Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1472 | 1473 | (Page 1474) | 1475 | 1476 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde amefanya ziara kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Hombolo Bwawani huku akiwahakikishia wananchi wa Mkoyo kuwa wataanza kupata huduma ya maji safi na salama kabla ya mwaka mpya kutokana na mradi huo kukamilika kwa asilimia 95.

  Mavunde amefanya ziara hiyo jana ambapo ametembelea kata hiyo na kufanya mikutano ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi, ambapo akiwa kijiji cha Mkoyo miongoni mwa kero walizolalamikia wananchi ni utekelezaji wa mradi ya maji.Kutokana na malalamiko hayo, Mavunde amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 95 lakini bado kuna mapungufu machache ambayo mkandarasi anatakiwa kurekebisha na kuukabidhi kwa wananchi ili waweze kupata maji safi na salama kabla ya mwaka mpya.

  Kwa upande wa sekta ya Elimu, Mbunge huyo ameahidi kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa shule mbili za msingi kwenye eneo la Ngh’ole na Ndachi kutokana na watoto wa wanatembea umbali mrefu kufuata elimu.“Hivyo kwa kuanza tunaanza na nguvu ya wananchi kwenye ujenzi wa shule ambapo kwa upande wangu nitachangia matofali 1000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili kuanza harakati za ujenzi wa shule hizi,”amesema 

  Akiwa katika mtaa wa Hombolo bwawani,Mavunde ameahidi kununua mota yenye thamani ya Tsh 4,000,000 na kuwafungia wananchi ili waanze kupata maji kwenye Mradi wa Maji wa Mtaa wa Bwawani B ambao mota yake imekufa.

  Aidha katika Mradi mkubwa wa Maji wa Hombolo ambao ulihujumiwa kwa kuibiwa solar panel,Mavunde amesema wamefanikiwa kuwakamata wezi waliohujumu mradi huo na taratibu za kipolisi zinafanywa ili vifaa hivyo virejeshwe Hombolo na wananchi waanze kupata maji.

  Kadhalika, Katika sekta ya miundombinu, Mbunge Mavunde amesema anatambua changamoto ya barabara ya Ihumwa- Hombolo na kwamba ameongea na Wakala wa barabara(Tanroad) ili kuangalia namna ya kuipandisha hadhi kupitia kikao cha bodi ya barabara ili ijengwe kwa kiwango cha lami.

  Aidha Mavunde kwa upande wa sekta ya Afya amesema kiasi cha Sh.Milioni 500 kimeingia kwa ajili ya kuboresha Kituo cha Afya Hombolo ili kiwe cha kisasa na wananchi hawatalazimika tena kufuata huduma Dodoma mjini.
  Mbali na hilo, amewaomba wakulima wa zabibu wajiunge katika vikundi ili kuwatafutia fursa ya uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kukamua zabibu ili waondokane na adha ya soko la zabibu na kushuka kwa bei ya zabibu.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Hombolo Bwawani.
  Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Assedi Ndajilo akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde wa kusikiliza kero za wananchi.
  Wananchi waliosimama kuwasilisha kero zao kwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde.
  Wananchi waliosimama kuwasilisha kero zao kwa Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde.
  Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara kata ya Hombolo bwawani
  Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi na viongozi wa kata ya Hombolo bwawani.


  0 0

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kulia) akiweka Jiwe la Msingi katika Mabweni ya Wasichana yaliyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya Sekondari Itilima wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu,(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, mhe Anthony Mtaka.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lagangabilili mara baada ya kufungua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya msingi Lagangabilili wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako( wa tatu kushoto) na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakielekea kukagua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake mkoani humo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (kulia) wakati akikagua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo(P4R) katika Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani Itilima.  Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako amesema Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) cha Mkoa wa Simiyu kuanzia mwezi Machi, 2018.

  Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani humo.“Kesho tarehe 28/12/2017 kwenye magazeti kutatoka tangazo la zabuni ya ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Simiyu na tunategemea kujenga VETA ya Kisasa itakayohudumia Mkoa na inayoendana na mahitaji ya sasa; tukitangaza zabuni kesho itachukua siku 30 kupokea zabuni unahitajika mwezi mmoja kufanya tathmini, nawaahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi Machi” alifafanua Profesa Ndalichako.

  Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inasisitiza juu ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatambua umuhimu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi ndiyo maana imejipanga kujenga vyuo hivyo pamoja na kuimarisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.Aidha, Profesa Ndalichako amepongeza ongezeko la wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza na akasisitiza kuwa Wizara ya Elimu ambayo ndiyo inayotunga Sera itahakikisha inasimamia kikamilifu ili wanafunzi wote wanaoanza darasa la kwanza wamalize masoma yao.

  Amesema ongezeko hilo ambalo limesababishwa na mwamko chanya wa wazazi baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango wa elimu bila malipo limepelekea upungufu wa miundombinu shule na ndiyo maana Serikali kuu inashirikiana na Halmashauri pamoja na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ili kukabiliana na upungufu kupitia Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo(P4R).

  “Kupitia mradi wa Lipa kulingana na Matokeo tumeshajenga jumla ya vyumba vya madarasa 1104, matundu ya vyoo 3396, mabweni 261. Tunaendelea pia kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu kwa ujumla, kwa maana ya ukarabati katika vyuo vya Ualimu ambapo tumeshakarabati vyuo 17 na shule kongwe 46 kati ya shule 88 zimeshakarabatiwa” alisema Waziri.

  Profesa Ndalichako amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Itilima kwa kutumia vizuri jumla ya shilingi bilioni 2.177 za Mradi wa Lipa Kulingana na matokeo(P4R) ambazo zimetumka kujenga miundombinu mbalimbali ya shule vikiwemo vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo wilayani humo.

  Akimshukuru Waziri wa Elimu kwa kupeleka fedha za Mradi wa Lipa kulingana na matokeo (P4R) katika Wilaya ya Itilima ambazo zimesaidia upatikanaji wa Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga amesema Wilaya hiyo imetekelezaji wa mradi huo kwa kufuata taratibu na miongozo yote ya Serikali kwa kushirikiana na wananchi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema katika kipindi cha mwaka 2018-2020 Mkoa huo umejiwekea mpango wa kujenga mabweni kwa wanafunzi wa kike katika kila shule ili kuwaondolea adha ya kutembea mwendo mrefu na changamoto nyingine.

  Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Ndalichako Mkoani Simiyu ambayo imempa nafasi ya kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kufungua vyumba vya madarasa, mabweni katika maeneo tofauti Wilayani Itilima ikiwemo Kijiji cha Habiya, Lagangabilili, Itilima, Mahembe na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Luguru.

  0 0

   


  Ramani ya msiba

  Msiba uko nyumbani kwake Mbweni Kijijini, Dar es Salaam, eneo la Mbweni Maputo,siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.

  Yaani ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni Kijijini, unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia inayokwenda kushoto ituate barabara hiyo kwa kuongozwa na vibao vinavyoelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu, ambaye ni maarufu kama Mzee Magazeti.

  Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Bagamoyo, shukia  kituo cha Mianzini Bunju.
  Hapo chukua bodaboda kwa gharama ya kama 3000/= hadi mbele kidogo ya Mbweni Misheni Hospitali. Ukifika hapo kata kushoto na muelekeze huyo bodaboda afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.

  Kwa wenye usafiri binfsi; unaweza kufika kwa njia mbili:

  1.Ukitoka Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju. Hapo kuna barabara ya lami kuelekea Mbweni. Ifuate hadi Mbweni Kijijini,utakapoikuta Hospitali ya Misheni Mbweni. Baada ya hapo kata kushoto.Fuata vibao vya msiba vitakufikisha. 

  2.Ukitoka Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni Jeshini, fuata njia ya daladala, yapite mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza kufuata maelekezo ya vibao vya msiba ambavyo vitakufikisha.

  Usafiri kwa Wanahabari

  Kwa mujibu kamati ya maandalizi kutakuwa na mabasi mawili ya UDA yatakayobeba wanahabari watakaokwenda kumuaga mwenzao.

  Basi la kwanza litakuwa Idara ya Habari Maelezo,Mtaa wa Samora, kuanzia saa 1:30 asubuhi ambapo litaondoka saa 2:30 kuelekea msibani Mbweni.

  Basi la pili litakuwa Mwenge,maeneo ya kituo cha mafuta cha BP, kuanzia saa mbili asubuhi ambapo litaondoka hapo saa 3 kuelekea msibani.

  Poleni sana,

  Imetolewa na Kamati ya Maandalizi
  Desemba 27, 2017.

  Kwa mawasiliano wapigie wanakamati ya Usafiri

  Peter Mgongo 0715 765 454
  Eric Antony 0755 755 551

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili ya  kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaa
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika Ofisi za za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. 
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.


  0 0


  Muonekano wa jiji la Arusha katika picha

  Na Dotto Mwaibale

  WANANCHI wa jijini Arusha wameiomba Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kuwapelekea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo mkoani humo kusherehekea Sikukuu ya Krisimasi walisema bidhaa hizo ni mkombozi kwao.

  "Binafsi napenda kusema bidhaa hizi za Sugar Free kwa hapa Arusha zitapata soko kubwa kutokana na watu wengi kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari" alisema Mzee Mollel mkazi wa Njiro.

  Mollel alisema watu wengi jijini humo wananchi kwa masharti ya ulaji na unywaji wa vitu visivyo na sukari jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa karibu familia nyingi.

  Alisema wakazi wa jiji hilo wamezipokea kwa mikono miwili bidhaa hizo ambapo wameiomba kampuni hizo kufungua tawi mjini humo ili bidhaa hizo ziweze kupatika wakati wote.

  "Tunaomba bidhaa hizi ziuzwe na maofisa mauzo wa kampuni hiyo wasiwape wenye maduka itakuwa changamoto kupata maelezo ya kina ya matumizi yake na tunahofu wakiachiwa wafanyabiashara wengine wanaweza kutupandishia bei" alisema mkazi mwingine wa jiji hilo aliyejitambulisha kwa jina la Laizer.

  Laizer alisema humo kumekuwa na unywaji na ulaji wa vyakula vyenye sukari lakini kuingia kwa bidhaa hizo zitasaidia sana wananchi hasa baada ya kupata maelekezo ya utumiaji wake.

  Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 

  Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

  "Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

  Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

  Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.

  Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 

  Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

  Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

  Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.


  0 0

  Na Said Mwishehe, Blogu  ya Jamii.

  TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi.

  Hayo yamesemwa leo  mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es  Salaam.Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua akipata kitandani Mayage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.

  Alisema msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage  S. Mayage katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi na alichojifunza ni upendo na uvumilivu. 

  "Alikuwa ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa zaidi ni kumuombea kwa  Mungu, "amesema Padre Kaniki. 
    
  Mayage S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani  na  nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.

  Ilipofika mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia Tanzania. 

  Akizungumza katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absaloum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika taaluma. Kibanda amesema mchango wa Mayage katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa."Mimi na Mayage pamoja na wengine tuliojaaliwa pamoja Habari Coparation, anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu kitaalum.
   Safari ya Mwisho ya aliyekuwa Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Marehemu Mayage Steven Mayage imefanyika jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu 
   Wawakilishi kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu John Chacha na Ankal Issa Michuzi kwa pamoja wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
   Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
   Mmoja wa aliyefanya kazi na Marehemu Mayage,Ndugu Haji Dillunga akiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
   Sala ya Maziko ya Marehemu Mayage Steven Mayage ikiendelea katika Makaburi ya Mbweni Maputo,kabla ya kumlaza mpendwa wetu katika nyumba yake ya Milele,jioni ya leo. 
   
   Katibu NEC-Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwandishi mkongwe hapa nchini,Marehemu Mayage S. Mayage nyumbani kwake leo,Mbweni jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.


  0 0

  Msanii wa muziki wakizazi kipya Rajab Abdulkahal au Harmonize amekula chakula cha mchana na watoto wanaishi katika mazingira hatarishi katika kituo cha kulelea Yatima cha kanisa LA EAGT mkoni Mtwara kama moja ya Kuwapa matumaini katika Maisha ya kila Siku.

  Harmonize akiongozana na rafiki yake wa kike wa karibu anayejulikana kwa Jina la Sarah amesema kuna watoto waliopoteza wazazi wao wakiwa na umri mdogo huku wakiwa na ndoto kubwa za kimaisha lakini zinaonekana kupotea kutokana hivyo wanahitaji kupewa moya na kuwa na bidii binafsi.

  Hata Hivyo Msanii Harmonize amepata fursa ya kubadilishana Mawazo na watoto wenye Ndoto mbalimbali zankimisha na kuwasihi kumshirikisha Mungu kwa kila wanachokifanya.
   Msanii Harmonize akiwa na Rafiki yake Sarah wakigawa chakula kwa Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi ambao wanalelewa katika kituo cha Kulea Yatima cha EAGT Mtwara.
  Harmonize akiongea na Wandishi wa Habari Mara baada ya kumaliza Chakula cha Mchana alichokiandaa kwa ajili ya Watoto Yatima Mtwara

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (mbele) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakiongozwa na Mhandisi wa Majengo kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo Ikungi.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akikagua Ujenzi wa Kichomea Taka katika kituo cha Afya Ihanje.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Viongozi wa Wilaya ya Ikungi katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya Ihanje.

  Nteghenjwa,Hosseah,Ikungi-Singida.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi nzuri  ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

  Mhe.Jafo alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua  miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ihanje.

  Aliongeza kuwa Kituo cha Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200  vitakavyopekea/vilivyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.

  Nimekagua majengo yote sita yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi  kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za ujenzi hupungua ukilinganisha na  wakandarasi; Hii  inanipa faraja kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu, Alisema Mhe.Jafo.

  Awali akitoa taarifa hiyo  Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  Sembua Mrisho amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa bohari ya dawa kwa ajili ya  vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.

  “Mara baada ya kupokea Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii imefanyika kwa kutumia “Local fund” na  inasimamia na Wakandarasi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.
  Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.
  Aliongeza kuwa  Kituo cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi  mahitaji kutokana na kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.
  Akizungumza kwa furaha Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a mtoto.

  Ukarabati sambamba na uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha Vituo vya Afya 161.


  0 0


  Na.Vero Ignatus Arusha. 

  Katibu mkuu baraza la Sanaa Tanzania amewataka wazazi na walezi wa hapa nchini kuwalea watoto na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la kwanza la Tanzania Tukuza Utalii Genesis 1,Godfrey Ngereza alisema kuwa tanzania imebarikiwa kwa tunu mbali mbali hivyo watanzania hawana budi kuzitunza na kuzilinda.

  Aidha alisema kuwa wazazi hawana budi kuwafundisha watoto uzalendo na kuhakikisha kuwa tamaduni zilizopo haziishi."Waswahili walisema samaki mkunje Angali mbichi tukiwalea watoto vizuri ni ngumu kuona maadili yanamomonyoka kwa kuwa tutakuwa tumetengeneza watoto wema" Alisema Godfrey

  Kwa upande wake Raisi wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili Tanzania(TAGOANE)Dkt.Godwin Maimu Nnyaka alisema kuwa watoto yatima hawahitaji mavazi na chakula peke yake bali kujengewa msingi bora wa maisha yake.

  Dkt.Nnyaka alisema wakati umefika wazazi kuwalea watoto katika misingi ya Imara na kuhakikisha wanakuwa wazalendo.Aidha alisema kuwa kupitia tamasha hilo litasiadia kujenga vijana wenye hofu ya Mungu na kurejesha uzalendo na maadili kwa vijana.

  Nao baadhi ya Washiriki akiwepo mmiliki wa kituo cha faraja Ophanage Faraja Maliaki aliishukuru TAGOANE na kuwataka wadau wengine kuungana na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kuwapa faraja kwa kuwa nao wanastahili kuheshimiwa kama watoto wengine.
  Katibu mkuu mtendaji Baraza la sanaa nchini( Basata)Godfrey Mngereza akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo.Picha zote kwa Idhini ya Vero Ignatus Blog
  Rais wa Mtandao wa Wasanii wa wasanii wa Muziki wa Injili Tanzania na maandili nchini Tanzania (TAGOANE) Dkt.Godwin Maimu akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha la Tukuza utalii Tanzania lililozinduliwa rasmi Jijini Arusha.

  Baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika mazinhira hatarishai na baadae wakachukuliwa na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Rais wa Tagoane Dkt.Godwin Maimu akiwa anacheza pamoja na watoto katika Tamasha lililoandaliwa la Tukuza Utalii Tanzania lililoandaliwa na Tagoane.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la sanaa nchini (BASATA) pamoja na Rais wa Tagoane nchini wakikata keki kama ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Kuza Utalii Tanzania .
  Shamrashamra zikiendelea 
  Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Faraja wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na mlezi Faraja Maliaki,wapo zaidi ya watoto 200 katika ukubi wa Club D Jijini Arusha.
  Mgeni rasmi kutoka Baraza la sanaa la Taifa (Basata)Godrey Mngereza akifurahi pamoja na watoto yatima katika tamasha lililoandaliwa na Tagoane Jiiini Arusha.
  Wakila chakula pamoja na watoto katika Tamasha 
  Meza kuu Rais wa Tagoane,Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la Sanaa nchini (Basata)Katibu mkuu Tagoane,na wakurugenzi wa vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es salaam Gifted Wilson akiimba katika uzinduzi wa tamasha la Tukuza Utalii Tanzania Genesis 1 Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog 
  Muimbaji wa nyimbo za Injili Miriam Makunja kutoka Arusha akiimba. Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog 
  Muimbaji Wolter Chilambo kutoka Jijini Dar es salaam akiwa anaimba katika Tamasha hilo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Hellen Masai akutoka Arusha kiimba .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa akiwa anafurahia kwenye ufunguzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania likilofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la sanaa Nchini (Basata)wa kwanza kushoto akiwa pamoja na Rais wa Tagoane katika uzinduzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
  Watoto wakionyesha mavazi ya ubunifu chini ya Mwanamitindo mbunifu Diana Magesa kutoka Mwanza,Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

  Picha za watoto yatima waliohudhuria katika tamasha la Tukuza Utalii Genesis 1 lililofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

  0 0
  Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo katikati akifungua duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hiyo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez ( Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)


  Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi akiingia katika duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAKambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hizo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,kulia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro


  Kulia ni Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya Gold Crest ya Mwanza na Arusha Mathias Manga mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK  Meneja Mkuu wa kampuni ya PiMAK ya kimataifa inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mapishai kwenye mahoteli akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea duka hilo

  Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akimuonyesha bidhaa za kampuni ya PiMAK mtaja aliyetembelea duka hilo siku ya uzinduzi Bi.Mary Mbajo


  Wahudumu wa duka hilo wakiwa na vepeperushi vya kampuni hiyo


  Muonekano ndani ya duka hilo
  Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo akizungumza mara baada ya kukata utepe,kushoto ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha ,Milance Kinabo


  Naibu Meya wa jiji la Arusha,Viola Likindikok akiangalia baadhi ya vyombo vinavyopatikana dukani hapo anayefatia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro

  Kulia Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akipozi na wadau katikati ni Maya wa jiji Kalist Lazaro
  Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo


  Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akitoa maelezo kwa mteja


  Wageni waliofika katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo  Na Pamela Mollel,Arusha

  KAMPUNI ya kimataifa ya PiMAK inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli , imefungua duka kubwa jijini Arusha kwaajili ya kuwarahisishia watumiaji wa vyombo hivyo kuvipata kwa wakati

  Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo la kisasa Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwepo kwa duka hilo hapa Tanzania tayari ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa mahoteli

  Kimambo alisema kuwa kampuni ya PiMAK kuja kuwekeza nchini itasaidia ajira lakini pia kuwainua wajasiriamali wadogo wenye ndoto ya kufika mbali.“Kuna hawa wajasiriamali wadogo ambao wanajihusisha na maswala ya upishi watapata fursa ya kutanua biashara zao kwa kuwa tayari vifaa vinapatikana kiurahisi”alisema Kimambo

  Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo yenye makao yake Uturuki imeamua kufungua maduka hapa Nchini Tanzania kwaajili ya kuwarahisishia wateja wake ambao walikuwa wakiagiza vyombo hivyo nje ya nchi.

  Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli

  0 0

  Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanziabar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni mwalikwa, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio mji wa Jeddah Bw. Salim Ali Shatri.
  Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wa Jeddah wakiwa katika picha na meza kuu baada ya mkutano.


  Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia

  Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia ' Tanzania Welfare Society' hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza. Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mhe. Pandu Amir Kificho alikuwa nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya 'Umrah' katika miji ya Makkah na Madina.

  Wanajumuiya walipata fursa ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na Balozi na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi. Vile vile waliweza kuuliza maswali na pia kutoa maoni na ushauri. 
  Katika hotuba zilizotolewa wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania. Habari zimeletwa na Mwandishi Maalumu wa Jeddah, Saudi Arabia. Kwa Picha na matukio mengine zaidi angalia youtube kupitia 'Prince eddycool' 
  Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kulia).  

  Na Hamza Temba, Dodoma
  ...............................................................
  Serikali imesikia kilio cha wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii nchini na kuamua kuongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu 95 vya uwindaji wa kitalii ambazo zilikuwa ziishe muda wake tarehe 31 Desemba mwaka huu (2017).

  Uamuzi huo umefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kikao cha majumuisho na watendaji wa Wizara hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkuano wa wadau wa sekta hiyo ulioandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma jana.

  Akizungumzia uamuzi huo Dk. Kigwangalla alisema, lengo ni kuwapa muda wawekezaji hao ili waweze kujiandaa na mabadiliko ya mfumo mpya wa utowaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada ikiwemo kurudisha baadhi ya gharama za uwekezaji walizoweka katika vitalu hivyo.

  Awali akizungumza katika mkutano huo wa wadau Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini, Michael Mantheakis alimuomba Waziri Kigwangalla kuwaongezea muda wa umiliki wa leseni zao kuanzia miaka mitano au mitatu na nusu ili waweze kurudisha gharama za uwekezaji walizowekeza katika vitalu hivyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, makambi na vifaa vyake pamoja na maji.

  Hata hivyo, Waziri Kigwangalla aliweka wazi msimamo wa Serikali wa kutimiza azma yake ya kuingia kwenye utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na kusema kuwa kamwe haitorudi nyuma na kwamba utekelezaji wa zoezi hilo hauwezi kusubiri muda mrefu kiasi hicho.

  Akizungumzia kuhusu hatua ya utekelezaji wa utaratibu huo, Waziri Kigwangalla alisema kwa sasa taratibu za kuandaa Sheria za usimamizi zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2018 pamoja na kanuni zake zinazotarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2018.

  Aidha, alisema mfumo maalumu wa kielektroniki unaandaliwa ambapo maombi yote ya leseni za umiliki wa vitalu vya uwindaji kwa njia ya mnada yatafanyika kwa uwazi kwa njia ya mtandao.

  Alisema baada ya kukamilika kwa taratibu zote na mfumo huo mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na maombi kuwasilishwa, mnada wa kwanza utaanza tarehe 1 Julai, 2018 kwa kuanza kunadi vitalu 61 ambavyo kwa sasa havina wawekezaji.

  Mnada wa pili utafanyika mwaka 2020 baada ya kuisha kwa muda huo wa nyongeza wa miaka miwili ukihusisha vitalu 95 vilivyoongezewa muda wa umiliki wa leseni pamoja na vitalu vingine endapo vitabaki katika mnada huo wa kwanza kwa sababu mbalimbali.

  Alisema sheria na kanuni zinazoandaliwa hivi sasa zitazingatia mambo muhimu ikiwemo kuwapa nafasi watanzania wenye mitaji midogo kuweza kuingia kwenye biashara hiyo pamoja na kuweka adhabu kali dhidi ya wafanyabiashara watakaohujumu biashara hiyo kwa makusudi.

  Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na waandhishi wa habari.

  Oktoba 22 mwaka huu (2017) wakatiakiongoza kikao cha wadau wa sekta ya Maliasili na Utaliimjini Dodoma, Waziri Kigwangalla alitangaza kufuta leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii zilizokuwa zianze mwezi Januari, 2018 ili kupisha utarartibu mpya wa utoaji wa leseni hizo kwa njia ya mnada ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuimarisha sekta hiyo.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini, Michael Mantheakis (kulia) akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano wa wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada.
  Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii, Dk. Licky Abdallah akizungumza katika mkutano huo. 
  Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii ambaye pia ni mmilikia wa kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Bushman Hunting Safaris, Talal Abood akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano huo. 

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisikiliza kwa makini mapendekezo ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii wakiwa katika mkutano huo. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto kwake). 
  Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake wakiwa katika mkutano huo. 

  0 0

     Mbunge wa Jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akikabidhi fedha kwa ajili ya kulipia kivuko kilichokuwa watu wakilipishwa 200 kwa kila wakipita.
   Mbunge wa Jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi  wa Mabibo wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi, ambapo aliweza kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja na kuamua kununua kivuko cha mtu Binafsi ili watu waweze kupita bure kuliko awali ambapo walikuwa wakilipishwa shilingi 200.
    Mbunge wa Jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi  wa Mabibo wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi
    Mbunge wa Jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea  akiwa katika mitaa ya  Mabibo wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi
    Mbunge wa Jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akitembea na wakazi  wa Mabibo wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi
   Mmoja ya wakazi wa mabibo akiwasilisha hoja yake kwa mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za Wananchi
   Mmoja ya wakazi wa mabibo akiwasilisha hoja yake kwa mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za Wananchi

  0 0

   Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani   akizungumza kabla ya kupokea Vifaa Tiba kwa ajili ya Hospitali za jeshi la Polisi vilivyotolewa na Chama cha kuweka akiba na Kukopa cha URA Saccos  katika Hospitali ya Kilwa Road Jijini Dar es Salaam
   Kamanda wa kikosi cha Afya nchini, Paul Kasabago akizungumza juu ya hali ya Vituo vya Afya vya Jeshi la Polisi nchini.
   Kikosi cha Bendi cha Jeshila Polisi nchini kikitoa Burudani kwa watu waliofika katika hafla ya kupokea vifaa tiba kutoka URA Saccos
   Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos  akizungumz akatika hafala hiyo yamakabidhiano ya vifaa Tiba iliyofanyiak Kilwa Road Jijini Dar es Salaam
    Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani, akikata utepe kuashiria uzinduzi na kupokea Vifaa Tiba kutoka URA Saccos
    Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akifanyiwa kipimo cha Presha na Sukari kutoka kwa Afisa Muuguzi PC Stella Sizya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Polisi Kilwa Road.
    Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani  akionyeshwa baadhi ya Vifaa  tiba vilivyotolewa na URA Saccos
    Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akisaini karatasi za makabidhiano ya Vifaaa na  Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos
   Kikundi cha Ngoma cha Jeshi la Polisi nchini kikitoa Burudani
  Picha ya Pmoja ya viongozi wa meza kuu na wakuu mwa vikosi mbalimbali

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akisalimiana na viongozi mbalimbali alipokuwa akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akipokea heshima kutoka kwa askari polisi katika ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akiwa na Kamanda wa polisi Dodoma Gilles Murotop wakikagua gwaride katika ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
  Vikundi vya Ulinzi shirikishi
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akiwa na Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akitoa cheti kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma
  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akimvisha utambulisho mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma

  ……………….

  Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.

  Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.

  “Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza nafasi za Ajira zaidi,”amesema

  Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na UTULIVU.

  Naye, Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa Dodoma,SACP Gilles Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi shirikishi ili kuimarisha usalama na amani katika mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Msimamizi wa Kituo cha kurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa cha Namanga mkoani Arusha Ndg. Joseph Nchinga (kushoto) akitoa maelekezo ya mtambo mpya wakurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (wa kwanza kulia) wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mkoani Arusha leo tarehe 28/12/2017. Kituo hicho kimekamilika na kimeongeza usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa umbali wa Kilomita 45 kwa pande zote mbili za mpakani mwa Tanzania na Kenya.
  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso (kulia) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi mtambo mpya wa kurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa wakati alipotembelea eneo ambalo mtambo huo umefungwa mtaa wa Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Mtambo huo utaongeza usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa kanda ya Arusha. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (katikati) akimuelekeza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Alkan CIT Ngd. Ali Mohamedi (Kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) zinazojengwa eneo la Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Kampuni ya Alkan CIT ndiyo inayojenga ofisi hiyo ambapo ujenzi unatarijiwa kukamilia mwezi Januari 2018. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso.
  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso (kushoto) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi chumba kitakacho tumika kama studio za TBC FM na TBC Taifa wakati alipo kagau maendeleo ya ujenzi wa ofisi za kanda za shirika hilo zilizoko Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Bi Susan ametembelea eneo hilo kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa ofisi mpya za TBC kanda ya Arusha, ujenzi huo unatarijiwa kukamilika mwezi januari 2018.
  Eneo la ofisi ya Shirika la Utangazaji la Taifa TBC linaloendelea na ujenzi lililopo Njiro mkoani Arusha. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Susan P. Mlawi alitembelea eneo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa leo Tarehe 28/12/2017.PICHA NA 
  OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM

  0 0

   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina (kulia) akipokea ripoti ya Kamati Ndogo ya kutathmini utendaji wa sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Bonaventure Baya anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia uvuvi, Dk.  Yohana Budeba hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dodoma jana.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Ndogo ya kutathmini utendaji wa sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria baada ya kukabidhi ripoti yako mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Bonaventure Baya Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi,  Dk Yohana Budeba
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akiwashukuru wajumbe wa Kamati Ndogo ya kutathmini utendaji wa sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria baada ya kupokea ripoti hiyo mjini Dodoma jana.  Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia uvuvi Dk. Yohana Budeba
  Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya kutathmini utendaji wa sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria,  Mhandisi  Bonaventure Baya (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya  Mifugo na Uvuvi  anayeshughulikia uvuvi, Dk Yohana Budeba mara baada ya kukabidhi ripoti yake kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina hayuko pichani Dodoma jana.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

  MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ameliagiza jeshi la polisi mkoani hapo ,kuwakamatana na kuwahoji viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kumi ,kutokana na kosa la kufanya udanganyifu wa ubora na uzito wa korosho ili kujipatia fedha .

  Amesema kuna baadhi ya AMCOS zimehusika kuchakachua na kutelemsha ubora wa korosho pamoja na kuweka mawe na michanga kwenye magunia ya korosho zilizokuwa zinauzwa kwenye minada .Aidha mhandisi Ndikilo ,amekemea maghala ya vichochoroni na majumbani ambayo yamejaa na kusababisha kuchafua na kuharibu minada inayofanyika mkoani Pwani.

  Akizungumza wilayani Mkuranga ,wakati akizungumzia kero hiyo iliyojitokeza alieleza,viongozi wa AMCOS hizo wakiwemo wenyeviti wake ,makatibu,kalani na wenye ghala wakamatwe na kueleza kiini cha kutelemsha ubora.

  Alisema lifunguliwe jalada la uchunguzi wahojiwe mazingira na kiini cha kubadili ubora kutoka kiwango kinachohitajika na kushusha kiwango cha chini.Mhandisi Ndikilo, alisema biashara hiyo haitaki kwani imesababisha wakulima wa korosho kushindwa kulipwa fedha zao.

  "Kuna hii Mchukwi A -Amcos Two ambayo imechakachua korosho kutoka grade 52 hadi 45.1 ,Misugusugu wameshusha kiwango na kufikia 43,Mchukwi A -Amcos One ,Kibaoni ,Ruaruke ,Mahege,Mlanzi na Tuamke hawa wote wamejipanga kabisa ,maana haiwezekani viwe vyama vya msingi kumi huu ni mpango ,haikubaliki ,jamani haikubaliki" alisisitiza .

  Akitoa maagizo mengine manne ,mhandisi Ndikilo alitaka wanunuzi walioshinda mnada na kushindwa kuwalipa wakulima fedha zao wakamatwe ."Wapo wanunuzi walioenda nje ya masharti ya mnada wanapaswa walipe fedha za wakulima ndani ya siku nne" alisema mhandisi Ndikilo.

  Mhandisi Ndikilo ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo ,aliagiza pia makampuni yaliyoshinda na kutolipa wakulima yakamatwe ama yahakikishe yanalipa ndani ya siku moja. na kufikishwa mahakamani kwa kuweka mawe na mchanga kwenye magunia na kuchanganya na korosho.

  Alibainisha huo ni wizi,uhujumu uchumi na kuaibisha sifa ya nchi ya Tanzania nje ya nchi kwani magunia hayo yangefika India na nchi nyingine ingekuwa aibu na fedheha.Mhandisi Ndikilo alisema kero hizo zilisababisha Mkoa kuchukua hatua ya kufanya uhakiki upya wa korosho ili kuaminika kwa wanunuzi ambao baadhi yao waligomea kuingia kwenye soko la korosho mkoani humo .

  "Amcos zote nazipa salamu zijiandae ,zile Amcos zinazong'ang'ania kutumia maghala ya vichochoroni ili kudhurumu wakulima ,;:"'. Watie akilini msimu ujao 2018/2019 hawatatumia maghala ya majumbani yatatumika maghala makubwa matatu likiwemo la Mkuranga, , Kibiti na Kwamfipa Kibaha."

  Alisema ghala la Mkuranga litakuwa na uwezo wa kubeba korosho tani 30,000 hivyo aliomba kuondoka katika maghala yasiyo na kichwa wala miguu.Naibu waziri wa mifugo na uvuvi ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega alisema watu wachache wenye uroho wa fedha na wasio waaminifu wanataka kuharibu biashara hiyo na kuumiza wakulima.

  Alisema kuweka michanga na mawe kwenye korosho imerudisha nyuma minada inayoendelea .Ulega alisema kuwepo kwa maghala makubwa itainua soko la korosho msimu ujao na kuondoa ubabaishaji wa maghala madogomadogo yanayoleta dosari .

  Mbunge huyo ,aliupongeza uongozi huo wa Mkoa kuingilia kati na kuchukua hatua ili kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika vinavyoondoa uaminifu .Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid alisema mfumo wa stakabadhi ghalani unaharibiwa na baadhi ya watu na kusababisha wakulima kuona mfumo huo hauna manufaa kwao .

  Alisema kuna ujanja mwingi kwenye kuchakachua ubora wa korosho ndio uliowafikisha walipofikia sasa .Abeid alisema korosho zipo hadi kwenye nyumba za watu ,kuna maghala Mkuranga zaidi ya 60 ,hivyo ni lazima maghala makubwa yakawepo ili kuondokana na kero zinazojitokeza.

  Licha ya minada hiyo ya korosho kuingia kizungumkuti lakini tayari zaidi ya tani 19,815 zimeuzwa na kuingiza kiasi cha sh.bilioni 39 huku wakulima wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano .

older | 1 | .... | 1472 | 1473 | (Page 1474) | 1475 | 1476 | .... | 1898 | newer