Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1468 | 1469 | (Page 1470) | 1471 | 1472 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Picha zote na KAJUNASON/MMG. 
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu akielezea mikakati ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitolea ufafanuzi juhudi za wizara yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. 
   Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti TBA, Mjumbe Baraza la Taifa mpango huduma jumuishi za kifedha, Dkt. Charles Kimei akitoa salamu zake za shukrani kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim kwa kuweza kuwazindulia Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amenyanyua kitabu cha mpango kazi wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, mwingine kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitambu cha mpango kazi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitabu cha mpango kazi, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. 
  Wajumbe walioweza kuandaa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliozinduliwa leo katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. 

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza kuanzishwa kwa mtaala wa elimu ya fedha mashuleni ili kuwajengea uwezo vijana wa kujua na kutambua kujua matumizi sahihi ya fedha. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 21, 2017) wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

   Akizindua mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, Waziri Mkuu alisema uwepo wa miundombinu muhimu iliyojengwa na inayojengwa na Serikali; na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini; na ongezeko la watumiaji wa mitandao ya simu na huduma za mawasiliano ni kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo. 

  “Kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo ni uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi. Tukijenga vizuri juu ya misingi hii tunaweza kupiga haraka hatua za maendeleo katika sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla wake,” alisema. 

  Alisema ameupitia mpango huo na kubaini kuwa umeainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hii katika harakati zake za kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwa mpango huo umeainisha fursa ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. “Changamoto zilizoainishwa ni pamoja na kuimarisha utawala wa matumizi ya fedha taslimu kwa ajili ya malipo badala ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya malipo; kukosekana kwa utambulisho wa kipekee (unique identification) kwa Watanzania walio wengi; uhalifu kwa njia za mtandao (cyber-crime); kukosekana kwa mifumo madhubuti ya taarifa za kutosha za watumiaji wa huduma za fedha na dhamana zao; na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha,” alisema. 

  Aliwataka wajumbe wa Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za kifedha waaandae mpango mahsusi wa kutoa elimu vijijini kuhusu faida na umuhimu wa huduma jumuishi za kifedha Tanzania, na akasisitiza kuwa kipaumbele kitolewe kwa makundi maalum ya vijana na wanawake. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema wataalam wa uchumi duniani wanaeleza kwamba jamii ambayo imejijengea utamaduni wa kujiwekea akiba katika asasi za kifedha ina fursa kubwa ya kupata maendeleo endelevu na ya haraka.

   “Hii ni kwa sababu uwekaji akiba ndiyo kiini na nguzo ya uwekezaji wa miradi ya maendeleo, na bila uwekezaji wa miradi ya maendeleo, hakuna maendeleo. Nchi zote zilizoendelea zimejijengea utamaduni huu wa wananchi wake wa kujiwekea akiba,” alisisitiza. Alitoa wito kwa wajumbe hao kuhakikisha kuwa mpango huo unajikita zaidi katika kuimarisha utamaduni wa Watanzania kujiwekea akiba kwa kila aina ya mapato ambayo mwananchi anapata, iwe katika kilimo au biashara au ufugaji au uvuvi au shughuli nyingine yeyote anayofanya ya maendeleo.

   “Taarifa ya Mpango wa Pili wa Huduma Jumuishi za Kifedha inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania (watu wazima) wanamiliki simu za mkononi na wanatumia simu hizo kufanya miamala ya kifedha. Kwa msingi huo, nashauri kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya wadau wa taasisi za fedha na wadau wa TEHAMA ili kuimarisha matumizi na mtandao wa kifedha vijijini ili iwe kichocheo cha uchumi,” alisema. 

  Mapema, Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu alisema matokeo ya tathmini iliyofanyika yanaonyesha kwamba wananchi walio karibu na huduma za fedha wameongezeka kufikia asilimia 86 mwaka 2017 ya Watanzania (watu wazima) ikilinganishwa na asilimia 29 ya mwaka 2012. Pia alisema Watanzania wanaotumia huduma za fedha hasa kupitia asasi za kifedha na mitandao ya simu wameongezeka kutoka asilimia 17 mwaka 2009 hadi asilimia 11 mwaka 2006, na hadi sasa (2017) takwimu zinaonyesha kwamba wananchi asilimia 65 wanatumia huduma za kifedha nchini.

  “Kutokana na mafanikio haya makubwa, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika na ya sita duniani kwa kuweka mazingira bora ya utoaji na upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi,” alisema. Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt, Charles Kimei alisema wenye mabenki wana haja ya kubadili mtazamo na kujikita kwenye ngazi ya chini ambako kuna watumiaji wengi zaidi.

   “Wenye kampuni za simu wameonyesha kuwa inawezekana kufikisha huduma kwa watu wa chini kupitia simu zao, nasi tukitumia vifaa hivyo tunaweza kuwafikia wananchi wengi kwa kuwapa huduma zetu,” alisema. Alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa ngazi zote wakiwemo wa mikoa, wilaya na wabunge walifanye suala la uwekaji akiba liwe ajenda kuu ya mikutano yao kwa kuwaelezea wananchi umuhimu wa suala hilo.

  0 0

  Wanafunzi watano wa shule za serikali  hapa nchini wameshinda shindano la uchoraji ambazo zinaeleza tukio halisi ambalo limetaribiwa na Jubilee Insuarance. Walioshinda wamepewa zawadi za bima za afya za jubilee insurance pamoja na kuahidiwa kushomeshwa elimu ya sekondari pindi watapofaulu.

  Shindano  hilo liliendeshwa kwa mikoa saba ambapo wanafunzi watano wameibuka kidedea baada ya kuchora picha hizo.Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba ameishukuru Jubilee Insurance kwa kuanzisha shindano hilo ambalo limeweza kuwapa maisha wanafunzi watano kwa kuwa na uhakika wa afya zao pamoja na kusomeshwa elimu ya sekondari watapofaulu darasa la saba.

  Amesema kuwa waendelee kuandaa mashindano mengi ambayo yatasukuma wanafunzi kushiriki  kutokana na kuwa na uhakika wa zawadi.Nae Mwenyekiti wa bodi  wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji amesema kuwa Jubilee Insuarance sasa imejikita katika kutoa huduma kwa jamii hasa kwa kaya maskini.

  Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya amesema kuwa mtoto wake amemfanya kufika Dar es Salaam na kuwa na uhakika wa afya kupata bima ya afya ya Jubilee Insuarance. 
  Amesema kuwa Jubilee Insuarance imekuwa ya kwanza kuwafikia wananchi wa kawaida kwa kutafuta vipaji vya wanafunzi.
  Mwenyekiti wa bodi  wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji akizungumza na wageni waalikwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda kwenye shindano la uchoraji wa michoro inayomuweka mtoto huru lililofanyaka hapa nchini.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba akitoa shukrani kwa Jubilee Insurance kwa kurudisha fadhira kwa jamii pamoja na na kuwasisitiza wajikite hasa kwa kaya maskini.
   Mkuu wa Kitengo cha Fedha Jubilee Life Insuarence Corparition, Helena Mzena akitoa historia ya ya shindano lililoshirikisha shule za msingi mbalimbali hapa nchini kwenye shindano la uchoraji kwa wanafunzi wa darasa la Tatu wakati wa ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi watano waliofanya vizuri. 
  Mkurugenzi Mkuu wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Dipankar Acharya akiwashukuru akizungumza jambo wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi waliofanya vizuri kwenye shindano la uchoraji.
   Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba akimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa shule ya msingi Msasa, Khadija Mohamed Ali aliyeshinda kwenye shindano la uchoraji.
  Meneja Mkuu wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Sumit  Kumar Gaurav (kushoto) akimkabidi zawadi Mwanafunzi wa Shule ya msingi Katete, Atupele Wiston wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kuchora.
  Picha ya pamoja.


  0 0
  0 0

  Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni Bima ya Mgen Tanzania Insurance Limited katika hafla ya kufunga mwaka iliyowashirikisha wateja na baadhi ya mawakala wa kampuni hiyo hapa nchini ili kufurahi pamoja, Hafla hiyo imefanyika jana katika makao makuu ya kampuni hiyo Masaki jijini Dar es salaam .
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi zawadi Hope Kaiza liyefanya kazi kwenye kampuni ya Mgen Tanzania kwa miaka 10 kwa mafanikio makubwa kushoto ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye .
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akifurahia jambo mara baada ya kuwakabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Lumumba Insurance Brokers Limited Bw. Jamal Lardhi kushoto na Tiraib Maghembe Mkuu wa Idara ya Fedha Lumumba Insurance Brokers Limited katikati anayewapongeza ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akimkabidhi zawadi Bw. Sudi Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group Ltd kwa ushirikiano wa kampuni hiyo kwa Mgen Tanzania Insurance katikati ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. Charles Sumbwe akizungumza na wafanyakazi pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo huku Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akisikiliza kushoto ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye 


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. Charles Sumbwe akizungumza na wafanyakazi pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo huku Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akipiga makofi.


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. Charles Sumbwe akizungumza huku akiwa na baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali katika kampuni hiyo.


  Bw. Ernest Kirumbi Mkuu wa Huduma Kampuni ya Mgen Tanzania Insurance Limited akikaribishwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.


  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.


  Mkuu wa Masoko MGen Tanzania Bw. Lugano Mkisi akiwa na kamati ya maandalizi ya hafla hiyo iliyoundwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi (katikati) na wajjumbe wa bodi ya Shirika hilo, wakipatiwa maelezo walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi


  Na Yasini Silayo

  Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limewahakikishia Umeme wa uhakika wakazi wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutokana na uboreshwaji mkubwa wa huduma za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji Umeme zinazoendelea katika Mikoa hiyo.

  Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi alipofanya Ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara akiambatana na wajumbe wengine wa bodi pamoja na viongozi waandamizi wa TANESCO Makao Makuu na Kanda ya Kusini.

  Akiongea na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Lindi, Dkt. Kyaruzi amesema kuwa tayari TANESCO imefanya matengenezo makubwa katika mitambo ya kuzalisha umeme wa Gesi wa Megawati 18. Mtambo huo unahudumia Mikoa ya Mtwara pamoja na Baadhi ya maeneo ya Lindi kupitia laini mpya ya 132kV Mtwara-Mahumbika iliyokamilika tangu mwezi Julai mwaka huu ikijengwa na mafundi wazawa kutoka ndani ya TANESCO kupitia kampuni Tanzu yake iitwayo ETDCO.

  "Mbali na hali ya umeme kuimarika hivi sasa kutokana na matengenezo ya mitambo ya Mtwara, Shirika hivi sasa linaendelea na maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Uzalishaji Umeme wa jumla ya megawati 540 Katika Mikoa hii pamoja na kuunga mikoa ya Kusini katika Umeme wa Grid ya Taifa kwa Laini kubwa ya Msongo wa Kilovolt 400. 

  Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Mradii huu itakuwa kutoka Kinyerezi DSM mpaka somangafungu Lindi ambapo patajengwa mtambo wa kuzalisha umeme wa Megawati 240, mradi tayari umekwishaanza kwa kulipa fidia wananchi walioko eneo la mradi ili wapishe kupitisha laini hiyo. Awamu nyingine itaunga Somanga mpaka Mtwara ambapo kutajengwa pia mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Megawat 300. Songea tayari inaunganishwa na gridi kupitia makambako na mradi unaelekea kukamilika kwa asilimia kubwa" alisema Dkt. Kyaruzi

  Aliongeza kuwa kutokana na mikakati ya muda mfupi, ya kati na muda mrefu iliyowekwa na TANESCO na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla, matatizo ya umeme katika mikoa hiyo yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu na hivyo kuchochea hamasa ya maendeo ya kiuchumi na Kijamii katika ukanda huo.

  Aliongeza kuwa TANESCO inatarajia kupanua mifumo yake ya kusambaza umeme na kuiunga na mifumo ya pamoja ya nchi za Kusini mwa bara la Africa, Southern African Power pool (SAAP) kupitia Zambia pamoja na ile ya Africa Mashariki Kupitia Nchi ya Kenya. Baada ya kuunganisha mifumo 
  hiyo Nchi itaweza kununua na hasa kuuza ziada ya umeme kwa Nchi hizo pale itakapohitajika.

  Aidha naye Mjumbe wa Bodi hyo Dkt. Lugano Wilson alisisitiza wakandarasi wa miradi ya umeme katika mkoa huo na mikoa mingine kwa ujumla kuhakikisha wanazingatia Viwango na Ubora wa kazi ili miradi hii iweze kutimiza lengo kusudiwa la kuwahudumia wananchi kwa umeme wa uhakika na kuchochea maendeo ya kiuchumi na kijamii.

  "Mnapotekeleza miradi hii kwa ubora na viwango vinavyotakiwa, wananchi watapata umeme wa uhakika na kwa Upande wa TANESCO mtatupunguzia gharama za matengenezo ya mara kwa mara yatokanayo na ujenzi wa laini yenye kiwango duni" alisema Dkt. Lugano 

  Kwa upande wa wananchi wa maeneo hayo walionesha kufarijika na kupata shauku kubwa ya kuunganishwa na kuboreshewa huduma za umeme ambapo mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Shabani alisema kuwa "Licha ya changamoto za Umeme tulizokuwa nazo kipindi cha nyuma lakini kwa kweli tumeshuhudia juhudi kubwa za viongozi wa Serikali, Wizara na TANESCO wanaotutembelea na kutufariji kuwa hali itakuwa shwari, na kweli sasa mambo yameanza kuwa mazuri umeme haukatiki tena mara kwa mara" alisema Mwananchi huyo
  Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi akiongea na wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO Katika mikoa ya Lindi na Mtwara

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udunavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata. Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti halmashauri hiyo, Mhe. Edward Shigela, Mwenyekiti wa halmashauri, Mhe. Boniphace Butondo na Afisa Lishe Wilaya, Avelina France.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo akifungua kikao hicho.
  Washiriki wa kikao hicho wakiwemo madiwani na watendaji kata wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
  Afisa Kinga na Uchanjaji Wilaya, Musa Doha akitoa mada kwa washiriki wa kikao hicho.
  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akichangia mada.
  Mtoa mada kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii, Perpetua Kilalo akitoa mada kwa washiriki wa kikao hicho.  Na Robert Hokororo, Kishapu DC

  Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imezindua mradi wa Mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la IMA WORLDHEALTH, Pamoja na Chuo cha Cornel.

  Lengo kuu la mradi huo ni kupunguza udumavu kwa asilimia 7 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao unatekelezwa katika halmashauri 36 zilizo ndani ya mikoa mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo amefungua kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata.

  Imeelezwa mradi huo utasaidia kuimarisha mikoa na halmashauri zake kwa kuzijengea uwezo wa watendaji wake wa sekta zote zinazohusika na masuala ya lishe kuhusu kupanga na kufanya ufuatiliaji wa shughuli hizo katika jamii.Pia utachangia fedha za utekelezaji kwenye bajeti na mipango ya mkoa na halmashauri 36 kwa njia ya ruzuku ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha zitakazotolewa hazitaifanya mamlaka hizo za Serikali zisitenge fedha kwa ajili ya masuala ya lishe.

  Hivyo badala yake utahamasisha ongezeko la bajeti ya shughuli za lishe kupanda katika kipindi chote cha mradi huo unapoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo(aliyeshika fimbo) akipima kina cha KIsima kilitengenezwa kienyeji kwa ajili ya kunyweshea mifugo katika eneo la Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera leo. Waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifana Halmashauri ya Missenyi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mikono) akiongea na wafugaji wa nchini Uganda leo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Omwaarogwamabaare. Kushoto ni Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Tanzania, bwana Richard Tumusiime Kabonero kulia (anayecheka) ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Martin Ruheta. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mkono)akimweleza jambo Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe.Richard Tumusiime Kabonero (kulia) walipokuwa katika ziara ya kikazi leo kwenye Mto Kagera katika kijiji cha Kakunyu. Wengine kushoto kwa Katibu Mkuu ni Dkt. Martin Ruheta Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kulia kwa Balozi ni Suleiman Ahmed saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo akiwa na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Tumusiime Kabonero (Mwenye suti nyeusi) na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athmani kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kagera.

  Picha na John Mapepele

  …………….

  Na John Mapepele –Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (0784 441180)

  Tanzania na Uganda leo wamekubaliana kuunda mara moja timu ya pamoja ya wataalamu wa mifugo itakayokuwa ikifuatilia hali ya mifugo ili kudhibiti milipuko ya magonjwa hatari ya Mifugo.

  Akizungumza leo mjini Bukoba kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na Uganda ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi wa Uganda nchini bwana Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo  siyo kitu cha hiari bali ni jambo la laziima ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili.

  Balozi Kabonero amesema njia bora ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na timu ya pamoja ya wataalam watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini kila wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi kushughulikia peke yake.

  “Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero

  Akizungumzia kwa upande wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amesema ushirikiano huo utasaidia kuboresha huduma za mifugo baina ya nchi mbili kwa kuzingatia kuwa taaluma ya udaktari wa mifugo imehuishwa na inadhibitiwa na bodi za taaluma hiyo kidunia.

  Aidha, amewataka wafugaji wa asili kote nchini wabadili mitazamo ya kutegemea serikali katika kukuza sekta badala yake washirikiane nayo ili kuharakisha mapinduzi ya sekta ya mifugo.

  “Bado kuna kazi ya kubwa ya kufanya ili kuikwamua sekta, lakini pia tukiamua kwa pamoja baina ya serikali na wafugaji nadhani tutakuwa na kipindi kifupi tu cha kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta hii” aliongeza Dkt. Mashingo

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Mifugo na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, bwana Victor Mwita anasema kuwa kuimarika kwa minada itakayosimamiwa kisheria katika mipaka ya nchi ya Tanzania na Uganda itasaidia kuongeza tija katika sekta ya mifugo hapa nchini.

  Aidha, Dkt. Mashingo alisisitiza kwamba wafugaji wenyewe ndiyo wanaoweza kuifanya sekta kupiga hatua kwa kuzingatia na kusimamia sheria mbalimbali za mifugo nchini. Alizitaja baadhi ya sheria ambazo ni kipaombele kwa wafugaji kuzingatia kwa sasa kuwa ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo namba 17ya mwaka 2003 na Sheria za Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.

  Akitolea mfano wa mafanikio yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt. Mashingo alisema wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

  Aidha alisema magonjwa kama Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa yasaidia kuongeza idadi ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia unachangia kuua 80% ya ndama wanaozaliwa.

  Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.

  Akitolea mfano wa mafanikio yaliyoletwa na wafugaji wenyewe nchini , Dkt. Mashingo alisema wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa wakati huo marehemu Joel Bendera waliweza kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

  Aidha alisema magonjwa kama Ndigana kali (ECF ) kama ikitokomezwa kabisa yasaidia kuongeza idadi ya mifugo nchini kwa kuwa ugonjwa huo ukiingia unachangia kuua 80% ya ndama wanaozaliwa.

  Akichangia katika kikao hicho Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo nchini(NARCO) Profesa Philemoni Wambura alisema bado kuna mahitaji makubwa ya mifugo katika viwanda vya nyama.

  “Mahitaji halisi ya ng’ombe wa kuchinjwa katika viwanda vyetu nchini ni 800 kwa siku lakini bado hatujaweza kufikia lengo hilo. Tuna kazi ya kufanya “ alisisitiza Profesa Wambura

  Kaimu Mkurugenzi Idara za Huduma za Mifugo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Martin Ruheta amesema ili sekta ya mifugo ifanikiwe lazima uzalishaji wa malisho uboreshwe malisho yanachangia kwa asilimia 70 hadi 80 kwa ng’ombe wa maziwa na kwa ng’ombe wa nyama inakwenda mpaka asilmia 90 Katika uzalishaji wa mifugo, hakuna miujiza mingine na ndo maana nchi za wenzetu kama vile Brazil wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta hii.

  0 0

  DODOMA: Shirika la LEAD Foundation linalojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira limezindua mradi wa Kisiki Hai Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

  Akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa ufunguzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la LEAD Foundation, Mhandisi Njamasi Chiwanga amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki Hai ni kuhakikisha wanafikia jumla ya kaya laki moja na themanini (180,000) ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira ziweze kutunza hekta 180,000 kwa kustawisha miti milioni 14 kwa njia ya Kisiki Hai (FMNR - Farmer Managed Natural Regeneration) ifikapo mwaka 2020.

  Njamasi amesema kuwa mikakati waliyonayo katika mradi huo ni pamoja na kujenga mshikamano wa wadau wote wa mazingira hususan viongozi wa wilaya, wakuu wa idara na taasisi mbalimbali, madiwani, watendaji wa kata pamoja na viongozi wa dini ili kuweza kushirikiana katika kufanikisha kukomboa mazigira. Kwa kuanzia mradi unatarajia kunufaisha tarafa mbili zilizo athiriwa zaidi na uharibifu wa mazingira katika kila wilaya ili kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa wa Dodoma.

  Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deo Ndejembi amesema anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofika katika ufunguzi wa mradi huo wamesema kuwa mpango wa Kisiki Hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Kongwa itakuwa ni historia.

  Kisiki Hai ni mradi wa miaka mitatu na unatarajiwa kufikia Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwa sasa umenza katika Wilaya ya Kongwa ambapo umeanza na tarafa ya Kongwa na Mlali za wilaya hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi akifungua rasmi mradi wa LEAD Foundation.
   Mkurugenzi wa Programu - LEAD Foundation Mhandisi Njamasi Chiwanga akiwasilisha mpango wa Programu
  Wadau walio hudhuria warsha ya mazingira ya Kisiki Hai.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Leo amefanya Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu. Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.

  Katika mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na upungufu wa madarasa,madawati na changamoto nyingine mbalimbali.Pia  kuweka mikakati ya kuondoa changamoto hizo ifikapo muda wa usajili.

  Katika kikao hicho Mh. Ndejembi alimuagiza Mkurugenzi kuwasimamisha  kazi waratibu wawili wa Kata ya Njoge na Lenjulu ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zao mbalimbali zinazopelekea kutowajibika vema katika vituo vyao vya kazi.

  Mkuu wa Wilaya aliwaasa waratibu hao kuachana na kufanya kazi kwa mazoea (business as usual),  na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya tano kwani Mh Rais amewawekea mazingira mazuri ya kazi ikiwemo posho kwa kila MEK Tsh 450,000/= kila mwezi pamoja usafiri. Hivyo wahakikishe  wanatoa huduma bora kwa wananchi.

  DC Ndejembi  alieleza kuwa kwa mwaka ujao wa 2018 wanatarajia kusajili wanafunzi wapya wengi sana wa Shule za Msingi na Kidato cha Kwanza kwani Sera ya utoaji Elimu Bure imeamsha Morali zaidi  kwa Wazazi kupeleka watoto Shule.

   Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza kwenye Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu, Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.


   

  0 0

  Mtendaji wa Mtaa wa Ufukoni – Mtwara akimthibitisha mmoja wa wakazi kwenye Mtaa wake kwa kumgongea mhuri wa Mtaa anakoishi kwenye fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa kabla mwananchi huyo hajaingia kwenye hatua ya mwisho ya kuchukuliwa alama za vidole, picha na saini ya Kielektroniki.
  Baadhi ya wananchi katika Kata ya Magomeni mkoa wa Mtwara wakichambua fomu zao za Usajili kwa ajili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za kibaiolojia.
  Mkazi wa shule ya Msingi Lilungu mkoani Mtwara akipigwa picha wakati wa zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa likiendelea.
  Mwananchi wa Kata ya Ufukoni akisubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa zoezi ambalo kwa sasa linaendekea katika shule ya Msingi ya Ufukoni mkoani Mtwara. Wananchi mkoani Mtwara wamekuwa miongoni mwa wananchi katika mikoa 15 ya Tanzania ambao wanashiriki kwenye zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa lilionza mapema mwezi Novemba mwaka huu. 

   Kwa Wilaya ya Mtwara kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika Kata za Magomeni na Ufukoni huku Kata za Shangani, Rahaleo, Tandika, Chikongola, Majengo, Reli na Vigaeni zikiwa zimekamilisha zoezi hilo. Wilaya nyingine ambazo zoezi hilo linaendelea ni Wilaya ya Masasi, Nanyumbu, Nachingwea na Newala.

   Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa Mtwara linategemewa kumalizika mwezi Februari 2018 kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho hivyo huku nchi nzima zoezi hili likikusudiwa kumalizika mwezi Desemba 2018. Mikoa mingine inayoendelea na zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa ni Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Singida, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Kilimanjaro, Arusha na Lindi.

  0 0

  Na Kajunason/MMG.

  Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa mpango wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) kuwa na uadilifu katika kufiatilia matumizi ya fedha za serikali. Hayo ameyazungumza leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo uliowakutanisha viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) uliofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). 

   Mhe. Senyamule alisema ni vyema watendaji hao wakafuata misingi imara itakayowezesha serikali kujua ni wapi wanamatumizi mabovu ya fedha katika halmashauli. Aliagiza halmashauri kushirikiana kwa karibu na watu hao kwani kazi wanayoifanya ni ya halmashauri, hasa ukaguzi na mipango. "Idara ya ukaguzi ina watumishi 3 tu wanaohitaji kukagua kila kitu, sio rahisi wakidhi kwa wakati; lazima tuwashirikishe wadau wa PETS ili taarifa zao ziwe ni moja ya misingi ya ufuatiliaji kwa halmashauri," alisema Mhe. Senyamule. Pamoja na yote Mhe. Senyamule aliomba CCT kuongeza idadi ya kata wanazofanyia kazi kutoka 11 hadi zote 34 zilizopo kwa sasa.
   Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) waliohudhuria semina iliyofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). 


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini katika ukaguzi wa miradi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini akiwemo Mbunge wa Morogoro vijijini Omary Mgumba katika ukaguzi wa miradi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Morogoro vijijini.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Morogoro vijijini.

  ………..

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya morogoro Vijijini Sudi Mussa Mpiri kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

  Pia ameshindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani kutoka kampuni ya Dimond ambapo matumizi ya fedha hiyo zaidi ya asilimia 90 hayafahamiki kilichofanyika. 

  Kadhalika, Mkurugenzi huyo anadaiwa kuwa na mahusiano mabovu kati yake na watumishi wa Halmashauri hiyo.

  Jafo alitoa agizo hilo akiwa Kijijini Mvuha kwenye makao makuu ya Halmashauri ya morogoro vijijini.

  Kutokana na hali hiyo,Jafo ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa mkurugenzi huyo kwa lengo la kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuna ufisadi na mapungufu ya kiuongozi kwa mkurugenzi huyo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Jafo hajarishishwa kabisa na miradi aliyo itembelea wilayani humo kutokana na miradi hiyo imeonyesha wazi kwamba Halmashauri hiyo imefanywa kama shamba la bibi. 

  Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia rasilimali za Halmashauri hiyo.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia uteketezaji wa zana haramu za uvuvi katka Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akimkabidhi cheti ndugu Mapango Thomas cha utambuzi ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali za uvuvi  Mkuu wa Wilaya ya Uviza,Mwavua Mrindo akizungumza na wananchi na viongozi mabli mbali katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kingoma wakivuka mto Malangalasi kuelekea katika kijiji cha Buhingu wilayani Uviza Kigoma.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Kigoma.  Kufuatia Wimbi la Uvuvi haramu nchini,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamisi Ulega janao ameshuhudia uchomwaji wa zana haramu za Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, kijiji cha Buhingu mkoani Kigoma.

  Mwenyekiti wa kikundi cha Usimamizi shirikishi rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Kijiji cha Buhingu Bw.Richard Nkayamba amemweleza naibu Waziri kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanakomesha Uvuvi haramu katika Kijiji cha Buhingu na kuweka mazingira safi.

  "Kwa kiasi kikubwa tumedhibiti  Uvuvi haramu pamoja na kutoa elimu kwa Jamii za Wavuvi, kuhusu Umuhimu wa Uvuvi endelevu kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi shirikishi BMUs 21 pamoja na shirika lisilokuwa la kiserikali la Tuungane lililopo katika kijiji cha Buhingu"alisema Nkayamba

  Aliongeza,"Tunakamata nyavu haramu bila kujali ni za nani,na hii inatujengea chuki kwa wamiliki wa Nyavu husika"Akiongea na uongozi wa Halmashauri ya Uvinza pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,Ulega amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuona ni namna gani wanaweza kuziwezesha BMUs zilizopo kijijini hapo.

  "Naombeni sana mziwezeshe hizi BMUs wapeni tenda za kukusanya Maduhuri ya Samaki kwa Wavuvi hawa ili hizi BMUs ziweze kujiendesha zenyewe"Mhe.Ulega alisisitiza kuwa kama wakipewa BMUs kukusanya Maduhuri basi watakuwa wametengeneza ajira kwa Vijana hao.VileVile aliwaasa sana BMUs kuwa Waadilifu ili waweze kuaminiwa"

  Katika hatua nyingine Mhe.Ulega aliwatunuku vyeti vya Utambuzi baadhi ya BMUs waliokidhi sifa za kusimamia rasilimali za Uvuvi katika ziwa hilo.Awali Mhe Ulega alikemea vikali asasi za Kiraia kujiingiza katika kushabikia siasa badala ya kufanya kazi za kuelimisha Umma.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi.Mwanamvua Mrindo amesema kuwa amefarijika sana kwa ujio kwa Mhe.Naibu waziri katika Wilaya ya Uvinza ili kutatua Changamoto zinazowakabili.

  Baadhi ya wananchi waliokuwa wakimsubiri mhe.Ulega katika kijiji cha Mgambo,walimweleza kero zao ikiwa ni pamoja na uingizwaji ovyo Mifugo katika kijiji cha chao.Naibu waziri amemwagiza MKUU wa Wilaya ya Uvinza kushughulikia kero hizo.

  0 0
 • 12/22/17--04:59: Article 2


 • 0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo 

  JESHI la polisi mkoani Tanga, limewahadharisha wananchi kuelekea katika msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kama ulipuaji baruti na fataki ikiwemo kuchoma moto matairi barabarani, kwa yeyote atakayefanya hivyo atachukulia hatua za kisheri. 

  Kamanda mpya wa mkoa huo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward Bukombe, alisema kwamba jeshi hilo linapiga marufuku kwa mtu yeyote kulipua au kusababisha milipuko ikiwemo baruti, fataki na Eksozi za magari, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria namba 13 ya sheria ya milipuko. 

  “Hivyo wakazi wa mkoa wa Tanga, ni marufuku kuchoma matairi hovyo na kulipua baruti bila kibali, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae kiuka agizo hili,” alisema RPC Bukombe. 

  Alisema uzoefu unaonesha kuwa siku za sikukuu watu wengi hujisahau kujiwekea ulinzi ikiwemo kuwaangalia watoto hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuhakikisha wanachukua hatua za kuwalinda watoto pamoja na nyumba zao ili wahalifu wasitumie mwanya huyo kufanya uhalifu wa kuvunja au watoto kupotea mitaani. 

  Kamanda Bukombe alisema kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bali aliwakumbusha kuzingatia taratibu za kumbi za burudani kufungwa nyakati za saa 6:00 usiku na hata ibada za mkesha wa Krismasi na Mwaka mpya zimalizike muda huo. 

  Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa polisi alisema mwenendo wa uhalifu mkoani humo, katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka 2017, umeendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu ma hakuna matukio yanayotishia usalama kwa wananchi baada ya kuyadhibiti kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola. 

  Hata hivyo, alisema kwamba katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu, katika misako waliyoiendesha na operesheni mbalimbali waliweza kukamata wahalifu waliofanya matukio mbalimbali ambapo kesi za bangi zilikuwa 237 kwa bangi yenye uzito wa kilogramu 76.1 na mirungi kesi zilikuwa 37 na uzito wa mirungi ilikuwa kilogramu 5,396.740. 

  Kwa upande wa wahamiaji haramu jeshi hilo walikamata wahamiaji haramu wapatao 224 kati ya hao Wasomali walikuwa 55 na Waethiopia walikuwa 149 na Wakenya walikuwa 20 ambao wote walifikishwa katika vyombo vya sheria. 

  Kamanda huyo pia alisema kuwa katika kudhibiti ujambazi na unyang’anyi wa kutumia silaha, jeshi hilo katika kipindi hicho lilifanikiwa kukamata jumla ya silaha 14 za moto ambapo bastola zilikuwa 2, shortgun 3 na magobore yaliyotengenezwa kienyeji yalikuwa 9.
  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa, kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo Mkoani Tanga,Leonce na kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
  Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa 

  0 0


  0 0


  Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii.

  UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) imetaja majina sita kati ya wanane ya wajumbe walioteuliwa  katika Kamati ya kuchunguza na kufuatilia mali za chama.

  Hatua hiyo imekuja kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Umoja huo Kheir James kutaka kuhakikiwa kwa mali zote za umoja huo.

  Akizungumza leo katika Makao Makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa umoja huo Shaka Hamdu Shaka ametaja majina ya wajumbe wa kamati hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Maria Chaurembo.

  Wengine ni Peter Kasera, Zelote Saitoti, Rose Manumbu, Sofia Kizigo na Elly Ngowi."Jukumu la kamati hiyo ni kufuatilia mali zote za umoja wetu, namna ambavyo zinatumika na mlolongo wa matumizi yake.

  " Itaanza kazi haraka na wajumbe wengine wawili wa kamati hii wataungana na wenzao kufanikisha majukumu waliyopewa. Itakapomaliza kazi tutakuja kwenu kuelezea ambacho tumekibaini na nini cha kufanya,"amesema Shaka.

  Amesema Mwenyekiti wao baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo moja ya majukumu ambayo ameamua kuanza nayo ni kufuatilia mali za chama na jukumu langu ni kuhakisha maagizo ya mwenyekiti wetu yanafanyiwa kazi tena kwa uhakika,"amesema Shaka.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dr. Mohamed Seif  Khatib  aliyevaa shati rangi Nyekundu akimkaribisha Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kufunga Kongamano ya kwanza la Kimataifa la Kiswahili. Kati kati yao ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri.
  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akiongozwa na Viongozi wa Baraza la Kiswahili kuingia katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar kulifunga Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kiswahili.
   Baadhi ya Wataalamu na wadau wa Kiswahili walioshiriki Kongamano ya kwanza la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika  Siku Mbili Visiwani Zanzibar.
   Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akitoa vyeti kwa Mmoja wa Washiriki wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika Zanzibar kwa Siku mbili.
  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kushoto akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bakiza Dr. Mohamed Seif wakiangalia baadhi ya vitabu vya Kiswahili vilivyotungwa na Magwiji wa Lugha ya Kiswahili na kusomeshwa katika skuli na vyuo mbali mbali ndani na nje ya Nchi.
  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Dr. Khatib wakifurahia moja ya Kitabu  mashuhuri cha Mtungaji Gwiji Zanzibar Bwana Mohamed Said  (Maarufu Bwana Msa).
  Picha na – OMPR – ZNZ.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wafanyabiashara wakubwa Nchini kuwekeza katika uchapishaji wa Vitabu vya Kiswahili pamoja na kujenga Maduka makubwa ya kuuzia kazi za Kiswahili kwa vile bidhaa zinazotokana na lugha hiyo zinauzika.

  Alisema Mwanataaluma au mswahili anayehitaji vitabu vya Waandishi Mahiri wa Lugha hiyo wa Zanzibar kama Profesa Said Ahmed Mohamed, Shafi Adam Shafi, Bwana Msa na wasanii wengine kama Mohamed Seif Khatibu kamwe kwa wakati huu anashindwa kuvipata.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipokuwa akilifunga Kongamano la Kimataifa la Siku mbili la Lugha ya Kiswahili lililokuwa likifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar.

  Alisema ni faraja iliyoje kwa sasa kuona kiasi gani Lugha ya Kiswahili inavyoendelea kupata heshima ya kutambuliwa na kukubaliwa Kimataifa hasa kutokana na upatikanaji wa mwitiko mkubwa wa kuwa na Wataalamu waliobobea katika nyanja mbali mbali.

  Balozi Seif aliwataka Wafanyabiashara, Wataalamu pamoja na watumiaji wa Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Nchi kushirikana kwa pamoja katika kuhakikisha Lugha hiyo inatumika ipasavyo na hasa ikitambulika wazi kwamba hakuna mtu anayeelewa kila kitu.

  “ Hakuna Mtaalamu anayejuwa kila kitu. Utamkuta Mtaalamu wa Fasihi Sarufi inampiga chenga au Mtaalamu wa muundo wa L ugha Sarufi inamuendesha kindumbwe ndumbwe ”. Alisema Balozi Seif.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza waandaaji wa Kongamano hilo la Kimataifa la Kiswahili ambalo limewaweka pamoja Wataalamu wa Kiswahili kutoka Tanzania Bara, Ulaya Marekani baadhi ya Nchini za Bara la Afrika na wenyeji Zanzibar.

  Alisema ni kawaida katika mijadala kama hiyo ya Kitaaluma washiriki huchangia kwa kuhoji,kuboresha au kutokubaliana na baadhi ya vipengele vya Hoja mambo ambayo yanapaswa kuigwa na kuzingatiwa na wadau wengine kwani huzidi kukipa uhai zaidi Kiswahili Kitaaluma.

  Alieleza kwamba Kongamano hilo la Kiswahili limetoa fursa ya mkusanyiko wa Wataalamu wa Taaluma ya nyanja mbali mbali, kukutana na kubadilishana uzoefu, ujuzi na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa kwenye harakati za kukiendeleza Kiswahili.

  Balozi Seif alifahamisha kwamba mkusanyiko huo sio tu utaimarisha na kukuza Lugha ya Kiswahili, bali pia utajenga wigo mpana zaidi kwa wanataalamu wa Lugha hiyo Dunia nzima kusaidiana katika kukieneza Kiswahili.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwasisitiza wana kongamano hao wa Lugha ya Kiswahili kuwa hivi sasa ni wakati muwafaka wa kufikiria uandaaji wa Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu vya Kiswahili hasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

  Alisema maonyesho hayo ambayo ingependeza yakafanyika kila baada ya Miaka miwili au zaidi yatasaidia kuongeza kasi ya uchapishaji na pengine usomaji wa kazi mbali mbali zinazotokana na Lugha ya Kiswahili.

  Mapema Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar { BAKIZA} Dr. Mohamed Seif Khatib ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuthamini Lugha ya Kiswahili inayopelekea kutumika katika Taasisi zake za Umma na Jamii.

  Dr. Khatib alisema kitendo hicho kinaendelea kuleta faraja kwa Wana Baraza la Kiswahili Zanzibar na kusisitiza kwamba lazima Lugha hiyo iimarishwe ili iweze kurahisisha Maisha ya Mswahili.

  Alifahamisha kwamba Mswahili tokea anazaliwa, anakua na kusoma, anaingia katika harakati za Kimaisha, anafariki kwa kumaliza muda wake wa kuishi anaombewa Dua kwa Lugha ya Kiswahili.

  Akimkaribisha Mgeni Rasmi kulifunga Kongamano hilo la kwanza la Kimataifa la Kiswahili Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mheshimiwa Rashid Ali Juma aliupongeza Uongozi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar kwa juhudi kubwa zilizopelekea kufanyika kwa Kongamano hilo Visiwani Zanzibar.

  Mh. Rashid alisema Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Mic hezo itakuwa chachu ya kusimamia yale yote yaliyokusanywa katika Kongamano hilo ili yasaidie kunufaisha Kizazi cha sasa na kijacho.

  Waziri wa Habari alisema wakati Zanzibar ikiendelea kuimarisha miundombinu ya Sekta ya Utalii Kiswahili ni moja ya kivutio kinachoshawishi wageni wengi kupendelea kutembelea Zanzibar kujifunza Utamaduni wa Visiwa hivi kupitia lugha ya Kiswahili.
  Alisema Mataifa mengi Duniani hivi sasa yameshaelewa umuhimu na thamani ya Lugha ya Kiswahili kwa kufundisha Wananchi wao. Hivyo kitendo hicho ni vyema kikatiliwa mkazo katika kuona walimu wa kutosha wa kusomesha lugha hiyo hasa kwa wageni wanapatikana katika dhana nzima wa kuilinda lugha hiyo isipotoshwe.

  0 0


   Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Jeremiah John Jilili akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jonas Kamaleki na Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa.
   Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Jeremiah John Jilili na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Mambo ya Nje Jumuiya za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Malisa Martine.
   Waziri wa Habari, Mawasiliano na Mambo ya Nje Jumuiya za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Malisa Martine akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Katiba Sheria na Utawa Bora wa Daruso Ibrahim Bimbalirwa. 
  Baadhi ya W3aandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu mchango wa vijana kuelekea uchumi wa viwanda leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)


older | 1 | .... | 1468 | 1469 | (Page 1470) | 1471 | 1472 | .... | 1898 | newer