Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

JPM aunda Tume ya 'Makinikia' ndani ya Chama cha Mapinduzi kufuatilia mali ya chama hicho nchi nzima

$
0
0



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Katibu Mkuu wa (CCM) Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwasili katika eneo la Mkutano na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya (CCM) NEC uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya (CCM) NEC (hawaonekani pichani) katika eneo la Mkutano mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa (CCM) Abdulrahman Kinana
Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano wa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya (CCM) NEC uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya (CCM) NEC mjini Dodoma. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein aliyeketi pamoja na Katibu Mkuu wa (CCM) Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya (CCM) NEC mjini Dodoma.
Wajumbe mbalimbali wa NEC wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasikiliza wajumbe mbalimbali wa NEC walipokuwa wakijitambulisha katika mkutano huo wa NEC mjini Dodoma.

WAFANYAKAZI WA ZANTEL WASHIRIKI ZOEZI LA MPIRA WA MIGUU, UWANJA WA MALINDI ZANZIBAR.

$
0
0

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakishiriki kucheza mpira wa miguu hivi karibuni mjini Zanzibar, baada ya wafanyakazi hao kukutana mjini humo katika hafla ya kupanga mikakati ya Kampuni hiyo kwa mwaka 2018.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kushiriki shindano la mpira wa miguu hivi karibuni mjini Zanzibar, baada ya wafanyakazi hao kukutana mjini humo katika hafla ya kupanga mikakati ya Kampuni hiyo kwa mwaka 2018.

JAFO AAGIZA MANISPAA DODOMA IPIME HARAKA VIWANJA NA AMFAGILIA MBUNGE MAVUNDE KWA KUWAJALI WANANCHI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza na wananchi kata ya Iyumbu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni katika shule ya msingi Iyumbu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika kata ya Iyumbu.
Mbunge wa Viti maalum Felista Bura akizungumza na wananchi wa kata ya Iyumbu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akifurahi jambo na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akisalimia na baadhi ya viongozi wa kata ya Iyumbu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akiwapungia mkono wananchi wa Iyumbu.
baadhi ya waannchi kwenye mkutano Iyumbu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipokea zawadi

……………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi kuhakikisha wanapima viwanja haraka ili kuufanya mji wa Dodoma uendane na kasi ya ongezeko la idadi ya watu wanaohamia Dodoma na kuufanya mji uliopangwa kwa utaratibu unaoeleweka.

Jafo ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Shule ya Sekondari Iyumbu-Dodoma Mjini,ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake wa Jimbo la Dodoma Mjini.

Mbali na hilo, Jafo ameagiza fedha kiasi cha sh.milioni 10 zilizopo kwenye akaunti ya kata hiyo ambazo zilitakiwa kutumika kupaulia darasa la shule ya sekondari Iyumbu kutumika kujenga madarasa manne.

Kwa upande wake, Mavunde amesema katika Manispaa ya Dodoma kuna upungufu wa vyumba vya kusomea zaidi ya 1000.Amesema wamekubalina na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuanzisha kampeni maalumu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kupitia wadau mbalimbali ambapo wao watapokea vifaa tu kama Saruji.

Awali katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Manispaa Kunambi amesema tayari Manispaa imeshatoa Sh.Milioni 10 kusaidia ujenzi huo na pia ameahidi kusimamia ujenzi wa Sekondari hiyo ili kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule za Sekondari.

Wakizungumzia hatua hiyo, Wananchi wa kata Iyumbu wameshukuru sana jitahada za viongozi katika kuwaletea maendeleo na kutatua changamoto zao na kuahidi kujitolea kukamilisha ujenzi huo.

SHONZA AFUNGA MICHEZO YA VYUO VIKUU TANZANIA (TUSA) MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akimvisha medali golikipa wa timu ya mpira wa miguu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Ahmad Suleiman wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. Chuo Kikuu cha Zanzibar waliibuka washindi wa mpira wa  miguu kwa wanaume.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. OUT waliibuka washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume dhidi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na washiriki wa Michizo ya Vyuo Vikuu (Hawapo Pichani) wakati akifunga fainali za Michezo hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. Waliokaa kulia kwake wa kwanza ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde,Wa pili ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris Kikula na Mtangazaji wa Clouds Fm Ndg. Shafii Dauda. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijiandaa kufunga kikapu wakati wakufunga Michezo ya Vyuo Vikuu kwenye Mchezo wa Fainali ya mpira wa kikapu kati ya timu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tanzania (OUT) na Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM) iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017, wa Pili kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde. OUT waliibuka washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume.

Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China

$
0
0
Wziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya Nje cha China kabla ya wawili hao hawajaelekea kwenye ukumbi kuhutubia wanafunzi. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augastine Mahiga akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China. Dkt. Mahiga alieleza ushirikiano wa Tanzania na China ulipoanza hadi leo na kuwasihi wanafunzi hao waangalie namna y kuuimarisha kutokana na nafasi zao. 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China wakisikiliza Hotuba ya Dkt. Mahiga. Wanafunzi hao ambao walikuwa wadadisi sana walifurahi sana kutokana na elimu ya siku moja waliopata kutoka kwa Mbobezi wa masuala ya Diplomasia. 
Dkt. Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu vingi sana. 
Ujumbe uliomsindikiza Waziri Mahiga, kutoka kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Gerald Mbwafu, Katibu wa Waziri na Kanali Remigius Ng'umbi, Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China. 
Mstari wa Mbele kutoka kushoto ni Kamishna msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mtagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Vwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Zanzibar, Bw. Khams Omar na Balozi wa Tnzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki wakifuatilia hotuba hiyo. 
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China akiuliza sawali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga. 
Picha ya Pamoja. Ziara katika kampuni ya magari ya Foton Motors Group
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kampuni ya Foton Motors Group kabla ya kuanza kutembelea kampuni hiyo kujionea shughuli zake. 
Baadhi ya aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya karakana ya Foton Motors Group kuangalia shughuli za uzalishaji wa magari zinavyofanyika. 
Baada ya kuona shughuli za kampuni hiyo, Waziri Mahiga alifanya mazungumzo rasmi na viongozi wa kampuni hiyo ambapo walimuomba awasaidie ili waweze kuwekeza nchini Tanzania. Kampuni hiyo inataka kufungua kiwanda cha kuunganisha magari yao kwa lengo la kuuza Tnzania na soko la Afrika. Walisema kampuni yao inatengeneza magari ya aina yote makubwa, madogo, mabasi na malori ndio inayoongoza kwa mauzo nchini China kwa kipindi cha miaka 13 sasa. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea zawadi ya mfano wa moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant inayowekeza kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Makamu wa Rais huyo pamoja na mambo mengine alielezea kufurahishwa kwake na uamuzi wa Serikali kuidhinisha rasmi utekelezaji wa mradi huo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO DECEMBER 21,2017

TANGAZENI MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI-MWAMANGA.

$
0
0

Na Estom Sanga- TASAF

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- bwana Ladislaus Mwamanga amewaagiza Maafisa Ufuatiliaji na Waratibu wa Mfuko huo ngazi ya halmashauri za Wilaya nchini kote kushirikiana na Vyombo vya Habari kutangaza mafanikio ya utekelezwaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwenye maeneo yao.

Bwana Mwamanga amesema serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- imefanikiwa kuzikifia kaya za wananchi waliokuwa wanakabiliwa na hali ya umaskini wa kipato ambao wameanza kukabiliana na kadhia hiyo kwa kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Akizungumza katika siku ya pili ya kikao kazi cha watumishi, Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ametoa mfano wa Mafanikio yaliyoanza kupatikana tangu kaya za walengwa kujumuishwa kwenye shughuli za Mpango, amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa katika uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana miongoni mwa walengwa na hivyo kukuza mitaji yao na kuibua shughuli za kiuchumi hususani biashara ndogo ndogo.

Aidha bwana Mwamanga amesema walengwa wa TASAF wameanza kuboresha makazi kwa kuezeka nyumba zao kwa mabati baada ya kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kutokana kutokana na ruzuku inayotolewa na serikali kupitia TASAF huku kukiwa na mwitikio chanya katika sekta za elimu, afya na lishe kwa kaya za Walengwa.

Kutokana na mafanikio hayo,Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema jitihada hizo zilizofanywa na serikali kupitia TASAF zinapaswa kuwekwa bayana na hivyo kuwaagiza Watendaji wote walioko kwenye halmashauri za Wilaya kushirikiana na Vyombo vya habari kutangaza mafanikio hayo ili kuwawezesha wananchi kutambua jitihada za kukabiliana na umaskini .

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesisitiza watumishi wa Mfuko huo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa ili Mfuko huo uendelee kuaminiwa na Serikali na Wadau wengine wa Maendeleo kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mwelekeo wa siku zijazo za utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo ni kuhakikisha kuwa walengwa wake wanatumia vyema fursa hiyo kwa kushiriki kwenye shughuli za ujenzi wa miradi ya Maendeleo na kujiongezea kipato kama njia mojawapo ya kuboresha maisha yao. 
Mmoja wa Walengwa wa TASAF katika halmashauri ya mji wa Tabora, akimwonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika nyumba aliyoanza kuijenga baada ya kujiongezea kipato kwa kuanzisha mradi wa biashara ya mboga na matunda kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF. Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza wakati wa kikao kazi cha watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya Watumishi wa TASAF wakimsikiliza meneja wa miradi ya kutoa Ajira, Mhandisi Barnabas Jachi aliyeshika kipaza sauti) alipokuwa akielezea manufaa ya miradi ya ajira za muda katika kuongeza kipato cha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Baadhi ya Watumishi wa TASAF wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi (hayupo pichani )alipozungumza kwenye kikao kazi cha taasisi hiyo kinachojadili pamoja na mambo mengine namna uboreshaji wa huduma zake  kwa wananchi.

WAUGUZI NI CHACHU YA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Gustav Moyo akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya maadili kwa wauguzi wakuu wa Mikoa na hospitali za Kitaifa na za Rufaa za kanda unaoendelea chuo cha Uuguzi Mirembe Mkoani Dodoma.
Wauguzi wakuu toka mikoa mbalimbali wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mafunzo hapo.mafunzo hayo yana lenga kuwakumbusha uadilifu na maadili ya uuguzi wakati wa utoaji huduma za afya nchini.
Baadhi ya wauguzi wa mikoa wakijadili kwenye makundi mikakati ya nini kifanyike katika kutekeleza majukumu yao ili kuondokana na malalamiko ya taaluma yao kutoka kwa wananchi.
Wauguzi wakuu wakiendelea na kazi kwenye makundi.
Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga Gustav Moyo akiongea na wauguzi wakuu wa mikoa kwenye mafunzo hayo.

Muuza mpunga wa Kisaki ashinda milioni 86. 2 ya M-Bet

$
0
0
Mkazi wa Mvua, Kisaki mkoani Morogoo, Fredy Masawe (35) ameishinda Sh milioni 86.2 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

Masawe ambaye ni shabiki wa timu ya Manchester United ya Uingereza alifanikiwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 17 za mchezo na kufanikiwa kuwa mshindi pekee wa droo ya 20 ya mchezo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley alisema kuwa Masawe ni mshindi wa tatu kwa mwezi huu kupaza zawadi kiasi kikubwa cha fedha na serikali kupata ya jumla ya Sh milioni 15 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria. “M-Bet ipo kwa ajili ya kuwanufaisha mashabiki wa soka hapa nchini, watashindi kibao wamefanikiwa kubadili maisha baada ya kujishindia fedha nyingi na sasa amekuwa mtu wa kipato kingine tofauti na alivyokuwa awali,” alisema Malley.

Alisema kuwa kiasi cha Sh 1,000 tu kimeweza kumnufaisha Masawe ambaye sasa ataweza kuendesha maisha yake tofauti na kuanzisha biashara mbalimbali. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Masawe alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa kupanua biashara yake ya kuuza mpunga.

“Sikuamini nilipoambiwa kuwa nimeshinda kiasi hiki cha fedha, kule kwetu Mvua, tumeweka eneo la kubashiri mchezo huu chini ya mwembe, nimebeki mara nyingi sana, na kupata fedha ndogo ndogo, sikukata tamaa kwa kukosa kushinda na leo nimekuwa mshindi, kwa fedha hizi pia nitamalizia nyumba yangu ya kuishi na kuwa ya kisasa, ” alisema Masawe.

Mke wa Masawe, Elizabeth Chifungo (26) alisema alikuwa anamzui mume wake kucheza mchezo huo kwa kuamini kuwa alikuwa anapoteza fedha. “Nilimzuia sana, akakataa na kuendelea kucheza, nimeamini kuwa michezo hii ya kubashiri ni ya ukweli, nawaomba watanzania kuendelea kubashiriki, kwa ushindi huu, nami nitaongeza mtaji wa biashara yangu,” alisema Elizabeth.
Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (kulia) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Fredy Masawe (katikati) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 86.2. anayeshuhudia ni baba wa Mshindi huyo, Geofrey Masawe.
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Fredy Masawe (kushoto) akiwa na mkewe, Elizabeth Chifungo wakifurahia mara baada ya kukabdhiwa zawadi yake. Masawe alishinda kitita cha sh milioni 86.2

TANESCO "YALIA" NA WAHARIBIFU WA MAZINGIRA MITO INAYOLISHA BWAWA LA MTERA

$
0
0
 Taswira ya daraja la Mtera, ambalo pia hutumika kama milango ya kupitishia maji ya kusukuma mashine za kufua umeme. picha hii imepigwa Desemba 20, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtera


UHARIBIFU wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za kibinadamu kwenye bwawa la Mtera sio tu unaathiri kiasi cha maji kwa matumizi ya Kituo cha kufua umeme cha Mtera bali pia unaathiri pakubwa kituo kingine cha kufua umeme cha Kidatu mkoani Morogoro, Mtaalamu wa Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote amewaambia waandishi wa habari waliotembelea Kituo cha Kufua Umeme wa Maji cha Mtera, kilichoiko mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa.

Ukiachilia mbali mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kibinadamu kandokando ya mito, kunachafua mazingira ya mito hiyo na kupunguza kiasi cha maji na hivyo kuathiri uzalishaji umeme wa maji.

“Tatizo hili ni kubwa watu wanaingilia mito hii, kuna wakulima na wafugaji wanathiri sana, shughuli za kilimo na ufugaji zinaleta mchanga mwingi kwenye maji na hivyo kupunguza kina cha mto na maji yenyewe tunaita siltation, na hiyo ikitokea ujio wa maji kwenye mitambo unapungua na hivyo uzalishaji unapungua kama hivi sasa mnavyoona maji yamepungua.” Alisema.

Bw. Kamote aliwaasa wananchi kuacha kuaharibu mazingira kwani athari zake ni kubwa katika kuendesha mitambo ya kufua umeme ambao ni muhimu kwa uchumi wanchi.“Yawezekana wanafanya shughuli hizo kwa kutokujua athari zake katika uzalishaji umeme, kwa hivyo tunashauri wananchi waelewe kwamba hilo ni tatizo na waache.” Alisetoa rai Bw. Kamote.

Naye Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji Mtera, Mhandisi David Myumbilwa, ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa Ujenzi, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 1988 lilikuwa ni kutunza maji kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kufua umeme wa maji kwenye kituo cha Kidatu mkoani Morogoro kabla ya kuongeza matumizi ya kituo hicho na kufanya kazi zote mbili kufua umeme na kutunza maji (water storage).

“Kidatu ndio kilikuwea kituo lengwa cha kufua umeme wa maji wakati huo, lakini baada ya wataalamu kuona maji yanayotumika kwa kazi hiyo ni kidogo ukilinganisha na mashine zilizokuwepo pale ikaonekana upo umuhimu wa kutengeneza storage ya maji hapa Mtera na bwawa hili ndio kubwa kabisa katika mabwawa ya kufua umeme wa maji nchini.” Alisema Mhandisi Myumbilwa.

Alisema, kiwango cha juu cha ujazo wa maji kwenye bwawa hilo ambao unahitajika kwa ajili ya kuendesha mitambo ni 698.5 m.s.a.l na kiwango cha chini ni 690 m.s.a.l, chini ya hapo kwa usalama wa mitambo lazima izimwe.Mhandisi Myumbilwa amesema, Bwawa hilo linategemea maji kutoka mito mitatu, Mto Kizigo unaotoka mkoani Singida, Ruaha Mkuu, na Ruaha ndogo.

“Mto Kizigo ni mto wa msimu wakati wa kiangazi unakauka, Ruaha ni mto asili na hapo nyuma ulikuwa na kiwango cha juu cha maji lakini hivi sasa maji hakuna kabisa, na huu ndio mto mkubwa unaotegemewa na Kituo cha Mtera.” Alifafanua.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji alisema lengo la ziara hiyo, ni kuweapa uelewa wahariri ili kujionea juhudi za TANESCO katika kuhakikisha vyanzo vya maji yanayozalisha umeme vinatunzwa kwani umeme wa maji ndio umeme nafuu zaidi.

“Mtakumbuka kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri katika kipindi cha tunatekeleza alisema baadhi ya mashine za kufua umeme wa maji zinatengenezwa na kama zinatengenezwa maana yake haitatoa umeme kwa kiwango chake cha kawaida.” Alisema.
Milango ya kuruhusu maji kupita kwenye Bwawa la Mtera.
Mtaalamu wa Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote, akielezea jinsi mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za kibinadamu zinavyoathiri bwawa la Mtera. Kushoto ni Mhandisi Myumbilwa
Daraja la Mtera, ambako pia ndiko iliko milango ya kupitishia maji ya kufua umeme
Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji Mtera, Mhandisi David Myumbilwa, akielezea jinsi mashine za kufua umeme zinavyotegemea maji.
Wahariri na maafisa wa TANESCO, wakiwa kwenye eneo la Bwawa la Mtera, ambalo linategemewa kutoa maji ya kuzalisha umeme kwenye kituo cha Mtera na Kidatu mkoani Morogoro, na hii ndio hali halisi kama picha hii ilkiyopigwa Desemba 20, 2017 inavyoonyesha
Mhandisi Myumbilwa na baadhi ya wahariri
Mwendesha mitambo Mwandamizi kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji cha Mtera, Mhandisi Asanterabi Naaman, akitolea ufafanuzi wa jinsi wanavyosimamia mitambo hiyo wakiwa shimoni, (mgodini), kwenye kituo hicho,
Wahariri wakiangalia jinsi moja kati ya mashine mbili za kufua umeme wa maji inavyofanya kazi
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kushoto), akiwa na wasimamizi wa chumba cha udhibiti mwenendo wa mitambio kilichoko chini ya ardhi kwenye kituo cha kufua umeme wa maji Mtera.
Mhariri wea Mwanancvhi, Bi. Lilian Timbuka.
Bi. Leila Muhaji, akiwapongeza wasimamizi wa chumba hicho
Fundi wa umeme mdogo, Elisha Kamenya akiwa kazini.

MASHEHA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAPEWA TAARIFA YA UJENZI WA BARABARA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Mustafa Aboudjumbe kushoto akijibu maswala mbalimbali yalioulizwa katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Sheha wa Shehia ya Matemwe Denge Khamis Silima akiuliza maswali katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa  Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Hassan Ali Kombo akiliza maswali katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa  Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud kulia akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Vuai Mwinyi Mohammed kulia akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.PICHANA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

ANTU MANDOZA KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUIGIZA NA RAMSEY NOAH KUTOKA NCHINI NIGERIA

$
0
0
 
 Antu Mandoza akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwigizaji nyota wa filamu na Mkongwe wa tasnia hiyo kutoka nchini Nigeria ,Ramsey Noah ametamani kufanya kazi na nyota mwingine wa movie anaechipukia kwa kasi katika tasnia hiyo hapa nchini,ambae ameng'ara vilivyo katika filamu ya 'KIUMENI' , Antu Mandoza wa Tanzania . 
"Anaonekana ni binti mweye kipaji,anaejiamini,kwa hakika natamani nipate muda wa kubaini kipaji chake zaidi kwa kufanya nae angalau hata filamu moja,itaweza kumsaidia zaidi kujitanua na kutambulika Kimataifa",alisema Ramsey huku akimtazama Antu kwa tabasamu laini la ucheshi.
Antu Mandoza ni Binti wa makamo hivi,lakini amejaaliwa kuwa na kipaji cha uigiza wa filamu na mwenye uthubutu wa kufanya jambo.Antu Mandoza na Ramsey Noah walikutana katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Sahara Group iliyofanyika hotel ya Hyatt Dar Es Salaam mnamo Desemba 16 2016,ambayo pia iliwahusisha wasanii mbali mbali wa bongo movie .
 Ikiwa ni movie yake ya kwanza 'KIUMENI', Antu Mandoza amefunguka na kusema kuwa mwaka ujao utakua ni mwaka wa kazi tu, kama ilivyo Slogan ya Raisi Dkt John Pombe Magufuli,na anategemea kufanya kazi na Ramsey Noah na wasanii wengine wengi wa Ndani na Nje ya Tanzania. 
Antu alijipatia Umaarufu katika filamu ya Kiumeni aliyocheza na Ernest Napoleon,ambayo lishinda tuzo 2 ZIFF mwaka 2017.

Sanlam General Insurance Empowers General Insurance Agents

$
0
0
Sanlam General Insurance conducted a day long training session at Serena Hotel in Dar es Salaam. The event was attended by over 45 agents from different firms and regions.

The train focused on different areas such as Use of Modern Technology on Premium Payments and Collections the insuring public, Finance management, Market Developments and new regulations.

The Chief executive Officer, Mr Manasseh Kawoloka, who officially opened this event shared with gathering new developments and regulations that have been recently introduced in insurance industry. He emphasized the requirement that all agents should understand and comply with the regulatory changes introduced in the market. The new law requires the client to pay premium before or on the date of commencement of the insurance cover.

On the other hand, as part of improving service delivery on how Agents do business, Sanlam General has introduced a new system to their Agents that will assist to improve the work flow and business in general. The system will reduce manual transaction between the Agents, their Clients and Sanlam General especially on covernote issuance, premium payments and collections.

“Sanlam General believes that training Agents is part of doing business the right way and it is something that is enjoyed and like to do. Trainings on this nature offers opportunities to interact with agents more freely and in informal way”, said Business Development Manager Mr. Jabir Kigoda.

Agents were very excited and pleased with the training and they are looking forward for more opportunities for training in the year ahead 2018.
 Sanlam Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka.
 Sanlam Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka.Introducing Sanlam General Insurance Management Team. On his right is Business Development Manager -Mr. Jabir Kigoda, on his left is Chief Finance Officer, Mr. Geofray Masige, and Chief Operating Officer, Mr. Lester Chinyang’anya (gray suits)
 Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka opening the event
Business Development Manager, Mr. Jabir Kigoda taking questions from.

TAKUKURU TANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAHASIBU WAWILI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA KWA MASHTAKA MATATU YA RUSHWA

$
0
0
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Tanga(Takukuru) imewafikisha mahakamani wahasibu wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga Josiah Mwaipela na Julius Idana kwa mashtaka matatu ya rushwa. 

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya
uchepushaji,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni 276,095,106.9 za mishahara ya watumishi ambaowalikoma utumishi wao wa umma kati ya Machi 3 ,2012 na Novemba 2013. 

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana Desemba 18 mwaka huu. Alisema washtakiwa hao walifikishwa mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Tanga,Crisencia Kisongo na kusomewa mashtaka na waendesha mashitaka wa Takukuru Noel Gabba na Neema Kazoka. 

Alisema washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa ya uchepushaji,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni 276,095,106.9 za mishahara ya watumishi ambao walikoma utumishi wao wa umma kati ya Machi 3 ,2012 na Novemba 2013. 

Aidha alisema katika shitaka la kwanza upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa kati ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013 washtakiwa walifanya uchepuzi wa sh.milioni 276,095,106 ambazo ni mali ya serikali kwa malengo yasiyokusudiwa. Katika shtaka la pili upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa kati ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013 washtakiwa walifanya ufujaji na ubadhirifu wa sh.milioni 245,500,000 walizoaminiwa na kukabidhiwa na serikali. 

Alisema katika shtaka la tatu upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa kati ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013 washtakiwa kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuziweka sh.milioni 276,095,106.96 za mishahara isiyolipwa kwenye akaunti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT). Kamanda huyo wa Takukuru alisema washtakiwa walikana mashtaka dhidi yao na upande wa mashtaka uliiambia Mahakam kuwa uchunguzi wa shauri umekamilika na uko tayari kuendelea na shauri kwa tarehe itakayopangwa na mahakama. 

“Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 2 mwakani itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali “Alisema Kamanda huyo wa Takukuru. Hata hivyo alisema mshtakiwa wa kwanza Josiah Mwaipela aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na Mahakama ambapo aliweka bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 69,023,776.74 iliyowekwa na mahakama na mdhamini mmoja. 

Aliongeza pia mshtakiwa wa pili Julius Idana alipelekwa gereza kuu la Maweni Tanga baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kukabidhi fedha taslimu sh.milioni 69,023,776.74 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo pamoja na kuwa na mdhamini mmoja. 

Kamanda huyo wa Takukuru alisema kati ya kiasi cha sh.miloni 276,095,106.96 zilizofanyiwa uchepuzi na washtakiwa sh.milioni 25,602,855.31 ziliokolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru na kurejeshwa serikalini.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAZINDUA VYOMBO VYA KUSIMAMIA BIASHARA YA UTALII NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Wajumbe na Wenyeviti  kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha  Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na  Mwenyekiti wa Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii  Saleh Pamba ( wa pili kushoto)   katika hafla ya uzinduzi wa  vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii (TTLB) nchini iliyofanyika  leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Alovce Nzuki,     ( wa tatu kushoto) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, ( wa pili kulia)  Mjumbe wa Bodi ya TTLB, Michael Kamba  (wa  kwanza kushoto) ( Picha na Lusungu Helela- MNRT) 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii  Saleh Pamba ( wa pili kushoto) akizungumza na  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia)   katika hafla ya uzinduzi wa  vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii (TTLB) nchini iliyofanyika  leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Alovce Nzuki, ( wa tatu kushoto) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, ( wa pili kulia)  Mjumbe wa Bodi ya TTLB, Michael Kamba  (wa  kwanza kushoto) ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
 Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufaa ya Utalii, Balozi Mwanaidi Maajar akizungumza na Wajumbe na Wenyeviti  kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB)  vikijumuisha  Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
 Mwenyekiti wa Kamati ya  Ushauri ya Utalii, Prof. Wineaster Anderson akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekeiti kwenye kamati hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha  Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT
 Baadhi ya Wajumbe na Wenyeviti waliochaguliwa wakiwa   katika hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha ni  Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Wajumbe na Wenyeviti  kwenye hafla ya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia Biashara ya Utalii nchini (TTLB) vikijumuisha   Bodi ya Leseni ya Biashara ya Utalii, Kamati ya ushauri ya Utalii na Mamlaka ya Rufaa ya Utalii zilizonduliwa leo jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)

Wizara ya Maliasili na Utalii  imefanya uzinduzi wa vyombo vya kusimamia biashara ya utalii nchini katika Chuo cha Taifa cha  Utalii kilichopo jijini Dar es salaam, ambapo vyombo hivyo vimejumuisha kamati ya ushauri,Mamlaka ya rufaa pamoja na Bodi ya mamlaka ya leseni.

Akiongea leo katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japheth Hasunga amewapongeza wanakamati wote waliochaguliwa na kusema kuwa anaamini kuwa watafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inapiga hatua kusonga mbele.

Pia, Naibu  Waziri Hasunga amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya kusimamia biashara ni vyombo muhimu sana katika kuendeleza sekta ya utalii na wajumbe wa vyombo hivyo ni muhimu kwa kusimamia sekta ya utalii nchini.

"Ni vyombo muhimu sana katika kuendeleza sekta ya utalii na wajumbe wa vyombo hivi ni muhimu sana kwa kusimamia sekta ya utalii hapa nchini" amesema Hasunga.

Aidha, Hasunga ameiomba Bodi ya Leseni ya Utalii iliyochaguliwa kufanya kazi katika misingi mikuu mitatu ya utawala bora ambayo ni Uhuru, uwazi, usawa na uzalendo ili kuepukana na migongano na kutokuelewana nyakati za kazi.

"Nawaomba mfanye kazi katika misingi ya utawala bora Uhuru, usawa, Haki na uzalendo"amesema Hasunga.

Katika hatua nyingiune, Naibu Waziri Hasunga amesema  kuwa sekta ya utalii ni sekta  inayochangia  kiasi kikubwa pato la Taifa  pia inasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni kwa urahisi, hivyo amewaomba watanzania kuwa wazalendo kwa kuhamasisha uhifadhi wa mazingira pamoja na utamaduni wa mtanzania ili vivutio vizidi kuwepo kwani wasipotunza mazingira utalii hautaendelea kuwepo.

Pia amesema kuwa japo Tanzania ina vivutio vingi vya utalii bado mapato ni madogo ukilinganisha na vivutio vilivyopo hivyo ameeleza mikakati ya serikali kuwa imepanga kufikia watalii milioni mbili mpaka ifikapo mwaka 2020 ambapo jukumu hilo ni la kila Mtanzania.

"Mapato ni madogo ukilinganisha na vivutio vilivyopo na serikali tumepanga kufikia watalii milioni mbili ifikapo mwaka 2020 ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafikia idadi hiyo. amesema Hasunga.

Pia ameisistiza Bodi ya leseni ya utalii kuhakikisha leseni za biashara zinatolewa kwa wakati na kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zilizopo.

"Mhakikishe leseni zinatolewa kwa wakati sahihi bila kucheleweshwa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria kama inavyosema"amesema Hasunga.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.

Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.

Makamu wa Rais alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .

“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.

Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo  za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.

Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.

Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji .

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya kampeni ya kupanda miti  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiandaa mti wake kabla ya kuupanda mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti  mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SHAKA ATEMA NYONGO,ASEMA YUPO TAYARI KUWAJIBA IWAPO KUNA UFISADI

$
0
0

Na Said Mwishehe,blogu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Shaka Hamdu Shaka amesema yupo tayari kuwajibika iwaoi itabainika anefanya ufisaidi wa aina yoyote katika utendaji wake kwenye nafasi aliyonayo sasa.

Shaka ametoa kauli hiyo kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam leo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Kheir James Denis ambaye amepokelewa rasmi na kutambulishwa kwa vijana wa mkoa huo.

Amesema katika nafasi hiyo amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kutetea mali za umoja huo na kwa bahati mbaya hatua hiyo imemfanya apigwe vita na kumkwamisha.Amesema chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Dk.John Magufuli ataendelea kusimama imara kusimamia rasilimali za umoja huo na hatarudi nyuma.

Amesema amekuwa katika mazingira magumu yanayotokana na kupigwa na ikafika mahali baadhi ya watu wakaanza kumzushia mambo ambayo hayana ukweli wowote.Ametumia nafasi kueleza wazi yupo tayari kuchunguzwa na kuwa tayari kuwajibika iwapo itabainika ameshiriki kufuja mali za umoja huo."Nimeshambuliwa na kupigwa vita kwasababu tu ya kuwa na msimamo thabiti wa kusimamia mali za jumuiya na maadili.

" Naomba niseme leo hii ni siku ya historia kwangu kwani nimetoa la moyoni ambalo nimekuwa nalo muda mrefu,nimeshambuliwa na kupigwa vita bila sababu.Niseme nipo tayari kuwajibika kama nitabainika kufanya ufisadi kwa kutumia bafasi yangu,"amesema Shaka.

Amesema katika kusimamia mali za umoja huo amebaini kuliwa kwa zaidi ya Sh milioni 250 katika mabanda ya maduka ya biashara eneo la Ukumbi wa Vija a Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuliwa fedha hizo wakaamua kusimamisha shughuli za kibiashara na kinachoendelea kwa sasa ni kubomoa eneo hilo na kujengwa jengo la kitega uchumi ambalo litaingizia fedha umoja huo.

Ameelezea namna ambavyo amekuwa akitiwa moyo na Rais Magufuli na kufafanua hatarudi nyuma atashirikiana na mwenyekiti wa umoja huo taifa kuusimamia umoja huo.

DK. KIGWANGALLA ATEUA WAJUMBE WENGINE WA KAMATI YA KUANDAA MWEZI WA URITHI WA TANZANIA

$
0
0


Na Hamza Temba, Arusha
..............................................................
Wadau wa Utalii Jijini Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.


Chambulo alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.


“Tunakupongeza sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.


Awali akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za Kimarekani 200.


Kwa upande wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000, magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za Kimarekani 15,000.


Kwa upande wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000 na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.


Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya kutekeleza kanuni hizo.


Alisema sehemu kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.


Katika hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake uanze mapema mwakani, 2018.


Akizungumzia wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watalii nyuma ya pazia bila kulipia leseni, alisema Wizara yake inaandaa mfumo maalumu wa kielektroniki utakaowezesha ukaguzi wa magari kwenye mageti ya kuingilia hifadhini ili kudhibiti vitendo hivyo.



Aidha, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara hao na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa weledi na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kulipa ada ya leseni husika kwa mujibu wa sheria. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.

 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wadau wa Utalii walioshiriki mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitambulishwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) kwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Merywn Nunes muda mfupi baada ya kikao na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. 

Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara yake leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi. 
Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong  akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) walipokutana katika hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO) 
  Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke akimwelezea jambo Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong  walipokutana katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong  wakitia saini hati ya makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  walipokutana katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  walipokutana katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KESHO KUFANYA MKUTANO NA WADAU WA PAMBA SHINYANGA

$
0
0
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (pichani) amesema mkutano huo utakaokutanisha pamoja wadau wa pamba utafanyika katika shule ya sekondari Savannah iliyopo katika eneo la Ibadakuli manispaa ya Shinyanga. 

“Mkutano huu utahudhuriwa na watu zaidi ya 1,000 wakiwemo mawaziri,wabunge, watendaji wakuu kutoka ngazi ya wizara,mikoa,wilaya,taasisi ,mashirika ya umma na wadau mbalimbali”,alieleza Telack. 

“Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa wananchi wanalima zao la pamba kwa wingi na kulifanya zao hilo lililokuwa limedorora sasa linakuwa na tija na kuwanufaisha wakulima hivyo mkutano huu utakuwa na majibu kwa wakulima na wadau wote”,aliongeza Telack. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema waziri mkuu pia atatembelea kiwanda cha Nyuzi kilichopo katika kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga. 
Aidha alisema pia kutakuwa na maonesho ya biashara na shughuli mbalimbali zinazofanyika mkoani Shinyanga. 

Telack alisema katika msimu huu wa kilimo cha pamba zaidi ya wakazi 80,000 wanatarajiwa kulima zao la pamba na wamepanga kulima katika ekari 67,579.9. 
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kesho Ijumaa Disemba 22,2017 atafanya mkutano na wadau wa pamba kutoka mikoa 16 nchini. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Waziri mkuu Kassim Majaliwa mkoani Shinyanga .
Waaandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa kikao hicho. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images