Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1469 | 1470 | (Page 1471) | 1472 | 1473 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga limefanya kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga.
  Kikao hicho kimefanyika leo Alhamis Desemba 21,2017 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za manispaa ya Shinyanga.
  Akizungumza katika kikao hicho, Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO, Shangwe Kimath alisema lengo ni kuwakutanisha watoto hao na wajumbe wa kamati hiyo ambao wanashiriki katika utengenezaji wa bajeti ya manispaa ya Shinyanga.
  “Mradi wetu unatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji,lakini leo tuna watoto wa manispaa ya Shinyanga,kupitia kikao hiki watoto wanaeleza changamoto wanazokutana nazo zinazopaswa kuchukuliwa hatua ngazi ya manispaa ikiwa ni pamoja na kushawishi bajeti ya manispaa iwe na mlengo wa kusaidia watoto”,alieleza Kimath.
  “Rafiki SDO na Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo nchini Sweden (SIDA) tuliamua kuunda baraza la watoto kutoka kata 17 za manispaa hii kwa lengo la kuongeza ushirikishwaji wa watoto katika kutoa maamuzi hususani masuala yanayohusu watoto”,aliongeza Kimath.
  Alisema kikao hicho cha kamati ya uchumi,elimu na afya na baraza hilo la watoto linaloundwa na watoto waliopo shuleni na ambao hawapo shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu ya ushawishi katika utengenezaji wa bajeti inayomlenga mtoto.
  Wakizungumza katika kikao hicho watoto walizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uhaba wa madarasa,walimu na watoto wa kike kukosa vifaa vya kutumia wakiwa katika hedhi hivyo kuomba serikali na mashirika mbalimbali kuangalia namna ya kutoa pedi kwa wanafunzi shuleni.
  “Wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo wanapokuwa katika hedhi,wanakosa pedi hivyo kuona aibu kufika shuleni lakini pia tunahitaji kila shule iwe na vyumba maalum vya kujihifadhi watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi”,alieleza Nancy Aloyce kutoka Shule ya msingi Mwenge.
  Naye Sara Chacha kutoka shule ya msingi Ushirika alisema bado kuna changamoto ya uchafuzi wa vyoo vya shule unaofanywa na wananchi wanaopita katika maeneo ya shule kwani shule nyingi hazina uzio hali inayohatarisha afya zao.
   Mjumbe mwingine wa baraza hilo la watoto,Maeja Geofrey kutoka shule ya msingi Bugoyi A aliomba serikali kuwa na bajeti inayolenga kusaidia watoto kwani baadhi yao wanaishi katika mazingira magumu hali inayowafanya wakatishe masomo na kuwa watoto wa mitaani.
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya alisema kamati hiyo imezipokea changamoto za watoto na mapendekezo yao na watajitahidi kuhakikisha bajeti yao inalenga watoto.
  Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya akifungua kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna leo Disema 21,2017. Kushoto ni Katibu wa kamati hiyo Raymond Kilindo ambaye ni Afisa Mipango wa manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya akizungumza wakati kikao hicho ambapo alilipongeza shirika la Rafiki SDO kwa kuona umuhimu wa kuandaa kikao kwa ajili ya kuwapa nafasi watoto kueleza changamoto zinazowakabili mbele ya kamati hiyo.
  Wajumbe wa Baraza la watoto manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya.
  Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath  akielezea lengo la kikao cha ushawishi kati ya wajumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga.
  Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali ya manispaa ya Shinyanga limeona ni vyema kuwapa nafasi watoto kueleza changamoto zinazowakabili mbele ya kamati hiyo
  Wajumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
  Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Shirika la Rafiki SDO Eliud Lazaro akitoa mwongozo wa majadiliano wakati wa kikao hicho
  Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya watoto shule ya msingi UshirikaSara Chacha, akielezea kuhusu changamoto wanazokutana nazo.Kushoto ni Nancy Aloyce kutoka Shule ya msingi Mwenge
  Maeja Geofrey kutoka shule ya msingi Bugoyi A akichangia hoja wakati kikao hicho ambapo alisisitiza umuhimu wa serikali kutenga bajeti inayosaidia watoto wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
  Mtoto Abdalah Said akichangia hoja wakati wa kikao hicho
  Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dossy akizungumza katika kikao hicho
  Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Shela Mshandete ambaye pia ni diwani wa viti maalum (CCM) akichangia hoja wakati wa kikao hicho
  Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Moris Mugini ambaye ni diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza katika kikao hicho
  Wajumbe wa baraza la watoto wakiwa ukumbini
  Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga Hamis Ngunila ambaye ni diwani wa kata ya Kitangiri (Chadema) akichangia hoja katika kikao hicho
  Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga Zena Gulam ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini (Chadema) akizungumza katika kikao hicho
  Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Zuhura Waziri ambaye ni Diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli akichangia hoja wakati wa kikao hicho
  Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza katika kikao hicho
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Kampuni ya Viva Legency inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu kinachojulikana kama "SOTE TUNAWEZA" kikiwa na lengo la kusaidia harakati za mabadiliko pamoja na kukuza utamaduni wa mtanzania.

  Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Viva Legency Fortunata Temu amesema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa msomaji uwezo mkubwa wa kubadili fikra na kupiga hatua ya kimaendeleo.

  "Kitabu cha sote tunaweza kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa uwezo msomaji kubadili kifikra na kupiga hatua kiamaendeleo" amesema Fortunata

  Amesema kuwa katika uandishi wa kitabu hicho wametumia mifano ya watu mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za dunia waliofanikiwa na kusema kuwa wametumia mifano hiyo ili kumtia hamasa msomaji na kumfanya kufuata nyendo za hao watu waliofanikiwa.

  Fortunata ameongeza kuwa mafanikio yanaweza kupatikana kwa kuangalia fursa zinazopatikana ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili kama fursa kwa kuhabarishana na kuelimishana .

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk.Ave Maria Semakafu ameipongeza kampuni ya Vivalegency na kusema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati.

  "Sote tunaweza kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati" amesema Dk.Semakafu.

  Amesema Tanzania inachangamoto kubwa katika utamaduni wa uandishi na usomaji vitabu na kuwaomba watanzania watumie fursa ya kuandika vitabu vyenye dhima yenye kuleta maana na kuachana na utamaduni wa kuandika vitabu ambavyo havina dhima yoyote ya kubadili fikra na kuleta chachu ya maendeleo.
   Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy (T) Bi. Fortunata Meela Temu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Avemaria Semakafu na Mwajiri Msaidizi wa Viva Legacy (T) Ltd Bi. Neema Seleman.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa VIVA lEGACY lTD (t) Bi. Fortunata Meela Temu.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Stadi Dkt. Avemaria Semakafu (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy Ltd (T) Bi. Fortunata Meela Temu wakiwaonyesha Waandishi wa Habari kitabu cha "SOTE TUNAWEZA"  leo Jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimetungwa kwa lengo la kuimarisha mfumo wa utendaji na hasa kuboresha rasilimali watu. 
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na  na Mkurugenzi wa Viva Legacy (T) Ltd  alipokuwa akizungumzia kuhusu uzinduzi wa kitabu cha SOTE TUNAWEZA leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO)

  0 0

  Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (wakwanza toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (wa pili toka kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza za Wafanyakazi mapema leo jijini Dar es Salaam.  Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha 
  Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo.

  NA K-VIS BLOG, FELIX ANDREW 

   WAAJIRI Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha wafanyakazi wao kabla ya kufanya maamuzi mbali mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi. Ushauri huo ulitolewa jjini Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC) Alisema kuwa uongozi shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo.

  “Lengo kuu la uongozi shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali mbali na kuzitatua kwa nia ya kufikia malengo,” alisema. Mavunde aliwaasa wafanyakazi nchini kuondokana na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa jamii.

  “Urasimu katika utoaji wa huduma ni changamoto kubwa sana ambayo inaisumbua nchi naomba sana msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema. Aidha naibu waziri huyo alisisitiza kwa waajiri wasio jiunga na Mfuko huo kufanya hivyo mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake  Alisema kuwa serikali itaanzisha msako mkali mwakani wenye lengo la kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waajiri wote ambao bado hawajajisajili na mfuko huo. 

   Aliongeza kuwa serikali ilikwisha toa muda wa kujisajili kwa wasiofanya hivyo ambao ulimalizika tarehe 30 Septemba mwaka huu. Mnamo mwezi Januari mwakani tutaanzisha msako wa kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola waajiri wote ambao wameshindwa kujisajili na mfuko hadi sasa, alisema Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la WCF Bw Masha Mshomba, alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi katika maamuzi mbali mbali ya kiutendaji tayari menejimenti kwa kushirikiana na tawi la chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) imekamilisha uundaji wa baraza hilo. 

   Aliongeza kwa mfuko huo umeendelea kutimiza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya taifa, husani uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuwahudumia wafanyakazi wanoumia au kuugua kutokana na kazi kwa nia ya kuwawezesha kurudi kazini. 

   Aidha mfuko pia unashiriki moja kwa moja katika kujenga uchumi wa viwanda kwa njia ya ubia na Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini. Katika kusogeza huduma jirani na wadau wote , alisema mfuko umepanga kufungua ofisi zake katika mikoa minne katika robo ya tatu ya mwaka 2017/18. Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Arusha , Mwanza na Mbeya huku lengo likiwa ni kuwa na ofisi katika mikoa ishirini.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.  Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili awagawie Wenyeviti wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo. 
   
   
  Wananchi wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora. 
   
  Kauli hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno. Mhe. Mchembe alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua matofali ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600. Aidha amekaribisha wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu.
   
   "Hamasa ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule. Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda wanatuharibia watoto wa kike. Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto hii. Mkuu wa Wilaya aliipongeza Kamati ya Ujenzi kwa kazi nzuri ya kukusanya michango ya maendeleo na kazi ya ujenzi ambayo tayari imeanza. Tunategemea kuanza ujenzi mapema Januari katika eneo la ekari 15. Wilaya ya Gairo ina madarasa zaidi ya 30 yote yamejengwa kwa nguvu ya wananchi hadi ngazi ya boma, bado kuezeka. 
   
  Madarasa haya ni nje ya madarasa 16 yaliyomalizika ndani ya mwaka mmoja. "Mpaka sasa hatuna darasa la nyasi wala wanafunzi wanaokaa chini. Tumemaliza nyumba za waalimu 8, maabara 6 na tuna maboma yanahitaji nguvu ya ziada," alisema.

  0 0


  0 0

   Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Kidatu
  MATENGENEZO makubwa ya mashine namba moja kati ya nne za kufua umeme wa maji kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro yamefikia zaidi ya asilimia 95 kukamilika.

  Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kituo hicho Desemba 22, 2017.

  "Kwa sasa tumeanza majaribio ya mashine kuzunguka bila kutumia nguvu za maji, mafundi wanazungusha mashine hiyo kwa kutumia mikono ili kuangalia usahihi wa unyookaji wa shafti,”alisema.

  Alisema hatua itakayofuata ni kuunganisha kipande yanapoingilia maji ili kuzungusha huo mtambo na sehemu ya kuzalishia umeme na Jumapili mafundi hao wanaoshirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia wataanza majaribio ya kuzungusha mtambo wenyewe.
  Aidha Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi Amesema Kidatu kuna mitambo minne na kila mmoja unauwezo wa kuzalisha umeme Megawati 51 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 204 za umeme ambao unaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

  ”Tuliona tufanye matengenezo makubwa kwani kila baada ya miaka 20 huwa tunafanya zoezi kama hili ili kurejesha mashine kufanya kazi bora kwa kipindi hicho ili kuhakikisha mtambo unarejea kwenye hali yake ya kawaida.” Alisema.

  Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, umeme unaozalishwa kutokana na maji ni wa bei nafuu na kupongeza juhudi za serikali katioka kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme.

  “Tunaishukuru sana serikali kwa hatua inazochukua kama kuboresha upatikanaji wa maji kwa kutunza vyanzo vya maji (mazingira), hususan bonde la Mto Rufiji, timu iliyoundwa na Makamu wa Rais ambayo imefanya kazi nzuri nahuenda baada ya muda matokeo mazuri tutayaona.” Alisema.
  Akifafanua zaidi alisema, juhudi zinazofanywa na serikali kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vya maji kama vile Stigler Gorge zitasaidia sana nchi yetu na hii inaonyesha serikali ilivyodhamiria kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa vitendo.” Alisema.

  Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Bi. Leila Muhaji, amesema Shirika limekuwa karibu na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji na vituo vya umeme ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutunza mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji.

  “Na ushirikiano wetu na wananchi uko katika maeneo mbalimbali kama vile kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wanaoishi jirani na vituo vyetu vya kufua umeme, shule za awali lakini pia hata usafiri yumekuwa tukiwapatia usafiri wa bure wananchi ambapo hutumia magari yetu ya wafanyakazi kwenda maeneo jirani na vituo.
  Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro.
   Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
    Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
   Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia), akizungumza kuhusu kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu, mkoani Morogoro. Katikati ni Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
   Mhandisi Ikwasa, (kulia), akibadilishana mawazo na Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote.
   Geti la kupitishia maji Kidatu.
   Meneja wa Kituo cha kufua umeme Kidatu mkoani Morogoro, Mhandsi Anthony Mbushi (kushoto), akifafanua masuala ya kiufundi kwenye chumba cha udhibiti umeme kilichoko chini ya ardhi kwenye Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
   Maafisa wa TANESCO na baadhi ya wahariri wakiangalia mashine iliyoharibika, a,mbayo kwa sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
  Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
  Peter Rauya, (kushoto) na Senorina Maganga  wa chumba cha udhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini.
  Wahariri wakipatiwa maelezo na maafisa wa TANESCO kuhusu utendaji kazi wa mashine za kufua umeme (Turbines) kituom cha Kidatu.
  Waharorio wakiangalia mashine iliyoharibika ambayo sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
  Mameneja wa vituo vya kufua umeme kutoka mikoani wakiwa kwenye kituo cha kufua unmeme Kidatu mkoani Morogoro. Mameneja hao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
  Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (wapili kushoto), akiwa na baadhi ya Mameneja wa vituo vya kufua umeme vilivyoko mikoani ambao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
  Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
  Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
  Wasimamizi wa chomba cha udhibiti mifumo ya umeme cha Kidatu mkoani Morogoro; kutoka kushoto ni Peter Rauya, Senorina Maganga na Nicomedy Mhina.
  Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda (kushoto), akiwa sambamba na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar ya Croatia wakati wakiendelea na matengenezo hayo.
  Sehemu ya kuingilia "mgodini" chini ya ardhi kwenye mitambo ya kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro.

  0 0


  0 0

  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Katikati), akizungusha king’ora kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Thobias Andengenye, wakati wa Tamasha la hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.

  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza na Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi rasmi wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa Umma, wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.

  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (Watatu Kulia), akiwa kwenye banda la mmoja wa mdau aliyeshiriki katika tamasha hilo, wakati wa Tamasha la Zimamoto la utoaji elimu kwa umma lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo eneo la Kawe mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.
  Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mrakibu wa Zimamoto Peter Mabusi (wanne kushoto) akitoa maelezo kwa Kamishna wa Operesheni Billy Mwakatage (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benedict Kitalika (Wapili Kushoto), na Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Temeke Laizer Loshpy (kushoto), pindi vikosi mbalimbali vya zimamoto vilivyokuwa vikioonesha zoezi la utayari wakati wa tamasha la Zimamoto na Uokoaji la utoaji elimu lililofanyika katika viwanja vya Kawe Tanganyika Packers mapema mapema jana asubuhi tarehe 22/12/2017.
  Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini wakionesha utayari wakukabiliana na majanga ya moto.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

  0 0

  Kamanda wa polisi Mkoani Pwani ,Jonathan Shanna mwenye kifimbo akiwa pamoja na askari wa polisi Mkoani hapo ,wakati wakijifua na mazoezi kuelekea kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka,viwanja vya Mailmoja Kibaha.Picha na Mwamvua Mwinyi


  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  JESHI la polisi Mkoani Pwani limetoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka ,wabadili mawazo yao kabla ya hatari kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu kulinda raia na mali zake.

  Aidha jeshi hilo limewataadharisha watu wote wanaokwenda ndani ya Mkoa huo hususan kwenye fukwe za bahari ya Hindi zilipo kwenye wilaya ya Bagamoyo ,kuwa wastaarabu na kutii sheria za nchi na watakaokiuka hawatakuwa na muhali nao ili iwe mfano kwa wengine.

  Kamanda wa polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna ,alitoa wito huo viwanja vya Mailmoja Kibaha wakati akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wananchi waliojitokeza kujionea askari waliokuwa wakifanya mazoezi ,kuelekea kipindi cha sikukuu ya X-Mas na mwaka mpya.

  Alitoa wito, kwa wenye kumbi za starehe kuzingatia sheria za usalama kwa kutojaza idadi kubwa ya watu kwenye kumbi zao na wale watakaokaidi watakiona .Pamoja na hayo ,kamanda Shanna aliwataka wananchi kuhakikisha wanapotoka majumbani mwao ,wasitoke wote na waache walinzi kwenye nyumba zao. 

  Aliwaasa pia wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaachia watoto wao kwenda kwenye shamrashamra za sikukuu pasipo kuwa na wangalizi ili kuepuka upotevu wa watoto.Kamanda Shanna alieleza kuwa ,askari wa jeshi hilo Mkoa wapo kamili ,shupavu na majasiri katika kuzuia matukio ya uhalifu kupitia mbinu za kimedani walizowapatia .

  “Sisi jeshi la polisi Mkoa tumejipanga katika kuhakikisha usalama ndani ya mkoa wetu unakuwa ni jambo endelevu sio wakati huu wa sikukuu pekee ,ili kuunga mkono kauli mbiu ya serikali yetu ya Tanzania ya na Tanzania yenye amani’alisema Kamanda Shanna.Kamanda huyo Mkoani hapo alielezea kwamba,usalama ni bidhaa adimu ,usalama unapotoweka watu huweza kukimbia nchi yao na kuitwa walimbizi katika nchi nyingine .

  Hivyo ,Kamanda Shanna alisema watahakikisha wanatunza tunu ya amani iliyopo ili kuweza kuwavutia wawekezaji kuendelea kuwekeza katika Mkoa huo.Jeshi hilo limeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaojaribu kuchezea usalama uliopo mkoani humo .

  Katika hatua nyingine aliwashukuru waandishi wa habari mkoani hapo ,kwa ushirikiano wanaouonyesha kwa jeshi hilo .Kamanda Shanna alibainisha ,ushirikiano huo umemsaidia kwa kiwango kikubwa katika mapambano ya kuzuia na kutanzua uhalifu.

  Aliwaomba ushirikiano uendelee ili kuhabarisha umma juu ya matukio yanayotokea na mikakati wanayoendelea nayo

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akitaka ufafanuzi kuhusu aina ya nyuzi zinazozalishwa na kiwanda cha JOC kutoka kwa Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Jim Liu katika ziara fupi aliyofanya kiwandani hapo leo asubuhi, Desemba 22, 2017. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bibi Maimuna Tarishi na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Tellack.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akipatiwa maelezo na Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC, Bw. Jim Liu wakati alipozuru kiwanda hicho kuona uzalishaji mjini Shinyanga leo asubuhi, Desemba 22, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Tellack.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia bandali la nyuzi zilizosokotwa na kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC, mjini Shinyanga leo Desemba 22, 2017 na kubainishwa kwamba zimetoka Tanzania. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Jim Liu. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  Ataka wampe maelezo ya kina upotevu wa mali za mabilioni

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewanusuru viongozi 19 wa vyama vikuu vya ushirika vya mikoa ya Shinyanga (SHIRECU) na Mwanza (NCU) kwenda selo na badala yake amewapa siku 23 wampe maelezo yatakayomridhisha juu ya mahali zilipo mali za vyama hivyo viwili.

  Amefikia uamuzi huo leo Ijumaa, Desemba 22, 2017 wakati akifunga kikao cha siku moja cha wadau wa zao la pamba alichokiitisha mkoani Shinyanga. Viongozi hao wanatuhumiwa kwa upotevu wa mali zilizokuwa zikimilikiwa na vyama hivyo vya ushirika. 
  “Nataka kila mtu akaandae taarifa kuhusu mali za ushirika zilipo, au zimeenda wapi na kama mlizikopea, mseme ni wapi, lini na kwa ridhaa ya nani. Nataka maelezo ya kutosha kuniridhisha mali za ushirika zimeenda wapi,” alisema Waziri Mkuu. 
  “Hawa nitakaowataja walipaswa kuchukuliwa na RPC, wakatoe maelezo yao na hatua dhidi yao zichukuliwe. Sasa nataka nikutane nao Dodoma ifikapo Januari 15, 2018 saa 3:30 asubuhi ofisini kwangu,” alisisitiza. 
  Kuhusu tuhuma za viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mwanza (Nyanza Cooperative Union - NCU), Waziri Mkuu alisema chama hicho kati ya mwaka 2001 na 2017, kilikuwa jumla ya mali 10 ambazo ziliuzwa kinyemela katika mazingira yenye utata na kwa bei ndogo ikilinganishwa na thamani halisi ya mali hizo zilizopo jijini Mwanza. 
  Aliwataja viongozi waliohusika na upotevu huo ambao wanatakiwa kutoa maelezo yao kuwa ni  Murtazar Alloo ambaye ni mnunuzi wa maghala matatu mali ya NCU, Bw. Samson Ng’halida (mnunuzi wa New Era Oil Mills), Bw. Amos Njite Lili (mnunuzi wa ghala la Igogo), Bi. Antonia Zacharia (mnunuzi wa jengo la KAUMA), Bw. Timothy Kilumile (mnunuzi wa jengo la KAUMA), Bw. Robert Kisena (mnunuzi wa pili wa New Era Oil Mills), Bw. Peter Ng’hingi (aliyekuwa Mjumbe wa Bodi), Bw. Daniel Lugwisha (aliyekuwa Mhasibu Mkuu - NCU), Bw. George Makungwi (aliyekuwa Afisa Miliki - NCU) na Bw. Sospeter Ndoli (aliyekuwa Afisa Utumishi -NCU). 
  Kuhusu mali za Nyanza zinazoshikiliwa na benki ya CRDB. Waziri Mkuu alisema benki hiyo inaidai NCU mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 2.123 na kwamba benki hiyo inashikilia mali 16 zenye thamani ya sh. bilioni 18.132. Alitaka vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili kubaini uwiano wa mikopo na mali zinazoshikiliwa na benki ya CRDB. 
  Kwa upande wa viongozi wa SHIRECU, Waziri Mkuu alisema wanatuhumiwa kwa upotevu wa zaidi ya sh. bilioni 11 ambazo wanadaiwa na benki ya TIB yakiwemo madeni ya mishahara ya watumishi ambayo yanafikia sh. bilioni 1.2.  
  “SHIRECU kwa sasa haina mali zozote kwa sababu mali zote zinashikiliwa na TIB kutokana na mikopo,” alisema.  
  Aliwataja viongozi wa SHIRECU ambao wanatakiwa kutoa maelezo yao kuwa ni Bw. Joseph Mihangwa (Meneja Mkuu), Bw. Sillu Mbogo (Kaimu Mhasibu Mkuu), Bw. Maduhu Nkamakazi (Kaimu Mkaguzi wa Ndani), Bw. James Kusekwa (Kaimu Meneja Uendeshaji) na wajumbe wa Bodi ya SHIRECU.  
  Wajumbe hao wa Bodi ni Bw. Robert Mayongela (Mwenyekiti), Bi. Mary Mabuga (Makamu Mwenyekiti), Bw. Sigu Maganda (Mjumbe), Bw. Clement Bujiku (Mjumbe) na Bw. Charles Lujiga. 
  Waziri Mkuu ambaye aliwasili mkoani humo leo asubuhi, alikwenda kwanza kukagua kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha JOC na kisha kurejea ukumbini kuendelea na kikao cha wadau wa pamba ambacho kimeshirikisha wakuu wa mikoa 16, wabunge, ma-RAS, wakuu wa wilaya, wakulima, wanunuzi wa pamba na wenye viwanda.
  Waziri Mkuu ameondoka Shinyanga kuelekea Ruvuma ambako atakuwa na ziara ya siku moja.  0 0

  Wasimamizi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka wametoa washindi watatu wa sh. Milioni 10 katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka ili kuwapa wachezaji wa droo hiyo kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao, Mmoja wa Maafisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious amesema droo hiyo inachezwa majira ya saa tatu na nusu usiku ambayo inakwenda hadi mwishoni wa mwaka.

  Dina aliwataja washindi hao watatu kuwa ni Hilda Mwaibako,Asha Hamisi pamoja na Anna Ankya,ambao wanatoka katika vitongoji tofauti lakini wote ni wakazi wa jiji la Dar Ess Salaam.

  Dina amesema kuwa washindi wote waliopewa hundi ni kutokana na kushinda mchezo huo kwa kufuata taratibu zilizowekwa za mchezo,Amesema Watanzania waendelee kuchangamkia fursa ya mchezo huo na kuibuka washindi na kufurahi msimu wa sikukuuu na ziku zinazoendelea.''Droo ya walioshinda ni maalumu na wakiona umuhimu wataweza kuitumia na droo zingine zikiendelea,''alisema Dina.

  Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akimkabidhi hundi ya milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka, Anna Nkya kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani), uliofanyika jana jijini Dar. Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Dina Marious akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ,mapema jana jijini Dar,kuhusiana na washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka.
  Washindi watatu wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka waliojishindia kitita cha Milioni 10 kwa kila mmoja, katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka,wakia katika nyuso za furaha kabisa.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (katikati) akimaliza mbio za kilomita tano wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu leo tarehe 23/12/2012
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza akipiga risasi juu kuashiria kuanza kwa mbia za kilomita kumi wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika leo tarehe 23/12/2017 mjini Karatu,kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (katikatika) akishiriki mbio za kilomita tano wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu leo tarehe 23/12/2017, kutoka kulia wakwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo,Afisa utamaduni na michezo wiliya ya Karatu Ndg Laurent P. manonha na wakwanza kushoto kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu Ndg. Waziri Mourice

  0 0


  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta, akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga.

  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta, akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza mahafali ya 16 kampasi ya Dar es Salaam.

  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro (kushoto) akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi.

  Brass Band ikiongoza maandamano.
   Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali. 
  Maandamano ya kitaaluma kuelekea sehemu ya mahafali.

  Maandamano ya kitaaluma kuelekea sehemu ya mahafali.

  Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali. 

  Meza Kuu.

  Wanataaluma.

  Wahitimu.
   Mlau, Prof. Binamungu akitoa nasaha zake.
   Wahitimu wa Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Menejimenti ya Rasilimali Watu. 

  Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.

  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Mathew Luhanga, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. 
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta. 
   Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi (kushoto) akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, wakifuatilia kwa makini mahafali hayo. 

  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akiwatambua wanachuo na wahadhiri waliofanya vizuri.

  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Gloria Mbigiri wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam. 

  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Elihuruma Mabelya wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

  Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Umahiri ya Uongozi wa Biashara katika Menejimenti ya Biashara wakitunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu, Barnabas Samatta (hayupo pichani), wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.

  Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri.

  Wahitimu.
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro.

  0 0

  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk.Edmund Mndolwa amesema ndani ya siku 100 kuanzia jana atahakikisha analipa madeni yote wanayodai watendaki wa jumuiya hiyo huku akitoa onyo kwa wale wenye tabia ya kutengeneza makundi.

  Amesema hayo wakati anazungumza na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumpokea rasmi ambapo amesisitiza kusimamia vema majukumu yake kwa maslahi ya jumuiya na CCM kwa ujumla.

  Kuhusu madeni,amesema anatambua changamoto zilizopo ikiwamo ya watendaji wa ngazi mbalimbali kudai fedha zao lakini hilo atalishughulikia ndani ya siku 100 kwani fedha zipo."Najua changamoto zilizopo kwenye jumuiya yetu,nitumie nafasi kuwahakikishia watendaji wanaodai ndani ya siku 100 tutalipa madeni yote.

  " Nitaboresha maslahi na kubwa zaidi tutanunua vitendea kazi kwani vilivyopo vimechakaa na viachache.Lengo na kuifanya jumuiya yetu kutimiza majukunu yake na tutaendelea kujiimarisha hatua kwa hatua,"amesema.Ametumia nafasi hiyo kuelezea kusikitishwa kwake na tabia ya uwepo wa makundi ambayo kimsingi hayana nia njema zaidi ya  kukiharibu chama chao ,hivyo lazima wakomeshe makundi .

  "Atakayebainika anajihusisha na makundi atachukuliwa hatua,sisi ni wamoja na lazima tusimame katika hilo.Chaguzi zimekwisha ndani ya jumuiya ,sasa tufanye kazi," amesema Dk.Mndolwa.Ametoa onyo kuhusu tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzungumzia mambo ya jumuiya na chama bila kufuata utaratibu.

  Hivyo amesema lazima anayetaka kuzungumza basi ahakikishe anatumia vikao halali ambapo atajenga hoja na kusikilizwa."Atakayezungumza bila kufuata utaratibu hatutamuacha,lazima kanuni na taratibu ziheshimiwe na kila mmoja wetu,"amesisitiza.

  Akizungumzia uchumi,ameweka wazi atatumia elimu yake na maarifa yote kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzisha vitega uchumi na vilovyopo kuvisimamia imara ili viwe na tija.Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ,Frank Kamugisha amempongeza Dk.Mndolwa na kuitumia nafas hiyo kueleza mipango ya kimaendeleo ambayo wampanga kuifanya.

  Baadhi ya mipango ya jumuiya ya wazazi Dar es Salaam ni kuanzisha Saccos na azma yao ni kuwa na benki ya wazazi ambapo amesema kila kitu kinakwenda vizuri na wanachokizungumza si porojo.Pia amesema wanaomkakati wa kuwa na kiwanda ambacho kitakuwa kinazalisha sare na Aprili mwakani timu ya wataalam itakwenda Afrika Kusini ambako lina kiwanda cha kutengeneza sare kujifunza na baada ya hapo watakwenda China kuangalia bei ya mitambo.

  "Haya ambayo tunakueleza mwenyekiti wetu tumejipanga na tunadhamira ya kweli ya kuleta maendeleo katika jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam.Tunaomba tu ushirikiano wenu tutakapopiga hodi mtupokee," amesema Kamugisha.

  Wakati huo aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Wananchi(FUC)Omari Kimbau ameamua kujiunga CCM.

  Amesema  sababu kubwa ni kwamba haoni sababu ya kuwa mpinzani wakati Rais John Magufuli anafanya kazi nzuri kiasi cha wapinzani kutokuwa na ajenda tena.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga. Wengine picha ni kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
  Sehemu ya wakuu wa mikoa inayolima zao pamba wakifuatilia matukio katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati mwenye miwani) akifurahia wimbo na viongozi wengine mara baada ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.

  Wakuu wa wilaya za Shinyanga ambazo ndizo miongoni mwa wakulima wa pamba, kuanzia kushoto ni Fadhil Nkurlu (Kahama), Nyabaganga Taraba (Kishapu) na Josephine Matiro (Shinyanga) na kulia pichani Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi wakifuatilia matukio.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ikiwa ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa pamba, Stephen Magoiga (mwenye kaunda suti aliyeshika karatasi) akifuatilia matukio katika kikao hicho.
  Sehemu ya wakuu wa mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga.
  Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akichangia katika kikao hicho cha wadau wa pamba.
  Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi akichangia katika kikao.
  Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba akizungumza wakati wa kikao hicho.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akitoa neno katika kikao hicho.


  Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Kishapu

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija.

  Ametoa agizo hilo katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga ambapo alizitaka halmashauri hizo kuratibu shughuli za kilimo hicho kwa kuwapangia ratiba maafisa ugani kuwatembelea wakulima kuwapa elimu.

  Akizungumza katika kikao hicho kilichoikutanisha mikoa zaidi ya 10 inayolima pamba aliwataka watendaji wakuu wa halmashauri hizo kuhakikisha kila kata na kijiji kunawepo na maafisa ugani ili wasimamie kikamilifu kilimo.

  Majaliwa aliwataka maafisa ugani waliopo katika halmashauri hizo kuwafikia wakulima mashambani ili kuwapa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu kilimo hususan cha pamba.“Tunataka kuhahakikisha pamba inaleta heshima na inaongeza mapato ya mkulima mmoja mmoja na hata taasisi zetu yaani halmashauri na mikoa zinaingiza mapato kupitia zao la pamba hivyo kila mmoja awajibike,” alisisitiza.

  Pia, aliagiza pia ziweke mpango kazi wa namna ya kukiletea mafanikio kilimo hicho huku akisisi kuwa na kwamba atafanya ziara kukagua akisema atataka apewe taarifa ya maendeleo ya kilimo hicho.

  Aidha alizitaka halmashauri kuwa na takwimu za misimu ya pamba na ziwe zimehifadhiwa vizuri kwenye kompyuta ili popote zikihitajika zipatikane kwa urahisi.“Tumejipanga kusimamia zao la pamba kwani awali uzalishaji haukuwa mzuri mkulima anatumia nguvu nyingi sasa tutasimamia kikamilifu kuanzia maandalizi hadi masoko,” alisema Majaliwa.

  Katika hatua nyingine aliwataka wadau wa kilimo cha pamba maarufu kama dhahabu nyeupe watimize wajibu ili kukifanya kiwe na tija hivyo kuinua uchumi.Majaliwa pia aliagiza wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kujipanga na kuelekeza kuhusu dawa zilizo bora kwa ajili ya zao hilo na Bodi ya Pamba iwajibike kufuatilia maendeleo yake.

  Mkutano huo umewakutanisha pia mawaziri wenye dhamana ya Kilimo, Dk. Charles Tizeba, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala, wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, taasisi za kilimo, wakulima na wanunuzi wapamba.

  PICHA ZOTE NA ROBERT HOKORORO

  0 0

  Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Lydia Joseph (aliyevaa kofia nyeupe) akiendelea na ukaguzi wa bwawa la Rungwa-Itigi, nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola.
  Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola akiwa na watendaji wa serikali na wawakilishi wa Mkandarasi wa bwawa la Rungwa wakitembelea eneo la Bwawa hilo mapema jana.
  Baadhi ya vibarua wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika bwawa la Rungwa – Itigi, Serikali Mkoani Singida imeagiza kazi hio ifanywe na mashine ili kuleta ufanisi na kasi huku vibarua hao wakitakiwa kuendelea na kazi nyingine katika bwawa hilo.
  Sehemu ya Bwawa la Rungwa –Itigi linalojengwa na serikali kwa zaidi ya shilingi milioni mia saba ili kutatua kero kubwa ya maji katika kijiji cha Rungwa.


  Mkandarasi anayejenga bwawa la Rungwa katika Halmashauri ya Itigi amepewa siku saba na Serikali Mkoani Singida kuhakikisha anapeleka vifaa muhimu vitakavyoongeza kasi na ufanisi wa ujenzi wa bwawa hilo.

  Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola ametoa agizo hilo mapema jana mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo na kukuta ukiwa katika asilimia 35 wakati ulitakiwa kuwa asilimia 60 huku baadhi ya vifaa muhimu vikikosekana.

  Nyamkomola amemueleza Mhandisi mwakilishi wa kampuni ya Proactive Independent Group Ltd Elias Gamba kuwa wananchi wa Rungwa hawana maji na juhudi za serikali kuwapatia maji kupitia mradi huo wenye thamani ya zaidi ya milioni mia saba unatakiwa kufanyika kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu.

  Ameeleza kuwa baada ya kufanya ukaguzi katika bwawa hilo wamebaini kuwa baadhi ya kazi zimekuwa zikifanywa kwa kasi ndogo kutokana na kutokuwepo kwa mashine na badala yake kazi hizo kufanywa na vibarua huku vifaa vingine vikiwa pungufu tofauti na makubaliano katika mkataba.

  “Kuna kazi ya kutengeneza zege kwa ajili ya kujenga ukuta katika bwawa hili, ile zege tumeona inachanganywa na vibarua badala ya mashine tuliyokubaliana, mkandarasi unapunguza ubora na kasi inakuwa ndogo, unatuchelewesha kuwapa wananchi maji, hata huu mchanga unaotumika haufai uache kutumika mara moja”, amesisitiza Nyamkomola na kuongeza kuwa,

  “Sasa hivi mlitakuwa kuwa mmeshachimba mtaro wa bomba la kusafirisha maji kwenye matenki kwahiyo ndani ya siku saba hakikisheni kijiko cha kuchimba mtaro huo, mabomba na vifaa vyote vitakavyotumika katika kujengea viwe vimewasili hapa Rungwa”, amefafanua.

  Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Lydia Joseph amesema ujenzi wa bwawa hilo unatakiwa kukamilika kabla ya mwezi Februari mwakani ili serikali na Mkandarasi wapate muda wa matazamio na kurekebisha dosari endapo zitajitokeza pamoja na kuwahi msimu wa mvua ili kuvuna maji hayo.

  Mhandisi Lydia amemueleza mhandisi mwakilishi wa Mkandarasi kuwa anatakiwa kuzingatia makubaliano ya mkataba ikiwemo ubora wa vifaa vya kujengea pamoja na kuleta mashine zote zinazotakiwa ili kazi ifanyike kwa ubora uliokusudiwa.

  Kwa upande wa Mhandisi mwakilishi wa kampuni ya Proactive Independent Group Ltd Elias Gamba amekiri kutumia vibarua kuchanganya zege pamoja na kutumia mchanga tofauti na makubaliano kutokana na mvua zilizonyesha huku akiahidi kurekebisha dosari hizo.

  Mhandisi Gamba amesema kampuni hiyo italeta vifaa hivyo kama walivyoelekezwa na serikali ili kuharakisha kazi hiyo na kuifanya iwe na ubora wa juu kwa kuwa na wao wangependa kuona bwawa linakamilika ndani ya muda waliopewa na likiwa na ubora mzuri.

  Ameeleza kuwa wamekuwa na changamoto ndogondogo ambapo hakuna ambazo zimesababishwa na serikali na kueleza kuwa changamoto hizo ni pamoja na mvua kunyesha na kusababisha kazi kusimama huku mchanga na mawe vikipatikana mbali kutoka eneo la bwawa na huku vibarua wengi wakipungua kutokana na kuanza msimu wa kilimo.

  Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Rungwa Mashaka Juma ameishukuru serikali kwa kufanya jitihada za kutatua kero ya maji kwa wananchi wa kijiji hicho ambao wamekuwa wakinunua maji shilingi mia tano kwa dumu au ndoo yenye ujazo wa lita ishirini.

  “Wananchi wana hamu kubwa kuona bwawa hili linakamilika, maji ni ya shida sana sio wananchi wote wenye uwezo wa kununua maji kwa shilingi mia tano kwa lita ishirini, ndio maana utaona wananchi wengi wanakuja huku bwawani mara kwa mara kuangalia hali ikoje hivvyo tunaomba huyu mkandarasi aongeze kasi”, amesisitiza Juma.

  Mhandisi wa Maji halmashauri ya Itigi Evaristo Mgaya ameeleza kuwa ujenzi wa bwawa la Rungwa lenye mita za ujazo milioni 1.7 umeanza mwezi Septemba 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2018 kwa fedha za serikali zaidi ya milioni mia saba na bwawa hilo linajengwa na kampuni ya Proactive Independent Group Ltd kwa kushirikiana na Bahati Investment and Supply.

  Mgaya amesema maji kutoka katika bwawa hilo yatasafirishwa katika matenki matatu ya kuhifadhia maji ambapo matenki mawili yenye ujazo wa lita laki moja na nusu yatatumiwa na wanakijiji wa Rungwa na tenki moja lene ujazo wa lita elfu 22 litatumika katika hifadhi ya wanyamapori ya Rungwa.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika Manispaa ya Songea leo Desemba 23, 2017 ambako alienda kusikiliza kero yao ya muda mrefu ya kutolipwa fidia.

  Mkazi wa Msamala katika Manispaa ya Songea, Bibi Monica Joseph Miti akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mwengemshindo. Bibi Miti aliomba asaidiwe kurejeshewa nyumba yake aliyotapeliwa na mtumishi wa Manispaa hiyo baada ya mumewe kufariki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

  Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa hiyo.Amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani, Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.

  “Alipotoka kutibiwa India alikuaja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lililkuwa ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi wa kituo cha mabasi cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.

  “Leo nimefanya ziara maalum kwa ajili yenu kwa sababu serikali ya awamu ya tano iko kwa ajili yenu na hasa wananchi wanyonge. Na tatizo hili inalijua. Kabla sijafika hapa, nilipita kwenye eneo husika na afisa mipango miji akanionyesha ramani ya eneo lenu hili,” alisema.

  Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba eneo hilo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo wawekezaji watatu tayari wamekwishajitokeza na wanataka kujenga viwanda vitatu. “Kutakuwa na kiwanda cha kusindika mahindi, kutengeneza pumba za kuku na ng’ombe na mbolea. Kiwanda cha pili kitakuwa ni cha kusindika kahawa na cha tatu kitakuwa ni cha kukamua mafuta ya mbegumbegu,” alisema na kuongeza kwamba reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbaba Bay inatarajiwa kupita kwenye eneo hilo. 

  Akitoa ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa amlipo yao, Waziri Mkuu alisema kwamba katia ya wawekezaji hao watatu aliyekwishalipa fidia ni mmoja tu, na kwamba kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji, fidia inapaswa kulipwa na mnunuzi wa eneo husika.
  Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwepo kwa mapungufu wakati wa ulipaji kwa sababu walifuata orodha ya majina (kialfabeti) badala ya kutoa malipo kwa wakazi wa eneo husika. “Sasa hivi mwekezaji anataka kuanza ujenzi, lakini ndani ya eneo lake kuna watu ambao bado hawajalipwa, kwa hiyo hawawezi kutoka hadi wale waliobakia nao walipwe. Serikali itawafuatilia hawa wawekezaji wengine ili nao walipe fedha zao haraka ili waliobakia waweze kulipwa,” alisema.

  Jumla ya watu 2,179 walifanyiwa uthamini mwaka 2008 na gharama yao kubainika kuwa ni sh. 3,254,737,622. Kuanzia Juni 8-19, 2015, Serikali iliwalipa wakazi 1,179 sh. 1,920,242,121 ambapo kati ya hizo, sh. 1,210,078,261 zilikuwa ni malipo ya thamani ya mali za wananchi na sh. 710,163,860 zilikuwa ni riba kutokana na malipo hayo kuchelewa kufanyika. 

  Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 2,033 (sawa na ekari 5,000) lilitwaliwa na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Ruvuma na Manispaa ya Songea tangu mwaka 2007. Eneo hilo linajumuisha mitaa ya Luwawasi (Mkuzo), Mwengemshindo na Luhira.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Afisa Ardhi wa Manispaa ya Songea, Bw. Kundaeli Fanuel Ndemfoo afuatilie suala la Bibi Monica Joseph Miti na wanae ambao walidhulumiwa nyumba ya urithi na aliyekuwa mwanasheria wa manispaa hiyo.

  Ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mwengemshindo baada ya kupokea bango lililoandikwa na Bibi Miti kuomba arejeshewe umiliki wa nyumba ya marehemu muwewe.

  Alipopewa nafasi ya kueleza tatizo lake, Bibi Miti ambaye alimtaja mwanasheria huyo kwa jina moja la Bw. Mwakasungura, alidai kuwa mwanasheria huyo alighushi hati ya nyumba, na kuwatoa ndani ya nyumba yeye na watoto wa marehemu. 

  Alipoulizwa na Waziri Mkuu aeleze alipo huyo mwanasheria wa manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bibi Tina Sekambo alijibu kwamba alishahamishiwa wilaya ya Ukerewe.
  Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na Afisa Ardhi wa Manispaa wafuatilie suala hilo na wampe majibu mapema iwezekanavyo. Pia amemuomba Bibi Miti na wanawe wafike kuonana naye Januari 3, mwakani atakapokuwa Songea kwa mapumziko mafupi ya mwisho wa mwaka.

  Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku moja mkoani Ruvuma.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMAMOSI, DESEMBA 23, 2017.

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave-Maria Semakafu (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha 'Sote Tunaweza', wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye Bustani ya Target Mbezi Beach Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata Temu (kulia) ni Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Gaudence Temu. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata, akizungumza jinsi alivyoweza kuandaa, kuandika hadi kuprinti kitabu hicho pamoja na changamoto alizopitia hadi kukamilika.
  Uzinduzi ukiendelea

  Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave-Maria Semakafu, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
  Dkt. Ave-Maria Semakafu, akikielezea kitabu hicho jinsi kilivyosheheni masuala mbalimbali yanayohusu fursa na hasa kwa vijana.
  Baadhi ya Warembo wa Kampuni hiyo waliokuwapo katika hafla hiyo kuhakikisha kila jambo linakwenda swa.


  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini changamoto za mtunzi wa kitabu hicho aliyekuwa akielezea hadi kufikia mafanikio.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini changamoto za mtunzi wa kitabu hicho aliyekuwa akielezea hadi kufikia mafanikio.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini changamoto za mtunzi wa kitabu hicho aliyekuwa akielezea hadi kufikia mafanikio.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini changamoto za mtunzi wa kitabu hicho aliyekuwa akielezea hadi kufikia mafanikio.
  Baadhi ya wageni waalikwa....
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini yaliyoandikwa ndani ya kitabu hicho kama yalivyokuwa yakisomwa na Asha Mtwangi.....


  Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini yaliyoandikwa ndani ya kitabu hicho kama yalivyokuwa yakisomwa na Asha Mtwangi.....
  Umakini wa kusikiliza matamu yaliyo ndani ya kitabu hicho  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata Temu, akisaini katika baadhi ya vitabu vilivyouzwa kwa wadau mbalimbali wakati wa hafla hiyo....
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata Temu, akimkabidhi mmoja wa wageni waalikwa aliyenunua kitabu chake wakati wa hafla hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viva Legancy Ltd, Fortunata Temu, akipozi kwa picha na baadhi ya 'Class Mate' wakati wa hafla hiyo

  0 0

  Na Joel Maduka, Geita

  Wafugaji Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,wamemuomba Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega kuingilia kati manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka kwa watu wa maliasili ambao wamekuwa wakichukua mifugo yao na mwisho wa siku kupigwa mnada bila ya kufikisha mahakamani hali ambayo imekuwa ikiwasababishia umasikini.

  Imeelezwa kuwa baadhi ya Minada ya Ng’ombe wanaokamatwa katika Mapori ya Hifadhi imekua ikifanyika kinyume na kwa udanganyifu hasa ambapo katika mnada uliofanyika hivi karibuni Wilayani Bukombe imegundulika katika Ng’ombe waliopigwa mnada 1600 kati yao 500 haijulikani ilipo huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa Wafugaji.

  Akizungumza kwa niaba ya wafugaji Bw,kwa niaba ya wafugaji Bw,Emmanuel Maricholi wanzake amemweleza naibu waziri kuwa wamekuwa wakikutana na shida kubwa pindi mifugo yao inapokamatwa na kwasasa wafugaji wengi wamefilisika kutokana na hali ya mifugo yao kukamatwa na kupigwa mnada bila ya kuwepo kwa maelewano baina yao na watu wa maliasili na kwamba ni vyema wakaitazama kwa makini sheria ambayo inafanyiwa kazi kwa sasa kwani imewafanya kuwa masikini zaidi.

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko alisema ana taarifa ya baadhi ya Watu wanafaidika na Mnada huo kwa manufaa yao wenyewe lakini pia amewataka Wafugaji kuvuta subiri juu ya mabadiliko ya sheria ambayo yanaendelea kwani ukiangali sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 ilikua inatoa adhabu ya vitu vitakavyokamatwa katika Mapori ni kutaifishwa na Marekebisho yameplekwa bungeni na ishasomwa mara moja yenyewe inaondoa adhabu ya kutaifisha na badala yake kuna faini.

  Aidha,Mh Doto Biteko ameongeza kuwa anatambua serikali imeendelea kujishughulisha na watu masikini na kwamba ni lazima wafugaji wakaelimishwa hili wajue sheria na wajue kuyatunza mazingira kabla ya kuendelea kuwahukumu kuwa wanaharibu mazingira na kwamba kuna watu ndani ya idara wamekuwa na tabia ya kukamata mifugo kwaajili ya kujipatia fedha hata kabla ya mnada.

  Hata hivyo kwa upande wake Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega,amewataka wafugaji kutokukataa tamaa na kusubili hadi pale watakapo kuwa wameweka sheria mpya huku akivitaka Vyombo vya Dola kuchunguza tuhuma za uendeshaji wa minada ya Ng'ombe na hatua za haraka zichukuliwe kwa wote ambao wamefanya minada hii kujinufaisha na kuwanyanyasa .
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa Ng'ombe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe wakati alipofika kuwasikiliza kilio chao. 
  Naibu Waziri akifatilia kero mbalimbali ambazo zimetolewa na Wafugaji ikiwemo kukamatwa kwa Ng'ombe zao lakini hawapewi taarifa ya aina yoyote hata wakipelelkwa mahakamani na matokeo yake Ng'ombe zao zinapotea katika mazingira ambayo yanadaiwa ni ya uonevu. 
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko akizungumza na kuelekezea matatizo ambayo yameendelea kuwakumba wafugaji ambao wapo kwenye jimbo analoliongoza ndani ya wilaya ya Bukombe. 
  Baadhi ya Ng;ombe ambao wamepigwa mnada.


  0 0

   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi wa wana CCM waliofurika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambao walifika kumlaki katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam, jana.
   Gari la Dk. Mndolwa likiwasili lango Kuu la Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi hayo
   Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar  Abdallah Haj Haidar akimpokea Dk Mndolwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam
   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisilindikizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba kwenda kusaini vitabu wa wageni na kuzungumza na uongozi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
   Dk. Mndolwa akisaini kitabu wa wageni katika Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alipowasili. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kalokola Kamngisha
   Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Abdallah Haj Haidar akisaini kitabu cha wageni, huku Dk. Mndolwa akiendelea kufanya hivyo pia.
   Abdallah Haj Haidar akisalimia
   Mama Patricia Rukia Mndolwa akisalimia
   Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Bara Burhan Rutta akisalimia
   Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kusilawe akisalimia
   Kalokola akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, amkaribishe Dk. Mndolwa kuzungumza na Uongozi
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alizungumza kabla ya kumkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza
   Kate Kamba akimkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza na uongozi
   Dk. Mndolwa akizungumza na Uongozi
   Mwafongo na Katibu wa CCM Kata ya Ilala Habib Nasser ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, wakitoka nje kumsubiri Dk Mndolwa kutoka nje tayari kwa safari ya kwenye kwenye eneo kuu la mapokezi ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala
   Gari lilobeba Dk Mndolwa likiwasili kwenye Viwanja vya Ofisi ya Tawi la CCM Mwinjuma 
   Kijana wa CCM akimvisha Skafu Dk. Mndolwa baada ya kuwasili CCM Mwinjuma
   Dk. Mndolwa akipokea kwa ukakamavu saluti ya kijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu
   Dk Mndolwa akiongozana na baadhi ya viongozi kwenda eneo la tukio
   Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya wana CCM wakati akienda ukumbini
   Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wakati akienda ukumbini  
   TOT wakitumbuiza kumlaki ukumbini Dk. Mndolwa
   Dk. Mndolwa akienda meza kuu
   Dk. Mndolwa na Makamu wake- zanzibar wakiwa tayari meza kuu
   Viongozi wa meza kuu wakiungana na Dk Mndolwa kushangilia baada ya kuwasili eneo hilo
   Mmoja wa viongozi katika Baraza la Wazee wa jumuiya ya Wazazi Mzee Mkali akisalimia
   Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akifanya utambulisho wa viongozi ndazi ya mkoa
   Viongozi ndazi ya mkoa wakisalimia baada ya kutambulishwa 
   Baadhi ya viongozi waliohudhuria mapokezi hayo wakiwa ukumbini
   Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya wazazi Tanzania Ndugu Rutta akitambulisha viongozi ngazi ya taifa  
   Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi tanzania Seif Shaban Mohammed akifafanua maana na umuhimu wa neno 'Mapinduzi'  baada ya kutambulishwa  
   Ndugu Mwafongo akiendeleza ratiba
   Mwenyekiti wa CCM Temeke ndugu Almish akizungumza baada ya kutambulishwa 
   Ndugu Kalokola akizungumza kumtambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Haj
   Kakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Hajj akizungumza
   Shabiki wa CCM akimuombea maisha marefu na uongozi bora Dk. Mndolwa tukio ambalo lilikuwa la ghafla
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Mndolwa kuzungumza na hadhara 
   Omar Kimbau aliyewahi kuhamia CUF akitangaza kurudi CCM mbele ya Dk. Mndolwa
   Dk. Mndolwa akimpongeza Kimbau kwa kuzinduka na kurejea CCM
   Dk. Mndolwa akihutubia kweye mapokezi hayo

  CHAKULA CHA JIONI SERENA HOTEL
   Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akiwakaribisha Dk. Mndolwa na Mkewe walipowasili hoteli ya Serena kwa ajili ya chakula cha jioni
   Mwafongo akiwaongoza kwenda eneo la kuketi 
   Dk. Mndolwa akimsalimia Mwenyekiti  wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kalokola
   Dk Mndolwa akimsalimia  Ndugu Kizigha
   Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania- Zanzibar Ndugu Hajj akimsalimia Mama Mndolwa
   Dk Mndolwa akizungumza jambo wakati wakisubiri muda wa chakula
   Ndugu Mwafongo akiwa amesimama kuwakaribisha rasmi waalikwa wote 
   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Kalokola akizungumza maneno ya ukaribisho kwenye chakula hicho cha jioni
   Dk Mndolwa akiongozana na Ndugu Hajj kuchukua chakula
   Angela Kizigha akimsaidia Dk. Mndolwa kubeba chakula
   Mweneyekiti wa CCM Kinondoni akichukua chakula
   Viongozi mbalimbali wakichukua chakula
   Ndugu Mwafongo akiongoka na chakula chake kwenda sehemu ya kuketi
   Ndugu Hajj akichukua chakula 
   Baadhi ya waandaaji wa nyama choma hotei ya Serena
   Waalikwa wakila chakula 
   Dk Mndolwa na mkewe wakipata chakula na waalikwa wengine  

   Dk Mndolwa akitoa nasaha zake baada ya chakula   
  Kisha Dk. Mndolwa akapozi kwa picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali aliopata nao chakula hicho cha jioni. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

older | 1 | .... | 1469 | 1470 | (Page 1471) | 1472 | 1473 | .... | 1897 | newer