Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1470 | 1471 | (Page 1472) | 1473 | 1474 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba ulioundwa baina ya RANCHI ya Taifa NARCO na kampuni ya Overland  kwa pamoja na kuunda kampuni ya OVENCO uliyokuwa na mapungufu ya kisheria na kiutendaji kufunjwa ifikapo mwisho wa mwezi huu wa December na kutoa mwezi mmoja kwa  NARCO kuunda mkataba mpya wenye mwongozo wa kisheria.
  Mpina aliyasema hayo jana alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa Ranchi ya Mzeri iliyopo wilayani Handeni Mkoani Tanga yenye ukubwa kwa Hekta 41,000  ambapo hekta 21,000 zinamililiwa na Muwekezaji kampuni ya Overland muwekezaji ambaye, amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na  NARCO ambapo baada ya Waziri Mpina kusililiza pande zote mbili na kujiridhisha  na kumuona muwekezaji kutokuwa na uwezo wa kufikia malengo ya kuendeleza eneo lote la ardhi  ambalo amekuwa akiliendeleza bila makubaliano yoyote ya kisheria, jambo ambalo limempelekea Waziri Mpina kuagiza  NARCO  kuingia katika hatua ya kuunda mkataba mpya baina yake na muwekezaji huyo utakaozingatia masharti mapya ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa muwakilishi wa NARCO Katika kitalu hicho.
  Aidha Waziri Mpina ameagiza muwekezaji huyo asihamishwe kwa kuwa ameonyesha nia ya kuendeleza eneo hilo kwa kuwepo kwa ng’ombe wambegu aina ya Borani pamoja na miundombinu mingine
  Akizungumzia eneo la hekta 20,000 linalomilikiwa na wawekezaji wengine wadogo, Mpina aliwataka wawekezaji hao kulipa na kumaliza madeni yote ya kodi ya serikali wanayodaiwa  katika vitalu vyao ifikapo January mosi 2018.
  “Wawekezaji wengine wengine wanaomiliki vitalu katika ranchi hii ya Mzeri mnatakiwa kulipa madeni yote ya kodi mnayodaiwa na Serikali kodi mnayolipa ya shilingi elfu moja (1000) kwa mwaka ni kidogo sana lakini bado hamlipi, kinyume na hili ni bora muondoke wenyewe au tutawaondosha kwa nguvu muda huo ukifika. “ Alisisitiza Mpina.
  “Baada ya kumaliza kulipa nawagiza NARCO kuwapa miezi mitatu wawekezaji hawa kuhakikisha wanaweka miondombinu inayolingana na ukubwa wa eneo na matumizi ya ardhi , tunataka wawekezaji wafikie malengo na mashamba haya yafanye kazi.” Alisema Mpina.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema kuwa, Wiaya ya handeni itaendelea kulinda  mazao na rasilimali za Mifugo kupitia sheria ndogondogo ambazo wilaya hiyo imejiwekea.
  Akizungumza kwa namna ambavyo ameyapokea maagizo wa Waziri Mpina , mmiliki wa kampuni ya Overland Bw. Faisal Edha alisema kuwa amekubalina na maagizo ya Mpina na yupo tayari kuendelea na uwekezaji na anaamini kuwa mkataba mpya utanufaisha pande zote mbili.
  Awali akipokea taarifa ya Mifugo ya wilaya ya Handeni, Waziri Mpina alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe  kwa kuzitambua sheria za usimamizi wa mifugo na kuzitumia jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwa uonevu kwa watu wa jamii ya wafugaji na kuzitaka wilaya nyingine nchini kuiga mfano wa wilaya hiyo kwa kuunda sheria ndogo ndogo zitakazowaongoza katika sekta  ya mifugo.
   Ng’ombe aina ya Borani inayomilikwa na muwekezaji kampuni ya Overland katika Ranchi ya Mzeri , Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

   Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Luhaga Mpina akiongea  vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi wa  baadhi ya vitalu katika Ranchi ya Mzeri iyopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, na kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Overland Bw. Faizal Edha.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Handeni kulia Godwin Gondwe pamoja na wataalam kutoka Wizarani na Mkoani Tanga wakiwa katika zoezi la kukagua baadhi ya vitalu  vilivyopo katika Ranchi ya Mzeri Wilayani Handeni.
  Aliyesinama wa pili kulia ni Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakiangalia sehemu ya kunyweshea ng’ombe maji katika ranchi ya Mzeri wilayani Handeni.

  0 0


  NA Estom Sanga-ZANZIBAR

  Takribani wananchi 14,420 wa Shehia za Vijibweni ,Mbiji,Karange,Mtambile na Njia ya Mtoni Kisiwani Zanzibar wamepunguziwa adha ya kufuata huduma ya vipimo vya afya mbali na eneo lao baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kugharamia ununuzi wa kifaa tiba kilichokosekana tangu kuanza kwa kituo hicho .

  Akikabidhi Kifaa hicho kwa uongozi wa kituo cha Afya cha Donge Vijibweni, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ Mhe. Mihayo Juma Nung’a amepongeza hatua hiyo ya TASAF ambayo amesema inatekeleza kwa vitendo lengo la serikali la kuwaondolea wananchi kero ya upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ile ya afya.

  “ninawaagiza kutunza mashine hii ili wananchi waweze kunufaika kwa muda mrefu na kusahau madhira waliyokumbana nayo kabla ya kupata mashine hiyo” alisisitiza Mhe.Mihayo.

  Aidha Naibu Waziri huyo amezungumzia umuhimu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF kuwa ni mkombozi kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika umaskini mkubwa na hivyo kuzitaka kaya husika kutumia ruzuku inayotolewa kwa uangalifu huku akitilia mkazo suala la uanzishaji wa miradi ya kiuchumi ili kujiongezea kipato.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ambaye pia alihudhuria hafla ya kukabidhi mashine hiyo amesema taasisi yake itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha maisha ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo ile ya afya.

  Amesema kwa kutambua umuhimu wa uboreshaji wa afya za wananchi, TASAF imeweka kipengele cha afya kuwa moja ya masharti katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kuhudhuria kliniki kila mwezi.

  Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Miza Ali Ussi amesema kituo kilikuwa na ukosefu mkubwa wa mashine hiyo na hivyo kuwalazimu wananchi kufuata huduma hiyo katika maeneo yaliyoko mbali na eneo hili jambo lililokuwa linawatatiza kwa kiwango kikubwa. 

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Mihayo Juma Nung’a (aliyevaa shati la drafti) akimkabidhi mashine ya kupimia damu afisa tabibu Miza Ali Ussi wa kituo cha afya cha Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.Kifaa hicho kimenunuliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF-.Kushoto nio Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bw. Ladislaus 
  Mwamanga.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga,(aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia maradhi kilichonunuliwa na TASAF kwa ajili ya kituo cha Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.Kushoto kwake ni Naibu Waziri katika ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa SMZ,Mhe. Mihayo Juma Nung’a.
   Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ,Mhe. Mihayo Juma Nung’a  (hayupo pichani) katika hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia maradhi iliyonunuliwa na TASAF kwa ajili ya kituo cha Afya cha Donge Vijibweni huko Zanzibar. 
   Sehemu ya jengo la kituo cha Afya kinachohudumia takribani wananchi 14,420 kilichojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF katika eneo la Donge Vijibweni kisiwani Zanzibar.

  0 0

  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Seleman Jafo wa kulia akitoka kukagua mradi wa bwawa kubwa la kuhifadhia maji lililopo kata ya Chole ambalo litaweza kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani kuweza kupata huduma ya maji.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Selemani Jafo akikagua daraja la Gologombe ambalo limejengwa katika kata ya mafizi wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Kisarawe kwa ajili ya kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maenedeleo na kujione a changamoto zilizopo.
  Waziri Jafo baada ya kutembelea mradi wa shule ya msingi Mtengwe ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati wa baadhi ya madarasa ambayo yalikuwa yapo katika hali mbaya kutokana na uchakavu wa miundombinu yake.

  NA VICTOR MASANGU, KISARAWE 

  WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ameahidi kulivalia njuga suala la baadhi ya wakandarasi hapa nchini ambao ni wazembe na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati waliopangiwa ikiwemo sambamba na watendaji wavivu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha juhudi za seriklali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi na badala yake watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

  Jafo ametoa kaui hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu ya barabaraba, afya pamoja na sekya sambamba na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ii kuweza kusisikiliza na kizitafutia ufumbufu wa kudumu.

  Alisema kwamba alibaini kuna wakandarasi wengine wanapewa kazi lakini cha kushangaza wanakamilisha mradi ambao unajengwa chini ya kiwango kinachotakiwa hivyo amesema kamwe hawezi kulifumbia macho suala hilo na kuongeza kuwa atakayebainika amehusika kuhujumu miradi hiyo atafikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi ii iwe fundisho kwa wengine.

  Hata hivyo katika hatua nyingine Jafo aliwatoa wasi wasi wananchi wa Kisarawe, Mkoani Pwani kuimaliza changamoto sugu ya iliyodumu kwa kipindi cha muda mrefu cha ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo amebainisha serikali ya awamu ya tano imetenga kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji ambao chanzo chake kitaanzia mto Ruvu na kusambazwa katika maeneo mbali mbali ya Kisarawe.

  “Kuhusiana na changamoto hii ya wananchi wa kisarawe juu ya tatizo la ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu nadhani sasa linakwenda kufikia mwisho kwani serikali imeshatenga bilioni 10 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji ambao utaanzia kutokea mto Ruvu hivyo nipende kuwahakikishia kuwa tatizo hilo linakwenda kufikia mwisho na wananchi wataweza kupata maji ya uhakika,”alisema Jafo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile amesema kwamba kukamilika kwa baadhi ya miradi mbali mbali hususan wa kivuko cha daraja la Gologombe kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi ambao hapo awali walikuwa wanapata adha kubwa ya kuvuka hasa katika kipindi cha masika na kushindwa kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

  “Kwa kweli hapo awali wananchi wetu walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ya usafiri, maana kuvuta ilikuwa wanapata tabu sana hasa katika kipindi cha mvua hivyo daraja hii litakuwa ni msaada mkubwa sana na wataweza kupata fursa za kuendelea kufanya shughuli zao mbali mbali za maendeleo, “alisema Mwenyekiti huyo.

  Pia aliongeza kuwa ujenzi huo wa kivuko cha darala imegharimu kiasi cha shilingi milioni 127, ambapo kwa sasa limeshafikia hatua za mwisho, ambapo aliwaomba wananchi hasa wanatumia njia hiyo kuhakikisha kwamba wanaitunza miundombinu ya barabaraba ili iweze kudumu kwa kipindi cha muda mrefu bila ya kiharibika.

  Akiwa katika ziara yake ya Kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Kisarawe Jafo ameweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya barabara, kukagua madaraja, shule za msingi, na sekondari ,vituo vya afya, pamoja na ujenzi wa bwawa la kutunzia maji lililopo katika kata ya chole.

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifurahia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, wengine ni Mkurugenzi wa Mashamba na Mifugo Kiwanda cha, Rob Nethersole na Mratibu wa SAGCOT Ofisi ya Waziri Mkuu, Girson Ntimba.


  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa.  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj, wakati alipofanya ziara mkoani Iringa, kukagua viwanda vinavyofanya kazi na Kongani ya Ihemi inayotekelezwa na Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, kiwanda hicho kinahitaji tani 7,000 za Soya kwa siku kwa ajili ya uzalishaji lakini hadi sasa wanapata tani 2,000 kwa siku hivyo kupelekea kiasi kingine kuagizwa kutoka nje ya nchi. Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.
  Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kusindika maziwa, Asas Milk Diary mkoani Iringa, kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika lita 50,000 za maziwa kwa siku lakini kinapata lita 20,000 kwa siku. Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.  Na.Mwandishi Maalum.


  Katika moja ya jitihada za kuhakikisha mafanikio ya mkakati wa kujenga Uchumi wa Viwanda nchini serikali imeendelea Kuboresha mazingira bora ya biashara kwa wawekezaji kwa kuendeleza kilimo ili kuchochea maendeleo na sekta ya kilimo kupitia Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

  Akizungumza baada ziara ya Kukagua shughuli za SAGCOT mkoani Iringa kwa kutembelea kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Silverlands na kiwanda cha kusindika Maziwa cha Asas Diary Milk, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora alifafanua kuwa njia ya kuliwezesha Taifa kuwa na uchumi imara utakaohimili ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa ni kuboresha mazingira ya Uwekezaji.

  “Tunaweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa kiuchumi katika sekta ya kilimo hasa kwa kuishirikisha sekta binafsi na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, tunao Mpango wa SAGCOT tunataka kutumia fursa hizi katika kilimo kukuza uchumi, tuondokane na kilimo cha kujikimu na kuhamia kilimo biashara. Wawekezaji wanahitaji kuona utayari wa wakulima ili wawekeze. Tukumbuke zaidi ya asilimia 70 ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo”, alisema Kamuzora.

  Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ,Wamoja Ayoub, alifafanua kuwa tayari mkoa huo umeanza kupata mafanikio kwa utekelezaji wa SAGCOT mkoani humo kwa wakulima kuweza kulimochenye tija , kuongeza thamani mazao yao na kupata masoko ya uhakika.

  “Kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya pembejeo kumekuwa na ongezeko la tija kwa mazao kutoka tani 2.2 za mahindi kwa hekta kwa msimu wa mwaka 2014/2015 hadi tani 2.7 za mahindi kwa hekta kwa msimu wa mwaka 2016/2017na Mpunga kutoka tani 3.2 kwa msimu wa mwaka 2014/2015 hadi tani 4.6 kwa msimu wa mwaka 2016/2017”, alisema Wamoja.

  Kwa nyakati tofauti wawekezaji katika Kongani ya Ihemi, Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara Kiwanda cha kuzalisha Vifaranga na chakula cha kuku Silverlands, Sean Johnson na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa Asas Diary Milk, Fuad Faraj, walieleza kuwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na kupunguza gharama za kufanya biashara, wameiomba serikali kufanya mapitio ya kodi hasa katika uzalishaji wa bidhaa za viwanda.

  Wawekezaji hao walibainisha kuwa serikali itafanikiwa zaidi katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwa kutaanzishwa kituo kimoja cha kufanyia kazi “One stop Centre” kwa mamlaka zote za udhibiti, usimamizi na uratibu wa shughuli hizo kwa Kongani ya Ihemi (Iringa na Njombe).

  Pia walishauri serikali kuweka ruzuku katika mbegu za viazi na alizeti za viazi mviringo na ili kuwezesha wakulima wadogo kumudu kununua mbegu bora zitakazo ongeza uzalishaji na kuchangia malighafi za viwanda vilivyo katika kongani ya Ihemi (Iringa naNjombe)

  Awali, akieleza utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga alieleza kuwa wanaendelea kuboresha ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuweza kuboresha mazingira bora ya uwekezaji na biashara katika kongani ya Ihemi

  “Tunaamini kilimo ni fursa kwani ni wazi wawekezaji wanategemea kwa kiasi kikubwa mavuno na mazao bora ili kuzalisha bidhaa nzuri. Uchumi wa viwanda unategemea kilimo chenye tija na ninyi mnatuhakikishia kuwepo tija hiyo.”

  Programu ya SAGCOT inatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Katavi na imegawanywa katika kongani (cluster) sita za Ihemi (Iringa na Njombe), Rufiji, Kilombero, Mbarali, Ludewa na Sumbawanga. Program hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2011 na mwisho wake mwaka ni 2030. WafadhIli wa SAGCOT ni Serikali ya Tanzania, Shirika la misaada la Uingereza (UKAID), Shirika la misaada la Marekani(USAID), Benki ya Dunia (WBG), Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na AGR.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na  Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam jana . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo
  Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dos Santos Silayo akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
  Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRTBaadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
  Picha na Lusungu Helela-MNRT


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia

  Wakala ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.Amesema uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.

  Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam.Amesema TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi.

  Wakati akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe kipaumbele.Katika hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.

  Amesema chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo kujali ubora wake.Amesema kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe hafifu.

  ‘’ Halafu unaenda kumshindanisha na mtu anayeuza mbao ambazo miti yake imevunwa ikiwa na miaka 18 haziwezi kushindanishwa ubora kati ya mbao hizo lazima kiwepo chombo cha kuthibiti kama vile kwenye chakula kuna TFDA na kwenye bidhaa kuna TBS’’ alisema

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga amemtaka kila mtumishi ahakikishe anapambana na rushwa kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa TFS Prof. Silayo kuwahamisha watumishi pale inapotokea fununu kuwa mtumishi fulani anajihusisha na rushwa hata kama bado haijathibitika kwa vile fununu hizo haziwezi kuanza tu bila ya kuwa harufu ya mazingira ya kupokea rushwa yanayotengenezwa.

  Amesema katika suala la ugawaji wa vitalu kuna vitendo vya rushwa vinafanyika kwani baadhi ya watu wanapewa vibali vya kuvuna kwa muda wa miezi minne lakini uvunaji ule unaendelea kwa muda wa mwaka mmoja wakati ilitakiwa kitalu hicho kivunwe kwa muda wa wiki mbili tu.’’ Alisema

  ‘’Mimi sikurupuki kwenye maamuzi yangu na sio kwamba nasema nimekuja kuwatumbua leo lakini nina taarifa nyingi kuhusiana na rushwa inavyotembea katika ugawaji wa vitalu’’‘’Mtendaji ifanyie kazi taarifa hii ya rushwa ila nikiona mambo hayaendi kama ninavyotarajia nitakuja kivingine. alisisitiza

  Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Hasunga ameiagiza TFS iongeze ukusanyaji wa mapato kwa vile mapato yalipo sasa bado hayatoshelezi na yaliyokusanywa yatumike vizuri.‘’Taarifa nilizonazo kuna maeneo manne mapato yanavuja paangalieni hapo mparekebishe ‘’ alisema

  Wakati huo huo, Hasunga ameiagiza TFS ianze kuwekeza katika maeneo ambayo inaona inaweza kuzalisha zaidi kwa mfano kwenye maporomoko ya Kalambo ili iweze kuongeza mapato‘’Yale maporomoko ukikaa Zambia huwezi kuyaona vizuri ila ukikaa Tanzania unayaona vizuri’ tumieni fursa hiyo baada ya miaka miwili ijayo kinaweza kikawa kituo kikubwa cha utalii nchini.’’Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo amemhakikishia Naibu Waziri Hasunga kuwa atatekeleza maagizo yake yote aliyoyatoa kwa maslahi mapana ya TFS.

  0 0


  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House) katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji ch a Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo, Juzi 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.  Na Mathias Canal, Mtwara

  Wakufunzi wa Vyuo vya Kilimo kote nchini wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kufanya kazi kwa Weledi, Ubunifu na Maarifa ili kuongeza tija katika majukumu yao ya kufundisha wanafunzi ambapo baadae wanazalisha wataalamu mbalimbali katika sekta ya Kilimo.

  Kauli hiyo imetolewa juzi 22 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini.

  Alisema kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazowawezesha kuwa na kipato cha ziada kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

  Alisema kuwa kufanya hivyo kutawanufaisha kuwa na kipato kitakachowawezesha kuendesha chuo pasina kutegemea serikali kwa kina jambo ambalo litapunguza malalamiko dhidi ya serikali kufanya kila kitu.

  Aidha, alisisitiza viongozi wa vyuo vyote vya Kilimo nchini kutumia vyombo mbalimbali vya Habari sambamba na mitandao ya kijamii ili kutangaza maudhui ya vyuo na kozi zinazofundishwa ili kurahisisha wanafunzi kupata wepesi katika uchaguzi wa vyuo vya kusoma.

  Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembelea na kujionea miundombinu ya Taasisi na kazi za mafunzo ikiwa ni pamoja na kuangalia shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali.

  Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo alimpongeza Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Kilimo kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na hatimaye kuteuliwa kumsaidia katika majukumu yake ambapo pia ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.

  0 0  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya ya Kisarawe katika ukaguzi wa mradi wa maji Kwala-Chole.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kisarawe wakikagua ujenzi unaoendelea wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mitengwe.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua nyumba ya daktari ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi katika kituo cha Afya Maneromango.
  Baadhi ya miondombinu iliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Maneromango.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amezipongeza kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’ hapa nchini kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye ubora na inayozingatia thamani ya fedha.

  Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe ambapo alifanikiwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi Mitengwe, Kitonga Mango, Boga, mapoja na kituo cha Afya Maneromango.

  Amesema ujenzi huo umetumia utaratibu huo wa ‘Force Account’ ambapo miundombinu mbalimbali imejengwa kwa gharama nafuu pamoja na kutoa ajira kwa mafundi wanaopatikana katika maeneo miradi hiyo inapotekelezwa.

  Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kukagua jengo jipya la upasuaji, maabara, wodi ya kinamama, nyumba ya daktari, jengo la kuhifadhi maiti, vyumba 12 vya madarasa mapya, matundu ya vyoo 30, pamoja na Ofisi za walimu 3.

  Mbali na hilo, Waziri Jafo amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kwala-Chole ambao unagharimu zaidi ya sh. billion 1.8 na ameagiza mradi huo ukamilike ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi 2018.

  Amewataka wananchi kote nchini kushiriki kulinda na kusimamia rasilimali fedha zinazopelekwa katika vijiji vyao kwaajili ya maendeleo.

  0 0

  Chama kikuu cha Ushirika Cha Masasi,Mtwara Cooperative Union(MAMCU) kimelazimika Kusimamisha Minada ya zao la Korosho Iliyokuwa Ikifanyika kila Ijumaa kwa Kipindi cha Wiki Mbili kutokana na Wakulima Kukusanya Korosho ambazo hazijakauka hali inayoathiri Soko hilo.

  Kaimu Meneja wa MAMCU Potency Rwiza amesema Kupungua kwa mzigo katika Maghala yanayosimamiwa na Chama chake, pamoja na kuwapo kwa Korosho ambazo hazijakauka kunaisababisha Korosho kushuka Kilo na Kupungua Ubora Mara Inapouzwa kwa Wanunuzi ambao Wengi wao kutoka Nchi za Nje.

  Hata Hivyo Wakulima wa Korosho wa Mkoa wa Mtwara wanafurahia Kuuza korosho zao kwa Shilingi Elf4,055 kwa kilo, Bei ambayo ni kubwa ukilinganisha na Minada iliyopita.

  Mpaka Kufikia Sasa Chama kikuu cha Ushirika cha MAMCU kimefika Mnada wa Tisa na tayari wameuza Korosho Tani Elf 84 na 97 Zenye Thamani ya Shilingi Billion 332.

  Pichani ni Kaimu Meneja wa MAMCU Potency Rwiza akizungumza na Wakulima wa eneo la Ziwani Mtwara Vijijini katika Mnada wa Tatu wa Zao LA Korosho.Pichani.

  0 0

  Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wamewalalamikia askari wa pori la Akiba la Kigosi Myobosi kwa madai ya  kuwanyanyasa pindi wanapokamata ng'ombe zao katika pori hilo. 

  Wakiongea mwishon mwa wiki ,mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega,wafugaji hao wamesema kuwa Mifugo yao inauzwa bila kufuata utaratibu pindi inapokamatwa kwenye pori hilo na matokeo yake wafugaji wanabaki Maskini. 

  "Magufuli anafanya kazi nzuri sana na hatuamini kabisa kuwa hapendi Mifugo,lakini kuna baadhi ya watendaji wake sio waadilifu kabisa,askari wa Pori la akiba Kigosi Myobosi wakikamata ng'ombe hawatupi fursa ya kulipa faini,badala yake wanataifisha Mifugo yetu na kuipiga mnada bila kufuata utaratibu wa serikali uliowekwa na sisi tunabaki Maskini"alisema mfugaji mmoja. 

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko ameiomba serikali kutafuta masoko ya uhakika ya mifugo Ili  wafugaji wewe na uhakika wa soko la Mifugo yao. 

  "Tunaomba serikali ijenge viwanda vya kutosha vya kuchakata nyama Ili wafugaji wenye Mifugo mingi waweze kuuza Mifugo yao,inayobaki wafuge kwa tija" 

  Kwa Upande wake naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega amesema kuwa Sheria ya Maliasili na utalii inaruhusu kupigwa mnada Mifugo yote inayoingia kwenye mapori ya akiba. lakini wamepeleka mswada Bungeni ili kuzipitia upya sheria hizo .

  "Katika Bunge la mwezi wa pili 2018,sheria hizo zitapitiwa upya,nawaombeni sana ikifika wakati huo mjipange vizuri nanyi mtoe maoni yenu" 

  Awali katibu tawala wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw.Paul Cheyo, akitoa taarifa fupi ya Wilaya hiyo alimwambia Mhe.Ulega kuwa wao wametekeleza zoezi la kitaifa la upigaji chapa mifugo kwa Asilimia 73. 

  "Halmashauri inaendelea na zoezi la upigaji chapa mifugo.Wilaya yetu ina jumla ya ng'ombe 130,750, hadi sasa ng'ombe waliopigwa chapa ni 95,743 sawa na asilimia 73".alisema Cheyo.
   Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kupokea  taarifa fupi ya  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
   Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wafungaji  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
   .Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji  Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko  (kushoto)akizungumza katika mkutano huu.
   Mmoja wa wa wafungaji wa akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
   Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.
   Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

  0 0

  Mayage S.Mayage enzi za uhai wake.

  Tunasikitika kuwatangazia kuwa mwenzetu Mayage S Mayage tuliyekuwa tukijichangisha kwa ajili ya matibabu yake, ametutoka

  Kwa mujibu mke wa Marehemu,Digna Mayage, mwenzetu amefariki majira ya saa 3 asubuhi, leo Desemba 25, 2017, kwenye hospitali ya Misheni Mbweni alikokuwa amelazwa

  Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Mbweni.Tutapeana taarifa zaidi kadri tutakapozipata

  Bwana alimtoa na sasa ameamua kumtwaa

  Jina lake lihimidiwe

  Ni Sisi Admins

  0 0

  Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa kuitupa rufaa iliyowasilishwa na mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha AFP.

  Mgombea huyo alikuwa akipinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ramadhan Kailima amesema leo jijini Dar es Salaam kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

  Kailima kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, NEC ilipokea rufaa moja kutoka kwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

  Pia NEC ilipokea rufaa mbili, ya kwanza iliwasilishwa na mgombea wa udiwani Kata Keza – Halmashauri ya Wilaya Ngara kwa tiketi ya CCM akipinga uamuzi wa Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea mgombea wa NCCR - Mageuzi.

  Wakati rufaa ya pili ilitoka kwa mgombea wa udiwani Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya Korogwe kwa tiketi ya CCM akipinga aumuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomuwekea mgombea wa Chama cha Wananchi(CUF.

  Kailima amefafanua kwenye kikao chake cha kawaida kilichofanyika Desemba 24, mwaka huu, NEC ilipitia rufaa hizo na kutoa uamuzi. Akizungumzia rufaa ya mgombea ubunge,NEC imekubaliana na uamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi,hivyo mgombea aliyekatiwa rufaa aendelee kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

  Amesema kuhsu rufaa za wagombea udiwani kata ya Keza na Kwagunda, NEC imekubaliana na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. “Hivyo wagombea udiwani waliokatiwa rufaa waendelee kuwa wagombea wa udiwani katika kata husika,”amsema Kailima.

  Ametumia nafasi hiyo kueleza tayari NEC imetuma taarifa ya uamuzi huo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili watoe taarifa kwa wahusika kuhusu kilichoamriwa.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bw. David Mahiba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakati wakitoa elimu kwa wananchi walioshiriki zoezi hilo kwa asilimia 100 kwa amani na upendo.
  Wananchi wakifuatilia mkutano huo.
  Vibanda vya wavamizi wa Hifadhi ya Misitu Gairo vikiteketezwa kwa moto.
  Miti ya asili yenye zaidi ya miaka 35 ikiteketezwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa. Sehemu kubwa ya miti hii ni miti ya mbao ngumu aina ya mitondoro.  Wadau wa mazingira nchini Tanzania wameombwa kujitokeza kuinusuru wilaya ya Gairo ambayo inahekari zaidi ya 3,000 zilizokuwa zimevamiwa waharibifu wa mazingira.

  Kauli hiyo imekuja hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa lakuwaondoa wavamizi wa Misitu ya Hifadhi kabla ya Disemba 31, 2017.

  Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo alipokuwa akiahitisha Bunge la mjini Dodoma Novemba 18, 2017. Kati ya maeneo ambayo yalikuwa na uvamizi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni Misitu ya Hifadhi Wilaya ya Gairo.

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walifanya vikao na wananchi huku wakipitia muhtasari ya vikao vya nyuma vya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa vya kuwaondoa wavamizi hao. 

  Aidha kupitia taarifa ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho ambayo ilisomwa na mwenyekiti wa Kijiji ikibainisha utengwaji wa maeneo mbalimbali zikiwemo ekari 1,000 za hifadhi walizogawiwa wananchi kwa ajili ya kilimo.

  Vikao vilifanyika kuanzia mwaka 2012 wakati huo Mkuu wa Mkoa akiwa Mhe. Kanali Machibya. Baadae Mkuu wa Mkoa alikuwa marehemu Joel Bendera ambapo nyumba kadhaa ziliteketezwa.Licha ya juhudi zote hizo bado wavamizi hao waligoma kutoka. 

  Hivyo basi, kwa kauli ya Waziri Mkuu zoezi limefanikiwa wavamizi wote wameondoka katika Misitu Hifadhi ya No. 30 Kijiji cha Kumbulu Kata ya Chanjale na nyumba zote ziliteketezwa kwa moto.Eneo hilo la misitu lina ukubwa wa ekari 3,000 limepakana na Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa na kutokana na uharibifu huo mkubwa umesababisha hali kubwa ya ujangwa kwa Gairo na maeneo ya Dodoma. 

  Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Gairo inategemeana sana na Mkoa wa Dodoma kwenye hali ya hewa kwani uwanda wa juu wa Gairo kupitia milima iliyopo Tarafa ya Nongwe ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa nzuri makao makuu ya nchi Dodoma. Ipo misitu mingine kama misitu ya Hifadhi ya Ukaguru ambayo ni namba tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Ipo misitu mingine mikubwa mitatu.

  Zoezi hilo liliweza kukamilika kwa asilimia 100 lkinachofuata ni operesheni kubwa ya kupanda miti inayofanywa Wilayani kwa usimamizi makini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Meneja wake, Bw. David Mahiba.

  0 0

  Kutoka kushoto, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem, Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa, na Mwenyekiti wa Dr Amon Mkoga Foundation. Ubalozi wa Kuwait umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.

  0 0

   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.  Luhaga Mpina akishiriki kusafisha shamba lake la mpunga lililoko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro alipokuwa kwenye wa mapumziko ya sikukuu ya  Krismas leo.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akishirikiana na wafanyakazi wake kusafisha shamba lake liliko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga leo wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas.
  Moja ya matrekta yaliyoko katika shamba la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina yakiendelea na shughuli za kulima kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga wakati Waziri huyo (hayupo pichani) alipokwenda kushiriki shughuli za shamba wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas leo.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Ule msimu wa watu kufurahi na kujumuika umewadia tena!

  Haina ubishi kwamba sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka ambayo huambatana na sikukuu za Krismasi (Desemba 25) na mwaka mpya ndiyo huwa na shamrashamra nyingi zaidi duniani.
  Ni kipindi hiko ndicho familia, ndugu, jamaa na marafiki hukutana kwa pamoja na kufurahia kuumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya unaofuatia. Mbali na hilo, kutokana na shughuli za mwaka mzima katika kutafuta kipato na kujenga maisha, hiki ni kipindi ambacho watu hupumzisha mwili na akili kwa kufurahia matunda waliyoyachuma kwenye kipindi cha mwaka mzima lakini hata kutafakari namna watakavyoukabili mwaka mpya ambao huja na majukumu na matarajio mapya.


  Katika kipindi hiki cha sikukuu mambo mengi hutokea ambayo kwa namna moja ama nyingine endapo hautokuwa makini yatakuacha kwenye hali mbaya. Jumia Travel ingependa kukumbusha wakati ukiwa kwenye ari ya shamrashamra za msimu huu wa sikukuu kuepuka kuyafanya mambo yafuatayo.


  Tumia muda wa kutosha na familia. Itapendeza endapo sikukuu ya Krisimasi na mapumziko ya mwisho wa mwaka ukazitumia kufurahia na familia yako. Ni kipindi ambacho miongoni mwenu mpo likizo, watoto wamefunga shule na ndugu hupata fursa ya kutembeleana. Ni jambo la kawaida kuona watanzania mbalimbali kilo kona ya nchi wakifurika kurudi makwao au wengine wakialikana ili kufurahia kipindi hiki. Kamwe usiipoteze fursa hii ya kujumuika na wale uwapendao kwani hutokea mara moja tu kwa mwaka na ni vema ukaitumia ipasavyo.

  Zingatia kiwango na aina ya vyakula unavyokula. Kwa sababu katika kipindi hiki kunakuwa na vyakula vya kila aina, ndiyo ukawa unakula tu bila ya kuwa makini. Ulaji wa vyakula tofauti bila ya mpangilio na kiwango maalumu unaweza kukusababishia madhara kwenye mwili wako na kukusesha raha ya kufurahia sikukuu. Hivyo basi, kama inawezekana basi jaribu kuendana na utaratibu wako uliojiwekea wa kula. Usizidishe kwa sababu siku hii vyakula ni vingi.


  Kuwa makini na kiasi cha pombe. Ndiyo ni sikukuu, hauna wajibu siku inayofuatia au mtondogoo. Lakini hii isiwe sababu ya kutokuwa makini na kiwango cha pombe unachokunywa. Unywaji wa pombe kuzidi kiwango unaweza kukusababishia mbali tu na uchovu kwenye mwili wako na kushindwa kufurahia matukio ya muhimu na familia yako bali pia hata madhara kwako na watu wanaokuzunguka. Jaribu kuwa mvumilivu kwa kipindi hiki kifupi, furahia kwa kunywa kiasi na familia pamoja na wapendwa wako. Kwa kuongezea, unywaji wa pombe kupitiliza unaweza kukusababishia ukaingia matatani na vyombo vya sheria, kwa sababu ni kipindi cha mapumziko haimaanishi kwamba sheria na taratibu za nchi zimelala.


  Tumia pesa kwa makini. Kipindi hiki pia watu wengi hushuhudia wakitumia kiwango cha pesa bila ya kutarajia. Ni vema ukawa umetenga kiwango fulani cha fedha kwa ajili kutumika kwenye msimu huu wa sikukuu. Kama haukufanikiwa kutenga mapema bajeti ya kutumika kipindi hiki basi hakikisha fedha utakayoitumia haitaathiri matumizi yako ya baadaye. Unaweza kufanya hivyo kwa kubana matumizi kwani sio lazima kuwa na shamrashamra kubwa. Kwa sababu ni kipindi cha mwisho wa mwaka na tunafahamu namna maisha yetu watanzania yalivyo, mwaka mpya huja na majukumu kama vile kodi za nyumba, karo za shule, pango za sehemu za biashara, leseni au vibali vya vyombo vya moto nakadhalika.
  Usijibane sana, furahia! Inawezekana mipango haijakaa sawa kwenye msimu huu wa sikukuu hivyo kukunyima fursa ya kufurahia vilivyo. Kumbuka, kipindi hiki hutokea mara moja tu kwa mwaka na hautakiwi kujuta sana kwamba kwa nini haukufanikiwa. Ni mafanikio kuwa mzima mpaka kufanikiwa kuuona msimu huu wa sikukuu kwani wengine hawajafanikiwa. Jumia Travel inaamini kwamba kwa kuumaliza mwaka ukiwa na matumaini kutakupa fursa ya kujipanga vema zaidi na mwaka ujao.

  0 0

  Kutoka kushoto, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem, Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa, na Mwenyekiti wa Dr Amon Mkoga Foundation. Ubalozi wa Kuwait umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.

  0 0

  Mayage S.Mayage kuzikwa Mbweni Jijini Dar Alhamis

  MWANDISHI wa habari mwandamizi, Mayage Mayage, (56), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda.

  Mayage amekutwa na umauti katika Hospitali ya Misheni ya Mbweni, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili.Taarifa kutoka kwa mdogo wake Emmanuel Mayage, alisema kuwa madaktari waligundua kaka yake kuugua saratani na kifua kikuu (TB).

  Emmanuel alisema kuwa Mayage atazikwa Alhamis Desemba 28, 2017 katika makaburi ya Mbweni, eneo linaloitwa Maputo.Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Mbweni Kijijini, eneo la Maputo ambako ndugu na jamaa wanakutana.


  NAMNA YA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU.


  Msiba uko nyumbani kwake Mbweni Kijijini, Dar es Salaam, eneo la Mbweni Maputo,siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.

  Ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni, unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia inayokwenda kushoto ituate hiyo.Ifuate barabara hiyo kwa kuongozwa vibao vinavyoelekeza kuelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu, ambaye ni maarufu kama Mzee wa Magazeti.

  Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Magamoyo, shukia  kituo cha Mianzini Bunju.
  Hapo chukua bodaboda kwa gharama ya 3000/= hivi hadi mbele kidogo ya Mbweni Misheni Hospitali.Hapo kata kushoto na muelekeze bodaboda afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.

  Kwa wenye usafiri binfsi; unaweza kufika kwa njia mbili:

  1.Ukitoka Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju.Hapo kuna barabara ya lami kuelekea Mbweni.Ifuate hadi Mbweni Misheni Hospitali.Baada ya hapo kata kushoto.Fuata vibao vya msiba.

  2.Ukitoka Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni,fuata njia ya daladala, pita mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza kufuata maelekezo ya vibao vya msiba.


older | 1 | .... | 1470 | 1471 | (Page 1472) | 1473 | 1474 | .... | 1897 | newer