi mtarajiwa (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya wana familia kabla ya kuingia ukumbini
Wazazi wa Bwana harusi wakiingia ndani ya ukumbi kwa madaha wakiiongoza familia yao

Wazazi wa Bwana harusi wakiipokea familia ya Bi harusi wakati walipokuwa wakiingi ndani ya ukumbi wa Makonde Kuringe Hall,  Dar es Salaam 
Familia ya Biharusi ikiingia ukumbini
Bwana na Bi harusi wakiingi ndani ya ukumbi

Bwana na Bi harusi wakiingi ndani ya ukumbi wakiwa na nyuso za  furaha mara baada ya kufunga ndoa
Mwenyekiti wa nguvu wa Shughuli hiyo ya hafla fupi ya kuwapongeza maharusi, Monica Hillary Doe akizungumza jambo  kwa waalikwa

Bwana harusi Juma na Mkewe Flora wakinyweshana Shampeni
Bwana harusi na Mkewe katikati wakigonganisha glas na wapambe
Bwana harusi na mkewe wakikata keki
Bwana harusi Juma akimlisha mkewake Flora kipande cha keki
Bi harusi Flora akiwakabidhi keki wazazi wa Bwana harusi
Bwana harusi Juma akiwakabidhi keki wazazi wa Bi harusi



Mama wa bwana harusi katika picha ya pamoja na marafiki zake


Wazzi wa Bwana harusi
Wazazi wa Biharusi






MAKATIBU WAKUU WAJADILI UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani) kujadili Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, hivi karibuni mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, wakijadili utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, hivi karibuni mjini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, Mhandisi Leonard Masanja, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi huo, wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani), kilichofanyika hivi karibuni mjini Dodoma
Ramani ya Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge, utakavyoonekana baada ya kukamilika.
Wajumbe mbalimbali wakichangia hoja katika kikao cha Makatibu Wakuu, kilichojadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.



Na Veronica Simba 

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, hivi karibuni walifanya kikao kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.

Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Aidha, kikao hicho pia kilijadili majukumu ya kila Wizara husika katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huo.Akifungua kikao hicho, Dkt. Mwinyimvua alieleza kuwa mahitaji ya umeme nchini kwa sasa ni makubwa kutokana na kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda hali inayosababisha huduma ya umeme wa uhakika kuhitajika zaidi ya muda mwingine wowote.

“Serikali ya Awamu ya Tano inaelekeza nchi kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, hatua za makusudi za kuongeza uzalishaji wa umeme kwa ajili ya viwanda zinahitajika.”

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, akielezea umuhimu wa Mradi huo kwa Taifa alisema kuwa umeme wa uhakika unahitajika ili pamoja na mambo mengine kukidhi mahitaji ya mkakati wa kusambaza umeme vijijini ambao unaendelea nchini kote.

Awali, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi husika katika kikao hicho, Msimamizi wake, Mhandisi Leonard Masanja alieleza kuwa, Desemba 19 mwaka huu, Wizara ya Nishati ilitangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi huo ambao utekelezaji wake unakadiriwa kuanza mwishoni mwa mwezi Februari 2018.

Alisema kuwa, mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Rais John Magufuli aliamua kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo ambao ulibuniwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere miaka ya 1970.

Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), iliundwa ili kufanya maandalizi ya Mradi na baadaye kusimamia ujenzi mara baada ya Mkandarasi kupatikana. “Timu hiyo iliungana na timu ya wataalam kutoka Ethiopia katika utekelezaji wa jukumu hilo.”

Makatibu Wakuu walioshiriki au kuwakilishwa katika kikao hicho ni kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wengine ni kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.

WAFANYAKAZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR WAFANYA USAFI.

$
0
0
Na Maryam Kidiko / Kijakazi Abdala- Maelezo .

MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Hassan Vuai Mbarouk amewapongeza Wafanyakazi wa Idara hiyo kwa kujitokeza kwa wingi katika wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya kazi zao ili kwenda sambamba na shamra shamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kufanya usafi huo Ofisini kwake Raha leo Mjini Unguja alisema katika kuazimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar Serikali imetowa agizo kwa Taasisi zote za Zanzibar kufanya usafi wa mazingira kwa maeneo yote yaliyowazunguuka hivyo hatua iliyooneshwa na wafanyakazi hao inahitaji kupongezwa kwa hali ya juu.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na agizo hilo la Serikali lakini vyema jamii inapaswa kutambua kuwa suala la usafi ni jambo la kawaida kufanya katika mazingira yaliyotuzunguuka wala halihitaji kusubiri siku za sherehe ndiyo tufanye usafi huo jambo hilo si zuri kwani husababisha maradhi mbali mbali ya miripuko.

“Usafi wa Mazingira ni muhimu katika maisha yetu kwani huepukana na maradhi mbali mbali katika jamii hivyo tuendeleze usafi ili muonekano wa mazingira yetu uwe mzuri.”Alisema Mkurugenzi huyo.Hata hivyo alisema kuwa agizo jengine lilotolewa ni pamoja na kupamba mapambo mbali mbali yenye muonekano wa Bendera ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuweza kuleta muonekano mzuri.

Nae Muangalizi wa Ofisi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Arafa Othman Hamad alisema suala la usafi ni suala la watu wote hivyo ni wajibu wa wafanyakazi ngazi mbali mbali kushirikiana kwa pamoja katika kufanikisha shughuli au kazi hiyo.“Wafanyakazi sote pamoja na Wananchi kwa umoja wetu tushirikiane na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuweza kutimiza lengo lilokusudiwa”aliongeza Muangalizi wa Ofisi Arafa.

Nao Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar walisema kuwa wameitikia wito huo kwa kutekeleza agizo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanya usafi wa mazingira sambamba na kupamba mapambo katika Ofisi.

Sambamba na hayo walisema wameitikia wito huo kwa kuanza kukarabati Jengo la idara yao kwa kupaka rangi, kupamba ndani ya ofisi ili kuleta muonekano mpya wa mazingira ya ofisi na kumalizia kwa kufanya usafi pamoja na kuweka mapambo yaliyotakiwa.

Hatua hiyo ya ufanyaji wa usafi katika eneo la Idara ya Habari ni miongoni mwa agizo la Serikali kuu kwa Idara na taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi kufanya usafi katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo kilele chake kitafanyika January 12 visiwani humu.IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
 Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wafanya Usafi ndani ya Ofisi yao iliopo Raha leo Mjini Unguja, wakitekeleza agizo lililotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la kufanya usafi katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakiendelea kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo ya Ofisi yao Raha leo Mjini Unguja katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mfanyakazi kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dude David John akizowa taka baada ya kufanya Usafi katika eneo la Ofisi ya Idara ya Habari Maelezo Zanzibar .Picha na Maryam Kidiko - Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31

$
0
0

Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

VIONGOZI wote wa umma nchini wametakiwa kuorodhesha mali zao tena kwa usahihi na kisha kukabidhi kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kabla ya Desemba 31 mwaka huu.

Wamesisitiza kufanya hivyo ni utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria ,hivyo lazima watekeleze kwa wakati na watakaoshindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
 Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitangza tarehe ya mwisho kwa viongozi wa umma kukabidhi tamko la mali zao ambayo ni Desemba 31 mwaka huu.

“Kila kiongozi wa umma ajaze tamko hilo kwa kuorodhesha mali zake, mwenza wake na watoto wake walio na umri chini ya miaka 18,”amesema. Amefafanua viongozi wanaotakiwa kuorodhesha mali zao na kisha kukabidhi Sekretarieti ya Maadili ni wale wa kuteuliwa na kuchaguliwa.

“Pia ujazaji wa tamko hilo kisheria linawahusisha hata viongozi waliostaafu na wale wanaoelekea kustaafu,”amesisitiza. Ameongeza viongozi ambao wanastaafu wakati wanaingia waliorodhesha mali zao, hivyo wanapostaafu ni lazima waoredheshe ili ifahamike wanatoka wakiwa na mali kiasi gani.

“Hivyo ni muhimu kila kiongozi kujaza hilo tamko na tunachokifanya sisi ni kukumbusha tu.Fomu za tamko zipo kwenye tovuti ya sekretarieti ya maadili. “Huko nyuma tulikuwa tunawatafuta viongozi na kuwapa matamko wajaze lakini sasa ni lazima wao kuchukua na kujaza na jukumu letu ni kupokea na kisha kuchambua tamko la kila kiongozi,”amesema Jaji mstaafu Nsekela.

Amesema anaamini viongozi wanafahamu wajibu wao,hivyo wafanye haraka iwezekanavyo na hasa kwa kuzingatia muda uliobakia ni mchache. Alipoulizwa ni viongozi wangapi wamejaza fomu hadi sasa,Jaji mstaafu Nsekela amesema hana takwimu sahihi lakini baada ya muda ulioapngwa kumaliza watatoa taarifa sahihi huku akieleza yeye tayari ameorodhesha mali zake kwenye tamko na kukabidhi tena kwa Rais.

Kuhusu viongozi wanaostaafu ambao wamejaza tamko hilo amesema nao bado lakini katika eneo hilo kuna changamoto yake kidogo kwani viongozi wanapostaafu inakuwa ngumu kuwapata lakini nao watambue wanatakiwa kujaza tamko kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Ofisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Mmaadili Bw. Filotheus Manula ameongeza ujazaji wa tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na kuna adhabu kwa wasiofuata.

Ametaja adhabu hizo ni kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa kazi. 
 Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipowawataka Viongozi wote wa umma nchini kuorodhesha mali zao kisha kukabidhi kwa Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu Kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Bw. Filotheus Manula.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katikati akikaribishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Rodney Thadeus ili kuzungumza na waandishi wa habari, wa pili kutoka kulia ni Aisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manula na kushoto ni Ofisa wa Sekretarieti hiyo Bw. Waziri Kipacha

Washiriki shindano la Watanzania wenye umri mdogo na wenye ushawishi watajwa

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
Washiriki wa shindano la Avance Media kwa Watanzania 50 wenye umri mdogo na wenye ushawishi kwa mwaka 2017 wametajwa.
Watanzania hao 50 huchaguliwa kwa kupigiwa kura wakitokea katika sekta mbalimbali kama vile biashara, burudani, Sheria na utawala, sekta ya habari, sayansi na teknalojia, michezo, uwajibikaji katika jamii na kujitolea.
Kwa mujibu wa waandaji wa shindano hilo, washindi watatangazwa tarehe 16 mwezi January mwaka 2018
Ikiwa ni moja ya mashindano yenye heshima kubwa, shindano hili hutoa mchango wa kipekee kwa kutambua jitihada mbali mbali zinazofanywa na Watanzania wenye umri mdogo katika sekta mbali mbali
Mkurugenzi Mtendaji wa Avance Media, Prince Akpah alisema “Kwa mwaka huu, Mtanzania mwenye ushawishi Zaidi ni yule ambaye kazi yake pasipo na shaka imekuwa na mchango chanya kwa maisha ya Watanzania. Washiriki wote waliotajwa na wanaoshiriki, wamerweza kuvuka kigezo cha kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wengine kupitia kujituma, kufanya kazi kwa bidii ,kujitolea na kibubwa Zaidi kufanya maamuzi ya kijasiri,”
Pazia la upigaji kura tayari limeshafunguliwa kupitia tovuti ya tz.avancemedia.org ili kuweza kumpata mshindi mmoja mwenye ushawishi aidi katika sekta nane ambazo zitapigiwa kura
Zoezi hili pia linafanyika katika nchi za Cameroon, Ghana, Nigeria, South Africa, DR Congo na Kenya.

Washiriki waliotajwa ni wafuatao
Kwenye biashara (kwa kushirikiana na TANOE Business)
  1. Carol Ndosi (Alta Vista Events)
  2. Harun Elias (Javis International Trade Co.)
  3. Hellen Dausen (Nuya's Essence)
  4. Ian Ferrao (Vodacom Tanzania)
  5. Krantz Mwantepele (KONCEPT)
  6. Patrick Ngowi (Helvetic Solar)
  7. Yusuf Bakhresa (Azam Media Ltd)
Burudani (kwa kushirikiana na WatsUp TV)



    1. Ali Kiba (mwanamuziki)
    2. Diamond Platinumz (mwanamuziki)
    3. Jokate Mwegelo (muigizaji)
    4. Joti (mchekeshaji)
    5. Riyama Ally (mwigizaji)
    6. Vanessa Mdee (mwanamuziki)
    7. Wema Sepetu (mwigizaji)





Sheria na Utawala

  1. Albert Msando (mwanasheria)
  2. Benedict Ishabakaki (mwanasheria)
  3. Bonnah Kaluwa Mbunge)
  4. Fatma Karume (mwanasheria)
  5. Jebra Kambole (mwanasheria)
  6. Peter Kibatala (mwanasheria)
Maisha
  1. Benjamin Fernandes (Mwendesha kipindi cha Tv)
  2. Flaviana Matata (mwanamitindo)

  3. Jacqueline N Mengi (mwanamitindo)
  4. Millen Magese (mwanamitindo)
  5. Miriam Odemba (mwanamitindo)
  6. Osse Greca Sinare (mpiga picha)
Tasnia ya Habari
  1. Babbie Kabae (Clouds 360)
  2. Bdozen (Clouds Media)
  3. Dina Marios (E-FM Radio)
  4. Idris Sultan (SIO HABARI)
  5. Millard Ayo (Ayo TV)
  6. Salim Kikeke (BBC Swahili)
Sayansi na Teknolojia

  1. Edwin Bruno (Smart Codes)
  2. Evans Makundi (EvMak Tanzania Ltd)
  3. Fayaz Valli (GetCore Group)
  4. Johnpaul Barretto (Kinu Innovation Space)
  5. Jumanne Mtambalike (Sahara Ventures)
  6. Lilian Makoi (Jamii Africa )
Michezo
  1. Hashim Thabit Manka (Yokohama B-Corsairs)
  2. Juma Kaseja (Young Africans SC)
  3. Mbwana Samatta (KRC Genk)
  4. Mrisho Ngasa (Fanja SC)
  5. Shomari Kapombe (Simba SC)
  6. Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna)
Jamii na asasi za kiraia

  1. Faraja Nyalandu (Shule Direct)
  2. Irene Kiwia (Tanzania Women of Achievement)
  3. Jennifer Richard Shigoli (Tanzania Netherland Vocational Training Center)
  4. Nancy Sumari (The Neghesti-Sumari Foundation)
  5. Rebeca Gyumi (Msichana Initiative)
  6. Saira Dewji (Mo Dewji Foundation)

Shindano hili huandaliwa na Avance Media kwa kushirikiana na BioPlus, ReputationPoll.com, Abjel Communications, WatsUp TV, YCEO, TANOEBusiness.com, My Naija Naira, Dream Ambassadors Foundation GH, CliqAfrica na CELBMD Africa.


Msaada, Mtoto Amepotea

$
0
0
Tumepokea taarifa ya kupotea kwa mtoto huyu hivyo tunaomba ukiomuona utoe taarifa, tutashukuru sana na utabaribiwa.  

Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa

$
0
0
Mojawapo ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Prochess Mroso (kulia) mkaazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu ushindi wake katika mkutano na waandishi wa habari leo. Ameambatana na Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kati) na mshindi mwengine Editha Malyamoto wa Kibamba(kushoto). Tigo pia inatoa zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 kwa wateja wanaotumia Tigo Pesa

Mojawapo ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Prochess Mroso (kulia) mkaazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu ushindi wake katika mkutano na waandishi wa habari leo. Ameambatana na Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kati) na  mshindi mwengine Editha Malyamoto wa Kibamba pamoja na Afisa Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro (kushoto). Tigo pia inatoa zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 kwa wateja wanaotumia Tigo pesa. 
Baadhi ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde wakiwa na simu zao baada ya kupokea ujumbe wa simu uliothibitisha kupokea zawadi hizo  za pesa.Tigo inatoa zawadi ya shilingi milioni moja kila siku na zawadi nne za shilingi laki tano kila siku kwa wateja wanaotumia huduma ya Tigo Pesa, pamoja na zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5.
Mary Rutta, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi zawadi saba za shilingi milioni moja na zawadi 28 za shililingi laki tano kila mmoja kwa washindi wa wiki hii wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde'. Kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro.  




•             Wateja Wengine 28 Wajishindia Zawadi za TZS 500,000 Kila Mmoja. 
Dar es Salaam, 22 Desemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa imewaibua jumla ya mamilionea saba (7) wapya  katika droo ya wiki hii ya promosheni yake inayoendelea ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’. 
Washindi wengine 28 nao wamejinyakulia donge nono za kila siku za TZS 500,000 kila mmoja, na kufanya jumla ya wateja walipotakana hadi sasa kufikia 90. 
Akitangaza washindi wa wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema kuwa pamoja na zawadi hizo za kila siku, wateja wa Tigo Pesa wana fursa kubwa ya kushinda zawadi kubwa za TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni ambapo washindi watajulikana usiku wa kuamkia mwaka mpya. 
Kufikia sasa tumetoa until now we have given out Tzs 69 Million to 90 winners and we expect  to give out Tzs 51Million more to remaining 63 winners
‘Kufikia sasa tumtoa jumla ya TZS 69 milioni kwa washindi 90 na bado tuna zawadi za TZS 51 milioni zitakazotolewa kwa washindi wengine 63, ikiwa pamoja na mamilionea wapya tutakaowapata usiku  wa kuamkia mwaka mpya wa 2018. Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda, kwa hiyo nawaasa wateja wote wa Tigo wachangamkie fursa hii ya kutimiza ndoto zao za sikukuu na mwaka mpya’ alisema. 
Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA ASHIRIKI IBADA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA ILIYOANDALIWA NA UMOJA WA MAKANISA MKOA WA SINGIDA

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo(hawapo pichani) kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida  jana.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba( wa tano kulia) akifuatilia kwa makini mahubiri wakati wa Ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida jana  wengine pichani ni viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo  Mkoa wa Singida.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida  jana ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kutii Sheria za nchi bila shuruti.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada na kumbi za starehe katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

Ukweli kuhusu kutofanyika shindano la Miss Tanzania

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekua likifuatilia kwa umakini mwenendo wa shindano la Miss Tanzania na waandaji wake kampuni ya LINO Agency katika kuhakikisha taratibu, kanuni na miongozo ya kuendesha matukio ya Sanaa nchini inazingatiwa.

Hivi karibuni LINO wametoa taarifa ya kutokufanyika kwa shindano Miss Tanzania kwa mwaka 2017 ambapo pamoja na sababu ya kukosa wadhamini wametaja kucheleweshewa kibali na BASATA kama sababu ya kutokufanyika kwa shindano hili kwa msimu wa mwaka 2017.

Tunapenda kueleza kwamba sababu inayotolewa na LINO kwamba walicheleweshewa kibali na BASATA si ya kweli na pengine imetengenezwa kuficha uhalisia wa changamoto za shindano hili ambazo mara zote BASATA na hivi karibuni Waziri mwenye dhamana na sekta ya Sanaa Mh. Dkt Harrison Mwakyembe amezieleza na kuzitolea maagizo.

BASATA kama mtoa vibali vya matukio ya Sanaa nchini limeshangazwa na taarifa ya kutokuwepio kwa shindano kwa msimu huu maana tayari lilikwishatoa kibali cha muda kwa kampuni ya LINO ili kufanya maandalizi ya awali ya shindano hili sambamba na kuandaa mshiriki wa shinda la Miss World 2017 lililomalizika hivi karibuni mji wa Sanya nchini China amabapo Tanzania tuliwakilishwa na mshiriki Julitha Kabete aliyekabidhiwa bendera chini ya uangalizi wa Wizara na BASATA.

Kibali hicho cha muda ambacho kilitolewa mapema tarehe 08/09/2017 kinatoa fursa kwa mwandaaji wa tukio la Sanaa kufanya maandalizi yote ya awali ya tukio la Sanaa/Burudani huku akiwa chini ya uangalizi maalum wa kukamilisha taratibu mbalimbali za msingi kwa ajili ya kupewa kibali cha mwisho cha tukio husika hivyo kampuni ya LINO haina sababu yoyote ya kutaja kibali cha BASATA kama kikwazo cha kufanyika kwa shindano la Miss Tanzania mwaka huu maana tayari walikua na kibali hiki cha muda kinachowapa fursa za maandalizi yote ya awali ya shindano

Tunazidi kutoa wito kwa waandaaji wote wa mashindano/matukio ya Sanaa kuzidisha weledi na zaidi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kuendesha matukio ya Sanaa kama zinavyo fafanuliwa katika vikao vya mashauri mara kwa mara. Aidha tunazidi kusisitiza umuhimu wa kujenga taswira chanya kwa matukio ya Sanaa na kuyajengea uendelevu ili kuvutia wawekezaji zaidi na kuyapa mvuto mkubwa wa kibiashara.

BASATA kama msajili na mtoa leseni katika matukio ya Sanaa tutaendelea kuzingatia weledi na kutoa huduma zetu kwa haraka, ubora na kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa ambazo kwa pamoja wadau wote tumeziridhia.


KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA SANAA LA TAIFA – BASATA

Hatuna tatizo la dawa nchi nzima-Dk. Ndugulile

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa mkanoge wakati uzinduzi wa zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ya harakati zilizofanyika za kujenga Zahanati ya Mkanonge.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Faustine Ndugulile kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakizindua Zahanati ya Mkanonge.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Pwani.

Mkazi wa Kijiji cha Makanonge, Themed Mkale akimkabidhi Zawadi ya Mhogo,pamoja na Mpunga Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk. Faustine Ndugulile.
Sehemu ya wananchi waliofika kwenye uzinduzi huu wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge



Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii

Serikali imesema kuwa hakuna tatizo la dawa katika sehemu kutoa huduma za afya katika Hospitali, Vituo vya Afya , Dispensari pamoja na Zahanati.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge Kata ya Nyamato Wilayani Mkuranga.

Dk.Ndugulile amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya afya kumefanya Wizara kujipanga katika kuhakikisha wananchi wanapata dawa pale wanapokwenda kupata huduma za afya katika hospitali vituo vya afya, Zahanati pamoja na Dispensari.

Amesema kuwa licha na jitihada hizo serikali inakuja mpango wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya na ni lazima na sio hiari.Dk.Ndugulile katika uzinduzi wa zahanati hiyo ameahidi kuwapelekea jokofu la kuhifadhi dawa za chanjo ili kuwapunguzia wananchi wa kufuata chanjo mbali.

Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza katika utoaji wa chanjo duniani kwa asilimia 97.Dk.Ndugulile ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili Ujenzi wa nyumba ya Mkunga katika zahanati ya Mkanoge.

Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambae ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa jitihada za kuboresha huduma za jamii ni endelevu katika Wilaya hiyo.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images